Search This Blog

SENDAYE (MALKIA WA MOYO WANGU) - 2

 







    Simulizi : Sendaye (Malkia Wa Moyo Wangu)

    Sehemu Ya Pili (2)







    Dawa ya oma ya madega itapatikana?! Na utaft utafanikiwa pasina vikwazo vyovyote



    James na wenzake baada ya safari ndefu hatimaye waliingia katika kijiji kile kabla awajazuhiwa na walinzi walokuwa katika msako Mkali wa kumsaka Isaki!



    Kutokana na sura ya bandia aloivaa Isaki,sura aloonekana kama mzungu alishindwa kutambulika na walinzi wale wakawakokota kuwapeleka kwa mfalme Omoti



    "Enyi wageni mtokao katika himaya ya mbali mmefata nini katika himaya yangu?!"



    Mfalme Omoti akauliza kwa hasira ,akupenda wageni katika himaya yake akihofia pengine angeweza kugundulika maovu yake



    "Sisi ni watafiti kutoka mjini tunayetafiti dawa ya ugonjwa hatari Wa homa ya madega na lengo la kuja hapa kijijin Ni kujaribu kuchunguza mimea na mizizi mbalimbali pengine tunaweza kuvumbua chochote!....



    James akajibu kwa kujiamin, mfalme Omoti akaachia tabasamu ilikuwa ni kama bahati kubwa kwa ugeni ule katika kijiji chake , kama dawa ile ingegunduliwa kijiji chake kingepata sifa kwa furaha akasahau hatari ilokuwa juu yake



    " ha ha ha haaa vizuri sana karibuni Bomole na hii ni bahati pekee tuloipata Bomole! , Isanjeeeee?!.....



    "Naaaam mfalme!"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Piga mbiu la mgambo kuwaita wanakijiji wote tuwafa amishe juu ya ugeni huu mtukufu ulotutembelea"



    Mfalme aliongea kwa furaha kijana yule mlinzi alotambulika kwa jina la Isanjee akatoka na kwenda katika chumba kimoja akachukua ngoma na filimbi akaanza kupiga akielekea mtahani kuwashtua wananchi kama alivyoagizwa



    Jopo lile la watafiti hawakuamin kwa jinsi walivyopokelewa vizuri mioyo yao ilifarijika,waliandaliwa maji ya kuoga wakaenda kuoga wote walipokwisha kumaliza kuoga wakakaa na kuanza kula wakinawishwa mikono na wanamwali warembo walovutia katika macho yao!



    Mpaka muda huo James ( Isaki) alikuwa bado ajamwona Sendaye kitu kilichomkosesha raha na kumpa mawazo ya ghafla!



    Na si Sendaye tu Bali mke yeyote Wa mfalme Omoti akuonekana pale swala ilo likamuumiza kichwa James ila ilibidi atulie mpaka mwisho lazima angegundua kitu!



    Taratibu watu wakaanza kuja kwa mfalme makundi kwa makundi kutoka pande zote za kijiji kile cha Bomole



    "Bomole omatayeeeee"



    Mfalme akaongea wana kijiji wote wakaitika



    "Omatayeeeee"



    Mfalme akarudia tena kwa Mara ya pili!



    "Bomole omatayeeeee"



    "Omatayeeeee"



    Na kabla mfalme Omoti ajaongea jambo lingine ghafla kimya kikatawala na ghafla mlinzi alosimama katikat ya mlango akasogea kidogo na wanamwali wawili wa kike wakatoka! Nyuma yao wake Wa mfalme walifatia wakitoka kwa mstari akianza na mke Mkubwa Wa mfalme akafatia mke Wa pili na Wa mwisho alikuwa ni Sendaye na nyuma yake walifatia walinzi wawili!



    Moyo Wa Isaki ulianza kupiga alipomuona Sendaye malkia Wa moyo wake ni miaka saba sasa ilipita na Sendaye alikuwa ni binti Mkubwa mwenye miaka 23 mkumbuke Sendaye aliolewa akiwa na miaka 16



    Isaki alibaki kagandisha macho yake kwa binti yule aliye enda kukaa karibia na mfalme



    Mawazo ya Isaki yakaenda mbali ....



    "Isaki mpz wangu mfalme Omoti anataka niolewe naye na kashawaambia wazazi sijui ntafanyaje mpz nami nakupenda!....



    Isaki akashtuka!



    " uwezi olewa na mfalme kwanza kawaua wazazi Wangu naye kuwa mfalme ,leo hii akuchukue na wewe mpz Wangu hapanaaaaaaa...."



    Isike alikumbuka taratibu machozi yakaanza kutiririka katika macho yake kabla ajajishtukia na kuyafuta ili asitiliwe shaka!



    Kwa bahati mbaya mfalme Omoti akujaliwa mtoto ivyo mrithi wa kiti chake bado ilibaki ni ndoto ila ilisemekana mtoto wa mdogo wake alotambulika kama mkwabi ndo angerithi kiti kile!



    "Bomole Omatayeeeee"



    "Omatayeeeee"



    "Bomole omatayeeeeeeeeeeee"



    "Omatayeeeeeee"



    "Nawashkuru wana Bomole kwa kuitikia la mgambo na kama muonavyo leo na ugeni Mkubwa sana hapa kijijini kutoka mjini na kabla awajajitambulisha kwenu niwatambulishe kwa malkia Wangu waliyoko pembeni yangu hawa ndo wake zangu malkia Wa kijiji hiki naomba mje muwape mkono!"



    Vijana wale wakanyanyuka Isaki ( James) hakiwa nyuma yao wakaanza kupita kwa wake wale Wa mfalme akianza na malkia Wa kwanza wapili na wamwisho Sendaye ambapo pembeni yake ndipo aliposimama mfalme



    Vijana wale wakapita mmoja baada ya mwingine ambapo alipowamaliza alimpa mkono mfalme na kusimama pembeni Yale anayefatia hivyo hivyo na mwingine hivyo hivyo mpaka akafikia kijana Wa mwisho Isaki!



    Akaanza kwa mke Mkubwa,akafatia mke wa pili na hatimaye akapiga hatua na kumfikia Sendaye!



    "Isaki!...."CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Ghafla Sendaye akatamka kwa sauti baada ya macho yake kuangalia mboni ya macho ya James!...



    Isaki akabaki kaganda!



    "Unasema nini?!"



    Mfalme akamuuliza mkewe baada ya kusikiwa likitajwa jina la Isaki mdomoni kwa malkia wake!



    Isaki akabaki katika butwaa huku akiwa kaushika mkono Wa Sendaye pasina kuonesha juhudi zozote za kuuachia!



    "Isakiiiiii"



    Sendaye akatamka tena kwa sauti kubwa kuliko ya awali ilosikiwa sasa na kila mtu huku akimwangalia James kwa macho yake makali ya kutokuamini kile akionacho mbele ya macho yake!



    Eti Isaki wake yupo mbele yake!...



    *dah nini kitaendelea?, mfalme atachukua maamuzi gani Isaki atakubali kama yeye Ni Isaki na vipi ni kweli Sendaye kamgundua Isaki wake?!*



    Jibu ya swali hili na maswali mengi ujiulizayo Ni hapo Kesho kunapo majaliwa mapemaaaaaa tulisongeshe!



    Watu wote wakagutuka kumshangaa malkia mdogo



    Mfalme akamsogelea mke wake na kumvutia kifuani!



    "Una nini mke Wangu?!"



    Akamuuliza lakini Sendaye hakuwa na jibu kwa mume wake yule , yeye mwenyewe alijishangaa ila alijua mapenzi yake mazito aliyokuwa nayo juu ya Isaki ndiyo yalomfanya vile!



    Pindi macho yake yalipotazama macho ya James alihis katazama macho ya Isaki na pia angalia ya James pia aikutofautiana na ya Isaki wake!



    Ila yule hakuwa Isaki kisura mpaka kiasili,isaki wake alikuwa mwafrika lakini yule Ni mzungu tena hata sura zilikuwa tofauti!



    Basi baada ya tukio lile kumalizika mfalme Omoti akaeleza sababu ya wageni wale kutembelea kijiji chao akawapa na faida wanakijiji walifrah sana kwa kupata ugeni ule!



    Siku hiyo wakaimalizia kwa maandalizi na mapumziko Kesho yake wakipanga kuingia porini kwa utafiti!



    Ila moyoni mwa James alimpenda sana Sendaye wake,katika kichwa chake aliwaza ilikuwaje Sendaye akamtambua na kweli ni alimjua au alimuhis tu! ,James aliwaza pasina jibu stahiki



    "Mbona unamawazo ivyo best?!"



    Danieli mmoja hapo Wa wanafunzi akamuuliza James baada ya kumuona hayupo sawa kimawazo



    "Najikuta hisia zangu zikinituma kitu!...."



    Dani akashtuka akamsogelea James na kukaa pembeni yake



    "Kitu gani brother..."



    "Najikuta hisia zangu zikinivuta na kumpenda Sendaye!"



    "What?!,Sendaye mke Wa mfalme?...



    " ndio nampenda Sendaye....





    Sendaye alibeba mashuka tayari kuwapelekea wageni wake wagen wale walipewa vyumba vitatu ambavyo chumba kimoja walilala Wa nne cha pili wawili na cha mwisho wawili alimaliza vyumba vyote na sasa alikuwa akikisogelea chumba cha mwisho ambapo ndani alikwepo James na Danieli



    "Najikuta hisia zangu zikinivuta na kumpenda Sendaye"



    Sauti yake ikaenda na kupenya kwenye masikio ya Sendaye aliyeshtuka tayari alishafika mlangoni akabaki kaganda palepale akishindwa kuunyanyua mguu



    "What! ,Sendaye mke Wa mfalme?!"



    Dani akauliza pasina kujua kila kitu Sendaye anasikia na lau wangeangalia mlangoni wangepata kumuona



    "Ndiyo Nampenda Sendaye!"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    James akatamka kwa kujiamini!



    Ghafla wakasikia kishindo na wote wakaelekeza macho yao mlangoni kila mtu alishtuka baada ya kumuona Sendaye mlangoni kishindo kile Ni kutokana na kuangusha mashuka aloyabeba



    Akufanya jitihada zozote za kuyaokota akabaki akiwakodolea macho kuwashangaa bado akuamini kile alichokisikia katika masikio yake alihisi pengine yu ndotoni na muda wowote angezinduka



    Hata kina James walibaki na butwaa pasina kuamin yule aliyoko mbele yao ni Sendaye waliyekuwa wakimsema!



    "Hodi....



    Sendaye akatamka kwa sauti ya uwoga na aibu tele!



    " karibu!....



    Wote wakaitika pia kwa sauti ya aibu vile vile!



    Sendaye kama akusikia kitu akawafata na kuwakabidhi mashuka ile anataka kugeuza James akamkamata mkono na kumvutia kwake!



    "Umesikia nilicho ongea juu yako Sendaye?!..."



    James akauliza akiwa bado kaukamatia mkono Wa binti yule!



    "Ha...ha..pana sijasikia kitu!"



    Sendaye akajibu huku akitetemeka!



    "Najua umesikia kila nilichokisema na huo ndo ukweli Wa moyo wangu Nakupenda Sendaye nipo tayari kufanya chochote juu yako.....



    " unaongea nini lakini wewe?!....



    Daniel akamshtua akimtenganisha mikono jinsi alivyomshika!



    "Kumbuka huyo ni mke Wa mtu tena mke Wa mfalme unataka kutusababishia hatari?!...



    " aijalishi!... Nampenda na ukwel utabak huo siwez kusitisha Upendo Wang kwake



    Sendaye akujibu kitu taratibu akageuka na kuanza kupiga hatua kuondoka!



    "Sendaye!,....Sendaye..... Sendayeeeee"



    James aliita lakin Sendaye akugeuka kumsikiliza yule amwitaye....



    "Unafanya nini lakini James?!....



    " siwez ubadilisha msimamo wangu"



    "Kumbuka baba yako alivyosema Mbona kuna wanawake wengi wazuri tu huko mjini kwa nini uangaike na washamba Wa huku kijijini na kujiingiza katika hatari ya kupoteza maisha nadhani unazijua sifa za huyu mfalme...."



    "Yote najua na upaswi kuniingilia katika maamuz yangu!"



    "Na si maamuzi yako jua matatizo yakitokea ni kwetu sote fikiria wagonjwa wangapi wanateketea kwa homa ya madega penzi kitovu cha uzembe haya!....



    " ujui Dani,ujui kitu.....



    "Ha ha haaa sijui nini?!,sijui kwamba wewe unatamaa kwa wake za watu au!..



    Wakati mabishano ya kiendelea huku nyuma mke Mkubwa wa mfalme aitwaye Inyasa alilala kitandani akiwaza mengi



    'Lazima kesho nimwambie mfalme'



    Akajisemea akitabasamu alikuwa nimwanamke mwenye wivu aliyewachukia wake wenzake,tabia yake hiyo ya wivu ilimsukuma siku hiyo kujua mume wake kalala na nani kati ya mke mdogo na mke wa pili!



    Akajiamsha na akaamua kuanzia kwa Sendaye!



    " mke Wangu wapelekee hawo wageni mashuka"



    Alimsikia mfalme akimwagiza Sendaye Inyasa akatabasamu na kujificha



    Alimshughudia Sendaye akitoka na Mashuka akajikuta tu akimfata kwa nyuma pasina kujielewa kwa nini roho inamtuma kumfatilia Sendaye

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alimfatilia mpaka chumba cha mwisho alishughudia jins Sendaye alivyosita pale mlangoni Kama vile alikuwa akisikiliza kitu!



    Inyasa akajiulza Sendaye anasikiliza nini?!,ila hakupata jibu Sendaye alivyoingia tu naye akaenda kutega sikio



    Alishika mdomo kwa mshangao kwa kile alichokisikia!....



    Akatoka kabla ajakutwa na kurudi zake chumbani!....



    'Lazima Kesho nimwambie mfalme'



    Mke Mkubwa Wa mfalme akawaza hakiwa kitandani mwake!,pasina kujua hatar ambayo ingeikumba imaya yao pindi angemweleza ukwel mfalme:





    Wakati mke Mkubwa wa mfalme inyasa akifikiria kumweleza mfalme kila kitu juu ya alichokisikia kutoka kinywani mwa mgeni wao James hali ilikuwa Ni tofaut kwa Sendaye raha yote ilimyeyuka



    Mfalme Omoti alilitambua hilo lakini akuijua sababu ya mke wake kurejea na kutowesha raha yote aliyekuwa nayo alipouliza sababu Sendaye alijitetea kichwa kinamuuma mfalme ikabidi amwache kila mtu akalala kivyake



    Sendaye moyo wake ulizidi kumuuma akujua sababu maneno Yale ya James yalijirudia katika kichwa chake alijikuta akimpenda ila Uhuru Wa kuwa nae asingekuwa nao kwani ingepelekea ampoteze kama alivyompoteza Isaki wake!



    Katu hakujua kama yule ndo isaki chaguo la moyo wake!



    Asubuh vijana waliwah kuamka na kujiandaa tayar kwa safari ya kuelekea porini wakabeba vyakula vyao vya akiba na kuianza safari wakaingia katika pori lile



    "Kabla atuja anza utafiti kuna ishu nataka tuiongee Mara moja tuwekane sawa coz moyo Wangu auna raha kabisa"



    Daniel mmoja hapo wa vijana wale aliongea kwa masikitiko!



    "Nini tena d?!"



    Wenzake wakamuuliza wakisogea!



    "Ni juu ya hatari iliyoko mbele yetu!"



    "Hatari?!,hatari gani?!..."



    Muda wote James ( Isaki) halikuwa kimya japo alijua Dan alitaka kwenda kueleza nini

    Si kwamba akuiona hatari ambayo ingewakumba kama angeendeleza kile alichokitaka ila naye ndo aliitamani hatari hiyo!



    "Swala lenyewe Ni juu ya mwenzetu kiongozi wetu James si kampenda mke mdogo wa Mfalme yule Sendaye"



    "Heeee eti nini?!"



    Vijana wakauliza pasina kuamini!



    "Na mbaya zaidi ka apa kuendelea kumfatilia na kumtorosha"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Vijana wale wakamwangalia Jemes kwa mshangao!



    "Yasemwayo Ni kweli kiongoz"



    Patrick kijana mwingine akauliza



    "Yah! Ni kweli!"



    "Mama yangu tumekwisha"



    "Si niliwaambia!"



    "James achana na hayo mawazo yasowezekana katika kichwa chako kumbuka kilichotuleta humu kijijini usiingize mambo mawili nadhani unazikumbuka sifa za mfalme huyu tutapotea wote...."



    "Mwambieni nyinyi labda atawaelewa Mimi Jana niliongea naye akaweka nta katika masikio yake;"



    Dani akazidi kueleza



    "Kwanza nashkur kwa ushahuri wenu mlonipa ila niwa ambie kitu kwanza moja James aogopi mtu, pili James akiamua kitu ameamua hawez kubatilisha nimempenda Sendaye lazima nimtoroshe nkaishi naye mjini....



    " unaongea nini lakini wewe?!....



    "Yah huo ndo mpango Wangu siwez kurudi nyuma twendeleeni na kazi muda unaenda"



    Kwa kuwa yule alikuwa Ni kiongozi wao ikabidi wamsikilize na kuendelea na kazi!



    ***



    Inyasa moyo wake ulifarijika sana alijua sasa Sendaye anaenda kuachika anabaki yeye na mke Wa pili bi nwalau

    Ambaye naye alijua ipo siku tu angemtengenezea mazingira akaachika abaki yeye pekee malkia Wa himaya ile!



    Ila alipata wazo!,kumwambia mfalme pekee aliona isingetosha ilipaswa awe na ushahidi Wa kutosha labda kuwafumania au kingine kama icho ilikuwa lazima awatengenezee mazingira



    Alijua!,James asingeishia pale angeendelea kumfukuzia Sendaye hapo ndipo angetengeneza mazingira mazuri ya kuaminika kwa mfalme pindi angemwambia ukweli!

    Kikubwa sasa ingepaswa awe makini kwa kila akifanyacho Sendaye ahakikishe yupo nyuma yake kufatilia!



    Mfalme Omoti ndiye aliyekuwa akigawa kazi kwa wake zake siku hiyo aligawa kazi kuni kwa sendaye maji kwa Inyasa japo kulikuwa na vijakaz lakini katika kazi hata wake zake walifanya mke wake Wa pili siku hiyo alimwacha jikoni na kazi za nyumbani

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sendaye akaingia msituni na kuanza kukata kuni!



    Wakati James akiendelea kuchimba mizizi,Magome ya miti na majani ghafla akasikia kwa mbali kama kuna mtu anachanja kuni



    Hapakuwa mbali na hapo alipokwepo moyo ukamsukuma kwenda kumwangalia japo alijua pengine Ni wenzake au kijana Wa kijijini kwani walitawanyika!



    Macho yalimtoka pima,moyo ukaanza kumwenda mbio!



    Sendaye!,naaam ndio alikuwa ni Sendaye malkia Wa moyo wake ,James akajikuta ameganda kama sanamu la Michelin,macho yake yakakiangalia kifua kibichi cha binti yule alichokizungushia kakitambaa yakatua mpaka katika kitovu kilicho onekana!



    Machoz yakaanza kumlenga lenga!



    Bado Sendaye hakumuona alizidi kukata kuni pasina kujua nyuma yake kuna mwanaume alikuwa akimtazama na kumkagua kila idara!



    James akaanza kunyata kumsogelea pale alipo!,



    Katu akujua kuwa bi Inyasa alikuwa katika chaka akiangalia kila kitu, tayar yeye alishamaliza kazi zake alijua kwa kuwa kina James wapo porini na Sendaye anakuja kuchanja kuni porini lazima wangekutana!



    Hakutaka kuipoteza point hiyo akafanya kazi haraka haraka na kuja mbio katika msitu ule na kujificha pale kuangalia kile kinachoenda kutokea!



    James akanyata na alipomfikia Sendaye akamshtua kwa kumtekenya kwapani Sendaye akaachia kilio cha mahaba!



    Kugeuka ni James! Kama kawaida Sendaye alishtuka akataka kugeuka kukimbia ila James akamuwah mkono na kumvutia kifuani kwake!



    'Kabla awajaongea mengi inapaswa nikamwambie mfalme aje ashughudie mwenyewe'



    Inyasa akawaza akatoka nduki!



    "Unaenda wapi Sendaye malkia Wa moyo Wangu!"



    'Mi malkia Wa moyo wake?!'



    Sendaye akawaza akimkumbuka mtu pekee alomwita jina lile



    'Sendaye malkia Wa moyo Wangu'



    Naye si mwingine zaidi ya Isaki!



    "Isaki!...."



    Akajikuta akihita kwa sauti ya taratibu James alisikia sauti ile akafarijika alijua Sendaye kamjua kumbe ni hisia tu

    Akamvutia kifuani mwake akiwaza kumwambia yeye ndo Isaki wake



    Ila kabla ajafungua mdomo wake Sendaye akajitutumua na kumsukuma kule James akaanza kukimbia James akubaki nyuma kumkimbiza akichukulia ule Ni mchezo Wa kimapenzi



    Katu hakujua hatari inayokuja kutokea dakika kadhaaa zijazo na laiti angejua?!!!



    *****



    Mfalme hakiwa katika kiti chake cha enzi na washauri wake ghafla mke wake Mkubwa bi Inyasa anaingia huku akihema



    "Mtukufu mfalme Wangu Sendaye yu akusaliti na mwanaume mwingine Wa mjini yule mweupe...



    " nini unasema?!!!!!"



    Mfalme aliuliza pasina kuamini



    "Twende mwenyewe ukashughudie"



    "Una uhakika?!"



    Mfalme akahoji pasina kuamini



    "Hakika mfalme Wangu"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Isagooo....



    " mfalmeee" isago akaitika



    "Mwizaki"



    "Mfalmeeee"



    "Na twikas"



    "Mfalmeee"



    "Chukua upinde wa sumu ingieni porini mkachunguze ichi na mkiwakuta katika mazingira hatarishi mzungu mumlete mfu na wenzake Sendaye Wangu msimdhuru ntamuua Mimi peke yangu kwa mikono yangu haya nenden



    Vijana wale wakatoa ishara ya utwiii nao kutoka nduki



    Walikuwa Ni walinzi mashujaa waloaminika na mfalme



    Taratibu wakaingia porini....



    ****



    James alizidi kumkimbiza Sendaye na ghafla alimkamata na kumdondoshea chini!



    Tayari hisia zilishampanda na alichopanga Ni kumalizana naye palepale porini



    Penzi lake lingemjulisha Sendaye kwamba yule ndo Isaki wake!



    Sendaye ujanja wote ulimuisha alibaki chini akimwacha Sasa kijana yule afanye atakacho kwani alimbana ipasavyo



    Katu hawakujua kuwa vijana hatari watatu walishaingia katika msitu ule na sasa walikuwa wakiwasaka!



    " heeee wale pale tena wana...wana...Fanya.....mapenzi....."



    "Achia mshale!"



    Kijana mwingine akatoa amri!



    *duuu je James atapona kweli?;,vipi kuhusu Sendaye!*



    "Hapanaaaaaa msifanye ivyo kumbuka mfalme kasema msimguse malkia kikubwa tuwakamate tuwapeleke mbele ya mfalme atawahukumu yeye!"



    "Hapana mfalme kasema tumpeleke mtu mweupe akiwa maiti na malkia akiwa mzima!....



    Wakaendelea na mabishano wakati wakiwa katika tanuri lile la mabishano kule vijana wengine walipokuwa wakifanya utafiti kijana Junior alilitilia shaka jani moja lililokuwa na miibamiiba na ligumu katika utafiti wake aligundua madini yaliyokwepo katika jani lile yalikuwa na uwezo Wa kuponesha magonjwa mbalimbali



    'Bila shaka jani hili linaweza kuwa dawa ya homa ya madega'



    Aliwaza mwenyewe akawashtua wenzake ambao sasa kwa pamoja wakaanza kumtafuta James ambaye alikuwa kiongozi wao kumuonesha uvumbuz wao!



    " hee wale pale tena wana..fanya mape..nzi"



    Wakati wakiendelea kusonga mbele ghafla wakashtuka kusikia sauti mbele yao wakasimama na kujificha katika kichaka kimoja macho yao yakaangalia mbele....



    Wote walipigwa na butwaa kwa kile walichokiona!



    "Mi nilishawa ambia mapema James hatatuponza amkutak kunisikia mnaona sasa?!"



    Dani aliongea kwa kulalamika!



    "Jamani now si muda wa kumlaumu ila tufikirie tutamsaidia kwa namna gani asiuwawe na wale vijana!"



    Wakazidi kupanga mikakati wakiwa wamechukia



    ***

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwisho wa mzozo wao vijana wale Wa tatu ulikuwa ni kuwakamata Sendaye na James kuwapeleka kwa mfalme wakiwa hai



    Wakajitoa katika kichaka kile



    James alishtuka kuona kaelekezewa mshale moyo ukaanza kumwenda mbio akajitoa mwilini mwa Sendaye ambapo Sendaye aliwakimbilia walinzi wale na kuanza kuwapigia magoti!



    "Msimwambie mfalme kilichotokea jamani nawaombeni nitawapa chochote mtakacho!"



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog