Simulizi : Tozani (Pete Ya Ajabu)
Sehemu Ya Nne (4)
Taratibu akaufungua mdomo wake na kumwambia Silvar naye kwa kujiamini bila woga akajibu....
"Nasikitika Zena sitoweza kuendelea kuwa na wewe!"
"What?!...."
"Ndio Zena, unipendi wewe! laiti kama ungekuwa unanipenda usingeniacha muda mrefu miaka mitatu peke yangu eti ni mpz Wang...
Hayo ndo mapenzi?!"
" hapana Silvar nisamehe sikujua kama nitakuudhi huo kwetu ni muda mdogo sana nilikuacha usome sikutaka kukuchanganya"
"Muda mdogo!?,miaka mitatu ni muda mdogo! muda mdogo kwako ambaye si binadamu ila kwangu ni muda mkubwa sana nilishindwa kuvumilia Nina mchumba Zena na tupo katika harakat za kufunga ndoa"
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Zena alishtuka,mapigo ya moyo yakaanza kumwenda mbio kwanza alishangaa jinsi kijana yule alivyojiamini,akajaribu kumsoma tena mawazo
Patupu!...
Aliishia kuona ukungu katika mawazo yake!,halikuwa jambo la kawaida meno yakaanza kugongana hasira zikawa zikimja kwa kasi....
Bisau aliyoko katika pembe ya chumba kile akatabasamu tena,mambo yalikuwa yakienda kama alivyokuwa akihitaji akanong'ona kwa sauti ndogo,sauti ilomfikia Zena mubashara katika masikio yake kama sauti ya fikra zake!
"Zena punguza hasira,dhibiti hasira zako nenda naye taratibu ujue nini muafaka wa penzi lenu"
Zena alikuwa kaung'ata mdomo kwa hasira akauachia alikua kaitwii sauti ya moyo wake kama yeye alivyojua
Katu akujua kama zile si fikra za kawaida Bali zilisukumwa na kiumbe mwenye nguvu zaidi yake ambaye mpaka hapo hakujua juu ya ujio wake
Bisau!
"Ok! Silvar nakubali mi ndo namakosa lakini kwa nini unipe adhabu kama hiyo?! Nakupenda Silvar plz nsamehe turudiane"
Ghafla Silva akaisikia sauti ya Bisau katika maskio yake ikimnong'oneza
'Ihitaji Tozani"
Naye akaitwiii
"Zena kweli unanipenda?!"
"Nakupenda Silvar"
"Upo tayari kufanya chochote ntakachokwambia ili tuwe wote?!"
Zena akashtuka!!!, akutegemea swali kama lile akaanza kumwangalia kijana yule kwa macho ya wasiwasi,macho yalojaa majuto ndani yake
Lile alilofanya sasa lilianza kumgharimu,akajuta kumuacha kijana yule kwa muda wote ule ambao kibinadamu ni muda mrefu sana
Miaka mitatu!!!
Ila sasa huo aukuwa muda wa kujilaumu akatingisha kichwa chake ishara ya kukubali
"Zena kama kweli wanipenda naihitaji tozani!"
"Tozani?!" Zena akauliza kwa mshangao pasina kuamini......
25
Hakika hakuamini kile alichosikia
TOZANI?!!!
Alijiuliza lakini akupata jibu la moja kwa moja zaidi ya kuzalisha msururu kibao wa maswali ambayo pia akuyapatia majibu
Akabaki akiwa ameshangaa!
'Kaijuaje tozani?!,kajuaje kwamba mi nnayo, anaihitaji ya nini au ili awe tajir?!,'
Akabaki kazama katika dimbwi zito la mawazo, si kwamba hakuwa na uwezo wa kumpa,
Laasha!....
Uwezo huo yeye alikuwa nao kabisa,kwa kuwa alijua tozani ni Mali yake na wasaha wowote angerejeshewa , na yeye kama yeye hakuwa ana ihitaji kivile?!
Ndo maana hata aliamua akiirejeshewa angempa Abrah,lakini wazo lake kuu ni kwamba binadamu yule kipenzi cha moyo wake kaijuaje?!
"Umeijuaje Tozani Silvar"
"Ha haaa haaaaa unanchekesha sana Zena!, nadhani umesahau Mara ya kwanza Mimi na wewe kilichotukutanisha ni mganga Zena nilienda kwa mganga ili nipate utajiri
Mganga huyo akanikutanisha na wewe ukanipenda kwel au si kweli?!"
Kwa unyonge Zena akaitika "kweli beby"
Silva akacheka tena kwa dharau...
"Basi baada ya wewe kuondoka ndani ya miaka mitatu nilipomaliza chuo maisha yangu yalikuwa duni ndipo niliporudi tena kwa mganga kusudi nipate utajiri mganga akanambia mpz wangu ni tajiri na anamiliki Pete ya utajiri Tozani nikiipata nami nitakuwa tajiri na ili niendelee kuwa na wewe naitaji Tozani lasi ivyo Mimi na wewe
Basi utakuwa unipendi wew"
Zena akaangua kicheko,kila kitu ambacho Abrah alimwambia alikiamini moja kwa moja pasina kufikiria wala kuchunguza
Mawazo yake yalishachanganywa, katika uchunguzi wake ule wakati akiwa ujinini hakuwai kumuona kijana yule akienda kwa mganga achilia mbali maisha hayo magumu aliyo yaeleza
Zaidi ya kuona akifanya machafu na wanawake tofauti tofauti ila vyote alivisahau na kuyaamini Yale maneno ya Silvar moja kwa moja
Akahaidi kumletea Tozani muda mchache ujao aifate chini ya bahari katika himaya ya muzidu!
Hata lililompeleka pale juu ya kulazimishwa na wazazi wake kuolewa na mfalme wao Zuberi akulisema akiogopa kumkwaza mpenzi wake yule.
Hakika mapenzi yananguvu zaidi ya kitu chochote kwa Zena ili lilijidhihirisha
Maskini! Akuujua ugumu wa kuipata hiyo tozani yenyewe
Laiti angejua!!!
Bisau akatabasamu na kutoweka!....
"Basi mpz wacha niende nikirejea ntakuletea hiyo tozani yako"
Baada ya maneno Yale msichana yule akatoweka na kumuacha Silvar akipunga mikono hewani kushangilia.
Katu akujua kuwa kazi ndo ilikuwa inaanza.
***
Zena aliamua kurudi kwa njia ya kibinadamu,alikuwa ni mdada Mrembo kupindukia,
Aliingia katika msitu ule na kwa Mara nyingine akamwona tena yule mtoto...
Akukuwa na mtu yoyote katika pori lile,yule mtoto alitembea kwa kujiamini
Alikuwa akilia huku nguo zake zimechanika,mkono wake ulikuwa ukitoa damu na umevimba kutokana na alivyo pigwa
Ghafla mapigo ya moyo wake yakaanza kumwendea mbio
Kwa mara ya kwanza Akajikuta akimpenda,akawa akipambana na hisia zile
"Unateseka kisa umasikini , Abrah unadharaulika kisa umasikini naapa nitakutajirisha kwa kukukabidhisha tozani pindi nikiirejeshewa nawe utakuwa tajiri katika ulimwengu huu
Utakuwa bilionea wa kwanza duniani teseka kwa muda ila ntakutafuta ngoja nikamuone kwanza mahabaty wangu"
Akakumbuka Yale maneno aliyo ongea masaa kadhaa wakati alipoelekea kwa Silvar,
Ila sasa Silvar napo anaihitaji hiyo tozani,
Atampa nani?!
Akaachana na jambo ilo akampita dogo Yule na kuendelea na safari yake...
Ila moyo wake bado ulikosa amani juu yake
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***
CHINI YA BAHARI
HIMAYA YA BISAU
Baada ya Zena Kumpita dogo yule ghafla akajigeuza na kuwa Bundi,
Tena bundi mwenye spidi akatoka katika ule msitu ulomilikiwa na viumbe jamii yake na kuelekea usawa wa bahari
Dakika chache alikuwa akishuka katika bahari ile kubwa akageuka na kuwa samaki ( nguvu)
Akuna binadamu aliyemuona kwa nguvu za kawaida tulojaliwa
Akawa akishuka chini kwa spidi sana,mpaka chini ya bahari, kuelekea katika lango la ujinini!
Ghafla akapotea na kutokea ndani ya lango lile kabla ajaingia kwenye mtego ulomnasa!
Ilikuwa ni nyavu naye alikuwa ndani yake
Alipo jaribu kuitazama ni viumbe gani vilivyomkamata,alishindwa kugundua
Mtego ulimtega,na njia ya kusalimika aikwepo kabisa
Viumbe vile vikamvuta huku vikiongea lugha ambayo Zena kureysh hakuitambua ni lugha gani!,
katika ardhi ile alovutwa ilikuwa na shaba,shaba ilomuunguza nguva yule,lakin hakuwa na jinsi! wazo lililopita katika kichwa chake ni usaliti!
alijua lazima jini MUZIDU atakuwa kamgeuka kwa vyovyote vile...
hapo ndipo kwa mara ya kwanza hatari ikaonekana katika kichwa chake,
viumbe vile vikazidi kumvuta huku vikipiga kelele ambazo zilimuumiza maskio yake!
wakamuingiza katika chumba kilichotawala giza, hata alipojaribu nguvu zake alitambua zilidhibitiwa kwani hakuona kilichokuwa mule ndani zaidi ya viumbe vile vilivyokuwa vikipiga kelele
Ghafla pakatawala ukimya,kwa viumbe vile na ghafla taa ikawaka na viumbe vile vilivyo mpeleka zena mule ndani vikatoa heshima....
kilikuwa ni chumba kizuri mbele ya chumba kile kulikuwa na kiti ambacho aliketi kiumbe kilichokuwa mfumo wa binadamu ila kilivaa nguo nyeusi tii na kichwani alijifunga kitambaa chekundu
katika paji lake la uso alichorwa fuvu la kichwa cha mtu na mifupa miwili ilokata jumlisha au alama ya kosa!,
pembeni ya kiumbe kile kulikuwa na nguzo nyekundu mbili na juu ya nguzo hizo kulikuwa na mafuvu ambayo Zena hakuweza kuyatambua ni ya kiumbe gani!
"wewe ni nani?!" alisikia sauti ya ukali katika maskio yake,japo alipomtupia macho yule jamaa hakuonesha kufumbua mdomo wake japo macho yake yalimaanisha lile aulizalo!,
kwa kutumia fikra zake akatambua viumbe vyote vilisikia swali lile kutoka kwa mkuu wao na wote walikuwa wakisubiria jibu,
jibu kutoka kwake! ina maana hawajanifahamu?! hawa ni nan?! na mbona huku ni kwa MUZIDU?!
ghafla viumbe vile vikatazamana,ni wazi viliyasoma mawazo yale ghafla akaskia akijibiwa na sauti ile ilomuuliza awali
"mimi ni mkuu wa ulinzi katika himaya hii ya muzidu nawe umeingia bila taarifa katika himaya yetu hivyo jukumu langu nikukutambua wewe ni nani na lipi lengo lako la kuja huku!"
"Mimi ni mgeni wa mfalme wenu Muzidu nahitaji kuonana naye"
Zena akawaza,viumbe vile vilimuelewa
"Je anajua juu ya ujio wako?!"
"La hasha! Lakini ni muhimu sana kuonana naye sina nia mbaya naye"
Baada ya viumbe wale kuwa siliana kwa njia ya fikra
Jamaa yule alotambulika kama mkuu wa majeshi akampa ishara kiumbe mmoja ambaye alitoweka muda huo huo
"Hakika wew binti ni Mrembo sana nambie unatoka himaya gani au wewe ni aina gani ya jini"
"Kwa jina naitwa jini Zena natokea duniani katika pori Pande na pia ni jemedari himaya ya kuzimu katika ufalme wa mfalme jb"
Viumbe vyote vilishtuka, jemedari kuzimu?!
Hakika hakuwa mtu wa mchezo kama angeamua kutumia nguvu zake za kando nje ya zile zilizo dhibitiwa za asili!
Wakati wakiwa bado katika mshtuko yule kiumbe yule aliyepotea akarejea
"Mfalme kukubali nimpeleke"
Sasa alitoa sauti na ghafla akageuka na kuwa mnyama mkubwa!
,"tafadhali naomba upande katika mgongo wangu"
ZENA akamtwii na kumpandia.....
Wakatoweka
***
Muzidu alitetemeka baada ya kuletewa taarifa ya ujio wa jini Zena
Hakuwa na shaka kaifata tozani yake naye hakuwa nayo je angempatia nini
Bado watu alowatuma wamsake Bisau hawakufanikiwa kwa hilo,
Alitamani kutoruhusu kuonana na binti yule lakini alijua angemjengea picha mbaya
Na kama je angeenda kumshtaki kwa mkubwa wao ' lusifar ' laana tullah ni yapi maamuzi ambayo yangetolewa juu yake?!
Ilikuwa lazima aonane naye amweleze ukweli juu ya tozani naye ajue cha kufanya kama ni nguvu waziunge pamoja kuisaka pete ile.....
Dakika chache baadaye Zena aliwasili akiletwa na kiumbe kile,baada ya kumfikisha kikatoweka
Wakabakia Zena na mfalme Muzidu
"Nimeifata Pete yangu!"
Zena akaongea kishari
"Pete yako sina,sikurejeshewa"
"Eti nini?!,ilo siyo jibu Muzidu na hayo hayakuwa makubaliano...."
Zena aliongea kwa ukali
"Punguza Jazba Zena kuna kitu nataka nikwambie, ( Muzidu akaanza kumsimulia chanzo cha tozani ile tangia mtoto wa mfalme aitengeneze baba yake ampe mtihani wa kuitupa na kutoa idhini kwa wananchi wote kuisaka mpaka alipokuja kumuua yule mtoto na kuja kuzimu kuichukua alipoirejesha akuipewa tena....na mpaka muda huo wanaisaka bila mafanikio"
Istoria ile ikamfumbua Zena akili,akajua lazima washirikiane kuisaka ili kulinusuru penzi lake kwa Silvar
"Najua unaisaka Tozani umpe mpz wako lakini tambua pia huo ni mpango Zena"
"Una maana gani?!"
Zena akauliza kwa bashasha,hali ya sintofahamu ikikishambulia kichwa chake
",upo katika mapenzi , uwez elewa na maana gani ila tazama katika kiganja changu"
Muzidu akamnyooshea kiganja chake
Ikaonekana kama tv kiganjani pale....
"Mfalme wa HIMAYA hii tumefanikiwa kuzigundua nyendo za Bisau na mahali alipo ila uwepo wake kiualisia bado ni matatizo kwetu"
"Mlichogundua ni nini?!"
"Mganga mkuu aliweza kuyanasa maongezi yake na ya binadamu mmoja na inavyo onesha hana tozani, Bali ipo kwa binti mmoja ambaye pia ni jini ivyo kwa kuwa huyo binadamu ampendi huyo jini nia yake aipate hiyo tozani ili amdhibiti....maongezi yenyewe ndo haya dokta aloyanasa
"Najua kwa sasa umpendi Zena sasa nimekuja kwako kwa ajili ya msaada ni kweli Zena ana hasira juu yako na muda si mrefu atakuja
akija Mwambie yeye ndo anamakosa kuondoka na kukaa muda mrefu na ili mrudiane ihitaji tozani....
Mwambie akuletee tozani ili umsamehe hapo basi utaipunguza au kumaliza hasira yake nipo juu ya msaada wako
naomba utambue kwa kuwa a nakupenda basi ataisaka tozani
na Pete hiyo ina utajiri mkubwa sana na ukiwa nayo utaweza kumdhibiti asikudhuru kwa kuwa unaweza kunuia asiwe anakuona
Sina la ziada nikuage pindi ukinihitaji nitakuja...."
Kama ulivyo ona ni sauti tu iliyonaswa na vijana wangu wanajua wewe ndo unayo tozani japo hawajui kama ndo wewe hapo,ila kwa Mimi nishaelewa lengo la huyu mzee kwanza ni kutuchonganisha Mimi na wewe
Kusudi uje unidai tozani pengine ukanishtaki kwa mkuu niukumiwe....
"Basi inatosha sikutegemea kama silvar atakuwa namna hii, silvar wa kunihadaa Mimi?!,silvar wa kunidanganya ?! Uko wapi upendo wangu kwake
Eti alinambia ameenda kwa mganga ha ha ha ha ha ha mapenz yakunitesa Mimi jemedari,sikutegemea kwa kweli
Bisau wa kumuadaa mpz wangu na kumpa mbinu za kutengana na Mimi hili litakugharimu bisau"
Zena akatamka taratibu , akiamsha nderemo na vifijo katika moyo wa Muzidu, akakubali kuungana naye kuisaka tozani ile...
Ikawa kinyume na malengo ya Bisau
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
***
JUU YA WINGU LA KWANZA LA DUNIA
Bisau alikalia mswala miguu kaikunja mkononi akiwa na kitabu kitakatifu anakisoma!
",kazi imeenda vizuri , na sasa najua lazima Binti yule ataenda ujinini kuidai tozani baada ya kuikosa Mimi nitamtokea pindi akitoka katika lango lile na kuingia katika uso wa dunia ntamwambia kama anataka tozani amwangamize yule mshenzi kwa nguvu alizo nazo na upendo kwa binadamu wake najua lazima afanikishe ili"
"Asalam Aleykum warhamatullah taghala wabarakat,Mungu ndo hakimu wa kweli mwenye kuhukumu kwa haki,mfalme wa siku ya malipo
Samehe nawe upate kusamehewa,usiviingize viumbe katika dhambi ya kukusudia....jua kila kiumbe kitaukumiwa kwa mizani yake utopunjwa hata chembe kama umefanya mbaya mdogo mfano wa Punje la tende utalipwa na kama umefanya zuri dogo mfano wa tunda hilo pia utalipwa wabillah taufiq"
Ilikuwa ni sauti ilomnong'oneza sauti ya malaika ikimsihi achane na lile jambo ni kinyume cha sheria na dini yake hairuhusu.....
"Hapana sipo kiunyonge hivyo nilishaweka nadhiri juu ya damu ya mwanangu lazima nimwanganize Muzidu kamwe sitobadilisha"
Alitamka Bisau akijinyanyua katika mswala ule,ile sauti aikumjibu kitu
Tayari alishakumbushwa maamuzi ni yake 'kunyoa' au ' kusuka' wakati akiendelea kutembea tembea juu wa wingu lile ghafla jicho lake likatua duniani katika lango la kutokea ujinini akamwona Zena akitoka
Kimuonekano alikuwa kuchanganyikiwa,bisau akaachia cheko dogo ni wazi alijua kuchanganyikiwa kule ni baada ya kuikosa tozani
Katu akujua mambo yalikuwa kinyume na vile akapanua mikono yake na kutoa mbawa akajiachia akipepea kama ndege
Akielekea uelekeo wa halipo jini Zena
Zena kureysh
Akamfikia na kutoa salamu,ZENA akageuka
Macho ya jazba,pindi alipomuona hasira zi kamvaa....
Kumbuka hakukuwa na binadamu alowaona
Bisau alikuwa juu kidogo ila Zena alikuwa chini!,yani kasimama
Zena bila kuitikia salamu na kwa ghafla akaunyoosha mkono wake na kufetua kombora
Kombora lile kwa kuwa lilikuwa ni la ghafla na bisau akujiandaa kulikabili likamtungua....
Kudondoka kwa bisau kukusababisha tetemeko la ardhi maeneo Yale....
"Mfalme!,bisau na Zena wanapambana duniani"
Jini mmoja alimpa taharifa Muzidu
Chukueni jeshi akikisheni anauwawa na mnakuja na tozani hapa!,akikisheni zena ajeruhiwi
Viumbe vile vikatoweka!!!
Bisau baada ya kutua chini tayari taa nyekundu ilishawaka katika kichwa chake!
Akajinyanyua hakiwa na mshangao na mshtuko wa mfadhaiko
Akamkazia macho Zena na kujaribu kuyasoma mawazo yake!,
Zena aliendeshwa na hasira na kukosa umakini!,akafungua mdomo wake na kutema moto kumwendea bisau!
alokuwa bado yupo chini!,kabla moto ule ujamfikia bisau,akaunyooshea mkono ghafla ukatoweka!,
"kwa nin uliamua kuya ingilia mapenz yangu bisau?,kwa nin wataka kuntumia mimi katika uovu wako?"
aliongea zena huku akipepesuka,kwani alitumia nguv nyingi bila mafanikio,
Bisau akabaki ameuachama mdomo kwa mshtuko ulomkumba!
' ni nini kilichotokea?!'
akawaza...ghafla nywele zikaanza kusisimka,mwili kumtetemeka ile ilikuwa si alama nzuri,kwake pale hapakuwa si sehemu salama tena kwake,
akuwa na muda wa kujitetea zaidi ya kupotea eneo lile,
ni wakati akitoweka ndipo vile viumbe vilipotokea, vikamzunguka
"Zena yuko wapi? yuko wapi huyo fedhuli!"
wakawa wakimuuliza,hakika vilikuwa vinatisha walikuwa na meno mawili yenye ncha kati katika kila pembe ya midomo yao macho yao yalikuwa kama ya paka ila unjano wake ulizidi na kuwa na mng'ao wa ajabu,kichwan vilikuwa na pembe ndogo mbili!,vilijaa manyoya katika mwili wao na nyuma vilikuwa na mkia mrefu ulofika chini!
hivi vilikuwa ni viumbe vibaya sana vya kijini! na vyenye sumu kali..
"kashapotea" Zena aliwajibu kwa mkato na kuendelea na safari yake akiacha vile viumbe vikimshangaa
***
Dhamira,nia na dhumuni la kuisaka tozani kutoka mikononi mwa Bisau ilimwandama,...
Upendo wake kwa Silvar ukayeyuka kama nyika zilizoshika moto
Kwa Mara ya kwanza akamkumbuka Abrah....
Ndipo moyo wake ulipoamia baada ya kugundua Silvar hana mapenzi na yeye
Akajipa moyo kumtafuta!
***
"Zuber najua unanipenda sana na si wew tu ni wafalme wa koo nyingi wanaonihitaji Mimi"
Zena alikuwa akiongeq na Zuber, mfalme wa msitu Pande kijana alotokea kumpenda lakini Zena akumpenda kabisa
"Najua hilo Zena ila tambua hapa ndo kwako ndo uliko zaliwa nawe ni jemedari kwa nini usiwe malkia wa himaya hii?!"
"Hiyo siyo sababu Zuber mbona Mimi baba yangu alikuwa binadamu?!,na binadamu wengi sana wananipenda?!...nipo kwenye mtihani nimkubali yupi!?
Zuber akacheka " usitake kunambia una malengo ya kuishi na binadamu,viumbe wa saliti ushasalitiwa mara ngapi na hao binadamu?!"
"Hilo alijalishi mtukufu mfalme!,nitatoa mtihani na atakaye faulu mtihani huo atakuwa ndio mume wangu"
"Mtihani upi Zena?!"
",ok naitaji unitafutie Tozani Pete ya ajabu sitokwambia mahali ilipo Bali inatafutwa na viumbe wengi sana na atakayefanikiwa kuipata ndiyo atakuwa mpz wangu"
Zena akaongea kwa kujiamini lengo aongeze nguvu ya msako ule,ila akumpenda kijana yule kabisa
***
Zuberi akakusanya vijana wake na kuwapa maelekezo
Nguvu zao moja kwa moja zikaelekezwa kwa Abrah kutokana na viumbe vile kunasa mawazo ya Zena pale porini wakati Abrah akipigwa na wale watoto wawili Piter na Samwel
"Unateseka kisa umasikini , Abrah unadharaulika kisa umasikini naapa nitakutajirisha kwa kukukabidhisha tozani pindi nikiirejeshewa nawe utakuwa tajiri katika ulimwengu huu
Utakuwa bilionea wa kwanza duniani teseka kwa muda ila ntakutafuta ngoja nikamuone kwanza mahabaty wangu"
Wakaikumbuka kauli hiyo,
"Yah kwa vyovyote lazima huyu mtoto Zena atakuwa kampa hiyo Tozani lazima aitoe atafatwa katika ndoto na halisi lazima aitoe tozani"
Aliagiza Zuberi,viumbe vyote vikainama kutoa heshima,w akaingia rasmi kazini kumuandama Abrah kuhusu tozani.....
Katu awakujua kuwa Abrah ajui kitu chochote....
Si katika HIMAYA hii tu...
Sauti za majini zilipaa katika mawimbi na kuwafikia walinzi wa Muzidu walokuwa katika msako wa tozani
Nao bila kujua mchezo unavyoenda nao w akaingia moja kwa moja kumuhisi binadamu Abrah ndo anayo tozani
Nao wakaanza kumsaka wakijua binadamu yule tozani ile kapewa na Zena....
Kwani walijua Zena ndo mmiliki wa tozani ndo mahana hata walimteka na kumpeleka kwa Muzidu ( kilichoongelewa nyuma awakukijua)
Katu walijua tozani ni Mali ya HIMAYA yao na wala Hawa kujua kuwa Muzidu aliihitaji makusudi amrejeshee binti yule...
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya Zena kutoa mtihani ule kwa mfalme yule, akahamua kuweka ulinzi kwa Abrah...
Ambaye sasa maisha yake yalikuwa hatarini , bila yeye kujijua.....
Mambo hapo nyuma ndo yalikuwa hivyo.
Daaah ni kumbukumbu ndefu!,Zena kashajua ukweli kwamba Silvar ampendi upendo wake kauamishia kwa mtoto Abrah
SURA YA NNE
(29)
Hali ya hewa ilikuwa ni ya kimanyunyu manyunyu na kaubaridi ka mbali Kali chosababisha kuleta uvivu watu kuamka na kuzidi kuvuta mashuka na mablangeti
Tayari kulikuwa kumekucha lakini kutokana na hali ile ya hali ya hewa bado palionekana ni alfajiri kumbe tayari ilikuwa ni saa mbili ila ilionekana kama bado ni saa kumi na moja!
Watoto wengi sana walifurahia hali ile kutokana na kujua kuwa hawatoenda shule,na walizidi kufurahi pale radi lilipoanza kupiga na kushusha mvua Kali,mvua iliyoambatana na upepo
KATIKATI YA PORI PANDE
Usiku ule ule
Pori pande lilikuwa ni pori lenye kutisha,tena lenye viumbe wa Kali wenye sauti tofauti tofauti tena zenye kutisha
Viumbe jamii ya majini,lilikuwa ni pori lililoogopwa mtu alishindwa kuvuka mwenyewe lazima muwe wawili au zaidi tofauti na ivyo basi ni lazima ungekutana na mambo ya ajabu
Mbali na mambo hayo pia kulikuwa na wanyama wakali kama nyoka wengi wa wapita njia walipita kwa uangalifu sheria ilokuwepo enzi na enzi za mababu ni kutoua kiumbe chochote katika pori lile
Ikiwa utaua nawe utomaliza siku tatu nawe utakufa....
Pembezoni mwa msitu ule alionekana mtoto mdogo kiumri si chini ya miaka kumi na Tatu alikuwa akikimbia,alikimbizwa na viumbe visivyoeleweka,viumbe vile vilikuwa na pembe kichwani,midomoni vikitoa damu,meno mawili yalichongoka katika kila pembe ya mdomo wao viliwaongezea ubaya na mtisho kwa binadamu awaonaye
Ndiyo!
Kijana yule alizidi kukimbia pasina kujali vitisho vya sauti zao,akujali kule akimbiapo wala hakuona kwamba ndo kuna hatari
Akazama ndani ya msitu ule viumbe vile vilizidi kumkimbiza safari hii spidi zao ziliongezeka kwa kila hatua walopiga
Na sasa walibakisha hatua chache kumfikia mtoto yule na ghafla akawageukia,naye sura ilibadilika na kuwa ya kutisha
Viumbe wale wakarudi nyuma kidogo
Mmoja akanyoosha mkono wake na kuachia kombora,mtoto yule kwa ustadi akaufunua mdomo wake na kombora lile akalimeza
Viumbe vile vikapigwa na butwaa!
Vikabaki vinashangaa pasina kuamini jambo lile!...
Kiumbe kile kikageuka ghafla na kuanza kukimbia tena...akipiga hatua kubwa kubwa,alikuwa ni mwepesi balaa,viumbe vile vikazinduka toka katika mshangao na kuanza tena mbio kumkimbiza mtoto yule
Safari hii mtoto yule alijishangaa!,kwanza uwoga na Pili ile hali ya kujiamini hakuwa nayo tena ni ghafla tu!
Ni nini kilichomtokea?!
Akujua
Akazidi kukimbia alipoakikisha amewaaacha mbali maadui zake akauparamia mti na kupanda juu yake
Muda huo aliyekuwa juu ya mti,akitetemeka chini ya mti ule viumbe wale wasioeleweka kwa sura zao waliwasili na kusimama eneo lile
Wakawa wakinusa nusa na Mara mmoja akamuona mtoto yule juu ya ule mti....
Akaachia mlio wake wakutisha,ni kama alikuwa akishangilia kupatikana kwa mtoto yule
Kiumbe yule akaunyoosha mkono wake juu,mkono ukawa ukiongezeka urefu mtoto yule akawa akilia....
Viumbe vile vingine vikawa vikiruka ruka kushangilia
Mkono ule ukamfikia mtoto yule na kumkamata kwa nguvu akawa anaurudisha mkono chini na kadri anavyourudisha mkono ulipungua kimo mpaka ukawa kawaida...
"Twaitaji tozani yetu!"
"Tozani?!"
Kabla ajajibiwa kibao kikalia katika paji lake la uso
"Usijifanye kutuuliza wewe ni kiumbe mdogo sana mwenye nguvu ndogo sana uwezi shindana na majini ya himaya hii kuokoa maisha yako tupatie tozani!"
"Sina tozani! Jamani tozani ni nini?!"
" ujui siyo utatupatia tu twende utatueleza"
Wakawa wanamkokota mtoto yule kwa nguvu,bila kujali kelele alizokuwa akipiga
Ajabu moja sasa
Ni katika ulimwengu waliokuwepo,baada ya yule mtoto kuingia katika pori pande lile
Palibadilika!,nje ya pori palikuwa na mvua ya manyunyu manyunyu ila ndani ya msitu hali ile aikwepo na sasa akiwa mikononi mwa viumbe wale mkono ulojaa miba na kumchoma choma pia mazingira Yale yalibadilika
Akuelewa!
Nyumba zilitawala kule alipokuwepo,anga lilikuwa jekundu na alipishana na viumbe pia visivyoeleweka
Alizidi kuachia yowe labda pengine alijua kulia kwake vile kungemsaidia
Alijidanganya
"ABRAHAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA...."
akashtuka anaitwa ghafla akaacha kulia,wale walomteka ni wazi awakuisikia sauti ile...wao walistaajabu kumuona kaacha kulia ghafla
Nguvu zake za kimaajabu zikawa zinamjia
Ndani ya mdomo wake meno yakaanza kubadilika,hasira kumtawala
"ABRAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA"
Akazidi kuitwa safari hii hata wale viumbe pia waliisikia sauti ile wote wakapiga magoti ishara ya heshima
Juu kidogo ya mawingu alionekana kijana mzuri akiwa kavaa nguo nyeupe na kofia ya kifalme alikuwa mweupe ni mzuri haswaa mwarabu si mwarabu muhindi si muhindi , msomali si msomali
Mtoto yule Abrah akabaki kamkodolea macho akiusanifu uzuri wa kiumbe kile
"Abraaaaaaaa naitaji tozani abraaaaa"
Akatamka akimwelekezea upanga wake ulowaka waka!
"Tozani?!"
Akajiuliza tena ni wazi akuijua tozani hiyo ilosemwa na viumbe vile waloihtaji
Baada ya kiumbe kile kumuona Abrah ana dalili ya kumuonesha akapiga kibao hewani
Kibao kile kikamfikia mtoto yule,akaangua kilio
Mtu yule alokuja akaonesha ishara ya kunyonga
Maumivu makali ya kunyongwa yakamfikia kijana yule akaweka mikono shingoni akikohoa,nyota nyota zilipita katika macho yake
Mtu yule ni wazi alikuwa na hasira na alipania kumuua mtoto yule
Abrah akadondoka chini na kuanza kutapatapa,kiumbe kile kiliamua kuua lengo wakose wote
Wakose wote?!.....................
Ni wakati huo kiumbe yule akiendelea kutetemeka kwa hasira na kuzidi kuikunja mikono yake ishara ya kunyonga ngafla mtoto yule akajitutumua na kuachia kombora moja,kiumbe kile kilichokuwa juu kikatua chini
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ilikuwa ni kama Abrah kakitungua,nacho kikaamka kwa ghadhabu, sasa kijana yule mzuri aliongozwa na hasira
Ghafla pale aliponyanyua kichwa chake kumtazama mtoto yule, akuiona kabisa sura ya mtoto yule zaidi ya kuiona sura ya binti Mrembo,binti alotokea kumpenda akimwangalia kwa tabasamu baya!
"ZENA KUREYSH?!" Mtu yule akaita kwa hamaki!
"Mfalme Zuberi,icho utakacho kufanya siyo kwa nini uue kiumbe kisicho na hatia kisichojua nini maana ya TOZANI,ntamlinda mpaka tone la mwisho la uhai wangu hakuna atakaye mgusa yeye ndiyo anayeimiliki TOZANI,yeye ndiyo moyo wangu....
Yalikuwa ni maneno makali yalotoka katika mdomo wa Dada yule maneno yalomchoma mfalme yule,maneno ya ukweli
baada ya Dada yule Mrembo kumaliza maneno Yale akageuka na kuondoka
Viumbe vyote vilibaki vikimtazama mfalme wao kwa kukaachia katoto kale kaondoke,wao hawakujua kilichomtokea mfalme wao kwani wao waliiona sura ya mtoto ilipobadilika awakuiona
Kijana yule mzuri kisura mfalme wa majini wa pori lile alilia
Alilia kuikosa tozani
Alilia kumkosa Zena!
Ghafla yeye na wenzake wakatoweka walipanga kwenda kujipanga upya
**************
Abrah baada ya kufanikiwa kuwatoroka viumbe vile alizidi kukimbia,akujua anakimbilia wapi
Alikuwa bado yupo katikati ya pori njia ya kutokea akuiona wakati akiendelea kukimbia ghafla akakanyaga mtego
Mtego ule ukamfunga mguu mmoja juu ya mti akabaki akining'inia ghafla akashtuliwa na sauti ya vicheko vya watu
No,hapana si watu wale ni vile viumbe vya kutisha vyeusi tiiii!,macho yao mekundu ya duara yaliwaka waka,meno yao yalitawaliwa na njano mdomoni walifoka moshi,katika vichwa vyao walikuwa na pembe walivaa nguo nyeusi
Hawa walikuwa ni tofauti na wale wa kwanza!
(Hawa walitoka himaya ya Bisau)
Abrah mwili ulimsisimuka, ulimwisha nguvu,akujua ataokokaje katika mtego ule
Katu akujua kuwa kuna kiumbe kinachomlinda wakati analia ghafla akasikia kibao
Alipigwa na mmoja wa viumbe wale
Ghafla Abrah akashtuka!.....
Kumbe ilikuwa ni ndoto,pembeni yake alisimama mama yake wa kambo akimtazama kwa chuki sana
Na pale alipohisi kapigwa na kiumbe yule wa ajabu kibao ni pale mama yule alipomnasa kibao
"Haya amka uende shule"
Ilikuwa ni sauti ya amri, mvua kubwa nje ilinyesha,na ni mvua haswa
"Lakini mama mbona mvua inanyesha ntaendaje mama?!"
"Ilo sijui ila nenda kajiandae uondoke hapa"
"Peter na Samwel je"
"Staki kuulizwa maswali amka uende!"
Yule mama hakuwa na u binadamu kabisa,akumpenda mtoto yule wa mume wake, alimnyanyasa,sa hiyo wanawe walikuwa wamelala bila kujali mvua inyeshayo akataka kumtoa mtoto yule raha yake anyeshewe
"Haya amkaa,amka saa mbili sasa"
Abrah kwa unyonge akajiamsha na kuchungulia nje,alikutana na mvua kubwa,akageuza macho kumwangalia mama yake yule akakutana na macho makali
Mama yule akazivuta nguo za Abrah za shule na kumtupia
"Haya vaa,vaaa uende"
"Pori pande ntapitaje mama!"
"Kwani siku nyingine huwa unapitaje na ona unijui Mimi ngoja nkakuletee fimbo ndo itakufanya ufanye haraka"
Baada ya mama yule kuongea vile akatoka,kwa uoga Abrah akaanza kuvaa nguo haraka haraka mpaka akamaliza
Mama yule aliporejea na fimbo alimkuta tayari kashamaliza kuvaa
"Haya sasa toka toka nje uende elimu ni ufunguo wa maisha yako ila naona wewe unazembea zembea"
Akaongea mama yule kwa ukali!
"Mama sijanywa chai!"
"Chai uliamka hasubui ukapika embu ntokee hapa"
Akaitimisha mama yule huku akimshika mkono mtoto yule na kumvuta!
Akamsukumia nje!....
Abrah akaanza kukimbia,mvua ilizidi kunyesha na kumlowanisha akujali hilo
Alichowaza ni msitu pande je angevukaje?!
Alijua asingekuta mtu pale langoni wa kuvuka naye ni vipi angevuka
Ghafla akakumbuka ndoto
Akaikumbuka tozani alodaiwa na viumbe vile vya ajabu,ajabu
TOZANI ni nini?!
Akawaza ila akupata jibu,mwisho mshawasha wa kutaka kufika shule haraka ukamwingia
Nia ni kumuuliza mwalimu wake wa kiswahili maana ya neno hilo
Akazidi kukimbia tena kwa moyo mmoja
Alikuwa kalowana chapachapa
Ila sasa moyo wa kijasiri ulimvaa,mpaka hapo alipofikia hakukutana na mtu hata mmoja sasa alilikaribia pori lile
Pori ambalo usiku aliliota
Pori ambalo alilijua habari yake
Moyo ukaanza kumwenda mbio,nywele kumsisimuka
Ghafla tabasamu likamvaa,baada ya langoni pale kumkuta mwanafunzi mwenzake
Tena wa kike, lakini yule akulowana hata chembe,alikuwa akimwangalia Abrah kwa tabasamu mwanana
Mwanafunzi yule alikuwa ni msafi tofauti na wanafunzi wa shule yao
Shati lake jeupe lilinyooka na kumwongezea umaridadi,sketi yake nayo ilipigwa pasi,hakika alikuwa kivutio machoni mwa Abrah
Wakabaki wanatazamana
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Mambo"
Mtoto yule akatoa salamu kwa sauti tamu huku akimpa mkono abrah , Abrah akaupokea na kukutana na joto lililomfanya asitamani kuachanisha mkono wake na wa mtoto yule.
"Poa mbona wewe ujaloana?!"
Kijana yule akaitika na kuuliza swali
"Mimi Nina mwamvuli huu hapa"
Macho ya Abrah yakauangalia ule mwa mvuli aloushika yule binti ambaye akuuona kabla na taratibu akayashusha macho yake chini katika miguu ya binti yule viatu hata havikuwa na tone la tope
Abrah akastaajabu!!!
"Mbona ujachafuka mguuni?!"
Akamuuliza safari hii akimwangalia kwa wasiwasi
"Nimeshushwa katika gari na baba yangu hapa"
Lile jibu alikumridhisha mtoto yule,akaangalia barabara akitegemea kuona alama za matairi ya gari
Ayakuonekana!!!....
Akaamua kupotezea
"Unaitwa Nani?!"
Kwa sauti tamu mtoto yule akauliza huku akilitoa begi lake mgongoni
"Abrah Tuesday"
"Unajina zuri sana" aka jibu huku akifungua begi lake na kutoa vikopo viwili vya chai na kamfuko ka mandazi,tena yale mandazi ayapendayo Abrah
Mate ya tamaa yakaanza kumtoka kijana yule binti yule akamtupia kikopo kimoja abrah akakidaka na kukifungua na kuanza kunywa
"Wewe unaitwa nani?!"
"Zena bint Kureysh"
Ghafla Abrah akashtuka baada ya kuskia jina lile....
Kikopo kile kikamdondoka
31
Ni kama jina lile alilisikia mahali!,ila ni sehemu gani kumbukumbu zake zilikataa kabisa kumkumbusha
Wakabaki wanatazamana
"Mbona umeshtuka sana Abrah"
Zena akamuoji kwa sauti ya upole
Abrah akaona aibu na kutazama pembeni
Mvua sasa ilikuwa imekatika na kuwapa wasaa watoto wale kuendelea na safari
Njia nzima Abrah alijihisi mwingi wa amani alipokuwa akimtazama binti yule
Moyoni mwake alikiri ni binti mrembo,na hakupata kumuona mwanamke Mzuri kama yule katika maisha yake.
Japo Abrah kiumri alikuwa ni mdogo lakini hilo alikuzuhia hisia Kali za mapenz kujenga kiota ndani ya moyo wake.
alijikuta akimpenda Zena na kumuitaji kimapenzi
"Lakini sisi ni bado wadogo Abrah wazazi wakijua?!"
Zena alijitahidi kupinga
",hawawezi kujua na tulivyo wadogo ni vizuri hatuwezi kupata mimba"
Abrah akazidi kusihi
"Ok nimekubali"
Na hatimaye binti yule akakubali hakika abrah akuamini akamkumbatia Zena kwa nguvu na kuanza kummiminia mvua ya mabusu
Baridi ile ilowatawala ikaondoshwa na joto Kali la miili yao
Walitembea wakiwa wameshikana mkono mpaka katika shule yao ambapo Zena alimuonesha darasa alilokuwa akisoma
Kwa kuwa bado hapakuwa na mwanafunzi hata mmoja alowasili waliendelea kukaa pamoja wakipiga stori na hisia zilipowazidi walizipunguza
Ni wazi penzi la binti yule lilimlevya,dakika chache baadaye wanafunzi walianza kuwa sili na kulazimika Abrah kuelekea darasani kwake wakiahidiana kuonana tena baadaye
Lakini haikuwa ivyo....
Baadaye muda wa mapumziko Abrah alijitahidi kumtafuta mwenzake bila mafanikio na hata mchana hali ilikuwa ile ile ikamlazimu kwenda kumuulizia darasani kwao
Jibu alilopewa hakukuwa na mwanafunzi kama huyo
Zena Kureysh?!
Akalikumbuka jina lile ni wapi alipolisikia,ni katika mdomo wa mfalme Zuberi aliyekuwa akihiitaji TOZANI
Ni katika ile ndoto aliyo ota
Ni Mara kadhaa kijana yule alilitaja kabla ajamponyoka na kukimbia
Wasiwasi ukaanza kumvaa
Mawazo juu ya TOZANI yakamrejea
Akatabasamu baada ya kugundua kipindi kinachofatia ni kiswahili....
Ni wazi ange uwasilisha msamiati wa neno lile apate kutambua viumbe vile viliitaji nini!
'Lazima kuna kitu nyuma ya pazia'
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Akajiwazia akielekea darasani
Dakika chache mwalimu aliingia,alikuwa ni mwalimu mpole, kwa jina alitambulika kama mwalimu SILVANUS wengi walipenda kumuita mwalimu Silvar mwenyeji wa Moshi mjini (ni baada ya kupata kazi)
Baada ya kuweka vitabu vyake katika meza na kuchukua kipande cha chaki na kuanza kuandika ubaoni
Alifundisha na baadaye aliruhusu maswali,Abrah akanyoosha mkono...
Mwalimu akamruhusu....
"Mwalimu ni nini maana ya neno TOZANI?!"
"TOZANI,?!"
Mwalimu yule alishtuka macho a kayatoa pima ni wazi akutegemea swali kama lile
Si mwalimu pekee aloshtuka,
Hata na baadhi ya wanafunzi pia,wengi wao wakistaajabu jinsi mwalimu yule alivyoshtuka!....
Na si katika darasa lile viumbe wale walishtuka hata baadhi ya viumbe visivyo onekana vingi vilishtuka na kusimama kusikiliza mwalimu angejibu nini
KATIKA FALME YA KUZIMU
Na si duniani tu baada ya Abrah kutaja jina lile viumbe vingi vilitega maskio kusikia mwalimu angejibu nini
Katika kitanda kilichozungukwa na dhahabu alilalia binti Mrembo
Zena Kureysh alozungukwa na wasichana wazuri kama yeye wakimpepea
Wote walikuwa na mabawa
Hata binti yule pia alishtuka baada ya mtoto yule kutaja jina lile
"Ooh shit Abrah unafanya nini?!"
Akapiga kelele,ni wazi maisha ya kijana yule yalikuwa hatarini
"Jaduuuuuuu"
Akaita kwa nguvu
Ghafla kijana mmoja akajitokeza
"Naitaji ukamuwekee ulinzi mfalme wa badae wa himaya hii"
Kijana yule akainamisha kichwa ishara ya kukubali....
Akatoweka.
Mwalimu akazidi kumkazia macho abrah
"Ni..nan... Ka..kwa....mbili.a?!"
Akauliza kwa kigugumizi
Abrah akaachia tabasamu pana kumuondosha woga mwalimu yuke
"Hapana ni Mimi mwenyewe nataka kujua"
"OK nifate ofisini"
Mwalimu akasema kwa mkato na kuachia miguno kwa wanafunzi
Akuangaika nao akabeba vitabu vyake na kutoka abrah akimfata nyuma
Kelele zikazuka darasani
Hatimaye Silvar na Abrah wakutana,na Silvar alimwagiza Zena ili aendelee kuwa naye amletee TOZANI mpaka muda huo akumuona tena Zena
Leo hii mwanafunzi amuuliza juu ya hiyo tozani
*****
Abrah alifika katika ofisi ya mwalimu wake yule mwalimu akampa ishara akae,mtoto yule akatii!.
Kimya cha dakika kadhaa kikachukua hatamu maeneo yale ilhali kila mtu akiwaza lake kichwani!,
mwalimu kwa dakika zile kadhaa macho yake aliyatambaza katika kitabu chake cha sarufi,lakini ukweli uliodhahiri mawazo hayakuwa katika kitabu kile.
Mawazo yake yalikuwa mbali,swali aliloulizwa na mwanafunzi wake yule lilimtatiza!
"kwa nini niumize kichwa hali ya kuwa mwenye majibu yupo mbele yangu?!'
akawaza
taratibu akakinyanyua kichwa chake,na kumtazama mtoto yule mdogo!
"ok! nambie sasa Abrah swali lako!" akauliza kwa Sauti ya utulivu,sauti ya utaratibu
"ndiyo mwalimu!,nlikuwa nataka kujua maana ya neno tozani."
Abrah akaweka tuo,mwalimu yule akaachia tabasamu,kusudi lake amwondoe na kujiondosha hofu ilokuja kwa kasi katika moyo wake
alifanikiwa
"hilo neno umelisoma wapi! au umelitoa wapi?"
Akampachika swali mtoto yule kusudi ajue pa kuanzia!,
"amna mwalimu sijalisoma mahala popote wala sijalitoa mahali!"
"ok umelijuaje hilo neno?!"
mwalimu akazidi kumbana,kutokana na akili ya kitoto alokuwa nayo Abrah akaona ili apate jibu ni bora amsimulie mwalimu wake juu ya ile ndoto ya kimaajabu aloiota
katu akuiona hatari ilokuwa mbele yake!,kwa nje mwalimu Silvar alionekana mwema,ila hakuwa mwema kabisa! ni mmoja wapo wa waanga wa viumbe waloisaka TOZANI ile!
"usiku nikiwa nimelala,niliota ndoto mbaya sana mwalimu,kuna viumbe sijui madubwasha gani yalikuwa yakinikimbiza na kunlazimisha niwape hiyo tozani"
"what? uliwapa?!" akauliza yule mwalimu kwa mshangao ilhali alisahau kuwa yule mtoto yule alikuwa hata ajui maana ya neno ilo
Abrah akapatwa na mshangao!,ndio alishangaa kushtuka kwa mwalimu wake yule kwa vitu vya kufikirika!
"Sikuwa nayo mwalimu!,na hata
siifahamu hiyo tozani yenyewe walokuwa wakiitaka,"
"kweli uifahamu tozani?!"
Mwalimu akamuuliza akiwa kamtolea macho makali,...
Abrah akashangaa tena!
'huyu mwalimu vipi!,lau kama ningeifahamu au ningekuwa nayo je ningemuuliza?!'
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Abrah akawaza,ni wazi alishaanza kumchukia mwalimu yule
"kama unayo Abrah tafadhali nipatie nitakupa ela yoyote utakayotaka plz mtoto mzuri!"
mwalimu akajitahidi kubembeleza
"kha!!!" Abrah akapatwa ma mfadhaiko,alihisi mwalimu lazima atakuwa anachanganyikiwa kwa namna yoyote ile!
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment