Search This Blog

TAREHE 9 SEPTEMBER - 1







    IMEANDIKWA NA : YOZZ PIANO MAYA



    *********************************************************************************



    Simulizi : Tarehe 9 September

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mnamo mwaka 2007,,alionekana binti mrembo kupita kiasi akitokea bafuni,, akazipiga hatua kuufuata mlango wa chumba chake,,,binti huyo anaitwa  shamy! akaufungua mlango wa chumba chake akaingia ndani,, Shamy alikuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu,,maarufu ka MLIMANI/UDSM....huu ulikuwa mwaka wake wa mwisho chuoni,,, akichukua shahada ya udaktari... 

    Shamy akajifuta matone ya maji yaliyokuwa mwilini mwake kisha akavaa gauni lililoshikilia mwili wake na kuonekana vyema uhalisia wa umbile lake lililokuwa linamvuto wa aina yake! wanaume wengi walimtaka Shamy kimapenzi,, lakini Shamy alikuwa na msimamo mmoja tu,,,,, akili na mawazo yake yaliwaza masomo,,,

    Shamy alipomaliza kuchana nywele zake akachukua mkoba uliokuwa na madaftari pamoja na Laptop,, kisha akazipiga hatua kutoka nje ya chumba chake akaufunga mlango wa chumba chake,,, kisha akazipiga hatua kuelekea chuoni!

     baada ya dakika kadhaa Shamy akafika chuoni akaingia darasani kwa ajili ya somo maalumu kwa siku ya leo!



    baada ya masaa saba kupita, muda wa masomo ulikuwa umekwisha, Shamy akazipiga hatua kurudi kule anapoishi! akiwa njiani akakutana na kijana,,,kijana huyo alikuwa ni mtu wa kawaida sana!  akamsimamisha Shamy! 

    Shani akaendelea kuzipiga hatua bila kugeuka!  ingawa alisikia kuwa kunamtu amemuita,, Kijana huyo aitwae Zack, hakukata tamaa akaendelea kumuita shamy,, huku akimfuata kwa nyuma!  Shamy aliposikia kijana huyo anamuita mfululizo akaamua kugeuza shingo yake kisha akasimama!

    Zack akamsalimia Shamy,, 'habari yako dada.

    Shamy akajibu salamu kwa uchangamfu,, "Safi mambo vipi?

    Zack akasema,, "kwanza nimefurahi san kuongea na wewe,, pili nilikuwa ninaombi,, je?  naweza kupata namba zako za simu? CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Shamy akasita akabaki kimya kwa sekunde kisha akasema,, "bila shaka.. lakini nipe sababu mbili je?  kwa nini unataka namba yangu?

    Zack akatabasamu kisha akaongea kwa kauli ya kujiamini!,, "nitakueleza jambo lakini

    si vyema kuongea hapa barabarani! Shamy akasema ,,"hakuna tatizo lakini nakusihi usipige simu usiku huwa sipendelei kuongea na simu usiku!

    Zack akatoa simu yake ndogo iliyoonekana kuchakaa kupita kiasi huku ikiwa imefungwa kwa rababendi!! maarufu kwa jina(KIMEO), Shami akaipokea simu hiyo kisha akaandika namba zake za simu na kuirudisha simu hiyo kwa Zack,, kisha akasema,, "kwaheri.

    Zack akabaki anamtazama Shamy kwa macho ya matamanio.



    Siku zilizidi kusonga,, Zack alihakikisha haipiti siku pasipokumjulia hali Shamy!

    kutokana na bidii ya Zack kuwasiliana na Shamy mara kwa mara wakajikuta wamekuwa marafiki,,

    Siku moja Zack alimpigia simu Shamy,  siku hiyo ilikuwa ni jumamosi. Zack akasema,, naomba nije kukutembelea siku ya leo,, Shamy akasema,, "bila shaka unakaribishwa.. siku ya leo huwa sitoki nakuwepo tu nyumbani.. nikijisomea,, Shamy akatoa maelekezo jinsi ya kufika anapoishi, Zack akapafahau akasema,, "maeneo hayo huwa nakuja mara kwa mara.. kuna rafiki yangu anaishi maeneo hayo!



    Baada ya lisaa limoja Zack alifika nyumbani kwa Shamy,, Shamy akamkaribisha...

    Zack akaonekana kama anataka kuongea jambo lakini alikuwa anasita.. akaamua kubakinalo moyoni!

    ilipofika saa moja za jioni Zack akaondoka na kurudi nyumbani kwake!



                       ********************************************



    Siku zilizidi kusonga,Zack akawa na ukaribu zaidi kwa Shamy,, akawa anampelekea zawadi,, Shamy akajikuta anaanza kumpenda Zack kwa sababu Zack alionyesha kumjali,, ingawa hana kipato,,,

    Siku moja Zack akajikaza kiume,, akaamua kutoa dukuduku lake moyoni,, akamtamkia Shamy kuwa anampenda!

    Shamy akawa hana jibu la kumjibu Zack....lakini vitendo vyake vilimfanya Zack apate matumaini ya kumiliki Shamy!

    miezi ilizidi kusonga,,wakajikuta wamezama kwenye penzi zito!!  watu wengi walimshangaa Shamy,, kwa nini kajiingiza kwenye mapenzi na mtu ambaye sio hadhi yake!  kutokqna na hali duni ya maisha ya Zack,, alionekana kutokupendeza,,mavazi yake yalionekana kuwa ya kizamani(Old fasion)

    lakini Shamy alionekana kuzama kwenye penzi la Zack kwa sababu Zack alikuwa anamjali,, na kumthamini,, pia alimpa ushauri mbalimbali, ambao ulimjenga Shamy!

    Wanaume wengi waliokuwa na kilato walimsumbua sana Shamy kutokana na urembo aliokuwanao! Shamy alikuwa anauzuri wa asili,, hata asipopaka urembo usoni/kujirmba bado alionekana ni mrembo kuliko!

    Siku moja Shamy akamwambia Zack ahame kule anapokaaa ahamie nyumbqni kwake,, Zack hakuwa na kipingamizi,, akakubali kuhamia nyumbani  kwa Shamy!

     

                 ******BAADA YA MWAKA MMOJA KUPITA*******   



    Shamy alimaliza masomo yake,,ya shahada  akisubiri ajira! maisha ya Shamy yalikuwa mazuri kwa sababu alipewe kila kitu alichokihitaji kutoka kwa wazazi wake..

    Siku moja Zack akamsimulia Shamy historia ya maisha yake,, akasema,, "baba yangu alimtelekeza mama yangu akiwa na mimba changa...

    maam alipojifungua akanilea yeye pekee... ingawa alinionyesha baba yangu.. lakini bado baba yangu hakuonyesha upendo kwangu!  nilipoanza elimu ya sekondari.. nikiwa katika kilindi cha mitiahani,, maam yangu alifariki,, nikalelewa na mama yangu mdogo,,, lakini kwa sasa ni mlemavu,, kapooza upande mmoja... pamoja na hayo nawatambua baadhi ya ndugu zangu upande wa baba!  kuna shangazi yangu mmoja hapatani kabisa na baba baada ya kumwambia kuwa hajafanya jambo jema kumtelekeza mwanamke akiwa na mimba,, mama yangu alikuwa na urafiki wa karibu na mdogo wake baba ambaye ni shangazi yangu.... mara nyingi huwa nakwenda kumtembelea anaishi KIGAMBONI.

    Shamy akamtazama Zack  kwa macho ya huruma,  kisha akasema,, "usijali mpenzi Mungu atasimama na wewe mja weke!  mimi pia nipo pamoja na wewe,, nimekupenda na nitaendelea kukupenda hivy ulivyo!!

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Siku zilizidi kusonga,, Siku moja Shamy akapigiwa simu ikitokea nyumbani kwao kuwa aende kwenye harusi ya kaka yake huko Jijini mwanza!

    Shamy akalazimika kuondoka kesha yake kuelekea Mwanza! kwa ajili ya maandalizi wiki moja kabla.... akamuacha Zack ndani ya chumba chake kisha akasema,, "baada ya harusi nitarejea,,



    baada ya siku mbili kupita Zack akaenda kumtembelea shangazi yake..alipofika shangazi yake akasema,, jiandae wiki ijayo tutasafiri mimi na wewe tutaelekea Mwanza.....kunandugu yako ulande wa baba yako anaoa..

    Kauli hiyo ikamfanya Zack afurahi sana kwa sababu anajua kuwa Shamy pia yupo mwanza hivy wataonana!

    baada ya wiki moja kupita safari ikawadia.. Zack na shangazi yake pamoja na mjomba wake ambaye ni mume wa shanga yake,, wakaingia ndani ya gari na safari ikaanza..

    siku ya leo ilikuwa ndio siku ya harusi.  hivyo walichelewa wakakuta tayari watu wapo ukumbini na sherehe inaendelea,,,, Zack akaketi meza moja yeye na shangazi yake!

    alipoangaza angaza macho yake akamuona binti mmoja kavalia gauni refu lililoshikiria maungo ya mwili wake vyema.. na kuonyesha uhalisia wa umbo lake.. binti huyo alifanana sana na Shamy....

    Sherehe ikaendelea......ukafika wakati wa utambulisho wa ndugu..... wakatambulishwa wazazi wa bwana harusi....... Zack akafurahi kumuona baba yake lakini hawezi hata kumsalimia kwa sababu baab yake alimtelekeza wala hataki kumuona!

    Zack akamuuliza shangazi yake,, "inamaana huyo anayeoa ni kaka yangu wa damu?

    shangazi yake akajibu,, "ndio ni kaka yako wa damu,, pia unamuona yule binti aliyevaa gauni la bluu?  huyo pia ni dada yako!  wa damu... kisha akamuita mmoja kati ya wahudumu wa sherehe hiyo.. akauomba amuite yule binti aliyevaa gauni labluu....

    baada ya dakika moja kupita alionekana binti huyo akija kwenye meza hiyo.... kumbe binti huyo ni mpenzi wa Zack,, hakuwa mwingine bali ni Shamy! 





    Wakati huo Zack alikuwa kanyanyuka pale kwenye kiti, alikuwa chooni,, Shangazi yake Zack akamwambia Shamy,, "nimekuita nikusalimie mwanangu.... Siku hizi mbona hauji kunitembelea! tatizo ni nini?

    Shamy akatabasamu kisha akazema,, "samahani shangazi nilikuwa natingwa na masomo!  lakini kwa sasa nimeshamaliza chuo nakuahidi nitakuwa nakuja kukutembelea mpaka utanichoka! Shamy aliongea maneno hayo huku uso wake ukionekana kuwa na tabasamu muda wote, kisha akasema,, wacha nikawaambie wahusika wa upande wa vinywaji wawaongezee vinywaji!

    Shamy akazipiga hatua na kuondoka zake,,



    Wakati huo huo alionekana Zack akitokea chooni akija pale kwenye meza!  alipofika Shangazi yake akasema, umechelewa dada yako alikuwepo hapa,, lakini utamuona tu na mtafahamiana!

    Zack akawa na shauku ya kutaka kufahamiana na dada yake,,, akasema,, "sawa shangazi kwani tunaondoka lini?

    Shangazi yake akajibu,, "kesho mchana!

    Zack akasema,, "sawa,,kisha akatoa simu yake,, akaandika ujumbe mfupi wa maneno(sms) akautuma kwenye simu ya Shamy... akimuuliza kuhusu sherehe inaendeleaje!  baada ya sekunde kadhaa kupita Shamy akajibu ujumbe wa Zack akisema,, "huku sherehe imependeza sana natamani ungekuwepo,, lakini sina namna,, vipi sherehe yenu?  alafu nilisahau kukuuliza,upo mwanza sehemu gani?

    Zack akataka kumuuliza Shangazi yake, kuwa hapo walipo panaitwaje lakini akamuona shangazi yake yupo qnaongea na mumewe!  akaona si vyema akikatisha maongezi ya watu wazima!  akabaki kimya huku akiendelea kuchezea simu yake!



    wakati huo huo alionekana Shamy akiendelea kuwasiliana na Zack kwa njia ya meseji(sms)

    baada ya lisaa limoja kupita sherehe ilikaribia kufika ukingoni,, akaonekana maam yake Shamy akimfuata Shamy akamkabidhi ufunguo wa gari akasema,, "itabidi utangulie na wageni wale... Shamy akatazama ule upande alioonyeshwa na mama yake.. akaona ni bibi na babu yake... Shamy akamtazama mama yake huku akitabasamu kisha akasema,, "hakuna shaka mama,, kwanza wale ni wazee sio vyema wakae macho mpaka muda huu,, usiku umeenda sana,, wacha niwapeleke,,, Shamy akanyanyuka na kuzipiga hatua mpaka pale alipokuwa  ameketi bibi na babu yake... akawachukua akaongozana nao mpaka nje ya ukumbi,, wakalifuata gari na kuingia ndani ya gari hilo! 

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Zack alimuona dada yake akitoka nje ameongozana na wazee wawili,, akaamua kuwafuata kwa nyuma,, ili angalau akafahamiane na dada yake kwa sababu tayari alionyeshwa kuwa huyo ni dada yake.. lakini hawakuweza kuongea..

    Zack alipofika upande wa nje akaangaza angaza macho yake,, lakini hakumuona tena dada yake!! alipotazama upande ambao yameegeshwa magari akaliona gari moja likiondoka,,, akajisemea moyoni,, "bila shaka wameondoka na gari hilo!

    Zack akazipiga hatua na kurudi ndani ya ukumbi!  lakini akawa anajisemea moyoni!  dada yangu anafanana sana na Shamy!! lakini dada ni mweupe kupita kiasi kuliko Shamy,..... Zack hakuweza kutambua kuwa huyo ndiye Shamy mwenyewe!  kwa sababu hakuwahi kumuona Shamy kajiremba usoni kiasi hicho..... yeye anaamini kuwa Shamy huwa hapendi kupaka vipodozi usoni wala kuchora kope,, na kuchora midomo yake kwa rangi..



    Zack alipofika pale kwenye meza, shangazi yake akasema,," muda mchache ujao tutaondoka kwenda kupumzika kwa sababu sherehe imekwisha....

    baada ya lisaa limoja kupita wakanyanyuka kutoka kwenye meza hiyo wakazipiga hatua kutoka nje ya ukumbi wakaingia ndani ya gari,, na safari ya kuelekea VIZANO HOTEL ikaanza,,,

    wakati wanatoka ndio muda Shamy alikuwa anarudi kuwafuata wazazi wake waondoke pamoja kurudi nyumbani,,, magari hayo mawili yakapishana pale getini,, Shangazi yake Zack akasema dada yako huyo amerudi! kisha wakaendelea na safari..

    hapakuwa na umbali mrefu,, walitumia mwendo wa dakika kumi mfululizo wakawa wamefika VIZANO HOTEL,

    zack akapatiwa chumba chake kwa ajili ya mapumziko,, pia Shangazi yake na mumewe walichukua chumba kingine!



                         *********************************************



    kule chumbani alionekana Zack akiwa amejilaza kitandani,, akachukua simu yake akampigia Shamy,,,

    Shamy akapokea simu kisha akasema nivumilie kipenzi cha moyo wangu,.,nipo naendesha gari nikifika nyumbani nitakupigia simu! kisha akakata simu hiyo.

    Shamy alipofika nyumbani,, akaingia chumbani kwake akaingia bafuni kuoga kisha akajilaza kitandani,, akachukua simu yake Akampigia Zack,,,,

    katikati ya maongezi Shamy akamuuliza Zack kafikia sehemu gani?

    Zack akajibu,, "VIZANO HOTEL....nimo kwenye chumba namba 57.

    shamy akafurahi sana akasema sio mbali na nyumbani kwetu.. kesho mapema,nitakuja, wewe unatarajia kuondoka lini?

    Zack akajibu,, "kesho mchana,

    Shamy akasema,, "nitajitahidi kuwahi kabla haujaondoka.



                              ***************************************



    Asubuhi palipokucha,,. Zack akaletewa chai,, mule ndani ya chumba chake..

    ilipofika mida ya saa tano za asubuhi,, Shangazi yake Zack akampigia simu Zack akimsisistiza ajiandae kuwa wanaondoka muda mchache ujao.. Zack akachukuwa simu yake akapigia Shamy akamsisitiza awahi,,



    Upande mwingine alionekana Shamy akiwa ndani ya taxi,, akimsisistiza dereva aendeshe gari kwa mwendo wa kasi ili Shamy amuwahi Zack kabla hajaondoka..

    awalipofika maeneo ya MWANZA HOTEL wakakuta kunamsongqmano wa magari.. kulikuwa na msafara wa chama cha siasa.. Shamy akaamua kumlioa dereva taxi,, kisha akashuka na kukodi bodaboda.....

    baada ya dakika kadhaa akawa amefika VIZANO HOTEL... akamuuliza muhudumu aliyepo upande wa mapokezi,,, muhudumu huyo akachukua kitabu cha orodha ya majina ya wateja waliolala hapo,, akaona jina la Zack limewekewa alama ya tiki.. alama hiyo inamaanisha kuwa mteja huyo ameshatoka ndani ya HOTEL hiyo!!!



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Shamy akatoa simu yake kwenye pochi,, akampigia Zack,,

    Zack akapokea simu ya Shamy,, akaongea kwa unyonge akimlaumu Shamy!

    Shamy akajikuta anakuwa mnyonge,, akaomba samahani kwa kuchelewa kufika!  Zack akamuelewa Shamy kisha akamuuliza wewe unarudi lini Dar es salaam?

    Shamy akasema itabidi nije kesho kutwa,, kwanza nimekukumbuka sana kipenzi changu! siku nilizokaa huku zinatosha!

    Zack akafurahi sana kusikia taarifa hiyo!



    Ilipofika majira ya saa saba za usiku,, wakawasili Dar es salaam,, Zack akaamua kulala nyumbani kwa shangazi yake kwa sababu ni usiku sana...





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog