Simulizi : Sundi
Sehemu Ya Pili (2)
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Upande mwingine,kule nyumbani kwa apolo,,alionekana Jumbe akitokea bafuni,,,akavaa nguo zake akazipiga hatua kuelekea sebuleni!
punde si punde,,,Apolo akaja,,,akamwambia kaka yake kuwa yeye anatoka hivyo atarejea baadae Jumbe akatabasam kisha akasema,,"sawa hakuna tatizo mimi nipo tu hapa nyum bani,,,lakini nitatoka baadae..
Apolo akazipiga hatua kuufuata mlango wa mbele,,,akaufungua,,,ghafla wazo likamjia akakumbuka kuwa kasahau ufunguo wa gari kule chumbani,,akaamua kwenda kuuchukua ufunguo huo.
wakati huo jumbe alikuwa akimtazama Apolo kwa macho ya umakini...akajisemea moyoni,,"huyu nbwege sijui ana Mungu gani,,kila akitaka kupita katika mlango huu,,vinajitokeza vikwazo,,,Jumbe alitamani hata amkamate Apolo na kumpitisha kinguvu katika mlango huo...wakati anawaza hayo yote...punde si punde Apolo akaonekana anazipiga hatua kurja sebuleni,,,akafungua mlango na kutoka nje.
Jumbe akabaki anamtazama Apolo,,aone anavyokufa...
lakini Apolo aliendelea kuzipiga hatua kulifuata gari lake,,,,akaingia na kuondoka zake,,,
Jumbe akafurahi sana,,akajilaza kwenye sofa akiamini muda si mrefu Apolo atakufa,hivyo utajiri unamkaribia siku chache zijazo..
baada ya dakika kadhaa kupita akaamua kumpigia simu Apolo,,akiamini tayari atakuwa amekufa,,,lakini cha kushangaza simu ya Apolo ikapokelkewa,,
akasikia Apolo anaongea! akaamua kukata simu hiyo..
baada ya masaa manne kupita akapiga tena simu ya Apolo,,ikapokelewa...kabla Apolo hajaongea chochote,Jumbe akakata simu.
akajisemea moyniu,,"mbona huyu mtu afi? au bado dawa haijaanza kufanya kazi? wacha tuone,
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
masaa yalizidi kusonga,,,Jumbe akawa bado anampigia simu Apolo mara kwa mara....kitendo hicho kilimshangaza Apolo kwa sababu Jumbe anapiga simu mara kwa mara alafu haongei kitu cha maana!
baada ya dakika kadhaa,,Apolo akaonekana akirejea nyumbani kwakee.
Jumbe akastaajabu mapaka muda huu Apolo yupo hai,,hata haonyeshi dalili yoyote ya kufa..akaamua kuondoka nyumbani..akijipa imani huenda Apolo akafa muda mchache ujao
akaamua kwenda baa kunywa pombe,,,ili akirudi nyumbani akute tayari Apolo amekufa,,hakutaka kushuhudia kumuona Apolo anavyokufa.
katika meza aliyokuwa ameketi Jumbe,,akasikia watu wawili wakiongea huku wanacheka kwa sauti kali.
ghafla aikasikika sauti ya mmoja wawtu hao wawili akimwambia rafiki yake....hivi utaacha lini utapeli? ipo siku utaingia matatizoni...
yule mtu akamjibu,,"wajinga ndio wanaoliwa,,,nitaendelea hivihivi kujifanya mimi ni mganga,,nakula pesa kiulaini...
Jumbe akageuza shingo yake kumtazama mtu anayeongea maneno hayo...akastaajabu kuona ni yule mganga, aliyempa ile dawa ya kichawi!
akajisemea moyoni,,"kumbe huyu mganga ni mganga bandia!! yani siku zote hizo napoteza muda wangu..kumbe ile dawa sio dawa ya kuuwa...
akaamua kunyanyuka kutoka pale alipoketi...akazipiga hatua kuifuata ile meza aliyokuwepo mganga...akasema,,"naomba pesa zangu ulizonitapeli..ulisema umenipa dawa....kumbe umenipa dawa bandia....
mganga akashtuka kumuona Jumbe,,kabla mganga hajaonge neno lolote...Jumbe akachukua chupa.iliyokuwa juu ya meza..slalomga mganga huyo kichwani,,chupa ikapasuka...mganga akadondoka chini akatulia tuli..
Jumbe akaingiwa na hofu.....alipojaribu kukimbia,,watu wakamkamata Jumbe..
walipomtazama mganga wakaona anatokwa na damu puani ja masikioni....walipojaribu kumpa huduma ya kwanza wakawa wamechelewa,,mganga huyo akafa!!
watu hao wakaanza kumshambulia Jumbe kwa kipigo kikali.
Walimshambulia kama mwizi! Jumbe akafanikiwa kupata upenyo...akachoropoka na kutimua mbio...
Kwa sababu ilikuwa ni nyakati za usiku,,hakuweza kuonekana kwa urahisi....akafanikiwa kufika nyumbani,,,akakuta Apolo ameshalala, Jumbe hakutaka kusimulia kilichomtokea....akaingia chumbani mwake akajifungia....akaandaa safari arudi kijijini kwao akajifiche,,,kwa usalama wa maisha yake!
Asubuhi palipokucha akadamka mapema,,akamuaga Apolo kuwa anakwenda kijijini kumsalimia mama yao...
Apolo akafurahi sana kusikia maneno hayo akiongea kaka yake...pasipokujua kuwa Jumbe alikuwa na mpango wa kumuuwa...pia usiku wa jana ameuwa mtu huko baa,,kwa kumpiga na chupa kichwani...
Apolo akaingia chumbani akatoka na kitita cha noti za zhilingi elfu kumikumi...akasema,,"hizi ni milioni tano,,,mpelekee mama,,pia mwambie nikipata nafasi nitakuja kumsalimia...
Jumbe akapokea pesa hizo kisha wakaongozana mpaka nje ya nyumba,,wakaingia ndani ya gari..kuelekea kituo cha mabasi...
Baada ya nusu saa kupita,,wakafika Ubungo,,Apolo akamuaga kaka yake na kumtakia safari njema huku akimsisitiza asisahau kumuomba Mungu amlinde,,katika safari yake afika salama.
Jumne akaitikia,,lakini mawazo yake hayakuwa hapo,,alikuwa anawaza kuhusu tukio la jana usiku!
akaingia ndani ya basi na kuketi kiti cha nyuma ya dereva.....
baada ya dakika kadhaa safari ikaanza...
ilipofika majira ya jioni,basi hilo likapata hitirafu lwenye upande wa injini....ikalazimika abiria wote wabaki hapo wasubiri basi hilo lifanyiwe matengenezo,,kisha waendelee na safari....
baada ya lisaa limoja kupita....mafundi waliokuwa wanalitengeneza basi hilo wakafanikisha kulitengeneza,,na safari ikaendelea.....lakini Jumne alikuwa na wasiwasi..hasa mtu akimtazama usoni,,alihisi huenda anafahamu kuwa yeye kauwa usiku wa jana! wasiwasi ulitawala juu yake..Akiofia kukamatwa na kufikishwa katika mikono ya sheria....akafungua begi lake na kutoa kofia,,anavaa kichwani mwake kisha akajifunika na koti lake kubwa alilokuwa amelishikilia mkononi..
Safari ikaendelea,,,ghafla kuna abiria mmoja akashikwa na tumbo la kuhara ghafla,,,akashindwa kuvumilia hali hiyo akaomba msaada,,dereva asimamishe gari,,,akajisaidie.
devera huyo hakusikia sauti ya abiria huyo, kwa sababu abiria alikuwa ameketi kiti cha nyuma kabisa.....
baada ya abiria huyo kulalamika kwa muda mrefu...baadhi ya abiria wakaanza kumshambulia dereva kwa maneno,,wakimtaka asimamishe gari....
dereva akapunguza mwendo,,akashimamisha basi hilo..kisha akageuza shingo yake kutazama upande wa nyuma,,walipokuwa wameketi abiria......akashtuka kumuona Jumbe akiwa amepanda basi hilo.!
wakati yule abiria anashuka kutoka ndani ya basi...
Dereva alikuwa akimtazama abiria aliyekuwa ameketi nyuma ya kti chake....ya wa dereva huyo ulionyesha wazi kuwa kunajambo fulani,,baina yake na abiria aliyekuwa ameketi nyuma ya kiti chake...ambaye ni Jumbe!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Jumbe akaanza kuingiwa na mashaka...baada ya kumuona dereva huyo anamtazama kwa macho ya msisitizo.......hofu ikazidi kuongezeka!
akajisemea moyoni,,"bila.shaka kuna jambo hapa....haiwezekani dereva huyu anitazame kwa muda mrefu kiasi hiki!
Kumbe huyo dereva,,ndiye yule rafiki wa yule mganga bandia aliyeuwawa usiku wa jana...akiwanae kule baa..aliikariri shura ya Jumbe,,ndiyo sababu inayomfanya akamtazama Jumbe kwa muda mrefu!
baada ya dakika kadhaa kupita...akaonekana yule abiria aliyekwenda kujisaidia,,akizipiga hatua kurudi ndani ya gari.....
na safari ikaendelea......lakini dereva bado alikuwa anatafakari
kufanya jambo fulani.....
baada ya mwendo wa lisaa limoja wakaukaribia mji mdogo..dereva wa basi hilo,,akakatisha kona kuifuata barabara nyingine inayoingia upande wa kushoto...
Jambo hilo liliwashangaza abiria wote waliokuwemo ndani ya basi hilo...wakaanza kuhoji wakimuuliza dereva anawapeleka wapi huko?
Dereva huyo hakujibu kitu chochote....aliendelea kuliendesha basi hilo....
kwa mbali kama mita hamsini,, kikaonekana kibao kimeandikwa KITUO CHA POLISI!
Jumbe akashtuka,,,hofu ikazidi kuongezeka,,,akajisemea moyoni,,"nilijua tangu mwanzo kunajambo litatokea,,, kumbe huyu dereva amenishtukia,,,bila shaka alishuhudia tukio la usiku wa jana...ghafla wazo likamjia,,akanyanyuka kutoka kwenye kiti alichokuwa ameketi....akaingiza mkono wake kwenye koti lake!!
TAHARUKI!!!!!!!!
Jumbe akachomoa bastola,,akanyoosha mkono wake kuuelekeza kwa dereva wa basi hilo, akasema,"simamisha gari haraka kabla sijasambaratisha kichwa chako.
dereva wa basi hilo akageuza shingo yake,,akaona bastola ikiwa imeelekezewa kichwani kwake! akaingiwa na hofu kwa sababu alimshuhudia jana Jumbe akifanya mauwaji ya rafiki yake,,ni yule mganga bandia aliyeuwawa usiku wa jana....akaamua kusimamisha gari...
abiria wote na hofu kuona bastola,,wakajua wametekwa..kila mtu akatulia tuli.
Jumbe akazipiga hatua akashuka kutoka ndani ya basi hilo...akatimua mbio na kutokomea kusikojulikana.
*******************************
wupande mwingine alionekana Apolo akiwa nyumbani kwake,,,nyakati za usiku,akatazama saa yake ya mkononi,,akajisemea moyoni,"sasahivi atakuwa ameshafika kijijini,wacha nimpigie simu,,,
Apolo akanyanyuka na kuingia chumbani akachukua simu akampigia Jumbe...lakikini simu ya Jumbeke... haikupatikana hewani!
wakati huohuo alionekana Jumbe akiwa ndani ya nyumba ya kulala wageni,,,akiandaa mikakati ya kusafiri kesho yake.
asubuhi palipokucha,akadamka mapema akasimama barabarani,,kusubiri mabasi yanayopita katika barabara hiyo yakitokea mikoa mabalimbali...alisimama hapo kwa lisaa lizima.....kwa mbali akaona basi moja akalitambua basi hilo kuwa linatokea jijini Dar es salaam kuelekea kijijini kwao.,akanyoosha mkono wake ishara ya kulisimamisha basi hilo.....dereva huyo akapunguza mwendo akalisimamisha basi hilo..mlango ukafunguliwa ...Jumbe akaingia ndani ya basi ,,akalipa nauli,,safari ikaendelea...
baada ya masaa miwili...wakafika kijijini...Jumnbe akashuka kutoka ndani ya basi akiwa ni mtu wa kwanza....akakodi bodaboda impeleke nyumbani kwao..wakati huo ilikuwa ni majira ya saa tatu za usiku.,
hapakuwa na umbali kutoka kwenye kituo cha mabasi.mpaka nyumbani kwao....alitumia mwendo wa dakika kumi kufika nyumbani kwa usafiri wa pikipiki.
Bi'Sundi akafurahi sana kumuona kijana wake mkubwa,,ni baada ya miaka mingi kupita pasipokumuona.
akamkaribisha ndani ya nyumba......hawakuweza kuongea kwa muda mrefu kwa sababu,,ilikuwa ni usiku.hivyo jumbe akaingia chumbani kupumzika,
asubuhi palipokucha Bi'Sundi akadamka mapema kama kawaida yake akaandaa chai kwa ajalili ya Jumbe,,,ilipofika saa tano za asubuhi,,Jumbe akadamka ,,akaoga kisha akaenda sebuleni ,,,akamkuta mama yake ameshamuandalia cha, akamsalimia kisha akafakamia chai utazani ananjaa ya siku mbili!
alipomaliza kunywa chai...akarudi chumbani,,,,kitendo hicho kilimfanya BiSundi astaaajabu! akajisemea moyoni ,,"inamaana Jumbe hata hajashtushwa na kifo cha mdogo wake! naimani Apolo alimueleza kuhusu kifo cha Nuru! hata kuulizi hajauliza hata kaburi la mdogo wake hataki kuliona? huyu mtoto sijui karithi tabia hizi chafu kwa nani?
Bi'Sundi akaamua kumfuata chumbani..akagonga mlango..Jumbe akafungua mlango ,akauliza kwa kufoka,," unasemaje mama?
Bi'Sundi akajibu,,"inamaana hutaki hata kwenda kuliona kaburi la mdaogo wako?
Jumbe akafunga mlango huku akisema,,"kila mtu atakufa,,si ameshakufa,,kwani nikienda kuona kaburi lake atafufuka? mama unazeeka vibaya...ebu niache.
Bi'Sundi akasimama hapo mlangoni kwa dakika nyingi,,,kauli ya Jumne ilimfanya asononeke kupita kiasi.....akazipiga hatua kutoka nje...akaelekea kwenye duka alilofunguliwa na Apolo...
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku zilizidi kusonga,,hatimae ikapita miezi mitatu...Apolo akaingiwa na wasiwasi,,akajiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu...kwanini kaka yake haruei Jijini Dar es salaam?
Akaamua kumpigia simu,,lakini kila akimpigia simu.... simu ya Jumbe haikupatikana takribani miezi mitatu...akaamua kumpigia simu Bi'Sundi...akamuulizia kuhusu kaka yake(Jumbe)
Bi'Sundi akasema kuwa hamuelewi Jumbe kutokana na tabia zake alizozianzisha..sikuizi amekuwa mlevi kupindukia,,akiondoka nyumbani asubuhi..anarudi usiku wa manane amelewa kila siku.....
Apolo akashangazwa sana na taarifa hizo!
Siku zilizidi kusonga..hatimae Jumbe akawa mlevi kupindukia...sikumoja nyakati za usiku... alionekana Jumbe kaongozana na jopo la watu sita,,ambao alikubaliananao na wakamlipa kiasi cha pesa,,kwa lengo la.kuiba bidhaa zilizokuwemo ndani ya duka la mama yake,, Jumbe aliamua kufanya jambo hilo kutokqna na kukosa pesa ya kunywa pombe na kuweka heshima katika sehemu aliyozoea kunywa pombe,,,kwa sababu alizoeleka kuwa yeye ni tajiri wa kununuq pombe katika baa hiyo!!! watu wakampachika jina la utani wakawa wanamuita mbigili,,maana yake ni kwamba miba midogomidogo ambayo huwezinkuikwepa...jina hilo lilizoeleka sehemu kubwa ya kijiji hicho wakawa wanamuita Mbigili.
walipofika katika duka hilo wakavunja mlango na kuiba bidhaa zilizokuwa na thamani ya milioni saba....lakini Mbigili akapewa milioni tatu,,kwa sababu ni mali ya wizi.....akafurahi sana.....ni haada ya jopo hilo la watu,,kuondoka na bidhaa hizo..
akarudi nyumbani usiku wa manane,,akagonga mlango kwa pupa.
Bi'Sumdi akashtuka kutoka usingiziji akamfungulia Mbigili mlango...Bi'Sundi akawikitika kumuona mwanae akiwa katika hali ya ulevi! akaingia ndani huku akimfokea mama yake pasipo sababu za msingi,,akisema,,"unachelewa kunifungulia mlango? inamaana ningekuwa nafatiliwa na wezi si wangenikaba?
kila siku nakwambia unazeeka vibaya..mimi ndiye tajiri ndani ya kijiji hiki......Mbigili alionge maneno hayo huku akizipiga hatua anayumbayumba kwa ulivi..akaelekea chumbani kwake.
Manno hayo yalimfanya Bi'Sundi awe mnyonge....akasikitika sana,,,Alainmba Mungu amnusuru mwanae katika janga la ulevi,,,akafunga mlango na kurudi chumbani kwake,,,Mbigili hakuwa na roho ya huruma kwa mama yake,,licha ya uzee aliokuwanao mama yake,,yeye haliona si kitu,,alijiamulia mambo atakavyo yeye.
Asubuhi palipokucha,,Bi'Sundi alidamka mapema akaenda buchani kununua nyama kwa sababu Mbigili alimwambia kuwa kila asubuhi atakapoamka akute supu....
kwa sababu Bi'Sundi alikuwa na upendo kwa watoto wake..alifanya hivyo kuhakikisha mwanae asikasirike,,ukizingatia ndiye mtoto wake wa kwanza....Bi'Sundi aliyafanya hayo yote lakini alikuwa anaumia sana moyoni,,wakati mwingine alitamamani asingemzaa Mbigili......
baada ya masaa kadhaa kupita..supu ilikuwa tayari.....akaziliga hatua kwenda kumuamsha mwane,,Bi'Sundi aligonga mlango huo mfululizo lakini Mbigili(Jumbe) hakuonyesha dalili zozozte za kufungua mlango,kwa lisaa limoja mfululizo! Bi'Sundi akaingiwa na hofu..akaamua kuita majirani wamsaidie kuvunja mlango huo!
TAHARUKI!!!!!
Mlango ulipovuniwa,,,wakamkuta Mbigili...amelala usingisi mzito huku jasho limamtoka,,,mwili uwake ulionekana kutetemeka kama utu aliyenyeshewa na mvua masaa mengi..na kupigwa na baridi kali! jirani mmoja akasema,,"bila shaka Mbigili anaumwa!
Wakafanya jitihada za kiloleka kwenye kituo cha Afya haraka iwezekanavyo!
alipofikishwa huko akafanyiwa vipimo,,,akagundulika kuwa anamaralia kali,,ambayo imejilimbikiza mwilini kwa muda mrefu pasipo kupata matibabu,,daktari akasema,,"mtu huyu amezidiwa kwa sababu anaonekana anakunywa pombe kupita kiasi kila siku,,hivyo si rahisi yeye kuhisi homa katika mwili wake!
Bi'Sundi akahuzunika sana,,akamuomba daktari angalau afanye jitihada za kunusuru maisha ya mwanae.....
akatoa pesa na kumkabithi daktari,,
daktari huyo alimtazama Bi'Sundi kwa macho ya huruma,,,akasema,,"mama,, asante mama huu ni wajibu wangu kutibu wagonjwa ndani ya uwezo wa taaluma yangu...ni vyema hizo pesa ukanunua dawa na mahitaji mengine kwa ajili ya mgonjwa wako.
daktari huyo aliongea maneno hayo,,huku akimfariji Bi'Sundi,,kwa kumpa.imani kuwa Mbigili atapona.
ikalazimika alazwa hapo kwa ajili ya matibabu...
***************************
Upande mwingine,,alionekana mwanamke mmoja,,akiingizwa ndani ya kituo chicho cha Afya...mwanamke huyo alikuwa ja hali mbaya kupita kiasi...
manesi wakampokea mwanamke huyo na kumuingiza ndani ya wodi kwa ajili ya matibabu! akalazimika kulazwa,,kwa ajili ya uangalizi wa madaktari. ndani ya kituo hicho cha Afya...
Muda wa kuona wagonjwa ilipokwisha,,daktari akasema,,hairuhusiwi mwanamke kubaki katika wodi ya wanaume....hivyo kama kunandugu wa kiume,,aitwe aje kumuhudumia kwa ukaribu,,
Bi'Sumdi akahisi kuchanganyikiwa,, kila akimtazama Mbigili,, hali ya Mbigili Ilionyesha kukatisha tamaa,,,akasema,,"samahani daktari,,mimi sina mtu yeyote ambaye atamuhudumia mgonjwa wangu kwa ukaribu,isipokuwa mimi pekee kwa sababu ndugu yake ambaye ni mdogo wake wa kiume, haishi hapa kijijini!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bi'Sumdi alifanya jitihada za kumshawishi daktari amruhusu yeye abaki hapo hospitali kumuhudumia Mbigili kwa ukaribu...lakini ikashindikana,,daktari alisisitiza kuwa huo sio utaratibu wa hospitali zote nchini!
Bi'Sundi akaondoka kwa unyonge,,huku akimuomba Mungu amponye Mbigili..
akazioga hatua za kizee,,kutoka nje ya hospitali hiyo!!! akasimama kando ya barabara..kutafuta usafiri wa kumpeleka kijijini.....lakini kila gari alilolisimamisha,, madereva wa magari hayo hawakusimamisha magari yao,,walimpita kama hawamuoni..
akaamua kuzipiga hatua akavuka barabara akazifuata bodaboda,,kwa lengo la kulipia apelekwe nyumbani kwake...
madereva wa bodaboda walimpuuza Bi'Sundi..kwa sababu ya uzee wake,,,ikasikika sauti ya dereva bodaboda mmoja akisema,,"hawa wazee wasumbufu...unaweza kumbeba ukamfikisha aendako...alafu asikulipe,,utamfanyaje?
Bi'Sundi alipojaribu kuongea,,
vijana hao walimkatisha kauli kwa kuongea mfululizo,,hivyo hakupata nafasi ya kuongea neno...
mmoja kati ya vijana hao akaonekana kumtazama kwa makini Bi'Sundi...kisha akasema,,"bibi panda nyuma ya pikipiki yangu nikupeleke uendako....
Bi'Sumdi akapanda pikipiki hiyo huku kashikiliwa na kijana huyo.
alipohakikisha kaketi vyema,,safari ikaanza...
hapakuwa na umbali mrefu,,walikwenda mwenda wa dakika kadhaa wakafika katika kijiji anachoishi,Bi'Sundi.....
Bi'sundi akasema,,"katisha kona lifuate lile duka...
walipofika Bi'Sundi akatoa pesa alikuwa kaifunga kwenye khanga aliyokuwa kajifunga..akachukua noti tatu za shilingi elfu kumi akamkabidhi,yule dereva bodaboda..
Dereva huyo macho yakamtoka,,hakuamini kile alichokiona,,akajisemea moyoni,,"yani hapa hakuna umbali wa kulipia pesa hii,,,kwa umbali huu nauli ni shilingi elfu tano....hata hivyo si vyema kumdhurumu mzee kama huyu...
akasema,,"bibi chukua chenchi yako..huku huwa tunabeba abiria kwa shilingi elfu tano....
Bi'Sundi akageuza shingo yake kisha akasema,,"usijali mjukuu wangu,,hiyo nimekupa kama shukrani,,kwa kunileta nyumbani kwangu...
Dereva huyo akashukuru kisha akaondoka zake.
Bi Sundi akazipiga hatua kuufuata mlango wa duka lake...akastaajabu kuona kufuri limevunjwa! akaamua kufungualango ja kutazama upande wa ndani!! akashtuka kuona baadhi ya bidhaa za thamani zimeibiwa....akajisemea moyoni,,"hapa kijijini kwetu hakuna wizi wa namna hii....lakini namuachia Mungu yeye ndiye mlipaji.
aliongea maneno hayo huku akizipiga hatua kulifuata sanduku lililokuwa chini ya meza....
kumbe ndani ya sanduku hilo huwa anatunza pesa za mauzo ya duka lake....zilikuwa ni pesa nyingi..kuliko thamani ya vitu vilivyoibiwa.....akachukua kufuli jipya akafunga mlango wa duka hilo..kisha akaondoka zake kuelekea nyumbani...alitembea huku akimuomba Mungu ampe afya njema mwanae..apone haraka.
Asubuhi palipokucha,,kule kwenye wodi aliyokuwa kalazwa Mbigili,,alionekana kupata nafuu,,Bi'Sundi alihakikisha anakuwa karibu na mwanae muda wote,,hasa ule muda wa kuona wagonjwa!
siku ya leo alifurahi sana,,akamshukuru Mungu kwa kumrejeshea Mbigili afya njema,,angalau kwa sasa anaweza hata kuongea,,
Mbigili akamtazama mama yake kwa macho ya aibu,,akidhani huenda Bi'Sundi ameshajua kuwa yeye anahusika na wizi wa kule dukani!
lakini Bi'Sundi hakuongea neno lolote kuhusiana na wizi wa dukani kwake!!!
Mbigili akasema,,"nimechoka kulala nahitaji japo kunyoosha miguu...aliongea maneno hayo akimwambia daktari...
daktari akasema ni jambo jema waweza kuzungukazunguka upande wa mbele kule maeneo ya getini..
Mbigili akanyanyuka kitandani akazipiga hatua akiwa akaongozana na mama yake..
CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati huohuo alionekana ye dereva wa lile basi,,alilolipanda Mbigili kutokea jijini Dar es salaam....ni yule dereva aliyeshuhudia Mbigili akimuuwa rafiki yake kwa kumpiga na chupa kichwani,,na kutokomea kusikojulikana..
kumbe yule mwanamke aliyeletwa hapo akiwa hoi taabani...ni dada wa dereva huyo..hivyo alipata taarifa,,na amekuja kumjulia hali dada yake....akashuka kutoka ndani ya taxi,,akazipiga hatua kulifuata geti la kituo hicho cha Afya!!!!
KIZAAZAA!!!!!
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment