Search This Blog

TOZANI ( PETE YA AJABU) - 5

 







    Simulizi : Tozani (Pete Ya Ajabu)

    Sehemu Ya Tano (5)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    mwalimu alianz kubadilika! woga,khofu ukamvaa,alitia huruma pindi akimwangalia usoni alionesha kuihitaji zaidi ya kitu chochote tozani ile...



    "mwalimu!" Abrah akaita kwa sauti ya upole



    "Naiomba kama unayo abrah plzzz"

    naona unanchanganya mwalimu lengo langu ni kukifahamu hicho kitu

    "ok pete! tozani ni Pete kama unayo naiomb ntakupa utakacho?"

    "pete?!" abrah akauliza kwa wasiwasi,kwake lilikuwa ni jambo jipya,akuijua wala kuikumbuka pete hiyo ila mwalimu Silvar alikuwa na uhakika abrah anaimiliki pete ile!

    Kwa kigezo cha kwa nini viumbe vile waitake?!

    "ina maana huna pete yoyote nyumbani?" abrah akatingisha kichwa ishara ya kukataa,mwalimu akamruhusu arudi darasani akawaze kwa makini niwapi alipoihifadhi tozani hiyo...

    abrah akuna alichojua.....

    Alijiinamia darasani akiwaza lakini akukumbuka kitu!....



    ****



    Huku nyuma mwalimu alishusha pumzi ndefu!...akaachia tabasamu la kifedhuli!



    "nahisi sasa utajiri upo mbioni!,lazima niimilike tozani,lazima nimmiliki malkia ZENA"



    Baada ya kukumbuka mambo yote yale, akachukua kitabu chake cha andalio la somo tayari kwa kuandaa somo la kesho yake!...



    Ghafla dirisha likajigonga,dirisha lililokuwa limefungwa



    Upepo mkali ukavuma na kupeperusha madaftar



    Silvar akabaki ameduwaaa, asijue nini kinachoenda kutokea



    Ghafla macho yakaanza kuwa mazito,ni kama alitumia kilevi kilicho mlevya,na ghafla akapotelea katika usingizi mzito



    ***



    ILIKUWA NI KATIKATI YA PORI



    PORI PANDE



    alikuwa amechoka,alikuwa anakimbia,alihema juu juu



    Alipotoka ni mbali anapoenda hakufahamu



    Alikuwa akikimbia huku akigeuka nyuma....



    Alikuwa akikimbizwa na viumbe vya kutisha



    Mdomoni vilikuwa vimejaa damu meno yalichongoka pembeni



    Hakuwa tayari kusimama akamatwe na viumbe vile,



    Ghaaa!!!, ghafla akajikwaa akadondoka....



    Pale chini alipodondokea , ghafla alihisi uwepo wa mtu akainua kichwa kidogo kuangalia Mbele



    Akakutana na miguu myororo,akapandisha kichwa kumwangalia mmiliki wa miguu ile

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akashtuka baada ya kumuona yule alosimama Mbele yake



    Naaaam, mmiliki wa miguu ile,akawasahau wale walokuwa wakimkimbiza,wakabaki wakitazamama....



    "Je umenletea tozani?!"



    Silva akanong'ona kumwambia binti yule...

    ",haa,haaa,haaaaa,haaaaaaaaaaaaa,haaaaaaaaa,haaaaaa,haaaaaaaaaaaaaaaaaaa,haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa,"



    Badala ya kujibu binti yule akaangua kicheko,Silva akabaki ameshangaaa



    "Zena si nnaongea na wewe umenletea tozani nlokwagiza?!"



    Badala ya kujibu Zena akaendelea kucheka



    Ghafla akasikia vishindo nyuma yake,Silvar akageuka.....



    Vile viumbe vilivyokuwa vikimkimbiza vilikuwa vimemkaribia sasa



    Akageuka Mbele kumwangalia Zena



    Akuwepo



    Mshtuko ukamvaa,kabla ajapiga hatua kukimbia kiumbe kimoja kikanyoosha mkono kumdaka, Silva akaachia yowe



    "Maaamaaaaaaaaaaaaaaaa"



    Ghafla akashtuka, kumbe ilikuwa ndoto,mwili wote ulimloa jasho



    Ghafla akashtushwa na kicheko kuangalia kicheko kilipotokea uso kwa uso na Zena



    Mapigo ya moyo yakaanza kumwendea mbio Silvar





    "Unanifuraisha sana Silvar,na si kunifuraisha tu,no bali pia unajidanganya...



    nilikupenda xna Silvar tena zaidi ya ufikiriavyo,ila nimeumia sana baada ya kugundua kuwa unipendi,



    unaitaji nikutajirishe then kwa kutumia hiyo hiyo tozani uniangamize!...."



    Silvar akashtuka akaweka mkono mdomon kwa mshangao!



    Zena akazidi kumchomekea kaa la moto katika moyo wake!



    "silvar umesahau kwamb mimi na uwezo kiasi gani!, naomba nikwambie wazi kwanzia sasa msaada wangu umeishia hapa naomba nikuache huru na maisha yako na mpz wako mpya Happy ,kila kitu ulichokuwa unakifanya nilikuwa nakiona kipindi ukiwa shule,sasa mimi si kikwazo katika penzi lako kuwa huru kwanzia sasa Silvar ha haaaahaaaaaaa haaaaaaa"



    Ghafla Zena akatoweka



    Bado silvar alikuwa katika bumbuwazi,pengine akutegemea kutokea kwa jambo lile



    Ghafla kama kuna mshale uliuchoma moyo wake, maumivu yakasambaa katika mwili wake



    Utajiri aloufikiria katika kichwa chake ulikuwa umeyeyuka,umeyeyuka bila yeye kujua umeyeyukaje!



    Na bisau je?!,si ali haidi kunsaidia?! Naye yuko wapi!



    Hapana!, hapana aiwezekaniiiii



    Japo hapo awali aliuhitaji Uhuru wa kuishi na Happy wake,lakini si kama ulivyomjia....



    Lazima afanye kitu!,lazima aongee tena na Zena Kureysh juu ya jambo lile...



    Ndiyo!....



    Alijua cha kufanya!,akanyanyuka na kuchukua kitabu chake akatoka ofisini mule...



    Alikuwa akielekea darasani kwenye kipindi.



    ***



    "Shoga amka usiwe mjinga wa kuendelea kumbeba yule mtoto jua wewe ukuwa mke wa baba yake wa ndoa na mwenye haki wa kurithi zile Mali ni yeye yapaswa ummalize sasa"



    Alikuwa ni mama mwenye umbo nene, wengi walipenda kumuita "jimama shostito" alikuwa akimshauri hivyo rafiki yake " mama Samwel"



    Mama yake Abrah wa kambo



    Mama Samwel akaachia tabasamu zito



    "Shostito si unaniamini,tena kale katoto nilivyo sikapendi na wiki hii lazima tukamalize lazima nirudi kwa yule mtahalamu"



    "Haya ndo maneno, ukikamaliza raha mustarehe wewe na wanao "



    Wakapigishana mikono Ki umbea



    "heeeee alooooooo"



    Ghafla katika pembe ya nyumba ile akazuka mtu,...



    Binti Mrembo alokuwa akiwa angalia kwa dharau



    Akasonya na kutoweka



    Alikuwa ni Zena Kureysh



    Wa mama wale awakujua juu ya ujio wake , mpaka anaondoka wenyewe waliendelea na maongezi yao



    "Kwa hiyo tutaenda lini?!"



    "Kesho shostito ntakuja asubuh asubuh kukupitia"



    "Sawa mamy"



    Mama Samweli akaomba ruksa na kuondoka zake.



    ***



    SURA YA TANO



    MIAKA KADHAA NYUMA



    Jimama Shostito alikuwa stendi kumsubiria mgeni wake , baada ya mabasi kadhaa kushusha watu hatimaye mgeni mwenyewe akashuka



    Japo alitokea kijijini lakini aiba yake ya uzuri aikufichika,umbo lake namba nane lililopendezeshwa na gauni lake refu lililombana na kumchora umbo lile,



    Kiumbo ni mrefu kiasi mwenye umbo la dondola



    rangi yake mng'aro wa chocolate,isiyochosha kuiangalia!,



    macho ya duara meupee,yalolegea kama katoka usingizini ila kumbe ndiyo yalikuwa asili yake



    pua nyembamba iliyochongoka,na kumuongezea urembo Mara dufu



    mdomo mdogo wenye lipsi pana za kuvutia



    kidevu kilichochongoka mithili ya yai

    kifua kilichobeba matiti madogp yaliyosimama yasiyoisha hamu kuyatazama na kuyatamani pia hasa kwa mwanaume rijali



    kiuno chembamba kama nyigu,...

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    hipsi pana zilizobeba mzigo wa haja nyuma,mzigo ambao aukuharibu umbo lake lile namba nane



    Japo aikuwa Mara ya kwanza kwa jimama kumuona binti yule ila kwa urembo ule alijua amepata chombo!....



    Katika wasichana alowamiliki akukuwa na hata alomfikia robo kwa uzuri ule



    Usingeweza kuamini kama yule alikuwa ni mama wa watoto wawili,bado alionekana binti mdogo chini ya miaka kumi na nane



    Basi jimama akamchukua na kumpeleka kwake , ambapo baada ya maelezo,binti yule Mrembo alotambulika kama Selina akaingia rasmi kazini



    Kazi ya umalaya,na jimama ndo alikuwa mmiliki wa danguro lile akiwauza.



    Baada ya miezi kadhaa , sasa Selina alikuwa mzoefu wa ile kazi , aliye mwingizia kiasi kikubwa cha ela mwanamke yule



    Jimama Shostito akazidi kumpenda Selina Mara dufu



    Mpaka siku hiyo mambo yalipokuja kubadilika....



    34



    Wateja wakawa wakija awamchagui tena,na hata wakimchagua baada ya tendo lile haramu lililo aramishwa basi awakumlipa



    Jambo lile si lilimuumiza tu yeye Selina la asha! Hata jimama shostito



    " hii si kawaida shosti lazima kuna kitu na urembo wote huo wiki mbili ujaguswa?!"



    " ndo ivyo shostito sijui mi nifanyeje"



    Selina aliongea kwa uchungu



    "Usijali Mimi ndo jimama kavae tutoke na usimwambie mtu kama unatoka na Mimi"



    "Sawa madam tunaenda wapi?!"



    "Haaaa na wewe nawe!,embu kavae huko usiniulize maswali yako ya kipuuzi"



    Kwa unyonge Selina akanyanyuka na kuelekea chumbani kwake,alipotoka alikuwa ni Selina mwingine si yule malaya , na changudoa



    Wakatoka!



    *****



    "Paaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa"



    Ulikuwa ni mlio wa gari kugongana,ajali mbaya sana ikatokea watu mbalimbali wakakusanyika na kuwatoa majeruhi



    Gari ya kwanza ilogongwa ilikuwa ni gari ndogo ya kutembelea Toyota Carina na ya pili ilogonga ilikuwa ni landrovar



    Bahati nzuri wausika wote awakupoteza maisha wakawaishwa hospitalini



    Katika ile Toyota Carina dereva alikuwa baba wa makamo alotambulika kwa jina la Jaduu Tuesday alitoka mapema na kuruhusiwa kwani yeye alikuwa na majeraha madogo



    Akabaki mke wake ambaye kwa bahati mbaya alivunjika uti wa mgongo na kuwa mlemavu!...



    Mzee jadu Tuesday na mke wake walibahatika mtoto mmoja tu alokuwa nasari alotambulika kwa jina la Abrah



    Mzee Tuesday aliangaika kumpeleka sehemu mbalimbali mke wake ikiwemo nje ya nchi bila mafanikio



    Mwishoe akakata tamaa na kuamua kukubali matokea,siku zikaenda,



    Pamoja na kuwa Tuesday umri ulienda kidogo hamu ya " x " ilimsukuma,



    Mwanzo alivumilia sana ila mwisho uvumilivu ukamshinda,hamu ya kufanya tendo lile ikamvaa



    Alijua mahala pa kuikata kiu yake...



    Ni kwa "jimama shostito" akafunga safari na kwenda kwake



    ****



    Baada ya kuingia mitaa kadhaa , hatimaye wakawasili walipokuwa wanaenda



    Ilikuwa ni kwa mganga wa kienyeji



    Mganga alotambulika kwa jina la mzizi mzizini



    "Heeee shostito huku tunakuja kufanyeje"



    Selina alioji akishangaa, kwani akutegemea jambo lile



    "Heeeeeee niache bibie kwani uoni mamikosi ulokuwa nayo ,wiki mbili ujachukuliwa na ',shape' ilo bado tu uamki?! Amka bibie hapa mjini watu wanatembelea nyota za wenzio"



    "Kwa hiyo mi nimelogwa?!"



    Kabla jimama ajajibu ghafla wakaitwa na kuingia kilingeni...



    "Haaaaaaaa mzizi mzizini sema tawile kama ntakalo sema ni sahii na kaa kimya kama ni uongo sawa?!"



    "Tawile babu,"



    "Haaaaaaaaaaaaaaaa"



    Kijana yule alicheka,kiumbo na kiumri alionekana ni mdogo



    Alikuwa ni kijana mwenye miaka 22,ila kutokana na heshima ya kazi ile wengi walimwita babu japo hakuwa katika makamo ya kuitwa hivyo



    Pamoja na miaka yake ile ila mzizi mzizini alikuwa na wake wa nne katika nyumba yake ile na wote waliheshimiana na walimpenda pia mume wao



    Hao wote walikuja kama wateja miaka hiyo wengine walikuwa ni wake za watu mwingine aliitaji utajiri, mwingine akiitaji mume na wote wakaangukia kuwa wake zake



    Tuachane na hayo tuendele....



    Akaanza kupiga manyanga....na ghafla akasema akimwangalia Selina



    "Najua shida yako ni utajiri!"



    Selina akamwangalia Jimama kwa uso wa mshangao,naye akapokelewa na uso wa mshangao vile vile



    Akakaa kimya bila kujibu



    Mzizi akacheka, akacheka Sana,tena Sanaa



    "Nilikuwa napima uelewa na tamaa zako na shukuru kwa kunielewa nimekupigia ' ramli' nimegundua kazini kwako kuna matatizo upati wateja ukipata awakulipi wakati mtoto unalipa?!"



    Mzizi akaongea kwa bashasha



    "Tawile babu" Selina akaongea huku akimwangalia bosi wake kwa furaha



    "Kuna mtu hapo hapo kazini kwako kakuchukulia nyota yako"



    Wakaangaliana tena



    "Ni nani mtu huyo Selina akauliza kwa hasira,"



    ",ha ha haaaaaaa mizimu airuhusu nikutajie jina kabisa ila ni rafiki yako wa karibu na Mara ya mwisho kuchukua bahati yako alikupa 500 unakumbuka?!"



    Selina akavuta kumbukumbu kweli kuna rafiki yake aliwah kumpa mia tano ya vocha kwa nzia siku hiyo ndo alinunua chuki dharau na mikosi ya kila namna



    "Sasa utatusIdiaje dokta"



    "Haaaaaaaa kwangu ni jambo dogo sana hili Leo itabidi mlale hapa usiku tufanye dawa asubuh ndo muende sawa"



    "Sawa babu"



    Wakakubaliana na jambo lile,katu awakujua kilichokuwa kichwani kwa kijana yule



    Alishampenda dada yule na alipanga usiku "amdonoe"



    Bado damu ya "u kijana" ilimchemka na kwa kuwa mizimu yake aikumkataza aliwachezea!...



    Basi Giza lilipoingia mzizi mzizini akampeleka Selina katika mapango aloyaita mapango ya mizimu w akaingia ndani



    Wote walivaa kaniki pasina nguo ndani

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mzizi akaweka beseni lake chini na kuchovya maji kwenye fagio akampiga nalo Selina huku anaongea maneno yasiyoeleweka



    Ghafla Selina akaanza kupandwa na hisia za ajabu



    Hisia za "x" mzizi akaendelea na zoez lile,maji Yale yenye mchanganyiko wa dawa yakawa yakiloanisha kile kitambaa na kumchora umbo lake...



    Mzizi ukasimama!



    "Kuna dawa inaitajika niingize ndani ya ofisi yako kesho utaona majibu hakika utakuwa mtamu kila utakaye kutana naye utoisha hamu kwake"



    Aliongea mzizi akitoa dubwasha lake na kuanza kulipaka dawa



    Ndio! hii dawa ya mnaso ukiingia unanasa



    Na kama ni mume wa mtu mkewe atakuwa na kazi kumrejesha kwake



    Selina alikuwa akimwangalia mzizi kwa jicho la matamanio wakati kijana yule akijipaka dawa ile.....



    Wakazama penzini!



    Baada ya kumaliza wakarejea nyumbani



    Selina akumwambia jimama kama amelala na dokta japo jimama alijua naye si alishafanywa?!



    Asubuhi na mapema wakaondoka kurudi nyumbani



    Na walipofika nyumbani kabla awajapumzika



    Mzee Tuesday jadu akawasili katika danguro lile......







    Macho yalimtoka mzee yule wa watu,ni baada ya kumuona Selina



    Wakaelewana na jimama akamlipa na kutoka na binti yule mpaka katika gesti iliyo nje kidogo ya mji ule....



    Ilikuwa ni Mara ya kwanza kwa mzee yule kutoka nje ya ndoa yake...



    Na alikuwa ni mwanaume wa kwanza kukutana naye toka alipotoka kwa mtaghalamu yule



    Kutokana na kukaa muda mrefu pasina kufanya tendo lile mzee alimvamia Selina ila binti yule alimtuliza na kuanza kumuandaa



    Mzizi mzizini alikuwa mkweli mzee wa watu aliweza,alilia kama mtoto mdogo kwa raha tamu alizozipata!



    Akajikuta amezama moja kwa moja,kwa binti yule



    Akampa alichoitaji , ikawa nyumba yake ndogo, akamtoa kwa jimama na kumjengea



    Kila alichoitaji alimpatia, urafiki wa jimama na Selina ukaongezeka maradufu



    Baada ya Selina kujengewa na kufunguliwa saloon kubwa akaenda kuwachukua wanaye



    "Samwel na Piter"



    Maisha yakaendelea



    SIKU KADHAA MBELE



    "Shostito unajua Jadu anatumia fedha nyingi sana kwa lile li mwanamke lake yani nilivyosilipendi?!'



    " mmmh bibie mbona ilo jambo dogo sana mi nilikuwa nakushangaa kwa kushindwa kuli ng'amua ilo mapema"



    Aliongea jimama akikaa sawa



    "Ndo ivyo shoga sijui Mimi nitafanyaje?!"



    "Mmmh eti ujui utafanyaje changamka mwanamke , yapaswa umuondoe yule duniani hivi si unajua yule ni mke wake halali kuna Leo na kesho ako kabwana chako kakifa ghafla unazanishia una kitu pale?!,zaidi ya aka kasaluni na ako ka nyumba"



    "Kweli shostito nishauri nakutegemea wewe ndugu yangu"



    "mzizi mzizini ndo jibu la matatizo yako si unamuamini yule kijana?!"



    Selina akaachia tabasamu jepesi,nuru ya mafanikio ikionekana katika uso wake,kimoyomoyo akajishangaa kutokuwa na mawazo Yale ya kwenda kule tangu mwanzo mpaka jimama amwambia,akajilaumu kimoyomoyo.



    "Tu naenda sangapi sasa?!" Akauliza kwa unyonge



    "Si sangapi linalowezekana Leo lisingoje kesho twende zetu hata saivi"



    Selina hakuwa na kikwazo wakatoka na kuingia katika gari tayari kwa safari ya kwenda kwa mtaalamu huyo



    *****



    "Mzizi mzizini najua kilichowaleta hapa kwangu!"



    Jimama na Selina wakaangaliana



    "Tawile babu"



    "Hahaaaahaaaaa wala hata msijali huyo mama tutamwondosha Leo duniani hahaaaaahaaaaaa"



    Wakaangaliana tena,Selina akatabasamu,moyoni alizidi kumuamini mzizi mzizini, mzizi akachukua yai katika chungu chake na kuanza kukiombea kwa mizimu wake....



    Akaomba mpaka mikono iloshika yai lile ikawa ikitetemeka,akamkabidhisha SELINA yai hilo binti Yule alishangaa joto lililokuwa nalo.....



    "Vunja yai hilo na likivunjika kazi yako itakuwa imekwisha"



    Selina huku mikono ikimtetemeka akalivunja hai lile chini na kiini chake ilikuwa ni damu yake, "kwisha kazi yake sas jaduuu ni wako tu" akaongea kijana yule akicheka



    "Asant dokta ila nilikuwa na ombi jingine"



    "Haaaa haaaaaaa aaah nishalijua wala usijali,aya yote ayana masharti ila ilo unalolitaka litakuathiri kwa kuwa utoweza masharti yake!"



    Wote wakaangaliana , wakaachia miguno mmmmmmh,jimama alikuwa na shauku la kutaka kujua ni ombi gani rafiki yake alilolihitaji kubwa zaidi ya lile



    '' dokta nisaidie nipo chini ya miguu yako sitovunja masharti"



    "Kukusaidia nitakusaidia ila nakwambia lazima utavunja tu masharti kwa nini usiachane na jambo hilo?!"



    Selina akamwangalia mganga yule kwa jicho lililolegea,jicho lililomtamanisha , mzizi mzizini akameza mate tayari alikuwa akibabaika,kila njia aloangalia ilimuonesha lazima tu angevunja masharti,ila kwa kuwa Aling'ang'ania ilibidi tu amfanyie alichoitaji



    "Sawa nimekubali itabidi ulale hapa usiku tuianze tiba"



    Selina alifurahi sana,wakaagana na jimama akapewa chumba chake apumzike kusubiri tiba ya usiku.



    ***

    Ni wakati mama Abrah alipo kuwa amelala ghafla akapaliwa na kuanza kukooa,koo likawa kavu akamuonesha Abrah kwa kitendo amletee maji



    Ndo pale ambapo Selina alivunja lile yao ,mama Yule ajatulia tuli,tayari alikuwa kashakata roho na ABRAH aliporejea alimkuta mama yake katulia akaanza kumuamsha, kimya, kwa mawazo yake ya kitoto akajua pengine amelala akamfunika vizuri naye akajilaza pembeni.



    ***



    Baada ya Giza kuingia mzizi mzizini na Selina wakaenda katika pango lile,kama kawaida mzizi akamuanzia kwa kumpa dawa ya mnato ambayo alimwingilia baada ya tendo lile wakaanza tiba nyingine....



    Tiba ilompa shaka mganga yule....



    Japo aliifanya moyo wake ulimuuma kwa kujua kuwa mwisho wake ni mbaya pindi Yule binti atakapovunja masharti!,ila akuwa na jinsi



    Jaduuuuuuuuuuuuuuuu........mzizi mzizini akaita kwa sauti kubwa,sauti ilikuwa kama mwangwi na kwenda mpaka katika masikio ya mzee yule



    "Jaduuuuuuuuuuuuu.... "Mzizi mzizini akaita kwa mara ya pili na ghafla kizungu zungu kikali kikamshika mzee yule pale pale akadondoka



    " jaduuuuuuuuuuuuuu" akaita Mara ya tatu na ghafla pale jadu alipoanguka ile sauti ikamzindua....



    Watu walikuwa wamemzunguka kunsaidia pindi alipodondoka wakatawanyika kwa uwoga!



    Macho yaliwaka waka,....

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwa jinsi alivyoamka na kuyaangaza macho yake kama vile anashangaa kitu kilimpumbaza kila kiumbe kilichokuwa pale,na ghafla akarudi tena chini....

    "Jamani itakuwa ni maleria awaishwe hospitalini"

    Mmoja wa watu waliokuwepo pale akasema wote wakaunga mkono na kumbeba kumwingiza katika gari yake,mmoja mwenye ujuzi wa kuendesha gari akaingia akifuatwa na wengine wawili katika gari safari ya kuelekea hospitalini ikaanza

    Naaam ni wakati mzizi mzizini akiita ile Mara ya tatu pale Jaduuuuu na mzee yule kuamka kabla ajarudi tena chini,pale jadu aliporudi chini ni mwili tu ndo ulirudi lakini kivuli cha mzee yule kilisafiri kuifata sauti ya mganga

    Mganga akachukua chupa ilokwepo ndani ya chungu , chupa ndogo tu akaifungua na kuanza kuimba.....

    "Ilenyaaaaaa nangalamsiya......." Akawa akirudia rudia maneno hayo sambamba na kuzunguka kile kibuyu kichupa chake mkononi

    Ghafla upepo mkali ukaanza kuvuma,upepe ule ukawa ukiingia kule ndani ukajikusanya na ghafla ukaingia ndani ya kichupa kile.....

    Mzizi mzizini akakifunga na kuachia kicheko

    "Hahaaahaaahaaa kazi imekwisha ulilotaka limefanikiwa mpz wako huyu humu ndani chochote utakachotaka atakufanyia utanuia katika chupa hii na kumfata kumwambia unachoitaji chupa hii isionwe na mtu yeyote na sharti hili ndilo utakaloshindwa"

    "Hapana dokta ntajitahidi!" Akaongea Selina huku alitetemeka tayari alisha mweka mpz wake " kiganjani mwake,"

    Ndilo jambo alilokuwa akilitaka mwanaume yule asiwe na kauli kwake amsikilize,baada ya kupewa chupa ile akaambiwa haya omba kitu hapa sasa

    "Tuesday Mme wangu nakuomba nikukute nyumbani"

    Sauti ile ikapaa na kufika katika maskio ya Tuesday Jaduu kule ndani ya gari alipo kuwa amelazwa ghafla akafungua macho na kushangaa kule alipokuwepo

    "Mnanipeleka wapi?!"

    Akauliza kwa sauti wale wasamaria Wema wakamwambia wanampeleka hospitalini baada ya kudondoka na kupoteza fahamu?!

    Kudondoka!?, Kadondokea wapi! Akajaribu kukumbuka bila mafanikio

    Akawaambia wazi yeye si mgonjwa na wamwachie tu aondoke,kwa kuwa wale jamaa waliridhika na hali yake kwa muda ule wakaona bora tu wa muachia,Jaduu akawaachia kiasi kidogo cha ela na kuliwasha gari lake kurejea nyumbani!

    Ila huyu alikuwa si Tuesday Jadu wa kawaida,....

    ***

    Simanzi ilitawala katika familia ile,mipango ya mazishi ikafanyika na mwili wa mama Abrah ukazikwa

    Baada ya siku chache Jaduu akamleta Selina pale nyumbani,ile nyumba alojengewa ikabaki ya kupangishia wapangaji!,

    Siku zikaenda mpaka hiyo siku ambayo piter mtoto mkubwa wa Selina alipofungua kabati lile wakati alipokuwa anatafuta ela

    Na ghafla akaikuta ile chupa wakati akiishangaa ikadondoka na kupasuka,damu zikazagaa ndani ya chumba kile,...

    Wakati Jaduu akiwa ofisini kwake ghafla alisikia maumivu makali ya kichwa na hapo hapo kichwa chake akakilaza katika meza

    Hakuwa na uhai tena!

    Tayari ilikuwa ni roho ilodhulumiwa,

    Mzimu, ulosafirishwa mpaka kuzimu,himaya ya kina Jb ( mzimu ulorejea) naye akapokelewa kwa mikono miwili.

    Akapewa nguvu na cheo kama mlinzi wa jemedari Zena bin Kureysh!

    Kazi aliyoimudu pindi alipokuwa akiishi huko,akaacha duniani mwanaye wa pekee Abrah akiteseka.

    ****

    Mapigo ya moyo yalimwenda mbio baada ya kupigiwa simu na kuambiwa mumewe amepelekwa hospitalini

    Sehemu ya kwanza kukimbilia ni nyumbani ambapo alistaajabu kuikuta chupa ile ikiwa chini na kumezagaa damu,hakika Selina alikuwa kuchanganyikiwa,akafungua safari mpaka kwa mganga mzizi mzizini

    "Haaaaaaa haaaaaaa aaah aaaah nilijua utavunja masharti si nilikwambia?!"

    "Nisamehe dokta ila naomba umrudishe mume wangu?!"

    "Aitowezekana mumeo kwa sasa ni mzimu ambao lazima urejee kulipiza kisasi"

    Selina akaanza kulia akipiga magoti asamehewe

    "Nilisita kufanya hii kazi,ntakufa Mimi sitoweza nilikwambia uachane na hayo mambo ukunisikiliza sitoweza kuutuliza huu mzimu ni kazi ngumu sana!"



    "Du tutajaribu ila sijui!, cha kufanya we nenda usiogope ukasimamie mipango yote ya mazishi,ila siku ya pili ambayo ni kesho kutwa urudi hapa ili tatu asb tuianze kazi kwani ndo siku atakayotaka kurudi duniani hili tujaribu kumzuia ikishindikana hapo basi tena akuna jinsi"

    Selina akatoka na kuelekea hospitalini kuuchukua mwili wa mumewe moyoni alionekana mwingi wa majonzi,alivaa simanzi kwa kila kiumbe amwonaye ilikuwa ni lazima amwonee huruma.

    Wakafanikiwa kuuzika ule mwili salama,na siku ya tatu kama alivyopewa maelekezo akarejea kwa mganga ambapo asb ya tatu wakatoa kafara ya damu ya kondoo kuutuliza mzimu yule

    Kweli alifanikiwa "upende kutoa sadaka ya damu Mara kwa Mara hiyo itasaidia sana" alishauri mganga Mzizi mzizini nalo pia Selina akalitwii akawa akichinja kondoo Mara kwa Mara nyama akizigawa kwa maskini, akaanza kulijenga jina lake,Mali zile zikaongezeka Mara dufu

    Akuacha kumnyanyasa Abrah mtoto halali wa Jaduu,kwa kuwa kuna baadhi ya Mali aliandikishwa Abrah kabla hata awajaanza uhusiano,hamu ya kuzimiliki zote ikamvaa,ndo akamfata rafiki yake Jimama na kumwambia juu ya jambo ilo,jimama akamshauri warudi kwa mganga kusudi amwangamize mtoto yule!

    Selina akakubali na kurejea kwa mzizi mzizini

    ***

    TUREJEE KIDOGO NYUMA

    (Kumbukumbu sehemu ya pili)

    "Mwalimu ni nini maana ya neno TOZANI?!"

    "TOZANI,?!"

    Mwalimu yule alishtuka macho a kayatoa pima ni wazi akutegemea swali kama lile

    Si mwalimu pekee aloshtuka,

    Hata na baadhi ya wanafunzi pia,wengi wao wakistaajabu jinsi mwalimu yule alivyoshtuka!..

    Na si katika darasa lile viumbe wale walishtuka hata baadhi ya viumbe visivyo onekana vingi vilishtuka na kusimama kusikiliza mwalimu angejibu nini!

    KATIKA FALME YA KUZIMU

    Na si duniani tu baada ya Abrah kutaja jina lile viumbe vingi vilitega maskio kusikia mwalimu angejibu nini

    Katika kitanda kilichozungukwa na dhahabu alilalia binti Mrembo

    Zena Kureysh alozungukwa na wasichana wazuri kama yeye wakimpepea

    Wote walikuwa na mabawa

    Hata binti yule pia alishtuka baada ya mtoto yule kutaja jina lile

    "Ooh shit Abrah unafanya nini?!"

    Akapiga kelele,ni wazi maisha ya kijana yule yalikuwa hatarini

    "Jaduuuuuuu"

    Akaita kwa nguvu

    Ghafla kijana mmoja akajitokeza

    Ni Jaduu baba yake na Abrah!

    "Naitaji ukamuwekee ulinzi mfalme wa badae wa himaya hii"

    Kijana yule akainamisha kichwa ishara ya kukubali....

    Akatoweka na kuelekea duniani

    Mwalimu akazidi kumkazia macho abrah

    "Ni..nan... Ka..kwa....mbili.a?!"

    Akauliza kwa kigugumizi

    Abrah akaachia tabasamu pana kumuondosha woga mwalimu yuke

    "Hapana ni Mimi mwenyewe nataka kujua"

    "OK nifate ofisini"

    Mwalimu akasema kwa mkato na kuachia miguno kwa wanafunzi

    Akuangaika nao akabeba vitabu vyake na kutoka abrah akimfata nyuma

    nyuma

    Kelele zikazuka darasani

    ***

    MSITU PANDE

    " huyu mtoto asakwe aletwe kwangu,haiwezek

    ani binadamu atushinde akili, yeye ndo anaimiliki tozani na malkia wenu kandhibitishia hili japo anamlinda na sijui tufanyeje!"

    "Lakini mbona Jana mkuu tulimkamata ukamuachia?!"

    "Hapana sikumuachia Bali alibadilika na kuwa Zena bin Kureysh"

    "Alibadilika?!"

    Viumbe vile vikauliza kwa mshangao

    "Mwalimu ni nini maana ya neno tozani?!"

    Ghafla w akashtushwa na sauti katika maskio yao,ni baada ya Abrah kumpachika swali mwalimu wake wakanyamaza kwa sekunde kadhaa kumsikiliza mwalimu wao angemjibu nini

    "Tozani ?!" Wakastaajabu baada ya kumuona mwalimu naye kashtuka.jibu kuwa yule mtoto anayo tozani alikupingika katika mioyo yao

    "Namuitaji haraka sana!"

    Zuberi akatoa amri, viumbe vile vikatoweka!

    ***

    SURA YA SITA

    Giza lilitawala na kuchukua nuru yote ya anga,hali ya hewa ilitulia upepo mdogo ukivuma,vindege na baadhi ya sauti za wanyama zikisikika kwa mbali, nje kidogo ya msitu ule

    Kwa mganga mzizi mzizini,usiku ulikuwa ndo muda wake wa kwenda kuchukua dawa au kutibu wagonjwa walohitaji kutibiwa muda huo

    Siku hiyo alikuwa na wafanyakazi wake wawili akiwaonesha aina za dawa,alikuwa katikati ya msitu ule,lakini nje ya msitu ule alionekana gari ikielekea kwa mganga ndani walikuwa wanawake wawili jimama na Selina

    Wakati mzizi akiendelea na kazi ghafla simu yake ikaita akatabasamu na kuipokea

    "Mambo vipi bibie mbona mnakuja usiku?!" Tayari alishang'amua juu ya ujio wao

    "Mchana kazi nyingine dokta" Selina akajitetea

    "Mmmh karibuni tena nlivyo na hamu na wewe!" Mzizi akachombeza kiutani japo alimaanisha,upande wa pili ukacheka

    "Mmmh wewe tena unizidi Mimi!" Selina akasema akiwa na tabasamu

    "Basi mamaa safari njema wacha na sisi tuje huku mdogo mdogo kukupokea"

    "Sawa mume wangu"

    Selina akakata simu,wote wakacheka,kwani wote walikuwa ni wapenzi wa kijana Yule mdogo mwenye miaka 23 lakini mwenye uwezo katika tiba na ata mapenzi pia...

    Basi baada ya kukata simu akazidi kukanyaga mafuta

    "Haya jamani dawa zinatosha tu naweza kuondoka sasa kuna wageni usiku huu" mzizi mzizini akatoa amri lakini ghafla upepo mkali ukavuma,upepo ulochota vumbi na kujenga kimbunga,

    Upepo wa ghafla,miti ikaanza kudondoshwa,ukawaacha vijana wale katika amaniko la mshangao,fedheeko ghafla hali ya hewa ikaanza kubadilika

    Wingu kuwa jekundu radi kupiga na ghafla mvua ukaanza kunyesha,mvua yenye upepo

    Upepo ukazidi mara dufu na ghafla kimbunga kile kikawafikia na kumchota mzizi mzizini wasaidizi wale wakawa wanashangaa jambo lile,

    Ajabu ingine baada ya mzizi kuchukuliwa na kimbunga kile,hali ya hewa ikarudi kama kawaida mvua na upepo ikawa ukisikika kwa mbali!

    "Ni nini kimemkuta dokta?"

    Wakajaribu kujiuliza pasina majibu,

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mzizi mzizini akabebwa na kimbunga kile alijaribu kupiga kelele lakini akukuwa na wakumsaidia!

    Ghafla akapigizwa chini,akaumia vibaya sana,hapa nipo wapi?! Akawaza mwenyewe akijaribu kuangalia mandhari ya eneo lile

    "Kwa nini waichezea taaluma yako vibaya?!"

    Akashtushwa na sauti kali ,...

    "Kwa nini uliamua kuniangamiza?!"

    Bado sauti ile ilizidi kumsimanga,bado akujua ni sauti ya kiumbe gani zaidi ya kuendelea kutetemeka!

    "Wewe ndo umeisambaratisha familia yangu,wewe ndo umemuua mke wangu na Mimi pia kwa namna hiyo sitokuacha mzima lazima ukateseke kuzimu wewe"

    Ghafla mtu yule alokuwa akiongea akajitokeza,mzizi akashtuka,alimjua fika alikuwa ni JADUUU,baba yake ABRAH, kwa Mara ya kwanza kijana yule akapiga magoti asamehewe

    "Utateseka katika moto wa kuzimu maisha yako yote mpaka MUNGU atakapoitwaa roho yako kwa heri"

    Baada ya kauli ile Jaduu akatoweka na kumuacha mzizi akiwa katika mshangao,alijar

    ibu kuomba mizimu yake lakini yote ilikuwa chini ya Jaduu Mkumbuke jadu alikuwa mlinzi wa Jemedari Zena Kureysh hivyo akukuwa na mwenye nguvu za kumsaidia

    Wakati akiendelea kuwaza ghafla likaibuka joka lililoitwa obishi nadhani wengi waloisoma jini HUSNAT mnamkumbuka kiumbe huyu ambaye alimmeza Vergan na kwenda kumtema kuzimu alipopokelewa na toxic viumbe vyenye mifupa mitupu

    Hivyo hivyo Kwa mzizi akuweza kumkwepa nyoka yule akambana na kummeza akaenda kumtemea kuzimu ambapo alibebwa na toxic waloenda kumtupa katika moto akiadhibiwa na mashetani wale wa kutisha

    ***

    Wakati wakiendelea kupiga stori ghafla kiumbe kikakatiza Mbele yake,Selina akashtuka...

    Ni kama alimfananisha na jaduu alokuwa mpz wake...

    "Mh watu wanafanana tu shost,!"

    "Yani walivyofanana nilipomuona moyo umepasuka paaaaa"

    "Si wewe tu hata Mimi pia nimeogopa sana"

    Basi wakaendelea na safari mpaka kwa mtaalamu yule,walipokutana na kizaazaa,mzizi kabebwa na kimbunga?!, mbona wameongea naye dakika chache tu ilikuwa ni vigumu kuamini

    Ila kwa kuwa ilikuwa ndo hali halisi ikabidi wakubaliane na khali ile,kwa kuwa ilikuwa ishafika usiku sana ikamlazimu kulala asb ndo waondoke,wasiwasi ulishaanza kuwashika.

    ***

    "Kwa nini umendanganya! Kuwa tunasoma darasa moja kumbe we muongo mi sikupendi baba alinambia nisimpende mtu muongo"

    Abrah alimwambia Zena walikuwa katikati ya msitu Pande, na ilikuwa ni usiku

    "Nisamehe mpz wangu Kwa kukudanganya"

    ",ni busu kwanza ndo nikusamehe"

    Zena akamuinamia na kumbusu

    "Nimekusamehe"

    Wakakumbatiana, "beby nikwambie kitu?!" Abrah akauliza kwa sauti ya upole

    "Nambie mpz!"

    "Eti tozani ni nin?!"

    "Mmmmmh" Zena akaguna kwake lilikuwa ni swali gumu alikuwa katika utawala wao Katika msitu ule ivyo alijua maongezi Yale yalisikiwa na viumbe zaidi ya yeye

    "Wengi walisubiri angejibu nini?!"

    Na kama angedanganya ni wazi angekuwa na la kujibu akakumbuka alivyoidanganya familia yake ambayo akuwa na shaka walisikia kila kitu alichokua akiongea

    AKAKUMBUKA...

    "baba na mama simpendi Zuberi tayari kuna mtu nlompenda binadamu!"

    "Staki kusikia upumbavu wako wewe una miaka 2000 umpende yule mwenye miaka kumi wapi na wapi,?!"

    "Aijalishi baba mapenzi ayaangali umri nimempenda Abrah naye ndo atakayenioa"

    "Kumbuka Silva kakusaliti utakuwa na binadamu wangap?!"

    "OK baba ntatoa mtihani ntatupa Pete atakayefanikiwa kuileta ndo mume wangu"

    Wote wakafurahia walijua hakuna binadamu mwenye nguvu kama za jini hivyo tozani ni lazima ingetua mkononi mwao tu

    Naye akaapa kuisaka amkabidhi abrah amvishe ili awe mmiliki wake

    Japo viumbe wengi walijua abrah anayo ndo maana penzi lao walifanya bila kuficho na ili aendelee kuwaweka Imani hiyo akazidi kumuongopea abrah

    "Tozani ni ile Pete uloiokota wakati ulipokuwa ukilima shimo la taka"

    Abrah alijaribu kukumbuka ila kabla ajauliza Zena akampachika swali

    "Kwa nini umeniuliza hivyo"

    "Kuna viumbe vinaitaka hata na mwalimu pia"

    "Basi usiwape"

    "Aku! Siwapi tozani yangu" wakati alipomaliza sentensi hiyo ghafla walizingirwa na majitu ya kutisha iloloa damu

    "Tupatie tozani yetu"

    Wakaongea kwa Shari!,

    "Atakaye mgusa huyu mtoto namwangamiza" Zena mwenye sura ya kitoto akaongea

    Yale majitu yakacheka,"wewe watutisha sisi siyo?!"

    Zena akawa angalia akirembua

    Jitu moja likaja mzima mzima kumwendea Zena, na kumpamia ila Zena alishagundua hilo mapema akajizungusha na kutoa miba,jamaa yule akaachia yowe na kudondoka chini....

    Wale wengine w akaachia yowe na kumvamia Zena,Zena akatoweka wakapamiana wenyewe kwa wenyewe na kuporomoka chini

    Walipokaa sawa Zena akwepo,zaidi ya ABRAH alikuwa alitetemeka,w akamwangalia kwa ghadhabu

    "Tunaihitaji tozani yetu,"

    Abrah akatingisha kichwa kukataa,ghafla akapata Kofi zito lililo myumbisha akaenda chini

    Ghafla akazinduka!!!

    Kumbe ilikuwa ndoto SELINA mama yake alikuwa pembeni akimwangalia kwa hasira yeye ndo alompiga kile kibao akashtuka

    "Watoto wangu walale mpaka saivi nawe ulale mpaka saivi,wikiendi hii yapaswa mtusaidie kazi,fagia osha vyombo fua nguo zako zangu na za wanangu , deki na mwisho kabisa uchukue jembe ukachimbe shimo la taka"

    Abrah akashtuka, akaduwaa,

    Akachimbe shimo la taka?!

    Akakumbuka "tozani ni ile Pete uloiokota wakati ulipokuwa ukilima shimo la taka"

    "Ghaaaaaa" akaguna

    Selina akamkata jicho Kali " naitaji uanze kazi sahivi"

    Abrah akujibu kitu akaanza kazi kudeki,watoto rika lake Piter na Samwel wakiwa wamelala

    ***

    Ni wakati alipopotea baada ya viumbe vitokavyo katika falme ya muzidu chini ya bahari kumuibukia,kama nilivyosema awali viumbe hivi vilijua tozani ni Mali ya ufalme wao

    Na si Mali ya Zena wala Muzidu mwenyewe,katu awakujua kuwa hata wangeipata wangempelekea Muzidu naye angemrejeshea Zena, naye Muzidu hakuwa tayari kuwaambia ukweli kwa kuofia kuonekana akukipata kiti kile cha ufalme kiaki,zaid ya kusaidiwa na mwanamke angejishushia heshima,ivyo hakuwa tayari kwa ilo.

    Ndo kisa cha kuwa kimya

    Zena aliibukia juu ya mlima na kuwaza

    "Hivi kwa nini huyu Muzidu anantumia watu wanidai tozani hali ya kuwa inapaswa anrejeshee na wapigane kabisa nami?!"

    Wazo hilo likapita katika kichwa chake

    "Muzidu kakugeuka! Sasa anajua wewe ndo unayo tozani ila unamsumbua tu aisake hali ya kuwa umemkabidhisha mpz wako Abrah"

    Akaskia sauti ikimnong'oneza,aliijua fika sauti ile,Zena akaachia kicheko

    "Mwanayuhani weee ulolaaniwa mwanaume ajifichi toka tupambane"

    Ghafla akaskia kicheko

    "Nina nguvu nyingi kuzidi jini yoyote katika ulimwengu huu namtumainia MUNGU akuna ashindwalo"

    "Acha mahubiri kama wewe wa kiume kweli tokaaaaaaaa"

    "Asalam aleykum warhamatullah taghala wabarakat"

    Ghafla Zena akasikia sauti nyuma yake akageuka

    Naaam alikuwa ni Bisau kavaa kanzu yake mubashara imenyokaaaaaa,kichwani anakofia,chini anakobasi mkononi kashika tasbih na msahafu wake mdogo

    Zena akuitikia salamu ile akanyoosha mkono upanga ukatua...

    Bisau akatabasamu!, akanyoosha mkono pembeni kidogo kiti kikatokea akauweka msahafu wake na tasbih yake,akaikunja kanzu yake kidogo naye akanyoosha mkono upanga ukatua mkononi kwake

    Akawa tayari kwa mpambano!



    Wakaangaliana kama majogoo yalotaka kupiga na ghafla Zena akaruka na kuuachia upanga wake kuelekea katika shingo ya BISAU lengo aicharange

    Tofauti na mategemeo yake akaachia yowe kwani ilitokea shoti kali kati ya shingo ya bisau na upanga ule ilikuwa kama shingo ile ni waya ulopitisha umeme usiozibwa na upanga ule ni maji aloyashika....

    Mkono ukawa mweusii,pale aliporushwa aliuachia ule upanga ukatua pembeni,bisau akaunyooshea mkono ghafla ukapotea

    "Nlishakwambia na nguvu zaidi ya jini yoyote ukunisikia nadhani umedhibitisha!,Zena sijaja kishari nimekuja kiamini embu tazama katika kiganja changu!"

    Zena akawaza macho kuitazama kiganja kile....akaona Yale yalokuwa yakiendelea MUZIDU

    "Mfalme Muzidu tumegundua Pete anayo huyu binti na kampa yule mtoto na anamlinda"

    "Asakwe huyo mwanamke na auwawe tozani irudiahwe katika utawala huu" muzidu akaongea kwa hisia....

    Ghafla Bisau akaukunja mkono wake

    "Mtu unaetaka kushirikiana naye kaagiza uwawe,je kwa nini uendelee kushirikiana nae?! Nadhani ujui kisa cha hii tozani na umesahau mfalme Jb alipowaambia ni kosa nilifanya ndio na inapaswa niukumiwe utakavyo lakini.....CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kabla ajamalizia kauli yake ghafla wakazingirwa , ni mijitu ile ya kutisha

    Pamoja na Muzidu mwenyewe Upanga wenye kuwaka waka ukiwa katika shingo ya Zena! " kumbe mnashirikiana Malaya wa kike wewe alafu wanlazimisha nikutafutie tozani Leo utanipa tozani Mali ya wana Muzidu tofauti na ivyo nakicharanga kichwa chako"

    Muzidu alikoroma watu wa nne walimuelekezea Muzidu upanga,upanga zile lilikuwa na uwezo kweli wa kumuondosha duniani

    "Nawe mzee mawazo yako nayasoma tutaenda kukuua adharani ukileta kujua hapa hapa tunamaliza kazi" bado Muzidu aliendelea kupiga biti

    "Utatoa tozani utoi?!"

    Akamgeukia Zena na kumuuliza swali

    "Tafadhali usimuuwe huyo kiumbe hana tozani mwenye tozani ni Mimi chukueni!,"

    Akanyoosha mkono na ghafla Pete ile ikatua katika mkono wake,ilikuwa ni ile ile tozani yenye kung'aa

    "Usijiguse rusha hapo chini"

    Bisau akatii na kuirusha,Muzidu akasogea na kuinama kabla ajaiokota ghafla Bisau akajizungusha na kuachia kombora,tayari alishampa ishara Zena naye akatoweka na aliporejea alikuwa na upanga wake,vita vikaanza

    Ni vita vilivyokuchua muda mrefu kwani Mara kadhaa ilimlazimu bisau kujigawanya na kutoka wengi ambapo walizidi kupambana na kwa kuwa Zena alikuwa ni jemedari mbinu zote za vita alizijua wakafanikiwa kuwafyeka walinzi wote walokuja na Muzidu akamwekea upanga Muzidu tayari kwa kumwangamiza!

    Akampa wasaa wa kuswali sala yake ya mwisho kisha akaunyanyua upanga ile anataka kuushusha ghafla kwa mbali ikasikika adhana!

    Bisau akaacha

    "Una bahati sana ningekuua ngurue uloaramishwa wewe potea" akafoka Bisau swala hilo la kumsamehe Muzidu lilimshangaza sana Zena!

    Muzidu pasina kuamini akatoweka

    "Ngoja niwahi katika ibada twaweza kuongozana sijui,?!"

    "Tangulia tu siku nyingine"

    Akatamka Zena akacheka

    "Kwa hiyo ntakukuta hapa,?!"

    ,"no saivi naenda duniani kwa mpz wangu ila ukitaka ibadani ntakuwa nishakuja"

    Bisau akujibu kitu akageuka na kuifata kanzu yake akaivaa na kuanza kuondoka pasina kugeuka nyuma

    Ghafla nyuma yake akstokea Muzidu mkononi kashika upanga kaunyoosha tayari kumwangamiza bisau

    Ila alishachelewa Zena akafyetuka na kuachia mshale wake,ukampata Muzidu mgongoni,Muzidu akatua chini akujitingisha tena

    Alikuwa tayari kashakata roho!

    Bisau akuamini

    Ghafla akatoweka alipokuja kutokea ni pembeni ya Zena akamkumbatia

    "Hakika siamini macho yangu kama umemuua ndilo nlilokuwa nataka" akaongea Bisau kwa furaha

    "Ulilokuwa unataka una maana gani ?!"

    "Swadakta tufanye ibada kwanza ndipo ntakuelezea"

    "Lakini Mimi simuabudu unayemuabudu" zena akasema

    "Umpendaye anamwabudu MUNGU mmoja,MUNGU anayesamehe MUNGU imara ,MUNGU alokuumba na kuwaumba hao wanaofanywa au kujiita mungu kwa nini usimuabudu"

    Zena akamfikiria Ibilisi na cheo alichonacho uko kama jemedari wa kuzimu

    "Mh! Lakini ayasemayo ni kweli kwa sababu mwisho wangu japo namuabudu LUSIFAR ni katika moto ule ana sifa ya kusamehe, ila huyu usamehe"

    Zena akatabasamu akikubali kumuacha cheo cha u jemedari

    Bisau akamsilimisha na kuwa muislsmu alokiri hapana Mola apaswaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa MUNGU mmoja na MUHAMMAD ni mtume wake

    Akamfundisha juu ya kushika udhu na wakaswali pamoja pale pale!

    Baada ya kumaliza ibada BISAU akaendelea

    "Naitaji kuurejesha mwili huu katika HIMAYA ya muzidu kuna vitu naenda kuzungumza kule ningependa twende wote

    " usijali mfalme wangu ila ningependa kufahamu ni kwa nini umefurah baada ya Mimi kumuua muzidu"

    "Hata ilo ni moja wapo ya utakaloenda kulifahamu"

    "Na vipi kuhusu tozani?!"

    Bisau akamkata jicho, zena akashtuka

    "Tozani ni ya wana himaya yangu itotoka nje ya hapo"

    Zena akakosa amani, ila kwa kuwa kuna kitu aliambiwa ataambiwa akatwiii kuongozana na bisau

    Wakatoweka

    ****

    Abrah baada ya kumaliza kazi zote akashika jembe na kuanza kuchimba shimo,lakini ghafla akashtuka

    Macho yakamtoka,ni baada ya kuiona Pete,

    Ilikuwa ni tozani ilowaka waka

    Akuamini kile akionacho....

    Akafikicha macho akijua pengine anaota kama kawaida ya ndoto zake za maajabu ajabu

    Ile aikuwa ndoto,akausogeza mkono kutaka kuichukua

    Lakini ghafla alitetemeshwa na kurushwa,tozani ilikuwa na nguvu zaidi yake....

    Daaaaah safari yangu insishia kikomo kesho jioni

    Zena ajakabidhiwa tozani akosa amani je ataridhika?!

    Wana MUZIDU na kundi lake la wachawi wataridhika au kuna kisas!

    Abrah aiona tozani ila imemrusha baada ya kumzidi nguvu na kumbuka HIMAYA ya Zuberi wanaisaka na wanajua huyu mtoto anayo





    Baada ya Abrah kurushwa mita kadhaa akajigonga katika ukuta,na damu kuanza kumchuruzika ila maumivu Yale akuyasikia,wala damu zile,akili na mawazo yake yalikuwa juu ya Pete ile ya tozani!

    Akajinyanyua na kulifata shimo lile akainama tena kuiokota,ghafla aikumtetemesha tena akabaki akiishangaa na kuivaa kidoleni

    Ilimkaa vyema,ghafla akasikia nyayo za mtu akiwa anakuja! Akawa akiitoa kwa nguvu

    Pete ikagoma,ghafla kizungu zungu kikali kikamvaa,akaporomoka chini ila hata pale chini akukaa ghafla kwa ajabu kabisa akatoweka!

    Pete ikiwa kidoleni mwake

    ***

    Selina alikaa avikukalika,ghafla simu yake ikaita alipoangalia alikuwa ni shoga ake jimama akaipokea...

    "Shoga kuna mganga huyo ni hatari anaitwa ndumbwendumbwele ni mbibi fanya hima tuonane!"

    Moyo wa Selina ukalipuka kwa furaha,akatoka nje kwa nia ya kwenda kuangalia Abrah kafikia wapi,ajiandae aondoke

    Ghafla akasikia kishindo nje akachanganya miguu na alipofika alistaajabu kumuona Abrah akitoweka

    Akafikicha macho pasina kuamini kile akionacho , ila ilo alikuubadilisha ukweli Abrah alikuwa ametoweka katika mazingira ya kutatanisha akaanza kuita kwa sauti kubwa Abrah Abrah hapakuwa na jibu sahii

    Alihisi yupo ndotoni ila ule ulikuwa ni ukweli Abrah alitoweka katika mazingira ya kutatanisha

    Akajiandaa tayari kwenda kwa shoga yake ili waende kwa mganga huyo

    ****

    CHINI YA MAJI

    HIMAYA YA BISAU

    Viumbe aina ya majini vilikuwa vimefurika,usoni vilikuwa na majonzi makuu,ni baada ya kupata taharifa juu kifo cha mkuu wao MUZIDU

    Katika kiti cha kifalme aliketi Bisau akiwa na tabasamu pana, moyoni alikuwa na furaha isiyo na kifani

    "Kwanza poleni kwa msiba,ulowapata kwangu ni furaha sana!

    Miguno ikazuka...hali ya mshangao ikatawala katika nyuso zao

    "Nadhani wengi amjuhi siri alokuwa nayo Muzidu mtawala wenu na Leo ntaweka bayana mabaya yake,Muzidu alikuwa mchawi anayetumia nguvu za kishetani kuwaongoza nyinyi Mimi niliichukua tozani ya mwanangu nikaitupa na kuagiza wote muisake ila Muzidu pasina kutumia nguvu zake

    Kwa kutumia nguvu za Giza akijua fika mwanangu ataipata akamuua

    Viumbe vyote vikaguna pasina kuamini kauli ile,Bisau akaunyoosha mkono wake na vita vile kati ya mwanaye na Muzidu vikaonekana bayana katika mkono wake

    Minong'ono ya chini kwa chini ikatawala,akatoa ishara ya kimya wote wakatii Bisau akaendelea....

    " sikutaka kumsaidia mwanangu kwa kuwa niliujua ujemedari wake na himaya hii yapaswa iongozwe na jemedari hivyo niliona mwanangu akiuwawa na nkaridhia kumtawaza Muzidu kuwa mfalme wa himaya hii

    Ila Muzidu alinigeuka na kuitaji tozani ambayo ilikuwa ni Mali ya mwanangu mnajua kwanini?!....

    Wote walikaa kimya umakini ukiongezeka,bisau akaendelea

    "Alofanikiwa kuipata tozani si Muzidu...

    Miguno ikafatia,ni wazi watu awakujua Bisau alikuwa na maana gani

    "Tozani niliitupa katika himaya ya kuzimu na alofanikiwa kuipata ni binti aitwaye ZENA KUREYSH ambaye ndo huyu hapa mumuonaye

    Ambapo dakika chache Muzidu alimuibukia na vita vikatokea binti bado alimshinda muzidu

    Bisau akaunyoosha tena mkono wake,na kuonyesha jinsi ilivyokuwa mpaka kuibuka kwa Lucifa na kumwagiza ampe tu ila angeirejesha kwa zena baada ya kuapishwa

    Nami baada ya kujua ilo nikakataa kuitoa tozani , ndo akaanza kunisaka wakisaidiana na wachawi wake pamoja na huyu binti....

    Badae alikuja kumgeuka huyu binti kwa kuwa huyu Zena alimwahidi mpz wake kumvisha tozani ikiwa angerejeshewa wakajua kuwa binti anayo hivyo vita vingine vikaibuka na zena akamuua Muzidu

    Kwa maana hiyo napenda kumtangaza Zena Kureysh kukaimu nafasi ya MUZIDU kama malkia

    Hakika Zena akuamini kile akisikiacho

    Yeye awe malkia?!

    Hapana alihisi ni ndoto na muda wowote angezinduka

    Je mfalme ni nani?!CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Likabaki swali ambalo katu akulijua jibu lake,si yeye tu hata kwa wana majini wale

    Muda wote bisau alikuwa katabasamu, "na ni muda wa kumtambua sasa mfalme wenu"

    Ghafla radi likapiga na Abrah akatokea katika kiti kile cha kifalme,kichwani alivaa kofia ya kifalme, kidoleni Pete ya Tozani

    Usoni alikuwa na tabasamu pana

    Watu wote wakashangilia,....

    "Ana nguvu zaidi ya kiumbe chochote kutokana na tozani alivaa , ila malkia wake ana nguvu zaidi.....

    Malkia itapaswa umwongezee mumeo nguvu uwe chini yake...."

    Zena hakuwa Mbishi akamuongezea mume wake yule nguvu kama ilivyoitajika,

    Sherehe sambamba na harusi kubwa ikafatia

    Wakaishi raha mustarehe.



    MWISHO



0 comments:

Post a Comment

Blog