Search This Blog

MERISA JINI MWITU - 1

 







    IMEANDIKWA NA : ZAYNABTALY



    *********************************************************************************



    Simulizi : Merisa Jini Mwitu

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      Ulikuwa usiku wa furaha,faraja,amani na ndelemo kwa wapenda nao wawili  Gabriel na Irene .Ambao walipenda siku ya leo waitangazie dunia kuwa baada ya muda mfupi watakuwa mke na mume,yote aliyafanya kijana geb baada ya kusubiri na kuangaika kwa muda mrefu akimtafuta mpenzi wake anna ambaye ndio msichana aliyekuwa chaguo sahihi la moyo wake kwa wakati ule.Ila leo aliamua kumsahau kabisa anna na kuamua kumuoa Irene.shamrashamra za maandalizi ya mwisho juu ya shughuri ile ya utambulisho zilizidi kupamba moto  hatimaye wageni waalikwa kuwasili wakiwemo ndugu jamàa na marafiki wa Irene na Geb.kwa upande wa Geb alikuwa akimsubiri kwa hamu kubwa mgeni wake rasmi aliyemualika katika hafla ile fupi ili aweze kutumbuiza jukwaani katika sherehe ile,



    Nusu saa ilikatika wageni wote walikuwa wamekwisha wasili katika shughuri ile isipokuwa mgeni ambaye Geb alimsubiri kwa hamu iliaweze kufungua hafla ile kwa kutumbuiza kwa mashairi yake mazuri ambayo yaliweza kupambwa zaidi na kwa uzuri kupitia sauti nyororo ya mwanadada huyo na kumfanya kila msikilizaji wa mashairi yake kupatwa na hisia za kweli juu ya maneno yatolewayo.Wakati bado Geb  anatafakali nikitu gani chaweza kuwa kimempata rafiki yake kipenzi ambaye kwake alikuwa kama mgeni rasmi katika hafla ile mara mlango ulifunguliwa na kuwa wazi kabisay hakuonekana mtu kuingia punde mpaka zilipo pita sekunde kadhaa,alikuwa msichana mrembo aliyevalia gauni jekundu lililo buruza mpaka chini na viatu virefu alivyovaa ndio vilikuwa msaada tosha wa kupunguza urefu wa gauni lile aliziweka nywele zake vizuri kwa kuzishikilia barabara katika kichwa chake nakuwa mfano wa kofia uso wake ulipangiliwa vyema  make up zake nakumfanya azidi kuvutia zaidi mbali na uzuri aliokuwa amejaaliwa na mungu ama kwa hakika alipendeza sana siku hiyo aliweza mzidi hata Irene ambaye ndie alikuwa muhusika mkuu juu ya sherehe hiyo.



    Haikuwa rahisi kumtambua msichana yule kwa haraka japo wengi walizoea kumuona kwenye runinga na katika macasino mbalimbali akitumbuiza ila kwa siku hii ili iliwawia vibaya. Ukumbi ulikuwa kimya kumtazama malikia yule akipita katikati yao hakuna aliyethubutu kusema chochote wote walikaa kimya na kumtazama ni wapi anaenda kuketi. Wakati huo geb alikuwa katika chumba ambacho alikuwemo mtarajiwa wake irene wakishauriana ni nn wafanye maana muda ulikuwa tayari ushapita karibuni dakika 45 lakini matumaini hayakuwepo.Ghafra Geb alishitushwa na ukimya uliokuwepo ndani ya ukumbi kutoka akakutana ana kwa ana na Angle aliyekuwa akionekana kujawa  na huzuni kubwa ndani ya macho yake ijapokuwa uso wake aliupamba vyema na tabasamu bandia kiasi kama aujamzoea  atajua ni kawaida yake kuwa vile alivyo,jambo hilo kwa geb  halikufichika aliweza kugundua  huzuni aliyokuwa nayo Angle  kwa kumtazama macho yake ambayo yalijitengeneza vyema machozi yaliyokaribia kutaka kufunika mboni za macho yake  na kuangukia mashavuni ghafra akayawahi na kitambaa chke cha mkononi na kusogea pembeni kidogo ya ukumbi ,Geb akuweza kukubali  kumuona Angle akilia peke ake bila ya yeye  kuhisi ni maumivu kiasi gani aliweza kuyapata rafiki yake yule,yapata  mwaka na nusu sasa tangu  geb kujuana na  angle.

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Katika moja ya sehemu ambazo Geb alipenda kwenda kujipumzisha na kwaajili ya kutuliza akili mara tuuu baada ya kutoka kayika mihangaiko yake ,Ila  haikuwahi kutokea kwa wawili hawa kuongelea kuhusu maisha yao kuwa ni wapi  wametoka na wapi wanaenda ilikila mmoja aweze kumjua vizuri mwenzake ila kwa upande wao hakukuwa na  umuhmu wowote na kujipq imani watazoeana na kujuana zaidi kadri siku zinavyozidi kwenda .Siku moja angle alipewa mualiko wakutumbuiza katika moja ya casino kubwa mjini arusha,Ndipo ambapo Geb aliweza kushuhudia uhodari wanmwanadada yule akiwa jukwaani akiimba na kucheza yeye pia alikuwa ni miongoni wa mashabiki wazuri wa mwanadada angle siku hii alipata kumuoona  libe alipenda kujenga ukaribu naye kama rafiki bila kujua alikuwa akitonesa kidonda cha angle ambacho kwa mbali kilianza kukauka na muziki kuwa ndio sehemu ya maisha yake na kuwani rafiki mkubwa kwake ambaye aliweza muondolea mawazo yote na kiasi akawa mwenye kufungua kurasa mpya ya maisha yake,alijisemea moyoni huku bado akimtazama Geb machoni ambaye bado alikuwa akisubiri kwa hamu kujua tatizo alilokuwa nalo angle



    "Merisa! Merisa, jini mwitu wewe ndie chanzo cha haya yote wew ndio chanzo cha chozi langu leo hii kuanguka merisa wewe ndio chanzo cha mimi kuhisi maumivu ya mapenzi wewe ndo chanzo cha misukosuko yote ya maisha yangu merisa.

     Aaaaaaaaah,,,,,,,,,,sijuihata niwapi nitaaanzia kumueleza geb na kumfanya anielewe kuwa mimi ndie yule anna wake aliyeniahidi mambo mengi lakini haya kutimia baada shetani mwitu kuingilia pendo  letu".





      alishtushwa toka katika mawazo yale baada ya geb kumuuliza " angle una nn?" hakuwa mwenyekujibu alijifuta tena machozi na kuinuka na kumtazama Geb "nipo sawa Geb! Shaka dhidi yangu ondoa "     huku akielekea kwenye jukwaa na kushika vizuri kipaza sauti na kuomba kusindikizwa na gita ambalo lilipigwa kwaahadhi ya kubembeleza na kuanza kukiweka kipaza sauti mdomoni na kuimba. Siku hii hakuimba nyimbo yake ila alichagua nyimbo ya msanii wa kitambo kidogo na kuiimba mbele ya hadhira ile ilikuwa nyimbo ya marlaw  iliyoenda kwa jina la daima na milele " pendo languuuu,,,,,,  halina mwishooooo,,,,wewe ndio wangu leo mpaka keshooooo,,,,sogeaaaa nikumbatieeeeee,kwani najuaaaaa uamini uko na mieeee,,,usilie ufurahieeeee mimi sikuachi kamweeeee Eeeeeeh eeeeheeeee utakapo sinziaaaaa na kitanda moyoniiii ili ukilala tuwe wote ndotoniiiiii,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,daima na milele nitakuwa nawe maisha yangu yote eeeeeh ooooooh,,,,,,,,,       wimbo ule ulimkumbusha zamani sana Geb kiasi chozi kumtoka  ilikuwa ni nyimbo ambayo aliwahi kuisikia kitambo sana akatega sikio vizuri na kusikiliza sauti ile nyororo ili fanana kabisa na ya anna alitamani kumuita anna ila alijistukia na kujisemea mwenyewe..



    " yule sio anna,geb ni sauti tuuu zimefanana"ila bado akili ilikuwa mbali alikumbuka siku ambayo alikuwa beach na anna wakicheza cheza kwenye maji anna aliimba nyimbo hiyo kwa hisia kali mpaka kutoa chozi akikimaanisha alichokuwa akikiimba kushtuka mbele yake alikuwa amesimama msichana angle ambaye tayari alikuwa ameshamaliza kutumbuiza mkononi alishika kitu mfano wa bahasha iliyokuwa na CD ndani yake na kumkabidhi Geb kisha akamwambia ni zawadi yako siku ya leo ikiwa juu imeandikwa maneno machache yaliyopelekea kumshawishi Geb kujua kilichopo ndani ya ile CD iliyoandikwa kwa herufi kubwa na kwa muandiko uliosomeka vizur maneno yake yalisomeka kama



    " MASIKINI ANNA MIMI" Baada ya angle kuhakikisha ameshamkabidhi Geb CD ile  alirudi nyuma  kabisa ya ukumbi akimuangalia Geb aliyepanda jukwaaani karibu kabisa na DJ aliyekuwa akitoa burudani siku ile  ndani ya ukumbi ulena kumuomba aweke ile CD iliawezevkuona kilichopo ndani ya CD ile .punde  ty screen kubwa iliyokuwa katika ukumbi ule iliwaka na kuanza kuonyesha chenga chenga haikutimia dakika alionekana msichna mrembo aliyeonekana katika majonzi makubwa machozi yakitililika katika mashavu yake alioneshakujutia jambo ila hakuna  aliyeweza kutambua alikuwa anajutia nini au alikuwa akiuzunishwa na jambo gani,akiwa  bado ameinamisha kichwa chake alianza kuongea kwa kusema 



    "samahani Geb kwa kuyasema haya leo,pia samahani sana Irene uwenda nikawa chachu na chamzo cha kuondoa furaha yako ,ila hilo sio kusudio langu ila mimi nilikuwa na hitaji Geb atambue tu kuwa masikini anna mimi nipo haijapo ni ngumu kuamini juu ya yale nitakayo yasema ila potelea mbali ,,,,," alikaakimya kwa muda kisha akainua kichwa hakuna aliyeweza kuamini kama msichana aliyekuwa akizungumza kuwa yeye na nna alikuwa ni angle ,



    Geb alishindwa kuelewa kulikoni ila ghafra ikasikika sauti kutoka kwa mwanadada yule ikiendelea kusema



    "najua lazima mtajiuliza sana yawaje angle mimi kuwa anna wa geb ila ni hivi, ,,,," alitazama juu kabla ajasema chochote akiwa kama anatafakari wapi anaweza kuanza .kila aliyesimama alitafuta pahali akaketi na kwa wale walio kawa mbali wslisogea karibu na kusikiliza kwa makini hata irene alitoka nje baada ya kusikia jina lake likitajwa Geb jasho lilikuwa likimtoka kiasi akavua koti la suti alilovaa na kuliweka pembeni na kufungua vifungo kadhaa vya shati lake na kujiweka sawa.mzungu mazaji alikuwa kama aliyepangilia muda na kuju hapa watakuwa wakijiandaa na baada ya dakika kadhaa watakuwa wamemaliza na  mimi nitaanza kuongea



    "miaka saba iliyopita nilikuwa nikiishi ja wazazi wangu wawili nikiwa kma mtoto wapekee katika familia yetu.si baba wala mama wote walikuwa wakinitegemea mimi kama mtoto wao wapekee ,siku moja asubuhi na mapema  nikiwa bado nimelala ,ghafra simu yangu iliita niliinuka kwa uchovu na kwenda kuipokea nilipo tazama katka kioo cha simi yangu ilikuwa namba ngeni kabisa katika macho yang n wala haikuwa ya tanzania uvivu ukazidi mara mbili nikaiweka kiganjani na kuipokea kisha sikioni ,upande wa pili wa ile simu aliwahi kuongea kabla yangu hiyo ni baada ya kujua kuwa tayari  simu ilikuwa sikioni  kwa muhusika sauti ilisikika " hallow?" nami niliitikia kwa kusua sua maana nilikuwa kmamwenyekuifananisha sauti ile na mtu fulani ila bado nilikuwa sijajua ni nani ,nikajivuta katika ile sauti iliyolewa usingizi



    "hallow!"



    "Geb hpa naongea " alijitambulisha yule aliyepiga simu



    " waow! Geb mpenzi umerudi???" nilipngea kwa shauku kubwa na furaha nikiwa nataka kujua kama amerudi au laa huku nikikaa vizur kitandani kusikiliza majibu yake



    " mmmh! Jaman hata salamu?" aliongea ilikunishusha papara nilizokuwa nazo pamoja na shauku nikashusha pumzi akaendelea



    " bado nipo GUENE mpenzi ila tumesha maliza kazi zote na tumesha dhuri misitu mitatu huku na nina taraji keshoasubuhi nirejeshe funguo za chumba na kuchukua baaadhi ya taharifa za ziara yetu huku kisha jioni nitaanza safari ya kurejea TANZANIA sawa mpenzi?" aliongea huku akionyesha unyenyekevu mkubwa sana kwangu kiasi nikawa muelewa kwa kila alichokisema " sawa Geb mpenzi karibu nyumbani"



    " asante mama nimeshakaribia mpenzi ila niaomba uje unipokee kesho kutwa asubuhi maana naweza ingia mida ya saa nne asubuhi hivi"      



    " usijali rubani wangu nitakuwa hapo pindi muda utakapo wadia". "



    "aminia mama ake ila hiyo siku iabidi uwahi mapemaaa kuamka ikibidi saa kumi alfajir maana nakujua ukianza kukaa kwenye kioo au malizi" aliongea geb kwa mzaha nami niliifatisha kwa masihara makubwa zaidi



    " mmmmh mpnz tangu lini mtoto wa mzee magesa mimi?"kwa nilikanusha  amakwa hakika alinielewa



    " basi kipenzi chngu yaishe utaniwiii?" naye pia alifanya kma nilivyofanya huku akinibembeleza na kunitupia swali,utani wanamna hiyo uliendelea mpka mapale niliposikia mlango wa chumbani kwangu ukigongwa ndipo nilipo muaga geb na kumruhusu aliyekuwa akigonga mlango wangu kuingia mlango uligiunguliwa aliingia mwanamke mzuri akiwa na umbo kubwa la kiutu uzima likionyesha tayari alikwisha zaauso wake ulipambwa vyema na rangi yake ya kahawia wengi waliita chocolate ,macho yake makubwa na pua nyembamba ya kuchongoka kama wahindi na mdomo wake mdogo viliongezea uzuri wa mama huyo mwenye adili yaki nyarwanda hakuwa mwingne ni mama yangu kipnz mama anna akiwa mkononi akishika tray ya kubebea chakula na ju yake kukiwa na chupa ya chai pamoja na kijisahani kifogo mbacho ndani yake kulikuwa na viji pande viwili vya mikate mapoka n  mayai ya kuchemsha maeili n kikombe kimoj bila shaka ilikuwani kwa ajili yangu ,nilianza kwa kumsalimia CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    " shikamoo mama?".   

    " marahaba ujambo mwanangu?".  

    " sijambo" huku nikijiweka sawa kiuvivu uvivu         

    " mmh ! Mwanangu mm mvivu jamn" alijisemea mwenyew mama angu huku akiweka vitu alivyokuja navyo chini na kujiweka sawa katika kitanda changu na kugungua chupa iliamimine chai kwwnye kikombe kidha akaendelea



    " hivi unajua saa ngapi saizi mama au unajilaza tun leo auendi chuo au?" kipindi hicho ilikuwa nfo kwanza nimeingia mwaka watatu sheria chuo na uvivu ndo ulikuwa umekithiri sasa nilimtazama mama yangu



    ",naenda mama" huku nikimuangalia kwa jicho la kudeka

    " sasa mboma mpka sasa upo kitandani?"aliongea huku akinipatia kikombe cha chai rohoni nilimtazama kwa makini mama angu na kutamani kuongea kitu ila nilijiona niatuwa nakosea sana kumwambia mama angu jambo lile tena kwa wakati ule ila sikuwa n jinsi maana geb alitaka kuja nyumbani kujitambulisha mara moja baada ya kutoka safari yake ni kajikuta nikianza kujiweka sawa



    ",mama" kwa sauti ya chini nilimuita mama angu naye akawa tayari kunisikiliza nini natka kuongea alinigeukia na kunitazama usoni " kuna jambo nataka kukueleza mama angu".                                 



    niliongea nikimaanisha ilikumfanya mama angu aweze kuwa makini zaidi kunisikiliza nilikohoa kidogo ilikuitengeneza sauti ile  iliyochanganyika na ile chai ya moto na kuendelea



    " mama najua mimi ni mtoto wenu wapekee na kwa hivi punde na tarajia kuhitimu elimu yangu ya juu kwa mwaka wa tatu ila kubwa nililotaka kukueleza leo hii mama nikuwa nime bahatika kumpata  mwenzangu"nilisita kidogo baada ya kumuona mama angu ananitazama kiumakini zaidi baada ya kusikia nimepata mwenzangu ila haukua mwisho wangu wa maongezi yale nilijikaza na kujiweka vizuri na kumalizia nilichokusudia" hivyo nilikuwa naomba ridhaa yenu iliniweze kumleta hapa nyumbani na kupata baraka zenu" hapo nilimuona mama angu akionyesha tabasamu sasa kiasi nikafarijika ila alionekana mwenyekutaka kuhoji kitu ikawa kama macho na hisia zangu zilivyo semana kuona



    "sawa mimi nimekuelewa muhimu umjue vyema mwenzio ilimsije kutupashida baadae ila hayo niyangu mimi ila nitaonge na baba yako bila shakaawezi weka kipingamizi na nilini unatarajia kumleta hapa nyumbani?" niliiyona shauku ya wazi ndani ya macho ya mama angu juu ya kutka kumuona na kumjua mkwe wake



    "kwa sasa yupo nje kikazi na ndo kesho anatarajia kurudi hivyo akirudi nadhani ndipo atakapo niambia kuwa ni lini anaweza kuja maana hata yeye sio mkaaji sana tanzania hivyo anataka jambo hili lifanyike upesi pale akipata tu nafasi." nilimjibu kwa kujiamini sasa baada ya kupewa jibu lililoniridhisha



    "anaitwa nani?" mama alihoji ilikutaka kujua anaitwa nani



    "GABRIEL MSIGWA" nilimtajia kwa kifupi jina la geb kamili bila kuongeza neno lolote ndani yake



    "na anafanya kazi gani?" baada ya kuridhishwa na jibu  nililo mpatia alihoji tena kuhusu kazi anayofanya geb



    "mmmmmmh mama Geb ni mwandishi wa habari kwa professional yake ila baada ya kufanya vizuri na kuchukua tuzo kadhaa za mwandishi bora Tanzania kwa kuandika habari za kweli na zenye uhakika alichukuliwa na   WORLD EVENT COMPANY  LTD kwa ajili ya kuandika maajabu mbali mbali yanayotokea katika ulimwengu huu na kumfanya kuwa ni mtu wa kuto tulia sehemu moja na kusafiri mara kwa mara" jibu nililoweza mpatia mama nilimtosheleza vyema na sikuona swali lingine tena lolote katika  macho yake. aliinuka na kuanza kuondoka alipoukaribia mlango aligeuka akatabasamu tena na kuniambia



    "nitahakikisha baba akoanakuwa muelewa juu ya jambo hili"na minilitabasamu kisha nikamjibu kwa unyenyekevu"nitashukuru mama angu" mama aliondoka na kuelekea chumbani kwake nami niliinuka kitandani na kwenda bafuni nikajimwagia maji kisha nikachukuanguo zangu sikusahau make up nilipo hakikishanipo sawa nilitoka zangu kisha nikamuaga mama na kuelekeachuoni siku hii nilijawa na furaha kupita kiasi ,furaha ambayo ilijificha zaidi ndani ya nafsi yangu kwa kuamini kuwa kwakuwa mama yangu amekuwa ,muelewa juu ya jambo hili hakukuwa na dalili yoyote ya baba angu kulipinga jambo hilo.



    *********************************************************

    Ilitimu saa tano kamili asubuhi nilipowasili chuoni kila mtualikuwa busy amejiinamia akijaribu kupitisha macho katika kurasa za daftari lake iliaweze kuambulia chochote ambacho kitaweza kumsaidia siku ya mtihani.Kwaupande wangu haikuwa hivyo maana nilionekana ni mwenyefuraha kupita kiasi kila aliyenitazama alipata shauku ya kutaka kujua nikipikilicho kuwa kikinipa furaha zaidi,siku weza kuwaeleza chochote maanahawakuwa wakifahamu chochote juu ya uhusiano wangu mimi na Geb .



    wengi walijua Geb alikuwa ni rafiki yangu tuuu,kitendo kilichopelekea wasichana wengi kuanza kujigonga gonga kwa geb wakimtaka kimapenzi ,wengi walishapagawa na uzuri wasura aliyokawa amejaaliwa Geb, muondoko wa geb pia uliteka hisia za wengi ambao aliuiba kutoka kaatika nchi mbali mbali alimokuwaakisafiri kwa ajili  ya shughuri zake za kiofisi ,mpaka ikafikia hatua  ya wasichana kuja kwangu na uihitajia namba ya geb mwisho kuambulia patupu bila kujua uharisia juu ya mimi na geb maana alikuwa akija chuo mara kwa mara na kunichukua na gari yakekisha kunipeleka mpaka nyumbani.



    Niliketi na kuitafuta simu yangu  na kutafuta namba ya rafiki yangu kipenzi Betha na kupigia ilikujua yuko wapi na kama ataweza kuja pale nilipo baada ya kama dakika kumi Betha alikuwa ameshafika pale nilipomuelekeza kuwa nipo naye alionekana kushangazwa na furaha yangu na kuanza kuhoji kulikoni .Huyu ndiye wapekee aliyekuwa akijua juu ya mahusiano yangu mimi na Geb hivyo siku mficha kitu nilimueleza kila kitu tangu kupigiwa simu na geb na kumfikishia tahariafa zile mama na jinsi alivyozipokea ni dhahiri wazazi wanguwalikuwa na moyo wa kumpokea Geb  na walikuwa radhi kwa kila kitu japo bado baba alikuwa ajanipa jibu la uhakika ila nilijipa moyo kwa kuwa mama akuweka kipingamizi ni dhahiri baba ange elewa kwa wepesi zaidi nakujikuta anakubali mimi kuolea.Tuliongea mengi mwisho tukaenda darasani na muda ulipoisha tuliweza kuondoka pamoja na betha na kuelekea kunako kituo cha daladala na tukiwa njiani tuliongea mengi na tamti tukafikia juu ya kesho yake kwenda kumpokea Geb ambapo Betha pia alitamani  kwenda mpokea Geb Airport na kwa upande wangu hakukuwa na tabu  nilimkubalia na kesho yake tulipanga kuonana nyumbani na kuongozana moja kwa moja mpaka Airport.



    *****************************************************************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Geb alikuwa akijiandaa vyema na wenzie wanne janeth,john,dev na mary ilikurejea Tanzania kwa ajilia yakukabidhi report na kuendelea na mapumziko mpaka pale itakapo patikana safari nyingne. Kwa upande wa Geb aliamini huo ndo ungekuwa muda mzuri sana wa kuweka mambo yake sawa na aliamini kama akipatasafari nyingne akirudi tayari mipango ya harusi itakuwa imefana maana alimtamani sana anna kwa kuishi naye na kuwa kana mkewe.



        Asubuhi na mapema tayari walikuwa wameshawasili katika uwanja wa ndege wa    GUENE INTERNATIOAL AIRPORT kwa ajili ya safri yao ya kurejea Tanzania na sasa furaha ya geb haikusita kujidhihirisha maana alitamani sana kwenda kwa kina anna na kujitambulisha na kuelezea nia aliyokuwanayo iliwaweze kupata baraka kutoka kwa wazazi wa anna kwa upande wake yeye wala hakuwa tatizo maana alijikuta mjini akiwa peke yake na kuishi huku akimtegemea anna kwa kuwandio mtu wake wapekee aliye karibu naye na kumfanya kuwa na furaha tangupalewalipo fariki dunia wazazi wake Geb kwa ajali ya treni walipokuwa wakitoka dar wakielekea  kigoma ,ilifahamika baadae kuwa katika mabehewa yaliyoripuka moja wapo walikuwamo wazazi wake geb na hatawalipojaribu kutafuta miili yao ilishindikana na mwisho kujikuta wakiamini kuwa ni kweli Baba na Mama yake walikuwa wamepotezamaisha.



         *************************************************************



    Hatimaye siku zilipita na ukawa umebakia usiku mmoja tuu na asubuhi yake nitakuwa Airport nikimsubiri kwa hamu kipenzi changu Geb.Ghafra nilishituka nikisikia naitwa ilikuwa sauti ya baba angu MZEE MAGESA niliitika na kutoka nikiifatiza sauti ile bila kujua wapiilitokea.Nikweli alikuwani baba angu mzazi MZEE MAGESA alikuwa ameketi na mkewe wote walinitazama nilikuwa kama niliyefahamu nilichoitiwa nikashindwa kuwatazama usoni hii ni kwa mara ya kwanza tangu nizaliwe kuwaonea aibu wazazi wangu niliitika ilikuwa juza kuwa niko tayari kusikia juu ya kile walichoniitia



    "abee baba" ilikuwa ni sauti ya unyenyekevu kabisa iliyojawa na hofu ndani yake babaalinitazama na kuniruhusu niketi,kisha akanitazama kwa muda na kukohoa ilikuweza sauti yake sawa iliaweze kusikika vyema bila makwaruzo



    "Anna mama?"



    "abee!baba"niliitika tena katika hali ile ile kama ya mwanzo



    "Nimepata taharifa zako kwamba umepata mchumba ni kweli?"aliongea huku akinitazama usoni ,hofu na uwoga ulizidi ndani ya nafsi yangu nilimuona baba angu kama nimwenye hasira na ambaye hakupendezwa na jambo lile,ila kwa upande mwingne wa shilingi nilimuona akiwa na moyo wakuyalidhia maombi yangu japo na hofu niliyokawanayo sikutaka kuzunguka sana japo majibu yangu yalidhihirisha uoga nilio kawa nao ndani ya nafsi yangu



    "ndi,,,ndi,,,,ndio baba" alinitazama nikaliona tabasamu likijitengeneza katika mashavu yake matumaini nilianza kuyaona ,alipohakikisha matumaini ndani ya nafsi yangu yatakuwa tayari yamekwisha jengwa aliendelea" unajua anna wewe ni mtu mzima sasa yabidi kutambua lililo baya na zuri ila sio hilo tuu pia umeshamaliza masomo yako nasi jukumu letu tumemaliza hivyo atuwezi pinga chochote uamuacho tangu sasa kwakuwa huyo mwanaume umempenda basi si mimi wala mama yako wote hatuna kipingamizi na tunawatakia kheri na baraka tele ndani yenu ila umrete tumuone kwanza hapa nyumbani.



    " Ilikuwa nifuraha ya ajabu ndani ya nafsi yangu sikuweza kuamini kama kweli baba ange nikubalia ombi langu.Niliwashukuru na kuwakumbatia kisha nikarejea chumbani kwangu,nikashika laptop yangu na kumtumia Email Geb kuhusu yote yaliyotokea nyumbani kisha nikajitupa kitandani nilikuwa katika dimbwi kubwa la mawazo na furaha ndani yake niliona dhahiri matarajio yanazidi kuongezeka na nika elewa wazi Geb ndio mwanaume wa maisha yangu sikuwahi kuwaza kutotimia kwa ndoto zangu hata siku moja japo mara kwa mara huwa niwatu wa kugombana ila yote hayo utengenezwa na wivu uliopo ndani ya nafsi zetu,Ghafra usingizi ukanichukua  mwisho siku ikapinduka na kuwa  siku nyingne wakati bado nimelala nilisikia simu yangu ikinguruma nikafungua macho nikaona simu yangu ikitoa mwanga nilihakikisha ilikuwa ni massage maana ilitoa mngurumo mmoja tuu, nikaishika na kufungua ujumbe ule huku nikiwana shauku ya kutka kujua ujumbe ule ulikuwa umetokea wapi na kwanani hakuwa mwingne ni geb



    "hallooow,,,,? my love bila shaka bado umelala ila pindi utakapo soma ujumbe huu nakuomba uamke na kujiandaa na uje Airport kunipokea maana mida ya saa nne hivi na dakika kadhaa nitakuwa nimeshafika TANZANIA" sasa furaha yangu ilizidi kifani ikabidi nifanye kama alivyosema na kabla ya kufanya chochote nilimtaarifu kipenzi changu Betha ilinayeye aweze kujiandaa, Nami nikaingia bafuni kuoga kisha nikavaa na kumuaga mama nilikutana na Betha kituo cha kupanda daladala ila kwa siku ile siku jisikia kabisa kupanda daladala nilichukua Tax na kuondoka mpaka Airport.

    ...................*************......................





                   

    Yapata saa tatu na dakika 45 Geb alikwisha wasili Tanzania sasa aliangaika na mabegi yake akiyatoa nje ya Airport ghafra alihisi mtu akimsukuma kwa nguvu nyuma ya mgongo wake na kumdaka kisha alipeta kwa mbele hakuwa mwingne ni Anna pekee kipenzi na ndo ua zuri la nafsi ya Geb .Nilishindwa kujizuia nilimkiss mbele ya hadhira  ile bila kujari watu wote waligeuka kunitazama sio kwa wale waliojua mimi na geb tuna uhusiano gani na hata wale wasiojua janeth,john, Dav na mary pia walikuwa miongoni mwa walio shuhudia yale na kila aliyetutazama alijuawazi kuwa tulikuwa tunapendana sana. Niliporidhika nilishika beg moja mkononi na jingine alibeba Betha mpaka palipo parking ya tax napo ndipo safari ilipoanza kuelekea magomeni ambapo ndo mahali ambapo Geb alikuwa akiishi .



    Geb alikuwa akiishi katika nyumba ya kampuni ambapo aliishi na marafiki zake wawili aliokuwaakifanya nao kazi Dav na John .Betha aliishia njiani baada ya kupigiwa simu arudi nyumbani haraka sana na kuniacha mimi na Geb tukiendelea nasafari yetu mpaka magomeni  tulipofika niliweza kulipia Taxi na kuingia ndani. Tulipoingia ndani geb aliniomba aingie bafuni kuoga nami nipange nguo zake kwenye kabati wakati nayafanya yote hayo Ghafra simu ya Geb iliita nilipoitazama hakuwa mwingine ila ni rafiki yake na mfanyakazi mwenzie na Geb ambaye jina lilitokeza kama David ,nikaona sio vyema kupokea simu yake bila ridhaa yake nikamuita



    "sweetyy,,?simu inaita" alijibu akiwa chooni bado "ni nani huyo tena ,,,?"



    "david ndo anapiga"



    "daah wepokea umsikilize"



    "ok pouw"nikaichukua nakuipokea ilikuweza kumsikiliza anacho hitajia alianza kwakusema"hallow Geb?" "Eeeh Hallow shem Geb yupo chooni anaoga,,,,,"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ooooh!kumbe mtoto mzuri bado upo ok! basi sawa we mwambie mkurugenzi amenipigia simu muda huu amesema kesho tunahitajika ofisini wote na kesho kutwa tujiandae na safari ya kwenda CANNADA,,," yalikuwa maneno mafupi na yenyekueleweka na yalipita katika tundu za masikio yangu barabara yote ilikuwa ni kutokana na ukaribu ulio kawepo baina ya masikio yangu na simu ile niliyaelewa vyema maneno yale ila siku taka kuamini kamakilichosemwa kilikuwa ni sahihi kweli nikauliza



    "nini,,,,?kwa hiyo Geb anaondoka tena"



    "ndio anna," David alijua dhahiri Taharifa zile zimeniumiza ila hakua na jinsi hata kama angeesema amsubiri Geb iliamwambie bado yange kuwa yale yale maana sio David wala John wote walitambua jinsi nilivyo dhaifu kwa Geb ila hakukuwa na namna, nilihoji tena ilikuona uwezekano wa Geb kutoenda safari"Kwani shem amna wafanya kazi wengine zaidi yake?"



    "wapo shem tena wengi sana ila Geb ana elimu ya tofauti na sisi wengne maana yeye mbali na yote pia alishawahi kusomea journalism(uandishi wa habari) na yupo peke ake hivyo ni mtumuhimu sana   katika kampuni"



    "Daah pouw ujumbe umefika"



    "sawa shem ila usimkataze maanando sehemu zenyewe kwakujipatia kipato hizi"



    "najua hilo shem wala usijali"nilijitahidi kutengeneza tabasamu ila lilikataa sauti ilitoka ya upole sana nilijua dhahiri Dav atakuwa ameju nini kilichopo ndani ya nafsi yangu sikuwana jinsi taharifanilizopewa ilibidi nizifikishe kwa Geb kama zilivyo baadaya muda kidogo Geb alirejea kutoka bafuni akiwa ameshika taulo lake mkononi muda huo nilikuwanimejiinamia alisogea taratibu mpaka pale nilipo aliponigusa nilishituka na kumtazama usoni



    "anna???"aliniita kwa upole baada ya kumtazama machoni"kunatatizo mama?"aliniuliza tena na kwa upole zaidi nilimtazama napo sikuwa na jibu la kumpa nilichukua simu yake na kumkabidhi bado alikuwa njia panda kunielewa nikitu gani haswa nilikimaanisha nilivuta pumzi ilikuzishusha hasra nilizokuwanazo kisha nikamtazama tena Geb"ni Dav ndo aliyekuwa akipiga simu" alinisikiliza kwa umakini na mimi sikusita nikaendelea "amesema amepigiwa simu na mkurugenzi kesho asubuhi unahitajika ofisini na kesho kutwa kujiandaa na safari ya kuelekea CANNADA"nilifikisha ujumbe kama ulivyo Geb alionyesha kuchoka ndipo akasimama kidete sasa na kushika kiuno alionekana kama wakufikilia jambo ilanilishindwa kumuuliza alizunguka kila kona ya chumba chake akionekana ni mtuwakutafakari jambo huku  miminikimsindikiza na macho yangu kila kona aliyopita nikijipa moyo uwenda atasema chochote ila haikuwa hivyo.   Baada ya nusu saa nilimsikia akianza kuongea mwenyewe kwa sauti ya chini



     "hivi mbona wananifanyia hivi mimi sipatia hata muda wakupumzika na kujua nitajenga vipi familia yangu mbona hivi lakini"ndiponikajua kumbe sio mimi tuu hata yeye anaumia kukosa muda wa kuwa na mimi nilinyanyuka nilipoketimpaka pale alipokawa amesimama nikamkumbatia kwa nyuma nilijikaza lakini nilishindwa nikajikuta machozi yakanitoka na kudondokea katika mdongo wa Geb, naye pia alinigeukia nakunikumbatia tukabaki tukishare maumivu yale "anna mama?"aliniita tena na kwa upole zaidi ya mara ya kwanza nilimtazama usoni kumsikiliza



    "nivumilie nikirudi nitakuoa sawa mama" ilikuwa ideal inzitokwangu kuikubali moyo wangu ulikuwa mgumu kukubaliana na wazo lake siku taka kabisa Geb aende CANNADA moyo wangu ulisita kabisa kukubali juu ya safari ya geb na kila nilipojiuliza sababu hasa ya kumzuia geb kutoenda safari bado jibu lilikuja anioe ila bado halikukamilika maana bado moyo ulikuwa mgumu mwisho niliridhia safari ya Geb ilailikuwalazima aende nyumbani kwanza. Tulipo fikia muafaka Geb aliendelea kuvaa  nami nikampangia nguo zake na nilipomaliza tukaondoka wote kwa ajili yakupata lunch nilifurahi kumuona Geb kwa siku ile ijapo kuwa alikuwa anasiku chache tuu angeweza kuondoka tena ila nilipenda kufurahia zaidi maana sikujua huko aendako pia atachukua muda gani mpaka kurudi,moyoni nilijuwa dhahiri kuwa atachukua muda mrefu sana ila nilijifariji nakujipa moyo kuwa baaada ya muda mfupi atarejea siku hii tulipenda kuitumia vyema kwa upanga mipango yetu hasa juu ya utambulisho n harusi .



    Utambulisho ilibidi ufanyike siku ya pili yake kisha Geb ajiandaae na safari na harusi ilikuwa baada ya Geb kutoka safari aliahidi kulitimiza hilo punde tuuu atakaporejea tanzania.Tulipangamengi sana siku hiyo tulijaribu kuangalia jinsi siku yetu ya harusi itakavyokuwa nzuri kwa furaha amani na ndelemo  kila mmoja wetu alisahau yaliyopita hatimaye  jua lilizama mwezi ukaonekana na giza likaingia kutoa ushirikiano kuwa siku inabadilika sasa.Geb alinichukua na kunirejesha mpaka nyumbani ambapo hapakuwa na mtu kwa wakati ule baba alikuwabado ajarudi kazini na mama pia alikuwaajarudi katika miangaikoyake ,niliagana na Geb na mimi nikaingia ndani nikaandaa chakula na kukiweka mezani na kufanya kazi zingine ndogo ndogo kisha nikaingia bafuni nikaoga na kuingia sitting kuangalia Tv.



    punde nikasikia honi ya gari baba na mama walikuwa wanarudi walionekana wakiwa na furaha ya ajabu wakichekeshana na kutaniana wakipiga story za hapa na pale bila shaka walikuwa wakikumbukia enzi zao,sikutaka kuwa katisha niliwapokea mizigo yao na kuwasaidia kuingiza ndani nilipowaona wamefikia tamati ya maongezi yao niliwasalimia nakuwakaribisha mezani nao waliingia chumbani mwa baada ya muda  walitoka wakiwa tayari wamekwisha oga na wapo tayari kukaa mezani waliketi nami nikaanza kuwahudumia chakula kisha na mimi nikajiudumia na kuketi bado stori ziliendelea bila kikomo mwisho nilikohoa ilikuwaweka sawa kunisikiliza, "baba na mama" walinitazama wote na kuweka nukta katika sahani zao na kutaka kusikia ninachotaka kuwa ambia







    "Geb amesha wasili tanzania tangu leo asubuhi ilaalikuwa anaomba kesho ajekujitambulisha maana anasafari nyingine hivi karibuni na bado ajajua nilini atarejea tanzania ila anataka atakapo rudi tuoane"niliongea kwa heshima zote na adabu na unyenyekevu wa hali ya juu iliwanielewe na kweli haikuwa kazi ngumu kwao walinielewa,tulimalizia chakula na wao kuingia chumbani kwao na mimi nikaingia kwangu nikajitupa kitandani na kupapasa upande wa pili wakitanda changu ambapo nikaivuta simu yangu ya mkononi na kuanza kuitafuta namba ya Geb na kumpigia haikuita sana simu ilipokelewa na sauti ilisikika



    " hallow xweety ?" na mi nilikuwa tayari kujibu



    "yes honey, bado aujalala tuu?"niliuliza kwa sauti ya kudeka "bado mpenzi ila ndo nipo kitandani hapa ndo nilikuwa najiandaa nakulala "



    "oooh basi vyema ilanimeongea na baba na mama wamekubali kesho ujenyumbani"



    "waow kweli anna?"



    "ndio nimewaeleza pia juu za safari yako ila wamesihi sana ujekwanza nyumbani"



    "Ooooh basi usijali mpenzi  kesho nitakuwa kazini kujua nini kinaendelea ikiwemo na kuniongezea siku za kurelux alafu nitakuja mama sawa?"

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "ok Geb nimekuelewa  mpenzi"



    "ok basi wacha nipumzike mama tutaongea vizuri kesho "



    "sawa usiku mwema kipenzi changu"



    "na kwako pia " maongezi yetu yalikuwa kama hivyo na ndo ukawa mwisho wa simu yangu kwa Geb nilikata na kuvuta shuka nikalala asubuhi nilipoamka nilimkuta mama akiwa na pirika pirika za kufanya usafi na kupika chakula



    "shikamoo mama?"



    "marahaba , umeamka je?"



    "namshukuru mungu mama, naona ndo unaandaa mazingira ilikumkaribisha mkweo"



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog