Search This Blog

SOSO - 3

 







    Simulizi : Soso

    Sehemu Ya Tatu (3)



    Alistahajabu sana hakuamini alichokiona alivua miwani aliyokuwa ameivaa....

    kumbe kuna Tariji mmoja alituma kikosi cha majasusi wakaharibu kila kitu kilichokuwa mule ndani kisha wabomoe mahabara hiyo....kumbe tajiri huyo aliewatuma majasusi hao aliona kama Doctor john anaelekea kuwa bilionea kutokana na dawa hiyo aliyoigundua hivyo... angeweza kumzidi kifedha na umaarufu... kwa sababu wote ni watafiti wa Tabia za mimea na Wanyama.. na kila mmoja alikuwa na maabara yake""" john alikwenda kuripoti kwenye vyombo vya dola (polisi) maabara yake imevamiwa na kuvunjwa usiku wa kuamkia leo...



    **********

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwenye jumba moja ambalo halijamaliziwa ujenzi alionekana yule mtu aliyekuwa kachomwa sindano ya majaribio na john... alianza kuhisi kuwa anahitaji kula nyama mbichi alijizuia kwa masaa mengi na aliposhindwa kuvumilia aliamua kutokomea na kuelekea mbali na makazi ya watu akajificha katika jumba hilo.... alifanya hivyo ili kuhepusha ile hamu ya kula nyama mbichi.... hasa zaidi kila alipokuwa akiona binadamu au mnyama yoyote akipita mbele yake alihisi kula nyama yake... mtu huyo alianza kubadilika kila siku inapopita macho yake yalianza kubadilika na kuwa mekundu makucha ya mikono na miguu yakawa marufu kuliko makucha ya binadamu kichwa chake kilianza kuongezeka ukubwa na meno yake ya mbele yalikuwa marefu kuchomoza nje ya mdomo... alianza kujishangaa na kujiogopa... alijutia kwa nini alikubali kufanyiwa majaribio...



    kumbe wale majasusi walimuacha hai kutokana na kuonekana kuwa na afya mbovu walihisi atakufa muda mchache hivyo walimfungulia kwenye kile chumba na kumuacha aondoke zake akafie mbele ya safari. kisha wakaleta katapira aina ya BULL-DOSSIER 170 na kuanza kubomoa maabara ile..



    **********



    Ule upande mwingine john alihisi kuchanganyikiwa inamaana ndoto zangu zinaishia hewani na ni nani aliyefanya hivi!!! john alijiuliza bila kupataa majibu ukizingatia fomula yote ya kuanzia hatua ya kwanza mpaka dawa kukamilika utengenezaji... kila kitu pamoja na Nyaraka zote zilikuwa ndani ya maabara.. alisikitika sana...... alikuwa na shauku ya kutaka kumuona yule mtu aliyemchoma ile sindano ya majaribio je? anaendeleaje? agh lakini sikumuona mtu yule kuwepo pale... kama angekufa kwa kuangukiwa na kuta za jengo lile basi maiti yake pia ingeonekana.... bila shaka mtu huyo bado yupo hai,,,""alijisemea john.... kisha akarudi nyumbani kwake... alipofika aliwasha Runinga (Television ) ghafla alistuka baada ya kusikia habari huku ikionesha matukio ya mauwaji ya kikatili... mauwaji yale yalifanywa na mtu asiye julikana"" ni kule ambapo liligunduliwa fuvu la kichwa kikubwa fuvu hilo lilionekana kufanana na fuvu la binadamu lakini meno yake ya mbele yalionekana kuwa marefu kuliko meno ya binadamu wa kawaida. habari hiyo ilisema kuwa Walinzi wote waliokuwa wanalinda eneo la mapango ya SOSO

    wamekutwa wameuwawa na watu wasiojulikana....baadhi ya maiti hizo zilikuwa hazina utumbo na nyingine zikiwa hazina miguu..

    john alistuka sana... alikumbuka juzi alipokuwa huko alishuhudia mlinzi mmoja akiwa kalala chini huku utumbo wake umemwagika... poa aliona mlinzi mwingine akivurutwa kwa kasi kuingizwa ndani ua pango ingawa hakufanikiwa kumuona vizuri mtu aliyekuwa akimvuruta mlinzi... haiwezekani bila shaka kizazi cha hawa viumbe bado wanaishi.....alijisemea john..

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    baada ya siku kadhaa kupita kiumbe yule aliamua kukimbilia mistuni alikwenda mbali sana....

    John aliamua kuandaa safari ya kurudi kwenye mapango ya SOSO ili akatafute kitu kitakacho msaidia kufanikisha kutengeneza tena dawa ile.... na baada ya wiki moja safari ikawadia... alikwenda mpaka kwenye mapango ya SOSO alipofika aliingia ndani ya pango alistahajabu kuona wale viumbe walikuwa wengi wakiweo watoto waliofanana na viumbe hao... pia aliona mwanamke mzee alipomtazama vizuri john aligundua ni binadamu kabisa na hakufanana na viumbe wale wenye mfano wa binadamu



    kumbe bibi huyo ndiye yule mary mtoto wa waziri mkuu....sikuile sande pamoja na lawi waliuwawa na watu wale wa ajabu kwa kukatwakatwa mapanga kisha wakamchukuwa mary na kuomdoka nae akiwa hai kumbe watu wale walimfungia mary na kumfanya kama mke wao""" walimuingilia ki mwili kila mmoja kwa wakati wake siku moja waliamua kumuuwa yule dereva binadamu wa kawaida aliyekuwa akishirikiana nao kuuwa watu na kuwafanya vitoweo.... walimuuwa kwa sababu ya wivu baada ya mwaka mmoja kupita tangu walipomchukua mary na kuishi nae kwenye mapango ya SOSO mary alianza kuwa karibu na dereva yule kuliko wale watu wa kutisha... kwa sababu dereva yule alikuwa ni binadamu wa kawaida.... .. hatimae baada mwaka mmoja mary alishika ujauzito na kuanza kuzaa watoto wenye sura zinazofamana na watu wale wa kurisha....baada ya miaka mingi kupita mary aliwazoea watu wale pia alizaa watoto wa nne... na baada ya miaka sabini kupita viumbe wale wawili ambao ni baba wa watoto hao walikufa na kumuacha mary pamoja na wale watoto wanne wenye sura za ajabu...



    john aliogopa sana akaanza kutimua mbio kuelekea kule alipolipaki gari mara ghafla.....



    mara ghafla alikoswa kupigwa na kishoka kidogo kilichorushwa na mmoja kati ya watu wale wa ajabu... kishoka kile kilipiga kwenye kingo za pango hilo"" john alikimbia kwa kasi akafungua mlango wa gari lake..... alipochomeka ufunguo ili awashe gari mara ghafla ufunguo ulikatikia ndani akabaki kashikilia kipande cha juu cha ufunguo... akili ilimruka alihisi anaota.... wakati huo huo wale watu wallikuwa wanakimbia kuelekea ule upande ambao john alikuwepo... john alipotaza kupitia kioo cha mbele ya gari... haja kubwa ilimtoka kwa uwoga.....kutokana john kuwa na uzoefu wa magari kwa miaka mingi.... wazo lilimjia kuwa akate nyaya mbili ambazo moja inatoka kwenye AUTONETA na nyingine inayotoka kwenye STARTER kisha azigusanishe zipige shoti gari liwake... alifanya hivyo haraka.... wakati huo wale watu wa kutisha walikuwa jirani kabisa kulikaribia gari la john..



    *********

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ule upande mwingine katika msitu alionekana yule Mtu aliyechomwa ile sindano....alizidi kubadilika akaanza kuwa mtu wa ajabu na mwenye kutisha.. ...alihisi njaa kali sana kwani hakula kitu chochote tangu siku aliyochomwa sindano... hata yeye alijishangaa.....kwamba bado yuhai siku zote hizo bila kula chakula.... alikuwa anajizua kwani hakutamani kula chakula cha aina yoyote ile isipokuwa Nyamba mbichi.... lakini safari hii uvumilivu ulimshinda.... kwa mbali alimuona mnyama aina ya pundamilia...alianza kumkiza mnyama yule.... inashangaza sana mtu huyo alikuwa na kasi ya ajabu alikimbia kama upepo na kumnasa pundamilia yule... na kumrarua tumboni kwa kutumia kucha zake ndefu na imara utumbo wa mnyama yule ulimwagika chini...kisha akaanza kula maini na figo pamoja na bandama mbichi....mnyama yule alianguka na kukata roho...

    baada ya kula nyama mbichi mtu yule wa ajabu alianza kujisikia vizuri kabisa.... lakini alijishangaa na kujiuliza mimi ni nani??? kumbukumbu zilianza kutoweka katika fikra zake akaanza kutoka kabisa katika hali ya kibinadamu.... na kuwa SOSO... tena soso huyu ni moto wa kuotea mbali... kwa sababu ana chembechembe hai za damu ya binadamu.. pia anachembe za viumbe aina ya soso... hivyo alikuwa na nguvu kuliko viumbe wale wote...



    **********



    Ule upande mwingine yule Tajiri Doctor.. aliyefanya njama ya kuharibu maabara ya doctor john,, sasahivi alikuwa anaandaa mikakati ya kumuangamiza kabisa john....john alionekana kumzidi ujuzi na maarifa hivyo watu wengi walimuamini sana john kuliko yeye.. alionekana akiwa na mkubwa wa kikosi cha majasusi katika hotel ya kifahari iitwayo SEECLEAF HOTEL wakijadiliana juu ya mpango wa kumuangamiza john...



    **********



    ule upande mwingine kule kwenye mapango ya soso... john alifanikiwa kuzikata nyaya zile lakini kabla hajazigusanisha mara ghafla... watu wale wa ajabu walikuwa wameshafika yule mmoja alivunja kioo cha mbele kwa kutumia panga kubwa na refu

    likapenya na kuingia ndani ya gari... john alilikwepa huku akiendelea kugusanisha nyaya zile.... punde yule mtu mwingine alikuwa akiuvita mlango wa upande ule aliokuwepo john kwa sababu mlango alikuwa kaufumga kwa loki (lock) haukuweza kufunguka...yule mtu wa kutisha aliyevunja kioo kwa kutumia upanga alipanda juu ya boneti ili amshambulie john kwa kumkatakata mapanga mara ghafla...



    Mara ghafla gari liliwaka... John aliingiza gia na kuondoka kwa kasi ya ajabu... yule mtu aliyekuwa kapanda juu ya boneti alianguka chini na kukanyagwa na gari.... john aliliendesha gari kwa kasi bila kigeuka nyuma... aliifikia barabara kuu inayopita kati kati ya msitu huo... aliondoka na kutokomea..... alipokuwa njiani alianza kumuomba mungu kwa kusali... pia alimshukuru kwa kumnusuru na kifo kule kwenye mapango ya soso..... kabla hajafika mbali gari lilianza kupunguza kasisi alijitahidi kukanyagia mafuta lakini gari lilikwenda kwa mwendo wa taratibu ghafla lilisimama.... john alihisi kuchanganyikiwa jasho lilimtoka huku mapigo yake ya moyo yakipiga kwa kasi"" alitoka haraka haraka ndani ya

    gari kisha akalifungua boneti la mbele ya gari...alipotazama aligundua kuwa rejeta imetoboka.. maji yote yaliisha kwa kuvuja kupitia tundu lile..... injini ilichemka ndiyo maana gari lilizima...wakati anatafakari nini cha kufanya wazo lilimja kuwa mule ndani ya gari alikuwa na gundi aina ya puti gundi hii ni maalumu kwa kuwekwa kwenye bati la gari kabla haijapakwa rangi.... alichanganya puti kisha akajaribu kuweka kwenye tundu lile... na baada ya muda alichukuwa dumu la maji mdani ya gari na kuyamimina kwenye rejeta....alisubiri kwa dakika kadhaa kisha akachungulia aligudua kuwa maji hayavuji.... aliingia ndani ya gari na alipojaribu kugusanisha zile nyaya mbili zilipiga shoti na gari liliwaka akaendelea na safari....



    *************

    CHANZO : http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog