Search This Blog

NABII WA UONGO - 5

 

    Simulizi : Nabii Wa Uongo

    Sehemu Ya Tano (5)





    Yalikuwa ni maneno ambayo niliyazungumza moyoni mwangu, huku nikiongoza ibada ya maombi siku ya Ijumaa. Kanisa lilifurika kama kawaida, wananchi mbalimbali kutoka duniani kote, walifika kuombewa, baada ya kupata taarifa zangu za uponyaji kupitia redio na televisheni. Kwa kutumia vifaa vyangu vya ajabu, maji ya ajabu, kitambaa pamoja na pete ambayo nilikuwa nimeivaa mkononi mwangu .Viwete waliweza kutembea, na wenye magonjwa mbalimbali waliweza kupona.



    “Let me take this opportunity to thank the son of God, apostle Hakika, for healing me “(Nachukua nafasi hii kumshukuru mwana wa Mungu, nabii Hakika, kwa kuniponya)  yalikuwa ni maneno ya furaha na shukrani, kutoka kwa mwanaume mmoja raia wa Kenya aliyesumbuliwa na ugonjwa wa ukimwi kwa miaka mingi, lakini baada ya kumgusa na pete yangu kichwani, aliweza kuwa mzima wa afya, na ripoti ya daktari iliweza kudhibitisha jambo hilo, baada ya kumfanyia uchunguzi mala baada ya kumuombea, na kisha kuleta majibu yake haraka sana baada ya saa moja.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Aim from America, I was suffering from Cancer, but i thank the son of God, apostle Hakika for healing me, I got his information from BBC, and decided to come in Tanzania  to get healed “( Ninatokea Marekani ,nilikuwa nasumbuliwa na kansa, lakini namshukuru mwana  wa Mungu, nabii Hakika kwa kuniponya, nilipata taarifa zake kupitia BBC, na nikaamua kuja Tanzania nipate kuponywa)  ilikuwa ni sauti ya mzungu mmoja raia wa Kimarekani, aliyeonekana kuongea lugha fasaha ya kingereza, akiwa na furaha sana baada ya kuponywa. Sauti za shangwe na nderemo ziliweza kusikika, hakuna aliyeamini kama kweli niliweza kuwaponya wangonjwa wale, hasa mgonjwa wa Ukimwi, raia wa Kenya.



    Waandishi wa habari walipiga picha na kurekodi kila tukio ambalo lilifanyika kanisani kwangu, huku chaneli ya ITV ikirusha laivu kipindi changu. Hivyo basi, sifa zangu zilienea kila mahali, na kunifanya nizidi kuwa maarufu. Hakuna aliyefahamu kama nilitumia nguvu za giza kuwaponya watu, bali niliendelea kupata wafuasi wengi zaidi kila kukicha. Japokuwa mzimu wa Juliet ulijaribu kunichafua na kusema ubaya wangu kanisani kwangu, lakini haikusaidia chochote kwani mkuu wangu nyoka aliweza kufuta kumbukumbu zao, na kuwafanya wasahau kila kitu ambacho Juliet aliweza kuwaambia, kuhusu unabii wangu wa uongo, na kuhusika na mauaji yake.



    …………………………………



    Ilikuwa ni jioni njema, jioni ya siku ya ijumaa, wazazi wangu pamoja na wazazi wake Juliet, wakiwa wameshakamilisha siku mbili za kufunga na kuomba ,ili mzimu wa Juliet upate nguvu kwa mala nyingine tena, ili aweze kunikomboa kutoka katika utumwa wa kishetani.



    Matumaini ya kunikomboa yaliweza kufifia, kwani japo walikuwa wametimiza siku mbili za maombi, lakini hawakuweza kusikia chochote kuhusu mzimu wa Juliet. Tangu uondoke siku ya Jumatatu, mzimu ulikuwa bado haujarudi na kuwapatia matokeo mazuri, kuhusu ukombozi wangu.



    “Mwanangu jamani, anazidi kumchukiza Mungu, ona anavyosifiwa kuwaponya watu, Eeeeeh Mungu msamehe kijana wetu, halijui alitendalo ” ,yalikuwa ni maneno yenye uchungu wa mwana, maneno mazito kutoka kwa mama yangu mzazi, mama ambaye alinilea kwa uchungu tumboni mwake kwa muda wa miezi tisa. Japo alinilea kwa uchungu, kwenye shida na raha, lakini nilishindwa kumlipa fadhira na kutaka kuwaua, niwatoea kafara yeye na baba yangu mzazi. Lakini kwa msaada wa mzimu wake Juliet, sikuweza kufanikiwa kutimiza malengo yangu. Kwahiyo basi, mama yangu alizungumza maneno hayo mazito ya uchungu, baada ya kutazama kipindi changu katika chaneli ya ITV, alishuhudia jinsi ambavyo niliweza kuwaponya watu kwa kutumia nguvu za pete yangu, na kumfanya aweze kusononeka sana. Alitambua kuwa nilikua na shetani ndani yangu, akinitumikisha na kumsahau Mungu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Usjali mama Hakika, kila kitu kitakua sawa, Mungu wetu hashindwi! ” ,yalikuwa ni maneno ya hekima kutoka kwa baba yake Juliet, akimtia moyo mama yangu, aliyeonekana kuhuzunika na yale niliyokuwa nikiyafanya. ………



    ……………………………



    Kuzimu; Masaa sita nyuma



    Ilikuwa siku ya ijumaa, mida ya mchana, kivumbi kiliweza kutimka kuzimu. Gereza la kuzimu, gereza ambalo lilitengenezwa kwa vyuma, vyuma ambavyo vilikuwa vya moto sana kiasi kwamba hakuna binadamu yoyote wa kawaida ambaye angeweza kusogelea vyuma vya gereza hili. Vyuma hivi vya gereza viliweza kuyeyuka na kuwa kama uji, macho ya Juliet, macho ya ajabu ndiyo yaliyoweza kuyeyusha vyuma hivi baada ya kutoa mwanga mkali sana. Maombi ya wazazi wangu, pamoja na wazazi wake Juliet, yaliweza kufanikiwa ,kwani nguvu za Juliet ziliweza kurudi na kuwa za kutisha sana. Uji ule wa moto, uji ambao ulitokana na vyuma kuyeyushwa na macho ya Juliet, uliwaunguza nyoka waliokuwa wakimlinda Juliet kwa kumuimbia nyimbo zenye kumdhoofisha nguvu zake na kumpulizia filimbi.



    Kiongozi msaidizi wa Jeshi la shetani, kiongozi ambaye ndiye aliyetupokea siku tuliyoenda kuzimu, na kunieleza mambo ya kufanya kama nitataka kuishi nao kuzimu, kiongozi ambaye alivalia mavazi ya kifalme. Alipiga tarumbeta, tarumbeta ambalo liliashiria hatari ili askari wake waweze kujiandaa kwa mapambano.



    “Taaantii …tantaa, tantiii …tantaaa, yeeeeeh!!!!! ” ,ilikuwa ni sauti ya tarumbeta kubwa sana ya kijeshi, tarumbeta ya kuzimu ambayo ilitofautiana sana na tarumbeta zetu za duniani. Ilitoa amli ya kuanza mapambano, huku mkuu wa jeshi hili akishangilia sana kuashiria ushindi zidi ya Juliet. Mala tu baada ya kumaliza kupuliza tarumbeta lake  na kuruhusu mapambano. Askari wake walianza kukimbia, kuelekea sehemu ambayo kulikuwa na gereza ambalo Juliet alikuwa amefungwa.



    “Iiiiiiiih………wiiiih …………iiiiih ……wiiiiiih “,sauti za vilio zilisikika, sauti zenye kutia huruma, walikuwa ni askari wa kuzimu wakipiga kelele za maumivu, baada ya kupigwa na shoti kali za macho ya Juliet. Kwakweli Juliet alibadirika sana, alikuwa na nguvu za ajabu  nguvu ambazo zilisababishwa na wazazi wangu, pamoja na wazazi wake Juliet, kufunga na kuomba kwa siku mbili bila kukata tamaa.



    Askari wengine waliyeyuka baada ya kukanyaga uji ambao ulitokana na vyuma vya gereza la Juliet vilivyoyeyuka  ,walipiga kelele huku wakifa na kuteketea kama nzige.



    “Unaitwa nani ,mbona sijawahi kuona kiumbe na mzimu wa ajabu kama wewe ……” ,kiongozi wa Jeshi la kuzimu aliongea na kumuuliza swali Juliet, ni baada ya kujikuta akiwa peke yake huku askari wake wote wakiwa wameteketea.



    “Mimi ni Juliet, niliyekufa bila hatia, na kurudi tena duniani kuwateketeza watu waliosababisha nife ” ,Juliet aliongea na kisha kumnyoshea vidole kiongozi yule, muda mfupi badae, askari yule aligaa gaa na kupoteza maisha. Kwani moto ulitoka katika vidole vya Juliet na kumuunguza, japo  askari yule alijaribu kuuzuia moto kwa dakika kadhaa bila mafanikio.



    …………………………………



    Ijumaa; jioni ………



         Nyumba ya kina Juliet ilionekana kuwa na simanzi, mama yangu alihuzunika na kujuta kunizaa, kwani nilionekana kama mkosi katika familia, kutokana na kumkufuru Mungu kwa matendo yangu mabaya, na kumtumikia shetani.



    “Usilie mama, nimerudi, asanteni kwa kutii maagizo mliyopewa na malaika, kesho haya yote yataisha “,ilikuwa ni sauti ya mzimu wa Juliet, baada ya kutokea sebuleni na kusababisha baba yangu atimue mbio kutokana na uoga. Juliet aliongea huku akimsogelea mama yangu, aliyekuwa akibembelezwa na mama yake kwa muda wote.



    “Usikimbie baba Hakika, japo mimi sio binadamu wa kawaida, lakini sio mtu mbaya kama unavyofikilia, nimetumwa duniani kwa makusudi ya kuteketeza watu wote wabaya, na kumgeuza adui kuwa mtu mwema “,Juliet aliongea maneno mazuri, maneno ambayo yalimfanya baba yangu arejee sebuleni. Lakini wakati hayo yote yakitokea, baba yake Juliet alikuwa amepigwa na butwaaa, akimshangaa Juliet kutoka chini mpaka utosini, hakuamini kama kweli mwanae aligeuka kuwa wa ajabu kiasi kile.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Dar es salaam,



    Juliet hakuweza kupumzika, alitaka kumaliza misheni iliyomrudisha duniani haraka iwezekanavyo, kwani siku hadi siku, nilizidi kupotosha jamii na kuwa na wafuasi wengi sana… Kwakuwa nilipanga kutoa kafara nyingine ya watu watatu, Juliet aliweza kulitambua hilo na hakua na sababu kuzuia lengo langu lisiweze kutimia.



    Jioni ile ile, jioni ya siku ya ijumaa. Juliet alitoweka nyumbani kwao, baada ya kufanikiwa kutoka kuzimu. Hali aliyoikuta duniani, haikuwa ya kawaida, alishangaa sana kwani wazazi wake pamoja na wazazi wangu, walikosa furaha. Waliumia sana, kila walipoona nikiponya watu na kusifiwa, huku nikitumia nguvu za giza. Kitendo cha kupata wafuasi wengi sana  kupita wale wa awali, kilimtisha sana na hakua na budi kujitoa kwa nguvu zote kupigana na watu wabaya, ambao walinitumikisha na kubadilisha fikra zangu. Fikra ambazo zilijali pesa, kuliko Mungu na binadamu alio waumba. Nilikua tayali kutoa uhai wa mtu yoyote yule, ilimradi nipate utajiri na sifa kubwa katika jamii.



    ………………………………



    “Ninaondoka kwa mala nyingine tena, sina muda wa kupoteza, lakini kabla jua halijazama siku ya kesho, nitarudi hapa nikiwa na mchungaji, akiwa amebadilika na kuwa mtu mwema, na mimi nitawaaga kurudi kwetu…………”, ilikuwa ni sauti nzuri, sauti ya msichana mrembo Juliet. Msichana ambaye nilimuua na kisha kumtoa kafara kwenye chama changu cha kishetani, katika hali ya kushangaza, Juliet alirudi duniani  kama mzimu, kwa ajili ya kunikomboa kutoka katika utumwa wa kishetani. Utumwa wa kumtumikia shetani kama nabii wa uongo, na kufanya anasa mbalimbali za kidunia, ambazo hazikumpendeza Mungu. Kwahiyo basi, Juliet hakua na sababu kuaga ili akaweze kuikamilisha misheni yake, na kuahidi kurudi nyumbani kwao, na kunikabidhi kwa wazazi wangu nikiwa mtu mwema………



    Wazazi wangu, pamoja na wazazi wake Juliet, walimtazama Juliet na kumsikiliza kwa makini, maneno ambayo aliweza kuyazungumza. Mwili wake uliyeyuka na kupotea kama upepo, hali iliyoashiria, alitoweka kuelekea kwenye mapambano ya kunikumbatia. Familia nzima waliketi sebuleni, walishindwa kwenda kujipumzisha mpaka Juliet atakapo rudi, akiwa amekamilisha misheni yake ya kunikomboa.



    Waliamua kukaa palepale sebuleni, kusubili hatma ya maisha yangu. Kwani walikuwa wamechoshwa na taarifa zangu kila kukicha, taarifa ambazo zilizungumzia habari zangu za unabii,na kuwaponya watu matatizo yao, kwa kutumia nguvu za kishirikina, huku wengi wakiamini, nilitumia nguvu za Mungu jambo ambalo halikuwa la kweli. Pete yangu niliyoivaa mkononi, kitambaa pamoja na maji ajabu niliyowanyunyizia watu, na kudai yalikua ni maji ya baraka. Ndiyo siraha pekee nilizotumia kuwatibu watu, na kulifanya jina langu kufahamika duniani kote, kwa muda mfupi tu.



    …………………………………



    Bagamoyo;



          Mzee Jabir aliamua kubakia Bagamoyo kwa siku kadhaa mala baada ya kutoka kuzimu, hakutaka kurudi Dar es salaam haraka sana bila kumaliza shughuli zote ambazo zilihusiana na chama chetu ……



    Kama wasemavyo wahenga, siku ya kufa nyani miti yote huteleza. Ndivyo ilivyotokea katika kasri letu ambalo lilikua Bagamoyo, Nyoka ambaye alikuwa ndiye mkuu wa chama chetu, baada ya kazi nzito hakuwa na nguvu tena za kumfanya aweze kupambana. Kwani ni muda mrefu tangu apate chakula, siku ambapo meli iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es salaam kwenda Zanzibar kuzama. Tangu siku hiyo alipomeza wahanga wa ajari hiyo, alikuwa bado hajapata chakula chochote kile cha kumuongezea nguvu.



    Nyoka alilala tu muda wote, bila hofu yoyote ile kwani aliamini Juliet asingeweza kutoroka kutoka kuzimu, na kusababisha matatizo yoyote yale. Mganga pia aliendelea kufurahia na kujiona mshindi, alilala fofofo huku mguu mmoja ukiwa huku, na mwingine kule. Uchovu aliokuwa nao baada ya shughuli nzito haukuwa wa kawaida, kwa takribani siku mbili tangu atoke kuzimu, uchovu wa safari ulikua bado haujamtoka katika mwili wake ………



    Upepo mkali kutoka baharini ulivuma, na kufanya eneo lote la Bagamoyo kuwa na baridi kali siku ya ijumaa usiku wa manane. Baridi hii iliufanya usingizi wa mzee Jabir, mganga pamoja na nyoka kuwa mtamu sana na isitoshe walikuwa wana siku chache tangu watoke kuzimu, safari ndefu ambayo iliweza kuwachosha.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hivyo basi, mzimu wa Juliet ulifika Bagamoyo, na kuikamilisha kazi yake kwa urahisi ambao haukua wa kawaida. Ukimya uliweza kutawala katika kasri letu, na kwa kutumia uwezo wa ajabu, aliweza kugundua kuwa hakuna kiumbe yoyote yule aliyekuwa macho.



    Juliet aliamua kufanya jambo la ajabu sana, na kuonesha uwezo wake, alifumba na kisha kufumbua. Baada ya kufumbua, mapipa kadhaa ya petroli yalikua mbele yake. Alinyoosha kidole, mionzi mikali ilitoka na kutoboa mapipa yale ya mafuta. Hakuishia hapo, alipandisha kidole chake hewani, na kisha kuchora mduara hewani. Mapipa yale yalipanda hewani kufuata ishara ya kidole cha Juliet, na kisha kumwaga mafuta kulizunguka jengo lote, kufuata ishara ya duara ambalo Juliet alichora. Ndani ya sekunde chache tu, jengo lote la chama chetu, liliweza kulowa mafuta ya petroli.



    “Puuuuuh ……puuuu ……,kila jambo linamwisho wake, haya ndiyo malipo ya dhambi zenu “,mzimu wa Juliet ulitema mate mala mbili, na kisha kuongea maneno ya kulaani vitendo vibaya ambavyo mzee Jabir, mganga pamoja na kiumbe wa ajabu nyoka, waliweza kuvitenda duniani.



    Baada ya Juliet kutema mate tu, mate ambayo yalimtoka mdomoni kama cheche za moto, na kusababisha jengo letu lote kulipuka na kusambaratika kabisa. Baada ya kitendo hicho, Juliet aliweza kupotea na kurejea Dar es salaam kama umeme.



    ………………………………



    “Aiiiiiih………aaaaii…ii…ih “,ulikua ni mlio wa huzuni, mlio ambao niliusikia usiku wa manane siku ya ijumaa. Nilishtuka sana kwani niliona mabadiliko makubwa sana ndani ya mwili na fikra zangu. Haraka haraka niliamka, na kisha kuelekea chumba changu cha siri, chumba ambacho kuliweza kutokea kelele.



    “Mungu wangu, nini hiki! ……”,nilishangaa sana kwani nilikuta nyoka wangu mdogo aliyekuwa akinilinda, na kulinda chumba changu cha siri akiwa amekufa huku akionekana kubabuka na moto. Kitambaa changu, pete yangu pamoja na maji ya ajabu, na yenyewe yalionekana kuteketea kwa moto. Kumbe baada ya jengo la Bagamoyo kuungua, jengo ambalo lilikuwa na kila kitu, siri pamoja na nguvu zetu, ndipo vifaa vyangu pamoja na nyoka Wangu waliweza kuteketea.



    “Mmmh mbona sielewi nyumba yangu imeenda wapi?, ” Hatimaye jengo langu liliweza kupotea katika mazingira ya kutatanisha, sikubaki na kanisa wala gari hata moja. Eneo lote ambalo kulikuwa na jengo langu, palibaki tambalale na kunifanya nibaki nikiwa nimepigwa na butwaa.



    “Usihofu chochote, tayali umekua mtu mwema ,fikra zilifumbwa na kusababisha uwe mtu mubaya sana, ukaniua mimi, na ukataka kuwaua wazazi wako “,



    “Siweziii! Kamwe siwezi kuwaua wazazi wangu, wala kuua mtu!, kama nimekuua mbona uko hai? ” ,



    “Huwezi kuamini kwa urahisi, fikra zako zilibadilishwa kishirikina, twende kwa wazazi wako ukawaone, udhibitishe maneno yangu “,



    Yalikuwa ni mazungumzo kati yangu na Juliet, baada ya kunitokea, kwa vile alikuja akitembea kama binadamu wa kawaida na kukuta nikijishangaa, sikuweza kutambua kama hakua binadamu wa kawaida. Nilikuwa na hamu kubwa ya kuwaona wazazi wangu, ni muda mrefu tangu nitoke Kigoma na kuonana uso kwa uso na wazazi wangu, kusema ukweli niliwamisi sana.



    Sikuwa na budi kumsikiliza Juliet, na kusikiliza maneno aliyoniambia. Nilimshika mkono, na baada ya kumshika tu mkono wangu, tulijikuta tukipaa juu kama ndege na kwa kasi ya ajabu. Niliona kama mazingaombwe, lakini haikuwa hivyo. Wakati mwingine nilifikiri nilikuwa ninaota, lakini haikuwa kweli, nilikuwa ninapaa hewani kweli kabisa, na sikuwa nikiota.



    Kitendo hicho kilinifanya niamini maneno ambayo Juliet aliniambia, niliamini kuwa Juliet hakuwa binadamu wa kawaida na kila kitu alichokiongea inawezekana kilikua sahihi …



    …………………………………



    Mwanga mkali uliangaza sebuleni, katika jengo la aliyekuwa mmoja wa viongozi wa kanisa langu, baba yake Juliet.. Mwanga ule uliwafanya waweze kuamka, kwani wote walilala sebuleni wakisubili Juliet afanikishe kunikomboa na kunikabidhi kwa wazazi wangu …………



    “Mwananje, ndashimye chane kukubhona, imana ishimweeh “,(mtoto wangu, nimefurahi sana kukuona, Mungu asifiwe)  mama alitamka maneno ya furaha kwa lugha ya kiha, huku akinikimbilia baada ya kutokea sebuleni katika mazingira ya ajabu sana. Wazazi wake Juliet nao hawakusita kuonesha furaha yao, walitukimbilia na kutukumbatia ……

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Baba yake Hakika, ulimuuliza swali kiumbe aliyekuja kuwapatia taarifa kuhusu kufunga na kuomba, yule ni malaika wa Mungu ……asanteni kwa kutii maagizo yote!!  Naomba muishi kwa upendo kama ndugu, msisahau kumtegemea Mungu kwa kila jambo kwani nimuweza wa yote, mimi ninaondoka, hamtaniona tena ……”,mzimu wa Juliet hatimaye uliweza kutuaga huku machozi yakimtoka, kiasi kwamba kila mmoja baina yetu alilia baada ya kusikia maneno mazito kutoka kwa Juliet.



    Nilijiona mwenye hatia, lakini sikuwa na jinsi yote yalikuwa ni mapenzi ya Mungu. Kwa mbali nilijiona mwepesi na huru, nilijiona kama nilitua mzigo mzito ambao ulizidi uwezo wangu, na kufanya asubuhi ile ya siku ya jumamosi kuwa ya kukumbukwa maisha yangu yote …………



    *MWISHO **



    Hali halisi ya dunia ya leo, iliyojaa uovu wa kila aina ……Eee……Mungu …tuhurumie!

0 comments:

Post a Comment

Blog