Search This Blog

CHOZI LA YATIMA - 4

 









    Simulizi : Chozi La Yatima

    Sehemu Ya Nne (4)







    Moyo wa Frank ulizidi kumsumbua kuhusu Musa, ikambidi amuite Suzan na kumueleza kila kitu kuhusu Musa.

    SUZAN: Unamaanisha ni mtoto wako?

    FRANK: Ndio ni mwanangu.

    SUZAN: Unaweza kuniambia sababu kubwa ya wewe kukataa mimba!

    FRANK: Nilikuwa bado nasoma Suzy na huyo Sada mwenyewe alikuwa ni mwanafunzi, ningekubali ningefungwa Suzy. Niliogopa hilo.

    SUZAN: Ila ni haki yake kabisa huyo binti kukufananisha na Israeli maana hata yeye atakuwa amekufa kwaajili ya msongo wa mawazo juu yako.

    FRANK: Jamani Suzy!!http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    SUZAN: Hakuna cha jamani sasa, cha msingi ni Musa atambue ukweli na amjue baba yake.

    FRANK: Sielewi nitaanzia wapi kumwelewesha.

    SUZAN: Musa ni mtoto wa kiume, itakuwa rahisi kukuelewa mwanaume mwenzie haswa wewe Israeli, hahaha.

    FRANK: Suzy acha masikhara bhana, mwenzio nipo serious.

    SUZAN: Basi ngoja tufikirie namna ya kumwambia.

    FRANK: Hapo sawa.

    Kwakweli swala hili lilimuumiza sana kichwa Frank kwani alifikiria vitu vingi na mambo mengi.



    Siku hiyo Suzan akaamua kumuuliza Musa kiutaniutani kuwa endapo atamjua baba yake atafanya nini. Akakutana na majibu ya ajabu sana yaliyojaa kwenye kichwa cha Musa.



    Siku hiyo Suzan aliamua kumuuliza Musa kiutani utani kuwa akimjua baba yake atafanya nini.

    Akakutana na majibu ya ajabu sana yaliyojaa kwenye kichwa cha Musa.

    MUSA: Unajua ni vigumu sana mimi kumjua baba yangu kwani mtu pekee anayemjua ni mama ila nae ameshakufa.

    SUZAN: Musa dunia ni pana sana, huwezi jua siku moja ukamtambua baba yako, hapo utakapomtambua utafanyaje?

    MUSA: Kwanza nitamuogopa sana huyo mtu, pili kwavile mama yangu alimfananisha na Israel mtoa roho nadhani huyo baba atakuwa ni mtu mbaya sana na mkatili, ataweza kuniua muda wowote.

    SUZAN: (Akapumua kidogo), ila Musa yote ni mapito katika maisha. Mama yako alimuita Israel labda sababu ya hasira zake juu ya baba yako kipindi hicho ila haimaanishi kuwa baba yako ni mtu mbaya kiasi hicho.

    MUSA: Atakuwa mbaya tu, kwamaana alinikataa tangu tumboni. Si mtu mzuri kwakweli.

    SUZAN: Musa, mimi unavyoniona ni mtu wa aina gani?

    MUSA: Wewe ni mtu mzuri sana sijapata kuona, mtu mwenye upendo na kujari.

    SUZAN: Nashukuru, je kamanda Frank naye unamuonaje?

    MUSA: Kwakweli ni mtu wa kipekee sana kwani amebadilisha maisha yangu.

    SUZAN: Kwamfano ikatokea kwa bahati mbaya tukafanya kitu na kukokosea je unaweza kutusamehe?

    MUSA: Kwakweli siwezi kuwa na kinyongo na nyie, na sidhani kama kuna baya la mimi kushindwa kuwasamehe. Nyie ndio wazazi na walezi wangu sasa.

    SUZAN: Basi Musa, mwenzio mimi nilikataliwa na baba yangu kama wewe, na hata nilipokua kua akaendelea kunikataa ila najua ipo siku atanikubali nami niko tayari kumsamehe kabisa.

    MUSA: Unamaana gani mamA?

    SUZAN: Maana yangu ni kuwa hata wewe pindi ukibahatika kukutana na baba yako na akakubali kuwa wewe ni mwanae, basi jifunze kumsamehe. Maana maisha ya ujana hufanya watu wafanye vitu bila kufikiri ila badae hujutia ila hilo liwe funzo kwako na kwamaisha yako.

    MUSA: Nimekuelewa, na mimi siko tayari kukataa damu yangu kwani mtaani ni mateso sana.

    SUZAN: Sawa sawa, na unapokuwa na tatizo lolote usisite kunieleza.

    Musa alijikuta akimuelewa sana Suzan na alijikuta akimpenda sana kwani Suzan alikuwa ni mtu mwenye huruma.



    Frank aliendelea kujifikiria namna ya kumueleza Musa ukweli.

    SUZAN: Ni vyema sana mtu akaujua ukweli wa maisha yake kwani kunamuwezesha kujitambua kuwa yeye ni nani?

    FRANK: Sasa nifanyaje ili niweze kumweleza ukweli?

    SUZAN: Nakushauri mchukue Musa na kwenda nae sehemu tulivu, uwe kama unapiga nae story za hapa na pale na hapo umwambie ukweli naimani Musa atakuelewa tu.

    FRANK: Nitaweza mwenyewe kweli Suzy?

    SUZAN: Wewe ni mwanaume na Musa nae ni mtoto wa kiume atakuelewa tu. Hata hivyo nilishajaribu kumvuta kifikra.

    FRANK: Ila nadhani itakuwa vyema tukaenda wote, hata kama nitaongea na Musa, wewe utakuwa hata pembeni kutungoja.

    SUZAN: Usijari Frank, wee nenda nae yeye tu.

    Frank akamuomba Musa kuwa amsindikize mahali, Musa akajiandaa na kuondoka nae.

    Frank akampeleka Musa kule alipokusudia kumpeleka.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Frank akamueleza Musa kila kitu kilivyokuwa na sababu ya kumkataa kabla hajazaliwa.

    FRANK: Tafadhari Musa mwanangu nisamehe, kwakweli najutia makosa yangu.

    MUSA: Kwanza hadi sasa nahisi kuwa naota, yani nimeweza kukutana na mtu aliyejulikana kama Israeli!!

    FRANK: Kwakweli sikukusudia mwanangu.

    MUSA: Hivi unajua shida nilizopata wewe?

    FRANK: Naelewa mwanangu, nisamehe.

    MUSA: Niachie muda kufikiria.

    Musa akamuomba Frank warudi, na

    waliporudi nyumbani Musa akajikuta amekosa amani, akamfata Suzan.

    MUSA: Kumbe baba uliyekuwa unanieleza ndio huyu ninaeishi nae? Kwanini awe yeye jamani?

    SUZAN: Musa yote ni katika mapito ya ujana tu, unapaswa kumsamehe.

    MUSA: Nimsamehe mtu aliyefananishwa na Israeli mtoa roho na mama yangu?

    SUZAN: Kila jambo hufanywa kwa makusudi flani, mama yako alikupa jina la mbele kama Israel akijua ipo siku utafahamiana na baba yako na hiyo ndio itakuwa furaha yake.

    MUSA: Kwahiyo inawezekana aliniita hivi kwasababu hiyo eeh!!

    SUZAN: Hiyo ndio maana yake na ndiomana baba yako akakutambua.

    Musa akainama na kutafakari sana, akajikuta akiinua kichwa na kusema

    "Nimemsamehe baba"

    Kwakweli Suzan alifurahi sana na akamuita Frank, kufika pale Musa akamkumbatia baba yake. Ikawa ni furaha kubwa sana kwa Frank.

    Usiku wake ikabidi amtambulishe rasmi Musa kwa Safina na Shida kuwa ni mwanae mzazi. Wakafurahi sana kwa kutambuana.

    Kwakweli Frank alijivunia kuwa na mtu kama Suzan ndani ya nyumba yake na moyo wake ukakiri kwamba yule ndiye mwanamke wa kumuoa.



    Musa akajikuta amekuwa ni mtu wa furaha muda wote.

    MUSA: Nimefurahi sana kumjua baba yangu na hii inaonyesha kuwa hivi karibuni Safina maisha yako yatabadilika kabisa.

    SAFINA: Kwanini unasema hivyo wakati ndoto za maisha yangu zilishakufa.?

    MUSA: Safina, leo usiku nimeota kuwa wewe unaishi katika maisha mazuri sana, na mimi naamini ndoto zangu kwani nilipokuwa mtaani nilishawahi kuota kuwa nitamjua baba yangu na imekuwa kweli.

    SAFINA: Unaamini sana ndoto?

    MUSA: Ndoto zangu nikiota zaidi ya mara moja daima huwa kweli.

    SAFINA: Napenda ziwe kweli ila sijui ni nani atakayeweza kunirudisha katika maisha yangu ya zamani labda anko Mike.

    MUSA: Anko Mike ndio nani?

    SAFINA: alikuwa rafiki mkubwa wa baba yangu ila ni mzungu na anaishi Marekani.

    MUSA: Pengine siku moja anaweza kufika nchini kwetu.

    SAFINA: Mmh sidhani.

    Mara Suzan akawa amerudi na kuwasalimia kisha kuingia ndani.

    MUSA: Kwakweli Safina, huyo mamako mdogo ana roho nzuri sana.

    SAFINA: Ndiomana nampenda, ila siwapendi ndugu wa baba kwakuwa wana roho mbaya kama mashetani.

    MUSA: Mmh!! Usiwaze sana Safina yote yataisha tu.

    Musa na Safina wakaongea mambo mengi, kumbe Shida alienda kuwachukua wenzie wengine wa mtaani ili wapate kumuona baba yake na Musa.

    SHIDA: Karibuni, hii ndio sehemu tunayoishi sisi kwa sasa.

    SIKUZAN: Khee, pazuri kweli. Mmepata bahati sana Shida.

    SHIDA: Hapa ni nyumbani kwa babake Musa.

    MIRIUM: Babake Musa? Kwani Musa ana baba?

    SHIDA: Ndio kampata babake.

    TIZO: Kweli Musa ana bahati. Hivi anaweza kuturuhusu na sisi tuishi hapa?

    SHIDA: Anaweza kwani ana roho nzuri sana.

    Shida akawakaribisha basi Musa na Safina wakafurahi sana kuwaona wenzao. Na wakaongea mengi.

    Suzan alipotoka nae akashangaa kuona wamekuwa wengi, baada ya salamu wakamtamburisha, na baadae wakamuomba kuwa watoto hao waishi mahali hapo.

    Frank aliporudi ikabidi Suzan amweleze kuhusu wale watoto na ombi lao la kuishi hapo.

    FRANK: Hivi Suzy nitaweza kweli kukaa na familia yote hiyo?

    SUZAN: Itabidi uweze na iwe njia yako ya kujutia yale yote ambayo mwanao amepitia akiwa mtaani.

    FRANK: Suzy ila ni wengi sana kwakweli, nitafilisika jamani.

    SUZAN: Frank, hawa si watoto wadogo kusema kwamba utahangaika nao, ni wakubwa sasa hawa. Ungewaruhusu tu ili wapate mwangaza wa maisha yao.

    FRANK: Umenipa mtihani mkubwa sana Suzy.

    SUZAN: Huu mtihani ni saizi yako Frank, tena unakufaa kabisa. Kila kitu huwa na sababu, kubali tuwalee tu hao watoto, watakula tunachokula sisi.

    FRANK: Sawa nimekubali.

    Basi watoto hao wakawa wanaishi nyumbani kwa Frank, jumla wakawa kama watu kumi nyumbani kwake.



    Suzan akaamua kumpeleka Safina nyumbani kwa Modesta ili akamsalimie na pia Modesta nae ajisikie vizuri kwa kumuona Safina, ila walipofika hawakumkuta na walipouliza wakaambiwa kuwa Modesta alihama na hata hawaelewi ni wapi alipohamia.

    Wakiwa njiani wanarudi, mara wakakutana na mtu aliyeonyesha kuwa anamjua vizuri Safina.

    Mtu huyo aliita na kuwafanya Safina na Suzan wageuke nyuma.



    Wakiwa wanarudi, gafla akatokea mtu aliyeonyesha kuwa anamjua vizuri Safina.

    Mtu huyo aliita, kitendo kilichofanya Safina na Suzan wageuke nyuma.

    Ndipo hapo Safina akapatwa na mshangao kuona amekumbukwa na mtu huyo, kumbe walipishana nae kwanza na ndipo kufika mbele huyo mtu akageuka na kumuita Safina.

    SAFINA: Aaah madam Lucy!!

    Basi wakakumbatiana.

    LUCY: Unajua nilipowapita hapo sura yako ikanijia sana ndiomana nikajaribu kukuita nijue kama ni wewe, kumbe ni wewe kweli jamani!

    SAFINA: Ndio ni mimi madam.

    LUCY: Umebadilika sana Safina, ni sura yako tu ndio haibadiliki. Unaishi wapi kwani?

    SAFINA: Naishi na mamdogo (huku akimuonyeshea kwa Suzan).

    Basi Suzan na Lucy wakasalimiana na kufahamiana pia.

    LUCY: Kwahiyo wazazi wako bado wako Marekani?

    SAFINA: Hapana (huku machozi yakimlengalenga), walishakufa kitambo sana.

    LUCY: Jamani Safina, pole sana mama.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    SAFINA: Nimeshapoa madam, vipi siku hizi bado unaendelea kufundisha pale shuleni?

    LUCY: Hapana, nipo na biashara zangu tu. Ila kuna watu wametoka ulaya huwa wanakuja kwangu kujifunza kiswahili.

    SUZAN: (Akaingilia kati), Safina hebu nitambulishe vizuri.

    SAFINA: Mmh!! Mamdogo nawe, huyu alikuwa mwalimu wangu, anaitwa madam Lucy.

    LUCY: Ni vizuri kufahamiana, ila kwangu sio mbali na hapa tafadhari naomba niwapeleke mpafahamu.

    Kwahiyo Safina na Suzan wakaenda hadi kwa Lucy kupafahamu.

    LUCY: Ingieni basi ndani mnywe hata maji!

    SUZAN: Usijali mwalimu, tutapanga tu siku nzuri ya kuja kukutembelea.

    SAFINA: Madam, hao wanafunzi wako huwa wanakuja hapa kujifunza?

    LUCY: Hapana, huwa nawafata mahali walipofikia ila hapa huja mara moja moja kunitembelea.

    Walikuwa na maongezi mengi sana ila Suzan akaona waage ili waweze kuwahi kurudi nyumbani.

    Kwahiyo Lucy akawasindikiza na wao wakaenda zao.

    Kwakweli Lucy nae alimsikitikia sana Safina.

    "Ama kweli maisha yanabadilika, yani Safina alivyokuwa mzuri ndio amechusha vile!! Dah, inaonyesha kapitia magumu sana. Eeh Mungu mrehemu." akajikuta ananyoosha mikono juu na kumuombea Safina.



    Kesho yake Suzan akiwa kazini, Pendo akamfata.

    PENDO: Kheee mwenzangu, una tenda ya kulea watoto yatima?

    SUZAN: Na wewe kwa umbea, umewaonea wapi?

    PENDO: Jana nilifika kwako Suzy.

    SUZAN: Wale hawana pa kwenda Pendo.

    PENDO: Sasa pale pana raha gani zaidi ya karaha na kero. Hapo ulipo huna mtoto halafu unaishi na mijitu yote ile loh!! Pale ilitakiwa uishi na watoto wawili tu Musa na Safina. Ila huruma yako itakuponza Suzy.

    SUZAN: Pendo, fikiria kwanza wale watoto hawana wazazi, hawana pa kuishi wala pa kwenda.

    PENDO: Lakini wale wameshazoea maisha ya mitaani Suzy, kumbuka kunguru hafugiki.

    SUZAN: Jamani Pendo maisha ya mtaani si mazuri.

    PENDO: Hivi unataka ndoa kweli wewe rafiki yangu? Nakwambia pale Frank hafurahii chochote, usije kujikuta umekazana kulea mitoto isiyokuhusu wakati mwenzio anatafuta mwanamke wa kujiliwaza nae.

    SUZAN: Jamani Pendo, usiseme maneno hayo. Unafikiri mi nifanyaje?

    PENDO: Wapelekee wanapolelewa yatima wenzao, hilo ni wazo tu kama hutaki lipotezee.

    Kwakweli Suzan alijiona yupo kwenye wakati mgumu ila bado aliendelea kuwaonea huruma watoto hao.



    Mtaa mpya aliohamia Modesta kipindi hiko akajikuta akiwa na urafiki na mdada aliyesadikika kuwa na maruhani.

    Mdada huyo alikuwa na asili ya kiarabu ila chotara kwani alikuwa ni mchanganyiko wa mwafrika na mwarabu, alijulikana kwa jina la Yusra.

    Wakiwa wanapiga stori kuna mtu alimdokeza Modesta kuwa Yusra akipandisha maruhani ana uwezo wa kuzungumza mambo mengi yaliyopita na yanayowazunguka. Kwavile Modesta alijihisi kuwa na matatizo kwa kipindi hiko akajiweka karibu zaidi na huyo binti ili pengine aambiwe matatizo yake hata kwa njia ya stori.

    Siku moja akiwa yupo ndani kwake na huyo binti, akatokea mtu mwingine aliyeitwa Rhoda na kuwasha marashi ambayo yalimuhamasisha Yusra kuongea kile anachokiona.

    MODESTA: Unajua kaka na wifi yangu walikufa kifo cha gafla sana.

    YUSRA: Kifo chao ni mipango ya wanadamu, tena ni ndugu zako, wabaya sana.

    MODESTA: Na mbona wifi anapenda kunitokea mimi?

    YUSRA: Ule ni mzimu wake, na katika wote kwenye ukoo wako amekuona ni wewe mwenye huruma.

    MODESTA: Na ile ajali niliyoambiwa mtoto wao amepata?

    YUSRA: Ile haikuwa ajali ya kawaida kama mnavyodhani, ulikuwa ni mpango wa ndugu zako kumuangamiza na yule mtoto ila mwenyezi Mungu amemponya.

    MODESTA: Jamani amepona kweli?? Hata siamini.

    YUSRA: Amini kuwa amepona, ila ndugu zako wanajua amekufa. Usiwaambie chochote hadi pale mtoto mwenyewe atakapoamua kujitokeza kwao.

    MODESTA: Na vipi kuumwa kwangu mimi?

    YUSRA: Ulikuwa na ugonjwa wa kawaida ila badae ndugu zako wakauzidisha ili kufanga mdomo wako.

    MODESTA: Mmh!! Inamaana ndugu zangu ni wachawi?

    YUSRA: Hapana si wachawi ila wanatabia za kichawi, yote hayo wamefanya kwa ushirikina wakisaidiwa na mganga mmoja hivi, ila tambua kwamba siku zote Mwenyezi Mungu ndiye muweza.

    Kwakweli Modesta alisikitika sana kuhusu ndugu zake, akajisemea

    "yote haya ni sababu ya tamaa za mali"

    kwakweli alimuhurumia sana Safina, huku akiwachukia na kuwaogopa ndugu zake.



    Siku hiyo Frank akatembelewa na shangazi yake na dada yake aliyeitwa Mwasiti. Walipofika nao walishangaa kuona vijana na mabinti nje ya nyumba ya Frank.

    SHANGAZI: Mwasiti, vile visichana na vivulana vinatafuta nini pale nje ya nyumba ya Frank? Wakati Frank hana hata mtoto wa kusema watacheza naye.

    MWASITI: Hata mimi nashangaa shangazi.

    Walipofika, wale watoto wakawasalimia na Suzan akatoka nje na kuwakuta, akawakaribisha ndani.

    Suzy alikuwa anawajua ndugu karibia wote wa Frank na wao walikuwa wanamjua ila hawakujua kama anaishi na Frank kipindi hicho kwani ni muda mrefu hawajapata habari zake.

    MWASITI: Suzy!! Usiniambie sasa hivi unaishi na Frank!!

    SUZAN: Ndio naishi naye.

    MWASITI: Ndio hatakuja kututembelea!

    SUZAN: Nilipanga kuja na Frank ila mambo yakaingiliana.

    SHANGAZI: Kwani Frank yuko wapi na wakati tumemwambia tunakuja?

    SUZAN: Ametoka mara moja ila atarudi muda si mrefu.

    SHANGAZI: Samahani kwanza nataka niulize kitu.

    SUZAN: Bila samahani shangazi.

    SHANGAZI: Suzy sijaelewa hao watoto hapo nje wanafanya nini, je ni majirani?

    SUZAN: Hapana, tunaishi nao humu ndani.

    SHANGAZI: Mnaishi nao!! Kivipi??

    Mara Frank akawa amerudi, basi akasalimiana nao. Ile kukaa tu, shangazi mtu akaendelea na hoja yake.

    SHANGAZI: Niambie Frank, hao watoto unaishi nao kivipi?

    FRANK: Hao ni watoto yatima shangazi.

    SHANGAZI: watoto yatima? Sasa hiki ni kituo cha kulelea watoto yatima?

    FRANK: Hapana ila nawasaidia tu.

    SHANGAZI: Kumbe wewe ni mtoa misaada? Mbona kuna ndugu zako wanateketea huko huwasaidii??

    FRANK: Jamani shangazi!!http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    SHANGAZI: Siwezi kabisa kukubaliana na jambo hili najua hata kaka hawezi kukubali. Ngoja niondoke zangu.

    FRANK: Shangazi yani ndio unaondoka?

    SHANGAZI: Ndio naondoka, unataka nifanye nini hapa? Nitazame ujinga wako huu! Mwasiti inuka twende.

    MWASITI: Jamani kwaherini.

    Shangazi yake akamvuta kwa hasira ili waondoke kabisa eneo hilo, nao wakaondoka.

    Frank nae akainuka na kwenda chumbani, Suzan akamfata nyuma.

    FRANK: Suzy haya yote umeyataka wewe.

    SUZAN: Nimeyataka mimi kivipi?

    FRANK: Wewe ndiye umewaalika hawa watoto hapa nyumbani?

    SUZAN: Nimewaalika kivipi wakati wewe mwenyewe ulikubali kuwa waishi hapa!

    FRANK: Nilikubali sababu ulinilazimisha.

    SUZAN: Ila hakuna haja ya kubishana Frank, cha muhimu ni kujua tunabebaje huu mzigo wetu.

    FRANK: Ngoja kichwa changu kitulie kwanza maana hata sielewi kitu chochote.



    Frank akiwa kazini kwake akatembelewa na Shangazi na baba yake, akajua wazi ni juu ya uwepo wa wale watoto nyumbani kwake.



    Frank akiwa kazini kwake akatembelewa na shangazi na baba yake, akajua wazi ni juu ya uwepo wa wale watoto nyumbani kwake tu.

    BABA: Hivi mwanangu huo upolisi ndio umekufundisha kufuga wezi ndani?

    FRANK: Baba nitafugaje wezi wakati mimi napingana nao?

    BABA: Hao watoto wa mitaani ndio wanaoongoza kwa kuibia watu na wewe umeenda kuwaweka ndani kwako unategemea nini wewe?

    FRANK: Baba unajua wale watoto wanaiba sababu ya maisha magumu lakini sasa sidhani kama wataiba tena.

    SHANGAZI: Usiwe mjinga wewe, watu husema kuwa mtu haachi asili yake, sasa wale toka utotoni wanaiba sasa waje kuacha leo?

    FRANK: Basi niacheni nifikirie mliyoniambia.

    SHANGAZI: Ufikirie nini? Tunachotaka ni uwafukuze pale nyumbani.

    FRANK: Dah! Kuwafukuza siwezi.

    BABA: Kwanini huwezi?

    FRANK: Maana kwa kupitia wale watoto nimeweza kumjua mwanangu.

    Wote wakashtuka na kumuuliza,"mwanao? Kwani una mtoto wewe?"

    FRANK: Ndio mwanangu tena mwanangu mzazi.

    WOTE: Kivipi?

    Basi Frank akaamua kuwaeleza kila kitu kuhusu Musa na wote wakabaki wanastaajabu. Pia akawaeleza kuhusu Safina na kuwafanya waendelee kushangaa.

    SHANGAZI: Safina mtoto wa Sam?

    FRANK: Ndio mtoto wa Sam.

    SHANGAZI: Aaah maskini, kumbe ameishi maisha ya mtaani wakati baba yake ni tajiri sana na ana mali nyingi.

    FRANK: Lakini wazazi wake hao wameshakufa.

    SHANGAZI: Yani Sam na Latifa walikufa!! Maskini mbona Aisha hajaniambia wakati nimekutana nae mara nyingi tu.

    FRANK: Tena huyo Aisha ndiye aliyemfukuza Safina kwenye nyumba ya wazazi wake.

    SHANGAZI: Kumbe Aisha ni mtoto mbaya kiasi hicho!! Hafai kabisa katika jamii.

    Walijikuta wakisikitika sana, nao wakahitaji kuwaona Safina na Musa. Kwahiyo wakaondoka hapo na Frank hadi nyumbani kwake, na Frank akawaita Safina na Musa kuwatambulisha kwao.

    SHANGAZI: Poleni sana watoto wazuri jamani.

    MUSA na SAFINA: Asante bibi.

    SHANGAZI: Si halali kabisa kumnyang'anya mtoto wa marehemu urithi wake, Frank wazijua sheria msaidie Safina kupata kilicho chake.

    FRANK: Najitahidi kutafuta wakili atakae saidia ila mambo yanabana sana.

    SHANGAZI: Kila mtu ana haki hata kama ni mtoto.

    Waliongea mengi na walifurahi sana kumjua mtoto wa Frank na wakapanga kufanya sherehe ya kumkaribisha Musa kwenye ukoo wao kwani walimuona kama vile mwanampotevu.



    Baada ya wiki, familia ya Frank wakafanya sherehe ya kumualika Musa kwenye familia hiyo, ilikuwa ni siku ya furaha sana.

    Frank akaitwa na dada zake,

    MWASITI: Inabidi uoe sasa kwani ushakuwa mtu mzima kaka.

    FRANK: Unanishauri nimuoe nani?

    MWASITI: Nani mwingine zaidi ya Suzy!!

    ESTA: (Akadakia), kwakweli kwa mimi hapana hata sikushauri umuoe Suzy.

    FRANK: Kwanini dada yangu?

    ESTA: Frank, tafuta mwanamke anayekwenda na wakati, unajua Suzy ana mambo ya kishamba sana!!

    MWASITI: Acha zako Esta, wewe mjanja mbona hujaolewa? Mwache kaka amuoe Suzy.

    ESTA: Ili azidi kumrundikia mitoto ya kuokoja.

    MWASITI: Kwanza hiyo mada ya watoto ilishaisha.

    ESTA: Ila na mimi ni mawazo yangu, sipendi kaka amuoe Suzy.

    Wakagombana sana ikabidi Frank awaamulie.

    FRANK: Acheni ujinga jamani, leo ni siku ya furaha.

    Frank hakufurahishwa kabisa na ule ugomvi kwani yeye ndiye wa kuamua kuwa atamuoa nani.



    Frank akatafakari sana na kweli akagundua kuwa umri wake umeenda na anahitajika kuoa kweli.

    FRANK: Suzy nahitaji tujihalalishe kabisa.

    SUZAN: Kivipi Frank?

    FRANK: Nataka tufunge ndoa Suzy.

    SUZAN: Kweli Frank?

    FRANK: Ndio hivyo Suzy au wewe unaonaje vipi??

    SUZAN: Mi niko tayari Frank.

    Frank akafurahi sana na kumkumbatia Suzan.

    Tatizo la watu wengine ni vie kuingilia mambo yasiyo wahusu.



    Frank aliamua haswa kufunga ndoa na Suzy na ndicho kitu alichofanya, akaamua kumuoa Suzy ili wawe mke na mume kwa uhalali kabisa. Harudi yao nzuri ilifanya sana, huwa MC hakosei pale anaposema wenye wivu wajinyonge kwani anajua wazi kuwa kuna watu wenye wivu mahali hapo.

    Baada ya ndoa, shangazi wa Frank akamfata Frank na kuzungumza nae.

    SHANGAZI: Mwanangu sasa sina ubaya ila nina jambo zuri tu.

    FRANK: Jambo gani hilo?

    SHANGAZI: Napenda kuwaona wewe na Suzy mkiwa na furaha, ila watoto wengi namna ile hamuwezi kuwa na furaha nakwambia.

    FRANK: Sasa shangazi unataka nifanyeje? Lakini kuwafukuza hapana.

    SHANGAZI: Hapana, sina nia kwamba uwafukuze, ila nakushauri kama unaweza wale watoto wapeleke shule ya bweni ili wawe wanalala huko huko hiyo pia itaimarisha ndoa yako.

    FRANK: Mmh shangazi!!

    SHANGAZI: Najua unapata shida kunielewa maana yangu, ila ukifanya hivyo utatambua. Wawe wanakuja kukaa kipindi cha likizo tu, itakusaidia sana Frank.

    FRANK: Gharama za hizo shule za bweni je?

    SHANGAZI: Usijari utapata msaada tu, ila fanya hivyo kwanza.

    FRANK: Sawa shangazi nitafikiria.

    Frank akafikiria sana kuhusu ushauri aliopewa na shangazi yake, na kujisemea kuwa anatakiwa aufanyie kazi. Akakumbuka matukio ya ugomvi wa wale watoto mule ndani ambapo kuna siku alimkuta mmoja kamshikia kisu mwenzie akimtishia kumuua, akafikiria sana na kuona kwamba itakuwa ngumu kwa yeye kuwalea watoto hao hapo kwake, ni bora wakakae shule ambapo watakuwa karibu sana na walimu katika kuwaangalia na kugundua matatizo madogo madogo waliyonayo na kuyatatua. Akaona wazo la kuwapeleka shule za bweni ni nzuri sana.



    Frank akaamua kuwaita watoto wote wa mule ndani na kuwaambia kuwa wanatakiwa kusoma kwa makini sana, kwahiyo ameamua kuwatafutia shule za bweni. Nao wakafurahi sana kwani waliona kubanwa sana wanapokaa mule ndani bila kujua kama shuleni ndio kubanwa zaidi.

    Akawapeleka shule tofauti tofauti, hakutaka kuwapeleka wote shule moja, alifanya hivyo ili na wao wapate uelewa unaotakiwa.

    Kwahiyo wote wakapelekwa shule za bweni kasoro Safina na Musa.



    Modesta alikuwa ni mtu mwenye mawazo sana na alijiuliza mambo mengi baada ya kugundua ukweli halisi, kwani ulimsaidia kuwagundua ndugu zake kuwa ni watu wa aina gani, jinsi walivyo na roho za kinyama.

    "kwakweli hawa wanaweza kuniua hata mimi jamani, roho zao si za binadamu wa kawaida."

    alijisikia vibaya sana moyoni, akamkumbuka sana marehemu baba yao na jinsi alivyokuwa anaongea kuwa watoto wake hao ni watu wakatili, kwasasa ndio Modesta ameelewa kuwa ukatili wa ndugu zake hao uko wapi.



    Suzan akapata ujauzito na kufanikiwa kujifungua watoto wawili mapacha waliowaita Jeni na Jerry.

    Walifurahi sana kuwapata watoto hao, ilikuwa ni furaha kubwa kwenye familia.

    Safina alitamani sana kwenda kumtembelea madam Lucy ila alimngoja mamake mdogo ili waende wote kumtembelea.

    SAFINA: Mama, naona Jeni na Jerry wamekua sasa. Kwanini tusiende kumtembelea madam Lucy?

    SUZAN: Unahitaji kumuona?

    SAFINA: Ndio, nahitaji kuongea nae.

    SUZAN: Basi sawa tutaenda kesho kutwa.

    Siku ilipofika Suzan na Safina wakajiandaa na kwenda kumuona madam Lucy, na walipofika kule wakakutana na kitu ambacho hawakukifikiria kabisa.



    Siku ilipofika Suzan na Safina wakajiandaa na kwenda kumtembelea madam Lucy. Na walipofika kule wakakutana na kitu ambacho hawakukitarajia kabisa kwani waliona kama vile kutakuwa na ugeni mwingine kwenye nyumba hiyo, Lucy aliwakaribisha kwa furaha sana. Baada ya salamu akawakaribisha vizuri sana.

    LUCY: Karibuni sana jamani, kwakweli leo nimekuwa mtu mwenye bahati sana.

    SAFINA: Bahati ya nini madam??

    LUCY: Yani nyie mmekuja kunitembelea na wale wanafunzi wangu nao wamekuja kunisalimia na kuniaga.

    SAFINA: Wanataka kurudi ulaya? Kwani washajua kiswahili?

    LUCY: Wanataka kurudi ulaya ndio, yani wamejua kiswahili kabisa.

    SUZAN: Kumbe wewe ni mwalimu bora sana, hadi watu wanaelewa duh!!

    Wote wakacheka na kufurahi, huku madam Lucy akiendelea kuwakaribisha sebleni.

    Walipofika sebleni, wakakaa kwanza ili kupata utambulisho vizuri.

    LUCY: Karibu sana jamani, ngoja niwatambulishe kwa wageni wangu.

    SUZAN: Itakuwa vizuri sana.

    LUCY: Jamani hawa ndio wale waliokuwa wakijifunza lugha kiswahili kwangu, hapa kuna Joseph, Chuck na Blenda.

    Safina akawa anawaangalia kwa makini huku akitafakari anayoyaona kwani hakuamini amini.

    LUCY: Jamani na huyu anaitwa Safina ni......

    Kabla hajamaliza Blenda alipatwa na mshangao kwani muda wote alikuwa kamkazia macho Safina na kujiuliza ni yeye au sio yeye.

    BLENDA: Safina?

    LUCY: Yes, Safina. Mbona unashangaa Blenda??http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    BLENDA: Safina Samwel?

    Blenda aliuliza kwa mshangao, hadi Safina akashtuka na kutambua kuwa kweli anamuona ni Blenda na amemkumbuka vilivyo kwani ndio jina ambalo huwa anatumia, jina la Safina Samwel.

    SAFINA: Ndio mimi ni Safina Samweli, nilikutana nawe Germany na USA.

    BLENDA: Yes, i know you.

    Wakakumbatiana kwa furaha, ndipo Blenda akawaambia Joseph na Chuck kuhusu Safina. Na wote wakajikuta kumkumbuka na kumkumbatia kwa furaha. Wakajikuta wakijadili mambo mengi na kumuuliza maswali mengi kuwa kwanini hakutokea kwenye lile tamasha kubwa.

    CHUCK: Nilikutafuta sana Safina ili nikuombe msamaha kwani ni mimi niliyecrush gari yenu ukiwa wewe na mama yako pale supermarket.

    SAFINA: Usijari Chuck yashapita hayo.

    JOSEPH: Tulikungoja sana Safina kwenye ile tamasha but hukuja.

    BLENDA: Kweli Safina tulikungoja sana, whats happen to you??

    Safina akajaribu kuwaelewa kwa muhtasari kilichomfanya ashindwe kurudi tena Marekani na kushindwa kuhudhuria lile tamasha.

    BLENDA: Pole sana Safina.

    SAFINA: Namuhitaji prof. Mike ndio msaada wangu kwa sasa.

    BLENDA: Safina, we promise you. Tutafanya the best as we can hadi tumpate prof. Mike.

    Wakamuahidi Safina kwa kila hali kuwa watamsaka Mike hadi wampate ili wamweleze kama Safina mwenyewe alivyowaambia.

    Walifurahi sana kuongea na Safina siku hiyo, ikabidi na waagane mahali hapo kwani wakina Blenda walishajiandaa kwaajili ya Safari kwa kesho yake. Wakampa matumaini makubwa sana ya kuonana na prof. Mike na wote wakawa wenye furaha.

    Ilikuwa ni siku njema sana kwao kwani hata uwanja wa mazungumzo waliutawala wao wengine walibakia kucheka pa kuchekesha na kuhudhunika pa kuhudhunika.



    Waliporudi nyumbani, Safina alikuwa na furaha sana, tena sana.

    SAFINA: Mamdogo, unajua mimi kukutana na wale watu kunanipa matumaini makubwa ya kukutana na anko Mike.

    SUZAN: Kwani wanajuana nae?

    BLENDA: Anko Mike anajulikana sana kwahiyo ni rahisi wao kumjua.

    SUZAN: Inamaana huyo Mike ni mtu tajiri sana?

    SAFINA: Ana uwezo ndio tena ni mwanasheria anayetambulika na wengi.

    SUZAN: Utafurahi kuonana nae eeh!!

    SAFINA: Nitafurahi sana kwani nitapata mwangaza mpya wa kushughulika na hawa ndugu zangu walionitesa. Nawachukia sana.

    Waliongea mambo mengi sana. Kipindi chote ambacho Safina ameanza kukaa hapo, muda mwingi Frank alikuwa akitumia kujua ukweli wa mali zote za Safina, ila kwa mali alizozijua alikutwa zimeshauzwa. Yeye alijua nyumba na maduka makubwa mawili aliyoacha Sam ila vyote vina wamiliki wapya.

    Aliporudi alimuita Suzan chumbani na kuzungumza nae.

    FRANK: Suzy, unajua kitendo cha kvotambua mali alizoacha marehemu kinatupa shida kujua urithi halali wa Safina.

    SUZAN: Naelewa Frank, kazi ni ngumu sana. Sijui itakuwaje?

    FRANK: Unajua Safina aliachwa akiwa mdogo sana. Na sasa miaka kama nane imepita bila ya kushughulika na chochote.

    SUZAN: Naelewa hilo swala ila haki ya mtu ni yake tu.

    FRANK: Halafu wale ndugu zake wameuza kila kitu jamani.

    SUZAN: Hivi wamewezaje kuuza kila kitu? Walikuwa na hatimiliki kweli?

    FRANK: Sidhani, kwanza Sam alikuwa ni mtu msomi bhana halafu tajiri. Inawezekana alikuwa na mwanasheria wake wa kujitegemea.

    SUZAN: Inawezekana, tatizo Safina hamjui yoyote hapa nchini zaidi ya huyo mzungu walieishi nae Marekani.

    FRANK: Ni haki yake kutokumkumbuka wa huku, alienda Marekani akiwa mdogo sana ndiomana anamjua huyo huyo.

    Wakamuita Safina na kumuuliza tena, nae akawatajia huyo huyo Mike anayeishi Marekani ikabidi wakubali tu kumngoja huyo Mike kwani Safina aliwahakikishia kuwa huyo Mike akipata habari zake lazima atafika tu.



    Siku moja Safina na Musa wakaenda kuwatembelea wenzao kwenye hizo shule za bweni, siku hiyo wakaifanya maalum kwa matembezi hayo tu.

    Na kila walipowatembelea hao wenzao walionyesha kumshukuru sana Frank kwa wema aliowafanyia.

    TIZO: Sikutegemea kabisa kama nitasoma mwenzenu, hii imekuwa furaha kwangu, ingawa wenzangu wananiona kuwa nimekuwa mtu mzima ila nitasoma tu niweze kupata mwangaza wa maisha.

    MUSA: Ni kweli Tizo, madarasani wanatuona kuwa tumewazidi umri ila tusikate tamaa, tusome tu ili tuweze kutoa ujinga.

    MIRIUM: Kwakweli kamanda Frank ametufuta machozi na ujinga.

    TIZO: Uzuri ni kuwa katuahidi kila mmoja kumsomesha fani aipendayo, ni furaha sana kumfahamu mtu huyu.

    Wote walifurahia na kumsifia kamanda Frank.

    Musa na Safina wakarudi nyumbani, wakamsikia Frank akizungumza na Suzan.

    FRANK: Unajua inaniuma sana kuona tunashindwa kumsaidia Safina kwenye mali zake.

    SUZAN: Tatizo ni kuwa tutampataje huyo Mike!!

    FRANK: Hapo pa kumpataje ndio mtihani.

    Mara Safina akaingilia mazungumzo yao,

    SAFINA: Mmenisaidia sana jamani hata Mungu mwenyewe anaona, iliyobaki ni kumwachia yeye kwani ndiye mtatuzi wa matatizo yetu.

    SUZAN: Inaonyesha umekata tamaa mwanangu.

    SAFINA: Pengine lakini najua ipo siku moja Mungu atamshuhudia anko Mike hata kwa ndoto ila sijui ni lini, ninachojua atakuja tu.

    SUZAN: Ila usikate tamaa mwanangu.

    SAFINA: Naelewa mama, ila niliwapenda sana wazazi wangu kupita chochote ulimwenguni, ni bora wangechukua mali zote na kuniachia wazazi wangu.

    SUZAN: Usijari, Mungu atakulipia.

    SAFINA: Natambua hilo, kama ni ni huyu Mungu ninayemuomba kila siku ndiye muumba vyote basi haki itapatikana.

    FRANK: Pole sana ila yote yataisha.

    SAFINA: Chozi langu mimi Safina najua limefika kwa Mungu naye atawahukumu hawa ndugu zangu.

    Kwakweli Safina alikuwa akiwasikitisha na maneno amcyo aliongea, walimuhurumia sana.



    Modesta akaona afanye uwezekano wa kukutana na Suzan ili aweze kumuona Safina. Ilimbidi aende kwenye hospital ambayo Suzan alimuelekeza, kufika pale hospital hakumkuta Suzan, akaelekezwa na kwenda kuzungumza na rafiki wa Suzan ambaye ni Pendo, naye akamwambia siku ya kwenda ili ampeleke anapoishi Suzan.

    Siku ilipofika Modesta alifika kwa Pendo na kumkuta Pendo ameshajiandaa kwahiyo wakafanya safari ya kwenda kwa kamanda Frank. Walipofika wakamkuta Suzan na kufurahiana sana, naye akawakaribisha ndani, ile Safina kumuona Modesta tu akakimbilia chumbani na wote wakamshangaa, kwakweli Safina hakuwataka kabisa ndugu wa baba yake.

    Suzan akaongea nao mambo mengi, Modesta akamuomba Suzan akamuitie Safina japo amsalimie kidogo tu.

    Ikabidi Suzan aende chumbani aliko Safina ili kumshawishi akamuone shangazi yake.

    SAFINA: Siwataki siwataki kabisa ndugu wa baba.

    SUZAN: Safina usifanye hivyo jamani, Modesta hana nia mbaya.

    SAFINA: Siwataki kabisa ndugu wa baba, wote ni sawa. Sitaki kuwaona. Suzan akajitahidi sana kumshawishi ila Safina akagoma kabisa.

    Ikabidi Suzan arudi tu sebleni na kumueleza Modesta.

    SUZAN: Amekataa kabisa Mode.

    MODESTA: Usijari Suzy, ipo siku ataelewa kuwa sina nia mbaya.

    Kwakweli Modesta aliumia sana kwa kupata hukumu ya vitendo vya nduguze ila akajisemea hatokata tamaa.

    Akamuaga Suzan na kuondoka na Pendo waliyeenda naye.



    Blenda na wenzie walipofika Marekani ikabidi wafanye kile walichomuahidi Safina.

    Ikabidi Blenda aende kumuulizia Mike, akaelekezwa nyumbani kwa Mike. Kwahiyo akaamua kwenda, ila alipofika akaambiwa kuwa Mike hayupo pale na sehemu ambayo ametajiwa kuwa yupo ilimsikitisha sana.



    Ikambidi Blenda aende kumuulizia Mike, akaelekezwa nyumbani kwa Mike na kuamua kwenda huko. Ila alipofika nyumbani kwa Mike akaambiwa kuwa hayupo pale, mahali alipotajiwa kuwa yupo palimsikitisha sana.

    Kwani aliambiwa kuwa Mike amelazwa kwa muda mrefu sana.

    Blenda akawaambia mwenzake habari hiyo. Basi wakaenda huko kwenye hiyo hospitali waliyoelekezwa.

    Kwakweli hali ya prof. Mike haikuwa nzuri hata kidogo kwani alikuwa amepalalaizi.

    Wakamweleza kila kitu lakini kwa hali ile hakuwa na uwezo wa kufanya kitu chochote zaidi ya kufanyiwa, kwahiyo kukawa hakuna kitu chochote cha kumsaidia Safina kwani prof. Mike mwenyewe alikuwa hajitambui.



    Safina alikuwa ni mtu wa kusikitika sana kwa kipindi hicho kwani ni muda mrefu ukawa umepita bila kupata taarifa yoyote kuhusu prof. Mike.

    SAFINA: Ni mwaka sasa tangu wakina Blenda waondoke lakini sijapata taarifa yoyote.

    MUSA: Usijali Safina kwani mvumilivu hula mbivu.

    SAFINA: Nakubaliana na wewe Musa ila siwezi kusahau mambo yote waliyonitendea ndugu zangu. Yaani wamenifanya nijute kuwa na ndugu kama wale.

    MUSA: Yote ni mipango ya Mungu Safina.

    SAFINA: Ndio nakubali kuwa yote ni mipango ya Mungu, lakini kwanini mimi? Kwanini Safina? Inamaanisha watu wote duniani hawajaonekana ila Safina pekee ndiye aliyeonekana kuwa anastahili kupata adhabu hii, maana hii ni adhabu kwenye maisha yangu.

    Kwakweli Safina alikuwa anaona kuwa ni mtu anayeonewa sana kwenye maisha yake. Tangu wazazi wake wafariki anaona kuwa maisha yake hayana muelekeo mzuri. Ingawa anaishi na Frank lakini moyo wake unaumia sana hasa akikumbuka alivyofukuzwa na ndugu zake.

    Safina akabaki akimuomba Mungu tu ili amsaidie katika maisha yake.

    "Nakuomba Mungu wangu unisaidie kwani wewe ndiye msaada pekee nilio nao. Ulikuwa nami toka hapo mwanzoni hadi leo hii naamini uko nami maana hamtupi mja wako. Endelea kuwapa moyo bamdogo Frank na mamdogo Suzy wa kuendelea kunilea mimi kwani mimi ni mzigo wao sasa. Pia nakuomba umwezeshe anko Mike popote pale alipo asikie kilio na sauti yangu, kama ni mgonjwa basi malaika wako wakashughulike naye ili apone. Wewe ndiye msaada wangu na kimbilio langu, nionyeshe mlango wa kutoke. Amen!!"

    Alimaliza kuomba na kumshukuru Mungu, kumbe alipomaliza kuomba tu ndio wakati huo huo prof. Mike alipata uwezo wa kuamka kitandani, watu wote walimshangaa kwani ilikuwa ni kitu cha ajabu sana, walishapoteza matumaini ila ni kweli Mike aliamka siku hiyo na kuweza kuinuka. Kweli ulikuwa muujiza, hapo inaonyesha jinsi gani imani hufanya kazi.



    Prof. Mike akafanya mazoezi ya hapa na pale na baada ya siku kadhaa akaweza kuwa mzima kabisa.

    Akapata ruhusa na kurudi nyumbani kwake.

    Blenda akaamua kwenda tena hospitali lakini akaambiwa kuwa prof. Mike ameshatoka na alikuwa mzima wa afya njema. Kwakweli alifurahi sana kusikia hivyo, ikabidi afunge safari na kwenda nyumbani kwa prof. Mike ili amweleze kikamilifu kuhusu Safina.

    Alipofika akamkuta prof. Mike, kwakweli Blenda alifurahi sana, ikabidi aanze kujitambulisha kwake na kumueleza kila kitu kuhusu Safina.

    Mike alishangaa sana kusikia yote hayo, akamwambia Blenda kuwa itabidi aende nae ili kumsaidia Safina.



    Safina aliendelea kumuomba Mungu bila kuchoka. Na alikuwa akiwashukuru sana wanaomlea.

    SAFINA: Mamdogo, naona faraja sana kuwa na ninyi hapa.

    SUZAN: Usijari ni jukumu letu kukulea.

    SAFINA: Maisha ya mtaani ni magumu tena magumu sana, uyasikie tu kwa watu kwani kule mvua yetu, jua letu, pa kulala shida, pa kupumzika hakuna na chakula vilevile kukipata ni bahati nasibu.

    SUZAN: Acha kufikiria sana ulikopitia iliyobaki ni kusonga mbele.

    Suzan alipenda sana kumfariji Safina ili asijione kuwa mpweke.

    Musa nae alikuwa akimsifia Suzan mara nyingi anapoongea na Safina.

    MUSA: Tangu mama yangu alipokufa sikudhani kama nitakuja tena kupata mapenzi ya mama. Lakini huyu amekuwa kama mama yangu mzazi yani ananipenda, ananilea na ananitunza.

    SAFINA: unajua mamdogo Suzy ana moyo wa kipekee sana.

    MUSA: Kweli kabisa, nimekuwa nikiteseka mitaani zaidi ya miaka kumi.

    SAFINA: Kwani mama yako alikuacha na umri gani?http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MUSA: Miaka mitano, toka nikiwa na umri huo nimeweza kujua maisha ni kitu gani.

    SAFINA: Pole sana Musa, mie miaka michache niliyokaa mtaani nimeweza kuuona ugumu wa maisha. Je wewe uliyekaa zaidi ya miaka kumi!! Dah.

    MUSA: Machozi na maombolezo yangu na mambo yote mabaya niliyoyapitia sasa yamefutwa na furaha na amani niliyoipata hapa nyumbani.

    SAFINA: Kwakweli tumshukuru Mungu kwa kutuondoa kwenye lile jana.

    MUSA: Nitamshukuru Mungu milile kwani nilijua yale ndio maisha yangu daima.

    Kwakweli Musa alikuwa na furaha sana kwa upendo alioupata toka kwa Suzan.

    Suzan alikuwa ni mwanamke mfano wa kuigwa kwani alijua kuwa wale watoto wanahitaji faraja ndiomana akazidi kuwapenda sana na sana.

    Kwakweli mateso na vilio vya watoto wale vilizimwa na furaha aliyonayo.





    ITAENDELEAPseudepigraphas

0 comments:

Post a Comment

Blog