Simulizi : Sitasahau Tanga
Sehemu Ya Tano (5)
Tukafika mahali kuna nyumba ila ukiziangalia ni kama vichuguu, nikaingizwa chumba cha kwanza humo nilikuta maji yakitokota kwenye pipa kubwa na yule aliyenipeleka akaniamuru nidumbukie kwenye lile pipa ila nikasita huku nikiomba msamaha, ila wala haikusaidia nilimshuhudia yule mtu akinibebea juu juu na kunitumbukiza kwenye hilo pipa linalochemka maji kwakweli nilijua hapo ndio
Nikawa nimenyong'onyea kupita maelezo, nikaanza kujisogeza pale alipo yule mtu mwenye panga. Huku nikizidi kutetemeka.
Nilipofika pale nikajilaza chini yani tayari kwa kuchinjwa, nikashangaa muda unapita bila ya kusikia panga likipita kwenye shingo yangu, mara gafla nikashikwa kichwa kugeuka nakutana uso kwa uso na mwanamke mrembo sana, akaniamuru niinuke pale machinjioni nami nikainuka akaniamuru nimfate nami nikafanya hivyo.
Nilienda naye mpaka kwenye chumba ambacho hakikuwa na kitu chochote ndani, akaniuliza,
"unajua kwanini nimekuleta humu?"
Nikatikisa kichwa nikiashiria kwamba sijui sababu ya mimi kuwa humo, mara gafla yule mwanamke akayeyuka na kupotea nikabaki peke yangu kwenye kile chumba.
Nikawa natetemeka kwani chumba chenyewe hakikueleweka mara kiwe na rangi nyekundu mara blue mara nyeusi ila ilikuwa ikija rangi nyeusi mule ndani kunatisha sana.
Nikiwa bado sijielewi elewi akaja yule binti wa kitanga na kuanza kuniongelesha,
BINTI: Je unajutia kuwa na mimi?
Nikaonyesha ishara ya ndio kuwa najutia.
BINTI: Unadhani unaweza kuniepuka maishani mwako?
Sikujua kama nikubalia au nikatae nikabaki kutoa macho tu.
Akanishika mkono nikatoka nae nje, akanipeleka mahali kwenye dimbwi ila dimbwi hilo lilijaa damu, akaonyesha kwa kidole,
"umeona juisi ninayopenda?"
Nikatikisa kichwa kuwa nimeona, basi akanishika mkono na tukarudi tulipotoka, akaniambia,
"nataka ukaniletee ile juisi ninywe"
Akanikabidhi kikabu nikabebee ile juisi, akanionyesha ndoo iliyokaribu nae kuwa niijaze, sikuweza kuhoji zaidi ya kubeba kile kikapu hadi kwenye lile dimbwi, nikataka kuchota nikakutana na tangazo,
"HAIRUHUSIWI KUANGUSHA HATA TONE MOJA CHINI"
Nikawaza sasa nitabebaje na kile kikapu maana kila nikikijaza na kukiinua juu damu ile ambayo ilikuwa nyepesi kama maji ilimwagika.
Nikaamua kurudi na hata kikapu nikakiacha hapo kwa kuogopa kuangusha hayo matone.
Nilipofika kwa yule binti akachukia sana,
"mbona hujaleta nilichokuagiza?"
Nilimuangalia tu na ukizingatia mahali hapo sikuwa na uwezo wa kuzungumza, gafla mambo hapo hapo yakabadilika kwani nikajikuta nipo peke yangu sehemu yenye giza nene sina pa kwenda wala kupapasa wakati nashangaa hayo mara kukabadilika tena nikamuona mmama mbele yangu akipika chakula ila mkono wake ndio aliutumia kama mwiko wa kupikia chakula, nikawa nimetoa macho naye akaniuliza,
"unashangaa nini? Jishangae wewe unaetaka kujitoa kafara mwenyewe"
Bado nilikuwa nikishangaa laiti kama ningekuwa na uwezo wa kuongea hapo ningesema mengi.
Nikamwona yule mama akiwa makini na kazi zake na wala hakuogopa moto, akaniuliza,
"unahitaji chakula?"
Nikaitikia kwa kichwa kuwa nahitaji, akaenda na kuniletea sinia ambalo limejaa minyoo, mmh nilipatwa na kinyaa cha ajabu huku nikijisemea moyoni mmh hadi minyoo ni chakula! Sikuweza kula kwakweli.
Yule mama akawa anacheka sana, akaniuliza tena,
"unapapenda huku?"
Nikatikisha kichwa kuashiria kuwa kule sipapendi, yule mama akacheka sana, na akauliza tena
"unataka kurudi ulipotoka?"
Nikaonyesha ishara kuwa nahitaji kurudi, akaniambia tena,
"nikuonyeshe njia?"
Nikaonyesha ishara ya ndio. Akauliza tena,
"je utaweza kukwepa vishawishi?"
Nikaonyesha ishara kuwa naweza, akachukua yale mavitu anayopika na kunimwagia usoni, nilihisi kama vile sura inatoka, maumivu niliyoyapata hayaelezeki nilijikuta nikigalagala chini kama mtoto mdogo. Nililia sana huku yule mmama akicheka sana.
Maumivu yalipopungua yule mmama alinishika mkono na kunipeleka mpaka pale kwenye dimbwi la damu akaniamuru ninawe ile damu usoni nami nikafanya hivyo kuja kushtukia nilijikuta nipo kwenye chumba na yule mdada mrembo aliyeniokoa kwenye kuchinjwa.
Nikiwa naye mule ndani, akawa ananifanyia visa kama vile mwanamke afanyavyo mitego kwa mwanaume kwakweli sikutamani hata mwanamke wa aina yoyote, alifanya vitu vingi ila nilimwangalia tu.
Akanisogelea na kuniuliza,
"unanienda au hunipendi?"
Nikabaki nimemkodolea macho tu hata nisijue cha kumwambia. Naye akazidi kuniangalia nahisi alikuwa akiipima akili yangu, akaniuliza tena,
"unanipenda?"
Nikamwangalia tu, nikaamua kutikisa kichwa nikiashiria simpendi, mara yule mdada akageuka kuwa joka kubwa, nikaanza kuogopa na kukimbia, nikakimbia sana ila kila nikiangalia nyuma lile joka nalo lilizidi kunikimbiza, nilikimbia hadi nguvu ziliniishia nikaanguka kuangalia naona lile joka limekuwa na vichwa saba tena likizidi kunikaribia.
Nikiwa nimechoka kukimbia, nikaanguka chini na lile joka likanisogelea karibu kabisa nilikuwa natetemeka sana.
Lilipofika karibu yangu likabadilika tena na kuwa mwanamke mzuri sana tena mwenye kuzidi mvuto na urembo kushinda yule wa kwanza, nikawa naogopa sana, yule mwanamke akanishika mkono na kunisimamisha, akaniangalia sana kisha nae akaniuliza tena kwa sauti ya kubembeleza,
"vipi mimi unanihitaji?"
Nikawa nimetoa mimacho na kutikisa kichwa, gafla niliona yule mwanamke amegeuka na kuwa simba nikaanza kukimbia tena yani nilikimbia sana, ila nikigeuka nyuma naona ni bonge la simba likinikimbiza.
Nilizidi kukimbia ila mbele nikakutana na mto ile wakati nauvuka nikiwa nimejawa na uoga tela nikajikwaa na kuanguka chini ila niliangukia jiwe kubwa kwahiyo nikapoteza fahamu.
Kwa matumaini yangu nilijua nikishtuka pale basi nitakuwa duniani yani kwenye ardhi yenye watu wa kawaida kama mimi.
Ila niliposhtuka nilijikuta nimewekwa kitandani tena nimevuliwa nguo zote na kubaki mtupu kabisa, pembeni yangu alikuwepo mwanamke mrembo sana nae akiwa mtupu kabisa alikuwa ananipaka vitu kama mafuta ya maji ila ni malaini sana, akawa ananisiliba na kufanya kama vile ananikandakanda mwili mwangu. Mmh nikawa natetemeka sana, nikamwomba Mungu anipe ujasiri mkubwa kwa wakati huo tena ikiwezekana basi niwe kama mwanaume asiye na nguvu za kiume tena.
Yule mwanamke alizidi kunikandakanda kwa mtindo wa kupapasa mwili wangu, alishuka hadi sehemu zangu za siri, nilizidi kutetemeka tena niliogopa sana ni kweli sikupatwa na hisia zozote kwa wakati ule najua Mungu alinisaidia.
Yule mwanamke kuona kuwa hata sionyeshi dalili yoyote ya mshtuko wa hisia akachukia sana, akaanza kunifanyia mambo ya ajabu ajabu hata hayafai kuelezea, nilikuwa kama kifaranga cha kuku kilichoachwa na mamaye, kwakweli nilikuwa mpweke na mwenye huzuni kubwa.
Yule mwanamke akaniamuru niinuke pale, nami nikainuka, akiwa vile vile mtupu akatangulia mbele ili nimfate nyuma, nilijitahidi kukwepesha macho yangu maana haya macho haya ndio yanayotutia majaribuni vijana wengi sana.
Nikaongozana nae hadi kwenye kisima, kile kisima kilikuwa cha maajabu kwani maji yake yalikuwa yakitokota sana.
Nikiwa nae pale kisimani, akaniuliza,
"unanihitaji?"
Nikazidi kutetemeka mahali pale, nikawa nimemkodolea macho tu, akasema tena,
"nijibu, unanihitaji?"
Niliogopa kujibu kwani nilijua wazi ni jambo gani lingefatia, nilizidi kutetemeka, yule mwanamke akanikazia macho kuashiria kuwa anahitaji jibu, nami nikatikisa kichwa kuashiria kuwa simuhitaji, akachukia sana na pale pale akanitumbukiza kwenye kile kisima kwakweli niliiva tena sana nilitokota kama vile napikwa ili niliwe, nililia mule kisimani hadi nikapoteza tena fahamu.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kuja kushtuka nilijikuta nipo Tanga tena eneo lile lile ambalo nilikutana na yule binti, na tena mbele yangu alikuwepo yule yule binti wa kitanga.
Akanishika mkono na kunipeleka eneo lile lile ambalo mimi na yeye tulikuwa tukikutana na kupiga story nyinginyingi, nikawa natetemeka kwani sikujua ni nini anachotaka kunifanyia.
Alikuwa na mkoba, mara akatoa boxer kwenye ule mkoba wake, akaniuliza
BINTI: Unaikumbuka hii? (akinionyeshea ile boxer).
MIMI: (Nikashangaa gafla nimepata uwezo wa kuongea), ndio naikumbuka.
BINTI: Uliiacha wapi?
MIMI: (Nikijaribu kuvuta kumbukumbu ya sehemu nilipoiacha ile boxer).
BINTI: Hakikisha uwe sawa na majibu utakayo toa kwani jibu lako linaweza kukuokoa au kukuangamiza, na pia usinipe jibu la kubuni nataka jibu la ukweli na uhakika. Ninazo hapa kama hizi tano na zote ni za kwako kwahiyo uwe na majibu ya uhakika.
Nikawa nimemtumbulia mimacho tu huku nikifikiria cha kumjibu.
Nikiwa sina kumbukumbu nzuri juu ya ile boxer nikawa nimetoa macho tu hata nisijue cha kujibu. Akaniuliza tena,
BINTI: Inamaana hukumbuki uliiacha wapi?
MIMI: (Nikiwa nasua sua cha kujibu), eeh ndio sikumbuki.
BINTI: Unamkumbuka Penina?
MIMI: (Nilishtuka sana na hata sikujua huyu binti wa kitanga amemjulia wapi Penina), aah eeh ndio namkumbuka.
BINTI: Haya niambie unamkumbuka kivipi?
Hapo nikakumbuka wazi kuwa ile boxer niliisahau kwa Penina, nikamwambia yule binti wa kitanga kuwa nimemkumbuka penina sababu ya ile boxer.
BINTI: Kwanini uliacha hii boxer kwa penina?
MIMI: Penina alikuwa mke wa mtu, siku hiyo hatukujua kama mumewe anarudi katika purukushani ya kukimbia baada ya kufumaniwa ndio nikasahau boxer yangu.
BINTI: Nini kilifuata baada ya kufumaniwa?
MIMI: Penina alifukuzwa na mumewe na hivyo akaja kwangu na kudai kuwa ana mimba yangu kwa kuogopa msala na mimi nikamfukuza.
BINTI: Je unajua kilichompata Penina baada ya wewe kumfukuza?
MIMI: Hapana sijui.
BINTI: Penina alilazimika kwenda kutoa ile mimba na huko ndiko akapatwa na umauti. Je nikikupa lawama juu ya kifo cha Penina nitakuwa nimekuonea?
MIMI: (Nikiwa nimetumbua mimacho tu kama mtu nisiyejielewa), aaah mmh sijui.
BINTI: Na kwanini ulitembea na Penina wakati ulijua ni mke wa mtu? Je ulikuwa na lengo la kumuharibia ndoa yake?
MIMI: (Bado nilijiumauma wala sikuwa na jibu la moja kwa moja).
Yule binti wa kitanga aliniangalia kwa macho makali sana hadi nikaanza kuogopa, akaingiza mkono tena kwenye mkoba wake na kutoka na boxer nyingine, akaniuliza tena.
BINTI: Na hii je uliiacha wapi?
MIMI: (Nikiwa na mshangao mkubwa kuwa amezipata wapi zile boxer, ambazo hata mimi mwenyewe sina kumbukumbu ya mahali nilipoziacha. Nikabaki kutumbua mimacho tu.), mmh sijui.
BINTI: Unamkumbuka Aisha?
MIMI: Ndio nimemkumbuka, hiyo boxer niliiacha kwake wakati baba yake ametubamba kwahiyo nilivyokimbia nikaisahau.
BINTI: Baada ya wewe kukimbia nini kilifuata?
MIMI: Aisha alikuja nyumbani na kudai kuwa ana mimba yangu kwavile sikutaka makubwa ikabidi nikimbie ila hata niliporudi sikupata tena habari zake.
BINTI: Haya, Aisha naye alienda kutoa ujauzito wako ili arudi kwao akiwa mtoto safi kwa bahati mbaya umauti ukamshika. Je na yeye hujasababisha wewe kifo chake?
MIMI: (Nikiwa natetemeka kuwa vipi mimi nikawa vile hadi hao wakapatwa na umauti).
Nikiwa natafakari, akatoa tena boxer nyingine,
BINTI: Na hii uliiacha kwa Nana, naye alikuwa mke wa mtu. Kwanini uliiacha?
MIMI: Niliogopa mumewe angenifumania.
BINTI: Sasa boxer hii ndio ilimfanya Nana apigwe na mumewe hadi mauti ikampata. Je nimlaumu mume au wewe?
MIMI: Hata sijui kitu.
BINTI: Siku zote hujui kitu, inamaana wewe hutambui uyafanyayo?
MIMI: Natambua.
BINTI: Je adhabu ulizopata umeonewa?
MIMI: Hapana sijaonewa.
Akaingiza tena mkono kwenye mkoba,
BINTI: Na hii uliiacha kwa Salma kwanini?
MIMI: Salma alikuwa ni demu wa rafiki yangu ili mwenyewe asigundue katika harakati nikaiacha hiyo boxer.
BINTI: Unajua kilichofuata?
MIMI: Rafiki yangu alipoikuta, Salma akamwambia ukweli ila Salma alipokuja kwangu nikalazimika kumtimua kwani sikutaka kugombana na rafiki yangu sababu ya mwanamke.
BINTI: Na Salma alikosa mwelekeo akanywa vidonge na kujiua kwaajili yako.
MIMI: (Nikiwa nashangaa sana, kwani sikujua kama Salma alijiua kwaajili yangu).
BINTI: Mabinti wengi wametoa mimba kwaajili yako na hiyo ni sababu tosha ya mimi kwenda kuivuruga mimba ya demu wako wa dar.
MIMI: (hapo ndio nikaelewa kwanini mimba ya demu wangu wa dar ilitoka), haaa kumbe!!
Akaingiza mkono tena na kutoa boxer nyingine,
BINTI: Hii pia uliiacha kwa Tamari, niambie kuhusu Tamari.
MIMI: Tamari alikuwa ni rafiki wa demu wangu, nakumbuka ni yeye alinilazimisha niache boxer kwake.
BINTI: Vipi alipokwambia anaujauzito wako?
MIMI: Nilijua ni mbinu zake za kuniachanisha na mpenzi wangu, kwahiyo nikamkana.
BINTI: Naye akaenda kutoa mimba na kufa. Je unajua kwanini wasichana wengi wanakufa wakienda kutoa ujauzito wako?
MIMI: Hapana sijui.
BINTI: Nitakwambia sababu.
Akaniangalia na kunikazia macho sana, safari hii alitoa boxer na kuongea kwa ukari,
BINTI: Katika boxer zote na matendo yake machafu, hii ndio boxer iliyonikera na ndiyo itakayofanya upate adhabu tena.
Akainuka na kuniambia kuwa nimuandalie majibu yanayoeleweka juu ya ile boxer. Bado sikujielewa kwanini nilikuwa naacha zile boxer na kwanini ziniletee matatizo kila sehemu nilipo ziacha. Na bado nikajiuliza kwanini hao wadada walikufa wakati wanatoa ujauzito wangu, bado sikuwa na jibu ila nikangoja majibu kwa huyu binti wa kitanga ambaya hadi muda huo sikuelewa ni jini au ni mchawi au ni mzimu au ni mtu wa aina gani kwani bado alinichanganya sana.
Nikiwa sijielewi elewi kabisa na huku nikijiuliza maswali mengi mengi.
Yule binti wa kitanga akarudi na kunishtua,
BINTI: Haya niambie ni wapi uliacha hii boxer?
MIMI: Samahani, niliacha kwako kwa bahati mbaya.
BINTI: (Akacheka sana), bahati mbaya! Ulikuwa na maana gani?
MIMI: Sikuwa na maana yeyote ile nilijisahau tu.
BINTI: Ulijisahau tu au ulitaka kuonyesha jinsi gani wanipenda?
MIMI: Aaah mmh sijui.
BINTI: (Akacheka tena), kwahiyo hukunipenda?
MIMI: Naam!
BINTI: Kwani nimekuita au nimekuuliza, kwahiyo hukunipenda?
MIMI: Mmmh Sijui.
BINTI: Wewe una matatizo sana, yani hujui kama ulinipenda au la?
MIMI: Mmmh ndio sijui.
Akaniangalia kwa macho makali sana kama vile anasoma kitu kwenye ubongo wangu. Nikawa na mawazo ya uoga kichwani mwangu, akanigeukia na kuniuliza tena.
BINTI: Unamjua Leila?
MIMI: Ndio namjua.
BINTI: Eeh kwanini ulimdanganya yeye na familia yake kuwa unaenda kutoa mahari?
Nikabaki natoa mimacho tu na kushangaa huyu binti ameyajuaje yote hayo, maana nilipokuwa na Leila nikapenda niwe nae karibu zaidi kwahiyo nikaenda kupeleka barua kwao ili nitambulike ila ilipofika kipindi cha mahari hapo ndio utata ulianza maana sikuwa na jinsi zaidi ya kuwadanganya kuwa nitaenda ila nikawapotezea. Nikashangaa sana huyu binti amejuaje.
Akaniuliza tena,
BINTI: Kwanini hukumfatilia tena Leila?
MIMI: Ujana tu ndio ulinisumbua dada.
BINTI: Heeee, nishakuwa dada yako tena?
MIMI: Mmmh aaah sijui.
Akacheka sana na kuniangalia kwa dharau,
BINTI: Haya unajua kwanini wanakufa wakitoa mimba zako?
MIMI: Sijui chochote.
BINTI: Wanakufa kutokana na zindiko ulilofanyiwa ukiwa mdogo, mama yako ukimuuliza atakwambia.
MIMI: Mmmmh
BINTI: Je unajua hatma ya Leila ilikuwaje?
MIMI: Sijui.
BINTI: Leila alichanganyikiwa sana kwa aibu uliyompa kwao, akaamua kujiua. Tatizo umetembea na wanawake wengi ndiomana ukimwacha mmoja humfatilii tena.
Bado nikawa sijielewi na mawazo lukuki juu ya huyu binti wa kitanga.
Akaniambia nimuulize swali nitakalo.
MIMI: Vipi mchumba angu wa dar, je ni mzima?
Akacheka sana, kisha akaniambia nimfuate. Nikainuka na kuanza kumfuata, mara gafla nikamuona Leila amesimama mbele yangu, nikaanza kutetemeka na kuogopa sana, nikiwa sijielewi nilistukia nikichapwa viboko kila sehemu. Mbele yangu alikuwepo Leila na yule binti wa kitanga, nilichapwa sana hadi nikapoteza fahamu.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliposhtuka nilikutana na giza nene yani sioni chochote cha mbele yangu. Nilipoinuka mahali pale, nikaanza kutembea kwa kupapasa ila kila nilipokanyaga nilikanyaga mwiba kumbe pale chini palijaa miba mitupu.
Kwahiyo ikanipasa kutembea kwa tahadhari, nilipofika mbele nikakutana na yule binti wa kitanga, akaniambia "njoo huku" nikawa namfata, kufika mbele gafla akatokea binti mmoja niliyemjua kwa jina la Salma, huyu alikuwa ameshika gongo kubwa sana akanibamiza nalo kichwani, nikaanguka na kupoteza fahamu.
Kuja kushtuka nilikuwa kwenye mto mkubwa tena katikati, nilitetemeka sana mwili ulipatwa na baridi ya ajabu, nikaogopa sana pale katikati ya mto.
Nikaanza kujikongoja taratibu ili niweze kutoka kwenye ule mto, wakati nafika juu yani nimeshatoka mtoni akatokea mtu na kunisukuma tena gafla mtoni nikawa natapatapa na kuhangaika, kumwangalia vizuri yule mtu ni yule binti wa kitanga, nikabaki natahamaki na nikaamua kumuuliza.
MIMI: Je hizi ndio adhabu zangu?
BINTI: (Akacheka sana), hapana hapa tunacheza tu kama kombolela, adhabu yenyewe ni moja tu utaipata.
Nikanyong'onyea gafla kwani mwili wote ulikuwa una niuma yani kila sehemu ni maumivu tupu.
Nikawa natetemeka sana ndani ya ule mto na yule binti wa kitanga alizidi kunicheka pale juu.
Nikaanza tena kujitoa kwenye ule mto, nikajitahidi kutoa na kujikongoja tena hadi juu, nikawa namfata yule binti wa kitanga cha kustaajabisha akatoweka, nikaanza kuogopa na hofu kubwa ikanitanda moyoni. Mara mvua kubwa ya gafla ikaanza kunyesha, nikaamua kukimbilia mti uliokaribu ili nijikinge na ile mvua, nilipofika pale chini ya mti, mara upepo mkubwa ukaanza kuvuma na kusababisha ule mti kudondoka, nilitoka mbio na kuwa mbali na ule mti wakati unaanguka.
Mvua nayo iliendelea kunyesha tena kwa wingi kabisa, nikawa kama mnyama porini, nilitetemeka sana na hata nisijue cha kufanya kwani nilikuwa natembeatembea bila uelekeo wa maana, mvua iliendelea kunyesha na kufanya nizidi kutetemeka kwa baridi.
Mara gafla likaanza kuwaka jua kali sana tena lile jua la kuchoma utosini, nikazidi kushangaa na kustaajabu.
Mbele yangu ikatokea nyumba, nikaanza kujiuliza mbona ile nyumba sikuiona mwanzoni. Nikaamua kuisogelea ile nyuma na kujaribu kubisha hodi ila hakuna aliyeniitikia.
Nikaamua kuingia ndani hivyohivyo, nikakutana na mbibi akiwa anaota moto hata nikamshangaa kwa jua lile anaotaje moto, ikabidi nianze kwa kumsalimia
MIMI: Bibi shikamoo.
BIBI: Marahaba, nilijua tu ukiona nyumba utakuja.
MIMI: Na mbona unaota moto wakati kuna joto?
BIBI: Unajua mara nyingine inabidi tufanye vitu kinyume chake, usipende kuishi kwa mazoea.
MIMI: Kivipi bibi?
BIBI: Ndio kama hivi, mimi naota moto wakati ni joto. Wewe umezoea nini maishani?
MIMI: Nimezoea maisha ya kawaida bibi.
BIBI: Kwahiyo maisha unayoishi sasa ni ya kawaida?
MIMI: Hapana, naona majanga tu.
BIBI: Najua mambo yameenda kinyume, hukutarajia jambo hili. Ngoja nikwambie.
MIMI: Niambie bibi.
BIBI: Siku zote katika maisha unapofanya jambo kinyume huwa linaumiza wengine, au mimi sikuumizi wewe hapa ninavyoota moto wakati ni joto?
MIMI: Kweli naumia bibi.
BIBI: Basi unapofanya jambo kinyume na ukalizoea linakuwa kawaida ingawa linawaumiza wengine, ndio hivyo na wewe unapopatwa na kinyume cha uliyozoea lazima utaumia. Umejifunza nini hapo?
MIMI: Nimejifunza kuwa kinyume nilichofanya mazoea ndio kimekuwa kinyume changu sasa.
BIBI: (Akacheka), unapenda wasichana wazuri na wakuvutia, kila uwaonapo macho yako hayakuishi hamu. Mjukuu wangu, hii ni Tanga, mji mzuri wenye matunda ya kupendeza na mabinti wazuri.
MIMI: Unamaana gani bibi?
BIBI: Nina mabinti wengi sana tena ni wazuri sana kazi yao ni kuwapata vijana wenye tamaa kama nyie.
MIMI: (Nikiwa nimetoa mimacho tu), sielewi bibi.
BIBI: Damu za wengi zimekulilia wewe ila mabinti zangu wanafanya kazi nzuri sana kwani mwanaume yeyote mwenye tamaa kama yako awaonapo lazima ashtuke. Ngoja nikuitie watano uwaone.
Yule bibi akanyosha mkono juu kama ishara ya namba tano, mara wakatokea mabinti wazuri sana na wenye mvuto wa kipekee, nikabaki kuwaangalia tu.
BIBI: Unamtaka yupi kati yao?
MIMI: Hapana bibi sihitaji mwanamke yeyote.
Yule bibi na wale mabinti wote wakacheka sana halafu wale mabinti wakatoweka.
BIBI: Sogea karibu nami ili tuote moto vizuri, (huku akiendelea kuchochea kuni zake).
Nikawa nasita kuusogelea moto ule, akaniamuru tena nimsogelee pale. Duh kufika karibu ni kama jehanamu ndogo maana ule moto unaunguza taratibu mmh!! Yule bibi akaniangalia, yani ingawa ni mzee ila alionyesha kuwa na sura nzuri sana. Akaniuliza,
BIBI: Unajisikiaje sasa?
MIMI: Naungua bibi.
BIBI: Basi hii ni raha ya kufanya vitu kinyume mjukuu wangu.
Nikabaki nikimwangalia yule bibi na hata nisimmalize, mara akachukua glasi na kumimina kitu ndani yake na kunikabidhi,
BIBI: Karibu maziwa mjukuu wangu.
MIMI: (Nikapokea huku nikiangalia na kustaajabu), bibi mbona hii ni damu?
BIBI: Mbona unakuwa si muelewa mjukuu wangu? Nimekwambia kuwa hapa tunafanya vitu kinyume, sasa unashangaa nini kunywa!
Nikiwa bado nimeishika ile glasi na kuendelea kutafakari, mara yule bibi akasema,
BIBI: Na usistaajabu utakapotakiwa kutembelea kichwa badala ya miguu, (akacheka sana).
Bado nilikuwa kama mtu niliyepigwa na bumbuwazi bila ya kuwa na majibu na pale ule moto ulizidi kunichoma tu.
Mara yule bibi akainuka ila akawa anatembea kinyumenyume huku akicheka, na akarudi akitembea kinyumenyume vilevile.
BIBI: Hata ukitaka kuyarudia maisha ya kawaida utakubidi utembee kinyumenyume hadi utakapofika.
MIMI: Nionyeshe njia basi bibi.
BIBI: Kunywa maziwa kwanza.
Akatoa na bakuri na kunikabidhi,
BIBI: Tafuna na hizo karanga, ni tamu sana na hayo maziwa.
MIMI: Jamani bibi, mbona ni mavi ya mbuzi?
BIBI: Jifunze kuwa muelewa utashinda.
Nikawa nimeshika kile kibakuli chenye mavi ya mbuzi na ile glasi yenye damu hata nisielewe nakula vipi vitu hivi.
BIBI: Unapotumia kitu kinyume na wewe fanya kinyume chake utajikuta umekizoea na kuona cha kawaida.
MIMI: Jamani bibi, ndio nile mavi ya mbuzi na damu kweli?
BIBI: Bora ule maana nitakapokuletea maji ya kunywa hapa ushushie utakuwa umepata uzoefu kidogo.
MIMI: Khaaaa kama damu ndio maziwa na mavi ya mbuzi ndio karanga je hayo maji ni nini?
BIBI: (Akacheka sana), na hata nikikwambia hiyo damu ni damu gani utazidi kupagawa ni kheri ule ushibe hicho nilichokuandalia.
Bado maswali mengi yaliniandama, je hii damu ni damu ya nini? Bado sikupata jibu nikawa najipanga kumuuliza huyu bibi aniambie ukweli vyovyote vile sina jinsi.
MIMI: Samahani bibi, niambie hii ni damu ya nini?
BIBI: Unataka kujua kweli?
MIMI: Ndio nataka kujua bibi.
BIBI: Kunywa kwanza nikwambie.
Bado moyo wangu ulisita kunywa ile damu na kula yale mavi ya mbuzi.
Nikawa bado naiangalia ile damu na kuitafakari, bibi akaendelea kuniamuru kuwa ninywe.
BIBI: Uzima wako upo humo, ni bora unywe tu kwa hiyari yako.
Nikajaribu kunywa ile damu ila kinyaa kilizidi kunishika.
Bibi akaniangalia kwa jicho kali sana na kusome.
BIBI: Nimeshakwambia unapokula vitu hvyo weka kinyume chake utaona ni kawaida tu. Narudia tena, uzima wako upo humo.
Ikabidi nifanye kama alivyosema kuwa damu ni maziwa na mavi ya mbuzi ni karanga. Ila nikala kidogo tu na kumrudishia,
MIMI: Asante bibi nimeshiba.
BIBI: Hapana, hutakiwi kubakisha unatakiwa umalize vyote na kikombe ukilambe kuonyesha kuwa umeridhika na ladha yake.
MIMI: Bibi ila vimenishinda kwakweli.
BIBI: Hiyo ni lazima ule, yani utake usitake. Je ungependa nikwambie hiyo damu ni ya nini?
MIMI: Ndio niambie.
BIBI: Mwanamke akiwa kwenye siku zake huwa anatoa uchafu, na uchafu huo huwa kwenye mfumo wa nini?
MIMI: Huwa ni damu.
BIBI: Basi hiyo ni damu ya mwanamke akiwa kwenye siku zake.
MIMI: Aaargh mbona umenipa uchafu jamani?
BIBI: (Akacheka sana), haya kunywa sasa.
MIMI: Hapana, siwezi kunywa uchafu.
Mara yule bibi akanipulizia kitu, nikawa kama nimepumbazika nikajikuta nikiyala yale mavi ya mbuzi na kuinywa ile damu, ila nilipomaliza tu nikawa kawaida, nilitamani kutapika kabisa yani.
Mara akanipa glas nyingine na kuniambia,
BIBI: Chukua na maji ya kunywa ushushie.
MIMI: (Yani ile kuangalia hadi kichefuchefu), jamani bibi mbona ni mate tena yamechanganyika na makohozi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
BIBI: Inakupasa unywe na hapo utajifunza kuona kinyaa cha yale uliyoyafanya.
MIMI: Aaah bibi, siwezi kunywa mate kwakweli.
Akanifanyia kama mwanzo, nikajikuta nikinywa ile galsi yenye mate hadi kuimaliza, halafu nikawa kawaida. Yule bibi akawa ananiangalia na kusema,
BIBI: Kuna juice pia inapaswa unywe, ngoja nikupe.
Akachukua glasi na kunikabidhi.
MIMI: Loh bibi jamani ndio usaha kweli?
BIBI: Ndio, kunywa juisi hiyo.
MIMI: Siwezi bibi yani ninywe usaha kweli dah!
Akafanya kama mwanzo, na ule usaha nao nikanywa. Mara gafla nikaanza kuumwa na tumbo hadi nikawa nalia na kugalagala chini, yule bibi alikuwa akicheka sana, na mimi nilizidi kuugulia.
Wakati nalia vile, wakaja wasichana wazuri na kunizunguka mahali pale, kwakweli sikuona hata uzuri wao kwa maumivu yale ya tumbo, niliugulia sana na hakuna aliyenisaidia.
Baada ya kuugulia kwa muda mrefu, bibi akanipa glasi na kuniambia.
BIBI: Kunywa hii ni juisi ya machozi itapoza maumivu yako ya tumbo.
Kunywa machozi haikuwa shida kwangu kwani nilishakunywa vingi visivyonywewa, nikaichukua ile glasi ya machozi na kunywa, ilikuwa ina ladha kama ya chumvichumvi hivi. Nilipomaliza kunywa tu na yale maumivu yakakatika.
BIBI: Unajua kwanini umeumwa na tumbo?
MIMI: Sijui bibi.
BIBI: Kwasababu ulikuwa unakataa kula chakula chetu.
MIMI: Nahitaji kurudi kwenye maisha ya kawaida, nirudisheni tafadhari.
BIBI: Unadhani ni kazi rahisi?
MIMI: Sijui kwakweli.
BIBI: Je unaweza kuifanya jana kuwa leo?
MIMI: Siwezi.
BIBI: Lazima ifanyike kazi ya ziada ili uwe kawaida na si kinyume tena.
MIMI: Basi bibi nisaidie.
Bibi akaniangalia tu, mara akawaita tena wale mabinti wa tano.
BIBI: Chagua mmoja uwe nae kila utakapokwenda.
MIMI: Hapana bibi, sitaki mwanamke.
BIBI: Sasa wewe unataka nini?
MIMI: Nataka niwe kwenye maisha ya kawaida.
BIBI: Ngoja uone kwanza.
Akanionyesha mahali kwenye watoto wengi wakilia na mahali pengine wanawake wengi wakilia. Halafu akaniuliza.
BIBI: Upande upi unaonyesha huruma zaidi?
MIMI: Pande zote zaonyesha huruma ila zaidi Ni ule upande wa watoto.
BIBI: Umewaonea huruma watoto, ni sawa kabisa. Na kwanini hukupenda kuwahurumia wakiwa tumboni ili nao watoke wakiwa kama wewe?
Nikakaa kimya kwani sikuwa na la kujibu.
Bibi yule akanichukua na kunifungia kwenye chumba, kile chumba kilikuwa na sisimizi na siafu wengi nao wakaning'ata sana hadi vidonda vikanijaa. Baada ya muda akanifungulia na kuniuliza,
BIBI: Umejisikiaje wakati wale wadudu wanakung'ata?
MIMI: Nimeumia sana na maumivu yake hayaelezeki.
Akachukua majivu na kunipaka mwilini, huku akiniambia,
BIBI: Ukitaka tusiendelee kukufatilia fata kile watachokwambia.
MIMI: Nitafanya vyote bibi, sitapuuza hata kimoja.
Akachukua na damu nayo akanipaka mwili mzima, kisha akasema,
BIBI: Umependeza sana mjukuu wangu.
Nikabaki namtazama tu huku macho yangu yamejawa na huruma tupu na yakionyesha kuwa nahitaji msaada na kuhurumiwa.
Kufumba na kufumbua, sikuwa tena kwenye ile nyumba na wala yule bibi hakuwepo ila nilijikuta niko peke yangu chini ya mti, cha kushangaza ule mti ulikuwa na mdomo na macho. Nilitetemeka sana. Kila nilipouangalia nao ulinichekea, nikatetemeka sana mahali pale na kuanza kurudi kinyumenyume, wakati nafanya hivyo uli mti ulikuwa ukizidi kucheka huku nao ukinifata. Kwakweli mkojo ulinitoka, wakati narudi vile kinyumenyume kuna kitu nikakigonga kwa nyuma kwa haraka kabisa nikageuka na kuangalia, Mungu wangu, alikuwa mtu mrefu sana mbele yangu sikuweza hata kumtazama, akachukua mkono wake na kushika shingo yangu huku akinining'iniza juu juu nikawa natetemeka huku ninalia sana.
Alichokifanya sasa ni kunitupa toka kule juu hadi chini, na hapo hapo nikapoteza fahamu.
Kuja kushtuka, Mungu wangu sikutegemea nilichokiona mbele yangu.
Sikutegemea nilichokiona, niliposhtuka nikajikuta nipo kitandani, nikamwona mpenzi wangu akiwa pembeni yangu pale kitandani, nikawa nashangaa shangaa tu.
Nikamwona yule mpenzi wangu akifurahi sana kuwa nimeamka na akaharakisha kwenda nje, kurudi ndani akawa ameongozana na yule mdada aliyekuja na mke wa rafiki yangu, yule mdada mwenye maruhani.
Nikawa bado nashangaa shangaa tu. Bado sikuelewa kitu, nikazidi kushangaa shangaa tu. Kitu cha kwanza kabisa nikawaambia,
MIMI: Naombeni maji ya kunywa.
Kabla sijajibiwa, mara simu yangu ikaanza kuita muda ule ule niliposhtuka, nikawa napapasa ili niipokee, mara yule mdada wa mwanzo akaniamuru nimpatie ile simu, nilipompatia akaniambia,
MDADA: Hii ndio imekusababishia mambo yote.
Nikashangaa kivipi simu imenisababishia mambo yote yale. Na alipoichukua yule dada ile simu ikaacha kuita.
Kwanza nikawa sielewi wala siamini kama nipo kwenye ulimwengu wa kawaida. Nikaanza kuwashangaa tu yule mdada na mpenzi wangu, huku nikijiuliza maswali mengi mengi imekuwaje wakawa pamoja na wengine wako wapi. Pia nikashangaa kile chumba kwani kilikuwa ni chumba tofauti kabisa na chumba changu.
MIMI: Mbona humu sio chumbani kwangu? (huku nikizidi kushangaa).
MDADA: Ipo sababu kubwa ya kukuondoa mule kwenye chumba chako.
MIMI: Mbona sielewi?
MDADA: Ndio huwezi kuelewa mpaka utakapoeleweshwa.
MIMI: Niambieni kwanza, nipo dunia ya kawaida au dunia ya kinyumenyume?
MDADA: (Akacheka), upo kawaida, na upo salama sasa. Ila usalama wako utaongezeka pale utakapoamua kuinuka hapo ili twende baharini ukaoge maji ya bahari, na hii simu(akionyesha ile simu yangu aliyoshika), tunaenda kuitupa baharini.
Sikuweza kubisha wala kupinga, nikainuka pale nikiwa mimi yule mdada na mpenzi wangu. Tukakodi kibajaji kikatupeleka hadi baharini.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Kufika pale baharini, nikajishangaa nimekuwa mzito sana kuitupa ile simu, nikajikuta nikisita kufanya hivyo. Yule mdada akaniambia,
MDADA: Unapenda kuishi maisha ya kawaida?
MIMI: Ndio napenda.
MDADA: Basi tupa hiyo simu.
MIMI: Ila simu yangu ni ya gharama sana jamani.
MDADA: We itupe tena uirushe mbali kama unayapenda maisha yako, nitakupa sababu ya kufanya hivyo.
Roho iliniuma sana kila nikiangalia ile simu, nilizidi kuumia moyoni. Yule mdada akaniangalia tena kwa macho makali na kusema,
MDADA: Tupa hiyo simu.
MIMI: Ujue nilinunua laki tano hii simu!
MDADA: Haya, laki tano na maisha yako kipi bora?
MIMI: Bora maisha yangu.
MDADA: Basi itupe hiyo simu.
Bado nikawa nasitasita, nilimtazama mpenzi wangu naye aliniangalia kwa jicho la huruma sana, nikapatwa na mfadhaiko wa moyo nikakumbuka yote niliyowatenda wadada kwa tamaa zangu. Nikakumbuka mateso niliyopata kwenye dunia ya kinyumenyume.
Hapo nikaamua kuchukua maamuzi magumu na kuirusha ile simu katikati ya maji, mara gafla nikashtuka,
MIMI: Aaah laini yangu!!
MDADA: Imefanyaje?
MIMI: Nimeitupa nayo.
Kabla hajaniambia kitu tena mara gafla tukaona moshi mwingi ukitokea pale nilipoirusha ile simu, nikaanza kutetemeka kwa uoga. Yule dada akaniambia kuwa niingie kwenye maji ili niweze kujisafisha zile nuksi na mabalaa. Ila bado sikujua wale ndugu niliowaacha ndani ni nini kimewapata, je ni wazima au wamekufa, nikaamua kumuuliza yule dada,
MIMI: Na ndugu zangu je ni wazima au wamekufa?
MDADA: Hilo swali niulize baada ya kujisafisha ndio nitakupa jibu. Nikamwangalia tena yule mpenzi wangu bado alionyesha huruma sana na hata sikumwelewa kuwa ananihurumia mimi au anaonyesha huruma ya nini.
Nikaangalia tena pale nilipoirusha simu yangu bado palikuwa panafuka moshi.
Yule mdada akaniamuru tena kuwa niende kwenye maji nikaoge, ila nikawa nasita kufanya hivyo na yule mpenzi wangu alizidi kunyong'onyea na pia alizidi kuonyesha huruma.
Nikaamua kwenda kuoga hayo maji ya bahari, yule dada akanielekeza sehemu ya kwenda kuoga ilikuwa ni mbali kidogo na pale nilipoitupa ile simu yangu na pia akanionya kuwa nisifike pale nilipoitupa simu yangu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikiwa ndani ya maji ya bahari, wazo likanijia kuwa nisogee karibu zaidi na nilipoitupa ile simu labda nitaiona tena.
Nikawa nimesogea karibu huku nikiwa kama naogelea kumbe najaribu kupapasapapasa, ili kama nikiipata basi niitoe ile laini yangu tu. Mara gafla maji yakawa ya moto sana mule baharini hadi yakawa yananiunguza, wakati nataka nikimbilie nchi kavu, nikakuta kuna mtu amenishika bega kwa nyuma ile kugeuka ni macho kwa macho na binti wa kitanga, amefikaje na anataka nini sijui.
Nilipogeuka nyuma nikakutana macho kwa macho na binti wa kitanga, nilianza kutetemeka kwa hofu na uoga, akawa ananiangalia huku anacheka nikazidi kutetemeka. Nilipoangalia kule nchi kavu nilimwona yule mdada akininyoshea mkono kama ishara ya kuniita, nikawa najitahidi nitoke ila yule binti wa kitanga alining'ang'ania na hadi nafika nchi kavu yeye alikuwa nyuma yangu.
Yule mdada akaniuliza tena kwa ukali,
MDADA: Umefanya vitu gani wewe?
MIMI: Sijui.
MDADA: Hujui nini? Unadhani angekufuata huyo bila sababu?
MIMI: Naomba nisaidie basi, nilienda kule nilipoitupa ile simu.
MDADA: Yani wewe umeharibu kila kitu.
Nikamwona yule dada akichukua kiwembe na kuja karibu yangu, akanichana kwenye mkono, nilipatwa na maumivu makali akanizuia kusogea popote mpaka pale aliponichana pakikauka damu.
Nikiwa naugulia yale maumivu, nikamwona yule dada akienda pembeni na kuongea kitu na mpenzi wangu, mara wote wakanisogelea pale.
Nikamwona yule dada akichukua tena kiwembe na kumchana mpenzi wangu mkononi halafu akachukua ile damu iliyokuwa inamtoka mpenzi wangu na kunipaka shingoni halafu yeye na yule mpenzi wakasogea mbali.
Kwa muda mchache nilihisi kama nataka kukata roho kwani maumivu yaliyonipata pale shingoni yalikuwa makubwa sana, hadi nikajikuta nikianguka kwenye maji na kuanza kutapatapa.
Ninachokumbuka nilipoteza fahamu.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliposhtuka nilijikuta nipo nyumbani, nimelala kwenye jamvi na wote ninaowafahamu wakiwa wamenizunguka, hadi yule mdada nilimwona pale kasoro mpenzi wangu tu ndiye hakuwepo pale.
Wote niliwakuta wamefurahi na nilikuwa kama mtu niliyepoteza dira.
Wakaniacha nipumzike bila kuniuliza chochote.
Baada ya siku mbili, ikabidi niongee nao kwani nilikuwa sielewi chochote.
MIMI: Mama mbona sielewi chochote, ilikuwaje kwani?
MAMA: Ni vigumu kuelezea ila umetufanya kupata majeraha yasiyosahaulika kamwe.
MIMI: Na kile chumba changu imekuwaje mama?
MAMA: Kile chumba tulikirudisha kwa mwenye nyumba kwani ungeendelea kukaa pale kungekuwa na makubwa zaidi.
MIMI: Ila mama, inaniwia vigumu kukuelewa.
Basi mama akamwita yule mdada ili nipate kuzungumza naye pia.
MDADA: Sikia, janga ulilolipata ni kubwa sana. Mimi nisingeweza kukusaidia ila babu yangu ni mtu wa huko na anajua vitu vingi.
MIMI: Kwahiyo watu walioanguka chumbani kwangu, waliamkaje?
MDADA: Kuna dawa niliwapaka wakaamka, ile dawa iliwezakufanya kazi baada ya wewe kukubali kujitoa kafara.
MIMI: (Kuna kitu nikajifikiria na kuamua kuuliza), mbona wakati nipo kwenye ulimwengu usio wa kawaida simu yangu sikuiona halafu niliposhtuka kawaida ikaanza kuita?
MDADA: Simu yako haikuwa simu ya kawaida, yule dada alikubadilishia simu muda mrefu sana ndiomana kila jambo ulilotaka kufanya ukiwa na ile simu aligundua kwa haraka.
Nikawa nawaza amebadilishaje, na mbona nilikuwa naiona kawaida.
MIMI: Ila ndugu zangu ni wazima?
MDADA: Ndio ni wazima ila...
MIMI: (Nikadakia), ila nini na yuko wapi mpenzi wangu?
MDADA: Ndio huyo ninayetaka kumuongelea.
MIMI: (Huku mapigo ya moyo yakienda mbio), kafanyaje?
MDADA: Amejitoa kwaajili yako.
MIMI: Sikuelewi, unamaanisha nini?
MDADA: (akainamisha kichwa chini na kuniambia), kwa bahati mbaya tumeshindwa kumwokoa kwahiyo amekufa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilihisi utumbo ukijisokoto na tumbo likaanza kuniuma gafla.
MIMI: Hapana hapana sitaki kuamini.
MDADA: Huo ndio ukweli.
Niliona machozi yakinitoka, nilijisikia vibaya kujua yule msichana ambaye ni mpenzi wangu amekufa kwaajili yangu. Roho iliniuma sana.
Wakawepo watu pale kunifariji na kunipa moyo. Nikajiona nimepata kovu ambalo sitalisahau tena.
Rafiki yangu akaja pale na kunipa moyo.
RAFIKI: Pole sana ila yote ni mapito tu.
MIMI: Asante ila nimeumia sana.
RAFIKI: Hata sisi hatuelewi, na je sikuzote ulizopoteza fahamu ulikuwa wapi? Maana yule dada alituambia kwamba upo eneo la hatari sana.
MIMI: Ni kweli tena yalikuwa majanga sana ila ninachoweza kusema hadi sasa ni kuwa SITAISAHAU TANGA.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment