Search This Blog

NABII WA UONGO - 1

 







    IMEANDIKWA NA : HAKIKA JONATHAN



    *********************************************************************************





    Simulizi : Nabii Wa Uongo

    Sehemu Ya Kwanza (1)



    Anga jeusi lilitanda huku harufu kali ya moshi wa viwandani ulipenya vilivyo katika matundu mawili ya pua yangu, lakini sikuweza kujali karaha hiyo bali niliendelea kusukuma mkokoteni wangu  uliojaa taka mbalimbali za soko kuu la Kariakoo na kwenda kutupa dampo kuu la jiji. Nikiwa nimekata tamaa na maisha yangu magumu niliyokuwa naishi, huku jua kali la kila siku la  Dar es salaam likiwa sehemu ya maisha yangu, ghafla nilishangaa kuona prado nyeusi ikipaki pembeni ya mkokoteni wangu, na kunifanya niwe na hofu, kwani kioo cha gari kilishushwa na mzee mmoja aliyekuwa akiendesha gari lile aliweza kuniita kwa kutumia ishara ya mikono yake. “Pole sana kijana wangu kwa kazi nzito ,kazi ngumu sana ya kimaskini isiyo na kipato, lakini unaweza kuwa bilionea kama ukipenda, chukua bisinesi kadi yangu utanitafuta nikusaidie “,mzee yule alizungumza na kuahidi kunisaidia, na kufanya uso wangu kutabasamu kwa furaha kwani nilikua nimechoshwa na maisha ya kifukara niliyokuwa naishi. “Asante sana mzee wangu, mungu akubariki, nakuahidi nitafanya kazi hiyo kwa nguvu zote, nimechoshwa na maisha haya ya kulala njaa kila siku “,niliongea kwa furaha sana huku nikipokea bisinesi kadi pamoja na pesa kutoka kwa mzee yule aliyeonekana kuwa na maisha mazuri sana, na kisha akaliondoa gari lake mbele ya macho yangu na kuniachia maswali mengi kwani si rahisi mtu kukusaidia bila malipo yoyote.



    Kutokana na furaha kunizidi, nilitelekeza mkokoteni wangu kwani pesa niliyopewa na mzee yule ilinitosha sana kwa matumizi ya siku mbili tatu mpaka atakaponipatia kazi, hivyo nilipanda daladala na kisha kuelekea mbagala, sehemu niliyokuwa nimepanga chumba changu kidogo nilichokilipia   shilingi elfu kumi tu kwa mwezi kwani kilikuwa hakina sakafu wala umeme. “Haloo mzee, mimi ni Hakika, kijana msukuma mkokoteni uliyeahidi kunisaidia “,nilijitambulisha huku nikiwa nahamu sana ya kusikia jibu nitakalopewa, baada ya kumpigia simu mzee yule ,nikiwa nyumbani nimejilaza katika kigodoro changu ambacho nilikitandika chini, kwani sikuwa na uwezo wa kununua kitanda. “Ahaa nafurahi sana kama umeweza kunipigia, inaonekana utafanikiwa sana, kesho njoo nyumbani kwangu masaki kisha tutaelekea sehemu kwa ajili ya kukuelezea kazi yenyewe “,mzee yule alinipatia maelekezo na kufanya furaha yangu izidi kuongezeka, kwani maneno yale yalinifanya nizidi kuwa na hamu ya kuwa tajiri. “Mzee huyu anahuruma sana, nikipata kazi mshahara wa kwanza sichukui, itakua ni zawadi yake “,niliongea peke yangu baada ya kukata simu, huku nikibonyeza simu yangu na kuitafuta namba ya mama yangu ili nimfahamishe juu ya mimi kupata kazi ambayo niliambiwa itanifanya kuwa tajiri, bila kujua hatari na madhara makubwa ambayo yalikuwa mbele yangu.



    Usiku ulikua mrefu sana kwani sikuweza kupata usingizi, nikisubili asubuhi ifike niweze kuelekea nyumbani kwa mzee yule, mzee niliyemuona kama mkombozi wangu kwani nilikua sina thamani katika jamii, kutokana na umaskini wangu. “Waoooh hatimae siku yangu ya mimi kuwa bilionea imefika, “niliongea kwa sauti kubwa baada ya mwanga wa jua kupenyeza chumbani kwangu, na kisha kujiandaa haraka sana kuelekea masaki kwa mzee yule, ambaye sikuweza kufahamu kazi yake wala jina lake, zaidi ya kuwa na namba yake ya simu kwani jina lake liliandikwa kwa lugha ya Kiarabu katika bisinesi kadi yake hivyo sikuweza kulielewa.



    …………………………http://deusdeditmahunda.blogspot.com/……



    Mandhari mazuri ya kuvutia, huku nyumba nzuri za kifahari ziliupamba vizuri mtaa wa Masaki, mtaa ambao vigogo na matajiri wakubwa ndiyo makazi yao. Nikiwa nimevalia jinsi yangu pamoja na tisheti, nguo ambazo nilizivaa katika matukio maalumu nilifika nje ya geti ya jengo ambalo nikielekezwa na mzee yule, na kisha kubonyeza kitufe cha kengele kilichokuwa ukutani na bila kuchelewa mzee yule aliweza kutoka nje na kunikuta nikiwa namsubili  “Kijana kumbe ni wewe, nilizani utapotea, nisubili hapa nje nitoe gari yangu tuelekee Bagamoyo ” ,mzee yule aliongea huku akitabasamu, na kunifanya niwe na maswali mengi kwani sikujua kama tutakua na safari ya kutoka nje ya jiji “mmmh kazi gani hii, na Bagamoyo tunaenda kufanya nini?? “,maswali yalikisumbua kichwa changu bila majibu, na kujikuta furaha yangu niliyokuwa nayo ikipungua.



    “Ukikubali na kufata masharti ,kesho tu utakua bilionea “,mzee yule aliyekuwa na ndevu nyingi zilizopakwa dawa na kumpendeza vilivyo, alianzisha mazungumzo baada ya kimya kutawala kwa muda mrefu tukiwa ndani ya gari, lakini maneno aliyonieleza yalizidi kuniongezea maswali kichwani mwangu kwani sikujua kama kuna masharti yalikuwa yakihitajika ili mimi nifanikiwe. “Usjali mzee wangu, nitajitahidi kadri ya uwezo wangu “,nilizungumza maneno yaliyoonekana kumfurahisha mzee yule, huku tukiikanyaga ardhi ya Bagamoyo baada ya dakika arobaini ndani ya gari.



    “Tumefika, hapa ndipo patakuondolea umasikini, hata utajiri wangu niliupatia mahali hapa “,mzee yule alinielezea siri ya utajiri wake, baada ya kuanza kukatiza mitaa mbalimbali ya Bagamoyo iliyokuwa na majengo mengi ya kale. “Kweli mzee, nafurahi kusikia ivo “,niliongea na kutabasamu, huku nikiwa nahamu ya kufahamu kwa undani zaidi jinsi mzee yule aliweza kuupata utajiri wake.



    Tulipaki gari pembeni ya jengo moja ambalo sikulifahamu, na kisha kuingia ndani ya jengo lile lililochakaa sana. Lakini ghafla mapigo ya moyo wangu yaliongezeka na kwenda kasi sana ,kwani nilishangaa baada ya kugundua chumba tulichoingia palikuwa ni kwa mganga wa kienyeji kutokana na mavazi yake pamoja na tunguli zilizokuwa zikining’inia ndani ya chumba kile. “Mungu wangu, nakufa uwiii!!”,,nilipiga kelele na kutaka kukimbia kwani joka kubwa liliinuka na kisha kujiviringisha huku mganga yule akilikalia kwa ajili ya kutusikiliza, lakini kwa upande wa mzee aliyenipeleka hakuweza kuogopa chochote kile na alionekana kupazoea sana mahali pale.



    “Mtukufu nyoka ,huyu ndiye kijana niliyemleta atusaidie kazi zetu “,mzee yule alizungumza huku akipiga magoti mbele ya joka lile, huku mganga aliyelikalia akimminia kichwani damu iliyokuwa katika kichupa kidogo sana. “Asante sana, na utajiri wako utadumu milele “,Joka lile lilizungumza kwa sauti nzito sana na kuzidi kunigopesha ,kwani tangu nizaliwe sikuwahi kushuhudia nyoka akiongea tena kwa kutumia lugha ya kiswahili na kueleweka. Nikiwa nazidi kushangaa, mzee yule alinishika mkono na kunisihi nipige magoti mbele ya joka lile kubwa, lenye vichwa vingi sana ambavyo sikujua idadi yake.



    “Kuanzia sasa wewe ni Nabii Hakika, utafanya kazi ya unabii wa uongo, kupotosha watu wanaomwamini Mungu “,Joka lile lilitamka maneno yaliyobadilisha fikra zangu na kujikuta nikichukia watu waliomtegemea Mungu katika dini zote, huku nikikabidhiwa fimbo, kitambaa cheupe pamoja na maji yaliyokuwa katika kichupa kidogo kutoka kwa joka lile la kutisha pamoja na mganga.. “Nimekubali mtukufu nyoka “,niliongea maneno ya kukubaliana na kazi niliyopewa, huku nikitabasamu bila kujitambua kwani fikra zangu zilikuwa zimefutwa kishirikina bila kujitambua.



    …………………………………



    Kwa muda wa wiki moja tu, jiji la Dar es salaam lilifurika maelfu ya watu kutoka mataifa mbalimbali, kufata huduma ya uponyaji na maombezi katika kanisa langu ambalo niliwezakukusanya mamilioni ya pesa kama sadaka kutoka kwa waumini wangu. “,Ukinywa maji haya, utapona maradhi yanayokusumbua, pamoja na mapepo yote “,niliongea huku nikimnywesha mmoja kati ya maelfu waliokuwa kanisani kwangu, na kumfanya kugaagaa chini akipiga kelele baada ya kunywa maji yale. Huku kelele za shangwe sikisikika kwani nilionekana kama Mungu mtu kwa kutatua shida zao kwa kutumia nguvu za giza nilizokuwa nazo, huku nikitumia maneno machache niliyoyakalili kwenye bibilia kudanganya watu.





    Dar es salaam;



    Ilikua jumapili moja tulivu sana, kama kawaida ya Dar es salaam, joto ndio kama mahali pake. Maelfu ya watu wakiwa wamefurika kanisani kwangu ,kanisa kubwa ambalo nililianzisha mtaa wa Mtoni kijichi _mbagala kuu.,walikanyagana na pengine wengine walisukumana ili wapate nafasi ya kuniona, na kupokea uponyaji.



    Kwa upande wangu, joto sikulihisi kabisa, kwani nilikuwa nimevalia suti nzuri sana na ghali zaidi duniani. Suti hii ilikuwa na air condition ndani yake,na pia ilikuwa na uwezo wa kuzuia risasi, si nyingine bali ni suti aina ya Diamond Armor. Jina ambalo limetokana na madini ya almasi ambayo yamenakishiwa kwenye suti hiyo, na kuifanya iwe ya kupendeza sana.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Karibuni wote katika kanisa langu la Hakika worshiping center …”,nilizungumza kwa sauti yenye kujiamini, huku kila mtu aliyekuwepo mahali pale akipiga makofi mengi sana, makofi yaliyonivimbisha kichwa na kujiona kama mungu mtu kwa wakati ule.



    Kama kawaida yangu siku zote, niliangaza kila kona ndani ya kanisa langu kubwa.Ilikuwa ni kawaida yangu kutazama wanawake wazuri waliofika kanisani kwa ajili ya kupatiwa huduma mbalimbali za maombezi, lakini huduma hiyo niliyoitoa mimi ilikuwa tofauti kabisa na jinsi walivyokuwa wakinifikilia.



    “Na leo watanitambua!, kwa jinsi nilivyopendeza, ndoano lazima inase zaidi ya samaki kumi kwa mpigo hahaahaa “,niliongea moyoni huku nikishika suti yangu na kujishangaa, kusema ukweli suti yangu niliyoinunua kwa dola za kimarekani 3.2M ilinipendeza sanaa na kuonesha utofauti mkubwa uliopo kati yangu mimi na walalahoi waliopata pesa kwa jasho lao, na kuja kunitolea mimi kwani nilionekana kama mtatuzi wa matatizo yao.



    “Swatzirlend wanajua!!, hatimae leo wamenitengenezea suti ya kujidai na kunipa masifaaa”,nilizidi kuongea maneno ya kejeli moyoni, huku nikilifumba jicho langu la kushoto.Ama kweli duniani kuna mambo!, nilimkonyeza dada mmoja aliyekuwa mrembo sana. Weupe wake, umbo lake zuri pamoja na nywele zake nzuri alizosuka kwa mtindo wa kipekee, ni baadhi ya mambo yaliyonifanya niipeleke puta ibada ya siku hiyo, ili tu niweze kupata nafasi ya kuongea nae.



    Kutokana na pesa nyingi nilizokuwa nazo, nilikuwa na uwezo wa kutembea na mwanamke yoyote niliyemtaka ndani ya kanisa langu. Na pengine mume wake akingudua, nilimtupia mamilioni ya pesa mezani na kumziba mdomo, kusema ukweli siri ikabaki kuwa siri, na uaminifu wangu ukazidi kuongezeka.



    Na pia mwanamke yoyote aliyejifanya kushika dini, na kutotaka kumsaliti mume wake, alijikuta analainika pale tu alipokanyaga ndani ya nyumba yangu, nyumba ambayo niliitengeneza pembeni tu ya kanisa langu. Asikwambie mtu! nyumba yangu ilikua ni nzuri sana, japo ilikuwa ni ya ghorofa moja tu lakini madini mbalimbali yaliyotumika kuipamba, yaliifanya ing’are na kupendeza.



    Lakini pia, wale wanawake waliopenda wanaume wenye magari tena mazuri ,ndio wengi ambao niliowakamata, na wakakamatika kwelikweli. Kwani parking yangu ilijaa magari ya kifahari zaidi ya matano, likiwemo  gari zuri aina ya bugatti ambalo mchezaji maarufu wa mpira duniani Christian Ronaldo kalinunua majuzi tu.



    “Ndugu mzee wangu wa kanisa, naomba kaniitie yule dada, nina mazungumzo nae katika ofisi ya mchungaji “,yalikuwa ni maneno yangu niliyoyazungumza baada ya ibada kuisha, niliamua kumtuma mzee ambaye alinisaidia katika kazi mbalimbali kanisani kwa moyo wote bila kutambua undani kuhusu maisha yangu na kazi ya unabii.



    “Sawa mtumishi wa Mungu, tangulia ofisini atakukuta huko ” ,mzee yule alinijibu kwa heshima zote, huku mimi nikimpatia noti kadhaa za shilingi elfu kumi kumi na kisha kuelekea katika ofisi yangu kumsubili dada yule, dada ambaye nilimfanyia kitendo kibaya ambacho mpaka leo ninakikumbuka na kujutia.



    ********



    Jua kali lilizidi kuwaka na kuwakera watu wengi sana,na msichana mrembo Juliet ni mmoja kati ya watu ambao walionekana kukerwa na jua hilo na kuzidi kuongeza joto.



    “Mchungaji ofisi yako ni nzuri sana, nimeingia humu ndani lakini mwili wangu umepoa ghafla “,msichana mrembo Juliet, msichana aliyenifanya nimkumbuke milele kwani ndiye msichana pekee aliyeyabadilisha maisha yangu, aliongea huku akitabasamu mala baada ya kuingia katika ofisi yangu.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Karibu uketi, na ujiskie uko huru, usiniite mchungaji, niite tu Hakika inatosha, sio lazima uweke na cheo changu, mimi ni kijana mwenzako bwanaaa “,niliongea huku nikimtazama msichana yule machoni, na kumfanya ashindwe kujiamini.



    “Kwa nini sasa hutaki kuitwa hivyo, wewe si mchunga………!!”,



    Alitaka kumalizia, lakini mimi nilimkatisha kauli yake kwani niliona kama inanipunguzia maksi za kummiliki msichana yule, aliyesababisha mpaka nikatishe ibada mapema sana kwa ajili yake.



    “Anyway! tuyaache hayo, umeolewa? nilimuuliza swali kwa kumtega kwani kwa wakati huu nilimkazia macho, na kumfanya ashindwe kabisa kujiamini, na kubaki akinishangaa tu, hakuamini kama maswali yale yalikuwa yakitoka kwa mchungaji, tena mtu aliyeniamini sana.



    “Hapana sijaolewa, ndio nimemaliza chuo kikuu mwaka huu wa 2017,lakini mungu akipenda labda nitafanikiwa kuolewa mwakani “,msichana yule alizungumza huku kidole chake cha kushoto akiwa amekiweka mdomoni, na macho yake yakirembua kwani aliweza kuhisi kile kilichokuwa moyoni mwangu.



    “OK…!,nakukaribisha nyumbani kwangu, muda wowote tupate chakula pamoja, na kutafakali maneno ya Mungu, “nilizungumza huku tayali Juliet akiwa ameshika kitasa cha mlango, na kujiweka tayali kwa ajili ya kuwahi nyumbani, kuwapikia chakula cha mchana wazazi wake.



    ********



    Nikiwa nimeketi nyumbani kwangu, jioni ya siku hiyo. Pombe kali za kila aina zikiwa juu ya meza yangu, bila kupoteza muda nilinyenyuka na kuelekea kwenye friji na kuchukua chupa kubwa ya lita moja,  chupa ya maji ya Kilimanjaro.



    Mziki mnene uliendelea kupiga, tena haukua mwingine, ulikua ni wimbo wa,sorry! wimbo ulioimbwa na mwanamziki wa kiume kutoka Marekani ,Justin Bieber.



    Taratibu nilitikisa kichwa changu kufuatisha mapigo ya mziki huo, huku nikishangaa jinsi wadada wazuri wa kizungu walivyokuwa wakiucheza na kutikisa makalio yao na kuzidi kunipagawisha.



    Siku zote raha jipe mwenyewe! taratibu msemo huo ulipita katika fikra zangu, na kunifanya nizidi kuwa na uchu wa kuifurahia siku ile ya jumapili,kwa kufanya anasa tofauti na jinsi ilivyokuwa ikitakiwa.



    Nilifungua kizibo cha konyagi na kisha kumimina katika grasi, lakini nilipotaka kuchukua chupa ya maji niweze kuchanganya, ghafla nilisikia kengele ikilia, kengele ile iliashiria kulikuwa na ujio wa mgeni nyumbani kwangu.



    “Mungu wangu !,leo nimeumbuka “,nilizungumza maneno huku nikiwa nina hofu sana, na bila kupoteza muda nilizima tv yangu kubwa ya ukutani, na kutoa frash ya miziki na kuchomeka frash ya nyimbo za kwaya na kisha kuwasha tv kwa mala nyingine tena.



    Baada ya hapo, nilitoa chupa zote za pombe zilizokuwa mezani na kisha kuweka chupa kadhaa za soda, halafu nikaenda kufungua mlango wa nyumba yangu.



    “Jumba lote hili, huogopi kukaa peke yako, yaani mnaishi wawili na mlinzi wa getini kama vile wafungwa, “Juliet aliongea huku akiwa ameshika biblia, lakini mimi nilitabasamu kuficha hofu yangu kwani nilisahau kutoa grasi yenye konyagi mezani.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nimeaga nyumbani naenda kwenye maombi, tutafakali maneno ya mungu, halafu nirudi nyumbani haraka mchungaji siunajua ni usiku ,lakini ninakiu sana ………haya maji si ninaweza kunywa?, naona wewe umejaza soda tu mezani “,Juliet aliongea baada ya kuketi kwenye sofa, huku akitazama wimbo wa nibebe!, ulioimbwa na mwimbaji maarufu wa nyimbo za injili nchini Rose Muhando.



    “Hapana usinywe! ngoja nikakuchukulie maji masafi ya baridi siunaona joto “,nilimnyanganya grasi yenye konyagi haraka sana na kisha kuelekea sehemu ambayo friji ilikuwepo, pale pale sebuleni.



    Nilitembea haraka sana!,kwani huo ndio ulikuwa wakati pekee wa kufanya ukatili wangu. Nilichukua unga kama watu wengi wa kizazi hiki cha Makonda wanavyouita, na kunyanganya na maji kwenye grasi bila Juliet kuniona na kisha nikampelekea.



    “Tusome za …bu… rii zabu…rii “zaburi haikusomeka tena!, kwani kabla Juliet hajamalzia kusoma biblia kitabu cha Zaburi, ili tuweze kutafakali. Nguvu zilimuishia na kisha kujilaza katika kochi lile, huku kitabu kitakatifu cha Mungu kikidondoka chini.



    “Tayali dawa imefanya kazi, utajuta kunywa maji yangu leo “,nilizungumza huku nikimnyanyua Juliet, msichana mweupe, mrefu na mrembo sana na kisha kumpeleka chumbani kwangu.



    “Hakika, Hakika Hakikaaa!, usiku huu wa saa sita utakua usiku wa mwisho kwa utajiri wako, maisha yako na umaarufu wako, tangu uingie kwenye chama chetu hujatoa sadaka kwa nyoka wetu, tumekutalifu mala nyingi lakini hutaki kutii amli yetu “,ilikua ni sauti nzito iliyosikika chumbani kwangu, na kusababisha nyumba yote kutetemeka. Mala tu baada ya kumfikisha Juliet katika chumba changu, na kisha kuvua nguo zangu, lakini kabla sijamfanya chochote ndipo nikasikia sauti ya kutisha bila kujua ilitokea wapi.



    “Sawa mkuu, leo nitatii amli yenu, “,nilizungumza kwa ujasili huku nikivaa nguo zangu, na kujiweka tayali kwa ajili ya kumtoa sadaka Juliet. Kwani ili sadaka isiwe haramu, haikutakiwa nimuingilie kimwili, kwani sadaka hiyo ingekuwa najisi kwa mizimu.



    Nilielekea katika kabati la vyombo, nilipojalibu kuangalia saa yangu, ilikuwa bado mapema, tena saa mbili usiku. Lakini nilikuwa na mambo mengi ya kufanya, ili sadaka iweze kukamilika, ningefanya mzaha, saa sita ingefika huku sijakamilisha hatua zote za kutoa sadaka.



    “Nisamehe sana Juliet, sina jinsi “,niliongea huku nikiwa nimejifunga kitambaa chekundu kichwani, na kumchinja Juliet kama vile kuku huku damu yake ikitapakaa kila sehemu ndani ya chumba cha siri, chumba ambacho kilitofautiana na vyumba vingine, kwani kilipambwa kwa mashuka ya rangi nyeusi, nyekundu na cheupe kiasi kwamba ukuta ulikuwa hauonekani.



    Nikiwa ndani ya chumba changu cha siri, jasho jembamba lilianza kunitoka kutokana na hofu niliyokuwa nayo, hasa baada ya kumuua kikatili Juliet. Kwani tangu nijiingize kwenye unabii wa uongo, sikuwahi kuua hata siku moja japokuwa nilitakiwa nitoe sadaka ili nizidi kukubalika katika jamii na kujipatia utajiri mwingi.



    “Hapa inatakiwa  nitamke maneno ya kumwita mtukufu Nyoka, aweze kupokea sadaka yangu “,damu zikiwa zimenitapakaa mwilini, niliangalia saa lakini muda ulikuwa unazidi kwenda, kwani tayali ilikua imefika saa tano usiku.Nilizungumza peke yangu huku nikijiweka tayali kwa ajili ya kumuita  Nyoka yule wa ajabu, nyoka aliyekuwa kama Mungu wangu ili aweze kuipokea sadaka yangu niliyomtolea na asiweze kuniazibu.



    “Nyoka njoo Nyokhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/a!, Ni mimi Hakika Nyoka!, Njoo uchukue chakula Nyoka!, nimekuandalia Nyoka……!”,niliimba wimbo huu huku nikirudi kinyume nyume. ,na kisha tena niliweza kusogea mbele. Huu wimbo, ndio wimbo ambao mzee Jabir alinifundisha na kunitaka niweze kuuimba pale nitakapotaka kumtolea Nyoka sadaka.



    Lakini baada ya kuimba kwa muda mrefu huku nikicheza, nilijikuta nikikata tamaa kwani Nyoka yule wa ajabu hakuweza kutokea. Taratibu nilianza kupunguza kasi ya kuimba tofauti na mwanzoni, huku nikiwa uchi wa mnyama na kichwani kwangu niliweza kujifunga kitambaa chekundu vazi pekee nililotakiwa niwe nalo wakati wa kutoa sadaka.



    “Nyoka njoo Nyoka!, ni mimi Hakika Nyokaa!, nimekutayalishia chakula Nyokaaa, njoo ule nyo…ka…a “,kabla sijamalizia kutamka maneno ya wimbo, wimbo ambao nilikuwa naimba kwa sauti ya chini sana, kwani nilikuwa tayali nimechoka kuuimba kwa muda mrefu bila mafanikio, nilishangaa kumuona Nyoka yule akimmeza Juliet bila kutambua kuwa alitokea wapi. Baada ya kummeza Juliet, joka lile lilipotea katika mazingira ambayo sikuyaelewa lakini sikujali sana zaidi ya kumshukuru mungu kwani sadaka yangu iliweza kupokelewa na Nyoka wa ajabu, nyoka ambaye nilimshuhudia Bagamoyo kwa mala ya kwanza baada ya kupelekwa na mzee Jabir.



    “Una bahati sana!, sadaka yako imekubalika kwa kiwango cha juu, kwani umekuwa mtu wa kwanza katika chama chetu kumtoa sadaka msichana wa kike ambaye bado ni kijana, na hivyo basi kichwa kimoja cha Nyoka wetu kitapungua, na hivyo basi utaishi na Nyoka nyumbani kwako akikulinda …!,akikulinda …akikulinda!, “yalikuwa ni maelezo marefu ya mtu nisiyemfahamu, aliyekuwa akinifahamisha juu ya kupewa nyoka mmoja kama zawadi kwa ajili ya kunilinda. Nyoka huyo atatoka katika mwili wa joka lile kubwa tuliloliabudu, na kulitolea sadaka kwani lilikua na vichwa vingi sana.



    Nilitikisa kichwa kuashiria kukubaliana na sauti ile ya ajabu, huku nikijifungua kitambaa chekundu kichwani na kisha kutoka nje ya chumba cha siri, chumba ambacho nilikitumia kufanyia ibada kwa mungu wetu Nyoka  tuliyemwabudu,mungu ambaye hakupenda kuona wanadamu wakimtukuza na kumwabudu Mungu wa kweli,bila kujali dini zao walizotoka.



    Baada ya wiki moja;



    Baada ya takribani siku tano kupita,huku nikiwa tayali nimeshaanza kumsahau Juliet,msichana pekee na wa kwanza kanisani kwangu  kumuua.Nilishangaa sana usiku wa jumamosi,usiku ambao haukuwa wa raha katika siku zote ambazo nilikuwa nimeishi duniani.



    “Samahani mchungaji,jana usiku Juliet alituaga anakuja kanisani kwenye maombi,alifika mahali hapa?,hajarudi nyumbani mpaka sasa!”,yalikuwa ni maneno ambayo yalijirudia rudia kichwani kwangu tangu asubuhi mpaka usiku wa siku ya jumamosi nikiwa nimeketi sebuleni kwangu.Haya maneno waliweza kunitamkia wazazi wake Juliet,siku ya jumatatu walipokuja kumtafuta mtoto wao kwani Juliet nilimuua na kumtoa sadaka jumapili usiku,alipokuja nyumbani kwangu.



    “Itabidi kesho nitangaze kanisani,kuhusu Juliet kupotea”,nilizungumza maneno haya huku roho yangu ikinisuta,kwani wazazi wake Juliet niliwaogopea na kukataa kuwa Juliet hakuweza kufika nyumbani kwangu.Lakini walipojaribu kumtafuta kila kona ya jiji la Dar es salaam,hawakuweza kumpata huku taarifa juu ya kupotea kwake ikitangazwa na vituo vingi vya televisheni kwani niliweza kulipia pesa kwa ajili ya matangazo hayo,sikuwa na jinsi ilibidi nifanye hivyo na kutoa ushirikiano wa hali ya juu nisiweze kugundulika kama mimi ndiye niliyeweza kumuua.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Mimi sijafa,bado ninaishi,bado ninaishi!bado ninaishi!”,ilikuwa ni sauti ya mwangwi iliyokua ikijirudia rudia masikioni kwangu,lakini nilipotaka kuikimbia sauti ile nilishangaa kukutana na Juliet uso kwa uso,huku alama ya kisu ikiwa shingoni,sehemu ambayo niliweza kumchinja kwa kutumia kisu.



    Nilitetemeka sana kwa hofu,,huku mkojo ukinitoka.Ilibidi nisimame tu kama zezeta kwani sikuwa na chochote cha kufanya,na kubaki nikimshangaa tu Juliet.



    “Sitaki kukuua wewe kama ulivyoniua mimi,wewe nitakuaibisha ulimwenguni wajue siri zako,lakini nitafanya hayo yote mpaka nitakapokamilisha kazi ya kupambana na wakubwa zako waliokutuma”,ilikua ni sauti ya Juliet,msichana aliyegeuka mzimu na kunitokea huku akiwa amevalia kanzu nyeupe iliyofunika mpaka miguu yake.









    ITAENDELEAPseudepigraphas

0 comments:

Post a Comment

Blog