Search This Blog

JENEZA LA AJABU - 5

 

    Simulizi : Jeneza La Ajabu

    Sehemu Ya Tano (5)





    Mwamutapa;



    Askari wa mfalme, wanakuta kundi kubwa la wananchi wakishangaa mwili wa mama Njoshi ukiwa umefukuliwa, huku Grace akiwa pembeni akilia sana. Askari hawa walikuwa wametokea kumuua Ngesha na mama yake, na sasa walikuwa wanaelekea ikulu kwa mfalme, kwani nyumba ya kina Njoshi ilikuwa pembeni ya barabara iliyokuwa inaelekea kwa mfalme. Wakiwa wanajiuliza maswali mengi, bila kufahamu mtu aliyesababisha watu waweze kujua siri hii na kujaa mahali pale, jambo ambalo hata Grace hakulifahamu, waliondoka haraka bila kutamka jambo lolote na kuelekea ikulu kumpatia taarifa mtoto mkubwa wa kiume wa mfalme, kwani walizani Grace ndo aliyafanya hayo yote, bila kutambua kuwa mzee Njiti, mzee aliyepewa jina hilo kutokana na mwili wake kuwa mdogo,ndiye aliyewatangazia watu kuhusu kifo hicho.



    Msitu wa majini;



    Malikia akiwa analiongoza jeshi lake kumfuatilia Njoshi, walishindwa kumkamata kwani tayali alikua ametoka nje ya msitu. Kitendo hiki cha  Njoshi kufanikiwa kutoka nje ya msitu na fimbo pekee ya ajabu iliyokuwa imebakia mikononi mwao, ilibidi malikia atafute njia nyingine ya kujikomboa mwenyewe pamoja na majini wenzake wa msituni kutoka kwenye kifo, kwani muda wowote wangeweza kuvamiwa na majini wa ajabu kutoka baharini na kuuawa.



    “Aiweeeh mtukufu Gutamanya, mkuu wa majini wote wa msituni, tunaomba utupe nguvu ya ajabu, nguvu ambayo itaweza kuzishinda nguvu za fimbo iliyoko kwa mfalme Mutapa, tuweze kuvuka msitu wetu na kumfuatilia adui yetu aliyetuibia fimbo ya pili, fimbo pekee iliyokuwa imebakia kutulinda sisi tusiuawe na majini wenzetu wa baharini. Tunaomba utuwezeshe tumkamate adui yetu kabla hajatamka maneno matano mbele ya fimbo ya kifalme, kwani tayali fimbo hiyo haitakuwa mali yetu tena “, malikia aliomba kuongezewa nguvu na mkuu wao wa majini wa msituni, kiongozi wao ambaye walimwabudu. Hawakuwa na njia nyingine kwani tayali Njoshi alikuwa ameuvuka msitu, na majini hawakuwa na uwezo wa kuvuka msitu wao kutokana na kudhibitiwa na nguvu ya ajabu kutoka kwenye fimbo ya mfalme Mutapa.



    Kweli maombi ya malikia yaliweza kukubaliwa,kwani tetemeko kubwa la ardhi liliweza kutokea kwa sekunde kadhaa huku radi nyingi zikipiga angani. Nguvu za majini wale ziliongezeka, na hatimaye wakauvuka msitu wa ajabu huku wakipaa kama ndege na kuendelea kumkimbiza Njoshi, waweze kumnyanganya fimbo ile ya kifalme, kabla hajatamka maneno matano mbele ya fimbo ile.



    ********



    Njoshi akiwa na furaha sana huku akijiona mshindi, alizidi kutembea kwa maringo akielekea nyumbani. Kwani aliamini majini hawakuwa na uwezo wa kutoka nje ya msitu kumfuatilia, kutokana na kuambiwa na baba yake miaka kadhaa iliyopita kuwa majini wa msituni hawakuwa na uwezo wa kuuvuka msitu, kwani fimbo ya mfalme Mutapa ingewapiga na kuwaua.



    Lakini Njoshi alishindwa kukumbuka maneno muhimu sana aliyoambiwa na baba yake, maneno matano ambayo unatakiwa uyatamke mbele ya fimbo ya kifalme baada ya kuandika jina lako. Maneno hayo matano, unatakiwa utamke kulingana na mahitaji yako, kwa mfano mfalme Mutapa, babu yake mfalme Mutapa wa sasa aliyemtuma Njoshi jeneza la ajabu, alitamka maneno matano yafuatayo;



    “,Utajiri “,



    “,Ufalme wa miaka mingi “,



    “,Watoto wengi “,



    “,Majini wasivuke msitu na kuniua “,



    “,Ujasili “,



    Hayo ndio maneno ambayo mfalme Mutapa aliyaongea mbele ya fimbo, na kisha kuyaandika katika fimbo hiyo. Tangu hapo ukoo wake umetawala miaka mingi sana, huku akiwarithisha ufalme ndugu zake, mpaka sasa anatawala mjukuu wake Mutapa, ambaye kamwagiza Njoshi jeneza la ajabu, ili afufuke baada ya kufa. Pia ufalme wake ukawa tajiri, huku yeye akiwa jasiri sana kwani aliua watu bila huruma na jambo la mwisho majini wa msituni walishindwa kuuvuka msitu kwenda kumuua kwani aliwaibia fimbo hiyo.



    Mfano wa pili, ni majini wa msituni, baada ya kuiba fimbo hizo mbili walipofukuzwa baharini, walitamka maneno matano mbele ya fimbo hizo, na kisha kuyaandika katika fimbo hizo. Maneno hayo ni;



    “,Wamiliki msitu ,msitu ambao waliupatia jina la msitu wa majini”,



    “,Wasiuawe na majini wa baharini “,



    “,Msitu wao uwe tajiri “,



    “,Wawe na umoja “,



    “,Wapendane “,



    Baada ya kutamka maneno hayo, kuanzia wakati huo waliweza kuumiliki msitu, huku adui zao wa baharini wakishindwa kuwaua .Pia utajiri yakiwemo madini ya dhahabu na almasi yalipatikana kila kona katika ardhi ya msitu wao, huku upendo na umoja ukitawala baina yao.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hivyo basi, Njoshi ilitakiwa na yeye atamke maneno yoyote matano aliyoyataka, na kuanzia hapo majini wasingeweza kumfuatilia kwani tayali alikua na mamlaka kama mmiliki halisi wa fimbo hiyo ya kifalme.



    “Ngoja nile ubuyu, njaa imekua kali,”Njoshi aliongea huku akiketi chini ya mti wa ubuyu, mti ambao alipumzika siku ya jumatatu usiku akiwa safarini kuelekea msituni. Aliketi mahali hapo kula na kupumzika, bila kutambua kuwa viumbe hatari wa msituni, viumbe wa ajabu walikuwa njiani wakiwa na kasi ya ajabu wakimfuatilia.



    Ikulu kwa mfalme;



     Baada ya askari wa mfalme kumfikishia ujumbe mtoto mkubwa wa kiume wa mfalme, ujumbe uliohusu kugundulika kwa kifo cha mama yake Njoshi na wananchi, huku Grace akiwa mhusika mkuu wa jambo hilo. Anaamua kutuma watu waweze kumuua Grace, kwani walimuona kama msariti wa mfalme kabla hajatoa siri zote zinazomhusu mfalme na kuhalibu kila kitu.



    “Rudini mkamuue Grace, mtoto msariti wa mfalme kabla hajatoboa siri, na kusababisha tunampoteza kabisa mfalme Mutapa na utawala wake ” ,amli ilitolewa na mtoto mkubwa wa mfalme, huku baadhi ya wanafamilia hasa wake wote wa mfalme wakilia sana kwani walipingana na kauli hiyo ya kumuua Grace, mtoto pekee wa mfalme, bila kutambua kuwa kulikua na chuki binafsi kati ya watoto wa kiume pamoja na Grace, kwani siku zote walikuwa wakitafuta njia ya kumuua Grace bila mafanikio. Grace alitafutwa sana na ndugu zake ili waweze kumuua, kwasababu walihisi angeweza kulisishwa fimbo ya kifalme, na kuwa malikia wa Mwamutapa, kutokana na kupendwa sana na baba yao mfalme Mutapa kwani alikuwa mtoto wake pekee wa kike.



    Hivyo basi, wakati huu ulionekana kuwa wakati sahihi wa kumuua Grace, huku mama zake wakilia kwa uchungu bila mafanikio, huku kundi kubwa la askari wenye siraha nzito wakitoka ikulu, kuelekea kijijini kumuua Grace.



    Bahari ya hindi;



    Sherehe kubwa inafanyika chini ya bahari, na kusababisha bahari kuchafuka. Hali ya hewa ikiwa mbaya baharini, huku upepo mkali ukivuma, na kusababisha mawimbi makubwa ya maji kutokea na kupelekea ajari nyingi za meli pamoja na boti. Ajari hizi zinaua mamilioni ya watu wa mataifa mbalimbali, watu waliotumia usafiri wa maji katika bahari ya hindi siku ya jumatano. Viumbe hatari sana, majini wa baharini, waliamua kuichafua bahari ili waweze kujipatia chakula cha sherehe, nyama pamoja na damu ya binadamu.



    Sherehe hii ya majini wa baharini haikuwa nyingine, bali ni sherehe ambayo walisherekea kuibiwa kwa fimbo ya kifalme, fimbo pekee iliyokuwa imebakia kwa maadui zao. Maadui ambao waliowafukuza baharini na kuiba fimbo hizo za ajabu, fimbo ambazo ziliwalinda wasiweze kuuawa.



    “Kuleni nyama, kunyweni damu, na tukimaliza tukawaue maadui zetu, majini wenzetu waliotukosea na kuwafukuza mahali hapa, katika ufalme huu wa ujinini”,mfalme wa majini wa baharini alitoa tamko la furaha, huku shangwe, nderemo, na vifijo sikisikika, kufurahia tamko lake bila kutambua kuwa majini wa msituni walikuwa tayali wakijalibu kufuatilia fimbo iliyoibiwa, ili waweze kuyaokoa maisha yao.



    Njoshi akiwa ameketi kupumzika chini ya mti ,alishangaa kuona kundi kubwa la ndege wa ajabu likielekea uelekeo ambao yeye alikuwepo. Hakuweza kuogopa kwani alifikili ndege wale walikuwa wa kawaida tu,lakini kadri ndege wale walivyozidi kumsogelea, ndipo alipotambua kuwa alikuwa hatarini. Kwani aliweza kutambua kuwa, wale walikuwa ni majini wa msituni na wala sio ndege wa kawaida kama alivyodhani.



    “Hapa niko hatarini, wamewezaje kunifuatilia mpaka huku?, “Njoshi aliongea huku akinyanyuka mahali alipokuwa ameketi, na kisha kulinyenyua jeneza la ajabu ili aweze kutokomea haraka sana.



    “Kazeni mwendo mkamateni,na mnyanganyeni fimbo, lakini msimuue, “malikia akiwa mmojawapo kati ya kundi kubwa la majini wenye mabawa, ambao walikuwa wakimfuatilia Njoshi Alizidi kuwatia moyo viumbe wake hatari waweze kusonga mbele, lakini aliwaonya wasiweze kumuua Njoshi, kwani moyo wake tayali ulikuwa umeshampenda binadamu yule, bila kujali makosa yote aliyowatendea, kwani siku zote kipenda roho hula nyama mbichi.



    “Ngoja nilishike vizuri jiwe hili la ajabu, linaweza kunisaidia “,Njoshi akiwa amebeba jeneza la ajabu, huku akiwa ameshika fimbo ya kifalme katika mkono wake wa kushoto, alitembea haraka sana kuusogelea mji wa Mwamutapa aweze kujiokoa dhidi ya majini wa msituni. Majini ambao walikuwa umbali kama wa mita miatano nyuma yake, wakipaa angani kama ndege wakimfuatilia.Aliamua kushika jiwe la ajabu katika mkono wake wa kulia aone kama jiwe lile lingeweza kumkomboa kutoka katika hatari hiyo.



    Bahari ya hindi;



    Kundi kubwa la majini wa ajabu wa baharini, wanatoka chini ya bahari huku radi za kila aina zikipiga katika anga. Kusema ukweli viumbe hawa walitisha sana, kwani walikuwa na sura pamoja na maumbo ya ajabu.



    “Kila mmoja aruke juu kwa kutumia mabawa yake, aelekee kwenda kuua adui zetu, kwani huu ndio wakati sahihi tuliokuwa tukiusubili “,kiongozi wa majini wa baharini, akiwa na manyoya marefu sana pamoja na kichwa cha sokwe mtu, alitoa amli huku akiruka juu na kuongoza kundi lake kwenda kuwaua majini wenzao wa msituni, kabla hawajaitia mikononi mwao fimbo ya kifalme kwa mala nyingine tena baada ya kuibiwa na Njoshi.



    Mwamutapa;



    Hali ya hofu inatanda katika ardhi ya Mwamutapa,mala baada ya wananchi wa Mwamutapa kushirikiana na Grace kumzika mama yake Njoshi kwa heshima, tofauti na awali alivyokuwa amefukiwa kama mnyama. Hofu hiyo ilitokana na tetemeko lililosikika, tetemeko ambalo lilifuatiwa na radi kali zilizopiga angani. Wengi walifikili kifo cha mama Njoshi, mganga aliyerithi taaluma hiyo kwa mumewe ndiyo chanzo cha radi pamoja na tetemeko kutokea.



    Hawakuweza kutambua kuwa viumbe hatari wa msituni waliongezewa nguvu na mungu wao, mtukufu Gutamanya waliyemwabudu na kuweza kuuvuka msitu salama bila kudhurika na fimbo ya mfalme Mutapa, na kumfuatilia Njoshi ambaye tayali alikuwa amekalibia kufika katika makazi ya watu wa Mwamutapa, akitokea msituni.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Turudini ikulu kwa mfalme, huyu mwanamke ni hatari, tutakufa “,kiongozi wa askari wa mfalme, aliwaambia wenzake waahirishe kumuua Grace,ili kuyaokoa maisha yao, baada ya kushuhudia radi zilizopiga mala tano mfululizo, na kufikili kuwa mzimu wa mama yake Njoshi ndio uliwaonya wasiweze kwenda kumuua Grace, binti kipenzi wa Njoshi, na   mtoto pekee wa kike wa mfalme.



    ********



    Ikulu kwa mfalme;



    Hali ya woga ikiwa imetawala katika ngome ya mfalme, baada ya kusikia radi zikipiga mala kwa mala na kufuatiwa na tetemeko la ardhi. Kauli inatoka kwa mganga mwenye nguvu za ajabu, mganga kutoka Mwamuyeshi, ambaye alikuwa bado yupo katika ikulu ya mfalme Mutapa akimsumbili Njoshi alete jeneza la ajabu kutoka msituni, na kisha wamzike mfalme katika jeneza hilo ili afufuke wiki moja itakapokamilika.



    “Waambie askari wako wote wajiandae kwa vita muda wowote kuanzia sasa, Njoshi tayali amefika na jeneza la ajabu, twendeni tukampokee, lakini majini wa msituni wako wanamfuatilia “,mganga yule alimweleza mtoto mkubwa wa kiume wa mfalme Mutapa, mtoto aliyekuwa msaidizi wa mfalme wakati mfalme akiwa hayupo. Bila kupoteza muda jeshi lote la Mwamutapa, lilitoka ikulu na siraha nzito za kivita kuingia mtaani kumpokea jeneza la ajabu Njoshi, huku hali ya majonzi na huzuni ikiwafanya wake za mfalme pamoja na vijakazi kuingia katika mahandaki kuyaokoa maisha yao kipindi cha vita.



    ********



    “Mtukufu mfalme tumeshindwa kumuua Grace, kwani huku mtaani tulikotoka ni hatari sana kwa sasa “,askari wale walimweleza mtoto wa mfalme baada ya kukimbia kutokana na radi nyingi kupiga mtaani, na kuwafanya washindwe kumuua Grace kutokana na woga, lakini wakati wanarudi ikulu, bila kutegemea walikutana na askari wenzao wakiwa wamejiandaa kwa vita, huku wakiongozwa na mtoto wa mfalme



    “Hebu ueni kwanza hawa wasaliti, kisha tusubili hao majini wapuuzi wanaoivamia ardhi yetu “,Mtoto wa mfalme hakusikiliza maneno yale, bali aliwaona kama wasaliti, na kutoa amli wauawe haraka sana. Kitendo ambacho kilifanyika kwa sekunde tu, kwani baada ya muda mfupi walikuwa tayali wamegeuka mizoga.



    ********



    Viumbe hatari ,wote wakiwa wamejigeuza kama ndege,wakipaa kwa kutumia mabawa yao,wote wakiwa wanaruka katika anga la dunia.



    Majini wa baharini waliruka kwenda kuwaua wenzao wa msituni,safari ambayo ilikua ni ndefu sana,kutokana na umbali mkubwa uliopo kati ya Mwamutapa na bahari ya hindi.



    Lakini pia,majini wa msituni wao waliruka kama ndege kumkimbiza Njoshi,waweze kumnyanganya Njoshi fimbo ya kifalme, fimbo ambayo ili walinda wasiuawe na majini wa baharini.





    Mwamutapa;



    Njoshi baada ya kushika jiwe la ajabu katika mkono wake wa kuume, aliweza kuwanyoshea viumbe hatari wa msituni ,kila walipojaribu kumsogelea na kutaka kumnyanganya fimbo ya kifalme. Mionzi mikali ilitoka katika jiwe, na kuwafanya majini wale waweze kurudi nyuma, majini ambao walikuwa na mabawa makubwa sana huku wakiruka kama ndege kumsogelea Njoshi.



    Njoshi alitumia jiwe hilo kuwapiga majini na mionzi mikali ya jiwe, kila muda ambapo majini walimsogelea karibu sana ili wamnyanganye Njoshi fimbo ya kifalme,na waweze kuyaokoa maisha yao. Hatimae Njoshi alifanikiwa kufika Mwamutapa, na bila kupoteza muda aliamua kufika nyumbani kwanza kabla ya kuelekea kwa mfalme, kwani alitambua kuwa mama yake angeweza kumsaidia kupambana na majini wale wa msituni, kutokana na nguvu alizonazo, nguvu za kiganga ambazo alirithi kutoka kwa mumewe baba yake Njoshi.



    Lakini bila kutegemea alishangazwa na kundi kubwa la watu alilolikuta nyumbani kwao, na kusababisha kulitua jeneza la ajabu chini, kwani tayali mfalme asingefufuka hata kama angezikwa katika jeneza lile, kwani wananchi walishaliona jeneza la ajabu, hivyo isingekuwa siri tena.



    “Grace kuna nini hapa?, haraka sana inatakiwa watu wote wakajifiche, majini wa msituni wako wananikimbiza waniue na kuichukua fimbo ya kifalme “,Njoshi aliongea maneno yaliyowashtua watu wengi sana, ambao walikuwa wakimshangaa sana kutokana na jeneza lile la ajabu alilokuwa amelishusha chini, huku wengine wakitabasamu baada ya kumwona akiwa ameshika fimbo ya kifalme, kwani walitambua kuwa uhuru wao ulikuwa umekalibia.



    “Njoshi mama yako kauawa, ndio tumemalza mazishi, mimi sirudi tena ikulu nabaki na wewe, hata hivyo nikirudi ikulu kwa mfalme lazima nitauawa na ka…ka za…ng…uuuu”,Grace kabla hajamalzia kumweleza Njoshi maneno yaliyomuumiza sana na kumwongezea hasira, Malikia wa majini aliyekuwa amevaa vazi jeupe huku akiwa na mabawa makubwa, alimkosakosa Grace kumchukua na kupaa naye juu, kwani tayali Grace alikua amempokea Njoshi fimbo ya kifalme.



    Haraka sana Njoshi alimkimbiza ndani Grace,huku kila mwananchi aliyekuwepo mahali pale akitafuta mahali pa kujificha.Lakini wanaume wengi walikuwa wamepigwa na butwaa wakimshangaa malikia yule aliyekuwa msichana mrembo sana,bila kujali mabawa yake aliyokuwa nayo.



    “Bahati yake!,ningemuua,Njoshi tayali nina mpenda, siko tayali kumuona na msichana mwingine ,”malikia aliongea huku akipaa juu, ili arudi tena chini akiwa na kasi ya ajabu na kupitia kibanda cha kina Njoshi walichokuwa wamejificha.



    “Lakini tunalotaka kufanya sio sahihi, Njoshi anatakiwa awe mfalme wa nchi hii, awakomboe watu kutoka katika mateso ya mfalme, tunachotakiwa kufanya nikumweleza atamke maneno matano,kwani hatambui chochote kuhusu umuhimu wa maneno haya, na katika maneno hayo matano atakayoyatamka mbele ya fimbo ya kifalme, inatakiwa atupatie hata sisi kipaumbele, tukiendelea kugombana naye tutakufa kwani majini wa baharini wako njiani wanakuja kutuua”,Malikia wa majini akiwa angani anaruka ruka na mabawa  yake ,alitoa wazo zuri ambao liliungwa mkono na kundi lote la majini wa msituni, ambao wengi wao walikuwa tayali wamechoka kumfuatilia Njoshi.



    ********http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Tulia msishambulie kwanza, subilini tuone mwisho wa ndege hawa wa ajabu, majini wa msituni “,mganga kutoka Mwamuyeshi alimweleza mtoto wa mfalme kusitisha zoezi la kutaka kuwashambulia kwa mishale, ndege wa ajabu ambao walionekana wakiruka kuzunguka nyumba ya kina Njoshi, nyumba ambayo Njoshi na Grace walikuwa wamejificha.



    ********



    Radi nyingi zinapiga, radi ambazo hazikuwahi kusikika hata siku moja katika ardhi ya Mwamutapa. Baada ya radi kutoweka, tetemeko kubwa la ardhi liliweza kutokea, tetemeko kubwa zaidi kuliko yote na kupelekea wananchi wote kutoka katika nyumba zao walizokuwa wamejificha, wakiogopa kudondokewa na nyumba hizo. Tetemeko hili lilisababisha hata Grace na Njoshi, waweze kutoka nje ya nyumba waliyokuwa wamejificha, ili kuyaokoa maisha yao.



    “Njoshi Nyangoma, kijana hodari na mwenye hekima, majini wa baharini wanakuja kutuua kwa sababu umetuibia fimbo yetu iliyokuwa ikitulinda tusiuawe, fimbo ambayo ilikuwa imebakia baada ya fimbo ya kwanza kuibiwa na mfalme Mutapa miaka mingi sana iliyopita, hivyo basi hatuna haja ya kukunyanganya tena fimbo, bali tunataka utamke maneno matano yatakayokufanya uwe mmiliki halisi wa fimbo hiyo. Lakini kwa sharti moja tu, hayo maneno unayoyatamka lazima utupe ulinzi na kuwa wamiliki namba mbili wa fimbo hiyo “,malikia aliongea maneno mengi ya hekima na busara sana, maneno ambayo yaliwafanya wananchi kujua siri iliyohusu fimbo ya ajabu ya mfalme Mutapa, pamoja na fimbo ambayo Njoshi alirudi nayo kutoka msituni.Hivyo basi,kila mwananchi wa Mwamutapa aliweza kukubali ombi la malikia wa majini, huku kila mmoja akiwa amekaa kimya akiwashangaa viumbe hawa wa ajabu kutoka msituni.



    Lakini hali ilikuwa tofauti kwa jeshi lote la mfalme na washirika wake, kwani hawakuwa tayali kumuona Njoshi akiwa mfalme mpya wa Mwamutapa.





    Mwamuyeshi;



    Kutokana na mfalme kumsubili mganga wake aliyeelekea katika nchi jirani, nchi ya rafiki yake Mutapa tangu asubuhi mpaka saa tisa jioni akiwa hajarudi, anaamua kukusanya jeshi lake haraka sana ili waweze kuelekea huko, waweze kujua kilichokua kikiendelea.



    “Vijanaa kazeni mwendo, inaonekana ufalme wa rafiki yangu umevamiwa na viumbe hatari tena viumbe wa ajabu “,mfalme alisikika akihamasisha vijana wake wasonge mbele baada ya kukanyaga mpaka wa Mwamutapa, lakini mala tu walipofika mpakani walishangaa viumbe wa ajabu waliokuwa wakiruka kama ndege wakielekea katika ufalme wa rafiki yake Mutapa, na kusababisha radi nyingi kupiga huku tetemeko kubwa la ardhi likifuatia. Ishara hizi ziliashiria viumbe wale waliotoka baharini na kuivamia nchi ya Mwamutapa hawakua wamchezo mchezo, kitendo ambacho kilimtia hofu mfalme Muyeshi, kwani alikuwa na hofu ufalme wa rafiki yake ambaye angefufuka baada ya wiki moja, ungeteketezwa na viumbe wale.



    “,Sawa mfalme, muda sio mrefu tutafika Mwamutapa na kutoa msaada “,askari wa Muyeshi, wakiwa wamepanda farasi wao huku wakiwa wameshikilia siraha zao, walizungumza kwa ujasiri na kumtoa hofu mfalme wao Muyeshi.



    Mwamutapa;



     Wananchi wengi wakiwa wamekusanyika karibu na nyumba yakina Njoshi, wakiwashangaa majini wa ajabu wa msituni.Njoshi kwa kujiamini,alishika fimbo ya kifalme katika mkono wa kushoto,huku kalamu kubwa ya ajabu ikiwa katika mkono wake wa kulia.Kalamu ambayo aliikuta msituni ikiwa pembeni ya fimbo ya kifalme,katika kabati la malikia wa majini.



    “Viumbe wa msituni,viumbe wenye hekima ,mkiongozwa na malikia wenu,nimekubali ombi lenu.Maneno yangu matano ni kama ifuatavyo”,Njoshi aliongea huku umati wa wananchi wa Mwamutapa wakimsikiliza kwa umakini,huku wakiachia tabasamu kwani tayali walielekea kutua mzigo mzito wa mateso na ukatili kutoka kwenye uongozi wa mfalme wao Mutapa.



    “Ufalme wa milele”



    “,Utajiri kwa kila mtu anayeishi Mwamutapa”



    “Majini wa msituni wawe wamiliki namba mbili wa fimbo ya kifalme”



    “Malikia wa msituni asinipende kimapenzi”



    “Grace awe malikia milele”



    Njoshi aliongea maneno matano bila upendeleo,huku kelele za furaha zikisikika kwa kila mwananchi wa Mwamutapa,kwani waliruka juu  huku wengine wakimnyenyua Njoshi na Grace,na kuwaona kama Miungu wao.



    “Tayali tuko huru,turudi msituni”,Malikia mrembo wa majini wa msituni alitoa amli kwa wenzake,huku hisia za mapenzi kwa Njoshi zikitoweka ghafla kwani tayali fimbo ya kifalme ya Njoshi ilianza kufanya maajabu.Kipindi hayo yote yakiendelea,baadhi ya wanaume wa Mwamutapa,hawakuweza kuamini kuwa Njoshi alikuwa na bahati kiasi kile,bahati ya kupendwa na malikia mrembo wa majini,pamoja na kupendwa na Grace.Japo hawakufahamu kuwa Njoshi alijuaje kuwa alikuwa akipendwa na malikia wa majini,wakati hajamutamkia jambo hilo mahali hapo.



    Ndugu msomaji,kumbe Njoshi usiku uliopita ,malikia alipoamka na kumtolea nge pamoja na siafu waliokuwa wakimtambaa mwilini katika mti wa mateso.Njoshi hakuwa amezimia bali aliigiza tu ,na aliweza kusikia kila kitu ambacho malikia alikiongea kuhusu hisia zake kwa Njoshi.Na pia,kila ambapo majini walipokuwa wakimshambulia,malikia alionekana kuhuzunika jambo ambalo lilimfanya Njoshi aweze kua makini,kuepuka kujiingiza katika mapenzi na malikia huyo.Hivyo basi,fimbo ya kifalme iliweza kumwepusha katika mapenzi na malikia,baada ya kutamka maneno matano katika fimbo hiyo ya kifalme.



    ********



    Ghafla ndege wa ajabu,majini hatari wa baharini,waliweza kupigwa na shoti kubwa,baada ya Njoshi kutamka maneno matano na kuwapatia ulinzi majini wa msituni dhidi ya maadui zao.Wakiwa na hasira sana ,waliamua kugeuza njia na kurudi baharini,huku wakiapa kuwa ipo siku lazima watafanikiwa kuwaua maadaui zao.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Turudini kabla hatujafa,kwani tayali adui zetu  wamerudi kuwa wamiliki namba mbili wa fimbo ya kifalme”,kiongozi wa majini wa baharini aliyekuwa anafanana kama sokwe ,alitoa amli kwa majini wenzake waweze kugeuza haraka sana na kurudi baharini,kabla hawajapigwa na shoti zenye nguvu zaidi kutoka katika fimbo ya ajabu ya kifalme na kufa.



    ********



    Njoshi haraka sana aliwaomba Wanamutapa kumshusha chini,na waliweza kufanya hivyo.Haraka sanaa alichukua jeneza la ajabu,na kulipeleka ndani kwani hakuwa tayali kuwaona askari wa mfalme wakilichukua na kulipeleka wakati waliweza kumuua mama yake.Aliona ni bora mama yake azikwe katika jeneza hilo na kufufuka,kuliko mfalme mwenye roho mbaya,roho mbaya ambayo aliwaambukiza hata na watoto zake wote isipokuwa Grace.



    “Hachukui mtu jeneza hili,nimelitengeneza kwa nguvu zangu na jasho langu,lakini nyinyi wapuuzi mmekuja na kumuua mama yangu”,Njoshi aliongea kwa hasira sana,huku akiwazuia askari wa mfalme waliokuwa wanataka kuelekea ndani kwa kina Njoshi,kuchukua jeneza la ajabu,ili mfalme katili Mutapa aweze kufufuka,japo ilikuwa ni ngumu sana kwani wananchi wote walikuwa tayali wanaijua siri iliyokuwa imefichika,kuhusu kifo cha mfalme.



    Ikiwa jioni siku ya jumatano, siku ambayo ilionekana kuwa ya kihistoria, kwani mambo mengi ya ajabu yaliweza kutokea katika nchi ya Mwamutapa. Jua likiwa tayali limeshazama, tayali kwa ajili ya kulikalibisha giza, ndege wa ajabu, majini wa msituni waliendelea kuruka juu wakirudi katika makazi yao ya msituni.



    “Mtukufu malikia, mimi naomba turudi tukamsaidie Njoshi, kwani tumemuacha hatarini dhidi ya majeshi ya mataifa mawili, bila sisi ni ngumu kushinda vita hivi, na tayali sisi ni wamiliki namba mbili katika fimbo yake ya ufalme, hivyo ni sehemu ya uongozi wake “,jini mweupe ambaye alikuwa ameongozana na kundi kubwa la majini wa msituni, alitoa wazo ambalo malikia hakuweza kulipinga, japo hakuwa akimpenda tena Njoshi, lakini alikuwa na wajibu wa kuulinda ufalme wa Njoshi, kama wamiliki namba mbili wa fimbo yake.



    “Haraka sana tugeuze,tukawasaidie “malikia wa msituni aliamua kuusikiliza ushauri wa jini mweupe, na kisha kujiweka tayali kwa vita na binadamu.



    ********



    Mwamutapa;



    Wanamutapa wote, wakiume na wa kike, wanazuia njia huku wakiwa wameshikana mikono. Walizuia njia kumsapoti Njoshi, kwani alipinga jeneza la ajabu lisiweze kutoka katika himaya yake.



    “Grace ongozana na hawa wanaume, mfukueni mama, na kisha muingizeni katika jeneza la ajabu kutoka msitu wa majini “,Njoshi alizungumza huku akiwa ameshika jiwe la ajabu mikononi mwake, akiwa tayali kwa ajili ya kupambana na askari wa mfalme Mutapa. Askari ambao waliongozwa na mtoto mkubwa wa kiume wa mfalme, na mganga kutoka kwa mfalme Muyeshi.



    “Sawa mfalme wangu mtarajiwa, mume wangu mpenzi “,Grace alimjibu Njoshi, huku kundi kubwa la Wanamutapa wakiungana na Grace, kwenda kuufukua mwili wa mama yake na kuuweka katika jeneza la ajabu.



    ********



    “Ua kila kiumbe kinachopinga utawala wa mfalme Mutapa, na hakikisheni mnalichukua jeneza la ajabu “,mfalme Muyeshi, mfalme ambaye hakua na masihara wala utani wowote, alifika na kukuta jeshi ra rafiki yake mfalme Mutapa, likishangaa tu bila kuanzisha tifu lolote na kuchukua jeneza la ajabu kutoka katika mikono ya Njoshi.



    “Tunakufaa! turudini nyum…a…aaaaaaaa”,askari wa Muyeshi walipiga kelele, na kujuta kwanini waliweza kumsogelea Njoshi ,waligundua ni kwanini askari wa Mutapa walikuwa wameshindwa kumsogelea Njoshi na kumtia mikononi, kwani waliambulia shoti zilizowababua ngozi zao, kutokana na mionzi ya jiwe la ajabu ambalo Njoshi aliweza kulishika. Bila kupoteza muda, askari waliweza kurudi tena nyuma kuyaokoa maisha yao.



    “Tumia fimbo hiyo ya baba yako, ina nguvu katika mapambano, “mfalme Muyeshi alitoa ushauri kwa mtoto wa rafiki yake Mutapa, aweze kutumia fimbo ya kifalme ambayo ilikua ya kwanza kuibiwa kutoka katika msitu wa majini, miaka mingi sana iliyopita. Siku zote usilolijua ni kama usiku wa giza, kwani mtoto wa mfalme alipojaribu kunyenyua fimbo ya baba yake juu, mfalme Mutapa ambaye tayali amekufa, jiwe la ajabu la Njoshi liliweza kuyeyuka na kupotea.



    “Mutapa juu, juu, juuu zaidi!!! “Shangwe za askari wa mfalme Mutapa na mfalme Muyeshi zilisikika ,huku wakiwa wanakimbia kwenda kumuangamiza Njoshi na watu wake, na kisha wamuue huku wakilichukua jeneza la ajabu kutoka katika himaya yake, wakamzike mfalme Mutapa, ili apate kufufuka baada ya wiki moja.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hofu ikiwa imetawala, kwani Njoshi alikuwa tayali amekata tamaa, na kutaka kujisalimisha mikononi mwa adui zake. Kila njia aliyoitumia kupigana na adui zake ilishindikana, na kubaki wakiwa wameduwaa, yeye, Grace, na watu wote wa Mwamutapa ambao walikuwa wakichukizwa na ukatili wa mfalme wao Mutapa.



    Walikiona kifo kikiwa mbele yao, kwani jiwe la ajabu ambalo Njoshi alilitumia kupambana na maadui liliweza kuyeyuka baada ya kuzidiwa nguvu na fimbo ya mfalme Mutapa, lakini Njoshi hakukubali kushindwa. Alichukua fimbo yake ya kifalme, fimbo ambayo ilikuwa inafanana sana na ile ya mfalme Mutapa, lakini alipojaribu kuitumia, haikuweza kutoa msaada wowote kwani fimbo ya mfalme Mutapa ilikuwa na nguvu nyingi kushinda fimbo ya kifalme aliyonayo Njoshi.



    Hivyo Njoshi hakuwa na jinsi, ilibidi asimame tu akiwa ameduwaa pamoja na watu wake.



    Lakini siku zote, mwenye haki hajikwai, na hata akijikwaa usitarajie kama ataanguka. Ikitokea ameanguka basi sizani kama ataweza kuumia, na hilo ndilo liliweza kumtokea Njoshi.



    Kwani akiwa amemkumbatia Grace, huku akifumba macho, akiwa hataki kushuhudia namna watu wake wakichinjwa, pamoja na yeye akiwemo. Kwani maelfu wa maadui zake walikuwa na mapanga wakitaka kuwaua kikatili, lakini alishangaa kusikia kelele za kilio kwa adui zake.



    Alipojaribu kufumbua macho yake, hakuweza kuamini, kwani alishuhudia majini wa msituni wakilishambulia jeshi la Mutapa, pamoja na jeshi la mfalme Muyeshi kwa mishale ya ajabu. Mishale hiyo iliwafanya askari wale waweze kugeuka punda, asikwambie mtu, duniani kuna maajabu.



    “Mfalme Njoshi na malikia Grace, tumeamua turudi kukusaidia kutoka katika hatari hii, kuanzia leo, punda hawa watakutumikia wewe na wananchi wako mashambani, na Wanamutapa wote watakua matajiri kutokana na mazao mengi ya shambani. “,malikia wa majini aliongea na kisha kupaa tena juu na majini wake, huku makofi ya pongezi yakisikika kwani Wanamutapa walifurahi sana kuokolewa kutoka kwenye kifo.



    “Sina cha kuwalipa, majini wa msituni, mdumu milele “,Njoshi alimjibu malikia huku akitazama juu, na kumpungia mikono kwani tayali adui aliweza kugeuka mkombozi.



    *******



    Kelele za vifijo zilisikika huku kundi kubwa la Wanamutapa wakimunyenyua Grace pamoja na Njoshi kuelekea ikulu, lakini wananchi wengine waliweza kunyenyua jeneza la ajabu ambalo lilikuwa na maiti ya mama yake Njoshi ndani yake.



    “Tutokeni tukawapokee, wameshinda “



    “Hapana tusitoke katika mahandaki haya, walioshinda sio watu wetu, siunasikia kelele za kumsifu Njoshi “



    Yalikuwa ni majibizano baina ya wake wa mfalme Mutapa, pamoja na vijakazi,wakiwa ndani ya mahandaki wamejificha wasiweze kuuawa kipindi cha vita.



    Hawakuwa na namna kwani tayali mfalme mpya Njoshi aliweza kuingia ikulu, ilibidi wajisalimishe na kuomba msamaha kwa Wanamutapa wote, kwani ufalme wa mume wao uliwanyanyasa wananchi. Waliweza kusamehewa, kwani Grace aliweza kuwaombea msamaha na kulipiza mema, kwa mabaya yote ambao wazazi wake waliyatenda.



    ******http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Wiki moja baadaye;



           Baada ya wiki moja kupita, shangwe na nderemo zilisikika ikulu kwa mfalme Njoshi. Kwani jeneza la ajabu lilifanya maajabu yake, mama yake Njoshi aliweza kufufuka na kushuhudia ufalme mpya wa mwanae Njoshi. Ama kweli, mtu ambaye alitamani afe aweze kupumzika kutoka katika mateso ya dunia, leo hii kaweza kufufuka.



    Lakini, ambaye alipenda kuishi milele, na kutuma mtu akalitafute jeneza la ajabu aweze kufufuka, si mwingine bali ni mfalme Mutapa, kafa milele bila kutegemea.



       *MWISHO *






0 comments:

Post a Comment

Blog