Sehemu Ya Tano (5)
Ibra akamuuliza Sophia,
“Umekipata wapi hiko?”
“Nilikitunza, siku zile sikukikata chote kukitafuna na hiki nilichoacha ni kwa matumizi mengine”
“Kwahiyo umekitafuna?”
“Ndio na nikakuona uliyokuwa unayafanya nyumbani”
Ibra alikiangalia kwa makini kile kijiti kwani kilikuwa ni kile ambacho mkewe alipewa na Yule bibi, kisha Ibra akamuuliza tena mkewe
“Eeeh kimekusaidia nini sasa?”
“Sikia Ibra, siku ile kuna masharti kidogo tulikosea ingawa vingi tuliviona. Tulisahau kusema asante Mungu”
“Kwani asante Mungu inamsaada gani na hiko kijiti?”
“Yule bibi aliniambia ni vyema kumshukuru Mungu kabla ya mambo yote huku ukiamini kuwa atatenda”
“Kheee umekuwa mlokole?”
“Hapana ila akili zangu zimefunguka”
Ibra akatulia kimya kwa muda kisha akamwambia mkewe,
“Unajua Sophy sikuelewi!”
“na huwezi kunielewa maana akili zako zimevurugika, hivi Ibra unawezaje kula chakula ambacho humjui hata muandaaji?”
“Kwani tunapokula hotelini huwa tunamjua muandaaji?”
“Je pale nyumbani ni hotelini? Yani ndani uko peke yako, unakuta chakula kimeandaliwa unakula je ni nani ameandaa?”
“Huwezi ukanielewa ila nadhani na wewe ungetafuna kidogo hiki kijiti ila kabla ya kutafuna useme asante Mungu”
Ibra alichukua kipande kidogo alichopewa na mkewe na kusema asante Mungu kisha akatafuna kile kijiti na muda ule ule alihisi kizunguzungu na kuangukia kwenye kitanda alicholazwa mkewe ambapo Sophia alijisogeza kidogo na kumuacha pembeni.
Muda kidogo Lazaro nae aliingia kwenye wodi aliyolazwa Sophia na kumkuta pale mwenzie akiwa ameanguka pembeni,
“Vipi tena na huyu shemeji?”
“Mwache akili zake zikae sawa”
“Duh! Cha kushukuru hapa wodi zao hazina wagonjwa wengi maana sijui ingekuwaje”
Lazaro akajitahidi kumuhamisha Ibra kwenye kitanda cha jirani maana wodi ile ilikuwa ni ya kulala wagonjwa wawili.
“Ila shemeji kuna tatizo”
“Tatizo gani tena?”
“Ni Yule kiumbe ambaye mumeo ameongozana nae kama dereva, si binadamu wa kawaida Yule”
“Nimetambua hilo shemeji na ndiomana nimemgomea kuondoka. Kwanza nashukuru sana kwa ujio wako kwani ulinifumbua macho sana”
“Unajua nilivyoambiwa tu kuwa umelazwa nikashtuka sana na kuamua kuja halafu kitendo cha kumuona Ibra kama kachanganyikiwa kilinishtua ukizingatia nilivyomuona nje hapo nilimuita lakini hakuniitikia. Ndiomana nilipoingia tu nilikwambia moja kwa moja kuwa mumeo hayupo sawa”
“Na kitendo cha wewe kuniambia vile kimenifungua sana ndiomana alipokuja ili tuondoke nikamgomea. Hebu angalia mida ni usiku tayari halafu tungeenda wapi? Kwakweli bora ulikuja shemeji”
“Sawa, basi mi naenda. Nitakuja kukucheki tena kesho”
Lazaro akaaga pale na kuondoka zake, Sophia nae alitulia kwa muda ila nesi alipokuja na kumshangaa Ibra pale Sophia alimuomba nesi asimuamshe mumewe amuache kwanza apumzike ila kwavile wote waliishuhudia akili ya Ibra ikabidi wasikilize anachokisema mkewe.
Kulipokucha Ibra alishtuka na kujishangaa sana kujiona pale hospitali, kisha akainuka na kwenda pembeni ya mkewe na kumshtua ambapo mkewe aliamka na kumsalimia,
“Sophy imekuwaje nimelala hospitali? Wameweza kuniruhusu kweli?”
“Hospitali hii wana roho nzuri sana mume wangu, walikuona tokea mwanzo kuwa una matatizo ndiomana wakaruhusu tu ulale. Eeeh niambie”
“Nimeona mambo ya ajabu sana kwenye ndoto”
“Kama yapi?”
“Kwanza kabisa ni kuhusu Yule dereva bhana kumbe hakuwa dereva wa kawaida na mpango wake ulikuwa ni kututeketeza”
“Duh! Akili imekufunguka sasa mume wangu. Asante Mungu, eeeh baada ya kuona hayo?”
“Ila je unajua huyo dereva alikuwa ni nani?”
“Mmmh kama ni Yule mtu usimtaje tafadhari, nionee huruma nina matatizo ya miguu sitaweza kukimbia mimi”
“Pole mke wangu simtaji”
Kisha Ibra akamuomba mkewe ruhusa ya kwenda kutafuta chai,
“Nakuruhusu ila tafadhari usifanye ujinga kama wa jana”
“Siwezi kurudia tena makosa mke wangu”
Ibra alipotoka Lazaro naye aliwasili akiwa ameambatana na mkewe huku amebeba chakula cha asubuhi kwaajili ya mgonjwa na rafiki yake Ibra ila walimkuta Sophia akiwa mwenyewe, wakamsalimia pale na kumuuliza kuhusu Ibra,
“Ametoka, kasema anaenda kutafuta chai”
“Dah angejua angetusubiria sie tu, hivi shemeji ngoja nikuulize”
“Uliza tu”
“Hivi ndugu zenu wanajua kama upo hospitali?”
“Mmmh sidhani, ila labda Ibra kawataarifu”
“Kwani wewe huna namba zao hapo tuwataarifu?”
“Mimi sikumbuki namba kichwani ila nilipopata ajali simu nayo ilipotelea huko huko sababu sikuwa na fahamu yoyote ile”
“Pole sana”
Mke wa Lazaro alimsaidia Sophia pale kunywa chai kisha na yeye akaanza kuzungumza naye.
“Ila hivi unajua kwamba kuna roho inawafatilia?”
“Roho kivipi?”
“Kuna roho chafu sana inawafatilia na sijui ni kwanini ila nadhani ni kwavile hamjasimama kwenye imani”
“Mmmh sasa mnataka tusimameje jamani?”
“Inatakiwa nikufundishe kwa urefu zaidi, ukiwa sawa nitakufundisha ila kwasasa ngoja tukuache upumzike kwanza kwani hata madaktari hawataweza kuturuhusu zaidi”
Kisha Lazaro na mkewe wakaondoka huku Sophia akiwa amejawa na mawazo juu ya hiyo roho inayowafatilia.
Ibra alipomaliza kunywa chai, akabeba vitafunwa kwenye mfuko ili akampelekee mke wake nae apate kifungua kinywa ila alipokuwa pale nje ya hospitali gafla akamuona mtu mwenye muonekano kama dereva aliyeenda nae jana kwa lengo la kumchukua mkewe, Ibra alimsogelea mtu huyo na kumshika bega ambapo mtu Yule aligeuka na alikuwa ni Yule Yule dereva,
“Hivi unajua kama nimeshakutambua?”
“Kunitambua kivipi?”
“Unadhani ukijiweka kwenye maumbo tofauti sitakujua?”
Huyu dereva alikuwa akimshangaa tu ibra na kwavile Ibra hakupata ushirikiano kutoka kwa huyu dereva aliamua kumkaba mpaka watu walipokuja kuingilia kati,
“Kaka vipi mbona unamkaba mtu bila makosa?”
“huyo sio mtu ni shetani”
Watu wakawa wanamshangaa Ibra,
“Shetani kivipi kwani kakufanyia nini tena jamani?”
“Nawaambia huyo sio mtu, kama hamniamini ngijeni muone kitakachotokea”
“Hebu acha masikhara bhana, huyu tupo nae kila siku hapa, haya sasa huo ushetani kauanza lini?”
Gafla Yule mkaka aliyekuwa amekabwa na Ibra mwanzo akaanza kutapika damu tena zilimtoka mfululizo na kufanya wenzie wamuingize pale hospitali na kumkimbizia kwa daktari, Ibra alikuwa akishangaa tu yale matukio na kujiuliza,
“inamaana shetani nae huwa anaumwa jamani?”
Ila akawasikia wale vijana wa pale kijiweni wakimwambia,
“Gharama zote za kumuhudumia huyu mtu utazitoa wewe maana ndio umemsababishia matatizo yote hadi kutapika damu sababu ya kumkaba kwako”
Ibra hakutaka kubishana nao sana, kisha akaingia hospitali nay eye akiwa hana hata vitafunwa kwani alishaviangusha wakati wa kumkaba Yule kijana.
Ibra alienda moja kwa moja alipolazwa mkewe huku akimuomba msamaha kwakutomletea vitafunwa,
“Usijali lakini nimeshakunywa chai”
“Umepata wapi?”
“Lazaro na mkewe walikuja kuniona na ndio walioniletea”
“Dah afadhali ila mimi nimepatwa na majanga bhana”
“Majanga gani tena?”
Ibra akamsimulia mkewe alivyomuona Yule mtu na jinsi alivyomkaba na yaloiyoendelea,
“Mmh mume wangu hivi una uhakika kuwa huyo mtu ndio Yule Yule dereva wa jana?”
“Nina uhakika ndio ni yeye, nilimuona vizuri na nilikariri sura yake”
“Sasa na hao wanosema huwa yupo hapo siku zote wana maana gani?”
“Hata nimeshindwa kuwaelewa”
Muda kidogo wakaletewa mgonjwa mwingine mule wodini ambaye alikuwa ni Yule kijana kwakweli ibra lishtuka sana na kujiuliza kwanini wamempeleka wodi hiyo hiyo, inamaana wodi zingimne zimejaa? Akashindwa kujizuia na kumuuliza nesi,
“Hivi kwani wodi zingine zimejaa? Kwanini huyu mmemleta humu?”
“Kaka samahani sana hayo matatizo yako ya akili sijui wanayajua hao wengine. Mimi siyajui na wala sitaki kuyajua, huwezi kutupangia cha kufanya. Hii sio hospitali yako”
Nesi akaweka sawa pale kitandani na kumsaidia Yule mgonjwa kupanda pale kitandani, Sophia akamuuliza mumewe kama mtu mwenyewe ndio Yule,
“Ndio ni huyo huyo”
“Mmmh mbona naanza kupatwa na mashaka Ibra?”
Yule nesi alipomaliza kumlaza Yule mgonjwa katoka kidogo kisha akarudi tena ndani na kumuangalia Ibra halafu akamwambia,
“Muda wa kuangalia wagonjwa umeisha kwahiyo naomba uende kaka. Nadhani umenisikia”
Kisha Yule nesi akatoka tena na kusonya, hata Sophia alimshangaa sana nesi huyu,
“Kwani vipi huyu nesi anamatatizo gani jamani au anakutaka mume wangu?”
“Hata mimi nimeshindwa kumuelewa kabisa”
“Kama anakutaka aseme ila sio kukusakama hivyo”
Muda kidogo Yule nesi akarudi akiwa ameambatana na askari,
“Nitolee huyo hapo maana muda wa kuangalia wagonjwa umeisha ila yeye anang’ang’ania kutoka hataki”
Yule askari akamuomba Ibra kwa ustaarabu kabisa kuwa atoke kabla hajafanya shurti lolote ikabidi Ibra aamue kutoka tu kwani heri nusu shari kuliko shari kamili.
Sasa wodini alibaki Sophia na Yule mgonjwa ambapo Sophia aliamua kumuuliza maswali Yule mgonjwa ili kujiridhisha,
“Kaka samahani, unaitwa nani kwani?”
“Nimezoeleka kwa jina la bonge”
“Bonge!! Ila mbona wewe ni kimbaumbau na sio bonge?”
“Ndio, huwa wananiita hivyo sababu ya wembamba wangu”
“Sawa, jina lako halisi je?”
“Naitwa Samson”
“Aaah, eeh imekuwaje?”
“si huyo jamaa sijui ndio mumeo kaja kanikaba balaa yani kama ningemchukulia hatua basi angekuwa polisi kutoa maelezo saizi. Halafu cha kushangaza nikaanza kutapika damu”
“Dah! Pole sana, na je ni kweli jana alikukodi wewe?”
“Anikodi mie saa ngapi? Kwanza jana sikuwa maeneo haya kabisa, kuna jirani yetu alifiwa na jana tulikuwa kuzika hata sikuja huku siku nzima yani nimeshangaa kweli kuja kunishutumu mimi”
“Pole mwaya, msamehe bure yule ni mume wnagu ila kuna matatizo Fulani yanamkabili ndiomana”
“Asante, ila alichonifanyia sio sawa kabisa ukizingatia hakuna nilichomkosea”
“Ila wewe jana mlivyoenda kuzika kuna kaburi ulikaa eeeh”
Bonge akashtuka sana na kumuuliza Sophia,
“Umejuaje? Maana kuna kaburi nilikaa kweli tena nilikaa peke yangu baada ya kuchoka kuchimba, wewe umejuaje?”
“Nikipona nitaomba unipeleke kwenye hilo kaburi”
“Niambie umejuaje dada? Mbona umeanza kunitisha?”
“Kuna kitu nimeona, na nimejua kwanini mume wangu amejua ni wewe na nimeelewa kwanini ulikuwa ni wewe”
“Nilikuwa ni mimi kivipi?”
“Hukuwa wewe kiuhalisia ila mwili wako na sura yako ndio vilivyotumika”
“Kwenye nini mbona sikuelewi”
Sophia akakaa kimya na kumuomba huyu mgonjwa apumzike kwanza kwani kuna mengi alikuwa akiyaona, kwakweli Sophia hata yeye mwenyewe alianza kujishangaa kwani vitu vingi sana vilibadilika kwake na alikuwa akiona mambo mengi sana ingawa mengine alikuwa akimficha mumewe na kuogopa kumueleza waziwazi. Akafikiria mengi sana huku akimuangalia huyu bonge ambaye hakuna alilokuwa akilijua zaidi ya kujua vile alivyokabwa na Ibra kiasi cha kuzindua tatizo linguine kwenye mwili wake.
Ibra alikaa pale nje akisubiri muda wa kuona tena wagonjwa ufike huku akiwa amekerwa sana na yule nesi aliyemtoa mule wodini, muda wa kuona wagonjwa ulipofika Ibra akaenda tena kumuona mkewe kwani hakuwa na imani kabisa na mtu aliyelazwa pamoja na mkewe.
Akiwa mule wodini mara akaja tena rafiki yake Lazaro akiwa ameambatana na baba John, baada ya salamu na pole baba John akamwambia Ibra,
“Kuna habari mbaya ndugu yangu”
“Habari gani tena hiyo?”
Lazaro akawa anamzuia baba John kusema hiyo habari mule wodini ila baba John hakutaka kusikia na kumwambia Ibra kilichojiri.
Kwakweli ilikuwa ni habari mbaya sana kwa Ibra na kumfanya aanguke chini na kuzimia.
Lazaro alimuangalia baba John na kumlaumu,
“Umeona sasa, unajua kuna vitu vingine havitakiwi kusema juu juu kiasi hiko ukizingatia mtu tayari ana matatizo mengine”
Ikabidi wasaidiane kumnyanyua na kumpeleka kwa daktari, Sophia alibaki kashika tama tu huku akiwaza kuwa yale mambo mabaya juu yao aliyokuwa akiyafikiria ndio hayo yanatokea,
“Mungu wangu, kwanini lakini? Nipo hospitali sijiwezi, halafu tena yanatokea kama hayo tutasaidiwa na nini jamani?”
Sophia hakupata jibu ila alikuwa na mawazo kupita maelezo ya kawaida. Baba John na Lazaro walirudi tena ambapo Sophia alihitaji kujua kwa undani zaidi, kwanza kabisa baba John akaomba msamaha kwa kutoa habari ile bila ya kufikiria,
“Nisamehe sana shemeji, nilijua Ibra ni jasiri”
“Hivi hata ungekuwa ni wewe unaambiwa kuwa biashara yako unayoitegemea, inayokulisha na kukufanya ujione mtu kati ya watu imeteketea yote ungekuwa kwenye hali gani?”
“Nakubali nimekosea jamani ila hata mimi nimepaniki ndiomana yametokea yote haya”
“Eeeh daktari amesemaje?”
“Kasema amezimia tu, tumuache apumzike halafu akizinduka atakuwa sawa”
“Haya, hebu nielezeni nini chanzo cha yote hayo maana hapa nilipo sijaamini wala kuelewa”
“Kiukweli shemeji hakuna anayejua chanzo ni nini, yani tumefika kazini kama kwaida, wakati tumetulia tukaanza kusikia harufu ya moshi na hakuna aliyeshtuka wala kuwa na habari yoyote ila badae tukasikia kelele za mtu nje akisema moto jamani moto, tulipotoka tulikuta duka la Ibra likiteketea yani tumejitahidi kuzima wapi kiukweli limeteketea lote yani hakuna kilichobaki na moto uliishia pale pale kwenye duka lenu, hakuna duka linguine lolote lililoathirika”
“Oooh Mungu wangu, jamani ndio mambo gani haya?”
“Poleni sana shemeji, nilijaribu kumpigia Ibra ila sikumpata hewani ndio nikampigia Lazaro ambapo alipofika alikuta duka lote limeshateketea na ndiye aliyetupa taarifa kuwa upo hospitali na nikaamua kuja kuwaona na kuwapa taarifa hii”
Sophia alijikuta akitokwa na machozi tu kwani duka lilikuwa ndio maisha yao, kila kitu waliwekeza kwenye duka hilo, maisha yao yote yalitegemea hapo. Aliwaza bila ya kupata jibu na kumfanya aanze kulia sana, ikabidi Lazaro asogee karibu zaidi na kumbembeleza shemeji yake.
Muda kidogo Sophia alitulia ila hakuwa na raha hata kidogo, Lazaro na baba John nao wakatakiwa kuondoka kwahiyo wakatoka na kuondoka kwenye lile eneo la hospitali. Kwakweli Sophia alikuwa na mawazo sana hadi akili yake ilikosa kufanya kazi kabisa, kwanza kabisa akafikiria kuhusu maisha watakayoishi na mumewe maana biashara ndio hiyo imeteketea kwa moto,
“Mmh sijui hata kama Ibra ana hela benki jamani, maisha gani haya tutaenda kuishi? Na gharama za hospitali je zitalipwa na nani? Mbona umasikini nauona machoni mimi? Jamani yale maisha tuliyokuwa tunaishi yote yanaenda kupotea”
Yule bonge alimsikia Sophia akilalamika, alimuhurumia na kumpa pole
“Pole sana dada, naweza kuona jinsi gani umeumia”
“Yani wee acha tu, maisha yote yameporomoka”
“Na je, hilo swala uliliona kama ulivyoniona mimi kuwa nilikaa juu ya kaburi?”
“Hapana sijaona chochote, hili limekuwa ni swala la kushtukiza sana kwangu”
“Pole sana, ila me bado umenipa maswali je umeonaje kuwa mimi nilikaa makaburini jana?”
“Ni historia ndefu ila akili yangu haipo sawa kabisa nadhani tutaongea siku nyingine”
Muda kidogo alikuja Ibra kwani alisharuhusiwa na daktari, kwakweli Ibra alikuwa amepoa sana akamfata mke wake
“Naomba turudi nyumbani Sophia”
“Mmmh turudi wakati sijapona vizuri?”
“Dozi nyingine tutaendelea nazo nyumbani, unajua nimechanganyikiwa kabisa hata sijui tutaanzia wapi na kumalizia wapi. Biashara yangu jamani dah!”
“Pole mume wangu, hii ni hasara yetu wote”
“Au ngoja kwanza nikashuhudie mwenyewe maana siamini kabisa”
Ibra akamuaga mkewe na kuondoka pale hospitali kwani imani ilimpotea kabisa kama duka lake linaweza kuungua bila ya sababu.
Ibra alifika maeneo ya duka lake na aliweza kujishuhudia ambavyo limeteketea, wakina baba John walipomuona ikabidi wawe nae karibu kwa lengo la kumtuliza ili asije akapaniki kama kule hospitali, Ibra alikaa chini kwanza huku akikuna kichwa chake maana ilikuwa moja haisomi wala mbili haisogei.
Alipotulia, rafiki zake wakamuomba arudi nyumbani akapumzike kwanza, akakubaliana nao kisha akawaaga na kuondoka, alielekea hospitali kumfata mkewe kuwa warudi nyumbani.
“Tafadhari Sophy kubali tuondoke hapa hospitali kwani sitakuwa na pesa za kulipia zaidi”
“Na zile pesa zetu kwenye kabati je?”
“Hakuna pesa kwenye kabati Sophy, tafadhali nielewe mke wangu”
Sophia akafikiria sana, hakupenda kurudi nyumbani ila akifikiria kuhusu uchumi wao hakuwa na namna zaidi ya kuafikiana na mume wake kuwa watoke tu.
Kisha Ibra aaenda kuomba kibali cha kutoka na mkewe, hawakutaka kumzuia leo kwani walimpa tu ruhusa kuwa waende na kumpatia dawa zote ambazo Sophia anatakiwa kutumia kisha Ibra akaenda kumkongoja mkewe ambaye alikuwa amepewa magongo ya kutembelea na kutoka naye nje. Kama kawaida aliiona gari yao ikiwa pembeni pale hospitali,
“Vipi mke wangu tukapande tena ile gari?”
“Hapana, itatupoteza tu. Wewe kwa muda wako utakuja kuifata mwenyewe”
Wakakubaliana kisha Ibra akaita gari ya kukodi na wao kuanza safari ya kurudi nyumbani ambapo walifika na kuingia ndani kama kawaida na nyumba ilikuwa shwari kabisa. Ibra akapata wazo la kumpigia simu Siwema na kumpa habari zao ambapo aliwaahidi kufika mahali hapo muda sio mrefu.
Haikuchukua muda mrefu sana Siwema nae alikuwa amewasili akiwa amewabebea chakula kwani jioni ilikuwa imeshaingia, walimkaribisha naye aliwapa pole sana.
“Ikabidi nipike kabisa kwani najua wazi mtakuwa na njaa tu, poleni sana jamani”
“Asante dada, na umefanya jambo la maana sana kutubebea chakula”
“Hivi ni mambo gani yamewasibu lakini?”
Sophia akaanza kumueleza Siwema toka siku ile ambayo alienda kwake na kuzungumza na yule bibi mpaka matukio ambayo yaliwapata.
“Uwiiii jamani si niliwaambia lakini kuwa yule bibi mchawi msimsiklize”
Sophia leo alikuwa kwenye kipaumbele kabisa cha kumtetea yule bibi,
“Hapana dada, yule bibi si mchawi ila sisi tuna matatizo tu”
Ibra akamuongezea Siwema kuhusu habari za kuungua kwa duka lao pia,
“Jamani, hivi mnajua kama kuna mtu anawaroga nyie au mnajifanya hamjui jamani! Nyie mnarogwa tena wazi kabisa, hivi hushangai hayo maajabu ya kuungua kwa duka? Maajabu ya kupata ajali mke wako, nikiwaambia niwapeleke kwa mganga huwa mnasumbua sana ila kwa hali hii ya mdogo wangu nitawapeleka”
“Dada, mimi sina haja ya mganga kwakweli ila nina haja na yule bibi naomba utusaidie kuhusu hilo”
“Hapo ndipo mnaponivuruga kwakweli, yani mimi nianze kuwaunganisha na wabibi wachawi? Siwezi jamani, siwezi kabisa”
Ibra aliafikiana na swala la Siwema kuwa wapelekwe kwa mganga tu ingawa kwa waganga karibia kote walikopita hawakuweza kufanikiwa,
“Kwakweli mimi naafikiana na wewe, tupeleke kwa mganga yani kuna mtu anatuchezea kabisa akili. Hata bado siamini kama duka langu limeungua kweli”
“Ila nyie mlinikera sana kipindi kile yani sana hata nikasema sirudii tena kuwapeleka ila nitawapeleka. Na kwa hali ya Sophia ilivyo leo nitalala hapa hapa”
Wakafurahi kwani waliona wazi watapata klampani kwa siku hiyo.
Usiku ulipofika walikula kile chakula kwa pamoja huku wakiongea mawili matatu kuhusiana na mambo ambayo yamewapata,
“Nyie msijali, huyo mganga ni kiboko nawaambia mali zenu zote zitarudi yani duka lenu litakuwa kama mwanzo”
“Nitafurahi sana maana imani imenikatika kabisa na maisha haya ukizingatia lile duka ndio biashara pekee ninayoitegemea kuendesha maisha yangu”
Wakaongea ongea pale kisha wakamuelekeza Siwema chumba cha kulala ambacho kilikuwa pembeni na kile chumba alichokuwa akilala Neema ila hawakumwambia kama kile chumba cha pembeni ndicho alichokuwa akilala Neema, kila mmoja alienda kulala sasa.
Sophia na mumewe walikuwa chumbani huku wakitafakari mambo mbali mbali yaliyowapata, ila bado Sophia alikuwa akimsisitiza mume wake kuwa wamtafute yule bibi
“Ibra, mi nadhani kuna vitu yule bibi anavifahamu kwanini tusimtafute yeye kuliko kuhangaika kwa waganga?”
“Sasa wewe unamuamini huyo bibi, je amewahi kukusaidia nini?”
“Na hao waganga je nao wametusaidia nini mume wangu? Hakuna ambacho wametusaidia, bora twende kwa huyo bibi labda akatupe muongozo way a kufanya”
“Sophia, siku zote ubishi wako ndio huwa unaharibu mipango yetu. Hebu mambo mengine ya msingi usiwe unabisha sana”
Sophia akakumbuka kitu, ni kuhusu yule mtoto akaamua kumuuliza mume wake
“Hivi na yule mtoto imekuwaje?”
“Hata najua basi! Sijawahi kumsikia tena toka siku ile ya vimbwanga hadi leo, sijui amekufa”
“Kama amekufa itakuwa vizuri sana maana nay eye ndiye anayetuletea matatizo. Halafu nimekumbuka kitu mume wangu”
“Kitu gani?”
“Yule mtoto ndio yule yule mtoto wa maajabu ambaye tulikuwa tukikutana nae njiani”
“Mmmh usiku huu mke wangu, hebu tuachane na habari hizo tulale”
Sophia akakubaliana na mume wake kisha wakalala.
Kwa upande wa Siwema sasa huwa ana kawaida ya kujiimbisha kidogo kabla ya kulala, akiwa mule chumbani huku akiangalia mandhari ya chumba kile ambacho kilikuwa na choo humo humo. Alienda chooni kwanza kujisaidia kisha akarudi na kuanza kujiimbisha imbisha ili alale kama anavyofanyaga nyumbani kwake, akashangaa gafla kuna karatasi imeangushwa kitandani kwake. Akashtuka sana na kujiuliza kuwa imeangushwa na nani, alijaribu kuangaza huku na kule ila hakumuona aliyeangusha ile karatasi ila iliandikwa kwa herufi kubwa tena kwa wino mwekundu. Siwema alisoma na kushangaa, ‘USINIPIGIE KELELE’
“Kheee makubwa haya, hii nyumba vipi? Inamaana ni sababu ya kuimba kwangu au karatasi hii iko hapa siku zote?”
Akaamua kwamba ahisi ile karatasi ilikuwepo tu siku zote hivyo akaendelea kuimba, gafla akasikia mtu akipiga makofi matatu. Hapo ndipo Siwema aliposhtuka na kuogopa na kabla hajakaa sawa alishtukia akinaswa kibao shavu la kulia na kunaswa kingine shavu la kushoto, Siwema alijihisi kuchanganyikiwa akainuka ili atoke nje ila hakuona mlango wa kutokea yani hapo ndio akachanganyikiwa zaidi na kisha akaanza kusikia sauti ya mtu akicheka sana, Siwema alikuwa akitetemeka huku amejibanza pembezoni mwa kitanda.
Hofu ilianza kumtawala gafla taa ikazimwa, hapo alihisi kuzimia kabisa, muda kidogo ikawashwa. Akajaribu kupiga kelele ila ilionekana inaishia mulemule chumbani kwani kelele zake hazikufika popote pale.
“Nisaidieni jamani, nisaidieni nakufa”
Hakuna aliposikika kokote, muda huu taa iliwashwa na akaanza kuona kivuli cha mtu hapo ndio alipochanganyikiwa kabisa kwani aliona kivuli na sio mtu, akajikuta akianza kujitetea
“Jamani kwani mimi nimewakosea nini jamani, sina makosa mimi naombeni nitoke humu”
Kicheko kikaanza kusikika vizuri sasa na kumfanya Siwema aishiwe maneno ya kuongea na kuzidi kutetemeka. Gafla akahisi ameshikwa miguu na imeanza kuburuzwa, aliburuzwa chumba kizima na kurudishwa tena kitandani bila ya kumuona muhusika anayemfanyia hivyo.
Gafla akaona macho ya mtu, hapo ndipo ujasiri ulimshinda na kujikuta akianguka chini na kuzimia.
Kulipokucha, Siwema aliamka pale chini huku kichwa chake kikiwa kizito sana na kumfanya ainuke kwa shida sana. Muda huu aliuona mlango na kutoka nje ambapo sebleni aliwakuta Ibra na mkewe ambao walimuuliza hali yake, Siwema alikumbuka matukio yote yaliyompata usiku.
“Hivi nyie mnawezaje kuishi kwenye hii nyumba? Nimekoma yani nimekoma kabisa sirudii tena kuja kulala hapa”
“Kwani vipi dada?”
“Yani usiku mmoja nimeona kama mwaka! Hapana jamani siwezi mimi siwezi nimekoma”
“Kwani imekuwaje maana hata kukaa hukai jamani!”
“Nikae ili iweje? Yaliyonipata yanatosha jamani, kweherini tena mnikome hii nyumba yenu siji tena. Sio nyumba hii, nawaambia tena sio nyumba hii. Kwaherini”
Wakati Siwema anafungua mlango ili atoke nje kabisa, ikasikika sauti
“Mbona mapema sana, hata chai hujanywa?”
Wote wakatazamana kwani hakuna aliyeongea muda huo, katika kushangaa zaidi wakamuona yule mtoto mchanga akija sebleni.
Hakuna aliyeweza kustahimili jambo lile na kujikuta wakiinuka ili kuanza kukimbia ila walianguka chini, kisha yule mtoto akasogea kwa Siwema na kumvuta kwa ndani kwakweli Siwema alikuwa akitetemeka sana kwani alishangaa jinsi mtoto mdogo hivi alivyoweza kutembea na alivyokuwa na nguvu za kumvuta. Wote wakawekwa pale sebleni kisha yule mtoto akaanza kucheka na gafla akageuka na kuwa Neema,
“Yani nyie mmefanya kazi ya kunitafuta sana, hata sikuwa na shida ya kuwasumbua mapema hivi kwani mida yangu ni usiku ila kwavile mmehitaji niwasumbue mda huu subirini sasa”
Neema akatoweka na kuwashtua zaidi ila kila walipojaribu kuinuka ili waweze kukimbia miguu yao ilikataa kuinuka kabisa na ilionekana kuishiwa nguvu kila muda unavyoenda mbele.
Gafla wote wakapitiwa na usingizi na hakuna aliyejua tena kinachoendelea pale sebleni.
Ule usingizi ulimpeleka Sophia sehemu nyingine kabisa, alikuwa mahali na kuwaona wale watoto watatu ambao huwa anawaona kwenye ndoto huku mmoja mmoja akimuaga na kuondoka. Sophia aliwaangalia wale watoto na kutabasamu kisha akawaambia,
“Mmerudi tena kwenye maisha yangu, nitafurahi sana. Je mmerudi?”
Hawa watoto wakatikisa kichwa na kumfanya Sophia aseme tena,
“Tafadhali msinifanyie hivyo, najua nyie ni wanangu naomba mrudi katika maisha yangu. Nawapenda sana.”
Ila hawa watoto wakapotea kisha akatokea yule mtoto waliyemuokota na kutabasamu ila Sophia alikunja sura kisha huyu mtoto akamwambia,
“Kuna kitu nitakufanyiaa na kamwe hutokuja kukisahau katika maisha yako”
Sophia akauliza kwa hamaki,
“Kitu gani hiko?”
Huyu mtoto akacheka sana, kisha akamwambia tena,
“Subiri utakiona, najua kitakuumiza sana maisha yako yote ila ndio nitakuwa nimeshakifanya tayari”
Sophia akapatwa na uoga huku akihitaji kufahamu kuwa ni kitu gani anachoambiwa kuwa atafanyiwa, ila yule mtoto akatoweka mbele yake na hapo ukawa mwanzo wa kushtuka kwa Sophia.
Ibra na Siwema walikuwa hawajitambui pale chini, hivyo Sophia alianza kwa kuwashtua ili nao waamke ila hakuweza kumuamsha hata mmoja kati yao na alipojaribu tena kuinuka hakuweza kabisa kwani miguu yake ilijawa na uzito sana. Wakati akijishangaa pale, ilikuja Neema huku akitabasamu na kumuangalia Sophia, kwakweli kwa wakati huu Sophia alikuwa amejawa na uoga uliopitiliza kwani hakujua hatma ya maisha yake, Neema alianza kumwambia Sophia
“Unajua nini Sophia, mwanzoni nilikupenda sana kwani nilikuona ni binti mpole na mwenye huruma ndiomana ulipopata mimba nilijitolea kukusaidia kazi mbali mbali kwa huruma yangu juu yako. Nilijitolea kukuandalia chakula kizuri cha kukupendeza kwaajili ya mtoto wako ila mlinikera sana wewe na mumeo siku yule mtoto mliyemkuta njiani halafu akapanda kwenye gari yenu, mlimtoa kwa nguvu na kumtupa. Yule mtoto alikuwa ni mimi, kwavile mliniudhi ndiomana nikapanga njia ambayo nyie mngenikaribisha wenyewe ndani kwenu na ndivyo ilivyokuwa, mlinikuta njiani na mkanikaribisha wenyewe nyumbani kwenu. Sikutaka muwe na mashaka na mimi ila kutwa kucha kutaka kunichunguza ndio kilichowaponza, nikaja tena kwa njia ya mtoto pia ukagoma kuninyonyesha”
Sophia akashtuka na kuuliza,
“Inamaana yule mtoto ni wewe?”
Neema akacheka kisha akamuuliza Sophia,
“Ulidhani yule mtoto ni nani?”
“Sijui, sasa ni maziwa gani uliyokuwa unanyonya kwangu?”
“Mimi sikuwa nikinyonya maziwa, nilikuwa nanyonya damu kwani damu yako inanipendeza sana ni tamu kwangu na inanipa afya”
“Sasa si inamaana ulikuwa unanimaliza damu? Je nimewezaje kuendelea kuishi hadi leo?”
“Mbona mbu nao huwa wanawanyonya damu nab ado mnaendelea kuishi!”
“Kwani wewe ni nani?”
“Mimi ni Neema”
“Ndio wewe ni Neema, ila ni mtu wa aina gani?”
Neema akacheka sana kisha akamwambia tena Sophia,
“Usitake kunijua kwa undani zaidi kwani unaweza kushindwa kuendelea kuishi na mimi lengo yangu si kuwaua”
“Ila lengo lako ni nini?”
“Lengo langu ni kuwatesa”
“Na kwanini unatutesa jamani?”
“Kilichowaleta humu ndani ndio kitawaambia kwanini nawatesa”
“Na kama lengo lako si kutuua, mbona wanangu mmewaua?”
“Sophia, Sophia sina muda wa kuendelea kukujibu zaidi ngoja niwaamshe wenzio ili mjaribu kupanga mipango ya kunitokomeza”
Neema akacheka sana na kutoweka, muda kidogo Siwema na Ibra walishtuka kutoka kwenye ule usingizi mzito waliokuwa wamelala.
Siwema alikuwa akijifikicha macho, Ibra nae vivyo hivyo huku kila mmoja akijaribu kurudisha kumbukumbu ya matukio yaliyowapata kabla ya kupatwa na usingizi na kila mmoja akakumbuka kila kilichotokea. Siwema akajikuta akitokwa na machozi tu,
“Jamani nisaidieni tafadhali niweze kutoka humu ndani kwenu, kwani na mimi nimefanyaje jamani?”
“Pole dada, hata sisi tunatamani kutoka hivyo hivyo ila hatujui tunatokaje dada yangu”
“Kumbukeni nina familia jamani, yani mambo yaliyonipata usiku kweli ndio yanaenda kunipata tena dah! Nisaidieni nitoke jamani”
Wote walikuwa kimya kwani kiukweli hakuna aliyekuwa na uwezo wa kufanya chochote ili waweze kutoka kwani kila mmoja ni kama alikuwa gizani hata miguu yao bado haikuweza kuinuka na kikubwa zaidi ni njaa kwani kila mmoja alikuwa na njaa ya kutosha ukizingatia ni tangu walipokula jana yake, na wakiangalia hali ilivyo ilikuwa ikionyesha kuwa usiku nao ulikuwa unaingia. Siwema akawauliza tena,
“Kwani nyie huyu Neema mlimfanya nini?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hatujamfanya chochote ila tunashangaa kwanini anatufanyia hivi”
“basi nisaidieni mimi nitoke”
Muda ulipita na kimya kikatanda, Siwema alipoona vile akaamua kujikongoja kwa kujisukuma hadi mlangoni aangalie uwezekano wa kufungua mlango ili aweze kutoka. Aliweza kufika mlangoni na akaanza kujitahidi kuinuka hadi kufanikiwa kufungua mlango, ila mlango ule ulipofunguka aliingia Neema huku akicheka sana na kumuuliza Siwema,
“Eeeeh unaenda wapi? Tena wewe una kiherehere sana, nilijua tu ipo siku utaingia kwenye anga zangu ndiomana nilikuwa nikikuangalia tu. Unafikiri ni rahisi hivyo kutoka humu ndani? Labda niamue mimi mwenyewe, na ili niamue muweze kutoka mnatakiwa kufanya kitu kimoja nitakacho waamrisha”
Ibra alijibu huku akiwa ametazama chini kwani kiukweli alishatambua kuwa Neema hakuwa binadamu wa kawaida kwahiyo aliogopa hata kumtazama usoni,
“Tupo tayari”
“Kuna chakula mezani, nitakapo waruhusu kuinuka nahitaji wote muelekee pale mezani na kula kile chakula”
Hakuna aliyepinga ukizingatia njaa ziliwashika sana, Neema kama alivyopanga akatoa amri moja na wakaweza kuinuka kutoka pale chini kisha kuelekea mezani, aliyekuwa wa kwanza kukipakua kile chakula na kuanza kukila alikuwa ni Ibra ila Siwema na Sophia waliogopa,
“Jamani, tuleni hiki chakula tuepuke matatizo. Kwani tukila kuna tatizo gani? Hebu tuleni jamani, sitaki kuona mkiumia ndugu zangu”
Siwema nae akaamua kupakua kile chakula na kuanza kukila kwani alikuwa na lengo kubwa sana la kurudi nyumbani kwake, kwahiyo alikula kile chakula ukizingatia na njaa yake basi akala sana tu. Ila tatizo lilikuwa kwa Sophia kwani hakutaka hata kukionja kile chakula na kujihisi kuwa atarudishwa nyuma alikotoka ambako hakutaka kurudi tena.
Walipomaliza kula walirudi na kukaa kisha kupitiwa na usingizi kasoro Sophia, kisha Neema akasogea na kumwambia Sophia
“Si umegoma kula eeeh! Utakula jeuri yako”
Neema akapotea, Sophia akajaribu kuwaamsha wenzie lakini hawakuamka na kumfanya azidi kupatwa na uoga wa maisha yale. Ila kwavile yeye alikuwa na maumivu ya miguu kutokana na ile ajali ikawa ni ngumu kwake kuweza kutembea mwenyewe mpaka asaidiwe, na wa kumsaidia kutembea mwenyewe ndio huyo amepatwa na usingizi na hata kushtuka hashtuki.
Muda kidogo Sophia akaanza kujihisi maumivu kwenye miguu na yote ni sababu ya kutokunywa dawa ambazo zilikuwa chumbani, ila kutokana na majanga yaliyowakumba sebleni kwa siku hiyo hakuweza kunywa dawa kabisa kwahiyo muda huu miguu ilikuwa ikimuuma sana na kumfanya hata alie lakini hakupata msaada kwavile hawa wa kumuhudumia walikuwa hoi na usingizi.
“Nitafanya nini mimi jamani, miguu inaniuma sana”
Kidonda kilikuwa kimevunda, alitaka kujaribu kujisukuma ili aweze kwenda kuchukua dawa ila kila alipojisukuma ndio maumivu nayo yalivyomzidia na kumfanya akose raha kabisa huku machozi nayo yakizidi kumtoka.
Giza liliingia na hapakuwa na mtu wa kuwasha taa kwavile Ibra na Siwema walikuwa hoi na usingizi, kuna upande mwingine war oho yake Sophia ukamlaumu kuwa kwanini hakula kile chakula usikute asingepata mateso yale ya kusumbuka na kidonda, huku upande mwingine ukimsifu kwa ujasiri wake kwani alihisi kile chakula cha Neema ndio kilichokuwa na mtindo wa kuwavuruga akili, ndani palikuwa na giza sana hadi kuanza kutisha mara akasikia sauti ya chura na kumfanya ashtuke sana huku akijiuliza kuwa chura ametokea wapi mule ndani kwakweli hakupata jibu ila uoga ulimjaa mwili mzima, huku akitamani nay eye apitiwe na usingizi ila usingizi haukuja kabisa na kujikuta akichanganyikiwa zaidi.
Usiku wa manane Ibra alishtuka na Siwema nae alishtuka na kuogopeshwa na lile giza walilolikuta ambapo Ibra akainuka na kujikongoja taratibu akitafuta sehemu ya kuwashia taa na alipopapata akawasha ile taa ambapo iliwaka ila walichokiona mbele yao baada ya taa kuwaka kiliwaogopesha zaidi kwani mbele yao waliona jeneza likiwa limepambwa kwa mauwa. Hakuna aliyepata ujasiri wa kuinuka na kwenda kuchungulia kwenye lile jeneza kuwa kuna nini kwani kila mtu alikuwa amejawa na uoga uliopitiliza.
Wakamshtua Sophia aliyekuwa akilia, ambapo nay eye alipoona lile jeneza alishtuka sana na ndipo hofu ilipomjaa zaidi ya mwanzo,
“Jamani tunakufa, tunakufa jamani. Tutafute msaada”
“Tutapata wapi msaada?”
“Tutoke nje, tutapata msaada tu”
Siwema alikuwa wa kwanza kuinuka na kwenda kufungua mlango ili atoke ila alichokutana nacho mlangoni kilimshtua zaidi na kumrudisha nadani kwa kasi ya ajabu,
“Vipi tena Da’Siwema?”
“Hamuwezi kuamini, hapo nje kwenu yamejaa makaburi”
“Makaburi?”
“Ndio makaburi”
Ibra akajivika ujasiri na kujaribu kwenda kuchungulia nje ambapo naye alirudi ndani kwa haraka,
“Yamejaa makaburi kweli, tutafanyaje jamani?”
“mambo haya yanamaana gani jamani?”
“Hakuna anyejua hapa, sasa tutafanyaje?”
Mara wakaona lile jeneza likifunguliwa, hapo sasa hakuna aliyeweza kustahimili kwani walijikuta wote wakizimia hata Sophia ambaye mwanzo hakulala ila hapo alizimia.
Ilikuwa ni karibia panakucha ambapo Ibra alishtuka mapema sana na kumshtua mke wake ambaye alishtuka pale pale aliposhtuliwa na Siwema vivyo hivyo ila muda huu hapakuwa na chochote pale sebleni palikuwa kimya kabisa, Siwema alikuwa wa kwanza kuongea kwa muda huu
“Jamani kwani mimi nimepatwa na nini jamani mpaka siwezi kwenda nyumbani kwangu!”
“Jaribu kutoka muda huu ila ukifanikiwa kufika nyumbani kwako tafadhari tupatie msaada maana sijui hata na sisi tunatokaje humu”
Sophia nae akaongea,
“Ila kama Da’Siwema atafanikiwa kutoka inamaana na sisi tunaweza tukatoka pia”
Basi hawakutaka kupoteza muda, ndipo Siwema alipoinuka na kuweza kufika mpaka mlangoni akafungua mlango na kutoka nje ambapo hakutaka hata kugeuka nyuma. Aliondoka kwa kasi ya ajabu hadi getini na kutoka nje kabisa ila pale nje alikutana na Neema ambaye alimwambia,
“Iwe mwanzo na mwisho kujishughulisha na mambo ya nyumba hii, ukiwa kiburi nitakuja kukukomesha nyumbani kwako. Haya potea”
Yani siwema alikimbia kama chizi na hakuangalia nyuma tena.
Ibra nae akajaribu kuinuka na kumkongoja mkewe ili waweze kutoka ila walishtukia kama mtu akiwasukuma na kuwakalisha chini.
Kisha akaona Sophia akisukumwa zaidi na kulazwa kwenye kochi ila aliyekuwa akifanya hivyo hakuonekana kabisa, Sophia akaonekana akijinyonga nyonga tumbo huku pale chini damu zikitapakaa.-
ekana akijinyonga nyonga tumbo huku pale chini damu zikitapakaa.
Ibra alimuhurumia sana mkewe ila hakuwa na la kufanya kwani hata ule uwezo wa kuinuka eneo lile hakuweza, Sophia alizidi kuugulia pale chini na baada ya muda alikuwa kimya kabisa hata kuendelea kuugulia hakuweza na ilionyesha wazi kuwa amezimia. Ibra nae akajaribu tena kuinuka na kujikuta akiweza kuinuka, kisha akasogea alipo mkewe na kumbeba kwa lengo la kumpeleka hospitali huku akijiuliza kuwa atampeleka kwa usafiri gani ila akajipa moyo kuwa ataomba msaada kwa watu nje ili wamsaidie na akaamini kuwa ni lazima atapata msaada.
Wakati anatoka nje na mke wake, akashangaa kuona gari yao ikiwa pale nje hivyo Ibra hakutaka kufikiria mara mbili kwani alifungua ile gari na kumuingiza mkewe hata hakujiuliza kuwa ile gari ililetwa na nani pale nyumbani na kwanini funguo zake zilikuwa zikining’inia muda wote kwenye mlango. Akaanza kuendesha huku akimuwaisha mkewe hospitali.
Kwa bahati akaona jingo la hospitali, ingawa ile hospitali ilikuwa ngeni kabisa machoni pake ila aliingia na gari yake kwani nia yake ni kumuwaisha mkewe kwa lengo la kupata huduma ya haraka.
Alisimamisha gari na kumshusha mke wake ambapo kuna nesi alimpokea na kumpeleka Sophia moja kwa moja kwa daktari kisha Ibra akaachwa nje na kuambiwa kuwa asubiri, Ibra akamuuliza huyu nesi
“Kwani sitakiwi kwenda kutoa maelezo ya chanzo cha ugonjwa maana mimi ni mume wa mgonjwa na mgonjwa huyu hawezi kuzungumza”
“Hata usijali juu ya hilo, kama daktari angehitaji maelezo yako basi angekuita ila kwavile hajakuita jua kwamba maelezo yako hayana umuhimu kwake”
“Samahani dada, hivi hii hospitali ni mpya eeeh maana sikuwahi kuiona hapo kabla”
“Hii hospitali ni mpya ndio na imefunguliwa mahususi kwa matatizo ya mkeo”
Kisha huyu nesi akaondoka na kumuacha Ibra akiwa na mawazo kuwa hospitali imefunguliwa mahususi kwa matatizo ya mkewe kivipi ila hakupata jibu, na pia alitamani sana kujua hali ya mkewe huko kwa daktari ila hakuwa na namna yoyote zaidi ya kusubiri majibu atakayoletewa na huyo daktari.
Ibra alikaa pale mapokezi na kujikuta akipitiwa na usingizi wa hali ya juu hata hakuweza kushtuka kwa muda huo, usingizi huo ulimpeleka mbali sana na akajikuta akiyaona maisha ya zamani aliyokuwa akiishi na mkewe na jinsi yalivyokuwa na amani yani ni tofauti kabisa na maisha waliyokuwa wakiishi kwasasa.
Sophia alipokuwa kule kwa daktari, muda huu akazinduka na kushtuka sana kwa sura ya daktari aliyoonana nayo. Daktari huyu alikuwa ni Neema na alikuwa akitabasamu tu, Sophia alianza kulia huku akimuomba Neema kuwa amuhurumie,
“Nihurumie Neema, naomba nihurumie usinitende vibaya. Kwanini uniumize hivi ilihali sijawahi kukufanyia jambo lolote baya jamani!”
Neema alikazana kucheka tu kisha akamwambia,
“Hiyo nihurumie yako haitasaidia chochote kwani nishakufanyia kitu kibaya sana”
“Kitu gani?”
“Nimekutoa kizazi”
Kwakweli Sophia alihisi kama kuchanganyikiwa aliposikia ile kauli kuwa ametolewa kizazi na kujikuta akilia zaidi,
“Jamani Neema jamani, mmekula watoto wangu ila ukaona hiyo haitoshi hadi kunitoa kizazi jamani. Kwani nimekukosea nini mimi? Niambie Neema, ni kitu gani nimekosea jamani, mbona nahukumiwa bila kosa?”
“Kumbe kosa lako hulijui?”
“Sijui kosa langu, niambie Neema”
“Kosa lako ni kukubali kuishi kwenye ile nyumba, na pia kosa la mumeo ni kununua ile nyumba”
“Kwanini jamani mnifanyie hivi, nyumba imenunuliwa mimi nakataaje kuishi? Kwani ile nyumba ina uhusiano gani na wewe? Umenitoa kizazi Neema, furaha yangu yote ya kuwa na watoto umeipoteza”
Sophia alikuwa akiongea huku akilia kwa uchungu sana kwani uonevu huu aliofanyiwa hakuwahi kuufikiria katika maisha yake ila Neema alikuwa akicheka tu na kufanya Sophia aulize tena,
“Ni nani kanileta huku mimi?”
“Ni mumeo ndio kakuleta ili nikusafishe sehemu nilipokutoa kizazi”
“Jamani, kwanini Ibra ananifanyia hivi? Je mnajuana na Ibra? Kwani mimi kosa langu kubwa ni nini jamani?”
“Ibra najuana nae sana tu ila hajui kama najuana nae, Ibra usimuone vile aliwahi kumfanyia vibaya sana mdogo wangu na ndiomana nilifurahi sana kumuona ananunua nyumba ambayo ni himaya yangu ila wewe kiherehere chako cha kuhamia pale ndio kimekuponza”
“Ibra alifanya unyama gani sasa?”
Sophia alikuwa akilia huku akimsikiliza huyu Neema kwani kwasasa uoga wote ulimuisha na hatakama angeendelea kuwa na uoga basi Isingesaidia chochote kwani Neema alishatawala nusu ya mawazo yake.
Neema akamuangalia Sophia kisha akamwambia,
“Sitakuelezea kwa maneno ila ngoja nikuonyeshe ili usifikirie namsingizia mume wako, na kama mkipata muda wa kuongea muulize atakujibu kuhusu hizi tuhuma zangu”
Sophia alitulia tu, kisha Neema akanyoosha mkono wake ambapo ilikuwa kamavile Sophia anaangalia sinema.
Alimuona Ibra akiwa amekaa mahali na binti mmoja, yule binti alisikika akimwambia Ibra
“Ibra jamani, tulikuwa wote halafu leo hii unaikana hii mimba yangu?”
“Hivi Nancy kwa haraka haraka unataka nikwambie nini? Maisha yangu unayajua, kula kwa shida kulala kwa shida, hiyo mimba siitambui na siko tayari kuitwa baba kwasasa”
“Najua kwanini unanikataa, ni kwasababu ya yule mwanamke uliyemposa”
“Yule mwanamke nampenda na hata familia yangu inampenda pia na amekubali kuishi na mimi kwa hali yoyote ile halafu gafla aibuke mtu ana mimba unafikiri atakubali? Hiyo mimba siitambui”
“Inamaana mimi ulikuwa hunipendi eeeh!”
“Sikia Nancy nilikuwa nakupenda vizuri ila unajua wazi ni kwanini mimi na wewe hatuwezi kuishi pamoja wala kuoana. Kwahiyo sahau kuhusu mimi. Kwanza familia yenu kwa maelezo yako tu inaonyesha wazi nyie ni Malaya, dada zako wote hawajaolewa na hakuna mwanaume anayeweza kuwaoa nyie, yani sahau kuhusu mimi kabisa”
“Na hii mimba je?”
“Nimekwambia siitambui, hivi kwanini hutaki kunielewa? Kwanza haiwezekani ikawa mimba yangu, na wala haitakuwa ajabu wewe kuzalia nyumbani maana kwenu wote wamezalia nyumbani na ambao hawajazaa nadhani hawana vizazi hivyo achana na mimi kabisa, niache na maisha yangu, niache niishi kwa amani na mwanamke wa maisha yangu, mwanamke ninayempenda na anayependwa na familia yangu, mwanamke ambaye naendana nae na ninaweza kuishi nae na kufunga nae ndoa”
Huyu binti alionekana akiinama na kuanza kulia, Ibra akainuka ili kuondoka na kutaka kumuacha yule binti kwenye lile eneo, ambapo huyu binti aliinuka na kumfata Ibra kwa nyuma ila Ibra alipogundua anafatwa akageuka na kumsukuma yule binti ambapo alimuacha akiwa ameanguka chini na kuondoka. Ila huyu binti alisikika akisema neno moja tu,
“Ibra asante”
Ile picha ikapotea kisha Neema akamuangalia Sophia na kumwambia,
“Mdogo wangu alirudi nyumbani akiwa analia sana na kwakweli nilimuonea huruma iliyopitiliza, kumbe mdogo wangu akapanga kutoa ile mimba na kwenda kunywa vidonge vilivyopelekea kupatwa na umauti. Niliapa kulipa kisasi kwa Ibra ila kwa bahati mbaya na mimi nikaja kupatwa na majanga yaliyopelekea niwe nilivyokuwa sasa”
“Majanga gani?”
“Hiyo sio kazi yako kujua, ila tambua kwamba kitendo change cha kukutoa kizazi wala sijakuonea yani ni saizi yako kabisa”
Sophia alikuwa kimya akilia muda huu kwani bado hakuona kama alistahili kubeba lawama za mume wake, yani makosa yaliyofanywa na mumewe kipindi cha nyuma huko haikupaswa alipiziwe yeye, alilia sana huku akimuomba Neema aweze kumuachia sasa aondoke.
“Nakuruhusu ondoka ila nenda kauamshe mzoga wako pale nje maana ule mzoga wako hautumii akili hata kidogo nab ado nitawaendesha sana hadi pale akili zenu zitakapowakaa sawa”
Sophia akajitahidi kujaribu kusimama na akaweza kisha akaanza kujikongoja ili aweze kutoka pale nje, alishangaa kuona ile hospitali haikuwa na mtu mwingine yeyote zaidi ya Neema na kujiuliza kuwa kwanini Ibra aliamua kumleta hapo.
Alimkuta Ibra akiwa kalala hajitambui kabisa, akajaribu kumuamsha naye Ibra akaamka na kumuangalia mkewe,
“Sophia! Umepona, unaendeleaje mke wangu?”
“Naomba tuondoke mahali hapa Ibra”
“Unaendeleaje? Je tushalipia bili?”
“Naomba tuondoke Ibra”
Basi Ibra akaamua amsikilize mkewe na kuanza kumkongoja hadi kwenye gari lao ili wapande,
“Hivi wewe Ibra hiyo akili yako itarudi lini? Nilikwambiaje kuhusu hili gari, kwanini bado waling’ang’ania kila leo kuwa tuwe tunalipanda? Na nani aliyekutuma kunileta hapa? Hiyo gari sipandi, haya tuondoke”
“Sasa tutaondoka na usafiri gani Sophia?”
“Wowote ila hilo gari sipandi”
“Kwahiyo niliache hapa?”
“Unataka ulipeleke wapi sasa ikiwa gari lenyewe huwa linakufata ulipo”
Sophia alikuwa akiongea hayo huku akijikongoja mwenyewe ili atoke kwenye eneo lile ikambidi Ibra afatane tu na mke wake na kukongojana hadi kutoka, walipofika nje kabisa ya eneo lile
“Haya sasa tunaendaje nyumbani?”
“Tutafute usafiri wowote tu, na tena sitaki unirudishe kule nyumbani. Nataka unipeleke nyumbani kwetu”
“Sophia, Sophia jamani unajua fika kwenu kulivyo mbali halafu twende bila usafiri hivi tutafikaje ilihali gari tumeliacha ndani ya hospitali? Ngoja nikalichukue bhana”
Ibra akageuka nyuma ili akachukue gari yao ila alishtuka sana kwa alichokiona kwanoi hakuona tena lile jingo kubwa la hospitali na badala yake akaona makaburi na kumfanya amkumbatie mkewe kwa nguvu sana,
“Angalia Sophia”
“Nini tena?”
“Weee angalia”
Sophia nae akageuka kuangalia akashangaa pia kuona makaburi kisha akasema,
“Nilijua tu, Neema si mtu mzuri. Upumbavu wako Ibra ndio unaonitesa sasa”
Ibra hakutaka kuulizana chochote hapo na mke wake hivyo akaamua kumkongoja na kuanza kutoka kwenye eneo lile, alikongojana nae hadi barabarani na walipofika walikaa chini kwa muda ila Sophia bado alikuwa na kinyongo sana na aliendelea na msimamo wake ule ule kuwa usafiri ukipatikana basi apelekwe moja kwa moja nyumbani kwao
“Kwanini tusirudi nyumbani kwetu tu Sophia?”
“Ibra tafadhali, yaliyonipata yananitosha sana tu tena hayakustahili kunipata, sitaki makubwa zaidi naomba nirudishe kwetu”
“Kwani ni mambo gani yamekupata?”
“Hivi unajua kuwa mimi sina kizazi tena!”
Huna kizazi! Kivipi?
“Neema amenitoa kizazi na yote ni kwasababu yako”
“Kwasababu yangu! Kivipi?”
“Unamfahamu Nancy?”
“Nancy? Ndio nani huyo?”
“Mwanamke uliyekuwa nae kabla ya kuniposa mimi”
“Kheee yule Malaya, nani kakudanganya kuwa nilikuwa nae?”
“Basi kwa taarifa yako, yule Neema ni dada yake na huyo Nancy”
Ibra akashangaa na kumuuliza mkewe,
“Sasa undugu wa Neema na Nancy unahusiana vipi katika maisha yetu?”
“Wewe si ulikataa mimba ya Nancy?”
“Haikuwa mimba yangu ile”
“Ila si ulitembea nae?”
“Sophy tafadhali tuachane na hizo habari, hayo mambo yalishapita kitambo sana”
“Yalipita wakati ndio umenisababishia matatizo yote haya, yani mimi sitaweza kuzaa tena kwasababu yako na ufirauni wako”
“Sophy, wewe ni mke wangu, habari za hivyo si nzuri zitaharibu ndoa yetu”
“Ziharibu mara ngapi? Ibra, nirudishe nyumbani tu akili yangu ikawe sawa kwanza”
Kwavile Ibra alishamuona mkewe kapaniki akaamua kutafuta usafiri ili waweze kuondoka kwenye eneo hilo kwani alihisi ndio kunakomfanya mkewe apaniki zaidi huku akijiuliza kuwa ni nani kampa habari zisizoeleweka mke wake.
Ibra akasimama ili aangalie usafiri, mara akaiona gari ya kukodi na kuisimamisha kisha akamuomba mke wake waweze kwenda kupanda gari lile,
“Hapana Ibra siwezi kupanda hilo gari sina imani nalo”
“Sophy, Sophy tafadhari usinichanganye. Umeniletea mada za ajabu hapa halafu natafuta usafiri tupande unaleta mada zingine, sitaki ujinga”
Ibra akamuinua mkewe kwa nguvu na kumpakia kwenye lile gari, ila baada ya kupanda tu wote wakashangaa kwani yule dereva wa mwanzo alikuwa mwanaume na mara hiyo hiyo akawa mwanamke. Wakati wakishangaa mara lile gari liligeuka na kuwa jeneza.
Hakuna aliyeweza kustahimili wakajikuta wakianza kupiga kelele lakini hakuna mtu yeyeto aliyejitokeza kuwapatia msaada na kufanya wazidi kushikwa na uoga tu, wakahisi kama kuna mtu pembeni yao kwenye lile jeneza kwani walikuwa wamelazwa kabisa, Ibra akajaribu kuangalia ni kweli akaona mtu amewekwa pamba puani na mdomoni kwa maana kwamba mtu huyo alikuwa ni marehemu. Hapo ndio uoga uliwazidi maradufu na kujikuta wakitetemeka kupita maelezo ya kawaida huku kila mmoja akishindwa kustahimili hali ile. Kwa uoga waliokuwa nao wakajikuta wamezimia.
Wakati wamezimia, Ibra alikuwa akijiona kwenye eneo la tofauti kabisa, kwani muda huu alijiona yupo kwenye jeneza na anaenda kuzikwa, nke aliwasikia watu wakizungumza,
“Hivi imekuwaje huyu hadi amekufa?”
“Alikuwa akitoa mimba, sasa kwa bahati mbaya ndio huyo amekufa”
“Kheee jamani masikini, si bora angejizalia tu loh!”
“Yani nasikia aliyempa mimba aliikataa mimba ile ndiomana akaamua kuitoa ila mweisho wa siku ndio hiyo imempelekea kwenye mauti”
“Dah! Wanaume ni viumbe wabaya sana, ona sasa kasababisha dada wa watu kujiua”
Ibra akiwa mule kwenye jeneza akawa najiuliza kuwa imekuwaje chanzo cha kifo chake ni kutoa mimba ilihali yeye ni mwanaume na hawezi kubeba mimba, na vipi wasemwe wanaume ni watu wabaya wakati nay eye ni mwanaume? Akaendelea kusikilizia, na akawasikia kuwa wameshafika makaburini sasa wanataka kumzika huku vikisikika vilio kutoka kwa watu mbali mbali. Mara aliona kamavile jeneza limeshashushwa kwenye shimo kisha akasikia akianza kumwagiwa mchanga, Ibra akaogopa sana kuona vile kuwa anataka kuzikwa, akajikuta akipiga kelele kwa nguvu sana.
“Jamani msinizikeeeeeee……….”
Akajikuta akishtuka huku akiangaza macho huku na kule, akashangaa kuona watu wengi sana wamejaa na moja kwa moja akahisi kuwa watu hao wanataka kumzika kwahiyo Ibra aliinuka pale na kuanza kukimbia, wale watu walijaribu kumkimbiza bila ya mafanikio na kuamua kumuacha atokomee tu.
Mahali pale alibaki Sophia sasa huku akiwa amezungukwa na watu wengi sana, ambapo kuna wengine waliamua kumsaidia kunyanyuka na kwenda nae pembeni wakitaka kujua kilichompata ilihali hata yeye mwenyewe alihitaji kujua kilichotokea hadi yeye kuwa pale alipozungukwa nao, aliwauliza watu wale kwa mshangao,
“Kwani nini kimetokea kwangu?”
“Tumekukuta hapo pambezoni mwa barabara, wewe na yule kijana aliyekimbia mlikuwa hamjitambui kabisa ndipo tukaamua kuchukua maji na kuwamwagia ili mzinduke ila cha kushangaza yule kijana alipozinduka alipiga kelele kwa nguvu kuwa tusimzike kisha akaanza kukimbia na tumejaribu kumkimbiza bila ya mafanikio. Kwani nini kimewapata?”
“Kwakweli hata sijui yani sijui kabisa”
“Je yule kijana unamfahamu?”
“Ndio ni mume wangu”
“Dah! Pole, sana. Eeeh tukusaidiaje sasa, tukupeleke hospitali au?”
“Mi nitafurahi kama mkinipeleka nyumbani kwetu jamani maana hata sijui kama wanajua ninavyoendelea”
“Sawa, basi utatuelekeza huko kwenu tukupeleke ila nadhani itakuwa vyema kama ukila kabisa”
Kisha watu hawa wakamletea Sophia chakula ambapo alianza kula kama anakimbizwa kwani alikuwa na njaa sana, kila mmoja alimuhurumia kwani alionekana wazi kuwa ana matatizo.
Sophia alipomaliza kula sasa aliweza kukumbuka matukio yaliyompata mwishoni kabla ya kukutwa wakiwa wamezimia na mume wake, akakumbuka kuwa mwishoni walipanda gari ya kukodi na kujikuta kwenye jeneza badala ya gari. Sasa akafikiria ukarimu wa watu hawa waliowasaidia kama ni watu kweli au ni kati ya yale mauzauza yakiendelea, akawa anajiuliza moyoni tu,
“Hivi hawa ni watu kweli wameamua kunisaidia au ni kati ya mauzauza jamani?”
Wakati akiwaza hayo, kuna mmoja alimsogelea Sophia na kumwambia kwa sauti ya chini kabisa,
‘Hawa si watu kama unavyofikiria, yani watu kweli ni wale tuliwaacha nje ila hawa humu si watu hakuna mtu hapa”
Sophia akaanza kushikwa na uoga kwani kila muda unavyozidi kwenda mbele ndivyo anavyoona kuwa maisha yake yapo hatarini,
“Sina makosa mimi, nisameheni”
“Usipige kelele Sophy, kuwa mpole mimi nitakusaidia”
“Nitaamini vipi kama utanisaidia ikiwa na wewe ni mmoja wao?”
“Sikia nikufundishe kitu, wakikwambia uwaelekeze kwenu ili wakupeleke waambie naomba nikae kae hapa kwa muda halafu ndio nitaenda huko kwetu maana sina amani nako. Na wakikuuliza kama kuna jambo lolote unakumbuka kuwa lilikutokea kabla ya kupoteza fahamu waambie kuwa hukumbuki chochote umesikia?”
Sophia akamuitikia huyu mtu ambaye alionekana ni mtu wa kawaida tu kama wale wengine ingawa mwenyewe alidai kuwa wale si watu wa kawaida. Kisha huyu mtu akamwambia tena Sophia,
“ Na ukiona chochote mbele yako usishtuke hatakama ukiona jeneza hata usishtuke yani chukulia kawaida tu maana kushtuka kwako kutakupoteza”
Sophia akaitikia huku akijiuliza mahali atakapopata huo ujasiri wa kutokushtuka na uoga aliokuwa nao kwakweli alihisi kama kuchanganyikiwa sasa. Yule mtu akaondoka na kumuacha Sophia akiwa amebaki mwenyewe.
Muda kidogo wakaja wale watu waliomsaidia Sophia ambao walikuwa kama watano hivi ukiongeza na yule mmoja aliyekwenda kuongea na Sophia peke yake, wakaanza kumuuliza maswali Sophia,
“Je unakumbukumbu zozote za kilichokupata hadi tukakukuta pale?”
“Hapana sikumbuki chochote”
Sophia alijibu huku akiwaza kuwa huenda yule mwingine ndio mbaya, pengine hataki hawa binadamu waujue ukweli ila akajipa moyo tu kwani hakuwa na chochote cha kufanya ukizingatia mazingira yale alikuwa hayafahamu na wala wale watu waliomsaidia hakuwafahamu kwahiyo cha msingi na muhimu ni kuwa mpole tu. Kisha hawa watu wakamuuliza tena,
“Vipi tukupeleke kwenu? Tuelekeze ili tukupeleke”
“Nawaombeni nikae hapa kidogo, msinipeleke kwetu kwanza maana sikumbuki chochote labda mambo mabaya yalinipatia huko kwetu”
“Mmmh pole sana, kwahiyo hutaki kwenda kwenu kabisa?”
“Nitaenda tu, ila kwasasa nawaomba kwanza akili yangu ikae sawa maana haipo sawa na sina imani na nyumbani kwetu”
Hawa watu hawakuongea zaidi ila walimuacha Sophia pale na kutoka katika eneo lile, muda kidogo Sophia aliona kundi kubwa la watu likiingia mule ndani huku wakilia na kuomboleza, wakaonekana vijana wakiwa wamebeba jeneza. Hofu ikamshika Sophia ila akakumbuka maneno ya yule mtu kuwa asistuke wala nini kwahiyo akajipa moyo na kutulia, wale watu wenye jeneza walikuja na kukaa karibu yake huku wakilia sana ila Sophia alikuwa ametulia tu na ili kujiepusha kushtuka akaamua kuhamisha mawazo yake kutoka eneo hilo yani ingawa alikuwa pale akiwatazama alkini mawazo yake hayakuwa hapo kwabisa.
Muda mrefu kidogo ukapita huku wale waomboleaji wakiendelea na kazi yao ya kuomboleza na wengine kuendelea kulia huku wakiimba nyimbo, muda kidogo akasikia wakizungumza
“Tutaenda kumzika mpendwa wetu Sophia kwenye yale makaburi ya juu”
Alitaka kushtuka ila akasizi kidogo na kutulia ili ile hali isimsumbue zaidi, akawaona wengine wakizidi kulia kisha lile jeneza likabebwa na kutolewa mahali pale kisha kimya kikatawala halafu wakaja tena wale watu watano. Mmoja akamuuliza Sophia,
“Mbona unaonekana kuwa na mawazo sana?”
“Ni kweli nina mawazo sana ila ninachowaza ni kujaribu kukumbuka kilichonipata”
“Hujaweza kukumbuka chochote?”
“Sikumbuki kitu”
“Je hujaona watu humu ndani wakiwa wamebeba jeneza?”
“Saa ngapi hao watu wameingia?”
“Kweli inaonyesha kuwa na mawazo sana”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Yuel aliyekuwa akimtonya Sophia mwanzoni kabisa alionekana kutabasamu na ilionyesha wazi akifurahia majibu yale ya Sophia, wenzie wakamuangalia na kumuuliza
“Mbona unafurahi sasa?”
“Sifuwahi kama mnavyofikiria ila ananishangaza sana huyu binadamu”
“Kivipi?”
“Anakosaje kumbukumbu jamani?”
“Kwahiyo tufanyeje?”
Mmoja akaonekana kuwatahadharisha wenzie,
“Jamani taratibu, asije kugundua”
Kisha wakaondoka tena na kumuacha Sophia eneo lile, moja kwa moja Sophia aliweza kuelewa kuwa hawa hawakuwa binadamu wa kawaida ila tu hakuelewa kuwa wamepanga kumfanyia jambo gani. Akatulia sasa huku akijiuliza zaidi kuwa hatma yake itakuwa ni nini maana hakuelewa mwanzo wala mwisho.
Wakati akitafakari, yule mtu wa mwanzo akamjia tena Sophia na kuzungumza nae kwa sauti ya chini kabisa.
“Usiogope chochote, kwa hili mimi nitakusaidia”
“Utawezaje kuwasaliti wenzio si watagundua?”
“Wee jiulize tu, nawezaje kuja hapa na kuzungumza na wewe bila ya wao kujua. Nakuhurumia sana Sophia, adhabu ulizopata zinatosha kabisa wala hazistahili kuendelea juu yako na wala sioni kosa lako ndiomana nasema nitskusaidia”
“Nitashukuru sana ukinisaidia”
“Usijali kuhusu hilo kabisa, amini kuwa nitakusaidia Sophia”
Kisha kimya kidogo kikatawala, na huyu mtu akaanza tena kwa kumwambia Sophia kuhusu mpango aliopangiwa sasa,
“Wanahitaji kukupeleka porini, kwahiyo wakija hapa na kukwambia kuwa twende nje ukapunge hewa unatakiwa ukatae”
“Wakinilazimisha je!”
“Tambua kwamba uwezo wa kukulazimisha kufanya chochote kile wanao ila kwasasa inatakiwa ukubali mwenyewe kwa hiyari yako kwani lengo kubwa ni kukumaliza kabisa na ili kukumaliza lazima wewe ukubali mwenyewe kwa hiyari yako”
Sophia akabaki kushangaa tu na kujiuliza kwanini wanahitaji kummaliza kabisa na kwanini anatakiwa kukubali mwenyewe kwa hiyari yake, huyu mtu akamjibu Sophia,
“Iko hivi, mfano ukiwa umelala gafla kwenye ndoto akatokea nduguyo aliyekufa miaka mingi iliyopita na kukuomba umfate kwani alipo ni pazuri sana, unapokubali ni kwamba umeridhia kwa hiyari yako na mara nyingi hazitapita siku nyingi sana utakuwa umekufa kweli na kumfata ndugu yako huyo ila ukikataa ndio pona yako hata kama ulianza kuumwa utashangaa unapona sababu ya kukataa kuongozana nae. Kuna vitu huwa tunafanya kwa kulazimisha ila vingine inatakiwa muhusika akubali mwenyewe kwa hiyari yake, na kwa hali iliyofikia kwako kwasasa unatakiwa ukubali kwa hiyari yako mwenyewe ili tukumalize kabisa”
Sophia akatulia kimya kwa muda na kujikuta akikumbuka stori za zamani alizowahi kuambiwa na mama yake, akakumbuka kuwa mama yake aliwahi kumsimulia kuhusu kifo cha mamake mdogo amabpo inasemekana aliitwa na kaka yao ambaye ni mjomba wake marehemu. Mamake mdogo kipindi hiko alianza kuumwa taratibu na baada ya kusimulia huo mkasa wa kuitwa na kukubali alikufa baada ya siku mbili, mama yake alikuwa akiwasimulia huku akiwasisitiza kuwa wasipende kuitika wakiwa ndotoni na wasikubali chochote kama kuitwa na marehemu wakiwa ndotoni kwahiyo akahusisha matukio haya na alichokuwa akiambiwa na huyu mtu. Kimya kilitawala kwani huyu mtu alihitaji Sophia aweze kutafakari, kisha akaendelea kumwambia.
“Chochote watakachokwambia uwe unakataa kabisa yani usikubali chochote kile, halafu itatubidi twende kwa mkuu kushtaki kuhusu jambo hili na kuomba ruhusa ya kutumia nguvu. Wakati wa kwenda kwa mkuu mimi nitabaki hapa na kudai kuwa natakiwa kukulinda kwani bado hatuna imani na eneo hili kisha wao wataondoka. Hapo nitakusaidia kurudi kwenu na tafadhari nikikufikisha njia ya kwenda kwenu usigeuke nyuma”
Huyu mtu akaondoka na kumuacha Sophia peke yake akiendelea kutafakari kwani alikuwa kama mti asiyejielewa kabisa kwa wakati huo na alionekana wazi kutokujua cha kufanya.
Wakati Sophia amekaa hapo, wale watu watano wakaja tena huku wakiwa na zile hoja alizoambiwa na yule mmoja wao.
“Sophia, tunahitaji twende wote nje ukapunge upepo. Tafadhari inuka twende”
“Hapana jamani, niacheni kwanza hapa”
“Kwanini lakini Sophia? Hutaki kuona hali ya nje? Hutaki kuona kama ni usiku au mchana?”
“Mi najiona salama zaidi nikiwa hapa, tafadhari niacheni hapa”
“Basi simama kidogo ujinyooshe”
“hapana, hata sijisikii uchovu wa kujinyoosha”
“Hata kusimama kidogo hutaki jamani?”
Sophia aligoma kabisa na aliona wazi sura za hawa watu zikijawa na hasira kwa kugoma kwake na walionekana wazi wakitamani kumlazimisha ingawa hawakufanya hivyo, wakainuka na kutoka nje kisha kimya kirefu kikatawala.
Muda kidogo alirudi yule mmoja na kumwambia Sophia,
“Haya sasa wameondoka, rudi nyumbani kwenu. Fumba macho”
Sophia akafumbua macho na gafla akajiona kuwa amesimama mahali, huyu matu akamwambia Sophia,
“Fumbua macho”
Sophia akafumbua na kujiona yupo kwenye njia ya kuelekea nyumbani kwao, huyu mtu akamwambia tena Sophia
“Kumbuka usigeuke nyuma, hata ukisikia mtu anakuita usigeuke nyuma. Hakikisha hadi unaingia ndani kwenu bila kugeuka nyuma, yani kosa la kugeuka nyuma utajutia maisha yako yote kupita unavyojutia sasa. Kwaheri”
Huyu mtu akatoweka kisha kimya kikubwa sana kikatawala kwenye eneo lile ambapo Sophia alisimama kwa muda kwanza.
Kisha Sophia akaanza kusonga mbele kurudi kwao, ni kweli akasikia sauti nyingi zikimuita kwa nguvu ila Sophia hakugeuka nyuma kabisa hadi alipofika nyumbani kwao.
Alishangaa pale kwao kukiwa kuna watu wengi sana, na sauti zilisikika wakilia na kuomboleza huku wakitaja jina lake.
Sophia alisita kusogea kwa muda huku akitafakari kuwa pale kwao kwanini watu walijaa na kwanini walikuwa wakilia huku wakitaja jina lake, akawa amesimama kwanza akisikilizia mara akasikia sauti ikimuita kwa nguvu sana ila akakumbuka maneno ya yule mtu kuwa asigeuke nyuma hadi atakapoingia ndani kwao kwahiyo akajipa ujasiri wa kutokugeuka. Wakati amesimama hapo, akahisi kuna mtu amemshika bega kanakwamba ageuke ili amtazame ila Sophia alijivika ujasiri wa hali ya juu na kuendelea kutembea mbele bila hata ya kugeuka, huyu mtu alisikika akimwambia Sophia,
“Jamani Sophia wewe, hata kugeuka kidogo jamani. Hivi unajua ni kitambo sana hatujaonana!”
Ile sauti ilikuwa ni sauti ya rafiki kipenzi wa Sophia ila bado alijipa ujasiri wa kutokugeuka kabisa.
Akafika mlangoni sasa na kuingia ndani huku akiwa amewapita watu wote pale nje bila ya kugeuka wala nini, alimuona mama yake akiwa amelala hini akilia, akamuona mdogo wake akionekana kuomboleza sana. Sophia akaita,
“Mama”
Sauti hii ilimshtua kila mtu aliyekuwepo eneo lile, na gafla watu wakaanza kupiga kelele huku wakikimbia hovyo hovyo ila Sophia alisimama eneo lile lile akiwaangalia tu.
Kisha akaamua kusogea alipo mama yake ambaye alikuwa akitetemeka tu, Sophia akamuita tena mama yake;
“Mama”
Mama aliinama kwa muda kisha akainua macho yake na kumuuliza mwanae,
“Ni wewe kweli mwanangu au naota? Siwezi kukimbia, sina nguvu mimi. Kama ni mwanangu kweli basi namshukuru Mungu kwa hilo”
“Ni mimi mama, mimi ni mwanao Sophia”
Mama Sophy akamgusa mwanae, kisha akamkumbatia huku machozi yakimtoka, huyu mama alilia sana na alilia kwa muda mrefu na kumfanya Sophia nae alie huku akimbembeleza mama yake.
Baada ya muda wakatulia sasa, mama Sophy alimshika tena mwanae na kumuuliza,
“Nini kimekupata mwanangu?”
“Ni historia ndefu sana mama, ila mbona watu wote hapa wamekimbia kwanini?”
Huyu mama akapumua kidogo na kuanza kumueleza Sophia,
“Mwanangu, hapa tupo kwenye msiba wako na leo ilikuwa ni siku yako ya mazishi yani hapa. Ndiomana kila mtu amekimbia, hata mimi bado siamini kama ni wewe najihisi kamavile nipo ndotoni”
“Sasa mama, mnanizikaje bila maiti yangu?”
Huyu mama akashtuka sana, kisha akamuangalia tena mwanae
“Sophy mwanangu umekufa, na maiti yako ipo hospitali yani hivi ninavyoongea kuna nduguzo wameenda kuichukua ili tuje kuzika. Hapa watu wote walikuwa wakingoja maiti yako ili tukazike”
Sophia akapumua kidogo kwani alishindwa kuelewa moja kwa moja kuwa tayari hata kufa alishakufa, machozi yakamtoka na kumwambia mama yake
“Lakini mama, mimi ni mzima kabisa sijafa mimi”
“Mwanangu, mimi ni mama yako na ninaamini kuwa umerudi tena mwanangu na nimefurahi sana lakini najua kwa wengine itawachukua mud asana kuamini hilo”
Mama Sophy akamkumbatia tena mwanae.
Mara gafla wakasikia sauti kutoka nje,
“Kheee imekuwaje hapa, mbona watu wote hawapo?”
“Sijui jamani, maana nahisi kuchanganyikiwa kabisa. Jana nilihakikisha kwa macho yangu maiti ya Sophy kisha ikarudishwa tena monchwari eti leo haipo kwakweli haiwezekani jamani”
Sasa wakawa wanazungumza hivyo huku wakiingia ndani na kukutana macho kwa macho na Sophia, kwakweli hakuna aliyeweza kustahimili kwani wote walikimbia na hawakugeuka hata nyuma kwahiyo bado Sophia alibaki pale na mama yake huku Sophia akijaribu kumdadisi mama yake kuhusu hiko kifo chake kuwa ilisemekana aliumwa na kitu gani hadi kufa.
“Tuliambiwa ajali mwanangu, yani kwenye hiyo ajali umekutwa mwili wako tu. Inasemekana ulikuwa na mume wako ila nasikia alikimbia baada ya kuzinduka. Tena tumeambiwa wiki imepita na ulipelekwa hospitali wakitafutwa ndugu zako na tulipopatikana wakaenda dada zako kuhakikisha na kweli wanasema walikukuta ni wewe”
Sophia aliishia kushangaa sana kwani hakumbuki kama na mumewe walipata ajali ila anachokumbuka ni kuwa walikutwa pale chini kisha yeye kuchukuliwa na wale watu waliojifanya kuwa ni wasamalia wema wanataka kumsaidia.
Kimya kikatanda kisha mtu mmoja mmoja akaanza kurejea pale nyumbani kwakina Sophia huku wakiogopa kumsogelea Sophia mpaka pale mama Sophy alipokuwa akiwahakikishia kuwa yule ni Sophia tena ni mzima kabisa, walifurahi kusikia vile kuwa Sophy ni mzima kabisa ila bado walishikwa na uoga juu ya uzima wa Sophia.
Mwishowe karibia familia nzima iliwasili pale nyumbani huku wakijaribu kuzungumza mawili matatu na Sophy waweze kuhakikisha kuwa ni yeye ila mama Sophy alimuhurumia mwanae kwani alionekana kuchoka sana hivyo akamtaka mwanae apumzike, Sophia aliamua kwenda kuoga kwanza kisha wakampa chakula na kwenda kupumzika ambapo mama yake alienda na kulala pembeni ya mtoto wake.
Familia ya Sophy bado hawakuelewa kuwa ni nini kilichotokea mpaka imekuwa hivyo ukizingatia kuna ndugu zake kabisa waliohakikisha maiti ya Sophy na kugundua kuwa ni kweli amekufa. Kitendo cha wao kwenda na kuikosa kiliwashangaza sana na kuhisi kama wanafanyiwa mchezo hospitali ila kitendo cha kumkuta Sophia nyumbani ndio kilichowashangaza zaidi.
Kwa upande wa Sophia hakuweza kulala wala nini kwani picha ya matukio katika maisha yake ilikuwa ikimjia kichwani mara kwa mara haswaaa tukio lake la kutolewa kizazi, yani lilikuwa likijirudia kama sinema vile ila ndio jambo halisi lililomtokea katika maisha yake ingawa kila alipolifikiria mwili wake wote ulisisimka na ndipo alipowaza pia kuhusu Ibra ila hakupata jibu kuwa mumewe huyo yupo mahali gani. Kwakweli Sophia hakuweza kulala kabisa, kwani alikuwa akilala kidogo na kushtuka, bado alikuwa na uoga na nyumba aliyokuwa akiishi.
Kuna muda usingizi ukampitia na akaona kitu kwenye ndoto, alimuona yule mtu aliyemsaidia akimwambia,
“Kuna umuhimu wa wewe kwenda kukutana tena na yule bibi aliyekupa dawa za kurudisha akili yenu, nenda ukaonane nae na kwa hakika utatambua mengi sana na pia atakusaidia kwani hapa sio mweisho wa wewe kufatiliwa. Ilimradi uliingia kwenye ile nyumba basi utafatiliwa siku zote, kwahiyo kwa ushauri wangu jitahidi ukaonane na yule bibi kwanza kabla mambo hayajawavurugikia hapo kwenu pia”
Sophia alionyesha kuelewa vizuri sana na alipoamka sasa hivi kulikuwa kumekucha kabisa.
Sophia akamuamsha mama yake, ambaye alimka na kutoka nae nje ambapo bado kulikuwa na hali kama ya matanga vile kwa uoga ambao walikuwa nao.
Muda huu wa asubuhi walikuja wazee wa eneo lile na kuwataka wafanye tambiko juu ya Sophia kwani ni jambo la ajabu sana lililotokea,
“Ilitakiwa tambiko hili lifanyike jana ila kwavile kila mtu alishikwa na mshtuko basi hatunabudi kulifanya leo. Tulijua Sophia amekufa na tukachimba kaburi kwaajili ya kumzika ila kwavile imetokea yupo hai basi hatunabudi kufanya tambiko na kwenda kufukia lile kaburi ili tuondoe huu uchuro.”
“Sawa, sisi kama familia tumeafikiana na hilo. Kwahiyo tutafanya tambiko gani?”
“Tutachinja mbuzi, kisha mbuzi huyo tutaenda kumzika kwenye lile kaburi kwa niaba ya Sophia”
Wakakubaliana juu ya hilo kisha ndugu wa Sophia wakajitoa kwenda kutafuta huyo mbuzi wa kumfanyia kafara na walipompata walikuja nae ambapo yalifanyika matambiko kisha yule mbuzi akachinjwa halafu wote kwa pamoja wakaanza safari ya kuelekea makaburini kwa lengo la kumzika mbuzi huyo katika kaburi ambalo lilichimbwa mahususi kwa lengo la kumzika Sophia. Nyumbani walimuacha Sophia, mama yake na baadhi ya ndugu zake ila wengine wote walielekea makaburini kwa lengo la kumalizia hiyo kafara.
Cha kushangaza walipofika pale makaburini walikuta lile kaburi walilolichimba kwa lengo la kumzika Sophia likiwa tayari limeshafukiwa kanakwamba kuna mtu mwingine amezikw hapo,
“Imekuwaje jamani? Au sio hapa?”
“Ndio hapa hapa, na tuliochimba ni sisi wenyewe”
“Au pengine kuna watu walijiongeza na kuja kufukia?”
“Inawezekana ikawa hivyo”
“Sasa tutafanyaje na huyu mbuzi?”
Mmoja akatoa wazo kuwa wachimbe pembeni yake na wazike huyo mbuzi kwani lengo lao ilikuwa ni kumzika na si vinginevyo, hivyobasi wakaamua wafanye hivyo na kuchumba pembeni kidogo ya lile kaburi na kumzika yule mbuzi kisha wakaondoka na kurudi nyumbani.
Walirudi moja kwa moja na kuwataarifu yaliyotukia huko makaburini kisha wakaondoka zao na kuwaacha ndugu tu pale.
Sasa waliamua kuweka kikao cha familia ambapo walielezana kwa urefu kuhusu kule makaburini,
“Nadhani vijana wa hapa waliamua kujiongeza baada ya kuona mambo yale wakaamua kwenda kufukia lile shimo”
Sophia alikuwa kimya tu kwani mashaka yake ilikuwa ni huenda Neema ndiye amefanya yote hayo na wala sio vijana wa mtaa huo, wakati wanafamilia wanajadili Sophia hakuchangia mada yoyote ile ikabidi wamuulize kutokana na ule ukimya wake,
“Sophia”
Kwanza akashtuka kwa kuitwa na kusikilizia wamemuitia nini,
“Wewe unashauri kitu gani kuhusu hili?”
“Nashauri mnipeleke huko makaburini nikaone hilo kaburi mlilonichimbia”
Wote wakamuangalia kwa makini kisha wakamuuliza tena,
“Hivi unajua tunazungumzia kitu gani?”
“Kwani mnazungumzia nini?”
Ni wazi kuwa Sophia hakuwa eneo hilo kimawazo kabisa ndiomana alijikuta akiongelea kitu cha mwanzo kabisa ambacho alisikia wakiongea,
“Pole sana, inaonyesha mawazo yako hayapo hapa kabisa, usijali huko makaburini tutakupeleka kesho nawe pia utaenda kuona. Ila hapa tulikuwa tukijadili jambo la kifamilia haswaa kuhusu mumeo, tulihitaji kujua ni wapi pa kuanza kumtafuta ndio tukakuuliza maoni yako”
“Sawa nimewaelewa, kwakweli akili yangu haipo sawa kabisa. Chochote mtakachoamua ni sawa tu kwangu”
Ikabidi wamuache kwanza kwani ni wazi akili ya Sophia haikuwa sawa na wala alikuwa hawaelewi kwa chochote ambacho walikuwa wakizungumzia.
Kuna muda alikaa mwenyewe na kutafakari akaona kuna umuhimu mkubwa sana way eye kwenda kwa yule bibi tena akahisi kuwa inawezekana itakuwa rahisi kumpata hata huyo mumewe ingawa moyo wake haukuwa na imani na Ibra tena kutokana na yote yaliyompata. Akajipa moyo tu kuwa atapatikana lakini hakuwa na imani ya kuendelea kuishi nae kwa maisha yake yatakayokuwa baada ya mambo yote haya. Mama Sophia alimfata mwanae na kujaribu kuzungumza nae ili kujua ni kipi haswaaa kilichompata mtoto wake,
“Mama weee acha tu, yani hapa nilipo mwanao sina kizazi tena”
“Huna kizazi kivipi Sophy?”
Sophia aliinama na kuanza kulia kisha akamwambia mama yake,
“Kizazi change kimetolewa mama”
Mama Sophy alimsogelea mwanae na kumkumbatia ingawa hakuelewa kisa na mkasa hadi mwanae kufikia hatua ya kutolewa kizazi.
“Jamani mwanangu imekuwaje tena? Kwanini utolewe kizazi?”
“Sijui mama yani sijui kabisa lakini ndio hivyo nimetolewa kizazi mama. Sitaweza kuzaa mimi, sitaweza kuwa na mtoto kamwe, hakuna mwanangu atakayekuita bibi mama yangu sina kizazi mimi”
Kwakweli mama Sophia alishikwa na uchungu wa hali ya juu kwa kauli hizi za mwanae hata yeye alijikuta akilia kwa uchungu huku akimbembeleza mwanae.
“Nyamaza mwanangu, kutokuwa na kizazi sio mwisho wa maisha. Tunachomshukuru Mungu kwasasa ni kukuona wewe ukiwa mzima mwanangu. Usilie Sophy wangu”
“Inaniuma sana mama, nilitamani watoto mimi. Nilitamani apatikane mtu wa kuniita mama, kunitania, kunichekea, kulia nimbembeleze lakini hayupo mtu huyo na hatokuwepo kamwe. Nimeishia kuwaona wanangu kwenye ndoto tu wakinipungia mkono na kuniaga kwa sura za simanzi. Oooh wanangu mimi, hawataweza tena kukaa kwenye tumbo langu maana sina kizazi”
Mama Sophy alipata kazi kubwa sana ya kumbembeleza mwanae na kuhakikisha kuwa anarudi kwenye hali yake ya kawaida, hadi pale alipokuwa sawa akamuomba mwanae kuwa waende kupumzika ili kuyaacha yale mawazo mabaya yawapitie mbali.
Kesho yake kama ambavyo Sophia alivyowaomba ndugu zake kuwa wampeleke mahali ambako walichimba kaburi lake wakaamua kufanya hivyo ambapo walijiandaa pamoja nae kisha kwenda nae huko makaburini, Cha kushangaza walipofika pale waliona yule mbuzi amefukuliwa na kuwekwa juu ya kaburi ambalo walipanga kumzika Sophia halafu mbele ya lile kaburi kulikuwa na kibao kilichoandikwa kwa herufi kubwa ‘MAREHEMU NEEMA’ kwakweli walistaajabu sana ila Sophia hakuweza hata kutafakari mara mbili na kuanza kukimbia ikabidi ndugu zake wamkimbilie na kumshika kisha kuanza kurudi nae nyumbani.
Walifika wakiwa wanahema sana, hata watu ambao hawakwenda eneo hilo walishangaa na kuwauliza kuwa ni kitu gani kimetokea huko ikabidi wawasimulie kitu walichokikuta.
“Mbona ni maajabu hayo?”
“Tena maajabu makubwa, hata sikuyafikiria mambo haya jamani. Hivi ile inamaanisha nini?”
“Inabidi twende tukawaeleze wazee tu”
Kwavile ilikuwa ni jioni na giza nalo lilikalibia kuingia, Sophia akawakataza kwenda kuwatafuta hao wazee kwa muda huo na kwenda kuwaambia.
“Tafadhalini sana ndugu zangu, wale wazee nendeni mkawaeleze kesho mapema na sio sasa”
“Kwanini Sophia wakati huu ndio muda mzuri ili wajue kabisa”
“Hata kama huu ni muda mzuri, watahitaji kwenda kushuhudia na sidhani kama ni muda mzuri wa kwenda huko makaburini”
Hawa ndugu waliamua tu kukubaliana na Sophia kisha kuendelea na mambo mengine ya hapa na pale.
Siku hiyo hiyo kwenye mida ya usiku saa sita wakasikia mtu nje ya nyumba yao akisugua masufuria na kufanya washtuke sana na kuamshana,
“Jamani mmesikia huko nje kuna mtu anasugua masufuria?”
“Hata mimi nimesikia”
“Je huenda ni nani?”
“Nadhani tujipange tutoke nje tukamshuhudie ni nani”
Sophia uoga ukamshika na kufanya awazuie ndugu zake kutoka nje,
“Tafadhali msitoke nawaomba sana”
“Kwani unajua ni nani?”
“Sijui, ila nawaomba msitoke nje”
Mdogo wa Sophia aitwaye Tausi akaamua kufunua pazia la dirishani ili achungulie ni nani, ila alipofunua tu alipiga kelele za uoga na kuanguka chini.
Mule ndani wakazidi kupatwa uoga huku kaka wa Sophia akisisitiza kuwa atoke nje na kujua ni nini kinaendelea,
“Kaka tafadhali, naomba unisikilize dada yako. Jamani familia yangu mimi nimepitia mengi sana nawaombe msadiki ninayoongea sasa, kwanza kabisa msitoke nje subirini pakuche nina maana yangu kabisa”
“Maana yako ni ipi Sophy?”
“Ingekuwa ni enzi zile ambazo sikuwa na ufahamu basi ningekuwa wa kwanza kushauri kuwa tutoke ila baada ya kula kijiti cha yule bibi zaidi ya mara mbili akili yangu iko vizuri sana, nawaomba tusitoke niliyopitia yanatosha na sitaweza kuwaeleza kwasasa kwasababu maalum ila nitawaeleza tu sema si kwa muda huu ambapo kuna mauza uza nje”
“Haya sasa na huyu mdogo wako tutafanya nae nini?”
“Msijali atazinduka tu ila nje tusitoke”
Wakatulia kimya kwanza kwa muda kwani hakuna aliyeweza kumuelewa Sophia kwa haraka, ule ukimya wao ukafanya wasikie kwa zaidi masufuria yakisuguliwa nje, mmoja akauliza muda kwanza
“Hivi kwani ni saa ngapi saa hizi?”
“Saa nane usiku”
“Mmmh makubwa haya, saa nane mtu tusiyemjua asugue sufuria nje kwetu kweli!”
Wakati wakitafakari hayo wakasikia mtu akigonga mlango wao na kufanya waogope zaidi, mama Sophia alishindwa hata kujisogeza kwa uoga ila Sophia alizidi kuwapa ujasiri ndugu zake kuwa wasiogope na wala wasijishughulishe kufungua mlango,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Yani msiogope chochote ndugu zangu, na kwavile zilianza mbwembwe za kusugua sufuria na sasa ni mtu anagonga mlango hata msiwe na uoga kwanza. Tutulie tu na wala tusiende kufungua kwani hakuna miadi na mtu yeyote kuwa atakuja usiku huu.”
Ikabidi wamsikilize Sophia tu na kutulia pale pale sebleni huku muda ukizidi kwenda na yule mtu akizidi kugonga, ila ilipofika saa kumi alfajiri yule aliyekuwa akigonga aliacha kugonga na kukawa kimya kabisa, muda kidogo yule mdogo wa Sophia naye aliweza kuzinduka na kukaa huku akiangalia huku na kule.
Mama yake aliyekuwa karibu naye aliendelea kumsogelea mwanae na kumtuliza, kisha wakamuuliza alichokiona dirishani wakati amefungua pazia,
“Mmmh mama eti niliona mbuzi ndio anasugua sufuria, nimeogopa sana sijui ni uchawi loh!”
“Pole sana mwanangu, ndiomana dada yako alitukataza kuangalia nje ila usijali kila kitu kitakuwa sawa”
Walitulia kimya pale huku kila mmoja akijaribu kufikiria kuwa huyo mbuzi alikuwa anasuguaje hizo sufuria.
Kulipokucha waliweza sasa kutoka nje na kuendelea na shughuli zingine kama kawaida huku wakipanga kwenda kwa wale wazee wa mtaa huo kuwaeleza kile ambacho wamekikuta makaburini na vile ilivyokuwa usiku kwenye nyumba yao.
Kaka wa Sophia walitoka pale na kwenda kwa wazee, kisha wanawake waliendelea na shughuli za hapa na pale huku wengine wakienda kulala ukizingatia usiku hawakuweza hata kusinzia.
Muda kidogo kaka wa Sophia walirudi na wazee watatu wa mtaa ambao walifika hapo ili kuelewa zaidi kutoka kwa Sophia, walikaa na Sophia na kuzungumza nae sasa
“Kwanza kabisa ningependa tujue kabla ya sisi kuletewa taarifa ya msiba wako huku ulikuwa wapi? Na vipi uliweza kufika hapa siku yako ya mazishi?”
Sophia aliamua kuwaeleza toka mahali pale ambapo yeye na mumewe walikutwa kisha yeye kusaidiwa na watu na aliyoyakuta kwa watu hao,
“Mmmh inamaana hawakuwa watu wa kawaida?”
“Kwa mujibu wa yule mwenzao ndio hivyo hawakuwa watu wa kawaida”
“Mmmh habari yako kidogo inanichanganya akili kutokana na hayo mambo halafu na kile mlichoenda kukikuta makaburini jana na jinsi mlivyotueleza yaliyotokea hapa kwenu usiku. Sasa najaribu kutafakari kwanza, ngoja nikuulize, kwanini jana ulihisi kuwa huenda ni kitu kibaya na kuwakataza wenzako kutoka nje?”
Sophia aliwaeleza kwanza kuhusu bibi aliyewahi kukutana nae na kupewa dawa ambayo aliambiwa kuwa itamsaidia kurudisha akili yake na imemuwezesha kugundua kwa urahisi kabisa kitu kizuri na kibaya kikitaka kutokea.
“Je unamfahamu huyo bibi?”
“Nikimuona namfahamu ila sijui anapoishi kwani mara nyingi huwa ananikuta nyumbani kwa rafiki yangu ila nahisi rafiki yangu anajua anapoishi huyo bibi”
“Itakuwa ni vyema kwenda kuonana na huyo bibi, nadhani anaweza kutusaidia juu ya hili pia. Hivyobasi jipangeni mpate siku nzuri ya kuonana na huyo bibi”
Kwavile mama Sophia naye alikuwepo hapo akawaomba sana kuwa inawezekana kwahiyo hata kesho waweze kwenda huko kuonana na huyo bibi.
“Basi itakuwa vizuri sana, ngoja na sisi tukajaribu kupita huko makaburini na kuona kitu kilichoendelea”
Hawa wazee wakaaga kisha wakaondoka na kaka zake Sophia kuelekea huko makaburini ili kuona kama walichoelezwa kina ukweli wowote au ni nini.
Walianza kufika karibia na eneo la makaburi na kusikia kuna harufu ya mapishi inaendelea, ikafanya wajiulize
“Ni harufu gani ya mapishi itoke huko kwenye nyumba za watu mpaka huku kwenye eneo la makaburi?”
Hakuna aliyekuwa na jibu ila walipofika makaburini walishangaa sana, wakaona lile kaburi walilopanga kumzika Sophia likiwa limeota nyasi kwa juu kisha yule mbuzi waliyemzika pembeni alikuwa juu ya kaburi hilo akila zile nyasi, kisha yule mbuzi akawaangalia na kutabasamu hapo ndipo amani ya moyo ilipowatoweka kabisa na kujikuta kila mmoja akikimbia kwa nija yake na sehemu ya kwanza kufika ilikuwa ni kwakina Sophia tena mahali hapo hata wale wazee hawakukaa tena wakaondoka na kuwaacha tu wakaka wa Sophia huku pale nyumbani wakishangaa kuwa wamekumbwa na kitu gani, kaka wa Sophia alieleza kwa kifupi tu
“Ni bora tuliyokutana nayo jana kuliko leo”
“Kivipi jamani, hebu tuambie”
“Ushawahi kuona mbuzi anatabasamu?”
“Mbuzi anatabasamu? Kivipi mbona ni habari ya ajabu sana!”
“Ndio hivyo mama yani mimi hadi nashangaa na ninaanza kuwa na mashaka na uwepo wa Sophia jamani sijui kama na yeye ni mtu”
Sophia alijisikia vibaya kwa hilo kwani hakutegemea kama ndugu zake wanaweza kuwa wanamfikiria vibaya kiasi kile cha kusema kuwa hata yeye wana mashaka nae, alitamani kesho yake ifike tu ili aweze kwenda kwa yule bibi na kuzungumza nae kwa undani zaidi akihisi kuwa huenda anaweza akapata amani ya moyo pamoja na familia yake. Hakutaka kupoteza muda kwa kubishana na watu wa familia yake kwahiyo muda huo aliamua kwenda kupumzika ukizingatia hakupumzika kabisa.
Usiku ulifika huku Sophia na wote kwenye familia yao walikuwa wamelala, muda huu Sophia akajiwa na ndoto na kwenye ndoto hii alijiona yupo kwenye ile nyumba yake na mumewe, muda kidogo akamuona Neema aliyekuwa akimuangalia na kumuuliza,
“Hivi kwanini nakuja kwenu na kukonga mlango hunifungulii? Kwa madai yako unaogopa makosa mliyofanya ya kuniokota?”
Sophia alikuwa kimya tu akimtazama huyu Neema, kisha huyu Neema akamwambia tena Sophia,
“Wewe ulitakiwa uwe kwenye hali niliyokuwa nayo mimi kwasasa ila nakushangaa sana, hebu niruhusu tuondoke pamoja ili uweze kuepukana na haya yanayokupata pia ukapate pumziko la moyo”
Hapa sasa Sophia akapata ujasiri wa kumjibu,
“Sina haja ya kwenda na wewe Neema”
“Sasa unafikiri unafaida gani kwenye maisha ikiwa huna kizazi? Unadhani mumeo atakupenda tena bila kizazi? Na kwanini hujawaambia kwenu kuhusu mumeo na maovu yake yanavyokutesa?”
“Sitakuwa binadamu wa kwanza kukosa kizazi, kwahiyo bado nina nafasi kubwa ya kuendelea kuishi kwanza kunitoa kizazi wala sio kikwazo kwangu”
“Basi tuachane na hayo Sophia, kwa usalama wako na usalama wa familia yako nifungulie mlango niingie ndani kwenu”
Sophia akashtuka kutoka kwenye ule usingizi, na gafla akasikia mlango wao ukigongwa tena kama jana usiku huku ndugu wote wa Sophia wakiwa wameamka na kujiuliza kama wafungue ule mlango au la. Sophia alisogea kwa haraka sana na kuwaomba ndugu zake,
“Tafadhali msifungue”
Mara gafla akasikia sauti kutoka nje,
“Sophia acha roho mbaya hebu nifungulie bhana”
Wote walishtuka mule ndani kwani ile sauti ilikuwa ni ngeni masikioni mwao ila ilikuwa ni sauti iliyozoeleka kwenye masikio ya Sophia, ingawa Sophia alikuwa akitetemeka ila alipata ujasiri wa kuongea kwa nguvu,
“Sikufungulii, ondoka kwetu shetani wewe”
Kikasikika kicheko kikubwa sana, kisha sauti ikasema,
“Unajua kabisa kuondoka ni maamuzi yangu Sophia, naomba unifungulie kwa amani tu kabla sijafanya chochote kibaya. Nifungulie Sophia”
“Nimesema Sifungui”
“Unajua wazi kitu ambacho naweza kufanya, unajua wazi nilivyo na roho mbaya. Sasa kwa amani yako fungua Sophia”
Ndugu wa Sophia walikuwa wakitetemeka sana huku wakimuangalia ndugu yao na kungoja atakachosema huku wengine wakijaribu kumshawishi Sophia akubali kufungua ila Sophia alitulia na wazo lake lile lile la kuto kufungua, ile sauti ya nje sasa iliongea kwa ukali zaidi,
“Nakupa sekunde kumi Sophia usipofungua kijiji kizima kitasimulia nitakachokifanya”
Sophia alikaa kimya kwa muda huku akitetemeka kwani hakujua cha kufanya kisha akajikuta akikunja mikono yake huku akisema,
“Asante Mungu, asante Mungu”
Alikuwa akirudia hayo maneno huku mule ndani kwao wote wakimshangaa Sophia kwani hakuna aliyewahi kumuona Sophia akiwa vile hata mara moja, Sophia alikazana kumshukuru Mungu kwani bado alikuwa na maneno ya yule bibi kuwa amshukuru mungu hata kwa jambo ambalo halijafanyika huku akiamini kuwa Mungu anaenda kufanya jambo hilo.
Na ukapita muda mrefu huku kimya kikitawala pale nyumbani kwao, haikusikika sauti ya kugongwa kwa mlango na wala sauti ya yule mtu wan je, ila hata hivyo hakuna aliyeweza kulala pale nyumbani kwakina Sophia kwani kila mmoja bado alikuwa na uoga katika moyo wake.
Kulipokucha kila mmoja alikuwa akimwambia Sophia kwenda kwa huyo bibi ili waweze kuepukana na hayo yanayotaka kuendelea hapo nyumbani kwao, kisha Sophia aliamua kuwapa ushauri ndugu zake wa kugawanyika kutokana na usalama wao kuwa waondoke waote hapo nyumbani na nyumba ifungwe kwa muda kwani inawezekana huyo kiumbe akienda kupambana na Sophia alipo na kushindwa akarudi tena kwenye familia yake.
“Jamani mimi nawaomba ndugu zangu, nawaomba sana. Dada zangu mrudi kwa waume zenu na kaka zangu mrudi kwenu au hata muende kwa ndugu kisha mimi nitaondoka hapa na mama pamoja na Tausi ila nyumba tutaifunga mpaka pale tutakaporudi kwani inatakiwa tuepuke mabalaa haya, huyu kiumbe anaweza akaja hapa wakati hatupo na kufanya uharibifu zaidi ingawa shida yake kubwa ni mimi kwahiyo cha msingi ni kutengana wote humu ndani.”
Wakakubaliana hivyo kisha kila mmoja kuanza kujiandaa kwaajili ya kuondoka, mpaka kufikia saa kumi jioni karibia kila mmoja alikuwa ameondoka kisha wakina Sophia wakafunga milango na wao kuondoka wakiwa na funguo ili asije yeyote akarudi kabla ya muda ambao wamekubaliana.
Sophia akiwa na mama yake huku akiambatana na mdogo wake Tausi pamoja na kaka yao aliyekuwa akiwasindikiza, walifika mahali na kuweza kupanda mabasi ambayo yangewapeleka mjini ili waweze kufika mahali anapoishi Siwema. Kisha kaka yao naye akaondoka zake na kuelekea nyumbani kwake na yeye kwenye mke na watoto wake.
Wakiwa kwenye lile basi lilifika mahali na kuharibika kisha wakaanza kusubiri litengenezwe,
“Mmmh tutafika usiku”
“Sio tatizo kufika usiku, cha msingi tufike salama”
Muda kidogo ilionekana gari ya kukodi ikipita kisha ikasimama karibu yao kisha wakamsikia dereva akisema,
“Buku buku mpaka mjini”
Tausi akamtazama dada yake na kumwambia,
“Dada tungeenda kupanda hiyo tax si unaona anatangaza buku buku yani bei sawa na hili basi tulilopanda”
“Kuwa makini mdogo wangu, kwanini bei ya hiyo tax tuisikie sisi tu ilihali hapa kuna abiria wengi tu? Acha iende tu”
Tausi hakuwa na hoja ya ziada ikabidi tu akubaliane na dada yake kisha wakasubiri mpaka lile basi lilipokuwa sawa na kupanda kisha kuendelea na safari yao.
Walifika kituoni saa mbili usiku na kuamua kwenda moja kwa moja kwa Siwema ambapo walipofika palikuwa kimya sana huku taa zikiwa zinawaka tu ikabidi wagonge mlango ili wamuombe ifadhi ya muda hadi kesho watakapoenda kuonana na yule bibi, waligonga kama mara tatu hivi ndipo Siwema alipotoka ndani ila alipofungua mlango tu alishangaa sana na kumuuliza Sophia,
“Huyo wa nyuma mmekuja nae wa nini?”
Sophia akageuka nyuma na kushtuka sana kwani alimuona Neema.
Alijikuta akitetemeka tu na kushindwa hata cha kuongea, ila mama Sophia na Tausi inaonyesha hawakuona chochote kwahiyo walikuwa wakishangaa tu. Siwema akamuuliza tena Sophia,
“Umekuja nae wa nini huyo?”
“Dada, hata mimi sijui”
Sophia akajisogeza zaidi kwa Siwema kwani hofu ilimshika sana, ila Siwema aliendelea kuongea,
“Kama mpo pamoja na huyo mtu kwakweli siwezi kuwapokea”
“Hapana hatupo nae, hata mimi nashangaa amefata nini hapa”
Mama Sophia ikabidi aulize,
“Kwani huyo mnayemuongelea ni nani na yuko wapi?”
Siwema akauliza,
“Kwani nyie hamumuoni au? Si huyo hapo anawachekea”
Wakati mama Sophia na Tausi wakijaribu kupepesa macho ili waweze kumuona mtu huyo, naye alitoweka kabisa kwani hata Siwema na Sophia hawakumuona tena, wakatazamana kisha Siwema akawakaribisha ndani nao wakaingia. Muda kidogo Siwema akawaomba wamruhusu awaandalie chakula kwanza.
“Mnajua mmekuja bila taarifa ila ngoja niwaandalie kidogo nilichonacho”
Wakatulia pale wakisubiria Siwema aandae, ambapo alikuwa na viazi na kuamua kuvichemsha ili waweze kula na kunywa chai.
Muda kidogo Siwema alimaliza na kuwaandalia kisha kuanza mazungumzo ya hapa na pale kuwa nini kimewasibu mpaka kufika usiku ule,
“Dada, ni makubwa sana yaliyotusibu”
“Kwanza nisamehe bure mdogo wangu, yani siku ile niliambiwa ole wangu niende kueleza yaliyotokea mule ndani kwenu itakuwa ni mwisho wangu basi nikaogopa sana kumuelezea mtu yeyote ila laity kama ningepata ujasiri wa kueleza basi huenda mngepata msaada”
“Usijali dada, kwanza hapa penyewe bado hakuna usalama kabisa. Hivi huwa unalala kwa amani kweli?”
“Siku hizi kabla ya kulala huwa nawasha ubani ili nisifatwe na viumbe wabaya na inanisaidia sana tu”
Mama Sophia akashangaa sana na kumuuliza Siwema kwa mshangao,
“Ubani?”
“Ndio ubani, kwani vipi?”
“Ubani si huwa unaita majini?”
“Unajua hivi vitu mama huwa vinaenda kwa imani, kwa mimi naamini kuwa kuna majini ila pia wapo wazuri na wabaya. Hata hivyo sina imani kama ubani unaita majini kwani ingekuwa ni kweli basi majini wangejaa sana maana ni watu wengi wanaowasha ubani. Kila mtu huwa anawasha kwa maana yake. Mbona ubani unachomwa Makanisani na Miskitini, kwanini mimimnisiweze kuchoma ndani mwangu?”
“Kwahiyo huwa ukichoma unafanyaje?”
“Nanuwia watu wabaya wasinifate wala nisitokewe na chochote kibaya”
“Mmmh leo umenipa mapya kabisa, mi huwa sina imani na ubani na siku zote huwa nahisi kazi yake ni kuita majini. Yani nikisikia mtu ananunua ubani jibu ninalopata ni kuwa mtu huyo ana majini”
“Si vizuri kumdhania mtu vibaya, kila mtu analindwa na imani yake.”
“Sawa nimekuelewa”
“Sawa mama, eeh Sophia niambie kwanza ulipomtoa mama na imekuwaje kuja usiku huu?”
Sophia aliamua kumueleza kwa kifupiu uhitaji wake wa kuonana na yule bibi ila kama kawaiada ya Siwema kuhusu yule bibi aliwaka sana muda huu na kudai tena kuwa yule bibi hafai na hatakiwi kabisa kuwa karibu naye,
“Hivi Sophia kwanini bado unaendelea kumng’ang’ania yule bibi?”
“Dada, hujui tu. Yule bibi amefungua akili yangu sana na pia naamini anaweza kunisaidia juu ya jambo hili tafadhali usinizuie kuonana nae”
“Mimi simuamini yule bibi yani simuamini kabisa, kuna stori mbaya sana kumuhusu hapa mtaani kwakweli hafai”
Ikabidi Sophia amueleze Siwema kuhusu kufa kwake hadi pale nduguze walipotaka kumzika na jinsi alivyorudishwa nyumbani nay ale mambo yaliyotokea kwenye kaburi alilotaka kuzikwa. Hii stori ilimsisimua sana Siwema na kumpa uoga wa hali ya juu hata akashangaa Sophia anaendelea wapi kupata ujasiri kwa mambo kama yale yaliyomtokea.
“Ujasiri huu ni kwasababu ya ile dawa niliyotafuna. Imenifungua akili sana na kunifanya nihitaji kufahamu kwa undani zaidi namna ya mimi kuepukana na hili tatizo”
“Pole sana mdogo wangu, kesho nitajitahidi ili tuweze kumpata”
Walizungumza sana kisha ukafika muda wa kulala, ambapo Siwema aliamua kutandika godoro pale sebleni kwao ili kupata nafasi kubwa zaidi ya kuweza kulala.
Wakati wamelala wakasikia mtu akigonga mlango, wa kwanza kushtuka alikuwa Tausi ambaye alimshtua dada yake kwa uoga,
“Dada, dada eti kuna mtu anagonga”
Muda huo huo Siwema nae akaamka na kusikia mlango ukigongwa, akataka kwenda kuinuka kufungua mlango ule, Sophia akamzuia Siwema
“Tafadhali usiende kufungua nakuomba”
“Kwanini wakati mtu anagonga”
“Je unamjua ni nani?”
“Atakuwa ni Tuma tu huyo, ndio zake kuchelewa kurudi sasa kwao wasipomfungulia ndio huja kwangu”
“Je huyo Tuma huwa anakuja muda huu?”
“Kwani saa ngapi saizi?”
“Saizi ni saa nane”
“Kheeee ishafika saa nane kumbe! Mara nyingi Tuma huwa anarudi saa sita, labda leo kachelewa tu”
“Hapana si yeye, tafadhali usiende kufungua”
Siwema aliweza kuona hofu kubwa aliyokuwa nayo Sophia na kumfanya asite kwenda kufungua, mama Sophia nae akashtuka na kusikia ile kugonga, huyu mama alijikuta akiinua mikono juu na kushika kichwa huku akisema
“Mungu wangu, hadi huku!”
Huyu mama machozi yalikuwa yalimlenga lenga, Siwema aliweza kuwaelewa sasa kwani akakumbuka hata vile alivyosimuliwa na Sophia muda mfupi kabla ya kulala.
Wakati ile hodi ikiendelea huku kila mmoja akiwa na hofu, Siwema akajikuta akibanwa na mkojo wa hali ya juu,
“Jamani mkojo umenibana sana, sina jinsi lazima nitoke nje nikakojoe jamani”
Sophia aliendelea kumsihi huku akimuomba akojolee hata ndoo ila asitoke nje,
“Kheee nikojolee ndoo yangu?”
“Kakojolee tu, kwani tatizo ni nini si kesho asubuhi itasafishwa”
Basi Siwema akaafikiana nao na kuchukua ndoo yake ya chooni kisha kwenda nayo chumbani kukojoa.
Wakati akitoa haja ndogo hiyo akasikia kama mtu akigonga dirisha lake kumbe Sophia naye alisikia na kumfanya ainuke na kukimbilia chumbani kwa Siwema ili kumzuia kuwa asifungue hata dirisha,
“Kheee Sophia mdogo wangu umeanza kuchanganyikiwa eeeh!”
“Kwa yaliyonipata nina haki ya kuchanganyikiwa dada yangu, nakuomba hata hilo dirisha usifungue”
Siwema alimsikiliza Sophia kwahiyo alimaliza na kurudi sebleni ambapo ile hodi ilidumu kwa muda wa nusu saa na kuwa kimya kabisa, mama Sophia akakumbuka kitu na kumwambia Siwema.
“Ila leo hujawasha ule ubani wako”
“Aaah bora umenikumbusha”
Siwema alinyanyuka na kusogelea jiko lake la mkaa huku akiangalia kama kuna moto ulibaki, akaona vimoto akachukua na kuwasha ubani wake kisha akarudi na kuwaambia,
“Tulale sasa”
Wote waliweza kuendelea kulala kasoro Sophia hakuweza kabisa kuendelea kulala hadi panakucha.
Asubuhi na mapema Sophia alifungua malango wa Siwema na kutoka nje, macho yake yaliangalia ule mpera wa Siwema moja kwa moja huku akijiambia,
“Laiti kama ningekuwa na ufahamu ile siku ya kwanza kabisa basi sasa hivi ningekuwa na mtoto wangu”
Akainamisha macho chini kisha akainua tena na kwenda kuufata ule mpera, alipofika alikaa chini yake huku akiendelea kutafakari na kukumbuka siku ya kwanza alipokuwa akitafuta pera kwenye mti huo wakati mimba yake ikiwa change kabisa. Sophia akaangalia tumbo lake na kujishika huku akisikitika na kusema tena,
“Laiti ningejua, ningekuwa na mtoto wangu sasa. Hivi kwanini sikumsikiliza yule bibi? Kwanini niliyapuuzia maneno yake? Kweli usilolijua sawa na usiku wa giza”
Sophia alikuwa akihisi kuwa huenda yule bibi atatokea tena kama kawaida yake ila huyu bibi hakutokea wala nini.
Wakina Siwema nao walivyoamka walishangaa kutokumuona Sophia, ikabidi Siwema atoke nje na kumuona Sophia akiwa chini ya mpera ametulia tu, Siwema alimsikitikia sana Sophia kisha akamuita ambapo Sophia aliinuka pale na kwenda alipo Siwema.
“Sophia mdogo wangu usifanye mawazo yakutawale kiasi hiko, jiandaeni na ndugu zake nioweze kuwapeleka kwa yule bibi kwani nina hakika tukiulizia tutafika nyumbani kwake tu”
Sophia alikubali na kwenda kujiandaa yeye pamoja na ndugu zake kwa lengo la kwenda kuonana na yule bibi. Mama Sophia alimuuliza mwanae kwa uhakika wa mwisho,
“Unaamini kuwa huyo bibi anaweza kukusaidia?”
“Naamini hilo mama kwani yule bibi anaonekana kujua vitu vingi sana vya kwenye nyumba niliyokuwa nikiishi kwahiyo naamini anaweza kunisaidia”
“Sawa mwanangu, unajua kama ningezoea kwenda kwa waganga wa kienyeji basi ningekupeleka mapema sana ila mimi huwa sina imani na waganga wa kienyeji. Na kwa maelezo yako nahisi kama huyo bibi ana uganga uganga flani hivi”
“Mfano kama ni mganga itakuwaje?”
“Ni juu yako ila mimi sina imani na waganga mwanangu, ni afadhali wale wazee wa jadi. Ila kwavile ni wao waliosema twende tukaonane na huyo bibi basi hakuna tatizo”
Walimaliza kujiandaa kisha kutoka pale nyumbani kwa Siwema na kuanza msako wa kumtafuta yule bibi huku wakisaidiwa na Siwema.
Kila walipopita na kuulizia walipewa majibu ambayo hayakuwaridhisha na pia majibu yalikuwa yakiwakatisha tamaa na kuona kwamba inawezekana wasiweze kuonana na yule bibi,
“Kwakweli yule bibi huwa namuona tu na hata sijui anapoishi, wengi huwa wanasema anaishi mtaa wa pili huko ila kila unayemuuliza naye atakwambia kuwa ameambiwa”
Siwema akamuuliza tena huyu mtu,
“Vipi kuhusu swala la uchawi la yule bibi?”
“Kama ilivyo kuishi kwake ndivyo ilivyo swala la uchawi, wengi utawasikia kuwa yule bibi ni mchawi sana ni mtu mbaya hafai kabisa ila ukimuuliza kuhusu uchawi wa yule bibi atakwambia kuwa ameambiwa na watu. Kwahiyo hakuna mtu yeyote mwenye uhakika na maisha ya yule bibi”
Siwema akapumua kidogo kisha kumshukuru huyu mtu na kuendelea na safari hadi walipoingia mtaa huo wa pili ambapo anahisiwa kuishi huyo bibi, wakati wanatembea na kuulizia huku kila mmoja akidai kutokufahamu anapoishi yule bibi huku wengine wakidai anaishi mtaa waliotoka wao wakajikuta wamesimama kwa muda kwanza na kukosa uelekeo, wakati wamesimama hapo Sophia akahisi kang’atwa na kitu na kushtuka sana, akafanya wote wageuke na kuangalia kuwa ni nini wakaona nyoka akikimbia,
“Mungu wangu ni nyoka!”
“Tutafanyaje sasa?”
Siwema akachukua kitambaa na kumfunga Sophia mguuni huku akisema watafute usafiri wamuwahishe hospitali, na kwa bahati nzuri kuna gari ilikuwa inapita pale mtaani wakaamua kusimamisha gari hiyo ila kabla hawajapanda wakamuona yule bibi kwa mbali akiwaangalia. Sophia akasita kupanda na kuwaomba wakazungumze na yule bibi kwanza,
“Sophia, sumu ya nyoka ni kali sana, tafadhali tuwahi hospitali kwanza halafu tutarudi kuzungumza na huyo bibi”
“Hapana jamani, najua vizuri kama nyoka ana sumu kali ila nina uhakika yule bibi ana dawa ya kuweza kuniondoa hii sumu ya nyoka”
Ikabidi wamwambie yule dereva aondoke kisha wao wakaanza kumfata yule bibi huku wakimsaidia Sophia kutembea kwani alikuwa akichechemea.
Walipofika tu karibia na yule bibi, kuna majani alichuma na kuyafikicha kisha akampaka Sophia machoni na muda huo huo yale maumivu ya kung’atwa yakapotea na Sophia akaanza kutembea kawida kisha yule bibi akamwambia Sophia,
“Si nyoka aliyekung’ata”
“Ni kitu gani bibi?”
“Ni mauzauza tu, hawakutaka uonane na mimi. Hujiulizi kuwa lile gari la haraka haraka vile limetokea wapi? Wanataka kuwarudisha nyuma ila kwasasa ni kusonga mbele tu.”
Huyu bibi alimuangalia mama Sophia na kumuangalia Siwema kisha akawaambia,
“Mimi si mchawi wala si mganga wa kienyeji kama mnavyofikiria ila mtaelewa mimi ni nani na kwanini wengi hunichukulia kama mchawi”
Kisha wakaendelea kusonga mbele kuelekea nyumbani kwa yule bibi, huyu bibi akamuuliza Sophia,
“Yuko wapi mumeo?”
“Hata sijui alipo bibi”
“Je, unahisi kuwa bado yupo kwenye nyumba yenu?”
“Sijui bibi, yani mimi na yeye tumeachana kwenye mazingira ya kutatanisha sana”
“Pole sana ila angalia nyuma kwanza”
Sophia akageuka nyuma na kumuona Ibra, kwakweli alishtuka sana.
Sophia akasema kwa sauti,
‘Si Ibra yule!”
Bibi naye akajibu,
“Ndio ni yeye, haya twendeni atatufata tu nyuma”
Wakaendelea kufatana na yule bibi hadi walipofika nyumbani kwake, kisha akawakaribisha
“Hapa ni nyumbani kwangu, karibuni sana. Hapa naishi peke yangu”
Walikaribia, ilikuwa ni nyumba ndogo tu ya vyumba viwili, Sophia aliamua kumuuliza huyu bibi kuwa kwanini anaishi peke yake kwani alimuona ni mzee sana kuishi mwenyewe ila huyu bibi hakujibu zaidi ya kucheka kisha akawaambia wamsubirie Ibra waliyemuona nyuma yao na muda kidogo tu Ibra aligonga mlango wa yule bibi ambapo alikaribishwa pia kwahiyo wote walikuwa kwenye sebule ya yule bibi ambapo kulikuwa na mikeka ya kutosha na kuwawezesha wote kukaa.
Huyu bibi akamuuliza swali Sophia kwanza,
“Kabla ya yote naomba uniambie sababu yaw ewe kunitafuta mimi”
“Kutokana na matatizo niliyoyapata na vile ambavyo ulinieleza mwanzoni kabisa nikaona kuwa wewe ndiye unaweza kunisaidia kwasasa”
Kisha huyu bibi akamuangalia Ibra na kumuuliza swali lile lile ambalo amemuuliza Sophia ila Ibra hakuweza kujibu na alikuwa kimya sana, huyu bibi akamwambia Ibra,
“Pole sana, katika maisha tunapitia mambo mengi na kujifunza vitu vingi sana. Najua uliyoyapitia ni zaidi ya adhabu katika maisha yako, pole sana”
Ibra hakujibu kitu ila ni machozi tu yalikuwa yakimtiririka, kisha huyu bibi aliwaangalia hawa ndugu wa Sophia pamoja na Siwema na kuwaambia,
“Jamani msimfikirie vibaya kijana huyu, kwasasa hana uwezo wa kuongea ndiomana mnamuona hivyo”
Kimya kikatawala huku wakionekana kumsikitikia Ibra ila ni Sophia tu ambaye hakuonekana na huruma yeyote dhidi ya Ibra kwani mpaka sasa alitambua kwamba matatizo yote yaliyomkabili ni sababu ya makosa ya Ibra, amekosa tena uwezo wa kuzaa sababu ya Ibra kwahiyo ndio kitu kilikuwa kikimuuma sana na kumfanya asiweze kumuonea huruma mume wake.
Bibi akainuka na kuchemsha maji ambayo aliweka dawa kama unga unga hivi kisha akaweka kwenye kikombe na kuwataka wote waliofika hapo wanywe ambapo alianza kunywa yeye mwenyewe kwanza na kuwapa wanywe wengine, wote walikunywa ile dawa kisha huyu bibi alikaa sasa na kumuangalia Sophia kisha akamuuliza,
“Unakumbuka kipindi ambacho ulikuwa ukiamka unakuta vyombo vyako vimeoshwa, mara nyingine umeshapikiwa chakula. Siku nyingine unakuta nguo zako zimefuliwa na kuanikwa kisha kuanuliwa na kupangwa kabatini unakumbuka?”
“Nakumbuka ndio, na nilikuwa nikishangaa sana”
“Je ulihisi ni nani aliyekuwa akifanya matukio hayo?”
“Mwanzoni nilikuwa nikihisi ni mume wangu”
“Ila je tabia za mume wako huzijui kwani? Hukujiuliza amewezaje kubadilika gafla vile?”
“Kwakweli sikujua tena kuna kipindi hadi nilikuwa nikigombana nae kwani nikimwambia yeye ndio amefanya akawa anakataa, nikajaribu kuomba ushauri kwa dada hapa akasema itakuwa mume wangu kaamua kunionyesha upendo wa dhati”
“Pole sana, katika maisha huwa tunatakiwa kutafakari kila tunachokiona mbele yetu na kujua mantiki ya kitu hiko. Mungu ametuumba na akili kwa makusudi kabisa ili tuweze kuchambua mambo, unajua ulitakiwa uwe na mashaka pale tu mumeo anapokukatalia kuwa si yeye kuliko kujiwekea imani kuwa ni yeye wakati kashakuambia kuwa si yeye. Ngoja nikufundishe kitu”
Wote walitulia kimya kabisa wakimsikiliza huyu bibi, kwa muda huu aliweza kuwaeleza toka siku ya kwanza walipoingia kwenye ile nyumba mpaka yale mauzauza yaliyokuwa yakiwapata mwanzoni,
“Siku nilipokutana na wewe Sophia niliweza kuona maisha yenu kwenye ile nyumba na ndio maana nilikwambia kuwa nyumba unayoishi ni nyumba ya maajabu ila ulibaki kushangaa tu na kuitana na dada yako huku mkinihisi mimi ni mchawi. Lengo langu lilikuwa ni kuokoa maisha yako ila kwa muda huo hukuchagua kunisikiliza”
Sophia alitokwa na machozi kwani alikumbuka vizuri siku ya kwanza kukutana na huyo bibi na jinsi alivyomwambia kuwa nyumba anayoishi ni nyumba ya maajabu, Sophia aliongea kwa uchungu muda huu na huyu bibi
“Kwakweli bibi waswahili walisema usilolijua ni sawa na usiku wa giza, kipindi hiko sikuelewa maana ya methali hii ila sasa nimeelewa. Ni kweli uliniambia wazi kabisa kwamba nyumba ni ya maajabu ila hata sijui kwanini sikusikiliza maneno yako au hata kukutafuta na kuhitaji ufafanuzi zaidi. Sasa nimebakiwa na kovu zito lisilo na mwisho”
“Pole sana, ila nataka kukufundisha kitu. Huruma ni kitu chema sana katika maisha ila kinachotakiwa ni kupima huruma zetu, kuna watu walikaribisha watu ndani kwa huruma kumbe walikaribisha majambazi. Nchi yetu ina sheria zake pale upatapo mgeni usiyemtambua, kama nyie mlimkaribisha mtu ndani asiyekuwa mtu”
Sophia akadakia hapo na kumuuliza kuwa Neema ni nani, na kama ni mtu basi ni mtu wa aina gani.
Bibi alitulia kwanza kisha akawaeleza kwa kifupi kuhusu historia ya Neema,
“Kwanza kabisa napenda mfahamu kwamba Neema si mtu wa kawaida kama mnavyofikiria”
Wote wakashtuka na kusikiliza kwa makini,
“Neema alishakufa miaka ya nyuma huko, hata kaburi lake ukienda kufukua utakutana na mifupa tu. Ila jambo linaloendelea kwa Neema ni kisasi alichojiwekea kabla ya kifo chake.”
Sophia akakatisha mazungumzo kwanza na kuuliza,
“Kwahiyo Neema ni marehemu? Yani sisi tulikuwa tukiishi na marehemu ndani?”
“Neema alikufa siku nyingi, na pale alipo ni jini. Ngoja nikupe tabia za majini, kama umekuwa makini basi ushawahi kusikia kuwa kuna majini wazuri na majini wabaya. Na hawa majini huwa ni kutokana na ulivyokuwa tangu hapa duniani. Majini wabaya wao wamekaa makini sana kuingilia watu wenye tabia mbaya, ndiomana unaweza kukuta mtu ana tabia za ajabu na gafla zimezidi kupita za mwanzo ujue jinni mbaya ameshamuingia na yote hiyo ni sababu ya tabia aliyokuwa nayo toka mwanzo”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Huyu bibi alinyamaza kwanza kisha akaenda kuchukua majivu na kuwapaka kila mmoja mule ndani na kuwaambia sababu ya kuwapaka bile,
“Nimewapaka kwa tahadhari tu maana tunaongelea vitu hatarishi na watu ambao walishakufa siku nyingi sana. Mkaa ni dawa sana, ndiomana hata kama unahisi kuna watu wanafanya chuma ulete kwenye biashara yako ukaamua kuweka mkaa kwenye pesa zako basi hawatachukua hizo pesa tena. Mambo mengine sio lazima uende kwa mganga wa kienyeji ila ni maarifa tu, kama mkaa ni dawa basi majivu nayo ni dawa pia”
Humu ndani wakaishia kutazamana tu kwani hawakuwahi kufikiria kuhusu hiki kitu, kisha huyu bibi akaendelea kuwaeleza,
“Maisha ya Neema yalikuwa ni maisha ya visasi sana yani yeye akifanyiwa ktu lazima alipize na ndiomana imekuwa rahisi kwa majini wabaya kumtumia vilivyo ingawa amekufa na hiyo inapelekea hata marehemu kutokupumzika kwa amani sababu duniani unatumiwa vibaya. Unakumbuka mtu aliyekusaidia hadi ukarudi nyumbani kwenu?”
“Nakumbuka ndio, je nay eye alikuwa ni mtu kama sisi?”
“Hakuwa mtu pia ila ni jinni, yupo kwenye mwili wa mtu aliyekufa siku nyingi sana ila mtu huyu hakuwa na kisasi chochote juu ya mtu yeyote ingawa aliishi maisha ya shida sana ila hakuwa mtu mbaya. Na kilichomuua ni kitendo cha kulala na kaka yake ingawa hakujua kama ni kaka yake mwanzoni, hiko ndicho kilichopelekea kifo chake ila bado hakufa kwa kinyongo. Kuna baadhi ya vifo watu wanapokufa hutumiwa na majini, hapo ndio inategemea na tabia yako ilivyokuwa na ndiomana yule alikusaidia wewe kwani hakupenda kuona unakufa bila sababu ya msingi. Na je unajua kilichompata baada ya kukusaidia wewe?”
“Nini kimempata?”
“Ni mateso, ila mateso haya yataisha baada ya sisi kumaliza tatizo kuu la mtu mmoja wa visasi aitwaye Neema ambaye si Neema halisi bali ameshavaliwa ndani ya jinni mbaya”
Wote walikuwa kimya kabisa kwani hakuna aliyeweza kumuelewa moja kwa moja huyu bibi.
Bibi aliendelea kuelezea sasa na alimpa Sophia maelezo yale yale ya Ibra kukataa mimba ya mdogo wake Neema,
“Ila jiulize kwanini mtu ambaye anafanyia mabaya sio huyo Nancy? Ni kwasababu alikufa na kuyaacha yote duniani, hakutaka kuondoka na kinyongo na alijiona kuwa anastahili kufa. Tofauti na upande wa Neema, kwanza kabisa alikuwa na hasira na Ibra kwa kusababisha kifo cha mdogo wake na pia alipatwa na matatizo yaliyomfanya sfe kwa kinyongo sana, mwisho wa siku ameweza kutumiwa kwa visasi. Cha kujifunza ni kuwa si kila unayemtendea baya anaweza kukulipizia, ila je ile jamii iliyomzunguka imeridhika na lile baya ulilolifanya? Cha muhimu ni kujitahidi kutenda mambo katika mlolongo mzuri kwani tunaweza kukosea leo ila baada ya miaka kadhaa tukawatesa tunaowapenda kama ambavyo makosa ya Ibra yalivyomtesa Sophia”
Familia ya Sophia ilishangaa sana kwani hawakuweza kufikiria kama kuna kitu kama hiko kuwa Ibra amewahi kukataa mimba kwani Ibra alionekana ni kijana mstaarabu, mkweli na muwazi sasa iliwashangaza sana hii habari na kujiuliza kuwa Ibra aliwezaje kuyaficha yote hayo kwa mke wake, mama Sophia alimuangalia Ibra na kusikitika sana kisha akamwambia,
“Ibra unakumbuka wakati umekuja kumchumbia binti yangu? Nilikuuliza kabisa, je umewahi kuwa na mke? Ukakataa, nikakuuliza, umewahi kumpa mwanamke mimba au una mtoto? Napo ukakataa kumbe kuna mambo nyuma ya pazia mmh!”
Mama Sophia aliinama huku akisikitika ila huyu bibi akamwambia,
“Usisikitike sana, cha muhimu ni kushukuru uzima tu”
Kisha akaendelea kuzungumza nao,
“Kuna mambo ya mihimu sana kuyafanya ili muweze kuishi kwa amani sasa”
Ila kabla bibi hajaongelea hayo mambo, Sophia aliamua kumuuliza kuwa ilikuwaje hadi mumewe kuangukia kuinunua hiyo nyumba wakati kuna matatizo hayo,
“Kwanza kabisa mnatakiwa mjifunze kitu, ukiona kitu kinauzwa tofauti na thamani yake unatakiwa kukiwekea mashaka, angalia ile nyumba na pesa ambayo Ibra alinunulia yani haifikii hata robo ya thamani ya ile nyumba. Swali la kwanza ni kujiuliza kuwa imekuwaje mwenye mali akaiuza kwa bei ya hasara kiasi hiko? Kitu pekee kilichopelekea yule mwenye nyumba kuuza kwa bei hiyo ya hasara ni kutokana na mauzauza yaliyompata kwenye nyumba ile. Akashindwa kuvumilia na kuamua kuiuza huku akiamini kwamba huenda atakayenunua atakuwa salama kwani vile vitu vibaya vya kwenye ile nyumba havifahamu. Sema kwa bahati mbaya sasa, aliyeweza kuingia mkenge na kununua ile nyumba alikuwa ni mbaya wao, ila mwenye ile nyumba alijitahidi kwa kila hali kuhakikisha kwamba ile nyumba inakuwa salama kwa mnunuzi wake.”
“Sasa kwetu haikuwa salama kutokana na makosa ya Ibra au?”
“Ni kweli Ibra ndio chanzo ila wote mmechangia, na ubaya mkubwa mlioufanya ni kuweza kumkaribisha yule kiumbe ndani kwenu. Majini yanapenda sana kukaribishwa, na unapoyakaribisha yanakuwa huru zaidi na kufanya chochote wanachohitaji kufanya tofauti na usipomkaribisha. Kwahiyo kitendo chenu cha kumkaribisha kilimpa mwanya zaidi wa kuwasumbua na kuwafanya anavyotaka. Mfano kule kwenu pia wakati anagonga mngejaribu kumkaribisha tu basi kwa hakika hata msingeweza kuonana na mimi kwasasa kwani ameshakuwa na hasira zaidi na nyie na angemaliza wote mule ndani kwenu tena ingekuwa rahisi zaidi kwavile mmemkaribisha. Katika maisha tunatakiwa kuwa makini katika maamuzi yote tunayoyafanya na tuangalie je yanaweza kutudhuru kwa kiasi gani.”
Walikuwa kimya kabisa, kisha Sophia akauliza tena,
“Wakati tunakuja huku niling’atwa na nyoka je ilikuwa ni maana gani?”
“Hakuhitaji muonane na mimi, alikuwa anafanya kila njia kuwazuia na yule wala hakuwa nyoka bali ulikuwa ni upepo wa kuwashtua tu. Ila lile gari lililokuja kuwachukua ili muende nalo hospitali ndio lingewapeleka na maji”
Wakabaki wanashangaa kwani karibia wote hawakuwa na ufahamu wa kutosha juu ya mambo haya, yalikuwa ni mageni kabisa kwenye masikio yao na mawazo yao.
Sasa bibi akaanza kuwaeleza mambo muhimu ya kufanya kwa wakati huo kwaajili ya kuwasaidia kutokana na jambo hilo,
“Tatizo kubwa ni moja tu, yule kiumbe ana nguvu na ni kiumbe wa visasi yani hapa tunatakiwa kuwa makini sana kuhakikisha tunamshinda kabisa na ikiwezekana apotee kabisa mbele yetu.”
“Sawa bibi, sisi tunakusikiliza ili utuambie cha kufanya”
“Kwanza kabisa Sophia, nakuomba uchukue viatu vyako ulivyoviacha hapo nje ndio tuendelee na mambo mengine”
Sophia akainuka na kutoka nje, akainama na kuchukua viatu vyake ila wakati anataka kuinua kichwa sasa ili aingie ndani akaona miguu ya mtu amesimama mbele yake, na alipomtazama alikuwa ni Neema, kwakweli Sophia alipiga kelele sana.
Kitendo hiko kiliwafanya washtuke wote mule ndani, hata Sophia naye pale nje hakuweza kusogea wala kufanya chochote zaidi zaidi alianguka pale pale.
Bibi ndani alielewa moja kwa moja kilichomkumba Sophia na kufanya atoke nje ambapo Sophia alikuwa ameanguka chini huku akitetemeka tu, bibi alimuangalia Sophia kisha akamuangalia aliyesimama mbele yake, bibi hakuongea chochote zaidi ya kumsaidia Sophia kuinuka na kumuingiza ndani kisha akabeba vile viatu vya Sophia na kuviingiza halafu akafunga mlango wake huku akiwa kimya kabisa.
Hakuna aliyeweza kuhoji wala kusema lolote ukizingatia uoga ulikuwa umewajaa kupitiliza ila bibi nae alikuwa kimya kabisa, mara mlango wa bibi ukaanza kugongwa na kuwafanya mule ndani wazidi kuogopa kasoro bibi mwenyewe ambaye hakuonyesha uoga wa aina yoyote ile na wala hakusema kitu chochote, alionekana akitengeneza dawa tu za aina mbali mbali kisha akainuka na kumpaka Sophia halafu akaenda kumpaka Ibra huku ile hali ya kugongwa mlango ikiendelea na mwishowe ikawa kimya kabisa.
Kisha sasa huyu bibi akaanza kuimba imba nyimbo ambazo hawa wwngine hawakuzielewa, aliimba zile nyimbo kwa muda kama wa masaa mawili hivi kisha akanyamaza na kuanza kuwaangalia mule ndani kisha akawasalimia tena, walishangaa imekuwaje anawasalimia! Waliitikia ila hawakujua kwanini wamesalimiwa, huyu bibi alianza kuongea
“Mizimu yangu nawaomba, angalieni hawa vijana wameteseka sana. Inatosha kwasasa. Mateso waliyoyapata yanatosha. Nawaomba jambo moja tu, huyu anayewasumbua mchukueni, najua hiyo sio kazi ngumu kwenu. Mchukueni ili aache kuwasumbua hawa watu, mateso yale yanawatosha”
Huyu bibi akawa kimya sasa na kimya hiki alikaa kwa muda kidogo kisha akanyanyuka na kuelekea chumbani kwake.
Pale sebleni hakuna aliyeweza kuzungumza chochote na walikuwa kimya kabisa, ikapita kama nusu saa ndipo huyu bibi alipokuja na kuanza kuzungumza nao tena, kisha aliwauliza
“Mnajua kuhusu mizimu?”
Wote wakatikisa vichwa kuwa hawajui ila ni mama Sophia tu aliyejaribu kujibu,
“Mi huwa nasikia kuwa mizimu ni watu waliokufa zamani sana”
“Ni kweli ila vile vile mizimu ni malaika wanaotulinda huwa tu wanavaa ngozi za watu waliokufa, lengo lao kubwa ni kutulinda ili tusiteketee ila muda huo huo tunapowakosea wanauwezo mkubwa wa kutuangamiza”
Sophia akauliza,
“Kwa maana hiyo Neema ni mzimu? Kwahiyo ni malaika?”
“Neema ni mzimu ndio ila si malaika ni jini, nyie humuona kama binadamu ila Neema si binadamu wa kawaida. Na nilishawaeleza kwa kifupi histroria ya Neema, ningewaambia kwa kirefu ila sipendi kupoteza muda juu ya jambo moja. Neema alikuwa na roho mbaya sana tofauti na jina lake, na katika maisha yake alikuwa ni mtu wa visasi sana, hakuna mtu aliyewahi kugombana nae bila ya kumfanyia visasi na hata alipokuwa anakufa alikufa na kinyongo moyoni ndiomana mwisho wa siku ametumiwa na jinni mbaya akiyaendeleza yale matendo yake. Kwa maana hiyo Neema hana amani na hawezi kuwa na amani kwani anatumika vibaya huku duniani kutokana na roho aliyokuwa nayo tangia alipokuwa binadamu wa kawaida”
Bibi akatulia kwa muda na kuendelea,
“Muda niliokuwa nikiimba nilikuwa nikiita mizimu yangu ili inisaidie kuniondolea Neema na kwasasa wameshamshikilia na wamenielekeza cha kufanya”
“Ni kitu gani hiko?”
“Tunatakiwa tukafanye kafara kwenye kaburi la Neema, na kafara hiyo ni kuchinja mbuzi ila huyo mbuzi atatakiwa achinjwe na Ibra”
Hakuna aliyebisha wala aliyepinga kwa wakati huo, kisha huyu bibi akajitolea mbuzi wake kwaajili ya kwenda kufanya hiyo kafara kisha wakaianza safari.
Walipofika makaburini, bibi alisimama kwanza na kumuangalia Sophia kisha akamwambia,
“Mimi sijui kaburi la Neema lilipo ila nimeambiwa kuwa wewe unajua kaburi lake lilipo”
Sophia akamkumbuka yule bonge wa hospitali na akakumbuka jinsi alivyoonyeshwa kaburi la Neema na jinsi alivyopewa maelekezo na yule bonge kwahiyo moja kwa moja aliongoza mpaka kwenye kaburi la Neema ambapo bibi aliwapaka dawa kisha Ibra akatakiwa kumchinja mbuzi juu ya kaburi hilo, kisha naye akafanya hivyo na muda huo huo Ibra akajikuta akiweza kuongea kama zamani. Kwakweli alifurahi sana kwani hakufikiria kama ataweza tena kuongea kama zamani kwahiyo kwake hili lilikuwa ni jambo la kushukuru sana. Alijikuta akimsogelea yule bibi na kuanza kumshukuru bila kikomo, ila huyu bibi alitabasamu tu na kuwaomba waondoke eneo hilo na kurudi nyumbani kwani giza nalo lilishaanza kuingia.
Walipofika tu, kabla hawajaingia ndani bibi akasikia sauti ya mbuzi ikitoka ndani kwake ilihali mbuzi wake wote wapo kwenye banda nje, kwahiyo bibi akawaomba wasiingie ndani kwanza mpaka pale atakapofanya dawa zake. Kwahiyo aliwataka wote kutulia pale nje kisha akaongea ongea maneno na kuingia ndani kwake ambapo alitoka na dawa na kuinyunyiza nyumba nzima kisha akarudi ndani na kuanza kuwaita mmoja mmoja kwa majina tena aliwataka waitike ndio waingie ndani, nao wakafanya hivyo kwahiyo alipowamaliza wote akafunga mlango. Giza nalo lilikuwa limeshaingia tayari, hivyo karibia wote mule ndani walikuwa wamejikunyata
“Jamani, usiku ndio unakuwa na mambo mengi sana, hivyo tunatakiwa kuwa makini sana na huu usiku wa leo kwani yule Neema ndio atamalizia hasira zake leo na kama tukiwa wadhaifu basi atatushinda kwa mara nyingine. Kwa tulichokifanya tumemshind tayari, sasa hatutakiwi kutetereka na chochote. Mkisikia anagonga mlango wala msishtuke, mkisikia anaongea wala msishtuke tuwe kimya kabisa na kama tumelala muda huo basi tulala vizuri kabisa yani hofu na mashaka vyote viondoeni. Huu ni usiku wa mwisho kwake”
Walikubaliana na bibi kisha kuendelea na mambo mengine.
Wakati wamelala yani usiku wa manane wakaanza kusikia mtu akigonga mlango na wa kwanza kusikia mlango ukigongwa alikuwa ni Sophia, uoga ulimjaa ila akashika maneno ya yule bibi kuwa wasiwe na uoga wa aina yoyote ile. Kadri muda ulivyozidi kwenda ndipo ile gonga ya mlango nayo iliongezeka na kuna muda mlango uligongwa kanakwamba anayegonga anataka kuuvunja kabisa. Uoga ulianza kuwajaa ila wakajipa moyo, Sophia alimuangalia yule bibi ambaye alikuwa amelala hoi kabisa na kufanya Sophia azidi kupatwa na wasiwasi ikiwa kama yule mgongaji akitaka kuwafanyia kitu kibaya ikabidi Sophia amuamshe yule bibi kwa kumtingisha ila huyu bibi alipoamka alimpa ishara Sophia kuwa alale tu, kitendo cha Sophia kuambiwa kwa ishara kuwa alale tu kilionwa pia na Tausi na mama yao ambao walikuwa wameshtuka pia hivyo wakarudi tena kuendelea na usingizi ambao kiukweli ulikuwa ni usingizi wa uoga kwani walilala bila amani.
Ulipita muda mrefu kidogo ndipo zile harakati za kugongwa kwa mlango zilipoacha na waliendelea kuwa vile vile hadi kunapokucha, na kulipokucha tu wote waliamka na kukaa huku wakimsikilizia huyu bibi kama wataendelea kuongea.
Huyu bibi alipoamka cha kwanza kabisa alicheka sana na kuwauliza,
“Mbona mpo kimya?”
“Ulisema tusiongee chochote”
Huyu bibi alicheka zaidi na kuwaambia,
“Nilisema msiongee ule usiku kwamaana ya kumkaribisha yule mgongaji ila sio kumekucha hivi na ameshaondoka”
Kisha huyu bibi akachukua dawa nyingine na kuwapaka,
“Hii dawa ni ya mwisho na kuanzia sasa mpo huru kabisa, ila cha msingi na muhimu msirudi tena kwenye ile nyumba”
Sophia akauliza,
“Na vitu vyetu je?”
“Hakuna mlivyoacha zaidi ya zile nguo zenu, kwanza kabisa mnachotakiwa kufahamu ni kuwa ile nyumba imejengwa chini ya majini, ile nyumba inalindwa na majini. Mwenye nyumba alikuwa na majini mengi sana. Jiulizeni kwanini ile nyumba unaweza ukajisahau ikawa wazi ila ukirudi hakuna kilichoibiwa! Kwenye ile nyumba vitu vyote mmevikuta mule ndani, hakuna cha kwenu mule zaidi ya nguo, je naongea uongo?”
Sophia akamtazama mume wake ili apate mrejesho wa majibu kwani yeye hakujua kama mumewe alikuta kila kitu ndani, Ibra akajibu
“Ni kweli bibi, aliyeniuzia ile nyumba aliniambia nichukue na vitu vyote vya mule ndani eti yeye havihitaji tena”
Sophia alijikuta akimuuliza Ibra kwa hamaki,
‘Kheeee, hadi Tv, makochi, Friji, vitanda na magodoro?”
“Sasa mke wangu unafikiri mimi nilikuwa na pesa gani kiasi cha kununua nyumba na kununua fenicha zote zile niweke ndani? Huwezo huo sikuwa nao kabisa, hata hivyo ile nyumba niliinunua kwa bei ndogo sana unaweza sema ni nyumba ya tope ila nikapewa na kila kitu kilichopo mule ndani ambacho gharama yake ilizidi hata bei ya nyumba. Ndiomana wakati tunahama kule tulipokuwa tunakaa mwanzo nikakwambia tusichukue chochote tubebe nguo zetu tu”
Sophia na wote mule ndani waliishia kusikitika tu kwani hata Sophia mwenyewe hakufikiria kama mule ndani walikuwa wakiishi kwenye misingi hiyo.
Bibi aliendelea kuwaambia,
“Kwahiyo kama mtataka nguo zenu labda niwape dawa za kwenda kuchukua hizo nguo na kuachana na ile nyumba kabisa, aliyeachiwa tu ile nyumba ni ana mizimu hatari nay eye kama angeamua kuishi mule angalau angeweza kupambana na hayo majini ila nyumba ilimshinda pia. Je mtaweza nyie watu wa kawaida? Pale ukiwa ni mtu wa dini hakikisha umeshika dini kufa na kupona yani usitetereke hata kidogo maana kitendo cha wewe kutetereka basi ushawapa nafasi wale majini na hapo utajuta kuwafahamu. Ile nyumba kuna kipindi unaweza kwenda eneo lile ukatafuta na kutafuta usiione, kwahiyo jamani ile nyumba sio nyumba ya kawaida na ndiomana siku ya kwanza kabisa nakuona Sophia nilikwambia kuwa ile nyumba ni nyumba ya maajabu”
Wakakaa kimya kwa muda kwanza kwani hakuna hata mmoja aliyekuwa na hamu ya kurudi kwenye nyumba hiyo. Kisha mama Sophia akauliza kitu kingine,
“Je kitendo cha hawa kwenda kuchukua nguo zao kwenye nyumba ile hizo nguo hazitawadhuru kweli?”
“Tena umenikumbusha kitu, kuna jambo nililiona kwenye ndoto usiku kwahiyo cha kuwashauri kwasasa ni bora hizo nguo mkasamehe tu na mkaanze maisha upya kabisa. Achaneni na hizo nguo msije mkahama na majini bure”
“Huyo aliyejenga alikuwa na maana gani kujenga na majini?”
“Ni historia ndefu sana ila aliyejenga nyumba ile alitafuta utajiri kwa waganga ambapo alipewa jinni lililoita wenzie zaidi na zaidi halafu kulitoa jinni lile alishindwa kwani mganga aliyempa alikuwa ameshakufa kwahiyo majini yakawa ndio rafiki zake na akawa anawasaidia hadi kupata damu ya watu na kunywa. Kwahiyo mambo yake mengi sana aliyafanya kwa kutumia majini”
“Sasa itakuwaje ile nyumba kama akienda kukaa mtu mwingine?”
“Ile nyumba kwasasa ni picha tu na kama hamuamini mnaweza kwenda msiione, ila atakayejitia kiburi pale basi atakwenda na maji. Hakuna mwenye uwezo wa kuiteketeza ile nyumba zaidi ya yule aliyeachiwa ambaye hayupo nchini ila siku akirudi kwa hakika mizimu yake itamuonyesha mateso yenu na kumfanya akaiteketeze ile nyumba kwahiyo msiwe na mashaka yoyote”
“Kwahiyo tukirudi majumbani kwetu tunaweza kuishi kwa amani?”
“Ndio mtaishi kwa amani kabisa ila kwa ushauri nawaomba kila mmoja aende kwa kiongozi wake wa dini akapate ushauri wa kiroho, mfanyiwe sala na maombi kisha muwe na imani kwa Mungu ili muweze kuendelea mbele. Mfano kama wewe Sophia na hivyo kizazi kilishatoka basi hata raha ya maisha umekosa ila mrudie Mungu na utapata amani na furaha”
“Inamaana wewe unafanya mambo ya kiganga na maombi pia?”
“Tunatakiwa tuamini juu ya uwepo wa Mungu katika maisha yetu, yani kama unatembea na humuamini Mungu basi ujue wewe una matatizo kushinda hata huyo tunayemuita shetani. Wote tumeumbwa na Mungu na tunapaswa tumuamini katika maisha yetu.”
Sophia na Ibra wakawa kimya kwa muda huku kila mmoja akijitafakari kivyake kwani wao hawakuwa watu wa maombi wala ibada na wakashangaa mtu kama huyu anayetumia madawa ya kienyeji bado anawashauri wamuamini Mungu na wamrudie Mungu.
“Nawaambia kweli, laity kama mngekuwa ni watu wa ibada basi kwa hakika kuna mambo mngeyaepuka kabisa hata kwenye ile nyumba msingekaa hata wiki mngehama wenyewe na mngejiokoa na mambo mengi ila kwavile hamkuwa watu wa ibada ndiomana akili zetu zilimalizwa kwa urahisi sana”
Wakaafikiana na huyu bibi, wakakumbuka hata vile Jane alivyokuwa akiwashauri kuwa wafanye maombi jinsi gani walivyokuwa wakimponda ila kwasasa walibaki kujutia tu. Bibi aliwaruhusu kuondoka na kurudi makwao.
Safari ya kutoka pale kwa bibi ikawadia na sehemu ya kwanza ilikuwa kumuacha Siwema nyumbani kwake kisha na wao kurudi makwao, Ibra alirudi kwao na Sophia pia alirudi kwao na familia yake ambapo kama walivyoshauriwa na yule bibi waliamua kumtafuta mtu wa maombi aweze kusaidiana nao katika kuiombea familia yao ambapo alifika na kuwasaidia kwa maombi huku akiwasisitiza kuwa wasiache kufanya sala na katika maisha yao sala iwe ni kila kitu.
“Kwakweli tumejifunza vitu vingi sana, wengine hapa ilikuwa kitu kidogo tunakimbilia kwa mganga wakati kumbe tungetulia na kumshirikisha Mungu basi kila kitu kingeenda sawa ila tumejifumza sana”
Mama Sophia alikuwa akijilaumu yeye mwenyewe kwanza,
“Ila kosa ni langu la kutowafundisha wanangu maadili ya kumjua Mungu ndiomana yote haya yametokea ila tumepata fundisho sasa”
Wakaanza kujitahidi kufanya ibada kila siku na ikawasaidia kuishi na kulala kwa amani bila ya hofu wala tatizo lolote.
Baada ya muda kiliwekwa kikao cha familia mbili yani familia ya Ibra na familia ya Sophia ambapo Ibra alienda kumdai mkewe kuwa wakaanze maisha upya, kwa upande wa Sophia ilikuwa tofauti sana kwani alikataa katakata,
“Ibra, siwezi na sitaweza tena kwenda kuishi na wewe nisamehe tu kwa hilo ila sitaweza kabisa kabisa yaliyonikuta yanatosha”
“Kwani mimi niliyapanga hayo Sophia jamani?”
“Naweza sema uliyapanga ndio, kwanza fikiria kuwa ujinga ufanye wewe kwenye ujana wako huko halafu mateso nipate mimi yani sitaweza kuwa na mtoto sababu ya ujinga wako. Fikiria pia, kwanini hukuniambia toka mwanzo kiasi cha pesa ulichonunulia ile nyumba na kwanini hukuniambia kama kila kitu ulikikuta mule ndani labda akili yangu ingefunguka. Kwakweli Ibra sitaweza tena kuishi na wewe”
Wazee waliamua kumshauri Sophia na kumshawishi arudiane na mumewe ila Sophia alikataa katakata. Ikabidi kikao kihairishwe tu kwani hawakupata muafaka wa aina yeyote ile.
Kesho yake Ibra alienda tena nyumbani kwakina Sophia na kutimuliwa ila baada ya wiki alienda tena na kumuomba Sophia jambo moja tu.
“Jambo gani hilo?”
“Naomba twende mahali, halafu hapo ukaniache rasmi name sitalalamika tena”
Kwavile Sophia hakutaka usumbufu wa Ibra tena ikamlazimu akakubali tu kisha wakafunga safari na moja kwa moja Ibra alienda na Sophia mahali ambapo walianza wote maisha, Ibra akamwambia Sophia
“Unapakumbuka hapa?”
“Napakumbuka, si ndio tulipoanzia maisha! Ila kwangu hapana thamani tena laiti ningejua bora ningebaki hapa tu kuliko kule tulipohamia”
Kisha Ibra akaondoka pale na Sophia na kwenda nae kule walikohamia,
“Kwanini tumekuja huku tena?”
“Nilikuwa nakamilisha kuangalia mazingira yaliyofanya tuachane, pale kwa mwanzo tuliishi kwa amani sana ila huku ndio kumefanya tuachane. Na baada ya hapa sitakusumbua tena Sophia kwani najihisi nitakuwa chizi”
Ila kadri walivyosogea hawakuweza kuiona nyumba waliyokuwa wanaishi badala yake ulionekana uwanja mpana sana na ndani ya uwanja huo kulikuwa na maandishi yaliyosomeka kwa herufi kubwa ‘NYUMBA YA MAAJABU’ Sophia akashtuka sana na kuogopa kisha akamuangalia Ibra, muda huu Ibra akamwambia Sophia,
“Kwaheri Sophia maana kwa hakika sitaweza kupambana peke yangu, nilikutegemea wewe, nakupenda sana na sitaweza kuendelea kusema nina furaha wakati furaha sina. Mimi naenda kuingia pale kwenye kiwanja na nitakaa humo maisha yangu yote mpaka pale Mungu atakaponiita”
Ibra alimbusu Sophia kwenye paji la uso kisha kuanza hatua za kuelekea kwenye kiwanja kile ambapo kila aliposogea alianza kuiona nyumba waliyokuwa wakiishi ikijitokeza, Sophia hakuweza kustahimili Ibra arudi tena mule hivyo alimkimbilia na kumshika mkono kisha kusogea nae mbali kabisa, akamuangalia kwa uchungu na kumwambia,
“Nimekusamehe Ibra, nakupenda sana”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakakumbatiana huku wakilia kwa uchungu na kujikuta wakikumbuka yale yote waliyokuwa wakiyapitia.
------------------------------
---------------MWISHO---------
------------------------------
0 comments:
Post a Comment