Search This Blog

JENEZA LA AJABU - 3

 

    Simulizi : Jeneza La Ajabu

    Sehemu Ya Tatu (3)





    Mwamutapa;

    Mama yake Njoshi akiwa mwenye huzuni,

    huku mawazo mengi kuhusu mwanae, yakishindwa kumtoka kichwani mwake. Anachukua

    jembe lake, pamoja na kikapu na kisha kuanza safari kuelekea shambani, lakini

    pia kitendo cha Ngesha kuondoka bila kumuaga na kushindwa kutambua mahali

    alipoelekea ghafla . Kilizidi kumwongezea maswali, kwani alihisi kuna jambo

    ambalo Ngesha alitaka amweleze Njoshi, jambo la muhimu sana, na ndio maana

    alishtuka baada ya mama yake Njoshi kumweleza kuhusu mahali ambapo Njoshi

    alielekea,kitendo kilichomshitua rafiki yake,na kisha kuondoka haraka sana bila

    hata kuaga.

    “Labda kaelekea

    kwa mfalme kuangalia usalama wa rafiki yake,lahasha!,si angeniambia tu kuwa

    anaelekea huko,”mama yake Njoshi alizungumza peke yake,huku akiwa njiani

    kuelekea shambani,akiwaza na kuwazua kitendo cha rafiki yake mwanae ,kuondoka

    ghafla bila hata kumuaga.

    Msitu wa majini;

    Njoshi akiwa na hofu,huku akitetemeka

    mithili ya mtu aliyenyeshewa na mvua ya masika,mnvua inayoandamana na baridi

    kali.Alinyanyuka kutoka mahali alipokuwa amejificha,huku akiwa haamini,kama

    kweli kundi lile la askari hatari wa msituni walimpita bila hata kumwona ,na

    kisha kutokomea upande mwingine wa msitu,kwenda kumtafuta.

    “Hapa ngoja nipite

    upande mwingine nielekee kwenye ngome ya malikia,lazma leo nifanikishe misheni

    yangu na kisha kesho nirudi nyumbani”,Njoshi aliongea peke yake kama

    kichaa,na kisha kushika panga lake,ambalo tayali alikuwa amelitelekeza chini bila

    kujitambua,kutokana na hofu aliyokuwa nayo kipindi akiwashuhudia askari wale wa

    msituni,wakipita mbele yake.

    “Eeeeh mizimu wa

    mababu,niokoeni na balaa hili kijana wenu”,Njoshi aliomba mizimu huku

    akifumba macho yake kwa dakika chache,na kisha kutamka maneno ya kitamaduni

    bila kutoa sauti,na baada ya sala hiyo,Njoshi alitokomea kuingia ndani kabisa

    ya msitu,kwa kupitia upande mwingine tofauti kabisa na upande ambao jeshi

    lililokuwa likiongozwa na jini mweupe,waliweza kuelekea huko.

    “Miii……zi…mu

    niokoeniii……na ku…faaa!!”, zilikua ni kelele za Njoshi ghafla,kwani sehemu

    aliyokuwa akipita,ni kama vile aliruka mkojo na kukanyaga mavi,kulikua na shimo

    ndefu sana kuelekea chini, likiwa limetegwa huku juu kukiwa kumefunikwa na fito

    nyembamba kama kuni,ambazo zingevunjika pale tu

    mtu atakapozikanyaga .Pia fito hizo zilifunikwa na majani makavu pamoja

    na udongo,kiasi kwamba mtu asingeweza kugundua kitu chochote,bali sehemu hiyo

    ilionekana kuwa kama njia nyingine,kwani kulikuwa hamna tofauti yoyote ile.

    Mtego huo kweli

    ulifanikiwa kumnasa Njoshi,ujanja wote aliokuwa nao,pamoja na uhodari,uliweza

    kumwishia,na kumfanya kuwa mpole,tangu alipoikanyaga ardhi ya msitu wa

    majini.Alijilaumu sana kupita njia ile ,njia ambayo ilionekana kupaliliwa

    vizuri bila kutambua kuwa katika njia hiyo kulikuwa na mtego wa shimo uliotegwa

    na kisha kufunikwa na udongo.

    “Pwaaaaah…………”,ilikua

    ni sauti ya maji mengi ikimpokea Njoshi,baada ya kusafiri umbali wa  kama mita mia mbili kwenda chini,sawa na

    urefu wa viwanja viwili vya mpira wa miguu.

    “Duuuh kweli leo

    nimepatikana,lakini mimi nishujaa,kwa vyovyote vile lazima niishinde vita

    hii”,Njoshi aliongea maneno ya kishujaa na kujipa moyo,huku akiziba pua

    yake kutokana na harufu kali ya maji yale yaliyoonekana kuwa machafu sana,maji

    yaliyomfika Njoshi kifuani mwake

    “Mungu wangu!,nini

    tena hiki……yalaa……aaa”,.Njoshi alipigwa na butwaa,huku sauti kubwa ya hofu

    ikimtoka kinywani mwake,kwani alipojaribu kupapasa maji yale kwa kutumia mkono

    wake,alijikuta ameshika kichwa cha binadamu kilichokuwa kimeliwa na kuoza

    vibaya,kitendo kilichomfanya akitupe haraka sana na kisha kupiga kelele

    kutokana na hofu kubwa aliyokuwa nayo.

    Ikulu kwa mfalme;

    Ikiwa yapata mida kama ya saa nne

    asubuhi,Ngesha anafanikiwa kutoboa tundu,baada ya tofali moja kupasuka na

    kuachia nafasi katika ukuta uliozunguka ngome ya mfalme,nafasi hiyo iliweza

    kuonesha kila kitu kilichoendelea ndani ,kama mtu akiweza kuchungulia.

    Kijana Ngesha baada ya

    kuangalia huku na kule,na kugundua kuwa hakuna mtu yeyote aliyekuwa akimtazama,tofauti

    na siku zote kwani walinzi wa mfalme walizunguka muda wote,kuhakikisha hakuna

    mtu yeyote aliweza kuusogelea ukuta huo.

    “Duuuh leo,pako

    shwaliii,kulikoniii??,yaani hamna hata wale mbwa wanaojiita askariii

    “,Ngesha aliongea maneno ya kejeli huku yakiwa na mshangao ndani yake,na

    bila kupoteza muda aliweza kuchungulia ndani ya ngome ya mfalme,ngome ambayo

    ilijitenga mbali kidogo na makazi ya watu,huku msitu mdogo ukiizunguka ngome

    hiyo,na haikuruhusiwa mtu yeyote kuuvuka msitu,na kisha kuisogelea ngome hiyo

    bila sababu maalumu,ukikamatwa adhabu ilikuwa ni kifo tu na sio kitu kingine.

    Kutokana na sheria

    hiyo,watu wengi waliogopa sana kuisogelea ngome ya mfalme,na ndio maana Ngesha

    alifanikiwa   kutazama ndani bila kuonwa

    na mtu yeyote,baada ya kujidhihirisha kuwa askari hawakuepo eneo lile.

    “Aiweeeh……mizimu
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    wa mababu,mbona watu wanalia!!,mbona Njoshi simuoni,mmmh mfalme

    kafa???” maswali mengi yalimuandama Ngesha, mala tu baada ya kuchungulia

    ndani ya ngome ya mfalme,alishangaa kuona familia yote ya mfalme ikilia

    sana,wake kwa waume,wakubwa kwa wadogo.Lakini pia alipojaribu kuangaza vizuri

    kila kona,hakuweza kumuona Njoshi,hali iliyomfanya azidi kupigwa na butwaa.

    Lakini bila kutegemea, kuna jambo kubwa sana lilimshitua kuliko yote,

    alishangaa kumuona binti mfalme, na si mwingine, alikuwa ni msichana Grace,

    msichana ambaye rafiki yake Njoshi alimpenda sana, akilia kwa kwikwi huku

    akimtazama mfalme aliyeonekana kulala bila kumjibu chochote kile. Grace

    alitamka maneno ya kumtaka baba yake asife, na kumwacha akiwa hana baba,

    kitendo kilichomfanya Ngesha kushtuka, kwani hakuona sababu ya kumfanya mfalme

    afe haraka sana kiasi hicho.

    “Mmmmh au ndio

    maana mfalme haonekani mtaani, na imepita mwezi sasa, manyanyaso yamepungua,

    lakini kwanini baba yake Njoshi kauawa?, sababu ilikuwa nini nini?, inawezekana

    kweli mfalme kafa, ngoja nielekee shambani kwa mama yake Njoshi nikampatie

    taarifa hii, ninaweza kutambua kitu fulani “,Ngesha aliahirisha

    kuchungulia ndani kwa mfalme, na kisha kufunga safari kuelekea shambani kwa

    kina Njoshi, huku maswali lukuki yakimsumbua bila kuwa na majibu yoyote ya

    maswali hayo.

    Shambani kwa kina

    Njoshi;

    Mama yake Njoshi akiwa amejipumzisha

    chini ya mti wa maembe, mti pekee uliopatikana shambani kwake, aliendelea kula

    chakula chake taratibu, huku akishushia na maji kwani tayali ilikua imeshafika

    saa sita, mida ambayo tayali jua lilikuwa limechanganya vilivyo na kuwa kali

    sanaa.

    “Eeeeh mizimu ya

    mababu, muokoeni mwanangu “,ilikua ni sauti ya mama yake Njoshi akimuombea

    mwanae kwa mizimu, iweze kumpatia msaada, kwani kutokana na uwezo wa kitabiri

    pamoja na uganga ambao mumewe alimrithisha, aliweza kutambua kuwa mwanae yuko

    hatarini, tena hatari kubwaa, baada ya ndege aliyekuwa juu ya mti ule wa

    maembe, kumnyea na kisha kinyesi chake kudondoka katika matiti ya mama yake

    Njoshi. Mama yake alikitafakali kitendo kile, na kugundua kuwa ilikuwa ni kama

    ujumbe kwake, kuwa mtu aliyenyonya maziwa kutoka katika matiti yake, yuko

    kwenye shida na matatizo, huku kinyesi cha ndege yule kikisimama kwa niaba ya

    matatizo yanayomsibu mwanae. Utabiri ambao ulikuwa sahihi, kwani wakati huo

    Njoshi alikuwa ndani ya shimo kubwa msituni, huku akisubili kukamatwa na majini

    hatari wa msituni.



    Msitu wa majini;



    Jeshi la msituni, wakiwa wanamtafuta adui aliyevamia msitu wao bila mafanikio, ghafla amli inatoka kutoka kwa kiongozi wao, jini mweupe, waweze kurudi nyuma, upande wa pili wa msitu, katika njia ya kuingilia katikati ya msitu wao, njia ambayo waliweza kutega shimo ambalo lingeweza kumkamata adui yoyote yule kama angekanyaga shimo hilo lililofunikwa kwa udongo,shimo ambalo lilitegwa katikati ya barabara..



    “Twendeni haraka sana katikati ya barabara tuliyotega mtego wa shimo, tayali adui ameshanasa “,Jini mweupe alitoa amli kwa jeshi lake, na bila kupoteza muda, walipotea  na kisha kutokea eneo ambalo shimo lilikuwepo.Jini mweupe alikuwa sahihi kabisa, kwani walikuta tayali mtego ulishamnasa adui, mtu waliyemtafuta tangu asubuhi, na ilikua tayali imefika majira ya jioni bila kumtia mikononi.



    “Fungeni kamba katika mti huo, na kisha dumbukizeni shimoni, harafu ingieni watu wachache mkamkamate,”jini mweupe alizidi kutoa amli na maelekezo, huku majini wale wakiweza kutekeleza maagizo waliyopewa haraka sana. Walishindwa kutumia nguvu za kijini, kumkamata adui yao, jambo ambalo ingekuwa rahisi kumkamata kijana Njoshi, na kujikuta wakitumia njia za kawaida bila kujielewa, njia ambayo isingefanikiwa, bali ingemrahisishia adui yao kutoka ndani ya shimo na kuwaponyoka. Hayo yote yalitokea kutokana na maombi ambayo mama yake Njoshi, aliweza kuomba mizimu iweze kumsaidia mwanae kutoka katika hatari, pamoja na maombi ambayo Njoshi mwenyewe aliweza kuyafanya kila wakati ambapo hatari ilimkabili.



    ********



    Sauti nzito za kutisha, zikiandamana na mwangwi mzito, Njoshi anazisikia akiwa shimoni. Hakuweza kuogopa tena, lolote ambalo lingetokea, alikuwa tayali kukabiliana nalo, kwani aliona akiendelea kuwa muoga, hatoweza kuishinda vita ambayo iko mbele yake.



    “Bila shaka watakuwa wamenifuata mimi, waweze kunikamata, hapa lazima nipambane, lazima nife kiume “,Njoshi aliongea huku akiitazama kamba iliyokuwa inashushwa taratibu ndani ya shimo, na kuona kama hiyo ndio ilikua njia pekee ya yeye kutoka shimoni. Na kulishika panga lake kisawasawa katika mkono wake wa kulia, akiwa tayali kuchinja kiumbe chochote kile kitakachoingia shimoni, huku akiwa amebeba kibegi cheusi mgongoni, kibegi kilichotumika kuhifadhia panga pamoja na kitambaa cheusi chenye nguvu za ajabu, kitambaa ambacho kajifunga kiunoni.



    “Huyu mshenzi hanioni, hii ndio dawa yake, “Njoshi aliongea huku akimfyekelea mbali jini mmoja, jini ambaye mwili wake uliundwa kwa mifupa tu, baada ya kushuka na kamba ndani ya shimo, na kuangaza huku na huku bila kumwona adui yake. Lakini Njoshi alishangaa sana, kwani baada ya kulitumia panga lake,  jini yule aliyeyuka kama vile kaunguzwa na moto, na kisha kutoweka kabisa.



    “Ahaaaa asante sana mama yangu, kumbe ndio maana ulinambia kuwa hii ndio siraha yangu ya kunirudisha nyumbani salama, ndio maana hata hawanioni, inaonekana huu mkanda pia unanisaidia “,Njoshi aliongea huku akitabasamu, na kushika kamba ili apande kuelekea juu, aweze kutoka shimoni, lakini alisita baada ya kusikia kelele za fujo na hasira, huku akihisi kama kuna viumbe wa ajabu, wenye hasira walikuwa wakiitumia kamba kumfata shimoni.



    ********



    Jini mweupe, pamoja na majini wote wa msituni ikiwemo malikia, wanapata maumivu makali sana, maumivu ambayo hutokea katika miili yao, pale tu jini mwenzao anapopoteza maisha. Kutokana na hasira ya kumpoteza mwenzao, baada ya jini mmoja kuingia ndani ya shimo kumkamata adui aliyeuvamia msitu, na kukutana na panga la ajabu shingoni mwake, panga pekee lenye uwezo wa kuangamiza majini.



    Baada ya jini huyo kupoteza maisha, maumivu makali yanawakumba majini wote wa msituni, na kupiga kelele nzito za hasira, kelele ambazo zilisikika katika nchi yote ya Mwamutapa, na nchi jirani, kelele ambazo zilimshtua Njoshi shimoni, na kushindwa kupanda juu kwa kutumia kamba, kutoka ndani ya shimo.



     “Huyu binadamu tukimkamata lazima tumle nyama ,lazima alipie maumivu haya “,malikia wa majini akiwa katika ngome yake, alizungumza kauli ya kisasi, kauli ambayo itamghalimu sana baadae kuitengua, kwani malikia wa majini akiongea kitu lazima akitimize, kuepuka kuteketea kwa watu wake, jambo ambalo itangua kwake kumla nyama Njoshi, kwa nini itakua ngumu?  endelea kufuatilia ,



    *******



    “Siwezi kuumia kiasi hiki ingieni mkamkamate, akiwa hai au amekufa “,ilikua ni sauti ya jini mweupe, kiongozi wa askari wa majini, askari ambao walifanya kazi ya kuulinda msitu wa majini,akiruhusu jeshi lake kuingia shimoni, baada ya mwenzao aliyetangulia mwanzoni kuuawa, kitendo ambacho kilimfanya Njoshi asite kuelekea juu, kwani alihisi kamba ikiwa nzito sana, alipoishika, kitendo kilichoashiria ujio wa kundi kubwa la majini ndani ya shimo, kwa kutumia kamba ile.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwamutapa



    “Aiweeeh mama nimerudi tena, pole na kazi, nimetoka kwa mfalme lakini sijamkuta Njoshiii, pia nimekuta kilio eti mfalme kafa, unaweza niambia chochote? ,kwani kwanini mfalme alimuua baba yake Njoshi ………”,Ngesha    ,rafiki yake Njoshi, alimuulza mama wa rafiki yake maswali mengi sana baada ya kumfuata shambani, lakini taarifa hiyo haikumshitua mama yake Njoshi, kwani alifahamu kila kitu.



    “Baba wa rafiki yako aliuawa kwasababu alishindwa kumtibu mfalme, kwani ni mwezi umepita sasa mfalme anaumwa, na ni siri haitakiwi Wanamutapa wafahamu, na pia ni kweli mfalme kafa lakini atafufuka japo sina uh…aki…ka “,mama Njoshi akiwa ameshika jembe, akipalilia polepole mahindi yake, alimjibu Ngesha na kushindwa kumalizia sentesi yake, baada ya kusikia sauti nzito za kutisha kutoka msituni, sauti ambazo ni adimu sana kuzisikia. Sauti hizo zilimwogopesha Ngesha, kiasi kwamba alitaka kukimbia, kwani ziliogopesha sana.



    “Wii…Wii…wiiii……ihiii…hii … hiii”,zilikua ni sauti za mwangwi zikitoweka kwa mbalii, kutokana na sauti za hasira zilizosikika kutoka kwa viumbe wa ajabu wa msituni.



    “Kuhusu sehemu alipo Njoshi, nazani umesikia sauti hizo za ajabu kutoka msituni, Njoshi kaelekea huko katika msitu wa majini, na tayali ameshaua  jini mmoja, na kila atakapoua, utazisikia kelele hizo za hasira kutoka kwa majini ,akirudi salama anaweza kuwa mfalme, ” Mama Njoshi aliongea, huku Ngesha akiwa amepigwa na butwaa, amekosa nini afanye kwa wakati ule, kutokana na maneno aliyo yasikia kutoka kwa mama Njoshi.



    Njoshi akiwa shimoni, aliamua kutupilia mbali fikra zake za kutopanda juu kutoka nje ya shimo, na kukamata kamba ile na kisha kuanza kupanda juu, aweze kutoka ndani ya shimo.



    Njoshi akiwa anaelekea juu, kutoka ndani ya shimo. Alikutana uso kwa uso na viumbe wa ajabu, majini wa msituni, wakielekea shimoni kwa kutumia kamba waliyoifunga katika mti, na kisha kuidumbukiza shimoni, ili waweze kuingia ndani ya shimo na kumkamata adui aliyeuvamia msitu wao.



    “Hiiii! ……uwiiiih………wiiiii ……ihiiiii”,sauti nzito kama za awali zilitokea kwa mala nyingine tena, sauti ambazo zilisikika tena mbali zaidi ya msitu, na katika ardhi yote ya Mwamutapa .Maumivu ambayo majini waliyasikia hayakuwa ya kawaida, walipiga kelele sana kwani waliteketea baada ya kuingia ndani ya shimo kwa kutumia kamba na kisha kukutana na Njoshi, aliyekuwa akipanda juu kutoka ndani ya shimo kwa kutumia kamba hiyo hiyo.



    Njoshi alitumia panga lake la ajabu, panga lililokuwa na uwezo wa kuua majini,kuwateketeza viumbe wale, viumbe ambao nguvu zao ziliisha kabisa, pale tu panga lile litakapotumika kuwaua.



    “Kwishaa habari yenu, dawa yenu nimeshaifahamu “,Njoshi aliongea na kujiona mshindi baada ya kuteketeza majini zaidi ya kumi, huku akitumia mkono wake wa kulia ulioshika panga lile kupambana nao, na mkono wa kushoto akiwa ameshika kamba kwa nguvu asiweze kudondoka na kurudi shimoni.



    “Wote rudini msiingie ndani ya shimo, inaonekana adui kuna siraha hatari anazitumia, kwani haonekani kwa macho, na pia ana panga lenye uwezo wa kutuangamiza, tukizubaa tutakwisha, turudini kwenye ngome yetu, tukajipange “,Jini mweupe alizungumza na kuwataka askari wake wasitishe zoezi la kuingia shimoni, baada ya kuigundua siri iliyokuwa ikimlinda adui wao. Hayo ndiyo maneno yaliyosikika ya jini mweupe,kiongozi wa askari wa msituni, akiwa anaugulia maumivu makali mwilini mwake, maumivu ambayo hutokea pale tu jini mwenzao anapofariki, lakini maumivu yalikuwa makali tofauti na mwanzoni, majini waliokufa walikuwa ni zaidi ya kumi, maumivu ambayo hayakuwa ya kawaida.



    ********



    “Sijawahi kuumizwa kiasi hiki, adui huyu ni kiboko, lazima atalipia, “Malikia wa majini aliongea huku akiwa anaugulia maumivu,baada ya majini zaidi ya kumi kufa kwa wakati mmoja.Hayo yote yalitokea huku malikia akiwa ameketi kwenye kiti kirefu cha umalikia, kiti ambacho kilitengenezwa kwa miti na kupambwa na maua mazuri ya msituni



    “Karibuni askari wangu, na poleni sana, hapa inatakiwa tujipange upya, adui anamiliki panga, pamoja na mkanda, mali ambazo baba yake aliziiba katika msitu huu, miaka mingi iliyopita. Panga hilo linauwezo wa kutuua sisi, na pia mkanda mweusi wa kitambaa alionao, unamfanya asiweze kuonekana na kutuua kirahisi, hivyo basi inatakiwa tumsubili asogelee ngome yetu, na akitaka kuingia ndani, ataweza kuganda pale pale alipo, kwani nimenyunyizia maji ya ajabu ambayo yanauwezo wa kumgandisha binadamu yoyote atakapokanyaga maji hayo.Maji hayo nimeweka sehemu zote kuzunguka ngome hii, na hivyo basi tutaweza kumkamata kirahisi “,malikia aliongea baada ya jeshi lake likiongozwa na jini mweupe, kufika katika ngome yake, baada ya kupotea kimaajabu kutoka katika eneo ambalo walitega mtego wa shimo, shimo ambalo lilifanikiwa kumnasa adui, lakini walishindwa kumkamata zaidi ya kuambulia kupoteza wenzao, baada ya adui kuwaangamiza kwa kutumia panga la ajabu.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mwamutapa;



            Ikiwa tayali imefika mida kama ya saa kumi na moja, jua likiwa linaelekea kuzama ,Ngesha baada ya kumaliza maongezi marefu sana na mama yake Njoshi, mama ambaye aliamua kusitisha shughuli zake za kupalilia mahindi yake na kisha kuzungumza na rafiki yake mwanae. Wanaamua kurudi nyumbani wote kwa pamoja, kwani tayali jua lilikuwa linaelekea kuzama.



    Lakini wakiwa njiani, walisikia sauti nzito, sauti kama za awali, sauti zilizosababisha ardhi yote ya Mwamutapa kutikisika mithili ya tetemeko.



    “Aiweeeh mizimu ya mababu, endeleeni kumpigania Njoshi arudi salama, tayali anazidi kuwaangamiza majini wa msituni “,Ngesha aliongea huku akitabasamu kwani tayali alikuwa ameshaelewa zile sauti kutoka msituni zilimaanisha nini, sauti ambazo husikika majini wanapokufa, baada ya kuambiwa siri hiyo na mama yake Njoshi, kuhusu maana ya sauti hizo kutoka msituni.



    “Mmmh kawaua tena!, lakini asiwaue bila sababu, anachotakiwa kufanya atafute fimbo ya ufalme, na kisha arudi, panga alitumie kujilinda na sio kuua ovyo “,mama Njoshi aliongea huku akiwa hajafurahia kitendo kile cha Njoshi kuzidi kuua majini wa msituni, bila kutambua kuwa Njoshi hakuwa na jinsi, ilibidi awaue ili kujiokoa kutoka ndani ya mtego wa shimo uliomnasa bila kutegemea.



    Ikulu kwa mfalme



            Sauti za vilio zilipungua, watu wote wa Ngome ya mfalme walikua kimya sana huku wakiwa na hofu kutokana na sauti za kutisha zilizosikika toka asubuhi, sauti hizo zilizotokea katika msitu wa majini, msitu uliopatikana katika ardhi ya Mwamutapa, kiromita arobaini kutoka katika makazi ya watu.



    Kutokana na kutojua maana harisi ya sauti hizo, kwani mtabiri ambaye alikuwa ni bwana Nyangoma, ambaye angewaeleza kuhusu sauti hizo alikuwa tayali ameshafariki dunia. Lakini pia, wasingeweza kumuita mama yake Njoshi awaeleze maana ya sauti hizo, mama pekee ambaye alibakia mtabiri baada ya kurithi kwa mumewe, kwani waliogopa angeijua siri ya mfalme. Bila kutambua kuwa tayali mama Njoshi alifahamu kila kitu kuhusu mfalme. Hivyo basi, waliendelea kuwa na hofu huku mtoto wa mfalme Grace akilia na kujilaumu kumruhusu kipenzi wake Njoshi kuelekea msituni.



    Mwamutapa;



            kila familia katika nchi ya Mwamutapa, wanaingiwa na hofu kubwa, baada ya kusikia sauti za kutisha kutoka msituni,asubuhi siku ya jumanne. Sauti hizo waliziipuuzia mwanzoni. Lakini, sauti hizo zilisikika tena kwa mala nyingine jioni ya siku hiyo hiyo, na tena sauti hizo zilikua nzito na za kutisha  kupita zile zilizosikika kwa mala ya kwanza. Kelele hizo zilisababisha familia nyingi kujifungia majumbani mwao, huku giza likiwa hata bado halijaingia japokuwa jua lilikuwa tayali limezama kutokana na uoga waliokuwa nao, kwani walifahamu sauti hizo zilitokea katika msitu wa majini bila kutambua chanzo chake, wala maana yoyote kuhusu sauti hizo.



    Familia ya kina Ngesha ilikuwa moja ya familia zilizokuwa na hofu sana, kwani mama yake Ngesha alifunga milango yote na kisha kuketi sebuleni, katika nyumba yao ya udongo, na kisha kumsubili mwanae ambaye alikuwa hajarudi tangu alipoondoka asubuhi, na kumuaga mama yake kuwa ameenda kumtembelea rafiki yake Njoshi.



    Lakini mama yake Ngesha alipojaribu kumsubili mwanae ili waweze kuelekea shambani pamoja, alishangaa mwanae alipochelewa sana. Kitendo kilichomlazimu mama yake kwenda shambani peke yake, kwani aliamini Ngesha atamkuta shambani,mala tu atakaporudi kutoka kwa rafiki yake.



    Ama kweli, nani kama mama ?,kwani mama yake Ngesha alifanya shughuli za shambani mpaka mchana, lakini bila kutegemea, hakuweza kumwona mwanae akimfuata shambani. Hali hii ilimfanya mama yake Ngesha kuwa na hofu sana, na ukizingatia alikuwa tayali ameshazisikia sauti za kutisha asubuhi, mida kama ya saa nne. Hivyo basi, mama yake Ngesha alitambua kuwa siku hiyo ilikua tofauti sana na siku zingine, na haikuwa kawaida mwanae kuchelewa kiasi kile na kushindwa kumfata mama yake shambani, jambo ambalo lisingewezekana kwani Ngesha alipenda sana kumsaidia mama yake kazi za shambani.



    Hivyo basi, baada ya mama yake Ngesha kuwaza na kuwazua, aliamua kusitisha shughuli zake za shambani mapema sana, mida kama ya saa sita hivi na kisha kurudi nyumbani, aweze kujua usalama wa mwanae, chezea Mwamutapa wewe!, muda wowote kifo kinaweza kukutokea bila mungu kupenda.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Ama kweli siku ya kufa nyani miti yote huteleza, mama yake Ngesha alifika nyumbani kwake, lakini hakuweza kumkuta mwanae. Haraka sana wazo likamjia na kisha kufunga safari kuelekea nyumbani kwa kina Njoshi. Huko pia alipofika getini tu,komeo la mlango  liliweza kumkalibisha,komeo lililomaanisha hakukuepo na mtu yoyote nyumbani pale.



    Asikwambie mtu,mama yake Ngesha alichoka!,alipigwa na butwaa huku maswali mengi yakimsumbua kichwani,kwani hakujua mwanae yuko wapi.Alihisi labda atakuwa hatarini,tena katika hatari kubwa sana.Hatari ya kutekwa na askari wa  mfalme,na kwenda kutumikishwa kazi nzito,kazi ambazo watu wengi walikamatwa na kwenda kuzifanya bila kupumzika ,na bila malipo yoyote.Na pale ambapo mtu yeyote alipojaribu kufumbua kinywa chake,na kudai haki yake,bila huruma kifo ndio zawadi na tuzo pekee aliyolipwa kama malipo ya jasho lake,chezea mfalme wa Mwamutapa wewe!.



    Haya sasa,tuachane na hayo.Jua likiwa linaanza kufifia huku ndege wa angani wakiruka ruka angani,na kuipendezesha anga ya Mwamutapa.Mama yake Ngesha anaamua kurudi nyumbani baada ya kusimama kwa dakika kadhaa mbele ya geti la kina Njoshi, huku akiwa haamini kile alichokuwa anakiona.



    Ikiwa tayali mida ya jioni, akiwa anarudi Nyumbani,bila kufahamu ilikua ni saa ngapi, alisikia kelele nzito na za kutisha kutoka msituni ,kelele ambazo alizisikia kwa mala ya pili japokuwa kelele hizi zilitisha sana kuliko zile za awali, kwani zilisababisha mpaka ardhi kutetemeka. Lakini bila kupoteza muda, mama yake Ngesha aliamua kutimua mbio kuelekea nyumbani, mbio ambazo zilimfikisha nyumbani baada ya muda mfupi tu, kwani alitimua kama swala. Na mala baada ya kufika nyumbani, jambo la kwanza lilikuwa ni kufunga milango na madirisha ya nyumba yake, na kisha kuketi sebuleni kumsubili mwanae.



    Msituni;



         Njoshi akiwa ameshikilia kamba yake kwa mkono wa kushoto, ghafla alishangaa majini wale wakipotea. Aliamua kutoka haraka sana shimoni, huku akiwa amelowa na mwili wake kutoa harufu mbaya, harufu ambayo ilisababishwa na maji machafu ya shimoni, maji ambayo yalichanganyikana na viumbe wengi wakiwa wamekufa na kuoza ndani yake.



    “Mmmh wamekimbia?, au wamenitega tena? “,Njoshi aliongea baada ya kutoka ndani ya shimo na kushangaa kutokuta kiumbe yoyote yule, kitendo ambacho kilimtahadharisha aweze kuwa makini, kwani alifikili labda atakuwa amebadilishiwa mtego, aweze kunaswa kirahisi ,jambo ambalo lilimfanya aweze kuwa makini na asiweze kunaswa kwa mala nyingine tena.



    “Hapa ngoja nisonge mbele, na giza tayali limeshaingia, inatakiwa nifike katika ngome ya malikia haraka sana, niweze kuiba fimbo ya kifalme na kuiandika jina langu, harafu nikachonge jeneza la ajabu kisha kesho asubuhi na mapema nirudi nyumbani “,Njoshi aliongea huku akianza kutimua mbio na kuelekea katika ngome ya malikia, kwa kutumia njia ile ile iliyokuwa imetegwa shimo na kufunikwa na udongo juu yake. Bila kutambua kuwa tayali kulikuwa na mtego mbele yake, mtego ambao ulikuwa katika ngome ya malikia, ngome ambayo ilihafadhi madini ya kila aina pamoja na vitu mbalimbali ikiwemo fimbo ya kifalme. Fimbo ambayo mtu anayetaka kuongoza Mwamutapa lazima aimiliki, na kuandika jina lake, na hiyo ndio itakua tiketi ya kuongoza nchi ya Mwamutapa.



    Njoshi alizidi kusonga mbele huku akipanga mipango ya namna ya kufanikisha kutengeneza jeneza la ajabu haraka sana ili aweze kurudi nyumbani siku ya jumatano asubuhi, siku ambayo ilikuwa ya mwisho kukaa msituni, kwani mfalme alitakiwa azikwe ndani ya siku tatu   baada ya kufa, na kama angezikwa katika jeneza la ajabu nje ya siku hizi tatu, au angezikwa huku wananchi wa Mwamutapa wakiwa wamefahamu kuwa amekufa, mfalme hatoweza kufufuka kwani inatakiwa iwe siri.



    Njoshi baada ya kukimbia ndani ya muda mchache tu ,kwa umbali kama wa mita mia moja aliweza kuiona ngome ya malikia, ngome ambayo ilizungushiwa nyasi na kisha kupambwa na maua mazuri sana, maua ambayo yalikuwa na harufu nzuri na kuwavutia ndege wengi pamoja na wadudu kuruka ruka katika ngome hiyo kufuata maua.



    “Adui hayuko mbali, muda sio mrefu tutamtia nguvuni, yani atajuta kuingia katika ngome na msitu huu “,Malikia alizidi kuongea kauli za laana, kauli ambazo baadae zitamgharimu kwani ilikua ni mala ya pili akitamka kauli mbaya na za visasi kwa Njoshi



    Hii ilikuwa ni kama miiko, kauli ambayo anaitamka malikia lazima aitimize, bila hivyo watu wake wataweza kufa ghafla,na  kisha ngome yake itateketea. Jambo ambalo baadae linaweza kutokea, kwani malikia alishindwa kumwadhimbu Njoshi na kulipiza kisasi ili atimize kile alichokuwa akikisema, na kuepusha balaa kwa watu wake.



    “Aiw…eeeh mizimu wa babu zangu, niepu…sheni na bal…aa h…ili “,Njoshi aliomba mizimu iweze kumsaidia kwani bila kutegemea, alishindwa kutoka mahali alipo, wala kujitikisa , baada ya kukanyaga maji ya ajabu, maji ambayo malikia alinyunyizia kuzunguka ngome yake, pale tu Njoshi alipotaka kuingia ndani, katika ngome hatari ya malikia wa majini wa msituni.



    “Aiweeh mtukufu Gutamanya, mkuu wa majini wote ulimwenguni, tayali nimemtia mikononi mwangu adui yangu”,malikia wa majini,msichana aliyekuwa mrembo sana,aliongea huku akiwaongoza majini wote kuelekea getini ,kwenda kumtazama adui wao na kumtambua,kwani maji yale yalikuwa na nguvu sana kiasi kwamba Njoshi aliweza kuonekana machoni kwa majini,bila kusaidiwa na  kitambaa alichokivaa kiunoni.



    Mwamutapa;



            Ngesha na mama yake Njoshi walishangaa kukuta kila nyumba ikiwa kimya huku milango na madirisha yakiwa yamefungwa baada ya kutoka shambani. Haikuwa kawaida mji kuwa kimya kiasi kile muda wa saa moja jioni, hali hii ilimfanya Ngesha kumuaga mama yake Njoshi na kisha haraka sana akaelekea nyumbani kwao, ili aweze kujua usalama wa mama yake.



    Akiwa katika hali ya mshangao, alishangaa mama yake akimkimbilia na kisha kumkumbatia huku akilia, baada ya kufungua mlango na kukuta mama yake akiwa ameketi sebulini akimsubili.



    “Uko salama mwanangu, nilikuwa na hofu sana juu yako “,mama yake Ngesha aliongea maneno mazito yenye upendo ndani yake, maneno yaliyomfanya hata Ngesha aweze kutokwa na machozi, kwani alijiona mwenye makosa makubwa kumfanya mama yake awe na hofu juu ya usalama wake, kwani aliondoka tangu asubuhi bila kurudi nyumbani mapema.





    Msitu wa majini;



    Giza likiwa tayali  limeshaingia, hali ya ukimya iliweza kutawala sana katika msitu. Kwani viumbe wengi wa msituni walikuwa tayali wamejipumzisha, isipokuwa katika ngome ya malikia, kwani ndege pamoja na wadudu waliendelea kuruka ruka na kuimba nyimbo nzuri sana, wakifurahia uwepo wa maua yale ya kupendeza katika ngome ya malikia. Nyuki nao hawakutaka kuwa nyuma, waliendelea kuruka katika maua yale, na kisha kufyonza maji yake ili wakapate kujitengenezea asali.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Ndugu msomaji,kijana hodari Njoshi akiwa amesimama  kama sanamu,tena kama sanamu lile la kariakoo, katika duka la nguo la muhindi baada ya kukanyaga maji ya ajabu bila kujitambua. Aliendelea kuzungusha macho yake huku na kule, akitazama maua yale ya kupendeza.Huku harufu nzuri ya maua ikipenya katika matundu yake mawili ya pua yake, na pia sauti nzuri za ndege zikisikika katika masikio yake na kumfariji Njoshi. Bila kujitambua alijikuta akisahau machungu yote ya msituni na kujikuta akitabasamu, kwani ndege wale walimfurahisha sana.



    “Aiweeeh mtukufu Gutamanya, kumbe ni wewe kijana, adui wetu wa msituni, kijana mzuri kiasi hiki, kwa nini umewaua ndugu zetu “,ghafla sauti nzuri na nyororo ilisikika na kumshitua Njoshi, kwani mawazo yake yalikuwa mbali sana, tena katika dunia nyingine wakati akiwatazama ndege wazuri katika ngome ya malikia na kusababisha ajisahau kuwa alikuwa katika hatari. Sauti hii nyororo iliyosikika, haikuwa nyingine bali ilikuwa ni sauti ya malikia. Baada ya kufika katika geti la ngome yake, na kumkuta Njoshi akiwa amesimama huku akiwa kashikilia panga lake, panga ambalo asingeweza kulitumia tena, kwani tayali alikuwa hawezi kutoka mahali alipo.



    Malikia alitokea kumpenda Njoshi mala baada ya kuitazama sura yake, kwani alikuwa ni kijana mzuri sana huku weupe aliokuwa nao ukimpendezesha zaidi na zaidi. Malikia akiwa anatazama kifua cha Njoshi, kifua ambacho kilionekana kuwa cha mazoezi na kusababisha sehemu za tumbo lake kujikata kama pingili, malikia alijikuta hasira alizokuwa nazo zikimtoka na kisha kumuulza Njoshi maswali, tena kwa upole hali ambayo iliwashangaza majini wengine akiwemo jini mweupe aliyekuwa amesimama nyuma ya malikia, na kufuatiwa na kundi kubwa la majini waliokuwa wamebeba siraha za kila aina, ikiwemo mishale pamoja na mikuki ya ajabu.Mishale hii pamoja na mikuki ilikuwa ni tofauti na ile ya binadamu, kwani ilikuwa na uwezo wa kumpiga adui na kumgeuza kuwa kiumbe yoyote yule kama walivyotaka, unaweza kugeuzwa nyoka au hata ndege na kisha kukamatwa na kukufungiwa katika banda lao dogo walilolitumia kwa ajili ya kuwafungia binadamu wote waliouvamia msitu na kisha kuwapatia mateso makali.



    “Aiweeeh malikia wa msituni, sikukusudia kuwaua ndugu zako, niuwie radhi malikia ” ,Njoshi alijitetea huku mmoja wa majini akimnyanganya Njoshi panga pamoja na kumvua kitambaa cheusi alichokivaa kiunoni. Baada ya kumnyanganya vitu hivyo, hakuwa na siraha yoyote ile ya kumlinda kwani walikagua begi lake jeusi alilolivaa mgongoni na  hawakukuta kitu chochote, kwani begi hilo lilitumika tu kuhifadhia panga pamoja na kitambaa kile cheusi.



    Baada ya kuamini kuwa Njoshi asingeweza kuwadhuru. Malikia alimzunguka Njoshi mala tano, huku akitamka maneno ya ajabu, maneno ambayo mimi na wewe hatujui, kwani viumbe wale walizungumza kila lugha waliyoitaka wao, kwani hawakuwa binadamu bali majini, viumbe hatari sana.



    “Ihiii………iwii……hii……”,malikia alizidi kutamka maneno ambayo waliyatumia kupiga kelele pale walipokuwa wana hasira na kuugulia maumivu, kipindi ambacho ndugu zao wameuawa huku akizidi kumzunguka Njoshi, na alipomaliza mzunguko wa tano Njoshi aliweza kuzinduka



    “Umefuata nini katika msitu huu, ewe mtoto wa Nyangoma “,malikia aliongea huku moyo wake ukiwa tayali umempenda Njoshi kimapenzi, na kujuta maneno ya laana ambayo tayali alitakiwa ayakimilishe, jambo ambalo lilianza kuwa ngumu kwani tayali alikuwa ameshampenda Njoshi mala baada ya kuiona sura yake.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nimefuata utajiri, “,Njoshi akiwa anajalibu kujinyosha huku akitupa mikono yake huku na kule akiwa haamini kama kweli ametoka katika mtego ule, mtego ambao ulimfanya asimame kama sanamu bila kutikisika. Aliweza kujibu swali la malikia na kumdanganya kwani msituni alifuata jeneza la ajabu pamoja na fimbo ya kifalme na wala sio utajiri.



    Msema ukweli ni mpenzi wa mungu, na pia ukweli siku zote utakuweka huru. Malikia pamoja na majini wote walikasirika sana kwani walichukia uongo kuliko kitu chochote kile, bola uwaue kuliko kuwadanganya.







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog