Search This Blog

SITAISAHAU TANGA - 2

 

    Simulizi : Sitasahau Tanga

    Sehemu Ya Pili (2)





    Nikabaki nimeduwaa tu na macho yamenitoka hata nisijue cha kufanya kwa wakati ule. Nikaamua kuinuka pale kitandani na kujinyoosha nyoosha ila cha kunishangaza sikuwa na njaa kabisa.

    Nikawa nimesimama huku nikitafakari yale majanga, mara simu yangu ikaita,

    RAFIKI: Vipi wewe mbona umenikatia simu bhana?

    MIMI: Hapana sijakata, imejikata yenyewe.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    RAFIKI: Halafu wewe naona akili yako imepinda. Haya vipi itakuwaje, nikupitie kesho asubuhi?

    MIMI: (nikiwa bado sijiamini amini kama siku imeisha kweli), aaah eeh haya poa basi.

    RAFIKI: Mbona hueleweki unajiumauma tu, au hutaki? Niambie bhana.

    MIMI: Hapana sio kama sitaki.

    RAFIKI: Ila nini sasa? Ongea bhana mtoto wa kiume acha kujiumauma hapo.

    MIMI: Aah sijui bhana

    Nikajikuta nimekata ile simu, hata nilikuwa sijielewi kabisa. Mara dada akawa anapiga

    DADA: Yani mdogo wangu siku hizi kweli umekuwa shetani, toka asubuhi hadi muda huu unashindwa hata kutujulia hali? Yaonyesha umefurahishwa sana na yaliyo mpata mwenzio.

    MIMI: Samahani dada, naomba mnisamehe sana sio kusudio langu.

    DADA: Ila ni kusudio la nani?

    MIMI: Sijui dada.

    DADA: Hivi wewe una kichaa au?

    Nikakata simu kwani naona wananichanganya tu na wakati sijielewi kabisa.

    Nikakaa chini na kujiinamia huku nikipanga mipango kuwa niondoke mahali hapo hata nikalale nje ili nisipitilize tena. Mara simu ikaita,

    BINTI: Mambo mpenzi, nimekumiss.

    MIMI: (hapo natamani hata kumtukana), poa tu hata nami nimekumiss pia.

    BINTI: Unaonaje leo twende tukatembee mpenzi?

    MIMI: (huku nimejawa na hasira), unajua usinichanganye wewe! Tukatembee vipi wakati tuko mbali mbali?

    BINTI: Ndio unanikaripia eeh!

    MIMI: (Nikawa mpole tena), hapana mpenzi nisamehe.

    BINTI: Sijazoea kukaripiwa, umeniudhi sana.

    Akakata simu, dah nikapagawa zaidi. Nikainuka tena na kwenda hadi mlangoni ili nifungue mlango nitoke. Mara simu ikaita,

    BINTI: Unaenda wapi?

    MIMI: Aaaah eeeh mmh!

    BINTI: Unakwenda wapi?

    MIMI: Aah maswali gani tena hayo?

    BINTI: Wewe kiburi eeh!

    MIMI: (nikiwa na hasira na mimi), niache bhana nikapunge upepo nje.

    BINTI: Kumbe wewe ni kiburi na jeuri!!

    MIMI: Ndio mambo gani hayo jamani mpenzi?

    Akakata simu, nikiwa bado nimesimama pale mlangoni akanitumia sms

    "huendi popote"

    Nikajikuta nikiwaza mambo mengi, mara dada akaanza kupiga tena.

    DADA: Vipi na leo unakuja au huji?

    MIMI: Aaah daah sijui bhana.

    DADA: Hivi mdogo wangu una nini wewe?

    MIMI: Sielewi kitu dada.

    DADA: Uko wapi sasa hivi?

    Ile nataka kumjibu simu ikakatika, kuichek eti imeisha chaji nikaamua kwenda kuichomeka kwenye chaji, huku mawazo mengi kichwani yakiwa yamenitawala. Nilipokaa kidogo nikaiwasha tena na hapo nikakutana na sms kutoka kwa binti wa kitanga,

    "nimekwambia leo huendi popote, utakula jeuri yako"

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilikosa raha kwakweli nikatamani hata nipae niondokane na hayo majanga. Nikajiuliza kuwa huyu binti ana mamlaka gani ya kunizuia mimi nisitoke? Nikajipa moyo na kujipigapiga kifuani huku nikisema, mimi kidume bhana nitatoka tu. Mara akanipigia simu tena, nikaitoa pale kwenye chaji na kupokea.

    BINTI: Unasemaje mpenzi?

    MIMI: Mbona sijasema chochote.

    BINTI: (Akacheka sana halafu akakata simu).

    Nikaamua kuirudisha simu kwenye chaji, huku kichwa changu kikiwa kama kimevurugika.

    Nikainuka na kwenda kufungua mlango ila ukawa mgumu kufunguka, nikasikia mlio wa sms nikarudi kuisoma,

    "hivi nilivyokwambia kuwa leo huendi popote ulijua masikhara?"

    Nikaiangalia ile sms mara tatu tatu, nikaona huyu mwanamke anacheza na akili yangu sasa. Nikiwa nimejawa hasira nikachukua simu na kumpigia ila haikupokelewa, nikapiga tena haikupokelewa na tangu nimerudi Dar huyu binti amekuwa na kawaida ya kutokupokea simu zangu. Nikachukia sana, hasira zikanizidi. Nikainuka tena kwa hasira nikaenda mlangoni na kuusukuma mlango lakini haukufunguka. Nikawa nimepatwa na joto la hasira huku jasho jingi likinitoka, nikarudi na kukaa kitandani mara sms ikaingia kwenye simu,

    "pole kwa joto mpenzi"

    Nikazidi kupandwa na hasira hata nisijue cha kufanya, nikachukua tena simu ili nimpigie rafiki yangu kabla sijapiga simu yangu ikaanza kuita.

    BINTI: Unataka kumpigia nani?

    MIMI: Nimekupigia simu hujapokea ila nikitaka kumpigia mtu ndio unajua?

    BINTI: Nijibu kwanza unataka kumpigia nani?

    MIMI: Rafiki yangu tu.

    BINTI: Ulitaka kumwambia nini?

    MIMI: (Nikiwa na hasira), unajua nimechoshwa na maswali yako?

    BINTI: Umechoshwa na maswali sasa ulipokuwa unanipigia ulitaka nini?

    Akakata simu, dah huyu binti nilitamani hata kumtukana matusi yote ya dunia.

    Njaa ikanianza, nikawa nawaza sasa nitatoka vipi kwenda kununua chakula. Simu ikaita,

    BINTI: Vipi una njaa eeh!!

    MIMI: (Hapo natamani kumtukana), unauliza majibu?

    BINTI: Kwahiyo unatakaje?

    MIMI: Nataka kwenda nje kununua chakula.

    BINTI: Leo hutoki ila chakula nitakuletea.

    MIMI: Dah!! Kwanini unanifanyia hivyo lakini?

    Akakata simu, nikawa ni mtu mwenye mawazo. Nikainuka tena na kwenda kufungua mlango bado ulikuwa mgumu, mara dada nae akaanza kupiga simu

    DADA: Uko wapi lakini? Si ulisema utakuja leo yani huwezi amini mwenzio kazidiwa vibaya sana huku.

    MIMI: (nikajikuta naropoka tu), Sasa jamani dada, kwani mi ndio daktari?

    DADA: Unasemaje wewe?

    MIMI: Aah samahani dada ulimi umeteleza.

    DADA: Endelea na hiyo tabia yako tu.

    Akakata simu. Nikawaza sana kuwa imekuwaje hadi nimemjibu dada vile. Mara sms ikaingia

    "umemjibu vizuri sasa dada yako, hongera mpenzi"

    Aah nikazidi kupatwa na hasira, mara akanipigia simu

    BINTI: Nikuletee chakula gani leo mpenzi wangu?

    MIMI: Niletee chakula kizuri cha kushiba.

    BINTI: Haya usijari, nitakuletea mpenzi.

    Akakata simu nikashangaa imekuwaje hata nikamjibu vizuri vile wakati nina hasira nae.

    Nikawa bado na mawazo nikaona sms kwenye simu,

    "angalia mezani mpenzi"

    kuangalia, dah kaniwekea vyakula vya kila aina, kutokana na njaa yangu uroho ukanijaa. Nikasogea pale mezani na kuanza kula, nilipomaliza akanipigia simu.

    BINTI: Hata kunikaribisha mpenzi?

    MIMI: Aah mmh nilisahau mpenzi, samahani.

    BINTI: Usijari sana, vipi umeridhika nacho lakini?

    MIMI: Ndio nimeridhika mpenzi, ila umekiletaje?

    BINTI: Nimekileta kwa hisia mpenzi, vipi unataka kuoga?

    MIMI: Ndio nataka kuoga mpenzi.

    BINTI: Haya ngoja kidogo mpenzi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Akakata simu, Nikawa kama mtu aliyepigwa bumbuwazi nilikuwa nikingoja huko kuoga kwa hisia nako kutakuwaje.





    Nikawaza pale ndani huku nikingoja huko kuoga kwa hisia.

    Mara akanipigia simu,

    BINTI: Mpenzi upo tayari kuoga?

    MIMI: Ndio mpenzi nipo tayari.

    BINTI: Haya vua nguo zako zote.

    Akakata simu, hofu kubwa ikanitanda moyoni nikawaza kama nivue kweli nguo au la, nikiwa bado naendelea kuwaza akanitumia sms "vua basi ukaoge mpenzi"

    Bado nikawa nawaza tu, akanipigia simu

    BINTI: Kwani unaogopa nini mpenzi?

    MIMI: Hapana siogopi kitu ila naomba kesho ndio nioge kwa hisia mpenzi.

    BINTI: (Akacheka sana), kwanini umeghairi mpenzi?

    MIMI: Hapana mpenzi ila sijajisikia kuoga usiku huu.

    BINTI: Haya usijari mpenzi.

    Akakata simu, nikawa nimekaa huku nikipanga mipango ya kesho tu kwenye kichwa changu.

    Nikiwa ndani ya mawazo rafiki yangu akinipigia tena simu,

    RAFIKI: Kesho nitakuja kukufata hapo kaka twende ile sehemu.

    MIMI: Poa kaka.

    Alipokata tu simu nyingine ikaingia

    BINTI: Mwambie huyo rafiki yako aache kabisa kujihusisha na mambo haya atapotea.

    MIMI: Mbona sikuelewi?

    Akakata simu, nikazidi kupagawa kwa mawazo hata nisijue cha kufanya kwa wakati huo. Mara taa ya chumbani kwangu ikazimwa kukawa na giza na utulivu uliopitiliza, nikaanza kuogopa huku nikitamani kupiga kelele lakini nikashindwa kufanya hivyo nilikiona chumba kikiwa kikubwa sana, jasho la uwoga likaanza kunitoka nililowa mwili mzima kama nimemwagiwa maji. Mara taa ikawashwa tena na simu ikaanza kuita,

    BINTI: Kumbe wewe ni muoga sana eeh!

    MIMI: Aaah mmh kiasi tu sio sana.

    BINTI: Kukuzimia taa tu jasho limekutoka kama unakimbizwa, nikikufanyia mengine je?

    MIMI: hapana usinifanyie vibaya mpenzi.

    Akakata simu na kupiga tena,

    BINTI: Ooh mpenzi nimesahau, je utapenda tukatembee leo?

    MIMI: Aah hapana mpenzi, tutaenda siku nyingine.

    BINTI: Kwanini jamani mpenzi?http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MIMI: Hamna sababu mpenzi ila tutaenda siku nyingine. Naomba kesho uniamshe mpenzi.

    BINTI: Sawa usijari, umekuwa muelewa sasa mpenzi nimefurahi. Ila nakuomba tukatembee.

    Akakata simu ilinibidi niwe mpole na nijifanye kuwa nafurahia vyote anavyonifanyia huku akili yangu kichwani ikiwaza mambo mbali mbali ikiwemo namna ya kumuepuka binti huyo.

    Nilikuwa nikijigeuza geuza tu pale kitandani huku mawazo mengi yakinitawala.

    Mara simu yangu ikaita,

    BINTI: Mpenzi leo hulali?

    MIMI: Nitalala tu mpenzi si utanishushia neti?

    BINTI: Dah nafurahi umenikubali mpenzi, nitakushushia usijari.

    Akakata simu, nami nikajilaza pale kitandani. Nikaota ndoto kuwa nipo sehemu nzuri sana na yule binti.

    Asubuhi kulipokucha, yeye akawa wa kwanza kunipigia simu. Nikaamka na kwenda kuoga nikarudi na kujiandaa ili nitoke, mara dada akaanza kunipigia,

    DADA: Mdogo wangu tafadhari tunahitaji pesa kidogo kwaajili ya kuongezea kulipia hospital na vitu vingine.

    MIMI: Hakuna shida dada, kwani mnataka kiasi gani?

    DADA: Ungetuma kama elfu thelathini hivi.

    MIMI: Sawa natuma sasa hivi kwa njia ya simu.

    Nikakata simu na kuanza kutuma pesa, nikafata muamala mzima ila badae naletewa sms kuwa salio halitoshi kuhamisha kiasi cha pesa ninachotaka.

    Nikaamua kuangalia salio duh nikakuta eti imebaki mia tano. Nikajisemea 'hata sikubali hawa wendawazimu washaniibia hela yangu kwenye simu yani laki mbili na nusu imebaki mia tano sikubali lazima niwafatie huko makao makuu'http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    nilikuwa naongea kwa jazba huku nikiangalia lile salio mara mbili mbili bila hata ya kuamini kama hela yangu imekatwa na mtandao kama kawaida ya wizi wao au ni vipi.

    Nikaanza kutoka ndani nikiwa na jazba za mtandao ule, mara akanipigia simu

    BINTI: Mbona una hasira sana mpenzi?

    MIMI: Si hawa wapumbavu wa mtandao wameniibia pesa yangu.

    BINTI: Hawajakuibia bhana.

    MIMI: Kama hawajaniibia pesa yangu yote imekwenda wapi?

    BINTI: Ngoja nitakwambia.

    Akakata simu, nikiwa bado nimesimama pale mlangoni huku nina uchungu na hasira ya pesa yangu, mara akanitumia sms

    "mpenzi, ulivyoshinda ndani jana na juzi ulifikiri unahudumiwa kwa pesa ya nani? Na tulipoenda kutembea usiku je? Pesa yako imetumika kwenye kukuhudumia kwahiyo usilaumu mtandao, hiyo pesa umeitumia mwenyewe"







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog