Sehemu Ya Nne (4)
"Saimon usinitenge unajua jinsi gani nakupenda, muda mrefu tupo wote sijawahi kukudhuru lakini mimi si mbaya kwako"
Nilijaribu kumueleza nikamsogelea, aliniogopa sana akakataa kulala namimi iliniuma sana ilikuwa usiku tayari sikuwa na jinsi kuondoka nyumbani kwake sababu aliniogopa namimi sikutaka kumdhuru, nililia sana Saimon anihurumie lakini alikataa nakusema awezi kuishi na jini, sikutaka kuladhimisha uwezo wakumdhuru ninao lakini nilimpenda nikaondoka kwa amani tu.
Nilifika baharini nakukaa usiku ule uchungu ulinishika nikajifungua nakukubeba adi kwenye nyumba moja kwa mama Samuel nikakuacha apo nje nakukuvalisha kidani chenye jina Skola alilipenda sana Saimon ilo jina akasema akiwa wa kike atakuita ivyo.
Tangu siku iyo sijui habari zake sijawahi kumfatilia wala kumuona ila nitakuelekeza wapi anaishi utaenda kumtafuta"
Alimaliza kusimulia Meyan uku machozi yakimtoka Skola pia alikuwa analia kwa babayake kumkataa mamayake,
"Nipeleke sasa mama natamani kumuona"
Alisema Skola lakini Meyan akamkatalia
"Kesho utaenda subiri kukuche"
Ilikuwa bado Usiku.
Meyan akaondoka nakumuacha Skola alale. Asubuh kulifika aliwahi kuamka akajiandaa nakuelekea shuleni alipomaliza tu masomo muda wakuondoka hakurudi nyumbani akaenda adi alipoelekezwa na mamayake anapoishi Saimon, akafika na kuiona iyo nyumba akaisogelea nakuanza kugonga kengere.
Skola alisogea adi kwenye iyo nyumba nakupiga kengere, Mara geti likafunguliwa na mlinzi akatoka.
"Shikamoo"
Alisalimia Skola
"Marahaba mtoto mzuri, karibu"
Alisema mlinzi uku akimtathimini Skola, japokuwa kavaa nguo za shule, lakini umbo lake halikujificha, bado aliuonyesha uumbaji wa mungu, mwanaume yeyote akimuona lazima amtamani avutiwe kumuangalia zaidi.
"Asante, namuulizia babayangu"
Alisema Skola, nakumfanya mlinzi ashtuke!
"Babayako anakaa humu? Anaitwa nani kwani?"
Aliuliza maswali mfululizo.
"Anaitwa Saimoni"
Alijibu nakumfanya mlinzi atoe macho adi kumtisha Skola
"Yesuuuu! Yani boss Saimon anamtoto mrembo ivi uwiiii, nitakuwa mkwe wake wallah ebu njoo ingia ndani mama tumsubiri babamkwe, ngoja nimpigie simu nimwambie umekuja yani amenificha miaka yote ajasema au alikutelekeza? Ivi mama yako nae ni mzuri kama wewe! Kwanza unaitwa nani?"
Mlinzi alipagawa maneno mengi yakamtoka bila kujielewa.
"Naitwa Skola"
"Jina lako zuri kama wewe mwenyewe"
Alisema akatoa simu yake nakupiga, muda huo Skola aliingia ndani nakukaa kwenye kiti akiangalia iyo nyumba ni kubwa nzuri ya kifahari, alitamani sana babayake aje amuone, aliomba asijekumkataa tu.
Mlinzi akaanza kuongea na simu
"Haloo eeh mwanao amekuja apa anaitwa Skola ...ndio njoo utamkuta"
Basi akamaliza nakumwangalia Skola
"Umekula we mtoto?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hakuwa mkubwa Skola kidato cha pili alikuwa ni miaka kumi na tano ata sura yake yakitoto kabisa umbo kubwa ndo lilimbeba nakuwasumbua wanaume wamuonapo.
"Tayari nimekula"
"Sawa baba anakuja sasa ivi"
Alimwambia nakumfanya atabasamu dimpoz zake zikaonekana
"Heee unadimpoz pia? Mbona umenimaliza wewe mtoto"
Alisema mlinzi nakumfanya Skola acheke alimuona anavituko sana.
Baada ya muda mfupi honi ya gari ikalia nje mlinzi akafungua geti nakuruhusu ilo gari liingie.
Alishuka mwanaume si mtu mzima, ni kijana wa kawaida tu ata miaka Arobaini ajafikisha anavyoonekana.
Alimsogelea Skola alipomuona akuuliza alimkumbatia sana uku akiwa haamini kama amemuona mtoto wake ambae alifanana kilakitu na mamayake,
"Skola mwanangu nisamehe"
Alisema uku machozi yanamtoka akamshika mkono nakuingia nae ndani.
"Baba kwanini ulimfukuza mama?"
Aliuliza Skola akilia.
"Nisamehe mwanangu sikupenda iwe vile ila nilijuta sana kumpoteza Meyan,. Nilitamani nimuone nimuombe msamaha lakini sikujua nitampata wapi miaka yote iyo nimeishi bila mwanamke nikijua ipo siku nitaonana nae tena"
Alisema Saimon nakuonekana kweli anajuta kwa alichokifanya.
Skola alimuelewa akamwambia amemsamehe ata mamayake pia kamsamehe, baada ya apo Saimon akamuomba binti yake asiondoke waishi pamoja.
Skola alifurahi sana akakubali nakuanza kuishi apo.
"Ila itabidi nitafute msichana wa kazi aweze kutusaidia apa"
Alisema Saimon na baada ya siku chache akaletwa msichana aitwae Hilda akaanza kazi.
Asubuhi wanatoka pamoja Saimon anampeleka shule binti yake nayeye anaenda kazini.
Jose ni yule mlinzi ambae ni rafiki mkubwa wa Skola kutokana na vituko vyake, Skola anamzoea nakukaa wakipiga Story sana, anapenda kumchekesha nakumfanya muda wote afurahi tu.
Jose ni kijana wamiaka ishirini na tano ambae alikimbia kijinini kwao kutokana na chuki za familia walimtenga sababu wazazi wake wote walifariki, akabakia akikaa na ndugu ambao walimuona hana faida kwao walimnyanyasa. Nakumsimanga mwisho akaamua kuondoka nakukimbilia mjini, bahati nzuri alikutana na Saimon akamueleza matatizo yake alimuelewa nakuamua kumsaidia akamuomba awe mlinzi wa nyumba yake lakini alikuwa na chumba chake ndani alimfanya kama ndugu yake wanaishi pamoja.
Hakuwa yule mlinzi wakukaa getini muda wote na marungu sijui yeye alikuwa handsome msafi kila muda akisaidia kazi ndogo ndogo ndani ya nyumba nakumfungulia geti Saimon alimuita boss sababu alikuwa analipwa pesa kwa kumlindia nyumba yake.
****
Siku zilizidi kusonga, Skola alizoea maisha ya kuishi na babayake.
Alienda kwa mama Samuel nakuwaaga ambapo walimkubalia ila wakamuomba asiwasahau kwenda kuwatembelea.
Hatimae wakaanza mitihani shule yakumaliza kidato cha pili, alikuwa bize kusoma uku maswali asiyojua babayake akimsaidia.
Hatimae alimaliza salama nakubaki nyumbani sasa.
Muda mwingi alikuwa yupo na Jose walijenga ukaribu mkubwa kiasi kwamba bila Jose hawezi kula chakula.
Ilo likamuogopesha sana babayake ikabidi awaite nakuwauliza kuna nini kati yao
"Hamna kitu baba nimemzoea tu"
Alijitetea Skola
"Kweli bro hamna kitu tuamini"
Jose nae akasema, hakutaka kuwabana akawaacha huru.
Yule msichana wa kazi akaanza tabia mbaya kumrembulia macho Saimon akiongea nae mara avae nguo fupi
"We Hilda ndo mavazi gani hayo unavaa?"
Skola alimuuliza siku moja alivaa kigauni kifupi sana.
"Wewe mtoto koma usinizoee"
Alijibu mara akaja Jose
"Mamaaa weee Hilda una laana eeh?"
Alishangaa kumuona mwenyewe hakujali ndo kwanza aliwaacha nakuingia jikoni.
"Kwani uyu anamatatizo gani?"
Waliulizana
"Anamapepo sio bure ila ngoja nitaongea na baba"
Alisema Skola.
Usiku ulipofika wakamueleza Saimon ambae alimuita Hilda nakumkanya avae nguo za kujistiri.
Alikubali akaitikia lakini bado hakubadirika aliendelea kuvaa vibaya wakaona wamuache tu.
***
Hatimae shule zikafunguliwa Skola akawa bize kusoma adi pale alipomaliza elimu yake majibu yalitoka alifauru akaendelea elimu za juu mwisho akaingia chuo sasa Mliman city.
Akiwa anasoma akaomba babayake Jose awe dereva wake akimpeleka shule na nyumbani akatafuta mlinzi wakulinda nyumba.
Kipindi yupo chuo baba yake akasafiri kikazi majukumu yote akakumuachia Jose ambae alikuwa ndo baba kwa Skola waliheshimiana sana.
Siku moja akamuomba waende sinema akitoka chuo Skola akakubali aliingia masomo yajioni adi saa kumi na mbili alimaliza, Jose alikuwepo akimngojea walipotoka tu wakaingia sinema ni saa moja inaanza.
Siku iyo ilikuwa love story picha wanayotizama, ilileta msisimko mkubwa kwa wengi walioangalia alafu kila mtu alikuwa na mpenzi wake humo ndani, bila kutarajia Jose na Skola wakasogeleana nakukaa kama wapenzi picha ilihamsha hisia za wengi ata Skola hakuweza kuvumilia akajikuta anaegamia kifuani kwa Jose ambae alipitisha mkono wake kwa nyuma nakumshika kiuno chake, waliangalia adi mwisho wakaimaliza nakuondoka kurudi nyumbani ambapo kwa mara ya kwanza walilala pamoja na wakashiriki tendo, Jose alifanikiwa kutoa usichana wa Skola siku iyo mapenzi yakachanua juu yao, baada ya mwezi kupita Saimon alirudi safari nakushangaa aliyoyaona nyumbani kwake.
Dalili zote zilionyesha Jose na Skola ni wapenzi, hakutaka kunyamaza akaamua awaulize ambapo walikubali nakumueleza wanampango wakufunga ndoa!
"Jose unauhakika utamuoa Skola?"
Aliuliza Bwana Saimonhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Ndio nitamuoa"
Alikubali
"Sawa hamna shida ila nataka ujipange kuna kazi nakutafutia itakayokulipa vizuri ujiendeleze kimaisha alafu si unakiwanja wewe anza ujenzi sasa mkishafunga ndoa nyumba iwe tayari mkaishi uko"
Alimwambia akakubali kilichobaki ni kutimiza tu.
Skola alifurahi sana kuona babayake amekubali aolewe na Jose.
Kesho yake ilifika akapelekwa kwenye kampuni inayohusika na usafirishaji bidhaa sehemu mbali mbali Tanzania.
Akaanza kazi yake rasmi nakuwa bize atakukutana na Skola ilikuwa mara moja moja sana, Skola alikuwa mwaka wake wa mwisho chuo akisomea uchumi na biashara hakupenda kuajiriwa alitamani awe mfanyabiashara mkubwa nchini mweye mafanikio mengi alijitaidi kusoma, hakutaka kumkubali mwanaume yeyote shuleni kwake Jose alikuwa ndo kilakitu alimpenda sana, alikuwa tayari akose pesa lakin si kumkosa Jose alimuitaji sana,
Ilipita kipindi kirefu bila kuonana na mamayake, siku moja akaamua amuite amsalimie alikuwa bado anayo ile pete ya dhahabu aliisugua na ghafla Meyan akatokea mbele yake!
"Mama nimekukumbuka mno"
Alisema akainuka kumkumbatia, lakini aligundua tofauti mamayake hakuwa na furaha alionyesha majonzi, akaamua kumuuliza nini tatizo.
"Mbona huna furaha kuna tatizo gani?"
Aliuliza
"Nakuonea huruma mwanangu maumivu unayoenda kuyapata"
Alisema Meyan
"Maumivu gani mbona sikuelewi?"
Skola alishangaa
"Usijali ipo siku utajua tu"
Skola hakumuelewa mamayake alikuwa na maana gani. Ghafla bila kutegemea Bwana Saimon akafungua mlango nakuingia chumbani kwa binti yake sababu alimsikia akiongea
"Haaa Meyan"
Alishtuka kumuona akapiga magoti nakumuomba msamaha
"Nisamehe sana kwa yote yaliyotokea nakuomba"
Aliomba uku bado amempigia magoti, Meyan alimsogelea akamuinua nakumkumbatia uku akilia nakumwambia
"Nimekusamehe usijali ila siwezi kuishi duniani"
Aliongea akamuachia nakuwaaga wote akatoweka ilikuwa zaidi ya maumivu kwa bwana Saimon akajikuta analia kama mtoto Skola alimuhurumia babayake akamsogelea nakumbembeleza anyamaze
"Mimi nitaongea na mama akubali muishi wote usijali baba"
Kidogo maneno yake yalimfariji babayake akakubali, alimsaidia kuinuka nakumpeleka chumbani kwake apumzike.
"Lazima Baba na Mama niwaunganishe muishi pamoja"
Alisema Skola akiwa amekaa kitandani anafikiria maneno aliyoambiwa na mamayake.
Asubuh kulikucha akajiandaa nakuelekea shuleni.
Kulikuwa na mwanafunzi mmoja aitwae Andrew alikuwa ni kijana mpole mwenye bidii yakusoma, hakuwa na makuu kama wengine sababu maisha yao yalikuwa duni sana tangu babayake amkatae akiwa tumboni ni mamayake pekee aliangaika nae adi alipofikia apo chuo, alipenda kusoma kwa bidii ili aje kumsaidia mamayake hakuwahi kuwa na mwanamke sababu alijua wanawake wanapenda sana pesa, yeye hakuwa na uwezo asingeweza kumtimizia mwanamke anachohitaji.
Siku moja akakutana na Skola alijikuta anavutiwa nae sana akaona si mbaya akimsalimia.
"Mambo dada"
"Poa za kwako"
Alijibu Skola hakuwa na maringo alipenda kuongea na wengi, tofauti na wasichana wengine wanaojisikia yeye alikuwa kawaida sana hakupenda majivuno ata mwanaume akimtaka kimapenzi atamjibu kawaida bila kumtukana wala kuonyesha hasira.
"Safi dadangu nimependa nikusalimie tu"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alijibu Andrew nakumfanya Skola amshangae sababu alijua yupo kama wengine wanaomtongoza ila uyu alikuwa tofauti hakumtamkia kuhusu mapenzi.
Huo ukawa mwanzo wa kujuana kwao, mara kwa mara walikutana nakusalimiana basi wakajikuta wanazoeana ghafla kupelekea adi Skola akatamani kupaona anapoishi Andrew bila hiyana alimpeleka kwao ni Ubungo maziwa.
Nyumba ya zamani iliyochoka ndio walikuwa wakiiishi humo alimuonea huruma sana maisha yake akajikuta anatamani kumsaidia alikumbuka alipewa uwezo pia anayopete anaweza kuomba lolote nalikatokea.
"Andrew na mama nahitaji kuwasaidia"
Alisema Skola
"Kutusaidaje mwanangu sijakuelewa"
Mamayake Andrew aliuliza
"Nahitaji kuwajengea nyumba mpya"
Alisema Skola nakuwafanya washangae mama akataka kupinga ila Andrew akamuwahi nakumkubalia Skola
"Sawa kwa kipindi nyumba inajengwa nataka mkae hotelini"
Aliwaambia wakakubali basi akaondoka nakurudi kwao uku akipanga kesho yake atafute mafundi ujenzi watakaojenga iyo nyumba.
Alirudi nyumbani jioni yule mfanyakazi akaanza maneno
"Mbona umechelewa kurudi ulikuwa wapi hee umeanza umalaya?"
Skola alimtizama hakuongea kitu akaingia chumbani kwake alikuwa anavua nguo akaoge Hilda akamfata uko uko
"Nakusemesha usikii unanidharau mimi?"
Skola alichukia sana House girl anajifanya mwenye nyumba aligeuka kumuangalia uku macho yake yamebadirika nakutisha sana akamnyooshea kidole
"Utakaa kimya milele poteaa mbele yangu"
Hidla alitoka mbio na tangu siku iyo akawa bubu hakuweza kuongea ilo lilimshangaza sana Bwana Saimon alichokifanya ni kumpa nauli arudi kwao kumbe Hilda alikuwa anampenda bwana Saimon alitamani amuoe awe mkewe ndo maana akawa anajitawala ndani nakujifanya mama mwenye nyumba hatimae mdomo wake ukamponza.
*****
Mawasiliano kati ya Skola na Jose yalipungua kilasiku Jose alijifanya yupo bize na kazi kipindi iko alikuwa ameshajenga nyumba yake nakuamia hakuwa akiishi nyumbani kwa Bwana Saimon tena.
"Baby nimekumisi jamani natamani kukuona"
Ni Skola alimwandikia meseji sababu simu hapokei akipiga
"Samahani nina kazi nitakucheki kesho"
Alimjibu ivyo.
Moyo wa Skola ulikuwa kwenye maumivu sana alijikuta anamlaumu babayake kumtafutia kazi mpenzi wake ambae muda wote yupo bize.
"Skola mbona sikuelewi mwanangu kazi gani awe bize uyo Jose ile kazi mwisho saa kumi wanatoka ni kukagua bidhaa tu sio kazi yakusema atalala uko uko huo ubize upi anaosema yeye subiri saa kumi na mbili sasa eeh twende uko ofisini ukaone"
Bwana Saimon alimchukua Skola wakapanda gari nakuelekea mwenge kwenye iyo ofisi ambapo walikuta imefungwa hakuna mtu.
Skola akachukua simu nakupiga ambapo Jose alipokea
"We mwanamke nipo kazini unapiga simu unataka nini ujui nafanya kazi kwaajiri yako?"
Alisema akakata simu
"Haya umejionea mwenyewe ulikuwa unanipa lawama bure"
Alisema babayake wakapanda gari nakurudi nyumbani.
Moyo wa Skola ulikuwa unamuuma sana hakujua kwanini Jose alibadirika.
Usiku ulifika aliingia chumbani kulala japo usingizi haukuja kabisa mara simu yake ikaita ni Andrew alimpigia kumtakia usiku mwema alifarijika kwailo nyumba yao mpya ilishajengwa nakuwafanya waonekane watu na wao waliutoka umasikini.
Usiku saa saba Skola anashtuka usingizini uku jasho likimtoka ile pete ilikuwa inawaka nakun'gara sana.
Aliishika nakujishangaa anapotea mule ndani nakujikuta yupo chumbani kwa Jose ambae alikuwa na wanawake wawili anafanya nao mapenzi
"Siwezi kuamini iki ninachokiona"
Wote waliokuwa ndani walishtuka sana, hakuna alieamini msichana waliemuona mbele yao, Alikuwa binti mrembo mwenye sura nzuri na umbo lakuvutia ata hao wanawake walimshangaa, zaidi kilichowaogopesha nakuwapa maswali mlango walifunga uyo msichana aliingiaje ndani hakuna aliejua!
Moyo wa Jose ulikuwa na uoga sana, alistaajabu nakupigwa butwaa kumuona Skola chumbani kwake usiku hakujua aliingiaje.
Jose alianza kujuta kwa yote aliyofanya tangu apate kazi nakujenga nyumba yake pesa ilimpa kiburi, alimsahau Skola nakuangaika na wanawake wengine.
Kulala na wanawake wawili kwa wakati mmoja hakuona tatizo ujana ulimsumbua! Hakujali Skola alikuwa anampenda nakumuhitaji hakukumbuka ni yeye ndo mwanaume wa kwanza kuujua mwili wake, alisahau ata izo pesa ni Skola ndie alisababisha apate yote ayo alikumbuka sasa nakushindwa chakujitetea.
"Siwezi kuamini iku ninachokiona"
Alisema Skola uku machozi yakimtoka kama maji maumivu aliyosikia hakuwahi kuzani kama kunasiku atayapata.
Moyo wake uliuma sanahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Jose siamini ni wewe kweli? Umkosa nini kwangu jamani?"
Aliuliza Skola uku machozi yakimtoka kama maji, moyo wake aliisi ukipasuliwa na kisu butu maumivu aliyoyasikia hayana mfano, hakika Mapenzi yanauma sana!
Ajabu yale machozi yalikuwa yanamwagika chini nakujiandika muuaji wa kike wote walishtuka kwani ndani hakukuwashwa taa ila yale machozi yalikuwa yametoa mwanga pale chini nakuonekana.
Ghafla macho ya Skola yalibadirika nakun'gara sana ilo liliwaogopesha wote waliokuwa ndani.
"Shogayangu tukimbie"
Msichana mmoja alimwambia mwenzie kumbe ni marafiki wanajuana.
Mmoja anaitwa Farida mwengine Halima ni machangudoa waliokubuhu wanaishi pamoja, wao kulala na mwanaume mmoja hawaoni tatizo muhimu wapate pesa tu ila kushiriki mapenzi na mwanaume mmoja kwao kawaida tena wanampa huduma vizuri kama ilivyotokea kwa Jose alikutana nao Maisha Club, akaongea nao bei wakakubali nakuwaleta nyumbani kwake.
Basi wakainuka kitandani nakutaka kukimbia Skola akawawah
"Mnataka kuondoka pesa zenu mshalipwa?"
Aliwauliza wakaanza kutetemeka.
"Bado ajatupatia"
Alijibu Halima, apo apo Skola akanyoosha mkono wake juu alipoushusha tu yakatokea mabunda mawili ya pesa akawapatia kila mtu moja, walipokea uku wanaogopa kijasho cha woga kinawatoka. Muda huo taa nyumba nzima ziliwaka wakaweza kuonana japo haikujulikana nani aliwasha izo taa ndani.
"Izo pesa mkafanyie biashara ziongezeke Ole wenu atakaerudia kujiuza huo ndo utakuwa mwisho wa maisha yake vaeni nguo muondoke"
Skola aliwaambia hao machangudoa aliwajua wanashida ugumu wa maisha ndo umewafanya wawe ivyo alichoamua ni kuwasaidia kama angewahukumu au kuwapa adhabu angewaua tu sababu hawana makosa.
Baada ya apo walivaa nakukimbia nje ajabu walipotoka tu wakaona bodaboda, ambapo waliisimamisha wakapanda na kuelekea nyumbani kwao wanapoishi uku wasiamini waliyokutana nayo tangu siku iyo ukahaba waliacha nakuwa wajasiriamali wakiishi kwa kufanya biashara si kutegemea wanaume.
******
Chumbani wakabaki wawili sasa Skola na Jose ambae alikuwa anatetemeka kwa uoga asijue Skola ni binadamu au jini.
"Skola nisamehe"
Alijaribu kujikakamua nakusema uku akiwa na khofu.
"Naanzaje kukusamehe ivi unajua ni maumivu kiasi gani umenipa?"
Skola aliacha kulia nakuwa kwenye hali ya kawaida yakibinadamu
Jose hakuweza kujibu.
"Sitaki kukuua nataka nikupe adhabu ambayo itakufanya ujute nakugeuza mbwa adi pale nitapojisikia nitakurudisha uwe binadamu"
Alisema Skola hakuwa na mapenzi tena juu yake moyo wake ulijenga chuki nakuisi kuchukia wanaume wote hakutaka kumuamini ata mmoja.
Jose alitaka kuomba msamaha ila alichelewa Skola akamnyooshea kidole na apo apo aligeuka mbwa.
Skola akamuamrisha atoke nje nayeye pia akatoka nyumba akaifunga.
Alimuacha nje ya nyumba Jose nakurudi nyumbani kwao ambapo alijifungia ndani nakulia sana.
Maisha ya mateso yakaanza kwa Jose
Alikuwa anajielewa yeye ni nani tatizo likaja kwenye umbo lake la mbwa, alipojaribu kuongea alibweka nakufanya watu wampige na mawe, alianza kupata mateso usiku ulipofika hakuwa na pakulala, alijiona bado binadamu asingeweza kulala jalalani au nje alitamani muda huo angekuwa kitandani lakini nyumba yake ilifungwa asingeweza kuingia ndani.
Akaanza kuzurura mitaani uku akiona watu anakimbia sababu wengi walikuwa wanampiga mawe, siku mbili zilipita hakuweka chochote tumboni alichoka ata kutembea akabaki amekaa ya dampo harufu kali inayotoka apo ilimsumbua pua yake akajikuta anajutia tamaa zake zilizomponza adi kumfanya Skola amtende vibayahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Skola kwanini ukusema wewe si binadamu"
Alijikuta anasemaivyo kwa hudhuni mwenyewe alijiona anaongea lakini alikuwa anabweka nakuwafanya watu waliokuwa maeneo ayo kuanza kumpiga nakumfukuza atoke eneo ilo anawapigia kelele.
Ghafla hali ya hewa ilibadirika nakuanza kunyesha mvua kubwa Jose hakuwa na pakikimbilia kila nyumba aliyokaa kibalazani walimtimua alikuwa kama mkimbizi alilia kilio cha samaki, machozi yalienda na maji alijuta moyo wake uliuma sana hakuona haja yakuendelea kuishi alitembea kwenye mvua adi alipofika sehemu moja kuna mto akaamua ajitumbukize humo afe, siku tatu alizoishi kama mbwa alipata mateso makubwa sana adi alikata tamaa yakuishi akaona bora afe.
Alipokuwa anataka kujidumbukiza mtoni akaisi kuna mtu amemshika nyuma hakuweza kuingia akageuka nakumuona ni Skola ambae alimshika kichwani apo apo akajikuta chumbani kwake akiwa mzima sio mbwa alishangaa ayo maajabu.
***
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment