Sehemu Ya Nne (4)
Nikajihisi kama kupagawa hivi na wala sikujua cha kufanya kwa muda ule. Mara mlango ukagongwa,
MIMI: Nani wewe?
KAKA: Mimi hapa kaka yako.
MIMI: Kaka si nimekwambia usije tena jamani!
KAKA: Acha masikhara wewe, hebu nifungulie mlango.
MIMI: Hapana kaka, wee nenda tu.
KAKA: Kwani una nini wewe? Hebu fungua huko.
Kaka akawa anasukuma sukuma mlango, ikabidi niinuke na kwenda kufungua mlango, kaka akaingia ndani moja kwa moja nami nikaurudishia mlango.
KAKA: Hiki ndicho ulichokuwa unanikataza nisiingie ndani, umemfanyaje mwenzio?
MIMI: Sijamfanya kitu kaka.
KAKA: Sema ukweli mdogo wangu, umemfanyaje huyu?
MIMI: Sijui kaka ameanguka mwenyewe.
KAKA: Aaah acha masikhara bhana, ataangukaje mwenyewe? Fanya fasta tumpeleke hospitali.
MIMI: Haitawezekana kaka.
KAKA: Haitawezekana kivipi bhana? Hebu njoo tuite msaada hapo nje tumbebe tumpeleke hospitali.
MIMI: Unajua nini kaka....(kabla sijajibu vizuri, simu yangu ikaanza kuita)
Nikaipokea ile simu,
BINTI: Kaka yako anataka kujua kilichompata rafiki yako?
MIMI: Ndio.
BINTI: Mpe simu nimweleze mwenyewe.
Nikampa simu kaka ili aongee nae ila kabla ya kuongea akaniuliza,
KAKA: Kwani ni nani?
MIMI: Wee ongea naye tu.
KAKA: Nitaongea vipi na mtu nisiyemfahamu?
MIMI: Ongea naye tu kaka.
Kaka akachukua ile simu, ikawa ni kitendo cha sekunde tu kwani kaka alianguka chini kama gunia huku jasho jingi likimtoka na macho akiwa ameyatoa tu, nikaanza kupatwa na uoga kwani kaka hakuongea chochote. Nikajiuliza yule binti kawafanya nini wale hadi hawajitambui tena. Roho ikawa inaniuma sana hata sikujua cha kufanya kwa muda ule kwakweli nilihisi kuchanganyikiwa kabisa nikatamani nichimbe shimo nijifukie.
Nikiwa bado natafakari yale yaliyopo, mlango wangu ukagongwa tena kwa nguvu.
MIMI: Nani wewe unagonga kwa nguvu hivyo?
DADA: Mimi hapa
MIMI: Wewe nani ndio? (kana kwamba nimeisahau sauti yake)
DADA: Dada yako ina maana huijui sauti yangu?
MIMI: Nenda tu dada.
DADA: Vipi tena jamani?
MIMI: Weee nenda tu bhana.
DADA: Niende wapi jamani mdogo wangu wakati nimekuja kwako?
MIMI: Nenda bhana, sitaki mgeni.
DADA: Kwani kaka yuko wapi?
MIMI: Sijui bhana, wee nenda.
DADA: Unajua unanichanganya wewe, unachogoma kunikaribisa humo ndani ni nini?
MIMI: Nenda bhana mbona huelewi wewe?
DADA: Ok, ngoja nikamchukue mama nije nae ili tujue unachoficha humo.
MIMI: Usifanye hivyo dada, dada dada (kimya alikuwa ameshaondoka).
Nikazidi kupagawa sasa dada ameenda kumchukua mama si balaa hili litanipata jamani mimi dah.
Yule binti akanipigia tena simu,
BINTI: Ndugu zako wanajua kufatilia mambo eeh?
MIMI: Sikuelewi jamani sikuelewi.
BINTI: Hunielewi eeh!! Ngoja utanielewa wakifika hao ndugu zako.
MIMI: Tafadhari usiwatende vibaya.
BINTI: Wameyataka wenyewe, na watanijua vizuri mtoto wa kitanga.
MIMI: Jamani jamani nakuomba tafadhari usinifanyie hivyo.
BINTI: Si nilikwambia uwakataze umeshindwa? Sasa ndio utajua vizuri leo.
Akakata simu nikabaki kupagawa tu na wala nisijue la kufanya. Nilijihisi kama vile mtu aliyechanganyikiwa.
Usiku ukawa umeingia na masaa nayo yakizidi kuyoyoma. Ikawa saa sita usiku mara simu yangu ikaita kuangalia imeandikwa shemeji1, kumbe ni mke wa kaka ananipigia maana yeye ndiye nilimsave shemeji1.
MKE WA KAKA: Shemeji, kaka yako alisema anakuja huko, vipi mbona hajarudi hadi sasa?
MIMI: Aaah mmh shemeji kulikuwa na tatizo kidogo ila atarudi tu.
MKE WA KAKA: Atarudi muda gani jamani shemeji, ujue hii ni saa sita jamani.
MIMI: Atarudi tu.
MKE WA KAKA: Nakuja hukohuko, hata msinitanie kwa kufichiana maovu.
MIMI: Usije bhana atarudi.
MKE WA KAKA: Nakuja.
Akakata simu, baada ya muda kidogo nikasikia muungurumo wa boda boda nje. Mara mlango ukaanza kugongwa kuwa nimfungulie. Sikuwa na jinsi nikamfungulia,
MKE WA KAKA: Eeh mume wangu yupo wapi? Nilijua tu kuna mambo mnanificha nyie bora nimekuja kuyashuhudia mwenyewe.
MIMI: Hapana shemeji sio hivyo unavyofikiria.
MKE WA KAKA: Wee usinitanie kabisa, niambie ukweli. Yani unamwona kaka yako akitenda ufirauni halafu unajifanya kumtetea.
Mara simu yangu ikaita,
BINTI: Anataka nini nae huyo?
MIMI: Anamtaka mumewe.
BINTI: Mpe simu niongee naye.
MIMI: Hapana siwezi kukupa uongee naye.
Mara mke wa kaka akadakia,
MKE WA KAKA: Kwani nani huyo?
MIMI: Eti anataka kuongea na wewe.
MKE WA KAKA: Sasa si unipe niongee nae jamani.
MIMI: Hapana shemeji, siwezi kukuruhusu uongee naye.
Shemeji akanipora ile simu na kuiweka sikioni ili aongee nae, muda huo huo nae akaanguka chini na kutapatapa, ikawa sasa kama yale matukio nimeshayazoea.
Yule binti akanipigia tena simu,
BINTI: Unaupenda mchezo wangu?
MIMI: Aah usinichanganye bhana.
BINTI: (Akacheka sana), angalia tena chini.
Akakata simu, kuangalia akawa amewarudisha wale watu wote, nikazidi kutetemeka hata nisijue cha kufanya.
Ilikuwa hakuna kulala wala kula wala kufanya chochote.
Kulipokucha nikashtuliwa na simu ya mke wa rafiki yangu.
SHEMEJI: Vipi shemeji jana hamkufanikiwa?
MIMI: Kumbe alikwambia jamaa, hatukufanikiwa.
Mara akakata simu, nikasikia simu ya rafiki yangu ikiita kwa mara ya kwanza toka mfukoni mwake. Nikaichukua ile simu alikuwa ni yule yule shemeji.
SHEMEJI: Nasikia kuna matatizo huko.
MIMI: Aaah hapana, kwani nani kakwambia?
SHEMEJI: Nina mdogo wangu ana marhani ndio kasema.
MIMI: Aaah kakudanganya huyo.
SHEMEJI: Unajua kwanini nimekata ile simu yako na kupiga huku?
MIMI: Kwanini?
SHEMEJI: Ngoja tuje tutakwambia.
MIMI: Tafadhari msije jamani sitaki matatizo mengine.
Akakata simu, nikiwa bado ni mtu mwenye mawazo, mara yule binti akapiga simu yangu.
BINTI: Umenikera sana, nani kakutuma upokee simu nyingine?
MIMI: Jamani kwani na hilo siruhusiwi?
BINTI: Ngoja nikuonyeshe tena.
Akakata simu, nikawa nimeshikwa na bumbuwazi kuwa yule binti anataka kunionyesha mbwembwe gani hizo tena...
Nikawa sijielewi kabisa nikajihisi akili yangu kama ikiniruka hivi, nikazidi kuwaza na kuwazua bila ya kupata jibu la maana.
Mara gafla giza nene likatanda pale chumbani, nikazidi kukosa amani moyoni mwangu, mara kuna kitu kikaja na kunikaba kooni nikaanza kutapatapa na kuhangaika kama kwa dakika kadhaa ile hali ikatoweka na mwanga ukarudi tena mule ndani. Mara yule binti akanipigia simu,
BINTI: Unajisikiaje mpenzi?
MIMI: Najisikiaje nini wakati umeniumiza wewe?
BINTI: Pole mpenzi.
MIMI: (Nikamjibu kwa ukali), pole yako haisaidii bhana.
BINTI: Kwahiyo unanikaripia eeh!
MIMI: Hapana sijakukaripia bhana.
Akakata simu, nikazidi kupatwa na hasira kila nikiwaangalia wale ndugu zangu pale chini nakosa raha na pia nazidi kukosa amani.
Nikakaa nikajifikiria nikachukua simu na kumpigia yule binti ila hakupokea baada ya muda akanipigia yeye,
BINTI: Eeh unasemaje?
MIMI: Tafadhari kuwa na huruma japo kidogo jamani, ona umetufungia humu toka jana na hatujala chochote.
BINTI: Kwahiyo shida yako ni chakula tu?
MIMI: Hapana sio chakula tu ila nataka uwazindue hawa watu.
BINTI: (Akacheka sana), chakula utakipata ila kuwazindua hao sio kazi yangu.
MIMI: Nihurumie tafadhari.
BINTI: Fumba macho.
MIMI: (Nikafumba kama alivyoniamuru)
BINTI: Haya fumbua macho yako.
Halafu akakata simu, Mungu wangu sikuamini kabisa nilichokiona mbele yangu, kwani nilikuwa chumbani ila cha kushangaza chumbani mule kulikuwa na shughuli mbalimbali zikiendelea, mara kuna watu wakiuza chakula na wengine wakiuza vinywaji tena walikuwa makini na shughuli zao tu, hofu kubwa ikanitanda moyoni, mara nikapokea sms,
"nenda ukajinunulie chakula sasa"
Nikahisi kupagawa kabisa na wala sikujielewa na sikuweza kuwasogelea kabisa, nilijihisi kuchanganyikiwa kwakweli, mara simu yangu ikaita,
BINTI: Unaogopa nini sasa?
MIMI: Aaah sijui hata naogopa nini?
BINTI: (Akacheka), wewe si umetaka chakula jamani, nimekusaidia kukuletea wauzaji nakushangaa huendi kununua, kwanini sasa?
MIMI: Aaah mmmh kwani aah sikuelewi.
BINTI: Inamaana hutaki chakula tena? Niwaondoe?
MIMI: Mmmh eeeh nini sijui kitu.
BINTI: (Akacheka sana), ukome kuchukua mizigo usiyoweza kubeba.
Akakata simu, ikawa ni kitendo cha kufumba na kufumbua wale wauzaji sikuwaona tena.
Nikashikwa na bumbuwazi tu hata sikujielewa.
Nikiwa mule ndani sijielewi chochote nikasikia watu wawili wakiongea pale nje, sauti ya mmoja wao niliitambua ni mke wa rafiki yangu. Wakaanza kugonga mlango, nami nikaenda na kuwafungulia nao wakapitiliza moja kwa moja ndani.
Yule mke wa rafiki yangu alikimbilia moja kwa moja pale chini alipolala mumewe huku akimtingishatingisha aamke ila kama kawaida hakuamka, yule mwingine ambaye alikuwa mdogo wa mke wa rafiki yangu alikuwa pembeni akiangalia tu na wala hakusema chochote.
Mara simu yangu ikaita,
BINTI: Hao nao wamefata nini?
MIMI: Sijui wamefata nini.
BINTI: Mpe simu mmoja nizungumze naye.
Nikataka kumpa yule mke wa rafiki yangu ile simu lakini ile anataka kuichukua mdogo wake akamkataza na kumwambia kuwa asiichukue ile simu. Mimi nikabaki nawashangaa tu, mara yule mdogo mtu akaniamuru niikate ile simu nami nikafanya hivyo. Akamgeukia dada yake na kumwambia kuwa atoe ubani kwenye mkoba na akaombe moto nje, ikabidi nimuulize,
MIMI: Samahani mdogo wangu mbona unataka kuniletea mambo ya mashetani humu ndani?
Nikaona kanigeukia na sura yote imebadilika, nikaanza kupatwa na uoga.
Akaniambia jambo moja tu kuwa inapaswa nikubali kumtoa ndugu yangu mmoja kama kafara ili niokoe maisha ya wale wengine au wote wapotee, akaniambia kuwa nichague kati ya wale watatu ambao ni mama, kaka na dada.
Kwakweli nguvu ziliniishia nikajihisi kujisaidia haja kubwa na ndogo kwa wakati mmoja kwani bado sikujua niamue lipi kumtoa ndugu yangu mmoja kama kafara au wote wapotee, na je ndugu huyo nitamtoa nani kati ya mama, kaka na dada bado sikupata jibu kwakweli.
Nikashindwa kujielewa kwa wakati huo niamue jambo gani, yule mdogo mtu akawa amenikazia macho huku yakiashiria kuwa anangoja jibu langu. Sikujielewa kabisa na wala sikuelewa niwaambie kitu gani. Yule mdada akaniambia kuwa niamue moja. Nikajikuta macho yakinitoka nilitia huruma sana na nilisononeka mno, mara yule aliyekwenda kuleta moto akarudi na ubani ukawashwa.
Yule mdogo mtu bado akaniashiria kuwa nichague ndugu yangu mmoja kwa kafara,
MIMI: Tafadhari nawaomba, ndugu zangu wasitendwe vibaya. Mimi ndio chanzo cha haya yote, naomba sana kama itawezekana basi hiyo kafara nitolewe mimi.
Nilijikuta nikiropoka kwani nilipatwa na mfadhaiko mkubwa yani atolewe ndugu yangu kafara kwa makosa yangu! Hapana huruma ilinijaa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Yule dada akanikazia macho tena, mara akaanza kuungurumisha kama simba nikawa naogopa huku jasho jingi likinitoka, mara yule mdada akaanza kuongea na mimi tena kwa sauti ya mtetemesho.
MDADA: Kwahiyo upo tayari kafara utolewe wewe mwenyewe?
MIMI: Ndio nipo tayari.
MDADA: Nipe sababu kubwa iliyokufanya kuamua hivyo.
MIMI: Sababu mimi ndio chanzo cha yote haya, ndugu zangu hawahusiki.
MDADA: Upo tayari kweli?
MIMI: (Huku nikitetemeka), ndio nipo tayari.
MDADA: Kweli kabisa kabisa upo tayari!
MIMI: (Nikizidi kutetemeke, huku nikitamka kwa sauti ya chini), ndio.
MDADA: Ngoja nikuonyeshe kwanza.
Nikiwa nimekaa chini huku natetemeka, nikamuona yule dada akichukua kama unga unga kwenye mkoba wake na kunipulizia, nikajikuta nikianguka chini.
Niliposhtuka ilikuwa ni mahali pengine kabisa, kwanza kabisa ilikuwa kama porini tena kumetulia kabisa ni sauti za ndege tu zilizosikika, nikainuka mahali hapo na kuanza kutembea bila ya kujua ninapoelekea, mara akatokea mtu mbele yangu na kunishika mkono huku akinipeleka ninapotakiwa kwenda.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment