Sehemu Ya Pili (2)
Nyumbani kwa kina
Njoshi;
Jua likiwa tayali
linazama, huku sauti za ndege zikipungua na kuufanya mji wa Mwamutapa kuwa
kimya.Ukimya huo unatokea pia katika nyumba ya kina Njoshi, ukimya unatawala
tofauti na siku zote, kwani familia ilibakiwa na mtu mmoja tu,ambaye ni mama
yake Njoshi huku mwanae akiwa hajarudi
kutoka kwa mfalme. Akiwa ameketi barazani, nje ya kibanda chao cha udongo,
kilichoezekwa kwa nyasi, aliendelea kupunga upepo huku akiwa na huzuni sana,
“Siamini,hatimaye
leo hii nimebaki peke yangu, sina cha kufanya ndio tayali imeshatokea ……,eeeh
mizimu ya babu zangu mlindeni mwanangu ” ,mama Njoshi aliongea peke yake
kwa huzuni huku akinyanyuka sehemu aliyokuwa ameketi, na kisha kuelekea ndani
kulala, hakuwa na njinsi kwani aliona kuketi pale nje kulizidi kumuongezea
machungu.
Ikulu kwa mfalme;
Giza likiwa tayali limeshaingia huku,
ukimya ukiwa umetawala katika ngome ya mfalme. Kijana Njoshi anamfuta machozi
Grace, huku akiwa amemkumbatia,
“Usijali Grace,
naamini nitarudi salama ndani ya siku tatu “,Njoshi alimtoa hofu binti
mfalme, msichana aliyempenda sana, na aliamini atamuoa atakaporudi kutoka
katika msitu hatari wa majini, msitu ambao aliambiwa na mama yake hana budi
kwenda huko, kwani huko ndiko angeupata ufalme na ukombozi wa Mwamutapa.
“Sawa Njoshi,
nakuamini wewe ni shujaa, nakuombea kwa mizimu yetu, urudi ukiwa mzima
“,Grace aliongea kwa huzuni huku akitoka mikononi mwa Njoshi aliyekuwa
amemkumbatia, na kumruhusu kuianza safari yake haraka sana, kwani alitakiwa
kuondoka usiku huo. Na bila kupoteza muda, kijana shupavu na hodari, kijana
pekee aliyeogopwa na askari pamoja na mfalme Mutapa kutokana na uhodari wake wa
kupambana, anatoka katika ngome ya mfalme iliyojengwa kwa ukuta mrefu, huku
wafanyakazi pamoja na familia nzima ya mfalme wakimtazama na kumtakia kila
laheri katika safari hiyo, bila kutambua kuwa Njoshi alikuwa na malengo
yaliyompeleka msituni huku swala la kuchukua jeneza la ajabu, likiwa la ziada
tu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mwamutapa
Kijana ambaye alikuwa ni rafiki yake
Njoshi, urafiki ambao ulitokana na kijana huyo kuokolewa katika kipigo kizito
kutoka kwa askari wa mfalme, mara tu alipofanya kazi asubuhi mpaka jioni katika
shamba la mfalme, na pale alipojaribu kudai haki yake, askari wale walimnyima
pesa, jambo ambalo kijana yule alishindwa kulivumilia, alijikuta akilusha
ngumi, na kuambulia kipigo kikali kwani asingeweza kuwashinda askari zaidi ya
kumi, huku yeye akiwa mmoja tu, lakini bila kutegemea ghafla alishangaa, askari
wale wakipigwa mateke ya haraka haraka na kutimua mbio.
“mimi naitwa
Njoshi, na pole sana ndugu yangu, hawa ndio askari wetu, inatakiwa tuungane
kuitafuta haki “,kijana yule aliikumbuka sauti ya mtu aliyemsaidia kutoka
mikononi mwa askari wa mfalme, ikijitambulisha na kisha kumuomba waungane
katika harakati za ukombozi wa Mwamutapa. Na huo ndio ukawa mwanzo wa urafiki
wao, urafiki ambao umedumu kwa muda mrefu na wamekuwa kama ndugu sasa.
“Inabidi kesho
niende kwao nikamuone rafiki yangu, tangu jana sijaonana naye “,rafiki
yake Njoshi, aliyejulikana kwa jina la Ngesha, alizungumza peke yake huku
akijifunika shuka lake na kisha kuuchapa usingizi, bila kutambua kuwa muda huo
ambao yeye analala, rafiki yake yuko safarini bila kujali giza wala hatari
yoyote usiku huo, akielekea katika msitu wa majini, msitu ambao ulipatikana
umbali wa kilomita arobaini kutoka katika makazi ya watu wa Mwamutapa.
Msitu wa majini;
Tangu asubuhi tetemeko lilipotokea, na
malikia kutangaza hali ya hatari katika msitu, mitego ya kila aina iliweza
kutegwa katika kila njia ya kuingilia msituni, huku jeshi la msituni likiwa
tayali limeshika dhana mbalimbali za kivita ikiwemo mishale, na kuuzunguka
msitu wote.
“Aiweeeh jini
mweupe, kiongozi wa askari wangu wa msituni, adui wetu yuko njiani anakuja,
nakuomba jiandae kwa mapambano, uko huru kutumia nguvu za kichawi na kijini
ulizonazo “,malikia alimpatia taarifa mkuu wa jeshi lake la ulinzi
msituni, na haraka bila kupoteza muda alitoweka mbele ya uso wa malikia, kwenda
kutekeleza amli aliyopewa ya kudumisha ulinzi kila kona ya msitu, na kujiandaa
kwa ajili ya kulipiza kisasi.
Giza likiwa linazidi
kuwa la kutisha,ikiwa imefika mida kama ya saa nne usiku, kijana Njoshi akiwa
amevalia bukta yake nyeusi, huku chini akiwa miguu peku, kwani watu wa
Mwanamutapa kutokuvaa viatu ilikuwa kama tamaduni yao, kijana Njoshi aliendelea
kutembea huku akinyosha balabala kubwa ya vumbi, balabala iliyokuwa
ikiunganisha nchi ya Mwamutapa na nchi zingine za jirani, ikiwemo nchi ya
Mwamuyeshi. Sauti za miguu yake ndizo zilizosikika balabala nzima, kwani watu
hawakupita balabala hiyo mida ya usiku, kutokana na kuogopa kutekwa na
kunyanganywa mali zao, na pengine hata kuuawa.
Ilikuwa tofauti kwa
Njoshi, hakuogopa jambo lolote lile, akiwa kifua mbele kwani hakuvaa shati
lolote lile huku akiwa amebeba begi jeusi alilopewa na mama yake, aliendelea
kusonga mbele huku akitembea kwa mwendo wa haraka, na muda mwingine alikimbia,
ili aweze kufika katika ardhi ya msitu wa majini kabla hapajakucha siku ya
jumanne.
“Mpaka sasahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
nimeshakimbia umbali mrefu sana, sina budi kuongeza bidii “,Njoshi
aliongea peke yake moyoni mwake, huku akiwa tayali ameshayaacha majumba ya
Mwanamutapa mbali sana. Kila alipokumbuka mateso yote ya Wanamutapa, nguvu za
ajabu ziliongezeka mwilini mwake na kumfanya azidi kuongeza mwendo ili apate
kuikomboa nchi yake haraka sana, huku mbalamwezi ikiangaza vema njia
aliyotakiwa kupita. “Hahaha eti jeneza, siamini kama kuna watu hawataki
kufa, yani uishi milele, na kututesa milele, hili ni jambo ambalo haliwezekani
“,Njoshi aliongea maneno ya kejeli kwa mfalme, huku akitabasamu na kumuona
mfalme kama mtu wa ajabu sana, mtu aliyemkabidhi fisi bucha na kula nyama zote
za buchani.
“Hapa mimi
ninachofuata ni fimbo ya ufalme, fimbo ambayo inapatikana katika ngome ya
malikia wa msituni, malikia wa majini, jeneza nitalishughulikia nikishapata
fimbo yangu ya kuiongoza Mwanamutapa “,Njoshi alizidi kuongea peke yake,
huku akisisitiza jambo lililompeleka msituni, kwani ili uwe mfalme nilazima
umiliki fimbo ya kifalme kutoka katika msitu huo, na mfalme Mutapa aliipata
fimbo hiyo ya uongozi kutokana na kurithi kwa wazazi wake,huku chanzo cha fimbo
hiyo kikisemekana ni katika msitu wa majin. Fimbo hiyo ilimpatia mamlaka mfalme
kutodhurika na majini wa msituni, kwani msitu wa majini ulipatikana katika nchi
ya Mwamutapa. Wengi walifunga safari kwenda msituni kuchukua fimbo nyingine ya
ufalme, inayofanana na fimbo ya mfalme lakini walishindwa kurudi wakiwa hai.
Pia wasingeweza
kupambana na mfalme kwani fimbo aliyonayo ilimpatia kiburi sana, hata
ukilishinda jeshi lake na kumuua, usingeweza kuongoza nchi, kwani fimbo
iliandikwa jina la mfalme Mutapa,. Hivyo
njia ambayo ni rahisi, ilikuwa ni kuitafuta fimbo ya ufalme msituni ,na
kuiandika jina lako binafsi ili majini wakutambue na wasikusumbue katika
uongozi wako,hapo ndipo ufanye mapinduzi na kumuua mfalme ili uongoze nchi ya
Mwanamutapa.
“Ngoja nipumzike
kidogo hapa chini ya mti ,ninywe maji, nichukue siraha zangu kwani muda wowote
nitaufikia msitu “,Njoshi aliongea huku akiketi katika majani mafupi chini
ya mti wa ubuyu, na kisha kufungua begi alilopewa na mama yake. Huzuni ya kutokumuona
tena mama yake ilimuandama, kwani aliyakumbuka maneno ya mama yake kuwa
hatomuona tena na kufanya machozi kumtoka , mithili ya mtu aliyefiwa na mtu
anayemtegemea. Alifungua begi na kutoa kitambaa cheusi, kitambaa ambacho
alitakiwa akifunge kiunoni kama mkanda, huku akishikilia panga kali, panga
ambalo linauwezo wa kuua majini. Ikiwa tayali imeshafika mida ya saa saba
usiku, Njoshi ananyanyuka sehemu aliyokuwa amepumzika kwa takribani dakika
tano, na kisha kusonga mbele kuusogelea msitu wa majini.
Msitu wa majini
Malikia wa majini anaingiliwa na hofu
kubwa sana kwani mtu aliyekuwa anakuja kuuvamia msitu alionekana kuwa hatari
sana, kwani kila alipojaribu kumtambua sura yake alishindwa, na ghafla
mawasiliano yalipotea, hakuweza kumuona tena katika kiganja chake, kiganja
kilichokuwa kikimuonesha mtu aliyekuwa njiani akielekea msituni. “Huyu
anayekuja huku natambua kuwa ni mtoto wa mtu aliyewahi kuja huku na kutuibia
mali zetu, lakini sura yake ningependa niifahamu lakini nimeshindwa, na kwanini
kapotea ghafla, nashindwa kumuona tena katika viganja vyangu “,Malikia wa
msituni alizungumza kwa hasira na mshangao mkubwa, bila kutambua kuwa Njoshi
aliweza kuvaa kitambaa cheusi kiunoni, na kumfanya kutoonekana kama akiwa
anafuatiliwa na majini.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Hapa nikizubaa,
watu wangu watakufa “,malikia wa
majini, msichana aliyekuwa mrembo sana, na mwenye umri sawa na Grace,
alizungumza huku akitafuta kichupa kidogo cha maji, na kisha kumpatia askari
wake mmoja, kunyunyizia maji hayo kuzunguka ngome yake yote ili kujilinda. Maji
hayo yalikuwa na uwezo wa kumgandisha mahali pale, mtu yeyote mwenye asili ya
ubinadamu, atakapokanyaga eneo lile.
“Hapa tayali
nimemaliza kazi, hata kama akifanikiwa kuwapita askari wangu msituni, mimi
lazima nitamkamata “,malikia aliongea kwa kujigamba, na kuachia tabasamu
zuri lililoonesha vema uzuri wake.
Nje ya msitu;
Kwa mbali kijana shupavu na hodari
Njoshi Nyangoma, anakamatilia panga lake kisawasawa, kwani alianza kuuona msitu
hatari wa majini, ukiwa kama hatua mia moja mbele yake, baada ya kutembea na
kukimbia kwa usiku mzima, na ilikua imeshafika mida ya saa kumi usiku, kuamkia
siku ya jumanne.
“Aiweeeh mizimu wa
mababu zangu, mizimu wa ardhi ya Mwamutapa, asanteni kwa kunifikisha salama,
naomba mnilinde tena na kunirudisha nyumbani salama “,Njoshi aliongea kwa
hofu na woga, kwani alikuwa na kazi nzito, tena ya hatari ikiwa mbele yake.
“Hapa ni mwendo wa
kuua tu kiumbe chochote, kitakachokatiza mbe…le…y…a…ngu “,Njoshi
alishindwa kumalizia sentesi yake baada ya kukanyaga mtego wa kamba, na kisha
mtego huo kumning’iniza juu ya mti huku miguu ikiwa juu na kichwa kikiwa chini,
mala tu alipokanyaga mguu wake msituni.
Njoshi bila kupoteza
muda, aliikata kamba ile mguuni kwake, kwa kutumia panga lake na kisha kudondoka
chini kama mzigo huku akiwa haamini kilichokuwa kimetokea ghafla namna ile, na
kumuongezea hofu na woga huku akitakiwa kuwa makini sana ndani ya msitu.
Msitu wa majini;
Viumbe hatari wa msituni ghafla
wanasikia kishindo katika moja ya mitego waliyokuwa wametega, hali hii
inawafanya wagundue kuwa tayali adui yao alikuwa ameshaingia msituni, kwani
hawakuweza kumuona katika ramani zao, na hata walipotumia uwezo wao wa kijini,
walishindwa kumuona adui yao, mala baada ya Njoshi kujifunga kiunoni kitambaa
cheusi alichopewa na mama yake. “Jamani tayali adui alishaingia msituni,
fanyeni kila njia mumkamate akiwa hai au amekufa “,jini mweupe, kiongozi
wa askari wa msituni, alitoa amli ya kuanza kumtafuta adui, baada ya kufika
katika eneo ambalo kishindo kikubwa kilisikika, na sehemu ambayo walitega mtego
wao, na kukuta kamba ya mtego ikiwa inaning’inia baada ya kukatwa huku adui
akiwa ameshatoweka.
“Nazani mnaisikia
harufu ya binadamu, hayuko mbali, mtafuteni haraka sana ” ,jini mweupe
alizidi kuongea na kuliamlisha jeshi lake la msituni, kumtafuta adui baada ya
kuhisi harufu yake katika eneo lile la mtego, eneo ambalo lilizungukwa na vichaka
pamoja na miti mirefu.
********http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya Njoshi kuponea
chupuchupu kutoka katika mtego, haraka sana anaingia ndani ya kichaka chenye
majani marefu, kwani alitambua kuwa majini wa msituni lazima wafike katika eneo
lile muda sio mrefu baada ya kusikia kishindo kile kikubwa, hivyo asingeweza
kukimbia na kufika umbali mrefu bila kukamatwa.
Lakini ukistaajabu ya
Musa, utayaona ya firauni, Njoshi alishangaa sana baada ya kuliona kundi kubwa
la majini, likifika eneo lile haraka sana huku akiwa hata hajajificha vizuri
kwenye majani. Kwani viumbe wale walikuwa na uwezo wa kupotea na kufika eneo
lolote walilolitaka wao, ndani ya sekunde tu, kwani hawakuwa binadamu bali
majini, tena majini hatari wa msituni, msitu ambao ulikuwa maarufu katika nchi
ya Mwamutapa, pamoja na ulimwengu mzima, kutokana na utajiri wake.
“Mungu wangu,
mbona hawanioni “,Njoshi alistaajabu sana kwani kiongozi wa askari wale,
jini mweupe alisimama karibu sana na kichaka kile, na ilikuwa imebakia kidogo
amkanyage Njoshi kwani alikuwa hata hajajificha vizuri katika kichaka, eneo
ambalo mtego ulikuwepo.
Njoshi ujasiri ukiwa
umetoweka, alianza kutetemeka kwa woga kwani majini wale walitisha sana kwa
kuwatazama, wengine walikuwa na mguu mmoja huku wakiwa na vichwa vingi sana,
pamoja na mikono zaidi ya miwili. Njoshi akiwa anatetemeka aliamua kufumba
kinywa chake asiweze kupiga kelele, kwani jini mweupe, aliyekuwa na kichwa cha
nyoka aina ya koboko, huku akiwa na mwili mweupe tena wa binadamu, alitoa amli
ya kumsaka Njoshi katika kichaka kile, kwani waliweza kuhisi harufu yake.
“Asante mizimu ya
mababu, sionekani, leo nilikuwa nimekwisha “,Njoshi akiwa amejifumba mdomo
wake kwa kutumia viganja vya mikono, aliishukuru mizimu, kwani majini waliokuwa
wanatisha sana walipita karibu yake bila kumwona, jambo ambalo lilimshangaza
sana kwani sehemu kubwa ya mwili wake ilikuwa wazi na hakufunikwa vizuri na
majani, bila kutambua kuwa mkanda ule wa kitambaa cheusi aliouvaa kiunoni,
ndiyo uliyosababisha majini wasiweze kumuona.
“Msitu huu niliuskia
tu, leo nimejionea mwenyewe “,Njoshi aliongea moyoni huku akiwa
anamshangaa askari mmoja wa msituni,mwili wake ukiwa umebakia mifupa tu,huku
akiwa ameshika mshale, na kusonga mbele, lakini Njoshi alishindwa kutumia hata
panga lake kuwaangamiza majini wale kwani hakutambua matumizi yake, huku yeye
akiwa anashangaa muonekano wa majini wale na kuzidi kumuongezea woga.
Mwamutapa
Asubuhi mida kama ya saa moja, kijana
Ngesha aliamka kutoka usingizini, na kunawa uso ili aelekee nyumbani kwa rafiki
yake, ili asikute wameshaondoka kwenda shambani.
“Mwanangu mbona
haraka sana asubuhi hii, unaenda wapi ” ,ilikuwa ni sauti ya mama yake
Ngesha, mama ambaye alibaki mjane baada ya mume wake kuitwa na mfalme,na
alipokwenda huko hakuweza kurudi.Kwani alipofika ikulu kwa mfalme,alikuta kundi
kubwa la wanaume wakiwa huko wanasaga unga wa mahindi kwa kutwanga kwenye
vinu,lakini baada ya kumaliza kazi hiyo na kudai malipo yao ,kundi lote
lilitupwa kwenye bwawa la mamba bila huruma ,amli iliyotoka kwa mtoto mkubwa wa
kiume wa mfalme.
Lakini mama Ngesha kilahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
alipojaribu kuulizia kwa mfalme kuhusu mumewe ,hakuweza kupatiwa jibu sahii
zaidi ya vitisho.Kitendo kilichomfanya mama Ngesha pamoja na mwanae kuweka
msiba nyumbani kwani tayali waliamini mzee wao aliyejulikana kwa jina la
Mugina,alikuwa ameuawa,jambo ambalo lilikuwa kweli.
“Naenda kumsalimia
rafiki yangu Njoshi,mara moja,” Ngesha alimjibu mama yake na kisha
kutokomea huku akikimbia ili kumuwahi Njoshi,kwani ilikuwa ndio mida ya Njoshi na mama yake kwenda shambani.
Ikulu kwa mfalme;
Asubuhi na mapema siku ya jumanne,siku
ambayo usiku uliopita kijana Njoshi alitoweka ikulu kuelekea katika msitu wa
majini,kwenda kuchukua jeneza la ajabu kwa ajili ya kumzikia mfalme atakapokufa
,na kisha kufufuka ndani ya wiki moja.
Vilio vinatawala katika
ngome yote ya mfalme,huku familia nzima ya mfalme pamoja na wafanyakazi wote
wakilia kwa kwikwi,ama kweli mkuki kwa ngurue kwa binadamu mchungu,leo hii
maneno haya yalijidhirisha waziwazi.Walizoea kuona wengine wakilia,lakini leo
ilikuwa ni zamu ya familia ya mfalme kulia.
“Baba rudi,baba
rudi baba yangu nakupenda”,msichana Grace alilia kwa huzuni,huku akitamka
maneno ambayo yaliongeza uchungu katika familia nzima ya mfalme.Walitamani sana
Njoshi afanikiwe kurudi na jeneza salama,ili mfalme afufuke ndani ya wiki moja
na kuishi milele,lakini hawakuamini kama kweli Njoshi atafanikiwa kurudi
salama,kwani huko msituni alikoenda ni hatari sana.
Nyumbani kwa kina
Njoshi;
Mama yake Njoshi,akiwa ameshika jembe
kama kawaida yake tayali kuelekea shambani,huku kichwani akiwa na mawazo mengi
juu ya hatma ya mwanae.
Akiwa anatoka nje ya
uzio wake wa nyumba,uzio ambao ulitengenezwa kwa nyasi,Kwa mbali alishangaa
kumuona kijana akija uelekeo wa nyumba yake huku akikimbia.Kitendo hicho
kilimfanya aweze kuweka jembe lake chini,pamoja na kikapu kilichokuwa na maji
ya kunywa pamoja na chakula kwa matumizi ya shambani siku nzima.
“Aiweee…mama
,Njoshi ni memkuta…aiweeh”,Ngesha alimsalimia mama yake Njoshi na kumuulza
kuhusu rafiki yake,huku mama akipumua baada ya kumtambua kijana aliyekuja
nyumbani kwake,na pia hakuweza kuleta taarifa mbaya.
“Aiweeeh
mwanangu,rafiki yako aliitwa na mfalme tangu jana asubuhi,mpaka sasa sina
taarifa yoyote,aiweeeh”,mama Njoshi alimjibu rafiki yake mwanae,na kumtia
hofu sana,kitendo ambacho kilimfanya Ngesha kutoweka bila hata kuaga kuelekea
ikulu,kwani alitambua kuwa rafiki yake lazima atakua hatarini kama kweli
alienda ikulu tangu siku iliyopita na hajarudi mpaka wakati ule.
Kifo chahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
mfalme,haitakiwi wananchi wa Mwamutapa wafahamu,zaidi ya familia ya mfalme na
mtu aliyelifuata jeneza msituni,lakini Ngesha kaelekea ikulu kwenda kujua nini
kinaendelea kwa rafiki yake Njoshi.…
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment