Sehemu Ya Tatu (3)
Bagamoyo;
Mzee Jabir alifika Bagamoyo haraka sana asubuhi na mapema siku ya jumapili, taarifa ya kutisha kutoka kwa mganga ndiyo iliyomfanya afunge safari kutoka Dar es salam, na kufika katika ofisi ya chama chao cha kishetani, ofisi ambayo ilipatikana katika makazi ya mganga wa kienyeji aliyekuwa akiishi Bagamoyo.
Taarifa kuhusu Juliet kumtokea na kumtisha mganga, ndiyo iliyomfanya mganga kufika Bagamoyo huku akiwa na hofu isiyo ya kawaida.
“Bora umefika! Juliet yuko njiani anaelekea kanisani kwa Hakika! Anaenda kuharibu kila kitu, inatakiwa tumzuie! Harafu pia, nyoka aliyetoka katika mwili wa Nyoka wetu mkubwa na kumpatia Hakika aweze kuishi naye! Ana hasira sana! Siku tano zimepita bila kula chakula chochote! Waliokuwa wanatakiwa kuliwa ni wazazi wa Hakika, lakini Juliet kawaokoa “,mzee Jabir baada ya kufika kwa mganga, alikutana na taarifa nyingi zilizoendelea kumshitua na kumuongezea maswali. Aliamini kuwa mzimu wa Juliet, haukuwa wa kawaida na ulionekana kuwa na nguvu nyingi na ndio maana uliweza kugundua kila kitu ambacho walikuwa wakipanga.
“Mganga tunafanya nini sasa kumzuia Juliet! ” ,
“Mimi mwenyewe nakusikiliza wewe tushauriane “,
“Haina jinsi inabidi mtukufu nyoka umwamushe atusaidie “
“Kuamka sio shida! Lakini hana nguvu za kutosha kupambana! na yeye tangu amtafune Juliet, hajapata chakula chochote kile ……
Yalikuwa ni majibizano yaliyokuwa yakiendelea, maongezi kati ya wanachama wawili wa chama cha kishetani cha kumpinga Mungu. Mzee Jabir, pamoja na mganga wa kienyeji maarufu nchini Tanzania na nchi jirani. Mganga ambaye alipatikana Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Mzimu wa Juliet unawapeleka wazazi wa Hakika kanisani! Nini kitatokea kanisani kwani Juliet ameshakufa, na wazazi wake hawatambui hilo.
Watu walifurika kanisani kama kawaida, lakini siku hii ya jumapili,watu walikuwa wengi kuliko siku zote. Waandishi wa habari hawakutaka kupitwa na chochote kile, siku hii idadi yao iliongezeka tofauti na jumapili zilizopita.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku hii ilikuwa siku ambayo taarifa kuhusu Juliet kupotea, ilitakiwa kutangazwa huku mimi kama mchungaji nikielezea jinsi msichana huyu mrembo alivyopotea katika mazingira ya kutatanisha.
“Jumapili hii watu wamekua wengi sana “,
“Watu wanataka kusikia kilichotokea mpaka mtoto wa mzee wa kanisa akapotea !”,
“Mimi siamini kama amepotea! binti yule ni msomi na tayali ni mtu mzima, hawezi kupotea kirahisi “,
“Ngoja tusubili kushuhudia mchungaji atasema nini! japo wengine wanasema inawezekana kahusika kwa namna moja au nyingine! “,
Yalikuwa ni majibizano ya baadhi ya waumini waliokuwa karibu kabisa na meza yetu .Meza ambayo tulikuwa tumeketi viongozi wa kanisa.
“Waaoh! today might be the blessed Sunday ever seen! (Waaooh! Leo inaweza kuwa jumapili ambayo imebarikiwa sana na haijawahi kuonekana), ilikuwa ni sauti kubwa ya mzungu mmoja, mzungu ambaye alionekana kutotambua chochote kuhusu wingi wa watu waliofurika kanisani siku hiyo.
“Mungu ni mwema leo, kesho na hata milele. Najua wengi wenu mnamfahamu Juliet, napenda kusema kuwa, mimi kama kiongozi wa kanisa sijafurahishwa na upoteaji wake. Mpaka sasa hatujui yuhai au amekufa, tunaomba kanisa zima tushirikiane bega kwa bega kumtafuta “,
“Mtoto wa jirani ni wa kwako pia, kazi ya kumtafuta Juliet siyo ya mchungaji, au wazazi wake peke yao! Hata wewe unaweza changia hata kwa maombi inatoshaa! “,
Makofi yalisikika, walikuwa ni waumini wakinipongeza kwa maneno mazuri niliyokuwa nikiongea. Hawakutambua siri nzito iliyokuwa kifuani kwangu, siri ambayo pengine muda wowote ingewekwa wazi na mzimu wake Juliet mala tu atakapokanyaga mguu wake kanisani kama jitihada za kumzuia zikigonga mwamba.
“Na…na…na taka nyama ya binadamu, nataka nyama! nataka chakula “,ilikuwa ni sauti ya nyoka wa ajabu, nyoka ambaye alikuwa na uwezo wa kuongea lugha yoyote ile. Maneno yake ya kutisha, yalinifanya nisitishe kabisa kuendelea kuongea.
Nilishangaa sana kwani baadhi ya watu waliokuwa wakinipigia makofi, walisitisha makofi yao baada ya kusikia sauti ya ajabu kutoka nyumbani kwangu.
“Mchungaji hapa kuna kitu sio bure, maombi ni siraha pekee ya kuitumia! “,alikuwa ni baba yake Juliet, mzee ambaye aliamini kabisa kuwa ipo siku ataweza kumuona tena mwanae. Alinyenyuka na kisha kuninongoneza maneno hayo, sikuwa na budi kukukubaliana naye ili wasiweze kugundua kuwa nilihusika asilimia mia moja na sauti za kutisha za kiumbe kilichokuwa kikisikika na kupiga kelele nyumbani kwangu.
“Hapana baba!, maombi yenu hayatasaidia chochote ,mimi nimekufa lakini kwa macho yenu hamtaweza kuamini!, mimi ni mzimu wa Juliet na wala sio Juliet,,, chanzo cha yoteee, ni mchungaji mnayemwona kama nabii kwenu, kanitoa sadaka kwa miungu yake ili aendelee kuwa tajiri, maarufu na kupata waumini wengi katika kanisa lake hili ,huyu sio mtumishi wa Mungu bali mpinga kristo!!! “,
Ilikuwa ni sauti ya Juliet aliyeingia kanisani akiongozana na wazazi wangu, na kuacha maswali mengi kwa umati wote uliokuwa kanisani kwangu.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bagamoyo;
Mganga pamoja na mzee Jabir hawakuamini kilichotokea, hawakuamini kama Juliet alifanikiwa kufika kanisani kwangu akiwa salama japokuwa walitumia uchawi wao wote kumzuia bila mafanikio.
Walituma radi, lakini radi ziliwarudia wao wenyewe na alimanusura ziwaue kabisa. Hawakukata tamaa, walijaribu kwa mala nyingine na kumtumia Juliet moto mkubwa na wa ajabu sana, lakini bila kutegemea moto ule uliweza kuwarudia tena na kuwaunguza wao japokuwa walifanikiwa kuuzima bila kupata majeraha yoyote. Japokuwa nguo walizovaa ziliteketea kwa moto huo, na kuwaacha wakiwa kama walivyozaliwa.
Juliet alikuwa na nguvu za ajabu, alifanikiwa kufika kanisani japo wazazi wangu walionekana kumuogopa sana tofauti na awali. Kwani walimshuhudia alivyokuwa akipambana na radi pamoja na moto uliotumwa kuwateketeza wakiwa ndani ya gari wakielekea kanisani kwangu. Waliamini kabisa Juliet hakuwa binadamu wa kawaida, na pengine alikuwa jini, lakini kilichowashangaza Juliet alikuwa ameshika biblia,jambo ambalo lisingewezekana kwa jini.Na kuwafanya waendelee kujiuliza maswali mengi bila majibu yoyote.
“Juliet ana nguvu kutushinda sisi,lakini Nyoka wetu ndiye mwenye uwezo wa kupambana naye!hatuna budi kusababisha ajari ili nyoka apate chakula na kumuongezea nguvu za kupambana na Juliet”,mganga alitoa ushauri,ushauri ambao ulikubaliwa na mzee Jabir kwa asilimia mia moja.
Vyombo vya habari nchini Tanzania vilikuwa bize kutangaza kuhusu ajari ya meli iliyotokea mida ya saa nne ,siku ya jumapili.Kama ujuavyo Waswahili,huyu alisema vile na yule akasema hivi.Lakini mashuhuda wa ajari hii,walisema chanzo cha ajari hii ni wingi wa abiria na mizigo.Wingi huu ulisababisha uzito wa meli kuongezeka,na kupelekea meli ya Mv Unguja kuzama.Abiria wote zaidi ya mia mbili,walizama maji na hakuna mtu yeyote aliyeweza kupatikana akiwa hai au amekufa.Tanzania ilishangaa,Afrika na dunia nzima kwa ujumla.Hakuna ajari ambayo iliwahi kutokea huku wahanga wakishindwa kupatikana,jambo hili liliwafanya watu wengi kulihusisha tukio hili na ushirikina.
Kusema ukweli walikuwa sahihi!,mzee Jabir na mganga ndio chanzo cha ajari hii.Hawakuwa na njia nyingine ya kumshinda adui yao Juliet,msichana mrembo niliyemuua na kugeuka mzimu.Nguvu za nyoka wao,nyoka ambaye alitakiwa kupambana na Juliet,zilitegemea sana idadi ya watu ambao nyoka yule aliwameza.
“Hatimaye tumeshinda! Mkuu wetu Nyoka,nenda kamzuie Juliet asitoboe siri zetu”,ilikua ni ombi kutoka kwa mzee Jabir na mganga,ombi ambalo lilitolewa baada ya mkuu wao Nyoka kumeza watu wengi sana,watu ambao walikuwemo ndani ya meli ya Mv Unguja,na kupotea katika mazingira ya kutatanisha bila kuonekana tena,mala baada ya meli kuzama.
“Sawa vijakazi wangu,nitamzuia binti huyu asiweze kuwadhuru “,Nyoka yule wa ajabu, aliongea huku akipotea na kisha kutoweka kwenda kupambana na mzimu wa Juliet, mzimu ambao ulikuwa tayali umewasili kanisani kwangu.
……………………………
Kanisa langu lilikua kimya sana, hakuna aliyeamini maneno ambayo Juliet aliweza kuyaongea. Aliposema kuwa yeye ni mzimu, na mimi ndiye niliyemuua, hakuna aliyeweza kuamini maneno yake. Waumini wangu walibaki wakimtazama tu, bila kufanya jambo lolote lile. Lakini kwa upande wa wazazi wangu, walielekea kuamini kile ambacho mzimu wa Juliet uliweza kuongea kuhusu ubaya na maovu yangu yote ambayo nilikuwa nikiyatenda.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mwanangu mbona hakuelewi, ulikua wapi siku zote hizo “,mama yake Juliet, aliongea huku akinyenyuka sehemu ambayo walikuwa wameketi wanawake, lakini cha kushangaza alipojaribu kumkumbatia mwanae. Hapo ndipo alipoamini maneno ambayo Juliet aliweza kuyaongea, kwani mikono yake ilipitiliza na kujikuta akikumbatia hewa tu. Hatimaye pilikapilika zikaanza, kila mtu aliyekuwepo kanisani pale alitaka kuiokoa nafsi yake baada ya kushuhudia jambo lile la ajabu.
“Mama mimi sina mwili tena, mimi ni mzimu, mchungaji kaniua na kunitoa sadaka ,huwezi kunikumbatia mama, mimi sio binadamu! “,Juliet alimaliza kuongea sentesi ndefu, na kusababisha watu wengi waweze kumuogopa.
“Mchungaji alitaka kuua mpaka wazazi wake, lakini kwa sababu mimi sio binadamu, niliweza kutambua mipango yake yote na kuwaokoa wazazi wake wasifike nyumbani kwake “,Juliet alizidi kuongea kila kitu ambacho alikifahamu kuhusu mimi, hatimaye siri haikuwa siri tena, nilibaki nimesimama tu huku wananchi wenye hasira kali wakitaka kunishambulia kwa kipigo.
“Mwanangu mbona umekua mnyama kiasi hiki, kwanini usitafute pesa kihalali na wala sio kwa njia hizi haramu za kumtumikia shetani “,mama alifoka!, maneno yake makali yaliugusa moyo wangu, lakini yalipita sikio la kulia na kutokea sikio la kushoto.
Waandishi wa habari walikua makini kupiga picha, na kuchukua kila tukio ambalo lilikuwa likiendelea kanisani kwangu. Waliamini walifanikiwa kwa asilimia mia moja, kwani walipata taarifa nyingi na ushahidi wa kutosha kuweza kunichafua.
Ghafla nyoka wangu niliyekuwa nimemfungia katika chumba cha siri aliweza kuvunja mlango na kuingia kanisani. Alikuwa na njaa sana, na jambo la kwanza kulifanya, ni kuanza kummeza mwandishi wa habari mmoja aliyekuwa mlangoni akipiga picha za matukio yaliyokuwa yakiendelea. Kivumbi kikatimka upya!, kiwete aliyefata huduma ya maombezi, alitimka mbio ,mwenye mapepo alipata nafuu na kukimbia kuyaokoa maisha yake.
“Nifuateni mimi, kama unataka kuishi, kama hutaki kimbia sehemu ambayo unaijua wewe! “,Juliet aliongea huku wazazi wangu na wa kwake wakimfuata kila alipokuwa akienda, na kuwaongoza kutoka nje. Kila mtu aliyejaribu kupita njia tofauti na maelekezo yake aliishia kumezwa na nyoka yule niliyekuwa nikiishi naye.
Hatimaye radi zilipiga!, tetemeko la ardhi likapita kwa dakika kadhaa, ulikua ni ujio wa mkuu wa chama cha kishetani, chama cha wapinga kristo. Nyoka huyu mwenye vichwa vingi alifika kunipatia msaada, japo alikuwa amechelewa sana.
Camera mbalimbali zilikanyagwa na nyoka yule kufuta ushahidi ili nisiweze kuchafuliwa, lakini pia waumini wote walifutwa kumbukumbu kichwani na kusahau kila kitu ambacho waliweza kushuhudia. Isipokuwa watu wachache ambao waliwahi kutoka kanisani mapema, wakiwemo wazazi wake Juliet, pamoja na wazazi wangu.
“Kidogo nimejalibu kukusaidia, kazi iliyobakia ni kuua kila mtu ambaye alishuhudia, na kuamini maneno ya Juliet kisha kutoka kanisani mwanzoni kabisa! “,Joka lile kubwa liliongea, huku kanisani kukiwa kumebaki kweupe, huku viti vikiwa vimevunjika vipande vipande mithili ya mchanga, kwani vurugu za watu kuyaokoa maisha yao hazikuwa za kawaida.
“Sawa mkuu! “,niliongea bila wasiwasi huku joka lile likipotea kama upepo, huku likizindikizwa na radi nyingi pamoja na ngurumo za kutisha!, mimi niliongozana na nyoka wangu kuelekea ndani, nyoka ambaye tayali alipata chakula, japo hakuwa na nguvu nyingi kunilinda, kwani hakuweza kuwala wazazi wangu, watu pekee ambao nilitakiwa niwatoe kwake kama sadaka ili kumuongezea nguvu.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Japo siri zangu ziliwekwa wazi na Juliet, lakini kwa upande wangu sikuathirika na jambo lolote lile. Nyoka yule mkubwa ambaye alikua kiongozi katika chama chetu cha kishetani, alifuta kumbukumbu ya kila mmoja aliyeweza kuhudhuria ibada siku ya jumapili, na kushuhudia mambo ya ajabu ambayo mzimu wa Juliet uliweza kuyazungumza kuhusu mimi.
Sio hilo tu! lakini pia hakuna chombo cha habari chochote kile ambacho kiliweza kutangaza yale ambayo Juliet aliweza kuyaongea kanisani kwangu, kwani joka lile kubwa lilipoingia kanisani lilikanyaga na kuvunja vunja kamera zote za waandishi wa habari ambao walikuwa wakirekodi na kuchukua matukio mbalimbali kanisani. Kwani kila mwandishi wa habari alikimbia ili kuyaokoa maisha yake pale alipolishuhudia joka lile kubwa lenye vichwa vingi sana, huku nyoka mdogo ambaye nilikuwa nikiishi naye akimeza mtu yeyote ambaye alikutana naye uso kwa uso.
“Hatimaye maisha yanaendelea! lakini yaliyotokea jana ni changamoto kwangu, na kwa chama chote! Inatakiwa tutafute namna ya kumzuia Juliet bila hivyo, mwisho wetu utakua mubaya “,niliongea peke yangu huku nikiwa nimeketi sebuleni kwangu siku ya jumatatu, nikitafakali matukio yote ambayo yaliweza kutokea siku iliyopita. Lakini cha kushangaza waumini wengi walinipigia simu kama kawaida na kunipongeza kwa huduma nzuri ya mahubiri niliyoitoa jumapili iliyopita, jambo ambalo lilinifanya nigundue kuwa, hawakutambua chochote kile ambacho kiliweza kutokea.
“Haloo! pastor Hakika! barikiwa sana mtumishi wa Mungu, jana umehubiri vizuri mpaka nikatamani mshahara wote wa mwezi huu nikupatie wewe kama zawadi “,yalikuwa ni maneno ya muumini mmoja wa kiume, mmoja wa waumini kati ya wengi ambao walikuwa wakifanya kazi TRA, akinishukuru kwa huduma nzuri niliyoitoa siku iliyopita na kuniahidi donge nono mala tu mshahara utakapotoka.
“Habari mchungaji! yaani, jana umenifanyia maombi mpaka mguu wangu umepona kabisa, na leo kwa mala ya kwanza tangu nisumbuke kwa mwezi mzima nimeweza kwenda kazini”,ilikuwa ni sauti ya binti mmoja mrembo sana, binti ambaye alikuwa wa kwanza kumlaghai kimapenzi na kunikubalia, japo alikuwa na kazi nzuri sana, kwani alikuwa muhasibu katika benki kuu ya Tanzania (BOT), lakini alikuwa bado na tamaa ya pesa. Hakuridhika na mshahara wake mzuri ambao alikuwa akiupata, na hapo ndipo nilipotumia udhaifu wake kwa kumuhonga gari zuri sana aina ya hummer, na kupanua mapaja yake bila kipingamizi chochote kile. Lakini tangu nimuhonge gari lile, nyodo ziliongezeka mtaani na kuwadharau wengine hasa wenye kipato cha chini, alitembea huku na kule kwa mwendo mkali sana kwani trafiki wengi waliogopa kuisimamisha gari hii ya kifahari, huku wakimuombea njaa msichana huyu kwani alikua kero sana kila alipokuwa akiendesha gari lake jipya aina ya hummer, gari ambalo nilimuhonga na kisha kunipatia penzi, huku mimi nikimcheka na kumuona kama takataka baada ya kulala naye.
Hatimaye Doreen alipatikana! maombi ya wenye kipato cha chini ambao walimuombea njaa siku zote, kwani aliwamwagia matope kila alipopita na gari lake, maombi yao yaliweza kutimia. Doreen alipata ajari akiwa njiani mida ya jioni akitoka kazini, kwani gari lake breki ziligoma na kujikuta akigongana uso kwa uso na basi dogo aina ya costa, basi la daladala lakini cha kushangaza hakuna abiria yoyote yule aliyeweza kuumia, wala costa lile halikuweza kuharibika kifaa chochote kile, huku gari la Doreen likisagika kabisa na kumvunja mguu Doreen.
Kitendo kile kilimshangaza kila mmoja, hakuna mtu yeyote ambaye alikuwa na majibu ya ajari ile zaidi yangu mimi. Kwani ajari niliisababisha ili niweze kutoa kafara ndogo ya damu kwenye chama changu, damu ambayo ilitoka katika mguu wa Doreen. Isitoshe, nilitaka binti yule asizidi kulimiliki gari lile, gari ambalo lilikuwa mali yangu japo nilimpatia kwa kumuhonga. Hatimaye jeraha la Doreen lilianza kuoza siku hadi siku, kila hospitali waliweza kushindwa na kujikuta akikaa tu nyumbani kwa mwezi mzima akiuguza mguu wake.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Lakini nilishangaa akinipigia simu na kuniambia niliweza kumuombea na kumponya mguu wake ijumapili iliyopita, ijumapili ambayo ilijawa na matukio mengi na ya kushangaza sana kanisani kwangu. Sikujua ninani aliweza kufanya muujiza huu, na kufanikiwa kulisafisha jina langu.
“Hakikaa usishangae, wewe ni mshindi, !! Mimi mkuu wako nyoka ndiyo nimekusafishia jina lako, endelea na huduma yako kanisani kama kawaida, hakuna mtu yeyote anayetambua siri zako, wale wote ambao sikufanikiwa kufuta kumbukumbu zao kwani waliwahi kutokomea nimeshawaua isipokuwa wazazi wako pamoja na wazazi wake Juliet, ndiyo pekee waliobakia wanafahamu uovu wako, nimeshindwa kuwafanyia chochote kile kwani Juliet anawalinda “,hatimaye nilipata jibu kuhusu muujiza wa simu za kunipongeza, ambazo nilikuwa nikipigiwa. Sauti ya kutisha kutoka kwa mkuu wangu Nyoka, nyoka mwenye vichwa vingi sana ndiye aliyenifahamisha kuhusu jambo hilo alilokuwa amenifanyia na kulisafisha jina langu.
“Hapa angalau nina amani, lakini wazazi wangu, Juliet kawapendea nini?, kwanini anawalinda kiasi hiki “,nilijiuliza swali kutokana na kushangazwa na kile ambacho Juliet alionekana kuwafanyia wazazi wangu, kila jambo ambalo alikuwa akilifanya. Alihakikisha wazazi wangu wakiwa katika mikono salama.
“Nina wapenda sana wazazi wako, kwani hawana hatia, wamekuzaa kwa uchungu, badala uwalipe mema, unataka kuwaua kwa tamaa ya pesa “,nilishangaa kusikia sauti, sauti ambayo iliongea huku ikijirudia rudia mithili ya mwangwi. Bila shaka alikuwa ni Juliet! kwani sauti yake niliitambua vilivyo.
Niliangaza juu sehemu ambayo sauti ilikuwa ikitokea lakini sikuona kitu, niligeuka na kuangaza nyuma yangu sikuona tena kitu. Nikajikuta Hatimaye nikabaki nimepigwa na butwaa tu, nikiwa nimekosa nini niweze kufanya, kwani niliamini msichana yule angeweza kunifanyia kitendo chochote kile kutokana na ushujaa wake aliouonyesha mbele ya mganga pamoja na mzee Jabir na kuwashinda nguvu.
“Naamini unayoyafanya ipo siku utayaacha, nitapambana na wakuu wako na kuhakikisha nakutoa kwenye dhambi ambazo unazifanya “,Juliet alitokea kimaajabu na kuketi karibu yangu, katika sofa ambalo nilikuwa nimekalia sebuleni. NIilitamani kukimbia, lakini roho ilisita na kubaki nikiwa nimeketi tu nikimtazama msichana mrembo Juliet, huku akiwa amevalia gauni jeupe ambalo lilifunika mpaka unyayo wa miguu yake.
Kwa mbali nilitafakali maneno ambayo alikuwa ameniambia, kuhusu kunitoa kwenye chama changu cha kishetani. Nilijikuta nikicheka kwa sauti kubwa kama kichaa, niliona kama alikuwa akiota ndoto ya mchana kweupe. Sikuwa tayali kurudi kuishi maisha ya kimaskini, maisha ya kula chipsi kavu za shilingi elfu moja kwa siku nzima, maisha ya kuishi stoo. Nilikuwa tayali kutoa uhai wa mtu yeyote yule, kukwepa kurudi maisha niliyokuwa nikiishi zamani.
“Nina nguvu za kutosha kupambana na kukukomboa, naamini wiki hii itaisha ukiwa katika mikono salama.”,maneno ya Juliet yalinifanya nisitishe kicheko changu mithili ya dereva wa gari afinyapo breki ghafla, na kujikuta nikitafakali sentesi aliyomalizia kuiongea na kisha kupotea kama upepo mbele ya macho yangu.
Ilibidi ninyanyuke kuelekea katika chumba changu cha siri, chumba ambacho nyoka wangu alikuwa akiishi, nikaweze kuzungumza naye na kumwelezea kila kitu ambacho Juliet aliweza kukiongea, nisikie ushauri wake ambao angeweza kunipatia, pamoja na kunihakikishia usalama wangu.
Mzimu wa Juliet unafanya kila njia kwa ajili ya kuokoa maisha ya wazazi wangu, pamoja na wazazi wake. Kwa uwezo wake wa ajabu aliokuwa nao, aliweza kuona vita kali ambayo ilikuwa mbele yake. Chama cha kishetani kilikuwa na nguvu ya kutosha kumdhibiti, hasa nyoka mkubwa mwenye vichwa vingi sana ambaye alikuwa ndiye mkuu wa chama hiki cha kishetani.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Juliet anaamua kuwapeleka wazazi wangu, pamoja na wazazi wake, katika nyumba yao. Nyumba ambayo wazazi wake walikuwa wakiishi siku zote, nyumba ambayo Juliet aliweza kuishi na wazazi wake kabla sijamuua na kumtoa kafara. Haya yote yalitokea baada ya kutoka kanisani kwangu, siku ambayo alijalibu kutoa siri zangu, lakini nyoka wa ajabu mwenye vichwa vingi sana aliweza kumzuia na kisha kunisafishia jina langu.
“Wazazi wangu, pamoja na wazazi wa mchungaji! Hapa ndipo mahali sahihi pa nyie kukaa salama mpaka nitakapokamilisha kazi ya kumkomboa mchungaji kutoka katika utumwa huu wa kishetani, “
“Mwanangu hapa nyumbani kwetu patakuaje sehemu salama, halafu bado sijaamini yale uliyoyazungumza kanisani, ni kweli mchungaji kakuua “,
“Ndio kaniua, lakini nimerudi kumkomboa kwani hayo yote anayafanya bila kupenda, !! sala zenu ndizo zitakazo walinda mikononi mwa watu hawa wabaya “,
Yalikuwa ni mazungumzo ya Juliet pamoja na wazazi wake siku iliyopita, siku ya jumapili. Mala baada ya kutolewa haraka sana kanisani kwangu, huku Juliet akiwalinda na kuwaongoza watoke salama. Juliet baada ya kuhakikisha wazazi wangu pamoja na wazazi wake wakiwa katika mikono salama, alitoweka na kisha kuanza kazi ya kunikomboa na kuyabadilisha maisha yangu.
Alitakiwa kuninyanganya pete ya ajabu, kitambaa pamoja na maji ambayo nilikabidhiwa siku ya kujiunga na chama cha kina mzee Jabir. Hiyo ndiyo ilikuwa njia pekee ya kuweza kuniokoa, lakini haikuwa kazi rahisi kwani hakufahamu mahali ambapo nilikuwa nikitunza vifaa hivi ambavyo siku zote nilivitumia siku ya jumapili, na kufanya miujiza iliyonifanya nionekane kama nabii wa kweli.
Siku hiyo hiyo ya jumapili, Juliet alitoweka haraka sana kuelekea Bagamoyo, katika jengo ambalo aliishi mganga, sehemu ambayo yalikuwa ndio makao makuu ya chama chetu. Aliamini kuwa, huko ndiko angeweza kufahamu sehemu ambayo nilikuwa nikitunzia vifaa vyangu.
“Tayali nimefanikiwa kumkomboa kijana wetu,lakini inatakiwa ulinzi uimalishwe katika chumba cha siri, kwani Juliet akifika katika chumba kile na kuchukua vifaa vya kijana wetu, tayali kijana huyu tutaweza kumkosa katika chama chetu “,ilikuwa ni sauti ya Nyoka, nyoka ambaye alikuwa ndiye mkuu wa chama chetu Nyoka huyu alikuwa akizungumza na mzee Jabir pamoja na mganga, jioni siku ya jumapili. Hawakufahamu kama mazungumzo yao Juliet aliweza kuyasikia, kwani hawakuweza kumuona kutokana na nguvu zake alizokuwa nazo.
Juliet alikuwa tayali amefika katika jengo letu Bagamoyo, na kufanya sala ambayo ilimuwezesha asiweze kuonekana kama alikuwa ndani ya makao yetu makuu. Sala yake iliweza kufanikiwa, kwani alikagua jengo lote akitafuta mahali ambapo nilikuwa nikitunzia vifaa vyangu, lakini hakuweza kugundua kitu. Akiwa amekata tamaa na kutaka kuondoka, ndipo aliposikia mazungumzo ya mkuu wetu pamoja na mzee Jabir yakiendelea. Hatimaye aliweza kugundua mahali ambapo nilikuwa nikitunzia vifaa vyangu, katika chumba cha siri ambacho nilikitumia kwa ajili ya kuua na kutolea kafara.
Aliamini lazima kutakuwa na ulinzi, ilibidi akajipange na kufika katika nyumba yangu siku ya jumatatu Akiwa na nguvu za kutosha kwa ajili ya kupambana na mlinzi yoyote yule atakayemkuta katika chumba changu cha siri.
Hatimaye siku ya jumatatu iliweza kufika, ilionekana kuwa siku nzuri sana kwani kulipambazuka huku hali ya hewa ikiwa nzuri. Jua liliangaza, huku ndege wa angani wakiruka ruka na kuifurahia dunia. Dunia ambayo ilijaa maovu ya kila aina, huku binadamu walioumbwa na Mungu wakiichafua, na kuijazia uovu wa kila aina.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Juliet alifika katika nyumba yangu asubuhi siku ya jumatatu. Alizunguka kila kona ya nyumba yangu lakini hakuweza kugundua chumba changu cha siri. Sikuwa na uwezo wowote wa kutambua uwepo wake ndani kwangu, niliendelea kuketi sebuleni na kufikilia juu ya kitu ambacho kiliweza kutokea kanisani kwangu siku iliyopita. Lakini fikra kuhusu mahali ambapo wazazi wangu walikuwepo ziliponijia kichwani, nilishangaa sauti ya Juliet ikinijibu. Nilipogeuka huku na kule kutazama sehemu ambayo sauti ya Juliet iliweza kutokea, lakini sikuweza kumwona.
Ghafla alijitokeza, na kuonana na mimi uso kwa uso. Alama ya kisu ikiwa shingoni kwake, alama ambayo ilibaki siku ambapo niliweza kutenganisha kichwa na kiwiliwili chake na kumtoa kafara. Maneno ambayo Juliet aliweza kuyazungumza niliweza kuyapuzia, japo alionekana kuwa na nguvu nyingi za kunikomboa.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment