Search This Blog

MTEMI NYANTUMU - 3

 

    Simulizi : Mtemi Nyantumu

    Sehemu Ya Tatu (3)









    “,Hapana hawezi kunidhuru, nataka nimtendee haki Nyantu, huyu nyoka namuua kikatili tena kwa mikono yangu miwili …”,  Kijana hodari na shupavu aliyejiamini kupita maelezo,hakutaka kutengua msimamo wake wa kutumia upinde katika mapambano ili kuepuka kujeruhiwa na nyoka yule aliyeonekana kuwa wa ajabu.Kwani alikuwa na umbo kubwa sana,umbo ambalo alikuwa na uwezo wa kutafuna ng’ombe wawili pasipo kutetereka.



    Hatimaye Nyoni aliukamata upanga wake kwa nguvu,huku upinde akimkabidhi dada yake Matumaini.Joka lile likiwa linaendelea kusogea uelekeo wa Matumaini pamoja na Nyoni huku mdomo wake ukitisha sana kutokana na kutapakaa damu,hivyo basi kijana Nyoni akiwa ameshika panga lake lililong’aa kwa makali yake alikimbia ili kukutana uso kwa uso na joka yule ambaye alianza kuachama na kutoa meno yake nje ili kumkabili Nyoni …



    “Kaka kuwa makini, jitahidi nyoka huyo asikudhuru …”,



    “Usjali dada Matuma…a…”, Nyoni alishindwa kumalizia sentesi yake kwani alikutana uso kwa uso na joka yule, kitendo ambacho kilipelekea nyoka yule kurudi nyuma kwani upanga wa Nyoni ulikuwa umeelekezwa kwa joka lile na kulifanya kusumbuliwa na miale mikali ya jua iliyong’ara kwa sababu ya upanga kuwa mkali.



    Nyoni aliweza kuutambua udhaifu huu, aliamua kutumia fursa hii ili kumshambulia na kumuua nyoka yule mkubwa na wa ajabu sana. Bila kuchelewa aliunyosha upanga wake juu uelekeo ambao jua lilikuwepo licha ya uwepo wa miti mingi katika pori la Nyankonko, kisha alianza kuelekeza mionzi ya jua iliyogonga upanga wa Nyoni uelekeo ambao joka lile lilikuwepo huku akilisogelea. Hatiamaye macho ya Nyoka yule mkubwa aina ya chatu yalianza kupata wakati mgumu, kiasi kwamba kiumbe yule alishindwa kuona mbele wala nyuma na kubaki akiwa amesimama na kutulia kusubili msamaha wa kijana Nyoni …



    “Kaka muue, mchome haraka tukimbie …”,



    Yalikuwa ni maneno ya kumuhimiza Nyoni kukamilisha zoezi la kumuua nyoka mkubwa aina ya chatu, nyoka ambaye alimtafuna mbwa  aliyekuwa rafiki kipenzi wa Nyoni. Lakini Nyoni badala ya kusikiliza maagizo ya dada yake, aliendelea kupigwa na butwaa huku akimuumiza macho yule nyoka kwa mwanga wa jua ulio gonga upanga wake na kuelekea katika macho ya chatu, kiasi kwamba chatu yule aliyafumba macho yake ili kuepuka mateso yale. Kama walivyosema wahenga, ukimuona mtu katulia ujue anatunga sheria, msemo huu ulionekana waziwazi kwani Nyoni akiwa amejisahau kabisa na kumsogelea kiumbe yule mpaka usawa wa miguu yake, ghafla joka lile lilimvaa Nyoni na alimanusura lifanikiwe kumtafuna na kuambulia  kumukwalua Nyoni miguuni. Nyoni alipona kutoka kwenye mkasa huo baada ya kuruka haraka sana kwani hata yeye machale yalikuwa yakimcheza, lakini wakati akijaribu kujiokoa alibahatisha kumchoma nyoka yule tumboni na ukawa ndio mwisho wake …
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Hongera kaka, lakini pole kakuumiza mguuni ……”,



    “Asante, hatuwezi kuendelea na safari tupumzike kwanza tuponye kidonda changu. Kinauma sana ……”,



    “Kaka jikaze,hapa tuko katikati ya pori, tukilala hapa lazima wanyama hawa watatuua, tena wakikuta mwezao yuko karibu yetu akiwa amekufa, lazima tulipe damu ya ndugu yao …”,



    “Kweli dada yangu, ngoja nijikongoje kutoka mahali hapa “, hatimaye Nyoni alikubaliana na dada yake, taratibu alianza kujikokota huku Matumaini akimshika kwa nguvu ili asidondoke kwani jeraha lilikuwa kubwa sana japo walifunga kamba sehemu ya goti kuepuka sumu kupanda katika sehemu za juu za mwili……



    “Kanikwalua na meno yake, bila shaka sehemu ya sumu yake imepenya mwilini maana kidonda kimeanza kubadirika rangi …”,



    “Inawezekana kakuuma, ngoja tufike sehemu salama tukichunguze vizuri kidonda “, Nyoni akiwa na maumivu makali, mumivu ambayo yalimtatiza sana kwani hakutambua kama aling’atwa na nyoka yule au alijeruhiwa tu kwani maumivu aliyoyasikia hayakuwa ya kawaida, na hawakupata muda wa kupeana huduma ya kwanza kutokana na mazingira waliyokuwepo kuwa ya hatari.



    “Nina imani kakung’ata, huwezi kusikia maumivu makali kiasi hicho mpaka ushindwe kutembea “,



    “Hapana, kanikwalua tu! maumivu haya ni kwasababu sijapata huduma ya kwanza kupunguza maumivu, angening’ata ningeshindwa hata kutembea kwa kuchechemea …”,



    Yalikuwa ni mazungumzo kati ya mtu na dada yake, mazungumzo ambayo yaliendelea wakati wakitembea taratibu kwa umakini wa hali ya juu kutoka katikati ya pori la Nyankonko.



    ……………………………



    Mtemi Nyantumu akiwa na hasira sana kwani amli aliyopewa kutoka kwa mzimu Nkuru ilikuwa ya hatari sana, hatari ambayo ingepelekea Mwantema kupata majanga ya kila aina kama Nyoni na Matumaini wakifanikiwa kutoroka bila kupatikana …



    Kama alivyopewa majukumu na mzimu Nkuru, safari ambayo ilikuwa ni ya kundi la pili kumfuatilia Nyoni iliweza kuanza, huku mtemi akiwa ndiyo kiongozi mkuu …,hakua na sababu ya kukaa ikulu mala baada ya kutoka kwa mzimu Nkuru, aliwaongoza askari wake kukamatilia siraha, na kuianza safari ya kuelekea pori la Nyankonko. Pori ambalo liliogopwa kwa kuwa na wanyama wenye sumu kali, wanyama ambao walikuwa na maumbo makubwa pasipo kawaida …



    ……………………………



    “Tupiteni njia hii ya mkato, bila shaka wamepita hapa ……”,



    “Weeeeh, hatuwezi kupita njia hiyo ya mkato inayopita katikati ya pori, nina imani hata Nyoni hawezi pita njia hiyo kwani ni hatari sana kwake, halafu hana nguvu kazi ya kutosha kupambana ……”,



    “Jamani tupite hapa njia ya mkato, nina imani wamepita hapa simnaona nyayo za miguu zimeishia hapa ……”,



    “Hapana, pita peke yako porini huko ufe kama sisimizi. Nina imani hakuna binadamu mwenye akili timamu na kujiamini kiasi hicho kupita njia hii hatari ya mkato, tuendeleeni na barabara hii tukawakamate …”,



    “Igweeeh, mimi ndio mkuu wa msafara huu!  tupite barabara kubwa, Nyoni na dada yake hawawezi kupita njia ya mkato lazima waya tetee maisha yao ……”,



    Yalikuwa ni mabishano baina ya kundi la kwanza la askari wa mtemi Nyantumu, mabishano ambayo yalihitimishwa na maamuzi ya kiongozi wao. Maamuzi ambayo yaliwafanya askari wa mtemi Nyantumu kuiacha njia ya mkato ambayo Nyoni na Matumaini walipita, na kusonga mbele kuwasaka kwa kupita barabara kubwa ya kuelekea kijiji cha Ukarimu, barabara ambayo ilikuwa ya kuzunguka kufika Ukarimu tofauti na njia ya mkato ambayo walipita Nyoni na dada yake, njia ambayo ilikua ya hatari kupita maelezo ……http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Nyoni aliendelea kusonga mbele japo alikuwa na maumivu makali katika mguu wake mala baada ya kujeruhiwa na nyoka ambaye alipambana naye muda mfupi uliopita. Japo Matumaini alikuwa mtoto wa kike,lakini ilibidi achukue jukumu la kumuongoza kaka yake katika safari ya kuelekea kijiji cha Ukarimu. Matumaini alitumia mkono wake wa kushoto kumpatia sapoti ya kutembea kaka yake Nyoni, huku mkono wa kulia akiutumia kufyeka matawi ya miti ambayo yalijitokeza katika njia ya mkato waliyopita. Njia ambayo haikupitwa na watu kwa miaka mingi sana kutokana na tetesi za uwepo wa wanyama hatari katika njia hii …



    “Dada mguu unauma! tupumzike mahali hapa, siwezi kuendelea na safari”,



    “Sawa kaka, ngoja tupumzike na kutibu kidonda chako ……”, dada yake Nyoni aliongea huku akikata matawi na kisha kuyatandika pembeni ya kinjia kidogo walichokuwa wakikitumia kuelekea kijiji cha Ukarimu, njia ambayo ilisemekana kuwa ya mkato kutokana na historia ya kijiji cha Mwantema.



    “Kidonda kitakauka, hajaning’ata bali kanikwalua tu. “,Nyoni aliongea huku akitazama kidonda chake mala baada ya kujipumzisha katika matawi ambayo Matumaini aliyakata na kuyatandika chini ……



    Lakini kipindi Nyoni akizungumza kuhusiana na hali ya kidonda chake, Matumaini alikuwa bize kuchunguza kitu cha ajabu ambacho alikiona katika kichaka kilichokuwa karibu na mahali walipokuwa wamejipumzisha.



    “Kaka! “,



    “Naam dada! “,



    “,Ona kulee kichakani …”,



    “,Wapi? “,



    “Kichaka kile pale, upande wako wa kushoto …”, ilikuwa ni sauti ya Matumaini, akimshirikisha kaka yake kuhusiana na kitu alichokishuhudia katika kichaka. Kitu ambacho kiling’ara na kuonekana kuwa cha ajabu sana …



    “Nenda kakichukue ukilete hapa! “,



    “Hapana kaka! mimi ninaogopa kwenda kichakani peke yangu ……”,



    “Sasa unaogopa nini? tumepita por,i msitu na vichaka vingi vinavyotisha  mpaka kufika mahali hapa, na isitoshe tumekutana na wanyama wa ajabu na wa kutisha bado hujawa jasili tu ……”,



    “,Hapana kaka, mimi naogopa. Twende wote ……”,



    “,Mimi siwezi kunyenyuka kutoka mahali hapa, kidonda kinauma sana! “, Nyoni aliamua kueleza hali halisi kuhusiana na hali mbaya aliyokuwa nayo, kwani kidonda chake kiliuma kupita kawaida kiasi kwamba hakutambua angejilinda vipi yeye pamoja na dada yake kama ingetokea hatari yoyote dhidi yao hasa wanyama wakali wa pori la Nyankonko ……



    “Sawa dada, ngoja niende “, msichana mrembo sana, msichana ambaye aliitwa Matumaini na dada yake na kijana hodari aliyeitwa Nyoni. Aliamua kujitoa muhanga kuingia katika kichaka, ili kuchukua kitu ambacho kilionekana kung’aa sana hasa kilipowekwa katika jua.



    ………………………………



    “Jamani tangu tutembee hatuoni dalili zozote za kuwafikia Nyoni pamoja na dada yake ……”,



    “Mimi niliwambia! Hii njia siyo, hawajapita huku lakini mlinibishia …”,



    “Kwa dalili hii ulikuwa sahihi, tumeamini hawajapita njia hii ……” ,



    “,Wangepita njia hii mbwa wasingebaki nyuma yetu, bali wangetutangulia kama mwanzo na kuendelea kufuata miguu ,lakini sielewi walifanyaje mpaka mbwa wetu walishindwa kugundua njia sahihi. Sasa mimi ndio kiongozi wenu, kama nilivyowaruhusu kupita njia hii. Naomba turudi na kupita njia ya mkato ……”,Sauti ya kiongozi wa kundi la kwanza, kundi la askari wa mtemi Nyantumu. Alizungumza na kuhitimisha mazungumzo ambayo yaliendelea miongoni mwao, mala baada ya kugundua kuwa walikuwa wamepotea njia. Kwani walitembea kwa muda mrefu, bila kuona dalili zozote zile kuhusiana na Nyoni pamoja na Matumaini. Hakuwa na budi kusitisha safari ya kusonga mbele, na kuamua kurudi nyuma ili waweze kupita njia ya mkato ……



    …………………………………



    “Wuuuu wuuuuh wuuh “, mbwa walikatiza njia ya mkato kwa kasi sana, na kuiacha njia kubwa ambayo kundi la kwanza walipita na kisha kupotea. Ni baada ya kugundua miguu ambayo mbwa wa Nyoni aliweza kupita, baada ya kunusa nyayo za miguu zilizoachwa kwa masaa kadhaa, kitendo cha mbwa wa kundi la kwanza kushindwa kupewa nafasi katika kunusa harufu ndicho kilichopelekea vijana wa kundi la kwanza kupita njia isiyo kuwa sahihi, tofauti na mbwa wa kundi la pili ambao walipewa muda mwingi katika uchunguzi. Chini ya usimamizi mkali wa mtemi Nyantumu …



    “Bila shaka wamepita njia hii ya mkato, songa mbele usiogope!”, mtemi Nyantumu akiwa amebebwa huku yeye akiwa ameketi juu ya kiti chake,aliwahimiza vijana wake waweze kusonga mbele.Kwani walisita kuwafuata mbwa waliokatiza njia ya mkato iliyosemekana kuwa hatari sana,na kubaki wakisubili kauli ya mwisho kutoka kwa mtemi Nyantumu…



    “Ninasema songa mbele,sitaki askari waoga katika jeshi langu……”, Kwa ukali mtemi Nyantumu aliwafokea vijana wake mala baada ya kuzitambua nyuso za uoga katika fikra zao,na haraka sana askari wake waliendelea kusonga mbele kwani sauti hiyo ya ukali waliitambua vilivyo.Siku zote haikumuacha mtu yeyote salama,kama alifanya upuuzi ambao haukuungwa mkono na mtemi Nyantumu……



    ……………………………http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Asante kwa kunisafisha……,nilitupwa hapa miaka mingi iliyopita ,hakuna aliyewahi kuniokota kutokana na uoga wa watu kupita njia hii……”,



    “Mamaaaaa! “, Matumaini alipiga kelele kwa uoga mala baada ya kusikia jiwe aliloliokota likizungumza.Kwani alilisafisha kwa kitambaa,huku akitumia mate yake kulifanya lizidi kung’ara.Katika hali isiyokuwa ya kawaida,jiwe lile la ajabu lilimshukuru Matumaini kwa wema alioufanya…



    “Igweeee mzimu Ntema,nakusalimu”, Nyoni akiwa ameketi palepale alipokuwa amepumzika mwanzoni ,alipiga magoti kisha kutamka maneno ili kujidhibitisha kwa kile alichokifikilia.Aliweza kugundua jiwe lile ambalo lilimtisha Matumaini na kulitupa halikuwa jiwe la kawaida,bali ni mzimu Ntema.Mzimu ambao uliabudiwa na Wanamutema miaka mingi iliyopita kulingana na historia aliyosimuliwa Nyoni na wazazi wake.Hivyo basi kutokana na urafi wa madaraka,na kupenda umaarufu.Ukoo wa Nyantumu ulitaka kujipatia sifa hizo na kuitawala Mwantema,hawakuwa na jinsi zaidi ya kusafiri mpaka kijiji cha Ukarimu.Huko waliweza kupatiwa siri ya kuongoza Mwantema na kiongozi wa kijiji hicho kwani walimuahidi kumpatia zawadi ya mazao na mifugo.Jambo ambalo lilikuwa adimu katika nchi ya Ukarimu,kwani walitegemea asali pamoja na matunda kama chakula.Kutokana na kiongozi wa kijiji cha Ukarimu kuchoshwa na maisha magumu ya watu wake,ilibidi atumie nguvu zake za kishirikina kuwasaidia ukoo wa Nyantumu kutawala Mwantema.



    Mtemi wa Ukarimu aliwapatia mti wa ubuyu wakaupande nje ya mji wa Mwantema,kisha wakauabudu kila mwisho wa mwezi na kutoa kafara ya Mbuzi.Kafara ambayo ilifanyika kwa kunyunyizia damu ya mbuzi aliyechinjwa katika mizizi ya mti ule.Kisha shariti la pili, waibe mzimu Ntema kutoka kwa mtemi aliyekuwepo madarakani na kwenda kuutupa katika pori la Nyankonko.Baada ya mti kutimiza miaka mitano,mtemi wa Mwantema atakufa kwa maradhi ya ghafla,kisha ukoo wa Nyantumu utateuliwa kuongoza kijiji bila mtu yoyote kujitambua.



    Shariti la tatu na la mwisho,wasichana wote watakaozaliwa baada ya mtemi Nyantumu kuingia madarakani.Watatakiwa kukeketwa na yoyote atakaye kiuka agizo hili,atatakiwa kuuawa.



    Hivyo basi mtemi Nyantumu aliingia madarakani na kushindwa kutimiza ahadi yake kwa kiongozi wa kijiji cha Ukarimu.Isitoshe alizuia raia wote kusafiri na kuingia kijiji cha Ukarimu kulinda siri yake iziweze kufahamika,ndipo kijiji cha Ukarimu kilianza kujuta baadaye.Kwani wananchi wa Mwantema waliteseka bila kujua chanzo,ndipo walipoamua kuwafahamisha watu wachache kuhusiana na siri hii hasa ukoo wa mzee Mbutu.Kwa kutumia shujaa mmoja wa Ukarimu aliyefanikiwa kuvuka pori la Nyankonko salama ,lakini aliliwa na wanyama wakati akirudi baada ya kufanikisha kufikisha ujumbe kwa ukoo wa mzee mbutu ,ukoo ambao ulifanya biashara na kijiji cha Ukarimu kabla ya kukatwaza na mtemi Nyantumu…



    “Aiweeh raia wangu mwema ,mimi ndio Mzimu Ntema,vipi umejuaje kuhusiana na mimi”, hatimaye mzimu Ntema alimjibu Nyoni ,huku Matumaini akishangaa mazungumzo baina ya Nyoni na jiwe lile.



    “Baba aliwahi kunisimulia kuhusiana na wewe,lakini sikuwahi kuamini..Lakini nilipo ona ukizungumza na kung’ara nilikumbuka simulizi niliyosimuliwa”,



    “Kwahiyo hujui kijiji cha Ukarimu unafuata nini?”,



    “Ndio sifahamu……”,



    “Sawa,unatakiwa ufike kwa mtemi wa kijiji cha Ukarimu.Kisha umwambie aukate mti wa mzimu Nkuru,utaenda na mimi nikikulinda na wanyama wakali wa pori hili,wanyama ambao mzimu Nkuru aliwaweka kuzuia watu wasivuke na kuingia Ukarimu kupinga uongozi wake na wa ukoo wa Nyantumu.Zamani hawakuwepo wanyama hawa”, jiwe la mtemi Ntema lilizidi kuongea huku Matumaini akilishika bila uoga,kwani alitambua kila kitu baada ya kusikiliza mazungumzo



    “Sawa nimekuelewa ,lakini mbona husimami mahali ulipo?”,



    “Nimekwaluzwa na Nyoka wa msitu huu,”



    “Matumaini nisogeze karibu na jeraha kisha kaka yako atapona”,



    “Umelijuaje jina langu?,”



    “Nilijua kabla hujazaliwa,na nilifahamu kuwa wewe ndiye utakuwa chanzo cha mimi kutoka katika msitu huu,ndio maana ulichelewa kuzaliwa ili kaka yako akue na kupata nguvu za kupambana”,



    “Duuuuh ,igweeeh mzimu Ntema na utemi wako urudi na kudumu milele”, Hatimaye Matumaini alitabasamu baada ya kuona jeraha la kaka yake likikauka ,mala baada ya kugusisha jiwe la mzimu Ntema katika kidonda cha Nyoni.Aliamini mzimu wao Ntema hakuwa katili kama Nkuru,ndio maana alikubali kumsujudia na kumuheshimu…



    Hali ya utulivu ilitawala katika pori la Nyankonko, isipokuwa ndege ambao waliruka ruka huku wakiimba nyimbo nzuri zilizomvutia mtu yoyote yule ambaye alikuwepo ndani ya pori hili hatari sana, pori ambalo lilijaa wanyama wengi wenye sumu kali. Wanyama ambao waliwekwa na mzimu Nkuru kwa ajili ya kupambana na mtu yoyote yule aliyeingia ndani ya pori la Nyankonko kwa lengo la kuelekea kijiji cha Ukarimu kutafuta dawa ya kupinga mila hatari ya ukeketaji katika kijiji cha Ukarimu …



    Siyo hilo tu, bali wanyama hatari wa pori la Nyankonko walilinda msitu ili asitokee mtu yeyote wa kupita njia ya mkato na kuokota mzimu wa kijiji cha Mwantema. Mzimu ambao uliabudiwa miaka mingi iliyopita kabla ya Nkuru, na kutupwa na ukoo wa Nyantumu katika pori hili kwa lengo la kuitawala Mwantema.



    Huo ndio ukawa mwanzo wa maisha magumu ya Wanamutema, kwani walianza kumuabudu mzimu Nkuru mala baada ya mtemi Nyantumu kuingia madarakani huku wasichana wa kijiji wakifanyiwa mila hatari ya ukeketaji na kupelekea vifo vingi kuongezeka. Kwani watoto wa kike walipoteza damu nyingi sana zilizopelekea vifo vyao, wakati wakifanyiwa mila hii hatari. Pia koo zote ambazo zilipingana na amli hii ya mtemi Nyantumu pamoja na mzimu Nkuru ziliuawa kikatili huku maiti zao zikifukiwa chini ya mti wa mzimu Nkuru.…

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    ………………………………



    Kundi la pili la askari wa mtemi Nyantumu liliendelea kusonga mbele kumtafuta kijana Nyoni pamoja na dada yake waliotumia njia ya mkato iliyopita katikati ya pori la Nyankonko kuelekea kijiji cha Ukarimu, lakini njia hii waliyopita ilikuwa ya hatari sana huku ikiwa na wanyama wakali kwani ndio njia pekee ambayo mzimu Ntema aliweza kutupwa na ukoo wa Nyantumu miaka mingi iliyopita ili waweze kupata madaraka ya kuitawala Mwantema na kuanza kumuabudu mzimu Nkuru. Mzimu ambaye alisaidia kuweka wanyama wengi wakali katika njia hii ili watu wasifanikiwe kupita, na utawala na mzimu Nkuru pamoja na mtemi Nyantumu uzidi kudumu …



    “Songa mbele!  lazima tuwakamate wapuuzi hawa kabla hawajafika mbali na kuharibu kila kitu ……”,



    “Hapana mtemi, mbele kuna tatizo! ” ,



    “Nimesema acheni uoga!songa mbele!  bila kuwa jasili kijana huyu atafahamu siri zetu, akimuokota mzimu Ntema. Utemi wangu utaishia hapa ……”, mtemi Nyantumu alizidi kulihimiza jeshi lake kusonga mbele, lakini askari wake waligoma. Kwani waliona kitu ambacho kilizuia njia mita kadhaa kutoka mahali walipokua.



    “Hebu nishusheni chini, nione kitu ambacho kinawafanya mshindwe kusonga mbele ……”,



    “Sawa mtemi wetu, udumu milele igweeeh ” ,



    Hatimaye mtemi Nyantumu aliamua kuutwaa mzigo ambao ulitaka kuwalemea askari wake, kwani uoga ulitawala mala baada ya kushindwa kukitambua kitu ambacho kilizuia njia umbali wa mita kadhaa kutoka mahali walipo kuwa. Kutokana kusikia historia ya msitu, na wanyama hatari ambao mzimu Nkuru aliwaweka. Walishindwa kuwa jasili, na kujikuta wakikataa katu katu kusonga mbele.



    Kitendo cha kundi hili kuwa na askari wachache sana tofauti na kundi la kwanza ambalo lilipotea njia, kilisababisha kundi hili la pili washindwe kujiamini kwani hawakua na siraha za kutosha kupambana, na isitoshe walikuwa wachache kwani hawakutegemea kama wangekuja ndani ya msitu huu. ……



    Mtemi Nyantumu aliomba ashushwe kutoka kwenye kiti chake, ili ashuhudie kwa macho yake kitu ambacho kilisababisha msafara ghafla. Kitendo ambacho kilimshangaza zaidi na zaidi, hata mbwa wake aliowaamini katika mawindo na upelelezi walishindwa kuendelea na zoezi la kuongoza msafara huku wakinusa mahali ambapo Nyoni na Matumaini waliweza kupita. …



    “Wuuuuuh wuuuuh ……”,



    “Songa mbele washenzi nyinyi, mnabweka tu kumbe waoga wakubwa.” , mtemi Nyantumu aliwafokea mbwa ambao walionekana kutazama kwa umakini kiumbe ambacho kilizuia njia, na kujikuta wakibweka huku wakiogopa kusogea kwani walikuwa tayali wameshanusa harufu na kuhisi uwepo wa hatari mahali pale …



    “Wuuuh wuuuh “, mbwa walipuuzia maneno ya kejeli kutoka kwa mtemi Nyantumu, bali waliendelea kupaza sauti kwa kutumia midomo yao kuashiria hatari katika eneo ambalo walikuwepo, hasa kiumbe ambacho kiliweza kulala barabarani na kuzuia njia …



    “Lile ni gogo au Nyoka?  Kama ni nyoka, nyoka gani mkubwa kiasi kile mwenye uwezo wa kumeza hata tembo? na kama ni gogo, kwanini linaonekana kujikunja kiasi kile mithili ya nyoka na lina mabaka ……”,



    “Hata sisi hatufahamu mtemi, ndio maana tumeshindwa kusonga mbele kwani tunaweza kushambuliwa na kuuawa ghafla bila kutegemea. “, askari mmoja miongoni mwa askari wanne wa mtemi ambao walifanya kazi ya kunyenyua kiti chake kikubwa, alimjibu mtemi swali lake ambalo lilionesha waziwazi kuwa mtemi Nyantumu hata yeye alishindwa kutambua kitu ambacho kilizuia njia yao wasiweze kupita ……



    “Wuuuuu wuuuu wuuuu wuuuuuh … “,mbwa wa mtemi Nyantumu walizidi kubweka pale mtemi Nyantumu alipotaka kuelekea sehemu ambayo kulikuwa na kikwazo, kitendo cha mbwa kubweka kilimfanya mtemi kuchezwa na machale …



    Alipojaribu kufikilia madhara atakayo yapata kama Nyoni pamoja na Matumaini wakifanikiwa kutoroka mpaka kijiji cha Ukarimu, na kuipata dawa waliyoifuata huko ya kupinga mila hatari ya ukeketaji kijijini Mwantema. Au wakifanikiwa kumuokota mzimu Ntema aliyetupwa miaka mingi iliyopita kando ya njia ya mkato katika pori la Nyankonko kuelekea kijiji cha Ukarimu. Ujasili ulimuingia ghafla, ni bora afe kuliko kushuhudia utawala wake ukianguka na kupotea kama upepo. Aliendelea kusonga mbele kwa kutembea kusogelea kikwazo kile, licha ya mbwa wake kuzidi kubweka wakimtahadharisha kwa kitendo cha hatari alichokuwa anakifanya ……



    “Igweeee, mlungu Nkuru!! walituongola na hatari …”, (igweeeh mzimu Nkuru, umetuepusha na hatari ……”,  mtemi Nyantumu alivuta pumzi ndefu, kisha akamshukuru mzimu Nkuru kwa kuwaepusha na hatari dhidi ya mnyama yule hatari kwa kutumia lugha ya Kimutema. Alimtambua kuwa alikuwa ni nyoka, tena aina ya chatu aliyekuwa ameuawa kikatili kwa kuchomwa na panga. Bila shaka aliamini askari wake wa kundi la kwanza ndio waliyo wafanya shughuli hiyo, kwani walikuwa wa kwanza kumfuatilia Nyoni na dada yake. …



    “Kuna nini mtemi! “,



    “Ni nyoka mkubwa aina ya chatu ndiye amezuia njia, lakini ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali bila shaka ni askari wetu waliotangulia. Kwani siraha kama hizi zinapatikana Mwantema pekee ……”, mtemi Nyantumu aliendelea kutamba, bila kutambua kuwa Nyoni ndiye aliyepambana na nyoka yule kisha kumuua huku yeye akijeruhiwa katika mguu wake. Jeraha ambalo liliponywa na mzimu Ntema baada ya kuokotwa na Matumaini pembezoni mwa njia …



    “Duuuuh kweli msitu huu ni hatari, nyoka gani mkubwa kiasi hiki ……”, askari wa mtemi Nyantumu walianza kujongea taratibu sehemu ambapo mtemi Nyantumu alikuwepo, karibu na Nyoka aliyekuwa ameuawa. Kama ilivyokuwa kwa mtemi Nyantumu, askari wake walionekana kushangazwa sana na umbo kubwa la nyoka yule …



    “Tayali giza limeanza kuingia, kwa aina hii ya wanyama inabidi tulale mahali hapa. Hatuwezi kuendelea na safari ……”, mtemi Nyantumu alizungumza na askari wake, kwani hata yeye uoga ulianza kumtawala baada ya kumshuhudia kiumbe yule. Hakuona sababu ya kuendelea kusonga mbele na kuyaweka maisha yao hatarini zaidi,ilibidi waweke kambi ya siku moja mahali pale kisha kuendelea na safari yao siku inayofuata  …



    “,Kweli mtemi, ni bora kukutana na viumbe kama hawa majira ya mchana kuliko usiku …”,



    “,Ndio, lakini hata usiku wanaweza kutuvamia tukiwa mahali hapa, kwahiyo ni kuomba ulinzi wa mzimu Nkuru atuepushe na wanyama hawa aliowaweka kwa ajili ya kulinda msitu huu …”, mazungumzo yalizidi kuendelea baina ya mtemi Nyantumu na jeshi lake. Huku baadhi ya askari wakianza harakati za kuweka mahema, na askari wengine wakiendelea kumshuhudia chatu yule …



    ……………… …………………



    “Wuuuu wuuuh wuuuh “,



    Mbwa wa kundi la pili walibweka huku wakikata kona kutokea barabara kuu ya kuelekea kijiji cha Ukarimu, kisha kupita njia ya mkato ambayo mtemi Nyantumu na jeshi lake waliweza kupita. Kwakuwa walikuwa tayali wameshapoteza muda mwingi, ilibidi wakaze mwendo kuwafuatilia Nyoni pamoja na dada yake.



    “Songa mbele, kazeni mwendo tukawakamate wapuuzi hawa. Lakini kuweni makini na njia hii, chochote utakacho kiona usisite kutumia siraha yako ……”, kiongozi wa kundi la pili aliendelea kuongoza kundi la kwanza ambalo lilikatiza njia ya mkato, huku mbwa wakiongoza msafara huu ambao mwanzoni ulikuwa umepotea.



    ………………………………http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Chochote ambacho mtakiona, msiogope kunitumia kujilinda “, jiwe la mzimu Ntema ambalo liling’aa kupita maelezo ,likiwa limeshikwa vizuri na Matumaini. Liliahidi kutoa ulinzi kwa Nyoni pamoja na dada yake, pale litakapotumiwa wakati wa hatari, njiani kuelekea kijiji cha Ukarimu …



    “Sawa mzimu wangu Ntema, utawala wako urudi na kudumu milele”, kwa heshima kubwa kijana Nyoni alimjibu mzimu Nkuru, na kuendelea na safari ya kuelekea kijiji cha Ukarimu licha ya giza kuanza kuingia. Kwani tayali walikuwa wamepumzika vya kutosha …



    Kijiji cha Ukarimu;



    Mtemi wa kijiji cha Ukarimu alikosa amani muda wote, moyo wake ulimsuta kwa makosa aliyoyafanya miaka mingi iliyopita kumsaidia mtemi Nyantumu kuingia madarakani katika kijiji cha Mwantema. Kwani damu nyingi ilimwagika na vifo vya raia wengi kutokea katika kijiji cha Mwantema, wakati wa utawala wa mtemi Nyantumu.



    “Magonjwa haya tunayo yapata, njaa na ukame katika kijiji chetu ni laana za makosa tuliyoyafanya. Kwa sasa hatuna asali ya kutosha pamoja na matunda kwa ajili ya chakula ……”, mtemi wa kijiji cha Ukarimu alishauriana na wazee wa kijiji, ili waweze kutambua namna ya kujikwamua kutoka katika hatari ya wanakijiji wote kufa kwa njaa …



    “Lakini miaka kadhaa iliyopita si tulituma mtu kuwafahamisha ukoo wa Mbutu kuhusiana na siri hii ……”, mzee aliyeonekana kuwa na umli wa miaka zaidi ya tisini, mmoja kati ya wazee tisa wa baraza la wazee la kumshauri mtemi wa kijiji cha Ukarimu. Alizungumza kuhusiana na tukio ambalo walilifanya miaka kadhaa iliyopita kutuma mjumbe kijiji jirani cha Mwantema, lakini hawakuweza kupata majibu kutoka kwa mtemi kuhusiana na jambo hilo …



    “Ujumbe aliufikisha sehemu husika, na walimsimulia mtoto wao wa kiume kuhusiana na jambo hili kabla hata binti yao hajazaliwa. “, mtemi aliweza kuwafahamisha wazee wa baraza lake, na kufanya kikao kukalibia kufikia muafaka …



    “Sasa kama alishatambua siri hii, na msichana ameshakua halafu wamekataa kumfanyia mila. Bila shaka lazima watoroke kuja huku kutafuta dawa ……”, mzee mwingine alichangia na kuzungumza jambo muhimu ambalo liliungwa na kila mtu aliyehudhulia baraza lile la wazee.



    “Ndio, nina amini watakua njiani wanakuja huku kwani kwa muda huu atakuwa tayali ameshafikisha miaka inayo takiwa. Lakini mtemi unauwezo mkubwa wa kutambua kinachoendelea kijiji cha Mwantema, siufanye hivyo ” ,



    “Kadri mti wa mzimu Nkuru unavyozidi kukua, ndio nguvu zake zinaongezeka. Kwahiyo mti wake umekua kiasi kwamba umenizidi nguvu na kunizuia nisitambue chochote kinachoendelea ili kumtoa madarakani yeye pamoja na Nyantumu. Na siwezi kuukata mti ulioko huku mpaka mzimu Ntema upatikane na kuwa mahali salama, hapo ndipo tutafanikiwa kuwatoa madarakani na mambo yetu yatanyooka ……”,



    “Kama ni hivyo, kwa nini tusitume jeshi letu kuingia msituni kutafuta mahali alipotupwa mzimu Ntema, kuliko kuwasubili watoto wa mzee Mbutu wafike mahali hapa …”,



    “,Hilo nalo liko sahihi tufanye hivyo …”,



    “,Hata mimi naunga mkono, tutume askari msituni kulikamilisha jambo hili. Bila hivyo laana itaendelea kututafuna …”,



    “,Sawa, nimekubali kutuma jeshi msituni. Huu ndio mwisho wa kikao chetu igweeeh “, mtemi wa kijiji cha Ukarimu alihitimisha kikao, kisha kuanza mipango ya kulituma jeshi lake porini kumtafuta mzimu Nkuru. Mzimu ambao ulikuwa na umbo kama la jiwe, huku liking’aa kama almasi.



    Hawakuwa na budi kuanza mipango ya kumtoa Mtemi Nyantumu madarakani wao wenyewe, ili kujiepusha na laana ambazo ziliwakabili na kupelekea vifo katika nchi yao kutokana na njaa. …



    Kwani wao ndio walikua chanzo cha matatizo yote ya Wanamutema, matatizo ambayo yalipelekea damu nyingi za watoto wa kike kumwagika bila hatia yoyote …



    …………………………………



    Mwamutema ;



           “Baba Nyoni ……”,



    “,igwee mama Nyoni …”,



    “,Mbona kimya, unawaza nini? “,



    “,Usalama wa wanangu, ndiyo unanifanya nikose furaha …sijui huko waliko ni wazima au wamekufa?  Je watafanikiwa kufika kijiji cha Ukarimu na kurudi huku wakiwa salama?  Pia yale ambayo tuliambiwa kuhusu siri ya mtemi Nyantumu, na tukaambiwa tufuate dawa kijiji cha Ukarimu kupinga mila hii na utawala wake ni ya kweli au tulidanganywa ……”,  baba yake Nyoni alidondosha chozi, japo aliwaruhusu watoto wake kutoroka na kwenda kutafuta dawa ya matatizo yao. Lakini hakuamini kuhusiana na uwepo wa dawa hiyo, na isitoshe hakuamini kama mtemi Nyantumu alitumia njia za kishirikina kuingia madarakani licha ya kusimuliwa kila kitu na mjumbe aliyetumwa kwake kutoka kijiji cha Ukarimu. Mjumbe ambaye alifikisha ujumbe salama, lakini alijikuta akitafunwa vibaya na simba wa pori la Nyankonko wakati akirudi.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “,Hata mimi pia, nina hofu tuliyo ambiwa hayakuwa ya kweli kwani mpaka sasa siku zinakimbia hatuoni jibu lolote lile. Halafu pia, hata wao wanauwezo wa kuingia pori la Nyankonko kumsaka mzimu Ntema wanaye sema alitupwa huko ……,”shangazi yake na Nyoni aliitikia, na kutoa ya moyoni kulingana na fikra zake. Kuhusiana na jambo kwani hata yeye siri ambayo aliambiwa na kaka yake mzee Mbutu miaka kadhaa iliyopita, haikumuingia akilini hata kidogo.



    “Kweli wifi yangu, ngoja tuendelee kuvumilia wiki kadhaa mbele!, “mama yake Nyoni alihitimisha mazungumzo ambayo yaliendelea kati yake, mume wake pamoja na ndugu zake. Japo walikuwa katika mazingira magumu sana, ndani ya kichumba kidogo cha gereza ambacho kilijaa kinyesi cha ng’ombe na kutoa harufu mbaya. Lakini hawakuacha kupiga stori za hapa na pale, stori ambazo zilifanya maisha yao kuwa rahisi na kuwaongezea uvumilivu siku hadi siku, wakijipa moyo kuokolewa na Nyoni siku moja atakapo rejea kutoka kijiji cha Ukarimu …



    …………………………………





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog