Search This Blog

NABII WA UONGO - 2

 

    Simulizi : Nabii Wa Uongo

    Sehemu Ya Pili (2)





    Kigoma;



    Wazazi wangu wanaiacha ardhi ya  kigoma,na kulishuhudia ziwa Tanganyika kwa chini likiwa linaonekana vizuri sana.Walikuwa katika moja ya ndege aina ya Bombadier inayomilikiwa na Air Tanzania,baada ya kuwatumia pesa waje kunitembelea Dar es salaam.Kwani nilipowatumia pesa ya kupanda treni aina ya deluxe waliweza kunigomea,basi pia walikataa,eti wataniaibisha wakipanda usafiri wa aina hiyo.Kusema ukweli walikuwa sahihi,kwani waandishi wa habari wasingeniacha salama,kutokana na umaarufu wangu kama mchungaji aliyeibuka ghafla na kuwa na pesa nyingi huku akijaza maelfu ya watu katika kanisa lake.Hivyo siku zote walifuatilia maisha yangu ili waweze kuuza magazeti yao,kwani taarifa zilizonihusu ziliwavutia watu wengi sana.



    Lakini mimi nilikuwa na maana yangu,kuwataka wazazi wangu waweze kupanda treni au basi,japo walinigomea kutumia usafiri huo.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Bagamoyo;



    Mganga wa kienyeji aliyekuwa na nguvu nyingi sana za kishirikina,akiwa ameketi juu ya joka lile la ajabu ambalo tuliliabudu ,mimi pamoja na wanachama wenzangu akiwemo mzee Jabir na kumpinga Mungu wa kweli,alijikuta akishangaa sana kwani alisikia kelele za vitisho ,bila kutambua sauti ile ilikuwa ikitokea sehemu gani,na nani aliyekuwa akitoa vitisho hivyo.



    Bagamoyo;



     Mganga alichoka! sauti zile za ajabu zilimfanya achanganyikiwe, kwani alitumia utaalamu wake wote kumgundua mtu aliyekuwa akimtisha lakini alishindwa.



    “Wewe ni nani uliyekuja kunitisha katika himaya yangu?, naomba ujitokeze “,mganga aliamua awe mpole tu, kwani kila utundu alioufanya ilikuwa ni sawa na bure. Mala achukue kibuyu ateme mate ndani yake kisha akipulize, na hakuishia hapo akachukua tunguli moja iliyokuwa karibu naye na kuiweka ndani ya kibuyu na kisha kuendelea kukipuliza bila mafanikio. Sauti zile aliendelea kuzisikia, huku akiwa hamtambui muhusika aliyekuwa akimtisha na kuamua kumuomba aweze kujitokeza.



    “Lazima nitawaua, kama nyinyi mlivyoua watu wengi wasiokuwa na hatia… “,sauti ile nzuri ambayo ilionekana kuwa ya msichana mrembo, iliendelea kumtisha mganga yule, mganga aliyekuwa amekalia joka lile la kutisha ambalo lilikuwa limejiviringisha na kutulia tuli!  Kama maji ya mtungini.



    “Ohooo! Kumbe ni wewe, tayali umeshaliwa na nyoka wetu, halafu wewe ni mtoto mdogo sana huwezi kupambana na sisi “,mganga aliongea huku akiwa ameshika tunguli zake, na kumzuia Juliet asiweze kumsogelea baada ya kujitokeza. Lakini kwa wakati ule joka la ajabu lilikuwa limelala, kwani mganga hakutaka kuliamsha liweze kumsaidia, aliona tatizo lilikuwa dogo sana kwake na angeweza kulimudu.



    “Muda ukifika, utajuwa kama mimi ni mtoto mdogo au laaa! mzimu wa Juliet uliongea huku ukitabasamu, tabasamu ambalo lilionesha kutowaogopa adui zake na kisha kutoweka mahali pale kama upepo huku mwanga mkali ukimsindikiza, hali hii ilimfanya mganga aweze kutambua kuwa lolote baya linaweza kuwatokea, yeye na wanachama wake wote japopokuwa alikuwa akimdharau Juliet.



    “Huyu binti kawa mzimu!!, ngoja tuone kama ataweza kupambana na sisi “,mganga aliongea huku akishusha pumzi ndefu, na kujifuta kijasho ambacho kilikuwa kinatiririka katika mwili wake.



    Dar es salaam;



    Nikiwa nimeketi sebuleni Kwangu nikimtafakali Juliet, huku nikiwa sitambui kama aliweza kufika mpaka Bagamoyo usiku ule ule alipotoka nyumbani kwangu na kwenda kumpatia vitisho vikali mganga, wazo jipya liliweza kunijia kuhusu wazazi wangu.



    “Mungu wangu! mpaka sasa hawajafika, nini kimewatokea! “,nilishtuka ghafla kwani nilikuwa tayali nimesahau kuwa wazazi wangu walikua safarini kwa usafiri wa ndege kuja kunitembelea.



    “Wameanza safari saa kumi na moja, bila shaka!mpaka sasa saa tatu usiku tayali wangekuwa wameshaikanyaga Dar es salaam “,nilizungumza bila kutambua kuwa simu yangu ilikua na missed call zaidi ya nane, huku nikiwa nimepigiwa bila kusikia simu yangu kama iliweza kuita.



    “Potelea mbali!, lazima watakua salama tu, ngoja nichukue biblia nifanye kukalili mistari, sunajua tena kesho jumapili ………!”,niliongea huku sauti mbili zikipingana katika fikra zangu, sauti moja ikiniambia nitazame simu yangu huku sauti nyingine ikiniambia niweze kuchukua biblia.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    *******



    Ilikuwa ni majira ya saa moja na nusu hivi,ndege ndogo ya kubeba abiria takribani sitini, iliweza kutua katika uwanja wa kimataifa wa mwalimu Nyerere.



    “Mke wangu hapa ndo Dar, bongo bahati mbayaa! najua umezoea kusalimia mwidiwe kule kwetu kila mtu unayekutana naye njiani, lakini hapa sio Kigoma! naomba zungumza kiswahili, staki kuaibishwa ohoooo “,ilikuwa ni sauti ya mzee mjanja sana, mzee aliyezaliwa na kukulia mtaa wa Bangwe Kigoma mjini. Mzee huyu alitegemea uvuvi wa samaki katika ziwa Tanganyika, shughuli pekee ambayo ilimuingizia kipato na kuitunza familia yake. Hivyo haikuwa mala  yake ya kwanza kufika Dar es salaam, kwani siku zote alisafilisha migebuka kutoka Kigoma hadi Dar es salaam.



    “Sawa mme wangu, ndategeje! “,ilikuwa ni sauti ya mama yangu kipenzi, mama ambaye alinikataza nisije Dar es salaam, lakini mimi sikuweza kukubaliana naye nilifunga safari kwa lazima, huku nikiwa nimeruhusiwa na baba yangu kipenzi mzee Hamenyimana. Mzee ambaye alikuwa kama kijana, kutokana na tabia zake za kitoto alizokuwa nazo,na kujikuta akipatiwa jina la mzee mjanja na wavuvi wenzake.



    “Nimetumwa na mtoto wenu nije kuwapokea …”,ilikua ni sauti ya Juliet, msichana ambaye alikuwa amegeuka mzimu mala tu baada ya mimi kumuua na kisha kumtoa sadaka.Sauti ile iliweza kuwashtua wazazi wangu  ambao walikuwa wanaangaza huku na kule katika eneo lote la kupokelea wageni bila kuniona, lakini baba aliweza kushauri watoke nje na kisha kuchukua taksi ili waweze kuja nyumbani kwangu kwani nilikuwa nimeshamwambia mtaa niliokuwa nikiishi.



    “Mbona hakuna taksi hata moja!!, “ilikuwa ni sauti ya mzee wangu, kwani alionekana kushangaa kutokuta hata taksi ya kubeba wageni eneo nyeti kama hilo, tena katika uwanja wa ndege mkubwa na wa kimataifa bila kutambua kuwa kulikuwa na mkono wa mtu ukisababisha yote hayo.



    “Sawaa! bila shaka wewe ndiye mama mchungaji hahaa! lakini mwanzoni tumeangaza kila sehemu hatujaona taksi mahali hapa, lakini nashangaa baada ya muda mfupi tu ulipotuita na kugeuka ,tunashangaa kuona taksi kibao mahali hapa!”,mzee wangu aliongea huku akiamini Juliet atakuwa mke wangu, japokuwa alionekana kushangazwa na kile alichokiona mahali pale.



    “Msijali twendeni mahali salama”,mzimu wa Juliet uliongea na kisha kumfanya mzee ajiulize maswali, labda kulikuwa na hatari yoyote imeweza kumtokea mwanae, hasa baada ya kukumbuka kuwa aliweza kunipigia mala tisa simu bila kupokelewa, huku mimi kipindi simu inapigwa nilikuwa nawaza  maajabu ya kumuona Juliet kageuka mzimu na kisha kunitokea.



    “Dereva tupeleke Mbagala kuu, “Juliet aliyekuwa amevaa gauni zuri, huku kovu la kisu likionekana kwa mbali shingoni kwake japokuwa halikuweza kuzuia uzuri wake usiweze kuonekana, alimuelekeza dereva taksi sehemu ya kuwapeleka huku mzee akionekana kutoshtukia chochote kile, kwani Juliet hakutisha hata kidogo!, alikuwa na mwonekano wa kawaida kabisa.



    Masaa yalikwenda, huku nikiwa naendelea kujisomea biblia. Mpaka nikajikuta napitiwa na usingizi pale pale sebuleni ,na kusema ukweli nilikalili mistari mingi sana, mistari ambayo ingenisaidia kanisani siku iliyofuata.



    “What …!,hawajafika!,”nilishangaaa sana baada ya kushtuka usiku wa manane ,wazazi wangu wakiwa bado hawajafika. Nilipojalibu kuangalia saa yangu ya ukutani ,ilikuwa tayali imetimu saa tisa usiku.



    “Hapa tayali mambo yamehalibika, jumamosi imekua ya majanga sana kwangu!au wamehisi jambo ambalo nilikuwa nataka kuwafanyia! “,niliongea huku nikiwa na wasiwasi sana, kwani kabla jua halijachomoza ilitakiwa nitoe sadaka, na sadaka iliyokuwa inatakiwa kutolewa ilikuwa ni ya watu ambao niliwapenda sana.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sebuleni hapakukalika tena, nilizunguka kama kichaa, kwani sikujua nilikua naelekea wapi.Jambo pekee ambalo lilikuwa likinisumbua kichwani, ni kuhusu nyoka ambaye nilipewa kama zawadi kwa ajili ya kuishi naye Nyoka huyu ilikuwa siku ya nne tangu niishi naye akiwa bado hajapata chakula, na chakula chake ni binadamu. Siku zote kichwa kiliniuma kwani sikujua napata wapi chakula chake, nilipojalibu kumuulza mzee Jabir kuhusu chakula cha Nyoka yule, nyoka ambaye sikutakiwa kumfungulia katika chumba cha siri tangu aingie ndani kwangu, kwani ningeweza kuliwa mimi kama sikuwa na chakula cha kumpatia.



    “Nyoka huyo atakuwa mtumwa wako maisha yote, atakulinda kila sehemu lakini nguvu zake ziko mikononi mwako. Inatakiwa umpatie chakula, tena chakula chake ni wazazi wako ,na ndipo mfungulie na atakuwa na nguvu za ajabu “,Hiyo ilikuwa ni sauti ya mzee Jabir pamoja na mganga, walipokuwa wakinipa masharti jinsi ya kuishi na nyoka niliyepewa kama zawadi baada ya kumtoa Juliet sadaka. Nikiwa nazunguka sebuleni bila mwelekeo, niliweza kukumbuka maneno ambayo niliweza kuambiwa na wakubwa wangu mala baada ya kukabidhiwa nyoka niweze kuishi naye.



    “Sawa nimekubali “,nilijikuta nakubali bila kujitambua, kwani tayali nilikuwa nimeshakuwa muuaji na katili. Nilichokifanya nikuwapigia wazazi wangu,wazazi ambao walinipigia kila siku wakitaka waje kunitembelea,lakini mimi sikutaka waje kunitembelea kwani pengine wangeweza kugundua siri zangu.Lakini baada ya kuambiwa kuhusu kutoa sadaka ya watu niliowapenda sana,mala moja fikra za wazazi wangu zikanijia kichwani kwangu.Ama kweli! shetani alinizidi nguvu kila sehemu,nilifanya maamuzi magumu na bila kujitambua.



    “Ngoja waje,kitakacho wakuta hawataamini,”nimaneno ambayo niliyazungumza mala tu baada ya kuwatumia wazazi wangu nauli ya ndege,waweze kuja kunitembelea.Lakini walikuwa wamenigomea kusafiri na basi au treni,kama vile walikuwa wamegundua mipango ya siri tuliyokuwa tumepanga na chama changu cha kishetani,kuwasababishia ajari na kisha kuikamilisha sadaka yangu.



    “Hapa kuna jambo sio bure! mitego yote wameikwepa”,niliketi tena kwenye sofa huku nikijilaumu,kwani  nisingeweza kuitoa sadaka yangu kwasababu  kulikuwa kunaelekea kupambazuka.



    ********



    Mzimu wa Juliet ulitambua kila kitu kilichokuwa kikiendelea, mipango yetu ya siri kuhusu kuwafanyia mauaji wazazi wangu mala watakapofika nyumbani kwangu, pamoja na kuwatoa sadaka kwa nyoka niliyepewa, yote Juliet aliyatambua. Hivyo hakuwa na budi kuwaokoa wazazi wangu, na pia kufanya kila njia nyoka ashindwe kupata chakula kwani kama angeweza kupata chakula. Juliet angefanya kazi kubwa sana kupambana naye, na asingeweza kuniokoa kirahisi kutoka mikononi mwa utumwa huu wa kishetani niliokuwa nikiutumikia.



    “Kuanzia leo mtaishi hapa, mtoto wenu kasafiri, atarudi baada ya siku mbili, mimi ndio mke wake”,Juliet aliwakalibisha wazazi wangu kwenye nyumba nzuri sana, pengine nyumba hiyo hata mimi na pesa zote za kishirikina sikuwa na uwezo wa kuimiliki. Mzimu wa Juliet uliongea, ukiwa na uhakika kabisa siku mbili zilitosha yeye kukamilisha kila kitu, na kufichua maovu yote niliyokuwa nikiyafanya.



    “Mtoto wetu kweli kapata pesa mjengo wote huu! ……kwelii imana ishimwe “,mama aliongea huku akishangaa jengo kubwa la kifahari, jengo ambalo Juliet alilitengeneza kimaajabu, kiasi kwamba hata mimi nilikuwa sifahamu alitumia uwezo gani wa ajabu kuwafanya wazazi wangu waweze kujiona kama wakiwa ndani ya jengo hili kubwa la Juliet. Jengo ambalo liliundwa katika mazingira ya kutatanisha sana, tena ya ajabu!



    Jua lilichomoza mapema sana kama kawaida! ,ilikuwa ni moja ya siku za ajabu sana. Kwani Joka lile ambalo nilipewa kuweza kunilinda na kunitumikia lilianza kupiga kelele na fujo nyingi sana nyumbani kwangu, na kunifanya nizidi kuwa na hofu isiyo kuwa ya kawaida.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Zikipita siku tano akiwa hajapata chakula,nyoka huyu atapiga kelele za ajabu ,kelele za hasira, jitahidi sana bila hivyo utaharibu kila kitu “,niliikumbuka sauti iliyokuwa ikinisisitiza kuhakikisha nyoka wangu niliyepewa anapata chakula chake ndani ya siku tano. Japokuwa ilikuwa asubuhi, lakini mwili wangu uliweza kulowa kwa jasho ambalo lilitokana na hofu iliyokuwa ikinikosesha amani.



    “Nimekwisha!, leo naumbuka !”,niliongea kwa sauti ya chini sana huku nikitoka ndani ya nyumba yangu kuelekea kanisani kwangu, kanisa ambalo lilikuwa karibu tu na nyumba yangu. Japo nilifunga madirisha ya nyumba yangu, lakini kelele za nyoka yule niliweza kuzisikia mpaka kanisani kwangu.



    Sauti zile waumini wengi wa kanisa langu hawakuweza kuzisikia, hasa watu ambao walikuwa watenda dhambi na walioingia kanisani kwangu kufuata maajabu yangu niliokuwa nikiyatenda. Lakini watu wachache waliomjua mungu kweli kweli, waliweza kuzisikia sauti za kutisha kutoka nyumbani kwangu, sauti ambazo zilikuwa za Nyoka niliyemfungia katika chumba cha siri kwa siku tano mfululizo bila kumpatia chakula chochote kile.



    “Kulikoni mchungaji!, naskia sauti za kutisha kutoka nyumbani kwako!



    “Mbona mimi sisikii? “



    “Hata mimi pia sisikii, “



    “Jamani! baba Juliet yuko sahihi! Hata mimi nasikia sauti hizo, tena sauti zenyewe sio za kimungu kabisaa!



    “Msiwe na hofu! Tuendelee na ibada, kama sauti hizo mnazosema mnazisikia zikiendelea tena, itabidi tuzikemee kwa maombi! bila shaka shetani atakua ananinyemelea kuniangusha nisiweze kumtumikia Mungu “,



    Yalikuwa ni majibizano yaliyokuwa yakiendelea kati yangu, na viongozi wenzangu wa kanisa. Ni baada ya kusubiliwa kwa muda mrefu niweze kuanza ibada, bila kutambua kuwa kiumbe ambacho waliweza kusikia kelele zake ndicho kilicho nichelewesha kuingia kanisani. Lakini nilijikuta nakutana na ujumbe ambao ulinishtua sana kutoka kwa baba yake Juliet, kwani ndiye aliyeanzisha mazungumzo kutokana na sauti za ajabu alizozisikia ,na kuzidi kutoniamini kwani siku zote alikuwa na mashaka juu ya uchungaji wangu. Mashaka yaliyoanza siku moja alipokuja kunitembelea nyumbani kwangu na kukuta chupa ya konyagi ikiwa mezani kwangu, na alipojaribu kuniuliza kuhusu chupa ile nilimzungusha zungusha tu bila kumpatia jibu lolote la kuridhisha.



    ****-***



    Juliet alionekana kuwa na haraka sana, japo alikuwa mzimu, lakini alifanya kila kitu kama binadamu wengine ili tu wageni wake, baba pamoja na mama yangu mzazi wasiweze kumtilia mashaka.



    “Twendeni haraka kanisani, kuna hatari! “,Juliet aliongea huku akiwa ameshika funguo yake ya gari, lakini pia katika mkono wake wa kulia alikuwa ameshika biblia.



    “Hatariiiii !!”wazazi wangu walishtuka, na kujikuta wakijibu kauli ya Juliet kwa wakati mmoja tena kwa mshangao.



    “Hapana! Ulimi umetereza tu, twendeni kanisani ibada imesha anza! Tunachelewa! “,Juliet alitengua kauli yake ,alijikuta akitamka ukweli ambao alikuwa amepanga kuuficha mpaka watakapofika kanisani. Lakini wazazi wangu hawakuendelea kushangaa, walifikiri kweli Juliet alikuwa amepitiwa tu kutamka maneno yale, la hasha!

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hatari ya nyoka kuvunja chumba cha siri nyumbani kwangu, na kisha kulishambulia kanisa kwa ajili ya kujipatia chakula, ndio hatari ambayo Juliet alikuwa akiizungumzia. Alikuwa ameshaona kila kitu ambacho kilikuwa kinaelekea kutokea.



    “Mtoto wetu anakuja lini, nani anahubiri leo?  Wewe au! ” ,baba aliuliza swali, huku akimshika mkono mama yangu mzazi na kumwongoza kupanda gari la Juliet. Siku zote baba hakupenda kuaibishwa, ndio maana alitembea na mama bega kwa bega ili tu mama asije kuharibu katika jambo lolote lile.



    “Mimi ndio nitahubiri! “,Juliet aliongea huku akiliondoa gari lake na kujisogeza katika mitaa ya kijichi, mahali ambapo kanisa langu lilikuwa likipatikana. Siku huyo Juliet alipanga kusema kila kitu kuhusu mimi, na kuweza kuokoa watu ambao wangezidi kuuawa kwa ajili ya kutolewa kama sadaka.



    *******









    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog