Search This Blog

NABII WA UONGO - 4

 









    Simulizi : Nabii Wa Uongo

    Sehemu Ya Nne (4)





    Baada ya Juliet kuzungumza na mimi alitoweka mbele ya macho yangu, hali ambayo iliweza kuniogopesha na hofu Yangu kuanza upya. Sikutaka kutoka ndani ya chama changu na kuwa maskini tena, ilibidi nielekee ndani ya chumba changu cha siri na kumuelezea nyoka wangu mdogo niliyepewa kwa ajili ya kuishi naye kile ambacho kilikuwa kimetokea.



    Kumbe Juliet alikuwa bado yuko ndani ya nyumba yangu akizunguka huku na kule akitafuta chumba cha siri, japo alitoweka mbele ya macho yangu.



    Hiyo ndiyo ilikuwa njia pekee ya yeye kufanikisha misheni yake,aliweza kugundua fikra zangu na kuanza kunifatilia sehemu ambayo nilikuwa nikielekea.Nilikatiza korido za kutoka sebuleni,na hatimaye kuelekea chumba ambacho niliweza kufunika mlango wake kwa pazia jeusi.Rangi ya pazia,ilifanana sana na ukuta wa nyumba yangu na ndio maana ilikuwa vigumu kwa mgeni yoyote wa nyumba ile kugundua chumba hiki cha siri.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilifunua pazia la nyumba yangu na kisha kuingia ndani,kumbe Juliet kwa uwezo wa ajabu aliokuwa nao,kabla hata sijafunga mlango na yeye aliweza kuingia haraka ndani ya chumba kile.Nilipofunga mlango tu ,sikuamini kile  ambacho kiliweza kutokea.



    “Nyankii,nyankii,ingririii!nyanki nyanki ingriiriiii……”,zilikuwa ni kelele za nyoka wangu,kelele ambazo zilipangiliwa kwa mpangilio mzuri,bila shaka nyoka yule alikuwa akiimba wimbo.



    Nilimshangaa sana nyoka wangu,hakuonekana kujali uwepo wangu ndani ya chumba kile,bali aliimba wimbo huku akionekana kutazama pembeni ya ukuta.Lakini kwa upande wangu,ilibidi nimshangae tu na kushindwa kumwelezea jambo ambalo lilinipeleka ndani ya chumba kile,chumba ambacho kilitisha sana kwani kilipambwa kwa mashuka yenye rangi nyeusi,nyeupe,pamoja na nyekundu.Rangi ambazo sikuzote sikujua zilimaanisha nini,na kwanini sikuambiwa kuweka mashuka yenye rangi tofauti na hizi.



    “Puuuuuuuuuuuh! ” ulikuwa ni mlio wa sauti nzito,sauti ambayo iliashiria kitu kizito kiliweza kudondoka chini.Haraka sana niligeuza macho yangu,kuangalia sehemu ambayo mlio wa sauti ile uliweza kutokea.Sehemu ile ile ambayo nyoka wangu alikuwa akiangalia huku akiimba.



    Sikuamini nilichokiona,Juliet alikuwa amedondoka chini huku damu zikimtoka mdomoni.Nyoka aliyepewa majukumu ya kunilinda,na kulinda chumba cha siri ,ndiye aliyesababisha Juliet kudondoka chini.Kwa upande wangu nilipigwa na butwaa kumshangaa tu Juliet,kwani sikufahamu kama alikuwa bado ndani ya nyumba yangu akinipeleleza aweze kutambua chumba changu cha siri.



    Hatimaye niliweza kutambua chanzo cha nyoka wangu kuimba nyimbo ile,nyimbo ya kiasili iliyoonekana kuwa na nguvu sana pale inapoimbwa mbele ya Juliet.Isitoshe! ndipo nilipogundua ni kwanini chumba changu Juliet hakuweza kukitambua kutokana na pazia jeusi nililoliweka katika mlango wa chumba cha siri,kuwa na nguvu za ajabu ambazo zilifanya viumbe wa ajabu kutotambua chochote kile.Na ndio maana ndani ya chumba cha siri,rangi nyeusi ilikuwa moja kati ya rangi za mashuka ambazo zilitumika kupamba chumba kile.



    Hatimaye Juliet alikuwa mikononi mwetu,kwa mbali nilimuonea huruma.Lakini sikuwa na la kufanya,mimi nilikuwa mdogo sana katika chama chetu na sikuwa na madaraka yoyote.Ghafla radi zilipiga,tetemeko la ardhi likapita kwa sekundee kadhaa.Kufumba na kufumbua,Nyoka mkubwa ambaye alikuwa ndiye mkuu wa chama chetu,mzee Jabir pamoja na mganga,walitokea ndani ya chumba changu cha siri.Sikutambua ni jambo gani walitaka kulifanya,mbele ya mzimu wa Juliet.



    Mzimu wa Juliet umekamatwa katika harakati za kumkomboa mchungaji wa uongo, Hakika!!



    Bila kutegemea, Hatimaye katika harakati za kunikomboa, na kunitoa katika utumwa wa kishetani. Mzimu wa Juliet unajikuta katika wakati mgumu baada ya kuishiwa nguvu na kisha kukamatwa na wakubwa wangu wa kazi.Nyoka wangu wa ajabu ndiye aliyemuimbia wimbo Juliet, wimbo ambao ulikua na siri kubwa kuhusu viumbe ambao walikufa na kisha kugeuka mizimu.



    Wimbo wa kiasili ambao nyoka wangu aliuimba, kumbe ulikuwa na uwezo wa kudhoofisha nguvu za Juliet.Siri hii nyoka aliweza kuitambua kutokana na nguvu alizokuwa nazo, kwani mwanzoni nyoka wangu alikua ni sehemu ya Nyoka mkubwa ambaye alikuwa ndiye mkuu wa chama chetu. Hivyo alikuwa bado ana uwezo wa ajabu na kufahamu mambo mengi sana, ikiwemo namna ya kupambana na viumbe hatari waliokufa na kugeuka mzimu kama Juliet.



    “Tumpeleke kuzimu , tukamfunge huko,naamini nguvu zake hazitarudi tena,na hataweza kutufuatilia” ,yalikuwa ni maneno ambayo nyoka mkubwa ,nyoka ambaye alikuwa na vichwa vingi sana,aliweza kuyaongea huku mzee Jabir pamoja na mganga wakimsikiliza.Kwa upande wangu nilikuwa nimepigwa tu na butwaa nikiwatazama,nikiwa sijui nini nifanye kwa wakati ule.



    “Mchungaji wewe baki,na endelea na majukumu yako,hakuna atakaye weza kukudhuru na kukuharibia sifa zako”,mganga alinipatia maelekezo,baada ya kunitazama usoni na kutambua fikra zangu.Aligundua kwamba nilikuwa nataka kuongozana nao,jambo ambalo lilikuwa sahihi kabisa.Nilitaka kwenda nao huko kuzimu niweze kupafahamu,na pia niweze kujua kitu ambacho walitaka kumfanyia Juliet.



    “Sawa nitabaki ,lakini nilitaka kwenda na nyinyi” ,niliongea bila hofu,na kuonesha nia yangu ya kutaka kuongozana nao ,bila kutegemea nilijikuta nikipata nafasi ya kuongozana nao kuelekea kuzimu.



    “Twende naye ,hajawahi kufika kuzimu tangu ajiunge na chama chetu,twende naye akaone jinsi chama chetu kilivyo na watu wengi”,nyoka wa ajabu ,nyoka ambaye alikuwa na vichwa vingi sana,mwenye uwezo wa kuongea kama vile binadamu wa kawaida,aliweza kunikubalia ombi langu.Kwakuwa alikuwa ndiye mkuu,hakuna aliyeweza kumpinga,na hatimaye haraka sana safari ya kuelekea kuzimu iliweza kuanza.



    Nilipewa maelekezo ,na kuyafuata kwa umakini. Sote kwa pamoja tuliweza kushikana mikono na kutengeneza duara,huku mzimu wa Juliet ukiwa umelala chini katikati yetu.



    “Fumbeni machoo! asifumbue mtu yoyote yule mpaka nitakaposema” Nyoka yule alitoa amli, amli ambayo tulipaswa kuifuata ili tusije tukapata matatizo. Ghafla upepo mkali, upepo ambao sikujua ulitokea wapi, kwani madirisha na mlango wa chumba changu cha siri ilikua imefungwa.



    Sehemu ya sakafu tuliyokuwa tumesimama ikafunguka, na shimo lenye usawa wa duara ambalo tulikuwa tumelitengeneza baada ya kushikana mikono likatokea. Upepo ule mkali, upepo ambao ulikua mithili ya kimbunga uliweza kutusafirisha kwa kasi ya ajabu kuelekea chini, ndani ya shimo lile.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Nilitamani nifumbue macho yangu niweze kushuhudia yaliyokuwa yakitokea, lakini nilishindwa kwani nilikuwa na hofu juu ya jambo baya kunitokea, baada ya kuonywa kabla ya safari kuanza.



    Upepo mkali uliendelea kutusafirisha kwa kasi ya ajabu, kuelekea chini kabisa ya shimo. Shimo ambalo sikuweza kutambua urefu wake, lakini bila shaka lilikuwa na umbali mrefu sana.



    “Puuuuh ……”,ulikua ni mlio wa sauti nzito, sauti ya kishindo ambacho kilisababishwa na sisi kudondoka chini. Kishindo hicho kiliweza kuashiria kufika mwisho wa safari, safari ambayo ilichukua takribani muda wa kama masaa mawili.



    “Karibuni sana katika dunia yetu, “,ulikua ni mlio wa sauti ya kiume, sauti ambayo bila shaka ilikua ni ya mtu mzima tena wa makamo. Alionekana kufurahia ujio wetu, na bila shaka alitambua lengo la sisi kuwepo katika nchi ile ya kuzimu.



    “Fumbueni macho, tumefika, “nilifurahi sana baada ya kuruhusiwa kufumbua macho, kwani muda mrefu nilitamani kufumbua macho na kutazama kile ambacho kiliendelea, na isitoshe niweze kutazama kwa macho yangu jinsi kuzimu kulivyofanana.



    “Waaaooh, kuzimu kuzuriii hivi, nilizani panatisha! “,nilifurahi sanaa, ni baada ya kufumbua macho na kutazama uzuri wa nchi hii ya kuzimu. Kulikua na maghorofa mazuri sana zaidi ya yale ya kariakoo, jijini Dar es salaam. Barabara nzuri za kila aina, zingine zilikua barabara za juu kwa juu huku zikipambwa kwa lami nzuri ambayo ilifanya magari kupita bila buguza yoyote ile.



    Sikuamini kama hata kuzimu kulikua na magari, tena ya kifahari kiasi kile. Nilishangaa kuona watu wakipishana, na kuendelea na shughuli zao kama kawaida. Kuzimu kulifanana sana na duniani, lakini tofauti yake, watu walioishi kuzimu walionekana kuwa na maisha mazuri na tena matajiri wakubwa sana.



    “Kijana usishangae, ukifanya kazi yako vizuri duniani, baada ya miaka kadhaa utakuja kuishi huku ” ,sauti ya mzee, mzee ambaye alitukaribisha mala ya kwanza baada ya kufika. Akiwa amevalia mavazi ya kifalme, baada ya kuniona nikishangaa uzuri wa kuzimu, alinitamkia maneno yaliyonifanya nizidi kutamani kuendelea kukitumikia chama hiki cha kishetani na kumsahau Mungu.



    “Sawa mkuu, nitafanya kazi kwa bidii nije kuishi huku, nimepapenda ” ,niliongea huku nikitabasamu, lakini mzee yule aliyeonekana kuwa na madaraka makubwa kuzimu ,alionekana kama vile alikuwa akitaka kusema jambo, lakini alisita baada ya kuona nikitoa jibu haraka na kumfanya asubili kwanza nimalize kuongea.



    “Mkuu wa chama changu duniani, naomba mchukueni huyo kiumbe mkafungie katika gereza, na huo ndio utakua mwisho wake, hataweza kuwasumbua ” ,amli ilitoka kwa mkuu yule wa kuzimu, na haraka sana, mganga pamoja na mzee Jabir walitii amli, kwani wao ndio walikuwa na vyeo vidogo, na kisha kumchukua Juliet na kwenda kumfungia katika gereza ambalo lilizungukwa na nyoka wengi wa ajabu Nyoka hawa waliimba nyimbo za kiasili, nyimbo ambayo nyoka wangu aliweza kuimba na kumfanya Juliet aishiwe nguvu na kudondoka chini.



    Hivyo basi, mzimu wa Juliet uliishiwa nguvu zote, na matumaini ya kunikomboa kutoka katika utumwa ule yakawa yamefifia, kwani nyoka wale waliomlinda Juliet, waliimba usiku na mchana na kumaliza nguvu zake zote, kiasi kwamba alishindwa hata kupata nguvu za kumfanya apambane.



    “Tayali, tunaweza kurudi duniani, mzimu wa Juliet hauwezi kutufuatilia tena “,mkuu wetu nyoka, nyoka wa ajabu mwenye vichwa vingi sana, aliongea na kutoa amli ya kurudi duniani, baada ya kukamilisha kazi ya kumfungia Juliet na kumuwekea ulinzi mkali kuzimu. Kwa upande wangu, fikra zangu zote zilitekwa na sikuweza kujitambua hata kidogo. Jambo pekee ambalo nilianza kuliwaza, ni kutoa kafara nyingi ili baadaye nipande cheo na kuja kuishi kuzimu.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hali ya wasiwasi iliwakumba wazazi wangu, pamoja na wazazi wake Juliet. Wakiwa bado na majonzi, kwani waliamini mtoto wao alikwisha kufa, na karudi duniani kama mzimu kwa ajili ya kunikomboa kutoka katika utumwa wa kishetani. Waliamua kumuachia Mungu, kwani yeye ndiye mwenye kuhukumu, na hawakua na budi kunisamehe kwa yote niliyoyatenda na kumtoa kafara binti yao kipenzi.



    “Msameheni kijana wetu, hakujua alitendalo ” ,wazazi wangu waliongea kwa uchungu, huku wakiwakumbatia wazazi wake Juliet. Kwa wakati huo, mama yake Juliet alikuwa akilia tu, kwani hakuamini kama nilikuwa mchungaji mnyama na katili kiasi kile, japo kwa mwonekano wa nje nilionekana mpole na mwenye roho nzuri sana.



    “Msiwe na shaka, nyie ni wazazi wenzetu, kijana wenu hafanyi haya yote kwa kupenda, inabidi tuombe sana kwa Mungu ili mzimu wake Juliet ufanikiwe kumkomboa “,yalikuwa ni maneno ya busara kutoka kwa baba yake Juliet, maneno ambayo yalikuwa ya hekima na ujumbe mzito ndani yake. Hawakutambua  mzimu wa Juliet ulikuwa umefungiwa katika gereza lililoko kuzimu, huku nyoka wakimlinda asiweze kutoroka na kuendeleza harakati zake za kunikomboa.



    “Lakini tangu aondoke hapa jana asubuhi, bado hajarudi, sijui atafanikiwa? Lakini naamini ananguvu za kutosha, kwani sio binadamu wa kawaida, bila shaka atafanikiwa kumkomboa mchungaji kutoka utumwani “,baba yake Juliet, aliendelea kuongea huku akionekana kama vile hakuguswa na kifo cha binti yake, aliona kama vile yalikuwa mapenzi ya Mungu, Juliet aweze kufa na kuokoa vifo vya watu wengi ambavyo ningeendelea kuvisababisha kanisani kwangu, kwa kuwatoa waumini kafara.



    …………………………………



    Hatimaye baada ya kumaliza shughuli iliyotupeleka kuzimu, tulishikana mikono na kutengeneza duara dogo kama awali. Tulifumba macho, kisha upepo mkali sana, upepo ambao ulikuwa na kasi kupita ule wa awali, ulianza kutusafirisha kwa kupitia shimo kama lile tulilolitumia kusafiria wakati tukielekea kuzimu.



    Safari ilikua ndefu, lakini baada ya masaa kadhaa tuliweza kutokea nyumbani kwangu. Katika chumba cha siri ambacho ndiyo sehemu ambayo safari ya kuelekea kuzimu, ilipo anzia.



    “Fumbueni macho tumefika duniani “,



    “Ooooh, duniani ni mbali kiasi hiki, nimefumba macho hadi nimechoka!! “,



    “Ndio ni mbali sana, lakini wewe ni mzoefu wa safari hizi, ilitakiwa mchungaji Hakika,  ndiye alipaswa kuchoka zaidi kuliko wewe “,



    “Sawa!, tuyaache hayo, inabidi sisi tuondoke kuelekea Bagamoyo, mchungaji abaki aendelee na majukumu yake ya kujenga chama chetu “,



    “Sawa mkuu, naamini hatotuangusha “,



    Yalikuwa ni mazungumzo kati ya mganga, pamoja na mkuu wetu nyoka. Lakini wakati mazungumzo yakiendelea, mimi pamoja na mzee Jabir tulikua kimya tukisikiliza kwa makini mazungumzo yao, huku tukitabasamu.



    Radi zilipiga mfululizo, sauti nzito za kutisha zilisikika ndani ya chumba changu cha siri. Baada ya sekunde takribani tano nilijikuta nikiwa peke yangu.Kwani kipindi radi zikipiga,ndipo mzee Jabir,mganga,pamoja na mkuu wetu nyoka,waliweza kutoweka na kurudi Bagamoyo.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nilibaki nikishangaa tu,na kutabasamu,kwani niliamini walimwengu ni watu wenye siri nzito,hasa baada ya kumfikilia mzee Jabir.Maisha yake ya nje alionekana mstaarabu,na mwenye utajiri mkubwa sana.Lakini nyuma ya pazia,alikuwa mshirikina,muuaji na mwenye roho mbaya kupita kiasi.Japo nilijiunga na chama chao niweze kuwa tajiri,lakini kwa wakati mwingine roho ilinisuta na kujiona mwenye makosa makubwa mbele za Mungu.



    …………………………………



    Wazazi wangu, pamoja na wazazi wake Juliet, wakiwa wameketi sebuleni wakati wa usiku, walishangazwa na kiumbe cha ajabu ambacho kiliwatokea na kuwapatia ujumbe uliowashtua sana.



    “Msiogope,msikimbie! Juliet alikufa na kisha kurudi duniani kwa ajili ya kuwalinda dhidi ya watu wabaya,na kisha kimuokoa Hakika kutoka katika utumwa wa shetan..Lakini kakamatwa na kufungwa kuzimu na watu wabaya,asiweze kutimiza malengo yake..Mnachotakiwa kufanya,ni kufunga na kuomba kwa siku mbili,ili nguvu zake ziweze kurudi”,yalikuwa ni maelezo marefu kutoka kwa mwanaumwe aliyewatokea wazazi wangu, pamoja na wazazi wake Juliet sebuleni,mwanaume huyo alikuwa na sura ya upole huku akiwa amevalia mavazi meupe yaliyong’aa sana.Hofu iliwatawala sana, kwani binadamu yule hakuwa wa kawaida na alileta taarifa ambayo iliweza kuwashtua sana.



    “Wewe ni nani,! ” Lilikuwa ni swali kutoka kwa baba yangu, mzee ambaye siku zote alikuwa jasiri, kwani kupitia shughuli zake za uvuvi katika ziwa Tanganyika. Mala nyingi sana alishuhudia mambo ya ajabu,kiasi kwamba uoga ukaweza kutoweka kabisa katika nafsi yake.



    “Hilo swali, muulize Juliet atakapo kamilisha kazi iliyomrudisha duniani, siku ambayo atawaaga kwa huzuni, huku nyie mkilia kwa majonzi kwani itakua ndio siku ya mwisho ya nyie kumuona mbele ya macho yenu “,mwanaume yule aliongea na kisha kupotea mbele ya macho ya wazazi wangu, huku baba yake Juliet akiangaza huku na kule kuhakikisha kama kweli kiumbe yule aliweza kutoweka.



    Kuzimu;



         Mzimu wa Juliet unajitahidi kuponyoka kutoka katika kifungo ,katika gereza ambalo lililindwa na nyoka hatari sana, nyoka ambao waliimba nyimbo za asili. Nyimbo ambazo zilidhoofisha nguvu za Juliet, kiasi kwamba alishindwa kujikomboa na kueendeleza harakati za kunikomboa.



    Nguvu zilimuishia mwilini mwake, damu zilimtoka mdomoni kadri ambavyo nyoka wale hatari walivyokua wakiimba nyimbo.Kadri damu zilivyozidi kumtoka mdomoni ndivyo nguvu zilimuishia zaidi na zaidi, kiasa kwamba kulikua na uwezekano wa kushindwa kukamilisha misheni yake iliyomurudisha duniani.



    Dar es salaam



            Hatimaye wazazi wangu, pamoja na wazazi wake Juliet, walianza harakati za kurudisha nguvu za Juliet. Walitakiwa kufunga na kuomba, kwa muda wa siku mbili, kama jinsi walivyokua wameambiwa na binadamu wa ajabu ambaye aliwatokea katika mazingira ya kutatanisha.



    “Ni siku ya kwanza ya maombi, tunapaswa kutimiza kama ambavyo tuliweza kuambiwa, maisha ya mchungaji yako mikononi mwetu ” ,



    “Nitashukuru kama mwanangu ataweza kubadilika, na kuwa mtu mwema, nashukuru sana kwa msaada na umumilivu wenu, mmempoteza binti yenu, lakini hamjaonesha chuki yoyote baina yetu”,yalikuwa ni mazungumzo ya wanawake wawili,wanawake ambao kwa muda mfupi tu tangu wafahamiane.Waliweza kupendana sana na kuwa kama ndugu.Mazungumzo yao,yaliendelea baada ya kumaliza maombi na kuketi kwa ajili ya kubadilishana mawazo.Wanaume wakiwa peke yao,wanaume ambao alikuwa ni baba yangu pamoja na baba yake Juliet.Lakini pia,wanawake waliweza kuketi peke yao,na kubadilishana mawazo.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Nisamehe ndugu yangu, sikujua kama mwanangu ni mtu mubaya kiasi hiki “,



    “Usjali mzee mwenzangu, watoto wetu wa siku hizi wanataka mafanikio ya haraka ,tofauti na enzi zetu!  Lakini naamini tukimaliza maombi ya siku hizi mbili, kila kitu kitakua sawa ……”, yalikua ni mazungumzo kati ya baba yangu, pamoja na baba yake Juliet. Baba yangu muda mwingine alijiona mwenye hatia, kwani Juliet aliuawa na mimi mwanae, ambaye nilijifanya nabii wa kweli kumbe sivyo, na kumtoa Juliet kama kafara kujiongezea utajiri, huku nikidanganya watu mbalimbali katika kanisa langu.



    Bagamoyo;



             Kasri la chama chetu cha kishetani, kasri ambalo liliundwa kwa jengo ambalo lilionekana kuwa la kale. Hali ya furaha ilitawala tofauti na awali, kwani mzee Jabir pamoja na mganga walionekana kuwa na nyuso zilizopambwa kwa tabasamu muda wote. Hofu za kuuawa na Juliet, zilitoweka kabisa, kwani waliamini Juliet asingeweza kutoroka na kutoka kifungoni, kuzimu.



    Tofauti kabisa na fikra zao, hawakutambua kama harakati za kumuokoa Juliet kutoka kifungoni, zilikuwa zimeanza. Muda wowote baada ya siku moja mbele, mzimu wa Juliet ungeweza kutoka kuzimu na kukamilisha lengo lake, lengo la kunikomboa kutoka katika utumwa wa kishetani.



    Kipindi yote hayo yakitokea, mkuu wa chama chetu, nyoka wa ajabu aliyekuwa na vichwa vingi sana, alikuwa amelala tu baada ya shughuli nzito aliyokuwa ameifanya kuweza kukamilika. Mawazo ya nyoka hayakutofautiana na mawazo ya mzee Jabir pamoja na mganga, aliamini kwa asilimia zote kuwa mzimu wa Juliet usingeweza kutoka kuzimu, kwani haukuwa na nguvu zozote za kufanikisha jambo hilo. Hata hivyo, kama mzimu wa Juliet ungefanikisha kutoka gerezani, lakini ilikua ni ngumu kulishinda nguvu ya jeshi la kuzimu, jeshi ambalo liliongozwa na mtu aliyetukaribisha mala ya kwanza nilipofika kuzimu, mtu huyu aliyeonekana kuvalia mavazi ya kifalme, sikuweza kufanikiwa kulifahamu jina lake, kwani niliogopa sana kumuuliza na kujikuta nikitoka kuzimu mala baada ya kwenda kumfunga Juliet, bila kulitambua jina lake.



    Kuzimu;



           Baada ya siku moja na masaa kadhaa kupita tangu wazazi wangu, pamoja na wazazi wake Juliet kufunga na kuomba, kama jinsi walivyokuwa wamepatiwa maelekezo. Damu zilianza kupungua kuchuruzika kutoka mdomoni mwa mzimu wa Juliet, alianza kufumbua macho kwa mbali sana, na kushuhudia nyoka waliokuwa wakimlinda, wakiendelea kuimba huku wakipuliza filimbi.



    Nyoka baada ya kumuona Juliet akifumbua macho kwa mala nyingine, tangu alipofungwa, walianza kuimba wimbo wao wa kiasili kwa fujo sana ili kudhoofisha nguvu zake zisiweze kurudi, na kuleta balaa.



    “Nyankii, nyakiii …nyakii! ingriiii ……!nyankii ingriiii ……nyankii ingriiiii”,sauti nzuri za nyimbo ziliendelea kusikika, nyoka walinzi ambao walikuwa wakimlinda Juliet katika gereza la kuzimu,  waliendelea kuimba ili kudhoofisha nguvu za Juliet. Hali ya taharuki iliwakumba walinzi hawa, kwani japo waliimba nyimbo hizi, nyimbo za ajabu ambazo zilikuwa na uwezo wa kunyonya nguvu za binadamu wa ajabu kama Juliet, lakini tofauti na awali, Juliet hakutokwa na damu mdomoni tena. Bali alifumbua macho na fahamu zilianza kumrudia taratibu.



    …………………………………



    Maombi ya wazazi wangu, pamoja na wazazi wake Juliet, ndiyo yaliyopelekea Juliet aweze kupata fahamu. Na kadri masaa yalivyosonga mbele, ili siku mbili ziweze kukamilika, ndivyo ambavyo nguvu za Juliet ziliweza kurudi maradufu, na kuwa za kutisha tofauti na awali.



    Mzimu wa Juliet utafanikiwa kutoka kuzimu?? Na kuendeleza harakati za kumkomboa mchungaji ………http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Ilikua siku ya ijumaa, siku ambayo ilikua ya maombi kanisani kwangu. Tabasamu zuri liliipamba sura yangu, kichwa changu kiliwaza tu kwenda kuishi kuzimu, sehemu ambayo ilionekana kunipendeza sana. Macho yangu yaliangaza huku na kule, na kukagua sura ya kila muumini aliyeingia kanisani kwangu. Neno kafara, kafara nyingi nilipaswa kutoa, ili niweze kupanda cheo, na kisha kwenda kuishi kuzimu. Hivyo basi, lengo la kukagua sura za waumini wangu jioni ile, ilikua ni kutafuta sura nzuri za wasichana warembo, na vijana wa kiume watanashati, niweze kuwalaghai na kisha kuwaua, kitendo ambacho kingeniongezea thamani ndani ya chama changu.



    “Pendo, mtoto wa mbunge wa manispaa ya Temeke, atanifaa sana, muone alivyo mrembo ……”



    “Jonson naye, nitamuwekea dawa kwenye soda akija nyumbani kwangu kwenye somo la biblia, harafu nitamuua “



    “Kwahiyo, ninapaswa kumuua Pendo, Jonson na Stephano ndani ya wiki hii, na mwezi ujao nitaua wengine “









    ITAENDELEAPseudepigraphas

0 comments:

Post a Comment

Blog