Search This Blog

NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA - 4

 

    Simulizi : Niliolewa Na Jini Bila Ya Kutarajia

    Sehemu Ya Nne (4)





    Moja kwa moja nikamfata mama aliyekuwa jikoni na kumuuliza swali,

    "Unanionaje mama?"

    Mama akashtuka na kuniangalia kisha akasema,

    "Nakuona ulivyo kwani tatizo ni nini?"

    "Unavyoniangalia unadhani nilikubali tu kuolewa na

    Carlos?"

    "Swali gani hilo Sabrina?"

    Nikaona mama hana majibu ya kunivutia, nikaamua

    kwenda chumbani kwa dada Penina kumuuliza.

    Nikamkuta kama kawaida yake akichezea kompyuta

    yake, nikamuuliza swali ambalo hata mimi

    lilinichanganya.

    "Dada, niambie baada ya harusi mlirudi vipi na mimi

    nyumbani?"

    "Kivipi?"

    "Wewe niambie tu"

    "Baada ya harusi wewe ulikuwa umechoka sana,

    Carlos akasema kuwa kwa mila za kwao

    hawaruhusiwi kuondoka na mke akiwa amechoka,

    hivyo ikatubidi turudi nawe nyumbani na moja

    ukaenda kulala mpaka muda ule ulipoamka na kuanza

    kulia"

    "Hivi mliyerudi nae nyumbani mlimwangalia vizuri

    kweli kuwa ni mimi?"

    "Ndio ulikuwa ni wewe, kwani vipi?"

    "Mmh!! Haya niambie hiyo ndoa ilifungwa kanisani au

    msikitini?"

    "Inamaana wewe hujui ulipofungia ndoa? Au

    umesahau? Na utasahau vipi kitu cha jana tu?"

    "Naomba uniambie dada"

    "Kiukweli sijui, ila ilikuwa ni jumba kubwa na sisi

    tulibaki nje baada ya muda kidogo mkatoka na

    kusema ndoa tayari hapo ndipo tukaenda

    kusherekea"

    "Kwanini mlibaki nje?"

    "Tulichelewa kidogo kufika kabla yenu hivyo

    tukazuiliwa nje, tulilalamika sana ila hatukuweza

    kuingia hadi mlipotoka"

    Nikajaribu kutafakari ila nikakosa jibu, maelezo yale

    yalizidi kunichanganya tu maana mimi niliona

    tumefika wote kwenye lile jumba ila wao wakabaki nje

    halafu sasa ananiambia kuwa walichelewa kufika

    kwakweli alinishangaza sana jamani.

    "Wakina nani walikuwepo?"

    "Ndugu na rafiki zako kama Lucy na Suzy"

    Nikashangaa sana kuona wote wale wameshindwa

    kugundua kuwa ni kitu gani kimetendeka pale kwenye

    jumba, kwakweli ni swala la kusikitisha sana yani

    wote wamefumbwa macho na Carlos.



    Nikatoka chumbani kwa dada na kurudi sebleni,

    nikamkuta mama amekaa nikamuuliza

    "Hivi mama yangu wewe ni muumini wa wapi?"

    "Swali gani hilo? Kwani hujui?"

    "Haya niambie, ndoa niliyofunga jana nani

    ameishuhudia?"

    Mama akawa mkali gafla na kusema kuwa hataki

    maswali, moja kwa moja nikahisi kuwa ni Carlos

    kamchanganya.

    Nikainuka pale na kwenda kuoga maana muda wote

    nilikuwa na mawazo tu.

    Wakati naoga, likanijia wazo la kuhusu Sam kuwa

    atakuwa wapi maana sina kumbukumbu zaidi ya

    kwenye ile nyumba ya wageni kuwa alikabwa na yule

    kijana wa ndotoni, gafla nikahisi kama kuna mtu

    akinisugua mgongoni, nikageuka haraka sikuona

    yeyote. Hapo nikaanza kujimwagia maji haraka

    haraka ili nitoke, mara nikasikia sauti

    "Sidhani kama ni vibaya kumsugua mke wangu"

    Sikuweza kukaa zaidi bafuni, nikatoka haraka na

    kwenda chumbani kwa mama huku nikihisi kuwa

    huenda kuna usalama ila nikahisi kuna mtu mule

    chumbani wakati mama alikuwa sebleni muda huo.

    Nikakimbia tena na kwenda sebleni, mama akaniuliza

    "Mbona unakimbia kimbia wewe?"

    "Kuna kitu kinanifatilia"

    "Hebu acha maruweruwe na utulie mwanangu"

    Nikamuangalia mama na kumuona kama mtu

    asiyejielewa, kisha nikaenda mwenyewe chumbani

    kwangu kuvaa tena bila uoga wa aina yoyote ile sijui

    ni kitu gani kilinivuta tena kwenda chumbani.



    Jioni ya leo sikuwa na raha ukizingatia kwa matukio yote niliyosimuliwa, inaonyesha Carlos anauwezo mkubwa kushinda ninavyodhani kwahiyo natakiwa kuwa mpole na kufanya vitu kwa ufanisi mkubwa sana.

    Wakati nawaza yote hayo, alikuja rafiki yangu Suzy ambaye ni kipindi kirefu sana sijaonana nae zaidi ya kuambiwa kuwa alikuwepo kwenye harusi.

    Alikuja moja kwa moja chumbani, nikafurahi kumuona na tukasalimiana nae, akaanza kuniambia

    "Bado hujafungua ubongo wako shoga yangu kuwa Carlos ni mtu wa aina gani?"

    Nikafikiria aliloniuliza Suzy, ukweli ni kwamba swala hili lilinichanganya ila nikapenda kujua kile ambacho wengine wanajua kuhusu Carlos.

    "Niambie tu rafiki yangu nijue"

    "Nimeshakwambia mara nyingi tu na sitoacha kukwambia, Carlos si mtu mzuri"

    "Kwanini unasema hivyo?"

    "Kwanza kabisa sijawahi kuona harusi inafungwa halafu bibi harusi na bwana harusi wanarudi makwao, yani bibi harusi anaenda kwao na bwana harusi anaenda kwao badala ya kwenda mahali pamoja mmh!! Ila sikushauri kwenda kuishi kwa Carlos"

    "Kwanini Suzy?"

    "Kwasababu Carlos si mtu mzuri rafiki yangu"

    "Basi niambie Carlos ni nani?"

    "Carlos ni jini....."

    Kabla hajamalizia alichokuwa anaongea, nikashangaa gafla akijishika shavu na kuanguka chini, Nikamfata Suzy pale chini na kumuuliza kuwa tatizo ni nini, akaanza kueleza huku machozi yakimtoka nadhani sababu ya maumivu

    "Humu chumbani kwako hapafai Sabrina hapafai kabisa"

    Akainuka na kuanza kukimbilia nje, nadhani alipigwa kibao cha maajabu kama ambavyo mimi hupigwa.

    Nikatoka hadi sebleni ila hakuwepo alikuwa ameshaondoka tayari, nikamuuliza mama

    "Hata sisi wenyewe tumeshangaa hapa, kapita nduki. Kwani mmegombana?"

    "Hapana mama"

    Dada Penina nae akaingia ndani na kutuuliza kwa mshangao

    "Tatizo nini jamani mbona nimemuona Suzy anakimbia?"

    Mama akamjibu,

    "Hata mimi sielewi, sijui kapatwa na nini."



    Nilikaa pale sebleni na kujiuliza maswali bila ya kupata majibu ya aina yoyote ile kwani sikuelewa kitu kwakweli, mama akaanza kuongea na dada,

    "Unajua hii harusi inanishangaza sana, yani bibi harusi yupo nyumbani kwao! Sasa huyo bwana harusi yuko wapi?"

    "Mama, itakuwa kama alivyosema. Ni mila zao hawaruhusiwi kuondoka na mke akiwa amechoka"

    "Mmh hizo mila ndio mara yangu ya kwanza kuzisikia toka nizaliwe kwakweli sijapata kukutana na mila za hivyo"

    "Huwezi kujua yote mama"

    Nilitulia nikiwasikiliza na kusema kuwa laiti wangejua kuwa Carlos yupo ndani ya nyumba yetu muda wote wala wasingeuliza kitu.

    Wakati nikitafakari hayo, Carlos alikuja gafla na kukaa pembeni yangu nikaogopa sana ila mama na dada hawakumuona.

    Akaanza kuongea na mimi,

    "Naona ndugu zako hawajapenda wewe kurudi nyumbani kwenu baada ya ndoa"

    Nilikuwa kimya nikitetemeka huku nikiwaangalia dada na mama labda na wao wamuone au kumsikia Carlos ila hata hawakujishughulisha na mimi bali waliendelea kuwa makini na mazungumzo yao, huku Carlos akiendelea kuzungumza na mimi

    "Nataka nikuchukue mke wangu ili twende kuishi kwetu, nia yangu ni kukutaka wewe unizoee kwanza kabla sijakupeleka kwetu kuishi ila sababu ndugu zako wameanza maneno itabidi leo nikuchukue ukaanze maisha mapya"

    Nikaogopa sana ila kuinuka pale nilipokaa ikashindikana, nikaamua kumuita mama kwa nguvu kamavile mama alikuwa mbali kumbe ni palepale sebleni

    "Mamaaaa...."

    Mama akashtuka sana, na kusogea pale nilipo na kuniuliza

    "Una nini wewe?"

    Nikamuangalia Carlos pembeni na kumgusa mama kuwa aangalie pale alipokaa Carlos ila mama hakumuona na Carlos alikuwa palepale akitabasamu

    "Mama ona"

    "Nione nini Sabrina?"

    "Kuna mtu hapa"

    Mama akapashika pale alipokaa Carlos na kusema,

    "Mbona hamna chochote Sabrina?"

    "Kuna Carl....."

    Kabla sijamaliza, Carlos aliniziba mdomo kwa mkono wake,

    Mama akashangaa na kuniuliza tena,

    "Mbona sikuelewi mwanangu?"

    Ikabidi nibadilishe maneno, baada ya kuachiwa mdomo na Carlos

    "Nashindwa kunyanyuka mama"

    "Unashindwa kivipi?"

    Mama akanishi ka mikono na kuninyanyua, moja kwa moja nikakimbilia alipokaa dada Penina ili niwe katikati ya mama na dada kwani mama nae alikuja kukaa pembeni yangu na kuniuliza,

    "Kwani nini tatizo mwanangu?"

    Nikaangalia pale alipokuwa amekaa Carlos, alikuwa palepale akitabasamu na uoga ukanijaa zaidi, nikawa namuelekeza mama kuwa aangalie pale nilipokaa mwanzo ila bado mama hakuona chochote kile.

    Mara tukasikia mtu akibisha hodi, dada Penina akaenda kumfungulia.



    Alipofika nae sebleni alikuwa ni Carlos, mama na dada walimpokea vizuri tena kwa uchangamfu mkubwa.

    Uoga ukanizidi maradufu kwani pale alipokaa mwanzo aliendelea kuwepo pale pale na tabasamu lake.

    Kilichonishtua zaidi ni kumuona yule Carlos aliyeingia sasa akienda kukaa juu ya yule Carlos wa mwanzo halafu akaonekana kama mtu mmoja, nilifikicha macho kamavile sioni vizuri maana nilihisi kuchanganyikiwa kabisa, mama akaniambia kwa ukali

    "Mbona hivyo wewe unakuwa kama mtu mwenye degedege!"

    Niliendelea kutetemeka tu, yule Carlos akanyoosha mkono wake toka alipokaa na kunishika mkono wangu.



    Niliendelea kutetemeka tu, yule Carlos akanyoosha

    mkono wake toka alipokaa na kunishika mkono wangu.

    Nikazidi kutetemeka na kujaribu kumuangalia mama na dada kama wanaona jambo hili ila ilionyesha hawaoni chochote maana wao walikuwa kimya

    kabisa na hawakushtushwa na chochote zaidi ya kuendelea na maongezi kama kawaida.

    Mkono wa Carlos uliendelea kushika mkono wangu na

    kunipa ubaridi usio wa kawaida hadi nikaanza

    kutetemeka mwili mzima sasa yani kama wale watu wanaosumbuliwa na magonjwa ya barudi, kule kutetemeka kwangu ndio waliponiona kuwa

    natetemeka. Mama akanigusa na kuniuliza kama naumwa,

    "Vipi mwanangu unaumwa?"

    Sikuweza hata kuongea chochote kwajinsi

    nilivyokuwa natetemeka, kisha dada akaenda kuleta

    shuka ndani na kunifunika.

    Nikapitiwa na usingizi palepale.



    Niliposhtuka ilikuwa ni usiku sana tena nilikuwa chumbani kwangu, moja kwa moja nikajiuliza kuwa nani amenileta chumbani? Nikajisenea kuwa labda

    mama ndio kanileta, sauti ikasikika

    "Hapana, ni mimi nimekuleta mke wangu"

    Nikashtuka na kuangilia sauti inapotokea maana

    hakuwepo mtu yeyote, nikaanza kuogopa halafu ile

    sauti ikawa kama ya kicheko na kusema

    "Usiigope mke wangu Sabrina, mumeo jini nipo"

    Hili neno jini huwa linanitisha sana na kufanya

    niogope zaidi ukizingatia mtu mwenyewe haonekani.

    Nikainuka kwa uoga pale kitanda i ili iweze kutoka nje

    labda nikimbie, sauti ikasikika tena

    "Ningekuwa mimi ni wewe Sabrina ningezoea hali na

    kufanya vile mwenza wangu atakavyo ila kiburi chako

    kinakuponza siku zote"

    Taa ya chumbani kwangu ikazimika gafla kukawa na

    giza kubwa hadi nikahisi umeme umekatika nyumba

    nzima hapo ndipo uoga uliponizidi.

    Nikahisi mtu akinipapasa mwilini, nilipojaribu kupiga

    kelele nilishindwa kabisa, nikatetemeka sana na

    kuanguka chini. Nikapoteza fahamu hapohapo.

    Nilipozinduka tena nilikuwa chini kama nilivyoanguka

    ule usiku.

    Nikainuka na kujishangaa tu, ila palikuwa pamekucha

    tayari.

    Sikujua nini kilitokea wakati nimezimia, nikaenda

    kukaa kitandani na kuanza kujiuliza maswali bila

    majibu. Mlango wangu ukafunguliwa, aliyeingia

    alikuwa mama, moja kwa moja akaanza kuniuliza

    "Sabrina mwanangu hivi huwa una matatizo gani kwa

    wageni?"

    "Kivipi mama?"

    "Nimekungoja kwa hamu uamke nikuulize mambo haya maana kila siku unanitia aibu tu kwa mambo

    yako"

    "Mbona sikuelewi mama?"

    "Kwanini jana umefanya fujo kwa mgeni wa muhimu

    kama yule?"

    "Mgeni gani mama wakati ni Carlos yule"

    "Hata kama ni Carlos, ndio umuite jini? Hata hivyo

    hakuwa Carlos yule"

    Nikajiuliza kuwa nimemuita muda gani jini? Nikakosa jibu, na je yule alikuwa ni na ni?

    "Sasa yule ni nani? Hata hivyo

    Carlos ni jini kweli"

    Mama akashtuka sana na kuniuliza kwa mshangao

    "Unasemaje Sabrina?"

    Nikataka kumwambia tena ila nikashtukia napigwa

    kibao na mtu asiyeonekana hadi nikaanguka chini kwa

    maumivu, mama akainama pale chini na kuniangalia

    kwani damu zilinitoka mdomoni ikabidi mama

    anisaidie kuinuka kisha tukatoka nje.

    Tulipotoka nje, mama akamuita dada na kumuagiza

    maji kisha akaanza kunisafisha zile damu, dada

    Penina nae akauliza

    "Kwani tatizo ni nini mama?"

    Mama akajibu,

    "Hata sielewi kabisa, maana tulikuwa tunaongea

    vizuri tu mara gafla akaanguka na damu kuanza

    kumtoka"

    Dada akainama kuniangalia vizuri, ambapo damu ni

    nyingi zilizonitoka hadi nikahisi jino limetoka maana

    mdomo ulikuwa mzito kupita maelezo yani sikuweza

    kuzungumza chochote kwa maumivu.



    Baada ya kunisafisha kidogo, tukarudi ndani.

    Nikatulia na kumsikilizia mama kama alisikia

    nilichomwambia mwanzo kuhusu Carlos, ila ndio

    kwanza akawa anaongea mambo mengine kabisa

    kuhusu Carlos.

    Dada Penina ndiye aliyeanzisha tena mada za Carlos

    "Ila huyu Carlos mama ni wa ajabu, maana tangia

    kwenye harusi alivyoturuhusu turudi na Sabrina hapa

    yani ndio hadi leo hajatokea! Mume gani huyu?"

    "Hata mimi nashangaa mwanangu, mume wa hivi

    sijawahi kumuona kabisa labda ndio staili mpya

    jamani"

    Laiti wangejua kuwa Carlos yupo ndani ya nyumba

    yetu siku zote hata wasingeulizana wanachoulizana.

    Wakati maongezi yao yakiendelea, kwa mara ya

    kwanza tangia haya mauzauza ya harusi yanipate

    nikasikia simu yangu ikiita toka chumbani kwangu.

    Dada Penina akaenda kuniletea, kwakweli sikujua ameipata sehemu gani huko chumbani,

    akanikabidhi ile simu kuwa niongee naye niliiangalia

    kwa uoga bila ya kuipokea toka kwa dada kisha dada

    akaiweka pembeni yangu na kukaa huku akiendeleza

    maongezi na mama.

    Niliiangalia ile simu wakati inaita bila kupokea kwani

    namba ilikuwa mpya kwahiyo nikaogopa, dada

    akaniuliza sasa

    "Mbona hupokei hiyo simu wakati nimehangaika

    mwenzio kwenda kukuletea?"

    Mama kamjibu,

    "Atapokeaje wakati domo limevimba jamani. Hawezi

    kuongea vizuri huyo"

    Ukaingia ujumbe kwenye simu yangu toka kwenye

    ileile namba, nikaufungua. Umeandikwa hivi,

    "Unajua Sam alipo?"

    Nikashtuka sana kisha wazo la kuhusu Sam likaanza

    kunitawala, nikaamua kujaribisha kuipiga namba ya

    Sam ila ilipopokelewa moja kwa moja akajitambulisha

    kuwa yeye ni Carlos, ingawa sikuweza kuongea na ile

    simu ila nilitetemeka sana na kuogopa zaidi kwani ni

    muda gani amechukua simu ya Sam au kule kumkaba

    ilikuwa kweli? Machozi yakanitoka kwa kumfikiria

    Sam wangu ambaye sijui alipo, dada akaniuliza tena

    "Mbona unalia? Umepata ujumbe mbaya nini?"

    Mama nae akanishangaa na kusema,

    "Huyu mtoto siku hivi anaundugu na machozi maana

    muda wote yanamtoka"

    Kwakweli swala la hawa ndugu zangu kutokunielewa

    liliniuma sana kwani ndugu zangu hawakuelewa kila

    nilichojaribu kuwaeleza kwavile ninavyoelewa mimi.

    Mawazo ya sasa ni juu ya Sam, sikujua Sam alipo

    ndiomana nikaumia sana.

    Ujumbe mwingine ukatumwa na Carlos muda huo

    huo, nikaufungua na kuusoma,

    "Sam ninae mimi, na sitomuachilia hadi pale wewe

    utakapofata kile ninachosema mimi"

    Nikaogopa kidogo na kumshtua dada kwa mkono

    kisha nikampa ile simu ili asome ule ujumbe.

    Dada akachukua ile simu na kusoma, nikamuona

    akishtuka sana kupita nilivyotegemea hapohapo

    mama akamuuliza,

    "Mbona umeshtuka hivyo kwani ni nini?"

    "Ngoja nikusomee mama"

    "Hebu usome"

    Dada akaanza kusoma ule ujumbe hadi mimi

    mwenyewe nikashtuka,

    "Nimekukomesha Sabrina, na bado hilo domo hadi

    linyofoke wa kuolewa utakuwa wewe! Mimi ndio

    Salome bhana"

    Mama nae akashtuka,

    "Yani Salome ndio katuma ujumbe huo?"

    Dada akaitikia kuwa ni Salome ndio,

    "Yani huyu mtoto ananitakia nini na familia yangu?

    Kumbe yeye ndio ameniumizia mwanangu jamani!

    Ona Sabrina alivyovimba mdomo, jamani uchawi

    huu!"

    Mama akasikitika sana huku akimlaani Salome na

    wachawi wote, nikatamani kumwambia ukweli ila

    mdomo wangu ulikuwa na maumivu makubwa sana

    yaliyofanya nishindwe kusema ukweli juu ya hili.

    Mama na dada waliongea maneno ya kumponda

    Salome na wachaMungu wote duniani kuwa

    wanajifanya watu wema kumbe ni waovu.



    Mchana wa leo tukaamua kwenda kukaa nje ili tupunge upepo wa nje, muda kidogo tukamuona dada Salome akiwa ameongozana na watu wawili

    waliokuwa wamebeba vitabu vya dini mkononi,

    walipokaribia tu mama akainuka na kusema,

    "Muishie hukohuko, sitaki mtu yeyote nyumbani

    kwangu"

    Ila wakaendelea kuja na kutusalimia,

    "Hivi nyie hamsikii? Haswa wewe Salome, una nini na

    familia yangu? Unataka nini kwetu?"

    "Nahitaji mkombolewe"

    "Nenda ukajikomboe mwenyewe na uchawi wako,

    hapa kwangu sikutaki kabisa"

    Yule kijana mwingine akajaribu kuongea na yeye,

    "Hapana mama sio uchawi, tumewaletea neno la

    uzima litakalowaweka huru"

    "Hilo neno la uzima nenda kaipe familia yako ili nayo

    iwe huru. Mimi na familia yangu hatujafungwa

    kwahiyo subiri tukifungwa ndio uje na hilo neno lako

    la uzima tuwe huru. Haya ondokeni"

    "Mmefungwa na shetani bila kujua"

    Hapo ndipo walipo mkera mama zaidi, akaongea kuwa ukali sasa

    "Nimesema ondokeni"

    Ila bado hawakutaka kuondoka na wakaanza maombi yao, mama akaenda ndani na kutoka na upanga hivyo kufanya wale watu

    wakimbie wote ila wakasema kuwa

    "Tutaendelea kuwaombea ili Mungu awafungue"

    "Mbona mmekimbia? Mngebaki hapa niwachalange mapanga"

    Dada Penina alikuwa kimya kabisa kamavile na yeye

    alifungwa kinywa kama mimi.

    Hakuna la kufanya pale, mama akasema tuingie ndani

    ikabidi tu tumsikilize na kuingia ndani.



    Usiku ulipofika huku nikiendelea na maumivu yangu,

    alikuja Carlos na kukaribishwa kama kawaida, mama

    akamuuliza

    "Mbona hukuonekana tena tangia ile siku ya harusi?"

    "Majukumu yalinizidi mama"

    "Basi pole sana"

    "Asante, ila nimekuja kumchukua mke wangu"

    Mama akashtuka na kuuliza,

    "Mbona ni usiku jamani! Utamchukuaje muda huu"

    "Mama, kwani kuna muda maalum wa mtu

    kumchukua mkewe?"

    "Hakuna muda maalum ila sitaweza kukuruhusu

    uondoke na Sabrina usiku huu, ngoja pa kuche ili

    twende wote nami nikapajue anapokwenda

    mwanangu"

    Katika siku zote leo ndio nilimsikia mama akiongea

    maneno yenye pointi kiasi hiki, haijawahi tokea

    kabisa maana tangia Carlos aingie kwenye maisha

    yetu huwa anaongea maneno yasiyo na maana

    kabisa.

    Carlos akamuangalia sana mama, nadhani hata yeye

    hakuamini kama maneno yale yanatoka kwa mama

    yetu.

    Akaendelea kumpa maneno ya kumlainisha,

    "Ila sioni tatizo mama, nitaondoka na Sabrina leo

    halafu nanyi nitakuja kuwachukua siku nyingine ili

    mkapafahamu tulipo"

    "Haiwezekani kuondoka na Sabrina muda huu"

    "Utanikataziaje wakati ni mke wangu? Mi naondoka

    nae kwakweli"

    Mama akajibu kwa ukali sasa utafikiri ni mtu mwenye

    mashetani,

    "Nimesema Sabrina haondoki muda huu, ukitaka njoo

    mapema"

    Carlos akainuka kwa hasira na kuondoka bila ya

    kuaga.

    Nilikuwa kimya huku nikiwaza kuwa leo muda wa

    kulala kuna kazi maana hili sekeseke la muda huu ni

    khatari.



    Muda wa kulala ulipofika, nikaogopa kwenda

    chumbani kwangu kulala kwahiyo nikaenda kulala na

    mama chumbani kwake.

    Wakati usingizi umetupitia, kama kawaida akaja wa

    kunibeba na kunirudisha chumbani kwangu ambapo

    nikashtuka nikiwa chumbani ila hakuonekana mtu wa

    aina yoyote ile.

    Nikaanza kuogopa ndani, sauti ikasikika

    "Nina uwezo wa kukuchukua muda wote nitakao ila

    kwavile mama yako amekataa sitakuchukua leo ila

    nitalala nawe hadi kunakucha"

    Nikaanza kuangaza huku na huku ili nimuone, ila

    nikahisi kuna mtu yupo nyuma yangu amenishika

    mabega yangu, nikahisi kutetemeka na kusisimka

    mwili mzima. Nikageuka nyuma ila hapakuwa na mtu,

    ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu yangu ulitoka

    kwa Carlos

    "Unamtafuta nani Sabrina wakati unajua wazi ni mimi

    ambaye nipo chumbani kwako"

    Nikashtuka na kujiuliza kimoyomoyo,

    "Lakini uko wapi?"

    Nikasikia sauti toka mlangoni,

    "Niko hapa"

    Carlos aliingia mlangoni bila ya kufungua mlango,

    nikaogopa sana na kujiziba sura kwa kiganja cha

    mkono wangu.

    Carlos akanisogelea karibu na kuanza

    kunishikashika, uoga ukajaa moyoni mwangu

    nikatamani muujiza utokee mahali pale.

    Carlos akaendelea kunishika shika atakavyo huku

    mimi nikitetemeka kwa uoga.

    Mara gafla mlango wangu ukafunguliwa, nikashtuka

    sana.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Aliyeingia alikuwa ni mama ambaye moja kwa moja

    macho yake yakatua kitandani, na safari hii

    akamuona Carlos pale kitandani tofauti na kipindi

    kingine. Carlos akaniachia na kumuangalia mama

    kisha mama akamuuliza Carlos kwa ukali,

    "Umeingiaje humu ndani wewe kijana?"

    Gafla nikayaona macho ya Carlos yakibadilika rangi.



    Gafla nikayaona macho ya Carlos yakibadilika rangi.

    Yalikuwa na rangi ya ajabu halafu yakiwaka kama

    macho ya paka, mama nae aliyaona yale macho

    akajiziba uso na kuuliza,

    "Vipi macho hayo?"

    Sura ya Carlos nayo ikaanza kubadilika, si mama

    wala mimi aliyeweza kumtazama tena Carlos.

    Ilikuwa ni kitendo cha muda mfupi tu, Carlos

    akainuka na kumfata mama aliposimama, niliweza

    kumuona kwa kutumia staili ya kufumba na kufumbua macho.

    Nikaogopa sana huku nikihofia kuwa atamdhuru mama yangu. Ila alipomkaribia akamshika bega

    mama na kuwa Carlos wa kawaida, nikamshangaa

    mama akinywea kwa gafla kamavile sio yeye aliyekuwa akifoka, kisha akaanza kutoka nae

    chumbani.

    Nikainuka na kuwafata hadi sebleni, nikamsikia

    Carlos akijaribu kumshawishi mama

    "Samahani mama, nilimkumbuka sana Sabrina na ndio

    yeye aliyenifungulia mlango"

    Kisha akaondoka, mama akainuka kufunga mlango na kurudi

    sebleni.

    Akakaa chini kama mtu anayetafakari na kuanza

    kuongea na mimi,

    "Unajua Sabrina haya mambo mengine yataniua

    kwakweli. Huyu mtu umemtoa wapi? Mbona ni wa ajabu sana? Nashindwa hata kulala tena kwakweli."

    Nikamkumbatia mama huku machozi yakinitoka na

    kumwambia kimoyo moyo kuwa ndio mambo ambayo huwa nakumbana nayo kila siku bila ya wao kujua chochote kile kwahiyo imekuwa angalau kwangu kwa

    wao kugundua japo kidogo tu kile kinachonisumbua

    kila siku.

    Mama hakutaka tena kwenda kulala chumbani kwake

    peke yake kwa muda huo, tulikaa pale pale sebleni

    hadi usingizi ukatupitia na kulala hadi panakucha.



    Tulipoamka pale ilikuwa kwenye mida ya saa mbili asubuhi ambapo

    dada nae alitoka chumbani kwake na kuja sebleni

    kisha akamsalimia mama

    "Mbona mmelala sebleni na mwanao?"

    "Nitakwambia tu ila mbona hadi saa hizi! Huendi kazini leo?"

    "Nitaenda tu mama, hakuna tatizo"

    "Kazi gani hiyo mwanangu hadi saa mbili hii inaenda

    saa tatu hujajiandaa wala nini, hiyo ofisi imekuwa ya

    baba yako?"

    "Hapana mama, ila huwezi amini kwa hii kazi

    ninayofanya sasa. Yani hakuna muda maalum wa

    kuripoti kazini, halafu muda wowote unaotaka

    kuondoka unaondoka tu. Yani tunachofanya ni kusaini

    basi, na kama siku hujisikii kwenda basi huendi"

    Kwakweli hii kazi ilinishangaza sana hata mama pia

    alishangaa na kumuuliza dada,

    "Ndio hiyo kazi uliyotafutiwa na Carlos?"

    "Ndio mama, tena mshahara tunalipwa kila mwisho

    wa wiki tofauti na kazi zingine ambazo hulipwa kila

    mwisho wa mwezi tena mshahara wa mawazo. Huko

    nalipwa mshahara mnono amakweli hii kazi ningeipata

    tangia zamani ningenenepa sana mama yangu"

    "Hebu niambie kwanza, hiyo kazi ni kazi gani? Mbona

    mmh!! Nakosa hata jibu kwakweli"

    "Kazi yenyewe ni ya kupanga mafaili tu kwenye

    kompyuta wala hutumii nguvu wala kutokwa na jasho,

    muda wote mnatulia hadi pale mafaili yanapotumwa"

    Si mimi wala mama aliyeelewa muktabali wa hii kazi

    kwakweli, mimi ndio ilinishangaza kabisa na kujiuliza

    maswali mengi bila ya majibu.

    Dada akamwambia mama kuwa atanunua gari hivi

    karibuni maana mshahara wake wa sasa ni mkubwa

    sana.

    "Ila mwanangu, usimuamini sana huyo Carlos halafu

    jaribu kuichunguza hiyo ofisi vizuri"

    "Nichunguze nini mama? Kila mtu yupo busy na kazi

    zake pale na sio muda wote utakaowakuta watu

    ofisini ndiomana na mimi naenda nitakavyo"

    Nilijisemea kimoyo moyo, kama kweli kuna kazi

    kama hizi basi kila mmoja atapenda kuipata hiyo kazi.

    Moyo wangu uliniambia kuwa zote zile ni njama za

    Carlos katika kuiteka familia yangu tu lakini sikuwa na

    la kufanya juu ya hilo.

    Baada ya muda kidogo, dada akaenda kujiandaa na

    kutoka ila mama bado alikuwa akitafakari na kusema,

    "Bado nina mashaka na hiyo kazi anayofanya Penina,

    sijui kwakweli"

    Nadhani ufahamu wa mama ulianza kurejea kwakweli

    ndiomana ameweza kutambua mambo mengi

    yaliyojificha tangia mwanzo kwenye macho yake.

    Tukaendelea na kazi za hapa na pale ndani ya nyumba yetu.



    Baada ya muda kidogo dada Penina aliwasili

    nyumbani, moja kwa moja mama akamwambia

    "Kweli hiyo kazi kiboko mwanangu, yani hata hujakaa

    sana mmesharudi?"

    Dada akacheka kwa furaha na kutuambia,

    "Leo kuna sherehe imeandaliwa na ofisi, walisahau

    kutuambia jana. Kwahiyo inabidi leo jioni tujiandae

    twende"

    Mama akashangaa na kuuliza,

    "Kwani na sisi tunaenda?"

    "Ndio, kila mmoja ameambiwa awaandikishe watu

    atakaokwenda nao kwahiyo mimi nimekuandikisha

    wewe na Sabrina. Itakuwa kubwa sana hiyo sherehe"

    "Basi tutaenda mwanangu ili na sisi tukajishuhudie

    hiyo ofisi maana bado inanishangaza"

    "Basi jioni mjiandae mama"

    Dada alikuwa kabeba mfuko mkubwa ambao sikujua

    una kitu gani kwa muda huo, na kwenda nao moja

    kwa moja chumbani kwake.

    Nikainuka na kwenda chumbani kwangu huku

    nikiwaza kuhusu hiyo Sherehe maana nilipata

    mawazo mabaya kuhusu hiyo sherehe ambayo dada

    ameisema na moyo wangu haukuafiki kwenda kwenye hiyo sherehe kwani nilihisi kama kuna kitu kimejificha kati hapa.



    Nikiwa chumbani nikapitiwa na usingizi mzito sana,

    nikajiona nimevaa nguo yenye maua maua ambayo

    haipo kabisa kwenye nguo zangu za kawaida.

    Nilikuwa nimeongozana na mama na dada, halafu

    akatokea Carlos mbele yetu kisha akanishika mkono

    na kuondoka na mimi.

    Akanipeleka mahali kuna mlima mrefu sana kisha akanipandisha kwenye kilele cha mlima huo, na

    kunionyesha upande wa pili kwa chini ambako kulikuwa na miti mikubwa

    na mawe kwakweli palitisha sana yani kwavyovyote

    vile sehemu kama ile haikosi kuwa na nyoka

    wakubwa kama chatu.

    Akatokea mkaka mwingine aliyekuwa anatisha sana,

    aliyekuja huku akimburuta mtu aliyefungwa kitambaa

    machoni. Kumuangalia mtu yule moja kwa moja

    nikagundua kuwa ni Sam, hofu ikanijaa sasa, Sam

    alikuwa amechoka sana yani kama mtu aliyepigwa

    sana.

    Nikamkimbilia pale chini ambapo Sam alikuwa akivuja

    damu tu mwili mzima na kumkumbatia, yule kijana

    anayetisha akanisukumia pembeni kisha akamvuta

    Sam hadi kwenye ukingo wa ule mlima na kutaka

    kumtupa.

    Nilikuwa nalia sana ila hawakunisikiliza, wakamtupa

    Sam ambaye alipiga kelele za kupasua moyo wangu.

    Nikashtuka toka usingizini huku jasho jingi na

    machozi kunitoka, yale maumivu ya mdomo yalikatika

    gafla.

    Nilikosa raha kwakweli roho ikaniuma sana, maumivu

    yalijaa moyoni na sikuweza kuyavumilia na kujikuta

    nikilia kwa sauti.

    Mama akaja kuniuliza,

    "Una nini Sabrina?"

    "Sam mama"

    "Kafanyaje? Amekufa? Wewe ni mke wa mtu sasa

    hutakiwi kukumbuka wanaume wako wa zamani"

    "Mama jamani!"

    "Umeshapona mdomo unaanza makeke yako sasa"

    Kisha akatoka bila ya kufikiria zaidi.

    Roho iliniuma sana na kuomba kuwa iwe ndoto tu na

    sio kweli maana sipo tayari kumpoteza Sam wangu

    kwakweli.

    Katika swala la kuolewa sikujihesabia kabisa kama

    nimeolewa maana ndoa yenyewe ilikuwa na

    mauzauza.

    Nikachukua simu na kujaribu kumtafuta mtu yeyote

    anayeweza kuniambia chochote kuhusu Sam, ila

    muda huo huo nikatumiwa ujumbe na Suzy

    "Sabrina, mwenzio Sam karudishwa kwao kimaajabu

    akiwa hoi kabisa hata hatujui kitakachotukia"

    Nilihisi kuchanganyikiwa kabisa maana ule ujumbe

    ndio ulionimaliza nguvu, nikajaribu kumpigia Suzy

    lakini hakupatikana.

    Nikainuka na kuzunguka zunguka ndani bila ya

    kupata jibu la aina yoyote ile wala cha kufanya

    sikujua kwakweli.

    Nikatoka na kwenda kukaa sebleni huku nikiendelea

    na mawazo yangu maana sikuwa na la kufanya ila

    nilitamani kutoroka nyumbani ili niende kwakina Sam

    kumuona, tatizo ni kuwa naondokaje hapa nyumbani?

    Simu ya mama ikaanza kuita, nikaichukua Mimi na kumpa mama, mpigaji alikuwa ni Dada Salome ila mama hakutaka kupokea kabisa nadhani alianza kufungwa tena.

    Dada Salome akatuma ujumbe,

    "Tafadhali mama, jaribu kutafakari upendo wa Mungu juu yako. Tutakuja kwao jioni kufanya maombi tena"

    Nilipomaliza kusoma, mama akasonya na kusoma,

    "Niache kwenda kwenye misosomolo huko eti ningoje maombi ya huyu mchawi loh"

    Nikajaribu kumkumbusha mama kuhusu tulichokiona usiku kwa Carlos,

    "Hayo tutajadili kesho mwanangu, nitakupeleka kwa yule mjomba wako ajaribu kusema na yeye maana mimi hata sielewi."

    Nikajaribu kumuelewesha ila bado hakuelewa chochote kile amekuwa kama sikio la kufa maana ameona ila haelewi nadhani anataka kuona makubwa kushinda haya.



    Jioni ya leo kulikuwa na harakati za kujiandaa kwaajili

    ya hiyo sherehe, sikutaka kwenda kabisa na nikaona

    kuwa muda huo ambao hao wataondoka ndio

    nitautumia muda huo kwenda kumwangalia Sam.

    Mama alikuja chumbani kwangu kuniuliza kuwa

    kwanini sijiandai, nikasingizia kuwa naumwa

    "Sasa utabaki peke yako hapa nyumbani?"

    "Ndio mama nitabaki"

    Mama akatoka na kuendelea kujiandaa, Dada Penina

    nae akaja chumbani kwangu na ule mzigo aliokuja

    nao mwanzoni, akaniambia

    "Fumba macha Sabrina"

    Nikafumba, akaniambia tena

    "Fumbua uone surprise yako"

    Nikafumbua macho na kuona gauni kitandani, kisha

    dada akaniambia tena,

    "Hiyo ndio nguo unayotakiwa kuvaa leo, nimepewa na

    Carlos"

    Nikashtuka sana ila Dada akatoka nje, kuliangalia lile

    gauni lilikuwa ni lile lile nililolivaa ndotoni mchana,

    nikaogopa sana kuwa huenda niliyoyaota yote yana

    ukweli ndani yake.

    Nikaogopa kwenda kwenye ile sherehe na kusema

    kuwa sitakwenda, sauti ikasikika kwangu

    "Ole wako usije, na ole wako usivae hiyo nguo"

    Nikaogopa sana na kumuita mama kisha nikamwambia

    "Mama naomba tumngoje huyo Dada Salome kwanza"

    Mama akachukia na kutoka, kisha sauti ikasikika tena

    "Kama hutaki matatizo zaidi ya uliyonayo, vaa hilo gauni na uje "

    Nikaamua kuanza kuvaa, na nikawa wa kwanza

    kungoja wengine sebleni huku moyo wangu ukidundika kwa uoga, mama alipotoka nae

    akanishangaa

    "Si umesema unaumwa wewe! Nilitaka nishangae

    uache msosi wewe mmh"

    Dada nae akatoka na kunisifia kuwa ile nguo

    Imenipendeza huku akituharakisha kuwa tuwahi,

    Mara akapigiwa simu, baada ya kuongea nayo

    akatuambia,

    "Ni mfanyakazi mwenzangu huyu amenipigia kasema

    yupo nje anatungoja twendeni sasa"

    Moyo wangu bado ukawa mgumu kutoa maamuzi ya

    kuondoka, nikawa najigelesha mara nikasikia kama

    mtu akinichapa fimbo miguuni kitendo kilichofanya

    nikimbilie nje ila ndugu zangu hawakunielewa kabisa

    ndio kwanza Dada aliendelea kusisitiza kuwa

    tuondoke.

    Mama akanivuta mkono hadi kwenye gari ambayo

    dada amesema ni ya mfanyakazi mwenzie kisha

    tukapanda ila yule mtu hakutuangalia kabisa na safari

    ikaanza.

    Kufika mahali akasimamisha gari kisha akasema kuwa,

    "Tumefika jamani"

    Dada akahamaki,

    "Mbona sio hapa?"

    Yule mtu akacheka sana na kutugeukia, nikashtuka

    sana kumuona kwani alikuwa ni yule kijana wa

    ndotoni.



    Yule mtu akacheka sana na kutugeukia, nikashtuka

    sana kumuona kwani alikuwa ni yule kijana wa

    ndotoni.

    Sura yake ilikuwa ni ya yule kijana wa ndotoni.

    Niliogopa sana, dada akahamaki tena,

    "Mbona wewe sio mfanyakazi mwenzangu?"

    Macho yake yakabadilika na kuwaka kama taa, mama nae akamshangaa na kuuliza,

    "Mbona macho yako yanatisha sana?"

    Dada akasema tena,

    "Halafu sura yako imefanana na yule anayetokeaga kwenye kompyuta yangu?"

    Kila mmoja wetu alimuangalia yule kijana kwa tahadhari ila mimi niliogopa sana.

    Akatuangalia tena na kuanza kucheka, kisha akapuliza kitu kama majivu kwa mama na dada Penina.

    Ikawa ni kitendo cha sekunde tu, hapohapo mama na dada wakalala tena usingizi mzito wa kukoroma na kufanya mimi nizidi kuogopa zaidi na zaidi.

    Kufumba na kufumbua, mimi, dada na mama tukajikuta tupo kwenye chumba ambapo mama na dada walikuwa wamelala vilevile, kisha yule kijana akanishika mkono halafu akageuka na kuwa Carlos ambapo nilikuwa naogopa muda wote huku nalia.

    Akanitoa nje na kuniweka kwenye ukingo wa bustani kisha akaniuliza,

    "Unajua maana ya ndoto uliyoota?"

    Nikatingisha kichwa kwa kukataa kwamaana ya kuwa sijui huku nikijiuliza kuwa na hii ni ndoto au ni kitu gani maana sikuelewa kabisa haya mambo kwakweli.

    Carlos alikuwa anatisha sana kwenye macho yake yani huwezi kumtazama zaidi machoni pake.

    Carlos aliendelea kuningalia na kuwa kama mtu anayecheza na akili yangu na kufanya niogope kabisa.

    Mara kidogo akatokea Sam mbele yangu akiwa ameinamisha kichwa, kisha Carlos akaniambia kuwa nimshike kichwa Sam ila moyo wangu ukakataa na sikutaka kufanya makosa tena yani ni bora mimi nipate shida kuliko kumtesa Sam kiasi kile.

    Kitecho cha mimi kukataa kilimchukiza sana Carlos, nikainamisha kichwa chini, Carlos akanyoosha mkono wake na kuinuka kichwa changu kisha akaniuliza

    "Kwanini hutaki kumshika?"

    Nikatikisa kichwa tu kuwa sitaki na kuzidi kumuudhi Carlos, gafla nikashangaa nikipigwa kwa nguvu mgongoni na kuanguka chini kisha nikapoteza fahamu kabisa na wala sikujua kilichotokea zaidi.



    Nilipozinduka nilikuwa mahali penye watu wengi sana, nikashangaa huku nikiangaza macho kila mahali kwani sikuelewa chochote.

    Mbele yangu nikawaona mama na dada nao wakishangaa nadhani na wao ndio wamezinduka muda huo.

    Nikawafata kuwauliza, dada akasema kuwa yale ndio maeneo ya ofisi yao kisha muda kidogo akaja Carlos mbele yetu ambapo nikaanza kuogopa tena kwa kujua kuwa mambo ya ajabu yanaenda kujirudia, cha kushangaza mama na dada wakakazana kumshukuru Carlos kwa kuwaokoa huku wakisema kuwa aliyewabeba kwenye gari hakuwa mtu mzuri bila ya kujua kuwa ni huyo huyo Carlos ndiye aliyewabeba kwenye gari, nikajiuliza sana kuhusu uongo uliofanywa na Carlos kwasasa na kuwafanya waamini kuwa yeye ni mtu mzuri wakati mimi ametoka kunifanyia mambo ya ajabu muda mfupi tu uliopita.

    Nikawaangalia mama na dada na kusikitika ila siku zote kila chenye mwanzo hakikosi mwisho maana hata mimi alinidanganya hivi hivi mwanzoni ila sasa nimeshamgundua kwahiyo najua kuna kipindi ndugu zangu nao watamgundua Carlos na mambo yake yote.

    Carlos alitabasamu tu pale na kujifanya kamavile ni mtu mzuri kumbe sio mtu kabisa kisha akatupakiza kwenye gari yake na kuturudisha nyumbani, ilikuwa ni usiku sana na kufanya tulipofika tu twende kulala baada ya Carlos kuondoka ila kila mmoja hakutaka kwenda kulala chumbani na badala yake wote tulilala pale pale sebleni.



    Sikupata usingizi kabisa na kuona maruweruwe ya kila aina na kuanza kuogopa, akaja mtu mbele yangu aliyekuwa na kichwa kikubwa sana halafu mwenye asili ya umbilikimo na kuanza kunisogelea kisha akasema,

    "Shika kichwa changu"

    Nikaogopa sana kwani moyo wangu ukaniambia kuwa nisikubali kutenda kosa tena nami sikutaka kufanya makosa kwakweli.

    Yule mbilikimo akasema kwa ukali zaidi sasa

    "Nishike kichwa"

    Kwakweli sikuelewa anataka nimshike kichwa ili iweje ila bado moyo wangu ukanikataza kufanya hivyo, mara damu zikaanza kumtoka yule mbilikimo kisha akaanguka chini, muda huo huo umeme ukakatika na kufanya nizidiwe kwa uoga.

    Nikachukua simu ya mama iliyokuwa karibu pale ili niwashe tochi angalau kuwe na mwanga kidogo, mama na dada hawakuelewa chochote kile kinachoendelea maana usingizi ulishawachukua tayari kwahiyo hawakuona lolote linalotendeka.

    Wakati mambo yote yale yanatendeka, kuna ujumbe uliingia kupitia simu ya mama.

    Nikauangalia kwa uoga sana, ulitumwa na dada Salome kwa maneno machache kabisa,

    "Sema Mungu nisaidie"

    Nikashangaa nikipata ujasiri wa gafla na kusema,

    "Mungu nisaidie"

    Sikuacha kusema, ikawa kama wimbo mdomoni kwangu kwasasa ingawa uoga ulinijaa ila haya maneno yalinitia nguvu.

    Akatuma ujumbe mwingine ukisema,

    "Mwambie Mungu Asante"

    Nami nilikuwa nikifatilia na kusema,

    "Asante Mungu"

    Haikupita muda sana, umeme ukawa umerudi na pale chini hakikuonekana kitu chochote kile na wala sikutishwa na jambo lolote tena.

    Basi nilikaa na kujisemea Mungu nisaidie na Mungu asante muda wote maana niliona kamavile yale maneno yamenitoa kwenye yale majanga ya usiku.



    Asubuhi na mapema niliondoka nyumbani na kumuacha mama na dada wakiwa wamelala vilevile.

    Sikutaka kuwasumbua ila nilihitaji kwenda kuzungumza na dada Salome kuhusu usiku uliopita na mambo yake yote.

    Nikiwa njiani kuelekea kwa dada Salome nikakutana na mtu ambaye simfahamu ila alikuwa ni mzee sana, aliponiona akanisimamisha kisha nikamsalimia

    "Shikamoo"

    Akainamisha kichwa chake ili nimguse kichwani, nikataka kumgusa ila mkono wangu ukasita.

    Yule bibi akaniamgalia sana, na kuniwekea kichwa chake tena.

    Nikanyoosha mkono wangu, ila kuna mtu akaniita nyuma na kunishtua

    "Sabrina"

    Nikageuka nyuma, alikuwa ni dada Zuhuru, akanionyesha ishara kuwa nimfate.

    Nikamkimbilia na kumkumbatia, naye akanikumbatia na kunishika mkono.

    Nikafika nae mahali akaniambia,

    "Pole sana Sabrina, ila kila kitu kina mwanzo na mwisho wake. Muamini Mungu atakupa wepesi"

    "Asante dada"

    Nikamueleza nia yangu na mahali ninapotaka kwenda, dada Zuhura akaamua kunipeleka na kusema

    "Najua tatizo lako Sabrina, ndiomana nimeamua kukupeleka mimi mwenyewe"

    Aliponifikisha, akanikabidhi kwa dada Salome kisha akaendelea na safari yake.

    Dada Salome akanikaribisha vizuri sana kisha akakaa na kuzungumza na mimi kuhusu mambo yaliyojiri usiku uliopita. Akaanza kuzungumza na mimi,

    "Afadhari umekuja mdogo wangu, Mungu anakupenda sana"

    "Niambie kwanza, kwanini ule usiku ukanitumia ule ujumbe? Maana nilikuwa kwenye matatizo kweli ila ule ujumbe ukanisaidia sana"

    "Jana nilikosa usingizi kabisa baada ya kuwakosa ile jioni kwenye nyumba yenu, nikaambiwa moyoni kuwa mnamatatizo natakiwa nifanye maombi kwaajili yenu. Usiku wote wa jana nilikuwa napambana na haya mambo, kwavile Mungu ndio kila kitu ndiomana nikawatumia ujumbe kuwa mnatakiwa kuomba msaada kwa Mungu"

    "Asante kwa hilo dada, na Mungu asante je ilikuwa na maana gani pale?"

    "Mara nyingi watu hukumbuka tu kuomba mahitaji yao kwa Mungu ila hawakumbuki kutoa shukrani. Tunapomuomba Mungu tunaamini kwamba tutapokea, na kama tunaamini kwamba tutapokea basi yatupasa kushukuru. Hakuna jambo jema kama kumshukuru Mungu, unapolala unatakiwa kushukuru na unapoamka pia unatakiwa kushukuru"

    Maneno ya dada Salome yaliniingia vizuri sana na kujikuta nikimuelewa kupita nilivyotegemea na kumuuliza maswali kwa uhuru zaidi ukizingatia familia yangu si kama familia zingine sababu huwa hatuna misingi ya kuomba toka mwanzo, kwahiyo leo nikapata wasaa mzuri sana wa kuuliza nitakacho bila tatizo lolote lile.

    "Eeh na vipi kuomba msaada kwa Mungu ni kila wakati?"

    "Unamuomba Mungu msaada pale unapohitaji, mfano ukiwa unataka kulala, kwanza kabisa unamshukuru Mungu kwa kukufikisha muda huo halafu unamuomba akusaidie kwa kukulinda ili ulale salama. Na unapoamka, unatakiwa kumshukuru Mungu kwa kukuamsha salama na pia unatakiwa kumuomba Mungu akusaidie kwa siku hiyo. Kumbuka kwamba siku njema huanza na Mungu na pia huisha na Mungu, muweke yeye kuwa msingi imara katika maisha yako"

    "Mmh nitaweza kweli dada?"

    "Utaweza ndio, hakuna kinachoshindikana chini ya jua. Kila kitu kinatakiwa kwenda kwa mpangilio, mambo yote yatakuwa sawa mdogo wangu. Akili yako na mawazo yako umtumainie Mungu tu"

    Maneno yake yakaniingia sana katika akili yangu, nikamshukuru kwa yale maneno yenye nguvu kisha akaniambia,

    "Nisubiri kidogo, nikachukue biblia halafu tuje tufanye maombi kwa ufupi"

    Akaingia ndani, muda huo huo nikatumiwa ujumbe kwenye simu yangu.

    "Njoo hapa barabarani upesi, Sam kapatwa na matatizo"

    Namba ilikuwa ni mpya kabisa, nilihisi kama nashikwa na kiwewe kwakweli maana sikufikiria hata kuaga, niliinuka haraka haraka na kuondoka.



    Safari ilikuwa ni ya kuelekea huko barabarani nilipoambiwa huku akili yangu ikiwa kama inataka kupoteza uelekeo.

    Kufika barabarani nikaona eneo watu wengi wamejaa kama wakishangaa kitu, moyo wangu ulishtuka na kudundadunda kwa nguvu nilihisi labda Sam kapatwa na ajali.

    Nikakimbilia lile eneo la tukio kama mtu niliye na kichaa na kuwapita wote waliozunguka hadi katikati, nikakuta damu imetapakaa eneo zima na kijana akiwa chini hajitambui, bila hata ya kuangalia yule kijana ni nani nikaangusha kilio kwani sura yake ilifanana sana sana na Sam.

    Wakati watu wanamtoa yule kijana pale chini na kumpakiza kwenye gari, nami nikapanda gari ya nyuma yake kuwafatilia ili nijue hospitali anayopelekwa.



    Machozi na kilio kikuu vilijaa kwenye sura yangu, nilihisi kuchanganyikiwa kabisa hadi tulipofika hospitali.

    Nikamfatilia hadi wodini, alikuwa ni Sam kabisa.

    Nililia sana na kuwa kamavile mtu asiyejielewa, sikufikiria jambo lolote zaidi ya kufikiria kuwa Sam amekufa kwakweli.

    Wakampeleka hadi kwa daktari, kwahiyo mimi nikabaki nje.

    Mara kidogo akatoka nesi kwenye kile chumba cha daktari na kuja karibu yangu, kisha akaniambia

    "Wewe si ndio ndugu wa marehemu? Unaitwa na daktari"

    Moyo wangu ukapasuka kama vile mtu kaupasua kwa kuuponda, mwili wote ulinyong'onyea na miguu ilikosa nguvu kabisa, nikajaribu kusimama lakini nilijikuta nikikaa chini mwenyewe na machozi yakakatika, kwakweli nilichanganyikiwa baada ya kusikia kuwa Sam ni marehemu.

    Yule nesi akanifata tena na kuniambia,

    "Unaitwa na daktari dada ukauone mwili wa ndugu yako"

    Kwakweli sikuweza kuinuka, kila kitu niliona ni kizito kwangu.

    Viatu nikavua na simu nikaiacha chini ila nikajipa moyo na kwenda huko kwa daktari huku nikilia kilio ambacho hakieleweki kabisa.



    Nilipofika kwenye mlango wa kuingia kwenye chumba cha daktari, nilihisi miguu yote kufa ganzi.

    Nilifungua na kuingia kama mtu nisiyejielewa, Sam alikuwa kafunikwa kwa shuka nyeupe hadi kichwani, moja kwa moja nikakimbilia kwenye ule mwili na kumfunua nimuone kama kafa kweli.

    Nikasikia sauti toka kwa daktari ikisema,

    "Usimfunue"

    Lakini tayari nilikuwa nimeshamfunua, macho yangu yakakutana na macho ya Sam aliyekuwa pale kitandani bila ya kufumbwa macho, moja kwa moja chozi langu likaanguka kwenye macho yake ila ile sauti ya daktari ilinishtua sana kwani ilikuwa ni sauti ya mtu ambaye namfahamu.

    Moja kwa moja na yale mawenge niliyokuwa nayo, nikageuka kumtazama alikuwa ni Carlos aliyetisha sana usoni.

    Sikuweza kuendelea tena kukaa mule ndani, nikaanza kukimbia tena nilikimbia bila hata ya kuangalia nyuma kuwa kuna kitu gani cha kunifatilia.

    Nilikimbia sana tena bila hata ya kuchoka, ila nikajishtukia nimeshafika nyumbani.

    Kuingia mlangoni nikashtuka sana baada ya kukuta michirizi ya damu iliyotapakaa ndani.



    Kuingia mlangoni nikashtuka sana baada ya kukuta michirizi ya damu iliyotapakaa ndani.

    Moja kwa moja nikahisi kuwa mama na dada wamepata matatizo, nikaingia ndani kwa tahadhari sana huku moyo wangu ukidundadunda kwa uoga niliokuwa nao kwakweli.

    Nikatembea taratibu huku nikijaribu kumuita dada na mama, mara akatokea mtu na kunishika mgongoni na kunishtua kiasi cha kuzimia.

    Nikageuka kwa uoga, alikuwa ni dada Penina ambaye moja kwa moja aliniuliza kwanini nalia maana aliniona nikiwa na machozi usoni.

    Nikamuonyesha ile michirizi ya damu ambapo gafla ikapotea na kufanya nishtuke zaidi, dada akauliza

    "Mbona hakuna hiyo damu unayosema?"

    Kuangalia ile michirizi ya damu ikapotea gafla na haikuwepo tena, ikabidi nimuulize dada kuwa mama yuko wapi, akaniambia kuwa alimuacha sebleni wakati anatoka ila pale sebleni hakuwepo, tukaenda kumuangalia hadi chumbani kwake pia hakuwepo.

    Hofu ikatanda moyoni mwangu na kuhisi kuwa inawezekana mama amepatwa na matatizo.

    Nikataka kumueleza dada kuhusu yaliyojiri kwa Sam lakini nilishindwa na kujikuta nikiwa kimya tu huku akili yangu ikiwa kama imefyatuka hivi.

    Dada nae alikosa amani na kukaa pale sebleni kamavile mtu anayetafakari kitu fulani.

    Ikasikika sauti ya mtu akigonga mlango, nikaenda kumfungulia.

    Alikuwa ni dada Zuhura, nikamkaribisha ndani ila alikataa na kuniambia,

    "Nyumba yenu si salama Sabrina, hapa nje itakuwa vyema kufanyia mazungumzo"

    Nikaingia ndani ili kwenda kutoa viti tukae.

    Ila wakati natoa viti, nikashikwa miguu na mtu asiyeonekana kisha nikazibwa na mdomo na kukalishwa chini.

    Nilifurukuta ili niachiliwe lakini sikuachiliwa, zaidi zaidi nikamsikia dada Zuhura akiniita nadhani baada ya kuona nilipokawia kutoka ila kuitikia sikuweza na niliendelea kufurukuta pale pale chini hadi machozi yakaanza kunitoka lakini sikuweza kunyanyuka.

    Usingizi nao ukanipitia palepale, tena nikalala usingizi usio wa kawaida kabisa.



    Ndani ya ule usingizi wa ajabu nikamuona mama yangu akiwa kwenye mateso makubwa sana huku jasho jingi likimtoka, nikajaribu kumuita mama lakini hakunisikia na akaendelea kuteseka.

    Akafika mahali na kufungwa kamba mwili mzima bila hata huruma, akawashiwa moto mbele ili achomwe.

    Akaja yule kijana wa ndotoni mbele yangu na kusema,

    "Hivyo ndivyo nitakavyomtesa mama yako ukikataa kwenda na mimi nyumbani kwangu"

    Nikamuuliza kwa mashaka,

    "Unataka nini kwangu?"

    Akacheka na kunijibu,

    "Nataka kuishi na wewe ila unatakiwa ukubali kwa hiyari yako"

    Nikajiuliza moyoni, hivi ni mtu gani atakayeweza kukubali kuishi na jini ambaye kashamtambua kuwa ni jini tayari? Yule kijana akajibu,

    "Ni wewe Sabrina, unatakiwa wewe kwa hiyari yako mwenyewe kukubali kuishi na mimi. Hapo ndio itakuwa mwisho wa mateso yako na mateso kwa ndugu zako wote"

    "Sam je atapona?"

    "Hata huyo Sam pia nitamuacha huru"

    Kisha akanipeleka mahali ambako nilimuona Sam akiwa amefunikwa shuka nyeupe hadi kichwani kama alivyofunikwa kule hospitalini na kuniambia,

    "Kosa lako ni kumfunua huyo Sam na kumuangushia machozi, umefanya kosa kubwa sana kwetu ila imekuwa ni nafuu kwako kwani haitawezekana tena kummaliza Sam kwasasa badala yake ataendelea kupata mateso kila siku hadi pale wewe utakapoamua kufatana nami"

    "Inamaana Sam angekufa kweli?"

    "Ule ulikuwa ni muda wake ila wewe umeharibu, na kumfanya aendelee kupata mateso yetu"

    Nilisikitika ila kwa upande mwingine nilijipongeza kwani siko tayari kumuona Sam akifa kwaajili yangu.

    Yule kijana wa ndotoni alizidi kunitisha kuwa atammaliza mama yangu kama sijafata kile anachosema, kisha akatoweka mbele yangu nami nikashtuka toka kwenye ule usingizi wa mauzauza.

    Nikashangaa kujikuta chumbani kwangu tena kitandani wakati nilipopitiwa na usingizi sikuwa kwenye chumba changu.

    Nikakaa sasa na kutafakari kuwa je nikubali kuondoka na lile jini ili ndugu zangu wapone mateso au niendelee kukataa na mateso nayo yaendelee kuniandama na familia yangu?

    Nikainuka na kwenda sebleni, ile kufika tu sebleni nikakanyaga kitu cha ajabu kilichofanya nipige mweleka hadi chini.

    Nikahisi kiuno na mgongo vimeacha kufanya kazi gafla kwa yale maumivu niliyoyapata, mama nae akatoka chumbani kwake huku anachechemea.

    Akashangaa sana kuniona pale chini,

    "Vipi na wewe Sabrina? Ulikuwa wapi muda wote?"

    "Nililala mama, ila hapa nimeanguka"

    Mama akakaa pale chini kwa lengo la kuniuliza na kunitazama vizuri.

    "Ila mimi nilikuja hadi chumbani kwako mwanangu nikakukosa"

    "Kweli mama nililala"

    Nikamuuliza kuwa na yeye mbona anaonekana kuchechemea kwani ana tatizo gani, mama akaanza kunielezea

    "Mimi sikuwepo ila niliporudi nimemkuta Penina ameanguka chini, kaniomba nimsaidie kunyanyuka na kumpeleka chumbani, nikamwambia kama anajisikia vibaya nimpeleke hospitali amekataa. Kwahiyo nikampeleka chumbani kwake. Wakati natoka ndio nimejikwaa ndiomana nachechemea sijui kuna nini humu ndani leo!"

    Mama alitulia tuli akitafakari kwa kina haya mambo yaliyopo humu ndani.

    Muda kidogo dada nae akatoka chumbani na kuja sebleni, akashangaa pia kutukuta pale chini.

    Mama akamuelezea kilichotokea, dada akasikitika sana na kusema.

    "Humu ndani kuna kitu hata mimi nimeligundua hilo maana haiwezekani kabisa kuwa kama hivi ilivyokuwa"

    Mama akauliza kwa haraka,

    "Tufanyeje sasa kwa hili?"

    "Sijui mama"

    Nami nikajisikia kusema na kujikuta nikisema,

    "Hakuna la kufanya zaidi ya kumuomba Mungu"

    Mama na dada waliniangalia na kuafikiana na mimi kwa nililolisema na kukubaliana kuwa tuanze maombi kama wengine, mimi nikawaeleza kile nilichoambiwa na dada Salome ingawa sikuwaambia kuwa nimeambiwa na yeye.

    Nikawaeleza kuwa tunatakiwa kumuomba Mungu atusaidie na kumshukuru kwakuwa tunajua atatenda.

    Mama akashangaa sana kwa maneno niliyoyatamka mimi, na kuniuliza

    "Umejifunza wapi maneno ya Mungu mwanangu?"

    "Ni Mungu mwenyewe kanifunulia"

    Mama na dada wakaanza kunicheka baada ya kusema hivyo, dada akasema

    "Makubwa mwaka huu, yani hadi Sabrina kafunuliwa na Mungu mmh!"

    Mama akadakia,

    "Mungu aache kuwafunulia watu wote duniani akakufunulie wewe Sabrina mwenye mauzauza! Mbona makubwa kweli"

    Wakacheka sana ila mimi nikatulia na kuendelea kutafakari, sikuwaona na kosa sababu hawayajui mengi yanayotokea kwenye nyumba yetu. Hawajui jinsi gani macho yetu yamefungwa ili tusione ila imani yangu ni kuwa yote haya yatakwisha siku moja tu.



    Usiku ulipofika kabla ya kwenda kulala nilichukua simu ya mama na kukaa nayo maana dada Salome anapenda sana kuitumia simu hiyo kuliko kuitumia simu yangu labda amegundua tatizo lililopo kwenye simu yangu.

    Ujumbe ukaingia kwenye ile simu ya mama, halafu mama nae akasikia kama kuna ujumbe umeingia na kuning'ang'ania kuwa nimpe simu yake.

    Ikabidi nimkabidhi yeye mwenyewe, baada ya muda akaguna na kutuambia

    "Eti Salome kanitumia ujumbe kuwa mkumbuke kusali, sijui anakichaa huyu ! Kwani sisi hatujui kama kuna kusali au umbea wake tu"

    "Ila mama, anachotuambia dada Salome ni kweli maana sisi huwa hatulikumbuki hilo hata mara moja"

    "Basi usijali mwanangu, leo tutasali"

    Tukafanya mambo yote hadi muda wa kulala ulipowadia, kabla ya kwenda kulala nikamkumbusha mama kuhusu kusali ila kabla hatujaanza kuomba tukasikia mtu akigonga mlango, ikabidi tuache na kwenda kumfungulia.

    Alikuwa ni Carlos kitu ambacho kilitushtua wote, mama akamuuliza kwa mshangao

    "Mbona usiku sana Carlos? Unajua ni saa tano saizi!"

    "Naelewa mama ila nimekuja kwasababu maalum"

    "Ipi hiyo"

    "Mtaijua tu muda mfupi ujao , hata msijali"

    Tukawa kimya wote huku tukijiuliza kuwa ni kitu gani kinachotaka kuendelea mahali hapo.

    Dada Penina nae akauliza,

    "Ila mbona unatutisha Carlos? Unajua ni usiku huu? Bora ungetuambia tu tujue kabisa"

    "Mimi sitaki kuwatisha ila ninyi ndio mnaotaka kunitisha mimi. Ngoja niwaulize swali"

    Tukatulia kimya kusikiliza swali la Carlos,

    "Nina tofauti gani na binadamu wengine"

    Tukajikuta tukiangaliana halafu mama akamjibu,

    "Huna tofauti yoyote na binadamu wengine"

    "Jibu zuri mama, hata nikiondoka nitaondoka kwa amani."

    Akaniangalia mimi kwa makini na kuniuliza,

    "Na wewe Sabrina, je kuna tofauti yoyote kati yangu mimi na binadamu wengine?"

    Huku nikitetemeka, nikamjibu

    "Ndio kuna tofauti"

    Akiniangalia kwa hasira zaidi akaniuliza,

    "Ipi hiyo?"

    Nikajibu kwa ujasiri sasa kwani najua uwepo wa mama na dada utanisaidia mimi,

    "Wewe upo tofauti na binadamu sababu wewe si binadamu ni jini"

    Carlos akacheka sana tena kicheko cha ajabu hadi mama na dada wakajiziba masikio kwa kile kicheko, kisha akasema

    "Kama umekubali na kusema mwenyewe kuwa mimi ni jini, basi leo nitakuonyesha ujini wangu ulivyo kwa faida na hasara zake"

    Na kuendelea kucheka sana.

    Uoga ukanijaa na kujikuta nikitetemeka na kujilaumu kuwa kwanini nimeropoka kitu cha namna ile, bora ningekuwa kimya tu.

    Carlos aliendelea kucheka tu, mama na dada walikuwa kama watu wasiojielewa kwani hawakuweza kusema wala kuuliza chochote kile.

    Carlos akatulia sasa pale sebleni na wala hakucheka tena ila aliniangalia tu tena sana utafikiri mtu anayenifananisha lakini mimi niliendelea kuogopa na kutetemeka.



    Baada ya muda kidogo Carlos akaniuliza,

    "Je, upo tayari kuuona ujini wangu"

    Nikatikisa kichwa kama ishara ya kukataa, akaongea kwa kufoka sasa

    "Nimekusaidia sana Sabrina, nimewasaidia sana ndugu zako lakini wewe kutoa fadhila kwangu japo kwa ufupi tu unaona kazi! Nia yangu ilikuwa ni nzuri sana kwako na kwa maisha yako ila wewe hutaki jema bali unataka mabaya, nami nitakuonyesha ubaya na mabaya yana sura gani na yana kuwaje"

    Machozi yakaanza kunitoka, akaniambia tena

    "Hutakiwi kulia Sabrina, unatakiwa kucheka na kufurahia kwa maana nitakupeleka kwenye nchi nzuri yenye watu wa kipekee ambao hawanashida ya madaladala ila wakitaka kwenda mahali wanaenda tu kwa mawazo. Ni watu wa kipekee, wenye uzuri wa asili"

    Nikaendelea kutokwa na machozi, huku nikijiuliza nitaponea wapi kwa lile janga ambalo limenikumba kwa sasa.

    Carlos hakuacha kuniangalia kwa macho yake makali na ya kutisha sana.

    Akanyoosha mkono, vikashuka visu viwili vinavyong'aa sana.

    Ilionyesha kuwa vile visu ni vipya kabisa.

    Akaviweka mezani, kimoja kiliangalia upande wa mama na kingine upande wa dada kisha akaniambia,

    "Unatakiwa kufata ninachosema mimi, ukikataa tu nitaruhusu hivyo visu viwachome ndugu zako"

    Leo nikayakumbuka maneno ya wifi Joy kuhusu Carlos kuwa sio mtu mzuri hata huyo wifi Joy sikujua alipo na anaendeleaje na lile sakata lake la mtoto.

    Nikamuangalia tu Carlos kwa jicho la huruma kuwa labda atanisamehe na kunihurumia, akanyoosha mkono wake kwangu kuwa nimpe mkono wangu, nikasita kumpa mkono, akaonyesha ishara kwa vile visu na vyote vikanyanyuka na kumuelekea mama na dada, nilipoona vinawakaribia nikampa mkono Carlos huku nalia kisha akashusha vile visu na kutoka na mimi hadi nje halafu akaniambia nifumbe macho kwakuwa nikiangalia nitaogopa sana, nami nikafumba macho na kujihisi kama nikipaishwa angani.

    Niliogopa sana ila sikuwa na la kufanya na wala sikuweza kufumbua macho tena.



    Muda kidogo Carlos akaniambia nifumbue macho, nilipofumbua nilikuwa kandokando ya bahari pamoja na Carlos kisha akasema

    "Mwisho wa Carlos sasa, karibu kwa jini bahari"

    Muda huo huo akageuka na kuwa yule kijana wa ndotoni.





    Muda huo huo akageuka na kuwa yule kijana wa ndotoni.

    Nikaogopa zaidi, akaniangalia na kutabasamu kisha akanyoosha mkono wake kwangu na kutaka niushike nikakataa na kuanza kukimbia ila hakunikimbiza wala nini bali alikuwa akicheka tu.

    Nilikimbia sana hadi nikachoka maana ilikuwa ni giza sana pale baharini, nikawa nahema kama jibwa koko.

    Nikashtukia kama mkono ukiviringita kwenye kiuno changu, kisha nikabebwa na kuvutwa.

    Nikajikuta nimerudishwa pale pale kwa yule kijana wa ndotoni huku akiendelea kucheka na kuniambia,

    "Ilimradi tumefika hapa mlangoni huwezi tena kunikimbia Sabrina, ngoja nikuonyeshe"

    Akatoa mkono wake tena na kuanza kuurefusha na ukawa mrefu kupita maelezo kisha akaanza kujirefusha na yeye. Akawa mrefu hadi haonekani tena na gafla akapotea hapohapo ndio nikapatwa na kiwewe kabisa nikaanguka na kuzimia.

    Sijui akanifanya kitu gani ila baada ya muda kidogo nikazinduka.

    Tulikuwa palepale baharini, yeye alikuwa pembeni yangu kwakweli nilikuwa natetemeka sana kwa upepo wa bahari na uoga pia.

    Akawa ananiangalia sana na kusema,

    "Muda umefika sana wa mimi na wewe kwenda kwetu"

    Nikajaribu kumuomba sana na kumsihi asinipeleke kwani moja kwa moja nilijua ndio utakuwa mwisho wangu na mwisho wa maisha yangu. Yani mwisho wa kuwepo kwa Sabrina mimi kabisa.

    Nikaogopa sana na kutetemeka kupita kiasi, yule jini akainuka kabla yangu na kusimama.

    Niliinama chini na kusema Mungu nisaidie, akaniangalia sana tena kwa jicho kali halafu akainua kichwa chake na kutazama juu ya anga gafla nikamuona kama akifikicha macho, nikatumia muda huo kuanza kukimbia tena.

    Nilikimbia sana tena sana, safari hii sikutaka kusimama kabisa hadi nikafika kwenye barabara kuu.

    Wakati navuka, ikatokea gari ambayo sikuiona kwakweli.

    Ile gari ilitakiwa kunigonga kabisa ila nilishangaa nikiinuliwa juu halafu lile gari likapita chini yangu.

    Sikujiamini pale juu na kuanza kuogopa kwani nilikuwa kamavile naning'inia.

    Nikaogopa sana kwakweli, ila gafla tu nikawekwa pembeni halafu yule jini alikuwa pembeni yangu akanizabua kibao ambacho kilinipa kizunguzungu hadi nikaanguka chini na kuanza kulia.

    Safari hii hakunivuta ila aliniburuta na kusema kuwa niache kumsumbua.

    Aliniburuta sana na kunirudisha kule kando kando ya bahari.

    Ikabidi niwe mpole na kutulia chini kwani sikuwa na la kufanya ingawa maumivu niliyoyapata wakati wa kuburutwa ni makubwa mno ukiachana na lile kofi nililopigwa pale barabarani.



    Nikiwa nae pembezoni mwa bahari, akaanza kunihoji maswali ambayo nilitakiwa nimjibu kwa ufasaha kabisa,

    "Niambie kati ya mwanamke na mwanaume ni nani anayetaka kuolewa?"

    Nikakaa kimya maana swali lake lilikuwa na utata, nilikuwa naogopa na kutetemeka hata usoni sikuweza kumtazama maana sura yake ilikuwa ikibadilika badilika kila muda na kunifanya mimi niogope sana na kuinama muda wote.

    Akakishika kichwa changu na kuniangalia huku akiniambia kwa ukali kuwa nimjibu, nikafumba macho yangu na kumjibu.

    "Ni mwanamke"

    "Wewe je ni mwanamke au mwanaume?"

    "Ni mwanamke"

    "Kati ya mimi na wewe nani kaolewa?"

    "Ni mimi"

    Akacheka sana na kuniuliza tena

    "Sasa kwanini unanisumbua?"

    Nikaendelea kulia, huku na yeye akiniuliza kwa ukali

    "Nijibu kwanini unanisumbua?"

    Nilijikuta nikimjibu hivi,

    "Kwasababu wewe sio Carlos"

    Akacheka tena na kuniambia,

    "Umejibu vyema, ni kweli kabisa mimi sio Carlos ila je ulitaka kuolewa na Carlos?"

    "Hapana nataka kuolewa na Sam"

    "Unakumbuka maneno uliyosema miaka ya nyuma wakati unasoma?"

    Nikatikisa kichwa kwamaana sikukumbuka chochote nilichosema kipindi ninasoma, kisha akaniambia

    "Mimi nitakukumbusha Sabrina na utaelewa kwanini nimefanya yote haya kwako"

    Nilikuwa nimeinama tu kama kondoo anayetaka kuchinjwa nikimsikiliza huyu mtu wa ajabu aliyekuwepo mbele yangu, anayefanya nikose raha na amani ya maisha.

    Akaniangalia tena na kuniuliza,

    "Unamjua Carlos vizuri?"

    Nikatikisa kichwa kuwa simjui,

    "Ni kweli humjui Carlos vizuri ila Carlos bila mimi hawezi kufanya jambo lolote lile. Nataka kukwambia mambo mawili ya kuchagua"

    Nikauliza,

    "Yapi hayo?"

    Kwani nilihisi kuwa labda itakuwa na unafuu kwa haya mambo ninayopitia kwasasa,

    "Chagua moja kati ya haya, moja kwenda kufatilia ukweli kuhusu Carlos hadi utambue kuwa Carlos ni nani na kwanini awe yeye katika kukufatilia ila baada ya hapo maisha yako yatakuwa ya shida kama binadamu wengine. Mbili, ukubali kwenda na mimi kwenye mji mzuri wa ujinini na baada ya hapo maisha yako wewe na familia yako yatakuwa mazuri kupita kawaida hadi wote wanaowazunguka watawashangaa na utaheshimika na kila mtu na kupata kila kitu unachotaka katika ulimwengu huu. Nitakupa uwezo wa ajabu na hakuna hata mtu mmoja atakayeweza kukusumbua tena"

    Nilisikiliza kwa makini sana, na muda huohuo yule jini akageuka na kuwa Carlos huku akitabasamu, nikaogopa sana, yeye akaniambia

    "Hutakiwi kuniogopa tena, unatakiwa kunizoea na kuna wakati ambao sitabadilika tena na kuwa Carlos."

    Nikamuuliza tena,

    "Kama wewe sio Carlos, basi wewe ni nani?"

    Akatabasamu na kunijibu tena,

    "Mara ngapi nikwambie Sabrina? Mimi ni jini"

    Neno lake la jini siku zote huwa linafanya niogope sana na kutetemeka sana, nikakaa kimya kabisa. Akaniuliza tena,

    "Jibu langu la machaguzi utanipa muda gani? Au unahitaji muda wa kufikiria?"

    Nikaona ni vyema kama akinipa muda wa kufikiria kile alichoniambia,

    "Nikupe siku ngapi?"

    "Siku tatu"

    "Sawa, nakupa siku tatu ila hizi siku tatu hutokuwa nyumbani kwenu, utakuwa na mimi mpaka pale utakaponipa majibu yangu"

    Nikawaza sasa, yani nibakie nae kwa siku tatu? Je nitaweza! Kama usiku mmoja tu wa leo nimejihisi kama roho inatoka je hizo siku tatu ndani ya mikono ya jini itakuwaje.



    Muda huohuo, nikajikuta kwenye nyumba kubwa yenye kila kitu ndani yake.

    Nikaanza kuishangaa ile nyumba na kila kilichomo ndani yake, nilikuwa peke yangu ndani yani hapakuwa na mtu yeyote yule zaidi yangu.

    Nikaona kuna karatasi limeandikwa na kuwekwa mezani, nikalichukua na kulisoma

    "Kwa siku hizo tatu utaishi humu ndani na baada ya hapo nitakuja kuchukua jibu ya kile nilichokwambia uchague"

    Nilikisoma kile kikaratasi mara mbili mbili, muda mwingine nilijihisi kamavile nipo ndotoni ila haikuwa ndoto bali ni ukweli mtupu.

    Tena ni ukweli ambao unanishangaza sababu umebeba sura ya kimaajabu.



    Nikiwa mule ndani, nikajaribu kuangaza kila mahali kuona kama nitapata mlango wa kutoka nje ila hapakuwa na mlango wa aina yoyote ile kusema ni wa kutokea nje, kila kitu kilikuwepo palepale mahali pamoja.

    Nikakaa kwenye moja wapo ya kochi mule ndani na kujitazama mwili wangu uliojaa michanga sababu ya kuburuzwa.

    Nilikuwa kamavile naangalia sinema ila ni kitu cha ukweli kabisa kinachonitokea, muda haukupita sana nikapitiwa na usingizi pale pale.



    Nilipoamka sikujua kama kumekucha au ni usiku unaendelea maana ile nyumba ilikuwa ni ya ajabu na sikuweza kufanya chochote cha kuniwezesha kujua kuwa kuna nini ambacho kinanizunguka nje kwahiyo sikuelewa jambo lolote lile.

    Nilikaa na kuangalia mwili wangu ambao ulikuwa bado umetapakaa michanga, nikatamani kuoga na bafu lilikuwepo ila nilikuwa naogopa sana.

    Wakati nikitazama huku na kule nikashangaa chakula kipo mezani, niliogopa kukila ila njaa ndio iliyonifanya nikile na kusema liwalo na liwe, hata iwe nimewekewa sumu kama nikifa iwe basi.

    Niliendelea kuishi kwenye hii nyumba kwa mashaka sana.



    Maisha ya humu yalinitisha kwakweli maana kuishi peke yangu sijazoea kabisa na ukizingatia nyumba yenyewe ni ya ajabu kiasi hiki.

    Kuoga ndio niliogopa kabisa kwani muda wote nilihisi kuchungulia na sikutaka mtu wa kunichungulia.

    Gafla ule mwanga uliokuwa ukiangaza kwenye ile nyumba ukapotea na kuwa na giza, hapo ndipo uoga uliponitawala zaidi kwani giza lilikuwa ni kubwa sana.

    Nikajaribu kupapasa papasa mule ndani lakini sikufanikiwa kupata chochote cha kunipa mwanga.

    Katika harakati za kuhangaika mule ndani nikashangaa nikiguswa na kitu kama mtu, kwa uoga nikarudi nyuma na kuanguka kwenye kochi huku nikitetemeka.

    Hisia zangu zikaniambia kuwa kwa vyovyote vile mule ndani kuna mtu na lazima atakuwa Carlos tu au yule jini ndiye anayenitisha, nikaogopa sana.

    Nikiwa pale kwenye kochi nikaguswa tena bega, nikapiga kelele na kurukia upande mwingine na yule mtu nae akapiga kelele.

    Nikajihisi kuwa nimeumia kwenye mguu wakati nimejirusha upande ule mwingine maana maumivu niliyoyapata yalikuwa makubwa sana na sikuweza hata kusimama tena nadhani nilijigonga kwenye ile meza ya pale ndani.

    Kwavile nilipopiga kelele nikamsikia yule mtu akipiga kelele pia, nikajikuta nikinyamaza gafla na kuuliza kwa upole.

    "Wewe ni nani?"

    Na yeye akaniuliza pia

    "Wewe ni nani?"

    Akafanya nizidi kuogopa ila sauti yake ilikuwa kama sauti ninayoifahamu, nikauliza tena

    "Niambie wewe ni nani?"

    Naye akarudia kama nilivyosema, nikamwambia kuwa mimi ni Sabrina.

    Akashangaa sana na kuuliza kuwa mimi kweli ni Sabrina, nikamwambia ni kweli.

    "Kweli kabisa au naota?"

    Muda huo huo mwanga ukarejeshwa mule ndani, alikuwa ni Sam na sikuamini kabisa ila mguu wangu ulikuwa unavuja damu nadhani ni kutokana na kujigonga kwenye ile meza.

    Sam akanifata na kuniangalia kwa makini, sijui na yeye alikumbwa na vitu gani hadi kuwekwa kule ila sikumuamini sana sababu mara ya mwisho nilimuona akiwa amekufa. Ingawa nilijua wazi kuwa zile zilikuwa ni njama za Carlos kuwa Sam amekufa lakini nikamuuliza ili nipate uhakika zaidi kuwa ni Sam ninayemjua mimi,

    "Si ulikufa wewe Sam?"

    "Hapana Sabrina sijafa ila nilikuwa kwenye mateso makubwa sana hadi muda ulipokuja kuniona kwenye ile hospitali nilikuwa nakuangalia Sabrina sema sikuweza kusogea wala kuongea ila chozi lako likanipa nguvu"

    Nikashangaa na kukumbuka neno alilosema Carlos kuwa nilifanya kosa kumfungua Sam wakati nimepewa taarifa kuwa amekufa. Nikamuuliza Sam,

    "Ni nini kilikutokea kwa mara ya mwisho kule guest?"

    "Ni historia ndefu Sabrina ila umefanya niweze kuingia kwenye maisha ambayo sikuyatarajia, umefanya niteseke. Sijui ndugu zangu walipo wala sijui mimi nilipo ila nateseka na kuumia kwa kosa dogo tu nililofanya katika maisha yangu"

    Nikajisikia vibaya sana kwani nilijua Sam ananilaumu kwa kila kitu kilichotokea katika maisha yake, kwa upande mwingine ni kweli mimi ndio ninayestahili kupata adhabu hii kwani ndiye niliyesababisha kila kitu.

    Nikamuomba msamaha Sam ila hakusema chochote, akaja karibu yangu zaidi na kuniinua kisha akanikumbatia, nami nikamkumbatia vilevile.

    Muda huo huo yani kitendo cha kufumba na kufumbua, tulijikuta tupo katikati ya umati wa watu tena tukiwa kama tulivyozaliwa huku tumekumbatiana vilevile.





    Muda huo huo yani kitendo cha kufumba na kufumbua, tulijikuta tupo katikati ya umati wa watu tena tukiwa kama tulivyozaliwa huku tumekumbatiana vilevile.

    Nikaogopa sana na kuzidi kumkumbatia Sam, gafla Sam akatoweka nikajikuta nimekumbatia mti.

    Kwakweli kilikuwa ni kilikuwa ni kitendo cha ajabu sana kwangu kutukia, kilinishangaza sana ukizingatia sikukitarajia kabisa.

    Wale watu walionekana kunishangaa sana, machozi yakanitoka huku nikizidi kuukumbatia ule mti.

    Kelele za wale watu zilisikika zikisema,

    "Mchawi huyu, amekutana na manguli hapa mtaani ameshindwa kuruka"

    Wengine wakasema,

    "Mchawi huyu amekosea njia, amepita njia za watu amenasa"

    Nilipata aibu na fedhea, wengine wakatamani wanipige mawe pale kwenye mti, wengine wakatamani hata kunichoma moto yani kila mmoja alitamani anachotamani juu yangu najua yote sababu watu wengi wamechoka kurogwa ndiomana anapoonekana mchawi huwa wanataka kumuadhibu lakini mimi sio mchawi, yani kamavile watu walivyochoka kuibiwa kwahiyo mwizi akikamatwa mahali popote huwa wanataka kumuadhibu na kummaliza kabisa na wapo ambao hupigwa bila hatia kama mimi hapa ninavyotaka kupigwa na hakuna wa kusikiliza utetezi wangu wa aina yoyote ile.

    Kuna baadhi ya watu wakanitetea ili nisipigwe na wengine walikazana kuwa nipigwe, nililia sana. Mmama mmoja alikuja na kipande cha khanga kisha akanifunga, alionekana kunionea huruma sana.

    Akainama na kuninong'oneza,

    "Mwenyezi Mungu anakupenda binti, unatakiwa kumtumikia yeye. Achana na haya mambo binti yangu"

    Uwepo wa yule mama karibu yangu ukasaidia kutokupigwa na wale wananchi wenye hasira kali, muda kidogo maaskari nao wakafika na kunichukua eneo lile kisha nikapelekwa polisi.



    Nikiwa pale polisi nikaanza kuhojiwa maswali na baadhi ya maaskari ambapo wananchi wengi walikuwa nje kusikiliza kuwa mimi ni mtu wa aina gani, polisi akaniuliza maswali ambayo baadhi yake sikuwa na majibu kwa muda huo.

    "Unaitwa nani?"

    Gafla tu jina langu nikalisahau tena nikalisahau kabisa, nikamjibu askari kuwa nimesahau.

    Yule askari akajua namfanyia masikhara, akanizaba kibao.

    Nikahisi kama mishipa ya damu inacheza cheza hivi, akaniuliza tena nami nikaanza kulia tu. Akanibadilishia swali,

    "Umetokea wapi?"

    "Sijui"

    Yule askari akazidi kuchukia, akaja askari mwingine na kunihoja maswali mengine

    "Kwenu ni mkoa gani?"

    "Dar"

    Yule askari akashtuka sana huku akiguna,

    "Mmh kweli wachawi ni kiboko, yani kutoka Dar hadi kigoma kwa ungo!!"

    Nami nikashtuka na kuuliza,

    "Yani hapa ni Kigoma?"

    "Kwa mawazo yako ulifikiri ni wapi?"

    Nilikaa kimya nikitafakari kuwa kwanini Carlos amenifanyia haya yote, kwa kosa gani haswaa? Sikuelewa kwakw eli.

    Yule askari akanitazama na kuniuliza tena,

    "Umeanza lini uchawi?"

    "Mimi sio mchawi"

    "Wewe ni mchawi, unaogopa nini kusema wakati umeshafumwa ukiwanga? Jiseme tu upate msaada. Na utushukuru askari tupo maana hawa raia wangekumaliza leo wewe"

    Nikajaribu kujitetea lakini hakunielewa wala kukubali utetezi wangu nilioutoa kabisa.

    Wakaniweka mahali kwanza kwa usalama wangu maana raia wa pale nje walikuwa na hasira sana na mimi yani kama ningeachiwa basi ningekuwa ni marehemu kwasasa.

    Machozi yalikuwa yakinitiririka tu huku nikiwaza kuwa nitarudi vipi Dar kutoka huko Kigoma.



    Wakati nawaza hayo, alikuja yule mama aliyenifunika khanga wakati nipo mtupu kabisa.

    Aliwaomba maaskari kuondoka na mimi ambapo walimwambia angoje kwanza watu wapungue maana ingekuwa tatizo.

    Baada ya muda wale maaskari wakamruhusu yule mama kuondoka na mimi amakweli kesi za ushirikina hazina mashiko kabisa maana serikali haiamini uchawi.

    Nikainuka na kuanza kuondoka na yule mmama ambaye alinipa khanga nyingine ya kujifunika huku akiniambia kuwa nisijari na atanisaidia kwa kila hali, kwahiyo nisiwe na mashaka wala wasiwasi wowote.

    "Kwanza niambie unaitwa nani binti?"

    Kwasasa nikakumbuka jina langu na kumtajia kuwa naitwa Sabrina, akafurahi naye akajitambulisha kwangu kuwa anaitwa mama Amina.

    Tuliongozana na yule mama huku akiniuliza maswali mbalimbali nami kumjibu kila alichoniuliza.

    Njiani tukakutana na mmama mwingine ambaye alimuhitaji mama Amina kwa pembeni ili azungumze nae.

    Nikasimama pembeni kuwasubiria, gafla nikajiona nainuka juu yani miguu yangu haifiki chini.

    Nikainuka juu zaidi na kuwa kamavile napaa, mama Amina na mwenzie waliponiangalia wakaanza kukimbia kwa uoga.

    Nikaogopa sana kuona kuwa nimeanza kupaa angani, ni kitendo cha ajabu katika maisha yangu ambacho hakijawahi kutokea wala sijawahi kumuona mtu yeyote akitenda.

    Nikapiga kelele za uoga lakini haikusaidia kitu, gafla nikatua mahali ambako sipafahamu ila palikuwa na nyumba mbele yangu.

    Nikawa nashangaa shangaa tu, muda huo huo mama Amina na mwenzie wakafika mahali pale huku wanakimbia sana.

    Waliponiona, wote wakashtuka na kuanguka chini walikuwa wamezimia na watu wakajaa kuwasaidia huku wakinishangaa mimi kuwa ni mtu wa aina gani.

    Nilisimama pale pale huku nikizidi kutetemeka kwa uoga, akanisogelea mdada mmoja na kuniuliza kuwa nina tatizo gani.

    Nilikuwa kimya tu, mara gafla nikaanza tena kupaa.

    Yule dada na wale watu wengine waliokuwa wakiwasaidia wakina mama Amina na mwenzie, wote wakaanza kukimbia hovyo hovyo kwa uoga.

    Kwakweli kila mtu akaamini kuwa mimi ni mchawi kwa yale yaliyokuwa yanatukia.

    Muda huu niliinuliwa juu zaidi kupita mara ya kwanza, gafla nikajikuta nipo tena ufukweni na mbele yangu alikuwepo yule jini huku akicheka sana tena sana yani kamavile mtu aliyefurahishwa na kitu.

    Akanisogelea na kuanza kuongea,

    "Ulidhani upo ndani na Sam? Uwe nae ndani ili iweje? Unadhani naweza kuruhusu jambo hilo kutendeka? Haitowezekana kwangu Sabrina, nilikuwa nakuonyesha tu uwezo niliokuwa nao. Naweza fanya chochote nitakacho na muda wowote nitakao. Nilikuweka kwenye nyumba nzuri ufurahie maisha, ila ukaona kamavile haikupendezi kuwepo ndani yake. Nikakupeleka kwenye umati wa watu ukiwa mtupu kabisa ili ujisikie fedheha, lakini sijakudhalilisha sababu nimekupeleka sehemu ya mbali kabisa na nyumbani kwenu"

    Akacheka sana na kuniuliza,

    "Unajionaje sasa Sabrina?"

    Nilijiangalia mwili mzima, bado nilikuwa na zile khanga nilizofungwa na yule mama Amina.

    Sikuwa na jibu la kumwambia, nilikuwa kimya tu lakini yeye aliendelea kucheka tu, akaniambia tena

    "Siku zako tatu zimeisha, chagua moja kwenda kuishi na mimi au kutafuta ukweli kuhusu Carlos"

    Nikafikiria sana, nikajua moja kwa moja kama nikikubali kuishi nae basi nami nitageuka jini.

    Nikaona ni bora niende kutafuta ukweli kuhusu Carlos ingawa sikujua pa kuanzia wala pa kuishia.



    Nilikaa kimya kwa muda mrefu kitendo kilichofanya yule jini aniulize tena kwa ukali, nami nikaamua kumjibu

    "Naomba nikatafute ukweli kuhusu Carlos"

    Akacheka tena na kusema,

    "Yani umeamua kuishi maisha ya shida na kuacha maisha ya raha! Kweli wewe Sabrina una matatizo"

    Nikamjibu kwa ujasiri sasa

    "Nahitaji kuwa huru"

    "Uhuru wako upo mikononi mwako Sabrina. Ngoja nikupe onyo kwa kitu ulichochagua"

    Nikatulia kimya kabisa kumsikiliza,

    "Hutakiwi kumwambia mtu yeyote kama unafatilia ukweli kuhusu Carlos, na laiti kama ukimwambia mtu basi mtu huyo hatokuwepo tena duniani. Usalama wako na familia yako ni baada ya wewe kutambua ukweli kuhusu Carlos"

    Kwa upande mwingine nilijiona kama najiongezea matatizo zaidi kwa kukubali kitu cha namna hii maana kwa vyovyote vile lazima kitu hiki kitanitesa mimi na maisha yangu yote hapa duniani na jinsi ya kukikwepa sikujua.

    Nikakubali masharti yote niliyopewa na huyu jini ili niweze kuwa huru maana utumwa huu uliniumiza sana na sikuwa na raha tena ya maisha.

    Yule kijana wa ajabu akaniambia kuwa nisimuogope tena maana atakuwa akinitembelea mara kwa mara ila mimi niliendelea kumuogopa maana hakuwa mtu wa kawaida.

    Akaniambia ndani ya wiki tatu niwe nimekamilisha nilichokisema kuwa nitakifanya.

    Akaniambia nitembee pembezoni mwa bahari nami nikafanya kama alivyosema huku nikiyajutia maisha yangu na yote yanayonitokea, nikatamani iwe ndoto ila haikuwa kwani ni kweli nimeolewa na jini na ndiye anayenitesa kiasi hiki.

    Akaniambia nifumbe macho, nami nikafumba. Kisha akasema kuwa nifanye kama nagonga mlango, nikaogopa sana huku nikihofia kuwa huenda nikagonga halafu ukafunguka mlango wa bahari kwahiyo nikasita kufanya hivyo.

    Nikamsikia yeye akicheka na kusema,

    "Kumbe hutaki kwenda kwenu? Haya rudi basi ubadili maamuzi tukae wote, na ukumbuke kwamba kuna mabinti wengi hapa duniani wanapenda kupata aina ya wanaume kama mimi na hao nitawafata baada ya kuvunja mkataba wa ndoa na wewe Sabrina. Haya gonga mlango, hapo ndio nyumbani kwenu"

    Nikaendelea kuogopa huku nikijaribu kufanya maombi hata yasiyofanyika.

    Nikagonga kwa uoga pale pale baharini huku nikiwa nimesimama kwahiyo nikagonga hewani,

    "Hodi"

    Nikasikia sauti ikinikaribisha,

    "Karibu"

    Nikaogopa sana na kutetemeka, kisha nikasema tena

    "Hodi"

    Ile sauti ikajibu kwa kufoka sasa

    "Karibu wewe, acha kutupigia kelele usiku usiku"

    Nikajua haya ni majanga tu, kisha nikasikia sauti kama ya Carlos ikicheka na kusema

    "Fumbua macho Sabrina"

    Kwa uoga kabisa nikajaribu kufumbua macho yangu.



    Ile kufumbua tu nikashangaa sana kujiona kuwa nipo nyumbani kwetu mlangoni, halafu dada Penina akiwa mbele yangu ila alishtuka sana nusu ya kuzimia nadhani hakuamini alichokiona mbele yake kwa wakati huo.



    Nikaingia ndani, nikiwa na zile zile pande mbili za khanga.

    Dada aliniangalia kwa uoga sana, na kuniuliza

    "Mbona umetokea kimaajabu? Yani ni wewe kweli uliyekuwa unagonga?"

    Kabla sijajibu, mama nae akaja, akashtuka sana kuniona na kuuliza

    "Ni wewe kweli Sabrina mwanangu? Amakweli Mungu ashukuriwe, siamini mwanangu kama umerudi"

    Sikujua ni mambo gani waliyokutana nayo wakati sipo, na hata wao hawajui yaliyonipata nilipokuwapo.

    Nikakaa kwenye kochi kama mtu ninayefikiria kitu kwani hata mimi sikuamini kama nimeweza kurudi nyumbani kwetu nikiwa salama kabisa.

    Mama na dada walikaa na mimi na kuniuliza nilipokuwa, mama alitaka nimueleze kila kitu ila sikuweza kwavile nilikuwa na kazi ya ziada ya kufanya Niliwaambia kuwa nitawaeleza kesho yake, kwasasa waniachie muda wa kupumzika.

    Nikainuka ili niende chumbani kwangu, ila mama akanishika mkono kama kunizuia na kuniuliza

    "Una funguo za chumba chako?"

    "Hapana kwani kumefungwa?"

    Dada Penina akajibu,

    "Ndio, tangu umeondoka hakuna mtu aliyeweza kuingia chumbani kwako"

    Bado kichwa changu kilikuwa na maswali bila ya majibu ya aina yoyote ile kuwa tangu nimetoweka na Carlos ilikuwaje? Na je familia yangu wao wanajuaje? Sikuwa na majibu ila nikajisemea kuwa muda upo nitawauliza tu.



    Kuhusu kufungwa kwa mlango wangu sikuwa na jibu ila nikaona ni vyema kwenda kujaribisha mwenyewe kama mlango utafunguka.

    Mama na dada walikaa pembeni wakiniangalia, nikanyonga kitasa cha mlango nao ukafunguka.

    Nikamuangalia mama na kumwambia,

    "Ona mama, mlango umefunguka bila hata ya funguo"

    Wakaishia kustaajabu, kisha nikaingia chumbani.

    Nikamuona kama mtu kalala kitandani kwangu ila kafunikwa shuka hadi usoni, kwa uoga nikasogea hadi pale na kufunua lile shuka.

    Nikamkuta Carlos akitoa funza yani kawa maiti kwenye kitanda changu, kisha mlango wa chumbani kwangu ukafungwa na mtu asiyeonekana.





    Nikamkuta Carlos akitoa funza yani kawa maiti kwenye kitanda changu, kisha mlango wa chumbani kwangu ukafungwa na mtu asiyeonekana.

    Kama siku zote huwa naogopa basi leo ilikuwa ni zaidi ya uoga, uoga niliokuwa nao ulipitiliza kabisa.

    Halufu mbaya ikaanza kutapakaa kwenye chumba changu, nilipiga kelele za uoga ila mama na dada walipojaribu kuja ndani kunipa msaada walishindwa kwakuwa mlango ulikuwa umefungwa, wakajaribu kuubamiza lakini haukufunguka.

    Niliweza kuzisikia jitihada zao zote nikiwa ndani.

    Nilitetemeka sana hadi kujikojolea, sikuweza kuangalia mara mbili mbili pale kitandani kwenye maiti ya Carlos, mara sauti ikasika

    "Unaogopa nini sasa wakati umekuwa nae karibu siku hizi zote"

    Nilikuwa nalia tu huku nikitafuta muujiza wowote pale kuwa labda nijikute sehemu nyingine.

    Wale funza waliokuwa wakimtoka Carlos wakaanza kutapakaa katika chumba changu na wengine kunifata mahali ambapo nilijibanza huku nikilia na kutetemeka kwa uoga.

    Mama na dada, wakafanya jitihada zao pale nje za kuweza kunisaidia lakini ilishindikana ukizingatia ni wanawake watupu wakaamua kuwapigia simu baadhi ya ndugu zetu.

    Yote hayo walikuwa wakinieleza ili nijue kwamba kuna jitihada zinafanyika kwaajili ya kuokoa maisha yangu ambayo yapo khatarini kwa sasa.

    Wale funza wakaenea sehemu niliyojibanza na kuanza kutembea mwilini mwangu.

    Nikawa naruka ruka kwa lengo la kuwatoa na kuwaua ila walikuwa ni wengi sana, waliponizidi uzalendo ulinishinda nilipiga kelele ambazo nahisi hata mtaa wa saba walisikia zile kelele na hapo hapo nikapoteza fahamu.



    Nikamuona mbaba mmoja aliyewahi kufika kwetu siku za nyuma zilizopita, nikakumbuka alizungumza na mimi ila akaondoka sababu ya ujio wa Carlos.

    Aliwahi kumpatia dada yangu chupa ya mafuta ambayo yaligeuka damu na kupotea baada ya kumwagika.

    Nikamkumbuka kwa uzuri kabisa, akanisogelea nikiwa nimelala pale chini, akainama na kunipaka mafuta kwenye pua zangu kisha akainuka na kwenda zake.

    Pale pale nikazinduka na kupiga chafya, nikajikuta nikiwa sebleni tena kukiwa kumekucha huku nimezungukwa na baadhi ya ndugu zangu.

    Nikainuka na kukaa ili kusikilizia yaliyojiri wakati nimezimia. Mama alikuja karibu yangu na kukaa huku amenishikilia. Nikamuuliza mama,

    "Niambie mama mliwezaje kuingia chumbani?"

    "Ilibidi tuvunje mlango mwanangu ila cha kushangaza chumba chako kina harufu mbaya kama ya kitu kilichooza, sijui ni kitu gani"

    "Kwani hamkukiona?"

    "Hatujaona chochote ila tumekuta kuna funza kiasi na hiyo harufu, kwani ni kitu gani mwanangu?"

    "Hata mi mwenyewe sijui chochote mama maana nilizimia"

    Dada aliyekuwa pembeni naye akadakia,

    "Itakuwa amezimia kutokana na harufu ya humo chumbani kwake, tena sijui alitoka kuoga na hizo khanga zake jamani"

    Nikajitazama mwilini, bado nilikuwa nimejifunga zile khanga za yule mama wa Kigoma, huyu dada aliyeshangaa alikuwa ni mtoto wa bamdogo kwahiyo hakuniona wakati naingia ndani na zile khanga.

    Moyoni nikajiuliza kuwa ni kwanini zile khanga haziwezi kunidondoka maana zilikuwa zimening'ang'ania mwilini kamavile zimeshonelezewa hapo hapo.

    Nikatakiwa kwenda kuoga ili tupate muda wa kuzungumza kama familia maana mjomba nae alikuwepo pale nyumbani.



    Dada Penina akaniletea khanga zingine ili niweze kuoga na kubadilisha.

    Nilipomaliza kuoga, nikavaa khanga zingine kisha nikaenda chumbani kwa dada kwaajili ya kuvaa nguo zingine maana chumbani kwangu nilipaogopa kabisa.

    Zile khanga zingine nilizokuja nazo, dada Penina alikuja na kuzichukua nadhani alitaka kwenda kuziloweka.

    Alipotoka nje, akatokea yule mkaka wa ndotoni mbele yangu, nikataka kupiga kelele ila akaniziba mdomo kwa mkono wake na kuniambia,

    "Nilikwambia Sabrina, unatakiwa kunizoea. Kwanini unapenda kuniogopa?"

    Nikawa kimya tu huku nimekodoa mimacho yangu.

    Akaendelea kuongea,

    "Zitunze sana zile khanga, siku moja utajua umuhimu wake kwako. Naendelea kukufatilia sababu nakupenda sana Sabrina na pia bado hujaniambia ni lini utaianza kazi yangu uliyoichagua"

    Nikaendelea kuwa kimya, akaniuliza sasa

    "Je, unataka ndugu zako waishuhudie ile maiti? Wataenda kuizikia wapi? Nenda ukawatafute ndugu wa Carlos kwanza"

    Nikashindwa kuelewa hapa, je inamaana Carlos ni mtu? Inamaana amemuua? Je amemuua kwasababu gani? Sikupata jibu. Naye alikuwa kimya kabisa akinisikiliza kuwa nitasema kitu gani, alipoona nipo kimya kabisa akataka kusema kitu ila muda huo huo dada Penina nae akarudi chumbani kwake na kunikuta nimekaa pale pale kitandani.

    Yule kijana wa ndotoni akaniachia na kusimama karibu yangu, kisha dada nae akanifata pale nilipokaa na kuwa kama mtu anayenishangaa

    "Yani hadi muda huu bado hujamaliza kuvaa Sabrina!"

    Nikanyoosha mkono mahali aliposimama yule mkaka wa ndotoni ili dada amuone, dada akageuka na kuangalia kisha akaniuliza

    "Kwani nini?"

    Nikamuangalia yule mkaka wa ndotoni ambapo aliweka kidole mdomoni kama ishara ya kuniambia kuwa nisiseme chochote.

    Nikabaki kimya nimeduwaa, dada akaniangalia tena na kuniambia

    "Vaa haraka haraka, twende kwenye kikao, wote wanakungojea wewe huko"

    Nikainuka na kuvaa haraka haraka ili niweze kutoka na dada.

    Wakati tunatoka, yule kijana wa ndotoni akanivuta na kuninong'oneza,

    "Usithubutu kusema chochote kuhusu mimi"

    Kisha akapotea na kufanya nishtuke, dada akageuka na kuniangalia kisha akasema

    "Bado una matatizo wewe sio bure"

    Tukatoka na kwenda hadi sebleni.



    Kikao kilifunguliwa na mjomba ambaye alieleza kustushwa sana na simu ya mama aliyopigiwa usiku,

    "Mnajua mmenishangaza sana, maana mara ya mwisho nakumbuka mlipiga simu na kusema kuwa Sabrina kapotea kwenye mazingira ya kutatanisha, halafu jana mkaniambia kuwa Sabrina yupo chumbani ila mlango wake umejilock hautaki kufunguka. Swali langu kwenu sasa, huyu Sabrina huyu si ndiye ambaye tulisherekea harusi yake wiki chache zilizopita? Naomba mniambie mumewe yuko wapi na haya mambo yanakuwaje maana kama ndugu tunashindwa kuwaelewa kabisa"

    Ikawa hakuna mwenye maelezo, na wote wakakubaliana kuwa kwavile mimi mwenyewe muhusika wa yote yale nipo basi natakiwa kujibu kuwa nilikuwa wapi na je huyo mume aliyenioa naye yuko wapi.

    Kwakweli sikuwa na majibu ya kuwapa maana sikujua nianzie wapi kuwaeleza kila kitu kilivyo, na je wataamini nitakayowaeleza?

    Najua hakuna atakayeamini maana watadhani kuwa ni simulizi tu kumbe ni kweli. Na kama wakiamini basi hawataamini vyote nitakavyowasimulia, wataamini vichache tu.

    Pia nikakumbuka kauli ya yule kijana wa ndotoni kuwa nisithubutu kusema, nikaogopa kujiweka kwenye matatizo zaidi na hivyo kujikuta nikiwa kimya tu bila ya kujibu kitu chochote.

    Mjomba alikazana kusema ili niseme ukweli,

    "Sasa bila ya kutuambia ukweli Sabrina unafikiri tutakusaidiaje? Unatakiwa kutuambia ukweli"

    Nikaamua kusema kuwa Carlos amepotea kwenye mazingira ya kutatanisha ili kama familia wafikirie namna ya kunisaidia kumtafuta Carlos.

    Mama akaniambia kuwa hilo halina tatizo,

    "Kwavile tunawafahamu vizuri wazazi wa Carlos basi hilo halina tatizo kwani inawezekana wao wakajua alipo mtoto wao"

    Mama akakubali kunisindikiza nyumbani kwa wakina Carlos ambapo tulipanga kwenda kesho yake.

    Ingawa ndugu zangu walichukizwa na mimi kwa kuificha siri hii ila ilinibidi nifanye hivyo tu.

    Kikao kikungwa na wote wakatawanyika na kutuacha wanafamilia tu pale nyumbani.



    Ilikuwa ni jioni ambapo mama aliniita na kunitaka nimwambie ukweli wa nilipokuwa,

    "Niambie ukweli mwanangu kwanini unanificha hata mimi? Kumbuka mimi ndiye mama yako"

    "Naelewa mama ila ipo siku nitawaeleza kila kitu nanyi mtaelewa"

    Nikajaribu kumuuliza mama kuwa anakumbuka chochote kabla ya kutoweka kwangu, akanipa maelezo mengine kabisa yani tofauti na jinsi ilivyokuwa na hapo nikaamini kweli yule jini aliweza kucheza na akili za ndugu zangu kiasi hiki.

    "Kwanza tulishangaa sana siku ile maana tulikaa wote hapa tukiongea vizuri tu, mara akaja Carlos na baada ya muda kidogo akatuaga kuwa anaondoka na kuomba umsindikize. Baada ya hapo hatukuwapata tena ila ilikuwa tukimpigia simu Carlos anasema mtarudi tu ndiomana tukawaamaia ndugu kuwa umetoweka ili watusaidie kutafuta maana hukupatikana hata kwenye simu yako. Ulitupa mashaka sana, halafu leo unasema Carlos kapotea ndio hapo tunazidi kukushangaa wakati mliondoka wote. Ni bora ungesema ukweli tu mwanangu"

    "Nadhani ukweli tutaupata tukienda nyumbani kwa wakina Carlos kesho"

    Mama hakuweza kunilazimisha zaidi, ikabidi akubaliane na kile nilichosema tu.



    Muda wa kulala ulipofika, wote watatu yani mimi, mama na dada tulilala pamoja chumbani kwa mama sijui dada nae aliogopa kitu gani chumbani kwake ila hakuweza kulala chumbani kwake.

    Wakati tumelala, alikuja mtu ndani.

    Niliweza kugundua kutokana na kivuli chake, tena alikuja moja kwa moja nilipo lala mimi ingawa nililala katikati ya mama na dada.

    Yule mtu alikuwa amebeba bakuli ya maji na kunimwagia mwagia, kisha nikainuka toka kitandani na kuanza kumfata.

    Alikuwa kama ananiita na kunipa ishara ya kumfata, wakati nakaribia kutoka mlango wa nje, mama nae alikuwa ameshashtuka na kuja karibu nadhani akaniita ila sikumsikia, nikaja kumsikia neno moja tu alilosema nalo ni

    "Shetani ushindwe"

    Nikashtuka kama mtu aliyeshtuliwa. Mama akanishika, na kuniuliza

    "Upo sawa Sabrina"

    "Ndio nipo sawa mama"

    Akamuita dada ambaye alikurupuka pia na kuja sebleni, mama akasema leo tufanye ibada.

    Tukakaa na kufanya ibada kwa ufupi ila wote hawakwenda tena kulala nadhani kila mmoja ndani ya nyumba yetu alishapatwa na tatizo la uoga tayari.

    Tulikaa pale sebleni hadi panakucha kabisa, ndio kila mmoja akainuka kwa kazi mbali mbali.

    Chumba changu ndio kiliogopwa na wote utadhani nao waliiona maiti ya Carlos kama ambavyo mimi niliiona.

    Wote watatu tukajiandaa na kwenda kwa ndugu wa Carlos.



    Tulipofika wakatupokea vizuri tu, tukasalimiana nao na kuanza kuzungumza nao kuhusu kilichotupeleka kwao ila wao hawakutaka kutuambia ukweli lakini baada ya kuwabana kwa maswali mengi wakaamua kusema ukweli kuhusu Carlos

    "Carlos ni mtu ambaye tunamfahamu tangia utoto wake, yani tangu anazaliwa tunamuona na alicheza hata na baadhi ya watoto zetu kipindi hicho tuliishi nao karibu kwenye kijiji kimoja huko Kigoma ila badae tulihama na kuja kuanzisha maisha mapya huku Dar es salaam. Kwa kifupi tu wazazi wa Carlos walikuwa jirani zetu huko Kigoma"

    Mama akadakia hapo hapo na kuwauliza,

    "Mbona mkatuambia kuwa nyie ndio wazazi wake?"

    "Bado sijamaliza kuwaeleza jamani"

    "Haya tueleze basi tujue"

    "Kwa miaka mingi sana hatukuonana na Carlos ila alikuja na kujitambulisha kwetu hadi tukamkumbuka mama yake aliyeitwa Dorothea na kumkaribisha vizuri hapa nyumbani. Baada ya siku chache akatueleza kuwa amepata mchumba na anahitaji kumuoa ila wazazi wa mchumba huyo wamesema hadi wawafahamu wazazi wake. Sasa Carlos akatueleza kuwa kwavile wazazi wake wako mbali na yeye anaona gharama kuwasafirisha toka Kigoma hadi hapa, akatuomba sisi tujifanye wazazi wake kwa muda. Kwavile ni mtoto tunayemfahamu, hatukuweza kumkatalia hadi tukafanya vile. Tafadhali mtusamehe bure tu kama kuna baya kawafanyia"

    Tukatulia kwanza na kutafakari maneno ya hawa watu jamani, na hii inaonyesha kuwa kuna wazazi wengi tu wanaokubali kuwa wazazi bandia. Ndani ya moyo wangu nikahisi kuwa ni lazima hawa wazazi walipewa pesa na ndiomana wakafanya yote yale.

    Wakatuambia kuwa kuna namba za simu ambazo Carlos aliwapatia na walikuwa wakizungumza na wazazi wa Carlos, lakini zile namba tulipozitafuta hazikupatikana.

    Nikawauliza kijiji chao na majina ya wazazi wa Carlos, wakatupa maelekezo ya kufika nyumbani kabisa kwa wakina Carlos.

    Kiukweli nilijikuta nikiwachukia hawa wazazi kuwa kwanini wajifanyishe? Ama kwa wakati huo ningekuwa na uwezo ningewafungulia mashtaka hawa watu.

    Tukawaaga na kuondoka.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Tukiwa njiani, akatokea Carlos mbele yatu. Mama alikuwa wa kwanza kumuona na kusema

    "Si Carlos yule?"

    Wote tukamuangalia kwa makini.

    Naye akageuka nyuma kutuangalia, ni kweli alikuwa Carlos.



    Kumbuka kushare rafiki yangu utakuwa umenisadia sana



    Tukiwa njiani, akatokea Carlos mbele yatu. Mama

    alikuwa wa kwanza kumuona na kusema

    "Si Carlos yule?"

    Wote tukamuangalia kwa makini.

    Naye akageuka nyuma kutuangalia, ni kweli alikuwa

    Carlos.

    Kila mmoja wetu alishtuka na kumuangalia vizuri,

    naye akatuangalia na kutabasamu kisha akaendelea

    na safari yake. Mama akanitazama na kuniambia

    "Nenda ukamkimbilie mwenzio Sabrina"

    Nikamtazama mama na kujua kuwa bado utambuzi

    kwake si mzuri.

    Mama akajaribu kumuita Carlos ila hakutuitikia wala nini. Kuona vile nikawaomba tuendelee na safari yetu

    bila kujali kama tumemuona Carlos. Mama na Dada

    wakaafikiana na mimi na kuendelea na safari.



    Tuliendelea na safari kurudi nyumbani, huku tukisemeshana haya na yale.

    Kufika nyumbani tukamkuta Carlos amekaa kwenye mlango wetu tena akiwa hana hata wasiwasi. Safari hii dada Penina ndiye aliyeanza kumuona na kutushtua sisi,

    "Jamani mwangalieni Carlos pale mlangoni"

    Wote tukatazama vizuri, Carlos nae alitutazama bila ya kusema kitu chochote.

    Kila mmoja akaogopa, ni mama pekee aliyekuwa na ujasiri wa kusema kitu chochote kile.

    "Anataka nini huyu kijana? Mbona anatuletea makubwa jamani?"

    Mama akaongoza mbele yetu na sisi tulimfata nyuma kwani wote tuliogopa kuwa mbele.

    Tukafika palepale ila Carlos hakuwa na shaka yoyote ile.

    Mama akamuuliza,

    "Unafanya nini hapa? Na mbona njiani hukuitika wakati tunakuita?"

    Carlos akainuka pale mlangoni na kufungua mlango kisha akaingia ndani.

    Wote tukaangaliana kwa mshangao, mama akatuuliza

    "Anamaana gani huyu?"

    Dada nae akauliza,

    "Amepata wapi funguo?"

    Hakuna mwenye jibu zaidi ya kutazamana tu huku tukiwaza kuingia ndani ya nyumba yetu wenyewe.

    Kila mmoja aliogopa kuingia ndani, ingawa tulikuwa tumechoka ila tutaingiaje ndani wakati kuna mtu anayetupa mashaka ndani yake?

    Tukasimama pale nje kama milingoti bila ya kujua cha kufanya.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya muda kidogo, tukamuona Carlos akitoka tena kwenye mlango wa nyumba yetu kisha akaondoka zake.

    Tukaangaliana kama watu tusiojielewa kabisa na kuambizana kuingia ndani huku tunasita. Mama akauliza,

    "Kwamaana hiyo leo tutalala hapa hapa nje?"

    Dada akadakia,

    "Na kama humo ndani ameweka vitu vyake je?"

    Mama akasema tena,

    "Sidhani maana hajakawia sana kutoka"

    "Mmh mama, kumbuka tumemkuta hapa mlangoni mtu huyu!"

    Mama akanitazama mimi sasa na kuniuliza,

    "Tufanyeje Sabrina?"

    "Sijui mama"

    "Hujui vipi wakati huyo Carlos ni mumeo halafu ni wewe uliyetuletea hapa nyumbani maana bila ya wewe sidhani kama Carlos angepajua hapa"

    Nikaona napewa lawama za bure tu, ila kwavile nimeshakutana na mambo mengi makubwa kwa madogo nikaona ni vyema nijitoe muhanga mimi mwenyewe kuingia ndani huku nikijisemea liwalo na liwe.

    Nikaingia ndani huku moyo unanidunda dunda kupita maelezo ila kwa nje najifanya jasiri, ikabidi mama na dada wanifate kwa nyuma kwani isingekuwa vyema kama wao wangeniacha mimi nidhurike mwenyewe.

    Hapakuwa na chochote cha kutisha wala kushtusha ndani kwetu, tulikagua vyumba vyote kwa pamoja kisha tukarudi kufunga mlango na kukaa sebleni kwa pamoja.

    Mama alianza kuzungumza na mimi,

    "Hebu niambie mwanangu, hivi kile chumba chako kina nini? Mbona kina harufu mbaya sana siku hizi?"

    Moja kwa moja nikakumbuka ile taswira ya Carlos aliyeoza chumbani kwangu, nikajihisi kusisimka mwili mzima na wala sikuwa na jibu la kumpa mama.

    Mama akaniuliza tena,

    "Niambie Sabrina, kuna nini chumbani kwako ambacho sisi wengine hatukijui?"

    "Sijui mama, kwanza mimi sikuwepo nyumbani siku zote hizo"

    "Hata kama, kumbuka mlango wako ulijilock hadi siku uliyorudi. Niambie ukweli Sabrina"

    Sikuwa na ukweli wowote wa kumwambia mama, badala yake ikabidi tukae na kufikiria kuwa tutakula chakula gani kwa usiku ule.

    Mama akasema kuwa kwavile mimi sijapika muda mrefu kwahiyo natakiwa mimi nikapike chakula cha leo, nami sikuona tatizo kwenda kupika.

    Nikainuka na kwenda jikoni, nikapika kila kitu kama kawaida.

    Nilipomaliza nikaend kuandaa mezani.

    Niliporudi jikoni nikakuta, simu yangu ikiwa pembeni ya jiko. Nikashtuka na kushangaa sana kwani tangu nimeondoka na kurudi sikuiona hii simu ndiomana ikanishtua sana.

    Nikaogopa kuichukua ile simu kwani ilikuwa na majanga sana, moja kwa moja likanijia wazo la Sam na kujiuliza yuko wapi na anaendeleaje maana sikujua habari yoyote kuhusu Sam.

    Nikarudi sebleni nikiwa nimenyong'onyea sana, mama akaniuliza

    "Vipi tena Sabrina, umeandaa vizuri chakula ila umerudi ukiwa umenyong'onyea sana?"

    "Nimemkumbuka Sam mama"

    Dada akadakia,

    "Mmh Sabrina una mambo mdogo wangu, yani janga la Carlos halijaisha unataka kulileta la Sam. Hebu tulia mdogo wangu na uangalie ni wapi ulipoteleza, usipende kuongeza tatizo juu ya tatizo"

    "Katika siku zote leo Penina umeongea maneno ya maana, huyu Sabrina hajielewi kabisa. Maswahibu aliyotuletea hapa ya mume asiyeeleweka anaona hayatoshi tena anataka kutuletea majanga kabisa yani. Sasa huyo Sam wa nini? Usitake kutuletea mabalaa na waume zako wa ajabu"

    "Lakini mama, Sam ana wazazi wake kamili na wanaoju likana, tofauti na Carlos mwenye ndugu bandia mama"

    Dada Penina naye akasema ya kwake aliyonayo moyoni kwasasa,

    "Yani huyo Carlos kanichefua jamani, kutudanganya wazazi wake! Halafu anaingia hapa kwetu kamavile kwake na wala hatuongeleshi na kutujibu, kwakweli simpendi kabisa maana kanikera sana"

    Mama akamkumbusha kitu,

    "Kumbuka amekutafutia kazi, unayojidai nayo kwasasa!"

    "Hata kama kanitafutia kazi, amenikera sana kwa uongo wake. Huwa sipendi watu waongo kabisa, ni bora angetuambia mapema kama wazazi wake wapo Kigoma. Ila mama hili ni fundisho kwetu, hata kama mtu amekutambulisha familia yake inatakiwa kuwa makini sana maana matapeli ni wengi sana siku hizi, watu wanadiliki kudanganya hata ubini wao kwa utapeli wa mapenzi. Sijampenda Carlos kabisa ila kupitia yeye nimejifunza mengi"

    Dada aliongea kwa jazba sana kuonyesha ni jinsi gani alikerwa na swala zima la kumfahamu Carlos.

    Tukainuka na kwena kula, kisha tukajiandaa kwenda kulala.

    Ile simu yangu niliiacha jikoni kulekule kwani niliogopa hata kuishika kwa kuhofia majanga mapya.

    Wote tulienda kulala kwa pamoja chumbani kwa mama.



    Usiku wa leo tulilala vizuri sana hadi panakucha, hatukupatwa na tukio lolote la ajabu.

    Dada alijiandaa kwenye mida ya saa mbili asubuhi na kuelekea katika kazi zake za kila siku.

    Mimi na mama tulibaki nyumbani kama kawaida huku nikiwaza safari ya kwenda Kigoma kuwaona hao wazazi wa Carlos, niliwaza sana bila ya kupata jibu.

    Kwanza kabisa nitapata wapi pesa ya kuniwezesha kwenda sehemu ya mbali kama hiyo? Sikupata jibu kabisa.

    Nikainuka na kwenda jikoni kufanya usafi, pale pembeni ya jiko ambapo kulikuwa na simu yangu jana yake nikaona kuna bahasha na ile simu ikiwa juu yake. Nikatamani kujua kuna kitu gani kwenye ile bahasha, nikataka kuichukua ila moyo ukasita nikaacha na kuendelea na shughuli zingine.

    Nilipomaliza bado nilitamani kujua kuna nini kwenye ile bahasha kwahiyo nikaichukua ile bahasha ambayo ilikuwa ni nzito nzito kidogo, nikaifungua.

    Nikashangaa kuona kuna hela, nikashtuka sana na kujiuliza kuwa ni nani ameweka pesa nyingi kiasi kile pale jikoni? Nikawaza kuwa labda ni dada ameweka ile pesa.

    Nikaenda na ile bahasha chumbani kisha nikazimwaga zile pesa kwenye kiti na kuanza kuzihesabu, zilikuwa milioni tatu kamili, halafu kulikuwa na karatasi ndani yake nikalitoa na kulisoma

    "Pesa hiyo ikusaidie kwa safari yako ya kwenda Kigoma"

    Nikashtuka na kujua kuwa ile pesa imewekwa na yule jini tu na kufanya mimi niogope zaidi kwani sikutegemea wala kutarajia.

    Mama akanikuta nikihesabu zile pesa, naye akashtuka sana na kuniuliza

    "Umetoa wapi pesa nyingi kiasi hicho Sabrina?"

    Nikamwambia mama kuwa natakiwa kwenda Kigoma kuwasalimia wazazi wa Carlos, na yeye ndiye aliyenitumia hizo pesa

    "Yani ndio uende peke yako mwanangu? Kwakweli siwezi kukuruhusu wala kukubali, na huyo Carlos amefika hapa muda gani? Mbona unapenda kunichanganya Sabrina? Nahisi kuwa sielewi kitu yani sielewi chochote. Kwanini huyo Carlos yupo hivi jamani?"

    Mama aliongea sana ila hakupata jibu lolote la maana kama ambavyo mimi mwenyewe sina jibu la maana kabisa.

    Nikafikiria pia maneno ya mama kuwa nitaondoka na nani kwenda huko Kigoma? Sikupata wa kumfikiria zaidi kwani nilihofia maisha ya kila mtu kuwa yatakuwa khatarini zaidi, natakiwa safari hii niende mimi mwenyewe ili kuyanusuru maisha ya watu wengine. Mama akakataa kabisa kuhusu mimi kusafiri, nikachukua zile pesa na kuzipeleka chumbani kwa mama kisha nikaweka kwenye kabati ambalo halikuwa na kitu chochote kile.

    Nikarudi sebleni na kuendelea na maongezi na mama ambapo aliendelea kunisisitiza kuhusu kutokwenda Kigoma.

    "Tafadhari sana Sabrina usiende huko, sitapenda tuongeze tatizo juu ya tatizo. Tulia hapa hapa nyumbani ili tuangalie ni jinsi gani tutaweza kukabiliana na hii hali iliyopo kwasasa"

    Nikamuitikia mama kuwa nitafanya atakavyo ila moyo wangu ulipanga kitu kimoja tu nacho ni kutoroka pale nyumbani kwani nilishamuahidi yule jini kuwa nitalifanyia kazi swala hili na kama nikigeuka basi lazima atanifanyia mambo mabaya zaidi kupita na yanayonitokea na kunipata kwasasa.



    Tukiwa pale sebleni mimi na mama tukizungumza, mara tukamuona dada Penina akiwa amerudi nyumbani huku amechoka sana.

    Hatukushangazwa sana na kuwahi kwake kurudi kwani imekuwa kawaida yake tangia amepata hii kazi aliyotafutiwa na Carlos. Ila aina aliyorudi nayo ilikuwa ni tofauti sana na siku za nyuma.

    Moja kwa moja alikuja na kukaa kama mtu aliyechoka sana, mama akamuuliza

    "Vipi na wewe? Umepatwa na maswahibu gani?"

    "Nimepatwa na maswahibu makubwa mama yani huwezi amini"

    "Tuambie tu Penina"

    Tulitulia na kumsikiliza dada kuwa amekumbwa na vitu gani,

    "Yani ninavyowaeleza sasa sina kazi tena"

    Wote tukashangaa,

    "Kivipi na kwanini?"

    "Hata mimi mwenyewe nashangaa, nimefika ofisini nikapata barua kuwa nimefukuzwa kazi tena hakuna sababu wala nini kwakweli nimeshangaa sana"

    Mama akacheka kiasi na kusema,

    "Ila umeyataka mwenyewe, kilichokufanya jana umseme aliyekutafutia kazi ni kitu gani? Labda amekusikia ndiomana umefukuzwa kazi mwanangu, pole sana"

    Nikatambua moja kwa moja kuwa ni yule jini tu ndiye aliyeyafanya yote yale na amefanya vile sababu hakutaka Carlos asemwe kwahiyo dada amepata fundisho sasa.

    Alikuwa akiongea kwa huruma sana,

    "Ila nimejifunza kitu mama, kazi za mdebwedo hizi hazifai kabisa. Ona kama hivi nilivyofukuzwa kazi bila hata sababu za msingi"

    "Pole mwanangu, haikuwa riziki yako. Mungu atakusaidia na utapata kazi nyingine Penina"

    Mazungumzo ya leo yalitawala vile ambavyo dada kafukuzwa kazi bila sababu na vile tulivyokuwa tukimzungumzia Carlos.



    Mchana wa leo tulipika chakula kama kawaida, ila wakati wa kula nikaona maandishi ya ajabu kwenye sahani yangu.

    "Utatekeleza muda gani tulichokubaliana?"

    Nikamuonyesha mama na dada lakini hawakuyaona yale maandishi na wala hawakuelewa. Nikatakiwa kufanya maamuzi magumu, natakiwa kutoroka na kuiacha familia yangu kabla mambo hayajawa magumu zaidi.



    Usiku ulipofika nikajipanga kwaajili ya kutoroka, nikaona muda mzuri wa kuondoka ni alfajiri kabla ya mama wala dada kuamka.

    Tukala wote na kujiandaa kwaajili ya kwenda kulala.

    Muda ulipofika wote tulienda kulala ila usingizi haukunipa kabisa, nilikuwa nawaza hiyo safari ambayo nimejipangia kwenda.

    Wakati wote wamelala hoi na usingizi kuwachukua, nikainuka na kutoa mkoba mdogo sebleni kisha nikatoa lile droo lenye pesa kwenye kabati ambapo niliziona kuwa kama zimezidi yani ni tofauti na nilivyoziweka.

    Nikaandika ujumbe kwanza na kuuacha mezani, nikiwataarifu kuwa naondoka naenda Kigoma ili wasiwe na wasiwasi tena na mimi.

    Nikaanza kuzihesabu tena zile pesa, nikatumia muda mrefu sana kuzihesabu. Nikashtuka sana kukuta ni shilingi milioni tano. Nikaogopa na kutetemeka kwani zilinitishia amani, nikahesabu tena na kuchukua milioni tatu za mwanzo kisha milioni mbili nikaziacha na kurudisha ile droo ndani.

    Muda ulikuwa umeshaenda tayari, nikachukua simu ya mama na kumpigia dereva wa magari ya kukodisha (Tax) ili aje anifate na kunipeleka kituoni.

    Nikatoka nje kumngoja kabla ndani hawajashtuka ndani.



    Ile gari ikaja nami nikapanda na kuondoka, moja kwa moja hadi kituo cha mabasi ya mikoani.

    Nikashuka, wakati namlipa yule dereva nikashangaa kumuona Sam nae akishuka kutoka kwenye lile lile gari.





    Ile gari ikaja nami nikapanda na kuondoka, moja kwa

    moja hadi kituo cha mabasi ya mikoani.

    Nikashuka, wakati namlipa yule dereva nikashangaa

    kumuona Sam nae akishuka kutoka kwenye lile lile

    gari.

    Nikamuangalia Sam kwa makini na kumshangaa ila yeye alitabasamu tu na kunisogelea.

    Nikashindwa hata kuhoji maswali kwa yule dereva kuwa Sam amepanda vipi.

    Yule dereva akapanda gari yake na kuondoka, nikamuangalia Sam mara mbili mbili bila ya kumuuliza chochote kisha nikaendelea na safari yangu ambapo Sam akaja kwa mbele.

    Niliogopa kuongea nae kwani sikuwa na uhakika kama kweli ni Sam ninayemjua mimi, na hata kama ndio yeye kweli amepanda vipi kwenye ile tax? Na mbona sikumuona muda wote hadi nashuka ndio nae anatokea?

    Nikakaa kimya nikimtazama mbele yangu huku nikihofia kuwa huenda mauzauza yanaendelea.

    Akanisogelea na kuanza kuniongelesha.

    "Mbona hutaki hata kuniuliza chochote Sabrina?"

    Nikawaza moyoni kuwa huenda akawa ni Sam kweli halafu mie nimemchunia, ikabidi nimuulize.

    "Kwani umepanda vipi kwenye ile tax maana unanitisha hadi naogopa kuwa wewe si Sam ninayemjua mimi"

    "Mimi ni Sam wa ukweli kabisa Sabrina, najua unapoelekea ndiomana nimekuja kukupa kampani"

    "Umejuaje ninapoelekea kama kweli wewe ni Sam wa kawaida?"

    "Nimeoteshwa Sabrina, huwezi amini. Afya yangu si njema kwasasa ila baada ya ile ndoto moyo wangu haukukubali kabisa kuona uende peke yako ndiomana niko hapa"

    "Hapana Sam haiwezekani kwenda pamoja na wewe, tafadhali rudi"

    "Siwezi kurudi Sabrina, nitaenda popote uendapo ilimradi nifanye kitu kukulinda."

    Nikajaribu kumshawishi arudi lakini akagoma, nikaona mlolongo utakuwa ni mrefu sana, inaweza kusababisha tukakosa usafiri kabisa. Nikaona ni vyema kama tukienda kukata tiketi kabisa, nikaongozana na Sam hadi kwenye mabasi na hatukuweza kupata basi la moja kwa moja hadi Kigoma kwa siku hiyo ikabidi tupande mabasi ya Mwanza kisha tuunganishe tukifika Mwanza.

    Tukapata siti za pamoja na kukaa kungoja safari.



    Safari ilipoanza, nikatumia muda huo kumuhoji Sam maswali yangu ambayo yananipa mawazo sana kwa muda huo.

    "Eeh niambie uliingiaje kwenye ile tax?"

    "Nimeondoka kwetu mapema sana, leo nililala pale stendi kwenu. Dereva wa tax uliyempigia simu nilikuwa nae pale, aliponieleza kuwa anaenda kumchukua mteja na aliponitajia mteja mwenyewe moja kwa moja nikajua ni wewe na kumuomba kupanda. Wewe ulipopanda hukuangalia siti ya nyuma ndio niliyokuwepo Sabrina"

    "Ila hii safari ni ya khatari sana Sam"

    "Naelewa Sabrina ndiomana nimekuja kukupa kampani, tafadhari usiniondoe Sabrina. Mimi nakujali ndiomana nafanya yote haya"

    "Ila unakumbuka mara ya mwisho mimi na wewe kuonana ilikuwa wapi?"

    "Nakumbuka, ilikuwa ni guest tukipanga kutoroka"

    Hapa ndio nilipokuwa napataka, nikamuuliza kwa makini sasa kuwa ni kitu gani kilitokea mpaka leo ambapo namuona kiukweli,

    "Kwakweli hakuna siku ya maajabu kama ile katika maisha yangu yote. Nilishtuka toka usingizini huku nikiona kama mawingu mawingu hivi, wewe ukatoka na kuondoka. Alikuja jamaa mwenye misuli mingi na kunikaba, baada ya muda kidogo nikasingiziwa eti nimekaa pale guest siku tatu bila ya malipo. Nikapelekwa polisi, nikakaa huko kama siku mbili nikatoka. Nikajipanga kuja kwenu ila njiani nikapata ajali, niligongwa na pikipiki"

    Akaanza kunionyesha makovu yake inaonyesha aliumia sana, nikasikitika na kukumbuka ile ajali ya Sam wa uongo kumbe ilikuwa ni kweli kwa Sam wangu wa ukweli.

    Akaendelea kunieleza ilivyokuwa,

    "Niliumia sana, na kulazwa kwenye hospitali ya ajabu hata ndugu zangu hawakuweza kufika kwenye hospitali ile.

    Nilikaa pale hospitali sijui kwa siku ngapi. Siku hiyo bila ya kuelewa wala kutambua, nikarudishwa nyumbani na mtu wa ajabu kisha akaondoka. Mtu yule simjui kabisa, ndugu zangu walinihurumia sana nakumbuka hata Suzy alikuja kuniona ila wewe hukufika. Sikujua sababu ila niliumia sana moyoni, nikiwa pale kitandani na maumivu yangu nikaletewa taarifa kuwa umeolewa na Carlos. Nimejiuliza maswali mengi sana bila majibu ila natumaini leo utanijibu. Tatizo ni nini Sabrina? Je kwavile mimi sina gari na nyumba? Kwavile sina pesa kama wengine? Ila kumbuka nina mapenzi ya dhati na wewe, nakupenda kupita ninavyojipenda mwenyewe"

    Sam akainama, kwajinsi nimjuavyo nikatambua moja kwa moja kuwa Sam analia tu. Nikamuangalia Sam wangu kwa maumivu aliyonayo juu yangu, nikajiweka kwenye kundi la watu wabaya duniani yani watu wanaosababisha maumivu kwa wengine ila kiukweli mimi sikutarajia kumsababishia Sam maumivu kiasi hiki, sikutarajia kuolewa na Carlos ila imetokea kwa bahati mbaya tu kwakweli.

    Nikamsihi Sam anisamehe kwanza maana hata kumueleza sikujua nianzie wapi na kuishia wapi, pia mlolongo wake ni mrefu inatakiwa nimueleze wakati ambao mambo yote yametulia. Nikamtazama kwa ukaribu Sam na kumuegamia kwenye mabega yake ambapo akaendelea kunieleza yaliyomsibu kwa siku hizo

    "Nimekuwa kitandani kwa muda mrefu sana huku nikitamani nipone ili niweze kuja kukuona Sabrina. Nilipopata unafuu, nilikuja kwenu majuzi nikamkuta Carlos akiwa nje ya nyumba yenu. Nikamshangaa, kisha akaniambia kuwa kama nayapenda maisha yangu basi niache kukufatilia. Akanitishia vingi sana, nikapata uoga na kuondoka ila bado nikasema kuwa nitaendelea kufatilia tu hadi nipate jibu la kuuridhisha moyo wangu"

    Siku ambayo Sam alikuja nyumbani ni ile siku tuliyoamua kwenda kwa ndugu wa Carlos ili kupata ukweli. Na ndiyo siku ambayo tulimkuta Carlos njiani na pia tukamkuta nyumbani, nikaanza kuoanisha matukio kwenye akili yangu na moja kwa moja ikanijibu kuwa Carlos sio binadamu wa kawaida.

    Nikampooza Sam kuwa asiwe na wasiwasi tena, naye akanieleza alichoota

    "Usiku wa jana nililetewa ndoto kuwa wewe unataka kusafiri leo ila katika kusafiri kwako huna nia ya kuaga, nia yako ni kutoroka. Nikaumizwa sana na ile ndoto kwani najua unaweza pata matatizo ukiwa mwenyewe ndiomana nikaamua kuja usiku kwa usiku, nimejitolea kwakweli yani liwalo na liwe ila nahitaji kuwa pamoja na wewe katika mapito haya"

    Maneno ya Sam yalinipa faraja kubwa moyoni hata moyo wangu ulijipongeza kwa kumpenda Sam, mwanaume anayejua thamani ya mapenzi, mwanaume anayejua raha, furaha na maumizi ya penzi kwakweli nampenda sana Sam mpenzi wangu haya mengine yamenipata tu wala sikutarajia kupata misukosuko ya kimapenzi kama ambayo nimeipata. Kila muda nitalalamika na kusema sikutarajia ila natakiwa kufanya kitu kwaajili ya kuokoa maisha yangu na familia yangu pamoja na mpenzi wangu Sam.

    Sam alionekana kunitazama muda wote wala hakuishiwa hamu kuniangalia kama ambavyo mimi sikuishiwa hamu kumuangalia yeye.

    Tukapitiwa na usingizi ndani ya basi.



    Tuliposhtuka tulikuwa Morogoro ambapo kuna baadhi ya abiria walishuka na wengine kupata ili kuendelea na safari.

    Nikawaona wafanya biashara wakizunguka kwenye madirisha na biashara zao, nikatamani kununua matunda ili nichangamshe mdomo hata hivyo njaa nayo ilinipata.

    Nikafungua mkoba kutoa pesa, ila nikakutana na ujumbe kwenye karatasi ambapo nikalitoa na kulisoma

    "Kwakweli binadamu mnaubahili wa ajabu, pesa nimekupa mimi ila bado umeona ubahili kuchukua ndege ili ufike mapema. Mnapenda mizunguko wakati njia ya mkato ipo. Na ndivyo ilivyo mpaka kwenye maisha yenu ambayo nayo mnayaonea ubahili pia. Unaonyeshwa njia ya mkato ili unufaike nayo ila kwa ujinga wenu mnataka mzunguko haswa wewe Sabrina sijui unamatatizo gani, wenzio wote wanapenda njia za mikato ila wewe unapenda mzunguko. Nadhani utapenda nikikufanyia muujiza mpya kwa sasa"

    Nikakisoma mara mbili mbili kile kikaratasi kisha nikamuamsha Sam ili nae apate kukisoma.

    Alipokisoma akaniangalia na kuniuliza,

    "Nani kakupa huu ujumbe?"

    "Nimeukuta kwenye pochi"

    "Nani kauandika?"

    "Hata sijui umeandikwa na nani"

    Sam akasema tutulie na tuwe makini sana kwani ule ujumbe ulimpa mashaka haswa lile swala la kusema kuwa atafanya muujiza mpya kwa sasa.

    Sam aliniangalia kwa makini sana kisha akaishika mikono yangu kwa nguvu kwa kutumia mikono yake na hata sikumuelewa kuwa anamaana gani kufanya vile ila nikatulia.

    Muda kidogo usingizi mzito ukatupitia wote wawili.



    Kuja kushtuka, hatukuwa tena kwenye lile basi kubwa la mikoani bali tulikuwa kwenye daladala. Moja kwa moja nikatazama pochi yangu kama ipo pamoja nami maana huu mchezo sikuuelewa kabisa yani, ila pochi ilikuwa palepale miguuni pangu.

    Nikamuangalia Sam ambaye alikuwa bado amelala, nikamshtua

    "Sam, Sam amka"

    Akashtuka kama mtu aliyeona kitu cha ajabu vile ila muda huo huo tukamuona konda wa lile daladala akisema kuwa tushuke

    "Mwisho wa gari jamani shukeni"

    Abiria wote walishuka ila mimi na Sam tulikuwa kama watu waliopigwa na bumbuwazi na kuuliza

    "Kwani hapa wapi?"

    Yule konda hakutujibu zaidi ya kutusisitiza kuwa tushuke, na tuliposhuka ile gari ikaondoka.

    Tukabaki tukitazamana tu na Sam, kisha Sam akaniuliza

    "Kwani tupo wapi hapa Sabrina?"

    "Sijui"

    "Tumefikaje fikaje?"

    "Sijui"

    Sam akaonyesha kuchukizwa na majibu yangu ya sijui wakati ni kweli kwamba sijui chochote wala lolote yani mimi nipo kama yeye tu alivyo.

    Kuna mdada alikatisha mbele yetu, nikaamua kumuita na kumuuliza.

    "Samahani dada, eti huu ni mkoa gani?"

    Yule dada akatabasamu kidogo na kutujibu

    "Hapa ni Kigoma mwisho wa reli"

    Akacheka tena na kuondoka.

    Nikamuangalia Sam naye akaniangalia na kujikuta tukisema pamoja kwa mshangao

    "Kigoma!!"

    "Tumefikaje fikaje Sabrina?"

    "Kwakweli sijui hata unavyoniuliza ni kazi bure tu maana hata mimi mwenyewe nashangaa kuwa hii Kigoma tumefikaje, lile daladala tumepandaje na tumepandia wapi hata sielewi naona miujiza tu"

    Tukaona mgahawa eneo lile, tukasema ni bora tukapumzike kidogo kwenye mgahawa ule ili kutuliza akili zetu zilizojaa mawazo yasiyoeleweka kwa sasa.

    Tukaagiza na chakula ila hatukuwa na hamu ya kula kwani kila mmoja alikuwa na mawazo kuwa tumefika pale kwa namna ipi na kwa mtindo upi.

    Nikajua yote haya ni mipango ya yule jamaa wa ndotoni kwani anauwezo wa kufanya chochote atakacho ukizingatia ameshanipa ujumbe kuwa atafanya miujiza yake. Hofu ikanijaa juu ya Sam na uoga kunishika, nikahisi kama kwenda na Sam hadi kijiji nilichoelekezwa kuwa ni cha kina Carlos ni kumuweka Sam mashakani.

    Ikabidi nimwambie Sam kuwa aningoje hapo mjini ili mimi niende ninakotakiwa kwenda, ila Sam akanikatalia kabisa na kusema

    "Ilimradi nimeamua kufanya hili basi niachie nifanye. Chochote kitakachotokea kwangu ni juu yangu mimi mwenyewe"

    Sikutaka kupoteza muda zaidi, nikawafata wenyeji wa pale na kuwauliza kijiji nitakacho kwenda.

    Wakanipa maelekezo yote yanayotakiwa, baada ya hapo mimi na Sam tukaianza safari ya kwenda mahali ambako tumepewa maelekezo.

    Tukapanda gari, Sam akaniuliza

    "Una uhakika kuwa hii safari ni ya muhimu Sabrina?"

    Nikamuitikia kwa kichwa, Sam hakuelewa umuhimu wa hii safari kwavile hakujua kuwa naenda kufanya nini ila mimi mwenyewe ndio nilijua umuhimu wake.

    Natakiwa kufanya hivi ili niinusuru familia yangu pamoja na huyu Sam asiyejua umuhimu wa hii safari kwangu.

    Sikupenda kusumbuliwa zaidi na lile jini, napenda kuwa huru ndiomana nimeamua kufanya jambo hili ingawa najua linaweza kuwa na madhara kwangu.



    Tulifika kwenye kijiji ambacho nimeelekezwa na kushuka, nikaangaza macho ili angalau nimpate mtu wa kumuuliza.

    Tukamuona mdada kwa mbali na kuamua kumuita, yule mdada akasogea karibu ila kabla sijamuuliza chochote alianza kukimbia huku akipiga kelele

    "Mchawi, mchawi, mchawiiii"

    Tukamshangaa sana na kujiuliza kuwa anamaana gani kutuita mchawi wakati hatujamuuliza kitu chochote bado?

    Hatukuwa na sababu ya kuendelea kusimama pale badala yake tulitembea tembea ili kuangalia uwezekano wa kumpata mtu mwingine wa kumuuliza.

    Tukamuona kijana akikatisha mbele yetu, tukamuita na kusalimiana nae kisha kuanza kumuuliza.

    Ila kabla hatujamuuliza vizuri, tulishangaa kumuona yule dada wa kwanza aliyekimbia akija na kundi la watu huku wakiwa wamebeba silaha mbali mbali, wengine magongo, mawe, fimbo nakadhalika, halafu wote walikuja tuliposimama mimi na Sam.

    Hofu ikatutawala na hatukujua cha kufanya.





    Tukamuona kijana akikatisha mbele yetu, tukamuita

    na kusalimiana nae kisha kuanza kumuuliza.

    Ila kabla hatujamuuliza vizuri, tulishangaa kumuona

    yule dada wa kwanza aliyekimbia akija na kundi la

    watu huku wakiwa wamebeba silaha mbali mbali,

    wengine magongo, mawe, fimbo nakadhalika, halafu

    wote walikuja tuliposimama mimi na Sam.

    Hofu ikatutawala na hatukujua cha kufanya.

    Wale watu walizidi kuja tuliposimama sisi, yule mkaka tuliyesimama nae akatuuliza kuwa kuna tatizo gani kwani

    "Kwakweli hatujui kaka yangu"

    Kisha akatuambia,

    "Kwa jinsi nijuavyo kijiji hiki, hapa lazima kuna khatari. Ni bora mkimbie tu maana mnaweza kuuwawa bila ya kutarajia"

    Tukashindwa kuelewa pa kukimbilia na wale watu walizidi kuja upande wetu.

    Sam akaona kamavile tunapoteza muda, akanishika mkono na kuanza kukimbia na mimi.

    Wale watu wakaanza kutukimbiza sasa, na sisi tukazidi kukimbia huku tukigeuka nyuma na kuangalia walipofikia.

    Walipofika kwa yule mkaka tuliyekuwa tukiongea nae wakasimama kidogo nadhani walikuwa wanachukua maelezo au kumpa maelezo kidogo ila na sisi tuliendelea kukimbia.

    Nikafika mahali na kuchoka sana nikasimama, kugeuka nyuma nikawaona wale watu wote na yule mkaka wameungana kutukimbiza.

    Sam akanivuta tena,

    "Twende Sabrina hapa si salama"

    Tukaendelea tena kukimbia, kwakweli nilichoka na kuhemea juu juu kwani sikujua tatizo ni nini na usalama wangu uko wapi.

    Kwa bahati nzuri tukaona gari ikikatisha pale njiani, Sam akaisimamisha nayo ikasimama kisha tukapanda na kuondoka huku tukihemea juu juu bila ya kujielewa.

    Dereva wa lile gari hakutuuliza chochote ila alitupeleka hadi mjini.

    Alipofika mahali pale mjini akasimamisha gari ili tushuke, nasi tukashuka.

    Nikafungua mkoba ili nimlipe, wakati nainama kumlipa akaniangalia na kutabasamu bila ya kupokea ile pesa kisha akaondoa gari.

    Nilishtuka sana, nikamsogelea haraka Sam na kumkumbatia kwani sikuamini nilichokiona. Yule dereva alikuwa ni yule kijana wa ndotoni, kwakweli niliogopa sana. Sam akaniuliza,

    "Kwani kuna nini Sabrina?"

    Sikuwa na maelezo kwakweli ila nikamuomba Sam kuwa tutafute hoteli ya karibu ili tuweze kupumzika maana nilihisi akili yangu kuanza kupoteza muelekeo kabisa.

    Sam hakupingana na mimi bali alikubali na tukafanya kama tulivyokubaliana, tukatafuta hoteli na kwenda kukaa na kupumzisha mawazo kwanza.



    Tukiwa pale hotelini, Sam akaendelea kunidadisi kwani hakuelewa chochote.

    "Unajua Sabrina haya mambo ni ya ajabu sana! Inatakiwa kuwa makini sana. Tusishangae tupo hoteli sasa Kigoma ila kufumba na kufumbua tupo baharini tena Dar, inatakiwa uniambie mambo yalivyo usifanye kama wale wasemao kwenye msafara wa mamba kenge nao wapo, nahitaji tuwe msafara mmoja Sabrina kama mamba basi wote mamba na kama kenge basi wote kenge"

    "Nakuelewa Sam"

    "Kama unanielewa niambie ukweli, lengo la kuja Kigoma ni nini na lengo la kwenda kwenye kile kijiji ni nini?"

    Nikapumua kwanza kwani maelezo yangu yalikuwa yakigongana gongana.

    Sam alitulia kabisa ili nimwambie kinachotakiwa kufanya.

    Nikaamua kumwambia kwa kifupi kuwa lengo langu la kuwa Kigoma ni kufatilia familia ya wakina Carlos kwakuwa siwajui, Sam akanishangaa sana na kuniuliza

    "Ulikubali vipi kuolewa na mtu ambaye huifahamu familia yake?"

    "Ni historia ndefu Sam, kwa kifupi niliolewa nae bila ya kutarajia."

    "Sasa familia yake unaitafutia nini kwasasa?"

    "Nahitaji kuijua"

    "Unadhani utaipata? Si nilikwambia mimi kuwa Carlos sio mtu wa kawaida ila hukutaka kunisikia. Ungenielewa toka mwanzo basi haya yote yasingekuwepo kwasasa"

    Ikabidi nimsimulie Sam kuhusu wazazi wa bandia wa Carlos, naye akashangaa sana. Nikamweleza nilipoambiwa nikawatafute wazazi wa ukweli wa Carlos kwa nia ya kumjua ni nani na pia kuweza kudai talaka.

    Sam aliposikia neno la taraka akafurahi zaidi na kuendelea kusema kuwa atakuwa bega kwa bega na mimi katika hili.

    "Ila kwavile muda umekwenda sana acha tupumzike halafu kesho tufanye hiyo kazi kwa uangalifu zaidi.

    Muda ulikuwa umeenda kidogo, tukaenda dukani na kununua baadhi ya nguo za kubadilisha kisha tukarudi pale hotelini kupumzika.

    Sikutaka kushirikiana chochote na Sam, ilibidi tuwe kaka na dada ili kuepuka matatizo yasiyo na lazima.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Wakati wa kulala kila mmoja alilala upande wake ingawa chumba kimoja, namshukuru sana Sam ni mwanaume muelewa na asiyekuwa na papara za makusudi.

    Usingizi ukanipitia, ikaja ndoto ya ile siku niliyokamatwa uchawi na kufanya mambo ya ajabu na kushangaza watu kisha nikaliona lile kundi la jana yake likitaka kunipiga.

    Nikashtuka sana toka usingizini huku jasho likinitoka kwa wingi, nikamuangalia Sam pembeni ila hakuwepo hapo ndipo uoga ukanishika kuwa ni kitu gani kimempata mtoto wa watu tayari kwani najijua kuwa mimi nina majanga ndiomana nilikuwa nakataa kuja nae huku, sikujua nimuulize nani maana ulikuwa ni usiku.

    Nikainuka pale kitandani na kutoka nje ili nijaribu kumuangalia alipoelekea.



    Nilipotoka nje kabisa ya ile hotel, nikamuona Sam akielekea kama maeneo ya barabara kuu.

    Nikaanza kumkimbilia, nilipofika nikamshika mkono wake kwa nguvu huku nikimvuta kuwa turudi ila ikawa kama kuna mtu ninayevutana nae yani mimi namvuta na huyo mtu anamvuta pia hadi nikaanguka chini.

    Sam alizidi kuondoka, nikapata wazo la kumuita kwa nguvu

    "Wee Sam"

    Akashtuka na kugeuka nyuma, akaniona pale chini ila Sam alikuwa kama mtu aliyepigwa na bumbuwazi kwani alinikodolea macho tu bila ya kusema chochote.

    Nikainuka pale chini na kumfata tena alipo, nikamtingisha kwa mkono na kumuita tena

    "Wewe Sam wewe"

    Sasa akashtuka kamavile mtu aliyetoka kuamka, akaanza kunishangaa mimi badala ya mimi kumshangaa yeye, kisha akaniuliza

    "Kwani imekuwaje?"

    "Imekuwaje nini? Hebu turudi ndani"

    Nikamshika mkono na kurudi nae, kwenye mlango wa ile hoteli tukakutana na muhudumu mmoja wapo wa pale ambapo alituuliza kulikoni.

    Nikamjibu kwa kifupi kuwa mwenzangu aliondoka gafla tena akiwa usingizini, yule muhudumu akatuambia

    "Hii ndio Kigoma jamani kuweni makini"

    Kisha akaondoka na kutuacha pale tukitazamana.

    Nikamshika tena Sam mkono na kurudi kwenye chumba chetu kisha nikamuuliza kuwa anatatizo gani

    "Hata mimi sielewi Sabrina"

    "Mmh haupo makini Sam"

    "Makini gani wakati nilikuwa nimelala jamani, ila gafla nikasikia kama naitwa hapo ndio nikaitika ila sikujua ni nani aliyeniita ila ndio sijajielewa hadi uliponishtua"

    "Usipende kuitika unapoitwa usiku, huwa ni wachawi hao wanaofanya hayo mambo"

    "Ila yote ni sababu ya kusahau kumuomba Mungu atulinde Sabrina yani tunalala tu kama kuku ndiomana tunapatwa na makubwa"

    Tukaamua kuomba kisha kulala maana ni kweli tulisahau kufanya hivyo kwakweli.

    Tukalala vizuri sasa hadi kunakucha.



    Mipango ya leo ilikuwa ni Sam kwenda peke yake kwanza kuchunguza kile kijiji hadi apapate kwakina Carlos kisha mimi na yeye tukiondoka twende moja kwa moja kwa wakina Carlos.

    Ila nilienda kununua simu kwanza ili niweze kuwasiliana na Sam akiwa huko maana ile simu yangu ya majanga niliiacha nyumbani, kisha Sam akanipa laini yake moja tuweze kuwasiliana.

    Nikamsindikiza hadi kwenye mabasi ya kuelekea kwenye hicho kijiji, njiani akanunua kapelo ili aonekane tofauti na wajana kisha mimi nikarudi pale hotelini.



    Nilipokuwa pale hotelini, wazo likanijia kuwa huenda wale wanakijiji ndio wale wale walioniona nilipopelekwa kimaajabu. Ingawa mimi mwenyewe sikikumbuki kile kijiji kwasababu ilikuwa kimiujiza lakini huenda wao wakawa wananikumbuka vizuri.

    Wazo likanijia kuwa nikanunue nywele za bandia na miwani ili nitakapoenda tena nionekane tofauti.

    Sikupoteza muda zaidi, nikaenda dukani na kununua nywele za bandia na miwani na mkoba mwingine.

    Kununua hivi vitu halikuwa tatizo kwangu kwavile pesa nilikuwa nayo kwa kipindi hicho, ni ile pesa niliyopewa na yule kijanda wa ndotoni kwenye bahasha.



    Wakati natoka kwenye lile duka la vipodozi njiani nikakutana na kijana ambaye nilikuwa simfahamu kabisa, akanisimamisha na kuanza kuongea na mimi kamavile mtu anayenifahamu

    "Za siku nyingi shemeji? Khee umepotea sana"

    Nilikuwa kimya nikimtazama kwavile nilikuwa simjui na wala sijawahi kumuona mahali popote pale, sasa huo ushemeji wa mimi na yeye umeanzia wapi? Nikamshangaa tu ila yeye aliendelea kuniongelesha bila ya kujali kama simjibu wala nini.

    Nikaachana nae na kuondoka ila akanifatilia nyuma huku akitaka nimjibu, nilimuangalia kwa hasira sana na kumuuliza

    "Kwani unatatizo gani wewe mkaka jamani?"

    Akatabasamu na kusema,

    "Nilitaka unijibu tu Sabrina"

    Nikashtuka na kumuuliza kuwa jina langu amelijulia wapi

    "Nakujua Sabrina, wewe ni shemeji yangu"

    "Shemeji yako kwa nani?"

    "Mwangalie yule"

    Akaonyesha kidole kwenye mti mmoja ambapo kulikuwa na mtu kasimama chini yake lakini sikumtambua na kumuuliza tena

    "Yule nani?"

    Kabla hajanijibu nikashtukia nipo pale chini ya ule mti huku nikitazamana na yule mtu, nikataka kukimbia kwa uogo ila akanidaka mkono na kucheka sana.

    Alikuwa ni yule kijana wa ndotoni, aliniangalia usoni ila sikuweza kumtazama mara mbili mbili kwani niliogopa sana na kujiziba sura yangu, akaniuliza tena

    "Utaniogopa mpaka lini Sabrina?"

    Nilikuwa natetemeka tu, akaendelea kusema

    "Ingawa nimekuachia kuwa karibu na umpendae ila bado unaniogopa, naweza kufanya chochote Sabrina hutakiwi kuniogopa sana"

    Bado niliendelea kujiziba usoni.



    Ukapita muda kidogo nikahisi kama nipo peke yangu, nikajitoa mkono usoni ili kuangalia kama kweli nipo mwenyewe.

    Nikajikuta nipo kwenye chumba cha hoteli, nikashtuka sana na kushangaa kwakweli mambo haya yamekuwa ya ajabu sana kwangu nikatamani hata kukimbia ila nitaelekea wapi?

    Nilijiangalia mara mbili mbili na kuogopa, nikatoka kwenye chumba kile.

    Nikaangalia pale nje palivyo, kwakweli huyu mtu ananitishia sana na kuitoa amani ya moyo wangu kabisa.

    Nikatazama miti inavyopepea huku nikiwaza mambo mengi hata nikiwaza kuwa kwanini nimekuwa binadamu ambaye nateseka bila sababu za msingi wala nini.



    Muda mfupi ukapita pale nje, nikashtuliwa na mtu alikuwa ni mdada ambaye pia sikumfahamu, akaniambia

    "Pole kwa usiku wa jana dada"

    Nikamtazama na kumuuliza

    "Pole ya nini?"

    "Nilijua na nyie ni wepesi kumbe wazito eeh! Pole sana kwa usumbufu"

    "Mbona sikuelewi dada?"

    "Yote ya usiku wa jana ni mimi niliyeyafanya, nilimuhitaji mwenza wako kwa usiku mmoja tu wa jana"

    Kisha akaondoka, nilimuangalia bila ya kupata majibu juu yake.

    Huyu msichana alinishangaza sana, nikaamua kwenda kukaa kwenye mgahawa ili ninywe angalau juisi huku nikimngoja Sam kwani nilikuwa natamani sana kujua yaliyojili mahali alipoenda.

    Nilikaa sana pale ila Sam hakurejea na wala simu yake haikupatikana. Mawazo mabaya yakanitawala ila mwisho wa siku nikaamua kurudi kwenye chumba hotelini.



    Nilipoingia nikamkuta Sam ameshafika ndani, inaonyesha kuwa amefika muda mrefu tu.

    Nikamsalimia na kumuuliza kuwa kwanini simu yake haipatikani

    "Hilo swali nikuulize wewe maana muda wote nimekutafuta sijakupata"

    "Sawa basi tuachane na hizo khabari, nieleze mambo ya uko"

    "Huko ni salama sana ila nimechoka kupita maelezo, nadhani itakuwa ni vyema kama ningepumzika kwanza"

    "Ila ungeniambia kwanza ingekuwa vizuri zaidi"

    Akacheka na wala hakutaka kuniambia na kusisitiza kuwa anatakiwa apumzike kwanza kabla ya kunieleza.

    Sikutaka kumlazimisha sana kwahiyo nikamuacha apumzike ila akaniomba nikaagize chakula na kukileta ila atakapoamka apate kula.

    Nikainuka kwa lengo la kwenda kutafuta hicho chakula.



    Wakati nanunua chakula nikapata ujumbe kwenye ile simu niliyobeba.

    Nikafungua na kuusoma,

    "Usidhani kazi niliyokupa ni rahisi kiasi hicho, wewe ni mwanadamu na lazima upambane ili mwisho wa siku mshindi ajulikane kati ya mimi na wewe"

    Nikashtuka sana, nikaangalia namba iliyotuma ule ujumbe sikuona namba yoyote yani hapakuwa na namba kabisa.

    Nikaacha maagizo pale kwenye mgahawa na kurudi chumbani kwa lengo la kumuonyesha Sam ujumbe huo.



    Nilipokaribia kwenye chumba nikashangaa kumuona mtu nisiyemfahamu akitoka kwenye chumba chetu.

    Nikakimbilia mlango na kufungua ili nione kuna nini.

    Nikashtuka sana na kuhisi kuchanganyikiwa nilipomuona Sam kitandani akiwa amechomwa na kisu halafu damu zimetapakaa kwenye kitanda kile.





    Nilipokaribia kwenye chumba nikashangaa kumuona

    mtu nisiyemfahamu akitoka kwenye chumba chetu.

    Nikakimbilia mlango na kufungua ili nione kuna nini.

    Nikashtuka sana na kuhisi kuchanganyikiwa

    nilipomuona Sam kitandani akiwa amechomwa na

    kisu halafu damu zimetapakaa kwenye kitanda kile.

    Nikakodoa macho kamavile mtu aliyefumaniwa na sikuelewa cha kufanya kwakweli.

    Nilitaka kupiga kelele ila nikashindwa kwavile sikuamini kilichopo mbele yangu.

    Nikaanza kusogelea taratibu ili kumuangalia vizuri, machozi yalikuwa yananibubujika.

    Nilipofika karibu nikataka kumchomoa kile kisu kwani nilimuona akitapatapa yani kama mtu anayekaribia kukata roho, ila kabla sijashika kile kisu kuna mtu alikuja nyuma yangu na kunivuta.

    Kwakweli hapo nilijawa na uoga na kutaka kupiga kelele ila yule mtu akaniziba mdomo.

    Nikazidi kutetemeka na kuishiwa nguvu kabisa, akanigeuza na kuangaliana nae. Alikuwa ni Sam, kwakweli nguvu ziliniishia kabisa, nikahisi kuchanganyikiwa na kuzimia pale pale.



    Haikuchukua muda sana nikazinduka, nilikuwa kwenye mikono ya Sam, huku nimelala chini yani kichwa changu kikawa kwenye mikono yake.

    Nilishtuka kwa uoga na kukaa, ilikuwa tupo mule mule ndani.

    Sam akaniambia kuwa nisipige kelele.

    "Tulia Sabrina, usiwe na papara bila ya utulivu hatutaweza kukomboka hapa"

    Kwakweli hata sikuwa na imani kama huyu anayeongea hapa ni Sam kweli, nikamwangalia kwa makini ni kweli alikuwa Sam ninayemfahamu ila swali likaja, je yule aliyelala pale kitandani na kuvuja damu sababu ya kuchomwa kisu ni nani kama sio Sam? Na yule niliyemuona akitoka ni nani pia? Maswali mengi bila ya majibu.

    Nikamuangalia tena Sam niliyekaa nae pale chini, kisha nikainuka ili nikamtazame tena wa pale kitandani maana nilihisi kamavile naanza kuchangnyikiwa ila Sam akanizuia na kuniambia,

    "Hapa mahali si salama tena kwetu, tunatakiwa kuondoka"

    Nikamuuliza kuhusu yule anayevuja damu pale kitandani,

    "Haya ni mauzauza Sabrina, kwanza kabisa huyo mtu kawekwa kama mimi ila sio mimi. Hapa hapatufai, inatubidi tuondoke kimya kimya watajijua wenyewe wenye hoteli. Tukiendekeza mambo hapa tunaweza kufungwa kifungo cha maisha kwa kosa ambalo hatujui nani kalitenda, ndiomana mimi nimekaa kimya nikingoja ushtuke maana tukipiga kelele na watu kulijua hili tutajikuta rumande hukuhuku ugenini"

    Ikabidi nikubaliane na Sam, ambapo akaniambia kuwa mimi nitangulie halafu yeye akafata nyuma yangu.

    Kufika nje, tukakodi gari na kuondoka maeneo hayo na kwenda maeneo mengine kabisa.

    Tukaenda moja kwa moja kwenye mgahawa wa karibu na eneo tuliloenda na kupumzika kwanza, kwakweli sikuelewa kitu hata sikujua nianzie wapi na niishie wapi kumuuliza huyu Sam.

    Nikaamua kumuuliza swali linalonipa utata zaidi

    "Hivi wewe ni Sam kweli?"

    "Sasa unadhani mimi ni nani jamani Sabrina!"

    Nikamuangalia tena Sam na kumwambia,

    "Wewe ni Sam, sasa yule wa kule ni nani?"

    "Yale ni mauzauza Sabrina"

    "Wewe umerudi muda gani?"

    "Nimerudi muda ule ule na kukuona ukitaka kwenda kukigusa kile kisu ndio pale nikakuzuia Sabrina, maana ungekigusa vidole vyako vingebaki kama ushahidi"

    "Inamaana niliyeongea nae mwanzo alikuwa ni nani hadi akaniagizia chakula?"

    "Sijui ila nadhani ni hayo hayo mauzauza yako Sabrina"

    Nikashindwa hata kumuuliza habari za alipotoka maana nilikuwa na mawazo sana na sikujua cha kufanya kwakweli ukizingatia nilishamuuliza yule wa mwanzoni ambapo nilihisi kuwa ni Sam, sasa kumuona na huyu mwingine akili ikanivurugika kwakweli.

    Nilihitaji kupumzika kwa muda huo ili kuweza kuweka akili yangu yangu, kwahiyo nikamuomba Sam akatafute mahali ambapo nitaweza kupumzika.

    Sam akaenda kutafuta mahali kisha nikaondoka nae na kwenda kwenye sehemu aliyotafuta, kilikuwa chumba kikubwa tofauti na chumba cha kwenye hoteli ya mwanzo.

    Sam alinisisitiza kuwa nile lakini sukuweza kula maana nilishindwa kabisa, nikatamani yale mambo yaishe muda wowote ule ili nirudi nyumbani nikiwa huru.



    Tukiwa mule chumbani Sam akaanza kunieleza yaliyojiri sasa

    "Yani kile kijiji kina mambo ya ajabu hakuna mfano, niliwauliza kinyemela kuwa juzi kuna watu walikuwa wakiwakimbiza kwa magongo kwanini? Wakaniambia kuwa mwanamke aliyekuwa juzi ni mchawi na wameshawahi kumfuma live hadi kumpeleka polisi yani ni wewe Sabrina nadhani kuna mtu wanakufananisha nae ndiomana yakatokea yote yale yaliyotokea."

    Sam hakujua ukweli kuwa walinibamba kweli na kupelekwa polisi ila hata kama nikimueleza nitamueleza vipi kuhusu yaliyojiri siku hiyo ambayo nilikamatwa uchawi ambao sijawahi kuufanya katika maisha yangu? Nikaamua kumuacha aamini kuwa wale watu wamenifananisha tu.

    "Basi usijali Sabrina, nimefika hadi sehemu husika kwahiyo kesho tutaenda moja kwa moja bila ya kumuuliza mtu yeyote yule"

    "Je, ulibahatika kuongea na wazazi wa Carlos?"

    "Hapana sijaongea nao ila nimepafahamu wanapoishi, sikuwa na cha kuongea nao kwakweli ni kheri wewe mwenyewe muhusika ukiwepo karibu na kuongea nao"

    Nikaelewana na Sam kuhusu hilo pia nikamueleza kuhusu wigi nililonunua ili wasinifananishe tena tutakapoenda, Sam akakubaliana na mimi bila ya tatizo lolote lile.

    "Itakuwa vyema sana kwani itasaidia kwa wale wanaokufananisha wasikufikirie tena"

    Tukaendelea kuongea mambo mbali mbali.



    Usiku ulipofika Sam akashauri kuwa twende tukale kwanza ndio turudi kupumzika.

    Ingawa sikujisikia hamu ya kula ila niliamua kwenda kwasababu ya kuogopa kubaki mwenyewe na pia nilitaka kumpa kampani Sam wakati anakula ili asijisikie upweke.



    Mahali tulipoenda kula tukakuta kuna taarifa ya habari ikitangazwa.

    Tulitulia na kuisikiliza taratibu huku tukingoja chakula tulichoagiza na kuongea habari za hapa na pale.



    Chakula kilipoletwa, tukajikuta tukizidi kukodolea taarifa ya habari maana habari iliyotangazwa ilionekana kutugusa kabisa.

    Macho yetu yalikodolea luninga iliyotangaza khabari hiyo

    "Mtu mmoja amekuta amekufa kwenye chumba cha hoteli moja mkoani Kigoma, chanzo cha kifo cha mtu huyo hakijajulikana hadi sasa ila amekutwa akiwa amechomwa kisu na kuachwa juu ya kitanda. Polisi wanaendelea na upelelezi wao juu ya kifo hicho huku wakihisiwa watu wawili kuhusika nacho ambao walikodi chumba hiko kwani hadi sasa hawajulikani walipoelekea"

    Mimi na Sam tukajikuta tukiangaliana kwani hata Sam hamu ya kula ilimuisha na kujikuta akiinuka kisha akinishika mkono kuwa niinuke ili tuondoke.

    Nikainuka na kuondoka kwenye ule mgahawa huku tukijiuliza njiani, Sam alikuwa wa kwanza kuniuliza

    "Hivi hii kitu ni nini jamani Sabrina? Mbona sielewi mama angu! Tutafanyaje sasa?"

    "Kwakweli Sam sijui lolote, cha msingi turudi ndani tukapumzike ili tupange huko cha kufanya"

    Tukarudi kwenye hoteli tuliyokodi sasa, kote ilitapakaa habari ileile ya mtu aliyekufa hotelini huku kila mmoja akiwa na mashaka kuwa wauaji ni wakina nani na wako wapi.

    Tukapitiliza na kwenda kwenye chumba tulichokodi, ile kuingia tukamkuta mtu yule yule kitandani akiwa amechomwa kisu na damu kutapakaa ila yule mtu hakuwa Sam kama ambavyo nilimuona mwanzo kwenye ile hoteli nyingine.

    Nikaogopa sana na kumkumbatia Sam ambaye naye aliogopa, tukachukua vitu vyetu na kuufunga ule mlango wa kile chumba na kuondoka eneo lile maana tulihisi kuchanganyikiwa kabisa yani.

    Tukakodi gari na kuondoka eneo lile, tukaenda eneo lingine na kushuka kisha kumlipa dereva.

    Tulienda kukaa kwenye gogo mojawapo bila ya kuelewa cha kufanya kwani kila mmoja wetu alihisi kuchanganyikiwa kabisa.

    Tuliangaliana bila ya kupata jibu la aina yoyote,

    "Tutafanyaje Sabrina jamani?"

    "Kwakweli sijui Sam"

    Nikahisi machozi yakinichirizika kwani kufungwa bila ya kutarajia kunanukia sasa yani maisha haya ni balaa kwakweli.

    "Haya ni mauzauza yaliyopitiliza Sabrina, tutafika kweli kwa hali hii! Mbona mambo yanazidi kuwa magumu jamani?"

    "Kwakweli sijui"

    Sam akatoa wazo kuwa tutafute nyumba ya kulala wageni ili tuweze kupumzika kwa muda huo maana hakuna cha kufanya.

    Tukatafuta nyumba ya wageni na kupewa funguo ya chumba, tukalipia na kwenda kwenye hiko chumba.



    Tuliingia tukiwa tumechoka kwakweli maana yale mambo ya maajabu yalitutishia maisha.

    Muda kidogo alikuja muhudumu wa ile nyumba ya kulala wageni, alikuja kutuletea sabuni.

    Nilimfungulia mlango vizuri, gafla nikamuona akishtuka na kuuliza

    "Nini ile?"

    Kugeuka nyuma, nikamuona tena yule mtu aliyechomwa kisu akiwa kitandani.

    Nikamshtua Sam ambapo nae alishtuka kumuona tena yule mtu na kutoka mule chumbani, yule muhudumu akajaribu kusogelea ili kuona kuwa ni kitu gani.

    Gafla akaanguka chini na kuzimia, kwakweli tukaona sasa ni kesi juu ya kesi.

    Sam akanishika mkono na kuanza kunitoa mule haraka haraka.

    Kwenye mlango wa ile nyumba tukakutana na muhudumu mwingine aliyetuuliza kuwa mbona tunaondoka, Sam akamdanganya kuwa tunaenda kutafuta chakula.

    Kisha tukamuacha pale mlangoni na kuondoka kwani tuliogopa kuwa kama akienda kwenye kile chumba anaweza kupiga kelele kisha watu kuja kutukamata.

    Tuliondoka kabisa eneo lile,

    "Tutafanyaje Sam?"

    "Sijui Sabrina"

    Tulikaa na kutafakari bila majibu, Sam akaanza kuniambia kitu anachoona ni vyema kwa wakati huo

    "Sabrina, naona ni vyema kama tukitafuta waombeaji kwa swala hili maana hakuna la kufanya kwa wakati huu"

    Tukakubaliana na Sam, tukamfata kijana mmoja aliyeonekana akifunga duka lake na kumuuliza kama amewahi kusikia habari ya waombeaji kwa eneo hilo, naye akatuuliza

    "Waombeaji kivipi?"

    Sam ndiye alikuwa muongeaji maana mimi sikuelewa kitu kabisa

    "Yani wale watu wanaoombea watu wengine wakiwa kwenye matatizo mfano wachungaji, mashekhe na mapadri"

    "Kwa hapa namfahamu mzee mmoja ni shekhe huwa anawasomea watu visomo kisha wanaondokewa na matatizo yao"

    "Basi tupeleke huko huko"

    Akatuambia tumngoje amalizie kufunga duka lake kwanza, nikamvuta Sam pembeni na kumuuliza

    "Una uhakika na hili Sam?"

    "Kivipi Sabrina?"

    "Yani una uhakika huyo mzee ataweza kutusaidia?"

    "Ndio nina uhakika, kwanza ushaambiwa kuwa amewasaidia watu wengi tu kwanini asitusaidie na sisi? Lazima atatusaidia hata kwa makazi ya usiku wa leo, usiwe na shaka na watu wa Mungu"

    Yule kaka alipomaliza kufunga akatupeleka kwa huyo mzee na kumwambia huyo mzee kuwa tunashida nae.

    Sam ndiye aliyezungumza na yule mzee lakini sidhani kama Sam alimueleza yule mzee matatizo yetu yote ila yule mzee alitupa hifadhi pale kwake.

    Mimi nikalala na binti zake kisha Sam akalala na watoto wake wa kiume, kwakweli tulilala vizuri sana tofauti na tulivyotegemea.

    Leo sikuota ndoto yoyote mbaya wala kujiwa na kitu chochote kibaya hadi kunakucha.



    Tuliamka na kuanza kujiandaa kuondoka, yule mzee akatuambia kuwa tuende muda wowote tutakao na wala tusisite kumtembelea wala kuogopa chochote kile.

    Tulimshukuru sana na kuanza kuondoka eneo lile tulilokuwepo huku tukitafuta eneo la kwenda kujibadilisha kwa muda kabla hatujaenda kwenye kijiji cha wakina Carlos kama tulivyopanga.



    Tukaenda mahali na kujiandaa kwa muda kwakweli tulivyotoka tulionekana wa tofauti sana.

    Kwa mtu ambaye hatufahamu vizuri hawezi kabisa kufikiria kuwa ni sisi, kisha tukaianza safari ya kuelekea kwenye kile kijiji.

    Tulifika salama kabisa, Sam ndiye aliyetangulia katika kuniongoza mimi hadi nyumbani kwa wakina Carlos.

    Tukakaribishwa na mama mmoja ambapo nilipomuangalia vizuri sura yake haikuwa ngeni machoni pangu ila sikuelewa niliwahi kukutana nae wapi na kwa wakati gani.

    Alitukaribisha vizuri sana, wakati anazungumza na sisi ndio nikakumbuka kuwa yule mama ndiye aliyenisaidia khanga zake kwenye yale mauzauza, ndiye yule mama aliyejitambulisha kwangu kwa jina la mama Amina.

    Nilimuangalia tu ila yeye hakunitambua kutokana na ule muonekano mpya niliokuwa nao.

    Hapo nikatambua kuwa ni jinsi gani yule kijana wa ndotoni alivyoweza kucheza na akili zangu kiasi kile, ndiomana wale wanakijiji walinivamia kwa kuniita mchawi.

    Kugundua kuwa hiki ndio kile kijiji niligundua ila sikujua kuwa mwanamke aliyenisaidia ndio mama yake na Carlos.



    Tukaanza kuzungumza na yule mama kuhusu Carlos ambapo alishtuka sana kusikia kuwa sisi tunafahamiana na mtoto wake huyo, kisha akatuuliza

    "Hivi huyo Carlos mnayemzungumzia ni mwanangu mimi au Carlos yupi?"

    Yule mama hakutuelewa kabisa tulichokuwa tunamueleza, kisha akainuka na kuleta picha za Carlos kuwa pengine tunamfananisha, mimi nikaziangalia na kumjibu

    "Ndio Carlos huyu huyu tunayemuongelea"

    Gafla yule mama akaanza kulia tena alilia kwa kuomboleza.





    Yule mama hakutuelewa kabisa tulichokuwa

    tunamueleza, kisha akainuka na kuleta picha za

    Carlos kuwa pengine tunamfananisha, mimi

    nikaziangalia na kumjibu

    "Ndio Carlos huyu huyu tunayemuongelea"

    Gafla yule mama akaanza kulia tena alilia kwa

    kuomboleza.

    Yule mama alilia sana hadi kutufanya tuanze kuogopa kwani hatukujua analia kitu gani, mtoto wake wa kike akaja pale karibu kumbembeleza na kumuuliza kuwa kuna tatizo gani huku akituhisi kuwa sisi kuna kitu kibaya tumemfanyia mama yake.

    Yule mdada nilipomuangalia vizuri ndio yule aliyenishangaa siku niliyoenda kimaajabu pia ndio yeye ambaye tulimuuliza na Sam kisha kuanza kupiga makelele ya uchawi na kuita watu watupige.

    Ikabidi nijikaushe sasa na kuwa makini sana ili asije akanigundua tena na kusababisha balaa lingine.

    Yule mama aliendelea kulia na kufanya yule dada atufokee kwa maswali yasiyo jibika

    "Mmemfanyaje mama yangu nyie?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hatujamfanya kitu"

    "Kuna kitu mmemfanya, niambieni upesi sana"

    Tukabaki kuangaliana tu maana hakuna tulichomfanya kwakweli ila na sisi pia tulikuwa tunamshangaa kwanini analia kiasi kile.

    Yule dada nae akazidi kutukolomea, mwisho tukamweleza kuwa mama yake tulikuwa tunamuuliza kuhusu mwanae Carlos. Yule dada akaguna na kusema,

    "Ndiomana ameanza kulia, basi mwacheni hadi machungu yake yatakapopungua ndipo mwendelee kuzungumza nae, maana mmemkumbusha mambo ya nyuma sana na yanayomuumiza kila siku."

    Ikabidi mimi na Sam tutulie huku tukimngoja yule mama awe katika hali ya kawaida na tupate kumuuliza ya kwetu tunayotaka kuyajua.

    Tukatulia kabisa huku tukimsikilizia yule mama, ambaye aliinuka na kuingia ndani huku ile albamu yenye picha za Carlos akiiacha pale pale.

    Nikaichukua na kuendelea kuangalia, kulikuwa na picha nyingi sana za Carlos akiwa shule, na marafiki zake, nyingine akiwa nyumbani na kwakweli zilivutia sana kuziangalia hata nikashindwa kuelewa kuwa kwanini ananifanyia mambo ya kishetani kiasi kile na kwanini akanitambulisha familia yake ya uongo wakati alikuwa na familia nzuri tu? Na kwanini huwa anabadilika badilika na kuwa shetani? Sikuwa na jibu ila najua wazi kuwa huyu mama yake mzazi lazima atakuwa anajua kuhusu mtoto wake na kwanini amefanya yote yale sababu yeye ndio mzazi wake, kwahiyo tukatulia tukimngoja pale atakapotulia atuambie ukweli kuhusu mtoto wake.







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog