Search This Blog

CHOZI LA YATIMA - 3

 

    Simulizi : Chozi La Yatima

    Sehemu Ya Tatu (3)





    Musa akaitwa kuhojiwa na askari kama kawaida yao kwani unaweza kujikuta unahojiwa hata mara kumi.

    ASKARI: Wee kijana mwizi unaitwa nani?

    MUSA: Musa Israel

    ASKARI: Nani?

    MUSA: Musa Israel.

    Ndani ya ofisi kulikuwa na askari mkuu wa hapo amekaa kwenye meza, gafla akajikuta kuna jambo linamjia kichwani baada ya kusikia jina hilo.

    "Nakwambia, hii mimba si umeikataa!! Basi huyu mtoto nitakayejifungua nitamwambia kuwa baba yake anaitwa Israeli, na wala sitakutaja wewe. Na hiyo Israel si jina la mtu yeyote kama unavyodhani bali namaanisha yule malaika mtoa roho za watu kwani wewe ni muuaji na unafanana nae"

    Hiyo sauti ya kike ikajirudia kama mara tatu katika akili yake, akajikuta akiwaamuru wale maaskari waache kumpiga yule mtoto na wamuingize ofisini kwake ili amuhoji.

    Musa alipoingizwa ofisini hapo akakalishwa chini, basi yule askari akawaamuru wale maaskari watote na akaanza kumuhoji Musa.

    KAMANDA: Umesema unaitwa nani?

    MUSA: Naitwa Musa.

    KAMANDA: Musa nani?

    MUSA: Musa Israeli.

    KAMANDA: Baba yako yuko wapi?

    MUSA: Simjui wala na yeye hanitambui.

    KAMANDA: Je! Israeli ni jina lake?

    MUSA: Hapana.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    KAMANDA: Sasa mbona unajiita Musa Israeli ikiwa Israeli si jina la baba yako?

    MUSA: Mama aliniambia nijiite hivi sababu baba alinikataa.

    KAMANDA: (Akapumua kidogo), mama yako anaitwa nani?

    MUSA: Anaitwa Sada Mwinyi.

    KAMANDA: Sada Mwinyi?

    MUSA: Ndio Sada Mwinyi.

    KAMANDA: Yuko wapi kwasasa?

    MUSA: Amekufa.

    KAMANDA: (Akashtuka sana), amekufa? Dah! Pole sana. Kwahiyo sasa unaishi wapi?

    MUSA: Naishi mitaani tu.

    KAMANDA: Mitaani? Kwanini?

    MUSA: Ndugu wa mama walinifukuza baada ya mama yangu kufariki.

    KAMANDA: Na kwanini unaiba?

    MUSA: Maisha ya mtaani ni magumu sana ndio yanayotufanya watoto wa mitaani tuibe.

    Yule kamanda akajikuta amekosa raha kwakweli, mara wakaingia wale maaskari ili kumchukua Musa wamrudishe rumande ila yule kamanda akawazuia na ikawabidi watoke nje.

    KAMANDA: Musa, nataka nikuchukue ili ukaishi nyumbani kwangu. Je uko tayari.

    MUSA: kweli muheshimiwa? Niko tayari tena nitafurahi sana.

    Basi yule kamanda akamchukua Musa ili aondoke naye, akaenda kuifuta kwanza kesi inayomkabili na kujiandaa kuondoka naye.



    Safina na Shida walipokuwa katika harakati za kwenda kituoni, ni hapo gafla Safina akawaona ndugu wawili wa baba yake kwa mbali.

    SAFINA: Shida tujifiche sitaki wale wanione.

    SHIDA: Kwanini Safina?

    SAFINA: Siwataki wale ni ndugu wa baba nawachukia sana.

    SHIDA: Ila si ndugu zako?

    SAFINA: Ndio, yule mwanamke ni shangazi Modesta na yule mwanaume ni bamkubwa Jese. Sitaki kabisa wanione.

    Basi Safina na Shida wakajificha hadi pale Modesta na Jese walipopita ndipo Safina na Shida wakatoka na kuendelea na safari.

    MODESTA: Kwakweli kaka sijafurahishwa kabisa na vitendo vyenu, na sitachoka kumtafuta Safina hata kama itapita miaka kumi.

    JESE: Tatizo lako Mode huna kazi za kufanya, yani wewe kila mwaka habari ni Safina Safina kama wimbo wa Taifa vile. Hata Nuhu alitengeneza safina kama vipi na wewe tengeneza yako.

    MODESTA: Nyie kweli mmevurugwa jamani. Ila siku zote nitawakumbusha hili kwamba jasho la mtu haliendi bure.

    JESE: Nimegundua kwanini wewe Mode hupatani na Aisha, kumbe ndio unaakili mbovu kiasi hicho loh!! Achana na mtoto wa Sam, mwache ahenye aone dunia ilivyo.

    MODESTA: Hivi ungekuwa wewe ndio umefanyiwa hivyo ungejisikiaje?

    JESE: Ushasema ingekuwa, kwahiyo fanya mambo yako, yangu niachie mwenyewe.

    Roho ya Modesta ilikuwa inamuuma sana juu ya upotevu wa Safina, amakweli si wote wabaya kwenye ukoo.

    Mara gafla Modesta akageuka nyuma na kwakweli akamuona mtu kama Safina, akamuangalia kwa makini na kuhakikisha kuwa ni yeye, Safina alipogundua kaonekana akageuka nyuma, ndipo Modesta akaanza kuita "Safina, Safina"

    Safina hakugeuka kumuangalia tena bali alianza kutimua mbio huku Shida akimfata kwa nyuma.

    Walipofika mahali wakapumzika.

    SAFINA: Nilikwambia Shida wale si watu wazuri.

    SHIDA: Huwezi jua, labda hakuwa na lengo baya.

    SAFINA: Huwajui ndiomana, haya tuendelee tu na safari yetu ya huko kituoni.

    Modesta aliumia sana moyo kwahiyo akaamua kwenda kwa kaka yake Peter.

    MODESTA: Kaka usiku wa jana nimemuota Latifa.

    PETER: Sasa mimi nifanyeje?

    MODESTA: Kaka tafadhari, nisaidie kumtafuta Safina. Tafadhari simama nami kwenye kumtetea Safina.

    PETER: Nilishindwa kumtetea wakati anafukuzwa na mke wa kaka sembuse sasa? Ila alitia huruma sana.

    MODESTA: Kaka, kumbuka hakuna kibaya tulichotendwa na Sam wala Latifa. Tumuhurumie mtoto wao basi

    PETER: Kweli huruma inanijia, ila inawezekana Safina ameshakufa sababu ni muda mrefu sasa.

    MODESTA: Natambua hilo ila Safina yu hai. Naomba tukimpata uwe nami katika kumtetea, nakuomba kaka yangu. Kwakweli sina amani wala raha kwa miaka yote hii naumia tu juu ya Safina.

    PETER: Umejuaje kama yu hai?

    MODESTA: Nimemuona mjini akiwa kachakaa sana dah!! Namuhurumia Safina kwakweli.

    Peter akajikuta naye akimuhurumia Safina ingawa ni muda mrefu umepita hata alikosa matumaini kuwa Safina yu hai, lakini kwavile Modesta alimuhakikishia kuwa Safina yu hai kwahiyo akaamini hivyo.



    Yule kamanda na Musa walipokuwa wanatoka pale kituoni, kufika nje tu mara Safina na Shida nao wakafika mahari pale. Musa alipomuona Safina alimkimbiria kwa furaha na kumkumbatia, lakini yule kamanda hakuelewa kinachoendelea basi Musa akawaelezea wenzake kuwa kuna kamanda amejitolea akaishi kwake. Basi akawavuta Safina na Shida ili nao waweze kusalimianda na yule kamanda na labda na wao wamuombe kuishi kwake.

    Ila kitendo cha Safina kumuona yule kamanda kikazua taswira mpya, kwani Safina alishtuka sana kumuona mtu huyo kwani hakumtarajia kabisa.



    Kitendo cha Safina kumuona kamanda huyo kilizua taswira mpya, kwani Safina alishtuka sana kumuona mtu huyo ambaye hakumtarajia kabisa.

    Safina akamuita yule kamanda, kitendo kilichowashangaza wote kuwa Safina anamjua yule kamanda.

    SAFINA: Bamdogo Frank!!

    Yule kamanda akashtuka sana kwani hakutarajia kama anafahamiana na binti huyo.

    Ilikuwa ni ngumu kwa Frank kumtambua Safina kwani alimuacha akiwa mdogo sana na sasa amekua ila amechakaa sana.

    FRANK: Umenijuaje?

    SAFINA: Nakujua, wewe si ndiye mchumba wa mamdogo Suzy?

    FRANK: Kwani wewe ni nani?

    SAFINA: Mimi ni Safina, mtoto wa Sam na Latifa.

    FRANK: Ooh!! My God, yani wewe ndiye yule mtoto uliyekuwa unaimbaimba vizuri!! Dah, nini kimekupata Safina?

    SAFINA: Ni historia ndefu.

    FRANK: Ok, twendeni mkapande gari niwapeleke kwangu.

    Wote wakaenda kupanda gari ya Frank na kwenda nyumbani kwake.



    Walipofika nyumbani kwa kamanda Frank, ikabidi kamanda huyo amuulize vizuri Safina kwani hali ya Safina ilimshangaza sana.

    FRANK: Safina hebu nielezee kilichokupata.

    SAFINA: Baba na mama walikufa (huku akilia).

    FRANK: Dah!! Pole sana Safina, inamaana Sam na Latifa walikufa?? Mmh hebu nieleze vizuri Safina.

    Safina akamueleza kila kitu kilichomtokea hadi kuwa na maisha aliyokuwa nayo sasa, maisha ya mtaani. Alimueleza yote hayo huku machozi mengi yakimbubujika.

    FRANK: nyamaza Safina, hii ni hali ya dunia ila siku moja itaisha.

    SAFINA: Sijui hiyo siku moja itakuwa lini? Miaka inakuja na kupita nikiwa natangatanga mitaani. Safina mimi wa leo si Safina yule aliyeweza kuonekana nchi za ulaya akionyesha vipaji vyake, Safina wa sasa ana kipaji cha ombaomba na kula majalalani.

    FRANK: Safina usijari, ilimradi mimi nipo hautakula tena majalalani. Sawa mama!!

    SAFINA: Nashukuru sana bamdogo, kwani mamdogo Suzy yuko wapi?

    FRANK: Sijaonana naye kwa kipindi kirefu sana na hata sijui anaishi wapi?

    SAFINA: Kwani umeachana na mamdogo?

    FRANK: Hapana, sijaachana nae, ni maisha tu ndio yakanitenga nae.

    SAFINA: Sasa mbona hujui aliko?

    FRANK: Nilisafiri, nikaenda India kimasomo. Tangu kipindi hiko mawasiliano na Suzy yakakatika na niliporudi sikujua Suzy anaishi wapi hadi leo hii sijui.

    SAFINA: Je, ulijaribu kumtafuta?

    FRANK: Ndio nilimtafuta, maana nilipoenda kwenu nikadhani labda nitamkuta Sam nimuulize ila nilikuta sura ngeni na wakaniambia kuwa Sam haishi pale.

    SAFINA: Inamaana shangazi kauza nyumba yetu?

    FRANK: Usijari Safina, jipe moyo utashinda.

    Safina akaongea mambo mengi sana na kamanda Frank, naye Frank akawaambia Safina, Musa na Shida kuwa amejitolea kuwalea kwahiyo wataishi hapo nyumbani kwake huku akiwa na lake moyoni kuhusu Musa.

    FRANK: Ningependa wote mniite baba, sawa eeh!!

    WOTE: Sawa tumekuelewa.

    Kwahiyo Frank akaishi nao hapo kama watoto wake.



    Sikumoja Modesta akiwa katika pita pita zake akakutana na Suzan, akaamua kumuita.

    MODESTA: Suzy jamani za miaka??

    SUZAN: Hata nikikwambia wewe itakusaidia nini?

    MODESTA: Sisi ni ndugu Suzy.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    SUZAN: Undugu wa mimi na nyie ulikufa pale dada yangu alipoingia kaburini.

    MODESTA: Najua una hasira Suzy, ila jaribu kunielewa. Nia yangu ya kukuongelesha ni Safina.

    SUZAN: (Kusikia habari ya Safina, ikabidi awe mpole), eeh Safina kafanyaje tena?

    MODESTA: Kuna siku nilimuona Safina mjini, kwahiyo inamaanisha Safina yupo. Ni bora tukasaidiana kumtafuta ili mtoto asitangetange.

    SUZAN: Hapo umeongea la maana sasa, eeh unafikiri tufanyaje?

    MODESTA: Suzan hakuna namna zaidi ya kumtafuta tu. Kama tungekuwa na pesa labda tungemtangaza. Basi nipe namba yako ya simu ili tuwasiliane.

    SUZAN: Mweeeh!! Hata hiyo simu ninayo basi!! Niliona inanitia gharama ya vocha tu bila umuhimu wowote kwahiyo nikaiuza. Labda wewe unipe yako.

    MODESTA: Nadhani hapa tumekutana majanga matupu sababu hata mimi sina simu.

    Ikabidi Suzan amuelekeze Modesta sehemu anayofanyia kazi ili kama akipata taarifa yoyote afike kumwambia.

    Kama kawaida ya Modesta akaenda tena kwa kaka yake mkubwa kumlalamikia.

    MODESTA: Hivi kaka roho yako haikuumi kabisa kuhusu Safina??

    JUTA: Ila wewe Mode sijui akili yako ikoje? Unataka kufufua mambo yaliyopita na kusahaulika kabisa kama yalikuwepo.

    MODESTA: Hata kama mud mrefu umepita kaka, wakati bado upo. Safina atafutwe na mmuombe msamaha.

    JUTA: Kweli wewe ulikosea kuzaliwa jamani, mbona akili yako haina akili Mode, yani mimi na akili zangu timamu nianze kumtafuta Safina?? Hebu kafie mbele huko wewe na huyo Safina wako.

    MODESTA: Najua mnaniona mimi kama chizi sasa ila ipo siku mtayakumbuka maneno yangu. Kama kufa nitakufa tu, wangapi wameshakufa sembuse mimi!!

    JUTA: Tatizo mdogo wangu hujielewi wewe.

    MODESTA: Kaka unajua wazi mkeo ana roho mbaya, alinifukuza mimi hadi Safina kamfukuza.

    JUTA: Nitolee mashetani yako hapa kwangu, kama umekosa ya kusema naomba uende. Na utakufa masikini wewe.

    MODESTA: Ndio nitakufa masikini lakini masikini shujaa, mtu nisiyechoka kupambana na maisha yangu mwenyewe sio kupambana na mali za watu.

    JUTA: Nenda bhana, umewehuka wewe sio bure.

    MODESTA: Naenda ndio ila siku zote nitaendelea kulilia haki ya Safina.

    Roho ya Modesta ilikuwa inamuuma sana kila akifikiria mambo mema aliyofanyiwa na Sam na Latifa.

    Akaondoka huku akijisemea "sitachoka na sichoki mpaka pale haki itakapotendeka juu ya Safina".

    Wakati anawaza hayo, mbele yake akamuona Latifa amesimama na mara gafla akampungia mkono na kupotea, kwakweli Modesta alihisi kama kuwehuka na hisia kubwa ikamjaa kuwa kaka zake wanahusika vilivyo na kifo cha Sam na Latifa, lakini akajiuliza kuwa hata kama angefungua mashtaka ya mauaji angewashtaki vipi wakati watu hao wameuwawa kishirikina na kikubwa zaidi ni kuwa serikali haiamini ushirikina. Imani ya Modesta inamuachia Mungu hiyo kesi ya kishirikina ila bado anajitolea kupambana na haki ya Safina, huruma kubwa inamjaa akikumbuka pale njiani alipomuona Safina na jinsi alivyopauka, moyo wake unazidi kumtuma tu kuwa anapaswa amsaidie Safina.



    Siku moja Kamanda Frank alishika picha ya Suzan akawa anaiangalia na kujiuliza kimoyomoyo,

    "hivi Suzy uko wapi jamani? Hata sijui nianzie wapi kukutafuta. Mawazo mengi yananisonga, natumai uwepo wako ungenisaidia kuyatatua"

    Mara Safina alienda pale alipokaa Frank, na kumkuta na picha ya Suzan mkononi.

    SAFINA: Ni picha ya mamdogo Suzy hiyo?

    FRANK: Ndio ni wewe, nilikuwa nawaza hapa pakuanzia kumtafuta.

    SAFINA: Hebu niione.

    Kamanda Frank akampa Safina ile picha, wakati Safina anaiangalia mara Musa na Shida wakasogea eneo lile. Na Musa nae akajiunga na Safina kuitazama.

    MUSA: Mmmh!!

    SAFINA: Mbona unaguna Musa?

    MUSA: Huyu dada kama namjua?

    SHIDA: Dada gani huyo?

    Wakampa picha na Shida nae akaitazama.

    SHIDA: Hata mimi namjua.

    Frank kusikia vile akashtuka,

    FRANK: Mmemjuaje?

    SHIDA: Mimi nilimuona hospitali, na wewe Musa je?

    MUSA: Hata mimi nilimuona hukohuko hospitali.

    FRANK: Hospital gani? Na anafanya nini?

    MUSA: Huyu dada yupo mapokezi kwenye ile hospitali aliyolazwa Safina.

    FRANK: Kweli?? Basi kesho twendeni tukamuangalie, pengine ni yeye.

    Safina alibaki na mshangao tu kwani yeye hakubahatika kumuona huyo dada.



    Kesho yake Suzan akiwa pale kazini mara kuna mtu akamfata huku akiwa na haraka nyingi sana ilionyesha sehemu anayopelekwa kulikuwa na tukio la hatari limetokea.

    Hakuweza kuendelea kubaki eneo hilo bali alienda kuchukua ruhusa haraka haraka na kuaga. Kwahiyo akaondoka na huyo mtu aliyemuita.



    Kesho yake Suzan akiwa pale kazini mara kuna mtu akamfata huku akiwa na haraka nyingi sana ilionyesha sehemu aliyopelekwa kulikuwa na tukio la hatari sana.

    Hakuweza kubakia hapo kazini bali alienda kuchukua ruhusa na kuondoka haraka haraka pamoja na yule mtu aliyemuita.

    Pendo alipofika pale hospitali nae alishangaa kumkosa Suzan mahali pale kwani siku hiyo aliwahi kufika. Alipouliza akaambiwa kuwa Suzan ameomba ruhusa kuwa kuna mahali anaenda mara moja.

    Hakujua kwakweli mahali alipoenda Suzan.



    Kamanda Frank kama alivyopanga jana yake, ikabidi aondoke na wakina Musa ili waweze kumuulizia Suzan kwenye hospital ambayo walisema kuwa wamemuona.

    Walipofika pale hospitali ikabidi amtume Musa ili aende kumuulizia na kumuita.

    Musa akaingia pale hospitali, akakuta mapokezi kuna wadada wawili wamekaa wanaongea.

    Ikabidi awafate na kuwasalimia, kisha akawauliza.

    MUSA: Samahani, namuulizia yule dada wa mapokezi.

    PENDO: Nani huyo? Suzy au?

    MUSA: Ndio ni dada Suzy.

    PENDO: Ooh!! Ametoka, kwani unataka nini?

    MUSA: Kuna mgeni wake pale nje anamwita.

    PENDO: Nipeleke nikaongee naye.

    ZENA: Loh!! Pendo kwa umbea sikuwezi.

    PENDO: Ushaanza maneno yako na wewe loh, hebu nipeleke mwaya.

    Basi Musa akaongozana na Pendo hadi alipo Frank kwani alitoka nje ya gari na akawa amesimama chini ya mti.

    FRANK: Habari yako!!

    PENDO: Nzuri tu ila Suzy ametoka ila mimi ni rafiki yake, niambie tu shida yako pengine naweza nikakusaidia.

    FRANK: Hivi wewe sio Pendo kweli?

    PENDO: Ndio mimi ni Pendo, kwani wewe nani?

    FRANK: Yani Pendo umenisahau Frank!! Dah!

    PENDO: Frank?? Aaah!! Kumbe wewe ni Frank jamani. Dah ulinipotea kabisa.

    Wote wakakumbukana na kukumbatiana.

    PENDO: Umebadilika sana Frank hata sikukutambua. Uko wapi siku hizi?

    FRANK: Nipo tu kwani masomo nishamaliza kitambo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Basi Pendo na Frank wakaongea mengi sana kwani ni kipindi kirefu tangu waonane.

    FRANK: Inamaana Pendo upo hapa na Suzy?

    PENDO: Kwanza umejuaje kuwa Suzy yupo hapa?

    FRANK: Ni stori ndefu, kwani yuko wapi?

    PENDO: Si nimekwambia kuwa ametoka!!

    FRANK: Sawa, kwani unamjua Safina mtoto wa Latifa?

    PENDO: Nilimuona kwenye picha tu.

    FRANK: Basi ngoja.

    Kamanda Frank akaenda kuwaita wakina Safina, Pendo alipomuona Safina alishangaa sana.

    PENDO: Huyu ndie Safina?

    FRANK: Ndio ni huyo.

    PENDO: Ooh!! Jamani nilikuwa namuhudumia hapa bila hata kumjua, pole sana Safina, na vipi unaendeleaje?

    SAFINA: Naendelea vizuri, asante.

    PENDO: Frank, umempata wapi huyu?

    FRANK: Ni stori ndefu.

    PENDO: Mmh nawe umezidi sasa kila kitu ni stori ndefu tu.

    FRANK: Na wewe kwa kupenda umbea, huachi tu tabia yako ya shule?

    PENDO: Hahaha, ila bora Safina kapatikana maana Suzy alikosa raha kabisa.

    Basi Pendo akaenda kuomba ruhusa ili awapeleke wakina Frank mahali anapoishi yeye na Suzy, aliporuhusiwa akawapeleka.

    PENDO: Hapa ndio tunapoishi.

    FRANK: Kwahiyo na Suzy anaishi hapa?

    PENDO: Ndio tunaishi wote.

    FRANK: Aah!! Hamuachani nyie yani hadi leo mko wote.

    PENDO: Urafiki wangu na Suzy ni wa kudumu.

    Basi wakaongea mengi, ikabidi Frank ampe Pendo ramani ya kumuelekeza nyumbani kwake ili aweze kufika na Suzy.

    Hadi muda wanaondoka, Suzy alikuwa bado hajafika nyumbani.



    Suzan akiwa na yule mtu aliyempeleka, mara akamuona Modesta akiwa mbele yake.

    SUZAN: Khee!! Vipi tena Mode nini kimekupata?

    MODESTA: Huwezi amini Suzy, nimemuona Latifa kabisa kwa mcho yangu ndiomana nikamtuma mtu akufate ili nawe umuone.

    SUZAN: (Akiangalia huku na kule), mbona hayupo?

    MODESTA: Ametoweka ila alikuwa hapa, nimemuona kabisa Suzy.

    SUZAN: Mbona makubwa haya, miaka yote hii bado dada anatokea.?

    MODESTA: Hawezi kuacha mpaka pale mtoto wake atakapopewa haki anayostahili.

    Mara Modesta akaanguka eneo hilo, ikabidi Suzan amuinue hata kushangaa ni kipi kimemuangusha.

    SUZAN: Pole jamani Modesta, kwani ni nini kimekuangusha?

    MODESTA: Sijui ila hisia zangu zinanituma kuwa kuna nguvu mbili zinavutana Suzy.

    SUZAN: Kivipi Mode!

    MODESTA: Kwasasa sijui ila ipo siku nitajua tu.

    Ikabidi Suzan amsindikize Modesta hadi nyumbani kwake anapoishi.

    MODESTA: Suzy tafadhari, ukimpata Safina kuwa nae makini sana. Nahofia wasije wakamtenda vibaya.

    SUZAN: Sawa Mode, nimekuelewa. Ila hata sijui nimkinge vipi?

    MODESTA: Kuna mambo mengi yanacheza kwenye ulimwengu tusioweza kuuona kwa macho yetu cha muhimu ni kwamba kuwa makini na Safina ukimpata, maadui ni wengi sana.

    SUZAN: Nakuahidi Modesta, nitajitahidi kwa hilo.

    Suzan akamuaga Modesta na kuanza kurudi mahali anapoishi.



    Suzan alipofika nyumbani, akamkuta Pendo yupo kwenye harakati za kurudi tena kazini.

    PENDO: Suzy leo kuna ugeni tuliupata.

    SUZAN: Ugeni gani huo?

    PENDO: Ni Frank na Safina ila nitakwambia vizuri nikirudi.

    Pendo akaondoka na kumuacha Suzan akiwa kwenye lindi la mawazo.

    "mmmh!! Mbona sielewi, Frank na Safina? Frank yupi na Safina yupi? Mbona Pendo kaniacha njia panda. Lakini leo anawahi kurudi nitamsubiri hadi arudi ili aniambie hata hivyo kesho ni siku yetu ya mapumziko."

    Suzan alikuwa na hamu kweli ya kujua kuhusu huo ugeni, kwahiyo akamsubiri Pendo ili aongee nae ingawa alichoka sana siku hiyo.

    Pendo aliporudi akamueleza vizuri Suzan na akamwonyesha ramani ya kwenda nyumbani kwa Frank.

    PENDO: Basi kesho twende pamoja huko kwa Frank.

    PENDO: Usijari, kesho tutaenda pamoja kwani ni siku yetu ya mapumziko.

    SUZAN: Nitafurahi sana nitakapomuona Safina.

    PENDO: Na Frank je?

    SUZAN: Nitafurahi pia.

    PENDO: Nilitaka nishangae, usimfurahie kipenzi chako tena.

    SUZAN: Mmh na wewe Pendo loh!!

    Wakajadili na kujipanga vyema kwenda kwa huyo Frank.



    Basi kesho yake Pendo na Suzan wakajiandaa na safari ya kwenda kwa Frank ikaanza.

    Walipokaribia kufika ikabidi waulizie vizuri, wakampata kijana mmoja wa kumuuliza.

    PENDO: Samahani, tunaulizia nyumba ya mtu mmoja anaitwa Frank iko mtaa huu.

    KIJANA: mnaulizia kwa kamanda Frank?

    SUZAN: Kamanda? Mmh!! Pengine ndio huyo huyo.

    Basi yule mtu akawaelekeza nyumbani kwa Frank, wakamshukuru na safari ikaendelea huku wakisemezana.

    SUZAN: Inamaana siku hizi Frank kawa kamanda?

    PENDO: Labda, maisha hubadilika Suzy.

    Walipofika, wakagonga mlango na kufunguliwa na Shida ambaye aliwakaribisha hadi ndani.

    Mara Frank akatoka na kuwakuta, kwakweli Frank alifurahi sana kumuona Suzan, alimsalimia na kuongea ya hapa na pale.

    Wote walifurahi pamoja na Pendo.

    SUZAN: Jamani nataka kumuona na Safina sasa, yuko wapi eti Frank!

    FRANK: Kuna muda alitoka na Musa, sijui hawajarudi. Ngoja niwaulizie.

    Kabla Frank hajainuka kwenda kuuliza, mara Musa akaingia ndani huku jasho jingi likimtoka.

    FRANK: Musa vipi? Kuna nini?

    MUSA: (Huku akihema sana) ni Safina.

    FRANK: Safina kafanyaje?

    MUSA: Safina kapata ajali.

    WOTE: Nini?

    MUSA: Safina kagongwa na gari na sasa yupo hospitali.

    Suzan alikaa chini, miguu yote iliishiwa nguvu kabisa kwani hakuelewa chochote wakati huo, ni Pendo tu ndiye aliyekuwa akimtuliza.



    Suzan alikaa chini miguu yote iliishiwa nguvu kabisa kwani hakuelewa chochote wakati huo. Ni Pendo tu ndiye aliyekuwa akimtuliza.

    Suzan aliwaza mengi sana, akaikumbuka na kauli ya Modesta kuwa amlinde Safina.

    Frank akamwambia Musa awapeleke huko hospitali, kwahiyo wakapanda kwenye gari lake hadi hospitali alipolazwa Safina.

    Walipofika pale wakaulizia kwa daktari ili waweze kumuona.

    DAKTARI: Sitaweza kuwaruhusu mkamuone kwa sasa, maana hali yake ni mbaya na bado tunamshughulikia.

    SUZAN: Dokta, atapona kweli?http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    DAKTARI: Msijari yote ni mapenzi ya Mungu.

    Daktari alivyosema hivyo Suzan akajikuta machozi yakimtoka, Pendo akaendelea kumbembeleza tu.

    Frank akaanza kumuhoji Musa maswali.

    FRANK: Musa, kwani ilikuwaje?

    MUSA: Tulikuwa tunavuka barabara, mi nilikuwa mbele ya Safina na nyuma gafla nikasikia amegongwa. Ila yule dereva alishuka harana na tukasaidiana kumpakiza kwenye gari na kumleta hapa hospitali.

    FRANK: Huyo dereva yuko wapi?

    MUSA: Sijui labda uwaulize madaktari.

    Frank akaenda kuwauliza madaktari na wakamuonyesha alipokaa dereva.

    FRANK: Hivi kwanini unakosa umakini barabarani hadi unasababisha ajali?

    DEREVA: Haikuwa kusudio langu kaka hata mi mwenyewe nimeshangaa nimeshagonga.

    FRANK: Sasa nakwambia omba sana Mungu mgonjwa apone kwani asipopona utaozea segerea.

    DEREVA: kweli kaka sikudhamiria.

    Mara Frank akapiga simu kituo cha polisi ili waje wamkamate yule dereva, na walipofika hawakutaka maelezo mengi zaidi ya kumkamata tu.

    Hali ya Safina iliwakosesha raha kwakweli na kujiuliza maswali mengi sana kuwa kwanini iwe vile ilivyokuwa.

    Wote walimuombea Safina apone ili waweze kwenda nae sambamba.

    Suzan alijikuta safari ya kumuona Safina hapo hospitali imepamba moto kiasi kwamba alibakiza kiasi kidogo tu kufukuzwa kazi, alitamani hata Safina ahamishiwe hospitali anayofanyia kazi ili awe anamuona kila mara.



    Safina alikaa miezi miwili hospitali kwenye chumba cha pekee na uangalizi mkubwa sana.

    Suzan alienda kwa Modesta kupata ushauri ila alimkuta Modesta akiumwa umwa.

    SUZAN: Mode, Safina amepatikana ila amepata ajali mbaya sana na mwezi huu ni wapili sasa yupo hospitali.

    MODESTA: Suzy cha muhimu ni kumuombea tu apone, naimani Mungu atamsaidia Safina.

    SUZAN: Na wewe vipi hali yako mbona haieleweki?

    MODESTA: Naumwa Suzy tangu kipindi kile uliponiacha.

    Mara Aisha dada wa Modesta akafika mahali hapo. Akashangaa sana kumkuta Suzy akiwa hapo.

    AISHA: Kheee kwani undugu bado unaendelea kati yenu?

    MODESTA: Kwanini usiendelee?

    AISHA: Ila wewe Suzy unapenda sana kujipendekeza.

    SUZAN: Sijipendekezi bali hata mimi naijali afya ya Modesta.

    AISHA: Hahaha, mwenzio Mode hapa ana ukimwi ndo mana kanyorodoka ila haya mambo ya kifamilia kwahiyo wewe Suzy hayakuhusu.

    Kwavile lililompeleka pale lilikuwa limeisha ikabidi Suzy aage na kuondoka.

    Akabakia Modesta na Aisha mahali hapo.

    AISHA: Sikia mode, kuna nyumba moja ya marehemu Sam imeshindikana kabisa kuuza, sasa kaka akasema itakuwa sababu ya mdomo wako, hebu tupe baraka wenzio ili na wewe ung'arishe maisha yako.

    MODESTA: Dada nilishakwambia, na tena nakwambia sitaki kugombania mali za marehemu, nyie endeleeni tu.

    AISHA: Yani mdogo wangu maradhi yote hayo yanayokusumbua bado hutaki msaada?

    MODESTA: Kama kusaidiwa basi nisaidiwe kivingine na si kwa kudhurumu mali ya marehemu ipo siku itawarudi tu.

    AISHA: Kweli mdogo wangu umevurugwa jamani, pole sana.

    Swala la kushindikana kuuzwa kwa hiyo nyumba kiliwapa mashaka sana ndiomana wakaweka wapangaji wao huku wakitafuta namna ya kuiuza nyumba hiyo.



    Hali ya Safina ikaanza kubadilika hadi akawa na hali nzuri na kuweza kuruhusiwa kurudi nyumbani.

    Ndipo na yule dereva aliyewekwa rumande na Frank akaruhusiwa kutoka.

    Walimshangaa sana wenzie alivyokonda, akawa anajisemea,

    "na kazi ya udereva siitaki tena kwani nimekaa rumande bila hata kusomewa mashtaka."

    RAFIKI: Umekonda sana John.

    JOHN: Jela si mchezo na ukizingatia sijazoea kabisa.

    RAFIKI: Pole sana ndio mambo ya ajali hayo.

    JOHN: Ndio hivyo wangu, siku zote ajali ikitokea dereva ndio unaonekana mwenye makosa dah!! Hata kama chanzo ni aliyegongwa.

    RAFIKI: Ndio maisha hayo.

    JOHN: Nashukuru Mungu amepona na mimi nimeweza kuwa huru.

    kwakweli yule dereva siku zote alijiuliza chanzo cha ile ajali ni nini kwani hakuelewa kabisa zaidi ya kujikuta kashaponga tayari.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Safina akiwa amerudishwa pale nyumbani kwa Frank, Suzan akawa anaenda kila siku kumuangalia Safina.

    SUZAN: Unaendeleaje mama?

    SAFINA: Naendelea vizuri mamdogo saivi nimepona, si unaona nimeanza hata kutembea!

    SUZAN: Kweli umepona mwanangu.

    SAFINA: Hivi mamdogo kwanini usije kuishi hapa na bamdogo?

    SUZAN: unapenda nije kuishi hapa?

    FRANK: (Akadakia), ndio napenda tuishi pamoja Suzy, Safina endelea kumshawishi mamako mdogo akubali na sisi tufurahi.

    Suzy akatafakari na kuona bora tu afanye maamuzi ya kuishi hapo.

    Kwahiyo baada ya wiki Suzy akahamia mahali hapo, huku akiendelea kumpa Safina mazoezi ya hapa na pale mpaka pale ili aweze kutengemaa.

    Ilimchukua muda kurudi katika hali ya kawaida, ila Mungu alimsaidia Safina na kujikuta amepona kabisa.







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog