Sehemu Ya Pili (2)
Nilipokuwa nimelala nikamuona mama Salome akivuka barabara mara kuna gari ilikuwa ikimfata kwa kasi sana kisha ikamgonga, kumuangalia dereva ni yule mkaka wa ndotoni ila gari ilifanana na ile ambayo Carlos huwa anaiendesha kisha yule mkaka akaniangalia na kutabasamu, nikawa nimesimama na kushikwa na bumbuwazi kisha watu wakajaa pale alipogongwa mama Salome na yule mkaka akashuka kwenye ile gari ila akawa na sura nyingine kabisa si ile ya ndotoni wala Carlos nikawa nashangaa tu na sikuweza kusogea eneo la tukio, nikiwa nashangaa yule mkaka aliyegonga akageuka kwangu na kuanza kunifata kisha akanishika bega na mara sura yake ikageuka na kuwa yule mkaka wa ndotoni halafu akatabasamu na kuanza kunitingisha hapo ndipo niliposhtuka vibaya sana kwani nilihisi kuna mtu ananitingisha kweli. Nikaamka na kukuta ni dada Penina anayenitingisha nikaropoka palepale.
"Mama Salome kapata ajali"
Dada akawa ananishangaa kwa kile nilichokisema.
"Unamatatizo gani wewe Sabrina?"
Nikamuangalia tu dada yangu Penina kwani sikujielewa na ile ndoto, dada akaendelea kuongea.
"Nimekuja kukuamsha maana umelala sana hadi unaanza kuwaotea watu mambo mabaya. Haya amka hapo twende kufanya kazi."
Nikainuka huku nikijisemea mwenyewe kuwa ndio tabu ya dada asipoenda kazini anapenda kumshurutisha mtu tu.
Nikamkuta mama sebleni, nikamsalimia na kwenda jikoni alipo dada halafu mama nae akatufata jikoni mara mlango ukagongwa halafu akaingia mkaka flani ambaye ni ndugu wa mama Salome, alifika akiwa anahema sana tena bila salamu akasema.
"Mama Salome amepata ajali"
Dada Penina aliyekuwa anapanga vyombe aliacha na kunitazama kisha nami nikamtazama halafu akasema.
"Umeona sasa Sabrina?"
Mama akatushangaa na kuuliza,
"Kuona nini tena?"
Sikujibu chochote bali niliwaacha na kwenda chumbani kwangu huku maswali mengi yakinitawala, nilijikuta nikisema "Mungu wangu msaidie mama Salome asife"
Nilikosa amani kwani nilijihisi mkosaji na nilijiona kamavile mimi ndio chanzo cha yote.
Mama alienda alipoambiwa kuhusu mama Salome kisha dada akaja chumbani kwangu na kuniuliza.
"Ulikuwa na maana gani uliponiambia asubuhi kuwa mama Salome kapata ajali na halafu ni kweli? Je unajua chanzo cha ajali yake?" "Sijui chochote dada"
"Kuwa makini na maneno yako Sabrina"
Kisha akainuka na kutoka chumbani kwangu, maneno ya dada nayo yalikuwa yakinichanganya tu kwani sikumuelewa ni umakini gani anaouongelea.
Nikiwa bado nimetulia chumbani, simu yangu ikaita kuangalia ni Suzy anapiga ila sikupokea, mara akanitumia ujumbe mfupi, "Niko njiani na Lucy tunakuja kwenu"
Pia sikujibu huo ujumbe, nikaangalia tu na kuupuuzia kisha nikaendelea na mawazo yangu mara nikasikia sauti ya mama akiita kwa nguvu sana.
"Wee Sabrina wee"
Ikabidi nitoke na kwenda kumsikiliza.
"Jiandae haraka haraka twende hospitali kumuona mama Salome huko maana njia nzima anakutaja wewe."
Ikabidi nijiandae bila kuuliza chochote na kuanza kuongozana na mama kwa safari ya kwenda huko hospitali aliposema.
Tukiwa njiani kuelekea hospitali ilipita gari ya Carlos na kutupa lifti kama kawaida yake, akatupeleka hadi hospitali alipolazwa mama Salome. Kwakweli hali ya mama Salome ilikuwa mbaya sana ila bado alihitaji kuzungumza na mimi, nikamsogelea karibu kisha nikainama kumsikiliza naye akaongea kwa shida sana sababu ya maumivu.
"Mapambano ni makali sana mwanangu unatakiwa....." Akaanza kupiga makelele kwa maumivu, daktari akaja na kutuamuru kuwa tutoke nje ili wamuhudumie. Bado nilijiona kuwa mimi ndio chanzo cha mambo yote, mama akaniambia. "Usiwaze sana mwanangu hii ni mipango ya Mungu tu na huwezi jua kwanini imekuwa hivi. Je mama Salome alikuwa anakwambia nini?"
"Kaniambia kuwa mapambano ni makali sana, kwakweli mama mi naogopa jamani hata sielewi kitu" "Usijari mwanangu yote haya yataisha"
Wakati naongea na mama pale akatufata Carlos na kudai kuwa ana mazungumzo nami kidogo. Nikamfata kwenda kumsikiliza.
"Kwakweli Sabrina una matatizo na unahitaji msaada wa hali ya juu"
"Ni kweli nina matatizo ila wewe umejuaje?"
"Nimejua tu Sabrina, na kama utahitaji msaada wangu basi usisite kuniambia"
Mara akaja Salome yani mtoto wa mama Salome kisha akatusalimia pale na hapo hapo Carlos nae akaaga na kuondoka kisha Salome akaanza kuniuliza.
"Huyu mkaka aliyetoka hapa ni nani yako?"
"Ni rafiki yangu tu dada"
"Unamjua vizuri?"
"Kiasi tu dada, kwani vipi?"
"Mmmh!?" "Mbona unaguna dada?"
"Hamna kitu mdogo wangu ila simuamini kwakweli"
"Kwanini humuamini dada?"
Mara mama akaja kuniita na kuniambia kuwa twende tukamuage mama Salome na kurudi nyumbani.
Tukaongozana na mama hadi kwenye wodi aliyolazwa mama Salome, kufika mlango nesi akatuzuia kuingia.
"Jamani ustaarabu ni kitu muhimu sana, muda wa kuona wagonjwa umeisha na kama muonavyo hakuna hata mtu mmoja wa kuona wagonjwa wodini, naomba muende na mrudi tena kesho"
Mama akajaribu kujitetea ili waturuhusu.
"Tunataka kumuaga tu mgonjwa wetu, tafadhari nesi"
"Hata kama, muda wa kuona wagonjwa umeisha, mimi nafata taratibu za kazi tafadhari naomba muende"
Ikabidi tukubaliane na nesi na kuanza kuondoka, tulipokaribia kutoka nje kabisa ya hospitali tukamsikia yule nesi akituita kwa nguvu, tukasimama na kisha akauliza.
"Kuna Sabrina kati yenu hapo?"
Nikaitika, ndio mimi hapa.
"Samahani, mgonjwa anaomba kuzungumza na wewe kidogo" Mama akauliza,
"Si ulisema muda umeisha wewe! Vipi tena?"
"Aah! Samahani mama, hii ni kwa taadhari tu."
Ikabidi niongozane na mama ambaye aliishia nje ya wodi akiongea na yule nesi na kuniacha mimi niingie mwenyewe wodini. Nikaingia na kwenda hadi alipo mama Salome ila kufika pale nilishtuka sana na kuanza kupiga makelele kwa uoga.
Nikaingia na kwenda hadi alipo mama Salome ila kufika pale nilishtuka sana na kuanza kupiga makelele kwa uoga kwani nilimuona yule mkaka wa ndotoni amesimama karibu na kitanda cha mama Salome halafu akaanza kunifata huku sura yake ikiwa inatisha sana leo.
Kelele zile zilimshtua kila mtu aliyekuwepo eneo lile kiasi kwamba kila mmoja alishtushwa na kuanza kuja eneo la tukio ila mimi nilikuwa nakimbia na kutoka wodini kama vile chizi.
Mama akanidaka mlangoni, jasho jingi lilinitoka na kuanguka palepale aliponidaka mama na kuzimia.
Nilipozinduka nilijikuta nikiwa kwenye chumba cha daktari na mama, ambapo mama aliandikiwa dawa ambazo nilitakiwa niende kuzitumia nyumbani kisha mama akanishika mkono na kuanza kuondoka eneo lile la hospitali.
Kufika nyumbani, mama akaanza kumuhadithia dada Penina mambo yaliyojiri hospitali.
"Mwenzangu, mdogo wako leo ule uchizi wake si umemuanzia hospitali loh ilikuwa balaa nakwambia"
"Huyu anahitaji tiba mama maana hali yake inasikitisha"
Mama akamwambia dada kila kilichotokea kule hospitali.
"Hivi ninavyokwambia, Sabrina amezuiliwa kwenda tena kumuona mgonjwa kwahayo yaliyotokea."
Nilikuwa kimya kabisa kamavile siwasikilizi ila moyoni mwangu iliniuma sana.
Muda wa kulala ulipowadia tulienda kulala na hapo nikalala na mama kwani niliogopa mauzauza yale ya hospitali.
Nikiwa nimelala na mama, nikasikia sauti toka sebleni ikiita jina langu.
"Sabrina, Sabrina"
Nikaanza kuogopa maana kwetu wote tulikuwa tumelala, sasa ni nani awezaye kuniita vile usiku ule.
Ile sauti ilianza taratibu ila badae ikawa inaita kwa nguvu hadi kunishtua zaidi, nilipoisikilizia kwa makini nikajua ni sauti ya Sam hapo ndio hofu ilizidi ukizingatia huyu Sam nimekuwa nikimuona mara mbilimbili.
Mara mlango wa chumbani kwa mama ukafunguliwa, na hapo ndipo nikaanza kupiga kelele za uoga huku nikimuamsha mama.
Mama aliposhtuka nilimueleza kuwa kuna mtu ananiita, mama akainuka na kuwasha taa kisha akaenda kuangalia sebleni akiwa ameongozana na mimi ila sebleni hapakuwa na chochote kile.
"Acha uoga mwanangu, si unaona mwenyewe hakuna chochote huku ni maruweruwe yako tu. Twende tukalale halafu kesho tutajua cha kufanya"
Nilikubaliana na mama huku uoga bado ukiwa umenitawala sana moyoni mwangu.
Asubuhi na mapema nikaamka wakati huo ambapo mama nae alikuwa ameamka, dada Penina alikuwa nyumbani na leo kwani ilikuwa ni mapumziko.
Tukafanya kazi za hapa na pale kisha dada akaniuliza.
"Mbona una roho mbaya kiasi hicho Sabrina?"
"Nimefanyaje kwani dada?"
"Yani wewe jana marafiki zako walikwambia watakuja hata kuwajibu loh! Na ulivyo na makusudi ukaondoka na kuacha simu hapa nyumbani ili wasikutafute, tabia mbaya hiyo."
Hapo ndio nikakumbuka kuwa Suzy alinitumia ujumbe kuwa yeye na Lucy wanakuja nyumbani.
"Kwahiyo walikuja dada?"
"Kama wasingekuja ningejuaje miadi yenu? Walikuja hapa, wakangoja hadi kuchoka na kuamua kuondoka. Tabia mbaya hiyo mdogo wangu, utakosa marafiki wazuri kwa upumbavu wako. Na ubaya ni kuwa kila wakipiga simu yako tukasikia ikiitia ndani na kujua kuwa uliiacha, itakuwa ulifanya kusudi wewe."
Hapo nikajifikiria sana na kukumbuka kuwa kweli simu niliiacha chumbani kwangu, hivyo nikaenda kuichukua nione.
Nikakuta ujumbe wa kutosha toka kwa Suzy na wote ukibeba lawama mwanzo mwisho, nikawaza cha kujitetea kwa haraka na nikaona ni bora kuwaeleza kuwa hata ule ujumbe wa mwanzo sikuuona nilikuwa tayari nimeshaenda huko hospitali.
Nikamtumia ujumbe Suzy kisha nikampigia simu kumuomba msamaha.
"Kwakweli Sabrina umenikera sana, hata hujui tulikuwa tunakuja kwasababu ipi jamani. Ilikuwa ni mambo ya kukusaidia wewe mwenyewe lakini umetupuuzia. Poa bwana, sie tushakusamehe."
Msamaha wa Suzy ulitoka ilimradi tu ili yaishe.
Mchana wake alikuwa kaka Deo ambapo alitukuta mimi na dada Penina kwani mama alienda hospitali kumuona mama Salome.
Tulifurahi sana kumuona kaka Deo na kuongea nae mambo mengi sana.
"Nia yangu kubwa ni kumchukua Sabrina tu maana wifi yake anamuulizia balaa"
Dada Penina akadakia.
"Inamaana wifi haniulizii mimi jamani!"
"Sio hivyo Penina, ila anajua wewe upo busy na kazi na huwezi kubali kuishi kule mbali na kazini kwako."
"Sawa nimekuelewa kaka, ila utamchukuaje Sabrina wakati mama hayupo?"
"Hilo ndio tatizo ila hakuna shida hata kesho naweza kumfata maana kuna project nafatilia inafanyika maeneo ya hukuhuku. Halafu kuna habari njema, sijui mama hajawaambia?"
"Habari gani hiyo kaka?"
"Wifi yenu ni mjamzito"
Kwakweli mi na dada tulifurahi sana kwa habari ile kwani ilikuwa njema kweli. Dada Penina alimpa sana hongera kaka Deo na mimi nikamwambia kaka.
"Yani kaka nina hamu kweli ya kubeba mtoto mchanga loh nitamleaje"
Dada Penina akadakia.
"Zaa wako na wewe"
Tukabaki kucheka tu huku tukimpongeza kaka, nikawa na hamu ya kumuona wifi na hiyo mimba yake. Dada Penina akasema,
"Natamani sana kumuona Joy na hiyo mimba loh sijui anafananaje jamani hahaha"
"Tena ina miezi saba kwasasa, mjiandae tu kuitwa na mashangazi na mama yenu kuwe bibi"
"Na wewe kuwa baba, Joy kuwa mama"
Wote tukacheka na kufurahi kisha kaka akatuga na kuondoka.
Mama aliporudi tukamuelezea uwepo wa kaka muda mfupi uliopita na kumwambia kuwa amesema atakuja kunichukua mimi kesho yake.
"Itakuwa vizuri maana hata mauzauza utayapunguza"
Dada Penina akadakia
"Atapunguza mauzauza? Wakati mwanao kawa mtabiri siku hizi."
"Mtabiri? Kivipi?"
"Unakupa siku mama Salome alipopata ajali?"
Mama akaitikia anakumbuka na hapo nikajua kuwa dada anataka kumwambia mama kuhusu nilivyomwambia kabla ya taarifa ya msiba.
"Basi mama, ile siku nilienda chumbani kwa mwanao kumuamsha moja kwa moja akaniambia kuwa mama Salome kapata ajali kabla hata ya taarifa kuletwa. Mwanao amekuwa mtabiri huyo."
Mama aliniangalia sana nadhani alikuwa akiyapima maneno ya dada, kisha akaniuliza.
"Eeh Sabrina mwanangu, ulijuaje"
Nikainama chini na kumjibu mama kuwa niliota tu.
"Kuotea watu mabaya si vizuri mwanangu, unaweza shikwa uchawi bila ya kutarajia"
"Kivipi mama?"
"Watu wanaweza kukushika uchawi bure mwanangu wakati hata uchawi kwetu haupo jamani"
Nikamsikiliza mama kwa makini na kumuelewa, kisha tukamuuliza habari za hospitali.
"Unajua jana muda umeenda kiajabu ajabu sana Sabrina, hata sijui ilikuwaje hadi muda wa kuona wagonjwa jioni ile ukatupita mmh!"
"Na nyie mna mauzauza sana, mtaua wagonjwa wa watu bila ya kutarajia?"
"Maneno gani hayo Penina?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Basi yaishe, tupe habari za mgonjwa anaendeleaje?"
"Anaendelea vizuri ila aliulizia sana uwepo wa Sabrina, sijui hata anataka kusema maneno gani ila ndo hivyo Sabrina kazuiliwa kwenda kule kwa muda."
Tukamgea mengi na kumuuliza mama kuhusu ujauzito wa wifi kuwa mbona hajatujulisha mapema.
"Mbaya kaka yenu, mi kama mama yake alitakiwa kuniambia mapema eti majuzi ndo ananipigia simu kunitaarifu kuwa mkewe ni mjamzito tena mimba kuwa kabisa ya miezi saba ila hata hivyo nilisahau kuwaambia."
"Hata huyo Joy nae ana tabia mbaya, kilichomfanya kushindwa kututembelea siku zote hizo nini?"
"Penina, usimlaumu sana maana hujui makubaliano yake na mumewe"
Ikabidi dada awe mpole kwani alishapoozwa na mama.
Mama akaniambia kuwa nianze kujiandaa kwaajili ya safari ya kwenda na kaka huko nyumbani kwake, nami sikusita nikaenda chumbani kwangu na kupanga baadhi ya nguo ambazo nitaondoka nazo na kwenda huko kwa kaka Deo.
Nikiwa chumbani napanga nguo, mara simu yangu ya mkononi ikaita kuangalia mpigaji alikuwa ni Sam, nikashtuka sana kwani Sam alikaa siku nyingi kidogo bila ya kunipigia simu.
Nikaamua kupokea ili kujua anachotaka kusema.
"Tafadhari Sabrina naomba tuonane"
"Sina muda huo Sam"
"Usinifanyie hivyo Sabrina, kumbuka wapi tumetoka, kumbuka jinsi gani nakupenda, kumbuka tunavyopendana Sabrana. Tafadhari nakuomba tuonane mpenzi."
Maneno ya Sam yaliniingia sana ila bado nikawa na mashaka na yale mambo ya kuwaona Sam wawili wawili.
"Kwanza nihakikishie kuwa Sam ninayeongea nae sasa ndiye Sam wa siku zote"
"Ni mimi Sabrina, kwani una Sam wangapi siku hizi? Inamaana hata sauti yangu umeisahau mpenzi? Tafadhari nielewe Sabrina"
"Poa, njoo karibu na maeneo ya nyumbani halafu utanishtua nitakuja ulipo."
Nikamaliza kuongoa nae na kuendelea na upangaji wa nguo zangu, baada ya muda kidogo Sam akanipigia simu na kunielekeza maeneo alipo na ilikuwa karibu na nyumbani kwetu.
"Upo mwenyewe au na mtu mwingine?"
"Nipo mwenyewe Sabrina, njoo utaniona mwenyewe"
Nikakata simu na kujiandaa kutoka pale nyumbani, nikamuaga mama kuwa naenda dukani mara moja.
"Usichelewe sana Sabrina, si unaona giza linakaribia kuingia!"
"Sawa mama sitachelewa"
Nikaondoka na kwenda eneo ambalo Sam amenielekeza kuwa yupo.
Nikiwa natokea nyumbani nikamuona Sam kwa mbali mahali alipo, mara nikamuona Lucy akitokea upande mwingine, nikaamua kujibanza kidogo ili niangalie picha itakwendaje.
Lucy alifika hadi mahali alipo Sam kisha wakakumbatiana, moyo wangu ulilia paaa kwa wivu kwani wivu ulinishika kupita kiasi ukizingatia si utamaduni wetu kuona mdada na mkaka wasiojuana kiundani zaidi wakikumbatiana.
Roho ikaniuma sana, Lucy akaongeza na mbwembwe zake pale kwani alimbusu Sam shavuni kwakweli nilitamani nikawatimue kwa viboko mahali pale.
Nikajitokeza na kuwafata ili wajue kama nimewaona, Sam aliponiona akamsukumia Lucy kwa pembeni kidogo.
"Unamsukuma wa nini? Nimeyaona yote mliyoyafanya hapo"
Sam akataka kuanza kujitete ila nikamkatisha.
"Subiri nikueleze ilivyokuwa Sabrina, ni...."
"Hakuna cha kunieleza Sam, kila kitu nakifahamu na hii leo umeamua kunithibitishia tu kuwa ni kweli mna mahusiano"
Lucy nae akataka kujieleza.
"Ila Sabrina na...."
"Tena wewe ndio unyamaze kabisa na umalaya wako, yani Sam katika wanawake wote ukaona bora unichanganye na huyu Lucy? Halafu leo ooh tuje tujadili mpenzi sijui nini na nini kumbe unafki tu"
"Jamani Sabrina usiseme hivyo!"
"Nisiseme hivyo kitu gani? Wakati wewe umeona ni vyema kuja kunionyesha kabisa kama upo na huyo malaya wako. Watazame sura zao zilivyo loh! Hamuoni haya wala kujihisi vibaya"
Kwakweli niliongea sana kwani hasira ilikuwa imenikaa kooni nikatamani hata kupigana na Lucy ila nikaona itakuwa ni ujinga tu.
Nikaamua kugeuza ili niondoke na kurudi kwetu, Sam akasogea na kunizuia kwa kunishika mkono ndio akawa kamavile ananipandisha mashetani kwajinsi nilivyoongea kwa ukari.
"Sam, niache! Nenda zako huko na Lucy wako, na usithubutu kunifatilia tena mjaa laana wewe usojua vibaya. Niache nakwambia."
Ikabidi Sam aniache kwani nilibadilika sana kwa wakati huo.
Nikatembea bila hata ya kugeuka nyuma kwa hasira, nilifika nyumbani na kujipangusa machozi kwanza kabla ya kuingia ndani ili mama asiweze kuniona kama nalia.
Niliingia ndani na kwenda chumbani kwangu moja kwa moja kwani uchungu niliopata ulikuwa ni wa kutonesha kidonda changu ambacho nilianza kukisahau maumivu yake yalivyo.
Nilikaa kitandani na kulia sana, nikaiona ile leso niliyopewa na Carlos kujifutia machozi, nikaichukua na kujifuta.
Ujumbe ukaingia kwenye simu yangu, kuangalia umetoka kwa Carlos.
"Ukiwa na tatizo lolote Sabrina usisite kuniambia. Nitakusaidia"
Nikausoma huo ujumbe mara mbili na kuuona hauna manufaa yoyote kwa sasa kwangu kwani moyo ulikuwa unaniuma sana kuhusu Sam na Lucy.
Mama akaniita kula ila nikamjibu kuwa nimeshiba, ukweli ni kwamba sikuwa na hamu ya chakula kabisa.
Usingizi ulinipitia mule mule chumbani kwangu, usiku wa manane nikasikia mtu akiniita toka sebleni na ikawa kama nilivyosikia jana yake. Uoga ukanishika sasa, mara mlango wa chumbani kwangu ukafunguliwa ila aliyeingia hakuonekana na mara nikaona ukifungwa.
Sauti ikaanza kusikika karibu sasa kuwa naitwa ila muitaji sikumuona, uoga ukanizidi.
Ile sauti ikasogea karibu na sikio langu na kusema.
"Sabrina si nakuita wewe mbona huitiki?"
Nikawa natetemeka kama nimewekewa barafu, mara nikaguswa na kitu kama mkono.
Nikawa natetemeka kama nimewekewa barafu, mara nikaguswa na kitu kama mkono.
Hapo nilitamani hata kuzimia huku natetemeka kwa uoga zaidi na sikuweza hata kugeuka nyuma, mara simu yangu ikaanza kuita kwakweli nilishtuka sana na kutamani hata kukimbia.
Yale mauzauza ya uwepo wa mtu ndani yakapotea na kukawa shwari kabisa, kuangalia mpigaji ni Carlos nami nikapokea.
"Niambie Sabrina, nimelala nikaota kuwa una matatizo ndiomana nimekupigia"
"Ni kweli nina matatizo Carlos"
"Ila mimi najua jinsi ya kukusaidia, kama ukihitaji msaada wangu utaniambia."
Hapo ndipo Carlos alipokuwa akinichosha maana kama anajua cha kunisaidia si angenisaidia tu, yani yeye anangoja hadi nitake msaada ndipo anisaidie.
Nikaongea nae mambo mengi tu usiku ule na kuniambia kuwa kesho yake atakuja kunitembelea kwetu.
Baada ya maongezi na Carlos nikalala vizuri hadi kunakucha.
Maswali mengi nilijiuliza kuhusu Carlos kuwa ni mtu wa aina gani na ana maana gani kwenye maisha yangu.
Asubuhi niliamka na kuwa kama vile mtu nisiye na tatizo lolote lile.
Mama akaanza kunipa wosia wake.
"Ukienda huko kwa kaka yako upunguze mawenge mwanangu halafu uvivu acha"
"Mmh jamani mama, kwani mi mvivu!"
"Ndio, wewe ni mvivu mwanangu. Kumbuka wifi yako huko ni mjamzito inatakiwa wewe ndio umsaidie sio yeye akufanyie kazi zako"
"Sawa mama, nimekuelewa"
"Unielewe na ufate nisemacho, uwe unawahi kuamka huko sio unalala hadi saa tatu saa nne mtoto wa kike na usaidie kazi najua wataogopa kukusema ila nitakuwa nawauliza kama utaendeleza uvivu wako"
"Mmh! Umeanza sasa mama, nitagoma kwenda mimi."
"Basi mwanangu, ila ndio hivyo"
Dada Penina leo hakuwepo kwani aliakuwa ameshaenda kazini kwake.
Wakati naongea na mama, nikapata ugeni naye alikuwa ni Suzy.
Nilikaa na Suzy na kuongea nae kiasi.
"Na wewe Suzy asubuhi yote hii upo kwetu?"
"Ndio, maana nikichelewa sikukuti"
"Na usingenikuta kweli, una bahati sana"
Nikamuacha Suzy na kwenda kuoga ili nirudi kuongea nae vizuri zaidi.
Nilipokuwa bafuni naoga nikasikia sauti ikiniuliza.
"Hivi wewe ni mtu wa aina gani Sabrina"
Nilishtuka sana baada ya kutajwa jina langu mwishoni na kujua kuwa ni mimi ndiye ninayeulizwa.
Nikajimwagia maji haraka ili nitoke, wakati natoka sauti ile ikaja kwa nyuma yangu.
"Madai yako unakimbia?"
Na kweli hapo nilikimbia hadi sebleni huku nikihema, Suzy akacheka kuniona na kuniuliza.
"Vipi wewe, au ndio kuoga fastafasta huko"
Nilitabasamu kwa tabasamu la uongo lakini ukweli wa nikimbiacho niliujua mimi na hata kama nikisema wataniona mzushi tu au mawenge, hivyo nikawa kimya na kwenda ndani kuvaa kisha kumfata Suzy alipo.
"Kwanza niambie Sabrina, ulikuwa unakimbia nini kutoka bafuni?"
"Mmh! Wee acha tu Suzy"
"Au ndio yale maruweruwe yako anayoyasemaga mamako?"
"Achana na hayo bwana Suzy"
"Niachane nayo kivipi wakati umerudi na povu sikioni!"
Hapo nikashtuka na kujishika masikio kweli yalikuwa na povu, nikainuka na kuchukua maji na kwenda nje kunawa kwenye masikio yangu.
Nilipomaliza kunawa nikamuona mtu amesimama karibia na kwetu, kumuangalia vizuri alikuwa ni Sam, nadhani alikuwa anataka kuja kwetu ika alikuwa kama anasita. Nami nikampuuzia kama vile sijamuona ingawa mcho yangu na yake yaligongana. Kisha nikaingia ndani na kwenda kuendelea kuongea na Suzy na wala sikumwambia kama nimemuona Sam nje kwetu.
Suzy akaanza kuniambia kilichomleta,
"Sabrina rafiki yangu, nimekuja kuongea nawe hapa kuhusu mambo matatu."
Nikawa namsikiliza kwa makini ili nijue mambo hayo ni nini.
"La kwanza ni kuhusu wewe mwenyewe, la pili ni kuhusu Carlos na la tatu ni kuhusu Sam"
"Nakusikiliza Suzy"
"Sabrina rafiki yangu una matatizo, tena unahitaji msaada wa karibu sana."
"Ni kweli nina matatizo shoga yangu, eeh niambie kuhusu huo msaada wa kunipa"
"Sabrina, sio mambo ya masikhara hapa. Na usifikirie kila aliyekuwepo mbele yako ataweza kukusaidia. Mengi ufikiriayo kuhusu sisi marafiki zako na mpenzi wako Sam ni kati ya matatizo uliyonayo Sabrina"
Nikaendelea kumsikiliza Suzy ili nijue alichonacho cha maana.
"Halafu kuhusu Carlos, napenda kukutahadharisha kuhuyu huyu mtu rafiki yangu. Carlos ni....." Kabla Suzy hajamalizia, alikuja mama na kukatisha mazungumzo yetu. "Sabrina, mgeni wako huyo amekuja"
Kumuangalia alikuwa ni Carlos, ikabidi nimkaribishe tu na hapo rafiki yangu Suzy akasita kunieleza kuhusu Carlos kisha akasema. "Cha tatu, nilifika na Sam yupo nje anahitaji kuzungumza na wewe Sabrina" Nilimuangalia tu Suzy aliyekuwa akiongea kwa uoga muda huu tofauti na alivyokuwa akizungumza mwanzoni kwa kujiamini.
Suzy akainuka ila kunipeleka alipo Sam, nami nikamfuata Suzy kumbe Carlos naye aliinuka kutufuata.
Akafika mahali pale nje na kutuangalia tukiwa tunaelekea alipo Sam, tulimkuta akiwa amekaa chini ya ule mti nadhani ni baada ya kuchoka kusimama, na alikuwa amesinzia pale pale ndipo Suzy alipomshtua na aliposhtuka tu akasema.
"Lucy!!"
Nikamuangalia sana Sam.
"Yani inaonyesha jinsi gani Lucy alivyokukaa katika akili yako loh! Hadi ndoto za mchana unamuota!"
Sam alibaki kunitazama tu mi na Suzy. Nikamgeukia Suzy na kumwambia.
"Yani mtu mwenyewe uliyetaka nizungumze naye ndio huyu! Amekaa hapo na kumuwaza mwanamke mwingine halafu unataka nijipe imani kuwa bado ananipenda mimi. Sikiliza Suzy, sina muda wa kuzungumza na Sam, nyie nendeni tu na mambo yenu"
Nikageuka na kuanza kuondoka, ingawa waliniita nikawasikilize lakini sikugeuka nyuma.
Nikaenda hadi aliposimama Carlos na kuongea nae.
"Mmh na wewe ni mmbea loh! Hadi umeamua kutufata ushuhudie kinachoendelea"
Carlos aliniangalia tu na kucheka kisha tukarudi ndaniIla hakukaa sana na wala hakusema chochote cha maana ila aliaga na kuondoka na kusema kuwa atakuja badae na wala sikumwambia kama anaweza asinikute kwakuwa sikutaka ajue kama badae nitaondoka na kaka Deo.
Akaniomba nimsindikize kwani siku hiyo hakuja na gari yake, wakati namsindikiza nikamuuliza kuwa gari ameiacha wapi kwani.
"Ina matatizo kwahiyo ipo garage"
Mi nikashangaa.
"Kheee ina matatizo!"
"Ndio, mbona unashangaa? Kwani mimi gari yangu haiwezi kupata matatizo?"
"Aah hapana nimeshangaa tu."
Akaendelea kuongea mambo mbali mbali na huku akijaribu kuniambia kitu kuhusu Suzy.
"Unajua kwanini rafiki yako Suzy aliponiona alishtuka?"
"Eeh kwanini?"
"Kwanza kabisa pale alikuwa ananisema mimi, pili kuna siri yake nimeijua"
"Siri gani hiyo?"
"Rafiki yako anatembea na mume wa mtu, mwambie awe makini sana kwani itamletea matatizo badae"
Nikashangaa na kutaka kumuuliza Carlos kuwa amejuaje, ila daladala ilifika akapanda na kuniaga kwahiyo sikuweza kumuuliza tena.
Nikarudi nyumbani nikijiuliza kuwa je ni kweli kwa nilichoambiwa na Carlos kuhusu Suzy, na mbona Suzy amenificha hilo wakati huwa ananieleza mambo yake mengi tu.
Ikabidi nichukue simu na kumuuliza Suzy kuhusu hilo swala.
"Nasikia una mahusiano na mume wa mtu Suzy!"
"Nani kakwambia?"
"Nijibu kwanza ni kweli au sio kweli?"
"Fanya yako, yangu hayakuhusu."
Kisha akakata ile simu, kwa mara ya kwanza leo namsikia Suzy akinijibu majibu ya mkato na kukatisha tamaa kiasi hicho. Nikabaki kumshangaa na kujiuliza kuwa kwanini amechukizwa na nilichomuuliza.
Ikabidi tu niendelee na mambo yangu kwamaana nilishashushuliwa, nikaenda chumbani kwangu kuweka vitu sawa huku nikimngoja kaka afike tuondoke.
Mama akaniaga kuwa anaenda hospitali kumtazama mama Salome kwahiyo ilitakiwa nimngoje hadi atakaporudi.
"Kaka yako akija mwambie mnisubiri kwanza"
"Sawa mama"
Kisha akaondoka na kuniacha mwenyewe pale nyumbani ila kwa uoga niliamua kwenda kukaa nje kumngoja kwani ndani kwetu kulinipa sana mashaka ya kukaa.
Nikiwa pale nje nimejilaza, akaja Sam na kukaa karibu yangu. Hapo nikainuka na kumuuliza.
"Yani hujaondoka tu?"
"Siwezi kuondoka Sabrina, nahitaji sana kuongea na wewe"
"Sikia Sam, umeshaniumiza vya kutosha hivyobasi sitaki tena kuumizwa na wewe."
"Inamaana Sabrina hunipendi tena?"
"Kukupenda nakupenda tena sana tu ila wewe ndio hunipendi"
"Nakupenda Sabrina"
"Kama ungenipenda usingenichanganya na wasichana wengine haswaa kunichanganya na rafiki yangu kipenzi, kwakweli imeniuma sana Sam"
"Sikia Sabrina, hakuna chochote kinachoendelea kati yangu na Lucy. Mimi nakupenda wewe, mambo yote uyaonayo kwangu hata mwenyewe siyaelewi ila Lucy si mpenzi wangu na hakuna chochote cha zaidi kati yetu"
Sam aliendelea kunieleza kwa makini sana ila gafla kichwa kikaanza kuniuma ikawa kamavile mtu ananigongagonga na nyundo hata Sam akanishangaa kuwa nina tatizo gani, ikabidi anisaidie kunipa huduma ya kwanza na kunipeleka ndani.
Nilikaa nae sebleni ambapo tulikaa kwenye kochi na akaweka kichwa changu kwenye mapaja yake.Muda kidogo kaka Deo alikuwa amewasili pale nyumbani na kunikuta mimi usingizi umenipitia nikiwa vilevile nimelaza kichwa changu kwenye mapaja ya Sam, huku Sam nae akinibembeleze kwa kunishika kichwani.
Kaka alitushtua sana pale ndani hadi niliamka na kukaa.
"Ndio mambo gani haya Sabrina? Mama yuko wapi? Na huyo ni nani yako?"
"Mmh kaka hata salamu?"
"Salamu ya kazi gani? Ni picha gani hii unanionyesha kaka yako? Sema, mama yuko wapi?"
Akawa anaita "Mama, mama"
"Mama hayupo kaenda hospitali kumuangalia mgonjwa."
"Kwahiyo mama kama hayupo ndio wewe unatumia nafasi hiyo kufanya upuuzi wako humu ndani?"
Kisha akamuangalia Sam kwa jicho la ukali sana.
"Wewe kijana toka humu ndani na upotee kabisa kabla sijakuharibu haribu"
Ikabidi Sam aondoke kwani kaka alionekana kuwa na hasira sana.
Baada ya Sam kuondoka nikajaribu kumuelewesha kaka lakini hakutaka kunielewa hata kidogo, aliendelea kuamini alichoamini tu.
Mama aliporudi, alisalimiana na kaka na kuongea nae mawili matatu kisha akamruhusu kuondoka na mimi.
"Kwakweli mama bora nikakae kidogo na huyu Sabrina ili akili yake iwe sawa"
"Ni kweli kabisa mwanangu, na mkifika huko mnipe taarifa kama mmefika"
"Hakuna tatizo mama"
Safari ya mimi na kaka ikaanza, nikapakia begi langu kwenye gari yake aliyokuja nayo na kuondoka.
Safari ilikuwa ni ndefu kiasi kwani kaka alikaa mbali kidogo na nyumbani.
Tulipokuwa tunakaribia kufika, kaka akagundua kuwa kuna mtu anatufatilia tangia tumeanza safari, akaniita na kunionyesha kwenye kioo cha gari na hapo nikashtuka sana.
Tulipokuwa tunakaribia kufika, kaka akagundua kuwa kuna mtu anatufatilia tangia tumeanza safari, akaniita na kunionyesha kwenye kioo cha gari na hapo nikashtuka sana.
"Huyo mtu amekuwa akitufatilia tangia tumeanza safari. Je unamjua?"
Nikasita kujibu kwani ile gari iliyokuwa ikitufatilia ilikuwa ni gari ya Carlos.
"Mbona hunijibu Sabrina, je unamjua?"
"Hapana kaka simjui"
Ikabidi kaka asimamishe gari ili amuulize yule mtu ni nani.
Gari ya kaka iliposimama na ile gari nyingine nayo pia ilisimama. Kaka akashuka ili amfate kumuuliza, wakati kaka anaikaribia ile gari, yule mtu akashusha kioo akaniangalia halafu akawasha gari na kuondoka kabla hata kaka hajalifikia.
Nilishtuka sana kwani hakuwa Carlos kama nilivyodhani bali alikuwa ni yule kaka wa ndotoni.
Nikajikuta nikitetemeka hata kaka aliporudi ndani ya gari alitambua kama nimeshikwa na uoga.
"Vipi na wewe una matatizo gani?"
"Sina tatizo kaka"
"Mtu mwenyewe namfata pale kaondoka, labda alikuwa kibaka yule."Nikaitikia kwa kichwa nikiashiria kwamba nakubaliana na maneno ya kaka na safari ikaendelea.
Kidogo tu, tulifika nyumbani kwa kaka na wifi akatupokea vizuri sana na kutukaribisha ndani.
Nilifurahiana na wifi yangu na kuongea nae mambo mengi ila giza lilishaingia kwahiyo mengine kupanga kuongea kesho yake.
Nilimzoea sana wifi kwavile aliwahi kuishi nyumbani kwetu kipindi ambacho kaka alikuwa safarini kwa muda mrefu kidogo, kwahiyo tulikuwa tumeshazoeana.
Baada ya chakula cha usiku, wifi akanionyesha chumba cha kulala nami nikaenda huko kulala.
Nikawaza mambo mengi sana haswaa kuhusiana na kufatiliwa na yule jamaa wa ndotoni, nikawaza kama je na huku kwa kaka itakuwa vilevile kama nyumbani au itakuwaje.
Niliwaza na kupitiwa na usingizi na nililala hadi asubuhi bila ya tatizo lolote wala kuota ndoto za ajabu ajabu.
Kulipokucha nilifurahi sana na kuona kuwa huku ndio kunanifaa kuishi na sio kule kwetu ambako nakumbana na mauzauza ya kila siku.Niliamka nikiwa na uchovu kiasi, wifi ndiye aliyenishtua kwani mimba yake ilikuwa ikimfanya awahi sana kuamka. "Umeamka muda mrefu eeh!"
"Ndio mdogo wangu si unajua tena"
"Mmh huyo mtoto atakayezaliwa naona atakuwa janja sana, maana anawahi kukuamsha balaa" Tukakaa na wifi tu kwani kaka alikuwa ameshaenda kwenye kazi zake. Wifi alikuwa akiisifu sana mimba aliyobeba kwani haikumpa uvivu kama watu wengine wanavyopataga shida na mimba zao. "Yani huwezi amini wifi, hii mimba na ukubwa wake bado naimba kwaya tena nakuwa namba moja kuwahi mazoezini, sina uvivu kabisa yani" "Mimba yako inaraha basi, yani bado nguvu ya kuimba unayo na tumbo lote hilo duh!" "Mmh! Huyu mtoto nitakayemzaa atakuwa mtundu sana na kama nikimzaa wa kike najua atafanana na wewe na nitamuita Sabrina." "Mmh! Akiwa wakiume je?"
"Atakuwa wakike bwana, sidhani kama ni wakiume"
Wifi alichangamka sana hadi nikaona raha kuishi nae kwani alinipa furaha na amani, pia nilikuwa huru kwa chochote kile.
Mchana wa siku hiyo wifi akaniomba kuwa nimsindikize kwenye mazoezi ya kwaya kanisani kwao, hakupenda kuniacha mwenyewe ndiomana akaniomba niende nae.
Tulipofika nilikuwa kimya sana nikiangalia mambo yanayoendelea kwenye ile kwaya, nilikb na mdada mmoja aliyejitambulisha kwangu kwa jina la Jack ila hakujua kama mimi ni wifi yake na Joy kwahiyo akawa anaongea mambo mengi sana kwa uhuru tu.
"Yani hiyo kwaya usione hivyo, humo kumejaa unafki tupu."http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Kwanini?""Yani huyo Joy na mtumbo wote huo lakini anapendelewa na James balaa, kila siku anaanzisha yeye nadhani wanaajenda yao ya siri"
Nikacheka kidogo na kuuliza tena, "Kwani James ndio nani?"
"Si yule mwalimu wa kwaya, yani wengine hata hatuonekani. Anayeonekana ni Joy tu, mara amsifie sijui ana sauti nzuri sijui nini na nini yani unafki mtupu"
Nilicheka na kujiambia moyoni kuwa huyu dada anasumbuliwa na wivu kwani ndio kawaida ya watu katika kundi lolote lile kutawaliwa na wivu, chuki na husda ila nami nikawa makini ili nione kama kweli huyo mwalimu wa kwaya anampendelea wifi yangu, ila kabla ya yote nikamuuliza swali la kizushi huyu Jack.
"Je ameanza kumpendelea baada ya ujauzito au kabla ya hapo?"
"Hata kabla ya ujauzito alikuwa akimpendelea ila saivi ndio amezidisha jamani loh kama kambebea ile mimba yeye!"Nikacheka sana na kumuuliza, "Kivipi?"
"Kwani wewe hujui mtu akikubebea mimba anavyokuwa? Yani unatokea kumpenda na unapenda kila afanyacho na kumuona mara zote hata yeye inakuwa hivyo. Kuna mwingine mimba yako itampenda na mwingine itamchukia ila kwa Joy na James imezidi sasa."
Nikamuangalia sana Jack aliyeonyesha kuchukizwa sana na kupendelewa kwa wifi yangu, badae wakainuka kwenda kuimba na baada ya hapo tukaondoka.
Nilimuona yule Jack akijisikia vibaya sana kuona nimeongozana na wifi Joy kuondoka kwani alijua yote aliyoniambia yatamfikia.
Nilipokuwa na wifi naye nilimuuliza kwa uzushi tu.
"Nasikia wifi yangu unapendelewa kweli na mwalimu wa kwaya eti kila siku unaanzisha wewe"
"Ile kwaya ni wanafki wifi, yani kuna chuki mule balaa mengine nikikuelezea hata utashangaa ila huwa tunakaa kimya tu na kuyaacha yapite mdogo wangu. Watu wanawivu mule, chuki binafsi na kila kitu"
Nilimuangalia wifi na kukubaliana na maneno yake kwani hata mimi niliona kuwa ni wivu ndio uliowasumbua watu wa aina ile ya Jack.Mara kuna kijana akatufata, kisha wifi akanitambulisha kwa yule kijana kuwa ndiye mwalimu wao wa kwaya hapohapo nikaelewa kuwa yule ndio James anayezungumziwa na yule Jack, nikasalimiana nae kisha akatuambia tumngoje ili twende wote kwahiyo mimi na wifi tukasimama mahali kumngoja.
Alipoondoka kidogo nikamuuliza wifi yangu,
"Kwani na yeye tunaenda nae njia moja?"
"Ndio, ila yeye tutamuacha njiani halafu sisi tutaendelea"
"Huwa unaongozana nae mara kwa mara?"
"Ndio, tena huwa ananisindikiza hadi nyumbani ingawa kwake ni nyuma. Yani huyu mkaka anaupendo sana wifi yangu"
"Kweli, anaonyesha kuwa na upendo"
Yule James akarudi na safari ya kuondoka ikaendelea, kufika njiani James akamnunulia wifi matunda na kumkabidhi kisha akamwambia.
"Kumbuka ulivyoambiwa kliniki, kula matunda kwa wingi na mboga za majani"
"Natambua hilo James hata usijali"
Tukaendelea na safari kisha yule James akatusindikiza hadi nyumbani.
Swali nililojiuliza ni kuwa huyu mwalimu wa kwaya anaelewa nini juu ya ushauri anaopewa wifi kliniki.Ila sikuuliza chochote tena nikawa kimya tu, naye wifi alifata ushauri kwani alipofika tu akaanza kula yale matunda ambayo kwakweli ni mazuri kwa afya na kunipa baadhi mimi.
Kaka aliporudi alitukuta tukiwa tumekaa na wifi huku tukisimuliana mambo mbali mbali.
"Naona mtu na wifiye, leo amani tupu humu ndani"
Wifi akawa anacheka, nami nikauliza.
"Kwani siku zingine amani hakuna?"
"Muulize wifi yako akujibu"
Kaka akaenda chumbani na wifi akaendelea kucheka tu kisha akasema.
"Amani ipo wifi ila kaka yako si unajua tena na ubize wake, yani muda wote amechoka sina hata mtu wa kuongea naye humu ndani. Ngoja huyu mtoto aje achangamshe nyumba tu"
"Na sisi tunamngoja kwa hamu huyo mtoto pia, akaiwa wa kike kweli nitakuwa namsuka vinywele vyake"
"Ndio unachowaza Sabrina, (wifi akacheka) na ndiomana nasema nitamuita Sabrina maana napenda mwanangu awe mcheshi na mpole kama wewe"
"Na kama wakiume basi afanane na kaka"
Wifi akacheka na kuuliza.
"Asipofanana nae je?"
"Namaanisha afanane nae upole maana kwetu wote wapole"
"Na je ataitwa jina gani?"
"Ataitwa James"
Wifi akashtuka sana nilipotaja hilo jina na kuuliza.
"Kwanini?"
"Ili awe na moyo wa upendo kama mwalimu wenu wa kwaya"
Nikamuona wifi akipumua kiasi na kusema.
"Aah kumbe!"
"Ndio, mbona ukashtuka ulidhani nini?"
"Hamna kitu wifi, nadhani itakuwa vyema kama tukienda kula"
Ikabidi tuinuke na kuandaa chakula kisha wifi akamuita kaka ili tule pamoja. Wakati tunakula simu yangu ikaita kwa nguvu sana kwani nilikuwa nayo mezani ukizingatia tangia asubuhi hakuna aliyenipigia. Kaka aliniangalia na kusema,
"Nani anayekupigia muda huu? Au ndio kale kajamaa kaka ka siku ile" Nilikaa kimya tu kwani ni kweli mpigaji alikuwa Sam, ikabidi niizime kwa muda ili kaka asiingee tena. "Mbona hujaipokea sasa?"
Wifi akajaribu kunitetea.
"Mmh! Muda wa kula huu sio wa kuulizana maswali Deo, utamkosesha raha mdogo wako" Mi nikatulia tu na kuendelea kula, nikahisi kuwa huenda kaka aliambiwa na mama kuhusu Sam na ndiomana amekuwa mkali kwangu na kuniuliza maswali mengi mengi.Nilipomaliza kula nilienda chumbani na kuwasha simu na jambo la kwanza ikawa ni kumpigia Sam. "Kweli nimeamini kuwa Sabrina hunipendi tena, yani unaondoka kwenu hata bila ya kunipa taarifa! Kwanini lakini?" "Niliamua tu sababu siku hizi wewe una watu wako unaowajali hata ningekwambia usingeona umuhimu wake" "Hivi Sabrina, nifanye nini ili uamini nakupenda?"
Nikamsikia wifi akiniita huku akigonga mlango wangu, ikabidi nimwambieSam kuwa nitampigia badae na kwenda mlangoni kuongea na wifi.
"Kakako anakuita"
Nikatoka na kumfata kaka alipo ili nikazungumze nae.
"Yani mdogo wangu kumaliza kula tu unakimbilia chumbani au uliogopa nilivyokusema wakati wa kula?"
"Hapana kaka"
"Nisamehe Sabrina maana si vizuri kumsema mtu wakati wa kula"
"Usijali kaka, nami nisamehe kwa kukaa na simu mezani wakati wa kula"
"Sawa mdogo wangu usijali, kuwa huru mama. Sawa eeh!"
Nikamuitikia kaka na kujigeresha kidogo kisha nikaenda tena chumbani ili nikaongee na simu.
Kufika chumbani, nikaiona simu yangu ikiwaka waka mwanga wa ajabu nikaogopa kuishika na kujiuliza au mauzauza yamenianza tena na kwenye ile nyumba ila nikakumbuka maneno ya wifi yangu kuwa niwe nasali kabla ya kulala, nikaamua kukaa mbali na ile simu ili niombe kwamba na kama ikiendelea vile nikamwambie kaka.
Nikapiga magoti na kuinama ila sikuelewa kilichoendelea kwani nilimsikia wifi tu akifungua mlango wangu na kuniambia.
"Mmh Sabrina unafanya nini?"Nikashtuka sana na kumuuliza.
"Kwani nini?"
"Unakoroma sana duh! Ndio mlalo gani huo?"
Nami nikawa najishangaa kwani nilikuwa vilevile nimeinama, kwakweli sikuamini kama nimelala vile muda wote.
"Kwani saa ngapi muda huu?"
"Ni saa mbili na nusu asubuhi"
Nikazidi kushangaa, wifi akaniambia kuwa alikuja kuniamsha ili nikapate kifungua kinywa.
Baada ya yote, wifi alitaka twende sokoni ili kununua baadhi ya mahitaji. Nikabeba simu yangu ambayo ilikuwa kawaida kabisa leo wala haikuonyesha tatizo lolote.
Tukiwa njiani nikapigiwa simu na Carlos aliyeniuliza nilipo nikamtajia naye akasema anakuja.
Baada ya muda tu kidogo Carlos aliwasili na kukuta nimesimama na wifi njiani, nikamuonyeshea ishara naye akafika mahali alipo.
Wakati Carlos alipokuwa anamsalimia wifi alimpa mkono, mara gafla wifi akapiga kelele.
Wakati Carlos alipokuwa akimsalimia wifi alimpa mkono, mara gafla wifi akapiga kelele na kuuachia mkono wa Carlos huku Carlos akionekana kutabasamu.
Kwakweli kitendo hiki kilinishtua sana kwani wifi alijawa na uoga uliopitiliza wakati Carlos alikuwa kawaida huku akitabasamu tu, sikujua Carlos alimfanya nini wifi yangu wakati wanasalimiana.
Nikajikuta nikiuliza,
"Kwani vipi jamani? Mbona sielewi!"
Wifi akanishika mkono huku akinivuta kuwa tuondoke.
"Tuondoke Sabrina, huyo mkaka sio mtu mzuri"
Nikazidi kushangaa kuwa wifi atamsemaje mtu kuwa sio mzuri wakati hamjui, wifi alizidi kunivuta kwahiyo ikabidi tuondoke hata safari ya kwenda sokoni ikaghairishwa na tukarudi nyumbani.
Nilimuona wifi akijiinamia huku akiwa na mawazo sana, kisha akaniambia kuwa anaenda kufanya maombi kwanza.
Alienda chumbani kwao na mimi nilibaki pale sebleni nikitafakari yale mambo kwani yalinichanganya tayari huku nikiwa na maswali mengi sana ya kumuuliza wifi atakapotoka kusali.
Baada ya muda, wifi alirudi pale sebleni nami nikafurahi ili niweze kumuuliza maswali yangu.
"Mmh afadhali sasa nina amani kidogo"
"Kwanini?"
"Kwasababu nimeomba, unajua Sabrina maombi ndio silaha kubwa na ya pekee katika mambo ya khatari"
"Sawa wifi nimekuelewa, ila kwanini umesema kuwa yule sio mtu mzuri?"
"Sabrina mdogo wangu, nakupenda sana yule sio mtu kabisa sijui hata umemtolea wapi?"
"Sio mtu kivipi wifi? Mbona unanitisha?"
"Yule sio mtu mdogo wangu, huenda akawa ni mchawi tena wa kuzimu"
"Mmh niambie vizuri wifi"
"Aliponipa mkono kunisalimia, ubaridi ulipenya katika mwili wangu wote halafu mtoto wa tumboni mwangu alishtuka sana. Umeyatizama kwa makini macho ya yule kaka?"
"Kwani yana nini mbona mi huwa naongea nae na kumtizama kila siku?"
"Mdogo wangu umefungwa hata huoni, macho ya yule kijana si ya kawaida"
"Ila kuhusu ubaridi ndio alivyo yule siku zote"
"Acha kutetea kitu usichokijua kwa undani zaidi, ila mimi nakwambia ukweli kwamba yule sio mtu wifi yangu. Kuwa makini sana"
Nikamsikiliza wifi ila bado sababu zake za kutaka niamini kuwa Carlos si mtu wa kawaida hazikuniingia akilini kwani Carlos nilishaanza kumzoea kwa sasa, ikabidi nijiweke katika mazingira ya kumchunguza Carlos kabla ya kuwa tatizo kubwa.
Tuliendelea na wifi katika kazi mbili tatu na kufanya mambo mengine ila wifi hakutaka tena kwenda sokoni.
Wakati tunakula chakula cha mchana, Sam akanipigia tena simu na haikuwa tatizo kuipokea kwani kaka hakuwepo.
"Naomba kuonana na wewe Sabrina, tafadhari sana"
"Nipo kwa kaka na sitaweza kuonana nawe na wala sina muda huo"
"Tafadhari Sabrina, kumbuka nakupenda"
"Hata kama, sitaki kuonana na wewe"
Nikakata ile simu na kuendelea kula, kumbe wifi alinisikiliza kwa makini sana.
Tulipomaliza kula akaniuliza,
"Ulikuwa unaongea na nani wakati ule?"
"Ni rafiki yangu tu"
"Mpenzi wako eeh"
Nikacheka kidogo na kuitikia kuwa ni kweli mpenzi wangu, wifi nae akacheka na kuniuliza.
"Sasa mbona hutaki kuongea nae wala kuonana nae kwanini? Humpendi au ni nini?"
Niliinama kidogo kama nafikiria jambo, kisha nikamjibu wifi.
"Kumpenda nampenda tena sana tu, tatizo amenisaliti tena kwa my best friend"
"Mmh! Umeshuhudia au umeambiwa?"
Ikabidi nimueleze kwa kifupi wifi ilivyokuwa, nikamueleza mengi ila sikumueleza kuhusu mauzauza yangu.
"Pole sana, ila kama anahitaji kuongea nawe bado ni lazima anakitu cha kukwambia"
"Ila mimi sijisikii kabisa kuzungumza nae, kwakweli ananiumiza sana na kila siku ananiongezea maumivu"
"Ila ndio mapenzi yalivyo, uvumilivu unahitajika sana. Me ningependa uzungumze nae, tena ikiwezekana aje hapa nyumbani"
"Mmh labda kaka asiwepo"
"Usijali Sabrina, huwa sipendi kuona mtu anakosa muafaka kwa kitu apendacho. Usikubali mtu wa mbali kuvunja mahusiano yenu, mtu mnayependana nae ndio anastahili kuwa naye katika ndoa ingawa mara nyingi huwa haiwi hivyo?"
"Je, wewe unapendana na kaka Deo?"
Wifi akacheka sana na kuniambia.
"Ndoa ni uvumilivu na kabla hujaolewa unatakiwa kuwa makini na mtu anayetaka kukuoa ili usijekujutia mbele ya safari"
Nilimuangalia wifi na kutafakari maneno yake aliyoyasema kwani hakunijibu swali langu kama anapendana na kaka Deo au la. Nikamuuliza tena,
"Kwani ni kitu gani kinaweza kufanya mtu uamini kuwa unapendwa?"
"Siku zote mtu anayekupenda anakuwa karibu yako, anakujali na kuwa bega kwa bega na wewe katika huzuni na furaha"
"Utajuaje sasa kama Sam bado ananipenda?"
"Atakuwa anakupenda ndiomana hakati tamaa kwako, usiache kumsikiliza maana watu wenye kupenda kweli siku hizi wamepotea"
Tukaongea mambo mengi sana na wifi yangu.
"Unaonaje swala la mwanamke kutembea na mume wa mtu au mke wa mtu?"
"Si vizuri kwakweli, kwanza kabisa fikiria je ukiwa ni wewe unafanyiwa kitendo hicho je utajisikiaje? Yani wewe ndio uwe mke halafu mumeo anamwanamke nje utajisikiaje? Kwakweli inauma sana tena sana"
"Na vipi mwanaume kutembea na mke wa mtu?"
"Nayo inauma pia kama ya mwanzo tu ila je umefikiria nini kuniuliza hivyo?"
"Hakuna kitu nimeuliza tu wifi yangu"
Muda wa kwenda kwenye kwaya ukawadia ila leo wifi hakujisikia kwenda, sikujua ni kwanini ila hakujisikia.
Jioni yake tukatembelewa na mgeni ambaye alikuwa ni James, mwalimu wa kwaya anayoimba wifi. Baada ya salamu akaanza kumtania wifi http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Sijakuona mazoezini leo nini tatizo au hali imeanza kuwa mbaya?"
Huku akishika shika tumbo la wifi lililokuwa kubwa sana sababu ya ujauzito, wifi nae alikuwa akitabasamu na kufurahi.
"Nimepatwa na uvivu leo, na wewe kutokuniona siku moja tu ndio hadi uje kuniulizia?"
"Ndio, lazima nije ili nijue hali yako ndio mapendo yalivyo"
Wifi alionekana mwenyefuraha sana kuzungumza na James hadi pale alipoaga na kuondoka.
Kaka aliporudi alikuta wifi ameshalala kwani kaka alichelewa sana leo, na mimi nikaenda kulala baada ya kumsalimia.
Nilipokuwa chumbani nikapata wazo la kumpigia Suzy simu ila kumuuliza vizuri kwani nilihisi huenda hasira zake zimepungua.
"Suzy shoga yangu, sikuwa na nia mbaya kukuuliza kama kweli unatembea na mume wa mtu"
"Nia yako ni nini sas?"
"Nia yangu ni kukutahadharisha tu, mume wa mtu sumu jihadhari sana shoga yangu sipendi kukuona ukiumia jamani!"
"Aliyekwambia kuwa nitaumia ni nani? Mi ni mtu mzima Sabrina najua jema na baya kwahiyo usiwe na shaka kuhusu mimi"
"Ila kama mimi ningekuwa ni wewe basi ningeachana na huyo mbaba"
"Simwachi ng'ooo ananisaidia sana, kwanza familia yake hainihusu yeye ndio ananihusu"
"Mmmh haya shoga yangu ila kuwa makini sana"
"Kuwa makini wewe na mambo yako, me acha nifurahie maisha"
Akakata simu, nikatambua kuwa Suzy hapendi kuongelea zile habari za mume wa mtu kwahiyo nikaachana nae na kulala kwani sikupenda malumbano katika mambo yasiyonihusu.
Nilipokuwa nimelala nikajiwa na ndoto kuhusu Suzy.
Nikamuona Suzy yupo baa na mbaba flani, baada ya muda wakainuka na kwenda nyumba ya kulala wageni wakachukua chumba kimoja chenye kila kitu ndani, ilikuwa kamavile naangalia video jinsi nilivyokuwa nawaona kwenye ndoto.
Wakiwa kwenye kile chumba, mara kuna watu wakagonga hodi halafu yule mbaba akaenda kufungua gafla wakaingia wamama watatu waliojazia sana wakamsukuma yule baba pembeni na kumfata Suzy aliyekuwa kitandani kisha wakampiga mfululizo na kumvuta hadi nje, nikamuona mama mmoja akichukua gongo na kutaka kumbamiza nalo Suzy kichwani.
Nikastuka na kupiga kelele,
"Usimpigeeeeeee...."
Kelele zile ziliwashtua wifi na kaka ambao walikuja haraka chumbani kwangu kuniulizia kuna nini na kunikuta machozi yakinitoka kama mimi vile niliyekuwa napigwa kwenye ndoto, hata sikujielewa.
Wifi akafanyakazi ya kunipooza kuwa ni ndoto tu na haina maana yoyote ile kwenye maisha yangu kwahiyo nisiwe na wasiwasi wala mashaka yoyote kuwa itatokea kwani ni ndoto tu.
Baada ya kutulia wifi akaondoka na mimi nikarudi tena kulala, safari hii nikamuona Suzy akiwa hospitali amelazwa huku akionekana kuwa na majeraha mwili mzima, wakati namshangaa na kusikitika kuhusu Suzy akatokea Carlos pembeni yangu huku akitabasamu na kuniambia.
"Nilikwambia Sabrina, mwambie rafiki yako ajihadhari si unaona sasa!"
Nikastuka tena na kujiuliza, kwani hii ni kweli au ndoto tu? Mbona matukio yake yananitisha, nikatafakari sana mara mlio wa ujumbe mfupi ukaita kwenye simu yangu, kuangalia umetoka kwa Carlos.
"Naomba badae tuonane, kuna kitu muhimu nataka kukwambia"
Nikashangaa kuona Carlos kanitumia ujumbe usiku ule, kuangalia saa ilikuwa tayari kumekucha kwani ilikuwa ni saa mbili asubuhi, ikabidi tu niamke na kutoka chumbani ili nikamsaidie wifi baadhi ya kazi kidogo.
Niliporudi tena chumbani kwangu, nikachukua simu na kumpigia Suzy ili kujua hali yake ila simu haikupokelewa, nikaamua kumpigia mama ili kujua hali ya mama Salome hospitali kuwa anaendeleaje maana tangu nilipoondoka sijaulizia.
"Kwakweli anaendelea vizuri tunamshukuru Mungu kwa hilo, tatizo amepararaizi upande mmoja"
"Hivi aliyemgonga mlimpata kweli?"
"Nasikia alikimbia na hata hajulikani alipo"
Nikaishia kuguna tu, ujumbe tena ukaingia kwenye simu yangu na alikuwa Carlos tena aliyenielekeza pa kumkuta.
Nikawa napanga jinsi ya kumuaga wifi, ila kwa bahati wifi akatembelewa tena na mwalimu wa kwaya ila leo aliongozana na mwanakwaya mwingine nikatumia nafasi hiyo kumuaga wifi kuwa kuna mahali naenda mara moja ila sikumwambia kama naenda kuonana na Carlos.
Nilifika eneo alilonielekeza Carlos na kumkuta, baada ya salamu nikaanza kuzungumza nae.
"Unakumbuka nilipokwambia kuhusu rafiki yako Suzy na mume wa mtu?"
"Ndio nakumbuka?"
"Je, ulichukua hatua gani?"
Nikamueleza jinsi nilivyomuuliza Suzy na yote niliyomwambia.
"Unajua kwanini wifi yako anasema kuwa mimi sio mtu wa kawaida?"
"Sijui"
"Kwasababu naijua siri yake, kuna siri kubwa sana katika ujauzito alionao"
Nikaanza kujiuliza kuwa ni siri gani hiyo, kisha nikamuuliza ili anijibu.
Ila kabla hajanijibu simu yangu ikaanza kuita, kuangalia mpigaji ni mama yake Suzy. Nikashtuka kwani hana kawaida ya kunipigia.
Nikaipokea ile simu, mama Suzy alikuwa anaongea kwa kilio kikubwa.
"Sabrina, Sabrina rafiki yako mwanangu mimi mwanangu...."
Kilio cha mama Suzy kilipasua moyo wangu kwa uoga wa kupewa habari mbaya.
Kilio cha mama Suzy kilipasua moyo wangu kwa uoga wa kupewa habari mbaya.
Nikaendelea kumsikiliza mama Suzy huku uoga mwingi umenishika ila mama Suzy hakuweza kuongea zaidi ya kulia kisha ile simu ikakatika.
Nikageuka kumtazama Carlos aliyekuwa amekaa kimya kabisa bila ya kuniuliza chochote nadhani alikuwa anangoja mimi ndio nianze kumuuliza ila alipoona namuangalia tu akaamua kuniuliza kuwa kuna nini, nami nikaamua kumjibu.
"Sijui rafiki yangu Suzy kapatwa na nini maana mama yake analia tu kwenye simu"
"Wewe unafikiriaje?"
"Sijui kwakweli, sijui amekufa"
Nikaanza kutokwa na machozi, kisha Carlos akanivuta karibu yake na kuweka kichwa changu kifuani mwake kama ishara ya kunibembeleza ila nilihisi kuna vitu vinatembea mwilini mwangu na kujitoa kwenye mikono ya Carlos, kisha akaniuliza.
"Kwani wewe unatakaje?"
"Sitaki rafiki yangu afe"
"Kwanini?"
Nikamuangalia Carlos na kumshangaa kuwa ni swali gani lile la kuniuliza, kisha nikamjibu.
"Sababu nampenda sana"
"Unampenda sana kupita Sam?"
Nikamuangalia kwa hasira sasa na kumjibu kwa ukali,
"Swali gani hilo unaloniuliza? Sina muda wa kujibu maswali yako"
Nikaendelea kutokwa na machozi, kisha Carlos akatoa leso na kunikabidhi ili nifutie machozi kisha akaniuliza tena,
"Kweli hutaki Suzy afe?"
Nikamuangalia sana Carlos kwani sikuona umuhimu wa maswali aliyoniuliza na sikuona msaada wake kwahiyo sikumjibu.
Nikachukua simu ili niangalie salio kisha niwapigie ndugu zake Suzy waweze kuniambia vizuri kuhusu Suzy, ila Carlos akanishika mkono na kunikataza kupiga simu na mimi nikamuuliza kuwa anamaana gani kuni kataza,
"Niambie kwanza, je hutaki Suzy afe?"
Ikabidi nimjibu ili aridhike kujibiwa.
"Ndio sitaki afe"
"Basi mimi nitakusaidia"
"Kivipi?"
"Wewe amini ju kuwa nitakusaidia tu"
Nikamuangalia kisha kumuuliza.
"Na mbona umenizuia kupiga simu?"
"Kama unahitaji msaada wangu na huhitaji rafiki yako Suzy afe basi fata ninachokwambia"
"Kwanini?"
"Usiwapigie wakina Suzy simu hadi watakapokupigia wenyewe kama kweli hutaki Suzy afe"
Nikamuangalia tu Carlos kwa mshangao kwani alikuwa ni mtu wa ajabu sana kwangu, kisha akaniaga na kuniambia kuwa atakuja badae kunitembelea tena ila nikamshangaa kwani muda ulienda sana na giza lilishaanza kuingia, nikashangaa kusikia atakuja badae na kujiuliza mwenyewe kuwa hiyo badae ni badae gani, kisha akaniomba nipande kwenye gari yake ili anipeleke karibu zaidi na nyumbani kwa kaka ndio aondoke. Nikapanda kwenye gari yake huku mawazo mengi kichwani yakinitawala, nilipofika karibu nikamwambia anishushe ili wifi asinione nilipotokea.
Kabla ya kushuka Carlos akaniambia tena.
"Usiwapigie simu ndugu wa Suzy hadi watakapo kupigia wenyewe, weka akilini na ukumbuke hilo muda wote"
Kisha nikashuka naye akaondoka, maswali mengi sana nikajiuliza bila ya kupata majibu.
Nikaingia ndani na kumkuta wifi amejilaza kwenye kochi.
"Kheee Sabrina tangia umeondoka ndio unarudi muda huu! Umepata marafiki gani huku?"
Nikamsogelea wifi na kumuuliza polepole.
"Je kaka amesharudi?"
"Bado hajarudi au ulienda kuonana na huyo Sam?"
Nikamuangalia wifi na kutabasamu ili kumpotezea anachoniuliza na kuanza kumwambia mambo mengine kabisa yasiyohusiano.
Tuliongea kidogo na kaka nae akawa amewasili, kisha akamfata mkewe alipo na kumshikashika tumbo lake halafu akasema.
"Atakuja lini huyu? Nina hamu nae"
Wifi akatabasamu kwa furaha na kumjibu.
"Atakuja tu muda wake ukiwadia na utacheza nae hadi uchoke"
Kaka nae akatabasamu kwa furaha, kisha akanigeukia na kuniambia,
"Otea Sabrina, eti atakuwa mtoto gani?"
"Mi nadhani atakuwa wa kiume kaka"
Wifi akainuka na kukaa kisha akajibu,
"Huyu ni wakike nyie sema hamjui tu"
Kaka nae akasema.
"Ni wakiume bhana, Sabrina yupo sahihi. Kwani mke wangu hutaki kuzaa dume?"
"Nataka sana"
"Sasa mbona unadai huyo ni wakike"
"Huyu ni wakike ndio mume wangu, nataka awe ananisaidia kazi hapa nyumbani"
Tukabaki kucheka tu na kaka maana mtoto anapangiwa majukumu akiwa tumboni.
Tukaongea mengi na kula kisha kupumzika na kwenda kulala. Nashukuru maongezi yale yalinisaidia kupotezea mawazo ya kumpigia Suzy.
Nikiwa chumbani kwangu, mawazo juu ya Suzy yakanitembelea kichwani nikatamani kuchukua simu kupiga ila nikasita kufanya hivyo. Mara simu yangu ikaanza kuita, kuangalia mpigaji ni Sam nikapokea kumsikiliza.
"Nasikia Suzy amepatwa na matatizo, hebu niambie kinachoendelea"
"Sijui chochote"
"Ulizia basi kwao tupate taarifa kamili"
"Kwani wewe umeambiwa na nani?"
"Aliyeniambia si wa muhimu kwasasa ndomana nikakuuliza wewe"
"Kama hutaki kuniambia aliyekwambia basi na mimi sitakwambia chochote"
"Sio muda wa marumbano huu Sabrina, nimeambiwa na Lucy tena amenidokezea tu ndomana nauliza ili nijue tatizo"
"Nilijua tu kama umeambiwa na malaya wako, sasa mwambie huyohuyo akueleze vizuri"
"Toka muda ambao Lucy aliniambia hadi sasa hapatikani, acha hasira Sabrina mambo mengine inatakiwa tushirikiane tafadhari"
Nikamsikiliza Sam kisha nikaamua kumpa moyo tu.
"Nikiongea nao nitakupa taarifa"
Kisha nikakata simu ili niweze kulala ila mawazo kuhusu Suzy yalizidi kuugusa moyo wangu na kunifanya nikose raha. Nikapitiwa na usingizi palepale.
Nikajiona nipo kwenye bustani nzuri sana, kisha akaja yule mkaka wa ndotoni na kukaa karibu yangu na kusema.
"Karibia unaingia kwenye himaya yangu Sabrina. Nitakupenda, kukujali na kukutunza"
"Ila mimi sikupendi wewe"
"Utanipenda tu Sabrina, sina sababu ya kukulazimisha bali utakubali mwenyewe kwa hiyari yako na utaolewa na mimi"
Nikashtuka na kusema kwa nguvu.
"Sitaki kuole...."
Kabla sijamaliza hayo maneno kuna kitu kiliziba mdomo wangu kama vile kuna mtu nyuma yangu halafu kaniziba mdomo kwa mkono.
Kisha nikasikia sauti ikipita sikioni mwangu kama vile mtu ananinong'oneza.
"Shiiiii usipige kelele Sabrina, kumbuka tupo ugenini wote watakuona chizi. Kwanini hupendi kunizoea?"
Nikawa nafurukuta tu pale kitandani kwani aliniziba mdomo kwa nguvu.
Nilipofanikiwa kugeuka sikuona mtu yeyote na ile mikono iliyoniziba mdomo sikuhisi tena, nikainuka haraka na kuwasha taa huku nikitetemeka sana, nikatamani niwaite wifi na kaka lakini nilisita.
Nikafungua mlango ili nitoke sebleni, nikamshangaa wifi akiwa pale sebleni akipiga maombi. Nakasimama na kumuangalia, alipomaliza akaniangalia na kusema.
"Unajisikiaje Sabrina?"
"Nipo salama tu"
"Njoo karibu yangu"
Nikamsogelea wifi ili nijue anachotaka kuniambia.
"Nilipokua chumbani kuna kitu kimeniambia kuwa kuna mapambano kwako, ndiomana nikatoka kuja kuomba hapa. Unaendeleaje lakini kwasasa?"
"Naendelea vizuri wifi"
"Kuwa makini sana mdogo wangu, nenda kalale sasa"
Nikarudi ndani na kulala hadi kulipokucha, sikupatwa na njozi yoyote ile iliyombaya nikashukuru maombi ya wifi yamenisaidia kwani maruweruwe yalitaka kunianza tena kama ilivyokuwa nyumbani.
Mchana wa siku hiyo nikiwa nimetulia pale nyumbani na wifi, mara simu yangu ikaita kuangalia mpigaji ni mama Suzy.
Nikapokea ile simu huku hofu kubwa imenitawala nikahisi kama sio habari mbaya basi nitape wa lawama tu, nikaweka simu sikioni ili kusikiliza.
"Asante sana Sabrina mwanangu, Mungu akubariki sana umetusaidi sana mwanangu"
Nikashangaa kuwa ile asante ya nini kitu kilichofanya niongee kwa kigugumizi sasa.
"Aah kwani kwani ni..."
"Umetusaidia mwanangu, yule kijana uliyemtuma jana ametusaidia sana. Kwasasa Suzy anaendelea vizuri na yupo hospitali kwaajili ya matibabu mengine."
"Sawa mama nashukuru kwa taarifa"
"Umwambie yule kijana tunashukuru sana"
Kisha akakata simu, maswali mengi nikajiuliza huyo kijana ni kijana gani niliyemtuma mimi na je amewasaidiaje wakina Suzy bado sikupata jibu, na je Suzy alipatwa na nini haswaa bado sikupata jibu. Nikabaki kujiinamia tu ila nikapata wazo la kumpi gia simu Lucy ili anipe taarifa kamili, ingawa sikutaka kuongea na Lucy ila ilinibidi ili kuijua hali ya Suzy.
"Niambie Lucy, kwani Suzy amefanyaje?"
"Mmh leo umenipigia simu! Kweli Mungu ashukuriwe"
"Niambie bhana Lucy, mambo mengine achana nayo"
"Nitakwambia kwa kifupi tu, kwakweli hali ya Suzy ilikuwa mbaya sana kuna watu walimpiga na kumtegeshea nyoka. Bila Carlos tungeongea mengine sasa, kwakweli Carlos ametusaidia sana hadi Suzy anapumua sasa na kuendelea vizuri kwa msaada wa Carlos"
"Sasa Carlos alimsaidiaje?"
"Tukionana nitakwambia vizuri Sabrina."
Bado akaniacha na maswali mengi tu bila ya majibu yoyote, ikabidi nimngoje Carlos akiwasili ili anijibu maswali yangu kwani yeye ndio atakuwa na majibu ya maswali yangu yote.Nikarudi kukaa na kuzungumza na wifi mambo mbalimbali kisha akaniomba nimsindikize kwenye kwaya kama kawaida.
Wakati tunaenda, tukampitia na yule mwalimu wa kwaya ili twende wote.
Wakati namsubiria wifi amalize mazoezi yake, ukaingia ujumbe kwenye simu yangu kutoka kwa Carlos akiniomba kuwa nikutane nae nilipokutana nae jana yake.
Nikainuka na kwenda kumuaga wifi kuwa kuna mahali naenda mara moja.
"Ila usichelewe kama jana"
"Nakuahidi wifi leo sichelewi"
Nikaondoka na kumuacha wifi akiendelea na mazoezi yake ya kwaya.
Kufika alipo Carlos nikamkuta akiwa makini kabisa kuningoja, jambo la kwanza ni kumuuliza kuhusu Suzy.
"Eeh niambie, ulitoa msaada gani kwakina Suzy jana?"
"Achana na habari hizo Sabrina hebu tuongee mambo ya maana sasa. Haya wifi yako umemuacha wapi?"
"Kwenye kwaya"
Carlos akacheka sana tena sana.
"Je, unataka nikwambie siri aliyonayo wifi ya ko kuhusu ule ujauzito wake?"
"Ndio niambie"
"Wifi yako ananichukia kwasababu kubwa moja tu, mi ni mtu wa kawaida tofauti na yeye anavyosema. Ngoja nikupe siri yake sasa."
Nikamuangalia Carlos kwa makini kisha nikamwambia.
"Niambie sasa, mbona husemi hiyo siri?"
"Ile mimba aliyonayo wifi yako si ya kaka yako"
Nikabaki kumshangaa Carlos kwani sikumuelewa, moja kwa moja nikajiuliza, kama mimba si ya kaka je ni ya nani? Na huyu Carlos amejuaje!
Moja kwa moja nikajiuliza, kama mimba si ya kaka je ni ya nani? Na huyu Carlos amejuaje!
Nikamuangalia vizuri ili kumdadisi maneno yake, Carlos nae alikuwa akiniangalia kwa makini kabisa nadhani alikuwa akicheza na akili yangu. Mara akasema,
"Najua unajiuliza maswali mengi Sabrina juu ya hili swala ila ukinisikiliza kwa makini utaelewa kila kitu"
"Ndio nahitaji kujua, je kaka anajua kama ile mimba si yake?"
"Kakako hajui chochote na ndomana nimekwambia kuwa ni siri, wifi yako ameitunza kwa muda mrefu sasa na hafikirii kama kuna mtu wa kuijua siri hii"
"Wewe umejuaje sasa?"
"Nina upeo mpana tofauti na unavyofikiri Sabrina, nilirithishwa na babu yangu. Niliposalimiana na wifi yako ndipo nikaijua siri hii na nikamwambia kisiri ila yeye akapiga makelele kama mtu aliyewehuka na kuongea maneno mengi ili wewe usiniamini mimi na unione ni mtu wa ajabu ila ninachokwambia mimi ni kitu cha kweli tena ni ukweli mtupu, kama huamini kamuulize wifi yako na kama akikataa mlete kwangu nimuumbue kwani ukweli wote naujua"
Maneno ya Carlos yakafanya nifikirie sana kwani nilikuwa siamini ingawa Carlos amekuwa akiniambia mambo mengi ya kweli.
"Ila je ile mimba ni ya nani?"
"Unataka kumjua Sabrina? Na ukimjua je utachukua hatua gani?"
"Kwakweli sijui, tena sijui kabisa hatua ya kuchukua ila lazima wifi nimuulize kuhusu hilo jambo"
"Muulize tu halafu upime maneno yangu, huwa siongopi mimi hata siku moja"
Nikamuangalia sana Carlos jinsi alivyoongea kwa kujiamini kabisa tena akionekana ni mtu mwenye uhakika wa kitu anachosema.
"Basi niambie kabisa kuwa ile mimba ni ya nani?"
"Nenda ukamuulize kwanza wifi yako, akikataa ndio nikutajie mwenyewe ile mimba kuwa ni ya nani"
"Tutaonana lini sasa tena?"
"Kesho, nitakuja tena hapahapa"
Nikakubaliana na Carlos kisha kuagana na kuondoka.
Nikaamua kurudi kule kwenye kwaya ili niungane na wifi kurudi nyumbani ila sikumkuta ikabidi nifanye safari ya kwenda nyumbani nako nikakuta mlango umefungwa kwa maana kwamba wifi alikuwa bado hajarudi, ikabidi nimngoje pale nje.
Baada ya muda wifi alirudi akiwa amesindikizwa na yule mwalimu wa kwaya na kunikuta pale nje moja kwa moja wifi alianza kuongea.
"Yani Sabrina umeniudhi leo balaa, kwanini hukuniambia mapema kama utachelewa kiasi hiki? Umefanya nikungoje muda wote kuwa utarejea, kwanini lakini?"
Nikamuangalia wifi bila ya kusema chochote.
Alikuwa akiongea huku akifungua mlango, kisha tukaingia ndani na yule mwalimu akaaga na kuondoka.
Wifi hakuacha kunisema hata tulipokuwa ndani akidai kuwa nimempotezea muda wake akiningoja kule kwenye kwaya.
"Nadhani itakuwa vyema nikimwambia kaka yako kuhusu hili, umenikera sana. Au nimwambie tu kakako?"
Mara kaka alikuwa amewasili na kusikia vile ambavyo wifi alikuwa akifoka,
"Kuniambia nini tena? Kwani tatizo ni nini?"
Wifi akagelesha kwa hilo na kusema.
"Hapana bhana, nilikuwa naongea na Sabrina kuwa mtoto atakayezaliwa kama akiwa wakike basi tumuite Sabrina, yeye akawa anaogopa kuwa wewe hutokubali ndio nikamwambia kuwa au nikwambie wewe"
Maneno ya wifi yaliweza kumlainisha kaka na akakubali kuwa ndio ilivyokuwa.
"Usiogope Sabrina, wifi yako amekupenda sana ndomana anachagua jina lako"
Nikatabasamu tu ili kisieleweke chochote kwani wifi aliniokoa kwa lile maana kaka angejua kuwa kuna mahali nilienda ingekuwa shida.
Tukapika na kula ila sikuweza kumuuliza chochote wifi kwani niliogopa pa kuanzia ukizingatia kaka yupo.
Muda wa kulala nikaenda zangu chumbani na kulala.
Nilipokuwa kitandani maswali mengi sana nilijiuliza na kusema kuwa lazima nimuulize wifi kuhusu kitu nilichoambiwa na Carlos.
Mara Sam akanipigia simu, nami nikapokea na kuongea nae.
"Nasikia ulimuagiza Carlos aende kwa wakina Suzy kuwasaidia. Naomba nikuulize kitu Sabrina"
"Uliza"
"Je, huwa unaonana na Carlos huko?"
"Ndio, kwani kunatatizo?"
"Hamna tatizo nimeuliza tu, Carlos ulimpigia simu muda gani kumwambia kuwa wakina Suzy wapo khatarini?"
"Muda nilipopewa taarifa kwani nilikuwa naongea nae muda huo huo"
"Kuwa mwangalifu Sabrina sababu Carlos sio kama unavyomuona. Simjui Carlos ila namuona kama kikwazo kwenye maisha yetu"
"Kwani Carlos rafiki yako au rafiki yangu?"
"Ni rafiki yako wewe Sabrina ila mimi kama mpenzi wako nina haki ya kukwambia rafiki bora na mbaya"
"Hayo mapenzi mimi na wewe yalishaisha Sam nenda tu ukaendelee na Lucy wako"
"Ilimradi najua na kutambua kuwa hakuna chochote kinachoendelea kati yangu na Lucy basi sitaacha kukufatilia wewe Sabrina hadi mwisho wangu"
"Unajisumbua tu kwa sasa"
"Na sitaacha kujisumbua kwa mtu nimpendaye, najua umevurugwa tu kwasasa"
"Nani kavurugwa?"
"Wewe hapo umevurugwa Sabrina"
"Umevurugwa mwenyewe"
Nikakata simu kwani alikuwa akinizidishia hasira tu, ila nikatafakari sana na kuona kweli Sam ananipenda. Nikachukua simu yangu na kumtumia Sam ujumbe mfupi wa maneno.
"Asante kwa kunipenda Sam, nitakupenda daima"
Kisha nilala baada ya kutuma ujumbe huo, kwenye ndoto nikamuona Sam na Lucy wakiwa pamoja na kufurahi sana, mimi nilikuwa pembeni kuangalia jinsi wanavyofurahia mapenzi yao huku roho ikiniuma sana kutokana na wivu, kisha nikawaona ndugu wa Sam na ndugu wa Lucy wakiwa pamoja kama vile watu wanaojuana sana halafu nikamuona Sam akimvisha pete Lucy, hapo nikashtuka na kusema kwa nguvu.
"Noooooo...."
Nikaamka na kugundua kuwa ni ndoto tu, nikachukua simu yangu ili nimpigie Sam kumwambia nilivyoota.
Nikakuta ujumbe kwenye simu yangu kutoka kwa Sam umeandikwa,
"Usijali mpenzi nakupenda sana Lucy wangu"
Hapo mapigo ya moyo yakaanza kunienda kwa kasi na machozi kunidondoka. Nikajiuliza nitaumia hadi lini kwaajili ya Sam? Kwanini anitese kiasi hiki halafu bado anadai kunipenda? Roho iliniuma sana, nikaghairi kumpigia tena Sam na usingizi sikupata sababu ya mawazo na machozi yaliyonitoka mfululizo hadi kunakucha sikuwa na raha yoyote.
Siku ya leo sikuwa na raha kabisa kwani nilijihisi mpweke na uchovu mwaingi huku nikitamani kumuuliza wifi kuhusu mimba yake ila sikujua ni wapi pa kuanzia kumuuliza. Nikabaki kumtazama tu kwa yote aliyokuwa akiyafanya.
Muda ulipotulia nilikaa na wifi huku tukitaniana akaanza tena kuniambia kuhusu jina la mtoo atakayezaliwa.
"Yani huyu mwanangu lazima nitamuita Sabrina"
"Hata kama wa kiume?"
"Wakike huyu, mbona unapenda kung'ang'ania jambo moja? Mimi ndio mama wa huyu mtoto na nimekwambia kuwea ni wa kiume"
"Sawa wifi, kuna swali nataka kukuuliza"
"Uliza tu, kuwa huru Sabrina"
Nikasita kidogo kwani swali langu lilikuwa na utata na sikujua wifi angelipokeaje swali lile.
"Mbona huulizi? Nipo makini hapa kukusikiliza ujue!"
Nikapumua kidogo kabla ya kuuliza swali langu. Nikaamua kutafuta njia ya kuuliza kwa urahisi nitakacho kujua.
"Wifi unadhani mtoto atakayezaliwa atafanana na nani?"
"Mmmh! Asipofanana na wewe basi atafanana na kaka yako"
"Kwanini wifi?"
"Kwanini tena?? Si kwasababu ni damu yenu"
Hapo ndipo nikabadilika na kumwambia kuwa wifi ni muongo.
"Muongo wifi"
"Mimi muongo? Uongo wangu uko wapi?"
Sasa nikapata ujasiri wa kumwambia na wifi akachukizwa sana.
"Hiyo sio damu yetu maana hiyo mimba sio ya kaka"
"Unasemaje Sabrina? Kama mimba hii sio ya kaka yako ni ya nani sasa? Wewe mtoto vipi umetumwa nini nyumba imekushinda hii eeh! Kukupenda kote Sabrina bado unanizulia maneno! Kweli binadamu wabaya"
Wifi aliongea maneno mengi bila hata ya kupumzika na akanichukia gafla.
"Sema sas, kama hii mimba si ya kaka yako ni ya nani?'
Nikabaki kutoa mimacho kwavile sikujua mimba ni ya nani.
Tangia hapo wifi hakutaka tena kuongea na mimi hata kwenye kwaya leo alienda peke yake nami nikabaki nyumbani.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikiwa mwenyewe nyumbani nikapigiwa simu na Carlos ambaye alihitaji kuonana na mimi, na kwa vile mimi nilitaka kuonana na yeye kwa sana nikamwambia aje pale nyumbani kwa kaka kwani wote hawapo na pia nahitaji kuzungumza nae.
Hakuchukua muda sana alikuwa ameshawasili pale kwa kaka, nikamkaribisha na kuzungumza nae.
"Wifi yangu amekataa kabisa na kunichukia"
"Nilijua hilo kabla ndiomana leo nimekuja"
"Sasa utanisaidiaje kwa hilo?"
"Wifi yako anadhani unakisia tu na huujui ukweli ndomana anakufanyia ukali ili usitambue kabisa kinachoendelea, sasa mimi nakutajia mtu aliyempa ujauzito wifi yako. Ukipata muda wa kumwambia mwambie tu halafu utaona kitakachoendelea"
"Niambie basi ile mimba ni ya nani?"
"Ile mimba ni ya kijana flani anaitwa James, mwambie wifi yako hivyo ataelewa halafu akigoma kukwambia ukweli nijulishe mimi nitakwambia kila kitu ilivyokuwa"
Kwakweli hakuna mtu aliyekuwa akinishangaza kama huyu Carlos kwani aliongea mambo mengi kwa kujiamini kisha akaniaga na kuondoka.
Nilitulia ndani nikimngoja wifi arudi huku hamu yangu ikiwa moja tu nayo ni kuujua ukweli wa mambo.
Kama kawaida wifi alirudishwa pale nyumbani na mwalimu wa kwaya kisha mwalimu huyo akaondoka,. Nilikaa na wifi ila hakunichangamkia tena halafu alionekana kuwa na hasira sana ila sikutaka kuacha kumwambia ukweli.
Nikamsogelea wifi na kumwambia,
"Hiyo mimba si ya kaka, ni mimba ya James"
Mara wifi akaanguka chini na kuanza kutapatapa kama mtu mwenye kifafa.
Mara wifi akaanguka chini na kuanza kutapatapa kama mtu mwenye kifafa.
Hofu ikatawala ndani yangu, nikaogopa sana kwani sikujua cha kufanya kwa wakati huo na sikujua ni kitu gani kimempata wifi yangu.
Wakati nahangaika pale chini na wifi huku nikimuamsha kwa kumtaja jina, kaka alikuwa amewasili na kukimbilia pale chini nilipokuwa na wifi.
"Vipi tena Sabrina, wifi yako kafanyaje?"
"Hata mi sijui, ameanguka gafla tu na kuanza kutapatapa"
Nikaogopa kumweleza kaka jambo lolote huku nikihofia kuwa kaka ataniona mimi mbaya.
Kaka akamnyanyua wifi na kwenda kumpakiza kwenye gari yake ili kumpeleka hospitali, bora kaka yangu ni mwenye nguvu maana mi mwenyewe nisingeweza kumbeba wifi na ile mimba.
Kisha nami nikapanda kwenye gari kwa lengo la kumpeleka wifi hospitali.
Kufika hospitali, wifi alikimbizwa moja kwa moja kwa daktari. Nilitulia kusikilizia kinachoendelea mara kaka akanifata na kuniambia kuwa nirudi nyumbani ili niandae vitu vya wifi kama khanga na vitenge na nguo, akanikodia gari.
Nami nikaondoka na kurudi nyumbani nikajua tu kuwa wifi atakuwa anataka kujifungua ndiomana wanahitaji hivyo vitu.
Nilifika na kuandaa kila kitu, nikaona karatasi iliyokunjwa vizuri kwenye kabati la kaka ila kabla sijafungua kaka alikuwa amewasili ikabidi nimkabidhi zile nguo na kumuuliza.
"Kwani wifi anaendeleaje?"
"Anaendelea vizuri ila ni kifafa cha uzazi kinamsumbua, tumuombe tu Mungu ili ajifungue salama maana kifafa kibaya sana"
"Basi unipe taarifa za huko kaka, uwe unanipigia simu"
"Hakuna tatizo, nimeshamtaarifu na mama kwahiyo atakuja hospitali. Wewe baki tu mdogo wangu kila kitu kitakuwa sawa, Mungu atasaidia"
Basi kaka akaondoka na kuniacha pale nyumbani, hamu ya kujua kilichoandikwa kwenye kile kikaratasi ilinijaa, nilitamani kujua maneno yaliyomo.
Nikaenda na kukichukua, kiliandikwa hivi:
"Nampenda sana mke wangu Joy, namuamini kuliko chochote duniani eeh Mungu nashukuru kwa kunipa mke muaminifu kama Joy"
Nikakisoma mara mbili mbili na kujiuliza, je ni kweli Joy ni mwaminifu? Kama ni mwaminifu mbona akabeba mimba ya mtu mwingine? Je uaminifu wake umepimwa kwa yapi?
Yote hayo ni mapenzi yao na sikutakiwa kuyaingilia ila je nitakaa kimya bila ya kusema ukweli? Maswali mengi nilijiuliza bila majibu, nikaamua kurudi chumbani kwangu huku nikiendelea na mawazo yangu hadi muda wa kulala ulipofika.
Nilipokuwa nimelala nilimuona wifi akijifungua mtoto mzuri sana wa kiume.
Nikashtuka na kutabasamu na kujisemea kuwa kumbe mawazo yangu yalikuwa kweli kuwa wifi atajifungua mtoto wa kiume, ila kuangalia vizuri ilikuwa ni ndoto sema siku hizi nimeanza kuziamini ndoto zangu, nikawa nangoja kukuche ili nipate uthibitisho wa ndoto yangu.
Asubuhi na mapema kaka aliwasili sababu alilala hukohuko hospitali kwaajili ya mke wake.
"Wifi anaendeleaje kaka?"
"Anaendelea vizuri sana, amejifungua mtoto wa kiume saa kumi na mbili asubuhi"
Nikafurahi sana,
"Ndio umuandaliage uji na kila kitu naenda kumchukua hivyo, nitarudi hapa na mama"
"Yupo hospitali na yeye?"
"Ndio yupo, nitarudi nae hapa"
Nikawa nangoja kwa hamu hata yale mawazo mengine kuhusu wifi yakapotea.
Nikaandaa uji kama nilivyozoea kuandaa kwani sikuzoea uji wa mzazi unatiwa nini.
Wakati naandaa uji, simu yangu ikaita na mpigaji alikuwa Carlos.
"Nini tatizo Carlos?"
"Nakusalimia tu, utampa jina gani mtoto wa wifi yako?"
"Mmh! Sijui, kwani umejua kama kajifungua?"
"Ndio najua, tena mtoto wa kiume"
Nikaishia kuguna kuwa huyu Carlos licha ya kuwa na upeo mkubwa basi atakuwa na upeo tofauti na wengine.
Nikakata ile simu ila akanitumia ujumbe mfupi wa maneno.
"Fikiria jina la kumpa mtoto wa wifi yako kwamaana wewe ndiye umeteuliwa kutoa jina"
Nikaanza kujifikiria sasa kuwa mwanzoni kabla wifi hajajifungua nilimwambia kuwa kama akijifungua mtoto wa kiume basi tutamuita "James" ila kwa sasa jina hilto lilinipa utata na nikashindwa kufikiria zaidi kwani ndio jina la kweli la baba wa mtoto.
Baada ya muda waliwasili nyumbani wifi, mama na kaka.
Mtoto alikuwa mzuri sana tena alichangamka na alipendeza kumuangalia, mama alienda kumuweka vizuri wifi, mimi na kaka tulibaki na mtoto.
Muda wote kaka alitabasamu huku akisema.
"Dah dume langu hilo"
Nilimwangalia tu kaka bila ya kusema chochote kwani nilihofia kwamba nitaanzia wapi kusema ukweli.
Mchana wa siku hiyo mambo yakawa shwari kabisa, wifi alitulia huku akimnyonyesha mtoto wake, mama nae alitulia pembeni na kaka yani kila mmoja alikuwa na hamu ya kumbeba mtoto ukizingatia mtoto mdogo anavutia sana.
Kaka akamuuliza mama,
"Mama eti tumuite nani?"
"Mi sijui, wazazi ndio muamue"
"Basi mdogo wangu Sabrina achague jina la kumpa mtoto"
"Mmh kaka mchagulie mwenyewe tu"
"Mi ningempa jina la mtu wangu wa karibu ila kwavile toka mwanzo wifi yako alitaka mtoto aitwe jina lako kama akiwa wakike basi ni wakiume na utatakiwa wewe utaje jina la kumpa"
"Kuna jina nilichagua kabla labda mmuulize wifi kama litafaa maana mimi nimelisahau"
Ikabidi kaka amuulize wifi
kuhusu hilo jina.
"Mmh hata mimi nimelisahau"
"Basi hilo jina litakuwa ni zuri, ukilikumbuka Sabrina ututajie tena"
Yani kaka alikuwa na furaha iliyopitiliza kwa yeye kupata mtoto tena mtoto wakiume.
Watu mbalimbali walianza kufika na kumuangalia mtoto huku wakimsifia kuwa mtoto ni mzuri sana na kumpa hongera wifi na kaka.
Moyo ulikuwa waniuma kila nikimsikia wifi akisifia kuwa mtoto kafanana na baba yake kwani sikuelewa anamaanisha kaka yangu au huyo James.
"Yani huyu mtoto mtundu kama baba yake, ona na macho yake ni baba yake mtupu"
Nilikuwa nikimuangalia tu na kukosa cha kufanya, kaka alikuwa akifurahia muda wote hata hakwenda mahali popote leo akimshuhudia mtoto aliyejua kuwa ni mwanae.
Ilipita wiki nzima bila ya mimi kutaja jina la kumpa mtoto, ikabidi kaka ampe jina lingine.
"Napendekeza huyu mtoto aitwe James"
Wifi akashtuka sana na kuropoka
"Kwanini asiitwe Deo?"
Kaka akacheka,
"Aitwe Deo kivipi? Itakuwaje mtoto Deo na baba Deo? Kwahiyo atakuwa Deo Deo! Mmh hata haipendezi"
Kisha kaka akanigeukia mimi na kuniuliza.
"Eti Sabrina hebu ona eti Deo Deo ndio nini? Itapendeza kweli!"
Nikaishia kucheka tu, kisha kaka akaendelea
"James Deo ndio itapendeza sio Deo Deo bhana"
Nikaguna na kujisemea moyoni je James James inakuwaje? Nikaishia na swali langu moyoni.
Wifi alikuwa kimya kabisa akitusikiliza kisa na yeye akaamua kumuuliza kaka.
"Kwanini umechagua jina hilo mume wangu?"
"Kwanza ni zuri, pili nina jamaa yangu anaitwa James dah ana roho nzuri sana. Ni mpole na mcheshi"
Nami nikachangia mada hapohapo.
"Hata mimi nilichagua jina hilohilo kaka"
"Kumbe mawazo yetu yanafanana, vizuri sana mdogo wangu"
Wifi alipokea jina lile kishingo upande, ni mimi tu niliyejua kwanini amenyong'onyea kwa kusikia hilo jina.
Wanakwaya wenzie walikuja kumuona mtoto wa wifi na kama kawaida watu hupenda kuanza na jina la mtoto ila wifi hakuwatajia huku akisema mtoto bado hajapewa jina.
Jioni yake nikapigiwa simu na Carlos,
"Badae nitakuja kwenu Sabrina"
"Utakuja kivipi mbona muda umeisha?"
"Nilisahau kama muda umeisha, basi nitakuja kesho"
Nikamaliza kuongea na Carlos na kuendelea kufanya mambo yangu mpaka muda wa kulala ulipowadia nikaenda kulala.
Nilipokuwa nimelala, nilihisi kuna mtu amelala pembeni yangu, uoga ukanijaa kwani niliogopa hata kugeuka huku nikihisi kuona mtu kweli nyuma yangu.
Nikahisi yule mtu akinipapasa mgongoni, hapo uoga ukawa zaidi ya mwanzo na nikatamani kupiga makelele ila sauti iliishia njiani, nikasikia kama mtu akiniambia.
"Acha uoga Sabrina, kwanini unakuwa muoga hivyo?"
Hofu ikazidi na kujibu nikashindwa, nikajikuta nikifumba macho kwa nguvu ili ile hali ipotee lakini haikupotea kwani nilihisi uwepo wa mtu kweli mgongoni mwangu.
Mara gafla mlango wa chumba changu ukafunguliwa na uwepo wa yule mtu ukapotea, hapo nilishtuka na kujifunika na shuka zaidi kwa uoga huku nikiwa nimejikunja.
Aliyeingia alikuja moja kwa moja na kunitingisha mgongoni kama kuniamsha.
"Sabrina, Sabrina"
Nilipoisikilizia ilikuwa ni sauti ya wifi Joy, hapo nikainuka na kumkumbatia.
"Una nini Sabrina?"
"Hamna kitu wifi"
"Mbona unaonyesha uoga halafu ulikuwa unaongea na nini?"
"Hakuna mtu wifi"
Akanishika mkono na kunivutia sebleni, kisha tukashikana mikono na kuniambia kuwa tuombe.
Kwakweli sikuwa muombaji mzuri kwahiyo ni wifi mwenyewe aliomba.
Baada ya maombi wifi alianza kunieleza.
"Unajua nilipokuwa nimelala chumbani, mtoto alikuwa anashtuka mara kwa mara nikajua kuna kitu tu. Unajua hawa watoto ni malaika huwa wanaona mambo mengi na vitu vingi ambavyo wakubwa hatuvioni, ndomana nikaja kukuamsha ili tusali"
"Asante wifi"
"Nenda ukalale kwa amani sasa"
Nilienda chumbani kwangu na kulala hadi kunakucha ila swala la wifi lilizidi kunichanganya kwani nilishindwa kujielewa kuwa ilikuwaje wifi hadi akamsaliti kaka, nilijiuliza sana bila ya majibu.
Siku ya leo niliamua kuvunja ukimya na kwenda kumuuliza tena wifi ili kupata ukweli ulio kamili.
Nilivizia muda ambao tulibaki wawili tu tena wakati mtoto amelala.
"Wifi niambie ukweli au unataka niseme kwa kaka?"
"Usifanye hivyo Sabrina, nihurumie wewe ni mwanamke mwenzangu"
"Hata kama mi ni mwanamke mwenzako, kumbuka mumeo ni kaka yangu wifi! Ilikuwaje hadi ukamsaliti na kwanini ulimsaliti? Hivi unajua ni kiasi gani unapendwa na kaka yangu? Yupo tayari kwa lolote kwaajili yako halafu unamsaliti kwa vazi la ulokole, mlokole gani wewe msaliti?"
"Usinitusi Sabrina, hujui nini kilitokea ni shetani tu huyu anataka kuharibu imani yangu"
Akainama akifuta machozi,
"Acha kumsingizia shetani, kwani huyo shetani hajakupeleka wewe huko kwenye mambo ya ajabu"
"Ndiomana nakwambia hujui kilichotokea mdogo wangu hujui, sikupanga wala kutaka kumsaliti kaka yako ila shetani anapitia kuvuruga watu wa Mungu"
"Nimekwambia acha kumsingizia shetani wifi unajua viapo vya ndoa wewe? Mi sijaolewa ila ninajua, hakuna mahali panaporuhusu kusalitiana."
"Mi sijamsaliti kaka yako wifi"
"Kama hujamsaliti ilikuwaje ubebe mimba ya mtu mwingine? Huo ni usaliti wifi, tena usaliti uliowazi kabisa tena huku ukiendelea kumuongopea kaka kuwa mtoto ni wake"
"Sabrina nielewe tafadhari, yaliyonipata mimi yanaweza kukupata hata wewe nihurumie wifi yangu"
"Huruma yangu kwako ni kumwambia ukweli kaka"
"Tafadhari nihurumie Sabrina, nitaenda wapi mimi? Nani atanihudumia jamani!"
"Akuhudumie huyo James, kwani anashindwa nini?"
"James hawezi kunihudumia Sabrina hawezi, nisaidie mwanamke mwenzio nateseka mimi"
Huruma ilianza kuingia moyoni mwangu ila nikamkazia.
"Msaada wangu kwako ni huo tu, kumwambia ukweli kaka Deo"
Wifi akainuka na kupiga magoti mbele yangu huku akilia. Huruma ikanijaa
"Nihurumie wifi nihurumie"
Mara kaka akarudi na kutukuta katika hali ile.
Mara kaka akarudi na kutukuta katika hali ile.
Moja kwa moja aliuliza swali.
"Kuna nini hapa?"
Wifi alishtuka na kutetemeka, sikujua ni kitu gani cha kusema wakati huo.
Wifi akajifuta machozi na kujibu kwa haraka.
"Tulikuwa tunaigiza mume wangu"
Huku akijichekelesha, kaka akabaki kushangaa na kuuliza.
"Kuigiza! Kuigiza kivipi na kuigiza gani huko mpaka machozi. Eti Sabrina?"
Kaka alinikazia macho huku wifi nae akiniangalia na kunikonyeza ili tu nikubali kuwa ni kweli.
"Ndio, tulikuwa tunaigiza kaka"
Kaka akakaa chini sasa na kuendelea kudadisi,
"Kwanza huko kuigiza mmeanza lini? Na ndio mniambie sasa hayo maigizo ni maigizo gani ya wewe Joy kumpigia magoti Sabrina tena huku ukitoa machozi na kumwambia akuhurumie"
Nadhani akili ya wifi ilifanyakazi kwa haraka sana na kupata cha kuelezea.
"Tulikuwa tunabishana hapa na Sabrina, alikuwa anasema kuwa mimi siwezi kuigiza kulia kama waigizaji wafanyavyo ndio tukawa tunajaribu hapo kuigiza kulia"
"Kwahiyo sasa umeweza?"
"Ndio hadi Sabrina kanikubali mwenyewe"
Huku akiendelea kujichekelesha kwa kujifanyisha, mara mtoto akaanza kulia.
"Nenda kamchukue mwanangu analia huko Joy, acheni ujinga wenu hapa"
Wifi akainuka na kaka akamfata, nikabaki mwenyewe nikitafakari bila ya kupata jibu la maana wala lililo kamili.
Nikiwa pale sebleni, kaka alikuja kukaa huku amemshika mtoto mikononi kisha akaongea nami.
"Unamuonaje James Sabrina, nimefanana nae eeh!"
Ikabidi niitikie tu na kumkubalia.
"Ndio unafanana nae haswaa rangi"
"Dume langu hili, dume la mbegu. Huyu ndio mwanamke bhana yani first born kaniletea dume, nimefurahi sana"
"Kwani angekuletea wa kike usingefurahi?"
"Ningefurahi ila furaha yange isingezidi niliyonayo
sasa. Kwakweli nimefurahi sasa kwasasa. Mtu unapata kipenda roho bhana"
Nikatabasamu tu huku nikitamani kumwambia kaka kuwa yule sio mtoto wake ila mdomo wangu ukasita na kujisemea kimoyomoyo kuwa kitanda hakizai haramu.
Tuliongea na kaka pale hadi muda wa kula, siku hizi alikuwa anawahi sana kurudi nyumbani tofauti na hapo mwanzoni.
Tulipomaliza kula nilienda chumbani kulala nikapigiwa simu na Sam.
"Hivi wewe mwanaume utaniacha lini mwenzio niweze kuishi kwa amani?"
"Siwezi kukuacha Sabrina sababu nakupenda, hujui tu jinsi gani unamaanisha kwenye maisha yangu"
"Porojo sitaki Sam, mtu gani wewe hadi massage za Lucy unanitumia mimi! Sikutaki Sam ingawa bado nakupenda"
Nikakata simu, muda huo huo simu ya Carlos ikaingia.
"Vipi Sabrina, naona namba busy ulikuwa unaongea na Sam"
"Ndio kwani vipi?"
"Ngoja, kesho nitakuja kukuonyesha kitu"
"Kitu gani Carlos?"
"Nitakuonyesha kesho hata usiwe na haraka"
Nikamuaga na kukata simu huku nikitafakari mambo ambayo Carlos anataka kunionyesha.
Siku ya leo nililala vizuri sana kwani hapakuwa na tatizo lolote.
Kesho yake baada ya kaka kwenda kazini nilikaa na wifi na kuzungumza nae haswaa kuhusu swala lake la kuzaa na mwanaume mwingine zaidi ya kaka.
"Ninachotaka toka kwako wifi ni unieleze ilivyokuwa hadi kufikia hatua ya kumsaliti kaka yangu"
"Kwanza kabisa naomba unielewe wifi yangu, kitu hiki sikukitarajia hata mara moja kuwa kuna siku nitamsaliti mume wangu"
"Ndio umeshamsaliti sasa, niambie tu ilikuwaje na kwanini. Pengine maneno yako yanaweza kunisaidia mimi kuificha siri hii"
"Nitakwambia kila kitu wifi yangu, na utaelewa kwanini nasema kuwa ni mipango ya shetani."
"Nakusikiliza wifi, nipo makini kuyasikia maelezo yako yote utakayoyatoa"
Wifi akatulia kwanza na kujifuta machozi yaliyokuwa yakimtoka, kisha akaanza kunielezea.
"Mimi ni mwimbaji mzuri sana wa kwaya na pia nina moyo wa huruma, huruma hiyo ndiyo iliyoniponza hadi imekuwa hivi.
Siku moja mwalimu wetu wa kwaya hakufika mazoezini halafu akatupigia simu kuwa anaumwa sana. Niliwaomba wanakwaya wenzangu kuwa twende tukamuone ila waligoma kwavile James alinipigia mimi kunitaarifu na sio wao halafu wakidai kuwa James ni mvivu wa kutembelea wenzie wakiwa wagonjwa.
Walivyogoma iliniuma sana, ingawa niliwasihi kuwa wasilipize ubaya kwa ubaya bali walipize ubaya kwa wema ila hawakunisikiliza wala kukubali na kusema labda wataenda siku nyingine.
Nikaamua kwenda mwenyewe nyumbani kwa James kuona hali yake ukizingatia anapoishi ni njiani na ninapoishi mimi.
Kufika kwa James nilimkuta amelala hoi kitandani hajiwezi kabisa akafurahi kuniona na kuniomba nikamtafutie chakula kwani hata kula alikuwa hajala, nilitoka na kwenda kumtafutia chakula na kumletea.
James alikula chakula kile hadi kukimaliza na mara gafla alichangamka sana na kuanza kuongea maneno mengi kamavile ugonjwa uliomsumbua ni njaa.
Ni hapo nilipomuuliza kuwa anatatizo gani akaniambia ni upweke unamsumbua tena huku akitoa machozi na kudai kuwa hawezi kuwa na mwanamke amtakaye sababu hana uwezo, nilimsikiliza na kumtia moyo kuwa aendelee kumwomba Mungu tu ipo siku atampatia amtakaye.
Kimya kikatawala nami nikaaga kuondoka, kabla sijainuka James alikuja na kusimama mbele yangu huku akinizuia kuwa nisiondoke.
Nikaanza kupambana nae ila James alikuwa na nguvu za ajabu na akatumia nguvu hizo kuniingilia kimwili kwa nguvu kwahiyo alinibaka. (wifi akainama na kujifuta tena machozi yaliyomtoka kama maji)
Nililia sana tena sana ila ndio hivyo nilikuwa nimeshabakwa.
Kaka yako hakuwepo kipindi hicho kwani alisafiri kikazi, nilirudi nyumbani na kulia sana huku nikitubu kwani sijui ni kwanini mimi nipitie haya yote.
Sikwenda kwenye kwaya wiki mbili kwani bado nilikuwa na uchungu wa kuonana na James ila nae alikuja kuniomba msamaha na kusema hakutarajia ila shetani alimpitia.
Baada ya muda nilijihisi mjamzito, kwenda kupima nikajikuta ni mjamzito kweli, kaka yako aliporudi tulikaa kama mwezi nikamfahamisha kuwa nina mimba yake na sikutaka aujue ukweli kwani angeniacha.
Kuhusu siri ya ujauzito huu ni mimi pekee nijuae hata James mwenyewe hajua sababu sijawahi kumwambia, huwa anadhani hii mimba ni ya mume wangu.
Kutoa nilishindwa wifi ndiomana nikaendelea kufanya siri hata sijui wewe umejuaje jamani ila naomba unisaidie Sabrina, mwanamke mwenzio mimi"
"Nimekuelewa wifi yangu, pole sana ila kama James alikufanyia vibaya hivyo mbona unapatana nae sana?"
"Sikuweza kuendelea kuwa na kinyongo nae, wakati nina mimba uwepo wake kwangu ulinivutia sana na sikuweza kumkwepa wala kumtenga Sabrina"
"Huoni kama itakuwa tatizo kama kaka akigundua jambo hili?"
"Ndiomana nakwambia nitunzie siri hii Sabrina, sina pakwenda mie. James hawezi kunihudumia"
"Ila ana haki ya kutambua uwepo wa mtoto wake"
"Tafadhari Sabrina, nisaidie mie. Deo ndio mwanaume anayeweza kunitunza na kunihudumia, James hawezi jamani nisaidie mimi"
"Ila wifi, ukweli humuweka mtu huru"
"Si ukweli kama huu Sabrina, ukweli huu utaniangamiza mimi jamani"
Kilio cha wifi kilinipa moyo wa huruma ila bado ni ngumu kwangu kuitunza siri hii tena kwa kaka yangu wa damu.
Jioni ya leo nilitulia kabisa huku nikitafakari yanayotokea na maana yake katika maisha yangu, bado sikuelewa.
"Kwanini siri hii niijue mimi na si mwingine?"
Nilikosa jibu kabisa, wakati natafakari nikapigiwa simu na Carlos na kunitaka tukutane.
Nikajiandaa na kumuaga wifi kisha nikaondoka.
Kama kawaida nilimkuta Carlos ameshawasili eneo lile akiwa na tabasamu kubwa sana. Nikasalimiana nae pale, kisha kuanza kuzungumza yaliyohitajika pale.
Kabla ya kuanza kuzungumza nikaona gari ya kaka ikipita pale karibu, nikashtuka sana kuwa kaka ataniona mara akanipigia
simu.
"Kuna mahali nakuona hapa Sabrina, ni wewe au sio?"
Nikapata kigugumizi cha kujibu na kumuangalia Carlos aliyeniambia niseme kuwa si mimi. Nikamjibu kaka kuwa si mimi ila inaonyesha kaka hakuamini maneno yangu, nikamuona akishuka kwenye gari yangu na kuja eneo nilipo kuhakikisha.
Nilikuwa natetemeka, Carlos akaniambia.
"Tulia hivyo hivyo Sabrina, hawezi kukujua huyo"
Nilizidi kutetemeka tu kadri kaka alivyosogea hata sikuelewa itakuwaje pale agundue ni mimi, nilihisi kupigwa vibao leo ila sikuweza kukimbia kwani hata nikikimbia ameshaniona.
Nilimuangalia kaka akizidi kusogea mahali nilipo na mimi nikizidi kutetemeka.
Kaka alifika hadi mbele ya mimi na Carlos akatuangalia kisha akaondoka, alipofika karibu na gari yake akanipigia tena simu.
"Kumbe nimekufananisha mdogo wangu, yani hadi sikuamini nikaenda kushuhudia mwenyewe mmh kufika pale sio wewe kabisa ni watu wengine"
"Usijali kaka"
"Uko wapi lakini muda huu"
Carlos akasema nijibu kuwa nipo nyumbani, nami nikamjibu hivyo hivyo.
"Sawa basi tutaonana badae"
"Hakuna tatizo kaka"
Nikakata simu na kupumua kidogo kisha nikamuuliza Carlos.
"Je akienda nyumbani bila kunikuta itakuwaje?"
"Kaka yako haendi nyumbani saa hizi"
"Umejuaje?" http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Nimejua tu kama haendi"
Nikaguna na kumuuliza,
"Na mbona hapa hajanitambua kama ni mimi?"
"Unajua mahali popote ukibambwa, wewe jikaushe tu yule mtu akikusogelea usionyeshe wasiwasi basi atajua tu amekufananisha"
Maneno ya Carlos niliyaamini nusu nusu.
"Haya sasa nionyeshe vitu unavyotaka kunionyesha"
Carlos akatabasamu na kuniangalia kwa makini sana kisha akaniuliza.
"Kweli unataka kuviona?"
"Ndio, nionyeshe"
"Utaweza kustahimili?"
"Nitaweza Carlos kwanini nisiweze?"
"Basi kaa tayari kuona utakacho"
Nikatulia kumsikilizia Carlos na kitu anachotaka kunionyesha, kisha akaniambia.
"Fumba macho Sabrina, usifumbue hadi nitakapokwambia ufumbue"
Nikafumba macho ila uoga ukanishika ukizingatia maneno ya watu wanaoniambia kuwa Carlos sio mtu wa kawaida.
Nikajikuta nafumbua macho kabla ya Carlos kusema nifumbue.
Ile kufumbua tu, nikayaona macho ya Carlos yakiwaka moto.
Ile kufumba tu nikayaona macho ya Carlos yakiwaka moto.
Nikashtuka sana na kujifunika usoni mwangu kwa kiganja cha mkono huku nikitaka kukimbia, Carlos alinishika mkono kwa kunizuia. Muda wote nilikuwa natetemeka.
"Acha uoga Sabrina"
"Uoga gani wakati macho yako yanawaka moto"
"Yanawaka moto! Acha uoga bhana, hebu toa mkono na ufumbue macho uone kama kweli macho yangu yanawaka moto"
Nikiwa naogopa sana na kutoa mkono usoni kwa uoga huku nikifumbua macho kwa uoga na kuogopa kumtazama Carlos huku nikihofia kuona mengine makubwa zaidi.
"Fumbua Sabrina usiogope"
Nikafumbua na kuyaona macho ya Carlos yakiwa kawaida kabisa kama ya wengine.
"Haya niambie, wapi yanawaka moto?"
Nikatikisa kichwa tu kuwa hakuna.
"Niangalie vizuri Sabrina, mimi ni mwanadamu wa kawaida kama wewe, maneno ya watu yanafanya uniogope na kufikiria mambo mengine ambayo mimi sihusiki nayo"
Nikawa namtazama tu Carlos na maneno yake.
"Najua kwanini umefikia kuwa hivyo"
"Kwanini?"
"Kwanza ulikuwa unafikiria maneno ya watu wanayokwambia kuhusu mimi pia hukufumbua macho bali mawazoni mwako uliwaza kuwa umefumbua na kuniona hivyo. Siku zote unapomuwazia mtu mabaya unajikuta ukiwa na wasiwasi nae muda wote. Kama ningekuwa mtu mbaya ningekudhuru muda mrefu tu Sabrina ila mimi ni mtu mwema na pia nina nia nzuri maishani mwako, huwezi kujutia kuwa na rafiki kama mimi. Niamini Sabrina kuwa mimi ni binadamu wa kawaida"
"Sawa nimekuelewa Carlos"
Mazungumzo yetu yakaendelea ila katika hali ya tahadhari sana, kisha Carlos akanikabidhi bahasha na kuniambia kuwa nikaifungulie nyumbani, halafu tukaagana.
Nikapanda kwenye gari yake hadi mitaa ya karibu, na kushuka kisha kwenda nyumbani.
Nilipofika ndani jambo la kwanza ni kumuuliza wifi.
"Kaka amerudi?"
"Hata bado hajarudi, amechelewa kweli leo"
Nikaenda chumbani kwangu na kuweka ile bahasha kisha kwenda kumsaidia wifi kazi mbalimbali, muda huo huo kaka nae akawasili akiwa na mizigo.
"Nilipitia kumnunulia mwanangu vitu vya kuchezea"
Wifi alionyesha furaha sana, tukavipokea vile vitu vilikuwa vingi sana na nguo nzuri pamoja na viatu vya mtoto.
Wifi akauliza kwa utani.
"Mmmh hata mama mtu nasahaulika zawadi jamani"
"Muda wa mwanangu kujidai huu, wewe mama mtu tulia"
Wote tukacheka na kuendelea kupanga mizigo, kwakweli kaka alimpenda sana mtoto James hata nikawaza kama itawezekana kumwambia kaka ukweli kuhusu mtoto huyo.
Tuliongea mengi hadi muda wa kula na kulala ulipofika.
Kama kawaida nilienda zangu chumbani kwangu mapema kabisa.
Nilipokuwa chumbani nikaikumbuka ile bahasha niliyopewa na Carlos, nikaichukua na kuangalia kilichomo ndani yake.
Zilikuwa ni picha, nikazitoa kuziangalia.
Picha zilionyesha Sam na Lucy wakiwa ufukweni moyo wangu ukapasuka kwa wivu, kwakweli nakiri wazi kuwa siwezi kuacha kumpenda Sam.
Roho iliniuma sana kwani nilihisi kuanza kumsahau Sam ukizingatia toka nije kwa kaka sijaonana nae tena na wala sitegemei kuonana nae kwa kipindi hiki ila kwanini nizione picha za kuumiza moyo wangu kiasi hiki? Lucy na Sam walionekana ni wenye furaha sana kwenye picha huku wakifurahia mapenzi yao.
Zile picha zilionyesha tarehe mwezi mwaka na muda ambao zilipigwa ilikuwa ni juzi, kwakweli sikuamini nikachukua simu yangu na kumpigia Sam ili kujua juzi alikuwa wapi.
"Ulikuwa wapi juzi jioni?"
"Nilienda beach kwani vipi Sabrina?"
"Ulienda na nani?"
"Marafiki zangu tu"
"Hawana majina?"
"Jamani Sabrina kwani ugomvi?"
Nikakata simu na kuamini moja kwa moja kuwa Sam alikuwa na Lucy siku hiyo moyo ukaniuma sana, nikajikuta natokwa na machozi na kujiuliza kuwa ni lini nitajifunza kumsahau Sam, mbona ananitesa sana!
Nilijililia tu, wakati naendelea kuangalia zile picha nikaona karatasi lenye maandishi kwenye zile picha limeandikwa;
"Mtoto mzuri kama wewe hutakiwi kulia lia hovyo, mimi nipo kuyafuta machozi yako yote na kukufanya binti mwenye furaha siku zote. Usilie Sabrina, tambua kwamba Carlos yupo kwaajili yako"
Nikakisoma mara mbili mbili na kujiuliza, inamaana Carlos ananitaka au? Itakuwa ananitaka tu ndiomana yupo karibu sana na mimi. Na kama kweli ananitaka je nimkubalie kweli? Ila anaweza akanisaidia mengi maana ana upeo mpana.
Nikajikuta nikiwaza hivyo kuhusu Carlos na mambo yake yote kwangu.
Ingawa picha ziliniumiza sana ila maneno ya Carlos kwenye kile kikaratasi yalinifariji moyo wangu.
Ili kujiridhisha zaidi na zile picha nikampigia Lucy simu kumuuliza.
"Samahani, unaweza kuniambia juzi jioni ulikuwa wapi?"
"Kwani unanidai? Nilikuwa beach"
"Na nani?"
"Swali gani hilo sasa? Nilikuwa na mpenzi wangu"
Nikakata simu na kuamini zaidi kuwa ni kweli walikuwa wote na moyo kuzidi kuniuma.
Nilikaa kitandani huku ninalia ila badae nilihisi kuna mtu ananibembeleza hadi kujikuta nimelala hadi asubuhi kulipokucha.
Nilitoka chumbani na kwenda kufanya kazi za usafi kwa ile asubuhi.
Wakati nadeki nikaona maandishi mekundu juu ya zile marumaru nyeupe pale sebleni, yameandikwa jina tu "JAMES" Nikashtuka sana na kumuita wifi, alipokuja yale maandishi hayakuwepo.
"Kwani ni kitu gani Sabrina?"
Nikakataa kuwa hamna kitu kwakuwa yale maandishi hayakuwepo tena kwahiyo nikaona kuwa wifi atanishangaa tu.
"Ila wewe Sabrina una matatizo ingawa hupendi kuyaweka wazi"
Nikamuangalia tu wifi bila ya kusema chochote.
"Badae tuongee kama utakuwa tayari kuniambia basi nijue jinsi gani ya kukusaidia"
Nikamuitikia wifi kuwa badae nitazungumza nae.
Nikaendelea na kazi zangu kama kawaida mpaka kuzimaliza.
Nilipokuwa nimepumzika sasa wifi akaona kuwa ni muda muafka wa mimi kuzungumza na yeye kuhusu matatizo yangu.
"Niambie Sabrina, usinifiche kitu tafadhari. Niko tayari kukusaidia kwa lolote lile"
"Ni kweli wifi nina matatizo, pia swala lako la kuniambia kuwa nikutunzie siri linanisumbua sana"
"Jamani wifi yangu, hayo si yalishakwisha jamani! Yani bado unayo tu!"
"Lazima niwe nayo wifi ukizingatia yanamuhusu kaka yangu wa damu"
"Nakuelewa mdogo wangu, tuachane na hayo kwanza niambie kinachokusumbua zaidi. Au ni kuhusu yule mpenzi wako?"
Nikainuka na kwenda chumbani kwangu na kumchukulia zile picha wifi yangu ili nae akazione.
"Hapo kuna mpenzi wangu na huyo rafiki yangu"
Wifi akaangalia zile picha huku akiguna na kusema.
"Ila siku hizi kuna picha za kutengeneza wifi yangu"
"Sio kama hizi wifi"
Mara wifi akazitupa zile picha pembeni huku akishtuka sana.
"Mbona hivyo wifi kuna nini?"
"Naomba uzitoe hizo picha mbele yangu wifi sitaki kuziona"
"Zina nini kwani?"
"Zitoe kwanza nitakwambia"
Nikazibeba zile picha na kuzirudisha chumbani, kisha nikarudi tena sebleni kumuuliza wifi.
"Kwani zina nini wifi?"
"Subiri kwanza"
Wifi alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa, akainuka na kwenda chumbani kwake.
Nikabaki pale sebleni huku nikijiuliza maswali mengi mengi bila majibu yoyote.
Baada ya muda wifi alirudi tena pale sebleni.
"Niambie basi wifi, zile picha zina nini?"
"Tuachane na habari ya zile picha, tufanye mengine mdogo wangu"
Nikamshangaa sana wifi kwani sikumuelewa kabisa kuwa kwanini amebadilika kiasi kile.
Ikabidi tuendelee na mambo mengine tu.
Jioni yake kama kawaida nilifanya kazi za ndani na kumaliza ila bado wifi hakuwa na raha kabisa siku ya leo tangu muda ule nilipomuonyesha zile picha.
Akaniita tena kuzungumza na mimi.
"Sabrina, hebu niambie ukweli kabisa kuhusu matatizo yako."
"Mmh wifi mbona unakuwa hivyo?"
"Nahitaji kujua Sabrina, au niambie aliyekupa zile picha ni nani?"
Maswali ya wifi yangu yalikuwa yananichanganya tu, ila nikasikia mlio wa simu chumbani kwangu na kwenda kupokea.
Mpigaji alikuwa ni Suzy nikashangaa kuona napigiwa simu na Suzy leo.
"Asante Sabrina, nasikia wewe ndiye ulinisaidia"
"Pole sana rafiki yangu, kwani tatizo lilikuwa ni nini?"
"Yote anayafanya Carlos"
"Kivipi?"
"Siku tukionana nitakwambia rafiki yangu ila kuwa makini sana na Carlos"
"Kwanini?"
"Amenisababishia matatizo makubwa sana, siruhusiwi kumweleza mtu yeyote ila nitakwambia wewe tukionana rafiki yangu"
"Mmh! Ila unaendeleaje kwa sasa?"
"Naendelea vizuri, asante sana rafiki yangu umeokoa maisha yangu ila..."
"Ila nini Suzy?"
"Nitakwambia tu tukionana, usijali Sabrina"
Suzy akakata ile simu na kuniacha na maswali mengi bila majibu ukizingatia siku za nyuma niliambiwa ni Carlos aliyewasaidia, sasa iweje Suzy aniambie kuwa Carlos ndiye aliyemsababishia matatizo yale.
Bado sikupata jibu na kurudi sebleni pale alipo wifi ili niendelee kuzungumza nae.
Wakati tunaongea tukasikia mtu akigonga mlango, nikamsikia wifi.
"Aliyekupa picha huyo"
Nikashangaa na kwenda kufungua.
Nikamkuta Carlos amesimama huku akitabasamu.
Nikamkuta Carlos akiwa amesimama huku akitabasamu.
Nikashtuka sana kwani sikumtegemea Carlos kwa wakati ule kabisa.
Ikabidi nimuulize kwanza kabla ya kumkaribisha ndani.
"Khee Carlos mbona gafla! Halafu umekuja moja kwa moja nyumbani"
"Kwani ni vibaya kukutembelea Sabrina?"
"Si vibaya ila ungekuja kwa taarifa kamili kuliko kunishtukiza kama hivi"
"Usijali Sabrina, nilikuwa napita hapa nje kwenu nikaona itakuwa vyema kama nikija kuwasalimia kwanza"
"Kwahiyo leo humwogopi wifi?"
"Sina kawaida ya kumwogopa mtu na nimekuja kwa lengo la kumwonyesha wifi yako kuwa mimi ni binadamu wa kawaida tu kama wengine."
Ikabidi nimkaribishe Carlos ndani kabisa kwani alijitoa kututembelea.
Kuingia ndani, tulimkuta wifi akiwa amekaa tena na mawazo sana.
Ile kumuona tu Carlos akiingia ndani kabisa, wifi akainuka na kuanza kuongea kwa hasira.
"Sabrina, kwanini umemkaribisha huyu mtu ndani?"
"Amekuja kututembelea wifi"
Wifi akamwangalia Carlos na kuanza kusema.
"Wewe shetani toka kwenye nyumba yangu"
Carlos akaanza kucheka tena kwa furaha kabisa.
"Unaniita shetani sababu nazijua siri zako! Au niziseme zingine hapa mbele ya Sabrina?"
Wifi akanywea kwanza na kusema.
"Najua unataka kunipunguzia imani kwavile umeona kuwa mimi ni mcha Mungu"
Carlos akacheka tena na kusema.
"Tatizo lako kubwa ni kuniita mimi shetani ndio useme sasa ushetani wangu uko wapi?"
Nikamuona wifi akiwa kimya kabisa na kukosa cha kujibu kwakweli. Wifi alikuwa akimuangalia Carlos kwa uoga tu.
"Unapokuwa mtu mwema jaribu kusema yote unayoyafanya siri ili uaminike. Wewe mwanamke, umeweka siri ngapi hadi leo? Niziseme kwa Sabrina?"
Wifi alitulia kimya kabisa na kushindwa kusema chochote, nilimuona akikaa kitini kwa uoga.
Carlos akamsogelea wifi na kumnong'oneza kitu sikioni kisha akanifata na kuniaga huku akitaka nimsindikize, kwakweli nilikuwa nimetulia kimya muda wote nikiangalia mabishano ya Carlos na wifi yangu.
Nikaongozana na Carlos hadi nje, akapanda kwenye gari yake na kuniambia.
"Nitakuja badae kukutembelea"
"Badae ya muda gani? Maana muda umeisha!"
"Ooh samahani, namaanisha kesho"
Kisha Carlos akaondoka.
Nikiwa bado pale nje nikaona gari ya kaka ikiwasili, naye akaingiza gari na kushuka kisha nikaongozana nae kuingia sebleni.
Tukamkuta wifi ametoa mimacho kama mtu anayeugua, kaka akamshtua wifi nae wifi aliposhtuka moja kwa moja akataja "James" kaka akadakia.
"Kafanyaje mtoto wetu James?"
Nadhani ni hapo wifi akarudiwa na ufahamu wa kawaida.
"Hajafanya kitu mume wangu"
"Mbona ulikuwa umetoa mimacho hapa?"
"Ni uchovu tu mume wangu"
Basi kaka akaongea pale mawili matatu na kupumzika kwa uchovu pale sebleni.
Muda wa kula ulipofika, tulienda kula.
Baada ya kupumzika nikainuka ili niende kulala, wifi akaninong'oneza
"Kuwa makini usiku wa leo Sabrina"
Nikamuitikia wifi na kwenda kulala huku nikiyatafakari maneno yake ila usingizi nao ukanipitia.
Wakati nimelala nikamuona yule kijana wa ndotoni akiwa mahali na mimi kwa mazungumzo.
"Unapenda kuumia Sabrina?"
Nikatingisha kichwa nikiashiria kuwa sipendi.
"Je, unapenda kuutesa moyo wako kwa maumivu?"
Nikakataa pia.
"Basi kama hupendi rudi nyumbani kwenu"
Hapo nikashangaa na kushtuka, ile sauti ikawa inapiga kama mwangwi mule chumbani.
"Rudi kwenu Sabrina, rudi nyumbani"
Nikaanza kuogopa na kutetemeka kwani mambo ya ajabu yalinianya tena, nikabahatika kuinuka pale kitandani na kukimbilia sebleni.
Nikamkuta wifi akimbembeleza mtoto wake aliyekuwa analia sana usiku ule, ila nae aliponiona akaniambia.
"Rudi nyumbani Sabrina"
Nikaogopa na kumuuliza vizuri.
"Unasemaje wifi?"
Wifi nae akajibu kwa mshangao.
"Kwani nimesemaje?"
"Inamaana hujui ulichokisema?"
"Sijasema chochote Sabrina, si unaona mwenyewe nahangaika na mtoto hapa hataki hata kulala"
"Mmh wifi! Umeniambia nirudi nyumbani"
Ni hapo ambapo wifi alishtuka na kuniuliza kwa makini nami nikarudia nilichosema.
"Kuna kitu Sabrina, kuna kitu kipo ndani humu. Siwezi kukwambia hivyo hata mara moja. Ona mtoto anavyolia hataki hata kutulia. Nipe mikono yako Sabrina"
Wifi akanishika mikono na kuanza kuomba, haikupita muda sana hali ikawa shwari kabisa ila sikujisikia tena kulala.
Niliongea na wifi pale hadi mtoto akalala, halafu mimi na wifi tukalala pale pale.
Kulipokucha tuliendelea na kazi kama kawaida kisha wifi akaniuliza kuhusu usiku uliopita.
"Hivi ni kweli ulinisikia mimi usiku nikiongea ulivyosema?"
"Ndio wifi, wewe ndio ulisema"
"Mimi siwezi kukwambia hayo maneno Sabrina, huyo ni shetani na lazima tumuaibishe"
"Kivipi wifi?"
"Lazima shetani aaibike, wewe huendi popote utabaki hapa hapa na kesho nitakupeleka kwa mchungaji akakufanyie maombi kamili"
"Sawa wifi yangu, nitafurahi ikiwa hivyo ili na mimi niweze kuwa huru"
"Najua hilo Sabrina, amekufanya kuwa mtumwa wake na lazima ashindwe"
Mara nikapigiwa simu muda huo huo na Carlos.
Nikapokea ili kumsikia anachotaka kuniambia.
"Naomba tuonane Sabrina"
"Tuonane wapi?"
"Palepale pa siku zote"
Sikuwa na pingamizi kwavile nimekuwa nikikutana nae mara nyingi tu.
Nikamuaga wifi kuwa naenda dukani, nae hakunizuia kwavile hakujua niendako.
Nilimkuta Carlos mahali pale akiwa na hasira sana hadi nikashangaa kwani sijawahi kumuona Carlos akiwa na hasira kiasi kile.
"Mbona umechukia hivyo Carlos?"
"Kuna watu wanataka niwaonyeshe kuwa nina uwezo wa kiasi gani na mimi ni mtu wa aina gani"
"Kwanini?"
Akaniangalia sana na kuniuliza.
"Unaniamini Sabrina?"
"Ndio nakuamini kwani vipi?"
"Vizuri sana kama unaniamini, nakuahidi kuwa nitakufanyia mambo mengi sana"
"Kama yapi?"
"Tulia utauona uwezo wangu niliopewa na Mungu"
Nikamuangalia tu bila ya kuelewa chochote, kisha akasema.
"Unajua kwanini wifi yako alishindwa kutoa ile mimba?"
"Mi sijui ila nadhani ni kwavile imani yake haimruhusu"
"Imani yake haimruhusu! Unajua ni mimba ngapi alitoa hapo kabla?"
Nikazidi kumshangaa Carlos, kisha akaniambia kuwa nikamuulize kuwa ni mimba ngapi alitoa kabla na kusema atakuja badae kunitembelea tena. Nikaondoka na kurudi nyumbani bila kuelewa nia na dhumuni la Carlos ni nini kwenye maisha ya wifi yangu.
Nilipofika nyumbani wifi alikuwa ametulia kama kawaida yake na aliponiona akafurahi kurudi kwangu.
"Bora umerudi wifi yangu"
"Kuna kitu nataka nikuulize wifi"
"Uliza tu"
"Ushawahi kutoa mimba?"
"Swali gani hilo Sabrina? Unajua wazi kutoa mimba ni dhambi, haina tofauti na kuua. Kwani umepata mimba mdogo wangu?"
"Hapana, sina mimba wifi"
"Mbona umeniuliza kuhusu kutoa mimba? Unataka nikwambie maumivu yake? Kama una mimba Sabrina usithubutu kuitoa, ni dhambi sana mbele za Mungu wetu"
"Sawa wifi nimekuelewa"
Ila hakujibu swali langu kama amewahi kutoa mimba au la.
Nikiwa nazungumza na wifi, nikapigiwa simu na Sam.
Ile kupokea tu akaanza kuongea moja kwa moja.
"Hata kama tumegombana Sabrina, si vizuri kunitumia ujumbe wa kunitusi kiasi hiki"
"Ujumbe wa kukutusi? Nimekutumia saa ngapi? Umechanganyikiwa wewe"
"Sabrina, asante sana hata kama unasema kuwa nimechanganyikiwa asante sana ila kunitusi si vizuri. Kukupenda sio kosa Sabrina"
Halafu akakata simu, nikabaki nashangaa tu. Mara kidogo ukaingia ujumbe kwenye simu yangu kutoka kwa Sam.
"Poa tu Sabrina kwa kunikatia simu"
Hapo nikahisi ni wazi Sam hajielewi kwa sasa na kudhani labda amechanganywa na Lucy, sasa hasira zake ndio anamalizia kwangu.
Na ubaya simu yangu haikuwa na salio hivyo nikashindwa kumpigia wala kujibu ujumbe wake kwahiyo nikawa kimya kabisa huku nikitafakari na kushangaa tu kuwa kwanini Sam amekuwa vile alivyokuwa.
Ila haukupita muda sana nikapigiwa simu na Carlos kisha akaomba kuzungumza na wifi yangu, nikamuwekea wifi ile simu sikioni ila baada ya dakika chache niliona wifi akishusha ile simu taratibu tena bila ya kusema chochote, nikamuuliza.
"Amekwambiaje kwani?"
Wifi alinitazama tu bila ya kunijibu, ikabidi nikaendelee na kazi zangu za jioni hadi pale kaka aliporudi toka kwenye kazi yake.
Nikamsalimia na kuendelea na mambo mengine, nikaandaa chakula mezani lakini hawakuja kula ikabidi nile na kwenda chumbani kwangu kupumzika kwani wifi hakunijibu chochote tangu muda alioongea na Carlos.
Usiku wa leo ulikuwa wa ajabu sana, nilikosa raha kabisa nikiwa mule chumbani ukizingatia hata chakula nilichopika hakikuliwa na wifi pamoja na kaka kwahiyo nikawa najiuliza nini tatizo mpaka inakuwa hivi.
Sikupata jibu lolote kwakweli, nikaamua tena kwenda sebleni kuona kama wifi na kaka wameenda kulala, ila niliwakuta pale pale tena kaka akiwa amelala kwa kujinyoosha kwenye kitu kitendo ambacho kilinichanganya.
Wifi alikuwa amekaa na mtoto mikononi, nikaamua kumsogelea na kumuuliza kuhusu kaka ili amwamshe akalale, na muda huu wifi alinijibu kila nilichomuuliza pale.
"Wifi mbona hivyo, mwamshe kaka akalale ndani"
"Mwangalie kaka yako alivyo Sabrina"
Moyo wangu ukalia paaa kwa uoga, na kuuliza kwa taharuki.
"Kwani ana nini?"
"Wee msogelee tu umwangalie"
Nikamsogelea kaka kwa uoga na kumwangalia kwa makini huku na uoga ukiniandama ila nilimuona kuwa yupo sawa.
"Mbona yupo sawa wifi!"
"Mwangalie vizuri Sabrina"
Huku wifi machozi yakimlengalenga nami hofu ikanizidi na kujaribu kumuamsha kaka ila hakushtuka wala kutingishika alikuwa kama vile mtu aliyekufa, uoga ukanijaa zaidi.
Nikajaribu kumuamsha kaka ila hakushtuka wala kutingishika alikuwa kama vile mtu aliyekufa, uoga ukanijaa zaidi.
Nikamuangalia vizuri kaka Deo na kumuuliza wifi.
"Mbona kaka haamki?"
Machozi yalikuwa yakimtoka wifi, huku akinijibu.
"Sijui Sabrina, sijui kwanini mume wangu haamki"
"Na mbona umekaa tu bila kufanya chochote?"
"Chochote kipi? Unafikiri ni hali ya kawaida hiyo? Akipelekwa hospitali ujue wanaenda kummalizia"
Maneno ya wifi yakaijaza hofu zaidi moyoni mwangu, nikaanza kukumbuka jinsi Carlos alivyosema kuwa ataenda kumuokoa rafiki yangu Suzy, wazo la haraka likanijia tena bila kufikiria zaidi. Nikaenda chumbani kwangu na kumpigia simu Carlos ili kama kunauwezekano basi aje atusaidie.
Ile simu haikuchukua muda sana kupokelewa, na Carlos nae hakuchukua muda sana kuwasili hadi nikajiuliza kuwa huyu Carlos anaishi nje kwetu kama jirani au! Mbona amefika muda huo huo baada ya kumpigia simu. Jibu nilikosa.
Carlos aliingia ndani kwetu kwa uhuru kabisa bila ya kuogopa kitu chochote kile, alipokuwa ndani ndio akaniuliza kuwa tatizo ni nini.
"Mtazame kaka yangu hapo"
"Huyu mwacheni nimpeleke hospitali"
Nikamuangalia wifi aliyekuwa kimya kabisa, Carlos akambeba kaka yeye mwenyewe bila msaada wowote na kumpakia kwenye gari yake kisha kuondoka nae, baada ya nusu saa Carlos na kaka walirudi nyumbani huku kaka akiwa mzima kabisa, nikashangaa sana hata wifi nae akashangaa hakuwa na la kufanya zaidi ya kuongea vizuri na Carlos kwani amemsaidia mumewe kurudi kwenye hali ya kawaida kama aliyokuwa nayo zamani.
Kaka alikuwa akimshukuru tu Carlos na kuona kuwa Carlos ni mtu mwema.
"Pole sana mtu wa watu, wamekusumbua usiku wote huu"
"Hata msijali jamani, mimi mwenyewe nilimwambia Sabrina kuwa endapo atakuwa na tatizo lolote lile basi asisite kuniambia"
"Basi ni vizuri kama ni hivyo"
Carlos nae akaanza kuzungumza yake kwani alijuwa wazi kuwa ni lazima atasikilizwa tu.
"Halafu huyu Sabrina kuna kitu kinamsumbua sana"
Kaka akadakia.
"Kitu gani?"
"Huenda ikawa mizimu ya kwenu, kinamtaka arudi nyumbani. Mimi naona ni bora mkamruhusu kuwa arudi tu kabla mambo hayajaharibika"
Kaka hakuwa na pingamizi lolote kwa Carlos, nadhani alishaiteka akili ya kaka kwahiyo imekuwa rahisi kumkubalia, wifi nae alishapumbazika.
"Ila kwa mwezi huu niko busy sana, hakuna wa kumrudisha nyumbani"
Mara hii nilicheka kwani niletwe na kurudishwa nimekuwa mtoto mdogo au! Carlos akamjibu kaka,
"Usijali kwa hilo, mimi nipo na nitahakikisha nampeleka hadi nyumbani kwenu. Mwenyewe utafurahi"
Waliongea mengi bila kujali kuwa ni usiku na watu karibia wote wamelala kasoro sisi, kaka akamkubalia Carlos kuwa aje anichukue na kunirudisha nyumbani, badae wakaagana nae bila ya kumuuliza kuwa na yeye je anaishi wapi maana anapoishi hata hapajulikani.
Alipoondoka kila mmoja akaenda kulala hadi kulipokucha.
Kulipokucha, nikiwa chumbani kwangu nikamsikia wifi akiniita.
"Hivi usiku kulikuwa na nini?"
"Inamaana hujui wifi kama kulikuwa na nini!"
"Hivi ilikuwa ni kweli au ni ndoto?"
Nikamshangaa wifi, tulikuwa wote halafu anashindwa kutambua kama ilikuwa ni kweli au ni ndoto.
"Wifi, inamaana huelewi chochote hapo ulipo? Ilikuwa ni kweli na wala sio ndoto wifi yangu"
"Mmh! Halafu mimi nikashindwa hata kukemea mdogo wangu! Inawezekana kweli? Labda kuna mtu alinipumbaza, sio bure kwakweli. Nakosa hata jibu."
"Pole wifi ila ndio ilivyokuwa"
"Ila si nilikwambia kuwa leo tutaenda kwa mchungaji, itabidi tufanyiwe maombezi"
"Hapana wifi, leo narudi nyumbani"
Wifi akabaki kushangaa bila ya kuelewa chochote kinachoendelea.
Mchana wa siku hiyo nilimsikia wifi akiongea na kaka, nikasikia akibishana nae kuhusu kuondoka kwangu pale na kurudi nyumbani kwetu.
Baada ya kukata simu akaniita na kuniuliza.
"Kaka yako nae kapatwa na nini? Yani amekubali kabisa wewe uondoke!"
"Ndio amekubali, mbona na wewe ulikubali wifi"
"Hapana, mi sijakubali bado nakuhitaji hapa"
"Ila mimi nikiendelea kukaa hapa nitamwambia kaka ukweli kuhusu huyo mtoto, unakubaliana na mimi!" http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
"Yanatokea wapi sasa hayo jamani Sabrina?"
"Kwasababu sitaweza kukaa kimya kwa kipindi kirefu, kumbuka mumeo ni kaka yangu wa damu. Acha tu nirudi nyumbani wifi"
"Nakuomba ombi moja mdogo wangu"
"Lipi hilo?"
"Ukienda huko kwenu usimwambie hata mama yako ukweli, nitaumbuka mimi jamani"
"Mmmh hadi mama!! Nitaweza kweli? Ungekuwa wewe wifi ungeweza kumficha mama yako mzazi kuhusu hili?"
"Nakuomba Sabrina, kama ulivyonyamaza kwa kaka yako fanya hivyo na huko. Fanya kamavile hakuna lililowahi kutokea. Nisaidie mimi wifi yangu."
"Nitajaribu wifi, je hiyo ndio sababu pekee ya kunizuia mimi kurudi nyumbani?"
"Hapana, nakuhurumia pia na maisha yako, nayahurumia na maisha yangu pia. Sijui kwanini siri hii inanitesa hivi!"
"Usijali kuhusu hiyo siri wifi ila matumaini yangu ni kuwa ipo siku utamwambia kaka yangu ukweli kuhusu huyo mtoto"
Nikaamua kufanya mambo yangu mengine, huku nikimsubiri huyo Carlos aje kunichukua ili niweze kurudi nyumbani.
Nikiwa chumbani kwangu huku nikitafakari baadhi ya mambo yanayoendelea, wifi akaniita tena nikaamua kumuuliza,
"Mbona unakuwa kama mtu mwenye mashaka sana wifi yangu?"
"Hata hujakosea, ni kweli nina mashaka sana"
"Nini unaogopa wifi? Bado unahofu na siri yako?"
"Aaah! Hapana, ila ni kuhusu zile picha hebu kaniletee tena"
"Zile ulizoniambia kuwa si za kawaida?"
"Ndio, hizohizo naomba uniletee"
Ikabidi nikazipekue tena kwani nilishaziweka kwenye begi, nikazichukua na kumpelekea. Akaziangalia kwa makini sana, na kuishika picha moja wapo na kuniuliza.
"Umesema kuna nani na nani hapa?"
"Mpenzi wangu na rafiki yangu"
"Una hakika kuwa huyu ni mpenzi wako?"
Nikaitikia kwa kichwa kuwa nina uhakika, wifi akaniangalia kwa umakini sana na kusema.
"Yani picha anaonekana kaka yako na mwanamke halafu wewe unasema mpenzi wako na rafiki yako! Ndiomana nilikwambia kuwa hizi picha si za kawaida, namuamini sana Deo hawezi kunisaliti kiasi hiki cha kupiga picha na mwanamke mwingine"
Nikamshangaa sana wifi kwani zile picha ziliwaonyesha Sam na Lucy wakiwa pamoja halafu yeye anadai ni kaka Deo na mwanamke, nikamuuliza tena wifi,
"Utakuwa umechanganyikiwa wifi, kaka Deo yuko wapi hapo?"
"Wewe ndio umechanganyikiwa Sabrina, huyu ni kaka yako na mwanamke halafu wewe unasema ni mpenzi wako! Wewe Sabrina umechanganyikiwa kweli kabisa nakwambia"
Nikamuangalia tu wifi ambaye nilikuwa nikimshangaa muda wote, akachukua zile picha zote na kuzichana chana vipande vipande huku akisema.
"Siamini kabisa kama Deo anaweza kunisaliti, hata siku ile ya kwanza uliponionyesha zile picha sikuamini. Ila za mwizi arobaini, kama kweli kaka yako ananisaliti basi nitajua tu"
"Usiwe na hasira sana wifi, kwani hata mimi sielewi unachosema"
Nilitulia tu na kuona kuwa ni wazi mimi na wifi tumevurugwa ila hakuna la kufanya na kueleweka kwa urahisi zaidi.
Nikiwa nimetulia ndani, Carlos akanipigia simu na kusema kuwa yupo njiani kuja kwa kaka kunifata.
Sam nae akanipigia simu.
"Hivi Sabrina, huko ulipo sasa na huku kuna umbali upi?"
"Kwanini umeuliza hivyo Sam?"
"Nijibu kwanza"
"Kwakweli ni mbali, yani kama masaa mawili au matatu kufika kama barabara haina foleni"
"Na Carlos je anaishi wapi?"
Hapa sasa ikawa kamavile Sam kanizindua akili yangu kwani hata mi mwenyewe sikujua mahali ambako Carlos anaishi.
"Kwakweli sijui"
"Basi muulize, akikupa jibu niambie halafu nitakwambia jambo fulani"
Sam akakata simu na kuniacha nikiwa na maswali mengi sana kwenye kichwa changu kuhusu Carlos, nikaanza kujiuliza sasa.
"Carlos anaishi wapi? Nilipokuwa kwetu alikuwa anakuja mara kwa mara, nipo huku napo anakuja kila siku. Je, anaishi wapi?"
Ni maswali yaliyokosa majibu kichwani mwangu ila nikajipanga kumuuliza Carlos atakapokuja kunichukua wakati wa kuondoka.
Muda ukapita kidogo na Carlos akawasili pale nyumbani kwa kaka.
Wifi alimuangalia Carlos kwa macho ya ghadhabu sana, kisha nikamsikia Carlos akimwambia wifi yangu.
"Na bado, utagundua mengi sana Joy"
Ila wifi hakujibu kitu chochote, alimuangalia tu.
Kaka nae akawasili muda uleule na kutukuta pale ndani pamoja na Carlos, baada ya salamu akaanza kuuliza.
"Nilifikiri mtakuwa mmeshaondoka, mbona mpaka sasa bado?"
Carlos akamjibu kaka.
"Mkeo hayupo tayari kuwa Sabrina aondoke, ndio tunangoja ruhusa kutoka kwake"
Mimi na wifi tukamshangaa sana Carlos kwa maneno yale, kaka akamuangalia wifi na kumuuliza.
"Eti hujawaruhusu? Si tulishaongea kwenye simu tayari!"
Wifi alizidi kuwa kimya, Carlos nae akaongezea maneno mengine.
"Tatizo ni kwamba Sabrina ana siri nyingi sana za wifi yake, sasa ......"
Kabla Carlos hajaendelea wifi alidakia kwa haraka sana.
"Mbona niliwapa ruhusa muda mrefu sana, nyie nendeni tu kwa amani"
Carlos akatabasamu na kuinuka ili tuianze safari ila kaka nae akauliza.
"Kwani hizo siri ni siri gani?"
"Hakuna cha siri mume wangu, huyo kijana ameongea yake tu"
Carlos alikuwa tayari ameshatoka nje.
Wifi akanifata na kuniambia kwa taratibu.
"Keshokutwa nitakuja hukohuko nyumbani na tutaongea vizuri ila kuwa makini sana huyo sio mtu"
Nikamuitikia na kwenda kupanda gari ya Carlos kwaajili ya safari.
Tukiwa ndani ya gari Carlos akaniuliza,
"Unataka tuwahi kufika au tuchelewe?"
"Kila mtu anapenda kuwahi kwakweli, hakuna anayependa kuchelewa"
"Wewe je unapenda lipi?"
"Napenda tuwahi ila itategemea na foleni barabarani"
Na tulipofika barabara kuu ni kweli kulikuwa na foleni sana hata yale matumaini ya kufika mapema yakapotea kabisa, nikamuangalia Carlos na kumwambia.
"Hatuwezi kuwahi tena kwani foleni ni kubwa sana"
"Ila bado kuna uwezekano mkubwa wa kuwahi"
"Upi huo"
"Fumba macho mpaka nikwambie fumbua, utaona mwenyewe"
Nikafumba macho ila kauli ya mwisho ya wifi ikatembea tena kichwani kuwa Carlos si mtu, nikajikuta natamani kufumbua macho ili nijue afanyacho hapohapo nikafumbua macho.
Nikaona lile gari tulilopanda limepaa angani kama ndege.
Nikaanza kupiga kelele kwa uoga.
Nikaona lile gari tulilopanda limepaa angani kama ndege.
Nikaanza kupiga kelele kwa uoga.
Hofu ikatanda moyoni mwangu, kwa kelele nilizopiga nadhani hata ndege angani walinisikia.
Nikamuona Carlos akiniangalia kwa macho makali sana na gafla nikalala usingizi mzito na sikujua chochote kilichoendelea tena mahali pale.
Carlos akanishtua toka usingizini, jambo ambalo lilinishtua sana.
"Mbona unashtuka hivyo Sabrina? Tumeshafika nyumbani kwenu"
Nikawa nashangaa kamavile mtu aliyepoteza kumbukumbu zake za maana, nikamuangalia Carlos kwa makini na kukumbuka kuwa mara ya mwisho tulikuwa tunapaa angani.
"Tumefika? Mbona tulikuwa tunapaa?"
Carlos nae akashangaa,
"Tunapaa! Muda gani huo?"
"Muda uliponiambia nifumbe macho, nikafumbua na kuona gari inapaa"
Carlos akacheka sana na kusema.
"Kweli Sabrina wewe una maruweruwe, hebu twende huko ndani kwenu nikakueleweshe vizuri"
Ikabidi tuingie ndani kwanza.
Ila hakuwepo mama wala dada Penina na mlango ulikuwa umerudishiwa tu, sikushangaa sana kwavile sikuwapa taarifa kama narudi leo.
Kwahiyo nikakaa pale sebleni na Carlos.
"Haya sasa nieleweshe nisichoelewa"
"Sikia Sabrina, nilikwambia ufumbe macho ili ulale na siku zote mtu anayelala wakati wa safari hushtukia tu wakati ameshafika, hilo ndio lilikuwa lengo langu kwako.
"Na mbona gari ilipaa?"
Niliuliza kwa ujasiri ila moyoni uoga ulinijaa kwavile sikuwa na amani kabisa na Carlos.
"Sabrina ulikuwa umelala, hizo ni ndoto tu. Tangu lini gari likapaa?"
Nikawa kimya nikimuangalia huku nikitafakari kama kweli ni ndoto.
"Ila nilifumbua macho kabisa"
"Hizo ni ndoto tu Sabrina usipende kuzitilia umakini sana"
Mama nae akawa amerudi na kutukuta mule ndani.
"Kheee Sabrina! Umerudi bila hata taarifa?"
Nikainuka na kumkumbatia mama kisha kumsalimia.
Halafu mama akasalimiana na Carlos aliyeanza kuaga na kusema kuwa atakuja kesho, kisha akaondoka.
Mama akaniuliza,
"Penina kaenda wapi?"
"Sijui ila nimekuta mlango umerudishiwa tu"
"Na bora umerudi maana huyu Penina atafanya tuibiwe humu ndani, vipi maruweruwe yako siku hizi yamepungua?"
"Ndio yamepungua mama"
Tuliongea na mama pale hadi aliporudi dada Penina, moja kwa moja mama akamuanzia na maswali.
"Ulienda wapi Penina na kuacha mlango wazi?"
"Khee mama, ngoja nimsalimie mdogo wangu kwanza"
Nikasalimiana pale na dada Penina.
"Nimemuona Carlos hapo njiani, nilikuwa na rafiki yangu basi alipomuona Carlos katoka nduki, sijui hata ana matatizo gani yule shoga yangu?"
Mama akamuuliza,
"Sasa vipi ulimfatilia?"
"Nimfatilie wa kazi gani wakati kajitia uwehu mwenyewe. Atajijua huko"
"Mmh! Roho mbaya hiyo Penina, ungemfatilia kwani huwezi jua matatizo yake hivyo hivyo bila ya kumfatilia"
Dada Penina hakujali na kuendeleza stori zingine anazojua yeye hadi muda wa kula na kulala ulipofika.
Nilienda kulala chumbani kwangu na nililala vizuri leo bila tatizo lolote hadi kunakucha.
Asubuhi yake nikapigiwa simu na Suzy.
"Bado upo kwa kaka yako Sabrina?"
"Hapana, nimesharudi nyumbani"
"Basi kesho nitakuja kwenu, nina mengi ya kuzungumza na wewe Sabrina"
"Hakuna tatizo Suzy, utanikuta tu"
Sikujua mazungumzo ya Suzy yatamuhusu Sam au Carlos maana wote wanahusika kati yetu.
Nikatulia kungoja hiyo kesho kuona nini Suzy ataniambia.
Nilitoka nje na kumkuta mama akiendelea na kazi.
"Sijataka kukusumbua leo maana hukawii wewe kusema kuwa mama ana roho mbaya"
Nikacheka tu na kumsalimia kisha kumsaidia kazi za hapa na pale.
Nikasikia simu yangu ikiita, nikaenda kupokea.
"Nasikia umesharudi nyumbani kwenu Sabrina!"
"Ndio nipo nyumbani"
"Ulimuuliza Carlos nilichokwambia?"
Hapo ndio nikakumbuka na kumjibu Sam kuwa sijamuuliza ila nitamuuliza iwapo nikionana nae. Sam akaniomba tukutane jioni ya leo ili aniambie baadhi ya mambo yanayompa mashaka, nami nikakubali wito wake.
Nikarudi jikoni ili kuendelea na kazi.
Jioni ilipofika nilijiandaa ili niweze kwenda kuonana na Sam, kabla sijatoka nikafikiwa na ugeni naye alikuwa ni Carlos aliyeongozana na kijana flani hivi ambaye sikumfahamu, ikabidi niwakaribishe ndani.
Mama nae akaja kusalimiana nao, ambapo Carlos alitutambulisha kuwa kijana yule ni ndugu yake.
Nikashindwa kutoka tena, ila nadhani Carlos alikuwa anajua kama mimi nataka kutoka, kwahiyo akasema,
"Nenda tu Sabrina uendako, sisi nia yetu hapa ni kuzungumza na mama yako tu"
Mama akashtuka na kuuliza
"Kwani Sabrina unataka kwenda wapi?"
Nikajiumauma kwani sikuwa na maelezo ya kueleweka, Carlos akasema tena.
"Mwache aende tu mama, akirudi atakwambia alipotoka"
Mama hakuwa na pingamizi, nae akaniruhusu niende hadi nikashangaa. Niliondoka huku nikijiuliza kuwa Carlos anataka kuzungumza nini na mama yangu na huyo ndugu yake hata sikuelewa kwakweli.
Nilienda moja kwa moja mpaka eneo nililoahidiana na Sam, nikamkuta Sam ananingoja.
"Pole sana, umenisubiri muda mrefu eeh!"
"Ndio salamu hiyo Sabrina?"
"Samahani, mambo vipi?"
Huku nikivuta kiti na kukaa.
"Yani hatujaonana kwa siku nyingi na salamu inaishia mambo vipi tu!"
"Aaah! Mada ya salamu imeisha bhana, tuongee mambo ya muhimu sasa"
Ikabidi Sam nae akae maana aliona kuwa sipo kama alivyonifahamu zamani.
"Nia yangu kubwa ni kumuongelea Carlos"
"Kafanyaje?"
"Carlos amekuja katika maisha yetu kwa lengo moja tu"
"Lengo gani hilo?"
"Anataka kuharibu maisha yetu na pia kuvuruga amani, halafu kikubwa zaidi anataka kututenganisha"
"Atutenganishe kwa lipi na kwanini?"
"Carlos anakutaka Sabrina, anataka uwe mpenzi wake. Tangia amekuja katika maisha yetu tumekuwa tukigombana kila siku. Nimejaribu kuchunguza na kugundua kuwa chanzo cha yote haya katika maisha yetu ni Carlos. Si mtu mzuri yule"
Nikajisikia kucheka kwani sikujua kama Carlos anaweza akanitaka na asiniambie siku zote hizo ambazo huwa nakuwa nae.
"Acha wivu Sam, Carlos ni rafiki tu wala hakuna chochote kinachoendelea kati yangu na yake. Tofauti kabisa na wewe ukiwa na Lucy wako"
"Kwanza Sabrina naomba utambue kuwa hakuna mahusiano yoyote kati yangu na Lucy, hata sisi wenyewe tunajishangaa"
Nikajua hapo Sam anatafuta njia ya kujitetea tu wakati kila siku nambamba akiwa na Lucy.
Sam akaendelea kuongea kuhusu Carlos.
"Halafu kitu kingine, Carlos sio mtu wa kawaida"
"Kama sio mtu wa kawaida ni nani? Na kwanini useme kuwa sio mtu wa kawaida?"
"Nitakwambia kilichotokea wakati Suzy amepatwa na matatizo, ndiomana nasema kuwa Carlos sio mtu wa kawaida"
"Niambie basi nielewe"
Sam akaanza kunielezea kuhusu Suzy, siku aliyopata matatizo na hapo kwa mbali nikaelewa kwanini Carlos alinikataza kupiga sinu kwakina Suzy kwani alijua lazima ningeshtuka tu.
"Siku ambayo Suzy alipatwa na matatizo, mimi na Lucy tulikuwa nyumbani kwao"
Hapo alipotaja jina la Lucy nilihisi kuchefuka moyoni ila nikaendelea kumsikiliza tu.
"Eeh ikawaje?"
"Kwakweli Suzy alikuwa na hali mbaya sana, hivyo tulikuwa kwenye harakati za kumsaidia"
"Ngoja nikukatishe kwanza, kwani Suzy alipatwa na nini?"
"Alikutana na watu wakampiga sana, halafu wakamtegeshea nyoka aliyemng'ata Suzy ila ukikutana nae atakusimulia vizuri zaidi, ngoja mimi niendelee na habari za Carlos"
"Haya endelea"
"Muda ule mama Suzy anakupigia simu wote tulikuwepo pale, alipokata tu haikupita hata dakika mbili Carlos aliwasili eneo la tukio na kusema amepewa taarifa na wewe kwahiyo amekuja kutusaidia. Swali langu sasa, hiyo taarifa ulimpa saa ngapi? Na je lile eneo ambalo Suzy alipatia matatizo amelijuaje wakati hata mama Suzy hakukutajia wewe?"
Hapo nikamkatisha Sam kwani nilikumbuka kuwa Sam alinipigia simu kuhusu Suzy.
"Kama ulikuwepo eneo la tukio mbona ukanipigia simu kuulizia hali ya Suzy?"
"Nia yangu nilitaka upige simu kwa kina Suzy na uweze kumtambua Carlos ni mtu wa aina gani! Hajulikani anapoishi wala hana ndugu, sasa huyo ni mtu gani?"
Hapo nikakumbuka kuwa leo Carlos amekuja na ndugu yake nyumbani kwetu.
"Kuhusu swala la ndugu, Carlos ana ndugu zake bhana. Leo alikuja na ndugu yake nyumbani kwetu"
"Tatizo lako Sabrina hutaki kukubali ukweli. Haya tuongelee mapenzi yetu sasa"
Nikatulia kwa makini ili nimsikilize hoja zake kuhusu mapenzi yetu, ingawa moyo wangu ukaniambia kuwa atakayoyasema Sam yote ni uongo tu kwani kashampenda mtu mwingine.
"Unajua Sabrina nakupenda sana, halafu...."
Kabla hajaendelea, alikuja Lucy na kusimama nyuma ya Sam kisha kuingilia yale maongezi huku akiwa amemuinamia Sam na mikono yake ikazunguka kwenye kifua cha Sam, huku akiongea sauti ya taratibu kama mtu anayenong'oneza sikioni kwa Sam.
"Halafu nini?"
Nikapatwa na hasira kwani muonekano wa Lucy kwa Sam ulinikela sana, kilichoniudhi zaidi ni kumuona Sam ametulia kama sanamu bila ya kufanya chochote hata kumzuia Lucy na mikoo yake iliyokuwa ikimpapasa hakumzuia.
Hasira ikanizidia na kuona cha msingi ni kupambana na Lucy tu kwani amezoea kunifatilia na mpenzi wangu.
Nikainuka kwa ghadhabu huku hasira zikiwa zimenijaa kooni tena bila hata ya kufikiria mara mbili, nikachukua chupa ya soda niliyokuwa nakunywa na kumpiga nayo Lucy kichwani.
Hapohapo, Lucy akaanguka huku damu zikimtoka puani na mdomoni.
Lucy akaanguka huku damu zikimtoka puani na mdomoni.Uoga ukanijaa na akili yangu ikasema haraka sana kuwa "Umeuwaaa" moja kwa moja nikawaza kifungo cha maisha au kuhukumiwa adhabu ya kifo, sikufikiria zaidi na kuanza kukimbia.
Nilikimbia sana bila ya kuangalia nyuma wala nini na hakuna aliyenikimbiza.
Nikapishana na gari ya Carlos njiani, nadhani walitoka nyumbani kwetu. Ingawa ilisimama ila sikulisogelea hata kidogo na kuendelea kukimbia, hatua ya kwanza ilikuwa ni nyumbani kwetu huku nikihema kwa nguvu kama jibwa koko.
Mama akaniona wakati naingia ndani huku nikihema juu juu na kuniuliza.
"Una nini Sabrina, mbona hivyo?"
"Mama nimeuaaa"
Hapo hapo nikaanguka chini na kuzimia kwani nguvu zote ziliniisha na sikuelewa tena kilichoendelea baadae.
Nilipozinduka, nilijikuta chumbani kwangu.
Nikainuka na kuanza kurudisha kumbukumbu nyuma, hapohapo nikakumbuka kuwa tukio la mwisho ni kumpiga Lucy kwa chupa ya soda kichwani. Nikakumbuka jinsi damu zilivyokuwa zikimtoka Lucy na jinsi nilivyokimbia huku nikiwaza kukamatwa.
Wazo jingine likanijia kuwa kwanini nilikimbia wakati makosa ni yangu na ilitakiwa mimi ndio nimsaidie rafiki yangu, ila nitamsaidiaje zaidi ya kukamatwa na kushtakiwa? Na je kukimbilia nyumbani ndio suluhisho? Wakati Sam anapajua kwetu na ataweza kuwaleta maaskari muda wowote ule, wazo likanijia kuwa hata kukaa nyumbani napo si salama.
Mara mlango wa chumbani kwangu ukafunguliwa, nikashtuka sana ila ni mama ndiye aliyeingia.
"Sabrina mwanangu umeamka? Eeh bora, kumbe Carlos alinipa ushauri mzuri"
Nikataka kuuliza kuwa ni ushauri gani ila kabla sijauliza ikasikika hodi toka nje, hapo pia nikashtuka na hofu kunitanda moyoni.
Mama akatoka kwenda kumkaribisha mgongaji, nikatamani hata kuingia uvunguni ili nijifiche.
Mara mama akaniita, nilitoka kwa uoga hadi sebleni na kumkuta mgeni mwenyewe kuwa ni Carlos, na moja kwa moja akaniuliza.
"Unaendeleaje Sabrina?"
Nikawa namjibu kwa wasiwasi huku uoga na hofu vikizidi kunitawala.
"Naendelea vizuri"
"Usijali kwa ulichokifanya, mimi nitashughulikia na kukusaidia"
Mama akadakia,
"Kwani amefanyaje?"
"Sabrina amegombana na rafiki yake huko baa, halafu amempiga mwenzie na chupa kichwani."
Mama akashtuka sana na kuniuliza kwa hamaki.
"Umeanza lini kupigana Sabrina?"
"Nisamehe mama, sikudhamilia"
Huku machozi yakinilengalenga.
"Hukudhamilia nini? Yani unampiga mtu na chupa kichwani? Unajua madhara yake kweli? Kwanza mmegombania nini hadi kupigana hivyo?"
Carlos akadakia,
"Walikuwa wanamgombea Sam, yule mpenzi wa Sabrina sasa siku hizi amekuwa na mahusiano na Lucy. Hapo ndipo ugomvi wao ulipoanzia"
Mama akapandisha hasira zaidi.
"Yani Sabrina unafikia hatua ya kumpiga na chupa rafiki yako mpenzi Lucy sababu ya huyo paka Sam! Mara ngapi nimekukataza kuwa na hiko kidubwasha? Mara ngapi? Wewe mtoto wewe utaniua mimi jamani"
"Nisamehe mama"
"Msamaha wako utasaidia nini wakati mwenzako anahangamia huko! Nitaiweka sura yangu wapi mimi nikikutana na mama Lucy? Mungu wangu, mtoto wewe umeniadhirisha jamani. Bora ungebaki hukohuko kwa kaka yako. Yani kujifanya unaharaka hapa walivyokuja Carlos na nduguye kumbe ndio ulikuwa unaenda kufanya huo upuuzi!"
Mama akainuka kwa hasira na kuanza kunipiga ila Carlos akamzuia mama na kusema.
"Usimpige, alikuwa na hasira tu. Hakudhamilia kumpiga rafiki yake ila imetokea kwa bahati mbaya tu na nitamsaidia kwa hilo. Lucy atapona na atakuwa mzima kabisa, msijali kitu kuhusu hilo"
Mama akamuuliza Carlos.
"Ila baba, si watakuwa wanamtafuta Sabrina kwa hilo kosa?"
"Ni kweli watamtafuta ila mimi nitashughulikia, hili swala niachieni mimi maana hata Sabrina alipokimbia, mimi ndio nilienda pale kuwasaidia. Jambo la muhimu kwasasa ni moja tu"
Mimi na mama tukajikuta tukisema kwa pamoja.
"Jambo gani hilo?"
"Sabrina unatakiwa kuwa makini kwasasa, usiwasiliane na Lucy wala Sam hadi mambo yatakapokuwa shwari. Na wala usitoke toke hovyo hapa nyumbani kwenu, tulia hapa hapa halafu kila kitu nitasawazisha"
Mama akaanza kumshukuru Carlos.
"Asante sana baba, endelea na moyo huo huo jamani. Kwasasa Sabrina yupo chini yangu, hatoenda popote. Tusaidie tu baba hatuna cha kukulipa"
Carlos akaaga huku akiendelea kunisisitiza jambo moja tu kuwa nisiwasiliane na Sam wala Lucy halafu nisitoke toke nyumbani. Mama nae aliendelea kumshukuru hadi alipoondoka.
Niliingia chumbani na kujifikiria sana bila hata ya kupata majibu, yani ni jana tu ndio nilifika nyumbani halafu leo nimeenda kufanya mambo makubwa kama yale. Kwakweli moyo uliniuma na kukosa majibu ya niwazacho. Nikajiuliza je huyo Carlos ananisaidia kwa namna gani? Sikujua ila ninachojua ni kuwa ananisaidia tu, naona maisha yangu yanaelekea pabaya kwani kila kitu kinanitesa, mawazo ya mapenzi, mawazo ya maisha vyote hivi vinanitesa sana na wala sikuelewa ni nini kinaendelea kwangu, nikatamani kuwa na kazi ya kufanya ila sikuwa na kazi, nalo likawa ni tatizo pia katika maisha yangu.
Mawazo yalikuwa mengi sana kwangu bila hata ya majibu.
Nikamsikia dada Penina akiongea na mama sebleni na kugundua kuwa dada amerudi.
Akaja chumbani kwangu,
"Pole mdogo wangu kwa matatizo, mbona hujawahi kuniambia kama wewe na Lucy mnatembea na Sam?"
"Nilikwambia dada, labda umesahau tu"
"Pole sana, bora hata Carlos alikuwepo kukusaidia mdogo wangu"
Nilimuangalia tu dada bila ya kusema chochote cha zaidi, tukaongea pale hadi muda wa kula.
Tukaenda kula, kisha nikarudi chumbani mwangu kwaajili ya kulala.
Nilipokuwa chumbani, mawazo mengi sana yalinitawala hadi nikakosa usingizi.
Nikawaza hali ya Lucy kuwa anaendeleaje, nikajilaumu sana kwa kuamua kumpiga rafiki yangu sababu ya mwanaume, nikajisemea.
"Kama hanipendi hanipendi tu, kupigana sio suluhisho. Ama kweli hasira hasara"
Sikuwa na uwezo wa kuonana tena na Sam wala Lucy, halafu nitakuwa ndani kama mfungwa. Nimepata hasara kweli kwani sikuwa na amani tena. Nikatamani kumpigia simu Sam ila moyo wangu ukasita, mara simu yangu ikaita kuangalia alikuwa ni Carlos anayenipigia.
"Umelala Sabrina?"
"Nipo macho"
"Vipi, bado una mashaka?"
"Kiasi, lazima mashaka niwe nayo"
"Ondoa hofu Sabrina, muda wote tambua kwamba Carlos yupo kwaajili yako. Nitakusaidia kwa chochote na kwa lolote, usijali kitu chochote"
"Sawa nimekuelewa, asante"
"Lala kwa amani, nitakutembelea ndotoni mwako"
Nikacheka kwani nilijua ni maneno ya utani kwavile si rahisi mtu kuamua kutembelea ndotoni kwa mwenzie, nikaishia kumjibu.
"Haya karibu"
Nikaagana nae na kulala sasa.
Nikajiona nipo kwenye bustani nzuri sana, yenye upepo mzuri unaopepea kwa utaratibu unaopendeza.
Nikakaa chini ya mti mmoja wa matunda, halafu akaja yule kijana wa ndotoni mbele yangu akaita,
"Hawa"
Nikamjibu, "Mimi sio Hawa"
Akacheka na kuniuliza,
"Kwanini wewe sio Hawa?"
"Mimi naitwa Sabrina"
Akacheka tena, leo ikawa mara ya kwanza kwangu kuongea vizuri na huyu mkaka wa ndotoni kwenye ndoto.
Kisha akaniuliza,
"Kwanini ulitaka kumuua mwenzio?"
Hapo nikachukia sasa, naye akaendelea kuongea.
"Najua yote sababu ya mapenzi, kwanini uangamie sababu ya mtu mmoja? Je huoni mimi ninavyokupenda?
Na lazima nikuoe Sabrina"
Nikajibu kwa ukali,
"Huwezi kunioa"
Akacheka tena na kusema,
"Ndiomana nimekuita Hawa"
Akaendelea kucheka, nami hasira zikanizidi kwani sikujua ni kwanini ameniita Hawa na kwanini ang'ang'anie kuwa atanioa. Nikajibu kwa nguvu sasa,
"Huwezi kunioa"
Nikashtuka toka usingizini na kuhisi harufu ya marashi mazuri ikiwa imetapakaa chumbani kwangu, hapo uoga ukanishika na kuhisi mauzauza yanaanza kujirudia tena ila sikuona chochote zaidi ya ile harufu ya marashi iliyotapakaa chumbani kwangu.
Ila kabla sijafanya chochote tena, usingizi ulinichukua nikalala hadi kunakucha.
Nilipoamka asubuhi nikaenda kufanya kazi zangu kama kawaida, leo sikutaka kushurutishwa na nikakumbuka kuwa wifi alisema atakuja leo, pia rafiki yangu Suzy nae alisema kuwa atakuja leo kunipa habari kamili kuhusu Carlos.
Ujio wa wifi sikumwambia mama nilitaka ashtukizwe tu kwani najua ni kitu ambacho hajakitegemea, na leo dada yangu Penina nae alikuwa nyumbani kwani ilikuwa ni mwisho wa wiki.
"Nakuona Sabrina unajishughulisha sana leo"
Dada alinitania, halafu mama nae akadakia
"Mwache ajishughulishe, hapo alipo hana pa kwenda kwa mauza uza yake aliyoyafanya"
Ila dada akanipa moyo,
"Usijali Sabrina, yote yataisha"
Tulifanya kazi zote za asubuhi na kumaliza, mchana wake tukafikiwa na mgeni ambaye ni wifi Joy, mama akafurahi sana.
"Bora umemleta mjukuu wangu nyumbani kwa bibi na babu yake jamani"
Mama akampokea mtoto kwa furaha sana huku wakiongea mengi ya hapa na pale.
Dada Penina nae alikuja kumsalimia wifi ingawa anavisa nae vya muda mrefu sana.
"Karibu Joy, na bora umekuja mwenyewe maana sikuwa hata na mpango wa kuja huko"
"Ndio maneno gani hayo Penina?"
"Mmh mama, nimeongea tu kusafisha koo"
Maongezi mengine yakaendelea, wifi akaniambia kuwa kuna jambo muhimu sana lililomleta leo kuzungumza na mimi.
Wakati mama amembeba mtoto na kucheza cheza nae, mimi na wifi tukaingia chumbani kwangu ili tuongee kwanza.
"Sikia Sabrina mdogo wangu, kuna jambo kubwa sana nimeligundua kuhusu Carlos"
"Jambo gani hilo wifi?"
Kabla hajanijibu tukasikia mlango wa chumbani kwangu ukifunguliwa halafu akaingia Suzy, nadhani mama alimwambia kuwa aingie moja kwa moja chumbani kwangu. Ila alivyoingia tu, mara gafla nikamuona wifi akiinuka na kumtazama kwa makini Suzy kisha akamzaba kibao.
Mara gafla nikamuona wifi akiinuka na kumtazama kwa makini Suzy kisha akamzaba kibao.
Nikashangaa kwavile sikujua kwanini wifi kamzaba kibao Suzy, kisha akamkunja.
Ikabidi niingilie kati,
"Kwani kuna nini wifi? Huyu ni rafiki yangu."
Wifi akaongea kwa hasira
"Huyu rafiki yako hafai, ni kahaba huyu. Anatembea na mume wangu"
Kwakweli hapo nikaduwaa na kushangaa, wifi aliendelea kumkunja Suzy ambaye hata kujitetea alishindwa. Ikabidi nimuite mama ili aje kusuluhisha, mama nae akaja kuuliza.
"Kwani vipi hapa?"
Wifi akiongea kwa hasira tena,
"Huyu mtoto anatembea na mume wangu"
"Yani Suzy akatembee na mwanangu Deo! Si kama kaka yake yule jamani! Eti Suzy ya kweli haya?"
Suzy alicki akijiuma uma tu kwa maneno wala hakueleweka, ikabidi wote tutoke twende sebleni tukaongee vizuri.
Mama akamuuliza wifi,
"Unaushahidi lakini Joy?"
"Ndio ushahidi ninao, si unaona anashindwa hata kujibu kwa aibu"
Kwakweli sikuelewa, yani mume wa mtu anayetembea nae Suzy ndio kaka yangu Deo! Sikuelewa kabisa.
Mabishano yalikuwa makubwa sana kwani wifi hakukubali kumwachia Suzy, alitaka kumkomesha.
Nikajaribu kumpooza wifi ila ilikuwa ngumu huku akidai kuwa mume anauma. Nami nikajisemea kimoyo moyo kuwa hata mpenzi anauma ndiomana mi mwenyewe nimemuumiza Lucy bila ya kutarajia.
Ikabidi itumike njia nyingine ya kumuondoa Suzy pale nyumbani kwani wifi alikuwa na hasira sana tena sana.
Suzy alipoondoka, wifi nae hakukaa sana akaaga na kuondoka nadhani hasira ilimzidia halafu akahisi labda na sisi tunajua kitu kuhusu Suzy na kaka Deo ndiomana tukamruhusu Suzy kukimbia, kumbe na sisi hatujui chochote ndio kwanza tumemsikia yeye.
Ikabidi mama ndio amsindikize wifi kituoni kupanda gari sababu mimi sikuruhusiwa kutoka kwenda mbali sababu ya mkasa nilioufanya jana.
Wifi alipoondoka nilikaa na kutafakari, au wifi kamuona Suzy kwenye zile picha alizosema? Ila yule hakuwa Suzy bali ni Sam na Lucy. Ni nini hiki, mbona mambo ya ajabu sana! Sikufikiria kama mume wa mtu anayetembea na Suzy ni kaka yangu Deo. Inamaana Suzy hamjui kaka Deo au kaka Deo hamjui Suzy hadi wakawa pamoja?
Niliwaza sana bila ya kupata jibu la maana mpaka pale mama aliporudi. Naye akaendelea kuzungumzia jambo hilo hilo,
"Hivi ni kweli kabisa Suzy yupo na Deo? Hata siamini jamani"
Dada Penina akaja na yeye,
"Kwakweli mimi nafurahi kusikia kaka Deo ana mwanamke nje sababu Joy anajishauwa sana ila kwanini mwanamke huyo awe huyo Suzy? Nilikuwa chumbani nikiwasikiliza tu, kwakweli hii ni fedheha kubwa sana"
Mama akamuuliza dada
"Kwahiyo wewe unaona sawa tu Deo kuwa na mwanamke mwingine?"
"Ndio naona sawa kwani hata rafiki yangu alipinduliwa na Joy ila sijapenda kusikia mwanamke mwenyewe ni Suzy. Yani kaka Deo kaacha wanawake wa maana na kwenda kwa kale katoto! Si udhalilishaji huu, sijapenda kwakweli. Suzy nae hafai tena hana adabu kabisa, mtoto mdogo kuparamia waume za watu ndio nini? Ndiomana kipindi kile alidundwa hivyo hivyo"
Mimi na mama tulikaa kimya na kuendelea kushangaa kwani hatukuwahi kuwaza hata mara moja kuwa Suzy anaweza kuwa na mahusiano na kaka Deo, ilikuwa ni kitu cha kustaajabisha sana.
Jioni ya leo hali haikuwa shwari kama siku zote sababu familia ilikumbwa na maswahibu mchana wake.
Nikaenda jikoni kwaajili ya maandalizi ya chakula cha usiku kwani nikiendekeza mawazo nayo huwa hayaishi bora nimalizie kazi kwanza.
Wakati naandaa chakula cha usiku, nikapigiwa simu na Carlos,
"Hallow, unafanya nini muda huu Sabrina?"
"Nipo kupika chakula cha usiku"
"Wow, natumaini leo utanialika na mimi kuja kula usiku"
"Hata usijali, karibu sana. Muda ukifika wewe njoo tu ujumuike nasi"
"Asante Sabrina, nakutakia mapishi mema"
"Asante"
Nikakata simu na kuendelea kupika kama kawaida hadi nilipomaliza, kisha nikaenda chumbani kwangu kupumzika kwanza na kutuliza akili.
Nilitulia ndani nikitafakari mambo yanavyokwenda kwani sikuelewa hata moja na sikujua kwanini imekuwa kama ilivyokuwa ila sina la kufanya ukizingatia na mimi nishafanya mabaya ambayo hayajaipendeza familia yangu.
Muda wa kula ulipofika wote tulikaa pamoja kama kawaida na kupata mlo wa usiku, nilitoka mezani nikiwa na shibe ya kutosha ila nilivyoenda kitandani nilianza kuhisi njaa, nikawa kama vile mtu ambaye hajala kabisa, yani njaa ilinipata sana tumbo lilikuwa tupu kabisa kama sijala kumbe nimekula.
Nikatamani kwenda kuchukua chakula kingine ila nikahofia kuwa mama akijua atasema nina minyoo kumbe sivyo.
Wakati njaa ikinisumbua nikapata ujumbe toka kwa Carlos.
"Asante kwa kunikaribisha mlo wa usiku leo, nimeshiba sana"
Nikashangaa bila ya kumjibu huo ujumbe huku nikijiuliza mara mbili mbili, inamaana amekula chakula changu kweli? Na kama amekula basi amekulaje wakati sijamuona!
Hofu ikanijaa moyoni na muda huohuo Carlos akanipigia simu.
"Hujalala hadi saizi unangoja nini?"
"Hakuna kitu, mawazo tu"
"Pole kwa mawazo, ila mimi nipo nitakuliwaza wakati wote utakaonihitaji"
"Asante"
"Je, nikaribie kwenye ndoto zako pia?"
Hapo nikajiumauma bila ya kutoa jibu, kisha Carlos akasema
"Nitakutembelea ndotoni"
Na kukata simu, maneno ya Carlos yakaanza kunitisha na kuniogopesha ila swali langu likawa, mbona Carlos hafanani na yule mkaka wa ndotoni? Au hii kitu inamaana gani katika maisha yangu?
Sikuelewa kitu na kuamua kulala tu.
Nikiwa ndani ya usingizi mzito, nikajiona tena nipo kwenye bustani yenye maua mazuri ila leo kulikuwa na utofauti kidogo kwani paliwekwa meza na viti viwili mahali pale tofauti na siku zingine ambazo huwa nakaa chini ya mti, halafu akaja yule kaka wa ndotoni mbele yangu kisha akaanza kuongea.
"Hujapenda nilivyoweka leo?"
Nikawa kimya tu,
"Mbona hukai?"
Kisha akanishika mkono na kusogeza kiti kimoja wapo na kuniambia nikae, nami nikakaa na kuendelea kumsikiliza.
"Leo umenikaribisha kwenu, umenipa chakula kitamu sana ulichopika. Unajua nini Sabrina! Nilikula chakula chote ulichoandaa ndiomana nimeshiba sana. Sasa na mimi nimekuandalia chakula kizuri sana muda huu kama asante yangu"
Kisha akanyoosha mkono, mara nikaona chakula kimewekwa mezani, kilikuwa na harufu nzuri sana.
Nikatulia tu huku nikimuangalia yule mkaka, akasema tena.
"Karibu ule Sabrina"
Nikasita ila gafla nikajikuta nikila kile chakula huku nikionyesha kukifurahia tu.
Nilipomaliza, yule mkaka akatabasamu na kusema.
"Nitakualika tena katika kufurahia kitu kizuri katika maisha yetu"
Nilikuwa kimya kabisa, sikuweza kumjibu chochote kile labda leo nilizibwa mdomo.
"Muda wa kukurudisha umefika, nitakuja tena badae kukutembelea nyumbani kwenu"
Halafu akanikumbatia, na gafla nikashtuka toka usingizini na kugundua kuwa kumekuchwa, kichwa changu kilikuwa kizito sana.
Simu yangu ikaingia ujumbe mfupi, nikachukua na kuangalia ulikuwa umetoka kwa Carlos ukisema kuwa,
"Badae nitakuja kwenu kukutembelea Sabrina"
Nikashtuka sana na kuanza kukumbuka matukio ya ndoto, kisha nikaoanisha matukio ya ndoto na Carlos nikaanza kuhisi kuwa huenda yule mkaka wa ndotoni akawa ni Carlos, nikawaza bila jibu ila nikajipanga kumuuliza huo muda atakaokuja ili nijue mbivu na mbichi.
Nikainuka na kwenda jikoni huku kichwa changu kikizungukwa na mawazo ya kila aina, nikahisi kama mkono wangu wa kulia unanata kwenye kiganja, nikaangalia na kuunusa nikapata ile harufu ya chakula kwenye ndoto halafu tumbo langu lilikuwa limeshiba sana, nikajiuliza je nilikuwa nakula kweli? Na kama ni kweli kwanini inakuwa ndotoni? Sikupata majibu kwakweli.
Wakati nipo jikoni dada Penina akarudi na nikajua moja kwa moja kuwa ametoka dukani, kisha akaenda mezani na kuandaa chai.
"Mbona leo mapema sana dada?"
"Yani wee acha tu, njaa inaniuma kamavile usiku sijala, ndiomana nimedamkia kwa mama muuza chapati kwanza ili ninywe chaji nipooze tumbo kwanza"
Mama nae akatoka chumbani kwake na kunikuta na dada tukiulizana pale.
"Khee jamani hata mimi njaa inaniuma sana yani kamavile sikula usiku wa jana, sijui chakula kimeyuyuka mdomoni!"
Dada akacheka kisha tukamsalimia mama, halafu dada akaendelea kuongea.
"Itabidi tumuulize Sabrina vizuri labda jana katupikia hewa"
Mama akacheka na kujiunga na dada mezani katika kunywa chai halafu mimi nikaendelea na kazi jikoni huku nikijiuliza maswali mengimengi, je huyo Carlos kama jana ndio alikaribia kwetu kwa chakula cha usiku ndio ale chote peke yake kweli? Hata sikuelewa kwakweli na maswali yangu yalikosa majibu, nikajiandb kwa maswali mengi sana muda atakaofika Carlos nyumbani.
Mchana wa leo nilijikuta nikimkumbuka sana Sam wangu, nikatamani kuwasiliana nae ila maneno ya Carlos yakanifanya nisite kwa muda, ila baada ya kutafakari zaidi nikaona si kosa kumpigia simu Sam na kumsalimia tu.
Nikachukua simu ili kumpigia ila hakupatikana, nikamtumia ujumbe ili atakapopatikana basi anitafute kwanza.
Mawazo juu ya Sam yalinitawala sana huku nikijiuliza kuwa atakuwa wapi na anafanya nini kwa muda huu, ni kweli nampenda sana Sam na moyo unaniuma sana kuona penzi letu limeingia madoa, ila kwasasa nilikuwa tayari kurudiana na Sam ili tujaribu kufungua ukurasa mpya wa mapenzi kwani nadhani kuwa Sam kashajifunza vya kutosha huku nikijipa moyo kuwa, kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa.
Mama alikuja na kunishtua katika yale mawazo ambapo nikaropoka,
"Kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa"
Mama akaikanusha kauli yangu na kusema,
"Hapana, kutenda kosa ni kosa ila kurudia kosa ni kosa kubwa"
Nikamuangalia tu mama na kutabasamu ili asiweze kugundua ninachowaza kwa muda huo.
"Nina maswali matatu ya kukuuliza Sabrina"
"Maswali gani hayo mama?"
"Muda bado ila muda ukifika nitakuuliza maswali yangu"
Hapohapo nikakumbuka kuhusu mama Salome ambaye sijaiulizia hali yake tangu siku niliyorudi nyumbani.
"Eeh mama, mama Salome anaendeleaje?"
"Anaendelea vizuri, ila si nilikwambia wewe kuwa mama Salome amepararaizi! Kwakweli anitia huruma sana, hawezi fanya chochote hadi afanyiwe"
"Mmh pole yake, ngoja haya mambo yaishe kwanza ili niweze kumuona"
"Itakuwa vizuri ukienda, ngoja hali itulie mwanangu"
Tukakubaliana na mama pale, kisha akaja dada Penina.
"Nimekutana na Suzy, yani kanywea kweli aliponiona. Anatembea na Deo kweli yule atakuwa ndomana anaona aibu" http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Sikutaka kuzungumzia habari ya Suzy, hivyo nikainuka na kwenda chumbani na kumuacha mama azungumze mwenyewe na dada Penina.
Ila baada ya muda wakaniita kuwa kuna mgeni wangu nikajua tu kuwa ni lazima atakuwa Carlos, nami nikatoka huku nikijiandaa na maswali yangu kichwani.
Nikafika sebleni, wakaniambia kuwa yupo nje ananingoja.
Nikatoka nje na kumkuta Carlos akiwa amesimama kwa kuegemea ukuta akiningoja.
Moja kwa moja nikamuuliza,
"Mbona leo hujaingia ndani?"
"Aaah nimepapenda hapa nje leo, nadhani patanifaa"
"Basi ngoja nikalete viti"
"Acha tu, mi sio mkaaji sana nimekuja kukuangalia tu"
Nikajua anataka kukwepa maswali yangu, sikutaka kupoteza muda nikaanza kumuuliza hapohapo.
"Samahani Carlos, hivi wewe ni nani na unamaana gani kwenye maisha yangu?"
"Kivipi Sabrina?"
"Jana umekuja kimazingara, umekula chakula chetu chote. Halafu usiku umenijia ndotoni na kunilisha mavyakula yako ya ajabu. Niambie ukweli Carlos, wewe ndio yule kijana anayenitokeaga kwenye ndo....."
Kabla sijamalizia, nikaona sura ya Carlos ikibadilika na kuwa sura ya yule kijana wa ndotoni.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment