Simulizi : Sitasahau Tanga
Sehemu Ya Tatu (3)
Nikiwa bado na mawazo, nikasikia sauti ya mama na dada nje ina maana nao wamefika kwangu. Nikajihisi baridi ikipenya mwilini mwangu, nilikuwa nikitetemeka balaa. Sikuwa na raha wala furaha.
Mara sms ikaingia kwenye simu yangu,
"yote yale yalikuwa ni majaribio sasa picha kamili itaanza."
Nikapatwa na hofu kubwa moyoni, sikuwa na furaha kwakweli. Nikahisi mama na dada wakizidi kusogelea mlango wangu, wakaanza kubisha hodi huku wakiniita jina langu sikutamani kuitika kwakweli nilijiona na mtu mwenye mkosi pale ndani, mama alizidi kubisa kuwa nifungue na nisipofanya hivyo atapiga kelele ili watu waje kubomoa mlango, aliposema hivyo nikahisi kupagawa kabisa kwani yule binti alinambia kuwa nikipiga kelele basi atauondoa kabisa uhai wa wale waliopoteza fahamu mule ndani, nilipofikiria hayo nikaenda mlangoni na kuwafungulia mlango. Baada ya kuwafungulia tu wakaingia moja kwa moja ndani nami nikaurudishia mlango,
MAMA: Mungu wangu, umemfanya nini kaka yako? (huku akimfata pale chini na kumtingishatingisha).
MIMI: (Huku nikitetemeka), hapana mama sijamfanya chochote.
DADA: Hivi una akili wewe? Yani wenzio wanatapatapa humu ndani na wewe umetulia kabisa kana kwamba hakuna kilichotokea.
MIMI: Dada sielewi kitu.
Mama akiendelea kumwamsha kaka pale chini huku akijisemea,
"jamani mwanangu, sijui amekufa".
Mama ndio alikuwa hajielewi kabisa bora hata ya dada, mara yule binti akanipigia simu,
BINTI: Mwambie mama asilie.
MIMI: Usinichanganye ujue! Wewe ndio umesababisha yote haya.
BINTI: Mpe simu mama nimueleweshe tafadhari.
MIMI: Hapana, naogopa nae utamfanya kama hawa.
BINTI: Unampenda mama yako?
MIMI: Ndio nampenda.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
BINTI: Ok mpe simu niongee naye.
Nikiwa bado sina maamuzi sahihi nikawa nimeganda na ile simu sikioni, dada akauliza
DADA: Kwani nani huyo?
MIMI: Eti anataka kuongea na mama.
DADA: Mpe basi mama aongee naye.
Nikampa mama simu, naye akaweka sikioni akiwa kakaa pale chini nikamwonga akiangukia pale pale, dada akapiga ukelele wa ajabu huku akimwita mama "mama mama mamaaaa".
Ilikuwa ni kitendo cha gafla dada nae akaichukua ile simu na kuiweka sikioni nahisi alitaka kujua ni nani huyo aliyeongea na mama, kufumba na kufumbua nae akawa chini akitapatapa.
Nilizidi kuchanganyikiwa kwakweli, na mimi nikachukua ile simu na kuiweka sikioni labda na mimi kinipate kilichowapata wenzangu ili nisiwe na ufahamu tena, ila nilipoiweka sikioni nikimsikia yule binti wa kitanga akicheka sana,
MIMI: Umewafanya nini ndugu zangu?
BINTI: Unataka kujua nilichowafanya?
MIMI: Ndio niambie umewafanya nini?
BINTI: Haya tazama hapo chini.
Halafua akakata simu, kuangalia pale chini hakuwepo mtu yeyote, wote walitoweka. Nikapagawa hakuna mfano nikahisi kurukwa na akili mule ndani, nikataka kwenda nje na kukimbia, simu ikaita tena,
BINTI: Usithubutu kwenda popote kama bado unawapenda ndugu zako.
MIMI: Unajua sikuelewi wewe? Yani sikuelewi kabisa, unamaana gani kunifanyia mambo haya?
BINTI: (Akacheka sana), maana yangu utaijua tu ila Kama unawapenda ndugu zako hawa, usiende popote pale.
Akakata simu, nikazidi kurukwa na akili mule ndani.
nakufa jamani, ama aliyesema kufa hufi ila chamoto utakiona wala hakukosea. Niliungua sana mule pipani, mara kuna mtu akaja kuniopoa kumwangalia ni yule yule mtoto wa kitanga, akawa anacheka sana.
BINTI: Vipi umejisikiaje hapo?
Nikataka kumjibu ila nashangaa sikuweza kufanya hivyo kwani mdomo ulikuwa mzito sana, akaniambia tena,
BINTI: Nina uhakika kama ukipona na haya nikufanyiayo hutorudia tena kubeba mizigo ovyo ovyo. (akacheka sana na kutoweka).
Nikawa natetemeka mahali pale ila kilichonishangaza ni kuwa nimechemka kwenye lile pipa halafu sijababuka mwili, mara akaja yule mtu aliyeniongoza mwanzo na kunishika tena mkono kunipeleka sehemu nyingine.
Tukaingia chumba ambacho akaniacha mimi peke yangu na yeye akatoka, yani chumba kilikuwa na siafu wengi sana walining'ata kila sehemu ya mwili wangu hadi nikajihisi mwili unakufa ganzi kwakweli ni maumivu yaliyopitiliza.
Baada ya muda akaja na kunifungulia nikatoka mule ndani nikiwa na madonda ya kila aina. Akaniuliza,
"unapenda sana wasichana?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nikatikisa kichwa nikiashiria hapana. Akanichukua na kunipeleka sehemu nyingine.
Tulifika sehemu ambayo mbele yake kuna wasichana wazuri sana tena wa kuvutia, yule mtu akanigeukia na kuniambia,
"kijana chagua mmoja hapo"
Nikakataa kwa kichwa kuwa simtaki yeyote, sikuwa na hamu na msichana yeyote kwakweli, yule mtu akaniambia tena,
"inamaana huwaoni walivyo warembo wale mabinti?"
Nikatingisha tena kichwa kuonyesha kwamba siwataki wale wasichana.
Tukaondoka mahali hapo, nikapelekwa sehemu ambayo nilikuta wanaume wenzangu wamepanga foleni halafu kuna mtu mmoja mbele ana panga kubwa sana yani ukimkaribia anakuchinja kama kuku dah nilihisi kupagawa nikatamani kukimbia ila sikuweza, yani yule mtu hakuwa na huruma kabisa kila aliyemfikia alimchinja kama kuku na mimi nikawekwa kwenye huo mstari.
Niliona mwisho wangu umekaribia, nikamaliza sala zote kimoyomoyo nikajikuta nikitubu kila aina ya dhambi niliyotenda, machozi yalinibubujika kila hatua niliyomsogelea yule mtu, nilijikuta nikilia kama mtoto mdogo sikuwa na jinsi zaidi ya kujisogeza ili nikabidhi kichwa changu iwe halali yao.
Nikakosa raha kwakweli, nikachukia moyoni na kuwaza mwisho wa mambo haya ni lini. Mara dada akanipigia,
DADA: Vipi tena mbona hutumi hiyo pesa?
MIMI: Aaah mmmh kuna tatizo kidogo dada ngoja nitatuma badae.
DADA: Nilijua tu mxyuuuu(akanisonya).
Akakata simu, bado akili yangu haikuwa sawa hadi pale mlango wangu ulipogongwa, nikaenda kufungua kumbe ni rafiki yangu alikuja kama alivyoniahidi jana.
RAFIKI: Vipi upo tayari tuondoke?
MIMI: Ndio nilikuwa nataka kutoka hapa kaka.
RAFIKI: Basi twende.
Mara simu yangu ikaita, nami nikaipokea,
BINTI: Mwambie rafiki yako aache kufatilia mambo yangu.
MIMI: Kivipi jamani mpenzi?
BINTI: Inamaana hujui rafiki yako amefata nini?
MIMI: Hapana sijui.
BINTI: Hivi unajua kama ninaouwezo wa kuwazuia msitoke hapo?
MIMI: Kwani vipi mpenzi mbona sikuelewi?
BINTI: Mpe rafiki yako simu nimuulize kitu.
Nikampa rafiki yangu simu ili aongee na yule binti, kilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua yani baada ya kumkabidhi simu rafiki yangu ili aongee naye nikashtukia rafiki yangu akianguka chini na povu jingi likimtoka mdomoni, moyo ukanipasuka kwakweli nilijikuta nikitetemeka na kuona baridi ila jasho jingi likinitoka. Kwakweli nilichanganyikiwa nilitamani ardhi ipasuke nidumbukie.
Nilimwangalia rafiki yangu pale chini akiwa katulia tuli hata nisijue cha kufanya, nikatamani kupiga yowe la msaada. Nilipotaka kufanya hivyo, simu yangu ikaita
BINTI: Usithubutu kupiga kelele kama unapenda kumuona rafiki yako akiendelea kupumua.
MIMI: Nihurumie tafadhari nakuomba nihurumie.
BINTI: (Akacheka sana).
Akakata simu, mapigo ya moyo yalikuwa yananienda kwa kasi balaa.
Sikujua msaada gani nimpe rafiki yangu pale chini. Nikainama na kujaribu kumuinua ili nimuweke kitandani ila alikuwa mzito kama jiwe tena alizidi kukoroma na povu jingi likimtoka mdomoni. Hofu ikazidi kutanda moyoni mwangu na mawazo mengi yakinitawala huku nikiomba sala zote ili nikomboke na lile janga.
Nikakaa pale chini karibu na rafiki yangu, nikatamani nichukue simu na kuwapigia watu ili niombe msaada ila nikasita kufanya hivyo.
Nikajifikiria tena, ikabidi nichukue simu nimpigie kaka.
MIMI: Hallow kaka nina matatizo tafadhari njoo nyumbani kwangu.
KAKA: Kwani vipi tena mdogo wangu?
MIMI: Tafadhari kaka njoo.
KAKA: Poa nakuja mdogo wangu.
Nikawa na matumaini ya kupata msaada sasa.
Mara kidogo yule binti akanipigia
BINTI: Aliyekutuma umpigie kaka yako simu nani?
MIMI: Aaah eeh sijui hata sielewi.
BINTI: Unampenda kaka yako?
MIMI: Ndio nampenda.
BINTI: Kama unampenda mpigie tena simu sasa mwambie asije.
MIMI: Itakuwaje sasa?
BINTI: Fanya kama nilivyokwambia.
Akakata simu, hata sikujielewa kwakweli nikachukua simu na kumpigia tena kaka lakini namba yake ikawa inaita tu bila ya kupokelewa.
Baada ya muda kupita kupita, kaka akanipigia simu.
KAKA: Nakaribia kufika mdogo wangu, naona missed call yako hapa vipi ulikuwa unasemaje?
MIMI: Nilikuwa nakwambia basi tena usije.
KAKA: Hebu acha ujinga wako huo, nimetoka haraka haraka nyumbani halafu unasema nisije tena! Mi nakuja.
MIMI: Dah usije kaka, tafadhari usije.
KAKA: Kwani kuna nini wewe? Nakuja bhana.
Akakata simu, nikawa ni mtu mwenye mawazo hata nisijue cha kufanya tena muda ule huku nikihofia maisha ya kaka yangu.
Nikamwangalia tena rafiki yangu pale chini, nikamfikiria na kaka yangu anaekuja nguvu ziliniisha kabisa. Mara akanipigia simu,
BINTI: Umeshindwa kabisa kumzuia kaka yako kuja hapo?
MIMI: Nimeshindwa, nihurumie tafadhari.
BINTI: Nitakachokifanya usinilaumu badae.
MIMI: Jamani nihurumie, nihurumie nakuomba.
BINTI: Huruma yangu utaiona akifika kaka yako mahali hapo.
Akakata simu, nikawa kama mtu aliyepagawa. Nikachukua simu na kumpigia dada,
MIMI: Tafadhari dada nakuomba umzuie kaka asije kwangu.
DADA: Kwani kuna nini?http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
MIMI: Hamna kitu ila mzuie.
DADA: Una matatizo gani wewe?? Na mimi nakuja huko nijue kinachoendelea.
MIMI: Mungu wangu, dada nakuomba usije.
DADA: Khaaa, nakuja sasa.
Akakata simu, nikazidi kuchanganyikiwa nilitamani hata nipae nitokana na haya maswahibu.
Yule binti akanitumia sms,
"ndugu zako wanacheza na moto"
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment