Search This Blog

MTEMI NYANTUMU - 2

 

    Simulizi : Mtemi Nyantumu

    Sehemu Ya Pili (2)





    Matumaini baada ya kumaliza shughuli zote za Nyumbani hasa kupika chakula, shughuli zote ambazo alizifanya kwa siri kubwa ili asitambulike na kuonekana na raia hata mmoja wa Mwamutema. Matumaini alielekea bafuni kuoga, na kujikuta akipuuzia sharti ambalo alipewa na mama yake mzazi … ,kwa mala ya kwanza aliuvua mkufu,na kuanza kuoga  kuusafisha mwili wake. Siku zote zilipita akiwa salama, hivyo aliamua kuvua mkufu aweze kuona kama kuna tatizo lolote ambalo lingeweza kumtokea na kumfanya kuamini nguvu za mkufu ule kama zilimlinda au sivyo …



    Hatimae Mzimu Nkuru uliweza kumtazama katika uso wake, na Kukariri sura yake kichwani, sura ambayo ilifanana kabisa na mama yake Nyoni, hatimae siri ikagundulika kijijini ……mala baada ya Matumaini kukiuka masharti na kuuvua mkufu wa ajabu kutoka shingoni mwake ……



    ………………………………



    “Mzimu Nkuru, nimekuja kwako Igweeeh, nchi yetu imekumbwa na ukame ,nahitaji msaada wako “,



    “Nalifahamu hilo tatizo, tayali matatizo yameanza kuwakumba, kumbukeni ishara ya mtoto wa kike kuzaliwa miaka kumi iliyopita, mtoto aliyezaliwa ni mtoto wa mzee Mbutu. Hivyo alivalishwa mkufu wa ulinzi, na ndio maana hatukumtambua, kuhusu mimba kuharibika tuliweza kudanganywa, hivyo nenda kaue familia na ukoo wote wa mzee Mbutu bila hivyo laana hazitaisha kijijini “,yalikuwa ni mazungumzo kati ya mzimu Nkuru na mtemi Nyantumu, baada ya mtemi Nyantumu kufanya tambiko katika mti wa mzimu Nkuru alipofika haraka sana kuomba msaada juu ya matatizo yaliyoikumba Mwamutema.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wazazi wa Nyoni, pamoja na Nyoni wakiwa wanaendelea na shughuli zao za shambani, shughuli za kupalilia mahindi ambayo yalibahatika kuendelea kuishi kwani mazao mengi yalikauka kutokana na ukame uliodumu kwa miezi kadhaa. Kutokana na kuishi na Matumaini kwa muda mrefu bila jambo lolote baya kutokea, walikuwa wameshasahau kwamba ukame huo ulisababishwa na umli wa Matumaini kufanyiwa mila kupitiliza, walisahau kuwa kama Matumaini hata keketwa kwa wakati sahihi, basi laana zingeweza kuikumba Mwanamutema.



    Ghafla nyuso zao zilibadilika, nafsi zao zilionekana kuhisi jambo fulani, tena jambo ambalo halikuwa la kawaida. Kwakua muda ulikuwa umeshaenda sana, na jua lilikua linakalibia kuzama, waliamua kusitisha shughuli zote za shambani na kuwahi nyumbani haraka sana ……



    “Nimechoka sana, na mapigo ya moyo yanaenda kasi, sijui hata tatizo ni nini ……??”,mama yake Nyoni alitupa jembe lake chini, na kisha kuongea maneno hayo huku akiusogelea mti wa maembe uliokuwa shambani pale kwa ajili ya kupumzika ……



    “Mimi naona nimechoka zaidi yenu, harafu nina hofu sana siku hizi, pengine ukame huu unaweza kusababishwa na laana za mzimu Nkuru, laana za kukataa kumfanyia mila binti yetu, naomba tuelekee nyumbani, siwezi kuendelea kulima ……” ,mzee Mbutu aliongea, huku mawazo mengi yakikisumbua kichwa chake. Japo Nyoni alionekana kutaka kuendelea kufanya kazi, lakini ilibidi asitishe na kuungana na wazazi wake kurudi nyumbani..



    …………………………………



    Mtemi Nyantumu alifika ikulu akiwa na hasira sana, hasira ambazo zilisababishwa na siri iliyoweza kugundulika. Moyoni aliwaza kuuwa tu na wala sio kitu kingine.



    “Chukueni mapanga na siraha zote ambazo zinaweza kuwasaidia, nendeni mkakamate ukoo wote wa mzee Mbutu ……,kesho tutawachinja mbele ya wana kijiji wote ili iwe fundisho kwa wengine ……”,mtemi aliongea kwa uchungu sana, kwani hasira iliweza kumtawala baada ya kugundua kuwa matatizo yao yalisababishwa na familia ya mzee Mbutu, baada ya kutaka kukwepa mtoto wao asiweze kufanyiwa mila ya ukeketaji, na kuamua kumvisha mkufu Matumaini ambao ulimfanya asiweze kuonekana mbele ya mzimu Nkuru. Hivyo basi, kundi kubwa la askari wa Mtemi Nyantumu, walishika siraha zao na kuanza safari ya kuelekea kijijini ……



    …………… ……………………



    Mama yake Nyoni alishtuka sana, kwani aliweza kugundua chanzo cha fikra zao kuhisi vibaya sana na kuwa na machale wakiwa shambani. Alisitisha kuendelea kuoga, na kuvaa nguo zake haraka sana ili kuyaokoa maisha ya binti yake pekee wa kike, msichana mrembo sana aliyeitwa Matumaini.



    “Igweeeh mume wane,Mwanawachu afwaah …!!(igweeeh mume wangu, mtoto wetu anakufa…!!) “,mama yake Nyoni alikurupuka kutoka bafuni huku akikimbia na kutamka maneno ya mshangao kwa lugha ya Kimutema, kiasi kwamba aliweza kuwashtua Nyoni na mzee Mbutu, na wote kwa pamoja waliweza kutoka nje.



    “Kuna nini mama!! “Nyoni aliongea baada ya kutoka nje, na kumkuta mama yake kashikilia kitu mikononi mwake, huku Nyoni akijitahidi kukitambua kitu kile ambacho hakikuwa kigeni machoni kwa Nyoni na alionekana kukifananisha na mkufu wa mdogo wake Matumaini ………



    “Amevua mkufu, hapa hakuna siri tena, kilichobakia ni nyie kutoroka kijijini haraka sana iwezekanavyo ……” ,



    “,Amevua mkufu …?? ,Igweeeeh mizimu ya babu yangu, mbona mnataka kunichukulia mwanangu kipenzi, naomba mniepushe na bala hilii ……”,baba yake Nyoni alizungumza kwa huzuni, huku akielekea katika kibanda ambacho binti yake Matumaini alikuwa akiishi na kujificha huko.. …



    “Matumaini binti yangu, umefanya nini  .……? Mbona unahatarisha maisha yako na wazazi wako, kwanini umevua mkufu niliokupatia …??”, mama yake Nyoni aliongea kwa sauti huku akiwa amelisogelea banda ambalo binti yake aliweza kuishi.



    “Nisamehe mama, imeshatokea!!  ……sikutegemea na sijitambui ilikuwaje mpaka nikasahau masharti uliyonipatia “, ilikua ni sauti nzuri ya binti mrembo Matumaini, mdogo wake kipenzi na kijana hodari aliyeitwa Nyoni ……

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sasa tuko hatarini kuuawa, haraka sana chukua kila kitu chako,vaeni mikufu shingoni na mtoroke kijijini wewe na kaka yako Nyoni. Nendeni katika kijiji cha Ukarimu, huko mtakua huru, na siku mkitaka kuja huku, mrudi na dawa ya kuangamiza mila hii hatari, mila ya ukeketaji inayopatikana hapa kijijini na kupelekea watoto wengi wa kike kupoteza maisha, kwani wanapoteza damu nyingi sana. “,mama yake Nyoni alimpatia maelekezo mwanae Matumaini jambo la kufanya, na bila kupoteza muda matumaini aliingia ndani kufungasha nguo zake kwa ajili ya kutoroka kijijini ……



    “Mwanangu Nyoni, miaka mingi iliyopita tuliweza kutabili kuhusu jambo hili kutokea, na siku zote binadamu analolitamka na kuliwazia sana, ndilo ambalo ataweza kulivuna. Hivyo basi, timiza kila kitu ulichotuahidi kuhusu ulinzi kwa mdogo wako. Hakikisha hapati kiu, njaa na hakuna kiumbe chochote kibaya kinasogeza mkono wake kumdhuru Matumaini ………igweeh mizimu ya mababu ikutangulie katika safari yako kuelekea kijiji cha Ukarimu,na ukirudi huku, hakikisha unakuja na dawa ya kuangamiza mila hii ………”,baba yake Nyoni aliongea huku Nyoni  akiwa ameshikilia upinde wake mkononi, na mishale mingi ikiwa imefungwa vizuri katika mgongo wake, tayali kwa ajili ya safari.



    “Sawa baba ,najua muda wowote mtakamatwa lakini hamtaweza kuuawa mpaka sisi tupatikane na muhusika kuwepo, hivyo basi nawa ahidi kurudi na dawa mapema sana iwezekanavyo na kukomboa kijiji kutoka katika mila hii ambayo ina madhara makubwa katika jamii ……”, Nyoni alimshika mkono dada yake ambaye tayali alikuwa ameshafungasha kila kitu chake, na kuwaaga wazazi wake kabla ya kuanza safari ndefu, safari ambayo ilikuwa na hatari nyingi mbeleni, hasa katika kuvuka pori hatari la Nyankonko lenye wanyama na viumbe wengi wa kutisha ……



    “Sawa mtoto wetu, safari njema igweeeh “,wazazi wake Nyoni waliwaaga watoto wao,huku wakitokomea katika giza la majira ya saa mbili usiku. Huku nyuma yao wakifuatwa na mbwa hodari sana katika mawindo, mbwa ambae alimfuata Nyoni kila sehemu aliyokwenda.



    …………………………………



    “Igweeeh mzee mbutu, toka nje na familia yako yote, safari na ujio huu nyumbani kwako sio wa heri …………!!!”,



    Ilikua sauti ya kutisha, sauti ya kiongozi wa kundi kubwa la mtemi Nyantumu, kundi la askari ambao walitumwa kukamata ukoo wote wa mzee Mbutu. Mama yake Nyoni pamoja na mzee Mbutu walitoka nje, huku wakiwa na wasiwasi sana pengine watoto wao waliweza kukamatwa tayali, kwani ni dakika chache tu walikuwa wametoweka nyumbani na kutokomea kuelekea kijiji cha Ukarimu.



    Tabasamu lilizipamba nyuso zao, wote kwa pamoja waliangaliana na kushukuru mizimu ya ukoo kwa kufanikisha Nyoni na Matumaini kutoroka salama. Kwani baada ya kutoka nje, walikuta askari wa Mtemi wakiwa na kundi kubwa la ndugu wa mzee Mbutu, shangazi zake, mjomba pamoja na ndugu katika upande wa mkewe. Lakini katika ndugu wote ambao walikuwa tayali wamekamatwa, Nyoni na Matumaini hawakuwa miongoni mwao, hivyo waliashiria kufanikiwa kutoroka salama usiku ule. Hivyo basi, ukoo wote wangefungwa katika magereza ya kijiji, kusubili mpaka Nyoni pamoja na muhusika mkuu ambaye ni Matumaini kukamatwa na ndipo waweze kuwaua.



    Mwantema;



    Fujo na kelele nyingi ziliendelea kusikika katika nyumba ya mzee Mbutu, kelele ambazo zilitokana na mabishano ya askari wa mtemi Nyantumu, pamoja na ukoo wa mzee Mbutu. Chanzo cha mabishano hayo, ni kitendo cha Nyoni pamoja na mtoto wa kike aliyesadikika kuzaliwa na kukulia kwa mzee Mbutu kutoonekana.



    “Nyoni na mtoto wenu wa kike mmewaficha wapi,?? “,ilikua ni sauti ya hasira iliyoambatana na swali kutoka kwa kiongozi wa askari wa Mtemi Nyantumu, swali ambalo liliulizwa kwa mzee Mbutu pamoja na ndugu zake.



    “Hatujui walipo, nazani hata nyie mmetafuta kote hamjawaona ……”, mzee Mbutu kwa ujasili alijibu bila woga swali la askari yule, jibu ambalo liliambatana na kejeli kwa askari wale. Kutokana na giza kuzidi kuwa kali kwani masaa yalizidi kwenda mbele, kiongozi yule aliamua kuwapeleka mzee Mbutu na ukoo wake ikulu kwa mtemi Nyantumu, huku baadhi ya askari wakitumwa kuelekea katika barabara kuu. Barabara ambayo ilipita katika pori la Nyankonko na kisha kuelekea kijiji cha Ukarimu.



    “Sawa mtavuna jeuri yenu, endeleeni kuwa na kiburi. Igweeeh askari hodari wa mtemi Nyantumu, naomba askari wawili ongozeni kundi hili pamoja na mimi kuelekea kwa mtemi Nyantumu. Askari wengine mliobakia fuateni njia kuu, nina imani watakua wameelekea kijiji cha Ukarimu ………”, yalikuwa ni maelekezo kutoka kwa kiongozi wa askari wa mtemi Nyantumu, maelekezo ambayo yalizingatiwa punde tu baada ya kauli hiyo kumalizika kutamkwa.



    “Igweeeh ……mbwa wa Mtemi Nyantumu, dimaaaah, dimaaaa …kijiji cha Ukarimu ……”,Askari yule aliamua kuamrisha mbwa hatari wawili,baadhi ya mbwa wa mtemi Nyantumu ambao waliongozana nao kukamata ukoo wa mzee Mbutu. Baada ya kutamka maneno yale kwa kutumia lugha ya Kimutema, mbwa wale waliongozana na askari zaidi ya wanne kuelekea barabara ya kijiji cha ukarimu huku wakitimua mbio na kupotelea gizani.



    Baada ya kundi dogo la askari takribani watano wa mtemi Nyantumu kutokomea gizani na kuwafuatilia Nyoni na Mazoea ,hatimaye ukoo wa mzee Mbutu uliweza kupelekwa kwa mtemi Nyantumu usiku ule chini ya ulinzi mkali. Huku wanakijiji wengi wakitamani kukuche mapema, na kushuhudia vifo vya ukoo wa mzee Mbutu kwani waliamini Nyoni na mtoto wa kike ambaye hakuwahi kuonekana kwa sura hata siku moja na wanakijiji, lazima wangekamatwa.



    ……………………………



    Pori la Nyankonko;



          Kijana hodari Nyoni aliweza kumubeba mgongoni dada yake kipenzi Matumaini. Matumaini aliweza kuchoshwa na safari ndefu ya kukimbia kwa muda mrefu bila kupumzika, lakini Nyoni hakuwa tayali kupumzika bila kufika katika pori la Nyankonko. Kwani aliamini huko ni mbali sana kuweza kufika kwa askari wa mtemi Nyantumu usiku ule na kuwakamata.



    Nyoni hakukata tamaa, hakutaka kumtesa mdogo wake na isitoshe alikuwa ni wa kike. Alijikaza kiume na kumubeba mdogo wake kusonga mbele, kulisogelea pori la Nyankonko. Barabara ilijaa mchanga pamoja na miba iliyodondoka kutoka katika miti iliyopakana na barabara ,japo miguu ya Nyoni ilididimia katika mchanga huku akichomwa na baadhi ya miiba. Nyoni alizidi kusonga mbele, huku mbwa wake akitangulia mbele na kumuongoza. Alijiamini kupita maelezo, huku akiwa makini kupambana na adui yoyote ambaye alitaka kuwadhuru.



    “Usjali dada yangu, hakuna wa kukudhuru. Atakayejaribu kukugusa nitatenganisha kichwa chake na kiwiliwili,sio mimi tu, hata Nyonta hayuko tayali kuona unapata madhara “,Nyoni aliongea  huku akiendelea kumfuata mbwa wake aliyeitwa Nyonta, mbwa ambaye alikuwa akimuongoza katika safari ndefu na hatari ya kutoroka katika kijiji cha Mwantema, kuelekea kijiji cha Ukarimu.



    “Sawa kaka nimekuelewa, asante kwa  kunilinda, nitajitahidi kulipa fadhira siku moja ……”,binti mrembo sana aliyeitwa Matumaini, akiwa na umli wa miaka kumi na mbili. Alizungumza kwa upole sana huku akiwa katika mgongo wa kaka yake shupavu aliyejulikana kwa jina la Nyoni.



    “Nyantuu ……!! Simama tupumzike kwenye mti huu, nazani pori la Nyankonko ndio hilo mbele, hatuwezi kuendelea na safari mpaka kesho asubuhi ……”, baada ya hatua kadhaa mbele, pori la Nyankonko lilionekana mbele ya macho ya Nyoni. Kutokana na wanyama wakali kuwemo ndani ya pori hilo hatari na maarufu katika kijiji cha Mwantema, Nyoni alishindwa kuendelea na safari. Alimuita mbwa wake aliyeonekana kusonga mbele kufuata barabara ,na hatimaye mbwa yule aliweza kusimama kisha kumfuata Nyoni kuelekea katika mti uliokuwa pembeni ya barabara.



    “Tulale hapa kwa umakini siunajua ni njiani, kesho asubuhi na mapema tuondoke ………”, ilikuwa ni sauti ya Matumaini, huku akishuka kutoka katika mgongo wa kaka yake. Alichukua jamvi ambalo alifungasha katika kiroba chake na kisha kutandika chini ya mti, tayali kwa ajili ya kujipumzisha .



    “Lala upumzike, bado tuna safari ndefu sana ……,mimi na Nyonta tuko makini kukulinda “,Nyoni aliongea huku akiwa amekamatilia upinde wake, huku mbwa wake aliyeitwa Nyonta akibugia viazi ambavyo vilikuwa vimechomwa. Viazi ambavyo walifungasha kama chakula kipindi chote watakapo kuwa safarini.



    …………………………………http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Mzimu Nkuru alishangaa sana baada ya kumpoteza tena Matumaini katika macho yake. Hakuwa na uwezo wa kumwona tena, kwani Matumaini aliweza kuuvaa mkufu wake kwa mala Nyingine tena. Jambo ambalo lilimfanya mzimu Nkuru azidi kuchanganyikiwa, ni kitendo cha kaka yake Matumaini, mtoto wa kwanza aliyeitwa Nyoni na yeye alitoweka katika macho ya mzimu Nkuru. Kitendo hicho kilimfanya mzimu Nkuru kuhisi kuwa, Nyoni na Matumaini wote kwa pamoja waliweza kuvaa mikufu ya kuwalinda shingoni. Mikufu ambayo ilimzuia mzimu Nkuru asiwaone na kuwadhuru, jambo ambalo lingewasaidia kutoroka kijijini kuelekea katika kijiji cha Ukarimu.. Huko wangeweza kupata dawa na kisha kurejea katika kijiji cha Mwantema kumuangamiza mzimu Nkuru, mzimu ambaye aliabudiwa na wananchi wa Mwantema huku akitaka wanakijiji wake kuwakeketa watoto wa kike. Kila mwanakijiji ambaye alikiuka mila hii ya mtemi Nkuru, ukoo wake uliweza kuuawa na maiti zake kuzikwa chini ya mti wa Ubuyu. Mti ambao ilisadikika mzimu Nkuru aliweza kuishi.



    Siku zote mzimu Nkuru akiwa na hasira, hasa pale watu walipopanga mipango ya kumuangamiza. Mti wa ubuyu, mti ambao aliweza kuishi, ulitikisika huku matawi yake yakianguka chini kwa fujo. Kitendo hicho kiliashiria mtemi kutakiwa na mzimu Nkuru kwa ajili ya kupatiwa maagizo, hivyo wananchi au askari wa mtemi waliposhuhudia mti ukitikisika na matawi kudondoka, walikwenda ikulu kwa mtemi Nyantumu kumpatia taarifa.



    Hayo yote ndiyo yaliyotokea, kwani mala baada ya Matumaini pamoja na Nyoni kutoroka kijijini usiku ule huku wakiwa hawaonekani machoni kwa mzimu Nkuru. Mti ulitikisika kwa fujo usiku kucha, lengo la mti huu kutikisika, ni mzimu Nkuru kutaka kuonana na mtemi Nyantumu ili ampatie maelekezo juu ya kuwafatilia Nyoni na Matumaini  ,kabla hawajafika kijiji cha Ukarimu.



    Usiku wa manane kijana hodari Nyoni, anaangaza kila kona kwa ajili ya kumlinda dada yake aliyekuwa amelala. Japo alikuwa amechoka sana kutokana na safari ndefu ya kutoroka kijijini Mwantema, lakini hakuona sababu ya kupiga usingizi karibu na pori hatari la Nyankonko.



    Kama alivyowaahidi wazazi wake kumlinda dada yake wa kike Matumaini, aliendelea kutimiza wajibu wake bila kukata tamaa.



    “Ninasikia hatua za kiumbe kikijongea kwa kunyata kuelekea mahali hapa, inatakiwa niwe makini ……”, Nyoni alikamatilia kwa makini upinde wake, huku akimtazama mbwa wake aliyeonekana kuwa na wasiwasi, hali iliyopelekea kuanza kuungurama na kubweka taratibu ……



    “Uuuuuuwhu wuuuh wuuuh…” mbwa wake Nyoni aliyejulikana kwa jina la Nyantu, alibweka kwa sauti kubwa zaidi ya mwanzoni. Kitendo hichi kilimfanya binti Matumaini aweze kushtuka usingizini kutokana na Nyantu kubweka kwa fujo ……



    “Kaka kuna nini?  …mbona Nyantu anabweka kiasi hiki? ……”,msichana mrembo Matumaini, msichana aliyetoroshwa kutoka katika kijiji cha Mwantema kukimbia mila hatari ya ukeketaji. Alimuuliza swali kaka yake baada ya kushtuka kutoka usingizini.



    “Kaa nyuma yetu, njoo haraka sana upande huu ……”,Nyoni alimjibu mdogo wake kipenzi na kumpatia maelekezo yaliyopaswa kufuatwa kwa sekunde tu, kwani simba mkubwa sana alikua tayali ameusogelea mti ambao Nyoni pamoja na dada yake walikuwa wameweka kambi na kujipumzisha.



    Kusema ukweli simba alikuwa mkubwa kupita kiasi, achana na simba ambao umeshawashuhudia kutoka katika mbuga ya Serengeti na Mikumi. Simba huyu alikua na mwili mkubwa mithili ya tembo, uso wake ulitisha sana huku manyoya mengi yakiifunika sura yake. Macho yake yalikuwa makubwa huku yakiwa mekundu, na isitoshe miguu yake ilikuwa mikubwa na imala, yenye uwezo wa kukanyaga kiumbe yoyote na kumdhamisha chini ya ardhi.



    “Mungu wangu!!  tumekwisha ……”, Matumaini baada ya kutii maagizo ya Nyoni, na kusimama nyuma yake pamoja na Nyantu. Mwili wake ulikufa ganzi na kuishiwa nguvu kabisa, alikiona kifo mbele yao kwani kiumbe alichokishuhudia hakikuwa cha kawaida, na isitoshe maisha yote alikulia ndani bila kutoka nje. Kwahiyo kila mnyama kwake alionekana kuwa wa ajabu, isipokuwa mbwa wao Nyantu aliyeishi nae nyumbani.



    “Usikate tamaa, baba alikupatia jina Matumaini kwakuwa ulipona kutoka katika hatari tangu ukiwa mtoto, usjali ……mnyama huyu hataweza kutudhuru!  mimi nitakulinda ……”, kwa ushujaa mkubwa kijana Nyoni alimuondoa hofu dada yake, huku akichukua mshale wake mgongoni tayali kwa ajili ya kupambana na simba yule wa ajabu, simba ambaye alionekana kutokea katika pori la Nyankonko ……



    …………………………………



    Mzee Mbutu pamoja na ndugu zake wanafika ikulu kwa mtemi Nyantumu, huku wakiongozwa na askari wa mtemi Nyantumu waliokuwa na hasira kali ,kwani siku zote waliishi na watuhumiwa bila kutambua.



    “Nyoni na binti aliyekuwa amefichwa wako wapi! bila binti huyu, mtakua mmefanya kazi bure, igweeeh askari wangu nipeni majibu sahihi ……”,Mtemi Nyantumu alifoka, kwani hakuweza kumuona muhusika mkuu miongoni mwa familia yote ya mzee Mbutu …



    “Nyoni na binti wa kufanyiwa mila, wametoroka!  Lakini askari wako watukufu wameelekea barabara kuu inayoelekea kijiji cha Ukarimu kuwafuatilia ,bila shaka wataleta jibu zuri kwako “,kiongozi wa kundi ambalo walitumwa na mtemi Nyantumu kwa mzee Mbutu, alimpatia maelezo mkuu wake kuhusiana na muhusika mkuu kushindwa kupatikana.



    “Peleka gerezani wapuuzi hawa, mmepona kifo kwa siku ya kesho mpaka Nyoni na huyo mjinga mwingine wapatikane, ” mtemi Nyantumu aliongea  kwa lugha ya ukali sana, lugha ambayo ilikera na kuwafurahisha ndugu wote wa mzee Mbutu …



    “Sawa mkuuu, igweeeh “,kiongozi yule wa askari wa mtemi Nyantumu alimjibu mkuu wake, huku ndugu wote wa mzee Mbutu wakilundikwa katika kijumba cha gereza kidogo sana, kijumba ambacho kilijaa kinyesi cha ng’ombe na kumkera mfungwa yoyote aliyefungwa ndani yake …



    …………………………………



    “Kaa makini, usikimbie!  moja mbili tatu ………”, Nyoni alimsihi dada yake aliyeonekana kuweweseka na kutaka kukimbia, bila kupoteza muda alianza kuhesabu huku akimlenga machoni kiumbe yule wa ajabu ……



    “Muuuuh …mu…uuu…uh “,Simba yule alipiga ukelele mkubwa sana, huku hasira zikimpanda na kuanza kumsogelea Nyoni na Matumaini ili awateketeze. Mshale mmoja ulizama na kudidimia katika jicho moja la simba yule. Kipindi simba yule akiendelea kutangatanga huku na kule, huku giza likimsumbua na kushindwa kumuona vizuri Nyoni na Matumaini ili kuwaangamiza.



    Kijana Nyoni kwaharaka sana alichukua mshale mwingine na kuupachika katika upinde wake, alivuta pumzi kwa kasi na kumlenga jicho la pili simba yule. Kutokana na uhodari wa kutumia upinde aliokuwa nao Nyoni mshale alioufyatua ulitua katika jicho ambalo alilikusudia na kupelekea kiumbe yule kuwa kipofu, kwani macho yote yalitobolewa huku mishale ikining’inia na damu kumutoka kwa wingi simba yule.



    “Puuuuuh ” kishindo kikubwa sana kilisikika, kwani Simba yule baada ya kutobolewa na Nyoni, hakuwa na uwezo wa kuona kitu chochote kile mbele yake. Hivyo basi alitumia kubahatisha uelekeo ambao Nyoni na Matumaini walikuwepo, na kupelekea mti mkubwa ambao walikuwa wamepumzika kusambaratishwa vipande vipande na Simba yule …



    “Nyantuu tukimbie, Matumaini nifuateni ……”, haraka sana walitoweka kutoka mahali pale na kumuacha simba yule akitapa tapa na kubahatisha maadui zake ili alipize kisasi, lakini alichelewa kwani Matumaini na Nyoni walikuwa wameshatoweka …



    ……………………………*



    Kwa muda mrefu sana kundi la askari takribani watatu waliendelea kufuata Njia ya kuelekea kijiji cha Ukarimu, lakini kinyume na matarajio yao, walitembea umbali mrefu sana bila kumuona Nyoni na Matumaini. Kwakuwa walikuwa bado hawajalifikia pori la Nyankonko, hawakua na sababu ya kukata tamaa kwani waliamini Nyoni na dada yake wasingeweza kulivuka pori hili hatari usiku wa manane …http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    “Mchanga huu unachosha kutembea  ,turudini basi!  Sina uhakika kama wanaweza kupita huku usiku huu, inawezekana bado wamejificha kijijini “,



    “Wuuuuh wuuuuuh wuuh ……”,



    “Mmmh hawa mbwa wetu wanabweka nini, mbona wananusa mchanga …”,



    “Ngoja tusogee tutazame, “



    “Igweeeh kuna giza, sioni wananusa nini! “,



    “Aaah, mawe haya hapa!  Ngoja tuyagongeshe na kuwasha moto majani haya machache, bila shaka tutaweza kugundua kitu ambacho kinapelekea mbwa hawa kunusa mchanga huu na kubweka ……”, yalikuwa ni majadiriano baina ya kundi la askari wa mtemi Nyantumu, majadiriano ambayo yalisitishwa na sauti za mbwa wao walioanza kubweka huku wakinusa lundo la mchanga mbele yao, mchanga uliokuwa katikati ya barabara.



    Hatimaye askari hawa waliamua kuwasha moto kwa kutumia vipande vya mawe vilivyozagaa barabarani. Wote kwa pamoja walistaajabu sana, huku furaha ikirudi upya na kuzipamba nyuso zao. Kwani walikuwa wameshakata tamaa ya kutambua sehemu ambayo Nyoni na mdogo wake waliweza kuelekea, kitendo ambacho kingepeleka kumukasirisha mtemi wao Nyantumu, na pengine kuuawa kabisa kama wasingefanikiwa kumrudishia majibu ya kuridhisha.



    “Jamaniii, wamepita hapa!  Simnaona miguu hii hapa, harafu inaonekana wameongozana na mbwa “,



    “Ndio! Mguu huu unatofautiana na huu hapa mbele, halafu inaonekana hawana muda mrefu wamepita hapa! “,



    “Sawa, tusipoteze muda!  turudi kwa mtemi tukamweleze jambo hili na kuongeza nguvu, hatuwezi kulivuka pori hili peke yetu, lazima tutakwisha. Mmewasahau Simba wa ajabu?  Vipi kuhusu chatu wanaomeza ng’ombe na ndugu zetu kijijini mmewasahau?  “



    “Hatuwezi kuwasahau wanyama hatari na wa ajabu kutoka katika pori la Nyankonko, twendeni kwa mtemi tukaongeze nguvu ……”,



    Hatimaye askari wa mtemi Nyantumu waliweza kuanza safari ya kurudi kijijini haraka sana, baada ya kugundua hatua za miguu walizopita Nyoni na Matumaini. Wanyama hatari wa pori la Nyankonko waliwafahamu vizuri sana, maumbo yao ya kutisha pamoja na sumu zao kali …



    Askari wa mtemi Nyantumu, wakiwa wameongozana na mbwa wao. Walifika ikulu kwa mtemi Nyantumu majira ya saa kumi na mbili asubuhi. Muda huo huo walipowasili, ndio wakati ambao mtemi Nyantumu alikuwa akijiandaa kwa ajili ya kuelekea kwa mzimu Nkuru kwa ajili ya kuzungumza naye na kuomba msaada.



    “igweeh mtemi wetu mpendwa ,habari za kuamka ……”, askari wa mtemi Nyantumu walimsalimia kiongozi wao mkuu wa kijiji cha Mwantema, mtemi Nyantumu aliyeonekana kuwa na mawazo mengi sana. Lakini baada ya kuwaona tabasamu kwa mbali lilionekana kwenye uso wake, kwani alifikili askari wake walifanikiwa kumnasa Nyoni pamoja na dada yake aliyeitwa Matumaini.



    “Igweeeh askari wangu, mmefanikiwa kuwanasa hawa wapuuzi wanaotuletea shida katika kijiji chetu??……mbona kimya! Nikiuliza swali nataka majibu, Nyoni na dada yake wako wapi, kama hamna majibu mazuri mtakufa kabla yao ……”, mtemi Nyantumu alizungumza na askari wake huku sauti yake ikibadilika na kuwa ya kufoka kadri ambavyo askari wake walichelewa kumjibu maswali yake.



    “Mtemi wetu mpendwa, tumejitahidi kadri ya uwezo wetu lakini tumeshindwa kuwakamata. Lakini tumefanikiwa kuona sehemu waliyopita na kuelekea kijiji cha Ukarimu, tumeamua kurudi na kuongeza nguvu kwani tusingeweza kuvuka pori la Nyankonko tukiwa wachache kiasi hiki na bila siraha za kutosha    ……”, vijana wa mtemi Nyantumu walijitetea kukikwepa kifo, kwani siku zote mtemi wao hakua na mchezo katika suala la kuchukua maamuzi magumu kwa yoyote yule anayeharibu kazi.



    “Sawa poteeeni hapa, chukueni askari wote na muelekee huko kabla hawajafika kijiji cha Ukarimu ……”,



    “,igweeeh mtukufu mtemi Nyantumu, tumekuelewa ……”, askari wa mtemi Nyantumu walimjibu mtemi wao na kisha kuanza harakati za kurudi kumsaka Nyoni na Matumaini kwa mala nyingine tena. Lakini kwa upande wa mtemi Nyantumu, alielekea kwa mzimu Nkuru mara baada ya maongezi huku akiongozana na baadhi ya askari wake waliokuwa wamembeba katika kiti chake cha utemi …



    …………………………………

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nyoni na Matumaini waliendelea na safari yao ya kuelekea kijiji cha Ukarimu, lakini waliamua kupita katikati ya msitu wa Nyankonko ili kuwachanganya askari wa mtemi Nyantumu watakapojaribu kuwafuata huku wakitumia nyayo zao za miguu …



    Lakini kitendo cha kupita katikati ya msitu, na kuachana na barabara kuu iliyokatiza katika msitu wa Nyankonko ,kuliyaweka maisha yao katika hatari ya kuliwa na wanyama wakali, wanyama wa ajabu wa msitu wa Nyankonko.



    “Kaka tunapita wapi, mbona tunaiacha barabara ……”,



    “Bila shaka askari wa mtemi wanatufuatilia,tukiendelea kupita barabarani watatukamata kirahisi. Harafu pia hii ndio njia ya mkato kufika kijiji cha Ukarimu, japo ni hatari sana zaidi ya unavyofikilia …”,



    “,Kaka mimi naogopa, kama ni hatari bora tupite barabarani. Kuuawa na binadamu ni bora kuliko wanyama wa pori hili …”,



    “,Usiogope mdogo wangu, mimi na Nyantu tupo kwa ajili ya kukulinda …”,



    “,Sawa kaka, nimekuelewa igweeh “,



    Yalikuwa ni mazungumzo kati ya Nyoni pamoja na mdogo wake, majira ya asubuhi siku ya ijumaa wakiwa katikati ya pori la Nyankonko wakitoroka kijiji cha wazazi wao, kijiji cha Mwantema na kuelekea kijiji cha Ukarimu.



    …………………………………



    Mtemi Nyantumu pamoja na askari wake wanne waliokuwa wamembeba katika kiti chake cha Utemi waliendelea kutembea kuelekea nje ya mji, mahali ambapo kulikuwa na mti mkubwa wa mzimu Nkuru. Kadri walivyozidi kuusogelea mti wa mzimu Nkuru, ndivyo walivyozidi kuongeza mwendo kuwahi kufika katika mti wa mzimu Nkuru, kwani walisikia sauti za ajabu kutoka katika mti ule. Sauti ambazo ziliashiria mzimu Nkuru kuwa na jambo ambalo alitaka kumfamisha mtemi Nyantumu …



    “Tembea haraka, wahiii ……bila shaka mti wa mzimu Nkuru unatikisika na kupukutisha majani.. Nina imani kuna jambo la hatari anataka kunifahamisha, simnasikia kelele hizo “, mtemi Nyantumu aliwahimiza vijana wake kukaza mwendo kuukalibia mti wa mzimu Nkuru, mzimu ulioabudiwa na kuheshimiwa na wanakijiji wa Mwantema.



    “Sawa mtemi, baada ya dakika kadhaa tutafika kwa mzimu Nkuru ……”, vijana shupavu wenye miili mikubwa walimtoa hofu mtemi wao, na kuendelea kuchapa laba kuusogelea mti wa mzimu Nkuru.



    …………………………………



    Kundi kubwa sana, lenye askari wenye siraha nzito za kijadi walianza safari haraka sana ya kuelekea pori la Nyankonko kumsaka Nyoni pamoja na mdogo wake, muhusika mkuu aliyesababisha Mwantema kupata maafa ya ukame kwani hakufanyiwa mila hatari ya ukeketaji baada ya kufichwa na wazazi wake tangu kuzaliwa mpaka umri wa miaka ya kufanyiwa mila kupitiliza. Hali iliyopelekea mzimu Nkuru kukasirika na kutaka kuusambaratisha ukoo wote wa mzee Mbutu, huku kijiji cha Mwantema kikikumbwa na Ukame pamoja na vifo vya kutatanisha…



    “Nyoni anajifanya hodari, tukimkamata atakiona cha mtema kuni …,hawezi kutupeleka sehemu hatari sana kama Nyankonko kirahisi namna hii …”,



    “Bora yenu nyie hamkuja safari ya kwanza,tuliteseka usiku kucha kumfuatilia na kuambulia nyayo za miguu tu ……”,



    “Yani  hakuna siku niliyokuwa na hasira kama jana, ilibakia kidogo mtemi atutoe roho kisa upuuzi wa vijana wadogo kama Nyoni pamoja na huyo dada yake ambaye hakuna mtu yeyote aliyewahi kumtia machoni …”,



    “,Jamani tuacheni mazungumzo, tusonge mbele haraka sana tuwahi kufika porini kabla giza halijaingia, tukichelewa basi maisha yetu yatakuwa hatarini kwani usiku ni kazi kupambana na wanyama hawa hatari “, yalikuwa ni mazungumzo kati ya askari wa mtemi Nyantumu, askari ambao walikuwa na uchu wa kumkamata Nyoni kisha kulipiza kisasi kwa yale yote aliyowafanyia, yeye pamoja na ukoo wote wa mzee Mbutu ……



    …………………………………



    “Eweeeh mzimu wangu kipenzi Nkuru, nimeitika wito wako!  Nieleze jambo ambalo unataka kuniambia “, mtemi Nyatumu alitoa kafara ya mbuzi na kunyunyizia damu katika mizizi ya mti mkubwa wa Ubuyu, mti ambao mzimu Nkuru aliweza kuishi. Haya yote yaliendelea mala baada ya kuukuta mti wa mzimu Nkuru ukitikisika kwa fujo na kupiga kelele za ajabu, kelele zilizoandamana na mti kupukutisha majani …



    “Nyoni na mdogo wake siwezi kuwadhuru kwani wamevaa mikufu yenye nguvu kubwa ya kuwalinda, na muda huu wako katikati ya pori la Nyankonko wanaelekea kijiji cha Ukarimu, lakini sina uwezo wa kuwaona kwa macho na kuwadhuru. Haraka sana fuata askari wako waliotangulia msituni Nyankonko nenda kamkamate Nyoni na mdogo wake kabla hawajafika kijiji cha Ukarimu ……”, hatimaye baada ya mizizi ya mti ule wa ubuyu kunyunyiziwa damu ya mbuzi aliyechinjwa na kutolewa kafara, ndipo mti ule ulianza kuongea na kutoa amli kwa mtemi Nyantumu. Sauti ya mzimu Nkuru iliyokuwa na hasira ambazo ziliandamana na mwangwi uliosikika kila kona ya kijiji cha Mwantema.



    …………………………………



    “Bweeeeh bwe…ee…eh “, hatimaye kilio cha mbwa wa Nyoni aliyeitwa Nyantuu kilisikika, kilio ambacho kilipungua kadri ambavyo roho ya Nyantu ilikuwa ikiuaga mwili.Nyoni  na Matumaini hawakuwa na msaada wowote, waliendelea kushuhudia jinsi ambavyo Nyantu alitafunwa na kumezwa kiulaini, mithili ya paka anapomnasa panya kisha kuanza kumtafuna.



    Kwakuwa Nyantu ndiye alikuwa anaongoza njia na kutangulia mbele, ilibidi wasimame ghafla baada ya kusikia kilio chake huku damu zikiwalukia.



    Walishindwa kusonga mbele au kurudi nyuma. Bali walibaki wamesimama huku wakiwa wamepigwa na butwaa. baada ya kushuhudia joka kubwa sana ambalo lilimmeza mbwa wao Nyantu, wakiwa hawatambui mahali lilipokuwa limetokea ghafla kiasi kile.



    Joka lile kubwa lilianza kujiburuta kuwasogelea Nyoni pamoja na Matumaini, huku Matumaini akiwa amesimama tu na kulishangaa kwani hakuwahi kumuona kiumbe wa ajabu kiasi kile tangu azaliwe. Kwa upande wa Nyoni alikua na hasira sana, hasira iliyopelekea mishipa ya damu kuvimba na kujionyesha katika paji lake la uso. Hakuamini kama rafiki yake kipenzi, rafiki yake waliye ongozana naye kila mahali ndiye aliyeuawa na kumezwa na nyoka yule.



    Safari ya Nyoni pamoja na dada yake Matumaini kutoroka kijiji cha Mwantema, inakumbwa na vikwazo vya kutisha mala baada ya kuufikia msitu hatari wa Nyankonko.Kijana hodari na shupavu Nyoni Mbutu hakukata tamaa ,alizidi kusonga mbele kumlinda dada yake mpaka hatua ya mwisho akiwa mshindi. Aliamini lazima ashinde kwa hali yoyote ile, na kuikomboa Mwamutema dhidi ya mila hatarishi ya ukeketaji …

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Moyo wake ukiwa na maumivu makali sana, maumivu ambayo yasingepona leo wala kesho. Aliushika upinde wake kwa makini huku hasira zikimpanda kichwani mpaka machozi kumtiririka, Nyoni aliwaza kulipiza kisasi kwa nyoka yule mkubwa aliyemtafuna Nyantu bila huruma.



    Kwa upande wa joka lile kubwa ambalo lilimmeza mbwa wake Nyoni aliyeitwa Nyantu, liliendelea kujivuta taratibu kumsogelea Nyoni pamoja na Matumaini huku likiendelea kumtafuna Nyantu polepole pasipo na haraka yoyote.



    Nyoni aliona kumuua joka yule kwa upinde atakua amempendelea, alistahili kufa kifo cha kikatili kama ambavyo alivyomtafuna bila huruma Nyantu. Kichwa chake kiliamua kufanya maamuzi ya haraka sana,alichukua panga lake aina ya jambia, panga ambalo alilitumia baba yake katika shughuli za shambani. Baba yake alimkabidhi kama moja ya siraha kumlinda dada yake, siku zote wakiwa safarini kuelekea kijiji cha Ukarimu …



    “Kaka mbona sikuelewi, huyo mnyama anatufuata kutuua, mimia naogopa!! ” ,



    “Usiogope, nitakulinda mpaka hatua ya mwisho …,shika upinde huu, ngoja nimkate kate na panga kama alivyo mtafuna Nyantu bila huruma …”,



    “Kaka atakuua, tumia upinde kwani sio lazima umsogelee kupambana naye ……”,





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog