Search This Blog

NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA - 3

 

    Simulizi : Niliolewa Na Jini Bila Ya Kutarajia

    Sehemu Ya Tatu (3)





    Kabla sijamalizia, nikaona sura ya Carlos ikibadilika na kuwa sura ya yule kijana wa ndotoni. Nikaanza kuogopa na kupiga makelele hadi mama na Dada Penina wakatoka nje kuja kushuhudia kuwa kuna nini. Mama akauliza kwa mshangao, "Kuna nini hapa?" Nikiwa nimejiziba uso kwa kiganja changu nikamsikia Carlos akimjibu mama. "Hata Mimi mwenyewe namshangaa Sabrina, sijui ana matatizo gani maana gafla tu kaanza kupiga makelele" Mama akasogea karibu ili anitoe mikono machoni na aweze kuona Kuwa nina tatizo gani. Sikutaka kuangalia tena, nikaamua kukimbilia ndani kwa uoga niliokuwa nao. Nikawaacha mama na dada wakiongea na Carlos pale nje. Nilipokimbilia ndani nikaishia sebleni kwani chumbani nako niliogopa kwenda, baada ya muda kidogo mama, dada Penina na Carlos nao wakaja pale sebleni kitendo kilichofanya uoga unishike zaidi na kusema kwa nguvu, "Jamani, huyo Carlos sio mtu" Mama akaniuliza, "Sasa kama sio mtu ni nani?" "Sijui ila sio mtu" "Umeshaanza maruweruwe yako mwanangu" Kisha mama akamgeukia Carlos na kumwambia, "Msamehe mwanangu, anamatatizo sana tumehangaika nae bila jibu. Ndio anakuwaga hivyohivyo maruweruwe yakimuanza. Msamehe sana" "Usijali mama, hata mimi naelewa kama Sabrina ana matatizo ila kila nikimuuliza anakataa. Ila mimi naweza kumsaidia na hayo matatizo yakamuondoka kabisa" Nikaropoka hapohapo, "Unisaidie nini wewe wakati wewe ndio tatizo" Kisha nikakimbilia chumbani kwangu kwani uoga ulishanitoka kwa kutambua kwamba dawa ya tatizo ujue kwanza chanzo cha tatizo, nikawaacha pale sebleni wakiendelea kuongea. Moja kwa moja nikaenda kukaa kitandani kwangu, mara gafla nikasikia sauti ikipenya masikioni mwangu huku ikiita kama kwa kunong'oneza, "Sabrina, Sabrina, Sabrina" Ile sauti ilikuwa kama ikigongwa gongwa na mwangwi na kujirudia rudia, nikaanza kuogopa tena na kupiga makelele nadhani hata watu wa mbali waliweza kusikia ila hawakuelewa kuwa kuna nini. Mama, dada Penina na Carlos wakaja chumbani kwangu ila sikutaka kumuona Carlos wala kuongea nae ikabidi aage na kusema. "Kama mtahitaji msaada wangu msisite kunipigia simu. Nitakuja kuwasaidia" Kisha akaondoka, halafu tukatoka sebleni ili tuweze kuongea vizuri. "Kwani una matatizo gani mwanangu?" "Sijui na hata sielewi" "Elezea kidogo ili tupate kukusaidia" "Hata sijui jinsi ya kuelezea mama" "Jaribu mwanangu" Nikataka kuwaelezea tangu mauzauza yalipoanza hadi hapa yalipofikia, ila mdomo ukawa mzito gafla, sikuweza kutamka neno lolote lile, mama akabaki kushangaa. Ikabidi dada aulize, "Mbona kimya cha gafla?" Nikawa nataoa machozi tu, mama akaona nitazidiwa akaamua kunipa dawa ya usingizi ili nipunguze maruweruwe, na muda huo huo nikalala kweli. Nilipoamka nilijikuta nipo chumbani kwangu, nadhani mama alinipeleka chumbani muda nilipoanza kulala. Ilikuwa ni usiku, nikachukua simu yangu kuangalia muda nikaona ni saa saba usiku. Nikajiuliza kama nimekula usiku wa leo na kupata jibu kuwa sijala. Mara nikasikia sauti ikiniambia. "Usijali Sabrina, chakula nimekuwekea mezani hapo" Nikashtuka sana na kujiuliza ni mawazo au ni kitu gani, ila nilipoangalia mezani nikaona kuna sahani na juu imefunikwa, nikaogopa. Nikatoka chumbani kwangu na kukimbilia chumbani kwa mama ambaye alikuwa amelala, nikamtingisha ili kumwamsha na kumuuliza. "Eti mama umeniwekea chakula mezani kwangu chumbani?" "Ndio, nilijua ukiamka lazima utakuwa na njaa ndiomana nikakuwekea" Nikapumua kidogo na kuona kuwa ile mwanzo yalikuwa mawazo yananisumbua tu. Mama akaniambia tena, "Nenda ukale tu mwanangu, usiogope" Nikatoka chumbani kwa mama na kurudi chumbani kwangu. Nikasogea pale mezani kuona mama ameniwekea chakula gani, nikafunua sahani ya juu na kukuta ni chips kuku, nikashangaa na kujiuliza. Inamaana leo kwetu wamepika chips kuku au mama ameamua kuninunulia tu, nikajisemea kuwa nitamuuliza kesho na kuanza kula. Nilipomaliza kula, nikaenda jikoni kuchukua maji ya kunywa. Kisha nikarudi chumbani kwangu na glasi ya maji mkononi, nikashangaa kuona soda mezani na kujiuliza nani kaiweka, sauti ikaja. "Nimeweka mimi Sabrina" Nikaanza kuogopa na kutaka kukimbia, sauti ile ikasema tena "Unaogopa nini sasa mbona chips zangu na kuku umekula!" Nikahisi kuchanganyikiwa kwakweli na kutaka kupiga makelele ila ikashindikana, nikahisi kama kuna kitu kinanigusa na kujikuta nimeanguka chini na kupoteza fahamu. Nilipozinduka ilikuwa kumekucha na nilijikuta kitandani, hapo nikaogopa pia na kukimbilia sebleni ambako nilikutana na mama. "Nani kaniweka kitandani?" "Khee, kwahiyo wewe uliona raha kabisa kulala pale chini!" Nikamuangalia mama na kumuuliza tena, "Chakula ulichoniwekea jana ni chips kuku?" "Chips kuku? Kwa lipi haswaa? Nilikuwekea wali, maharage na mchicha kwani hujala?" Majibu ya mama nayo aliyajua mwenyewe, hapo nikajifikiria na kuona kuwa zile chips kuku niliwekewa na lile jitu lililokuwa linaongea usiku, nikatamani hata kujitapisha lakini ilishindikana. Nikiwa nashangaa shangaa pale sebleni, mama akaenda chumbani kwangu na kutoka na sahani na chupa ya soda. Kisha akasema, "Ona sasa, chakula nilichokuwekea hujala hata kidogo. Bora hata usiku ule wakati unaniuliza ungekiweka kweje friji, kitakuwa kimechacha tayari" Huku akikinusa kile chakula, nikawa naangalia kama mtu nisiyeelewa na kujiuliza kuwa mbona usiku sikukiona zaidi ya zile chips kuku! Nikamuuliza mama, "Na hiyo chupa je?" "Unauliza nini wakati unaona ni chupa ya soda! Au unaona kingine mwenzetu?" Nikatulia na kujiona kweli nina matatizo na ninahitaji msaada wa hali ya juu saa, nikakaa kwenye kochi pale sebleni huku nikitafakari mambo yanavyokwenda katika maisha yangu kwani nilikuwa sielewi hata moja nipo kama sipo. Mchana nilitulia ndani nikiangalia video. Nikapata ujumbe toka kwenye namba mpya ukisema. "Una tabia mbaya sana wewe, sikutegemea kama Sabrina utakuja kuwa na tabia kama hii" Nikajiuliza ni tabia gani? Na nani kanitumia ule ujumbe? Nikajaribu kuipiga ile namba, naambiwa. "Namba ya simu unayopiga haipo" Basi nikazidi kuchukia kuwa kwanini iwe hivyo na wakati amenitumia ujumbe jamani! Mama akaja kukaa sebleni ili kuzungumza nami. "Mwanangu una matatizo" "Ndio nina matatizo mama" "Unaonaje kama tukimuomba Carlos atusaidie maana kasema kuwa anaweza kutusaidia" "Mama, sitaki msaada wa Carlos sio mtu yule" "Kwanini sio mtu?" "Mtu gani, hana ndugu na wala hajulikani anapokaa! Mimi simtaki kwakweli, sitaki kabisa anisaidie" sana hadi tukamshangaa pale nyumbani. Mama akamuuliza, "Mbona mapema leo Penina?" "Mmh! Nitakusimulia tu mama" Akaja kwangu na kunikabidhi bahasha. "Mzigo wako huo, kuna mtu kanipatia" Kisha akaondoka zake, nikajiuliza ni nini na kufungua ile bahasha. Nikakuta kadi yenye rangi nyekundu ndani yake imeandikwa, "NAKUPENDA" Ndani yake kulikuwa na pete ya dhahabu yenye jiwe linalong'aa sana katikati nikahisi itakuwa ni almasi. Nikajiuliza kuwa inatoka wapi maana ni vitu vya ajabu. Nikabeba ile bahasha na kwenda nayo chumbani kwa dada kumuuliza kuwa kaitoa wapi. "Dada, mbona sielewi hii bahasha! Umeitoa wapi?" "Kwani haijaandikwa ilipotoka?" "Haijaandikwa ndio, ila vilivyomo ndani yake sielewi" "Ina nini kwani?" "Kuna kadi nyekundu na pete" "Acha masikhara Sabrina, hebu ilete tuone" Nikampa dada, akaifungua. "Kadi na pete viko wapi sasa? Mbona kuna barua tu! Unajua nilipoitoa hii bahasha Sabrina?" "Sijui" "Nimepewa na Suzy, hebu angalia hapa ameandika sijui mkutane wapi" Nikashangaa na kuichukua tena, kuangalia ni kweli ilikuwa barua. Sikutaka hata kuisoma kwani nilipatwa na mashaka tayari. Nikaichana na kwenda kuitupa nje, kisha nikarudi sebleni huku nikijiuliza kuwa haya ni mambo gani. Dada akaniuliza Kuwa mbona nimeichana nikamjibu kuwa siiamini. Muda mfupi kidogo nikapigiwa simu na Suzy. "Bora nimekupata, maana kila nikikupigia haupatikani ndiomana nikaandika ujumbe na kumpa dada yako ila kaniambia umeuchana kwanini? Au ujumbe wangu hauna maana?" "Samahani Suzy, labda ungeniambia tu sasa hivi" Simu yake ikakatika, nikajaribu kumpigia lakini haikupatikana basi ikabidi niachane nayo. Usiku ulipofika nilijikuta nikikosa hamu ya kula, sikutamani chakula chochote kabisa hata mama na dada walipokuwa wanakula sikujumuika nao. "Naona umeshiba mwenzetu" "Hapana mama, ila sijisikii kula tu" "Kwanini wakati hata mchana hujala?" Dada akadakia, "Siku hizi mwanao anafanya diet, asubuhi nimeingia chumbani kwake nimekuta soda mezani akasema yeye hataki basi mimi nikainywa" "Kumbe ndio ile chupa niliyoitoa asubuhi!" Mama akanigeukia na kuniuliza, "Kwani ulinunua muda gani soda?" Dada akajibu, "Aliletewa na Carlos halafu mimi nikampelekea chumbani kwake" "Unapendwa na Carlos mwanangu, tatizo lako hupendeki" Nilikuwa kimya kabisa nikiendelea kutafakari maneno yao, kuwa snda alileta Carlos na usiku ule nikasikia sauti ya ajabu. Huenda kweli Carlos akawa ndio lile jitu la ndotoni. Niliinuka pale sebleni na kwenda chumbani ili nijaribu kulala maana ndio kazi niliyofanya, kula, kulala na kuzunguka ndani ukizingatia bado naogopa kwenda nje kuzurula. Nikiwa chumbani nikapata ujumbe kwenye simu kutoka kwa Carlos. "Unanionea tu Sabrina, mimi sio mtu mbaya na nina nia nzuri na wewe. Nipe nafasi nikusaidie na mambo yako yote yataenda sawa. Ukiwa karibu na mimi hakika utafurahia maisha. Usinitenge Sabrina, nipo tayari kukusaidia kwa kila hali. Ukiwa na tatizo lolote usisite kuniambia" Nikaweka simu pembeni kwani ujumbe wake haukuwa na maana yoyote kwangu. Nikatulia na kuangalia mezani nikaona ile kadi nyekundu na pete juu yake, nikashindwa kuelewa maana hata ile barua niliichana muda ule ule sasa ile kadi imetoka wapi tena, nikaogopa kusogelea na kutoka nje. Nilipofika sebleni nikamvuta dada mkono ili nae aone nilichokiona. Nikafika nae chumbani ila ile kadi haikuwepo. "Mbona hakuna kitu Sabrina?" Nikatoa mimacho tu, "Unajua wewe Sabrina una matatizo sana, kwanza kilichokuleta kulala mapema yote hii ni nini? Twende sebleni tukaangalie video" Nikatoka na dada kwenda kuangalia video ila sikuelewa chochote hadi muda ambao dada alichoka na kwenda kulala ndipo na mimi nikainuka na kwenda tena chumbani kwa lengo la kuchukua simu yangu kisha niende kulala kwa mama kwani nilishapata uoga wa kulala chumbani kwangu. Nikiwa chumbani, nikachukua simu ili nitoke. Nikasikia sauti ikisema, "Huwezi kunikimbia Sabrina" Uoga ukanijaa na kusogelea mlango, kabla sijaufungua ule mlango ukafunguliwa halafu akaingia yule kijana wa ndotoni.



    Kabla sijaufungua ule mlango ukafunguliwa halafu akaingia yule kijana wa ndotoni.

    Nikawa natetemeka pale karibu na mlango huku nimejiziba sura yangu kwa mkono, nikahisi yule mtu akinishika mkono wangu ili autoe mara nikasikia sauti ya mama karibu yangu.

    "Wee Sabrina una nini?"

    Nikatoa mkono wangu na kumuona mama mbele yangu, nikakimbilia sebleni halafu mama akanisogelea.

    "Una nini wewe mtoto?"

    Sikutaka kumtazama mama usoni na kumwambia.

    "Wewe sio mama, sitaki"

    "Sasa mimi kama sio mama ni nani sasa?"

    Dada Penina nae akaja kutuangalia,

    "Kuna nini hapa?"

    "Namshangaa mdogo wako eti anasema mimi sio mama"

    "Mama, huyu Sabrina ana mapepo si unaona jana kasema kuwa Carlos sio mtu! Halafu leo kachana barua aliyopewa na rafiki yake, ukimuuliza anasema sio barua. Itabidi asaidiwe huyu mama"

    Mama akamwambia dada,
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Hebu mpigie Carlos simu aje atusaidie kwa hili maana hata sielewi"

    Nilijiziba tu macho huku nikiogopa na machozi kunitoka.

    Dada akamwambia mama nadhani baada ya kumpigia Carlos simu.

    "Carlos kasema tumpe dawa ya usingizi alale halafu kesho atakuja na ufumbuzi wa hili tatizo"

    Mama akachukua dawa na kunipa, nilikunywa vilevile nimejiziba sura kwa mkono.

    Mama akanishika mkono hadi chumbani kwake na huko ndio nikaenda kulala hadi kunakucha.



    Nilichelewa sana kuamka, nikatoka hadi sebleni kuangalia mida kwenye saa ya ukutani.

    Ilikuwa ni saa nne asubuhi, na macho yangu yalikuwa mazito yani yalihitaji kuendelea kulala.

    Nikaenda jikoni na kumkuta mama yupo makini na mapishi yake.

    "Kheee umeamka mziwanda wangu! Njoo, mwanangu. Njoo uonje ninachopika"

    Nikamshangaa sana mama kuchangamka kiasi kile, ila nikamwambia asubiri kwanza nikaoge na kuondoa uchovu wa usingizi ndio niende kuonja.

    Nikiwa bafuni, nikaguswa mgongoni kugeuka nyuma hakuna kitu.

    Nikaendelea kuoga huku nikiimbaimba ili kukatisha mawazo ya uoga, mara nikaona kitu cheusi kikiingia chini ya mlango wa choo.

    Kuangalia vizuri ni nyoka, nikaanza kupiga makelele.

    "Nyokaaa, nyokaaa. Nakufa jamani nakufa"

    Yule nyoka akawa anatoa toa ulimi wake nje, hapo ndio uoga ukanizidi na kutoka bafuni siwezi maana yupo mlangoni.

    Alifika mama na Carlos, kisha Carlos akampiga yule nyoka na kumuua nami nikakimbilia ndani huku nikitetemeka kwa uoga.

    Carlos akaanza kunicheka.

    "Kweli Sabrina muoga jamani, yani umetoka na mapovu duh!"

    "Na wewe umefika saa ngapi?"

    Mama akadakia,

    "Si ushukuru amefika, mwenye ujasiri wa kuua huyo nyoka humu ndani nani? Mbona ingekuwa balaa, ila huyo nyoka katokea wapi jamani wakati hakuna hata nyasi kwenye uzio wangu?"

    Mama alijiuliza swali sawa na nilivyojiuliza mimi kuwa huyo nyoka katokea wapi.

    "Nenda kamalizie kuoga choo cha ndani mwanangu"

    Nikaenda kuoga choo cha ndani ila bado fikra za nyoka zilitembea kichwani mwangu na kunifanya niwe na wasiwasi muda wote.

    Nikajimwagia haraka haraka na kutoka kwenda kuvaa, kisha nikaenda sebleni kukaa ambako kulikuwa na mama na Carlos ukizingatia siwezi kupakimbia kwetu, nitaenda wapi? Bora nivumilie tu.

    "Tulimuomba Carlos aje atusaidie mwanangu kwa tatizo lako, kwahiyo usichukie"

    Nilitulia kimya kabisa nikiwasikiliza, kisha Carlos akaanza kuongea,

    "Unajua mama, huyu Sabrina ananishutumu kuwa mimi sio mtu wa kawaida kwa sababu kuu mbili"

    "Zipi hizo?"

    "Moja, najua siri nyingi sana za watu wake wa karibu na pili sababu hawajui ndugu zangu. Ila mimi nakuahidi mama, nitawaleta baba na mama yangu hapa muwafahamu na mahali wanapoishi mtapafahamu pia. Huwa sipendi mtu anifikirie sivyo"

    Mama nae akasema,

    "Mimi nakuelewa baba yangu, ila ningependa kufahamu hizo siri unazofahamu za watu wa karibu na Sabrina"

    "Kwanza kabisa najua kuhusu rafiki yake Suzy, na pia kuhusu wifi yake Joy. Yule Joy yule....."

    Nikamkatisha na kumkonyeza, huku mama akiwa makini kusikiliza.

    Nikaamua kusema neno la kubadilisha mada.

    "Nipo tayari kusaidiwa na wewe Carlos"

    "Kweli Sabrina! Upo tayari? Basi vizuri sana"

    "Nipo tayari ndio"

    Mama akafurahi sana kusikia nipo tayari. Sikupenda siri ya wifi ivuje kwani nilimuonea huruma sana ndiomana nikaamua kubadili mada.



    Nikaingiza mada zingine za namna ya kunisaidia, mara dada Penina akawa amerudi na leo ndio aliwahi kurudi zaidi kushinda jana. Mama akamuuliza,

    "Mbona mapema sana?"

    "Majanga mama"

    "Yapi hayo?"

    "Kuna mauzauza ofisini kwetu siku hizi, tunakimbia ofisi sijui nini tatizo" Carlos akadakia,

    "Mimi najua tatizo"

    "Ni nini sasa?"

    "Pale ofisini kwenu kuna mtu anaomba sana, huyo ndio tatizo"

    Mama akamuuliza dada,

    "Unamjua huyo?"

    "Ndio, ni Salome mwenye tabia hiyo hadi ofisini"

    Kisha wakamuuliza tena Carlos,

    "Kwani kuomba sana ni tatizo?"

    "Kuomba sana si tatizo ila yule binti ni mchawi sana na ndio anawatesa, pale ofisini jaribu kufatilia mambo yake" "Mmh tutafanyaje sasa?"

    "Labda afukuzwe kazi"

    Mama akamuuliza tena dada Penina,

    "Huyo Salome si ndio yule wa mama Salome aliyepata ajali?"

    "Ndio huyo huyo mama, nipo nae ofisi moja ni mtu wa dini sana hadi anakera" "Ila mbona haelekei na hayo mambo ya uchawi?"

    Dada Penina akajibu,

    "Mchawi huwezi kumjua kwa macho mama"

    Kisha Carlos akaendelea kusema.

    "Ni kweli, mchawi hauwezi kumjua kwa macho. Kama yule rafiki yako yule naye ni mchawi" Dada Penina akauliza,

    "Yupi huyo?"

    "Yule wa kuitwa Zuhura"

    "Mmmh! Mbona ni mtu wa ibada sana huyo!"

    "Hao watu wanaojifanya wa ibada waogope sana hawafai kwani wengi wao hutumia ibada kuficha makucha yao ila mimi nawaona" Nikamuuliza,

    "Wewe unawamaje sasa au mmoja wao?"

    "Hapana ila mimi nilichanjiwa na babu yangu nikiwa mdogo sana ndiomana naona na kugundua vitu vingi" Mama na dada waliamini kila alichoongea Carlos ila mimi imani yangu ilikuwa nusu nusu juu yake. Akaongea na kusema kuwa kesho anakuja na ufumbuzi wa swala langu, kisha akaaga na kuondoka zake.



    Muda kidogo tukasikia mtu anagonga mlango, nikamchungulia kuwa ni nani. Dada akaniuliza,

    "Ni nani kwani?"

    "Rafiki yako da' Zuhura"

    "Kafata nini na yeye na uwanga wake"

    Mama akatufata kuwa tukamfungulie mtu, nikainuka na kwenda kumfungulia kisha nikamkaribisha ndani.

    Dada akamsalimia kiunafki tu kuonyesha kuwa hapendezewi naye, mama akaja nae kumsalimia ili tumuone na uchawi wake leo maana hakuna hata mmoja aliyejua leo kafata nini ukizingatia ni kipindi kirefu sana hajafika kwetu.

    "Najua leo mnanishangaa sana na kuona ajabu mimi kuwa hapa"

    Dada akadakia,

    "Lazima tukushangae maana huna kawaida ya kuja kwetu, zaidi ya mimi kuja kwenu"

    "Rafiki yangu Penina, sio kwamba mimi sipendi kuja hapa. Mbona zamani nilikuwa nakuja hujiulizi hilo?"

    "Haya, niambie sasa kwanini huwa hufiki hapa? Na leo umekuja kwanini?"

    "Kwanza kabisa nimekuja kuwasalimia"

    Wote tukaguna

    "mmmh!!"

    "Halafu kuna jambo kubwa sana lililonileta hapa"

    "Jambo gani?"

    "Ni kuhusu Sabrina, nimekuwa nikimuotea ndoto mbaya sana"

    Mama aliyekuwa kimya kabisa tangu da' Zuhura anaongea akamkatisha sasa.

    "Wewe Zuhura wewe usituletee uchawi wako hapa, tafadhari ondoka nyumbani kwangu na hizo ndoto mbaya nenda ukawaotee ndugu zako mwanga mkubwa wewe"

    "Samahani mama kama nimekosea"

    "Hakuna cha samahani hapa, nenda kawaombe msamaha wanga wenzio. Ondoka kwangu sasa hivi usiniletee mapepo na uchawi wako hapa"

    Dada Zuhura akainuka na kuanza kuondoka huku akisema,

    "Ila mimi nilitaka kuwasaidia tu, Mwenyezi Mungu awarehemu"

    "Akurehemu wewe na uchawi wako, mwanga mkubwa wewe"

    Alipoondoka, mama akaanza kumtania dada.

    "Humsindikizi shoga yako?"

    "Nani amsindikize mwanga? Loh! Ndoto mbaya, ndoto mbaya anajua maana ya ndoto mbaya au shobo tu. Na leo umemuweza kweli mama"

    "Aende zake huko, siku zote hafiki hapa kaona tumemgundua ndio anakuja kujineng'enesha. Mwendawazimu kweli yule mtoto"

    "Umenifurahisha sana mama yangu leo, bado hiko kisalome nacho kitajileta tu"

    Mama na dada wakacheka sana ila mimi nilikuwa kimya kabisa nikitafakari mambo yangu kichwani maana yananichanganya sana.



    Usiku ulipofika, dada aliandaa chakula ili tuweze kula.

    Tulikaa na kula kile chakula, kilikuwa ni kitamu sana kupita kawaida.

    Wakati tunakula, tukasikia sauti ya kitu kama kimeanguka chini kwa nje kwetu.

    Kila mmoja akashtuka na kuambizana kwenda nje kuangalia nini ila ujasiri uliondoka sababu ya uoga na mimi ndio niliongoza kwa kukosa ujasiri, ikabidi mama ajitoe muhanga kwenda kuangalia ni nini ila hakuona chochote na kurudi ndani.

    "Hakuna chochote"

    "Mmh mama wakati wote tumesikia!"

    "Ndio, ila hakuna kitu tuendeleeni kula tu"

    Tukakaa ili tule, tukasikia kishindo tena na kushtuka.

    "Mmh mama kuna kitu huko nje sio bure"

    "Labda kweli kuna kitu, itabidi wote twendeni tukaangalie"

    Mimi nikagoma kwenda na kumuacha mama na dada kwenda peke yao kuangalia.

    Nikiwa pale ndani, nikasikia muungurumo kama vile wa simba, hapo ndipo uoga ukanizidi na kuinuka huku nikijaribu kutoka nje ila mama na dada wakarudi muda huo huo ndani na kusema kuwa nje hakuna chochote.

    "Ila mimi nimesikia muungurumo kama wa simba humu ndani"

    "Acha miujiza sasa, huyo simba atafute nini humu ndani kwetu Sabrina?"

    Dada penina akakumbuka kitu na kuuliza,

    "Au wale wachawi aliosema Carlos ndio wameanza kazi yao?"

    "Hebu mpigie simu atusaidie"

    Dada akampigia simu Carlos aliyesema anakuja, na baada ya dakika kadhaa alikuwa nyumbani kwetu.

    Kisha akaanza kusema nasi,

    "Leo alikuja mdada kajitanda ushungi eeh"

    Dada akajibu,

    "Ndio, ni Zuhura huyo"

    "Basi ndio anawatupia makombora yake ila mimi nitawasaidia"

    Mama akamuuliza,

    "Kwani wewe ni mganga?"

    "Hapana, mimi si mganga na wala siwaamini waganga hawafai ila mimi ninauwezo niliopewa na Mungu"

    "Ila ulisema umechanjiwa"

    "Ndio nimechanjiwa ili watu wabaya wasinipate"

    Tukamuangalia tu Carlos, ambaye alichukua maji nakujifanya kama anayaombea kisha akayamwagia nyumba yetu yote.

    Mama akamshukuru sana, kisha akatuaga na kusema kuwa atakuja tena kesho.

    Ikabidi dada Penina amsindikize Carlos kidogo kwani mimi na mama tulibaki ndani.

    Dada alilazimisha kumsindikiza Carlos nje ingawa Carlos alikataa ila dada akatoka nae.

    Mara gafla tukasikia dada akipiga kelele huko nje.





    Mara gafla tukasikia dada akipiga kelele huko nje. Tukapatwa na mashaka, na kuinuka ili twende nje tukaangalie kuwa kuna nini. Ila kabla ya kutoka nje, Carlos alikuwa amerudi huku amemshika dada mkono ambapo mkono mwingine alijiziba sura. Mama akauliza, "Kuna nini tena?" "Kuna vitu nje vimemtisha, mwacheni akapumzike kwanza halafu nitakuja kesho kuongea vizuri" Ikabidi mama amshike dada mkono na kumpeleka chumbani kwake kisha mimi na mama tukaenda chumbani kwa mama kulala kwani na leo nikaogopa kulala chumbani kwangu. Nikiwa chumbani na mama, akaanza kuniuliza maswali kuhusu Carlos. "Unamuonaje Carlos mwanangu?" "Kwakweli mama sina la kusema maana hata nikisema sidhani kama utanielewa" "Kivipi mwanangu? Nieleze tu nitaelewa" "Nimuonavyo mimi ni kama kijana wa kwenye ndoto zangu" "Kivipi mwanangu? Au unatamani awe mumeo?" "Hapana mama, simpendi name ndiomana nimekwambia Kuwa huwezi kunielewa hata kama nitakuelezaje" "Haya niambie basi unaonaje anaweza kutusaidia kweli?" "Sijui mama, kwa kifupi simjui Carlos tofauti na unavyofikiria" "Sawa mwanangu kesho nitafanya kitu fulani, nadhati kitakuwa kizuri kwetu na maisha yetu" Halafu tukalala. Leo mambo ya ajabu hayakutokea kabisa usiku hadi kunakucha ilikuwa shwari kabisa. Asubuhi ya leo kama kawaida Dada alijiandaa na kwenda kazini, akasahau yote yaliyotokea Jana yake. Nikabaki Mimi na mama ila mama nae akajiandaa na kutoka, akaniacha pekeyangu nyumbani nikaamua kuangalia luninga ili kujisahaulisha baadhi ya mambo. Nikapatwa na ugeni leo alikuwa ni dada Salome, nikamkaribisha ndani bila ya kuhofia uchawi wake ambao nimeambiwa. "Asante kwa kunikaribisha mdogo wangu, Nina mengi ya kuzungumza na wewe" "Usijari Dada, kuwa huru tu kuniambia chochote" "Kwanza kabisa ni kuhusu maisha yako, hivi hujioni kuwa umebadilika?" "Mi sijijui Dada, bora uniambie nilivyo" "Umejibu vyema Sabrina ni kweli kabisa hujijui wewe wala hujitambui kwa sasa, pia napenda nizungumze nawe kuhusu yule kijana uliyekuwa nae hospitali siku ile" "Nani huyo? Carlos?" "Nadhani ndio huyo huyo, yule kijana yule ni......" Mama alikuwa karudi akiambatana na rafiki yake mwingine, aliyeitwa mama Semeni na kukatisha mazungumzo ya mimi na dada Salome maana mama alimvamia Salome kwa maneno. "Eeeh kilichokuleta na wewe?" "Kwani vibaya mama?" "Mara yako ya mwisho kuja hapa lini ?" "Mwaka Jana" "Mwaka huu umefata nini" Dada Salome akabaki kimya. "Haya, kama ulivyokuja naomba uondoke hivyohivyo" Nikajaribu kumtetea, "Lakini mama...." "Hakuna cha lakini hapa, huyu binadamu simtaki nyumbani kwangu" Ikabidi dada Salome aondoke, nami nikaenda chumbani kwangu kwani sikutaka maswali zaidi toka kwa mama. Baada ya muda kidogo mama akaniita, nikaamua kutoka na kuwafata pale sebleni. "Kilichokukimbiza ndani ni nini? Hujui kama yote haya nafanya kwaajili yako?" Nikabaki kimya tu huku nikimuangalia mama, "Haya njoo ukae hapa" Nikasogea na kukaa karibu yao ili kuwasikiliza. "Huyu hapa mama Semeni kasema atatusaidia pia" "Atatusaidiaje?" "Atatupeleka kwa mtaalam" "Mtaalam??" Nikajua sasa mama ameanza na mambo yake ya imani za kishirikina. "Sasa unashangaa nini?" "Mmh mama! Huo ni ushirikina" Mama Semeni akaongea sasa. "Sio ushirikina Sabrina, yote haya ni katika kukusaidia wewe na maisha yako" "Basi kama ni vya kunisaidia mimi msinilazimishe kwanza, acheni nifikirie halafu nitawajulisha" Mama akachukia sana, "Huyu Sabrina kashaanza utahira wake" "Mwache tu Mama Penina, akiwa tayari atasema mimi nipo wakati wote nitawapeleka" Nikarudi chumbani kwangu na kuwaacha na mazungumzo yao. Nikawaza sana nikiwa chumbani kuwa mama ana maana gani kutaka twende kwenye mambo ya kishirikina ila sikupata jibu. Baada ya muda nikasikia kuwa mama Semeni kaondoka, nikaamua kwenda kumuuliza mama maswali yangu. Nikamkuta ametulia kabisa akiangalia video, ila kabla sijamuuliza alifika dada Penina akiwa ameongoza na Carlos. Tukashangaa kuwaona pamoja, mama akawa wa kwanza kuuliza. "Mmekutana wapi nyie leo?" Dada Penina akaanza kuelezea, "Yani huwezi amini mama jinsi Carlos alivyotusaidia ofisini yani mpaka Salome akaondoka mwenyewe" "Basi ndio akaja huku kutuletea mauzauza yake" "Khee! Alikuja huku mama?" "Ndio, nimemkuta akiongea na Sabrina. Nimemtimuaje" "Umefanya vizuri sana mama, huyu Sabrina ni mjinga na hajielewi hata kidogo. Kwakweli tumshukuru sana Carlos kwa moyo wake wa kusaidia watu" Carlos alikuwa akitabasamu tu kufurahia sifa alizopewa, dada Penina akaenda kupika kwa lengo kuwa leo jioni Carlos apate kula kwetu. Carlos aliongea kidogo na mama na kuahidi kuwa atarudi hiyo jioni. Kitu hiki kwa Carlos huwa kinanichanganya pia kwani sio mtu wa kusema utakaa nae muda mrefu kuongea, yeye akikaa kidogo tu huwa anaaga na kuondoka na hapo hufanya nizidi kupatwa na maswali mengi zaidi juu yake. Tulipokuwa tunaandaa chakula cha usiku ndio muda huohuo Carlos nae alifika tena. "Nimekuja kutimiza ahadi yangu ya kula hapa leo" "Bora umekuja maana kesho tungekulaumu sana" Sikuongea neno lolote, nilikuwa kimya kabisa. Tukaanza kula, kila mmoja na sahani yake. Wakati nakula, Carlos alikuwa akiniangalia na kunikonyeza, nikaishia kutabasamu tu. Niliposhusha macho kwenye sahani yangu nikaona kumejaa mchanga na mawe wakati kulikuwa na wali nyama, nikasogeza sahani pembeni na kupiga kelele. Mama akaniuliza, "Nini wewe? Una kichaa?" "Hapana mama, ona" "Nione nini?" Namuonyeshea sahani yangu, "Si wali huu na nyama! Au ni nini?" "Ni mchanga na mawe mama" Mama na dada wakacheka, "Kweli unawazimu wewe, yani wali nyama unasema mchanga na mawe!" "Kweli mama ni mchanga na mawe" Carlos akainuka huku akitabasamu na kusogea mahali nilipokuwa nimesimama, akanishika bega na kunikalisha kwenye kitu kisha akanisogezea ile sahani yangu ya chakula ambayo nimelalamikia kuwa ni mchanga ili nile. Akasogea na yeye na kula karibu yangu, nikajikuta nikila kile chakula bila mashaka tena yani kamavile sio mimi niliyelalamika kuwa kile chakula ni mchanga. Tulipomaliza Carlos aliaga kuwa anaondoka, mama hakuacha kumshukuru Carlos. Carlos akaniangalia na kuniambia kuwa, "Hunifikishi mlangoni Sabrina?" Mama akadakia, "Inuka Sabrina umsindikize mwenzio" Nikainuka na kumfikisha mlangoni, kisha akaniambia. "Nitakusaidia kila kitu endapo utakubali kitu kimoja tu kutoka kwangu" "Kitu gani hicho?" Hakuniambia ila akaondoka na kuniacha nimesimama pale mlangoni, kisha nikarudi ndani na kumkuta mama na dada wakijadili kuhusu Carlos. "Unaona mama, Carlos ndio anafaa kwa Sabrina. Atamsaidia huyu na uchizi wake" "Kweli kabisa maana alivyoanza pale kwenye chakula kuwa ni mchanga sijui ingekuwaje, bora Carlos alikuwepo" Nikawaangalia tu na kwenda chumbani kwangu kwani leo nilijisikia kulala kwenye chumba changu. Nilipokuwa chumbani ile kauli ya Carlos ikanirudia kichwani kuwa nimkubalie jambo moja tu, nikajiuliza tena. "Litakuwa jambo gani hilo?" Mara nikasikia sauti kama ikininong'oneza, "Olewa na mimi" Nikashtuka sana na kuangalia kila mahali kuwa ni nani anaongea, nikajijibu mwenyewe kuwa, "Sitaki kuolewa na wewe" Sauti ile ikasema tena, "Lazima nikuoe Sabrina" Uoga ukanijaa kuwa ni huyuhuyu Carlos au ni nani maana sikujielewa kabisa. Mara nikajiona kama nimelala halafu naota ila nilikuwa macho kama mtu aliyepumbazika, nikaona mbele yangu vitu vingi vya kifahari huku ile sauti ikijirudia ndani. "Lazima uolewe na mimi, lazima uolewe na mimi Sabrina" Nikajiona tena nimekuwa mwanafunzi, nimevaa sale za shule nimesimama barabarani nikiomba lifti. Ikaja gari na kusimama mbele yangu nikapanda, kwenye uskani alikaa dereva, nilipomuangalia ni yule mkaka wa ndotoni akitabasamu na kusema. "Lazima uolewe Sabrina" Hapo ndipo niliposhtuka kutoka kupumbazika kwangu na kushangaa nikiwa chumbani kwangu tena kitandani huku nimekaa bila hata ya kujielewa kwani uoga ulikatika gafla na kujikuta nikikumbuka matukio ya nyuma wakati nasoma. Nakumbuka nilipenda sana kusimamisha magari ya watu kwaajili ya lifti ila sikumbuki kama kuna siku yoyote niliyowahi kukutana na mtu wa ajabu. Hapohapo nikapatwa na usingizi na kulala hadi panakucha. Mama ndiye aliyekuja kunishtua siku ya leo. "Khee Sabrina, umelala hadi muda huu?" Nikaamka na kumsalimia mama, "Leo ni siku njema mwanangu, kuna habari njema zinakuja" "Zipi hizo mama?" "Sijui ila nimeoteshwa tu mwanangu" "Sawa mama, na ziwe njema kweli" Nikaenda kujisafisha mwili na kuendelea kufanyakazi za ndani kama kawaida. "Ila mama natamani kweli kwenda kuwatembelea rafiki zangu" "Sabrina mwanangu usitake kuniletea makubwa hapa, hebu tulia ndani. Ngoja mambo yawe shwari utaenda, kama umewakumbuka sana wasiliana nao kwa simu tu" "Hawapatikani mama, natamani sana kujua hali zao ila siwapati" "Usijali mwanangu, muda upo utawatembelea hadi uchoke" Kwakweli kukaa nyumbani kwa muda nilichoka tena nilichoka sana Tulipomaliza kazi na mama tulienda kupumzika sasa. Nikaenda chumbani kwangu na kujaribu tena kuwapigia simu rafiki zangu haswaa Sam, nilimkumbuka sana ingawa mengi yalitokea kati yetu ila sikuacha kumkumbuka ila hakupatikana hewani. Rafiki zangu wote hawakupatikana hewani hadi nikaona ni uchafu tu kuwa na simu isiyokuwa na maana yoyote ile kwani ilikuwa ikikaa bila kupigwa wala kutuma ujumbe, nikajisemea iwe isiwe lazima kesho niende kumtembelea Sam. Mawazo yalikuwa mengi sana, nikaamua kulala ilikupunguza mawazo. Wakati nimelala, nikawaona watu wengi sana wamekuja nyumbani wakiwa wameambatana na yule kaka wa ndotoni halafu mimi nilikuwa pembeni nikishangaa. Nikamvuta mkono dada Penina na kumuuliza. "Kuna nini kwani?" "Wamekuja kutoa mahari, mdogo wangu unaolewa" Nikauliza kwa mshangao, "Naolewa! Na nani?" "Si yule kijana pale" Akimuonyeshea yule kijana wa ndotoni. Nikashangaa na kusema. "Simtaki yule" "Khee! Humtaki mchumba wako?" "Sio mchumba wangu yale" "Awe mchumba wako asiwe mchumba wako lazima akuoe maana mahali yake ishakubaliwa" Nikaanza kulia na kusema kuwa kuwa sitaki kuolewa, dada akasema. "Usilie mdogo wangu, furahia ndoa. Ndoa ni furaha" Nikazidi kulia na kulia sana. Kushtuka pale kitandani, mahali nilipolaza kichwa pote palijaa machozi, hapo nikagundua kuwa nilikuwa nalia kweli wakati naota. Nikainuka na kukaa kitandani huku nikitafakari ile ndoto, ila nikasikia kama kuna watu wakizungumza sebleni nikaamua kujifuta machozi na michirizi ya usingizi ili nikawaone kuwa ni wakina nani. Nikatoka hadi sebleni na kuona watu kadhaa kabla sijawatambua vizuri, mama akainuka na kuanza kunipigia vigelegele.





    Nikatoka hadi sebleni na kuona watu kadhaa kabla sijawatambua vizuri, mama akainuka na kuanza kunipigia vigelegele. Hapo ndipo nikahisi kuwa huenda ile ndoto ni ya kweli na kuanza kulia tena huku nikisema kwa nguvu kuwa, "Sitaki kuolewa, nimesema sitaki kuolewa" Mama akanishika mkono na kusema, "Wewe mtoto una nini wewe? Mbona wanifedhehesha kwa wageni?" "Nimesema sitaki kuolewa mama" Huku nikizidi kulia, "Kwani nani anataka kukuoa hapa jamani!" "Hao waliokuja kutoa mahari, nimesema sitaki kuolewa" Niliwaangalia wale wababa huku sura yangu ikiwa imejaa machozi na kuwaambia. "Sitaki kuolewa, ondokeni na mahari zenu sitaki mie siwataki nimesema sitakiii" Mama akaanza kunituliza, huku akisema, "Mwanangu jamani una nini wewe? Unanitia aibu ujue! Hebu waombe radhi wageni" Nikaona mama ndio ananichanganya kabisa, nikaenda jikoni na kuchukua kisu huku usoni nikiwa na machozi. Nikawafata wale wababa mbele, "Ondokeni hapa sasa hivi, kama hamuondoki najichoma kisu" "Wewe Sabrina mwanangu wewe, usifanye hivyo mama. Nakupenda mwanangu" Ikabidi wale wababa wainuke na kutoka, bado niliendelea kuongea neno moja tu. "Sitaki kuolewa" Na machozi kunitoka zaidi, mama akanisihi kuwa niachie kile kisu, kisha nikamkabidhi na kukimbilia chumbani kwangu huku nikiendelea kulia kwa uchungu sana hadi nikapatwa tena na usingizi. Nikiwa ndani ya usingizi mzito sana, nikamuona yule kaka wa ndotoni akicheka sana na kufurahi huku akinionyeshea alama ya dole gumba yani kamavile mtu aliyekipenda kitu. Nikashtuka sasa na usiku ulikuwa umeshaingia, nikakaa kitandani na kujiuliza kwanini yule mkaka wa ndotoni alionyesha kufurahi, au alifurahia nilichofanya kwa ndugu zake au kuna kitu gani kikubwa alichofurahia, hapo nikakosa jibu. Ila sasa hivi nilikuwa na hali nzuri kidogo nilipoamka tofauti na wakati ule nilipowatimua wale wababa sebleni. Nilitoka chumbani na kumkuta mama na dada wakiwa http://deusdeditmahunda.blogspot.com/sebleni ila mama hakuniuliza chochote zaidi ya kuniangalia na kutikisa kichwa kama vile mtu anayenisikitikia. Nikaenda kula na kisha kurudi tena chumbani kwangu kwaajili ya kulala. Haikuchukua muda sana nikawa nimelala, kama kawaida ya yule kijana wa ndotoni na leo akaja tena ndotoni kwangu. Akaniangalia na kutabasamu kisha akasema, "Sabrina, wewe ni binti mwenye akili sana tena sana. Kwakweli leo umenifurahisha sana, kesho nitakupa zawadi yako kwa hakika utaipenda" Nikamuangalia tu huku akiendelea kuongea, "Na ukiendelea kufanya kama ulivyofanya leo, kwa hakika utafurahi daima" Sikuwa na uwezo wa kumsemesha wala kumjibu nilikuwa namsikiliza tu na alinisifia muda wote kwa nilichofanya leo hadi kunakucha. Asubuhi ya leo niliwahi kuamka kupita siku zote, wote ndani ya nyumba yetu walikuwa bado kuamka. Nikaanza kufanya usafi, hata dada alipoamka na kujiandaa kwenda kazini alinishangaa sana. "Naona leo mapepo yako yamepungua" "Sina mapepo bhana" Dada akacheka na kuniambia, "Yani wewe Sabrina wewe, maisha yako yana tabu sana" Nikamuangalia tu, naye akaondoka kwenda kwenye kazi yake. Mama alipoamka alinikuta nikiangalia video na kazi zote za asubuhi nimezimaliza, nikamsalimia pale mama kisha nae akaanza kusema yake. "Naona leo amani imetawala mwanangu" "Mbona siku zote ni amani mama" "Mmh wewe mtoto wewe, aibu uliyonipa jana sitokaa niisahau" "Aibu gani mama?" "Inamaana huelewi ulichofanya jana? Ngoja nikaoge kwanza ndio nije nikwambie mauzauza yako" Mama akaenda kuoga na kuniacha nikiwa na mawazo sasa maana mimi mwenyewe sikuona kama kile nilichofanya jana ni kitendo cha aibu ukizingatia kuolewa ni hiyari ya mtu na sio kulazimishwa, kwahiyo mimi niliona ni sawa kabisa kuwatimua wale wababa nyumbani kwetu. Wakati nawaza hayo, simu yangu ya mkononi ikaita, kuangalia ni Suzy anapiga. "Niambie mwanampotevu Suzy" "Wewe ndio mwanampotevu Sabrina, sijui hata kama unajua yanayoendelea kwasasa" "Yapi hayo?" "Sam yuko wapi?" "Sijui, niambie wewe" "Ona sasa Sabrina hadi mpenzi wako alipo hujui, nakuachia kazi wewe mwenyewe ukatafute Sam alipo ndio utapata jibu" "Jamani Suzy si uniambie tu" "Nikwambie kitu gani wakati barua yangu umeichana Sabrina, unajua niliandika vitu gani? Au ulisoma na kuipuuzia? Sasa kazi kwako kujua Sam alipo." "Jamani Suzy, tafadhari rafiki yangu nisaidie. Mimi nitajuaje alipo Sam kwasasa?" "Nilikuwa na moyo wa kukusaidia sana ila umeuvunja, inaonyesha wazi msaada wangu huutaki. Sam unapajua kwao kwahiyo utaenda kumuulizia" Kisha akakata simu na kuniacha na mawazo kichwani kuwa Sam atakuwa wapi, au atakuwa na Lucy kumfariji kwa lile tukio nililofanya! Sikupata jibu. Nilitulia pale nikiwa na mawazo, mama ndiye akanishtua tena. "Haya sasa mwanangu nimerudi" "Eeh mama niambie hiyo aibu niliyokupa jana" "Hivi wewe unaona kufukuza wageni kama vile ni jambo zuri?" Hapo nikawa mkali kidogo sasa, "Kwani mama kuolewa lazima? Mi sikotayari kuolewa" "Aliyekwambia unataka kuolewa nani?" "Si wale wageni mama walikuja kutoa mahari" "Una akili wewe? Uliona wapi mahali inatolewa na kupokelewa bila ya muhusika kukubali? Uliona wapi?" "Sijawahi ona" "Na hiyo mahari yako ni mahari gani hadi niipokee mwenyewe? Huna baba wadogo wewe? Huna wajomba? Mbona unataka kuniletea balaa mtoto! Na huyo wa kukuoa ni nani?" Ikabidi niwe mpole sasa, "Kwani wale wajana walifata nini?" "Kwa mawazo yako wewe wale wababa wanataka kukuoa? Hebu uwe na adabu mwanangu, wale ni kama baba zako tena wana wake zao, watoto wao kama wewe na familia zao. Yani umenitia aibu sana, unajua walichofata wale?" "Sijui mama" "Wale ni rafiki wa marehemu baba yako, walikuwa wakifanya nae kazi sehemu moja. Tena walikuja na habari nzuri sana ya kwako ila uchizi wako umevuruga kila kitu" "Habari gani mama?" "Sikia mwanangu, kipindi upo kwa kaka yako nilienda ofisini kwa wale maana nilikuonea huruma sana kukaa nyumbani wakati mwanangu umesoma. Nikaenda kuwalalamikia na kuwaomba kuwa endapo ikitokea nafasi wakuingize na wewe mwanangu, sikupendezewa kukaa kwako nyumbani hapa. Sasa jana walivyokuja, walikuja kutusalimia kwanza na pili waliniambia kuwa kuna nafasi ofisini kwao kwahiyo unatakiwa wewe ukafanye interview wakuweke" Hapohapo nikashtuka na kumuuliza mama, "Na mbona nilipotoka ndani uliponiona tu ukaanza kunipigia vigelegele?" "Furaha mwanangu, unajua furaha wewe? Nilikuwa na furaha iliyopitiliza mwanangu kuwa ombi langu limejibiwa, ndiomana nikapiga vigelegele. Kwahiyo kwamaana yako wewe vigelegele vinapigwa kwenye ndoa tu au mahari tu?" "Sijui mama, nilichanganyikiwa" "Uchanganyikiwe na nini mwanangu, hata kama wangekuwa watu wa kuoa ulitakiwa uulize kwanza maana humu ndani wa kuolewa hauko peke yako. Kumbuka hata dada yako Penina hajaolewa" "Sasa mama itakuwaje?" "Unadhani itakuwaje kwa yale uliyoyafanya jana? Hakuna cha kazi tena, nani atapenda kuajiri chizi kwenye kampuni yake?" "Ila mimi sio chizi mama" "Kwa ulichofanya jana ni chizi, umenitia aibu ya mwaka mwanangu hata sijui nitawaangaliaje wale wababa tena! Kwakweli umeniumiza sana Sabrina" "Nisamehe mama" "Nisamehe yako haina muhimu tena mwanangu, hii ni aibu na fedheha" Nikajisikia vibaya sana, nikatamani siku irudishwe nyuma ili nirekebishe nilichokosea ila ndio hivyo, maji yakimwagika hayazoleki. Machozi yakanitoka na kujilaumu kwa uchizi ambao nimeufanya kwa wageni wa muhimu kama wale. Nikakumbuka kuwa ndiomana yule mkaka wa ndotoni alikuwa akinisifia usiku kucha. Nilikuwa na mawazo sana leo na sikujua cha kufanya moja kwa moja, kila kitu kilinichanganya. Nikifikiria kuhusu kazi na jinsi nilivyowatimua wababa wa jana, nikifikiria kuhusu Sam niliumia sana. Nikaona kuwa itakuwa vyema kama nikifatilia kuhusu Sam kwanza ila je nitatokaje nyumbani wakati mama yupo? Nitamuaga vipi wakati nimekatazwa kutoka? Huo ukawa mtihani kwangu na maswali pasipo majibu, ila nikatulia kwanza ili nipate njia rahisi ya kutoka hapa nyumbani. Wakati nawaza nikapigiwa simu na Carlos. "Nina zawadi yako Sabrina" "Zawadi gani?" "Utaiona nikiileta" "Utaileta muda gani?" "Nitakuja jioni" "Poa karibu" Alipokata simu nikaendelea kutafakari njia ya kuondokea na nikaona hiyohiyo ya kuhusu Carlos ndio itafaa. Nikaenda kuongea na mama kwanza ili nimvute kimawazo, "Carlos kanipigia simu kasema ana zawadi yangu" "Zawadi gani hiyo? Carlos anakupenda sana mwanangu" "Sijui ni zawadi gani, ila kasema ataileta au ataniambia nikaichukue" "Leo leo?" "Ndio ni leo mama" "Basi hakuna tatizo mwanangu" Nikatulia na kujigelesha kufanya kazi ndogo ndogo, zilizobaki. Muda wa mchana nikaenda chumbani kwangu na kuandaa nguo za kuvaa kabisa, kisha nikategesha simu yangu kuwa ipigwe baada ya robo saa ili mama ajue kuwa napigiwa halafu nikaenda kukaa sebleni karibu na alipokaa mama kisha simu nikaiweka mezani na kuendelea na maongezi mengine na mama. Baada ya robo saa simu ikaanza kuita, mama akaangalia pale mezani na kuona kuwa Carlos ananipigia hakujua kama ni ya kudanganya yani (fake call), akanishtua na kusema, "Si unapigiwa na Carlos hapo, mbona hupokei?" Nikajigelesha kuwa sikuisikia kisha nikaichukua na kuipokea huku nikiongea kwa nguvu na pale pale ili mama anisikie kuwa kweli nimeitwa. "Hallow.... Ndio.... Nije muda huu?.... Sawa nakuja.... Nipe dakika tano tu nitakuwa nimefika hapo" Nikakata simu na kumwambia mama, "Carlos kaniambia niende stendi mara moja kuichukua ile zawadi" "Kuhusu watu je?" "Nadhani hakuna tatizo maana kaniita mwenyewe" "Sawa basi nenda uwahi kurudi" Nikaenda chumbani na kuvaa haraka haraka nguo zangu nilizoandaa kisha nikatoka na kumuaga mama kuwa nitarudi muda sio mrefu halafu nikaondoka. Mwendo ulikuwa moja kwa moja hadi kituo cha madaladala na kwenda nyumbani kwa Sam. Kufika pale nikakuta kufuli kwenye mlango wake, ikabidi nimgongee jirani wa chumba cha pili kumuuliza, alitoka mdada. Nikamsalimia na kuanza kumuuliza. "Samahani dada, eti Sam ulimuona alipotoka?" "Kwakweli huyo Sam sijamuona wiki ya pili sasa, hayupo kabisa. Hiko chumba kipo hivyo hivyo kila siku na kufuli lake" "Kwahiyo hajulikani alipo?" "Hilo ndio jibu maana hatujui kama amesafiri au yuko wapi" Basi nikamshukuru yule dada kwa taarifa na kuondoka pale, huku nikifanya safari ya kwenda nyumbani kwao kabisa na Sam. Nilipofika kwao sikumkuta mtu yoyote nje, hivyo nikagonga. Alikuja mama Sam na kunifungulia mlango, nilikuwa natabasamu ila yule mama alikuwa amechukizwa sana na sikujua ni nini kilichomchukiza. Aliniangalia kwa hasira sana, halafu akanizaba kibao.



    Aliniangalia kwa hasira sana, halafu akanizaba kibao. Nikabaki kuugulia kibao nilichopigwa bila ya kujua sababu ya kupigiwa haswaa na mama Sam ambaye nilikuwa naongea nae vizuri sana zamani. Yule mama baada ya kunizaba kibao akaanza kuongea maneno ambayo alitaka kuongea. "Mtoto mbaya sana wewe sitaki hata kukuona" "Kwani nimefanya nini mama?" Akaiga kwa kubana sauti, "Kwani nimefanya nini mama? Hujui ulichokifanya wewe mbwa?" Nikawa nimeduwaa kuwa leo nimeshakuwa mbwa. "Tena wewe ni shetani mwenye mapembe, hufai hata kidogo. Mtoto umenichefua wewe halafu bila haya unaleta ngwala zako hapa" "Ila mama sijui kosa langu" "Kosa lako kawaulize wazazi wako kwanini walikuzaa maana hilo ndio kosa kwao kumzaa shetani kama wewe" Machozi yakaanza kunitoka kwani sikuelewa kwanini nafokewa kiasi kile, "Nisamehe mama" "Tena unipishe mtoto wa kike, sina mtoto shetani kama wewe na uondoke hapa nyumbani kwangu sasa hivi" "Kwani kosa langu lipi?" "Nimekwambia uondoke na ole wako siku nikukute na mwanangu Sam nitakukata hiyo miguu yako. Ondoka sasa hivi usitake nitende zambi hapa" "Ila Sam nampenda mama" "Umpende kitu gani? Unajua kupenda wewe? Kumtesa mwanangu tu na ushetani wako. Unaujua uchungu wa Sam wewe? Nimekwambia uishie hukohuko kwenu, nikikukuta siku nakukata miguu hiyo." Nikajaribu kujitetea, akasema kwa nguvu. "Nimesema tokaaaaa" Ikabidi niondoke huku machozi yakinitoka kwani sikujua kosa langu ni nini kuwa vile. Nikaamua kwenda kwa dada wa Sam ambaye alikuwa akiishi sio mbali na hapo. Kufika nilimkuta ila nae alikuwa na hasira na mimi, nikamueleza kilichonileta kwake na jinsi nilivyopigwa kibao na kutimuliwa na mama yao. "Tena hicho kibao hata hakitoshi ilibidi akutwange kabisa" "Ila kosa langu ni nini?" "Kwani hujui?" "Sijui, naomba uniambie" "Mara ya mwisho Sam umemuacha wapi?" Nikashindwa kujieleza na kujiumauma tu. "Unaona hata kujieleza unashindwa sababu ya maovu yako, basi kwa taarifa yako Sam ameswekwa jela sababu yako. Mdogo wangu anahenyeka tu huko na wewe hata kwenda kumjulia hali umeshindwa halafu leo unajileta bila aibu!" Na yeye akanizaba kibao na kusema, "Hiyo ni haki yako na uondoke hapa hata mimi sitaki kukuona" Nikaendelea kutoa machozi kwani hata sikujua pa kuelekea, nikaulizia kituo alichopelekwa ila yule dada alinitimua bila ya kusema chochote. Nikawaza pa kuelekea ila sikuwa na pa kwenda, mawazo yalinijaa tele bila ya majibu hata kurudi nyumbani nikaona itakuwa kazi bure tu. Nikafanya maamuzi ya haraka haraka na kuamua kwenda nyumbani kwakina Suzy. Nilipofika sikumkuta Suzy ila niliwakuta wadogo zake na mama yao ambapo walinikaribisha vizuri sana, kwahiyo nikakaa sebleni kwao kumngoja Suzy. Mara usingizi wa gafla ukanipitia. Wakati nimelala pale, nikamuona Sam amewashiwa moto mbele halafu wanamsukuma ili wakamchome. Nikashtuka na kupiga kelele, "Msimchomeeeee...." Kumbe nilikuwa naota, nikaona aibu sana pale wadogo zake Suzy walipokuwa wakinishangaa na kucheka, kisha mama Suzy akaniuliza. "Nini tena mwanangu?" "Ndoto tu mama" "Pole sana" Muda huo Suzy nae akawa amewasili pale kwao, akafurahi kuniona na kuanza kuzungumza nae. "Bora umekuja Sabrina, nimekuwaza sana. Haya inuka twende maana nikikaa hatutaweza kwenda" Nikainuka na kuaga kisha kufuatana na Suzy tena bila ya kujua tunapoelekea. Kufika nje Suzy akaanza kuongea, "Unajua rafiki yangu, Sam ana wiki ya pili sasa yupo ndani. Siku ile nimekutumia ujumbe ili twende ila ukapuuzia, mi sijali shoga yangu. Kwenu siwezi kuja kwa yale mabalaa. Ila leo nilienda kituoni kumuangalia Sam, anatia huruma kwakweli na anahitaji sana kukuona hivyo nimeshukuru kweli kukukuta hapa nyumbani. Twende haraka haraka tuwahi kurudi" Nilikuwa kimya kabisa nikimsikiliza tu Suzy maana sikuwa na cha kusema kabisa. Wakati tupo kituo cha madaladala tukisubiri usafiri wa kwenda huko nikaamua kumuuliza Suzy. "Kwani ni sababu gani iliyofanya Sam afungwe?" "Inasemekana kuwa Sam amempiga sana Lucy kwasababu yako, halafu akammalizia kwa kumbonda na chupa ya soda kichwani. Hivi ninavyokwambia hadi leo Lucy yupo hospitali na Sam yupo polisi, ndugu wa Lucy wamesema asiachiwe hadi Lucy atakapopona" Nikaishia kuguna tu na kushangaa kuwa iweje aambiwe Sam wakati ni mimi niliyempiga Lucy kwa chupa? Hapa ndipo palinishangaza zaidi. Sikutaka kumueleza Suzy ilivyokuwa ila nilijiamulia moyoni mwangu kuwa nikifika huko polisi nitasema ukweli ili wamuache Sam huru, ila je Sam nae alishindwa kujielezea kuwa ilikuwaje? Au ameamua kutumikia kifungo kwaajili yangu? Sikupata jibu. Gari iliposimama tukapanda na Suzy na kuanza safari ya huko kwenye kituo cha polisi alipopelekwa Sam. Wakati lile gari lipo kwenye mwendo kuna kitu kikaniambia ndani yangu, "Shuka Sabrina, usiendelee na hiyo safari" Ila nikapuuzika na kuendelea, kituo cha mbele yake abiria wengi kwenye ile gari wakashuka nikabaki mimi na Suzy na abiria wengine wawili ambao sikuwajua, daladala ikaendelea na safari yake. Kufika njiani ile daladala ikapoteza uelekeo na kuanza kwenda hovyohovyo, mimi na Suzy tukaanza kuogopa. Ile gari ikafika mahali na kusimama kwa gafla, Suzy na wale abiria wengine wakafanikiwa kushuka ila wakati mimi nataka kushuka ile daladala ikaondoka na haikuwa na abiria wala konda wala dereva, nadhani wote walishuka. Nikapiga makelele lakini hakuna aliyenisikia, niliogopa sana na nikajua ndio mwisho wangu. Kweli kwenye matatizo hata kama hujui kuomba utaomba tu, nilijikuta nikisema. "Mungu naomba unisaidie, naomba unisamehe dhambi zangu zote" Nilijikuta nikitubu mara nyingi niwezavyo, kweli kifo ni kifo tu wanadamu huwa tunapenda kusema bora nife ila kiukweli tunaogopa kifo ingawa tunajua kipo na lazima kitupate. Uoga ulizidi zaidi pale lile gari lilipokuwa likiyumbayumba kila upande, nilijisemea kuwa mwisho wangu umewadia sasa, mwisho wa Sabrina na mauzauza yake umefikia. Niliziba uso wangu kwa mikono ili nisione kitakachotokea mbele yangu. Mara nikasikia lile gari likigonga kitu, hata kama nilifumba macho sasa nilifumbua kwa uoga, ile gari iligonga mti na ikawa inafuka moshi. Hapo ndipo nikatokea dirishani na kujitahidi kukimbia ila kabla sijafika mbali sana nikasikia mlio kama wa bomu ulionirusha na kuniangusha chini, kuangalia kwenye lile gari palikuwa na moto mkubwa ukiwaka ikionyesha kuwa lile gari lililipuka. Nilikuwa pale chini kama mtu nisiyejielewa, sikuona mtu yeyote eneo lile nilikuwa mwenyewe. Nikawa najitazama vizuri na kujiuliza, "Hivi mimi mzima kweli au nimekufa? Eneo gani hili lisilokuwa na watu?" Nikajaribu kujitingisha na kujifinya finya nione kama nitapata maumivu yoyote, nikajigundua kuwa mimi ni mzima ila nipo mahali ambako sipatambui kuwa nitaanzia wapi na nitaishia wapi. Nikaanza kujikongoja ili niweze kutoka kwenye lile eneo. Nikasikia sauti ikiniambia, "Kiburi chako ndio kinachokuponza hapo" Nikijaribu kuifatilia hiyo sauti najikuta sina uwezo wa kuifatilia zaidi ya ninavyoisikia. Cha kushangaza sasa, licha ya misukosuko yote hiyo simu yangu bado nilikuwa nayo kwenye mfuko wa suruali niliyovaa siku hiyo. Nilipojipapasa na kuikuta nilishangaa sana na kufurahi pia, nikaichukua na kumpigia Suzy hakupatikana, nikampigia mama na dada hawakupatikana yani wote niliojaribu kuwapigia muda huo hawakupatikana na wakati giza lilishaanza kuingia, sikuwa na la kufanya, nikaamua kutembea hovyohovyo ili hata nikiwakuta wenyeji wa eneo lile niwaulize vizuri ili wapate kunielekeza. Nilitembea sana hadi giza ilishaingia vizuri, nikakosa matumaini na sikujua cha kufanya. Kwa bahati nikakutana na kijana, sijui hata alikuwa ametokea wapi na anaenda wapi, nikajaribu kumsalimia ila yeye aliongea maneno mengine, kila nilichosema yeye alijibu vingine hapo nikagundua kuwa yule kijana hajui kiswahili, sasa tutaelewana vipi ikiwa na mimi sielewi anachosema? Kwavile ni mimi mwenye shida nikaamua kumfatilia nyuma nyuma hadi anapoenda. Akafika sehemu moja kuna nyumba ya nyasi tena iko peke yake wala hakuna nyumba ya karibu jirani yake. Wakatoka watoto wawili wakike kwa kuwakadilia kama wana miaka kumi hivi, wakampokea yule kijana. Kwavile na mimi nilianza kuogopa giza nikaamua kuwafata hivyohivyo huku uoga ukiwa umenijaa moyoni, niliogopa sana. Nikajaribu kuwaongelesha ila wakanijibu kwa kilugha chao, nikaamua kukaa hivyohivyo hata kama hatuelewani. Wakatenga chakula na kuniita kwa ishara ya mkono kuwa nijumuike nao, ingawa njaa ilikuwa inaniuma ila nilisita kujumuika nao ukizingatia hata chakula chenyewe sikukielewa, nilichokitaka hapo ni mahali pa kulala tu kwa usiku huo ukizingatia maeneo yenyewe hapakuwa na watu zaidi ya hao. Walipomaliza kula, wakanionyesha mahali nikajilaza. Wakati nimelala nikamuona mtu ameshika kisu anataka kunichoma nikashtuka na kupiga makelele. "Nakufaaaaa....." Kitu ambacho kiliwashtua mule ndani, nikashangaa yule kijana akija kwa hasira na kunivutia nje, nilikaa pale nje na kulia hadi panakucha. Asubuhi yake nikaanza kuondoka lile eneo huku sauti ikitembea kichwani mwangu, "Yote hayo yataisha ukikubali kuolewa na mimi" Nikawa naumia sana hukunikichukia kuwa ni mambo gani haya yanayoiandama akili yangu. Nilikuwa nimechoka sana muda huo, mara simu yangu ikaita kuangalia ni Carlos aliyekuwa akipiga ile simu nikaipokea huku ninalia. "Njoo unisaidie Carlos njoo" "Nakuja Sabrina" Nilichoka sana na njaa ilikuwa inaniuma, hata sikuwa na muda wa kumuuliza Carlos kuwa atafika vipi mahali ambako sijamtajia maana hata mimi mwenyewe sikujua nilipo. Nilikaa chini, kiu na njaa vilinisumbua sana maana hapakuwa na maji hata kidogo wala miti ya matunda nayo haikuwepo. Nikakaa chini ya mti mmoja na usingizi kunipitia palepale, akatokea mkaka wa ndotoni akitabasamu na kusema. "Yote yataisha ukiolewa na mimi" Nikashtuka na kusema, "Sitaki kuolewa na wewe" Simu yangu ikaita tena, ni Carlos aliyepiga na kuniambia kuwa yupo maeneo ya karibu na nilipo kwahiyo niinuke kumfata. Nikaamua tena kutembea taratibu, mbele yangu nikaona gari yake ambapo alishuka na kunifata nilipo, kisha akasema. "Napenda sana kukusaidia Sabrina ila unatakiwa kukubaliana na mimi jambo moja tu" "Lipi hilo?" "Olewa na mimi" Nikabaki nimeduwaa tu na kukosa cha kujibu.



    Nikabaki nimeduwaa tu na kukosa cha kujibu. Nikamuangalia kwa makini Carlos na kupata jibu la haraka kumjibu. "Naomba unitoe kwanza eneo hili halafu hayo mengine tutazungumza badae" "Hakuna tatizo Sabrina, najua unanihitaji kupita unavyofikiria" Kisha akaniongeza hadi kwenye gari yake nikapanda, kwavile nilikuwa nimechoka sana na usingizi kunizidia nikajikuta nimelala. Kuja kushtuka tayari tulikuwa tumefika nyumbani kwetu, mama akafurahi sana kuniona huku akimshukuru Carlos.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ "Nilikwambia mama usijali nitamtafuta Sabrina hadi nimpate, huyo hapo sasa" "Nimefurahi sana, asante baba angu" Tukaingia ndani na mama kisha Carlos akaenda zake. Mama akaanza kuniuliza sasa, "Ulikuwa wapi mwanangu?" "Sijui mama, sijui" "Utaniua mama yako wewe, utaniua kwa presha. Hivi huyo Sam wako atanizalia Sabrina mwingine mimi? Mbona unanitesa hivyo mwanangu?" "Nisamehe mama" "Na huo msamaha ungeombea kaburini nani angekusikia mwanangu? Unajua utaniua wewe mtoto! Kilichokupeleka kwa wakina Sam sijui ni kitu gani, nadhani unaombea hata mimi nife ila ubaki na Sam jinsi ambavyo umekosa akili wewe mtoto" Nikakaa kimya kabisa kwani sikupenda kubishana na mama na vilevile sikujua ni nani aliyemwambia kama nilienda kwa wakina Sam. Mama alipomaliza kusema yake nikaenda zangu kuoga ili kupata nguvu kidogo, kisha nikala chakula ambacho mama aliniandalia bila hata ya kujua kama mwenzie nimelala maporini usiku wote wa jana. Nilipomaliza kula, nilienda chumbani kwangu kwa lengo la kupumzika kidogo. Nikiwa nimetulia chumbani, nikaona mfuko wa rambo. Nikainuka na kwenda kufungua, nikakuta viatu vizuri sana vipo ndani yake. Nikabeba ule mfuko na kwenda kumuuliza mama. "Nani kaweka mfuko huu chumbani kwangu?" "Ni mimi nimeweka, ni zawadi yako hiyo uliyoletewa na Carlos halafu ukanidanganya kuwa unakwenda kuifata" "Nisamehe mama" "Nishakwambia kuwa msamaha wako hauna maana kwa sasa. Sema lingine tu" Nikaviweka vile viatu chini na kuvijaribisha, kwakweli vilikuwa vizuri na vilinipendeza sana. Nikaanza kujaribu kuvitembelea maana vilikuwa virefu kiasi, "Amekupatia sana Carlos, viatu vimekupendeza sana mwanangu" Nikawa natabasamu huku nazunguka navyo ndani kisha nikarudi chumbani kwangu, nikakaa kitandani ili nivivue niweze kupumzika. Nikavivua, mara gafla miguu ikawa kama inawaka moto halafu inauma sana sikujua tatizo ila kuna roho ikaniambia kuwa sababu nimevua vile viatu kwahiyo nikavivaa tena na ile miguu ikaacha kuuma na kuwa kama inawaka moto. Nikajiuliza mahusiano ya kile kiatu na mguu wangu ni nini nikakosa jibu, nikajaribu tena kuvivua nione napo miguu ikaanza tena kupwita, nikavivaa tena na kujiuliza nitalala na viatu miguuni leo? Ila sikuwa na jinsi kwani nilichoka sana na kuamua kulala navyo. Dada ndiye aliyekuja kunishtua pale kitandani. "Sabrina, Sabrina hebu amka tuongee" Nikaamka na kukaa, kisha nikamsalimia na kumsikiliza. "Ulikuwa wapi jana?" "Sijui dada" "Mmh Sabrina! Nasikia ulienda kwa wakina Sam umedundwa huko hadi umekoma" Nikawa kimya tu nikimsikiliza. "Viatu vizuri hivyo kakununulia nani?" "Nimevikuta humu ndani, mama kasema nimeletewa na Carlos" "Eeh vimekupendeza! Hadi unalala navyo duh!" Kisha akainuka na kutoka chumbani kwangu. Nikajitazama tena miguuni na vile viatu, nikajaribu kuvivua hali ikawa kama ya mwanzo. Nikajiuliza ni kwanini? Ila nikajisemea kuwa lazima Carlos anajua sababu, nikachukua simu na kumpigia ila hakupatikana hewani. Nikatoka sebleni. "Naona viatu havibanduki miguuni leo mwanangu" Dada Penina akadakia, "Chezea kitu kipya wewe" Wote wakacheka, nikatamani kuwaambia ninavyojisikia nikikivua ila mdomo ulikuwa mzito kusema chochote kuhusu kiatu. Nikatulia pale sebleni na kusikiliza mazungumzo ya mama na dada ambayo yalinivutia sana, nikajisemea kuwa badae nitamfata dada chumbani kwake ili kumuuliza vizuri. Usiku ulipoingia kama kawaida ya dada yangu alikuwa yupo chumbani kwake akicheza na kompyuta yake ya mezani, nikamfata alipo ili anijibu maswali yangu. "Eeh niambie mwali wa viatu vipya" Nikacheka tu na kumwambia, "Nimekuja kukuuliza kitu dada" "Kitu gani hicho? Uliza tu kuwa huru" "Ni kuhusu mazungumzo yako na mama, umesema yule rafiki yako dada Fatuma alikuwa akisumbuliwa na matatizo gani hadi akaachana na mchumba wake?" "Aah! Kumbe, alikuwa akisumbuliwa na jini mahaba yule" "Jini mahaba? Ndio yukoje huyo jini mahaba?" "Kwakweli mdogo wangu sijui ila itakuwa vyema kama hayo maswali ukienda kumuuliza Fatuma moja kwa moja, nadhani yeye atakuwa anajua maana ndio alikuwa nalo na likamsumbua sana" "Ila je hilo jini lilimuachanisha vipi na mpenzi wake?" "Nasikia lile jini likikupata huwa linataka likutawale lenyewe tu, utashangaa gafla huna maelewano na mpenzi wako mara unaona hakupendi mara anahisi hakuridhishi au hakufai tena na mengineyo hadi unafikia uamuzi wa kuachana nae" "Sasa suluhisho ni lipi hapo?" "Suluhisho ni kwenda kulitoa kama ukigundua unalo, je wewe unahisi kuwa na hilo jini?" "Sijui dada ila ninahitaji kufahamu zaidi" "Basi nitakukutanisha na Fatuma uongee nae na akuelezee vizuri" "Lini sasa?" "Hata kesho" "Mi nataka iwe kesho dada" Nikakubaliana na dada kuwa kesho yake atanipeleka kwenda kukutana na Fatuma nipate kuzungumza nae. "Nitawahi kurudi kesho halafu nitakupeleka" "Sawa dada, utakuta nimeshajiandaa" Akacheka kisha tukainuka na kwenda kula halafu kulala huku nikifikiria hayo mambo ya kesho na viatu vyangu mguuni ambavyo kuvivua sikuweza. Nikiwa nimelala, yule mkaka wa ndotoni akanijia kwenye ndoto kama kawaida na kusema. "Natumaini umeifurahia zawadi yangu" Nikashtuka na kujitazama miguuni ambako nimevaa vile viatu kisha nikavivua kwa hasira ila maumivu niliyoyapata sikuweza hata kusogea na kuamua kuvivaa tena maana sikuwa na la kufanya kwakweli. Nilipovivaa tena nikalala vizuri hadi panakucha na kuamka huku nikifanya kazi za hapa na pale. Mama kuniona tena na vile viatu akaanza kunitania, "Nadhani leo utaoga navyo hivyo viatu maana havivuliwi" Sikujibu kitu maana hawakujua jinsi ninavyoteseka na kile kiatu mguuni. Nilipomaliza kazi, nikaenda kuoga. Nilipofika bafuni nikajaribu kuvua kile kiatu ili nioge, nikakivua na wala miguu haikuniuma ila nilipomaliza tu kuoga ilianza kuniuma tena na kuamua nivae tena vile viatu wakati natoka bafuni. Nikaenda chumbani na kujiandaa ili kumngoja dada arudi na niende nae huko kwa rafiki yake. Dada aliporudi akapumzika kidogo kisha tukamuaga mama na kuondoka huku vile viatu vyangu vikiwa miguuni, "Naona umevipenda sana hivyo viatu Sabrina" "Ndio nimevipenda dada" Tulipofika kwa rafiki yake na dada, tulimkuta ametulia tu ndaki akisikiliza muziki. Dada akaongea nae kidogo pale na kutuaga kuwa kuna mahali anaenda mara moja akitoka huko ndio atapitia tena hapa. "Naona umeniletea Sabrina leo" "Ana maswali yake huyo atakuuliza mwenyewe" Kisha dada akaondoka na kuniacha na rafiki yake dada Fatuma pale. "Kuwa huru Sabrina, niulize chochote nitakujibu" "Jana nilimsikia mama na dada wakiongelea maswala ya jini mahaba na kusema kuwa hata wewe limewahi kukurumbua" "Kwahiyo unahitaji kujua kuhusu jini mahaba?" Nikatikisa kichwa kuonyesha kwamba nahitaji kujua. "Jini mahaba ni kiumbe mwenye tabia ya kukuingilia kimwili bila ridhaa yako, mara nyingi huja wakati umelala. Unakuwa unahisi kama unaota vile kuwa unaingiliwa na mtu, ukija kushtuka mara nyingine unajikuta umechafuka kwa mbegu za kiume, hapo utakuwa na jini mahaba tena aliyekubuhu" "Je mwanadamu wa kawaida anaweza kufanya mambo kama afanyayo jini mahaba" "Si rahisi ila akiwa mchawi anaweza maana atakupumbaza wakati umelala kama huna kinga thabiti dhidi ya watu wabaya" "Unaweza kumuona jini na kuongea nae kama binadamu wa kawaida?" "Majini ni viumbe wa ajabu sana, kwanza wanatisha huwezi kustahimili ukikutana nao. Halafu wananamna nyingi za kutembea na kusafiri, anaweza kujigeuza upepo au hata mdudu mdogo kabisa. Hata ukiwa katika shule zenye majini utashangaa gafla upepo mkali unapita, wanaojua watakwambia jini kapita" "Kwahiyo huwezi ukaonana nae kabisa yani" "Nakwambia huwezi kustahimili kumtazama jini, kwani hujawahi kusikia watu wakisema kuwa majini wanakwato za ng'ombe miguuni mwao, au kusikia kuwa majini ni warefu sana hata ukikutana nao lazima uchanganyikiwe. Si rahisi kukaa na kuzungumza na jini mdogo wangu" "Je wewe ukimuona jini utamjua?" "Inategemea ila kiukweli nawaogopa majini sitaki hata kukutana nayo nahisi nitakufa kabisa" "Nasikia jini mahaba alifanya uachane na mpenzi wako!" "Ndio, unajua sifa kubwa ya jini mahaba ni wivu. Huyu jini anawivu sana na huwa anataka akumiliki peke yake hivyo atakufanyia visa hadi uachane na unayempenda" "Sasa ulifanyaje wewe ulipogundua unae?" "Nilitafuta mtaalamu, kipindi kile nazunguka sana na Penina tukapata mtaalamu huko mbali, yeye ndio akatusaidia. Kwani unajihisi kuwa na jini mahaba wewe?" "Sielewi dada, maana nimejikuta mambo yangu yakienda sivyo na mpenzi wangu nae nimeachana nae. Basi nisaidie dada yangu, nipeleke kwa huyo mtaalamu" "Hayupo hapa kwa sasa, yupo mkoani ndio anafanyia shughuli zake. Akirudi nitakwambia twende mdogo wangu hata usijari" "Sawa dada, ila ni kweli kabisa huweza kumuona jini?" "Wanatisha mdogo wangu, sio kama sisi tulivyo wao ni viumbe wa ajabu." Nilikuwa nauliza kwa makini huku moyoni mwangu nikipima kuwa Carlos atakuwa ni mtu wa aina gani. Dada aliporudi, tuliaga mahali pale na kurudi nyumbani na giza lilishaingia. Nikiwa nyumbani nikatafakari sana na kuona kuwa yule wa ndotoni atakuwa jini mahaba tu, nikahisi mpaka atakaporudi huyo mtaalamu wa dada Fatuma nitakuwa nishateseka sana na kuolewa na Carlos sikutaka maana sikumuamini na yeye, nilihisi ni mchawi. Nikapata wazo la kwenda kuongea na mama kuhusu mama Semeni maana alisema yupo tayari kunipeleka. Nikamwambia mama kuwa nipo tayari, akafurahi sana na kumpigia mama Semeni simu muda huo huo ambapo akasema nijiandae kesho ili twende. "Ila mwanangu umekuwa mzungu wewe? Viatu umezurula navyo huko na bado upo navyo ndani" Dada akadakia tena, "Kipya kinyemi mama" Sikusema chochote huku nikiamini kuwa majibu ya maswali yangu yote yatapatikana kwa huyo mtaalamu kesho. Nikaenda kuoga ikawa kama asubuhi, nikiwa bafuni navivua na kuoga ila kutoka miguu inauma hadi nivivae. Nikazunguka vile vile na viatu hadi usiku wakati wa kulala ila leo nililala vizuri tu wala sikupatwa na ndoto yoyote ya kutisha hadi panakucha. Asubuhi na mapema, mama Semeni aliwasili nyumbani na kukuta mimi na mama tumeshajiandaa tayari. Safari ikaanza ya kwenda kwa huyo mtaalamu, ilikuwa mbali kweli ila tukavumilia hadi kufika. Ilikuwa ni kibanda cha nyasi, mama na mama Semeni waliingia nikabaki mimi nje kwani kila nikitaka kuingia mtaalamu ananiambia "Vua viatu" Vile viatu muda huu havikutaka kutoka miguuni kabisa, kila nilipojaribu kuvua ilishindikana. Nikamwambia yule mtaalamu, "Havitaki kuvuka" Yule mtaalamu akafanya dawa zake kisha akanifata yeye mwenyewe, akainama na kushika viatu vyangu. Mara gafla akarushwa kamavile mtu aliyepigwa na shoti ya umeme.







    Yule mtaalamu akafanya dawa zake kisha akanifata yeye mwenyewe, akainama na kushika viatu vyangu. Mara gafla akarushwa kamavile mtu aliyepigwa na shoti ya umeme. Akaanguka na kuzirai jambo ambalo lilitushangaza sana. Msaidizi wa mganga alituangalia kwa hasira na kuanza kutufukuza, "Ondokeni, nyie ni watu wabaya sana" Mama Semeni akajaribu kumbembeleza ila ilishindikana, tukaondoka pale na kumuacha yule mganga akiwa vile vile kazimia. Tulitembea njia nzima bila ya kusema chochote hadi tulipofika nyumbani, mama Semeni hakutaka hata kuingia ndani akaondoka huku akimwambia mama. "Hii ni aibu ndugu yangu, mwanao hafai" Nikaingia ndani na kumuacha mama aliyekuwa amemsindikiza kidogo mama Semeni. Baada ya muda kidogo mama akarudi ndani na kuanza kuniuliza, "Hivi hivyo viatu vina nini mwanangu? Kwanini hutaki kuvivua jamani?" "Havitaki kuvuka mama" "Unamaana gani? Si umeletewa na Carlos hivyo!" "Ndio mama ila havitaki kuvuka" "Kwahiyo ukienda kuoga unaogaje?" "Navivua naweka pembeni, nikimaliza kuoga navivaa tena" "Wewe Sabrina ni mwehu sana tena sana, ngoja nimpigie simu huyo Carlos anipe maana ya hivyo viatu ambavyo havivuliki" Mama akajaribu kumpigia Carlos kisha akanipa jibu kuwa hapatikani. Ikabidi kuendelea na mambo mengine tu kwani kilichotakiwa kufanyika kimeshindikana. Dada Penina aliporudi akaanza kumuuliza mama, "Mbona mmewahi sana kurudi? Nilijua sitawakuta" "Mwenzangu kiatu hicho" Huku akinyooshea kidole kwenye kiatu changu, "Kimefanyeje?" "Mwambie akivue" Dada akacheka na kuniangalia kisha akaninyooshea kidole na kuwa kama anataka kuimba na kusema, "Hicho kiatu kivue" Mama nae akacheka huku akitingisha kichwa kama ishara ya kusikitika na kusema, "Kiatu kimetuzulia mambo hicho leo" Dada akatulia kwa makini, kisha mama akaanza kumsimulia kilichotokea leo. "Sasa mganga wa watu anaendeleaje?" "Sijui maana msaidizi wake alitufukuza na kusema......." Nikinuka na kwenda zangu chumbani kwangu na kuwaacha na mazungumzo yao. Nikiwa chumbani nilijitafakarisha sana na kukosa jibu kabisa, sikujielewa hata kidogo. Muda kidogo dada nae akanifata chumbani kwangu na kukaa karibu yangu ili tuzungumze. "Nasikia hicho kiatu uliletewa na Carlos, sasa ukimuuliza kuhusu hayo mauzauza anakwambiaje?" "Carlos hapatikani dada" Dada nae akachukua simu yake kujaribisha kisha akanipa jibu kuwa hapatikani kweli na kusema. "Inamaana kakupa hivyo viatu kwaajili ya kukukomoa au?" "Hata sijui dada" "Ngoja, tutafanya kitu lazima tupate ufumbuzi wa hilo swala" Kisha akatoka na kwenda chumbani kwake. Nikabaki mwenyewe sasa na kuendelea na mawazo yangu. Nikakumbuka tena kuhusu Sam, na roho ya kuhitaji kujua anavyoendelea ilinisumbua sana na kujisemea kuwa lazima nikamtafute. Pia nikakumbuka tena kuhusu Suzy ambaye sijawasiliana nae kabisa tangu siku niliyopata matatizo, nikajaribu kumtafuta ila hakupatikana. Nikajaribu kumtafuta na Sam nione kama nitampata, kwa bahati simu yake ikaita hadi nikashangaa nikatulia kwa makini ila haikupokelewa, nikajaribu tena na tena haikupokelewa nikakata tamaa na kujilaza kwa mawazo. Wakati nimelala nikashtuka kusikia simu yangu inaita, ila nilipotaka kuipokea ikakatika na kugungua kuwa alikuwa anabeep halafu namba ilikuwa ngeni machoni pangu. Nikaamua kumpigia, "Hallow, nani mwenzangu" "Mimi ni Sam" Nikafurahi sana, "Jamani Sam wangu uko wapi?" "Nateseka Sabrina, naumia ila bado nakupenda sana" Machozi yalinidondoka, nilihisi maumivu moyoni mwangu. "Niambie ulipo Sam" Sam hakusema chochote zaidi ya kukata simu, roho ilizidi kuniuma nikajaribu tena kuipiga ile namba lakini haikupatikana. Baada ya muda kidogo nikapokea ujumbe kutoka kwenye ile namba. "Nakupenda Sabrina, haya ni mapito tu ila ipo siku yataisha. Sitaki kukwambia nilipo maana najua utateseka kulijua hilo, ila tambua nakupenda sana na upendo wangu kwako hauwezi kufa kamwe. Nakupenda sana Sabrina" Roho ilizidi kuniuma, nikajaribu tena na tena kuipiga ile namba sikuipata hewani. Nikajiinamia kitandani kwa uchungu nilionao muda huo huku nikijiuliza alipo Sam maana nilitamani kweli kuonana nae. Nikapata wazo la kwenda kwa kina Suzy tena kuangalia hali ya Suzy na kumuuliza alipo Sam ili niende mwenyewe. Wazo la kwenda kwakina Suzy lilikuwa kwa kasi sana na sikutaka kupoteza muda tena, nikatoka chumbani kwangu na kwenda nje bila ya kuaga nikaondoka. Nyumbani hawakuwa na mashaka kuwa naenda mbali, kumbe mwenzao sipo kabisa maeneo ya nyumbani. Kufika kwa wakina Suzy nikamkuta mama yake nje, baada ya salamu akaniambia. "Nakupenda Sabrina ila sitapenda uongozane na mwanangu tena" "Kwanini mama?" "Hakuna cha kwanini, fanya nilichosema.Namaanisha uondoke hapa kwangu, matatizo unayompatia mwanangu yanatosha kwa sasa" "Lakini mama....." "Hakuna cha lakini Sabrina, nilikuamini sana na kukuona kuwa ni mtoto mwema na mzuri, sikujua kama wewe ni mtoto mbaya kiasi hiki" "Ila sijui kosa langu mama!" "Nishakwambia, sitaki kukuona ukiongozana tena na mwanangu Suzy" "Sawa mama, ila ningependa kumuuliza Suzy jambo moja" "Niulize mimi nitakujibu" "Samahani mama, naulizia mahali ambapo Sam amepelekwa" "Nenda kituo cha kati" "Ndio kipi hiko?" Akanipa maelekezo na kusema kuwa niondoke. Niliondoka bila ya kujua nini kosa langu hadi mama Suzy kunichukia. Nikafika kituo cha polisi na kuwaomba kuzungumza na Sam, mwanzoni walinikatalia ila baada ya kuwaomba sana wakaniruhusu kuongea nae. Wakamuita Sam aliyekuwa amekonda sana, roho ikaniuma na kuhisi kuwa kama Sam ataendelea kuwekwa kwenye kile kichumba cha giza atakufa. Niliona machozi yakinitiririka, Sam alinikumbatia akilia huku akiniambia nikaze moyo. "Ila ni mimi Sam ninayestahili hukumu hii" "Sioni tatizo kuteseka kwaajili yako Sabrina, najua hii ni njia mojawapo ya kuniamini jinsi ninavyokupenda" "Sam nahitaji kukusaidia" "Ila usijitoe thamani yako kwaajili yangu, haya ni mapito tu" "Ila mbona wewe umeitoa thamani yako kwaajili yangu? Lazima na mimi nijitoe Sam" "Usifanye hivyo tafadhari utaniumiza zaidi, napata ndoto mbaya sana juu yako. Halafu nasikia ulimsukuma Suzy toka ndani ya gari na....." Askari akakatisha mazungumzo yetu na kusema muda umekwisha halafu akamchukua Sam na kumrudisha rumande, nililia sana huku nikijiuliza maswali mengi bila ya majibu. Kwanini inakuwa hivi kwangu, maana hata Suzy sikujua nilichomfanya na huko kumsukuma nilimsukuma muda gani? Kwakweli mengi nilisingiziwa na kuchukiwa na watu walionizunguka tu. Sikuwa na jinsi zaidi ya kurudi nyumbani. Kufika ndani nikajua nitapata lawama nyingi sana kutoka kwa mama sababu nimeondoka bila kuaga na niliporudi giza lilishaingia. Nilimkuta mama sebleni ila hakuniuliza chochote kuhusu kutoka kwangu, nilikaa kwa kusitasita mama akasema. "Na wewe mwanangu unalala sana, sijui hata usiku utalala usingizi gani" Nikastaajabu sana, yani muda wote ule niliotoka mama anajua nimelala ndani! Au kuna Sabrina mwingine ndani kwetu? Nikajiuliza na kukosa jibu ila kumuuliza mama nikashindwa, kisha nikainuka na kwenda chumbani. Nilipakuta vilevile kama nilivyopaacha, muda kidogo dada akaja chumbani kwangu. "Khee ushaamka?" "Kwani ulikuja muda gani ambao ukaniona nimelala?" "Muda sio mrefu nilikuja chumbani kwako nikakukuta umelala, tena hoi kabisa ila bora umeamka twende ukanisaidie kitu chumbani kwangu" Nikashangaa tu kuona kuwa wote ndani walijua nimelala, kisha nikainuka na kufatana na dada hadi chumbani kwake. "Ile picha imerudi tena kwenye kompyuta yangu, niondolee Sabrina" Nikakaa na kuiangalia kwa makini na kugundua kuwa ni ileile picha ya kijana wa ndotoni ila dada huwa anaitoa wapi? Wakati najiuliza ile picha ikatabasamu, nikashtuka na kuacha kufanya ninachofanya huku nikimshtua dada nae aweze kuona. Ila dada alipoangalia nae akatabasamu na kusema. "Asante Sabrina kwa kunitolea ile picha maana ilikuwa inanikera sana" Nikashindwa cha kusema sababu ile picha sikuweza kuitoa lakini ilitoka yenyewe. "Ila dada huwa unaitoa wapi hiyo picha?" "Sijui, labda kwenye mitandao hii mdogo wangu maana hata sijui ilipotoka kwakweli" Nikaachana na dada pale na kwenda sebleni kuzungumza na mama aliyekuwa akiniita. "Nasikia kuna tukio ulifanya majuzi" "Tukio gani tena?" "Ulivyonidanganya hapa nyumbani kumbe ulienda kwa kina Suzy, haya kilichokufanya umsukume mwenzio kutoka kwenye gari ni nini?" "Sijamsukuma Suzy mama na siwezi kufanya hivyo" "Shauri yako, utaua wenzio wewe. Lucy umempiga sababu ya mwanaume, Suzy umemsukuma bila sababu. Sina pesa ya kusimamia kesi zako mie, shauri yako" Kwakweli lawama kuhusu Suzy iliniuma sana, hata kuhusu Lucy niliumia pia ukizingatia Sam anateseka rumande kwaajili yangu. Sikuwa hata na hamu ya kula leo kwani matatizo yalikuwa mengi na kunikosesha raha kabisa, niliamua kwenda kulala tu. "Huli leo?" "Nimeshiba mama" "Njoo ule kidogo mwanangu" Dada akadakia, "Si ameshasema kuwa kashiba! Mwache akalale tena tu maana chakula chake kinapatikana usingizini" Huku akicheka nami nikaingia chumbani kwangu. Kwakweli nilikuwa nimechoka sana kwahiyo haikuchukua muda sana nikawa nimelala tayari. Wakati nipo usingizini, akatokea yule mkaka wa ndotoni na sahani ya chakula mkononi akanipa nile nami nikala chakula chote kisha akaanza kusema. "Asante kwa kula chakula changu Sabrina, nakupenda sana ndiomana nakujali. Si unaona leo umeondoka kwenu bila kuaga ila nyumbani kwenu hawakujua sababu nilikuja mimi na kulala kwenye kitanda chako kwahiyo wakajua ni wewe. Nimekuepushia lawama Sabrina sababu nakupenda. Nielewe Sabrina na ukubali kuolewa na mimi" Nilikuwa kimya kabisa nikimsikiliza, mara akasema. "Naomba busu lako Sabrina" Nikashtuka toka usingizini, nikakuta picha kitandani kwangu kuangalia ni ya yule kijana wa ndotoni nikaanza kuogopa na kuitupa. Nikasikia sauti, "Usiogope Sabrina siwezi kukudhuru" Huku nikitetemeka, nikamuuliza. "Wewe ni nani kwani?" "Mimi ni jini" Nilitamani nisingesikia hiyo kauli kuwa yeye ni jini kwani niliogopa sana na kutetemeka, aliendelea kuongea. "Naweza fanya chochote nitakacho ila sitaki kukuumiza, nataka ukubali kwa hiyari yako kuolewa na mimi" Ile sauti ilikuwa inaniogopesha sana, nikakimbilia mlango ili niweze kutoka lakini haukufunguka na kufanya uoga unizidi. Gafla sauti ile ikatoweka na kujikuta nikihema kwa nguvu sana kama mtu niliyekimbia sana. Nikatulia sasa huku uoga nao ukiendelea kunitawala, gafla nikasikia sauti ikipiga kama mwangwi na kusema, "Carlos, Carlos, Carlos" Nikajikuta nikilia kwa nguvu sana ila hakuna aliyenisikia, halafu nikapitiwa na usingizi pale pale mlangoni. Kulipokucha nilijikuta kitandani ila sikujua ni nani aliyeniweka kitandani. Nikaamka na kupatwa na wazo moja tu kwenda kumtazama Lucy ili niwaambie wazazi wake kama mimi ndio nahusika na wamuachie Sam wangu huru bora nikafungwe mimi mwenyewe muhusika wa yote. Nikaoga na kujiandaa kisha nikatoka bila hata ya kumuaga mama kwani najua atanikataza tu. Safari ilikuwa moja kwa moja kwakina Lucy, kufika pale mama yake alinikaribisha vizuri sana. "Umekuja kumuona mwenzio, karibu sana" "Asante mama" "Za tangu juzi?" Nikashangaa kuwa hiyo juzi ni juzi gani wakati nina miezi sijafika kwakina Lucy, na mara ya mwisho ilikuwa ni siku niliyoenda na Suzy halafu Lucy akaja na Sam basi. Sasa hiyo juzi anayoisema huyu mama ni juzi gani? Ikabidi niitikie kwa kujigelesha, "Nzuri tu mama" "Mwenzio yupo ndani na yule daktari uliyetuletea, kwakweli anaendelea vizuri sana tunashukuru kwa hilo" Hapo ndio akazidi kunichanganya kabisa yani maana sikumjua huyo daktari anayemuongelea na je ni muda gani niliompeleka huyo daktari? Sikujua kwakweli, nikawa nimeduwaa ila mama Lucy akaniambia niingie ndani baada ya kuona nimesimama tu pale nje. "Ingia tu, nenda moja kwa moja chumbani kwake utamkuta na mdogo wake Maria yupo huko huko" Nikaongoza hadi chumba cha Lucy, nikapishana na Maria mlangoni ambaye alinifurahia na kunikaribisha ndani halafu yeye akatoka. Nikaingia mule chumbani na kumuona Lucy amelala kwenye kitanda halafu mtu mwingine mwenye koti la kidaktari akiwa amesimama na kumpimapima, nikasogea hadi pale. Yule daktari akaniangalia, nikashtuka sana kwani alikuwa ni Carlos.







    Yule daktari akaniangalia, nikashtuka sana kwani alikuwa ni Carlos. Nikashangaa kuwa Carlos ni daktari tokea lini? Na vipi waseme kuwa nimemleta mimi? Nikawa namuangalia Carlos kwa uoga, nikatamani kupiga makelele ila nikashindwa kwani mdomo wangu ulikuwa mzito kupiga kelele. Nikajikuta nikimuuliza tu, "Wewe Carlos umeanza lini kuwa daktari?" Maria nae akarudi muda huo huo mule ndani na kuongea na mimi, "Huyu dokta wako ametusaidia sana dada Sabrina, maana dada Lucy anaweza hata kukaa na kula kwasasa tofauti na mwanzoni. Kwakweli tunakushukuru sana maana hapo amebakiza kurudisha kumbukumbu tu" Carlos akamuangalia Maria akitabasamu na kusema. "Msijali, kumbukumbu zake zitarudi tu" Kisha akaaga na kuondoka, Lucy alikuwa amelala kwasasa. Mama Lucy naye akaingia wakati Carlos akiondoka na kuendelea kumshukuru kwa sana Carlos huku akimsindikiza. Nilibaki pale na Maria bila ya kujua cha kusema wala cha kujielezea, je ni nani atanielewa? Sikujua kabisa. Muda kidogo mama Lucy alikuja mule ndani na kuniambia, "Daktari anakuita hapo nje Sabrina" Sikuwa na la kufanya zaidi ya kutoka na kwenda kumsikiliza Carlos, cha kushangaza leo vile viatu niliingia navyo hadi ndani kwa kina Lucy ila mama Lucy hakushangazwa wala kuniuliza. Nikamfata Carlos pale nje na kumwambia. "Nimekuja kukusikiliza Carlos halafu nina maswali yangu kadhaa nataka kukuuliza" "Najua kama una maswali ndiomana nikakuita" "Sasa nianze kukuuliza?" "Hapana, nenda ukaage halafu twende mahali ukaniulize" Nikarudi ndani kwa wakina Lucy na kumuaga mama Lucy kisha nikaondoka na Carlos, akanipeleka mahali ambako pametulia sana kisha kabla ya kumuuliza akaanza yeye kuniuliza. "Unampenda Sam?" "Ndio nampenda" "Kama unampenda basi hutopenda kuona anateseka si ndio?" "Ndio, roho inaniuma sana kuona Sam wangu anateseka vile" "Uhuru wa Sam unao wewe, unatakiwa kuamua moja kama unapenda Sam awe huru hata leo" "Natakiwa kuamua lipi?" "Suluhisho ni kukubali kuolewa na mimi" "Siwezi Carlos siwezi, kwanza sikuamini kama wewe ni mwanadamu" "Sasa mimi ni nani?" Nikajibu kumwambia kuwa yeye ni jini ila mdomo wangu ukasita na kusema, "Sijui tu" "Na kwanini sasa useme kuwa mimi sio binadamu?" "Hueleweki Carlos hata wazazi sijui kama unao" "Nia yako ni kuwaona wazazi wangu kumbe!! Nikupeleke sasa hivi?" Nikasita, kwani nikikumbuka zile stori kuhusu majini nikahofia ikinitokea mimi. "Naona unashaka na mimi, basi nitawaleta wazazi wangu nyumbani kwenu" "Eeh na huyo Sam atatokaje?" "Nimekwambia kuwa unatakiwa kukubali kuolewa na mimi halafu Sam atakuwa huru hata sasa" "Kweli?" "Sina tabia ya kudanganya" "Sawa basi niko tayari, mwachie Sam huru" "Upo tayari kweli Sabrina?" "Ndio, nipo tayari kwaajili ya Sam" "Utapata majibu yako muda mfupi ujao" "Haya niambie na hivi viatu ambavyo umenipa mbona ni vya ajabu" "Tatizo lake ni nini kwani?" "Havitaki kuvuka" "Kweli havitaki kuvuka Sabrina?" "Ndio havitaki kabisa" "Hebu tuone" Nikainua mguu wa kwanza, Carlos akanivua kile kiatu kwenye ule mguu na kuniuliza. "Unajisikiaje?" "Najisikia vizuri tu" "Nipe na huo mguu mwingine" Nikauinua na kumwekea nao akanivua, kabla hajasema chochote nilijishtukia nipo nyumbani. Tena kitandani nimekaa, nikajitazama miguuni vile viatu havikuwepo tena. Akaja mama chumbani, "Leo unaamka na kulala, unaamka na kulala sijui una matatizo gani mwanangu?" Nikamuangalia tu mama na kuinuka, nikatoka hadi sebleni ili kujiona kama kweli nipo macho au nimelala maana sikujielewa kabisa, ilikuwa kama ndoto vile lakini ilikuwa ni kweli yani sikuamini kabisa haya mambo kwakweli. Jioni nikiwa nimekaa na mama sebleni akaanza kuniuliza, "Mbona viatu ulivyosema havivuki leo umevua?" "Ni Carlos huyo mama" "Carlos kafanyaje?" Mara akaingia dada Penina ndani na kukatisha mazungumzo yetu. "Kuna mgeni wako nje Sabrina" "Nani huyo?" "Toka ukamuangalie" Nikatoka hadi nje na kukuta mgeni wangu ni Sam, niliruka na kumkumbatia kwa furaha. Kwakweli nilifurahi sana kumuona Sam wangu tena akiwa huru kabisa. Sam nae alinikumbatia huku akisema, "Nipo huru mpenzi wangu Sabrina, nipo huru sasa" Nilimkumbatia zaidi na kumkaribisha ndani ila Sam alikataa na kusema ni bora tukae palepale nje, nikaona haina tatizo. Nikaenda ndani kutoa viti kisha kukaa na Sam ili tuzungumze yaliyojiri. "Kwanza kabisa nimefurahi sana kukuona Sam wangu upo huru. Umetolewa lini kwani?" "Leo leo, alikuja baba Lucy kunitoa. Nilipofika nyumbani sikukaa sana nikaona nije kukushukuru" "Embu kwanza niambie, ilikuwaje hadi ukashikiliwa wewe wakati muhusika ni mimi?" "Kwanza hata mimi mwenyewe nashangaa, unajua lile tendo lilikuwa la kushtukiza sana. Yani muda huo huo umempiga Lucy kwa chupa watu wengi wakajaa eneo lile, mara wakaja mapolisi halafu watu wote wa pale wakasema kuwa wameniona mimi nikimpiga Lucy ngumi kisha kumponda kwa chupa. Kwakweli ni jambo la kushangaza sana, kisha nikakamatwa na kupelekwa polisi yani haikuchukua muda wakafika ndugu wa Lucy na kusema nikae ndani hadi nishike adabu na si unajua tena wakina Lucy wana hela! Basi wakatumia pesa yao hata dhamana nikakataliwa" "Sasa wewe hukuwaambia kama huhusiki?" "Nani angenisikia na kunielewa Sabrina? Wakati watu wote pale wamesema kuwa wameshuhudia mimi nikifanya hivyo. Yani wewe hukutajwa kabisa kamavile mtu ambaye hukuwepo kabisa eneo la tukio" Nikaishia kuguna maana mambo ni ya ajabu sana, Sam akaendelea kunielezea "Ndugu zangu niliwaambia ukweli, wakaniomba sana nieleze kwa maaskari ukweli huo ila sikutaka kwamaana ningekuangamiza wewe wakati nakupenda siku zote" "Pole sana Sam" "Asante, ila cha muhimu nipo huru kwasasa. Asante sana Sabrina" "Asante ya nini sasa?" "Ya kunisaidia kutoka jela" Hapo nikashangaa sasa na kuuliza, "Nimekusaidiaje kwani?" "Baba Lucy alipokuja kunitoa akasema amefanya hivyo sababu yako. Eeh na huyo Lucy anaendeleaje?" Kwanza nilikuwa nikijiuliza maswali maana sikuelewa, huyo baba Lucy nimeonana nae muda gani hadi kuongea kuhusu Sam? Hapo maswali yakanichanganya kwakweli. Sam akanistua kwenye hayo mawazo. "Mbona hunijibu Sabrina au bado una hasira kuhusu Lucy?" "Hapana Sam, Lucy anaendelea vizuri na wala sina hasira nae tena" "Sasa mbona upo hivyo? Hujafurahi kutoka kwangu mpenzi?" "Nimefurahi sana, hii ni furaha iliyopitiliza" Halafu tukaendelea na maongezi pale nje, mara mama akatoka ndani na kunikuta na Sam pale nje nikajua atafoka sana lakini alikuwa tofauti sana leo. Kwani aliposalimiwa na Sam akaitikia vizuri sana hadi tukashangaa, kisha akasema, "Mbona umeishia na mgeni hapo nje Sabrina? Hebu ingia nae ndani" Sam akajibu kuwa pale nje panatosha. Tukaendelea na maongezi pale mara mvua ikaanza kunyesha ikabidi tukimbilie ndani na giza nalo lilishaanza kuingia. Nikatamani hata kumkumbatia Sam ila tatizo tulikuwa nyumbani. Kwenye mida ya saa tatu usiku ndio ile mvua ikakatika na hali kuwa shwari, Sam nae akaaga. Dada akaniambia kuwa tumsindikize Sam kituoni. Kufika kituoni, Sam akapata gari muda uleule. Wakati tunarudi nyumbani tukakutana na gari ya Carlos, ikapita mbele yetu. Dada akaisimamisha lakini haikusimama, dada akaniuliza "Si Carlos yule?" "Ndio ni yeye" "Mbona hajasimama sasa au umegombana nae?" "Hapana" Kabla hatujafika nyumbani mvua ikaanza tena ikabidi tujibanze mahali ili ipungue kidogo ila ile mvua haikupungua iliendelea kunyesha tu na radi kupiga, mimi na dada tukaanza kuogopa kwani umeme ulikatika muda huohuo baada ya mvua kuwa kali sana, hatukuwa na la kufanya zaidi ya kumkumbatia dada tu na kwa uoga nilionao nikaanza kulia maana tulikuwa tumesimama kwenye ubaraza tu wa duka ambalo lilikuwa limefungwa. "Tuondoke dada" "Tutaondokaje? Ngoja ipite gari tuombe lifti" Mara gari ya Carlos ikapita tena, dada akaisimamisha, ikasimama na tukapanda. Dada akaanza kumuuliza, "Mbona mwanzo umepita kama hutuoni?" "Sikuwaona kweli ndiomana nikapita" Basi Carlos akatufikisha nyumbani, kisha akamnong'oneza kitu dada ambapo sikuelewa ni kitu gani. Kisha akanifata mimi kuniaga na kusema. "Msaada wangu kwako wewe hauepukiki na huwezi ukastahimili bila kuhitaji msaada wangu, hili la leo ni somo tu" Kisha akaondoka zake na kuniacha na msongo wa mawazo ila leo hakuingia ndani kwetu. Kwavile muda ulikuwa umeenda ikabidi twende kulala tu maana chakula tulishakula, na umeme ukarudi muda huo huo ambao tulikuwa tukijiandaa kulala. Usiku wakati nimelala nikajiona nipo mahali halafu karibu yake kuna bonde kubwa sana tena la kutisha, uoga ukanijaa kulitazama. Kuangalia upande wa pili wa bonde nikamuona Sam akiwa amefungwa kamba mwili mzima, nikatamani kwenda kumfungua ila nitamfunguaje wakati kuna bonde kati yetu. Nikaanza kuhangaika pale kwa lengo la kumsaidia Sam ila ikaahindikana, pembeni yangu akatokea yule kijana wa ndotoni huku akitabasamu na kusema, "Najua huwezi fanya chochote Sabrina bila ya msaada wangu, unahitaji msaada niambie nikusaidie" Nikamwambia, "Nisaidie kumuokoa Sam" Akanyoosha mkono kisha Sam akaletwa karibu yangu na kusema "Nimemuokoa tayari Sabrina, sasa wewe ni wangu" "Hapana mimi si wako" "Wewe ni wangu Sabrina na lazima nitakuoa na utakuwa mke wangu" "Siwezi kuolewa na wewe siwezi kuolewa na jini kamwe" Akacheka sana, nikamuangalia tu na kuongea maneno mengimengi maana leo niliachiwa kuongea. "Hivi karibuni nitakuja kukuvisha pete ya uchumba kwahiyo jiandae mpenzi" "Sitaki nimesema sitaki na siwezi kuolewa na wewe" Nikashtuka toka usingizini na kukuta giza limetanda chumbani wangu kumbe umeme ulikatika, na hapo ndipo uoga ukanijaa kwa lile giza. Mara nikasikia mtu akicheka sana kwenye chumba changu, uoga ukanijaa na kujikuta nikiuliza na Leo. "Wewe ni nani?" Sauti ikaaikika, "Unataka kila siku nijitambulishe?" Nikabaki kimya nikitetemeka, kisha akacheka tena na kusema "Mimi ni jini" Kwakweli hili neno la jini lilikuwa linanitisha sana ukizingatia umeme umekatika Leo basi nikazidi kutetemeka. Mara nikasikia kama mtu akinikuna mgongoni hapo nikashtuka sana na kutetemeka. Nikaogopa kuongea chochote huku moyo wangu ukiwa umejaa hofu tupu, muda huo huo umeme ukarudi ikawa bora kwangu maana ningekufa kwa presha ya giza. Ile hali ya kukunwa mgongoni ikatoweka muda huo, nikajipanga kwenda kumalizia usingizi kwa mama lakini kabla sikainuka nikapatwa na usingizi pale pale na kulala. Kulipokucha alikuja mama kuniamsha, "Kheee umelala sana mwanangu hebu amka kuna kazi nyingi Leo" Nikaamka na kujiandaa kwa hizo kazi, Kisha nikamfata mama anipangie. "Unajua hatujafua siku nyingi sana na nguo chafu zimejaa, angalia pale" Akanionyesha, kulikuwa na furushi la nguo chafu na hapo nikakumbuka kuwa tuna wiki kama tatu hatujafua. "Mmmh mama tutamaliza leo kweli?" "Tutamaliza tu mwanangu ila ndio tutafua siku nzima" Mama akatoa zile nguo zote nje na kuniambia mimi nianze kufua wakati yeye anamalizia kupika ili tukimaliza kufua tule. "Uwe unafua hapo, nikimaliza tu nakuja tusaidiane" Kwakweli nguo zilikuwa nyingi sana maana ni nguo za familia nzima. Wakati naanza kufua nikasikia sauti, "Nikusaidie kufua Sabrina?" Kabla sijajibu chochote nikashangaa ndani ya dakika mbili nguo zote zimeanikwa kwenye kamba na pale chini hapakuwa na nguo tena. Nikaogopa sana na kukimbilia ndani, mama akanishangaa na kuniuliza. "Vipi mbona umeacha kufua na kukimbilia ndani?" Nilikuwa kimya nikitetemeka, mama akachungulia dirishani, na kuuliza kwa mshangao "Inamaana umemaliza kufua Sabrina??" Mama hakuamini akaenda nje kuangalia, Mara sauti ikaniambia tena "Au nizikaushe kabisa na kuzikunja?" Nikaanza kutetemeka sasa.



    Mama hakuamini akaenda nje kuangalia, mara sauti ikaniambia tena "Au nizikaushe kabisa na kuzikunja?" Nikaanza kutetemeka sasa bila ya kujua cha kusema, ile sauti ikajirudia tena nikajikuta nikisema kwa nguvu "Hapana" Kwani najua yale maajabu ya zaidi sasa yatamuogopesha hata mama. Mara mama nae akarudi ndani na kuniuliza vizuri, "Hivi zile nguo Sabrina umefua au umezianika tu? Na hata kama kuanika tu ndio ndani ya dakika mbili kweli?" Nilikaa kimya nikimtazama mama aliyeendelea kuongea "Hata kama maajaabu hii ni too much jamani, kwakweli kwa mtindo huu basi hata watu hawana haja ya kununua mashine za kufulia, kwakweli Sabrina leo umenipa kali ya mwaka yani umenitoa jasho kabisa. Hivi nilizaa mtu au kitu gani jamani!" Nikatulia kimya kamavile sio mimi ninayeambiwa kuwa mtoto wa ajabu kwani hata cha kumuelezea mama sikuwa nacho, mama nae hakuacha kuongea najua sababu ya kutojielewa hata yeye pia. "Kwakweli leo Sabrina umefanya nibaki mdomo wazi maana hata cha kusema nakosa, hebu nikuulize kitu" "Niulize mama" "Wewe una majini au umekuwa mchawi mwanangu?" "Kwanini mama?" Mama akawa mkali kweli leo, "Usiniulize kwanini wakati unafanya mambo ya ajabu, usiku unaogopa unaogopa kumbe unawaogopa wenzio wanaoruka angani huko. Haya niambie uchawi umeutoa wapi?" "Ila mimi sio mchawi mama" "Kama sio mchawi umewezaje kufua zile nguo zote kwa dakika mbili? Umewezaje Sabrina?" "Sio mimi mama" "Kwahiyo ni nani?" "Sijui mama" "Si unaona ushetani wako, eti hujui! Kwakweli leo umenimaliza Sabrina" Mama akakaa chini kama mtu aliyechoka sana, sikuwa na la kufanya kwani hata mie ile hali ilinitesa sana na machozi kunitoka tu, mama hakutaka kabisa kuamini chochote nilichomueleza na kufanya nizidi kupatwa na mawazo. Mchana ulipofika dada alikuwa amesha wasili nyumbani na kufanya tushangae kilichomuwahisha na leo. Mama akaanza kumuuliza, "Vipi mbona umewahi sana leo?" "Fatuma alikuwa na matatizo kwahiyo tukaomba ruhusa na kuondoka" "Matatizo gani tena? Yale yale ya jini mahaba au?" "Mmh matatizo mengine tu, inabidi kesho nimsindikize tena kwa mtaalamu wake" "Ukienda uende na huyo" Akininyooshea mimi kidole, "Kwanini mama?" "Hebu angalia nyuma huko nikupe sababu" Dada akachungulia dirishani, "Khee mmefua nguo zote zile? Poleni sana" "Pole mpe huyo mashine ya kufua kwa dakika mbili" Huku akimuonyeshea kwangu, "Kivipi mama?" "Mdogo wako ana mashine ya kufulia kwenye mikono hata nguo ziwe zingi vipi zitafuliwa kwa dakika mbili tu" Dada akawa anashangaa tu kwamaana hakuelewa chochope, hapo ndipo mama akaamua kumueleza jinsi ilivyokuwa. "Mmh mama ya kweli haya? Yani ndani ya dakika mbili?" "Yani kufumba na kufumbua mwanangu nguo zote zimefuliwa na kuanikwa, kwakweli leo Sabrina kanipa kali ya mwaka yani sikufikiria kabisa" "Sasa mama huko kwa mganga ataenda kutibiwa nini?" "Chochote tu ilimradi nimpate Sabrina wangu wa ukweli maana mimi naona kama vile nimebadilishiwa mtoto jamani" "Usijali mama nitaenda nae" Dada aliniangalia tu ila hakuniuliza kitu chochote kile kuhusu nguo wala nini. Nami nikatulia tu bila ya kujua cha kufanya. Jioni yake nilienda chumbani kwangu kupumzika maana mawazo nayo yalikuwa ni mengi sana tena bila ya uelekeo wa maana, nilihisi kamavile naanza kutengwa na dunia. Simu yangu ikaingia ujumbe mfupi, ulikuwa umetoka kwa wifi yangu Joy. "Napenda kukusaidia Sabrina ila nasindwa sababu ya siri yangu, ikitoka nitaumbuka sana mdogo wangu" Nikatamani kupata huo msaada wa wifi Joy ila je atanisaidiaje wakati kasema kuwa ameshindwa, nikatunga sheria zangu na kuamua tena kutoka pale nyumbani nia yangu ni kukutana na Sam labda nimueleze yeye atanisikia. Nikampigia simu Sam, "Nataka kuonana na wewe Sam" "Basi acha nije kwenu" "Hapana, sitaki kwenu wala kwetu. Nataka tukutane mahali" Nikapanga mahali pa kuonana na Sam kisha nikaondoka nyumbani bila kuaga kwani hata nikiaga haina maana kwasasa. Nikiwa njiani kuelekea ambapo nimepanga kukutana na Sam, nikashtuliwa na mtu kwa kushikwa bega. Nikageuka kumwangalia ni nani, kumbe alikuwa ni dada Salome. Kisha akaniambia, "Yani hapa nilikuwa nabahatisha tu kukushika ili nijue kama ni wewe" "Kwanini dada?" "Sijui siku hizi mpo wawili au ni wewe mwenyewe" "Mmh dada kwanini?" "Nimekutana na Sabrina mwengine muda sio mrefu, kavaa gauni la pinki na viatu virefu" Nikamwambia anielekeze hivyo viatu, aliponielekeza nikagundua kuwa ndio vile viatu nilivyopewa na Carlos na aliponivua nilijikuta nikiwa nyumbani, iweje sasa nionekane na hivyo viatu? Nikamuuliza, "Je uliongea na huyo Sabrina?" "Ndio, inamaana sio wewe niliyekutana nae? Basi mpo wawili maana nilitaka kukuuliza hapa kuwa umerudi muda gani kwenu na kubadilisha nguo hadi sasa uko hapa!" Nikabaki kimya maana hata cha kuongezea nilikosa yani nimeanza kuonekana mara mbili mbili basi ni maajabu kwakweli. Nikaagana na dada Salome na kuendelea na safari yangu. Nilipofika nikamkuta Sam ameshafika tayari, "Khee, umewahi sana Sam" "Ndio lazima niwahi kwaajili yako" "Ila mbona kama una mashaka sana?" "Hapana Sabrina nipo kawaida tu" "Ila kutoka kule kwenu hadi hapa ni mbali sana, sikujua kama ningekukuta" "Leo nimepata usafiri wa haraka sana Sabrina, nimekuja kukusikiliza mpenzi" Nikaanza kumueleza matatizo niliyo nayo na mambo yote ninayokumbana nayo kila siku haswa hili la leo kuhusu nguo, kisha akaniuliza "Kilichokushtua zaidi ni nini?" "Kilichonishtua zaidi ni kuhusu nguo mpenzi wangu" "Sasa wewe Sabrina huoni raha hiyo? Yani unaweka tu nguo ndani ya dakika mbili zote zimefuliwa na kuanikwa, hiyo itatusaidia kwenye maisha yetu tunaweza hata kufungua kampuni na kula pesa za ufuaji tu" "Acha masikhara Sam, yani unaona ni kitu cha kawaida hiki mpenzi?" "Sijaona tatizo bado, naona kawaida tu kwani itatusaidia badae" "Na haya mauzauza ninayokumbana nayo je?" "Mbona sioni tatizo Sabrina! Usikuze mambo bhana, hivyo ni vitu vya kawaida tu ila punguza uoga" Majibu ya Sam leo yalinichanganya sana na kunipa maswali kuwa mbona kabadilika sana au kwasababu ya kukaa rumande! Sam wa leo alinichanganya sana maana kila nilichoongea alinipanga hadi kufanya nijute kuja kuonana na Sam na kumuelezea matatizo yangu, nikaamua kumuaga kuwa narudi nyumbani. "Poa safari njema" "Mbona umebadilika sana Sam! Yani hata kunisindikiza kidogo?" "Me sijisikii kutoka hapa muda huu kwakweli" "Kwahiyo utaondoka muda gani?" "Muda nitakaopenda mimi" Sikutaka kuendelea kubishana nae zaidi na kuamua kurudi tu nyumbani maana Sam alishanikera. Kufika tu nyumbani nikakumbana na maswali toka kwa mama, "Eeh umetoka wapi muda huu?" "Nimetoka hapo tu mama" "Kwahiyo umeanza kuondoka hapa nyumbani bila ya kuaga?" "Hapana mama, nisamehe" "Au ndio unataka kunionyesha uwezo wako wa kufua nguo kwa dakika mbili? Mbona umekuwa hivyo Sabrina? Hukuwa hivyo mwanangu, umebadilika sana" "Nisamehe mama" "Nisamehe ya kila mara haina nguvu, mtu gani wewe muda wote unafanya mauza uza halafu unaona kuomba msamaha ndio dili, kwakweli sipendezewi na tabia yako ya sasa Sabrina mwanangu" Nikaingia ndani tu huku mawazo yakinitawala kwani hadi familia yangu imeanza kunichukia kwa haya mauzauza ambayo nakumbana nayo. Muda wa kula ukafika, nikala na kwenda kulala chumbani kwangu maana najua hata mama hawezi kukubali kulala na mimi tena. Nikiwa chumbani kwangu, nikajaribu kupiga simu kwa Sam ili nione kama amesharudi kwao ila simu yake haikupokelewa nikaona Sam ananifanyia makusudi ukizingatia na majibu ya leo aliyonipa nikadhani Sam atakuwa amenichoka tu ila sikuwa na la kufanya kwavile bado nampenda sana tena sana. Usingizi ukanipitia wakati nipo kwenye mawazo. Nikiwa kwenye ndoto, nikamuona yule kijana wa ndotoni akija mbele yangu kwa tabasamu kali sana huku akisema, "Nimekukomesha leo Sabrina" Halafu nikawa kama naangalia video vile, nikamuona yule kijana wa ndotoni akitembea halafu mbele kidogo akajigeuza na kuwa Sam kisha akaja kukutana na mimi, akanipa mkono kumsalimia kisha akaanza kucheka na sura yake ikabadilika tena na kuwa kijana wa ndotoni akacheka na kusema, "Umeona Sabrina! Naweza fanya chochote nitakacho" Nikashtuka toka usingizini huku nikihema kwa nguvu sana kwa uoga wa ile ndoto. Nikajiuliza, inamaana niliyekutana nae leo sio Sam? Moyo wangu ukaniambia kuwa inawezekana ni kweli kwamba niliyekutana nae si Sam. Nikachukua tena simu yangu na kumpigia Sam ili kupata uhakika, iliita bila kupokelewa ila nilipopiga tena Sam alipokea na kuongea kiusingizi; "Mbona usiku sana Sabrina?" "Eti leo tumekutana wapi?" "Maeneo ya kwetu huku umesahau?" "Hebu nikumbushe nilivaeje?" "Mmh nawe Sabrina mbona una vituko, maswali gani hayo ya kuulizana usiku huu? Mi nina usingizi bhana, usiku mwema. Nakupenda" Akakata simu ila mimi bado nilihitaji kujua ukweli kwani hata mahali pa kukutana aliposema Sam sio penyewe, nikaamua kumpigia simu tena ili kumuuliza vizuri. "Samahani mpenzi wangu Sam, naomba unijibu" "Ulivaa gauni la pinki na viatu virefu" Hapo nikashtuka sana, nikakumbuka nilivyoambiwa na dada Lucy kuwa ameniona nimevaa hivyo kwakweli nilishangaa sana kuwa kweli kuna Sabrina wawili. Sam akanistua, "Vipi Sabrina, una tatizo gani kwani maana hata ulipokuja kuonana na mimi haukuwa sawa kabisa" "Kwani mimi nilikwambia tuonane wapi mwanzoni?" "Mwanzoni ulisema pale tulipokuwa tunakutana zamani ila badae ukanipigia simu na kusema unakuja mitaa ya kwetu huku, umesahau Sabrina! Tena uliwahi kweli kabla yangu hadi nikakuuliza kuwa umepaa nini. Umesahau?" "Basi Sam, tutaongea kesho" Nikakata simu na kubaki na mawazo kichwani na sikuelewa pa kuanzia wala kuishia. Gafla nikaitwa, "Sabrina" Nikashtuka sana nusu ya kuzimia kabisa jinsi nilivyoshtuka kumbe alikuwa mama ananiita, nikatoka chumbani kwangu na kumfata sebleni. "Mbona usiku mama?" "Usiku wa kikwenu huu? Ni alfajiri sasa, amka ujiandae maana unapoenda na dada yako ni mbali, Mwende mkayawahi yale mabasi ya asubuhi ya mikoani ili muwahi kurudi" Sikubisha, nikajiandaa kila kitu kwaajili ya hiyo safari. Dada nae alipomaliza kujiandaa, tukawa tayari kwa kuondoka. Mama akaniita tena kabla ya kuondoka, "Hebu nikuangalie kwanza isije kuwa na leo umevaa yale maviatu yako ya kichawi" Akaniangalia sana, aliporidhika akaniruhusu kuondoka na dada. Tukaenda moja kwa moja hadi anapoishi dada Fatuma, tukamkuta nae ameshajiandaa na kuendelea na safari. Kufika njiani tulikutana na Carlos aliyetupa lifti hadi karibu na eneo tunalokwenda huku akidai kuwa na yeye anasafari za maeneo hayo. Dada Penina na Fatuma walifurahi sana kuokoa nauli kwa lifti hiyo ya masafa marefu. Tulipofika, Carlos akatushusha na kuondoka zake kisha na sisi kuendelea na safari yetu hadi kwa huyo mtaalamu, kwakweli kulikuwa na umbali sana ila hadi tukafika eneo la tukio. Kuingia kwa mganga sasa, dada Penina na Fatuma wakaingia ila wakati naingia mimi tukashangaa yule mganga akipiga kelele na kuniambia, "Vua viatu hivyo" Nikashangaa maana leo nilivaa viatu vya kawaida na pale mlangoni pa mganga nilishavivua, ila yule mganga akaendelea kupiga kelele kuwa nivue viatu. Mara gafla yule mganga akaanguka chini na kuanza kutapatapa huku povu likimtoka mdomoni, kila mmoja alishtuka na kushangaa mambo yale ya ajabu. wakati nashangaa yale mambo nikainama na kujitazama miguuni. Nikashtuka sana kwani nilijikuta nimevaa vile viatu vya majanga.





    Wakati nashangaa yale mambo, nikainama na kujitazama miguuni.

    Nikashtuka sana kwani nilijikuta nimevaa vile viatu vya majanga.

    Nikajiuliza kuwa vile viatu vimefikaje kwenye miguu yangu, kwakweli sikuelewa.

    Hali ya mganga ilikuwa mbaya sana pale chini, akaja mtu mmoja ambaye alikuwa ni msaidizi wake na kutuambia.

    "Tafadhali naomba muende kabla mambo hayajaharibika zaidi"

    Nikajikuta nikiuliza,

    "Kwani nini tatizo?"

    Yule kijana akaniangalia kwa macho makali sana na kusema,

    "Kwani hujui? Tatizo ni wewe"

    Nikaogopa pale kwa jinsi ambavyo yule kijana aliniangalia kwa macho yake makali ila sikuwa na la kusema wala la kufanya.

    Ikabidi dada na mwenzie watoke mule ndani huku wakisikitika kwa kile kilichotokea pale kwani haikuwezekana tena kuendelea kukaa pale zaidi ya kuondoka tu maana hatukutakiwa kuonekana eneo lile.

    Tukiwa njiani kurudi, dada Fatuma akauliza.

    "Mnajua sijaelewa kwani nini tatizo?"

    Dada Penina akajibu,

    "Tatizo ni viatu hivyo alivyovaa huyo bi shost"

    Dada Fatuma akawa ananitazama huku dada Penina akinifokea.

    "Yani Sabrina huwa unapenda matatizo wewe, si unakumbuka tulivyokuwa tunaondoka nyumbani mama alikusisitiza kabisa kuwa usivae hivyo ila kwa kiburi chako umevaa na kutuletea matatizo huku, sijui yule mtu wa watu kama atapona"

    Dada Fatuma akauliza tena,

    "Kwani hivyo viatu vina tatizo gani?"

    "Mwambie mwenyewe avivue utamsikia"

    "Eti Sabrina mdogo wangu, kwani hivyo viatu vina tatizo gani?"

    "Sijui ila huwa havitaki kuvuka"

    "Si unaona majibu yake na mauzauza ya hicho kiatu, Sabrina ana kiburi tu ila angesikiliza wakubwa yasingempata hayo"

    Dada Fatuma akainama na kuwa kama mtu anayekumbuka kitu kisha akasema,

    "Ila kwa kumbukumbu zangu sikumbuki kama Sabrina alivaa viatu hivi mwanzoni"

    Dada Penina akamuuliza,

    "Ulimuangalia miguuni vizuri?"

    "Ndio nilimuangalia nakumbuka kabisa alivaa sendo fupi nyeusi"

    Moyoni mwangu nikashukuru kuona ametokea mtu mwenye kumbukumbu kuwa kile kiatu sijatoka nacho nyumbani, hapo ndipo akaniuliza tena.

    "Zile sendo nyeusi umeziweka wapi Sabrina na hivyo viatu umevaa muda gani"

    "Sijui dada"

    "Una tatizo Sabrina, tukifika nyumbani nitakupa dawa moja hivi nzuri sana itakusaidia kwa muda wakati unatafuta suluhisho zaidi"

    Ikabidi safari ile twende moja kwa moja kwa dada Fatuma ili nikapate dawa halafu ndio nirudi nyumbani.

    Kufika kwa Fatuma tukaingia ndani vizuri tu, gafla dada Fatuma akaanza kulalamika kuumwa na tumbo. Tukawa tunahangaika bila ya kujua cha kufanya, gafla akaanza kutapika na kuharisha.

    Alipotoka kujisaidia, alishikilia tumbo lililokuwa likiungurumisha kisha akatuomba tuondoke.

    "Tafadhari Penina ondoka na mdogo wako mtaniua hapa"

    Dada akauliza kwa mshangao,

    "Khee, na wewe Penina unatufukuza! Makubwa haya jamani, tatizo nini kwani?"

    "Naomba muende nitawaambia siku nyingine juu ya hili tatizo, mkiendelea kuwepo hapa mtaniua jamani"

    Ikabidi mimi na dada tuondoke na kurudi nyumbani.

    Dada alinipa lawama njia nzima,iliniuma kwavile nilihisi kuonewa kwani hata mimi mwenyewe sikupanga kuwa kwenye hali hii.



    Tulipofika nyumbani tulimkuta mama yupo nje akipunga upepo, ila alipotuona akainuka na kuuliza,

    "Vipi mmefanikiwa?"

    Dada akamjibu,

    "Tufanikiwe wapi? Angalia kiatu cha mwanao"

    Mama akanitazama chini kisha akauliza,

    "Kimefanyeje?"

    "Huoni kama ni kile kiatu cha majanga?"

    Mama akanitazama tena chini na kusema,

    "Mbona kavaa kiatu cha kawaida leo au nacho ni majanga?"

    Tukajikuta mi na dada tukitazama chini, nikastaajabu kuona vile viatu vifupi vyeusi nilivyovaa wakati naondoka nyumbani ndio nipo navyo mguuni.

    Dada akasema kwa mshangao,

    "Amakweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni ndio haya ya leo jamani"

    Mama nae akauliza kwa mshangao,

    "Imekuwaje kwani?"

    "Tuingie tu ndani nikakueleze mama, huyu Sabrina sio mtu"

    Mama akafatana na dada ndani kisha kuniacha mimi pale nje, nilikaa chini na kutafakari huku nikiuangalia mguu wangu mara mbili mbili bila ya kuamini kilichotokea.

    Nikakivua kiatu changu na kukiangalia mara mbili mbili huku nikijiuliza kwanini inakuwa hivi kwangu tu hadi nafikia hatua ya kuonekana kuwa si mwanadamu wa kawaida kwakweli niliumia, kisha nikajiinua pale nje na kuingia ndani.

    Kabla sijaenda chumbani kwangu mama akaniita,

    "Hebu njoo hapa tuongee kwanza"

    Nikaenda karibu na mama kumsikiliza

    "Hivi mwanangu utaacha lini vituko? Lini utaacha kutufanyia mambo ya ajabu? Lini mwanangu lini naomba uniambie leo"

    "Mama, mnanionea bure tu maana hata mimi mwenyewe sielewi kinachotokea. Lawama mnazonipa zinanitesa kwakweli, sijielewi mimi"

    "Hivi hujielewi kweli au unatufanyia kusudi?"

    "Mama, sijielewi kweli. Nyie ndio mnatakiwa kunisaidia na sio kunikandamiza kwa lawama"

    "Ngoja nifikirie cha kufanya maana unanichanganya sana wewe mtoto jamani"

    Nikamuacha mama pale na kwenda chumbani kwangu maana akili yangu ilipoteza mwelekeo kabisa.



    Nikiwa chumbani sasa nikapigiwa simu na Carlos kisha akaanza kuniuliza,

    "Vipi msharudi?"

    "Ndio tumerudi ila nina matatizo Carlos"

    "Najua kama una matatizo ndiomana nimekupigia simu kukufariji"

    "Inamaana matatizo yangu unayajua?"

    "Mmmh aaah mmmh siyajui"

    "Mbona unajiumauma Carlos?"

    Akakata simu, halafu nikaanza kuhisi kama kuna mtu chumbani kwangu na hapo nikapata hofu na kujiuliza,

    "Hivi nipo peke yangu kweli?"

    Sauti ikasikika,

    "Hapana upo na mimi"

    Nikaanza kuogopa na kukimbilia sebleni ila hakuwepo mama wala dada, ile sauti ikasikika tena,

    "Hata hapa tupo wote"

    Nikakimbilia nje, mara gafla mvua ikaanza kunyesha, nikakaa kwenye kiubaraza cha nyumba yetu ila sikuelewa kama dada na mama wametoka au ni vipi.

    Nikiwa pale kibarazani nikashikwa bega na kufanya nishtuke sana na kutamani kupiga makelele, kumbe alikuwa ni mama kanishika.

    "Mbona umekuja kukaa peke yako hapa kibarazani na kutupita mbio hapo sebleni?"

    "Sauti inanifata mama"

    "Sauti gani? ingia ndani mwanangu mvua itakulowanisha hii"

    Tukarudi ndani, kisha dada akamwambia mama

    "Huyo Sabrina atakuwa na mashetani kichwani humo"

    "Ni kweli ana mashetani ila dawa ya moto ni moto"

    "Unamaana gani mama?"

    "Yani shetani na shetani mwenzie"

    "Ila mama sidhani kama waganga watafaa tena, mwisho wa siku tutapoteza maisha ya mtu hapo"

    Nilitulia kimya kabisa wakati mama na dada wananijadili, nilikuwa nikitafakari pa kwenda ili niweze kuepukana na haya mambo, nikamwambia mama

    "Ila mama sitaweza kulala peke yangu leo, itabidi tulale wote usiku"

    "Hakuna tatizo ilimradi tu usiniletee hayo mauzauza yako"

    Nilitulia pale na mama na sikutaka tena kwenda chumbani kwangu, niliogopa kutokea na mambo mengine.



    Usiku wakati wa kula, nilitulia sana nikamuacha mama na dada wale kisha mimi nikaenda kula mwenyewe hata nikajishangaa maana kwa kawaida yetu huwa tunakula kwanza.

    Nikaanza kula, mara gafla kijiko kikapotea wakati nakula.

    Nikashtuka sana kwani ilikuwa ni kitu cha ajabu kijiko kupotea wakati wa kula, mara ile sahani iliyokuwa na chakula ikainuka juu kidogo na kuwa kama inaelea, nikamuita mama na kumwambia

    "Mama ona sahani inapaa"

    Mama akaja pale mezani na kusema,

    "Sahani inayopaa iko wapi? Ndio hii uliyomaliza chakula?"

    Nikashangaa ile sahani ikiwa pale mezani tena bila hata ya punje la chakula, nikashindwa cha kusema na kuipeleka jikoni tu kwakweli huyu mtu ameendelea kunisumbua sana na kunikosesha raha duniani.



    Muda wa kulala ulipofika nilienda kulala na mama kama nilivyomwambia mwanzo kuwa nitalala nae kwani mimi niliogopa chumba changu cha kulala.

    Usiku wa manane mama akashtuka kisha akanishtua na mimi na kuanza kuniuliza,

    "Unapenda kuolewma mwanangu?"

    "Kivipi mama?

    "Nijibu tu kwanza"

    "Napenda ndio ila niolewe na mwanaume nimpendaye"

    "Nimeota mwanangu, nimeota kuna mtu anakulazimisha uolewe nae. Basi yule mtu macho yanatisha hayo hadi nimeogopa,

    "Nani huyo mama?"

    "Nahisi ni mishetani, tulale mwanangu kesho tutaongea vizuri zaidi"

    Uoga ukanishika kusikia hadi mama nae kaota yale mauzauza yake, nikaogopa kulala nikawa macho kabisa kwani nilijua kuwa nikilala basi yale mambo yatanijia na mimi tena wakati siyataki.

    Nikiwa macho pale kitandani, nikajihisi kuinuliwa juu nikajaribu kupiga kelele ikashindikana yani ikawa kama vile kitendo cha kufumba macho na kufumbua, nikajikuta chumbani kwangu nikishangaa shangaa pale kitandani ila kabla ya kufanya chochote usingizi mzito ulinipitia na kulala bila mawazo ya aina yoyote ile.



    Kulipokucha, mama alikuja kunishtua chumbani.

    "Khee wewe mtoto, umenikimbia muda gani kule chumbani na kuja huku?"

    Nikawa najifikicha fikicha macho tu, nikakumbuka kuwa tangu mama aniambie kuwa ameota sikuweza kulala tena. Nikaanza kumueleza mama,

    "Ile ndoto yako ya usiku mama....."

    Kabla sijaendelea, mama akanikatisha na kuniuliza

    "Ndoto gani niliyoota?"

    "Si ile uliyonisimulia usiku mama!"

    "Mmh! Nimekusimulia ndoto mimi! Muda gani huo?"

    "Ilikuwa usiku sana mama"

    "Hapana, sijakusimulia chochote mimi labda ulikuwa unaota mwanangu. Kwanza swali hapa nimekuuliza lingine wewe unaniletea habari za ndoto, yanahusiana vipi hayo?"

    Nikataka kumueleza mama kuwa baada ya kunisimulia kuhusu ndoto ndio nikapaishwa kiajabu na kujikuta chumbani ila nikashindwa kumueleza maana mdomo wangu haukuweza kuongelea habari zile.

    Mama akaniangalia na kutoka chumbani kwangu, nami nikainuka na kumfuata anapoenda.

    Mama akageuka nyuma na kuniuliza,

    "Mbona unanifatilia nyuma Sabrina? Una matatizo gani wewe?"

    Nikarudi tena chumbani kwangu na kupata wazo la kwenda kwa dada Salome kuongea nae kwaajili ya tatizo langu kwani nilihisi huenda akanisaidia.

    Nikaenda kujiandaa.



    Nilipomaliza niliondoka bila kuaga maana mama akijua kama naenda kwa dada Salome itakuwa balaa.

    Safari ikaanza, nilipofika njiani nikakutana na Lucy akiwa mzima kabisa tena yeye ndio akanishtua mimi, tukasalimiana huku nikiwa na hofu kuwa Lucy anaweza kunikumbuka ila cha kushangaza naye alikuwa anajua kuwa alipigwa na Sam maana alianza kunishukuru.

    "Asante sana Sabrina kwa kuokoa maisha yangu, umenisaidia sana. Sikujua kama Sam ni mtu mbaya kiasi hiki"

    Sikuwa na cha kuongea zaidi ya kusikiliza maneno ya Lucy tu, tukaongea mengi kisha akaniomba nimsindikize mahali nikajikuta nikikubali tu bila pingamizi lolote na kusahau kama nimepanga kwenda kwa dada Salome.

    Kufika mahali aliposema Lucy, tukamuona Carlos, na hapo Lucy akanishtua.

    "Umemuona dokta Carlos, yule pale"

    Mara Carlos akafika eneo tulilokuwepo na kutusalimia kisha akasema kuwa anaenda kwenye hospitali yake mara moja.

    Nikajiuliza kuwa hiyo hospitali ni ipi? Nikatamani kuijua maana Carlos hakuwa mtu wa kawaida ila tukamuacha aende, nikamuuliza Lucy.

    "Je una uhakika kuwa Sam ndiye aliyekupiga?"

    "Ndio, nina uhakika kabisa Sabrina"

    Ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu yangu, kuangalia ulikuwa umetoka kwa mama nikausoma,

    "Rudi nyumbani upesi sana"

    Nikamuaga Lucy na kufanya safari ya kurudi nyumbani.



    Kufika tu nyumbani, jambo la kwanza mama akanizaba kibao.

    "Unataka kunifanya nini wewe mtoto? Unataka nife ndio ufurahi? Haya sema upesi umetoka wapi?"

    Machozi yakanitoka,

    "Ila mama, sijatoka sehemu yoyote mbaya"

    "Yani wewe unaona raha kufunga safari na kwenda kutukana watu hovyo huko, unataka watu wanionaje mimi Sabrina? Kuwa sijui kulea au ni vipi?"

    "Ila mama, sielewi unachozungumzia"

    "Angalia na hivyo viatu ulivyovaa ndio utaelewa"

    Nikajitazama miguuni, nilikuwa tena nimevaa vile viatu vya Carlos. Mama hakusikia kujitetea kwangu, akaendelea kunishutumu kwa vitu ambavyo sijavifanya.

    Muda huo huo wifi Joy nae akawasili nyumbani na kukuta yale marumbano na mama yangu, yeye ndiye akajaribu kutusuluhisha.

    Mama akakazana kuwa nitapatana nae endapo nitavua vile viatu,

    "Vivue Sabrina, acha kumtesa mama yako"

    Nikajaribu kuvivua ikashindikana kama kawaida, mama akachukia sana na kusema

    "Nakuvua mwenyewe viatu hivyo leo na ninaenda kuvichoma moto"

    Mama akainama kunivua, mara akaanguka na kuzimia nikataka kuinama pale chini ili nimpepee mama ila wifi Joy akanizuia na kusema,

    "Ni nguvu za giza hizo Sabrina, yatupasa kukemea kwanza"

    Wifi akamuweka mtoto wake pembeni, ila kabla hajafanya chochote zaidi tulishangaa kumuona Carlos pale sebleni.





    Wifi akamuweka mtoto wake pembeni, ila kabla hajafanya chochote zaidi tulishangaa kumuona Carlos pale sebleni.

    Mimi na wifi tulipigwa na bumbuwazi kwani hatukutarajia uwepo wa Carlos mule ndani, akatushtua na maneno yake ya kejeli aliyoanza kumwambia wifi.

    "Endelea Joy, mbona kimya?"

    Wifi aliendelea kuwa kimya kabisa huku Carlos akiendelea kuongea,

    "Eti unakaa hapa na kumdanganya Sabrina kuwa ni nguvu za giza, unaijua nguvu ya giza wewe? Yani mtu mzima kama wewe unaogopa giza? Hii sio nguvu ya giza kwanza kwataarifa yenu giza halina nguvu, giza halikusukumi wewe na kukufanya uanguke ila macho yako yaliyofumbwa na moyo wako usio na imani ndio unaokuangusha gizani. Endelea Joy, nini kimekunyamazisha?"

    Wifi Joy alikaa chini, nadhani alishindwa kustahimili kusimama, Carlos akasema

    "Si unaona mwenyewe, umeshindwa kusimama na kujitetea kwenye hilo giza kwahiyo bado Carlos nitaendelea kuwa na nguvu dhidi yenu"

    Mara akaingia dada Penina na rafiki yake Fatuma, dada alipomuona mama pale chini alimkimbilia huku akiniuliza kuwa mama kapatwa na nini ila Carlos ndiye aliyejibu,

    "Mama yenu kazimia hapo, anakuja wifi yenu anamdanganya Sabrina kuwa asifanye chochote eti ni nguvu za giza, mimi ndio nimekuja na kumuuliza Joy kuwa je ni kweli giza lina nguvu? Au ngoja niwaulize nyie, je giza lina nguvu?"

    Dada Penina na Fatuma wakaangaliana bila jibu, kisha Carlos akaendelea kuongea,

    "Kwa mtu mwenye upeo mdogo wa fikra atasema kuwa giza lina nguvu ila mimi nawaambia, kwa jinsi mnavyolipa nguvu giza ndivyo litakavyoendelea kuwatesa. Tazama vipofu, hawaoni chochote ila wanatembea gizani bila kujikwaa ila wewe mwenye macho unaogopa giza (Akacheka) kwakweli mnachekesha sana binadamu"

    Ni hapa ambapo wifi Joy akauliza,

    "Kwahiyo wewe si mwanadamu?"

    Carlos alimuangalia wifi Joy kwa macho makali sana na kumfanya wifi Joy aogope,

    "Unataka kujua mimi ni nani?"

    Nikamuona wifi Joy akitingisha kichwa ishara ya kukataa huku akitetemeka, kisha Carlos nae akarudi kama kwenye hali ya kawaida na kutabasamu, kisha akasema,

    "Mimi ni daktari, ngoja nikachukue vifaa vyangu kwenye gari tuweze kumtibia mama huyu"

    Akatoka nje na kutuacha mule ndani tukiwa kimya kabisa yani hakuna aliyemsemesha mwenzie.

    Carlos akarudi ndani akiwa amevalia koti la udaktari na kubeba baadhi ya vifaa vya mahospitalini mkononi.

    Tulikuwa kimya kabisa tukimuangalia, aliinama na kuwa kama mtu anayempima presha mama na baada ya muda kidogo mama akawa amezinduka tayari. Kisha akainuka na kukaa kwenye kiti, Carlos akatuamuru kumpatia mama maji ya kunywa, tukamletea akanywa.

    Halafu Carlos akaendelea kuongea maneno yake pale,

    "Tatizo lenu hamjielewi hata kidogo"

    Dada Penina akadakia nadhani baada ya kunitazama miguuni,

    "Tatizo ni hivyo viatu vya Sabrina"

    Carlos akauliza,

    "Vimefanyaje?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Ni tatizo sana, kila tunachotaka kufanya hivyo viatu vinazuia"

    Dada Fatuma nae akachangia,

    "Halafu vinaingia kwenye mguu wa Sabrina kiajabu sana"

    Carlos akaanza kutoa majibu anayoyajua yeye kuhusu kile kiatu nilichovaa kwenye miguu yangu

    "Tatizo lenu hamjielewi wala hamjitambui, hicho kiatu hakina tatizo ila sehemu mnayoenda ndio kuna tatizo. Nyie ni watu wa aina gani mmekalia imani za kishirikina? Tatizo lenu hakuna mganga atayeweza kulitatua, na uwepo wa hicho kiatu kwenye mguu wa Sabrina ni mambo ya kisayansi. Au hamjasoma nyie?"

    Dada Penina akauliza,

    "Sasa kama hakuna mganga wa kutusaidia basi tutasaidiwa na nani?"

    Wifi Joy akadakia,

    "Ni Mungu pekee ndi...."

    Carlos alimuangalia wifi kwa jicho kali tena, wifi akanyamaza bila ya kumalizia hoja yake kisha Carlos akasema,

    "Mimi ni daktari, naweza kuwasaidia matatizo yenu yote."

    Dada Fatuma akauliza,

    "Hata matatizo yangu?"

    "Tatizo lako ni dogo sana Fatuma"

    "Kheee! Umenijuaje kama naitwa Fatuma?"

    "Nakujua, mimi ni daktari na nina uwezo wa kucheza na akili yako sababu nimesomea saikolojia pia"

    "Sasa tatizo langu utanisaidiaje maana nimezunguka mahospitali yote nimeshindwa"

    "Tatizo hukufika kwenye hospitali yangu"

    Halafu akatoa kipakti chenye dawa ya ungaunga na kumwambia dada Fatuma,

    "Katumie hii ndani ya siku tatu uwaletee majibu wakina Sabrina"

    Kwakweli leo maongezi yote yalitawaliwa na Carlos, halafu wote tulikuwa kimya kumsikiliza kamavile watu tuliofungwa vinywa.

    Kisha akaniambia nivue vile viatu aende navyo ili visituletee matatizo tena.

    Mama akamshukuru sana Carlos kwa aliyoyafanya,

    "Sijui hata cha kukulipa kwakweli"

    "Usijali mama, malipo yangu ni kuniruhusu nimuoe mwanao Sabrina"

    Wifi Joy akashtuka hadi kupaliwa na kuanza kukohoa, alikohoa sana hadi kwenda nje kutapika na kuamua kukaa huko nje kwa muda.

    Niliporudi ndani nikamkuta Carlos akiendelea kuongea,

    "Na uzuri ni kwamba Sabrina amekubali kwa hiyari yake mwenyewe kuolewa na mimi"

    Mama akaniangalia kwa furaha,

    "Kweli mwanangu Sabrina?"

    Sikujibu chochote, mama alikuja na kunikumbatia huku akichezacheza kwa furaha aliyonayo siku hiyo.

    Dada Penina na Fatuma walikuwa wakinipongeza tu. Kisha Carlos akaaga na kuondoka, nilitamani kusema ukweli wa mambo lakini nilishindwa na kuwa kimya kabisa.

    Dada Fatuma akanipongeza sana,

    "Hongera Sabrina, ni raha sana kuolewa na daktari tena anayejua mambo mengi kama huyo Carlos"

    Akili yangu ikafanya kazi haraka muda huo na kukumbuka ya jana, kisha nikamuuliza dada Fatuma,

    "Jana ulisema kuwa kuna dawa utanipa, iko wapi?"

    "Ya kazi gani tena wakati daktari amepatikana? Cha muhimu ni wewe kuwa mzima na daktari tunaye tayari. Hata hivyo ile dawa sikuikuta sijui ilienda wapi Nilijaribu kuitafuta ile jana mlipoondoka lakini niliikosa"

    Sas nikaona maisha yangu yapo mashakani na msaada wangu sijui ni nini kwani hofu yangu dhidi ya Carlos ilikuwa kubwa sana. Nikatoka nje na kumfata wifi Joy.



    Nilimkuta amejiinamia tu chini, kisha akaniambia.

    "Hili ni tatizo Sabrina, peke yangu siwezi kwakweli. Sabrina wifi yangu, usikubali kabisa kuolewa na Carlos"

    Nilimuangalia wifi huku machozi yakinilengalenga, kisha wifi akaendelea kuongea,

    "Moyo wangu bado unaniambia kuwa Carlos si mtu wa kawaida, twende nikupeleke kanisani kwenye maombi. Tumkimbilie Mungu kwahili mdogo wangu"

    "Ila mimi sitaki kwenda huko makanisani"

    "Kwanini Sabrina?"

    "Wengi waongo, halafu wa kweli hawajulikani"

    "Ila mimi nitakupeleka kwa wa ukweli"

    "Hapana sitaki, labda uje nao hapahapa nyumbani"

    Ni kweli nilikuwa nateseka sana ila habari za maombezi sikuzitaka kabisa, kila nikimfikiria mama Salome ambaye kapararaizi hadi sasa kwaajili yangu sikutaka tena kwani nilihisi kuwa nitawaumiza wengi zaidi bora niumie mwenyewe tu.

    Tulirudi na wifi ndani ambaye hakukaa sana, aliaga na kuondoka.

    Mimi mwenyewe ndio nilimsindikiza wifi hadi kituoni, akapanda daladala na kuondoka.



    Wakati narudi, nikakutana na dada Zuhura ambaye alinisimamisha na kuanza kuongea nami,

    "Fanya maamuzi sahihi kabla hujachelewa na kujutia maisha yako yote"

    "Nifanye nini sasa?"

    "Fanya ibada, ibada ni msingi imara utakaokufanya usitetereke tena"

    "Yani nianze kuvaa kama wewe ulivyovaa?"

    "Hapana ila fanya ibada, mavazi yatabadilika vile moyo wako unapofunguka. Ibada ni kitu muhimu sana, nakuonea huruma maana kuna kitu kinazunguka maisha yako halafu wewe mwenyewe hukioni"

    "Kitu gani hicho?"

    "Sabrina una jini tena hilo jini linakufatilia kila uendako"

    "Wewe umejuaje kama na wewe sio jini?"

    "Nakuhurumia Sabrina ila ipo siku utakumbuka maneno yangu"

    Mara ikapita gari ya Carlos karibu yangu, ikasimama nami nikapanda na kumuacha dada Zuhura akiwa amesimama pale na kusikitika. Carlos akaniambia,

    "Wewe ni binti mwenye akili sana, sema chochote nitakufanyia"

    Nikamuuliza,

    "Wewe ni jini?"

    Nilikuwa na maneno ya ajabu mudu huu hata sikuelewa kwa nini,

    "Kwani wewe wanionaje Sabrina?"

    "Nakuona kuwa ni mtu"

    "Basi ukae ukijua hilo, mimi ni mtu kama ila tofauti ya mimi na wewe ni ndogo sana ambayo wengi hawajaitambua hadi sasa"

    "Kwahiyo wewe si jini?"

    "Na huyo jini unayemsema akiwa hapa hutoweza kuuliza hayo maswali yote unayouliza"

    Akanipeleka mahali ambako tulikuwa wawili tu yani mimi na yeye, na kusema.

    "Nitakuoa Sabrina"

    Huku akitabasamu na kuendelea kusema,

    "Na hiyo itakuwa siku yangu ya furaha kupita siku zote hata duniani"

    Nikamwangalia tu na kumwambia,

    "Lakini mimi nampenda Sam"

    "Kama kweli unampenda Sam, mwache aishi kwa amani kwasasa"

    Kisha akanirudisha nyumbani na kuondoka.

    Wakati wa kulala ulipofika nikaenda kulala chumbani kwangu.



    Kabla sijalala vizuri, maneno ya Carlos yakajirudia kichwani mwangu.

    "Nitakuoa Sabrina"

    Mara gafla nikasikia sauti nyingine ikisema,

    "Na baada ya ndoa nitajitokeza mwenyewe halisi unijue"

    Nikaogopa, kikafatia kicheko ambapo sikujua mchekaji yuko wapi, kisha akasema tena.

    "Baada ya ndoa tutaenda kuishi kwenye ulimwengu wetu wa peke yetu"

    Nikatamani kujibu ila ikashindikana, akaongea tena

    "Jiepushe na wafanya ibada, watakuangamiza hao"

    Maneno ya huyu mtu asiyeonekana ndio yaliyonitetemesha na kuniogopesha.

    Mara gafla nikaona chumba changu kimebadilika na ile sauti ikasema tena,

    "Kesho ni siku yetu Sabrina tena ni siku yetu kubwa sana, nitakuvisha pete ya uchumba na tangia hapo utakuwa ni mchumba wangu unayetambulika kwa wote"

    Nikaogopa zaidi, gafla nikashikwa na kitu mgongoni na kujikuta nimelala kabisa.

    Yule mkaka wa ndotoni akaja kwenye ndoto akiwa amebeba pete inayong'aa sana na kusema,

    "Nitakuvisha kesho pete hii, ni pete ya uchumba na itakaa kwenye hicho kidole chako"

    Nikashtuka toka kwenye msingizi na kukuta chumba changu kikinukia sana marashi ambayo yalinichanganya sana.

    Kisha nikajikuta nikilala hadi panakucha.



    Dada Penina aliingia chumbani kwangu asubuhi sana na kuniuliza,

    "Umepulizia marashi gani humu, mbona pananukia sana"

    "Mmh sijui"

    "Niambie bhana, au unahisi nitakuomba hayo marashi nijipulizie? Mmh ila yananukia sana kwakweli, sijapata kuona marashi ya kunukia kiasi hiki"

    Nikawa kimya tu nikimsikiliza dada anayoyasema, kisha akachukua alichokitaka na kuondoka.

    Nikaamka na kwenda kufanya usafi huku roho yangu ikiniambia kuwa kesho aliyoisema yule kijana wa ndotoni ndiyo leo, nikakaa na kuomba kuwa kitu hiko kisitokee huku nikijitazama vidole vyangu.

    Nikapigiwa simu na Sam,

    "Tafadhari Sabrina mpenzi wangu, nakupenda sana. Usifanye unachotaka kufanya leo"

    Nikashtuka na kumuuliza,

    "Kufanya nini kwani?"

    "Nimeota ndoto mbaya juu yako, tafadhari Sabrina usifanye hivyo"

    "Basi niambie cha kufanya Sam maana sielewi kitu"

    "Ni kweli huelewi, kuna watu nilijaribu kuwaeleza nilichoota wamesema niende na wewe ili tupewe ushauri wa kiroho, tafadhari Sabrina njoo upesi usipuuzie"

    Simu ikawa imekatika na kufanya nizidi kupatwa na mawazo, nikapigiwa simu na mtu mwingine tena kuangalia ni dada Zuhura.

    "Sabrina, leo ni siku mbaya sana kama utaweza ondoka hapo kwenu uje kwetu. Ningependa nikufate ila namuogopa mama yenu"

    Mawazo yakanizidi sasa kwani sikuelewa nifanyeje kwa wakati huo, nguvu zikanijia nikaenda kuoga na kujiandaa ili niondoke nyumbani huku nikijisemea kuwa popote nitakapowahi kufika patakuwa ni pazuri kwangu.



    Wakati nataka kuondoka, moyo wangu ukakumbwa na uzito wa gafla, nikatoka hadi nje na kurudi tena ndani na kujiuliza kuwa kwanini na kuwa na uzito wa kiasi hicho?

    Nilikaa kitandani na kujipa ujasiri, nikainuka ili niondoke, mara kama mtu amenikalisha kwa nguvu halafu sauti ikasikika

    "Umeshachelewa Sabrina"

    Halafu nikasukumwa na kulala tena nikalala usingizi mzito sana.

    Baada ya muda kupita, nikajiona nipo kwenye eneo halafu wamejaa watu wengi ambao siwafahamu kisha akatokea yule kijana wa ndotoni na ile pete yake mkononi, akavuta kidole changu na kunivisha ile pete, kisha akasema,

    "Kuanzia sasa wewe Sabrina ni mchumba wangu"

    Wale watu walikuwa wakishangilia na kupiga vigelegele, huku mimi mwenyewe nikiwa na sura ya huzuni.

    Nikashtuka kutoka kwenye ile ndoto, nikakuta watu wengi wamejaa chumbani kwangu, na niliposhtuka wakasema kwa pamoja,

    "Surpriseeeeeeeee....."

    Huku wakipiga makofi na vigelegele, moja kwa moja nikajitazama kwenye vidole vyangu.

    Nikakuta nimevaa pete ileile niliyovalishwa ndotoni.



    Moja kwa moja nikajitazama kwenye vidole vyangu.

    Nikakuta nimevaa pete ileile niliyovalishwa ndotoni.

    Nikashtuka sana na kuwatazama watu waliopo chumbani kwangu ambao walikuwa wakipiga makofi na vigelegele, kwa haraka haraka nikaweza kumuona mama, mama Semeni, dada Penina na rafiki yake Fatuma, Lucy, Carlos na watu wengine watatu ambao sikuwafahamu.

    Nikainuka pale kitandani nikiwa na hasira sana, nikaenda sebleni nao wakanifata nyuma, nikataka kutoka nje mama akanizuia huku akiniuliza,

    "Unataka kwenda wapi mwanangu?"

    Nikiongea kwa ukali,

    "Mama huu ni udhalilishaji, huwezi kuingiza watu wote hao chumbani kwangu bila ridhaa yangu"

    Mama akaongea kama kunipooza hivi,

    "Ilikuwa ni surprise mwanangu"

    "Surprise gani mtu nafanyiwa wakati nimelala mama? Uliona wapi bhana? Mmenikera sana"

    Nikarudi nyuma na kumsogelea Carlos, kwakweli nilikuwa na hasira sana muda huu na sikumuogopa mtu yeyote wala kitu chochote. Nikamuuliza Carlos,

    "Toka lini watu wanavishwa pete ya uchumba usingizini? Toka lini? Niambie upesi bhana, umenikera sana. Uchumba gani wa ndotoni"

    Nikachukua kidole changu ili kuivua ile pete, nia yangu ni kumtupia nayo Carlos usoni ila ile pete haikuvuka ilikuwa imeng'ang'ania kwenye kidole changu, nikakaa chini huku machozi yakinitoka.

    Dada Penina na Fatuma wakajaribu kunipooza, ila walishindwa kwamaana nilikuwa na hasira sana.

    Mara gafla watu wote wakatoka pale sebleni na kuniacha mimi na Carlos tu, nadhani Carlos aliwaambia kuwa waondoke tuzungumze.

    "Sasa Sabrina kilichokuchukiza ni kipi?"

    "Usijifanye hujui Carlos, unajua kila kitu. Uliyoyafanya ndotoni kwangu huyajui wewe?"

    "Yapi hayo Sabrina? Sijui chochote"

    "Unajua, nimesema unajua tena unikome sitaki kuolewa na wewe, sitaki kuolewa na jini mimi"

    Mara gafla nikasikia kicheko cha kutisha, nikaanza kuogopa na sikuwa na pa kujificha au kukimbilia pale sebleni, ikanibidi nikimbilie kwa Carlos aliyeonekana kama mtu kwangu.

    Nikamsogelea nae akanikumbatia, nikajikuta nimekuwa mpole gafla na ule ukali wote wa mwanzo umepotea.

    Kisha Carlos akanikalisha na kuwaita wale wa nje.

    Nilikuwa kimya kabisa yani kama vile sio mimi niliyekuwa nafoka sana muda mfupi uliopita.

    Carlos akaanza kutambulisha wale watu watatu ambao siwafahamu,

    "Hapo kuna mama, baba na kaka yangu"

    Mama alikuwa ameandaa chakula na wote wakajumuika kula kasoro mimi ambaye nilishindwa kula kabisa na kuwaacha wenyewe wale wamalize na wafurahie kitu

    ambacho mimi nakichukia.

    Walipomaliza kula, wakaongea mawili matatu na kuaga. Mama akauliza wanapokaa wale wazazi wa Carlos, wakamuelekeza ili na sisi tuweze kwenda.



    Jioni ya leo nilikaa na kuiangalia ile pete ambapo nilitamani hata nikate kidole niweze kuitoa kwangu maana ilinikera sana ila sikuwa na la kufanya tu.

    Muda wa usiku ulipofika napo sikujihisi kula na kuamua kwenda kulala hivyo hivyo.

    Nikiwa nimelala, akaja yule kijana wa ndotoni na kusema

    "Pole mke wangu mtarajiwa, najua una njaa na unahitaji kula. Nakuletea chakula upendacho."

    Akaniletea keki na maziwa na juisi.

    Nikajikuta nikila ile keki na maziwa, ila juisi nilikunywa kidogo na kuiacha.

    Kisha akaniambia,

    "Ulitaka kunitia aibu leo ila ni vizuri niliwahi kukudhibiti maana ungeniumbua kwa wageni wale, bora kwa mama yako na dada yako maana najua jinsi ya kuwaweka"

    Nikamsikiliza tu,

    "Hivi karibuni nitakuoa ila ndoa yetu haipaswi kuonwa na watu kamavile ila kuna viumbe maalum wa kushuhudia ndoa yetu"

    Nikashtuka usingizini na kusema kwa nguvu,

    "Viumbe gani hao?"

    Sauti ikasikika,

    "Ni majini wenzangu, wanaoishi baharini na mapangoni"

    Nikaanza kutetemeka kwa uoga, chumbani kwangu kulikuwa na harufu ya marashi iliyotapakaa chumba kizima.

    Nilipoangalia pembezoni mwa kitanda changu nikaona sahani yenye punje za keki, pakti ya maziwa na juisi iliyonywewa kidogo, hapo nikashtuka zaidi baada ya kugundua kuwa mambo yote yale ya kula na kila kitu yalifanyika chumbani kwangu, nikainuka ili nikimbie chumba. Sauti ikasikika,

    "Unaenda wapi Sabrina?"

    Nikazidi kutetemeka, wazo likanijia kuwa nimpigie simu Carlos, nami sikupoteza wakati nikachukua simu na kumpigia akapokea.

    "Acha kunitesa Carlos"

    "Nakutesaje Sabrina?"

    "Unanitisha hadi naogopa kulala"

    Nikamsikia Carlos akicheka sana kwenye simu hadi ile simu ikakatika, ila hali ikawa shwari mule ndani.

    Sikutaka kulala tena mule ndani, nikatoka na kwenda chumbani kwa mama na kulala pembeni yake hadi kunakucha.

    Mama alipoamka alishtuka na kuuliza,

    "Umekuja muda gani humu?"

    "Muda mrefu tu, ila mama nina ombi moja"

    "Lipi hilo?"

    "Naomba twende kwa wale watu ambao Carlos aliwaleta na kujifanya kuwa ni ndugu zake"

    "Inamaana huwaamini?"

    "Ndio siwaamini"

    Basi mama akaniambia kuwa hakuna tatizo na kwavile walimuelekeza wanapoishi basi itakuwa vyema kama tukienda leo leo kabla hatujasahau zaidi hayo maelekezo.

    Tuliamka na kufanya kazi za hapa na pale kisha kujiandaa kwa hiyo safari ya kuwafata hao ndugu wa Carlos.



    Tuliondoka na kufika eneo ambalo tulielekezwa na wale ndugu wa Carlos, tukawapigia simu wakaja kutupokea na kutukaribisha sana.

    Tulifika kwao na kuongea ya hapa na pale, nikaenda pembeni na yule ambaye alisema ni kaka wa Carlos.

    "Hivi kweli Carlos ni ndugu yako?"

    "Ndio ni ndugu yangu kwani vipi?"

    "Ni ndugu yako kabisa?"

    "Kwanini unamashaka?"

    "Unajua anapoishi?"

    Akasita kujibu kisha akaondoka bila ya kusema chochote.

    Nikarudi tena ndani ambako kulikuwa na hao waliosema ni wazazi wake na mama.

    "Samahani naomba niulize"

    "Uliza tu"

    "Eti nyie ni wazazi wake kabisa na Carlos?"

    Mama akanikatisha,

    "Ndio maswali gani hayo Sabrina?"

    "Mmh mama nauliza tu"

    Nikatulia tu huku nikingoja kujibiwa, yule aliyetambulishwa kama mama yake akaguna kwanza na kuanza kunijibu,

    "Mmh! Sisi ni kama baba yake na mama yake mdogo"

    "Kivipi? Inamaana nyie sio?"

    "Hapana, sisi ni ndugu zake"

    "Maana mmesema kuwa nyie ni kama, ndiomana nikapatwa na maswali hapa"

    "Usijali, Carlos ni mtoto wetu sana. Tangia akiwa mdogo tulikuwa nae"

    Mama nae akauliza,

    "Kwani nyie ni wenyeji wa wapi?"

    "Sisi ni watu wa Kigoma, Carlos amezaliwa hukohuko na kukulia hukohuko"

    Kidogo nikajiridhisha ila bado sikuwa na imani nao kwa sana.

    Tukaongea mengi na kuaga.



    Tulipofika nyumbani tulimkuta dada Penina akiwa ndani na rafiki yake Fatuma, tuliwasalimia kisha Fatuma akaanza kuongea,

    "Jamani kweli Carlos ni daktari wa ukweli mama, amenisaidia tatizo langu hata siamini"

    "Kwani ulikuwa na tatizo gani?"

    "Nilikuwa na tatizo la uzazi mama, yani kila hospitali waliniambia mimi ni mgumba. Kuna mganga nilienda akasema ndugu zangu wamenifunga nisizae, mwingine akasema ni lile jini mahaba lililonivaa kipindi kile ndio lilinifunga nisizae kwakweli nilikata tamaa. Siku ile tumetimuliwa kwa yule mganga mashuhuri sababu ya Sabrina niliumia sana tena sana ila Carlos kanitibia bure kabisa, dawa ile nimekunywa kwa siku moja tu nikaenda kukutana na mwenzangu kama ilivyoandikwa. Si alisema kuwa baada ya siku tatu nitapata majibu, basi leo nimechukua kipimo cha mimba na kujipima, nimekuta nina ujauzito wa siku. Kwakweli nimefurahi sana ndiomana nimekuja kuwaeleza habari hii"

    Mama nae akaifurahia sana ile habari,

    "Kwakweli bora nimepata mkwe daktari"

    Dada Penina akadakia,

    "Tena ni daktari wa madaktari"

    Wakaendelea kuongea pale nami nikaenda chumbani kwangu kupumzika.

    Baada ya muda kidogo nikapigiwa simu na Sam.

    "Sabrina, tafadhari naomba tuonane haraka sana"

    Nikakubaliana nae, kisha kisha nikatoka chumbani kwangu na kwenda kumuaga mama kuwa natoka mara moja kwani moyo wangu uliniambia kuwa kutokuaga kwangu ndio chanzo cha kutokea Sabrina wawili wawili huko njiani.

    "Uwe makini Sabrina, kumbuka wewe ni mchumba wa mtu sasa"

    "Usijali mama"

    Nikaondoka pale nyumbani na kuelekea mahali ambako nimepanga kukutana na Sam.



    Nilifika mapema kabla ya Sam kufika, nikatulia kumngoja afike na haikuchukua muda akawasili.

    Akachukua mkono wangu ili kunisalimia ila akarushwa pembeni kama na umeme, akasogea na kuniuliza.

    "Umeshika nini mkononi Sabrina?"

    Nikamuonyesha kile kidole chenye pete.

    Sam akasikitika sana na kusema,

    "Umeitoa wapi?"

    "Carlos kanivisha"

    "Nawe ukakubali?"

    "Nilikuwa nimelala Sam, alinivisha nikiwa usingizini"

    Sam akazidi kusikitishwa na kile kitu.

    "Sasa Sabrina umechukua hatua gani mpaka sasa?"

    "Sijafanya chochote ila leo tulienda kwa ndugu wa Carlos"

    "Hao ndugu sidhani kama wa kweli, kwanza niambie amekupa pete hiyo kwa misingi ipi?"

    Nikaogopa kumwambia Sam kama amenipa kama mchumba wake kwani nilijua Sam atachukia tu.

    "Sijui ila amenivisha tu"

    "Na bado hatujachelewa Sabrina, nadhani twende leo kwa wale watu"

    Nikainuka pale, Sam hakuweza kunishika hata mkono kwani alipigwa na shoti alipojaribu kunishika tena.



    Safari ikaendelea ila tulipokuwa njiani nikapotezana na Sam, hata sijui nilipotezana nae vipi ila hakuonekana nikajaribu kumpigia simu hakupatikgna kwahiyo nikaamua kurudi nyumbani tu.

    Kufika nyumbani nikamkuta Sam yupo nyumbani kwetu akiongea na mama,

    "Huyu mwenzio ni mchumba wa mtu sasa kwahiyo usipende kumfatilia"

    "Mchumba wa mtu kivipi?"

    "Kwani huelewi maana ya mchumba wa mtu wewe? Ni mke mtarajiwa wa mtu"

    "Ni nani huyo mumewe"

    "Kumbe hujui, ni....."

    Nikaingilia kati na kuleta habari za salamu kisha nikamvuta Sam,

    "Umefika muda gani huku?"

    "Uliponipotea nikajua lazima utarudi kwenu ndiomana nikaja huku moja kwa moja. Niambie ukweli Sabrina, au Carlos kakuvisha pete ya uchumba?"

    "Hapana Sam"

    "Niambie ukweli ili nijue jinsi ya kukusaidia"

    "Kama ni kweli utanisaidiaje?"

    "Niambie kwanza ni kweli au si kweli"

    Nikiongea kwa unyonge,

    "Ni kweli Sam"

    "Kwanini umenificha muda wote Sabrina?"

    Mara Carlos akawasili muda huo nyumbani kwetu, akatupita mimi na Sam pale nje bila ya salamu ila alimuangalia Sam kwa jicho kali sana na kuingia ndani.

    Mara gafla Sam akaanza kuwashwa, alijikuna sana hadi nikamuonea huruma, akaondoka nyumbani kwetu huku anakimbia nikajaribu kumuita lakini hakugeuka nyuma kuniangalia wala nini, akapotea kabisa maana giza lilishaingia.

    Nikarudi ndani kwa masononeko makubwa sana, nikawapita pale sebleni na kwenda chumbani kwangu halafu usingizi ukanipitia, kwenye ndoto nilimuona Sam tu siku ya leo, nilimuona Sam akiteseka na kuhangaika.

    Nikashtuka na kusikia harufu ya marashi chumba kizima, sikutaka maajabu ingawa ni usiku sana nikainuka na kwenda kulala chumbani kwa mama.

    Nikiwa nimelala tena, nikajiwa ndotoni na yule kijana wa ndotoni akasema,

    "Karibia nakuja kukuchukua mke wangu, Carlos na Sam hawatahusika tena"

    Nikamshangaa wakati Carlos ni yeye mwenyewe, nikaogopa sana.

    Akaendelea kusema,

    "Unaogopa nini sasa? Je nikikwambia kuwa muda huu upo chumbani kwako na si chumbani kwa mama yako kama unavyodhani? Na huyo uliyelala nae si mama yako bali ni mimi"

    Nikashtuka tena toka usingizini na kuangalia mandhari ya chumba ilikuwa ni chumba changu na harufu ileile ya marashi. Mara gafla nikaguswa mgongoni na kuitwa jina langu.





    Nikashtuka tena toka usingizini na kuangalia mandhari ya chumba ilikuwa ni chumba changu na harufu ileile ya marashi. Mara gafla nikaguswa mgongoni na kuitwa jina langu.

    "Sabrina geuka"

    Nikawa natetemeka hadi nikajikojolea kwa uoga, mara gafla nikajiona nipo chumbani kwa mama halafu sauti ya kunicheka ikasikika na kutoweka, mama nae akaamka na kunishangaa vile nilivyotoa mimacho.

    Akagusa pale nilipokaa na kushangaa,

    "Khee Sabrina umejikojolea?"

    Nilikuwa kimya tu kama mtu nisiyejielewa.

    "Yani na ukubwa wote huo unakojoa kitandani? Tena mchumba wa mtu, yani unajikojolea kitandani? Ona ulivyotoa mimacho kama mjusi kabanwa na mlango, haya toka kitandani kwangu nitoe mashuka"

    Mama alilalamika sana ila sikufanya kusudi kukojoa pale,

    "Najua nimelala na jitu zima kumbe kikojozi, unataka kunikumbusha kipindi cha utoto wako! Nishasahau kufua mikojo tayari, na chumbani kwangu usije kulala tena nenda ukaozeshe godoro lako kule kwahiyo mikojo yako"

    Nikatoka nje kwenda kuoga maana harufu ya mikojo hata mimi mwenyewe ilinichefua ukizingatia mkojo wa mtu mzima unavyotoa harufu mbaya.

    Mama aliyatoa yale mashuka na kuyaloweka, akatoa na godoro lake nje kulianika. Kwakweli niliona aibu sana ila ndio hivyo nilikuwa nimejikojolea.



    Nilikaa sebleni, mama nae akaja na kukaa karibu yangu kisha akaniuliza

    "Una tatizo gani Sabrina?"

    "Sina tatizo mama"

    "Huna tatizo! Umeanza lini kukojoa kitandani?"

    "Ni leo tu mama, ni bahati mbaya"

    "Itabidi mchumba wako akija nimueleze ili ajue mapungufu yako mapema, usije ukatia aibu huko mbele"

    Nikakaa kimya nikimsikiliza mama na hoja zake,

    "Ndio, lazima nimueleze Carlos ili kama anaamua kumuona mwanamke kikojozi ajue moja"

    "Jamani mama, kukojoa mara moja tu ndo nishakuwa kikojozi!"

    "Ona ulivyokosa aibu, na ukafue yale mashuka"

    Nikainuka kwani nilijua kuwa nikiendelea kubaki pale sebleni na mama basi mada itakuwa ndio hiyo hiyo ya kikojozi.

    Nikatoka na kwenda nje kufua yale mashuka, nikakaa na kuanza kufua. Mara akatokea mtu na kunikumbatia kwa nyuma, nilipogeuka alikuwa ni Carlos ambaye aliniambia,

    "Pole sana Sabrina"

    Sikumjibu na kuendelea kufua, akaniuliza

    "Nikusaidie kufua?"

    Napo sikumjibu, alikuwa na mfuko wa rambo mkononi uliokuwa na vitu ndani yake, akanipa na kuniambia nipeleke ndani.

    Nikauchukua bila ya kusema chochote na kuupeleka ndani, niliporudi niliyakuta yale mashuka yakining'inia kwenye kamba yani yalianikwa.

    Nikamuangalia Carlos na kumuuliza,

    "Umeyafua saa ngapi?"

    "Ulivyoenda ndani"

    "Hivi Carlos wewe unajiona ni mtu kweli?"

    "Ndio, mimi ni mtu. Kwani wewe unanionaje?"

    "Nakuona kuwa wewe ni jini"

    "Na huyo jini ukimuona hapa utaweza kustahimili na kusema hayo?"

    Nikabaki kimya, kisha nikasema tena,

    "Niambie basi wewe ni nani"

    "Mimi ni mtu Sabrina"

    Nikarudi ndani alipo mama, ila Carlos nae akanifata nyuma. Nikamuuliza mama,

    "Mtu wa kawaida anaweza kufua mashuka kwa dakika mbili?"

    Mama akanijibu,

    "Unashangaa vipi kuhusu mashuka wakati umewahi kufua nguo za mwezi mzima kwa dakika mbili!"

    Mama hakunijibu nitakavyo swali langu, ikabidi nikae kimya tu maana jibu nililolipata halikuwa jibu nilitakalo.

    Mama akawa anaongea na Carlos kuhusu mimi huku akinisifia muda wote, nami nikakatisha maongezi yao na kumwambia mama,

    "Si umwambie tu"

    "Nimwambie nini?"

    "Ulichosema kuwa utamwambia, mweleze tu ajue"

    "Kumbe ulifanya kusudi eeh!"

    Carlos akadakia na kuuliza,

    "Kwani mnataka kuniambia nini?"

    Mama akajibu haraka haraka,

    "Hamna kitu baba yangu"

    Nami nikajibu,

    "Alitaka kukwambia kuwa mimi ni...."

    Mama akanikatisha tena kwa kunipigapiga, Carlos akaendelea kusisitiza kuwa tumwambie tu.

    Mimi nikajisikia kumwambia kwani nilijua kuwa inaweza kuwa sababu ya yeye kuachana na mimi.

    "Leo usiku nimejikojolea"

    "Ndio mlichokuwa mnabishana kuniambia?"

    Mama akawa anajichekelesha tu huku akijaribu kumpooza Carlos ambaye alitujibu kuwa hili si tatizo kwake na anaweza kulitatua, nami nikajibu.

    "Pia si tatizo kwangu, usingenitisha usiku nisingejikojolea"

    Mama akauliza,

    "Kukutisha kivipi?"

    Nikataka kumueleza kila kitu mama kuwa Carlos si mtu wa kawaida ila Carlos alidakia na kujibu,

    "Labda ile simu niliyompigia usiku ndiyo ilimtisha"

    Nikajaribu kupingana na hilo ila sikuweza tena na kujikuta nikipatwa na usingizi pale pale ambapo mama akaniambia niende kulala chumbani.



    Wakati nimelala, akatokea yule kijana wa ndotoni na kuniambia.

    "Nakupa onyo Sabrina, wewe ni mchumba wangu kwa sasa sitapenda uende mahali bila ruhusa yangu wala kwenda kuonana na yeyote bila ruhusa yangu. Ukithubutu kukiuka hili na kufanya utakacho yatakayokupata usilalamike"

    Nikashtuka na kujiuliza, kwanini huyu mtu anapenda kunitawala? Na kwanini anipangie sheria zake?

    Nikainuka ili kutoka nje, ila kabla sijatoka nikapigiwa simu na dada Salome.

    "Nakuomba mara moja Sabrina"

    Akanitajia mahali pa kuningoja.

    Nikatoka hadi sebleni na kumkuta mama kasinzia ila Carlos hakuwepo, nikaona kuwa huu ndio muda muafaka wa kuondoka maana mama hajui.

    Nikabadili nguo haraka na kwenda mahali aliponiita dada Salome.



    Nilipofika nikamkuta akiningoja, akaniambia.

    "Sina njia yoyote zaidi ya hii katika kukusaidia wewe"

    "Mbona sikuelewi dada?"

    "Twende Sabrina"

    "Wapi?"

    "Utapajua tu, twende"

    Nikaondoka na dada Salome hadi aliposema, nikakuta watu wengi tu. Dada Salome akaniambia,

    "Kuwa huru Sabrina, wote hawa wana matatizo na wamekuja hapa kwaajili ya maombezi"

    Nilivyosikia maombezi nikatoa ule mkono wangu wenye pete, nikbngalia kidoleni ile pete haikuwepo. Nikamgeukia dada Salome na kumuuliza,

    "Ataniombea nini sasa?"

    "Atakuombea matatizo uliyokuwa nayo"

    Muda kidogo dada Salome akainuka na kuniaga kuwa anakwenda uwani mara moja, na hilo likawa kosa kubwa sana kwake.

    Mara gafla nikapatwa na nguvu za ajabu na kujikuta nikikimbia sana tena bila kuwa na uelekeo wa maana.

    Nilikimbia sana, nikafika mahali nikasimama na kujiuliza kuwa kwanini nakimbia maana sikuwa na sababu maalum ya kukimbia.

    Nikakaa chini ya mti ambao ulikuwa eneo hilo huku nikitafakari kuwa nimekuwa mtu wa aina gani kwani hata maombi nayakimbia.

    Mara nikahisi kama kitu kinanitembelea, nikajipukuta kikarukia mbele yangu, kungalia ni nyoka.

    Kwakweli nilishtuka sana na kuogopa, ukizingatia huyo kiumbe nyoka namuogopa sana.

    Nikaanza kutetemeka maana yule nyoka alikuwa akitoa toa ulimi wake nje, nilipobahatika kuinuka mahali pale nikaanza kukimbia tena hovyohovyo na mwisho wa siku nikajikuta nimefika nyumbani kwetu tena nipo mlangoni kabisa, nimefikaje fikaje sikujua. Kila nikikumbuka muonekano wa yule nyoka niliogopa sana, kabla sijaingia ndani nilijikagua kwanza na kuona kuwa simu yangu haikuwepo, roho iliniuma sana baada ya kuhisi kuwa nimeipoteza simu yangu.

    Nikakaa pale pale nje ila kila nikikumbuka muonekano wa yule nyoka ujasiri wa kukaa pale nje ukaondoka kabisa, sikuweza kukaa zaidi na kuingia ndani. Nilimkuta mama pale pale sebleni akaniuliza,

    "Umetoka wapi?"

    "Hapo nje mama"

    Nilimjibu hivyo ili nijue kama anajua kuwa ni muda mrefu sipo nyumbani. Mama akasema,

    "Umesahau mchumba wako alivyosema?"

    "Amesemaje kwani?"

    "Carlos si amekwambia kuwa usipende kutoka toka hovyo! Mbona unapenda makubwa mwanangu?"

    "Inamaana mama na wewe unajua?"

    "Ndio najua kwanini nisijue?"

    "Mateso yangu unayajua mama halafu unafurahia"

    "Mateso gani Sabrina?"

    Nikashindwa kuongea zaidi nilihisi kufungwa kinywa gafla, mama ndiye aliyeendelea kuongea.

    "Unapokuwa na mchumba unatakiwa kuwa mtulivu, msikilize anachokwambia. Usipende kufanya vitu kinyume na unavyoambiwa na mwenzi wako"

    Maneno aliyoongea mama yalikuwa sahihi ila aliongea kwa mtu ambaye si sahihi tena ukizingatia nina mawazo ya kupotelewa na simu yangu.

    Nikainuka na kwenda chumbani kwangu.



    Nilipofika chumbani nikashtuka kuiona simu yangu kitandani, nikashangaa sana na kujiuliza inamaana sikuondoka nayo? Na kama niliondoka nayo mbona wakati nimerudi na kujipekua sikuwa nayo na je pale chumbani imerudije?

    Nikakaa pale kitandani na kuiangalia vizuri simu yangu, nikakuta kuna ujumbe toka kwa Carlos

    nikaufungua na kuusoma,

    "Huwezi kupoteza kitu nilichokupa mimi hata mara moja"

    Muda huo huo nikajitazama kidole changu, nikaiona ile pete ya uchumba ikiwa tena kidoleni, hapo wazo likanijia kuwa ni lazima Carlos ndiye kijana wa ndotoni ila ni kwanini akija kwa umbo la Carlos anajifanya kuwa sio yeye? Hapo ndio huwa nakosa jibu la moja kwa moja.

    Nikainuka na kwenda kuandaa chakula cha usiku.



    Wakati wa kula, tulikuwa wote mezani kama kawaida ila nilikula kile chakula bila kushiba, nikaongeza tena ila sikushiba pia hofu ikanijaa kuwa huenda nakula na lile jamaa la ndotoni, nikamuuliza mama na dada.

    "Nyie mmeshiba?"

    "Sijashiba, yani hapa nataka nimuagize Penina akaninunulie chips maana hata chakula kwenye jungu kimeisha"

    Dada nae akadakia,

    "Hata mimi mwenyewe sijashiba mama, nipe tu hiyo hela sijui huyu Sabrina ametuwekea mavitu gani kwenye chakula chake"

    Mama akaniuliza,

    "Wewe mwenyewe umeshiba?"

    Nikawa najiuma uma tu kwani sikutaka kusema ukweli kuwa sijashiba ila njaa niliyoihisi ilikuwa kubwa sana, dada akatoka na kwenda kununua alichoagizwa na mama.

    Aliporudi wakaanza kula nami nikadonoa kidogo tu kwa mama kisha nikamuomba mama tulale wote.

    "Nani anataka kuozeshewa godoro lake? Siku hizi hufai kabisa wewe Sabrina, umekuwa mtu wa ajabu sana"

    Nikamuomba dada kulala nae ila akakataa pia, roho ikaniuma sana na kuona kuwa ninaonewa na hawa watu kisa kukojoa siku moja tu tena nikiwa macho kabisa bila ya kujua kuwa mimi nina matatizo.

    Nikaamua kwenda kulala mwenyewe.



    Nikiwa chumbani usingizi haukukawia kunichukua, nikawahi sana kulala.

    Wakati nimelala, akaja yule mkaka wa ndotoni akijisifu kuwa amenikomesha na kunionyesha nilichopika siku hiyo kumbe ilikuwa ni hewa yani nilichopika ni hewa na tulichokula ni hewa hapakuwa na chochote kile ndiomana hatukushiba. Yule kijana akajitapa kuwa anauwezo wa kufanya chochote akitakacho kwahiyo mimi nisipende kufanya vitu kinyume na asemavyo yeye.

    "Unakumbuka nilichokwambia mchana?"

    Nikatikisa kichwa kuwa sikumbuki chochote, akaniambia

    "Basi mimi nitakukumbusha"

    Huku akicheka, mara akageuka nyoka tena nyoka yule yule niliyemkimbia chini ya mti. Nikaogopa sana na kutetemeka, halafu nikashtuka toka usingizini.

    Kuangalia vizuri nikamuona yule nyoka kitandani kwangu.





    Nikaogopa sana na kutetemeka, halafu nikashtuka toka usingizini. Kuangalia vizuri nikamuona yule nyoka kitandani kwangu.

    Hapo sikuwa na ujanja tena, nikaanza kupiga makelele

    "Nyoooka nyoooka, jamani nakufa nyoka huku"

    Mama na dada wakaja mbio chumbani kwangu, walipofungua mlango wangu tu niliinuka na kukimbilia sebleni huku nikihema sana.

    Nikakaa kwenye kochi huku nikihema ila nikahisi kuwa nimekalia kitu tofauti juu ya kochi, kilikuwa kigumu gumu, nikainuka kukiangalia ni yule nyoka tena nikawa naruka ruka sijielewi huku nikimkimbilia mama na dada kwa kupiga makelele kuwa kuna nyoka, mama akawa ananitikisa huku akiniuliza.

    "Vipi wewe Sabrina?"

    "Nyoka mama"

    "Nyoka yuko wapi we mtoto? Na huyo nyoka atatokea wapi humu ndani jamani? Tungekuwa tunaishi porini labda, acha mawazo finyu mwanangu"

    Nikazidi kumkumbatia mama kwani yule nyoka alinitisha sana ukizingatia nilimkalia pale kwenye kochi.

    Mama na dada wakasogea na mimi pembeni na kuangalia pote hawakumuona yule nyoka.

    "Hakuna kitu mwanangu, acha maruweruwe. Nenda kalale tu mwanangu"

    "Siwezi kulala peke yangu tena mama, naogopa"

    Ikabidi mama anichukue tukalale wote maana niliogopa sana tena sana.



    Usiku wa leo ulikuwa ni mrefu sana kwangu, ingawa nilikuwa chumbani kwa mama ila uoga bado ulinijaa, ingawa mama alikuwa pembeni yangu ila bado niliogopa.

    "Lala mwanangu, acha uoga jamani"

    Mama alinibembeleza kama vile mtoto mdogo ili nilale.

    Baada ya muda kidogo usingizi ukanipitia tena, nikajiona niko mahali huku nikikimbia sana tena bila uelekeo, nyuma yangu kulikuwa na jitu la ajabu likinikimbiza nikafika mahali na kuanguka chini, mbele yangu akatokea tena yule nyoka hapohapo nikashtuka tena toka usingizini huku jasho jingi likinitoka na kupiga kelele kwa sana hadi mama akashtuka na yeye toka usingizini na kuniuliza,

    "Kwani una tatizo gani jamani Sabrina?"

    "Mama nyoka"

    "Umeanza kuchanganyikiwa mwanangu, ngoja nimpigie Carlos simu labda atusaidie"

    Mama akachukua simu yake na kumpigia Carlos ambaye alimwambia kuwa anaweza kufika muda huo huo.

    Baada ya dakika kadhaa, mtu akagonga mlango wetu, mimi na mama tukaenda kufungua na kukuta ni Carlos aliyejifanya kuwa kashtushwa sana na simu ya mama.

    "Kuna nini hapa mama?"

    Akaingia ndani moja kwa moja, mama akawa anamuelezea vile ilivyokuwa. Carlos akajibu haraka haraka,

    "Itabidi nije kumchukua mke wangu mama maana anatesema sana hapa"

    "Kweli kabisa, mwanangu anateseka sana"

    "Poleni, nitakuja kumchukua na kufunga nae ndoa kabisa"

    Nikahisi moyo wangu kushtuka sana baada ya kusikia neno ndoa toka kwa Carlos halafu mama akichekelea kabisa, kwavile ilikuwa karibu na alfajiri kwahiyo hatukulala tena na kubaki kuongea tu hadi muda ambao dada Penina aliamka na kujiandaa kwaajili ya kwenda kazini.

    Carlos akaondoka na dada halafu mimi nikabaki na mama nyumbani na kuendelea na mambo mengine.



    Mchana wa leo wakati mama amelala tukatembelewa na mgeni ambaye sikumfahamu kwa wakati huo, alikuwa ni mbaba wa makamo nikamkaribisha ndani akagoma na kusema kuwa nimletee tu kiti akae pale nje, nikamtolea kiti na kumwambia,

    "Nikakuitie mama?"

    "Hapana, shida yangu ni kuzungumza na wewe"

    Nikakaa chini kumsikiliza anachotaka kuzungumza na mimi, akaanza kwa kuniuliza

    "Unajua kwanini sikutaka kuingia humo ndani kwenu?"

    "Sijajua bado"

    "Tatizo lako hujui ni watu gani wa kuwakaribisha na watu gani sio wa kuwakaribisha"

    "Ila tunajifunza kumkaribisha kila mtu maana huwezi jua pengine ametumwa na Mungu"

    "Umejibu vyema Sabrina"

    "Kheee unanijua hadi jina!"

    "Ndio nakujua ndiomana niko hapa kuzungumza na wewe. Ngoja nikuulize kwanza, matatizo yako hayo yalianzia wapi?"

    "Yalianzia kwenye ndoto"

    Akadakia haraka na kunijibu,

    "Basi na yataishia kwenye ndoto"

    "Kivipi?"

    "Kama unakumbukumbu nzuri, kabla ya kuanza na tatizo alifika mgeni hapa ambaye hakuongea chochote. Mlimkaribisha ndani ila aliondoka bila kuaga"

    Nikaanza kukumbuka matukio ya nyuma kabisa, nikakumbuka kuwa ni kweli alishawahi kufika mgeni wa aina hiyo nyumbani kwetu hata tukashangaa sana na nilimwambia mama kuhusu hilo tukajisemea kuwa labda alikuwa ni chizi maana alifika hadi ndani ila hakuongea chochote na aliondoka bila ya kuaga.

    Nikamuuliza yule mbaba,

    "Unamaana gani kunikumbusha hayo yote"

    "Unajua kwanini hakuaga?"

    "Sijui"

    "Kwavile hakuondoka kweli, yupo kwenye nyumba yenu bado akiingia na kutoka atakavyo."

    Nikashtuka sana,

    "Inamaana vyote tufanyavyo humu ndani anaviona?"

    "Ndio anaviona, siku ukibahatika kumuona macho yake yanang'aa kama taa au mbalamwezi angani. Unaweza kujifunika macho ukimuona tena"

    "Mbona waniogopesha?"

    "Usiogope Sabrina, nimekuja kukusaidia"

    "Utanisaidiaje? Kwanza wewe ni nani?"

    "Utanijua tu Sabrina, unakumbuka ndoto zako zilipoanza?"

    Nikakaa kimya nikivuta kumbukumbu,

    "Ulimuona kijana anayekujia ndotoni kwenye picha iliyokuwepo kwenye kompyuta ya dada yako, taswira yake ikabaki kwenye mboni za macho yako hadi leo. Pole sana Sabrina, nitakusaidia"

    "Nisaidie basi, nateseka kweli"

    Yule mbaba aliniangalia sana, akasema nimpe mkono wangu. Nikampa mkono, akauangalia sana na kuniambia nimpe ule wenye pete ila kabla sijampa ule mkono akatokea Carlos mbele yetu halafu yule mbaba akaniachia ule mkono alioushika kwa haraka sana, kisha nae akainuka na kuondoka bila ya kuaga.

    Nikamuangalia Carlosa kwa makini na kumuuliza,

    "Umemfanya nini yule mbaba wa watu?"

    "Hakuna anayeweza kukusaidia zaidi ya mimi, ni mimi tu Carlos mwenyewe ndiye ninayeweza kukusaidia"

    Sura ya Carlos ilikuwa ni yenye hasira sana hadi mishipa ya sura ikamchomoza hata mimi mwenyewe nikaogopa kumtazama zaidi maana sura yake ilinitisha.

    Nikaamua kuingia ndani na muda huo huo mama nae akaamka na kunikuta pale sebleni.

    "Ulikuwa unaongea na nani Sabrina?"

    "Na Carlos ila msura wake ume...."

    Carlos akaingia ndani muda huo huo na kumsalimia mama, kisha akasema

    "Nimekuja kuangalia hali ya Sabrina inavyoendelea"

    "Ila mbona ulibaki nje?"

    "Nilikuwa napaki gari langu vizuri mama"

    Mama aliendelea kuongea vizuri na Carlos bila ya kuelewa yanayojiri kuhusu huyo Carlos anayemsifia bila kujua.

    Dada Penina akawasili nyumbani na kutusalimia kisha akaniita chumbani kwake, nikamfata kwa nyuma hadi chumbani kwake akakaa na mimi kuongea.

    "Mdogo wangu, nimekutana na mtu ameniambia kuwa ametoka kuongea na wewe"

    "Mtu gani huyo dada?"

    "Amenipa hiki kichupa cha mafuta, amesema kuwa alisahau kukupa"

    Akakitoa hiko kichupa na kunikabidhi, nikamshukuru na kumuuliza

    "Amesema kuwa ni cha nini?"

    "Hajaniambia ila amesema kuwa ni mafuta uwe unapaka usoni hasa wakati wa kulala"

    "Sawa dada nimekuelewa"

    Nikainuka na kile kichupa ili nikakiweke chumbani kwangu huku moyoni mwangu nikijua kuwa ile ni tiba kwa matatizo niliyonayo kwasasa.

    Wakati napita pale sebleni, gafla Carlos akainuka na kunipiga mkononi hadi kile kichupa kikapasuka na yale mafuta kumwagika.

    Nikashangaa, mara nikasikia sauti ya dada Penina akitokea kwenye korido ya ndani kuja sebleni, akasema

    "Tena nimesahau kukwambia, amesema hayo mafuta yasimwagike"

    Naye akafika eneo lile ambalo nilisimama mimi pale sebleni na kushangaa kwani yale mafuta yalibadilika rangi taratibu na kuanza kuwa na rangi ya damu, dada Penina akauliza

    "Kuna tatizo gani hapa?"

    Nikamuangalia na kumjibu,

    "Yale mafuta yamemwagika dada"

    Mama nae akainuka na kusogea eneo lile, kisha "Mafuta gani hayo yana rangi ya damu? Mmeyatoa wapi?"

    Dada Penina akamuelezea mama,

    "Tena aliniambia kuwa hayaruhusiwi kumwagika"

    Muda wote huo Carlos alikuwa kimya kabisa hakuongea chochote kamavile sio yeye aliyesababisha mpaka yale mafuta yakamwagika, mama akauliza tena.

    " Na mbona yamegeuka na kuwa damu?"

    "Hata mimi sijui mama"

    Nikaamua na kwenda kuchukua tambala na maji ili niweze kufuta.

    Wakati nataka kufuta Carlos akanizuia na kusema,

    "Acha Sabrina, usifute"

    Nikamuuliza,

    "Kwanini?"

    Hakunipa sababu na kukazana tu kuwa nisifute, nikaona hana sababu za msingi nikataka kufuta tu akanishika mkono kunikataza, mama akadakia na kusema.

    "Unapokatazwa jambo Sabrina, hebu jaribu kuelewa. Carlos si chizi hadi akukataze kuwa usifute"

    Mama akanivuta mkono na kwenda kukaa na mimi kwenye kochi kisha Dada Penina na Carlos nao wakaja na kukaa ila yale mafuta ya damu yaliendelea kuwa palepale, kisha Carlos akamuuliza dada Penina,

    "Huyo aliyekupa hayo mafuta alikwambia Sabrina ayafanyie nini?"

    "Alisema ayapake usoni"

    "Si mmeona wenyewe, mafuta gani yanamwagika na kugeuka damu? Bado tu mnayaamini mafuta hayo? Ni wazi hayafai, si mazuri kabisa kwa afya ya binadamu"

    Mama akaanza kumfokea dada Penina,

    "Utamuua mdogo wako wewe kwa kumletea vitu vya ajabu ajabu, ona sasa ile mimafuta kumbe ni damu"

    Kuyaangalia tena yale mafuta pale chini yalikuwa yameyayuka, Carlos akasema

    "Mnaona yale mafuta sasa? Hayapo tena yani yameyeyuka, je hapo unashindwa kutafakari kuwa yangekuwaje huko usoni? Vitu vingine si vya kupokea"

    Wote tukabaki kimya tukimsikiliza Carlos anachosema na giza nalo lilishaanza kuingia, kisha Carlos akamwambia mama kuwa angependa leo alale pale nyumbani na mimi ili kuepuka yale mambo yanayonitokea usiku, mama akamjibu

    "Hairuhusiwi kisheria, watu watanielewa vibaya mimi"

    "Sawa nimekuelewa mama"

    Aliendelea kubaki kwetu hadi pale tulipoandaa chakula cha usiku akajumuika pamoja na sisi.

    Baada ya hapo akaaga na kuomba nimsindikize kidogo, nikainuka na kumfikisha mlangoni ila kabla sijarudi ndani akanishika mkono na kuniambia

    "Leo lazima nije kulala kwenu, tena chumbani kwako"

    Nikashtuka sana na kuona dhahiri kuwa Carlos si mtu wa kawaida kabisa kisha nikarudi ndani huku nikiwa na mawazo mengi sana, nikamuomba mama niweze kulala nae na leo. Mama hakuwa na pingamizi kabisa labda kutokana na kilichonitokea usiku uliopita.



    Muda wa kulala ulipofika nikaenda kulala chumbani kwa mama kwani chumbani kwangu niliogopa hata kwenda kulala.

    Wakati tumelala nilimuomba mama anikumbatie naye akakubali na kunikumbatia kisha tukalala.

    Nikiwa kwenye usingizi mzito, nikaona kama mtu ameingia chumbani kwa mama kisha akaitoa mikono ya mama na kunibeba mimi juu juu halafu akanipeleka chumbani kwangu na kuniweka kitandani.

    Nikashtuka gafla kutoka usingizini, nikakaa kitandani na kujiona kuwa nipo mwenyewe mule chumbani tena ni chumbani kwangu.

    Nikainuka pale kitandani, ila kabla sijafanya chochote nikaona kitu na kushtuka sana.

    Nikamuona Carlos akiingia chumbani kwangu kwa kupitia pembe ya chumba.





    Nikamuona Carlos akiingia chumbani kwangu kwa kupitia pembe ya chumba. Uoga ukanishika na kuzidi kuona kuwa Carlos si mtu wa kawaida, nikataka kupiga kelele ila Carlos akanyoosha mkono na kujikuta nipo kimya gafla. Alinisogelea na kunikumbatia kisha akanibusu, huku akiniangalia kwa makini usoni. Nilikuwa kama gogo wala siwezi fanya chochote wala kuongea, Carlos akaniambia "Sina nia ya kufanya chochote na wewe kwakuwa muda bado ila ninachohitaji ni kulala pembeni yako leo, sikutaka kuja kama hewa sababu nataka utambue kuwa leo ulilala na mimi pembeni yako" Nikiwa nimesimama vilevile, akanishika mabega na kunikalisha kitandani, nami nikatii na kukaa kisha akanilaza nami nikalala halafu akanifunika shuka naye akalala pembeni yangu. Kwakweli usingizi haukunipitia upesi kwani muda mwingi nilikuwa namwagikwa na machozi tu sababu sikuwa na cha kujitetea, Carlos alikuwa pembeni yangu hadi kulipokucha. Kama kawaida, mama alikuja moja kwa moja chumbani kwangu na kuingia bila ya kugonga. Kwa haraka haraka nikajua kuwa mama atamuona Carlos maana bado alikuwa pembeni yangu. Ila cha kushangaza mama hakumuona, alianza tu kuniuliza. "Mbona ukahama na kurudi chumbani kwako bila ya kuniambia mwanangu? Kwani nini tatizo?" Sikumjibu kwavile sikuweza kuongea, nikainuka pale kitandani na kumuangalia mama. "Mbona hunijibu Sabrina? Umeanza tena kiburi chako eeh!" Nikawa namuonyesha mama kitandani kama ishara ya kuangalia, nilihisi labda na yeye atamuona Carlos. Mama aliangalia na kuniuliza, "Kwani kuna kitu gani hapo unaponionyesha? Mbona sioni chochote" Nikamuangalia tena Carlos aliyeonyesha kutabasamu kisha akainuka pale kitandani na kumpita mama yangu pale pale mlangoni bila ya kuonekana, kitu ambacho kilinishangaza sana nikatamani kumwambia mama kuwa mwangalie huyo lakini kusema ndio siwezi, sikuwa na la kufanya kwakweli. Carlos alipotoka, mama nae akafata kwa nyuma na kutoka, nilibaki mwenyewe chumbani nikijaribu kuongea lakini bado ilikuwa ngumu maana mdomo wangu ulikuwa mzito kutamka neno lolote, nikajiambia kuwa labda nimekuwa bubu machozi yakanitoka. Nikatoka nje na kwenda kuoga kisha kurudi tena ndani, mama akaniuliza "Unapenda tule nini leo mwanangu?" Sikuweza kumjibu tena, mama akachukia sana kwavile sikumjibu chochote. Mama akainuka na kuondoka, kwani alihisi kuwa namfanyia kiburi tu wakati ni kweli sikuweza kuzungumza chochote. Nikiwa naendelea na mawazo yangu pale sebleni, nikapata ujumbe toka kwa Suzy "Nipigie Sabrina, kuna jambo la muhimu sana nataka kukwambia" Nikausoma ule ujumbe mara mbili mbili kwamaana hata kama nikimpigia nitaongea vipi na yeye? Nikamuomba anieleze kwa njia ya ujumbe, akajibu "Haiwezekani, inatakiwa nikueleze kwa kuongea" Nikaona hayo majanga sasa maana sina ujanja. Nikiwa ndani nikasikia kama mama akibishana na mtu nje kwahiyo nikainuka ili kwenda kuona ni mtu gani anayebishana na mama. Kufika nje nikamuona ni dada Zuhuru, yeye alikazana kuwa anataka kuongea na mimi, huku mama nae akimzuia kwa kumuita mchawi. "Sitaki umfundishe mwanangu mambo ya ajabu naomba uondoke tu" "Kwakweli nashindwa kuvumilia kwa ndoto nizipatazo juu ya mwanao Sabrina, naumia sana ndiomana unaona niking'ang'ania wakati wanifukuza. Naomba niseme nae japo kidogo tu kwa leo" "Kila siku unavyoonana nae njiani huwa huzungumzi unayotaka kusema leo? Yani watu wengine ni wachawi kweli nyie, kusikia mwanangu anataka kuolewa basi nyie mnataka kuweka mambo yenu asiolewe. Safari hii nawaambia mmeshindwa, mliniweza kwa mwanangu Penina tu ila sio kwa huyu Sabrina. Nenda kawaambie wachawi wenzio kuwa mmekutana na kisiki cha mpingo" Mama aliongea hadi mishipa ilikuwa inamsimama ila bado dada Zuhura kwa upole kabisa alihitaji kuzungumza na mimi, ikabidi nitoke pale nje ila mama akaniangalia kwa jicho kali na kunifokea kama mtoto mdogo, "Rudi ndani wewe" Nilitamani kuongea kitu ila sikuweza, mdomo ulifungwa kabisa. Nikasimama pale pale nikiwaangalia, mama akaja na kunivuta mkono hadi ndani kisha akafunga mlango na kusema. "Tumia akili mwanangu, hawa watu ni wabaya sana" Nami nikaishia kusema kimoyomoyo kuwa tumia akili mama yangu maana kusema kwa sauti sikuweza. Dada Penina akawahi kurudi na leo, mama akamuuliza. "Hivi kazini kunakalika wewe siku hizi? Mbona unawahi sana kurudi?" "Shemeji kaniambia ananitafutia kazi nyingine nzuri na isiyo na mateso" Mama akafurahi sana na kucheza cheza, huku akisema "Si unaona mambo hayo! Sasa mtu kama Sam angeyawezea wapi? Yeye mwenyewe shida tupu pale alipo. Huyo ndio shemeji anayetakiwa bhana" Wakiendelea kuongea, tukasikia mtu akigonga mlango. Dada akaenda kumfungulia na kumkaribisha ndani, alikuwa ni Sam. Mama alipomuona tu akaanza kuongea, "Wewe kijana ukae mbali na mwanangu, huyu ni mke wa mtu mtarajiwa" "Mama, sina nia mbaya ila nakuomba niongee na Sabrina japo kidogo tu" "Hakuna cha kuongea na Sabrina hapa, nilipokuwa nakuchekea usifikirie nafurahia wewe kuwa na Sabrina tena ukae nae mbali kabisa sitaki kukuona" Sam alikuwa mbishi kutoka, mama akainuka ili amvutie kwa nje na kuanza kumsukuma ikabidi niinuke ili kumtetea Sam, tatizo ni kuwa sikuweza kuongea kwakweli mdomo pia ni silaha jamani. Nikajaribu kumtetea Sam pale kibubu bubu lakini ikashindikana kwani mama alifanikiwa kumtoa nje na mimi kunirudisha ndani. Nikakaa nikiwa na mawazo sana kwani sikuwa na cha kunisaidia wala kuwasaidia wenzangu. Dada Penina akaniongelesha pale ila sikumjibu, akaanza kumuuliza mama, "Mbona Sabrina haongei leo jamani?" "Hata mi mwenyewe namshangaa tangia asubuhi yupo hivyo hivyo sijui ana matatizo gani" Dada akaniuliza kuwa nina matatizo gani, nikainuka na kwenda chumbani kwangu kisha nikachukua peni na karatasi. Nikaandika na kumpa dada, "Siwezi kuongea" "Kwanini huwezi kuongea mdogo wangu?" Dada aliongea kwa huruma sana huku akiniuliza kwa upole, nikachukua tena lile karatasi na kuandika, "Carlos ameniziba mdomo ili nisiweze kusema siri zake" Nikampa dada, ambaye alishtuka sana na kuniuliza, "Siri gani hizo mdogo wangu?" Nikaandika tena, "Nimegundua kuwa Carlos si mtu wa kawaida, ananitisha usiku na anaingia humu ndani kimazingara" Nikampa dada ambaye alishtuka zaidi na kuniuliza, "Umejuaje mdogo wangu?" Nikaandika, "Yeye mwenyewe anajidhihirisha kwangu kupitia ndoto za usiku ila huwa anakuja kwa sura nyingine na kusema kuwa yeye ni jini" Dada akashtuka zaidi ya mwanzo na kumuita mama kwa nguvu aliyekuwa jikoni, "Mama njoo, njoo uone mama yangu" Nikajua sasa ukombozi wangu umefika maana siku zote ukweli humuweka mtu huru. Mama alikuja na kutulia pale, dada akampa lile karatasi ambapo mama aliomba asomewe na dada. "Nimemuuliza Sabrina hapa kwanini haongei, ndio akachukua karatasi na peni akaandika kuwa hawezi kuongea, nikamuuliza kwanini ndio akaanza kunielezea hapa kwa maandishi" "Nisomee nisikie mwanangu" "Ameandika hivi: Wifi Joy ameniziba mdomo sababu nimejua siri yake" Mimi nikashtuka, mama nae akashtuka na kuuliza, "Siri gani hiyo?" Dada akaendelea, "Hata mimi nimemuuliza, kanijibu hivi: Nimegundua kuwa yule mtoto aliyezaa sio wa kaka Deo" Nikashtuka tena, mama akapatwa na mshangao zaidi na kuuliza, "Kivipi? Na huyu Sabrina amejuaje?" Dada akaendelea kujibu, "Nimemuuliza pia kajuaje, ameandika: Aliniambia mwenyewe baada ya kumbana sana" Mama akatikisa kichwa na kusema, "Mungu wangu yani Sabrina amekaa na siri hiyo kipindi chote hadi kazibwa mdomo? Ndiomana watu wengi wanasema kuwa mtoto hafanani na Deo kumbe si damu yake! Huyu Joy atanitambua" "Ndiomana anakuja mara kwa mara siku hizi huku ili kuficha siri yao na Sabrina" Roho iliniuma sana kuona siri ya wifi imetoka bila kutarajia, inamaana Carlos kabadilisha yale maneno pale pale jamani dah roho iliniuma sana na kuongea sikuweza. Kwakweli machozi yalinitoka tu. Giza lilipoingia mama na dada wakapanga jinsi ya kumkabili wifi Joy na kumueleza kaka ukweli. "Itabidi twende kesho mama" "Hapana tusikurupuke, twende taratibu kila kitu kitakuwa sawa. Mi naona vyema kama tukimuita Deo na Joy mahali hapa ila itakuwa kimya kimya, waje wajulie hapa hapa. Kesho nitawapigia simu kuwa wajipange waje" Dada na mama wakakubaliana, kisha mama akanigeukia mimi na kuniuliza, "Sabrina, huyo Joy amewezaje kukuziba mdomo au ni mchawi?" Nikachukua karatasi na kuandika tena, "Wifi Joy si mchawi na wala hahusiki na hili, nyie mnapumbazwa na Carlos tu maana yeye ndiye aliyenifanya hivi" Dada Penina akaliwahi lile karatasi na kusema, "Nilidhani unaandika maneno mengi kumbe mawili tu" Mama akamuuliza "Kasemaje?" "Kaandika hapa: Ndio wifi Joy ni mchawi" Mama akaongea zaidi sasa, "Mweeeh kumbe tunalalamika wachawi wakati chawi lingine tumerikaribisha kwenye ukoo mmh! Atatumaliza huyu Joy, namuhurumia mwanangu Deo jamani" Roho iliniuma kwani ukweli hautoki, wote unageuzwa na kuwa uongo ila sikuwa na la kufanya zaidi ya kuumia. Muda wa kulala ulipofika nilimfatilia mama na kwenda kulala nae chumbani kwake, ila usingizi uliponipitia nikabebwa tena kama jana na kurudishwa chumbani kwangu, kushtuka nikamuona Carlos mbele yangu huku akitabasamu kisha akasema. "Leo nimekufunga kidomodomo, ukitaka kuwa huru uache kuropoka" Nikatamani kumuuliza ila sikuweza kufanya hivyo, yeye ndiye aliyetawala maongezi yote. Akafanya anachotaka kwenye chumba changu na hakuna wa kumzuia kufanya chochote alichotaka. Akasema tena, "Nataka kukufanyia vitu vizuri na vya kuvutia Sabrina, nataka ufurahi" Nikawaza moyoni mwangu hata kummeza huyu Carlos maana alizidi kunikera, muda wote machozi yalinitoka. Kisha Carlos akasema "Nadhani hupendezewi na uwepo wangu hapa" Baada ya dakika kadhaa akatoweka na kuniacha mwenyewe chumbani. Mara gafla nikasikia kama chumba changu kinatetemeka, nikaanza kuogopa na kuinuka pale kitandani ili nikimbilie kwa mama. Ila mlango uligoma kufunguka yani ulikuwa mgumu kabisa, uoga ulikuwa mwingi mara vile viatu vya majanga vikaletwa mbele yangu halafu kuna sauti ikaniamuru kuwa nivivae, nikawa natikisa kichwa kama ishara ya kukataa kuvivaa. Mara vile viatu vikageuka nyoka wa vichwa viwili.





    Mara vile viatu vikageuka nyoka wa vichwa viwili. Yule nyoka akaanza kunifata kwenye miguu yangu, nikaogopa sana ukizingatia sikuweza kupiga makelele kwavile mdomo ni mzito halafu ndani nilikuwa mwenyewe kwahiyo uoga ukanijaa zaidi. Yule nyoka akazidi kunifatilia, kwakweli nikashindwa kustahimili na kujikuta nimeanguka chini, yule nyoka akawa anatambaa kwenye miguu yangu. Ile hali iknifanya nipoteze fahamu kwani nilikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa. Sikujua kilichoendelea hadi kulipokucha. Nilipozinduka nilijikuta nikiwa nimelala kwenye kochi sebleni, nikashtuka sana ila pembeni yangu alikuwepo mama na dada Fatuma hivyo kunifanya nisiogope zaidi. Mama akaanza kuongea kwa kunipa pole. "Pole sana mwanangu" Nikatikisa kichwa tu kama ishara ya kuipokea ile pole. "Ila nini kimekupata mwanangu maana tumekukuta ukiwa umelala chini tena hujitambui kabisa. Nini Tatizo?" Dada akadakia, "Hawezi kueleza huyu itabidi tumpe peni na karatasi atuambie" Dada akanipa peni na karatasi ili niandike kilichonisibu, nikashika peni na karatasi huku nikihofia kubadilika kwa maneno. Mama akaniambia, "Andika mwanangu usiogope chochote, tupo hapa kwaajili yako" Nikajaribu bahati yangu ya mwisho ya kueleza kuhusu Carlos huku nikitumai kuwa wataona nilichoandika. "Jana usiku Carlos alikuja na kujigeuza nyoka mwenye vichwa viwili na kuanza kunitisha, sikuweza kustahimili hadi nikazimia" Nikamkabidhi mama ambaye alianza kukisoma kwa sauti, "Jana usiku....." Kabla hajaendelea, dada Penina akakipora kile kikaratasi na kutaka kusoma yeye, kwajinsi ambavyo mama alisoma nilijipa moyo kuwa ni lazima itakuwa kama nilivyoandika. Dada Penina akaanza kukisoma sasa, "Jana usiku sana, nilijiwa na watu wawili yani Salome na Zuhura wakanitishia kuniroga kama sijafata wanachosema, mara wakageuka kuwa nyoka mwenye vichwa viwili na kuanza kunitisha. Hapohapo nikazimia" Mama na dada wakasikitika sana huku mama akisema, "Nilihisi tu kuwa hawa watu wanahusika, si unaona Penina!" "Naona mama yangu, sijui wanatutakia nini sisi" "Wanataka roho zetu, yani wakishatumaliza ndio iwe furaha yao. Hamalizwi mtu hapa nitapambana nao hadi pumzi yangu ya mwisho" "Au siku ile ambayo Sabrina alisema nyoka nyoka ndio wao?" "Ndio ni wao tu hakuna mwingine" Nikajaribu kutingisha kichwa kama ishara ya kukataa lakini hawakunielewa, wakaendelea kuamini wanachoamini wao. Niliinuka pale na kwenda kuoga kwani sikuwa na cha kufanya, nilikuwa kama mtu mgonjwa tena ule ugonjwa usioonekana. Nilipomaliza kuoga, nilirudi na kukaa sebleni huku machozi yakinitoka kwani yote yanayotokea kwangu ni kama mazingaombwe. Sikuelewa moja wala mbili. Mchana wa leo, nilitoka nje na kukaa mlangoni huku nikitafakari mambo yanavyokwenda kiajabu ajabu. Kwa mbali kidogo nikamuona wifi Joy akija huku ameongozana na vijana wawili na mdada mwingine mmoja, nikainuka na kuwapokea ila waliponisalimia nilishindwa kuwajibu kwavile sikuweza kuongea, nikaongozana nao hadi nyumbani. Tulipofika mlangoni wifi akaanza kunieleza. "Kama tulivyoongea kipindi kilichopita Sabrina, nilikwambia twende kanisani ukakataa na kusema kuwa nikuletee wachungaji hapa nyumbani. Basi leo nimetimiza, hawa unaowaona ni wanamaombi wamekuja leo wafanye maombi kwenye nyumba yenu hapa. Natumai umewafurahia na wanakaribishwa." Nikaitikia kwa kichwa kuwa wanakaribishwa, "Ila mbona huongei Sabrina?" Machozi yalinitoka tu ukizingatia balaa ambalo wifi Joy atakutana nalo muda mfupi ujao toka kwa mama na dada. Wifi akawakaribisha wale wageni ndani, baada ya kuingia sebleni tu wakakutana na dada Penina ambapo akasema, "Tena afadhari umejileta wewe mwenyewe Joy mjaa laana usojua vibaya wewe" Wale wageni walikuwa kimya, wifi nae alikuwa kimya. Mara mama akatoka chumbani na kusema, "Umemuacha wapi mwanaharamu?" Wifi Joy akashtuka na kuuliza, "Mwanaharamu? Ndio nani?" "Mwanaharamu mwanao inamaanisha hujui?" Wifi akawa mpole sasa, "Jamani ndugu zangu hata salamu tena mbele ya wageni" "Salamu kampe huyo aliyekufanya utuletee mwanaharamu kwenye ukoo" Wifi Joy akaona kuwa hali si shwari ukizingatia alikuja na wageni, wifi akaamua kuwatoa nje wale wageni. Dada Penina akamwambia, "Unaogopa watajua siri zako eeh! Nilikuwa nakusikia unavyomwambia Sabrina hapo nje, ooh nimekuletea wanamaombi sijui nini na nini mbona unawatoa nje? Waache hapa wajue uchafu wako mbwa wewe" Kwakweli nilimuonea huruma sana wifi Joy kwani ataniona mimi mbaya wakati nimetoa siri yake bila kutarajia wala kutaka. Nami nikawa namfata wifi Joy kwa nyuma, mama akanirudisha. "Umefungwa mdomo kwa kurogwa halafu bado unataka kumfatilia huyo mchawi Joy na lazima atakuwa amempa limbwata mwanangu ndiomana limekuwa kama zezeta, kila utakachomwambia lazima amtaje Joy" Mama na dada waliongea sana tena bila hata nukta, machozi yalinitiririka tu kwani sikuwa na msaada wowote. Wifi Joy hakurudi tena, alitokomea hukohuko na wageni wake nadhani alijua kama akirudi basi atakutana na varangati. Dada na mama wakapanga kumpigia kaka simu ili aje nyumbani wamwambie ukweli na wamuulize maswali, nikafikiria sana jinsi kaka atakavyokuwa baada ya kujua ukweli, sikutamani ukweli ule ujulikane ila ndio hivyo Carlos alishafanya anayoyajua yeye na kuharibu kila kitu. Jioni ya leo nikiwa nyumbani nikapokea ujumbe toka kwa wifi Joy. "Mbona umenidhalilisha hivyo mdogo wangu? Kwakweli sikutegemea kabisa kitu cha namna hii toka kwako Sabrina, nilikuamini sana. Nitakuwa mgeni wa nani mimi? Nitafanya kitu gani mimi? Sikupenda hii kitu itokee kwangu, naumia sana. Deo akijua lazima atanifukuza, nitaenda wapi mimi? Huyu mtoto nitamleaje jamani, sina kazi, biashara wala chochote ninachokitegemea zaidi ya Deo hata kama nikirudi kwetu lazima watanifukuza kwa kosa hili, ukizingatia ndugu zangu wengi hawanipendi sababu tu niliokoka. Kwakweli kama ni majaribu basi jaribu hili limekuwa kubwa sana katika maisha yangu, sina cha kufanya wala pa kukimbilia. Nangoja hatma yangu ila Mungu pekee ndiye anayejua" Ujumbe wa wifi Joy ulikuwa ni mrefu sana na hakika uliniumiza, nilimuhurumia sana ingawa kaka Deo ni kaka yangu wa damu ila huruma ilinijaa kwa wifi Joy ukizingatia alivyonisimulia jinsi ilivyokuwa yeye na huyo James. Nilimlaani James na kumuona ni mtu anayetumiwa tu na viumbe wa ajabu kama Carlos ndiomana akafanya ujinga aliomfanyia wifi yangu. Nikatamani kuwaambia mama na dada kuwa wamuhurumie wifi Joy ila naelewa wazi hata kama ningeweza kuongea wasingekubali kunielewa kwani ni ngumu sana kukubaliana na hili. Mama alishawasiliana na kaka Deo kuwa aje nyumbani siku inayofatia ili wafanye nae mazungumzo. Roho yangu haikuwa sawa kabisa, dada Penina akaenda jikoni kuandaa chakula cha usiku muda huohuo nikatumiwa ujumbe na Carlos, "Nitakuja kula chakula cha usiku leo" Nikainuka na simu yangu mpaka jikoni na kumpa dada ili ausome ule ujumbe uliotumwa na Carlos. Nikaona dada akikodolea macho ule ujumbe kwa muda mrefu kisha akasema, "Kumbe ni kweli" Akanipa ile simu na kumfata mama sebleni na kuanza kumueleza kumbe dada Penina aliuona ujumbe ule ambao ulitumwa na wifi Joy, nilipotazama simu yangu nikauona ule ujumbe upo juu nikaufuta haraka sana ili kuondoa ushahidi hata kama dada ameona ila ni kwa bahati mbaya tu. Mama akahitaji kuusoma na yeye ule ujumbe. Nikafungua ujumbe aliotuma Carlos na kumpa, cha kushangaza nae mama akauona uleule ujumbe niliotumiwa na wifi Joy. Hapo nikajua kwamba lazima Carlos anafanya mambo yake ili yeye asionekane kuwa mbaya. Dada na mama wakazidi kumlaani wifi Joy na kumuita majina ya ajabu ajabu. "Kesho ndio mwisho wa kiburi na majivuno na huyu changudoa Joy kwakuwa Deo anaenda kujua kila kitu" Kila walichoongea ilikuwa ni kumponda wifi Joy tu. Muda wa kula ulipofika nilikuwa na mashaka sana ukizingatia Carlos ameshasema kuwa anakuja kula chakula cha jioni, dada na mama walikula sana leo. Mama akaanza kusema, "Mmh Penina umepika chakula kitamu sana leo yani hata hatushibi" Kwakweli huyu Carlos alikuwa mtu wa ajabu sana hata sijui aliwezaje kula chakula chetu chote. Ikabidi mama na dada washushie na maziwa sababu hawakushiba kile chakula tofauti na walivyowaza wao kuwa ni kitamu sana ila ukweli ni kwamba Carlos alikula chote. Muda wa kulala sikutaka kulala mwenyewe hivyo nikamfatilia mama ambaye alinisema. "Muda wa kulala unanifatilia tunalala wote ila usiku sana unarudi chumbani kwako, sijui unamatatizo gani wewe mtoto" Sikumjibu na kuendelea kuoatilia tu, kisha tukaenda kulala kama kawaida. Nilipopitiwa na usingizi mzito sikuelewa kinachoendelea ila nilishtuka na kujikuta nikiwa chumbani kwangu, nikakaa pale kitandani, mara nikasikia kama mlango wangu unafunguliwa ila nilipoutazama ulikuwa umefungwa vilevile halafu nikaona kivuli cha mtu karibu na mlango wangu, hapo ndipo nikaanza kuogopa halafu ule mlango ukabamizwa kama vile mtu anaufunga nikazidi kutetemeka maana mlango ulikuwa vilevile ila vitendo tu ndio vilisikika. Kile kivuli kikanifata hadi pale kitandani, nikahisi kuguswa bega ila hakuna mtu niliyemuona kisha sauti ikasikika. "Kesho nakuja kukuchukua mke wangu" Jasho jingi likanitoka, nikainuka pale kitandani ila nikahisi mkono ukivutwa na mtu asiyeonekana tena mikono yake ikiwa ya baridi sana, akanishika shavu na kunibusu. Nikausikia ule mlio wa busu ila mtu haonekani, nguvu zikaniisha na uoga kunijaa kabisa. Machozi yakanitiririka kwavile sikuweza kuongea, nikahisi nikikarishwa chini huku ile sauti ikiendelea kunisisitiza kuwa, "Utake usitake, kesho lazima nikuchukue mke wangu" Nikahisi kama kuzibwa macho kwa kitambaa kwani sikuweza kuona vya mbele tena, halafu baada ya muda macho yangu yakafumbuliwa nikadhani nitaona mandhari nzuri kama siku zote, ila leo nilichokiona ni makaburi, mbele na nyuma yangu kulikuwa na makaburi yani nilizungukwa na makaburi, nipo katikati ya makaburi tena giza. Uoga ulipitiliza, nikawa kama kichaa na kuanza kukimbia hovyo, nilipolipita kaburi moja wapo nikashikwa mguu hapohapo nikaanguka chini. Nilipozinduka kulikuwa kumekucha, nikashangaa kwani nilikuwa chumbani kwangu. Wakati nashangaa pale chumbani, gafla akaingia mama na kuniambia. "Amka ujiandae Sabrina, amekuja kukuchukua" Nikashtuka sana na kuanza kulia.



    Wakati nashangaa pale chumbani, gafla akaingia mama na kuniambia.

    "Amka ujiandae Sabrina, amekuja kukuchukua"

    Nikashtuka sana na kuanza kulia.

    Wakati nalia sauti ikatoka, mara gafla nikaanza kuongea moja kwa moja nikamwambia mama huku ninalia,

    "Sitaki kwenda makaburini mimi"

    "Wewe mtoto unamatatizo gani? Kwani huko makaburini mtaenda kukaa moja kwa moja? Si mnaenda na kurudi tu jamani!"

    Nikashangaa kuona kuwa mama nae anajua kama mwanae natakiwa kupelekwa makaburi halafu yeye anaona ni jambo jema kabisa jamani.

    "Yani mama kweli hunipendi, mwanao naangamia wewe unachekelea?"

    "Wewe ndio hunipendi Sabrina, maana yote haya nafanya kwaajili yako ila ubishi wako unakuponza wewe"

    "Nishasema sitaki kwenda makaburini, sitaki kabisa. Nisamehe kwa hilo mama yangu ila siendi makaburini na huyo mtu"

    Ikabidi mama atoke chumbani kwangu, nikabaki mwenyewe sasa.

    Kwanza nikafurahi kuona naweza kuongea tena kwani swala la kuzibwa mdomo imekuwa ni adhabu kubwa sana kwangu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Nikajigelesha kutoka chumbani huku nikingoja huyo mgeni niliyemdhania kuwa ni Carlos aondoke kwanza.

    Nilikaa sana chumbani bila ya kutoka nje, mara akaja dada Penina chumbani kwangu ila kwa muonekano wake ilionyesha kuwa kuna mahali katoka.

    Moja kwa moja akaanza kuongea na mimi.

    "Sabrina mdogo wangu, dada yako nimepata kazi mpya tena yenye mshahara mzuri zaidi. Jiandae tu kula mema ya nchi"

    "Hongera dada"

    Dada akafurahi sana kusikia naongea, kisha akanishika mkono na kunivutia hadi sebleni.

    Akaanza kumwambia mama,

    "Umeona dawa ya Carlos inavyofanya kazi, Sabrina ameanza kuongea"

    "Najua vizuri kama ameanza kuongea ila kanikera sana Sabrina leo"

    "Kafanyaje tena?"

    Mama akaanza kumsimulia dada kilichotokea,

    "Jana usiku nilipigiwa simu na babamdogo wenu kuwa anapata ndoto mbaya sana toka kwa marehemu kaka yake kuhusu Sabrina, hivyo akaniomba kuwa aje leo amchukue Sabrina ampeleke kwenye kaburi la baba yake wakatambike kidogo. Nilimwambia Sabrina usiku uleule na alikubali kabisa. Cha kushangaza leo asubuhi namfata kanibadilikia na kilio juu basi tena ikabidi nimwambie aende zake tu. Ndio mambo ya mdogo wako hayo"

    Nikawaza na kugundua kuwa leo nimefanyiwa tena mchezo na Carlos kama kipindi kile nilipowafukuza wale watu.

    Dada alikuwa akimsikiliza mama kwa makini sana wakati mimi niliumia kwa mawazo, nikaona kuwa mawazo hayatanisaidia chochote.

    Nikaamua kuongea yanayonisibu maana kuongea niliweza,

    "Mama na dada, nataka kuwaambia ukweli wa kila kitu"

    "Tuambie tukusikilize"

    "Kwa kifupi mimi nasumbuliwa na...."

    Kabla sijaendelea alikuja Carlos na kusimama mbele yangu, nikashtuka sana sababu hakugonga hata mlango.

    Nikashindwa kuendelea kuongea, nikashtukia nikipigwa kibao cha nguvu kwenye shavu, hadi nikainama kwa maumivu.

    Nikashangaa kuona dada na mama wakiwa kimya kabisa, nikajiuliza je hawamuona Carlos au ni vipi?

    Carlos akanishika mkono na kuniburuta hadi chumbani kwangu ila si mama wala dada aliyenifatilia.

    "Nadhani hujaupenda uhuru niliokupatia"

    Machozi yakanitoka tu na maumivu yakajaa moyoni mwangu.

    "Uhuru niliokupa si wa kuropoka, unatakiwa kuwa kimya. Nakupenda sana ila sipendi uwe kinyume na mimi"

    Kisha akaniburuta tena na kunirudisha sebleni tena palepale nilipokaa mwanzo, nilikuwa nalia sana ila mama na dada walionyesha ishara ya kusikitishwa bila ya kunisaidia chochote.

    Muda kidogo Carlos akatoweka na mimi kuendelea kulia, hapo ndipo nikamsikia mama akinipa pole,

    "Pole sana mwanangu"

    Akasogea karibu yangu na kunibembeleza, dada nae akasema,

    "Hawa watu watammaliza mdogo wangu jamani, lini wataacha kumuumiza?"

    Mama nae akaendelea kunibembeleza huku akisema,

    "Dawa yao inachemka, yani huyu Zuhura na Salome wake wananitakia mabaya mimi"

    Nikajua moja kwa moja mama na dada watakuwa wamepokea ujumbe tofauti palepale, kwakweli huyu Carlos sijui ana nia gani na mimi na sijui huwa anafanya vitu gani hadi kugeuza maneno mpaka maneno yake ndio yanaaminika kushinda yale ya ukweli.

    Nililia sana pale hadi kupitiwa na usingizi tena.



    Mchana wa leo kaka Deo aliwasili akiwa na wifi Joy maana mama alimwambia aje nae, najua wifi Joy hakuweza kukataa ingawa alijua ni kitu gani wameitiwa.

    Nikawakaribisha ndani, nao wakaingia kama kawaida. Kaka Deo hakuonyesha tofauti yoyote ile, alikuwa kawaida tu.

    Mama na dada walikuja na kuanza maongezi, mtoto James alikuwa amebebwa na kaka.

    Baada ya salamu, mama akaanza kuongea,

    "Unamuonaje mtoto uliyembeba?"

    "Huyu James mama? Aah ni mtoto mtundu sana huyu"

    Na kweli alikuwa mtundu maana hakutulia kabisa. Mama akaendelea kuongea,

    "Anafanana na wewe eeh!"

    Kaka akacheka na kusema,

    "Kafanana na wajomba zake huyu"

    Mama na dada wakacheka sana,

    "Ndio unavyodanganywa na mkeo hivyo? Ngoja tukwambie ukweli sasa"

    Wifi akakohoa na kupaliwa hadi akakimbilia nje, nami nikamfata kwa nyuma kwani nilihofia kuwa anaweza akafanya maamuzi mabaya.

    Wifi alikaa chini na kutokwa na machozi, nikakaa nae kumbembeleza,

    "Natamani nikimbie nikafiche sura yangu"

    "Usifanye hivyo wifi, kila kitu kitakuwa sawa"

    Wifi akainuka, na kutaka kuondoka, nikamshika mkono kwa kumzuia.

    "Utaenda wapi wifi? Fikiria maisha ya mtoto mdogo James asiyekuwa na hatia"

    Wifi akanitazama kwa jicho la huruma sana na kusema,

    "Bora nikimwifi yangu"

    "Usifanye hivyo wifi, mimi natakutetea hadi kaka akusamehe"

    "Deo hawezi kunisamehe"

    "Niamini mimi wifi yangu"

    Wifi aliendelea kulia tu, na muda huohuo kaka alitoka ndani akiwa na hasira sana,

    "Yani Joy unakaa na mimi ndani hata kuniambia ukweli hukutaka? Leo nimeamini, kweli siri ya mtoto aijuaye mama, yani siku zote naamini James ni mwanangu kumbe sio! Haya niambie baba wa mtoto ni nani haraka sana"

    Kaka akamvuta wifi hadi sebleni tena, muda huohuo Carlos nae akawasili na kuingia ndani.

    Wifi alikuwa analia tu bila ya kujibu swali la kaka, Carlos akapatia pa kusemea yake hapohapo

    "Huyo mtoto ni wa James, yani jina la mtoto ndio jina la baba yake. Ni mwalimu wa kwaya anayoimba Joy"

    Kaka Deo akazidi kupandwa na hasira na akakumbusha maneno ya wifi wakati aliposema kuwa mtoto aitwe Deo na sio James,

    "Ndiomana nilipokwambia ataitwaje Deo Deo ukasema ndio inapendeza kumbe unaogopa kuwa ataitwa James James! Nilikukataza sana hizo kwaya Joy lakini hukunisikia. Nadhani umefurahia kupata mtoto wa muimbaji mwenzio. Yani siamini kabisa kama wewe Joy ungenifanyia hivi"

    Kaka akaondoka kwa hasira na kumuacha wifi Joy na mtoto pale nyumbani, wifi alilia sana kwavile hakujua cha kufanya.

    Mama na dada nao bila ya huruma wakamtimua wifi Joy pale ndani.

    Wifi akatoka na mtoto wake huku akilia sana, nilimuonea huruma malaika huyu asiye na kosa na wala hajui chochote maskini mtoto mdogo James.

    Nikamfata wifi kwa nyuma kumbe Carlos nae akatufuata.

    Wakati tupo pale nje na wifi, akashikwa bega na Carlos kisha akamwambia

    "Naweza kukusaidia Joy ila kwa sharti moja"

    Nikawa namkataza wifi kukubali msaada wa Carlos maana najua kuwa lazima utakuwa na madhara tu, ila muda huo mama nae akanivuta na kunirudisha ndani.

    Nikachungulia dirishani na kumuona wifi akiondoka na Carlos, nikamuonea huruma sana kwani najua yote ni sababu ya kushindwa cha kufanya.



    Jioni ya leo haikuwa njema kabisa kwangu kwani mawazo yalinitawala kupita maelezo. Kila nikifikiria msaada alioahidiwa wifi Joy na Carlos ndio nilizidi kuumiza kichwa kabisa.

    Hata muda wa kula chakula cha jioni ulipofika sikuwa na raha wala hamu ya kula, nikaenda kukaa chumbani kwangu nikatumiwa ujumbe na Carlos

    "Yani wewe Sabrina ni mjinga sana, mimi nimejitolea kumsaidia wifi yako ila bado wewe unachukia hadi kula unashindwa. Kwani wifi yako nimemsingizia? Si kweli amefanya? Na kila mwenye kosa lazima aadhibiwe, mimi si mtu mbaya ila nawarekebisha wale wanaojifanya wema kumbe wanaubaya ndani yake. Ila usijari, umegoma kula nitakuja kukulisha ndotoni"

    Nikaanza kuogopa niliposoma ndotoni ukizingatia mambo ya kwenye ndoto yalikuwa ni mtihani kwangu, nikaona vyema niende kukaa sebleni a wenzangu. mamam akaniuliza,

    "Nilijua umelala"

    "Hapana mama nipo macho"

    "Bado unamsikitikia Joy? Mwache ale jeuri yake, kumsingizia mtu ujauzito si jambo jema kabisa"

    Nilikuwa kimya kabisa nikiendelea na masikitiko yangu, badae tukaenda na mama kulala kama kawaida.



    Tukiwa chumbani nikajisemea kuwa leo silali ili huyo Carlos asinichukue kizembe kama kawaida yake, nikatulia kimya kabisa kitandani na mama alikuwa hoi na usingizi ila mimi nikaanza kujiimbisha imbisha ili kujitoa na dhana ya uoga.

    Gafla nikasikia sauti,

    "Sauti yako ni nzuri sana Sabrina, unaniburudisha sana na hizo nyimbo mke wangu"

    Hapo pa kusema mke wangu pakanishtua sana na kuondolea ujasiri nilionao, nikajikia kusema neno hili na nikalisema kwa sauti kubwa

    "Mimi sio mke wako"

    Ile sauti ikaendelea,

    "Yani unanikana Sabrina?"

    "Ndio, nakukana sina mume jini na siwezi kuolewa na jini"

    Nilishangaa ujasiri huu ulitoka wapi wa kuongea na mtu asiyeonekana. Naye akaendelea kusema,

    "Wewe ni mke wangu Sabrina au kwavile hatujafunga ndoa?"

    "Siwezi funga ndoa na jini"

    Gafla nikainuliwa juu, nikapiga kelele lakini hakuna aliyesikia, halafu ile sauti ikaongea tena

    "Sikutaka kuharakisha hivi maswala ya ndoa ila utaolewa na mimi kinguvu"

    Huku akicheka sana, mara nikajiona kwenye mazingira tofauti na nyumbani halafu nimevaa shela kubwa, mbele yangu akatokea yule kijana wa ndotoni akiwa amependeza sana, akaanza kunisogelea nilimwangalia huku natetemeka.

    Nikageuka nyuma na kuanza kukimbia.



    Akaanza kunisogelea nilimwangalia huku natetemeka. Nikageuka nyuma na kuanza kukimbia. Na yeye alikuwa akinikimbiza kwa nyuma, lile gauni la harusi niliona linanipa uzito kwenye kukimbia ila nilipojaribu kulivua halikuvuka halafu yule kijana wa ndotoni alikuwa karibu yangu, alipotaka kunidaka tu nikaanguka chini na kuzimia. Sikujua kilichoendelea ila nilipozinduka nilikuwa chumbani kwa mama halafu mama nae yupo pembeni yangu ambapo alishtuka sana baada ya kuniona kuwa nimeshtuka kwa nguvu huku jasho jingi likinitoka tena nikihema kwa nguvu sana. Mama akaniuliza, "Una nini mwanangu" "Ndoto mama, nimeota naolewa" "Mbona ni jambo la kheri tu hilo mwanangu, kwani wewe hupendi kuolewa?" "Napenda mama ila napenda niolewe na Sam" Mama akachukia sana nilipotaja Sam na kuinuka pale kitandani, "Kwanza kumekucha, amka tukaendelee na majukumu mengine" Nikajinyoosha pale na kuamka, moja kwa moja nikatoka nje ya nyumba nikashangaa sana kumuona Sam nje ya nyumba yetu "Khee Sam, umefata nini asubuhi yote hii?" "Nimekufata wewe Sabrina, sipo tayari kukupoteza" Nikatamani nimkaribishe ndani ila najua mama atamtimua tu kwavile nimemwambia kuwa napenda kuolewa na Sam hivyo nikaamua kumwambia aningoje nyuma ya nyumba ili niweze kuongea nae vizuri. Nikaingia ndani na kuchukua fagio la chelewa kisha nikamwambia mama kuwa naenda kusafisha nyumba. "Leo maajabu, naona ndoto ya kuolewa imekukumbusha majukumu yako kama mwanamke, ni vizuri sana mwanangu nenda ukafagie" Mama hakujua kama nia yangu ni kuzungumza na Sam huko nje, nikamkuta Sam akinisubiri "Eeh niambie Sam" "Naomba tutoroke Sabrina" "Twende wapi?" "Popote pale, nimekuotea ndoto mbaya sitapenda itokee kabisa." Nikajaribu kumdadisi ni ndoto gani ili nijue, "Nimeota unaolewa na mtu wa ajabu sana Sabrina, bora tutoroke" "Naafikiana na wewe Sam, mi mwenyewe sitaki kuolewa na yeyote zaidi yako ila mama akijua nimetoroka itakuwaje?" "Wazazi na ndugu zako wamefungwa kwasasa hawajielewi, bora tutoroke mambo yakiwa shwari tutawapa habari" Nikaona wazo la Sam kuwa zuri sana kwangu ukizingatia nimeshachoshwa na mambo ya ajabu yanayonitokea kila siku. Nikataka kupanga jinsi ya kutoroka ila Sam akaniambia kuwa kama nikipanga basi lazima Carlos atanizuia au atafanya chochote kunizuia nisitoroke. Nikamwambia Sam kuwa inatakiwa nioge kwanza na kujiandaa ila Sam akasema kuwa ni kupoteza muda sababu ukipatwa na wazo la kufanya kitu fulani kwa watu hao ni lazima kuwawahi kabla hawajashtukia kama unapanga kitu. "Jamani Sam ndio niondoke hivi? Ngoja nikaoge bhana" Ikabidi Sam akubaliane na mimi kuwa nikaoge kwanza. Nikaenda ndani na kuoga kisha kuvaa nguo zangu kama kawaida. Kisha nikachukua nguo mbili tatu za kuondoka nazo, nikaweka kwenye mkoba wangu. Wakati nataka kutoka chumbani nikasikia sauti, "Unanikimbia mke wangu?" Nikaona uzushi wa mauzauza umeanza sasa, sikuijali ile sauti. Nikatoka hadi sebleni na kumtafuta mama ili nimuage kwa uongo ila hakuwepo pale, mara simu yangu ikaingia ujumbe kutoka kwa Carlos "Unaenda wapi Sabrina?" Nikaona uzushi sasa, cha muhimu ni kuiacha ile simu pale pale nyumbani. Nikamuangalia mama hakuwepo sebleni wala jikoni, nikajua yupo chumbani tu. Nikatoka nje kwanza kuficha mkoba wangu kisha nikaenda chumbani kwa mama ili nimuage, nikamkuta mama ameanguka chini huku damu zikimtoka, sikuwa na msaada zaidi ya kwenda kumuita Sam ili anisaidie kwakweli nilichanganyikiwa kabisa. Mimi na Sam tukajitahidi kumtoa mama hadi sebleni, Sam akaamua kwenda barabarani kufata gari ili tumuwaishe mama hospitali. Nilichanganyikiwa kabisa kwani sikujua kuwa mama amepatwa na kitu gani, muda kidogo akatokea Carlos pale sebleni huku akitabasamu na kusema "Sabrina, Sabrina! Utaenda wapi na kumuacha mama yako katika hali hiyo?" Akacheka kidogo, kwavile nilikuwa na tatizo tayari nikaanza kumuomba Carlos msaada. "Nisaidie Carlos nisaidie nakuomba" "Mimi kukusaidia wewe ni lazima, ila kwanini ulitaka kunitoroka?" Nilikuwa kimya huku nikiwaza kuwa Sam nae amekwamia wapi kuleta gari maana alikawia kurudi. Carlos akaniambia, "Nenda nje Sabrina ukamuangalie unayemuwaza" Uoga ukanishika kuwa Sam nae atakuwa amepatwa na nini, sasa nimuache mama nikamuangalie Sam bado nikawa njiapanda. Carlos akasema, "Unawaza nini Sabrina? Ulipokuwa unapanga kutoroka na Sam halafu kumuacha mama yako hukufikiri? Nenda kamuangalie Sam nami nimuhudumie mama yako" Maneno ya Carlos yalikuwa yananichanganya sana, nikainuka na kwenda kumchungulia Sam ila haikuonekana hata dalili yake, nikaona ni vyema nikachukue simu ili nimpigie na kumuuliza alipo. Nikarudi tena ndani, ila mama alikuwa amekaa kwenye kiti tena akiwa mzima kabisa nikashtuka sana maana hata Carlos hakuwepo tena, nikajiuliza kuwa amepitia njia gani nikakosa jibu kabisa, nikawa nimesimama huku nikimshangaa mama, nikamfata na kwenda kumshika kama ni mama kweli kumbe naye alikuwa ananishangaa "Una nini wewe Sabrina?" "Inabidi mimi nikuulize wewe mama, ni mzima kweli mama yangu?" "Kwani ninatatizo gani?" Nikamuangalia vizuri mama kuona zile damu zilizokuwa zinamtoka hazikuwepo tena wala alama ya damu haikuwepo yani ilikuwa kama mazingaombwe kwangu. "Mama, si ulikuwa unaumwa wewe?" "Mgonjwa ni mimi au wewe? Nakuona wewe ndio upo kama chizi maana unajiangaisha tu mara chumbani mara nje mara wapi hata hujielewi, kaa utulie mwanangu" Nikamuangalia mama mara mbili mbili hata cha kuuliza nilikosa, nikajua huo ni mchezo tu uliofanywa na Carlos ili nisiweze kutoroka na Sam kama nilivyopanga. Nikachukua simu ili kumueleza Sam mambo yaliyojiri ila nikakutana na ujumbe kutoka kwa Sam "Yani huwezi amini Sabrina, eti nyumba yenu imenipotea" Nikajaribu kumpigia simu lakini hakupatikana, kwakweli huyu Carlos alishafanya yake kunichanganya tu. Nikaenda chumbani kwangu huku nikiwaza mambo mengi sana, muda kidogo dada Penina alirejea nyumbani na kuja moja kwa moja chumbani kwangu, alinikuta nikiwa na mawazo sana ila hakutambua hilo kwa haraka, moja kwa moja alikuja kunionyesha picha na kusema "Angalia picha ya gauni lako la harusi nimepewa na Carlos" Ile picha ya gauni ilinishtua sana kwani ilikuwa ni gauni lile lile nililovishwa ndotoni, dada akaniuliza "Mbona umeshtuka sana?" "Hakuna kitu dada" "Karibu tutasherekea, gauni hili ni la gharama sana, kwakweli Carlos anakupenda Sabrina. Ngoja nikamuonyeshe mama" Dada akainuka na kutoka nje bila ya kujua nafikiria kitu gani pale aliponiacha. Wazo la kutoroka likanijia kwa kasi sasa kupita hata nilivyopanga na Sam. Nikajaribu kumpigia tena Sam, safari hii alipatikana. "Sam, tufanye sasa kile ulichopanga" "Mama anaendeleaje Sabrina?" "Nitakwambia, ila niambie ulipo nikufate sasa" "Huwezi amini, muda huu ndio nipo nje kwenu" Nikafurahi sana, kisha nikaiweka ile simu yangu kitandani kwani nilijua kutembea nayo itanisababishia matatizo zaidi. Nikatoka chumbani na kumkuta dada na mama wakifurahia ile picha ya gauni la harusi, "Mama, nafika hapo dukani mara moja" "Umeliona gauni lako lakini?" Nikaitikia kwa kichwa kuwa nimeliona, mama akasema, "Nitamwambia Carlos alilete ili ulijaribu tukuone" Dada Penina nae akafurahi na kumsapoti mama, halafu mimi nikaenda zangu. Kama nilivyoongea na Sam, kweli nikamkuta nje ya nyumba yetu kisha nikachukua mkoba wangu nilipouficha halafu tukaondoka. Safari ya kwanza ilikuwa moja kwa moja kwa Sam kisha tukakaa na kupanga pa kwenda. "Hatutakiwi kuwa hapa Sabrina maana hapa watakuja tu" "Naelewa Sam" Tukapanga Kulala hapo leo halafu kesho tusafiri na kwenda mkoani. "Ila huko mkoani tutaenda kwa nani jamani Sam?" "Kuna ndugu zangu wengi tu, nitakupeleka huko ukakae kwa muda kabla sijafanya maarifa mengine" "Vipi na kazi yako Sam?" "Nilipofungwa nikafukuzwa na kazi kwahiyo sina kazi kwasasa ila nilipotoka jela ofisi ikanipa kiinua mgongo ndiomana nimeona bora tutumie hii pesa kwenda mkoani kubadili maisha yetu" Nilimsikiliza Sam kwa makini sana na kumuelewa maana sikujua yaliyotukia tangu ametoka jela, kisha nikamsimulia kuhusu kilichotokea nyumbani. "Ndiomana nimehangaika sana maana nimefika na gari ya kukodi eti nyumba imepotea, tukahangaika sana na yule dereva bila mafanikio hadi yule dereva akachukia na kuondoka, nikabaki mwenyewe kupatafuta nyumbani kwenu halafu muda ule unapiga simu ndio napapata" "Pole sana Sam mpenzi wangu" Kisha nikamkumbatia, kwakweli siku ya leo ilikuwa ya furaha sana kwangu kwani nilijisikia raha kuwa karibu na mpenzi wangu Sam. Jioni yake nikiwa chumbani kwa Sam nikashtuka kuona simu yangu kitandani kwa Sam wakati niliiacha nyumbani. Nikamuita Sam kuona na yeye. "Ona hii simu Sam, niliiacha nyumbani jamani" "Mmh Sabrina labda umepoteza kumbukumbu" Sam akaichukua ile simu na kuiangalia kisha akanipa na kusema, "Tena kuna ujumbe umetumwa" Nikachukua na kufungua, ulikuwa umetoka kwa Carlos ukisema, "Umetoroka Sabrina, ila nitakukomesha leo" Nikaogopa na kumuonyesha Sam, kwakweli naye akashtuka na kusema, "Hapatufai hapa Sabrina, tuondoke." "Tutaenda wapi sasa?" "Twende kwenye nyumba za kulala wageni ili kesho tusafiri" Sikutaka kupoteza muda, tukajiandaa haraka na kuamua kuondoka ila simu yangu niliiacha pale pale chumbani kwa Sam. Tukapata chumba maeneo ya karibu na stendi kuu, ikawa vyema kwetu kwani itasaidia wakati wa kusafiri. Tukakaa na kuongea mengi sana, kisha kwenda kula chakula cha usiku ili kuwahi kupumzika kwaajili ya safari ya kesho. Tulipotoka kula nikashtuka kuona tena simu yangu ikiwa kitandani, "Sam, haya maajabu. Hii simu inanifatilia" Sam akachukia sana kuiona na kusema kuwa isitusumbue, kisha akaichukua na kwenda kuitupa chooni kisha akamwagia na maji ikaenda, roho iliniuma ila ni bora kuliko kukaa na simu ya maajabu kama ile. Tulirudi chumbani na kupumzika, Sam akapitiwa na usingizi mapema sana kupita maelezo kisha na mimi nikalala. Nikaanza kuota ndoto za ajabu ajabu yani kamavile nakabwa na majinamizi, kisha nahangaika sana na mwisho nikashtuka huku nikihema kupita maelezo, nikajisikia kunywa maji yaliyokuwa kwenye chupa mezani. Nikainuka ili nichukue nikakuta ile simu yangu ikiwa mezani. Uoga ukanijaa moyoni, nikamuamsha Sam wala hakuitika nikaanza kusikia sauti ya kicheko halafu gafla ikawa kama ilivyokuwa jana yake, nilijiona nimevishwa gauni la harusi na kuanza kuogopa halafu akatokea yule kijana wa ndotoni ila leo ilikuwa mulemule nilipolala na Sam, akaenda moja kuwa moja na kumkaba Sam nikamkimbilia kumtoa ila alinipiga kibao hadi nikazimia. Nilipozinduka nilijiona nipo nyumbani tena chumbani kwangu kitandani, nikainuka kwa uoga nilikuwa nimevaa lile gauni la harusi, nikajaribu kulivua ikashindikana, nikakimbilia sebleni ambapo nilikuta watu wengi halafu wakaanza kunipigia makofi.





    Nilipozinduka nilijiona nipo nyumbani tena chumbani kwangu kitandani, nikainuka kwa uoga nilikuwa nimevaa lile gauni la harusi, nikajaribu kulivua ikashindikana, nikakimbilia sebleni ambapo nilikuta watu wengi halafu wakaanza kunipigia makofi. Nikashtuka sana kwani ni kitu ambacho sikukitarajia kabisa, Carlos alikuwa mbele yangu amevaa suti nikajiuliza hivi naota au ni kitu gani maana sikuelewa kitu jamani. Dada na mama nao walikuwa wamependeza sana tena huku wakifurahia kile kitu. Walikuwepo marafiki zangu na baadhi ya ndugu zangu na wale ndugu wa Carlos, nikajiuliza yote yale yamepangwa muda gani? Nikajihisi kuwa nipo ndotoni. Wakati nikiendelea kushangaa, Carlos alinisogelea na kunishika mkono kamavile maharusi wafanyavyo, nikamtoa ule mkono na kumkimbilia mama yani hata sikujielewa na sikutambua kama ni ndoto au ni kitu gani, nikamuuliza mama "Kwani kuna nini?" "Swali gani hilo Sabrina? Kwani hujui kama unaenda kuolewa na Carlos?" "Sitaki kuolewa na Carlos mama sitaki" Mama akanivuta pembeni na kuanza kuniambia, "Hutaki kivipi wakati ulikubali mwenyewe jana mbele ya wajomba zako" Nikaanza kulia na kumwambia mama kuwa sitaki, "Acha kulia mwanangu utaharibu vipodozi ulivyopakwa jamani, ona ulivyopendeza halafu unataka kujichafua kwa machozi. Kama usingetaka kuolewa si ungesema tangia jana kwenye kikao! Unaona ushapendeza ndio unaleta mauzauza yako, hebu tulia mwanangu" Huyu mama nae alikuwa ananichanganya kabisa hiyo jana ipi wakati nilitoroka? Kumbukumbu zangu ni kuwa mara ya mwisho nilizimia nikiwa nyumba ya wageni na Sam, sasa nyumbani nimefikaje? Nikahisi labda naota kwakweli. Carlos akanisogelea na kunitoa mkono pale kwa mama na kuongozana na na mimi hadi nje, nikawa naangaza macho huku na kule kuwa labda nitaamka kwenye ile ndoto lakini haikutokea hivyo. Tukapanda kwenye gari na safari ikaendelea hadi kwenye jumba moja kubwa sana, mama na watu wengine wakabaki nje kisha mimi na Carlos tukaingia ndani ya lile jumba, kwakweli hii ilikuwa ni ndoto kwangu tena ndoto isiyo na mwisho na sikujua ni muda gani nitaamka kwenye ile ndoto maana nilipumbazwa sana. Ndani ya lile jumba kulikuwa na watu wa ajabu sijawahi kuwaona duniani, wote walivaa nguo nyeupe kabisa tena zinazong'aa kwakweli niliogopa ila nilikuwa najishangaa pia sababu sikuweza kufanya chochote, wale watu walinizunguka mimi pamoja na Carlos tukawa katikati halafu wao walikuwa wakicheza kwa duara huku wakizunguka zunguka kwa kupishana. Niliyastaajabu yote yale yanayotukia mbele ya macho yangu. Muda kidogo watu wale waliokuwa wakicheza cheza, waliacha kucheza na kurudi nyuma kidogo mara gafla Carlos akabadilika na kuwa kijana wa ndotoni, wale watu wakapiga makofi na kushangilia huku wakiongea maneno ambayo sikuyaelewa kabisa, nikaogopa sana kumtazama yule kijana wa ndotoni, nikajiziba macho kwa mkono nilihisi kuchanganyikiwa kwakweli. Yule kijana akautoa mkono wangu kwa nguvu huku akitabasamu na kusogea kwangu kama ananinong'oneza, "Leo ni siku yetu ya ndoa Sabrina" Nikatokwa na machozi na wala sikuamini macho yangu kama kile kitu kinatukia kweli. Akaniambia tena, "Tafadhali usiniaibishe kwa ndugu zangu" Kisha akanishika mkono na kunitoa upande wa pili wa lile jumba ambako hapakuwa na mtu yeyote zaidi ya mimi na yeye, machozi yalinitoka kamavile napelekwa machinjioni, nikatamani hata kumuona Carlos kuliko huyu mtu niliyemuona mbele yangu kwani alinitisha sana, gafla mavazi yake yakabadilika na kuwa mavazi ya ajabu halafu wakatokea watu sita wenye mavazi kama yake kisha yeye akatoweka mbele yangu na kufanya nishtuke sana, sauti ikasikika "Mchague mumeo kati ya hao sita" Wote walifanana, sikuweza kuchagua kwakuwa hakuna nimtakaye kati yao, nikaendelea kulia tu, halafu yule kijana wa ndotoni akatokea tena na kuniambia, "Umeshindwa kuchagua, kwahiyo mimi ndio mumeo. Unanipenda mimi Sabrina" Halafu akaongea kwa nguvu maneno ambayo sikuyaelewa, gafla wakajaa wale waliovaa nguo nyeupe huku wakicheza cheza zaidi na kufurahi. Macho yangu yalijaa machozi sikujielewa kabisa, gafla akatokea kiumbe wa ajabu anayeweza kuruka na kutua kama ndege akasimama mbele yetu, akatoa kitambaa chekundu na cheupe, halafu akaja mtu mwingine mwenye umbo la kike na kunifunga vile vitambaa, kimoja nikafungwa kwenye paji la uso na kingine shingoni halafu yule kijana wa ndotoni nae akafanyiwa vilevile. Sikuweza kuvumilia zaidi kwakweli, nikajikuta nikianguka chini na kuzimia maana wale watu walikuwa wa ajabu sana. Nilipozinduka, nilikuwa kwenye chumba kilichojaa mapambo ya kila aina na harufu mbalimbali za marashi haswa ile harufu ambayo mara nyingi huwa naisikia chumbani kwangu, mzee mmoja mwenye sura ya ajabu akaja mbele ya sura yangu na kunichekea, nikaogopa sana na kuanza kulia ila sauti haikutoka hata kidogo zaidi ya machozi tu, yule kijana wa ndotoni akaja na yeye mbele yangu na kunichekea pia huku akisema, "Usishangae sana, hapa ndio pa kuishi mimi na wewe" Machozi yalizidi kunitoka bila mwisho hadi nikazimia tena. Nilipozinduka safari hii nilikuwa nyumbani tena chumbani kwangu kitandani yani kamavile nimeamka toka usingizini. Nikainuka na kukaa kitandani kisha nikajiuliza, yaliyotukia ni ndoto au ni ukweli? Nikaanza kuangaza chumba changu, nikaona bahasha mezani nikainuka kuichukua kisha nikaifungua, nikakuta ni picha za harusi ya mimi na Carlos nikashtuka sana na kujiuliza kuwa kumbe ni kweli!! Nikaangalia kwenye kiti chumbani kwangu, nikaona lile gauni la harusi na viatu vikiwa pembeni yake nikajisemea, "Hapana, itakuwa bado naota tu" Nikatoka hadi sebleni, nikamkuta mama amekaa nikamfata na kumgusa kwa kumuita, "Mama" "Khee mwanangu umeamka? Pole kwa uchovu jamani, nakushukuru kwa kutokunitia aibu zaidi ile jana" Nikamuuliza kwa mshangao, "Inamaana ni kweli mama?" "Kweli nini?" "Kuwa mimi nimeolewa?" "Ndio, umeolewa na Carlos mwanangu. Inamaana umepoteza kumbukumbu?" Sikuamini kabisa, nikamwambia mama "Hapana haiwezi kuwa kweli, haiwezekani mama haiwezekani kabisa" Nikainuka na kukimbilia tena chumbani, mama akaja kunibembeleza "Nyamaza mwanangu ila ulikubali mwenyewe, wewe ni mke wa mtu kwasasa" "Hapana mama huku nikizidi kulia" Dada Penina nae akaja chumbani kwangu na kumuuliza mama kuwa tatizo ni nini, "Hata mimi mwenyewe sielewi jamani, jana tumesherekea hadi kalala hoi eti leo analia kwanini ameolewa" "Itakuwa wakina Zuhura hao wanamchanganya mama" Kisha akaenda kuchukua dawa na kuniletea, zilikuwa ni dawa za usingizi nikanywa huku nikijipa matumaini kuwa nitakapoamka tena hali itabadilika. Wakati nimelala nikaanza kuonyeshwa matendo yote yaliyofanyika nyuma, ilikuwa kama naangalia kwenye video vile: Nilikuwa na Sam asubuhi kabisa akiniambia kuhusu kutoroka, kosa nililofanya ni kwenda ndani kujiandaa. Maeneo yote yenye makosa ilitokea rangi nyekundu. Nikiwa najiandaa ndani, Carlos alinisogelea bila ya kumuona kisha akanipulizia kitu usoni ndipo nikatoka na kuanza kumtafuta mama, akaniwekea kitu nimuone mama kazimia kumbe hakuwa mama lilikuwa gogo tu ila mama alikuwa pembeni pale sebleni bila ya kuona chochote. Wazo la kutoroka liliponijia tena, nilibeba leso niliyowahi kupewa na Carlos hapo ikawa ni kosa pia. Nilipofika na Sam nyumbani kwake kisha kuiona simu yangu na kusoma ujumbe uliotumwa ikawa ni kosa pia kumbe ndio nilizidi kujichanganya mimi pamoja na Sam pia. Hadi muda tunaenda nyumba ya wageni,Carlos alikuwa nyuma yetu akitufatilia bila ya sisi kujua chochote, na swala la kukimbilia nyumba ya kulala wageni ilikuwa ni kosa pia. Kitendo cha kuitupa ile simu chooni kilimkera zaidi Carlos, muda wote huo ambao nilikuwa mbali na nyumbani kumbe kulikuwa na Sabrina mwingine nyumbani kwetu aliyewekwa na Carlos, yeye ndiye aliyekubali swala zima la kufunga ndoa na Carlos. Nikamuona yule Sabrina mwingine akifurahia na kuchekelea, ndugu zangu wote walijua ni mimi kumbe ni kiini macho kilichofanywa na Carlos. Yote nilikuwa nayaona ndotoni kamavile naangalia picha. Nilipozimia kwenye nyumba ya wageni, nilirudishwa nyumbani kimaajabu na kuvishwa nguo ya harusi na Carlos. Muda ambao nilishtuka ndio muda huo yule Sabrina mwingine alijifanya ameingia ndani kuvaa gauni la harusi ndiomana nilipotoka wakanishangilia wakijua ni mimi muda wote. Wakati tumeingia kwenye jumba lile la ajabu kumbe ndugu zangu wote hawakuelewa chochote maana waliachwa nje. Na baada ya ndoa, alitoka yule Sabrina mwingine kusherekea nao. Swali ni kuwa ndugu zangu hawakushtuka kuona ndoa inafungwa tukiwa wawili tu kwenye jumba na wenyewe kubaki nje? Mwishoni akatokea yule mkaka wa ndotoni na kusema "Wewe ni mke wangu sasa Sabrina" Nikamuuliza kwa mara nyingine tena swali hili "Wewe ni nani?" Akacheka na kujibu kwa kujiamini kabisa, "Mimi ni jini" Nikashtuka kutoka kwenye ile ndoto na kujisemea "Kumbe nimeolewa kweli!" Sauti ikasikika , ikawa kama vile ananijibu "Tena na jini" Nikatetemeka sana, kwakweli hii ndoa sikuitarajia kabisa ila imenijia kiajabu, nikakaa na kuanza kulia tena. Dada Penina alikuja chumbani na kuniuliza tena, "Jamani mdogo wangu hunyamazi? Kwanini lakini?" Huku nikilia zaidi nikamwambia dada, "Nimeolewa na jini bila ya kutarajia" "Unamaanisha nini Sabrina?" Nikataka kurudia tena, ila kabla sijarudia Carlos alikuwa mbele yangu.





    Huku nikilia zaidi nikamwambia dada,

    "Nimeolewa na jini bila ya kutarajia"

    "Unamaanisha nini Sabtina?"

    Nikataka kurudia tena, ila kabla sijarudia Carlos

    alikuwa mbele yangu.

    Nikatetemeka maana nilimwogopa sana Carlos

    kwasasa kwani bado akili yangu haikunipa jibu kuwa

    yule wa ndotoni ni nani na Carlos ni nani? Na kwanini

    akija kwetu anajitokeza kama Carlos halafu kwenye

    ndoto anakuwa mtu wa ajabu?

    Nikawa natetemeka na kumshtua dada ila yeye

    hakumuona Carlos zaidi ya mimi tu, dada akaniuliza

    tena

    "Mbona huendelei kusema ulichokuwa unasema?"

    Carlos akajibu,

    "Nimesema kuwa nimeolewa na Carlos bila ya

    kutarajia"

    Dada akajua ni mimi ninayeongea hata sikujua

    inakuwaje hadi kuwa vile ilivyo wakati mimi nipo

    kimya kabisa, dada nae akasema.

    "Ndio Carlos amekuoa kwa surplise kwakweli,

    hakuna aliyetarajia ilikuwa gafla sana. Ila mbona

    mwanzoni nimekusikia ukisema kama jini vile au

    masikio yangu tu?"

    Nikataka kumjibu dada ila Carlos akajibu kabla yangu,

    "Umesikia vibaya ndio maana mwanzoni nimesema

    kuwa nimeolewa mimi bila ya kutarajia"

    Dada akaendelea kuongea pale bila ya kujua kuwa

    anayeongea nae ni Carlos na sio mimi ila tu sikuwa

    na la kufanya kabisa, kisha dada akainuka na kutoka

    nje, Carlos akakaa alipokaa dada na kunichekea.



    Uwepo wa Carlos asiyeonekana na wengine mbele

    yangu uliniogopesha sana. Nikajaribu kuinuka ili

    nitoke lakini nilishindwa kwani ilikuwa kama

    nimepakwa gundi, nikamuangalia Carlos kwa jicho la

    uoga halafu akanishika bega ambapo nilitetemeka

    zaidi kwani ile mikono yake leo ilizidi ubaridi, kisha

    akasema

    "Huweza kuinuka hapo bila ruhusa yangu, mimi ni

    mumeo sasa"

    Huku nikitetemeka nikamwambia,

    "Naomba niinuke basi"

    "Mimi ni mume wako, huwezi ukaomba ruhusa kwa

    mumeo kama unamuomba mtubaki, unatakiwa uombe

    kwa unyenyekevu huku ukitaja cheo changu kwako"

    Nikawa kimya nikitetemeka, akaniangalia kwa jicho

    kali sana huku akicheka kisha akasogea karibu yangu

    zaidi na kutaka kunibusu, nikainamisha kichwa chini

    na kurudia yale maneno niliyoyasema mwanzo.

    "Naomba ruhusa ya kuinuka hapa"

    "Taja cheo changu kwako, mimi ni mumeo sasa.

    Unatakiwa ufate vile ninavyosema"

    Nikamuangalia Carlos kwa uoga bila ya kusema

    chochote, kisha akaniambia kwa nguvu

    "Sema mume wangu"

    Nikashtuka na kusema bila kutegemea,

    "Mume wangu"

    Naye akaitikia,

    "Eeh niambie mke wangu"

    Nikiongea kama mtu anayejifunza kuongea,

    "Naomba ninyanyuke"

    "Haya nyanyuka mke wangu"

    Nilipoinuka moja kwa moja nilikimbilia sebleni huku

    nikihema sana na kujiuliza maswali bila ya majibu.







    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog