Sehemu Ya Nne (4)
Ibra aliichukua ile barua na kuanza kuisoma kwa makini kwani maneno yake yalikuwa machache sana na yaliyoeleweka.
“Najua mnapenda sana watoto, tafadhari nawaomba mumlee mtoto huyu mfanyeni kama mtoto wenu make nae vizuri. Msimfokee na wala msithubutu kumpiga, tafadhari sana msimtupe mtoto huyu. Asante”
Ibra akatazamana na mke wake kwani ilikuwa ni kitu cha ajabu kilichowapa maswali mengi sana kwani walijiuliza kuwa ni nani anaweza kuwawekea mtoto kwenye buti la gari ila wakakosa jibu, wakati wakitafakari hilo yule mtoto alianza kulia tena na kumfanya Sophia huruma imjae na kumuinua yule mtoto kisha kuelekea ndani huku akifatwa na mume wake, Sophia alifanya kazi ya kumbembeleza yule mtoto na kuhisi kuwa huenda ni njaa iliyomfanya alie vile,
“Inatakiwa tumtafutie maziwa mume wangu”
“Itabidi tufanye hivyo, ngoja nikaangalie madukani huko”
Ilibidi Ibra atoke na kumuacha Sophia akihangaika kumbembeleza yule mtoto ambaye alilia tu mfululizo bila kunyamaza na kumfanya Sophia ajihisi kama kuchanganyikiwa vile.
Ibra alienda dukani moja kwa moja na kununua maziwa pamoja na chuchu ya mtoto, wakati anatoka pale dukani kuna mmama wa makamo ambaye alikuwa ni mteja pia akamfata Ibra kwa nyuma na kumuuliza,
“Hayo maziwa unampelekea nani?”
“Si maziwa ya watoto haya! Nampelekea mtoto akanywe”
“Hebu chukua hilo kopo na uangalie hapo chini pameandikwa nini”
Ibra akachukua lile kopo na kuangalia kwa makini kisha kulisoma,
“Maziwa ya mama ni bora zaidi”
“Eeeh kwanini ukampe mtoto maziwa ya kopo badala ya maziwa ya mama?”
“Aaah-mmh-aaah unajua aaah-mmmh”
“Mbona unajiuma uma, nini tatizo? Kwanini msimpe mtoto maziwa ya mama? Unajua madhara ya maziwa ya kopo wewe?”
Ibra akatikisa kichwa kuwa hajui, kisha akajitetea,
“Unajua sisi mtoto mwenyewe tumemuokota tu”
“Hata kama mmemuokota, mtoto wa mwenzio ni sawa na mtoto wako, kwanini umpe vitu ambavyo havifai mtoto wa mwenzio?”
“Sasa hayo maziwa ya mama tutayatoa wapi? Na hata hivyo, kama haya maziwa ni mabaya mbona yanauzwa?”
“Hivi si unazijua sigara wewe? Zinauzwa na pale chini zimeandikwa onyo uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako ndio hivyo hivyo kwa hayo maziwa, umesoma mwenyewe hapo kuwa maziwa ya mama ni bora zaidi, haya sasa jiulize kwanini umpe mtoto maziwa ya kopo na sio maziwa ya mama? Unataka mtoto awe tahira? Je unataka awe zezeta useme amerogwa kumbe sababu ya miziwa ya kopo hiyo, unataka mtoto awe mjinga?”
“Ila mbona kuna watoto wengi tu nawafahamu wamekulia maziwa ya kopo na hawako hivyo?”
“Nisikilize mimi ni mtu mzima, sijakurupuka kukufuata na kukwambia kuhusu hayo maziwa, wenzenu ni wafanyabiashara tu shauri yako. Narudia kukwambia maziwa ya mama ni bora zaidi”
“Sasa mimi nitafanyaje ikiwa mtoto mwenyewe tumemuokota?”
“Memuokota ndio, je huna mke wa kumnyonyesha huyo mtoto?”
“Mke wangu hajazaa bado”
“Hata kama mkeo hajazaa, kila mwanamke anaouwezo wa kunyonyesha, kuna vitu tu vya kumpa ale kisha maziwa yanamtoka na ananyonyesha kama kawaida”
“Ila hata hivyo mke wangu ni mjamzito”
“Kumbe mkeo ni mjamzito, sasa si ndio vizuri hivyo. Hujui kama wajawazito huwa wanatoka maziwa? Ukifika nyumbani mwambie mkeo akamue chuchu zake uone maziwa yanavyotoka, mnyonyesheni mtoto huyo mtamuharibu akili kwa hayo maziwa ya kopo”
“Sasa mwanamke mjamzito ananyonyeshaje jamani, kwani wanaruhusiwa?”
“Kwanini wasiruhusiwe? Kama ameweza kubeba kiumbe tumboni atashindwaje kunyonyesha kiumbe anachokiona? Mshauri mkeo amnyonyeshe huyo mtoto, acheni kumnyanyasha m,toto mdogo mnamnyima haki yake’
Ibra akamshukuru yule mama kisha kuingia kwenye gari yake na kuanza kurudi nyumbani huku akitafakari mambo m,engi bila hata ya majibu.
Aliupofika nyumbani alikuta yule mtoto bado akilia huku Sophia akihangaika kumbembeleza,
“Kheee jamani hajatulia toka muda ule?”
“Mwenzangu yani anatulia kidogo na kuanza tena kulia, huyu mtoto ni balaa. Lete hayo maziwa nikamtengenezee”
Ibra akamkabidhi mkewe yale maziwa ambapo aliyakoroga na kungoja yapoe ili amnyweshe yule mtoto ila muda huo alitulia kidogo kisha Obra akaanza kumwambia mkewe kuhusu hoja alizopewa na yule mmama aliyekutana nae dukani.
“Kheee yani nimnyonyeshe maziwa yangu mimi?”
“Ndio, nasikia ndio vizuri inamsaidia mtoto kuwa na nguvu na afya zaidi eti hayo maziwa ya kopo hayafai”
“Sasa mimi nitamnyonyeshaje wakati ni mjamzito?”
Ibra akamwambvia mkewe ajaribu kutoa ziwa lake na kulikamua ambapo Sophia akafanya hivyo na alipokamua kweli chuchu zake zikatoa maziwa,
“Eeeh si unaona kuwa maziwa yanatoka? Kwamaana hiyo una uwezo wa kumnyonyesha huyu mtoto”
“Ila kwa nijuavyo mimi, mwanamke ukiwa mjamzito huruhusiwi tena kunyonyesha. Nakumbuka hata dada yangu Rehema alipombebea mimba mtoto wake ilibidi amuachishe ziwa mara moja sasa hizo habari za kuniambia kuwa naweza kumnyonyesha mtoto ingawa nina mimba nazishangaa sana”
“Usishangae Sophia nimeshauriwa na mtu mzima kabisa, ni mmama wa makamo yani haya mambo yote anayajua vizuri sana”
“Hata kama, kwakweli siwezi Ibra yani siwezi kabisa kumnyonyesha huyu mtoto wakati nina mimba tayari labda nishauriwe na daktari”
“Sophy usiwe mbishi kiasi hiko mke wangu, halafu kumbuka kuwa tumeambiwa tumlee huyu mtoto kama mwanetu kabisa kwahiyo tunatakiwa kumnyenyekea sana”
“Nimeshasema siwezi, Ibra siwezi”
Maziwa yale yalikuwa tayari kisha Sophia akachukua na kuanza kumpa yule mtoto ila alionekana kuyakataa kabisa yale maziwa na kuanza tena kulia, safari hii alilia sana hadi sauti yake ilianza kukauka,
“Sophy mke wangu mjaribishe na maziwa yako”
“Jamani Ibra kwanini hunielewi? Siwezi”
“Hivi kwanini wanawake mnakuwa na roho mbaya kiasi hiko jamani Sophy! Hivi huna huruma hata kidogo kwa jinsi mtoto huyu anavyolia? Si unataka watu wajae hapa na kutuuliza kuna nini jamani! Hebu kuwa na utu basi”
“Sasa maziwa yangu ndio atakunywa?”
“Mjaribishe tu, huwezi jua”
Sophia huruma ikamuingia na akajaribu kutoa ziwa lake na kumpa huyo mtoto ambaye alilidaka vizuri sana na kuanza kunyonya mpaka akapitiwa na usingizi ambapo Sophy akamlaza kwenye kochi pale sebleni.
“Haya sasa mke wangu umemeguka wapi kwa kumnyonyesha huyo mtoto?”
“Nisamehe bure mume wangu, mi nilijua haiwezekani”
“Hakuna kinachoshindikana, tulikuwa tunamtesa tu muda wote”
“Basi yaishe mume wangu”
Kisha Sophia akaenda jikoni kwa muda huo kuandaa chakula chao.
Sophia aliandaa chakula mezani na kumkaribisha mumewe ambaye alisogea pale mezani na kuanza kula ila leo walisifia sana kile chakula kwani kilikuwa ni kitamu kupiliza,
“Kwakweli leo mke wangu hiki chakula umekipika na kimepikika”
“Halafu nimekipika kawaida tu mume wangu”
“Hongera sana, chakula kitamu sana ndiomana nakupenda wewe”
Sophia akatabasamu na kumuangalia mumewe kwa furaha huku wakiendelea kula, walipomaliza tu kula yule mtoto nae akaanza kulia na kufanya Ibra na mkewe watazamane,
“Haya kamchukue mtoto”
“Unajua haya mambo hatujazoea”
“Ndio tunatakiwa tuzoee sasa, maana tukipata mtoto ndio hivi hivi”
Sophia akamchukua na kuanza kumbembeleza ila yule mtoto alikazana kulia tu, Ibra akamwambia mke wake
“Ukiona analia hivyo ujue anataka maziwa”
“Jamani kila muda?”
“Ndio kawaida ya watoto, hujui kwani? Mtoto anatakiwa kunyonya kila muda”
Ikabidi Sophia aanze tena kumnyonyesha yule mtoto ambapo alinyonya sana tu hadi Sophia mwenyewe akahisi maziwa yake yanauma, alipotulia alimuweka pembeni
“Duh huyu mtoto ananyonya hadi maziwa yananiuma”
“Ni kawaida ya watoto Sophy mke wangu utazoea tu maana na wetu huyo yupo njiani anakuja”
“Hata kama Ibra, ananyonya sana bhana”
Yule mtoto alikuwa ametulia kabisa muda huu ingawa alikuwa macho ila hakulia wala nini, walikaa pale na kuongea ongea mwisho wa siku wakakumbuka hoja ya kwa mjumbe,
“Hivi kuna umuhimu wa kumpeleka huyu mtoto kwa mjumbe?”
“Sasa mtoto mdogo hivi tumpeleke kwa mjumbe akatafute nini jamani? Kwakweli sioni umuhimu Ibra, kwa mjumbe inatakiwa tukimuokota mtu mzima kama yule Neema”
“Ila kweli mke wangu, kwa mjumbe inatakiwa tupeleke mtu mzima na sio mtoto mdogo hivi”
Wakajadiliana pale na mwisho wa siku wakakubaliana kuwa waende kulala.
Wakati wamelala, Sophia akajiwa na ndoto ya mtoto mmoja ambaye sura yake ilionyesha kusononeka sana kama kawaida Sophia alihitaji kumsogelea mtoto huyo ila kila aliposogea huyo mtoto nae akasogea mbele zaidi na mwishowe hakumfikia kabisa kisha akamuona yule mtoto akiishia kwa kumpungia mkono kama wa kumuaga Sophia.
Akajikuta akishtuka gafla kutoka usingizini huku akihema sana, mara gafla akajihisi maumivu ya tumbo chini ya kitovu kwakweli tumbo lile lilimuuma sana na kumfanya ahangaike pale kitandani kwa maumivu ila alipotaka kumuamsha mumewe hakuweza kwani hata huyo mumewe mwenyewe hakushtuka hata kidogo kwahiyo Sophia alikuwa akiugulia peke yake tu lile tumbo hadi panakucha ambapo Ibra aliposhtuka tu na maumivu ya tumbo kwa Sophy yalikata palepale na kumfanya Sophia abaki akijishangaa tu,
“Vipi mke wangu unajisikiaje?”
“Hivi unajua sijalala usiku wote”
“Kwanini? Mtoto alikuwa ananyonya sana?”
“Hapana mume wangu, huyo mtoto tangu tumlaze hapo hajaamka kabisa, yani usiku wote nilikuwa naugulia peke yangu tumbo limeniuma sana”
“Tumboo? Kheee pole sana mke wangu, kwahiyo saivi unajisikiaje?”
“Nashangaa tu hapa uliposhtuka wewe na tumbo nalo limeacha kuuma muda huo huo”
“Kheee mbona majanga sasa jamani, kwahiyo mimi ndio nilikuwa dawa? Vipi lakini hakuna hali nyingine yoyote maana hadi uoga umenishika”
“Hali gani kwa mfano?”
“Yani labda unatoka damu?”
“Hapana ni tumbo tu, natumaini mtoto wetu yupo salama”
“Nina hamu sana na huyo mtoto wetu naamini pia yupo salama, pole kwa kutokulala mke wangu jamani”
“Asante sana, vipi leo utaenda kazini?”
“Hapana siendi, nitaenda kesho leo nitakusaidia kulea”
Kisha Ibra akaamka na kuelekea sebleni ambako alikuta chai imeandaliwa mezani na kumfanya ahisi kuwa Sophia alishaiandaa kwahiyo akaenda pale mezani na kunywa ile chai kisha akaenda kukaa na kuanza kuangalia Tv.
Sophia nae alipotoka chumbani na kukuta chai mezani akajua mumewe ameand ile chai kwahiyo naye akaenda kukaa na kunywa ile chai kisha akamfata mumewe alipokaa na kumshukuru.
“Asante mume wangu kwa chai”
“Kheee natakiwa mimi nikushukuru wewe, au unanitega kwavile sijashukuru? Asante mke wangu kwa chai”
Sophia akamshangaa mumewe kwani alijua kuwa yeye ndiye ameandaa ile chai, ila kabla hawajaanza kujidadisi ikasikika sauti ya yule mtoto akilia na kumfanya Sophia aelekee chumbani.
Alimkuta yule mtoto pale kitandani ambapo Sophia alimuangalia kwa muda kidogo bila ya kumnyanyua, mara gafla akamsikia yule mtoto akisema,
“Masma nipe nyonyo ninyonye”
Sophia alishtuka sana.
akamuangalia kwa makini yule mtoto ambaye alirudia tena ile kauli yake,
“Mama nipe nyonyo ninyonye”
Sophia kwa uoga akatoka chumbani na kukimbilia sebleni ambako alimshtua mume wake na kumwambia huku akihemea juu juu,
“Ibra yule mtoto anaongea”
“Anaongea? Kivipi?”
“Anaongea kama kuongea, unajua kaniambia eti mama nipe nyonyo”
“Mmmh hebu acha masikhara Sophy, mbona unayoyasema hayawezekani?”
“Nenda kajishuhudie mwenyewe”
“Basi twende wote”
“Nenda tu, mi niache hapa hapa”
Ibra aliinuka na kuelekea chumbani ambako alimkuta yule mtoto akiwa amelala fofofo, Ibra akatikisa kichwa na kutoka hadi sebleni na kumuangalia mke wake huku akisema,
“Unajua wewe hujaacha mawenge mke wangu, haya huyo mtoto aliyekuwa anaongea yuko wapi wakati mtoto amelala yule”
“Amelala? Huyo mtoto atakuwa ni muongo mume wangu maana mi nimeshuhudia kwa macho yangu akiongea”
“Hivi Sophy unawezaje kumuita malaika ni muongo? Au hujui kama mtoto ni malaika?”
“Sio kwa malaika yule, mi siwezi hata kulala nae leo.”
Ibra akahisi kuwa mkewe matatizo yamemrudia tena ndiomana anakuwa hivyo ila akajaribu kuzungumza nae ili aweze kumuweka katika hali salama lakini Sophia alionekana kuwa mgumu sana kuelewa mpaka pale Ibra alipoendelea kumsisitiza kuwa itakuwa ni ndoto tu.
Muda huu Ibra alijiandaa na kumuaga mke wake kuwa anatoka kidogo, kwani alihitaji kwenda kuonana na Jane ili aweze kumueleza kuhusu yule mtoto waliyemuokota na kusikiliza ushauri wake kuwa atamwambia afanye nini kwani alikumbuka alivyomshauri kwa Neema kuwa aende kwa mjumbe sasa alihitaji kujua na kuhusu huyu mtoto atamwambia nini.
“Tafadhari Ibra usitoke na kuniacha peke yangu”
“Kwani tatizo ni nini jamani Sophia? Kwahiyo hatutafanya tena kazi?”
“Sio hivyo mume wangu ila nakuomba usitoke kwanza, ngoja tuzoee pamoja kuishi na huyu mtoto”
“Kheee makubwa haya, mtu mzima atusumbue akili halafu leo hii mtoto nae atusumbue akili? Unataka tukamtupe mtoto huyu? Hebu fikiria mimba uliyobeba, hebu jaribu kuwa na uchungu kama mama. Fikiria mimba zilizotoka, fikiria maumivu uliyopitia ndio umuwazie mabaya huyu mtoto”
“Sikia Ibra, mimi sina nia mbaya na huyu mtoto ila tu sijisikii vizuri kubaki nae peke yangu. Naomba tubaki wote”
“Nimekuuliza, je tutakuwa hatufanyi kazi? Je maisha yetu yataendeshwa na kitu gani? Hebu fikiria hilo kwanza mke wangu, mimi leo sitatoka ila fikiria kwa makini jinsi maisha yetu yanavyoenda”
Sophia hakujibu kitu chochote, mara akasikika yule mtoto akilia huku Sophia akiogopa kwenda kumchungulia wala kumchukua, ikabidi Ibra ainuke na kwenda kumchukua yule mtoto na kutoka nae sebleni kisha akamuomba Sophia amnyonyeshe yule mtoto,
“Naogopa bhana”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sophia, umeitoa wapi hiyo roho mbaya? Kwani maziwa hayo unalipia bili jamani? Hayo maziwa ni bure tu sasa unashindwa nini kumnyonyesha mtoto?”
“Mtoto mwenyewe ananyonya sana”
“Hata kama ananyonya sana, si utakula chakula kwani tatizo liko wapi jamani mke wangu? Tunapomfanyia mabaya mtoto huyu tunatakiwa kwanza tufikirie kwa makini kuhusu mtoto wetu ajae.”
Sophia hakujibu kitu ila akamchukua mtoto yule na kuanza kumnyonyesha ambapo alinyonya kwa masaa kama mawili mpaka Sophia akaanza kulalamika kuwa maziwa yanamuuma sana, yule mtoto akatabasamu na kuacha kunyonya kisha akalala.
Ibra akampa pole mke wake na kumwambia kuwa anatakiwa kuwa mvumilivu.
“Hata hivyo Ibra, ila kwanini huyu mtoto ananyonya sana?”
“Mbona ni kawaida ya watoto Sophia”
“Unajua Ibra nimeshaishi na watoto wengi tu ingawa sijawahi kulea mtoto wangu mwenyewe ila naweza kujua jinsi ukuaji wa watoto ulivyo. Kwa nijuavyo mimi ni kuwa watoto wa kiume wanakula sana ila hawamfikii huyu mtoto, hata hivyo huyu ni mtoto wa kike iweje awe anakula kiasi hiki? Akiendelea hivi nampa uji au ugali kabisa”
“Sophia jamani mbona unakuwa hivyo? Wewe ulilishwa ugali wakati mdogo? Kwanini sasa umuharibu utumbo huyu mtoto?”
“Halafu kwanini unamtetea hivi huyu mtoto, kwanini mume wangu?”
“Unajua nini Sophia, tushapoteza watoto wetu wengi tu kwahiyo nikimuona huyu mtoto huwa naona kama mwanangu vile ndiomana namuhurumia sana”
Sophia alimuangalia tu mumewe bila ya kuongeza neno kisha akamlaza yule mtoto pale kwenye kochi.
Wakapitiwa na usingizi wote pale ndani kwao, yani hakuna ambaye alikuwa macho kwa muda huo. Sophia akajiwa na ndoto amapo katika ndoto ile alijiona akiwa na mumewe chumbani huku mumewe akimwambia,
“Sophy mke wangu ukizaa huyo mtoto namuua”
“Kheee kwanini umuue sasa jamani?”
“Lazima nimuue, kwakweli siwezi kukubali tupate mtoto mwingine wakati tuna mtoto tayari. Na vile vile mtoto mwenyewe huyo sina uhakika kama ni mtoto wetu kweli”
“Una kichaa au? Tuna mtoto tayari! Mtoto yupi jamani, au unamuongelea huyu tuliyemuokota?”
“Ndio, huyu mtoto anatutosha kabisa. Sasa ole wako umzae huyo mtoto au huamini kama nawaza kumuua?”
“Siamini na kamwe siwezi kuamini”
Gafla akamuona Ibra akimpiga teke la tumbo na kumfanya Sophia ashtuke sana kutoka kwenye usingizi ule huku akihemea juu juu na kumuamsha Ibra,
“Ibra, Ibra nimeota ndoto mbaya sana”
Ibra aliamka huku akiwa haelewi elewi, na kumuuliza mkewe
“Umeota ndoto mbaya kivipi jamani?”
“Yani, nimeota kuwa dah hata sijui nisemeje”
“Hebu niambie ilivyokuwa niweze kuelewa”
Sophia akamsimulia mumewe jinsi alivyoota huku akishika tumbo lake, Ibra akamsogelea mkewe na kumkumbatia kisha akamwambia,
“Sophy mke wangu, hiko kitu ulichoota hakipo yani hakipo kabisa kabisa sio kwa uhalisia wala kwa ndoto. Nakupenda mke wangu na pia napenda uzao wako. Watoto ndio furaha yetu na ndiomana tunafanya jitihada zote kuwapata sasa nawezaje kuanza kupinga uwepo wa mtoto wetu eti kwavile kuna mtoto tulimuokota tupo naye ndani? Huyu mtoto namjali na kumthamini kwavile natumai na sisi tutapata mtoto wetu kwahiyo hatutakiwi kumtenda vibaya mtoto huyu tutalaaniwa bure”
“Nashukuru kwa kunipa moyo mume wangu yani sitaki kumpoteza mtoto wetu huyu”
Sophia alikuwa akilishika shika tumbo lake huku akiliangalia kwa makini sana, ila walikaa pale bila ya kuhisi njaa wala nini yani si Sophia wala si Ibra hata wakawa wanashangaa tu,
“Sophy si unanyonyesha wewe yani na wewe huna njaa?”
“Hata nashangaa yani njaa imepotea kabisa, najihisi kushiba hatari”
Wakaamua kuendelea kujadili mambo mengine na kuachana na zile habari za njaa.
Muda kidogo sophia akaona ni vyema kuwa akamlaze yule mtoto chumbani sababu muda wote alilala hapo sebleni kwahiyo akambeba na kwenda kumlaza chumbani kisha yeye akarudi tena pale sebleni ila muda kidogo wakasikia hodi na kumfanya Ibra ainuke na kufungua mlango, alishangaa kuona mgeni mwenyewe ni Jane,
“Kheee Jane, nani amekufungulia geti?”
“Mbona geti lenyewe nimelikuta wazi jamani”
Akaingia ndani na kumsalimia Sophia ambapo leo aliitikia vizuri tofauti na siku zingine, baada ya ile salamu gafla mtoto wa chumbani akaanza kulia na kumfanya Sophia aende kumchukua na kurudi nae sebleni ambapo alipofika nae tu Jane akashangaa na kuuliza,
“Kheee kumbe mna mtoto jamani? Dada alikuwa na mimba kubwa? Mbona majuzi tu sikuwaona na mimba?”
Ibra akaamua amueleze ukweli kuwa yule mtoto wamemuokota na wameamua kumlea pia akamueleza mazingira waliyomkuta nayo huyo mtoto, kwakweli Jane aliwapongeza sana na kuwasifu kwa huo uamuzi wao,
“mmefanya jambo la maana sana, yani watu hawajui tu kama kulea watoto kama hawa ni vizuri”
“Ila changamoto iliyopo Jane ni kuhusu maziwa, yani huyu mtoto hataki maziwa ya kopo halafu vilevile Sophia nae hataki kumnyonyesha”
“Kheee dada jamani hebu acha hizo, yani mtoto mdogo hivyo unataka kumnywesha maziwa ya kopo? Sio mazuri yale, unatakiwa kumnyonyesha mtoto huyo ndio unampa nguvu na afya”
“Ila jane huyu mtoto ananyonya sana ndiomana inakuwa hivi”
“Kunyonya ni kawaida ya watoto dada yangu hata usishangae, unatakiwa kumpa maziwa mtoto kila anapohitaji wewe mnyonyeshe tu hata kama ananyonya kwa masaa matatu mfululizo mnyonyeshe tu”
“Bora umemshauri wewe, eeeh hivi mtoto huyu nae tumpeleke kwa mjumbe?”
Jane akacheka huku akiwajibu,
“Sasa mkimpeleka mtoto kama huyu kwa mjumbe si mtachekesha jamani, yani mtoto mdogo hivi eti mnampeleka kwa mjumbe inamaana mnaogopa kuibiwa au?”
“Ila hata mimi nilifikiria hilo na kuona kuwa halina umuhimu, kwakweli asante sana Jane kwa kuja”
Yule mtoto akaanza kulia tena na kumfanya jane amsisitize Sophia kuwa amnyonyeshe yule mtoto kisha akainuka na kuaga na kuondoka zake. Sophia alianza kumnyonyesha yule mtoto huku akizungumza na Ibra,
“Ila mbona kama leo Jane amebadilika sana?”
“Hata mimi mwenyewe namshangaa, yani kwajinsi anavyopenda kupinga yule binti yani lazima angetupinga kuhusu kumlea huyu mtoto ila cha kushangaza yeye ndio ametusapoti na kutupa nguvu zaidi”
“Kwakweli nimemshangaa sana, halafu leo sijamchukia kama siku zote eti nimempenda leo”
“Basi Jane kabadilika, tuwe tunamkaribisha. Mara ya mwisho naongea nae alianza kuniletea habari za mchungaji wao nikamshushua naona leo kajirekebisha”
“Alizidi sana, ila bora amebadilika kwakweli”
Ibra na Sophia waliongea kwa furaha sana muda huu huku yule mtoto akiendelea kunyonya.
Giza liliingia huku Sophia akiwa anaendelea kumnyonyesha yule mtoto na kumwambia mume wake,
“Nachoka Ibra nachoka sana, hebu ona masaa matatu sasa yamepita huyu mtoto ananyonya tu hivi kuna maziwa kweli humu au ananyonya damu jamani?”
“Pole mke wangu ila ndio uleaji mzuri huo, hukumsikia Jane alivyosema? Tunatakiwa kumnyonyesha sana huyu matoto bila kuchoka”
“Hivi unajua kama maziwa yananiuma kama yana vidonda vile?”
“Vumilia mke wangu jamani, kuwa mvumilivu”
Sophia akainuka na kwenda na yule mtoto chumbani ambapo baada ya muda kidogo tu yule mtoto alilala, kisha Sophia akatoka mule chumbani na kujikongoja hadi jikoni kwani muda huo njaa ilimshika sana kupita wakati mwingine, alipoingia jikoni alikuta chakula kipo tayari kwenye sufuria na kwavile njaa ilimshika sana hakuweza kuhoji kwahiyo aliamua kupakua na kuanza kula kule kule jikoni amabapo alikula na aliposhiba ndio aliinuka na kuelekea sebleni, ila kwa wakati huo ilionyesha kuwa Ibra alikuwa chumbani kwahiyo na yeye baada ya muda kidogo akaamua kwenda chumbani kulala kwani alimkuta Ibra akiwa amelala tayari.
Sophia alipopitiwa na usingizi akajiwa na ndoto, akamuona Neema nje ya nyumba yao na gafla yule Neema akageuka na kuwa Jane kisha akawagongea mlango na kuingia ndani. Sophia alishtuka sana na kuamka huku akishangaa, alikaa kitandani akitafakari kuwa Neema anawezaje kujigeuza na kuwa Jane? Na kwanini ajigeuze? Alikosa jibu kabisa ila aliogopa kumuamsha mume wake na kujipa matumaini kuwa ile ni ndoto tu kisha akarudi kulala.
Kulipokucha leo waliamshwa na sauti ya Yule motto akilia hivyo ikambidi Sophia aamke na kuanza kumnyonyesha Yule motto kisha Ibra nae aliamka na kwenda kuoga halafu akajiandaa kwaajili ya kutoka, akamuaga mkewe
“Vipi na leo tena hutoniruhusu kutoka?”
“Mmmh ngoja nifikirie kidogo”
“Ufikirie nini tena?”
“Nifikirie kuhusu kukuruhusu wewe”
“Tafadhali Sophia naomba niruhusu mke wangu maana nahitaji sana kujua kule dukani inakuwaje, hebu fikiria tangu lini hatujaenda kule. Naomba leo uniruhusu mke wangu”
“Sawa nakuruhusu ila tafadhali sana uwahi kurudi Ibra, usichelewe kama siku zote kumbuka nipo peke yangu”
“Haupo peke yako bhana upon a huyo motto”
“Hta kama, unadhani huyu motto atanisaidia nini sasa? Hapa ni sawa na kama nipo mwenyewe tu, tafadhali sana uwahi kurudi”
Ibra akamuahidi mkewe kuwa atawahi kurudi kwani hata yeye hawezi kumuacha ashinde mwenyewe kwa muda mrefu ukizingatia ana motto mdogo sana pale ndani.
Kama kawaida Ibra alitoka na kupanda gari yake kisha kuondoka pale nyumbani kwake, ila alipokuwa njiani akamuona Jane na kuamua kusimamisha gari ili amsalimie.
“Jane, za tangu jana?”
“Tangu jana? Kwani tumeonana na wewe jana kweli?”
“Si ulikuja nyumbani wewe!”
“Mmmh kaka labda kuna mambo unachanganya, mimi sijaja kwenu mud asana na hata hiyo jana sijaja kwenu sasa ni jana ipi unaiongelea?”
“Kheee wewe Jane jamani, si ulikuja na kuanza kutupa ushauri mule ndani jinsi ya kulea yule motto”
“Kwani mna mtoto? Dada kajifungua lini?”
“Unajua acha masikhara Jane, si nilikueleza jana kuwa mtoto tumemuokota”
“Mmemuokota? Je mmetoa taarifa polisi?”
“Unajua Jane usinichanganye tafadhali”
“Sikuchanganyi chochote ila wewe ndio unanichanganya mimi maana nashindwa kukuelewa”
Ibra hakuendelea kujadiliana na Jane bali aligeuza gari yake na kurudi nyumbani kwake ili akamuelezee mkewe vile alivyokutana na Jane na kukana kuwa hakwenda hapo jana.
Alipofika nyumbani alishangaa kuona kuna ukimya sana na kuhisi kuwa huenda Sophia na mtoto watakuwa wamelala, Ibra alifungua mlango na kukuta uko wazi tu,
“yani Sophy hakuinuka hata kufunga mlango!”
Akakumbuka kuwa alimuacha Sophia akimnyonyesha Yule mtoto, moja kwa moja akaenda chumbani, ila akashtuka sana kwani alimuona Sophia akiwa chini huku damu zikimtoka.
Ibra akahisi kuchanganyikiwa, akamtikisa mkewe pale chini alikuwa kimya kabisa na kumfanya Ibra apatwe na uoga kisha akamnyanyua mkewe na kumuweka begani halafu akatoka nae nje na kumuweka kwenye gari huku akielekea nae hospitali.
Walifika hospitali na kupokelewa amabapo moja kwa moja Sophia akapelekwa kwenye chumba cha huduma, Ibra alikuwa nje amechanganyikiwa kabisa hata akasahau kuwa nyumbani kwao kuna mtoto yupo ndani.
Muda kidogo daktari akamuita Ibra na kumuuliza maswali huku akijaribu kumueleza hali ya mgonjwa,
“Samahani ndugu, kwani huyu mgonjwa chanzo kilikuwa ni nini?”
“Hata sifahamu kwakweli, mimi nilimuacha nyumbani akimnyonyesha mtoto na niliporudi ndio nikamkuta na hali hiyo”
“Kwahiyo huyu ana mtoto mdogo?”
“Aaah aaah ndio tuna mtoto mdogo nyumbani”
“Halafu ndio alikuwa na mimba nyingine?”
“Aaah aaah ndio, kwani mimba yake inaendeleaje?”
“Kwa mlichomfanya huyu hakuna cha mimba inaendeleaje wala nini, kwa kifupi ni kuwa mimba ya huyu ilishatoka. Na ubaya zaidi ni kuwa kizazi chake kimeonekana kuwa na matatizo kwasasa”
Ibra alikaa chini kwanza kwani hakutegemea kupata habari kuwa mimba ya mke wake imetoka ukizingatia aliona kuwa kwa kipindi hiki watapata mtoto wao ukiacha na Yule waliyemuokota.
“Pole sana ndugu yangu, ila kwakweli mlichokuwa mkikifanya hakistahiki kwa mama mjamzito yani unajua kabisa huyu ana mimba halafu unamfanya mmnyonyeshe mtoto mwingine na wakati huo huo mnampa lishe hafifu hivi mlikuwa mnategemea nini kwa hali yake? Inaonyesha alianguka na aliangukia tumbo ndiomana akapata matatizo hayo, hata hivyo inaonyesha kuwa damu imepungua sana mwilini kwahiyo mnatakiwa kuwa makini sana vinginevyo mtakuja kumuongezea damu huyu”
Ibra alikuwa kimya tu akitafakari huku akiwa na matumaini ya kupona kwa mkewe ingawa alikuwa na uchungu wa kupoteza mtoto mwingine.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Muda ukapita kisha daktari akamuita tena Ibra na kumpa habari zaidi kuhusu mkewe,
“Unatakiwa uwe makini sana vinginevyo utampoteza huyu”
“Niwe makini kwenye kitu gani haswa?”
“Kuwa makini kwenye chakula kwa sana ili kumsaidia aweze kurudisha afya yake, hakikisha anapata mlo bora na kamili, mboga za majani na matunda visikosekane kwenye mlo wake”
“Sawa daktari, hilo sio tatizo kwangu kwani nahitaji mke wangu arejee kwenye afya yake”
Basi daktari akamwambia kuwa jioni atawapa ruhusa kwahiyo wataweza kurudi nyumbani na mkewe, Ibra alishukuru hilo kisha akatoka nje kwenda kumtafutia mkewe chakula na wala hakujisikia kurudi nyumbani kwa muda huo kwahiyo akaenda hotelini moja kwa moja kumtafutia hiko chakula.
Alifika hotelini na kuagiza chakula kwahiyo alikaa mahali akisubiri chakula hiko huku akiwa ameagiza soda ambayo alikuwa akinywa huku akisuburi wamalize kuandaa hiko chakula.
Kulikuwa na wadada wawili wamekaa pale hotelini wanaongea,
“Hivi unamkumbuka Neema?”
“Namkumbuka ndio aliwahi kuwa mfanyakazi wa hii hoteli”
“Ulisikiaga mazishi yake yalivyokuwa?”
“Mmmh nilisikia tu kuwa amekufa ila sikufika kwenye mazishi ila ni miaka imepita tangu afe”
“Yani mazishi yake haijawahi kutokea, kulikuwa na mambo ya ajabu mwanzo mwisho halafu kulikuwa na tetesi kuwa Neema alitembea na mwanaume wa ajabu na ndio aliyesababisha kifo chake. Ila jambo linalofanya nikumbuke mazishi yake ni kuwa, hivi majuzi kuna rafiki yangu kaniambia kuwa kamuona mtu kama Neema vilevile unajua nimeshtuka sana na nikikumbuka yale mazishi yake ndio nazidi kupatwa na uoga”
“Sasa uoga wa nini ndugu yangu, kwani kuna lolote baya ulilomfanyia Neema? Hata hivyo mi siamini juu ya mizimu ila naamini kuwa duniani watu ni wawili wawili kwahiyo huyo atakuwa kafanana tu na Neema acha uoga ndugu yangu mtu akifa amekufa”
“Weee najua hujui mengi sana kuhusu kifo cha Neema na ndiomana unasema hivyo, mi naogopa sana maana hata mimi nimehusika kutangaza kuwa kifo chake kilikuwa cha utata na kilisababishwa na mwanaume wa ajabu”
“Kumbe uoga huo ni sababu ya umbea wako pole sana”
Kimya kidogo kikatawala, kisha yule rafiki akamshtua mwenzie kwa kumwambia,
“Neema huyo”
Yani kile kitendo kilimshtua sana yule dada ila pia kilipasua moyo wa Ibra na akahisi ukimuenda mbio sana na uoga kumshika, mwisho wa siku wale wadada walianza kucheka sababu ya kutaniana ila walishangaa Ibra kuwa na hali mbaya sana ikabidi wamuombe msamaha kama wamemshtua na yeye.
“Kaka samahani sana, maana inaonyesha tumekushtua sana tusamehe tafadhali sisi tulikuwa tunataniana tu”
Ibra hakuweza hata kuwajibu kwajinsi moyo wake ulivyokuwa ukienda mbio, muda huo yule muhudumu wa chakula nae alikuwa amemletea kile chakula Ibra alichukua na kuondoka zake.
Alikuwa na mawazo sana huku akiendesha gari,
“Kama Neema waliyekuwa wanamuongelea ni yule tuliyeishi nae ndani je inamaana tulikuwa tukiishi na marehemu?”
Ibra alihisi kusisimka mwili mzima na kuamua kuachana na hayo mawazo kwa muuda.
Ibra alifika pale hospitali na kwenda kwa mke wake moja kwa moja kisha akampa kile chakula, kwakweli Sophia alikula kile chakula kamavile anakimbizwa na ilionyesha wazi kuwa alikuwa na njaa sana. Alikula mfululizo bila ya nkuongea chochote mpaka alipomaliza kile chakula, ndipo alipomuangalia mume wake na kumshukuru kisha akajilaza tena, kwakweli ile hali ilimshangaza sana Ibra na akazidi kumuhurumia mke wake na ndipo lile swala la mtoto nyumbani kwao likamjia,
“Mmmh yule mtoto nadhani atakuwa amelia leo hadi sauti imemkauka, na pia nadhani ni vyema kama mke wangu akiacha kumnyonyesha yule mtoto”
Gafla na yeye akasinzia pale pale pembeni ya mke wake. Dokta ndiye aliyefika na kuwashtua kwani jioni ilikuwa tayari imeshaingia, Ibra alishtuka huku akijishangaa kuwa imekuwaje hadin akapitiwa na usingizi kiasi kile, akamuamsha na mkewe ili wamsikilize dokta.
“Ibra, na wewe umelala kwa mgonjwa jamani, nimeshawaruhusu sasa mnaweza kwenda nyumbani”
Ibra akainuka na mkewe pale kisha wakatoka nje na kuelekea kwenye gari yao, walipopanda tu Ibra akamuuliza mkewe hali yake,
“Ila hali yako unaionaje kwasasa mke wangu?”
“Naendelea vizuri ila mwili umechoka sana”
“Pole mke wangu, yani hata ongea yako inaonyesha ni jinsi gani umechoka. Pole sana”
Ibra akaendesha gari hadi nyumbani ambapo Sophia alikuwa kimya njia nzima, walifika na kuingia ndani ambapo walikaa sebleni bila ya kwenda sehemu nyingine yoyote, Ibra aliamua kumuuliza vizuri mkewe kwani kupooza kule hakuelewa kabisa,
“Sophia unajua umepoa sana mke wangu, ingawa unaumwa ila umepoa sana hata sielewi nadhani kuna jambo linalokuchanganya zaidi”
“Sio jambo Ibra, kuna mambo mengi sana yanayonichanganya yani nahisi kupagawa kabisa”
“Pole sana mke wangu ila ni vyema tukashirikishana”
“Nawawaza wanangu, kwanini kila siku mimi ndio napoteza watoto? Kwanini jamani nabeba mimba zinatoka? Inaniuma sana Ibra yani sina raha kabisa”
Mara Yule mtoto wa ndani kwao akaanza kulia na kuwafanya washtuke, Ibra akajiuliza
“Kheeee kumbe huyu mtoto bado yupo!”
Kisha akainuka na kwenda kumchukua halafu akarudi nae sebleni, akamuangalia mkewe akamuona machozi yakimtoka
“Vipi Sophia nini tatizo mke wangu?”
“Tafadhali Ibra usinipe huyo mtoto nimnyonyeshe nakuomba sana usinipe”
“Huyu tutampa maziwa ya kopo leo hata usijali mke wangu”
Ibra akainuka na kwenda kumkorogea Yule mtoto maziwa ila walipompa kama kawaida aliyakataa kabisa,
“Mmmh tutafanyaje sasa mke wangu?”
“Mwache akiwa na njaa atakunywa tu”
Muda huu huyu mtoto alionekana kutulia ila alikuwa anawaangalia sana hata Ibra akashangaa kuwa imekuwaje.
Giza lilikuwa linaingia wakiwa pale pale sebleni huku Sophia akiendelea kusema kuwa anajihisi kuchoka sana,
“Hivi kwanza mke wangu niambie chanzo cha kuumwa kwako leo”
“Unajua toka ule muda nimeamka huyu mtoto alikuwa akinyonya yani muda wote ananyonya tu gafla nikahisi nguvu zikiniishia na kuamua kumuweka pembeni ila wakati nainuka nikaanguka chini na sikumbuki tena kilichoendelea”
“Pole sana, huyu mtoto hutomnyonyesha tena nisamehe mimi mke wangu. Huyu mtoto anakumalizia lishe kabisa na dokta kaniambia kuwa inabidi ule sana ili uwe salama kwahiyo huyu mtoto tutampatia maziwa ya kopo tu”
“Ila toka mwanzo nilikwambia swala hilo ila wewe Ibra ulikuwa mbishi sana ona sasa tumeshampoteza mtoto wetu kwa kuthamini watoto wa kuokota”
“Nisamehe mimi mke wangu tafadhali”
Sophia alimjibu mumewe kuwa ameshamsamehe ingawa bado anauchungu na ile mimba yake iliyotoka, kisha Ibra akamuomba mkewe kuwa wale kwanza ndipo wajiandae na kulala. Ibra alikuta chakula jikoni na wala hakuhoji sana zaidi ya kupakua kisha yeye na mkewe kula chakula hicho, walipomaliza kula Sophia aliamua kwenda kuoga ili aweze kulala, ila alipoingia bafuni alishtuka sana kwani alikuta damu imetapakaa kila sehemu.
Sophia alipiga kelele na kutoka nje,
“Nini tatizo mke wangu kuna nini?”
“Damu Ibra, damu zimejaa chooni”
“Damu? Zimetokea wapi tena?”
“Sijui ila damu zimejaa chooni Ibra”
Ibra akaamua kwenda kuangalia mwenyewe ila hakuona damu yoyote na kumwambia mkewe kuwa ni mawenge tu yalikuwa yakimsumbua kichwani kisha akaamua kwenda kuoga naye pamoja.
Walipomaliza kuoga walimkuta Yule mtoto ameshalala, wakatazamana na kuulizana
“Inamaana huyu mtoto leo atakula nini?”
“Atakunywa hay ohayo maziwa njaa ikimshika vizuri”
“Hivi unajua kama ni toka asubuhi hajala chochote?”
“Unataka tufanyaje sasa mume wangu jamani, kama kula hataki tusubiri tu muda njaa ikimshika vizuri atayanywa hayo maziwa”
Wakakubaliana hilo kisha na wao kupanda kitandani na kulala.
Wakiwa wamelala, Sophia alihisi maziwa yakimuuma sana na kumfanya aamke kisha akakaa kitandani na kuangalia maziwa yake ambapo alishangaa ziwa moja likivuja maziwa na linguine likivuja damu kwakweli akapatwa na uoga kisha akamuangalia Ibra na kuanza kumuamsha ila kabla Ibra hajaamka Sophia alijishangaa akipatwa na usingizi pale pale na kulala, tena safari hii alilala fofofo kushinda mwanzo yani hakuweza hata kujigeuza.
Usiku wa manane Ibra nae akashtuka kutoka usingizini na moja kwa moja akamtazama mke wake ila alichokiona kilimshtua sana, alimuona mkewe akiwa kalala chali huku Yule mtoto akiwa juu ya mkewe ananyonya.
Ibra alijifikicha macho kwani alihisi kamavile haoni vizuri ila bado alipoangalia alimuona yule mtoto akikazana kunyonya, Ibra alisogea ili ajaribu kumtoa yule mtoto pale kifuani huku roho nyingine ikimwambia kuwa labda mtoto ana njaa sana ndiomana imekuwa vile ila akajiuliza kuwa hata kama mtoto yule ana njaa sana je pale kifuani amewekwa na mke wake au imekuwaje? Maana yule mtoto ni mdogo sana na ni ngumu kufanya vile. Akajaribu kumtoa sasa ila yule mtoto alionekana kulishikilia ziwa vilivyo kwa mdomo wake na kumfanya Ibra ashindwe kumtoa, akajaribu kumuamsha mke wake ila alishtukia akipigwa kibao na mtu asiyemuona, kibao ambacho kilipelekea aanguke kitandani na kupitiwa na usingizi pale pale.
Ibra alikuja kushtuka tena wakati kumeshakucha kabisa na bado alimuona yule mtoto akiwa pale pale juu ya mkewe akinyonya, Ibra alishtuka sana na uoga ukaanza kumuingia sasa akajikuta akitetemeka huku akiita,
“sophia, Sophia mke wangu, Sophia”
Ila Sophia alikuwa kimya kabisa huku amelala chali vile vile na yule mtoto akiendelea kunyonya, Ibra akajivika ujasiri sasa na kuamua tena kumtoa yule mtoto ila safari hii alifanikiwa na kumuweka kitandani, kale katoto kalikuwa kakimuangalia tu Ibra kisha Ibra akaanza kumuamsha tena mkewe ambaye alichukua muda mrefu sana kuamka na alionekana kutokuwa na nguvu kabisa kwani hakuweza hata kuitika vizuri, kwakweli Ibra huruma ilimuingia sana na kumpa pole mkewe ambaye hata kujibu hakuweza ila aliishia kumuangalia Ibra tu.
“Sophy, tafadhali tutoke twende hotelini ukanywe supu maana nikisema tutapika muda huu itakuwa uongo mke wangu”
Sophia aliitikia kwa kichwa tu kwani alionyesha kuzidiwa na njaa, ikabidi ibra amsaidie mkewe kuvaa kisha akaanza kumkongoja kutoka naye pale ndani hadi nje ya geti kisha safari ya kwenda hotelini ikaanza.
Walipofika hotelini moja kwa moja Ibra akamsaidia mkewe kushuka kisha wakaenda kukaa na kumuagizia supu ambapo ilipofika Sophia alikunywa kamavile anakimbizwa kwakweli ilionyesha ni wazi kuwa Sophia alikuwa na njaa sana, Ibra alikuwa akimuangalia mkewe huku akisikitika tu. Alipomaliza ile supu ikaletwa nyingine ambapo aliinywa pia kisha akaanza kurudi kwenye hali ya kawaida, Ibra akampa tena pole mke wake
“Pole sana Sophy”
“Asante”
“Hivi yule mtoto ni vipi ukaanza kumnyonyesha tena usiku wakati tulikubaliana kuwa usimnyonyeshe tena?”
“Yani hata mimi mwenyewe nashangaa, unajua nimeshtuka usiku na kumkuta yule mtoto akinyonya yani kapandaje kifuani pangu sijui. Angekuwa ni mtoto labda wa miezi hata mitano ningesema anauwezo huo sababu amekua kua ila sio kwa yule mtoto jamani, basi nikajaribu kumtoa nikashindwa na nguvu zikaniisha kabisa huku yeye akiendelea kunyonya yani muda unaniita nilikuwa nasikia ila nashindwa kuitika”
“Dah pole sana mke wangu, unajua hii okota okota yetu ndio inatuponza kwakweli sasa tufanyaje juu ya yule mtoto na kumbuka tumeambiwa kuwa tusimtupe”
“Unajua mimi sina imani kabisa kama yule ni mtoto kama watoto wengine, yule mtoto sio wa kawaida na ananipe mashaka mume wangu kwakweli sitawea kulala tena mule chumbani kwa uwepo wa yule mtoto”
Ibra akafikiria kidogo kisha akamuuliza mkewe,
“Unaonaje yule mtoto tuwe tunamlaza chumba alichokuwa analala Neema?”
“Labda tufanye hivyo kwakweli maana siwezi kabisa kuendelea kukubaliana na hii hali, yani hadi nimepata wazo la kurudi nyumbani kwetu”
“Hapana usifanye hivyo mke wangu, hebu nifikirie mimi unadhani nitawezaje kuishi peke yangu jamani! Tafadhali sophy mke wangu usifikirie huko, yule mtoto tutaanza kumlaza chumbani kwa Neema na hatotusumbua tena”
“Sawa, ila pia naomba hili swala la mimi kutoka maziwa likome mara moja maana ningekuwa sitoki maziwa basi yule mtoto asingekuwa anapata cha kunyonya toka kwangu. Sijui utanisaidiaje juu ya hili?”
“Hilo sio tatizo mke wangu tutajua tu cha kufanya ila kwasasa tumalizane kwanza na huyu mtoto maana naona kabisa lengo lake ni kukuua mke wangu. Hivi ni mtoto gani yule maana pale alipo hana hata mwezi mmoja halafu anafanya vituko kiasi hiki, nimemchoka kwakweli”
Wakapanga pale na kufikia muafaka wao kuwa yule mtoto wataanza kumlaza kwa Neema maana Ibra alihisi kuwa yule mtoto anaweza kuzidi kummaliza nguvu mke wake.
Walipomaliza pale wakaanza safari ya kurudi nyumbani ndipo Ibra alipokumbuka lile tukio la kukutana na Jane na jinsi Jane alivyoshangaa alipoambiwa kuwa alifika nyumbani kwao,
“kheee kwahiyo Jane kakataa kuwa sio yeye?”
“Yani kakataa kabisa”
“Mmmh sasa mbona naanza kupatwa na uoga jamani? Alikuwa nani sasa aliyekuja kwa sura ya Jane kiasi kile?”
“Hata mimi nimekosa jibu ila Jane amekataa kabisa kuwa yeye hakuja nyumbani kwetu”
“Ila hata siamini labda kama Jane kaamua kutufanyia mchezo tu mume wangu, hivi unamuaminije Jane jamani?”
“Sio namuaminije, kuna vitu Jane huwa anaongea ukweli mtupu kama unakumbuka alivyotuambia kuhusu Neema, iweje tusimuamini? Mimi naamini kuwa hakuwa yeye ingawa sijui sasa alikuwa ni nani”
“Maajabu hayo ila bado siamini kwakweli, yani mtu mweingine ajibadilishe na kuwa Jane halafu aje nyumbani kwetu na kuongea vile kweli? Ila nilishangaa siku ile nilivyomfurahia Jane wakati si kawaida yangu”
“Basi ndio ujue kuna namna hapo”
Ibra akakumbuka kuhusu biashara yake na kumuomba mkewe kuwa wapite kwanza kwenye biashara kabla ya kwenda nyumbani,
“Hata mimi nilikuwa nataka nikwambie hicho kitu, unajua ni muda sana haujafungua biashara? Ndio mwanzo wa kufilisika huu mume wangu bora umekumbuka leo”
Ibra alipeleka gari moja kwa moja hadi kwenye biashara yao kisha wakashuka na kuelekea dukani, ambapo alifungua duka, ila alishangaa kuona kuna mzigo mpya umejaa ndani ya duka lao, Ibra akamtazama mkewe na kukosa jibu kabisa.
Muda kidogo alisogea baba John pale dukani kwa Ibra na kusalimiana nae, Ibra akamwambia baba John
“Za siku nyingi ndugu yangu?”
“Za siku nyingi kivipi tena?”
“Khee unasahau kama hatujaonana kwa siku nyingi sana, nilikuwa na matatizo mwenzio”
Baba John akacheka kisha akamwambia Ibra,
“Yani wewe ndio umesahau au unaogopa nitakuuliza kuwa mzigo unatolea wapi siku hizi nini? Wewe jana si ulikuwa hapa na tukaongea sasa unasemaje za siku nyingi”
Ibra akawa kimya kwa muda kisha akauliza,
“Jana nilikuwa hapa?”
“Sasa unaniuliza nini tena Ibra jamani? Jana si ulikuwa unashusha mzigo wewe huku ukijisifia kuwa biashara ni nzuri sana siku hizi!”
Sophia akaingilia yale mazungumzo,
“Ila jana yote nilikuwa na mume wangu na hatujafika hapa dukani kabisa, sasa ni jana gani unayoiongelea shemeji?”
“Mnajua msinichekeshe jamani, Ibra kama hukuwa hapa jana huu mzigo kashusha nani? Mzimu wako au? Na niliyekuwa nazungumza nae jana ni nani? Wewe si jana umeniambia kuwa nisikueleze tena habari za waganga wewe……..”
Kabla hawajaendelea na yale mazungumzo baba John akaitwa na kuelekea alipoitwa, Ibra na mkewe wakatazamana kwa muda kisha Ibra akamwambia mkewe,
“Ndio haya haya maajabu ya kumuona Jane nyumbani halafu yeye anakataa kuwa hakuj”
“Kweli haya ni maajabu mume wnagu, unajua nakosa jibu kabisa hiyo jana ni jana gani jamani loh mbona maajabu!”
“Maajabu haswaa, na zaidi ni huu mzigo hapa dukani kauleta nani? Yani Baba John ananishangaza sana kusema kuwa mzigo huu nimeushusha mimi, kwanza sina pesa za kushusha mzigo kiasi hiki mie”
Wakajikuta wakijadili bila kupata muafaka wala kupata jibu la aina yoyote lile.
Muda kidogo alifika mteja na kununua bidhaa kwenye duka lao, kisha wakampatia na kuchukua pesa ila wakati wanafungua droo ili kuiweka ile hela wote walishangaa sana na kutazamana kwani walikuwa droo ikiwa imejaa pesa,
“Ibra zimetoka wapi pesa zote hizo?”
“Sijui yani hata mimi mwenyewe nashangaa tu kuwa zimetokea wapi pesa zote hizo”
“Maajabu haya ujue”
“Ni maajabu kweli”
“Au uliacha pesa umesahau mume wangu?”
“Yani niache pesa zote hizo? Sophy uchumi wangu unaujua kabisa, yani nichukue mzigo halafu niwe na pesa zote hizo nitazitoa wapi? Na hata kama isingekuwa mzigo mpya bado siwezi kuwa na pesa nyingi hivyo”
“Basi tuzibebe twende nazo nyumbani”
Wakakubaliana hivyo na kuchukua mfuko na kuziweka zile pesa ambapo walijaza mifuko miwili kisha wakatoka na kufunga duka halafu wakaelekea kwenye gari yao huku wakipanga kuwa wakifika nyumbani waanze kuzihesabu hizo pesa,
“Yani Ibra hii hela imenipa imani sana moyoni dah! Hela nyingi hivi, umasikini kwaheri, sasa tutaanza kufanana na nyumba tunayoishi”
“Sophia unavyofurahia hiyo hela utafikiri unajua ilipotoka”
“Hata sijali ilipotoka yani cha msingi tumeikuta dukani kwetu, hapa nina furaha hatari natamani tufike tu nyumbani tuanze kuhesabu yani haya ni mamilioni mume wangu. Umasikini kwaheri, hizi hela tumezikuta dukani kwetu kwahiyo ni za kwetu. Kama kuna wezi waliiba huko na kuja kuficha dukani kwetu imekula kwao yani kama vipi hata kile kibiashara tutakifunga”
Ibra akawa anacheka tu kwani alishaona kuwa mkewe amepagawa na zile pesa ukizingatia hajawahi kuona pesa nyingi kiasi kile.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Walipofika nyumbani wakashuka na ile mifuko yao na kuingia ndani, kisha kuzimwaga zile pesa na kuanza kuhesabu kabla ya kufanya kitu kingine. Walitumia muda mrefu kidogo katika kuhesabu zile pesa na walipomaliza wakapiga mahesabu tena na kutazamana,
“Kheee Ibra milioni mia uwiiiii jamani umasikini kwaheri yani kwaheri kabisa, hivi zilikaaje kwenye droo pesa zote hivi? Yani tumejipatia pesa kiulaini kabisa, sisi sio majambazi wala sio mafisadi ila tumejipatia pesa kiulaini, umasikini kwaheri jamani”
“Unajua Sophy mimi bado nashangaa kuwa hizi pesa zimetokea wapi?”
“Acha kushangaa bhana, hebu nikumbushe tena kile kibiashara chako kinamtaji wa shilingi ngapi?”
“Kheee leo inaitwa kibiashara jamani, kuna milioni kumi pale”
“Sasa milioni kumi kitu gani katika milioni mia mume wangu? Kwanza wewe zamani si ulikuwa unauza genge wewe na mtaji wako ambao haukufika hata laki! Kwahiyo hata hiyo biashara ya milioni kumi kwako ilikuwa miujiza, na sasa tunamiliki milioni mia waoooo yani furaha yangu ya leo sijui nani ataizima”
“Ila asophy usifurahi sana hadi tujue chanzo cha hii pesa”
“Acha zako bhana, unataka kunigeuka nini? Tena na mimi nataka uninunulie gari yangu nianze kujidai mie yani watanikoma , watajua jina langu la utoto, watajua kabla sijaitwa Sophia nilikuwa naitwa nani. Uwiiiiii kama najiona vile kwenye maisha ya kifahari na kitajiri”
Ibra akamsikitikia mkewe kwani aliona wazi kuwa ameingiliwa na ulimbukeni wa ile pesa kabisa kwani alionekana kusahau yote yaliyomsibu.
“Ninunulie gari kwanza, yani nataka niende nyumbani na gari yangu ili majirani wote wanishangae mimi jinsi ninavyong’aa kila mtu ajue Sophia kaingia. Atakayenisalimia tu, namchapa na elfu kumi dah haya maisha nilikuwa nayatamani sana”
“Sawa mke wangu, basi tukaweke benki hizi pesa”
“Benki? Tuweke benki ili iweje? Hizi tunatumia mume wangu, kuna msemo unasema ukipata tumia ukikosa jutia hakuna caha kwenda kuweka benki wala nini hapa ni kutumia hizi pesa tu mwanzo mwisho halafu sasa tutakuwa hatuendi tena hoteli mchwara tunatakiwa kwenda zile hoteli babkubwa. Watu husema tumia pesa ikuzoee kwahiyo lazima tutumie hii ituzoee bhana”
Ibra hakubishana na mkewe kwahiyo akakubaliana na maamuzi ya mke wake ingawa kwa kiasi fulani hata yeye zile pesa zilimpagawisha kiasi.
Wakakubaliana kuwa zile pesa waziweke chumbani kwao na kuamua kufanya hivyo ambapo zile pesa wakaziweka kwenye kabati la nguo chumbani kwao huku nguo zingine wakizitoa na kuzihamishia sehemu nyingine kisha wakaamua kwenda kula kwanza,
“Sasa mke wangu tupike au?”
“Tupike!! Kwanini tupike kwanza? Leo tunaenda kula hotelini yani ndio furaha yangu halafu kesho utaenda kuninunulia gari”
“Sawa, twende basi ili tuwahi kurudi”
Wakatoka nje na kuingia kwenye gari yao na kuanza safari, njiani wakaona hoteli kubwa sana na wote wawili kuishangaa ile hoteli,
“Kheee imejengwa lini hii?”
“Nadhani itakuwa mpya”
‘Twende tukale hapo basi”
“Hapana Sophy, twende sehemu ambayo tumeizoea tayari”
‘Hivi nilikwambia nini Ibra? Mambo ya kwenda kwenye hoteli uchwara tuache, twende hiyo mpya tujue kuna nini jipya. Kwani unahofu gani wakati pesa tunayo ya kutosha!”
Ibra akakubali kisha wakakunja na kuingia kwenye hiyo hoteli ambapo waliagiza chakula na kuletewa na kuanza kula, walikula huku wakikisifia kile chakula kuwa kizuri sana mwanzo mwisho.
“Itakuwa hapa kuna wapishi mahili sana”
“Na kweli maana si kwa utamu huu wa chakula”
Walipomaliza vyombo vilitolewa na kisha akaja muhudumu kwaajili ya kuchukua pesa ya malipo ya chakula.
Ibra alifungua ile pochi yake ya mkononi aliyobeba ili kutoa pesa ila alishangaa kuona hakuna pesa ya aina yoyote, akamuangalia mke wake na kumuuliza
“Inamaana hatujabeba pesa?”
“Mmmh hatujabeba pesa kivipi?”
“Sioni hela kwenye waleti yangu”
“Tutafanyaje sasa?”
Mara wakamsikia yule muhudumu akiwaambia,
“Kama mmesahau hela msijali kitu, nitawasaidia”
Kwa pamoja walijikuta wakimuangalia kwa makini huyu muhudumu mwenye moyo wa kipekee, gafla walishangaa kuona kuwa yule muhudumu alikuwa ni Neema kwakweli walishtuka sana.
wakajikuta kwa pamoja wakisema
“Neema!!”
“Ndio ni mimi, vipi mmeona mzuka au?”
“Aaah unafanya hapa kazi?”
“Ndio, mimi ni mpishi mkuu hapa”
“Aaah imekuwaje hadi wakakuajiri hapa?”
“Kwani mimi nina kasoro gani ya kufanya nishindwe kuajiriwa?”
Ibra na Sophia wakatazamana tena, kisha Sophia kwa uoga akamwambia Neema,
“Je tunaweza kuondoka?”
“Njia nyeupe kabisa nimewaruhusu”
Wakainuka huku wakiwa wamejawa na uoga uliopitiliza, wakaelekea kwenye gari yao moja kwa moja na kupanda kisha safari ya kurudi ikaanza huku kila mmoja akishindwa kumuongelesha mwenzie chochote.
Walifika nyumbani na kuingia ndani, walifika sebleni na kukaa kisha wakaanza kuulizana
“Hivi imekuwaje tumetoka bila ya pesa?”
“Hata mimi sielewi imekuwaje”
“Hivi pale isingekuwa Yule Neema tungefanyaje?”
“Ndio hapo sasa, yani hadi saizi najishangaa kuwa ilikuwaje hadi kusahau kubeba pesa jamani!”
“Ila ndio tujifunze mume wangu kuwa tunatakiwa kuishi na kila mtu kwa upendo maana bila Neema pale angetusaidia nani jamani dah!”
“Ila dah najikuta nikiwa na maswali mengi bila ya jibu, kwanza ile hoteli imefunguliwa lini? Neema kaanza kazi pale lini? Mambo mengine yanachanganya sana jamani mmh”
“Halafu unajua nini, mi sikuwahi hata kuona kama kuna ujenzi eneo lile jamani, kweli kuna mambo mengine ni ya siri sana”
“Hivi unakumbuka kuwa lile eneo lilikuwa na nini kabla ya ile hoteli?”
“Hata sikumbuki, ila kesho twende tena tukamlipe Neema na kumpa pesa ya asante kwa kutusaidia”
Muda kidogo wakasikia Yule mtoto akilia,
“Mmmh hivi huyu mtoto ana muda wake maalum wa kulia nini”
Kisha Ibra akainuka na kwenda kumchukua Yule mtoto kisha akaenda nae sebleni,
“Eeeh tufanyaje na huyu mtoto?”
“Tumkorogee maziwa tumpe au umesahau kuwa tumekubaliana kutokumnyonyesha tena?”
“Nakumbuka mke wangu, basi nenda jikoni ukamkorogee hayo maziwa tuje tumpe”
Sophia akainuka na kuelekea jikoni kwa lengo la kwenda kumkorogea maziwa Yule mtoto ili anywe.
Sophia akiwa jikoni wakati anataka kubandika maji, gafla alijiona akisukumwa kwa nguvu na kuanguka chini kisha akahisi chuchu zake zikinyonywa tena kwa nguvu tu kwakweli Sophia alitamani kupiga makelele ila alishindwa na kujikuta akigugumia kwa maumivu tu huku akishangaa kuwa ni nani anayemnyonya maziwa yake bila ya kumuona kwahiyo alikuwa akihangaika tu.
Sebleni nako Ibra alishangaa kuona mkewe hatoki jikoni kwenye uandalizi wa hayo maziwa, ila kilichokuwa kikimshangaza ni kuwa kila alipomtazama Yule mtoto alimuona midomo ikicheza kanakwamba alikuwa ananyonya kabisa na kwa wakati huo alitulia tuli ila kwa haraka haraka Ibra alihisi kuwa ndio kawaida ya watoto kwani wote huwa na tabia hiyo ya kujinyonyanyonya hatakama hawanyonyi kwa muda huo. Akaamua kumuita mkewe ili aharakishe hayo maziwa,
“Sophia, vipi wewe hayo maziwa yanachukua masaa jamani!!! Huyu mtoto anajinyonya midomo atajiumiza bure, lete hayo maziwa bhana”
Sophia hakujibu chochote, na kufanya Ibra amuweke Yule mtoto kwenye kochi ili akamuangalie Sophia jikoni ila alipomuweka kwenye kochi tu Yule mtoto na kuinuka akaanza kulia kamavile kaangushwa chini kwahiyo Ibra alikuwa akirudi na kumbembeleza, alijikuta akifanya hivyo kama mara tano akaona ni vyema ambebe aende nae jikoni.
Alivyofika jikoni alishangaa kumuona Sophia chini akigalalagala, akamshtua
“Sophy, Sophy una tatizo gani mke wangu jamani?”
Sophia akashtuka sana na kumuangalia mume wake kwa jicho lililojaa hofu iliyowazi kabisa,
“Niambie mke wangu nini tatizo?”
“Aaah aaah maziwa yangu…..”
Yule mtoto alianza kulia tena kilio cha ajabu kama ameangushwa vile, Ibra akamkabidhi Sophia Yule mtoto,
“Unanipa wa nini jamani?”
‘Mshike bhana, watoto wa hivi wakiwa na njaa ni bora wakahisi jasho la wamama kuliko la sie vidume”
“Tatizo hujui kilichonipata hata usingenipa huyu mtoto nimshike”
“Nenda kakae nae sebleni ili mimi niandae hayo maziwa maana naona umeshindwa wewe”
Sophia hakuweza kuongea akainuka na Yule mtoto hadi sebleni ambako alifika na kumuweka pembeni ya kochi. Gafla, Sophia alishtukia akipuliziwa kama kitu usoni na kuanguka pale kwenye kochi. Ibra alipotoka jikoni alishtuka sana kwani alimuona Yule mtoto akiwa juu ya Sophia huku akinyonya kwakweli kitendo hiki kilimchukiza Ibra na kumshtua huku akiamini wazi kuwa Sophia hawezi kufanya hivyo, ikabidi amshtue Sophia ila Sophia hakushtuka kabisa na kumfanya Ibra aanze kuingiwa na uoga akaamua kwenda jikoni ili achukue maji aje ammwagie mkewe azinduke ila Ibra alipoingia jikoni tu alishangaa akipiga mueleka hadi chini na kupoteza fahamu kabisa.
Ibra alipokuja kuzinduka ilikuwa giza limeshaingia kabisa, akajikongoja na kwenda kuwasha taa huku akijinyoosha nyoosha bila ya kujua kilichotokea, akatoka mule jikoni na kuelekea sebleni ambapo alimkuta mkewe akiwa na hali ya kutokujitambua kabisa huku Yule mtoto akiwa pembeni kwa muda huu, Ibra akakumbuka kuwa mara ya mwisho alimkuta mkewe akimnyonyesha huyo mtoto kwahiyo moja kwa moja akahisi kuwa mkewe nguvu zimemuisha kutokana na kunyonyesha, Ibra akamsogelea mkewe na kujaribu kumuamsha, muda huu Sophia aliamka ila kwa shida sana na sauti yake ilikuwa chini kama asubuhi moja kwa moja Ibra akahisi kuwa mkewe kazidiwa na njaa akawaza pa kupata chakula kwa muda huo, akachukua simu yake na kuangalia muda akaona kuwa ni saa saba usiku.
“Kheee sasa saba? Jamani imekuwaje tena, yani saa saba hii tutapata wapi chakula sasa?”
Ikabidi ajishauri kuwa aende tu jikoni akampikie mke wake, ila alipofika jikoni alikuta chakula kikiwa cha moto kabisa kwenye sufuria kanakwamba kimepikwa muda sio mrefu, kutokana na hali ya mkewe ikamfanya Ibra asijihoji sana na kupakua kile chakula kisha kwenda nacho sebleni na kuanza kumlisha mke wake ambapo alikula hadi pale alipoonekana kurejewa na nguvu zake. Ibra alimpa pole sana mke wake huku akimuonea huruma sana, yani walikuwa wakizungumza muda huo kamavile kumeshakucha tayari.
“Unajua Ibra mimi nashindwa kuelewa mume wangu, imekuwaje huyu mtoto kuninyonya tena?”
“Hata mimi sielewi na ndio nilikuwa nangoja uwe sawa ili nikuulize kuwa huyu mtoto vipi maana nashindwa kumuelewa kabisa”
“Huyu mtoto si wa kawaida mume wangu, sio wakaida kabisa”
“Sasa tutafanyaje?”
“Tukamtupe, mimi siwezi kuendelea hivi, unajua naweza kufa mimi kwasababu ya ujinga wa huyo mtoto! Tumtupe mume wangu”
“Basi, basi ngoja pakuche ndio tukamtupe”
“Sasa pakikucha tutamtupaje jamani si watu watatuona?”
“Kwakweli mimi siafiki kumtupa huyu mtoto usiku huu, tunatakiwa kuwa na huruma ya kibinadamu kiasi. Pakikucha tutapata jibu tu.”
Walijikuta wakiongea usiku wote kwani hakuna aliyetamani hata kulala huku wakiambiana vitu vya kuwashangaza tu.
Kulivyokucha, Sophia alichukua simu yake na kumpigia Siwema kwa lengo la kumuomba ushauri.
“Yani wewe Sophia wa kunisahau mimi wewe? Leo ndio unanikumbuka loh, haya niambie kuna shida gani tena maana hupigi simu bila ya tatizo ila kama ni maswala ya kuwapeleka kwa waganga sipo tayari”
Siwema alikuwa akifunguka tu kwani tayari walishamkera kuhusu Yule babu aliyekufa,
“Tuna tatizo dada, kuna mtoto tumemuokota sasa katushinda kumlea na tumeamua kumtupa tena je unatushauri nini?”
“Kheee Sophia una akili kweli wewe? Yani mumtupe mtoto kweli? Sio jambo jema hata kidogo, mimi nawashauri labda mumpeleke kituo cha kulelea watoto yatima”
“Ndio wapi huko dada?”
“Hebu usinichekeshe Sophia yani hujui vituo vya kulelea watoto yatima wewe? Hebu kwanza ngoja nije huko kwenu”
“Itakuwa vizuri sana dada, asante”
Simu ikakatika kisha Sophia akamueleza Ibra vile alivyoongea na Siwema,
“Kama anakuja itakuwa vizuri sana mke wangu maana kiukweli nimechoka vituko vya huyu mtoto haswaaa kile kitendo cha kumuona akipanda kifuani kwako na kunyonya”
Muda huu wakaenda kuoga na kunywa chai kabisa kisha wakarudi sebleni wakimsubiri Siwema na kuendelea na maongezi yao ya hapa na pale.
Muda kidogo Siwema aliwasili na kuwagongea mlango, walimfungulia na kumkaribisha ndani. Aliingia na kusalimiana nao kisha kukaa kwenye kochi na kumuona Yule mtoto akiwa amelazwa kwenye kochi pia.
“Kwahiyo mtoto mwenyewe ndio huyo?”
“Ndio ni huyo dada”
“Mmemuokota wapi na nyie?”
“Kwnye gari”
“Kheeee msinichekeshe, kwenye gari mmemuokotaje?”
Ikabidi wamueleze ilivyokuwa hadi kumchukua huyo mtoto,
“Kwahiyo inamaana kuna mtu kawawekea huyo mtoto?”
“Ndio”
“Eeeh anaitwa nani?”
“Kwakweli hatujampa hata jina huwa tunamuitaga mtoto tu hivyo hivyo”
“Na je mlivyomuokota mlienda kuripoti polisi?”
“Hapana”
“Ila kwakweli nyie mnamatatizo sana sijui hata akili zenu huwa zinawaza vitu gani, haya sasa mnataka kumtupa tena bila hata ya kufikiria jamani. Huyu mtoto apelekwe kwenye kituo cha kulelea watoto yatima kama mmeshindwa kumlea, kwahiyo mmekaa nae hapa kwa muda gani na alikuwa anakula nini siku zote mlizokaa nae?”
Wakaanza kumueleza jinsi walivyoishi nae na chakula alichokuwa anakula,
“Mungu wangu, hivi nyie akili zenu ni nzima kweli jamani? Kheee mpo kama watu sijui wa dunia ya wapi? Ona sasa hadi mimba imetoka, ulishindwa hata kuomba ushauri jamani? Haya leteni nguo za huyu mtoto haraka tumpeleke huko”
“Hana nguo zozote zaidi ya hizo alizozivaa’
“Kheeee mnazidi kunipa maajabu, kwahiyo siku zote hizi alikuwa akinya na kukojoa mnamvalisha nguo gani? Hamumuogeshi huyo mtoto?”
“Kwakweli dada toka siku tumeingia na huyu mtoto humu ndani hatujawahi kumuogesha, hajawahi kunya wala kukojoa”
Siwema alizidi kushangaa Yule mtoto na kuwashangaa wanaoishi nae pia, hakutaka kupoteza muda akawaomba wambebe ili apelekwe huko kwa watoto yatima.
Wakambeba na kutoka nae nje kisha kuingia kwenye gari na kuanza safari ya kwenda huko kituoni.
Wakati wanatoka Sophia akaamua kumsimulia Siwema kuhusu hoteli waliyoenda jana na jinsi walivyokutana na Neema, Siwema alishangaa tu na kuwauliza mahali ilipo hiyo hoteli .
“Usijali tutakuonyesha ni mpya kabisa hiyo hoteli”
“Yani ndio imefunguliwa huku duh!”
“Kumeendelea huku siku hizi sio kama zamani”
Walipofika kwenye hiyo njia wakapanga kumuonyesha Siwema hiyo hoteli ila walishangaa ambavyo hawakuiona hiyo hoteli wala nini,
“Sophy, ile hoteli si ilikuwa hapo au nimesahau?”
“Mie nakumbuka vizuri ilikuwa hapo, imekuwaje tena jamani?”
Siwema alipoangalia kwa makini eneo lile alishangaa pia na kuwauliza,
“Mbona eneo lenyewe limeandikwa ni eneo la makaburi sasa hiyo hoteli iko wapi?”
Na wao wakaangalia kwa makini sasa wakaona kibao kilichoandikwa kwa herufi kubwa ‘ENEO LA MAKABURI’ wakatazamana na kushangaa, na walipoangalia vizuri wakaona makaburi mengi tu yamejipanga.
Ibra alimuuliza mkewe kwa hamaki,
“Eneo la makaburi kivipi? Tumesahau au?”
“Makubwa haya mume wangu”
Siwema akawauliza jina la hiyo hoteli lakini hakuna hata mmoja kati yao aliyekuwa na kumbukumbu ya jina,
“Hivi tuliangalia jina kwani?”
“Hatukuangalia bhana, mi nakumbuka tuliingia na kula kisha kuondoka”
Siwema alivyoona wanajiuma uma tu akawaomba waondoke eneo hilo,
“Tuondokeni hapa na tuendelee na safari yetu”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Ibra akaondoa gari kisha safari yao ikaendelea, Siwema alianza kuongea kwa kuwapa ushauri hawa watu wawili,
“Kwanza kabisa mnachotakiwa kufahamu ni kuwa Neema ni mtu wa aina gani? Je ni binadamu wa kawaida? Na kama ni binadamu wa kawaida aliwezaje kufanya yote yale? Ni binadamu gani anayeweza kufanya vile? Jiulizeni ili mpate majibu ila mkiendelea hivi mtakuwa mnakutana na maajabu kila siku, na mkiona mambo yamewafika shingoni kuna Sheikh fulani hivi huwa anafanya sana dua itabidi niwapeleke huko”
“Mmmh dada na wewe umeanza sasa, umemaliza ya waganga unatuletea habari za Masheikh”
“Kwani kuna ubaya gani? Linaloshindikan
a kwa mwanadamu basi ujue Mungu anaweza”
“Ndio Mungu anaweza, ila kwanini twende kote huko kwani sie Mungu hatusikilizi?”
“Uwiiiiii nyie watu ni wabishi sana sijui hata mmeumbwa vipi nyie halafu wote mmekutana akili zenu zinafanana, ila kuhusu waganga siwapeleki tena mlinitia aibu sana”
“Hata hivyo hatuna uhitaji wa kwenda kwa waganga tena, tutakapomtua huyu mtoto basi tumemaliza kila kitu. Maswala ya kutupeleka kwa Masheikh sijui wachungaji halafu waanze kutuomba sadaka hatupo tayari kwakweli”
“Aliyewaroga kafa maana angekuwa hai basi angewaonea huruma”
Kimya kidogo kikatawa huku ile safari ikiendelea mpaka walipofika eneo la tukio.
Ibra akasimamisha gari na kushuka kisha Siwema nae akashuka ambapo wakapanga kuwa wakazungumze kwanza na wahusika kisha ndio wampeleke mtoto, kwahiyo walimuacha mtoto na Sophia ndani ya gari.
Walifika mapokezi na kupokelewa vizuri tu kisha kuwakuta wale wahudumu wa kituo ambapo waliongea nao kwa urefu kidogo ili wapokelewe huyo mtoto,
“Ila kama na nyie mnauwezo mnaweza mkamlea tu huyo mtoto bila tatizo ila cha msingi tu ni kutoa taarifa polisi na kwenye ubalozi wako watambue hilo ili kama atatokea mtu yeyote kumdai mtoto huyo muwe na haki za kisheria kama mtoto wenu kabisa”
“Sisi tungemlea dada ila majukumu ni mengi sana, hata hivyo tutakavyomuacha hapa sio kwamba tumemtelekeza hapana ila tutakuwa tunakuja mara kwa mara kumtembelea.”
Basi huyu dada akawapa taratibu zote ambapo kuna fomu walijaza kisha akawaambia wampeleke huyo mtoto, wakainuka kwa lengo la kwenda kumchukua mtoto nje.
Walipofika nje Ibra alishangaa kuona gari yake ikiwa imefunguliwa milango yote yani iko wazi, akapata hofu na kujiuliza kama mkewe anaweza kufanya vile kweli. Wakasogea karibu na kuangalia ndani ya gari ila hakuonekana Sophia wala yule mtoto, Ibra alimshtua Siwema
“Dada, hivi unajua Sophia na mtoto hawapo humu?”
“Hawapo kivipi? Si tumewaacha humo? Na je ni nani aliyefungua milango yote ya gari hivyo?”
“Hata mimi nakosa jibu dada, ni nani anayeweza kufanya hivi kwenye gari yangu?”
Wakajaribu kuangaza huku na huko ila hakuonekana Sophia wala yule mtoto na haikujulikana ni wapi wameelekea,
“Makubwa haya dada”
“Sio makubwa ila ni maajabu, inamaana wametekwa?”
“Usiseme hivyo dada, kumbuka nampenda sana mke wangu Sophy”
“Sasa tutaanzia wapi kumtafuta?”
Wakaambizana wajaribu kuuliza watu wa hapo karibu ili kama kuna mtu amewaona awaambie, wakazunguka pale ila kila mtu waliyemuuliza aliwashangaa tu na kuwaambia kuwa hawajamuona huyo mdada aliyebeba mtoto, walizunguka sana na kuchoka mwishowe Siwema akatoa wazo kuwa waende kuripoti polisi ili kama Sophia ametekwa wajue ni wapi pa kuanzia.
Wakakubaliana hivyo na kuingia kwenye gari wakielekea kwenye kituo cha polisi, walipokuwa wanakaribia kituoni hapo wazo likamjia Ibra kuwa wampigie simu Sophia,
“Kheee halafu kweli, yani muda wote tumekazana kumsaka bila ya kumpigia simu duh! Hebu mpigie hapo shemeji”
Ibra akachukua simu yake na kumpigia simu Sophia muda huo huo ambapo baada ya sekunde chache tu kuita simu ikapokelewa na ni Sophia ndiye aliyekuwa akizungumza kwenye simu ile,
“Uko wapi Sophy?”
“Nipo nyumbani, kwani vipi?”
“Vipi? Hujui kwani jamani, si tumekuja wote huku kwa lengo la kumuacha huyo mtoto, kwanini umeondoka bila ya kunitaarifu?”
“Ibra usinichanganye bhana yani usinichanganye kabisa, wewe mwenyewe utoe wazo la kurudi nyumbani halafu saizi unilaumu, usinichanganye tafadhali. Leo umenifurahisha usitake kuibadilisha furaha yangu tafadhali, rudi nyumbani na ulete hiyo mboga uliyosema”
Kisha Sophia akakata simu, Ibra akamuangalia Siwema na kumwambia,
“Unajua dada huyu Sophia ni mwehu sana, yani hata haelewi ni jinsi gani wenzie tumehangaika kumtafuta jamani. Eti yupo nyumbani, yani nimeshindwa kumuelewa kabisa akili zake sijui zikoje”
“Nyie mnajuana wenyewe, yani hapa nimechoka balaa kwa ujinga wenu. Mtu nimeacha shughuli zangu ila mmeishia kunisumbua tu. Hebu nirudishe nyumbani kwangu mie”
“Basi tupitie nyumbani kwangu kwanza ukamseme mdogo wako”
“Weee Ibra tafadhali usinitie uchizi, mi nina akili zangu timamu kabisa. Hebu fikiria ni toka saa ngapi tunamtafuta huyo Sophia wako hadi jioni hii halafu unaniambiaje? Hebu nipeleke nyumbani mie, nyie mtajuana wenyewe na akili zenu mbovu hizo”
Ibra hakubisha sana zaidi ya kugeuza gari yake na kuanza safari ya kumpeleka Siwema nyumani kwake.
Walipofika nyumbani kwa Siwema ilikuwa jioni sana ila Siwema aliposhuka Ibra akamuomba maji ya kunywa kwahiyo Siwema akaenda ndani kwa lengo la kumletea maji hayo, wakati Ibra yupo pale nje akiwa amefungua mlango wa gari yake na kuangalia angalia mazingira ya pale huku akisubiri hayo maji akaja yule bibi ambaye aliwahi pia kukutana na Sophia. Ibra alimsalimia yule, bibi ila yule bibi kabla ya kuitikia akamwambia Ibra,
“Nyumba yako ni nyumba ya maajabu”
“Nyumba ya maajabu! Kivipi?”
“Wewe unaiona nyumba yako kuwa sawa? Je wewe mwenyewe unajiona kuwa sawa? Hilo gari unalotembelea je unahisi lipo sawa?”
“Sikuelewi, hebu nieleweshe”
“Nyumba yako ni ya maajabu, nimewahi kukutana na mkeo nikamwambia maneno haya na ilikuwa mapema sana ila hakutaka kunielewa. Mkihitaji msaada njooni niwasaidie ila ile nyumba ni ya maajabu”
“Sikuelewi bibi yani sikuelewi kabisaa”
“Ngoja nikueleweshe sasa”
Mara Siwema akatoka ndani akiwa na kikombe cha maji, na alipomuona yule bibi tu kama kawaida akaanza kufoka,
“Hivi wewe kizee unataka nini nyumbani kwangu jamani! Si kila siku nakwambia sitaki kukuona wewe, tafadhali ondoka, nimesema ondoka tena sasa hivi”
Ibra akamuangalia Siwema na kumwambia,
“Tafadhali usimfukuze, yupo kuniambia maneno ya maana sana hapa”
“Maneno ya maana atakuwa nayo huyo bibi? Hawezi kuwa na la maana hata moja, huyo bibi ni mchawi wa wachawi, mtaani kwake kashafukuzwa ndio anatanga tanga huku yani usimsikilize hata moja uatajuta zaidi ya unavyojuta sasa”
Kisha Siwema akamuangalia tena huyu bibi na kumfokea,
“Hivi bibi husikii jamani, si nimekwambia uondoke! Nenda zako bhana hakuna mwenye haja ya miushauri yako isiyo na maana”
Yule bibi alitikisa kichwa kisha akaondoka zake kisha Siwema akakzana kumwambia Ibra kuhusu mabaya ya yule bibi ambayo yeye amesimuliwa na watu wengine.
“Ila ushawahi kushuhudia?”
“Kushuhudia kitu gani? Mi nishakwambia kwamba huyu bibi ni mchawi na nilimuonya Sophia hivi hivi, mwisho wa siku hadi leo akibeba mimba zinatoka unafikiri ni sababu ya nini?”
“Mmmh usiniambie ni sababu ya huyu bibi?”
“Ndio, hiyo ndio sababu. Alikutana nae pale kwenye mpera wakati Sophy anatafuta pera, mi nikamkataza kuongea na huyu bibi ila yeye akakazana kuongea nae na mwisho wa siku ameishia kupoteza mimba kila leo. Ni huyu bibi tu anayekula watoto wenu”
Ibra alishangaa sana na kumfanya ashindwe kunywa hata yale maji kisha akamuaga Siwema,
“Kheee hata maji umeghairi kunywa?”
“Yani nimejisikia vibaya gafla dada, roho huwa ianiuma sana nikikumbuka watoto wangu. Ngoja tu akili yangu ikae sawa ila huyu bibi nitamkomesha”
Ibra akaingia kwenye gari yake na kuondoka zake akielekea nyumbani kwake.
Alipofika nyumbani kwake kuna kitu cha tofauti alikiona na kilimshangaza sana huku akiangalia mara mbili mbili na kujiuliza,
“Tuseme kuna mgeni amekuja au? Na kama kuna mgeni amekuja basi mgeni huyo ni nani?”
Alikosa jibu ila ile gari ya pale uwani kwake ilimchanganya sana kwani ilikuwa ni gari mpya kabisa tena ya gharama, Ibra akaingia ndani akitegemea kumuona mgeni ila alishangaa kumuona mkewe akiwa mwenyewe pale sebleni, akamsalimia ila kabla Ibra hajauliza chochote kuhusu ile gari, akaulizwa swali na Sophia
“Hiyo mboga uliyosema unaifata iko wapi?”
“Mboga? Mboga gani tena?”
“Halafu Ibra acha masikhara, sijui unafikiri tutapika nini usiku wa leo jamani”
Ibra hakuta kubishana na mkewe kuhusu maswala ya mboga kwahiyo moja kwa moja akamuuliza kuhusu gari aliyoiona pale nje,
“Na ile gari pale nje ni ya nani?”
“Gari gani hiyo?”
“Ile mpya”
Sophia akacheka kwanza kisha kumjibu mumewe kwa kicheko,
“Ila Ibra mara nyingine unatakaga kunichekesha tu. Ile gari si umeninunulia mwenyewe jamani!”
“Nimekununulia! Saa ngapi nimekununulia wakati mimi uliniacha kule”
“Weee Ibra wewe hebu kuwa makini basi yani kabisa unaniuliza kuhusu gari ulilonunua mwenyewe jamani! Hiyo gari si umeninunulia kama tulivyoongea kipindi kile kuwa nahitaji gari langu”
“Sophy acha kunichanganya bhana hebu niambie ukweli”
“Ukweli gani sasa zaidi ya huo?”
“Hebu niambie ulipotoka pale kituoni ulielekea wapi?”
“Si tuliondoka pamoja pale au umesahau?”
Ikabidi Ibra aseme amesahau kwani kila alipomwambia mkewe kuwa hawakutoka wote mkewe alibisha kwahiyo akamwambia kuwa amesahau ili amwambie ilivyokuwa maana alikuwa akishangaa tu yote aliyokuwa akielezwa na mkewe,
“Na kweli naona umepoteza uelekeo kwenye kichwa chako, ngoja nikueleze vizuri labda kumbukumbu zako zitarejea”
Ibra akatulia tuli kumsikiliza mkewe,
“Mimi nilibaki kwenye gari na mtoto, kisha wewe na Da’Siwema mkashuka kwenda ndani mule muda kidogo ukarudi na kuniambia kuwa umeona sio vyema tumuache mtoto mahali hapo sababu mazingira yake sio mazuri na malezi yao yanaonekana kuwa duni, kwahiyo ukasema turudi nyumbani. Nikakuuliza vipi Da’Siwema tunamuacha? Ukasema kuwa amesema tumuache tu kuna vitu anachunguza, halafu tukarudi wote hapa. Ukasema unaenda kuniletea zawadi, ukatoka na muda kidogo ukarudi na hiyo gari na kunikabidhi kila kitu kuhusu hiyo gari nikafurahi sana hapa ndio ukaniaga kuwa kuna mboga umeikumbuka sana unaenda kuinunua tule leo. Na ndio muda huu umerudi mume wangu eti unajifanya umesahau kila kitu loh!”
“Yani Sophy hata nikikuelekeza huwezi kunielewa kwakweli hata sijui nikuelekezeje”
Ibra aliinama akiwa na mawazo sana huku akijiuliza kuwa ni vitu vya aina gani hivyo maana alishindwa kabisa kumuelewa mke wake na kumfanya Sophia nae amshangae tu.
Sophia alifikiria kitu na kuhisi kuwa huenda mume wake amevurugwa tu, kisha akainuka na kumuomba funguo ili akaangalie kwenye gari ambapo Ibra alimkabidhi funguo hiyo.
Sophia alitoka nje na kwenda kufungua gari ambapo pembeni ya kiti cha dereva akaona mfuko mweusi kufungua akakuta mboga, akacheka na kusikitika kisha akasema.
“Huyu mwanaume sijui amevurugwa na nini jamani, mboga si hii hapa kwenye mfuko halafu anasema hajaileta loh! Huyu mume wangu nae kashakuwa tatizo tayari”
Akabeba ule mfuko na kuelekea nao ndani kisha akamwambia mume wake,
“Ibra, mboga si hii hapa umeleta halafu unasema hujaleta”
“Mboga gani Sophia? Hivi unajua kama unanichanganya tu”
“Nakuchanganyaje? Si ulisema leo unahamu na pweza wewe! Na hawa hapa umeleta, tena umeweka na chachandu inanukiaje”
Kisha Sophia akaingiza mkono kwenye mfuko ili kuchukua kipande aonje, Ibra akashtuka na kumkataza mke wake
“Tafadhali Sophy usile, mimi sijui ilipotoka hiyo mboga. Sijainunua mimi”
“Acha masikhara yako bhana”
Sophia akaingiza kile kipande mdomoni na kuanza kukitafuna huku akisifia kuwa ni tamu sana, kwakweli Ibra alitamani kufanya kitu ila alishindwa kwani aliiona akili yake kama ikichanganyikiwa hivi.
Mara gafla Yule mtoto akaanza kulia chumbani kwa nguvu kamavile kaangushwa, Sophia akakimbilia chumbani kwenda kumuona mtoto Yule kuwa kwanini analia vile.
Sophia alipomuona Yule mtoto alishtuka na kupiga kelele za kumuita Ibra,
“Ibra, Ibra njoo uone”
Ibra alikwenda kwa haraka sana, naye alishtuka pia kwani Yule mtoto alikuwa akilia sana halafu macho yake badala ya kutoa machozi yalikuwa yakitoa damu.
Ibra alimuangalia mkewe huku amejawa na hofu zaidi, kisha akamuuliza
“Tutafanyaje sasa?”
“Inabidi mimi nikuulize wewe maana hata sijui tufanyeje”
“Hebu kalete maji jikoni”
Sophia akatoka na kuelekea jikoni, ila ule muda Sophia alipotoka na yale machozi yaliyokuwa yakimtoka Yule mtoto kama damu yalikata na kumfanya Ibra ashangae zaidi kisha kumwambia mkewe kwa sauti,
“Basi usilete tena”
Sophia akarudi tena chumbani na gafla Yule mtoto akaanza kutoka tena machozi ya damu,
“Kheee huyu mtoto vipi wakati hiyo damu ilishakatika?”
“Labda hataki kuniona”
“Mara ngapi anakuona? Iweje leo?”
Ibra akamuangalia vizuri mkewe akaona akizunguka tu na ule mfuko wake wa pweza,
“Mbona unazunguka na huo mfuko jamani! Kauweke jikoni basi”
Sophia akatoka tena, safari hii Yule mtoto aliacha kulia na waala zile damu hazikumtoka tena. Sophia aliporudi alishangaa kumuona Yule mtoto akicheza tu wala damu hazikuwepo tena
“Kheee umemfanya nini hadi katulia hivi?”
“Sijamfanya chochote ila hata mimi mwenyewe nimeshangaa huo utulivu wake mara baada ya wewe kupeleka ule mfuko jikoni”
“Mmmh inamaana ule mfuko ndio tatizo?”
“Inawezekana”
Sophia hakukubaliana na hiyo hoja ya mumewe kwahiyo akataka kuhakikisha kama ni kweli, akaenda tena jikoni kuchukua ule mfuko na kuja nao chumbani. Gafla Yule mtoto alianza kulia kwa nguvu na macho yake kutoa machozi ya damu. Ikabidi Sophia atoke na ule mfuko tena na kuurudisha jikoni kisha akaenda tena chumbani, Ibra akamwambia mkewe
“Umeamini sasa kuwa ule mfuko ndio tatizo?”
“Mmmh yani nashindwa kuelewa ujue kuwa kuna mahusiano gani kati ya huyu mtoto na ule mfuko hadi atoe machozi ya damu”
“Hata mimi bado sielewi”
“Ngoja nikauchukue tena”
“Acha bhana Sophy usiende kuuchukua”
“Naenda kuuchukua, nataka kujua kisa na mkasa. Nataka kujua nini ni nini”
Sophia akatoka tena pale na kuelekea jikoni kwa lengo la kuuchukua tena ule mfuko.
Alipoingia jikoni alishangaa kuona ule mfuko hauonekani pale alipouweka, na kujiuliza kuwa huenda umeanguka ila kila alipoangalia hakuuona
“Mmmh ni nani anayeweza kuuhamisha mfuko ule ilihali humu ndani tupo wawili tu na muda wote huu mume wangu yupo chumbani!”
Sophia alijiuliza bila ya kupata jibu la aina yoyote ile na kumfanya abaki na maswali mengi kichwani mwake, akaamua kurudi chumbani alipo mumewe ambapo safari hii alimkuta amekaa kitandani
“Hivi unaweza kuamini kuwa ule mfuko haupo tena”
“Haupo tena kivipi?”
“Pale nilipouacha sijaukuta, unajua ni maajabu haya”
“Yani hayo ndio unaona maajabu ila swala la mumeo kuwa wawili hata hushangai”
“Mume kuwa wawili kivipi wakati uko peke yako?”
“Hivi wewe hata akili yako haijafunguka mpaka sasa kuwa uleyerudi nae mchana nyumbani hakuwa mimi”
“Mmmh kama hakuwa wewe, sasa lile gari amenunua nani?”
“Ndio ujitafakari hapo mke wangu ila hakuwa mimi”
Sophia akanyamaza kwa muda na kuwa kama akitafakari kitu kisha akamuangalia mume wake na kumwambia,
“Hivi unakumbuka kuna siku kabla ya kumuokota huyu mtoto tuliwahi kusikia sauti ya mtoto akilia kama huyu, unakumbuka?”
“Nakumbuka ndio na inanifanya nihisi kuwa kunakitu tumefanyiwa ila tu hatujajuwa kuwa tumefanyiwa na nani”
“Inamaana kwamba huyu mtoto alikuwepo ndani toka siku hiyo, je ni nani aliyemleta?”
“Umenifanya nifikirie kitu mke wangu, nahisi ni Neema aliyemleta huyu mtoto na ni yeye aliyetuwekea kwenye buti la gari na kuandika ile barua yenye vitisho vikali”
“Unahisi alikuwa na lengo gani?”
“Nahisi hakufurahishwa na swala la kuondoka hapa kwahiyo akatuletea huyu mtoto ili atusumbue na tupate shida halafu tuwe na uhitaji wake wa kutusaidia ndiomana akafanya hivi”
“Na kwakumkomesha hata tusimtafute wala nini, ni bora tuhangaike na huyu mtoto mdogo kuliko kuhangaika na Neema mtu mzima”
Wakapanga muda huu wamtengenezee huyu mtoto maziwa kwani hawana kumbukumbu kuwa alikula muda gani mara ya mwisho, baada ya majadiliano yao hayo wakasahau kabisa kuhusu ule mfuko uliokuwa na pweza.
Sophia aliandaa maziwa na yalipokuwa tayari akaenda nayo chumbani kwa lengo la kumnywesha yule mtoto ila kama kawaida yule mtoto aliyakataa yale maziwa,
“Anakataa mume wangu tufanyaje sasa?”
“Achana nae, nadhani huyu mtoto anataka kutusumbua tu kwahiyo hata asikuchanganye akili”
Yule mtoto alikuwa akiwaangalia tu kwani muda huu hakulia wala nini, Sophia na mumewe wakapanga kwenda kuoga kwanza kisha wale chakula na kulala ila walipotoka kuoga tu walijikuta wakijilaza kitandani na kila mmoja kuwa hoi kabisa.
Wakati wamelala Sophia akajiwa na ndoto na akaona kamavile kuna mtu mkubwa sana amekuja mbele yake, akamvua blauzi kisha akalalia kifua chake na kuanza kumnyonya maziwa alijikuta akihangaika sana kumtoa bila ya mafanikio na alipambana nae kwa muda mrefu sana. Alipokuja kushtuka alimuona yule mtoto akiwa juu ya kifua chake akinyonya ila Sophia hakuwa hata na nguvu za ziada za kuweza kumuondoa yule mtoto kifuani mwake kwani mikono yake ilikuwa ikitetemeka sana na kukosa nguvu kabisa kwahiyo hakuweza hata kujisogeza zaidi zaidi machozi yalikuwa yakimtoka kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata kifuani na kwenye maziwa jinsi yalivyokuwa yakivutwa.
Machozi yalimtoka sana Sophia kwani hata sauti ya kulia pia hakuwa nayo kabisa, kulipokucha Ibra naye aliamka na kumkuta mkewe akitoa machozi huku yule mtoto akiwa juu yake akiendelea kunyonya.Ibra akashikwa na hasira na kumsukuma yule mtoto pembeni ambapo aliangukia pembezoni mwa mke wake,
“Hivi wewe ni mtoto kweli wewe? Unataka kuniulia mke wangu kwanini? Sijapata kuona mtoto firauni kama huyu”
Ibra akamnyanyua yule mtoto na wala hakutaka kujiuliza mara mbili, moja kwa moja alimpeleka chumba ambacho Neema alikuwa akilala na kumfungia humo kisha yeye akarudi kumuhudumia mke wake kwani alikuwa karegea kabisa na nguvu ameishiwa.
Ibra aliingia kumpikia mkewe uji kwanza na kumnywesha, alivyorudiwa na nguvu ndipo alipoenda kupika chakula kingine kisha alikaa na kuanza kula na mke wake huku akimpa pole sana,
“Yani kale katoto ni kajinga sana, pole mke wangu”
“Asante, nimeumia sana yani kifua chote kinaniuma”
“Pole sana, ila nimemfungia kule kwa Neema, tukikaacha kule kwa siku tatu tu katakuwa kamekufa halafu tutaenda kukazika”
“Kheee tutakazika wapi sasa mume wangu si watu watatuona!”
“Hata usijali, kakifa tu tutavizia usiku tutakabeba kwenye gari na kwenda kukatupa baharini yani wala hatuhangaiki kukachimbia shimo. Katoto gani kale hata hakavutii, katoto kanafanya mambo kama mtu mzima mara katutolee machozi ya damu yani sina huruma nako tena. Sina mtoto ila sio kwa mtoto yule jamani simtaki kabisa na kama ukibeba mimba na kuzaa katoto kama hako nitakatupa pia”
“Usiseme hivyo mume wangu jamani”
“Lazima niseme hujui tu ni kiasi gani huyu mtoto ananikera mke wangu”
Wakajitahidi pale kula na kumaliza kile chakula kisha Ibra akainuka na mkewe kwenda kuoga na baada ya hapo wakawa na nguvu za kuendelea na maongezi mengine sasa ambapo Sophia alimueleza mume wake kuhusu ndoto aliyoota na jinsi alivyoamka na kumkuta huyo mtoto akinyonya,
“Mmmh unamaanisha kwamba huyu mtoto ni mtu mzima?”
“Sijui ila kwajinsi nilivyoona kwenye ndoto ndio hivyo, na kwanini basi nishindwe jinsi ya kumtoa kifuani pangu?”
“Ila Sophy tusiwekee wazo kuwa ni mtu mzima sababu naona kama itakuwa tatizo zaidi ila tuweke kama ni mtoto tu aliyekosewa kuzaliwa”
Kisha Ibra akamwambia mke wake kuwa waangalie Tv ili kuondoa mawazo waliyokuwa nayo ambapo walifanya hivyo na kuiwasha kisha kuangalia,
Muda kidogo wakapigiwa simu na mpigaji alikuwa ni Siwema ambapo Ibra alipokea simu ile na kuanza kumsikiliza baada ya salamu,
“Basi bhana yule mbibi wa jana si amekuja leo”
“Akasemaje?”
“Eti kaniambia kuwa mkeo amenyonywa damu usiku, unajua yule bibi ananishangaza sana. Mtu ananyonywaje damu jamani”
“Hebu nielezee vizuri dada”
“Ila nimemtimua bhana, sema kaniambiaje eti mumtafute haraka sana iwezekanavyo awasaidie ila mimi naona hana msaada wowote yule zaidi ya kutaka kuwatesa tu. Kumbuka kuwa ndiye anayefanya mimba za mkeo zitoke.”
Kisha akawaaga na kukata ile simu. Sophia akamuuliza mumewe kuhusu jambo lililokuwa likiongelewa na Siwema.
Ibra alikuwa kimya kwa muda akitafakari kisha akaamua kumuelezea mke wake vile ambavyo yule bibi alimwambia jana na jinsi ambavyo Siwema alivyopiga simu na yale aliyoyasema akihusisha na ndoto ya mke wake pamoja na huyo mtoto wao wa ndani.
“Nahisi kuchanganyikiwa mke wangu yani nachanganyikiwa kabisa”
“Mmmh inamaana nimenyonywa damu kweli?”
“Hebu kwanza niambie, je ni kweli ulikutana na yule bibi kipindi ukiwa na mimba ya kwanza ile?”
“Ndio na akaniambia kuwa nyumba yetu ni ya maajabu ila Da’Siwema alisema nisimsikilize eti yule bibi ni mchawi”
“Siwema kaniambia kuwa yule bibi ndiye anayefanya mimba zako zitoke, sasa mimi nadhani kuna ulazima wa kuonana na huyu bibi ili kujua ukweli ingawa Siwema anatukataza kufanya hivyo au wewe unaonaje?”
“Hata mimi nilikuwa na wazo kama lako ila sikuweza kukushirikisha mwanzoni kwani Da’Siwema alishanionya kuwa yule bibi ni mchawi na mwisho wa siku ndio kama hivyo kila nikibeba mimba zinatoka kumbe chanzo ni huyo huyo bibi”
“Usijali, tutapanga kwenda kuonana nae”
Muda kidogo wakamsikia Yule mtoto akilia kwa nguvu sana,
“Vipi tukamchukue?”
“Hakuna kumchukua, tujivike moyo wa kikatili huyu mtoto tumkomeshe mke wangu”
“Sasa tunawezaje kukaa hapa na makelele ya mtoto kiasi hiko? Tutaweza kulala usiku kweli?”
“Kuhusu kulala usijali, leo tutaenda kulala hotelini halafu kesho tutarudi hapa kusikilizia najua hadi kesho kutwa atakuwa ameshakufa huyo mtoto”
“Basi tuondoke sasa hivi”
Wakaamua kwenda kujiandaa kwa lengo la kuondoka hapo nyumbani kwao, wakati wanatoka nje sauti ya kilio cha Yule mtoto ilianza kukatika taratibu na walipofika nje kabisa haikusikika tena na kuwafanya wahisi kuwa Yule mtoto amenyamaza, ila kwavile walishapanga safari hawakuweza kurudi tena ndani zaidi ya kupanda kwenye gari yao na kuondoka.
Walikuwa wakitafuta hoteli nzuri ambayo itawawezesha kula na kulala kwa furaha zaidi,
“Vipi umekumbuka kubeba pesa lakini leo?”
“Nimekumbuka sana tena nimebeba za kutosha ili tusiumbuke kama siku ile”
Safari iliendelea ila kilichowashangaza ni kuwa hawakuweza kufika eneo la hoteli waliyokuwa wanahitaji kwenda na yakapita masaa kama manne wakiwa njiani hadi giza nalo likaanza kuingia,
“Inamaana umesahau njia mume wangu au ni nini?”
“Sijasahau ila nilikuwa nahitaji leo twende hoteli kubwa sana hapa mjini ila cha kushangaza hatufiki, sasa tufanyeje?”
“Tuingie hoteli yoyote tu mume wangu kuliko kutanga tanga hivi bila ya uelekeo maalum”
Wakakubaliana kuingia hoteli watakayoiona inapendeza zaidi, ikawa kama bahati kwani mbele yao wakaona hoteli kubwa sana na kuwafanya waamue kuingia hapo.
Ila hoteli hii ilikuwa na mandhari ambayo waliiona kwenye hoteli waliyoenda mara ya mwisho hadi kukutana na Neema ila hawakuiona tena siku waliyopita na Siwema.
Walitafuta mahali na kukaa huku wakijiuliza kuwa mbona inafanana na hoteli ambayo waliwahi kwenda, muda kidogo alifika muhudumu wa ile hoteli na kuwauliza mahitaji yao ambapo waliagiza chakula kisha wakahitaji wapewe chumba ili hiko chakula wapelekewe humo chumbani. Yule muhudumu aliwapa maelekezo yote ambapo moja kwa moja walielekea kwenye chumba na kuambiwa kuwa bili zote watalipia asubuhi.
Chakula kikaletwa na wakaanza kula, chakula hiki kilikuwa na ladha ile ile ya vyakula vilivyokuwa vikipikwa na Neema na kuwafanya wajiulize sana,
“Sio hoteli hii kweli tuliyokuja siku ile?”
“Nahisi ndio hii hii”
“Huyu muhudumu akija kuchukua sahani tumuulize kuhusu Neema”
Wakakubaliana hivyo ila ulipita muda bila ya Yule muhudumu kuja kuchukua sahani ingawa walipiga simu mapokezi kuwataarifu kuwa wamemaliza kula ila muhudumu hakuja kuchukua sahani na mwisho wa siku wakaamua kulala tu.
Kulipokucha, Ibra ndio alikuwa wakwanza kuamka kwakweli alishtuka sana na kujiangalia kwa makini, yeye na mkewe walikuwa wamelala makaburini tena kila mmoja kaburi lake.
Ibra aliinuka pale kwenye kaburi alilolala yeye huku akiwa amejawa hofu na uoga akasogea pale kwa mkewe akimuamsha kwa kutetemeka ambapo aliamka kwa kushtuka sana huku akijishangaa pia kuwa amelalaje kwenye kaburi,
“Tusishangae mke wangu tuondoke”
Sophia akainuka pia huku akiwa haamini kabisa na alijiona kama yupo ndotoni vile, wakatembea na kutoka eneo la nje la makaburi yao kisha walipoangalia pembezoni mwa barabara waliona gari yao ikiwa imepaki hapo, Ibra hakutaka kuhoji wala kujihoji akamshika mkewe mkono hadi kwenye lile gari ambapo alipofungua mlango ulifunguka na funguo ilikuwepo ndani ya gari. Ibra aliendesha gari lile hadi nyumbani kwao wakashuka na kuingia ndani, walikaa chini wakitazamana na kujikuta wakiulizana kilichotokea,
“Hivi imekuwaje hadi tukalala makaburini jamani? Yani mimi ninavyoogopa makaburi uwiiiiiii sijui hata imekuwaje”
“Hata mimi sielewi mke wangu, nakumbuka tu niliposhtuka nikajiona kaburini huku na wewe ukiwa kwenye kaburi la jirani”
Wakajaribu kuvuta kumbukumbu kuwa ilikuwaje, na wakakumbuka kuwa mara ya mwisho walikuwa hotelini na walikula na kulala hapo ila walichokuja kushtuka ni pale walipokumbuka kuwa kwenye hoteli hiyo wamewahi kumuona Neema,
“Na licha ya hivyo nakumbuka siku tunapita eneo lile na Da’Siwema tuliona makaburi na sio hoteli”
Wakashtuka wote kwani wakakumbuka vizuri sasa na kuhisi kuwa huenda wamefanyiwa kiini macho na Neema.
Gafla wakasikia mtu akichek na sauti ilikuwa ni ya Neema, wakashtuka sana ila walipotaka kugeuka ili kumuangalia mtu huyo walishangaa kuanguka kwenye kochi lao na kulala usingizi mzito sana.
Ilikuwa ni usiku tayari na Ibra akashtuliwa na mlio wa simu yakeambapo aliamka kutoka usingizini na kupokea simu hiyo, mpigaji alikuwa ni mama wa Ibra ambapo Ibra alimsalimia mama yake kimang’amu ng’amu kisha kuendelea na maongezi mengine,
“Inamaana ulikuwa umelala mwanangu, umechoka sana eeeh!”
“Kidogo tu mama”
“Haya sasa nisikilize kwa makini”
“Nakusikiliza mama”
“Hivi Ibra unamatatizo gani mwanangu? Kwanini huji kututembelea nyumbani? Kwanini hutaki kunijulia hali mama yako? Mbona umebadilika sana mwanangu?”
“Nisamehe mama”
“Nikusamehe kitu gani? Nilijua hili tatizo ni kwetu tu, nikapiga simu nyumbani kwao mke wako nao wanasema hawana mawasiliano yoyote na nyie, mmekuwa watu gani nyie mnaojitenga na ndugu jamani? Tuwaelewaje sasa?”
“Dah mama sijui hata niseme nini jamani”
“Najua huna cha kujitetea, hivi ni watu gani hamuwasiliani na ndugu wala nini. Nilienda kule mlipokuwa mnaishi naambiwa kuwa mlihama siku nyingi sana, sawa mlihama sio tatizo ila kwanini hamjatupa taarifa kuwa mlihama? Nasikia mnaishi maisha ya kifahari, hata kama mnaishi maisha ya kifahari ndio msahau familia zenu kweli? Kwani sisi tunashida na pesa zenu jamani! Mnahisi tutawaomba pesa, hapana kama mimi najitosheleza na shughuli zangu mwanangu jamani kwanini umekuwa hivyo? Sijakulea hivyo mimi”
Ibra aliishia kuomba msamaha tu kwani hata kujitetea alishindwa na hakujua aanzie wapi kujitetea na aishie wapi kwahiyo akajikuta akiishia kuomba msamaha tu ila mama yake alilalamika sana na kuonyesha wazi hajafurahishwa na kitendo cha mwanae, kisha Yule mama akaaga na kukata ile simu.
Ibra sasa aliweza kuitafakarisha akili yake kwani kiukweli ni kitambo sana hakwenda kutembelea ndugu zake na wala hakuwafahamisha ndugu zake mahali anapoishi kwa kipindi hiki. Akamuangalia mke wake na kumuamsha ambaye alionekana kuamka na uchovu sana,
“Mama kanipigia simu bhana”
“Mama!!”
“Ndio mama”
Kisha Ibra akamueleza mkewe vile walivyoambiwa na mzazi wao huyo,
“Kheee ila mume wangu hivi ni kwanini hatujawaleta ndugu zetu hapa? Kwanini maana hata mama yangu hajui kama nilishawahi kupata mimba na zikatoka”
“Ni kweli hawajui, hata mimi mwenyewe sijui ni kwanini hatujawaleta hapa. Usikute haya matatizo yote tunayoyapata ni kutokana na vinyongo walivyonavyo wazazi wetu”
“Ni kweli kabiisa”
Wakakubaliana waende kuoga kwanza kisha kupanga mikakati yao ya mambo mengine kwani ilionyesha wazi yanayowasibu ni mengi.
Wakainuka pale na kuelekea chumbani ila walipofungua mlango wa chumbani ili waingie walipokelewa na moshi mkubwa sana na mzito uliowakumba machoni na kuwaangusha chini kisha kupoteza fahamu kabisa.
Walikuja kushtuka pamoja na ilikuwa pamekucha tayari, kila mmoja alimuangalia mwenzie kisha kuanza kukumbuka kilichowatokea nyuma. Ibra akakumbuka kila kitu kisha akajinusa nguo zake,
“Unajua mke wangu tumeanza kutoa harufu ya umarehemu, maana ni toka tulipozinduka jana kule makaburini hatujabadilisha hizi nguo hadi leo”
Sophia nae akajinusa na kuanza kujiziba pua huku akisema,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Halafu kweli mume wangu mmmh, hebu twende tukaoge tubadili hizi nguo haraka”
“Ila jana si ndio tumeshindwa kuingia huko chumbani Sophia?”
“Sasa tutafanayaje? Na kwanini tushindwe kuingia chumbani ndani ya nyumba yetu wenyewe? Kwani kuna nini humu ndani?”
“Hata mimi mwenyewe sielewi, ila inuka tukaoge maana lazima tubadili hizi nguo la sivyo itakuwa hatari maana najihisi tupo kama marehemu hapa”
Wakainuka tena ila walipofungua mlango wa chumbani kwao ili waingie ule mlango ulikuwa mgumu na haukufunguka, Ibra akapata wazo kuwa wasing’ang’anize kufungua kwani wanaweza patwa na matatizo mengine ila Sophia nae akatoa wazo lake
“Kwanini tusiende kuoga kwenye kile chumba alichokuwa analala Neema”
“Weee Sophia hebu futa hayo maneno kabisa, hebu tutoke”
Ibra akamvuta mkewe mkono hadi kwenye gari kisha wakatoka kabisa kwenye lile eneo la nyumba yao ambapo mkewe akamuuliza kuwa wanaenda wapi,
“Mi naona twende kwa Siwema tukaoge huko kwake na akatununulie nguo mpya tuvae”
“Mmh mume wangu huoni aibu? Yani tukaoge kwa da’Siwema!”
“Hakuna cha aibu kwenye matatizo, twende tukaoge huko kisha tutajua cha kufanya baada ya yote”
Wakiwa njiani huku wakiendelea na maongezi yao ile gari ya Ibra iligoma kutembea tena, Ibra akashuka na kuangalia kuwa gari yao ina tatizo gani ila hakuweza kubaini tatizo lolote lile, kisha Sophia nae akashuka na kumuuliza mumewe kuwa tatizo ni nini na Ibra akamuweka wazi kuwa gari haikuwa na tatizo lolote lile,
“Sasa tutafanyaje?”
“Hata sielewi Sophy, hii gari sijui imekumbwa na nini pia?”
“Sasa turudi nyumbani au tufanyeje?”
“Hapana tusirudi nyumbani tuendelee na safari tu”
“Mmmh tunaendeleaje sasa na gari imegoma?”
“Kwani daladala zimeisha Sophy? Ilimradi tumeamua kwenda kwa Siwema basi tusighairi hata iweje”
“Na hii gari itakuwaje?”
“tutaiacha tu hapa, tukitoka huko nitakuja kuicheki kuwa tatizo ni nini? Siwezi kufanya chochote wakati najisikia vibaya na hizi nguo nilizovaa naona mikosi tu”
Sophia akawa anasua sua kuondoka eneo lile na kuiacha gari yao ila Ibra akamshika mkono na kumlazimisha kuwa waondoke.
Hawakufika mbali sana ikapita daladala hata Ibra akashangaa,
“Hii daladala vipi jamani mbona hii sio njia ya daladala?”
“Labda inakimbia foleni, tuisimamishe tupande tu mume wangu”
“Hapana Sophy nakosa imani na hiyo daladala”
“Kheee na wewe Ibra jamani kwani hujawahi kuona daladala zinazochepuka jamani?”
“Nimeziona nyingi tu ila hii sina imani nayo”
“Acha zako bhana Ibra”
Ile daladala nayo ikasimama na kuwafanya wapande kwavile ilikuwa haijajaa kwahiyo wakapata siti na kukaa, ila baada ya dakika chache wakapitiwa na usingizi yani walilala usingizi mzito sana na kuwafanya wasielewe kinachoendelea.
Walipokuja kuzinduka ilikuwa ni jioni sana, waliangaliana
“Inamaana tumekaa ndani ya hili gari muda wote jamani?”
“Nashangaa kwakweli”
Walipoangalia pembeni ndani ya lile gari wakaona jeneza na kuwafanya washtuke sana kwani wakati wanapanda hawakuona jeneza hilo, Ibra akainuka kwa uoga na kupiga kelele,
“Mnatupeleka wapi jamaniii?”
Mtu mmoja kwenye lile gari akamjibu Ibra,
“Kwani nyie vipi? Hamjui kama tunasafirisha msiba”
Ibra akashtuka zaidi kusikia eti wanasAfirisha msiba wale wakati mwanzoni waliona ni gari ya kawaida ya abiria, kwa jinsi walivyokuwa wakitetemeka ikabidi mtu mwingine kwenye lile gari awaulize
“Kwani nyie mnaenda wapi?”
Ibra alishikwa kama kigugumizi wakati akijielezea,
“Tulifikiri ni gari ya abiria”
“Poleni sana, sie tulihisi nyie ni wenzetu basi mnaweza kushuka sasa”
Ile gari ikasimamishwa kisha Ibra na mkewe wakashuka huku wamegubikwa na uoga na hofu moyoni.
Wakati wanaangaza macho yao kwenye lile eneo waliloshushwa lilikuwa ni eneo la makaburi, yani hapo hofu ikawatawala zaidi ya mwanzo, Sophia alimkumbatia mumewe kwa nguvu sana kwani alijihisi kamavile mwisho wao umefika huku uoga ukiwa umewajaana kuwafanya watetemeke. Ibra akajivika ujasiri wa kiume na kumshika mkewe vizuri huku wakianza kutoka kwenye eneo lile, kuna kaburi walipita na kusikia sauti ya mtu akicheka yani hapo uoga uliwajaa zaidi ya mwanzo na kuwafanya wahisi mwisho wao ndio umefika kabisa ila Ibra alijikaza tena kiume na kumshika mkewe vizuri huku wakitoka kwenye eneo hilo mpaka wakafanikiwa kuwa nje kabisa ya makaburi hayo na kuwa barabarani,
“Tunaenda wapi sasa mume wangu?”
“Sijui”
“Tutafanyaje sasa? Hivi haya mambo ni kweli au naota jamani?”
“Tusijadili hapa, inatakiwa tujue ni jinsi gani tunapona kutoka kwenye hali hii mke wangu”
“Sasa turudi nyumbani au?”
“Sielewi ila hamu ya kurudi nyumbani sina kabisa, nadhani tutafute uwezekano wa kwenda kwa Siwema kwa njia yoyote ile”
“Basi tukodi gari twende mume wangu”
Ikawa kama bahati kwani muda huo huo ilitokea gari ya kukodi na kupita mbele yao kisha kuwauliza kama wanaenda ambapo waliitikia na kupanda. Dereva wa lile gari alikuwa ni mwanaume wa makamo ambapo Ibra alimuuliza,
“Umejuaje kama sisi ni wasafiri?”
“Nimejua sababu mmekaa eneo langu la kazi na hata hivyo nafahamu hadi mnapoenda”
Ibra na mkewe wakatazamana na kumuuliza,
“Unafahamu tunapokwenda? Ni wapi kama wapafahamu?”
“Mnakwenda kwa mtu mmoja anaitwa Siwema”
Wakashtuka sana na kumuuliza tena,
“Umejuaje?”
“Nyie mmeshuka kwenye eneo langu kwahiyo mimi huwa najua kila kitu cha watu wanapozungumza kwenye eneo langu au karibia na eneo langu”
“Wewe eneo lako ni lipi?”
“Pale makaburini ndio eneo langu”
“Yani gari yako huwa unapaki pale?”
“Hapana ila ndio ninapoishi”
Ibra na Sophia wakapatwa na uoga kwani eneo lile hawakuona nyumba ya aina yoyote ile, Ibra akauliza kwa hofu
“Mbona pale hapana nyumba yoyote sasa wewe unaishi wapi?”
“Pale kuna kaburi langu ndio naishi humo ni nyumba yangu ile japo manaona ni kaburi”
Wakazidi kupatwa na uoga huku wakimuangalia Yule mtu kwa mashaka, ila Yule mtu akacheka kisha akawaambia
“Unajua mimi nimekufa miaka mingi sana iliyopita, kila mtu akiniona huwa ananishangaa sana ila mimi naona kawaida. Kwani kufa ni jambo la ajabu sana kwenu?”
Ibra na mkewe walizidi kutetemeka na kumuomba awashushe,
“Niwashushe vipi wakati bado hamjafika?”
Ibra na mkewe waliomba sana kushushwa, Yule mtu alicheka sana na kusimamisha gari ambapo walishuka na kuanza kukimbia hovyo hovyo, ikabidi Ibra amshike mkewe mkono kwani aliona wazi watapotezana na ilikuwa usiku sana ukizingatia na majanga yale watakimbiaje mmoja mmoja kwani walihisi yakiwakuta wakiwa mmoja mmoja watashindwa hata cha kufanya.
Wakati wameshikana mikono Ibra aliangalia pembezoni mwa barabara na kuona ile gari yao walipoiacha kwamaana kwamba wamerudishwa sehemu waliyoacha gari, Ibra aliongozana na mkewe hadi kwenye gari yao na kupanda tena wakati wanaiendesha safari hii ilitembea vizuri tu na kuwafanya warudi nyumbani kwao huku wamegubikwa na uoga na hofu moyoni.
Wakiwa wamekaa sebleni bila ya kuelewa hili wala lile la kufanya, gafla wakamsikia Yule mtoto akilia na kuwafanya washtuke sana kwani walishasahau kama kuna mtoto mule ndani na kabla hawajafanya chochote walishtukia Yule mtoto akiwa tayari pale sebleni.
Ibra na Sophia wakapata mshtuko uliowafanya wakumbatiana zaidi, yule mtoto akaanza kusema
“Mama ninyonyeshe”
Sophia hakuweza hata kujibu zaidi ya kutetemeka tu, kisha yule mtoto akasema tena
“Kwa usalama wenu na wako mama ninyonyeshe”
Gafla yule mtoto akatua mikononi mwa Sophia hata aliyembeba na kumuweka hakuonekana, yule mtoto alikuwa akimtazama Sophia ambaye alikuwa akitetemeka tu. Ibra naye alikuwa akishangaa kuwa yeye na mkewe wameachanishwa muda gani hadi yule mtoto kuwekwa kwenye mikono ya Sophia huku akidai kunyonyeshwa. Ibra kwa sauti ya kutetemeka akamuomba mkewe amnyonyeshe mtoto huyo ambapo Sophia hakupinga zaidi ya kutoa ziwa lake na kuanza kumnyonyesha.
Yule mtoto alikuwa ananyonya kama ng’ombe vile yani alikuwa akinyonya ziwa hili na kuhamia lingine kwa wakati mmoja, Ibra na Sophia walibaki kumuangalia tu bila ya kufanya chochote. Sophia alijikuta akimnyonyesha yule mtoto hadi palipokucha na nguvu zote zilimuisha hakuweza kufanya kitu chochote kile ndipo Ibra alipoamua kwenda kumuandalia mkewe chakula kwani hakuwa na nguvu hata ya kuongea.
Alipofika jikoni alishangaa kuona kuna sufuria kwenye jiko na jiko likiwa linawaka, akasogea na kufunua lile sufuria akaona ni nyama yani supu ndio inachemshwa pale na ilikuwa na harufu nzuri sana. Ibra hakutaka kuisumbua akili yake kwa kujiuliza kuwa nani amebandika zaidi ya kupakua ile supu kwenye bakuli kisha kwenda kumuwekea mkewe ili anywe, akarudi tena jikoni akakuta kuna chapati juu ya meza ya jiko ambapo alizichukua pia na kwenda kumuwekea mkewe. Zoezi alilokuwa nalo sasa ni kumtoa yule mtoto ili mkewe aweze kula na kurudisha nguvu, ila kabla hajamtoa alishangaa kumuona yule mtoto yupo pembezoni mwa kochi kanakwamba kuna mtu amemnyanyua na kumuweka pembeni. Ibra hakuhoji pia zaidi ya kumsogelea mkewe na kuanza kumnywesha ile supu na zile chapati.
Baada ya kumaliza kula, Sophia alianza tena kurejewa na nguvu ila mwili wake ulikuwa umechoka sana. Kisha Ibra akainuka na mkewe hadi chumbani kwao ambapo walipofungua mlango ulifunguka tu kisha wakaingia na moja kwa moja wakaenda kuoga kwanza na kubadilisha zile nguo walizokuwa wamevaa.
Walikaa kitandani kila mmoja akimuangalia mwenzie, Sophia akajikuta akimuuliza mume wake,
“Hivi hii nyumba ulinunua Ibra au ulipewa bure?”
‘Hivi ni swali gani hilo unaniuliza Sophia mke wangu jamani?”
“Unajua maisha yetu yalikuwa na amani sana, ni kweli tuliishi kiumasikini, tuliishi uswahilini lakini tulikuwa na amani sana. Tunachopata tunakula na kufurahi, usiku tunalala vizuri na kuamka vizuri. Sikuona kasoro yoyote kwenye maisha yetu ale zaidi ya umasikini wetu tu. Hivi kuna faida gani ya kuishi nyumba kubwa hivi na nzuri huku tukiteseka kiasi hiki? Hivi unahisi ni maisha ya kawaida haya mume wangu? Hivi uanahisi huyu mtoto ni wakawaida? Mtoto mdogo vile atawezaje kuongea? Nimekuuliza kwa uzuri tu mume wangu, hivi hii nyumba ulinunua au ulipewa bure?”
“Unajua wazi Sophia kuwa hii nyumba niliinunua mke wangu ingawa pesa niliyonunulia hii nyumba haiendani na thamani ya nyumba ila mwenye nyumba aliniambia kuwa anahama hii nchi ndiomana kaamua kuuza vitu vyake kwahiyo sikuona vibaya kuinunua hii nyumba. Sasa unamaana gani kusema hayo au unataka tufanye kitu gani?”
“Mimi naona ni bora turudi maisha yetu ya zamani hata kama watu watatucheka ila ni bora kuishi maisha yenye amani kuliko haya”
Ibra alitulia kidogo akitafakari maisha ambayu alikuwa akiishi na mkewe zamani, ni kweli yalikuwa ni maisha ya kimasikini ila yaliyojaa amani sana. Akakumbuka na jinsi mama yake alivyopiga simu na kuwalalamikia kuwa kwanini hawaendi kuwatemmbelea. Ibra alijiuliza sana na kukosa jibu kwani zamani ilikuwa ni lazima wawatembelee wazazi wao na ndugu zao au hata kuwaulizia hali zao ila kwa kipindi hiki imekuwa tofauti kabisa hawajawahi hata kuwapeleka wazazi wao hapo kwenye nyumba yao. Ibra akamuangalia mkewe na kumuuliza pia,
“Kwahiyo unataka tukapange tena?”
“Bora tukapange tena, mimi nimechoka kwakweli”
“Pole mke wangu, hata mimi nimechoka kwakweli ila hata sijui tuanzie wapi na tuishie wapi”
“Usijiulize mume wangu, chukua hela tafuta dalali atutafutie chumba tukaishi sehemu nyingine tuondoke kabisa hapa”
Ibra akakubaliana na mkewe kuhusu hilo swala, kisha akainuka na kwenda kabatini ili kuchukua pesa walizokuwa wamehifadhi. Alifungua kweli na kukuta pesa zimeongezeka zaidi akamuangalia mkewe na kumwambia
“Hivi unajua kama pesa zimeongezeka kwenye kabati?”
“Kheee zimeongezeka? Nani kaziongeza?”
“Sijui kabisa”
“Chukua hivyo hivyo mume wangu tukatafute nyumba sehemu nyingine”
Ibra akachukua pesa za kutosha kisha akatoka na mkewe ambapo walikubaliana kuwa akamuache mkewe dukani kisha yeye akazunguke na dalali.
Waliondoka pale nyumbani kwao na kuelekea dukani ambapo Ibra alimuacha mkewe hapo kisha yeye akaenda kumtafuta dalali ili amsaidie kutafuta nyumba. Sophia alikaa dukani huku akiwa na mawazo sana hata akatamani arudishe siku nyuma ili hata siku moja asiwe ameyaonja yale maisha ya kitajiri kwani yalimuweka kwenye wakati mgumu sana akakumbuka jinsi alivyokuwa akiwaota watoto wake na vile mimba zake zilivyokuwa zikitoka.
“Ningekuwa na kimtoto changu saivi nacheza nae, utajiri gani huu mimba zangu zimetoka zote watoto wangu wamelia kwa uchungu nakazana kunyonyesha sijui majini uwiiiii mimi jamani eeeh Mungu nisaidie”
Akawaza kidogo kweli na kujicheka huku akijisikitikia na kusema,
“Kweli mtu ukiwa na shida ndio wakati wa kumkumbuka Mungu jamani, nisaidie Mungu”
Muda kidogo akasogea Yule baba John na kumkuta Sophia hapo dukani kisha akamsalimia na kuanza kuzungumza nae,
“Naona leo umeamua ubaki mwenyewe dukani shemeji”
“Ndio, naboreka kukaa nyumani. Hata hivvyo tulikuwa na matatizo kidogo hapa karibuni”
“Poleni sana ila nini tatizo tena shemeji? Ila Ibra ni msiri sana sababu huwa namuona siku zote hapa akiwa na furaha tu”
“Mmh siku zote! Jana ulimuona?”
“Ndio, tena jana alikuwepo hapa hadi jioni kabisa tuliondoka wote na kumuacha mwenyewe ila sikuzungumza nae”
“Mmmh jamani, kwani siku hizi imekuwaje tena? Mbona sielewi elewi?”
“Huelewi nini kwani?”
“Ibra nilikuwa nae nyumbani jana kutwa yote sasa huku dukani alikuwa nani?”
“Halafu wewe na mumeo sijui mna matatizo gani jamani, kwani mkikubali mlikuwa hapa kuna tatizo? Ngoja niachane na hayo sio kilichonileta, hivi shemeji ile mimba yako yak wanza kwanini ilitoka?”
Sophia akamuangalia baba John bila ya kumjibu kwani aliona kamavile anataka kumkumbushia machungu yaliyopita tu.
“Naomba tuachane na habari hizo shemeji tafadhari”
Baba John akaamua kuondoka kisha Sophia nae akafunga duka na kuondoka huku akili yake ikimuelekeza kwenda kwa Siwema moja kwa moja.
Sophia alifika nyumbani kwa Siwema na hakumkuta hivyobasi akaamua kukaa nje akimsubiria kuwa huenda hakwenda mbali sana, wakati amekaa pale akakumbuka ule mti wa mpera na kuinuka hadi kwenye ule mti akiangalia angalia, muda kidogo Yule bibi ambaye mara nyingi huwa anazunguka eneo lile alisogea pale alipokuwa Sophia na kumsalimia.
Sophia akashtuka kisha na yeye akamsalimia tena Yule bibi, bibi akaitikia huku akisikitika na kusema,
“Nakuhurumia sana mjukuu wangu, najua hapo ulipo unamawazo sana ila inatakiwa mfungue akili zenu kwanza ndio muweze kuelewa mbichi na mbivu. Siku ya kwanza nilipokutana na wewe nilikwambia kuwa nyumba yenu ni nyumba ya maajabu ila hukunielewa. Najua hukunielewa kwavile hukutaka tu kunielewa ila kuna viashiria tayari ulishaviona kwenye nyumba yako kuwa si nyumba ya kawaida ila hukutaka kuhoji kuhusu hilo”
“Tafadhali bibi naomba unieleweshe maana nashindwa kuelewa kweli ingawa nipo kwenye wakati mgumu”
“Ile nyumba ni kama jela kwani kuingia pale ni rahisi sana ila kutoka si rahisi kama mnavyofikiria”
“Kivipi bibi?”
“Si mumeo umemuagiza akatafute nyumba nyingine? Jibu atakalokuletea najua utaelewa ni jinsi gani ilivyongumu kutoka kwenye ile nyumba tofauti na kuingia”
“Kheeee na umejuaje kama mume wangu ameenda kutafuta nyumba nyingine?”
“Mimi huwa naona vitu vingi sana ingawa watu nikiwaeleza huniona kamavile mimi ni mchawi na huwa wanasema kwavile nimetengwa na familia yangu ila maono yangu haya ndio yaliyofanya nitengwe ila siwezi kuacha kusema kile ninachokiona kwani sipendi kuona mwingine akiteketea wakati najua suluhisho lake”
Sophia akapumua kidogo kisha akamuuliza huyu bibi,
“Sasa sisi tutawezaje kutoka kwenye ile nyumba? Maana kiukweli tunateseka sana”
“Kabla ya kutoka pale inatakiwa akili zenu zifunguke kwanza, nyie mmefungwa kwenye akili zenu na msipokuwa makini mtateketea wote wewe na mumeo kisha mtaingia kwenye mkumbo wa kuwa viumbe vya ajabu”
Sophia akashtuka kidogo kisha kuvuta pumzi na kumueleza huyu bibi kuwa pale alipo hata anaogopa kurudi nyumbani kwake,
“Yani natamani hata nisirudi kabisa”
“Ni bora urudi tu kuliko kurudishwa, yani rudi kwa hiyari yako mwenyewe kuliko urudishwe pale. Tatizo ni moja hapo ulipo huna pa kujificha maana harufu ya damu yako inajulikana sana”
“Damu yangu tena?”
“Ndio damu, kwani wewe unafikiri Yule mtoto unayemnyonyesha kila siku unamnyonyesha nini?”
“Sijui, ninachojua mimi ni kuwa namnyonyesha maziwa”
Bibi akasikitika kidogo kisha akamwambia,
“Humnyonyeshi maziwa ila unamnyonyesha damu, maisha yako yapo kwenye hatari zaidi kuliko maisha ya mumeo”
Sophia akaogopa sana vile alivyosikia kuwa huwa anamnyonyesha Yule mtoto damu na kusikia kuwa maisha yake yapo kwenye hatari zaidi, alihisi kupagawa kabisa kwa uoga.
“Nitafanyaje sasa, bibi nisaidie tafadhali”
“Nitakusaidia ila kwanza akili yenu irudi ndio itakuwa rahisi kuwasaidia”
“Na akili yetu itarudije? Kwani haipo?”
“Nyie mnajiona mpo sawa ila akili yenu haipo sawa hata vitendo mnavyovifanya si vya kufanywa na binadamu wa kawaida ila nyie mnafanya, mnaweza mkarudi nyumbani kwenu na kukuta chakula si wewe wala mumeo aliyepika ila mnapakua chakula hiko na kukila tena huku mnakisifia kuwa ni kitamu sana. Unafikiri hiyo ni akili ya kawaida? Huwa manadhani chakula hicho kimeshushwa kutoka mbinguni au ni kitu gani? Mmefungwa akili zenu, ndiomana nasema kuwasaidia nyie ni mpaka pale mtakapofunguka hizo akili”
“Tusaidie basi akili zetu ziwe sawa, zirudi katika hali ya kawaida”
“Nitawasaidia”
Bibi alitoa dawa kama mzizi hivi kisha akamkabidhi Sophia na kumwambia,
“Mkiwa mnarudi nyumbani kwenu wewe na mumeo, mkifika getini sema asante Mungu kisha muingie ndani. Baada ya hapo endeleeni na shughuli zenu zingine kama kawaida, ikifika saa mbili usiku nenda na mumeo sebleni kisha sema tena asante Mungu, chukua hiyo dawa ikate na uitafune halafu mpe na mumeo nae aitafune kisha………”
Mara Siwema akatokea na akakunja sura sana baada ya kumuona Yule bibi,
“Uwiii uwiiii uwiiii wewe bibi toka nyumbani kwangu, nimesema tokaaaaaa”
“Jamani Da’Siwema usifanye hivyo huyu bibi anataka kutusaidia”
“Asaidie nini mchawi mkubwa huyu, wewe bibi tokaaaa hivi hunisikiii eeeh”
Yule bibi akainuka na kuondoka kwani hakuwa bibi wa malumbano, Sophia akataka kumfata Yule bibi ila Siwema akamvuta mkono na kurudi nae kwenye nyumba yake.
Siwema alianza kumlalamikia Sophia,
“Laiti ungejua huyu bibi anavyonikosesha usingizi wala usingethubutu kuzungumza nae nyumbani kwangu. Hana maana yoyote Yule bibi yani hafai kabisa”
Muda kidogo Ibra nae akawasili pale kwa Siwema, Sophia akamtazama mumewe na kumuuliza
“Kheeee umejuaje kama nipo huku?”
“Nilivyokukosa dukani, moja kwa moja nikahisi kuwa umekuja huku tu”
“Vipi umefanikiwa?”
“Nifanikiwe wapi? Yani majanga tu”
“Majanga gani tena?”
Ibra akamvuta mkewe pembeni na kuanza kumueleza,
“Yani huwezi amini kabisa, nyumbani pale si nimeondoka na hela! Basi nimemfata dalali kweli nyumba ipo ila kutoa hela sina sh kumi, nikabaki kujishangaa tu basi tafuta tafuta hamna hela yoyote ndio nikamwambia Yule dalali nije nae dukani, kufika pale na wewe umefunga haupo. Kwavile na mimi nina funguo za pale nikaamua kufungua ili niangalie pesa za mauzo nimpe kidogo za kumpooza lakini hapakuwa na pesa yoyote ile. Yule dalali akamaindi na kuondoka zake ndio nikapata wazo kuwa utakuwa huku. Vipi ulibeba pesa za pale dukani?”
“Sijabeba hela yoyote ndio nakushangaa tu hapa ila kuna kitu nataka nikwambie”
Ibra akamsikiliza kwa makini mkewe ambapo alimueleza kwa kifupi vile alivyoelezwa na Yule bibi, Siwema alipoona hawamalizi maongezi yao akawafata,
“Ni maneno gani manayoongea kwa kunificha? Haya ondokeni nyumbani kwangu, nimesema ondokeni”
Ibra akaongozana na mkewe na kwenda kwenye gari yao kisha kuanza safari ya kurudi nyumbani kwao, ilikuwa ni jioni tayari.
Walipofika getini Sophia akasema asante Mungu kama alivyoelekezwa na kuingia ndanui, walikuta nyumba iko shwari tu kisha wakaendelea na shuguli zao zingine ikiwa ni pamoja na kwenda kuangalia pesa kwenye kabati ambapo walizikuta zipo za kutosha tu.
Ilipofika saa mbili usiku, kama walivyoambiwa wakaenda sebleni na kukaa kisha Sophia akachukua ile dawa na kutafuna halafu akampa mumewe nae atafune. Gafla wakashangaa kujikuta wapo ndani ya damu.
Hakuna aliyeweza kujielewa kwa wakati ule kwani kila mmoja alijiona wa tofauti, gafla ikawa kamavile wapo kwenye sinema kwani walikuwa wakiona matendo mbalimbali mbele yao mengine yalifanyika vyumbani, jikoni, na sebleni ila yote waliyaona na matendo mengine waliyaona ila watu hawakuwafahamu kabisa.
Kwanza walimuona Neema akiwa na mwanaume ambaye hawakumtambua ni nani ila Neema na Yule mwanaume walionekana ni wapenzi na walifurahiana sana, gafla wakamuona kama Neema akiugulia sana hadi kufa kisha Yule mwanaume alionekana akisikitika sana. Kwa mbali wakaona makaburi kisha wakamuona Yule mwanaume amesimama mbali kabisa kisha ikanyesha mvua kubwa sana.
Gafla wakaona Yule mwanaume akiishi ndani na mwanamke mwingine ambaye hakuwa Neema na wakaona Yule mwanamke akiwa na mtoto mdogo ila Yule mtoto alionekana kuwa wa ajabu sana na alitenda vitu vya ajabu, kuna muda waliona Yule mtoto akiingiliwa na kitu ambacho kilikuwa kikibadili akili ya Yule mtoto na kutenda mambo ya ajabu na wakati mwingine kile kitu kilitoka na kufanya Yule mtoto aendelee kuwa mtoto mdogo, gafla hawakuwaona tena hao watu kwenye nyumba hiyo ila wakamuona Yule mwanaume akiwa na mwanamke mwingine ambapo sura ya huyu mwanamke ilimkumbusha kitu Ibra ala gafla wakamuona Yule mwanaume nae akitapatapa hadi kufa.
Muda huo huo wakajiona wao wakiwa wamekaa kwenye makochi na chini yao hapakuwa na damu tena, wakatazamana na kuulizana ili kutambua kama wako sawa kabisa,
“Sophia unanisikia?”
“Nakusikia Ibra?”
“Je umeona nilichoona mimi?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Nadhani wotw tulikuwa tunaona, je ni kitu gani umekihisi kwa haya tuliyoyaona?”
“Kuna kitu kimenishtua”
“Kitu gani?”
“Yule mwanamke aliyeonekana mwishoni kabisa ndiye mwanamke aliyeniuzia hii nyumba”
“Na je yuko wapi?”
“Mimi sijui alipo kwani tulipouziana nyumba tu kila mtu alishika ustaarabu wake”
“Nadhani huyo dada ni muhimu sana kumtafuta na ndiye atakayetusaidia”
“Hata mimi nadhani hivyo hivyo na ndiomana Yule bibi alisema ufahamu wetu urudi kwanza.”
“Na je unafikiria nini kuhusu Neema?”
“Naogopa hata kumuongelea kwani nahisi kuwa alishakufa siku nyingi sana”
Gafla kikasikika kicheko kisha Neema akatokea mbele yao huku akitabasamu, hakuna aliyeweza kustahimili na walijikuta wakianguka na kuzimia.
Walipozinduka walijikuta wakiwa chumbani kwao, wamelala kitandani. Ibra akawa wa kwanza kumuuliza mkewe
“Unajisikiaje?”
“Sijisikii chochote ila tu nakumbuka tulimuona Neema na tukapoteza kumbukumbu sasa imekuwaje tumeletwa humu chumbani?”
“Kwanza kabisa naomba tupungue kumuongelea huyo mtu halafu tupange cha kufanya maana kama mambo makubwa yashatupata tayari”
Wakaamua kuamka pale kwani palionekana kuwa pamekucha kabisa kisha wakaenda kuoga na kujiandaa kwaajili ya kutoka.
Wakati wanatoka wakakuta chai imeandaliwa mezani na vitafunio vizuri kabisa,
“Mmh haya maajabu ya humu yamezidi jamani, haya chaia kapika nani?”
“Tuachane na hayo mke wangu, hebu twende”
Ibra akamuongoza mkewe hadi nje kisha wakaingia kwenye gari na kuondoka zao, ila walipofika pale walipowahi kuona hoteli kubwa sana leo waliweza kuona makaburi yakiwa yamezunguka pale kwa uzuri kabisa, Sophia akamuuliza mumewe
“Je inawezekana kaburi la Neema likawa maeneo haya?”
“Sophy tafadhali tusimuongelee huyo mtu”
“Tusimuongelee kivipi wakati ndiye anayesumbua maisha yetu? Neema ndiye kikwazo kwetu na ndiye kikwazo kwenye nyumba yetu”
Ibra hakutaka kumsikiliza sana mkewe hivyobasi akaondoa gari na kuendelea na safari, sehemu ya kwanza waliyoenda ilikuwa ni dukani kwao ambapo walikuta mitaa ya pale imepooza sana kanakwamba hapakuwa na mtu yeyote kwenye eneo lile kabisa na kuwafanya hata waogope kufungua duka lao kisha wakarudi kwenye gari na kupanga tena kwenda kwa Siwema ili angalau wakaonane na Yule bibi.
Waliingia kwenye gari huku wakiulizana,
“Imekuwaje leo watu hawajafungua maduka?”
“Hata sielewi kwanini hawajafungua ingawa haijawahi kutokea hata siku moja eti maduka yote yawe yamefungwa vile”
“Labda kuna mgomo wa maduka”
“Inawezekana ila sidhani kwani tungejua tu kama kuna mgomo”
“Inawezekana hatujui kutokana na matatizo yetu maana mambo mengi yanatupita sana”
Wakakubaliana hivyo kuwa inawezekana hawajui kutokana na mambo mengi yaliyowapata na kuwafanya washindwe kupata taarifa kwa muda.
Walipofika nyumbani kwa Siwema napo palikuwa kimya sana kanakwamba Siwema hakuwepo kabisa, wakajaribu kugonga ila hakuna hata mtu aliyetoka kuwafungulia,
“Inamaana Da’Siwema hayupo?”
“Itakuwa hivyo maana kimya kimetanda sana”
“Je tutawezaje kumpata tena Yule bibi?”
“Huo ndio mtihani sasa hata sijui tutafanyaje”
“Ila mimi nina wazo”
“Wazo gani?”
“Kwanini tusiende kwa Yule mganga wakwanza kabisa tuliyepelekwa na Da’Siwema! Maana nadhani kule tutapata taarifa nyingi zaidi”
“Ila huyo mganga si ndiye aliyetuhakikish
ia kuwa Jane ni mchawi?”
“Sasa kwani Jane si mchawi?”
“Jane si mchawi, hivi mpaka sasa bado unaamini kuwa Jane alikuwa mchawi? Hizo zilikuwa ni mbinu tu za Yule kiumbe ili tusijue mabaya yake ila kiukweli Jane sio mchawi”
“Mbona Yule mganga alituhakikishia sasa!”
“Ndiomana nakosa imani nae kwani alituhakikishia kitu ambacho si cha kweli”
“Hata kama, bado tunapaswa kwenda kuonana nae na tutajua mambo mengi. Kwanza hawezi kubeba akili zetu kwasasa kwani zimesharudi”
Wakakubaliana pale kuwa waende kwa huyo mganga ambaye mwanzoni kabisa waliwahi kwenda pamoja na Siwema, wakaingia kwenye gari yao na kuanza safari ya kwenda kwa huyo mganga.
Walifika kwa huyo mganga na ilikuwa ni sehemu ile ile waliyopelekwa na Siwema ila ulionyesha kubadilika vitu vingi sana kwani mambo mengi yalionekana kuwa tofauti kabisa na kuwashangaza,
“Hivi ni hapa kweli?”
“Ndio ni hapa hapa, mimi nakumbuka kabisa. Nakumbuka hadi eneo ambalo tuliwachinja wale nwanyama”
Sophia akatazama kwa makini nay eye akakumbuka kabisa, wakasogea karibu na kilinge cha Yule mganga ila leo hapakuwa na watu kabisa tofauti na walivyokuja kipindi kile na kuwafanya wahisi kuwa huenda wateja wameanza kupungua kwa mganga huyo.
Walisogea karibu na kuingia mule kilingeni ambapo walimkuta Yule mganga akiwa amejiinamia, wakamsalimia na kukaa ambapo kabla hawajaitikiwa salamu Yule mganga aliwauliza,
“Mmekuja kufanya nini?”
“Tunashida mzee”
“Najua kama mnashida ila je ni shida gani?”
“Nyumbani kwetu kuna matatizo, kuna kipindi tuliwahi kwenda pamoja na ulituambia kuwa Yule jirani yetu ndiye mchawi ila kumbe kilichokuwa kinatutesa kilikuwa ndani ya nyumba yetu”
“Kwahiyo mmekuja kunizodoa kuwa niliwaambia uongo?”
“hapana, hatuna nia ya kukuzodoa kabisa ila tunaamini bado unaweza kutusaidia kwa jambo hili”
Yule mganga akatabasamu kisha akawaambia,
“Hivi mnajijua kama mnanukia kifo?”
“Tunanukia kifo kivipi?”
“Ni nani mliyeweza kuzungumza nae leo zaidi ya mimi?”
Ibra na mkewe wakatazamana kwa muda kwani kiukweli toka wametoka nyumbani kwao hakuna waliyeweza kuzungumza nae zaidi ya huyu mganga kwani kila sehemu waliyopita hawakuwakuta wenyeji wao, Ibra akamjibu huyu mzee
“Hakuna mtu yeyote tuliyezungumza nae kwani kila mahali tulipopita hatukuwakuta watu ambao tunaweza kuzungumza nao”
Huyu mzee akacheka tena na kuwaambia,
“Hivi mnajua kwanini mmeweza kuongea na mimi? Mnajua kwanini mimi mmenikuta?”
“Hatujui”
“Basi jibu ni rahisi kabisa, mimi I marehemu”
Ibra na Sophia walishtuka sana hata uoga nao ukaanza kuwaingia moyoni kwani hawakutegemea kitu kama hiki. Ibra akauliza kwa sauti ya kutetemeka,
“Ma-ma-marehemu kivipi?”
“Mimi ni marehemu, nilishakufaga siku nyingi sana na ndiomana mmeweza kuniona na kuzungumza na mimi”
“Una-unamaanisha nini? Inamaana na sisi ni marehemu?”
Huyu mzee akacheka tena na kuwaambia,
“Nyie si marehemu ila mnakaribia kuwa marehemu, na kama hamuamini maneno yangu basi mtakapotoka hapa na kukutana na watu njiani jaribuni kuwaongelesha muone kama mtajibiwa yani hamtajibiwa na wala hawatawaona kwavile nyie mnanukia umarehemu”
Uoga ukawazidi na kuwafanya watetemeke sana, kisha wakajikuta wakiomba msaada kwa huyu mzee ili awasaidie ila huyu mzee alikuwa akicheka tu na kuwauliza,
“Nawasaidia vipi wakati mimi ni marehemu tayari? Labda msaada wangu niwafanye na nyie kuwa marehemu”
Hapo wakashindwa kustahimili na kuinuka haraka kisha kutoka nje ya kile kilinge, walitazamana na kugubikwa na uoga kisha wakarudi kwenye gari na kuondoka eneo lile.
Wakaamua kurudi tena kwa Siwema ila ilikuwa vile vile kama mwanzo yani hapakuwa na mtu wa aina yoyote ile, Ibra akapata wazo la kupiga simu ila kila aliyempigia hakumpata hewani kabisa na kumfanya uoga umzidie kisha wakarudi tena kwenye gari na kuanza safari ya kuelekea popote na kila walipopita na kuona watu walijaribu kusimamisha gari na kuongelesha watu hao ila ilionekana kuwa hakuna aliyejali uwepo wao kwani hakuna aliyewajibu kabisa na kila waliyemwongelesha alionekana kuendelea na shughuli zake kanakwamba hajaongeleshwa kitu,
“Inamaana hawatuoni au?”
“Sijui”
“Na je inamaana ndio tumekufa?”
Sophia akamsogelea mumewe na kumkumbatia kisha akasema kwa uoga sana,
“Naogopa kufa mume wangu”
“Hata mimi naogopa ila wakati wetu ukifika tutakufa tu haiepukiki hiyo”
“Sasa kwani ndio wakati wetu umefika? Kwanini jamani? Sijaweza hata kuwaaga ndugu zangu”
Sophia alimkumbatia mumewe huku machozi yakimtoka, ila Ibra bado alijipa moyo,
“Ila naamini tutakomboka tu mke wangu”
“Hata sijui tutakombokaje, je ni nani atakayeweza kutusaidia? Inamaana Yule bibi ametupotosha zaidi”
“Ila mke wangu wakati mwingine tunatakiwa kuwa na shukrani tusimlaumu moja kwa moja Yule bibi halafu pia kumbuka hukumsikiliza Yule bibi hadi mwisho labda kulikuwa na ujumbe mwingine ambao tulipaswa kufanya kwahiyo tusimlaumu moja kwa moja tujilaumu na sisi wenyewe kuwa kwanini hatukuwa makini kumsikiliza? Hata baada ya Siwema kukatisha kwanini tusingemtafuta siku ileile? Kwahiyo tusimlaumu moja kwa moja”
Wakarudi tena kwenye gari na kuendelea na safari ambapo kwa wakati huo hawakuwa na uelekeo unaoeleweka kabisa kwani kila waliposimamisha na kuongea na watu hakuna jibu walilolipata.
Walikaa kwenye gari na kujadiliana kuwa ni bora warudi nyumbani tu kuliko kuendelea kuhangaika hivyo.
Wakiwa njiani kurudi nyumbani kwao, wakakutana tena na yale makaburi ya mwanzo ambapo moja kwa moja Sophia aliuliza tena swali ambalo halikutofautian
a sana na swali la mwanzo walipoyaona,
“Inamaana kaburi la Neema nalo lipo hapo?”
“Tusimuongelee huyo mtu tafadhali kwanini husikii mke wangu jamani?”
“Nasikia vizuri ila huyu Neema anatutesa sana mume wangu, anatutesa kwenye nyumba yetu sana”
Mara gafla wakasikia sauti ikitokea kiti cha nyuma kwenye gari yao,
“Nawatesa mpaka kwenye gari lenu”
Walipogeuka wakamuona Neema, uoga ukawajaa wakafungua milango ya gari na kuanza kukimbia, kwa bahati mbaya wakati wanakimbia likatokea gari na kumgonga Sophia kisha damu zikatapakaa eneo lile. Ibra alikuwa kama amepigwa na butwaa hivi kwani mwanzoni walikuwa hawaonekani ila gari imeweza kumgonga Sophia na muda huo huo watu wakajaaa kwenye eneo lile.
Ibra akasogea pale chini alipokuwa mkewe na kumshika huku damu nyingi zikimtoka, kuna wasamalia wema wakasogea na kuwasaidia kwa kuwapakia kwenye gari nyingine kwani hakuna hata aliyejua kuwa wale walifika na gari kwenye eneo lile, safari ilikuwa ni kwenda hospitali moja kwa moja ambapo walipokelewa kisha Sophia kupelekwa chumba cha wagonjwa mahututi, kwakweli Ibra alikuwa kama mtu asiyejielewa kwa wakati huo kwani hakujua hata imekuwaje hadi mkewe kugongwa na gari kiasi kile huku mawazo yake yakimpeleka kuwa huenda wanakaribia kufa kweli na pengine ndio mkewe ameanza hivyo, machozi yakamtoka kwa hofu na uoga alionao.
Wazo linguine likamtuma kuwa awapigie simu ndugu zao kuwaelezea yale matatizo ila wasiwasi ukamshika, hakutaka kufikiria sana wasiwasi wake na kuamua kupiga simu.
Ile simu aliyoipiga iliita mara moja tu kisha ikapokelewa ila aliyeipokea simu ile alikuwa akicheka sana na kumfanya Ibra ashtuke na kumuuliza kwa makini,
“Wewe ni nani umepokea?”
“Mimi ni Neema”
Ibra akazidi kupatwa na mashaka na kushusha ile simu haraka kisha akaangalia kwa makini kuwa ni nani aliyempigia, akaona jina la Neema akaikata muda huo huo ila kumbukumbu zake zilimpeleka kuwa alikuwa anampigia dada yake Sophy muda huo na wala hajawahi kuwa na namba ya simu ya Neema kwenye simu yake. Akatafakari sana na kukosa jibu kabisa, wakati akiwa na mawazo alikuja daktari na kuzungumza nae
“Mkeo ameumia sana, inatakiwa tumfanyie operesheni ili kuweka mfupa wake wa mkono na mguu sawa maana umepinda kabisa”
“Mfanyieni dokta, ninachohitaji ni uzima wa mke wangu tafadhari”
“Inatakiwa laki saba na elfu themanini kwaajili ya operesheni hiyo kwahiyo jitahidi ulete hizo pesa ili tuendelee nae”
“Nyie endeleeni nae, pesa kwangu sio tatizo kabisa. Naomba mumsaidie mke wangu”
Kisha akamuaga Yule dokta kuwa anaenda kuchukua hizo pesa na kuendelea kumuomba sana waendelee na kumtibu mke wake kwani alikuwa na hali mbaya.
Ibra aliondoka pale hospitali huku akiongea peke yake,
“Yani huduma za siku hizi jamani kila kitu hela, mgonjwa yupo hoi vile ila wanataka hela kwanza sijui hawa watu wakoje jamani dah!”
Ibra hakuwaza kabisa kuhusu gari lake kwani alihisi kuwa wameliacha sehemu ambayo hakuitambua kwa wakati huo, ila alipofika nje ya hospitali hiyo alishangaa kuona gari yake ikiwa pale nje akajiuliza
“Hivi hii gari nayo ni ya miujiza nini? Hebu ona ni nani kaileta na kuipaki hapa jamani? Au wasamalia wema? Inawezekana kweli? Haiwezekani, nikapande kweli? Mmh mbona moyo wangu umejawa na hofu sasa! Siipandi”
Ibra akaenda mpaka stendi na kupanda daladala ya kuelekea mitaa ya nyumbani kwake na alipofika akashuka na kuanza kutembea kuelekea kwake, njiani akakutana na mtu ambaye amewahi kumuona nyumbani kwa kina Jane,
“kama nakufahamu vile, nimewahi kukuona kwakina Jane wewe”
“Ndio, mimi ni ndugu yake Jane. Nimewahi kukuona pia, wewe si unaitwa Ibra?”
“Ndio naitwa Ibra kumbe hadi jina langu unalifahamu!”
Wakaanza kusalimiana vizuri pale kisha huyu ndugu wa Jane akaanza kumuuliza kuwa anatatizo gani, Ibra akamueleza habari za mkewe kuhusu kugongwa na gari,
“Daha pole sana jamani, amelazwa hospitali gani?”
Ibra akamtajia hospitali aliyolazwa mke wake, kisha Ibra akamuuliza huyu ndugu wa jane kuwa anaitwa nani,
“Mi naitwa Neema”
Ibra akashtuka sana na kuogopa hata kuendelea kuongea nae hadi huyu ndugu wa Jane akaanza kumshangaa,
“Kaka, kaka kwani vipi nini tatizo?”
“Niache, naweza kukufanyia kitu kibaya mimi! Nitakuua tena ukazikwe huko, najua hii ni michezo yako”
“Michezo yangu kivipi?”
Ibra hakumjibu na kuendelea kuondoka kitendo kilichoendelea kumpa maswali huyu dada na kujikuta akimfata Ibra kwa lengo la kuondoa utata kwani hakutarajia kama angemgeukia kiasi hiko, akamsogelea tena na kwa hasira Ibra akamsukuma huyu binti na kumfanya aanguke chini kisha Ibra akaendelea na safari yake.
Alifika nyumbani kwake na kuingia ndani, nyumba yao ilikuwa kawaida kabisa na hapakuwa na tatizo lolote na wala hapakuonekana kama kuna jambo lolote lile lililotokea.
Ibra akaelekea chumbani moja kwa moja na kufungua kabati ila alishtuka sana kwani haikuonekana pesa ya aina yoyote ile, Ibra alichoka kabisa kwa hali hiyo na kujihisi kuchanganyikiwa kabisa,
“Hela zote zimekwenda wapi? Nitafanyaje mimi? Itakuwaje hali ya mke wangu jamani?”
Ibra alijishika kichwa na kuelekea sebleni ila alikuta pananukia sana na alipoangalia mezani alikuta chakula kimeandaliwa, njaa nayo ilimshika sana kwani hawakula chochote na mkewe tangia jana. Ingawa akili yake ilimwambia kuwa chakula kile ni cha miujiza ila aliamua kwenda kukaa mezani na kuanza kukila sababu ya njaa,
“Bora nile tu ili nipate nguvu ya kwenda kutafuta hiyo pesa ya kumuokoa mke wangu, kwanza toka tumeanza kula vyakula hivi vya miujiza na mke wangu hatujawahi kudhurika hata siku moja bora nile tu nipate nguvu”
Alikuwa anakula huku akikisifia kile chakula kimoyo moyo, alipomaliza alianza kutafakari tena
“Sasa ile hospitali aliyolazwa mke wangu si salama tena kwamaana Neema ameshaifahamu hospitali ile, natakiwa nimuhamishe pale mke wangu ila pesa nitapata wapi?”
Akajikuna kichwa kisha akainuka na kwenda tena chumbani, akafungua tena kabati ila hapakuwa na hela yoyote kama mwanzo, akapata wazo la kumpigia simu rafiki yake ili aweze kumkopa kwahiyo akarudi na kukaa kitandani ila kabla hajapiga simu alishangaa kuona pembeni yake pale kitandani pakiwa na kibunda cha pesa. Ibra akajiuliza kuwa zile pesa zimewekwa na nani, akachukua na kuzihesabu alikuta kuna laki tisa, hakutaka kupoteza muda kwa kujihoji akachukua zile pesa na kuweka vizuri kisha akatoka mule ndani kwake na kuanza safari ya kuelekea hospitali huku kichwani kwake akiwaza kumuhamisha mkewe kwenye ile hospitali aliyolazwa kwani aliamini kuwa Yule aliyekutana nae njiani ni Neema na kwavile amemuelekeza hospitali asije akaenda bure, alisahau kuwa Neema Yule anayemuhofia huweza kwenda bila hata ya kuelekezwa.
Ibra alifika hospitali na kwenda kwa daktari moja kwa moja kisha akamwambia kuwa anataka kumuhamisha mkewe hospitali,
“Ila nadhani itakuwa vyema kama tukimfanyia operesheni kabisa, usimuhamishe gafla hivyo”
“Hapana, nataka mke wangu akatibiwe kwenye hospitali kubwa zaidi itakayo nipa amani ya moyo”
“Naelewa unavyomjali mkeo ila nakuomba sana, tumfanyie operesheni kabisa kisha utamchukua”
Ibra alimuhitaji sana mkewe ili aondoke nae ila huyu daktari alikuwa akisisitiza kuwa Sophia aachwe kwa muda kwanza, ikabidi Ibra alipie kabisa kisha atoke nje akisubiri wamfanyie hiyo operesheni na wamruhusu kuondoka na mke wake.
Akiwa pale nje akamuona ndugu yake Jane akienda pale hospitali huku akichechemea kumbe alivyomsukuma aliangukia mguu na kuteguka ila Ibra alipomuona ndio akahisi kila kitu kwa mkewe kimeharibika, huyu ndugu wa Jane muda huu alikuwa ameongozana na mama Jane.
Ibra alimuangalia huyu mama bila hata ya kumsalimia ila huyu mama alipomkabidhi Yule binti kwa daktari akatoka na kumfata Ibra alipokuwa amekaa,
“Nasikia mkeo amelazwa hapa, yupo wodi namba ngapi?”
“Yule mchawi ndio amekwambia? Mke wangu hajalazwa hapa na wala hayupo hapa”
“Huyo mchawi unayemuongelea ni yupi?”
“Si huyo uliyekuja nae, kwanza wewe ni mama Jane kweli au maigizo yanaendelea kwangu?”
“Kwani una matatizo gani wewe?”
“Sina matatizo yoyote, nijibu ni mama Jane kweli au maigizo yanaendelea?”
Mama Jane hakumuelewa kabisa huyu Ibra na hivi alivyogoma kusema mkewe alipo ndio kabisa, ikabidi mama Jane mwenyewe ainuke na kwenda kujaribu kuulizia mapokezi, ambapo wakamuelekeza wodi ambayo Sophia alikuwa amelazwa huku Yule nesi akimdokeza,
“Kama unafahamiana vizuri na huyu mtu tafadhari kamletee chakula ale, tunaogopa kumwambia mumewe kwani inaonekana kama akili yake haipo sawa kabisa kwahiyo yeye anajua kuwa mkewe bado yupo kwenye chumba cha operesheni yani usimdokeze chochote hata hatujui anataka kumpeleka wapi huyu maana anataka kumtoa hapa hospitali”
Mama Jane alisikitika ila hata yeye aliweza kuishuhudia akili ya Ibra kwahiyo alitoka kimya kimya na kwenda kumtafutia chakula Sophia.
Baada ya muda kidogo mama Jane alifika na chakula na kwenda nacho moja kwa moja wodini alipokuwa Sophia ambapo alipomuona machozi tu yalimtoka,
“Pole sana Sophy”
“Asante mama”
Kisha mama Jane akatoa kile chakula na kuanza kumlisha Sophia huku akiongea nae kidogo kidogo kama kumuulizia chanzo cha ajali,
“Ni kitu gani kilitokea Sophy?”
“Hata sielewi, nilishangaa tu nikiwa chini basi mpaka kuletwa hapa hospitali. Hivi na Ibra nae yuko wapi?”
“Yupo nje hapo ila madaktari hawajamwambia ukweli kama umeshaletwa wodini kwani wanadai kuwa kamavile anaonekana hayupo sawa kwani ameng’ang’ania kutaka kukuhamisha hospitali akidai kuwa hapa hawakuhudumii vizuri”
“Kwahiyo anataka kunipeleka hospitali gani?”
“Hata mimi sielewi ni wapi anataka kukupeleka”
“Ningependa kuonana nae tafadhali ili nijue nay eye kakumbwa na nini?”
“Basi kula kwanza kisha nitaenda kumuita umuone”
Mama Jane akawa na kibarua cha kumbembeleza Sophia ale na kwa bahati nzuri alikula vizuri tu kwani ilionekana wazi njaa ilimshika vilivyo.
Alipomaliza kula bado alihitaji kutimiziwa ile ahadi yake ya kumuona mume wake kwanza,
“Sawa nitaenda kumuita ila subiri kwanza nipewe ruhusa na manesi”
Sophia hakupinga kuhusu hilo na alijua wazi lazima ataruhusiwa na atamuona mumewe.
Mama Jane alitoka na kuelekea kwa wale manesi waliompa maelekezo ya alipolazwa Sophia, aliwaelezea haja ya Sophia kumuona mume wake.
“Kwa ushauri alioutoa daktari amesema tungoje usiku uingie kwani hatutampa ruhusa muda huo ya kutoka na mkewe halafu anaweza akatoka naye kesho baada ya kuangalia hali yake ndio ataenda kumuhamishia kwenye hiyo hospitali anayoitaka yeye”
“Sawa, sasa mkewe nimwambiaje?”
“Nenda kamtengenezee uongo tu, mwambie mumewe ametoka na hujui alipokwenda ila sisi tulishamruhusu aje amuone”
Ikabidi mama Jane aende kumwambia hivyo Sophia ambaye aliitikia kwa shingo upande tu.
Ibra nae pale nje alishangaa muda ulivyozidi kwenda bila ya yeye kupata jibu lolote kuhusu mke wake na kila alipoenda kumuuliza daktari alipewa jibu la bado wanamfanyia operesheni. Ila jioni hii Ibra alipaniki kabisa,
“Operesheni gani hiyo mnayomfanyia mke wangu muda wote jamani?”
“Hii ni kazi ya kitabibu kwahiyo unatakiwa kuwa mpole”
“Msinibabaishe jamani, hela ni yangu na mke ni wangu kwahiyo nina uhuru wa kuuliza na kujua. Hospitali zimejaa nyingi tu zenye huduma bora kushinda ya kwenu kwahiyo mnaweza mkanipa mke wangu niende nae. Operesheni operesheni, kitu gani hiko kisichoisha yani niendelee kukaa hapa na kuangalia watu wabaya wakija tu hapana nimechoka”
“Hivi wewe jamaa laiti ungejua kuwa wewe ni kati ya watu wenye bahati sana, huwa hatuna muda wa kubishana na watu kama wewe kwanza akili yako inaonekana imepotea kabisa kwa hali aliyokuja nayo mkeo bado unataka kumuhangaisha kwenye mahospitali kwani tumekwambia tumeshindwa au ni nini? Sasa kwataarifa yako mkeo tulishamfanyia operesheni muda mwingi sana na yupo wodini ila kwavile akili yako mbovu ndiomana hatukukwambia”
Ibra kusikia ameambiwa akili yake mbovu ndio akazidi kupaniki kwa Yule daktari kisha akatoka pale na kwenda wodini bila hata ya kuruhusiwa, alimkuta mkewe akiwa ametulia tu kitandani.
“Sophia tunatakiwa kuondoka hapa”
“Kwanini Ibra? Hata salamu, hutaki kujua naendeleaje?”
“Maendeleo yako ni muhimu sana kwangu ila kuondoka hapa ni muhimu zaidi”
“Sasa tutaenda wapi?”
“Hospitali nyingine nzuri ambayo hakuna mtu hata mmoja anayoifahamu”
“Hapana bhana, mbona hapa wamenihudumia vizuri tu?”
“Sophy nisikilize mimi mumeo, hapa hapafai Neema ameshapajua”
Sophia aliposikia Neema amepajua akashtuka kidogo ila akajipa moyo,
“Hata kama amepajua ila hapa ni salama zaidi”
“Nisikilize mimi mumeo Sophia sitaki upatwe na matatizo, nishalipia kila kitu hapa tuondoke”
Kisha akakumbuka kitu kuwa alikuwa na laki tisa akatoa laki saba na themanini kwahiyo amebakiwa na laki moja na ishirini, akawaza kidogo ila akaona itatosha tu.
Sophia akaamua kukubali na kumuuliza mumewe,
“Ila mimi nitatembeaje?”
“Usijali nitakubeba”
“Halafu tutaondoka kwa usafiri gani?”
“Gari yetu ipo nje hapo”
“Sipandi hiyo gari Ibra”
“Kwanini?”
“Nimeshakataa sipandi hiyo gari”
“Basi ngoja nikachukue tax”
Ibra akatoka na kwenda kutafuta gari ya kukodi.
Alipofika nje ya ile hospitali tu akakutana na gari ya kukodi kanakwamba ilikuwa ikimngoja yeye, akasogea na kuongea na dereva kisha kuingiza ile gari getini ili kuipaki karibu na atakapopanda mke wake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Wakati anatembea kuelekea wodini kuna mtu alimuita na alipogeuka akamuona rafiki yake Lazaro,
“Ibra ulikuwa unaongea na nani pale?”
“Nilikuwa naongea na dereva tax kwani vipi?”
“Kuna dereva tax pale? Umeanza kuchanganyikiwa ndugu yangu”
“Hivi na wewe nini kimekuleta huku? Hebu achana na maisha yangu?”
Ibra akaingia wodini na kumfata mkewe alipolala kisha akamshtua kuwa waondoke,
“Siendi popote Ibra”
“Kwanini? Tatizo ni nini tena?”
“Akili yangu imefunguka”
“Unaongelea nini Sophy?”
“Umekula tena chakula Ibra”
Ibra akashangaa na kumuuliza mkewe,
“Umejuaje?”
Sophia akafunua mkono wake na kumfanya Ibra ashangae kuona alichokishika Sophia.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment