Search This Blog

MUUAJI WA KIKE - 1

 







      IMEANDIKWA NA : LATIFA



      *********************************************************************************





      Simulizi : Muuaji Wa Kike

      Sehemu Ya Kwanza (1)





      Saa nane usiku Skola akiwa chumbani amelala anaamshwa nakusikia sauti ikimuamrisha mbele yake kikatokea kisu kikubwa

      "Skolaa skolaaaa Skolaaaa.......

      Amkaaaaa Amkaaaa nenda bagamoyo Money hotel chumba namba 10 kafanye mauaji wauweee wote waliokuwepo humo ndani chukua iko kisu fumba macho"

      Sauti ilizidi kumuamrisha nayeye bila kutaka akajikuta akichukua kisu nakufumba macho.

      Alipofumbua akajikuta yupo ndani ya chumba cha hotel nzuri yakifahari iliyokuwa bagamoyo akasogea adi kitandani nakuwakuta watu wawili mwanaume na mwanamke hakuuliza wote aliwachoma visu damu zikaruka chumba kizima.

      "Hahahhhahaha hongeraa sana skola sasa unaweza kurudi nyumbani"

      Ile sauti Ilimwambia akafumba machoa nakujikuta chumbani kwake akaingia kitandani nakulala.

      Asubuhi kulikucha akajiandaa nakuelekea shule alikuwa yupo darasa la tano binti mdogo sana.

      ***

      "Mauajii jamanii muheshimiwa waziri amekufaaa ukuuu"

      Mfanyausafi wa Money hotel alikuwa akipiga kelele zilizowashtua wengi wakakusanyika kutaka kuona ayo mauaji yametokeaje.

      "Ebu tuambie vizuri imekuwaje?"

      Meneja wa hotel alitaka maelezo kabla ajapiga simu kituo cha polisi

      "Iki chumba alikodisha muheshimiwa waziri Emanuel alikuwa na mwanamke wamekaa apa kwa siku tatu yeye alipanga akae wiki moja sasa leo nilipoenda asubuh kugonga mlango nifanye usafi nashangaa nakuta wamekufaa"
      http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      Aliongea Ester akilia sana nakuogopa asijekuhusishwa na mauaji hayo.

      Ghafla gari la polisi likafika polisi wengi wakashuka nakusogea kuanza kuhoji imekuwaje wakaingia ndani nakukuta maiti ya muheshimiwa pamoja na mchepuko wake.

      Ilikuwa aibu kwake muheshimiwa waziri kufa hotel na mwanamke mwengine waandishi wa habari wakapata taharifa waliwahi kwenda kwenye tukio nakupiga picha.

      Miili yao ilichukuliwa nakupelekwa hospital uku yule muhudumu Ester akichukuliwa kwa mahojiano zaidi pamoja na meneja wa hotel.

      "Waziri Emanuel kingiki amekufa gesti na mchepuko"

      Gazeti la uwazi linalotoka jumanne liliandika ivyo.

      "Aibu kubwa waziri aiba mke wa mtu mwenye mke amfumania nakuwaua wote kwa kuwachoma visu"

      Gazeti la Risasi likaandika ilikuwa habari iliyogusa wengi sana walioifatilia nakushangaa kifo cha uyo waziri kila mtu alisema lake.

      Maiti ikabidi isafirishwe nakuleta kwa mkewake anaeishi mbezi beach walipofika tu mlangoni wakamkuta mwanamke kavaa pensi la nguvu na t-shirt uku nywele kabana nyuma.

      Walishangaa mke wa marehemu mbona yupo ivyo

      "Haya uyo malaya mnampeleka wapi nauliza?"

      "Mama muheshimiwa huyu mumeo ndo maana tumemleta kwake"

      Alijibu polisi mmoja

      "Weee weee komaa tena ukomee mpelekeni kwa ndugu zake sio kwangu kaniaga anaenda bungeni Dodoma kumbe kaenda gesti na malaya mwenzake tokenii harakaaa nasema mtokee maiti pelekeni kwa wazazi wake"

      Aliongea kwa hasira bi Annastazia mayege ambae ni mke wa marehemu waziri.

      Hawakuwa na jinsi ikabidi wageuze nakuelekea kwa wazazi wake kuipeleka maiti msiba uwe uko

      "Mwananguuuu jamanii weeeee umeniacha na nani mimiiii"

      Walipofika tu wakapokelewa na vilio hakika ilitia simanzi sana.

      Wanaume wenye nguvu waliokuwepo apo wakasaidiana kuingiza maiti ndani.

      Watu wakaanza kuhoji mkewake yupo wapi? Minon'gono ilikuwa mikubwa sana adi ikawa zogo msibani, waandishi wa habari hawakuwa nyuma nao wakaanza kufatilia wapate chakuandika.

      Wakipiga simu yake apokei wakaamua kwenda nyumbani ambapo walikuta nyumba imefungwa kabisa hakuna mtu.

      "Mke wa marehemu akimbia nakususia msiba"

      Gazeti likaandikwa

      "Kisa mumewe kafia gesti mke wa waziri agoma kushiriki mazishi"

      Gazeti jingine likaandika ilikuwa habari iliyowagusa wengi sana.

      Msiba ukawa kivutio wengi wakajaa kumuaga marehemu uku waandishi wakichukua matukio yote zaidi yakusisimua ni mwanamke kugoma kumzika mumewake nakutokomea kusikojulikana ata watoto pia aliondoka nao.

      "Jaman si angekuja tu kumzika mumewake"

      "Wee inauma mwanaume kafia gesti"

      "Atakama mwenzangu angekuja kushiriki mazishi"

      "Kila mtu na moyo wake jaman mwacheni"

      Wanawake wambea hawakosekani misibani walikaa nakumjadiri mke wa marehemu.

      Hatimae ndugu wote walikusanyika na mazishi yakafanyika kwenye makaburi ya kinondoni huo ukawa mwisho wa muheshimiwa Emanuel kingiki waziri wa fedha.

      ****

      "Mama samweliiiii wewe mwanamke usikii nakuita?"

      "Abee mumewangu nakuja jamani"

      "Njoo huone uyu mtoto mdogo wamemtupa apa!"

      "Jesus Christ"

      Alisema uyo mama samwel akishangaa uyo mtoto aliewekwa nje ya nyumba yao! Ilikuwa ni Alfajiri muda ambao mwanaume alikuwa akitoka kuelekea kazini kwake.

      "Sasa tufanyeje mkewangu?

      "Mimi naona tumchukue tumpeleke polisi"

      "Aah ayo mambo ndo sitaki usumbufu tutakula nini sasa? Basi nenda uko polisi acha mimi nikaangaike kufanya kazi"

      "Sawa mumewangu si niende pugu shule pale au adi gongo la mboto?"

      "Nenda pugu tu apo karibu"

      Basi mwanaume aliondoka na mwanamke akajiandaa nakumbeba mtoto akaelekea kituoni kupanda gari Samweli alikuwa yupo shule anasoma darasa la tano.

      Mama samweli na mumewake wanaishi pugu sehemu moja inaitwa kigogo freshi

      Basi akatoka nakupanda gari adi Pugu shule akashuka nakuelekea kituoni ambapo alitoa maelezo yake polisi wakamsikiliza

      "Sawa tumekuelewa tunakukabidhi uyo mtoto ukamlee"

      "Hali ngumu jamani nitamleaje mie?"

      "Wewe mama huna mume kwani?"

      "Ninae lakini hana kazi"

      "Pole sana ila kajitahidini kumlea uyo mtoto kwaheri"

      Walisema hao polisi nakumfukuza Mama samwel akiwaza itakuwaje mumewake akijua amepewa mtoto amlee.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      Akafika nyumbani salama uyo mtoto alikuwa amelala tu akamlaza kitandani nayeye kuanza kupika

      "Haa mama una mtoto umempata wapi?"

      Samwel aliporudi shule aliuliza

      "Mdogo wako huyu"

      Alimjibu nakuingia ndani yule mtoto aliekuwa kama anamiezi mitatu aliamka nakuka kitako mama samwel alishangaa sana kumbe anakaa chini.

      Akamuona akijishika shingoni akamsogelea nakuona kavaa cheni ya gold imeandikwa Skola

      "Skola ndo jina lako eeh?"

      Alimuuliza uyo mtoto akawa anafurahi sana alikuwa mtoto mzuri wa kike akajikuta anampenda sana.

      Usiku uliingia baba samuel akarudi nakushangaa kuona yule mtoto bado yupo

      "Hee huyu mtoto vipi yupo apa polisi ujaenda kwani?"





      "Nilienda lakini nimeambiwa niishi nae"

      Alijibu Mama samuel

      "Lakini wewe mwanamke hali yetu ngumu unaijua bado unaongeza familia tutamleaje uyo mtoto sasa?"

      Mwanaume alichukia sana

      "Najua mumewangu ila ndo tumepewa tufanyaje haina jinsi tumlee ivyo ivyo"

      Basi wakakubaliana kumlea Skola ambae alikuwa mpole wala hakuwa msumbufu wa kulialia ovyo.

      Tangu siku hiyo Mama samuel akamuhesabia Skola ni mtoto wake alimpenda sana nakumlea kama amemzaa yeye.

      Baada ya mwaka mmoja Skolaakaanza kujifunza kutembea adi anafikisha miaka miwili alikuwa kazoea wakitoka sehemu anamshika tu mkono wanaenda.

      "Jamani huyo mtoto mzuri anaitwa nani?"

      "Skola jina lake"

      "Mzuri sana kama angekuwa wangu"

      Skola akawa kipenzi cha wengi kutokana na uzuri wake alikuwa maji ya kunde si mweupe wala mweusi rangi yake ilikuwa inan'gara nakuvutia sana.

      Zaidi akicheka dimpoz zinaonekana nakuongeza uzuri wake alikuwa mnene mtoto mwenye afya nzuri.

      Baada ya miaka mitano akaanza kupelekwa shule nursery ajifunze adi atapofikisha miaka saba apelekwe kuanza darasa la kwanza, kuna wakati usiku Skola akiwa amelala anaamka nakuakaa anafurahi sana kama kuna mtu anaonana nae lakini hakuna aliekuwa akijua anafurahia kitu gani hali iliendelea ivyo adi alipoanza shule ya msingi kigogo freshi.

      Alikuwa akiamka usiku nakuongea na mtu ambae hamuoni.

      alikuwa akilala chumba cha pekeyake anapoamka asubuhi utamani kumwambia mamayake lakini anajikuta amesahau chakusema.

      "Mama jana nimeota naniliu nini vile nikumbushe"

      Aliongea kwa lafudhi ya kitoto mamayake anajikuta akicheka tu.

      "Jamani mimi ndo najua ulichoota ebu njoo unywe chai uwahi shuleni mwalimu atakuchapa ukichelewa"

      Ikawa ni ivyo kila akitaka kusema anasahau.

      **

      Alipofikisha miaka kumi na moja akiwa darasa la tano alishangaa siku moja usiku akiwa amelala anasikia sauti ikimuamsha nakumueleza ikafanye mauaji alitamani kukataa lakini alishindwa akajikuta akiinuka nakushika kisu kisha kutokea sehemu nyingine nakuua watu wawili.

      Yote hayo aliona kama ndoto asubuhi kulipokucha alipokuwa shule alisikia wenzake wakiongea kuhusu vifo vya waziri na mwanamke waliofia gesti akajikuta nayeye akiumizwa na vifo vyao bila kujua muuaji ni yeye Skola.

      "Maskini wamekufa vibaya wamechomwa visu wote inauma sana"

      Alikuwa akisema Irene rafiki yake Skola

      "Mungu awalaani wote waliousika na mauaji"

      Skola alisema akiwaunga mkono wenzake basi wakaongea apo adi kengere ilipolia wakakimbilia darasani.

      Muda wakutoka shule ulifika ilikuwa saa nane mchana shule yao ipo ndani ndani kidogo kuna mapori miti miti mingi ya miembe na mikorosho.

      Wakati wakuondoka njiani alikuwa pekeyake Skola akamuona mwanamke amesimama kwenye mti anamuita akamsogelea ajabu akaona anafanana nae sana sura yake.

      "Shikamoo"

      Alimsalimia

      "Marahaba mwanangu ujambo za masomo?"

      "Salama tu"

      "Aya nilitaka nikusalimie tu Skola nimefurahi unaweza kwenda"

      "Kwani wewe nani?"

      "Usijal ipo siku utanijua"

      Alisema uyo mwanamke Skola akaamua kuondoka adi nyumbani alifika nakukuta wanakula nayeye akajiunga alitamani kumueleza mamayake kuhusu mwanamke aliemuona shule lakini alisahau kuongea.

      ***

      Siku zikazidi kwenda hatimae akafika darasa la saba umbo lake lilizidi kutanuka kwani akishaingia kwenye usichana nakutoka kwenye utoto, alipata marafiki wengi waliompenda kutokana na jinsi alivyo, alikuwa kawaida tu wala akili darasani sio nyingi kiasi kama wenzake.

      Siku moja mwalimu wa hisabati ambae anapoishi sio mbali na shule tena yupo pekeyake alimuita Skola nakumtuma nyumbani kwake apeleke vitabu ilikuwa mida yakuondoka nyumbani umefika

      "Skola nisaidie ivi vitabu peleka nyumbani funguo hii kuna kazi namalizia apa kisha nitakuja"

      "Sawa mwalimu"

      Alikubali Skola nakuondoka na vitabu kumi vya hisabati.

      Alipita njia ile ambayo alimuona mwanamke mzuri akashangaa siku iyo pia anamuona akamsogelea nakumsalimia uku akitabasamu

      "Unaenda wapi na vitabu?"

      "Mwalimu Steven kanituma nipeleke kwake"

      "Mmmh sawa kuwa makini Skola wangu"

      Alisema uyo mwanamke kwa hudhuni kidogo Skola akashangaa

      "Kwani wewe unaitwa nani?"

      "Usijal ipo siku utanijua aya nenda"

      Alisema uyo mwanamke Skola akaondoka adi kwa mwalimu akafungua mlango kisha akaweka vitabu akiwa anajiandaa kutoka akamuona mwalimu wake ameingia kisha akafunga mlango nakumsogelea Skola alipo

      "Kuna nini mwalimu naomba niondoke"

      Alisema lakini hakupata jibu akaona mwalimu wake akivua nguo nakubaki mtupu kisha akamsogelea alipo





      "Mwalimu unataka kunifanya nini?"

      Aliuliza Skola ila hakujibiwa mwalimu wake alimsogelea nakumshika kwa nguvu akamtupa kitandani

      "Unataka kunibaka mimi?"

      Alizidi kushangaa Skola uku machozi yakimtoka na mwili kutetemeka sana,

      "Skola unajua wewe ni mzuri sana nimeshindwa kuvumilia nahitaji penzi lako"

      Alisema mwalimu Steven nakujaribu kumvua nguo Skola ili amuingilie.

      Ghafla bila kutegemea alisikia akipigwa makofi usoni yaliyomfanya apige kelele, mara fimbo akaanza kuchapwa nakuvimba mwili Skola alikuwa akishangaa haelewi ni kitu gani akainuka nakufungua mlango kisha akakimbia adi nyumbani kwao akiwa hoi anahema.

      "Wewe Skola kunanini kwani?"

      "Mwalimu Steven ametaka kuni...bakaaa"

      "Yesuuu yule mwalimu anakichaa eeh akubake mwanafunzi lazima afungwe ni kosa kisheria ngoja kesho twende shuleni tukamshtaki"

      Alisema Mama samuel ambae Skola anajua ni mamayake mzazi.

      Basi alihudhunika sana uyo mama akimuonea huruma binti yake akamtengea chakula ale kisha yeye akaondoka kwenda barabarani kufanya biashara zake ndogondogo.

      Nyumbani alibaki Skola pekeyake alikuwa mnyonge sana akaingia ndani nakujilaza uku akimfikiria yule mwalimu ni kwanini alitaka kufanya vile.

      ***http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      Mwalimu Steven aliendelea kupigwa fimbo mwili mzima ulivimba nakumfanya awashwe sana alitamani kukimbia lakini hakuweza kuinuka alijaribu kuongea sauti haikutoka kabisa alitamani kuomba msaada kwa majirani akaishia kulia kwa maumivu makali fimbo zilizidi kumtandika alilia sana damu zikaanza kumtoka mwilini akaona kisu kikija nakuukata uume wake

      Ni zaidi ya maajabu hakuwahi kukutana na mauzauza ndo mara ya kwanza akajikuta anajuta kumtamani Skola maumivu aliyopata alikoma baada ya muda mfupi akafariki.

      *****

      Asubuhi kulikucha Skola na mamayake wakajiandaa kwenda shuleni kutoa taharifa ya Mwalimu Steven.

      Walifika nakukuta wanafunzi wapo darasani wakaelekea ofisi ya Mwalimu mkuu nakuingia bahati nzuri walimkuta

      "Habari yako mwalimu?"

      "Salama karibu"

      "Huyu ni binti yangu yupo darasa la saba kuna mwalimu anaitwa Steven jana alimpa vitabu apekele nyumbani kwake sasa kufika kule wakati anataka kuondoka yule mwalimu akataka kumbaka mwanafunzi wake ivi ni sawa kweli jamani?"

      Alielezea Mama samuel Mwalimu mkuu alibaki katoa macho asiamini ayasikiayo.

      "Subiri nimtume mwanafunzi akamwite ofisini uyo mwalimu"

      Alisema mkuu wa shule akatoka nje nakuagiza mwanafunzi ambapo baada ya dakika chache alirudi nakusema mwalimu Steven hakuja shule.

      "Unaona mwalimu kajua kosa lake ndo maana hajaja"

      "Inabidi tumfuate nyumbani kwake"

      "Anaweza kuwa amekimbia huyo"

      "Hapana twendeni au twende polisi tukashtaki kwanza"

      Basi walikubaliana wakaenda polisi kuelezea ilivyokuwa kisha wakaondoka adi nyumbani kwa Mwalimu Steven, waligonga mlango lakini kimya wakaamua kufungua nakuingia ndani walichokiona wote walishtuka.

      "Mungu wangu"

      Alisema mama samuel.

      Mkuu wa shule pia alistaajabu hakuamini alichokiona

      "Steven nini kimekukuta?"

      Polisi pia walishangaa sana, mwili ulikuwa umevimba wote uku sehemu za siri zimekatwa kibaya zaidi alionekana amefariki.

      "Tutoeni huu mwili tuupeleke hospital kwanza inabidi tuongozane kituoni kwa maelezo zaidi"

      Alisema polisi mmoja wakakubaliana nakuutoa mwili wa marehemu kisha kuupandisha kwenye gari la polisi nakumpeleka hospital.

      "Skola ebu tueleze ilikuwaje adi mwalimu akataka kukubaka na ulijinasua vipi kwake?"

      Mahojiano yalianza walipofika kituoni uku mwili ukiwa polisi.

      Skola akaelezea alivyotumwa na mwalimu kupeleka vitabu adi alipovua nguo nakumsogelea kisha akamlaza kitandani lakini hakusema kuhusu alivyopigwa makofi aligeuza nakusema alimsukumiza kitandani kisha yeye akakimbia nakuridi nyumbani.

      Wote walikuwa kimya wakimsikiliza Skola akielezea.

      "Muuaji ni nani sasa?"

      Walijiuliza lakini jibu walikosa.

      Kifo cha mwalimu Steven kilitangazwa shuleni na ndugu pia wakapewa taharifa, kilikuwa kifo cha kuhudhunisha sana wengi waliguswa na huo msiba marehemu alikuwa kijana bado ajaoa hakuacha mke wala mtoto hatimae mwili wake ulisafirishwa kupelekwa kijijini kwao moshi na huo ukawa mwisho wake.

      ******http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      Hatimae kipindi cha mitihani yakumaliza darasa la saba kilifika Skola akiwa mmoja wao alijitahidi kufanya pamoja na wenzake

      "Mmmh mtihani wa English ulikuwa mgumu"

      Alisema Irene rafiki yake mkubwa Skola

      "Umeona eeh mi sijui kama nitafauru"

      "Tuombe mungu tu maana maswali magumu sana"

      Walikuwa wamekaa nje baada yakumaliza kufanya mitihani.

      Siku zilisonga wakamaliza mitihani yote nasasa ni muda wakukaa nyumbani adi majibu yatakapotoka.

      Kipindi iki Skola alikitumia kumsaidia kazi mamayake ambae alikuwa akifanya biashara ndogondogo mitaani.

      Siku moja akiwa anatembeza sabuni Skola akakutana na yule mwanamke mzuri anaemuona shuleni

      "Skola ujambo?"

      "Sijambo mama shikamoo"

      "Marahaba unaenda wapi?"

      "Namsaidia mamayangu kuuza sabuni"

      "Sawa pole kwaheri"

      Alisema akiondoka haraka kuna kitu akakiangusha lakini hakukiona Skola akakiona nakuokota ilikuwa pete nzuri yakun'gara akaijaribu nakuivaa kidoleni kwake alipotaka kuivua ikagoma kutoka







      Pete aliyovaa Skola iligoma kuvuka nakumfanya hofu imjae

      "Nikome sasa kuokota pete za watu ona haivuki"

      Alisema akijilaumu sana mwisho akaachana nayo nakuendelea na biashara yake adi alipomaliza akarudi nyumbani.

      Usiku akiwa chumbani amelala akakumbuka ile pete nakuiangalia ilikuwa inan'gara sana.

      "Waoo ni nzuri hii pete naipenda sana"

      Alisema nakuisogeza mkono karibu kuiangalia vizuri hakika ilimvutia sana.

      Asubuhi kulikucha akaamka nakumsaidia kazi mamayake ayo ndo yalikuwa maisha yake kilasiku adi pale matokeo ya mtihani yalipotoka nakuonekana ni mmoja kati ya wanafunzi waliofauru,

      Alifueahi sana Skola lakini tatizo likaja wazazi wake hawana uwezo wakumsomesha alijikuta akilia sana

      "Hali ngumu unaona mwanangu natamani sana uendelee na masomo ya juu tatizo pesa babayako sina biashara yenyewe ngumu unaona leo tunapata kesho tunakosa"

      Aliongea kwa unyonge Babayake Skola na mamayake pia akaongeza

      "Skola mwanangu shukuru mungu adi umemaliza shule ya msingi uko kwengine acha tu hatuna uwezo"

      Alisema uyo mama nakumfanya Skola aangue kilio kama amefiwa alilia sana nakukimbilia chumbani kwake moyo wake ulimuuma kukosa kwenda shule.

      Mkono aliovaa pete ndio aliojichutia machozi nakuzidi kulia, ghafla akainuka nakutoka nje ilikuwa jioni akaenda adi dukani bila kujua anachoenda kununua nini. Alipofika akamuona yule mwanamke mzuri akamsogelea nakumsalimia.

      "Skola nimepita shuleni kwenu nimeona matokeo umefauru nataka nikusomeshe nilipe ada adi utapoingia chuo"

      Alisema uyo mwanamke

      "Hee umesemaje?"

      Aliuliza kwa furaha Skola akamrukia nakumkumbatia kwa nguvu uku akiwa anafurahi sana

      "Asante mama nashukuru sana yani siamini"

      Skola hakuweza kuficha furaha yake.

      Alimuomba uyo mwanamke akajitamburishe kwao nakuwaeleza wazazi wake kuwa atamlipia ada ya masomo, iko kilikuwa kikwazo kwa uyo mwanamke mzuri lakini hakuwa na jinsi alikubali

      "Skola nitakuja kesho sawa eeh leo kawaambie wazazi wajue kuhusu mimi"

      "Sawa mama asante"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      Alijibu Skola nakukimbia kurudi kwao kwa furaha aliwakuta wazazi wake wapo ndani akaingia nakurukaruka akishangiria wakashangaa amekuwaje wakati alikuwa analia.

      "Nimepata mfadhiri wakunisomesha"

      Aliongea akiringa mwenyewe

      "Mfadhiri uyo wakutoka wapi ni mwanaume eeh?"

      Aliuliza kwa ukali babayake

      "Wala si mwanaume! Ni mwanamke mzuri sana nimejuana nae tangu shuleni ameniambia atanisomesha na kesho anakuja mtamuona"

      Aliwaambia nakufanya wazazi wake wamsubiri uyo mwanamke akija.

      Basi kwakuwa muda ulienda Skola akaingia jikoni kupika na mamayake walipomaliza walikula nakuingia kulala wote.

      ****

      Akiwa amelala Skola aliota amekuja kuchukuliwa na yule mwanamke mzuri kisha wakatokea baharini

      "Fumba macho"

      Aliambiwa Skola akafumba na alipofumbua alijikuta yupo kwenye jumba kubwa kama hekaru uku kukiwa na wanawake wengi warembo waliovalia magauni marefu weupe uku wananywele ndefu walizoziachia nausoni wamejiremba nakupendeza

      "Waoo wazuri"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      Alisema Skola akiwaangalia na wao wakawa wanacheka nakuzidisha uzuri wao.

      "Skola njoo uku"

      Yule mwanamke mzuri alimwambia akamshika mkono nakumuingiza ndani alipowakuta mwanaume na mwanamke wote mzee wamevaa mavazi yakifalme uku wamekaa kwenye viti.

      "Heshima yako mtukufu Mfalme! Heshima yako mtukufu Malkia"

      Yule mwanamke mzuri aliwasalimia Skola pia akasogea nakufanya ivyo.

      "Wazazi wangu huyu ni binti yangu nimemleta kwenu mumpe baraka zenu"

      "Sogea mjukuu wangu"

      Alisema uyo Malkia Skola akasogea karibu nakumkumbatia akaanza kunena lugha za ajabu nakufanya Skola mwili wake upatwe na joto sana yule Mfalme pia alisogea akaungana na Malkia kumkumbatia Skola pamoja na uzee wao lakini walikuwa na nguvu sana Skola hakuweza kutoka mikononi mwao alikumbatiwa nusu saa alipoachiwa alijishangaa kujiona amebadirika nakuwa kiumbe mkubwa wa ajabu alipowaangalia wale wengine pia wote walibadirika nakuwa wanatisha sana

      "Karibu nyumbani Ewe mjukuu wa Malkia Zayuke"

      Alijishangaa wametokea kwenye ukumbi mkubwa uliojaa viumbe wa ajabu sana wanaotisha akasikia sauti ikisema nakumkaribisha.

      Vyakula na vinywaji vikaletwa wakaanza kula nakunywa ilikuwa sherehe kubwa yakumkaribisha Skola ujinini ambapo ni kwao na uyo mwanamke mzuri aliitwa Meyan ni mamayake mzazi Skola.

      Baada ya kumaliza kusherehekea Skola alichukuliwa nakutembezwa sehemu nyingi nakuona mengi yanayofanyika baada ya apo Meyan alimchukua Skola nakumrudisha duniani

      "Muda wako wakuishi uku haujafika bado naomba endelea kuwepo duniani mwanangu nakupenda sana mwaah"

      Alisema nakumbusu shavuni baada ya apo akatoweka na Skola akashtuka usingizini



      Skola alishtuka akihema sana kwa ndoto aliyoota aliikumbuka yote nakubaki akiwa haelewi Inamaana gani iyo ndoto.

      "Nitamwambia mama badae kukikucha"

      Alisema nakuendelea kulala. Asubuhi kulipambazuka aliamka nakumsaidia kazi mamayake ajabu alisahau kabisa kuhusu ile ndoto.

      Walikuwa mezani wanakunywa chai babayake Skola ndie alienza mazungumzo

      "Leo ndo anakuja mgeni Skola?"

      "Ndio baba anakuja leo"

      Alijibu wakaendelea kula adi walipomaliza uyo mwanaume aliondoka kazini kwake.

      "Skola baki angalia nyumba ngoja mimi nielekee kupitia madeni yangu tupate pesa yakula"

      Alisema uyo mama akaondoka nakumuacha Skola nyumbani pekeyake.

      Baada ya masaa machache alirudi mamayake Skola na mboga wakisaidiana na mtoto wake walipika nakumngoja baba Samuel arudi wajumuike pamoja kula.

      Muda ulifika uyo baba alirudi wakaungana kula.

      Walipomaliza walikaa ndani wanapumzika Ghafla wakasikia mlango unagongwa, Skola ndie aliwahi kufungua nakumuona yule mwanamke mzuri akiwa amependeza akamsalia nakumkaribisha ndani.

      Ile kuingia tu nyumba nzima ilinukia marashi mazuri,

      "Karibu sana"

      Wote walimkaribisha mgeni wao, Alionekana mwanamke mrembo sana mwenye pesa zake kutokana nakuvaa vito vya thamani mwilini mwake zaidi kilichowachanganya alifanana sana na Skola adi hao wazazi wanaomlea Skola wakabaki namaswali mengi juu yake.

      "Mimi naitwa Meyan naishi Osterbay napenda kumsomesha Skola sababu namuona anania yakusoma sana"

      Alianza kuongea uyo mwanamke ambae muda wote tabasamu lilichanua usoni mwake nakuzidisha uzuri wake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

      "Tunashukuru sana kwa kujitolea mungu akubariki"

      Alisema mama yake Skola, maongezi yaliendelea muda mfupi tu wakafahamiana nakuzoeana sana. Baada ya apo Meyan alifungua mkoba wake nakutoa pesa mabunda matatu zimefungwa akawakabidbi wazazi wake Skola ambao hawakuamini walimshukuru sana.

      Meyan akaaga anaondoka ila izo pesa alizowapa azihusiani na Skola atamsomesha yeye mwenyewe kwasasa wasubiri majibu tu, Aliwaaga anaondoka wakatoka nae nje kumsindikiza, gari kubwa lakifahari lilipaki apo Meyan akawaaga nakupanda kisha akaondoka.

      "Eeh mungu mkubwa jamani umaskini ndo basi tena"

      "Tumesota sana maisha magumu hatimae nasisi tutakuwa watu mbele za watu"

      Walijisemea hao wazazi wa Skola.

      Walikumbuka jinsi walivyopata tabu kumlea Skolaa adi sasa ni mkubwa ameweza kubadirisha maishayao Toka kwenye umaskini nakuwa matajiri walifarijika sana.

      Zile pesa wakaanza kuzipangia mipango kwanza kukarabati nyumba yao iwe ya kisasa pili kufungua biashara na nyingine kuweka bank.

      Walikubaliana nakufanya ivyo, baada ya miezi michache maisha yao yalibadirika sana.

      Kipindi chote iko hawakuwahi kuonana na Meyan.

      ***



      ITAENDELEA

    0 comments:

    Post a Comment

    Blog