Search This Blog

NILIOLEWA NA JINI BILA YA KUTARAJIA - 5

 

    Simulizi : Niliolewa Na Jini Bila Ya Kutarajia

    Sehemu Ya Tano (5)





    Muda ulienda sana bila ya yule mmama kutoka ndani kwake, na sisi tulichoka kungoja pale nje maana hata njaa nayo ilianza kusumbua kwenye matumbo yetu.

    Tukaamua kumuita yule dada na kumuuliza mahali pa kujipatia chakula, nikashangaa akiniangalia kwa umakini sana kisha akauliza

    "Kuna mahali popote mimi na wewe tumewahi kukutana? Naona kama sura yako si ngeni machoni pangu"

    Nikashtuka na kumkatalia kuwa hatujawahi kuonana itakuwa ananifananisha tu, akataka kutuelekeza pa kwenda kununulia chakula ila mama yake akatoka ndani na kumuuliza kuwa anatuelekeza wapi, naye akamjibu.

    Yule mama akaturudisha wote na kusema,

    "Nyie ni wageni wangu hivyo basi mtakula hapa hapa kwangu, watu wa huku hatuna roho mbaya kwahiyo karibuni"

    Tukajigelesha ila hakutaka tuondoke badala yake akamuita mtoto wake mwingine ambapo akamtuma akatuletee maziwa mtindi.

    Alipotuletea akatukaribisha na kutuambia kuwa tupooze njaa wakati chakula kingine kikiwa jikoni.

    Kisha akakaa na kuendelea na mazungumzo na sisi huku akituuliza maswali kwa umakini sana.

    Na mimi nilimuuliza huyu mama maswali kwa umakini ila kuna kipindi ilibidi niwe kimya huku nikimuangalia anavyougua kwa maumivu ya yale maswali.



    Alianza kwa kuniambia,

    "Hebu nielezeni kwa kifupi maana mwanzoni sikuwaelewa, umesema kuwa Carlos alikuoa?"

    "Ndio Carlos alinioa"

    "Mlifunga ndoa ya aina gani na mlifungia wapi?"

    "Kwakweli hapo sitaweza kukueleza mama yangu maana hata mimi mwenyewe sielewi ilikuwa ni ndoa ya aina gani"

    Nikamueleza pia jinsi Carlos alivyotupeleka kwa wazazi wake bandia na jinsi hao wazazi wake walivyokuja kujieleza kuwa ni bandia baada ya kuwabana sana.

    Yule mama alionekana kusikitishwa sana na kusema,

    "Hivi haya mambo mnayoniambia ni kweli au naota? Mbona mmeniletea uchuro jamani!"

    Ikabidi nimueleze pia majina ya wale wazazi bandia wa Carlos naye akakubali kuwa ni kweli hao watu anawafahamu ila walihama miaka mingi iliyopita

    "Sikia niwaambie, kinachonishangaza hapa sio hao wazazi bandia bali huyo Carlos mnayemuongelea. Nadhani hamjielewi kuwa mnamuongelea mtu wa aina gani, au mlikuwa mnamdai?"

    Huku akijifuta tena machozi, ikabidi nimwambie kwa utaratibu unaotakiwa

    "Hapana mama hatumdai ila hii ni kwaajili ya ukombozi wangu, Carlos amekuwa mtu wa ajabu sana kwangu, huwa anakuja na kupotea halafu mara nyingine anabadilika. Kilichonileta huku ni kuwa nahitaji kuwa huru, nahitaji niondokane na mauzauza yanayonisumbua. Tafadhali mama naomba uniambie ukweli kuhusu Carlos ila na mimi niweze kuwa huru"

    Yule mama alionekana kunionea huruma pia kwa yale maelezo yangu, akaendelea kunieleza kwa mshangao sana

    "Mnajua kinachonishangaza juu ya maelezo yenu ni kuwa, unamuongelea Carlos kuwa alikuoa wakati Carlos hajawahi kuoa halafu unasema kuwa huwa unaonana nae mara kwa mara halafu anakuwa mtu wa ajabu. Kwa kifupi ni kuwa, Carlos mwanangu alikufa miaka mitano iliyopita"

    Kwakweli tulishtuka sana kwani hatukutegemea jibu la aina hii kabisa, nilihisi kama naota ila ndio ukweli.

    Nikajikuta nikimuuliza yule mama mara mbili mbili,

    "Carlos alikufa? Tena miaka mitano iliyopita?"

    "Ndio, yani hata huko kaburini basi kumebaki mifupa ya mwanangu tu. Roho inaniuma sana maana mwanangu nilimpenda kupita maelezo na sitaweza kumsahau hata kesho"

    Yule mama akainama akijifuta machozi kwakweli hata mimi machozi yakanitoka, nikaanza kukumbuka jinsi nilivyokutana na Carlos na jinsi alivyokuwa akinisaidia mwanzoni kabla mauzauza hayajawa makubwa sana. Kwakweli Carlos alikuwa rafiki yangu mzuri sana yani nilijihisi kama vile ndio naambiwa kuwa Carlos amekufa leo kwani sikutaka kuamini kuwa kwa kipindi chote kile nilikuwa naishi na marehemu yani nakula nae kuongea nae na kufanya nae mambo mengi, nilijikuta nikiuliza kuwa

    "Kwanini alikufa?"

    Yule mama alionyesha huruma sana na kuanza kutuambia historia ya mtoto wake Carlos.



    "Carlos alikuwa mwanangu wa kwanza, ndiye aliyefungulia uzao wangu kwakweli nilimpenda sana na nilifanya kila kitu ili kuona kuwa mwanangu anaendelea kwani sikupenda aje aishi maisha ambayo mimi nimeishi.

    Nilijua Carlos ndio atakayekuja kuikomboa familia yangu na na kuitoa katika janga la shida na umaskini ila sikujua Mungu alipanga nini, sikujua binadamu wengine wanawaza nini juu yangu.

    Nilimsomesha Carlos kwa kila hali ili kutimiza ndoto yake kwani yeye alipenda kuwa daktari, na kweli alisoma chuo cha udaktari Muhimbili hadi akapata degree ya udaktari na akatimiza ndoto yake ya kuwa daktari. Mwanangu akaajiriwa na alikuwa na mshahara mzuri sana, alikuja huku kijijini kutusalimia na kuonyesha alichopata. Kwakweli tulifurahi sana na kuamua kufanya sherehe kama familia, yani huwezi amini ule usiku baada ya sherehe ndio ulikuwa usiku wa mwisho kwa Carlos (yule mama akainama na kulia kidogo kwa kwikwi, kisha akaendelea kutueleza)

    Kulipokucha, Carlos hakuamka kabisa ikabidi twende kumuangalia. Nikamuona mwanangu akiwa amekauka kabisa kama mti, alikakamaa na hakuweza kupumua tena. Mwili wake wote ulikuwa wa baridi, tulimpeleka hospitali na akaonekana kuwa amekufa na hapo ukawa mwisho wa mwanangu Carlos na ndoto zake za kutusaidia. Hadi leo siwezi kusahau kifo cha mwanangu mpendwa, huwa naumia sana. Natamani awe karibu na mimi anifariji kwa maumivu haya ya moyo wangu"

    Yule mama akalia sana, ikabidi mimi na Sam tuwe na kazi ya kumbembeleza. Kwakweli hata mimi mwenyewe nikaumia sana kamavile sijawahi kumchukia huyo Carlos katika maisha yangu.

    Moyo wangu ukaniambia kuwa si Carlos wa kumchukia bali ni yule jini aliyekuwa akicheza ndani ya mwili wa Carlos.

    Yule mama akatuambia kuwa ataenda kutuonyesha kaburi la Carlos na sisi tukakubaliana nae kwa hilo.

    Nilijiangalia mara mbili mbili kama kweli mimi ni binadamu wa kawaida, yani kukaa na marehemu na kukaa na jini ni kitu cha ajabu sana kwakweli sikujiona kuwa kawaida kabisa, nikajihisi nipo tofauti na watu wengine kabisa.

    Nilikaa karibu na yule mama huku akiongea kwa uchungu kuwa haelewi huyo ambaye alikuwa na mimi ni nani wakati mtoto wake alishakufa miaka ya nyuma iliyopita.

    "Nashindwa kuelewa kwakweli, labda mwanangu amefanywa kuwa msukule. Roho inaniuma sana"

    Tukampooza huyu mama ili asizidi kuumia maana ni kweli inauma kusikia kuwa mwanao aliyekufa miaka mingi iliyopita akionekana kwa watu wengine na kuendelea na maisha kama kawaida.

    Tulimpooza pale na kujaribu kuongea mambo tofauti tofauti, ndio hapa yule mtoto wake mkubwa wa kike alipokuja tena kisha yule mama akamuelezea yote tuliyomwambia kuhusu Carlos ambapo na yeye alihudhunika sana kwa ile taarifa na kuwalaani vikali watu wachawi na kusema kuwa anawachukia sana watu wachawi.

    "Kwakweli toka mwanzo nilijua tu kama kaka yangu hajafa ila amefanywa msukule, yote haya ni kuonyesha kuwa kuna mahali amewekwa ambapo sisi kama familia hatupajui. Nawachukia sana wachawi, yani yule mchawi wa juzi tungempata hakika tungemkatakata kama nyama buchani"

    Mama yake akamuuliza

    "Kwani juzi walikamata mchawi tena?"

    "Hapana, ila ni yule dada wa kipindi kile aliyetufanyia mbwembwe za kupaa hapa ndio alikuja juzi halafu akaniita mimi, loh nilipomuona tu nilikimbilia watu ili twende tukammalize maana yule atakuwa ni mchawi wa kuzimu kabisa"

    Nikahema kwa nguvu huku moyo ukinienda mbio kwani najua kwa vyovyote vile kama wakinijua ni mimi basi nipo kwenye hatari kubwa sana kwa hili.

    Nikatamani kuaga na kuondoka lile eneo lakini sikufikiria kama nimeshamaliza kazi niliyopewa na yule mtu wa ajabu ili niweze kuwa huru kabisa.

    Yule dada aliendelea kuzungumza huku akiniangalia kwa makini sana nadhani alikuwa anahisia kuwa ni mimi sema hakuwa na uhakika sababu ya zile nywele za bandia na miwani ukizingatia sio mtu anayenifahamu.



    Muda kidogo chakula kikaletwa na tukatakiwa wote tukae kwa pamoja na kula kile chakula, walikuwa wameandaa wali kwa maharage kisha tukakaa na kuanza kula.

    Wakati tunakula nikahisi kamavile kuna mtu zaidi yetu anayekula pale, kumbe mama Amina nae alihisi hicho kitu na kusema kuwa anahisi kuna kitu tofauti pale tunapokula ila yule mama alikuwa ni mwanamaombi na kuanza kukemea pale pale.

    Nikahisi kichwa changu kikivurugika, nilihisi kuchanganyikiwa hadi nikaacha kula na kuanza kukimbia.

    Sam akanikimbiza kwa nyuma na kunishika, hapo akafanya nishtuke na akili yangu kurudi. Sam akaniuliza kwa hasira

    "Unafanya nini sasa Sabrina?"

    "Sijui Sam"

    "Acha mambo ya kijinga, tutaaibika hapa kumbuka tupo kwa watu"

    Baada ya muda kidogo yule mama nae akanifata na kuniuliza

    "Una matatizo gani binti?"

    "Hapana, sina matatizo"

    "Sasa mbona ulikuwa unakimbia wakati wa maombi? Au una majini wewe?"

    Aliposema majini nikajikuta nikitetemeka kwa muda, kisha yule mama akanishika mkono na kunirudisha tena nyumbani kwake ila sikuwa na hamu ya kuendelea na chakula tena maana nilianza kujihisi vibaya.

    Yule mama akatubembeleza tule ili tuweze kwenda kulitembelea kaburi la Carlos.

    Niliwaacha waendelee kula huku mimi nikiwa na mawazo yangu yanayonisumbua.



    Baada ya kumaliza kula wakaanza kujiandaa kwaajili ya kwenda kuona kaburi la Carlos, nikajipa moyo na kujitia nguvu kwani sikuwa tayari kuamini kuwa kwa muda wote niliokuwa na Carlos nilikuwa naishi na marehemu.



    Walipomaliza kujiandaa, tukaanza safari ya kwenda huko makaburini.

    Tulipokuwa njiani nilianza kujihisi kuwa nainuliwa juu taratibu.

    Uwoga ukanijaa na kuhisi moja kwa moja kuwa watajua tena mimi mchawi.

    Wakati nikihangaika ili nishushwe nikajishtukia nikitupwa chini, hakuna aliyeona nikiinuliwa ila wote waliona nilipoanguka chini kwani nilitupwa vibaya sana hadi nikahisi kiuno kinakatika halafu wigi langu nalo likanivuka kabisa.

    Wote waliniangalia kwa mshangao, mara nikamsikia yule Amina akisema

    "Kumbe ni wewe!"

    Nikaanza kuogopa na kutetemeka sana.

    Yule dada akapiga yowe la ajabu na muda huo huo watu wakajaa eneo lile.





    Yule dada akapiga yowe la ajabu na muda huo huo watu wakajaa eneo lile.

    Wale watu wakazidi kuitana na kujaa kwenye eneo lile kitu ambacho kilizidi kuniogopesha.Wakaanza kuambizana na kunivuta vuta, yule mama Amina akaja juu yangu kunikinga huku akiwazuia wale watu.

    Sam nae akajitahidi kuwazuia wale watu ila walikuwa ni wenye hasira sana kwani hata na yeye walimsukuma na kumuangusha ila Sam hakuacha kuinuka na kunitetea.

    Mama Amina nae alizidi kunishikilia pale chini dhidi ya shambulio la wale watu mpaka pale maaskari walipofika na kunichukua pamoja na Sam na mama Amina, kisha mama Amina akawaambia askari kuwa wamenifananisha mimi na watu wengine wabaya ila akawaahidi kufanya vyote kunilinda kwavile mimi ni mgeni wake.

    Wale maaskari wakanihoji maswali mawili matatu nami nikawajibu na kukataa kuwa sijawahi kufika eneo hilo.

    Nilitaka wote wasiamini kuwa ni mimi waliyewahi kumuona kipindi cha nyuma kwani ilikuwa ni aibu sana kukubali ukweli kuwa mimi ndiye niliyeangushwa uchi eneo lile.

    Nilikataa hadi kutokwa na machozi na kuwafanya wale maaskari wajue kweli nimefananishwa ingawa na wao walikuwa na mashaka na kunihisia kuwa ni mimi.



    Mwisho wa siku wakaniruhusu kuondoka na yule mama Amina, ikabidi nirudi nae tena nyumbani kwake maana hatukuelewa cha kufanya kwa muda huo ila yule Amina hakutakata kabisa kuniona na alizidi kuchukizwa na uwepo wangu ila yule mama hakutaka tuwe mbali nadhani alitaka kujua mengi kupitia sie kwani bado alikuwa na maswali ukizingatia kuwa nimemwambia kuwa nimewahi kuishi na marehemu mtoto wake ambaye amekufa miaka iliyopita.

    Yule mama akatukaribisha tena nyumbani kwake na kuendelea kutupooza kwa yote yaliyotokea lea.



    Baada ya muda tukajipanga ili tumuage na kuondoka ila akatukatalia sababu giza lilishaingia na kusema

    "Huku kwetu si vizuri kutembea usiku, mtapata matatizo kwahiyo ni vyema mkikaa hapa ili kesho twendo huko makaburini halafu nanyi ndio mtaondoka kwa amani, maana mmeniambia kuwa mmekuja kutafuta ukweli kuhusu Carlos. Ukweli mmeupata kuwa Carlos amekufa, nadhani itakuwa ni vyema mkaona na nyumba yake ya milele. Carlos hatuko nae tena na hatorudi tena duniani, hata mimi nimeshangazwa na stori mliyonipa kuhusu Carlos nadhani ni mambo ya kishetani yanafanya kazi hapo ila Mungu amrehemu mwanangu Carlos popote pale alipo"

    Huyu mama alikuwa na majonzi sana kwa muda wote ambao atakuwa akimuongelea Carlos basi lazima umuone akiwa na machozi kwenye sura yake.



    Chakula cha usiku kikaandaliwa kisha yule mama akakiombea na wote tukaanza kula, ila bado kichwa changu kiligubikwa na mawazo ya kila aina, mawazo ambayo yaliutesa moyo wangu na fikra zangu pia.

    Bado moyo wangu ukasumbuliwa na swali kwamba kwanini Carlos afe? Kwanini afe wakati wa familia yake kuonja ladha ya matunda toka kwake? Kwakweli kifo cha Carlos kiliniumiza sana yani ikawa kamavile mtu niliyemfahamu kwa utofauti na ujini.

    Nikakumbuka ambavyo nilikuwa namkuta akijifanya daktari, kumbe ndio ilikuwa fani yake duniani.

    Kwakweli kwa swala kama hili moja kwa moja nilianza kulibebanisha na uchawi hata mimi mwenyewe kwani sikuamini kama kweli Carlos alikufa kihalali. Ila kwavile wengi wetu hatuoni yaliyojificha basi tunaamini kama tunavyoamini.

    Tulipomaliza kula, yule mama akatuelekeza namna ya kulala kwa usiku huo ambapo Sam alilala kwenye sebule yao kisha mimi akanitaka nikalale nae chumbani kwake maana isingewezekana mimi kulala na yule mtoto wake mkubwa ambaye inaonyesha kuwa kashanichukia tayari.



    Muda wa kulala ulipofika, yule mama akanionyesha mahali nami nikalala hapo.

    Usingizi uliponipitia nikawa mahali pengine kabisa yani kamavile naangalia sinema.

    Nikamuona Carlos akiwa kwenye umbile lake zuri la ujana tena akiwa na sura ya uchangamfu na furaha.

    Nikaona mahali ambako ndio nyumbani kwao na Carlos, watu wakiwa wamejaa akiwemo na mama yake wakicheza na kufurahi kwa pamoja halafu kulikuwa na mtu mwingine ambaye jina lake lilitajwa kila mara na walimuita kama baba yao mdogo, alikuwa kwenye kipaumbele sana.

    Nikamuona baba huyo akiingia kwenye chumba kimoja wapo nje ya nyumba, alikuwa na dawa mfano wa unga unga mkononi kisha akainyunyiza dawa ile kwenye kile kitanda huku akiongea maneno ambayo sikuyaelewa kabisa kisha akatoka.

    Huku nje shamrashamra ziliendelea na baada ya muda zikaisha na kila mmoja akajiandaa kwenda kulala, ni muda huo nilipomuona Carlos akiingia kwenye kile kile chumba ambacho yule baba alikinyunyuzia dawa.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Carlors akalala kwenye kile kitanda na kuanza kutapatapa, alihangaika kwa muda ila mwisho wa siku akawa kimya kabisa yani hatingishiki tena.

    Nikaendelea kuangalia ila ile ndoto ikageuka gafla na kuwa ndoto nyingine kabisa.

    Nikamuona yule Amina dada yake na Carlos akitoka chumbani kwake na kwenda pale kwenye sebule yao alipolala Sam na kuanza kumfanyia mambo ya ajabu yani kama wale wanawake wanaomshawishi mwanaume ili amwingilie.

    Hapo nikashtuka sana, nilikuwa na simu kwenye mkoba wangu uliokuwa pembeni nikaitoa na kuwasha tochi y simu kisha nikainuka na kutafuta mlango ili niweze kuelekea sebleni.

    Nikatoka hadi kwenye sebule yao, nikamkuta yule dada akiwa juu ya Sam wakati huo Sam nae akijitahidi kumtoa yule dada ila kwavile Sam ni mwanaume asingeweza kupiga kelele juu ya yule mdada.

    Nilipofika mimi nikamtoa yule mdada toka kwa Sam ambapo aliona aibu sana na sikuweza kwenda kulala tena bali nilikaa pale pale sebleni na Sam ambaye alikuwa akiniomba msamaha na kuniambia ilivyokuwa wakati mimi nimeona kila kitu kwenye ndoto.

    Sam akanitaka mimi nirudi kulala kwa yule mama ila nikagoma na kumwambia kuwa sijisikii kulala tena.

    "Ila tupo kwa watu Sabrina, unadhani yule mama akiamka na kukukuta hapa atakwambiaje?"

    "Nitajua cha kumwambia, wewe lala tu ila mimi sijisikii kulala"

    Nilikaa na kuitafakari ile ndoto ya kwanza bila kupata majibu maana kifo cha Carlos chote nilikiona ila sijaelewa chochote, nikajisikia vibaya sana na moyo kuniuma zaidi.

    Sam nae hakuweza kulala bali alikaa tu akiniangalia mimi kwa maumivu na hudhuni niliyokuwa nayo dhidi yake na dhidi ya kifo cha Carlos.



    Haikukawia sana pakawa pamekucha kwani niliwasikia wale majogoo wa alfajiri wakiwika, nikainuka na kutoka nje ambapo kulikuwa na kigiza bado.

    Hakuna aliyeniona kwani hata Sam alishapitiwa na usingizi tena.

    Nikiwa nje, nikasikia sauti ikiniuliza

    "Unajisikiaje kukaa na kuishi na mtu ambaye alishakufa siku nyingi?"

    Sura yangu ikainuka na macho yangu yakaelekea kwenye chumba ambacho nilikiona kwenye ndoto zangu, kile chumba alichofia Carlos.

    Nikamuona mtu akitoka mwenye umbile la yule baba niliyemuona kwenye ndoto, alikuwa amebeba kamzigo kadogo kwenye mfuko mweusi.

    Nikamuangalia sana hadi alipotokomea gizani, nikajiuliza maswali bila majibu ila nikajisemea labda anaishi pale.



    Kulipokucha kabisa Sam nae akatoka nje na yule mama wa Carlos baada ya salamu akaniuliza

    "Hivi wewe umelala kweli?"

    Nikatabasamu tu kwani hamu yangu ni kumuuliza kile chumba nilichomuona yule mbaba akitoka.

    "Samahani, naomba niulize kitu"

    "Wewe uliza tu hata usiwe na wasiwasi"

    "Eti kile chumba kuna mtu anaishi ndani yake?"

    Akakiangalia na kuniangalia kwa huzuni kisha akanijibu,

    "Kile chumba alikuwa anaishi Carlos kipindi cha uhai wake ila tangu amekufa hakuna mtu yeyete anayeishi mule"

    "Je kuna mtu huwa analala na kuondoka asubuhi?"

    "Hapana, kile chumba hakina mtu kabisa wamesema wasiende kulala wala kisivunjwe hadi miaka kumi ipite. Ila kwanini umeniuliza hivyo?"

    Nikaanza kumweleza kuhusu mtu niliyemuona akitoka kwenye kile chumba alfajiri ya leo.

    Huyu mama akataka nimuelekeze kuhusu muonekano wa huyo mtu nami nikamwambia jinsi yule mtu alivyo, yule mama akainuka na kurudi na picha kisha akaseme nimuonyeshe kwenye ile picha kama yupo.

    Nilipoangalia ile picha nikamuona na kumuonyesha, yule mama akashtuka ila hakusema chochote kile kisha akarudisha ile picha ndani kwake.

    Sam akanisogelea na kuniuliza,

    "Una uhakika wa kumuona kweli?"

    "Ndio nimemuona, siwezi kuongelea kitu cha ndoto kwa watu. Ni kweli nimemuona kwa macho yangu halisi kabisa."

    Mara yule Amina nae akatoka ndani ila hakutusalimia kabisa yani alitupita kamavile hakutuona, najua aliona aibu kwa mambo yake ya usiku ila mimi sikuwa na shaka nae wala sikumlaumu kwa chochote maana Sam nae alizidi kuwa na mvuto ndiomana dada wa watu akapagawa na kutaka kumtega.

    Tulikaa pale nje tukijadili mambo mbalimbali, mama Amina akatuambia kuwa itakuwa vyema kama tukienda kutembelea makaburi kwa ile asubuhi, na kweli tukajiandaa na kwenda mpaka makaburini.



    Tulipofika makaburini niliangalia kaburi la Carlos kwa uchungu sana, machozi yakanitoka kamavile nimewahi kuishi na Carlos halisia.

    Nilimweka Carlos kwenye kundi la watu wapole na wakarimu, kwani yale mabaya niliyokuwa nafanyiwa na yeye hakuwa yeye bali ni lile jini lililoutawala mwili wake na fikra zake.

    Mama Amina aliponiona nalia sana akanihurumia na kunitoa pale kwenye kaburi kisha tukarudi nyumbani kwake, ni kweli Carlos hakuwa mtu tena kama nilivyokuwa namfikiria, bali Carlos alikuwa ni marehemu aliyekufa akiwa na lengo la kuikomboa familia yake na kuitoa kwenye umaskini ambao uliwatawala pale kwao.



    Tulikaa pale nyumbani kwa wakina Carlos tukiwa na nyuso za huzuni sana, Sam akaniambia kuwa jioni tuondoke ilituweze kurudi mjini kisha kesho yake tufanye safari ya kurudi Dar, nami nikaafikiana nae juu ya hilo swala maana ukweli wote tulishaupata ingawa kuna sauti ilikuwa ikiniuliza

    "Una uhakika kuwa ukweli huo unajitosheleza Sabrina?"

    Nikajaribu kupingana na sauti ile ili niweze kusonga mbele na mambo mengine yaendelee.



    Mchana ulipofika tulianza kujiandaa kwaajili ya kuondoka eneo hilo.

    Nikaenda kuongea na Mama Amina kwaajili ya kuagana na kama ikiwezekana basi tupeane mawasiliano.

    Wakati nazungumza nae, alikuja yule baba niliyemuona kwenye ndoto na niliyemuona alfajiri akitoka kwenye chumba walichoniambia kuwa kilikuwa ni cha Carlos.

    Yule baba alimsalimia mama Amina na kutoa mfuko mdogo mweusi ili kumkabidhi mama Amina, ila nikapata mashaka na ule mfuko kwani ndio nilimuona akitoka nao.

    Kumbe mama Amina na yeye alikuwa na mawazo yake kwani gafla tu nikamuona akimgeukia yule baba na kuanza kuongea kwa ukali,

    "Kabla sijapokea huo mzigo wako naomba kwanza tukaingie kile chumba"

    Mama Amina alionyeshea kwenye chumba cha Carlos, kitu kilichofanya yule baba muulize kwa mshangao

    "Kwani unatatizo gani shemeji?"

    "Sio nina tatizo gani, leo umeonekana ukitokea mule na wakati umesema kuwa asiende mtu kwenye chumba kile. Sasa kwavile wewe mwenyewe umefuta hilo sharti basi nataka mimi na wewe muda huu twende mule ndani nikaone na mimi kuwa kuna nini humo ndani!"

    Yule baba akaonekana kuchukia na kuuliza kwa ukali,

    "Nani kaniona?"

    Yule mama akanionyeshea mimi kuwa ndiye niliyemuona, yule baba akachukia sana na kuja kunitingisha tingisha kwa hasira na kusema

    "Umeniona wapi wewe binti muongo?"

    Hapo nikapatwa na hasira na kuanza kuongea maneno ambayo yakawashangaza pale

    "Unataka kujua nimekuonaje? Unataka kuyajua na uliyoyafanya? Kumbuka kwenye sherehe ya Carlos ulienda kuweka nini kitandani kwake? Wewe ndio chanzo cha kifo cha Carlos"

    Sam akaingilia kati ili anipooze sema sikunyamaza na kuendelea kuongea kwa jazba dhidi ya yule baba

    "Na wewe ndio chanzo cha matatizo yangu, waambie ndugu zako vizuri, waambie ni wapi ulipomuweka Carlos"

    Yule baba alizidi kupatwa na hasira na kutamani hata kuniponda ponda ikabidi mama Amina aingilie kati.

    Kwakweli hata mimi mwenyewe sikuelewa ni jinsi gani nimeweza kuongea maneno yote yale kwa mtu nisiyemjua kama yule baba.

    Kilichoendelea pale ilikuwa ni varangati tu, Sam akashauri kuwa bora tuondoke kabla mambo hayajawa makubwa zaidi maana yule baba alikuwa na hasira sana kiasi kwamba angeweza hata kuua mtu.

    Watoto wa mama Amina walikuja kusaidia na kufanya mimi niweze kuchoropoka eneo lile na kuondoka na Sam.



    Wakati tunaondoka tukasahau njia tuliyokuja nayo na kujikuta tukipita njia ya kuelea makaburini.

    Kufika kwenye makaburi ndio tukashtuka kuwa tumekosea njia, Sam ndiye aliyenishtua.

    "Tumekosea njia Sabrina, tupo makaburini"

    Kuangalia pale chini nikajiona nipo juu ya kaburi moja wapo, kuliangalia vizuri ni lile kaburi la Carlos.

    Nikashtuka sana na kuanza kuondoka ila nikashikwa mguu na mkono wa mtu toka kwenye lile kaburi.





    Nikashtuka sana na kuanza kuondoka ila nikashikwa mguu na mkono wa mtu toka kwenye lile kaburi.

    Nikataka kusogea mbele tena ila mguu wangu ukavutwa zaidi na kufanya nikose uwezo wa kusimama zaidi hadi nikaangukia lile kaburi.

    Nikasikia sauti ya mtu akicheka sana wala Sam sikujua alipo kwa wakati huo.

    Nilitetemeka sana kwa kuwa juu ya kaburi ila ile sauti ya kicheko ilinitisha zaidi kwani ilikuwa ni sauti ya yule jini.

    Nikazidi kutetemeka pale juu ya kaburi na sikuweza kuinuka kabisa. Yule jini akatokea mbele yangu huku akiendelea kucheka kisha akaanza kusema kwa kuuliza,

    "Unadhani umekamilisha kazi yako Sabrina?"

    Nikatingisha kichwa kumaanisha kuwa sielewi kama nimekamilisha au la, kisha akaendelea kuongea na kuniuliza tena

    "Kama huna uhakika kwanini unataka kuondoka?"

    Nikaendelea kuwa kimya zaidi,

    "Wewe mwenyewe ndiye uliyechagua kufanya kitu hiki, unatakiwa kuwa imara. Huwezi kuondoka hiki kijiji kabla ya kukamilisha kazi uliyochagua"

    Hapo nikajikuta nikimjibu,

    "Lakini mimi ulinipa kazi ya kuujua ukweli na ukweli nimeshaujua"

    "Na baada ya kujua ukweli unadhani nini kifatie? Unatakiwa wewe Sabrina uwasaidie wale binadamu wenzako kisha mimi nitakuja kukwambia ni kwanini nimekusumbua siku zote hizi. Muda utakapogundua kuwa ulipenda mwenyewe basi hautonilaumu sana"

    Kisha akatoweka, nikajisikia kamavile nashtuka kutoka usingizini, niliangalia pande zote mbili na kuanza kukimbia baada ya kushtuka na kutazama yale makaburi.



    Wakati nakimbia, njiani nikamuona Sam akiwa chini ikabidi nisimame ili nimuangalie kwanza.

    Alikuwa hajitambui ila nilipomtingisha akaamka kama mtu anayefukuzwa vile na hata yeye akanishangaa na kuniuliza

    "Imekuwaje hapa Sabrina?"

    "Turudi kwa wakina Carlos Sam maana hata sijielewi"

    Sam akasimama vizuri na kuanza safari ya kurudi nyumbani kwa mama yake na Carlos, huku akiendelea kuniuliza maswali ambayo sikuwa na majibu yake kwakweli

    "Hivi kwanini inakuwa hivi Sabrina?"

    "Sielewi Sam, yani hata mimi mwenyewe nashangaa kwakweli"

    "Sasa mwisho wa haya yote ni nini?"

    "Sam, sijui mwenzio. Nahisi kuchanganyikiwa tu"

    "Ila yote haya umeyataka mwenyewe Sabrina, ona sasa ule ugomvi wa kule na yule mbaba tutauweza kweli?"

    Sikuwa na jibu zaidi ya kuendelea kutembea ili tuweze kurudi huko nyumbani kwa kina Carlos bila hata ya kujua kuwa tukifika mahali pale tutafanya kitu gani.



    Tulipokaribia kufika nyumbani kwa wakina Carlos tukawaona bado wakiendelea na ule ugomvi.

    Mimi na Sam tukajibanza mahali ili kungoja ule ugomvi uishe ila haukuisha bali waliendelea kugombana tu na kutupiana maneno.

    Sam akawa ananilaumu kwa yote.

    "Si unaona mwenyewe Sabrina ulichosababisha! Unadhani ule ugomvi utaishia wapi?"

    Nikajisikia nikimwambia Sam kuwa tujitokeze tu ila Sam akakataa

    "Hapana Sabrina, tukijitokeza tutazidisha tatizo juu ya tatizo"

    "Hapana Sam, twende tujitokeze tu maana yule baba analumbana na wale kwaajili yangu. Ni bora mimi mwenyewe nikajitokeze pale"

    "Huoni kama ugomvi wote utaamia kwako?"

    "Hata kama, ugomvi ukihamia kwangu nitajua jinsi ya kujikinga ila ule ugomvi unavyoendelea pale ni kitu cha khatari zaidi maana wanaweza wakaumizana na hata kuuana wale"

    Ikabidi Sam akubaliane na mimi ili tujitokeze na kuonekana kisha ugomvi ule niubebe mimi mwenyewe niliyeuanzisha.



    Tukajitokeza mimi na Sam kwa pamoja, nikashangaa wale wote waliokuwa wanagombana pale wameacha na kuanza kutushangaa mimi na Sam.

    Nikamgeukia Sam na kumuuliza kwani na yeye alikuwa ananishangaa,

    "Wanashangaa nini Sam?"

    "Wanakushangaa wewe Sabrina"

    "Mimi nina nini Sam?"

    "Ulivyovaa"

    Moja kwa moja nikajihisi labda nipo uchi kama kipindi kile waliponikamata na kuniita mchawi, nikashusha macho na kujitazama kwa uoga. Nikajikuta eti nimevaa gauni la harusi tena gauni lile lile nililovaa wakati napelekwa kufunga ndoa na Carlos ambapo badae akabadilika na kuwa lile jini, kwakweli nilijiogopa sana na lile gauni kwani hata sikujua kuwa nimevishwa muda gani.

    Mama Amina na wengine waliendelea kunishangaa na lile gauni nadhani walikosa hata cha kuniuliza, Sam nae alibaki akiniangalia tu hadi nikatamani kukimbia lakini hata kama nikikimbia nitakimbilia wapi? Sikuwa na la kufanya, nikaamua kutembea ili kuelekea mama Amina alipo.

    Wote walikuwa wakiniogopa utadhani wameona mzuka au mtu wa ajabu kumbe ni mtu wa kawaida tu.

    Nilijihisi kuwa nimevaa na viatu, kuvitazama ni vile viatu nilivyoletewa na Carlos kipindi nipo nae karibu na kunifanya nizidi kuogopa ukizingatia kuwa Carlos ni marehemu tayari.

    Mama Amina nae akaniogopa na kuanza kurudi nyuma, kwakweli sijui nilikuwa nafanana na binadamu wa aina gani, nadhani nilikuwa tofauti na binadamu wa kawaida kabisa.

    Nikaachana na mama Amina kisha nikajikuta nikimfata yule baba, wote walikaa kimya wakiniangalia hakuna hata mmoja aliyethubutu kuniuliza chochote wala kunifatilia kwa nyuma kwani hata Sam mwenyewe alikuwa ameduwaa.

    Yule baba nikampokonya ule mfuko wake mweusi ambao ulikuwa na vitu asili ya unga unga, kisha nikaufungua na kuelekea kwenye chumba walichosema kuwa ni chumba cha Carlos.

    Nikatoa ule unga unga na kumwagia mlangoni kisha ule mlango ukafunguka wenyewe, halafu nikaingia ndani na kumwagia ule unga kwenye kitanda kilichoonekana mbele yangu halafu nikatoka tena nje na kumfata yule baba ambaye alikuwa kama kapigwa na bumbuwazi kisha nikamwagia ule unga unga kichwani.

    Nikamshika mkono na kumuongoza hadi kwenye kile chumba.



    Tulipoingia kwenye kile chumba ndipo nikashtuka na kurudiwa na akili zangu za kawaida kwani nilimuona Carlos amerehemu akiwa pale kitandani kama ambavyo nilimuona kwenye chumba changu kipindi kile ambacho nilirudishwa nyumbani kimaajabu.

    Nikaogopa sana kwani alikuwa akitokwa na funza kama chumbani kwangu vile vile.

    Nikakimbia kwa uoga na kumkimbilia Sam, kitendo kile kilifanya wote wa pale nje waende ndani kushuhudia kuwa kwenye kile chumba kuna vitu gani.

    Nilimkumbatia Sam kwa nguvu huku nikiogopa na kutetemeka, kisha Sam akaniambia

    "Niangalie vizuri Sam wako Sabrina"

    Nikainua macho na kumuangalia, hakuwa Sam bali alikuwa ni Carlos.

    Muda huo huo uzalendo ukanishinda na kujikuta nikizimia.



    Wakati nimezimia, nikajikuta nimepelekwa eneo lingine kabisa yani nimekalishwa mahali halafu yule kijana wa ndotoni yupo mbele yangu na kuanza kusema

    "Ungekubaliana na mimi Sabrina wala usingepitia yote haya uliyopitia, ila kwavile umeamua kwa hiyari yako kutafuta ukweli kuhusu Carlos basi huna budi kumsaidia Carlos ili afe kweli"

    Nikajiuliza mwenyewe, inamaana Carlos hajafa kweli? Yule kijana wa ndotoni akanijibu

    "Carlos amekufa kidhahania ila kiuhalisia Carlos bado yupo hai na ni mmoja wapo kati ya binadamu wanaoteseka sana, unatakiwa wewe uliyejitolea kutafuta ukweli juu yake umsaidie ili afe kweli"

    Nikajiuliza tena, nitamsaidiaje aweze kufa tena? Yule jini akanijibu yeye,

    "Ile maiti mliyoiona ya Carlos mnatakiwa kwenda kuizika tena kwenye kaburi lile lile ambalo alizikwa mwanzo kwa uongo"

    Nikajiuliza tena, je Carlos hawezi kuwa hai tena? Akanijibu tena,

    "Haitawezekana kwakuwa Carlos si mtu tena, unatakiwa kukubali na kufanya nilichokwambia. Yote haya yafanywe na wewe Sabrina"

    Nikajiuliza tena, nitawezaje kubeba maiti mimi mwenyewe na kwenda kuchimba kaburi na kuzika tena? Akanijibu kwa swali

    "Kwani uliwezaje kukaa, kuongea na kula na maiti? Kama vyote uliweza basi na hili ninalokwambia utaweza tu"

    Akatabasamu kama mtu mwenye furaha sana na kunifanya mimi nizidiwe kwa uoga.



    Nikashtuka kutoka kwenye ile hali ya kuzimia na kuwa macho sasa, nikashangaa kuona kuwa nimezungukwa na watu wengi sana, nikaogopa kwakweli.

    Mama Amina akanisogelea na kuniambia,

    "Asante Sabrina kwa kutuonyesha ukweli, siku zote sikumjua mbaya wangu kuwa ni nani. Baada ya miaka mitano ya kifo cha mwanangu leo nimemjua aliyetenda yote yale tena amejisema yeye mwenyewe amakweli binadamu sio watu kabisa"

    Nikajikuta nikimuuliza

    "Na Carlos yuko wapi?"

    "Carlos alishakufa mwanangu, hatuko nae tena"

    "Maiti yake iko wapi?"

    "Mmh Sabrina, unaulizia maiti ya mtu aliyekufa miaka mitano iliyopita? Maiti itoke wapi? Tulishazika tayari, kifo cha mwanangu kinaniumiza sana"

    Nikakaa vizuri na kumkumbatia yule mama huku nikijiuliza kuwa je hiyo maiti niliyoambiwa nikaizike tena ni maiti gani? Sikuelewa kabisa na kuhisi kama nikianza kuwa na ukichaa maana akili yangu ilikuwa ikifikiri na kuwaza mambo yasiyowezekana duniani.

    Kwamaana hiyo hata ile maiti kwenye chumba cha Carlos ni mimi mwenyewe niliyeiona kwani haikuongelewa kabisa.

    Watu wote pale walikuwa wakiongelea habari za yule baba yao mdogo ambaye kajiumbua mwenyewe tu basi.

    Sam alikuwa amekaa pembeni akiniangalia ila niliogopa kumsogelea kwa kuhofia mambo yale yale ya muda ule ukizingatia giza lilikuwa limetanda.

    Sam akanisogelea mwenyewe na kutaka kunishika mkono, nikajikwepesha kisha akaniuliza.

    "Mbona unaniogopa Sabrina?"

    Nilimuangalia mara mbili mbili huku nikihofia kuwa atanibadilikia, ila Sam hakubadilika bali alikuwa Sam yule yule wa siku zote anayenielewa na kunitambua kuwa nina matatizo gani.

    Nikajiangalia na mwilini kuwa bado nina lile gauni la harusi ila halikuwepo tena mwilini mwangu bali nilikuwa na nguo zangu za kawaida.



    Usiku wa leo familia yote ililala pale sebleni kama wafanyavyo watu wakifiwa basi ndivyo ilivyofanya familia hii siku ya leo.

    Wakati tumelala huku nikiwaza kuwa kesho nisafiri na kurudi kwetu maana mambo yale yalishanichosha tayari.

    Usingizi uliponipitia, nikashtukia kama nainuliwa kutoka pale nilipolala, kisha kukawa na mtu ananiongoza kuwa nitoke nje nami nikaanza kumfata taratibu.

    Kufika nje kulikuwa na mtu mwingine aliyekuwa akinifata nyuma nyuma kama roboti, hata sikuelewa wala kutambua chochote.

    Kuja kushtukia nikajikuta nipo makaburini, pembezoni mwa kaburi la Carlos likiwa limechimbwa kabisa halafu pembeni yangu alisimama Carlos akiwa kama roboti. Mbele yangu alisimama yule jini na ndiye aliyeniita kimazingara toka usingizini.

    Mwanadamu wa kawaida nikiwa mimi mwenyewe kati yao nikaanza kuogopa sana.



    Yule jini akaanza kunipa amri zake kuwa nimuamrishe Carlos kuwa aingie kwenye kaburi lake, nilikuwa natetemeka sana kwani ujasiri huo sikuwa nao. Yule jini akaniambia tena,

    "Mwamrishe haraka kabla hapajakucha maana kama pakikucha itabidi na wewe uingie nae humo na mzikwe pamoja"

    Akawa anacheka huku mimi nikitetemeka, niliangalia kila mahali lakini sikuwa na uwezo wa kukimbia wala kufanya kitu chochote kile.

    Ikanibidi nitafute ujasiri na kumuamuru Carlos kwa kumwambia

    "Carlos ingia kwenye kaburi lako"

    Yule Carlos akatii amri na kuingia kwenye lile kaburi.

    Mambo haya yalikuwa ya ajabu sana kwangu hata natetemeka nikiyakumbuka.

    Carlos alitulia kwenye lile kaburi kisha yule jini akaanza kufukia lile kaburi, kugeuka nyuma nikamuona yule mbaba yani baba yao mdogo na wakina Carlos akilia sana huku akiwa kama mtu anayeniomba kutofanya kile nilichokifanya.

    Hapo hapo nikapatwa na nguvu za ajabu na kuanza kukimbia.

    Kufika kwa wakina Carlos ilikuwa tayari pamekucha halafu nikamuona yule mbaba nae akija mbio na kuanguka upenuni mwa nyumba yao na hapo kunifanya mimi nizidi kuchanganyikiwa.

    Moja kwa moja niliingia ndani na kumuamsha Sam kuwa tuondoke kwani sikutaka tena kuendelea kukaa pale wakati kazi nishaimaliza.

    Sam akaamka na kunishangaa nikiwa na matope miguuni ila sikutaka kupoteza muda tena yani nilikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa hata Sam akanishangaa ila ikabidi akubaliane na mimi na kutoka nje na kuondoka, yule mbaba tukamuacha pale pale chini.



    Njiani nikakumbuka kuwa pochi yenye hela zote nimeiacha kule kule hapo ndio penye utata na kurudi tena kwenye nyumba ile sikutaka.

    Sam akajitolea kuwa yeye arudi ila nikaogopa kubaki peke yangu pale njiani na kurudi sikutaka.

    Wakati nabishana na Sam, mbele yetu akatokea mtu wa ajabu hatujapata kuona.

    Alikuwa mrefu sana halafu ana kwato miguuni.





    Njiani nikakumbuka kuwa pochi yenye hela zote

    nimeiacha kule kule hapo ndio penye utata na kurudi

    tena kwenye nyumba ile sikutaka.

    Sam akajitolea kuwa yeye arudi ila nikaogopa kubaki

    peke yangu pale njiani na kurudi sikutaka.

    Wakati nabishana na Sam, mbele yetu akatokea mtu

    wa ajabu hatujapata kuona.

    Alikuwa mrefu sana halafu ana kwato miguuni.

    Tukaogopa sana kumuangalia kwani alikuwa anatisha sana, hatukuweza kumuona kichwa chake ila tulimuona miguu yake kuwa ni kwato za ng'ombe.

    Hofu ilizidi kutawala pale tulipoamua kukimbia ambapo alitukamata kwa mikono yake na kuturudisha pale pale alipo, hakuna aliyeweza kuzungumza kati ya mimi na Sam hatukuweza kuuliza chochote wala kuhoji maana tulikuwa tukitetemeka tu.

    Kwakweli hali ilikuwa mbaya, yule kiumbe alikuwa na mikono mirefu hakuna mfano, akatubeba na kutuinua juu kabisa karibu na sura yake.

    Hapo ndipo nikamtambua kuwa ndio yule jini anayenisumbua siku zote, macho yake yalikuwa yakiwaka moto kama ambavyo yaliwaka moto macho ya Carlos siku ambayo mama nae alimshuhudia na kushtuka.

    Si mimi wala Sam aliyeweza kutazama yale macho yanayowaka moto, kisha akatushusha chini na muda huo huo na yeye akawa katika umbo kama la binadamu ila macho yake yalikuwa yakicheza cheza sana, hayakuwa kama yalivyo kwa binadamu wa kawaida.

    Akatuamrisha kuwa tukae chini, nasi tulitii amri na kukaa pale chini bila ya ubishi wa aina yoyote kisha nae akakaa mbele yetu sina hakika kama kweli watu wengine hawakutuona ila hatukumuona mtu yeyote akikatisha eneo lile yani tulikuwa watatu tu.

    Yule jini alikuwa anatuangalia kwa macho makali sana kitu kilichofanya kuwa hata mimi niiname muda wote kwa uoga, kisha akaanza kuongea na kuniuliza mimi

    "Unakumbuka nini Sabrina?"

    Sikujibu kitu kwani niliogopa sana na sikujua anasema kukumbuka kivipi na kukumbuka lipi, kisha akauliza tena

    "Unakumbuka nini Sabrina?"

    Nikaogopa zaidi baada ya yeye kuwa kama mtu anayerudia maswali juu yangu, muda mwingine nikatamani iwe ndoto ila haikuwa, Sam nae alinyamaza kimya kabisa kama kawekewa gundi mdomoni ila hata kama akiongea ataongea kitu gani.

    Muda wote yule jini alikuwa akiniangalia huku akinitaka nimjibu ninachokumbuka ila nikashindwa kumjibu sababu hakuna chochote ninachokumbuka ukizingatia mambo ya ajabu yamekuwa mengi sana kwangu tena kwa wakati mmoja.

    Akazidi kunitazama na macho yake ya kucheza cheza, kisha akaniambia tena

    "Nikukumbushe Sabrina?"

    Bado sikuweza kujibu kwani nikifikiria kuwa huko kukumbushwa nitakumbushwa kwa njia gani? Nikaogopa kwani inaweza kuwa ni njia za kutisha sana. Aliponiona kuwa nazidi kuwa kimya, akanipulizia kitu machoni kwangu, hapo hapo zikaja kumbukumbu za kipindi nasoma ilikuwa kamavile maigizo jinsi nilivyokuwa naziona.



    Tulikuwa kwenye kituo cha madaladala baada ya kutoka shule, mimi na marafiki zangu wawili ambao ni Lucy na Suzy.

    Siku hiyo tuliamua kula pesa ya naulia na kushauriana kuomba lifti kama kawaida yetu kwani mara kwa mara tuliufanya mchezo ule.

    Pale stendi tukamuona mwanamke mmoja akiwa amebeba mtoto mgongoni halafu ni mjamzito, mkononi akiwa na mzigo wa mihogo na kichwani alibeba kifurushi kingine, mumewe alikuwa amesimama pale pale karibu yake. Walikuwa wanangoja kuvuka barabara, tuliwaangalia sana na kumsikitikia yule mwanamke.

    Muda kidogo alikuja mdada akiwa mjamzito ila usoni alikuwa amevimba na ilionyesha wazi kuwa alipigwa maana alikuwa akijifuta machozi muda wote.

    Nikawaangalia rafiki zangu na kuwaambia,

    "Ndiomana mimi sipendi kuolewa yani wanaume wapo kama mashetani"

    Suzy akacheka sana na kuniambia,

    "Kuolewa ni mzigo ila kwavile wewe ni mtoto wa kike jua kabisa ipo siku utatamani kuolewa na kuwa na familia yako. Tukiwa hivi na kuwaona watu wanavyotendewa kwenye ndoa zao huwa tunachukia ndoa ila kuna kipindi tutakuwa na uhitaji wa ndoa na itabidi tuolewe tu"

    Lucy nae akasema,

    "Kuolewa si lazima ila kuwa na mpenzi ni sheria ya kila mmoja wetu kwahiyo tusiepuke hilo"

    Ikabidi nimkatishe kuhusu swala la mpenzi kwa kumwambia kuwa yeye bado ni binti mdogo kwahiyo si vizuri kutangatanga na wanaume ila Lucy hakulitaka kabisa hilo na siku zote alijisifu kuwa yeye ni binti mrembo

    "Kwakweli mimi ni mzuri sana, najua wanaume wengi wanavutika kuwa na mimi kwahiyo falsafa yangu ni kutosumbuliwa akili na mwanaume kwani najua akiniacha yeye mwenzie atanichukua"

    Tukaendelea kutaniana na kucheka huku tukiangalia gari za kuomba lifti maana mara nyingi huwa tunaangalia gari yenye mtu mmoja au wawili ili sisi wote watatu tuweze kupanda na kwenda nyumbani.



    Ikapita gari dogo ikiwa na dereva pekee tukaisimamisha ile gari nayo ikasimama ambapo Lucy na Suzy wakakaa nyuma nami nikakaa mbele na dereva, tukamsalimia kisha safari ikaendelea.

    Pale mbele ya gari palikuwa na magazeti, nikachukua moja wapo maana habari ya juu ilinivutia sana, nikataka kujua kulikoni imekuwa vile.

    Habari ile iliandikwa kwa herufi kubwa ikisema,

    "MWANAMKE APIGWA NA MUMEWE HADI KUZIMIA KISA KAUNGUZA MBOGA..."

    Niliguna baada ya kusoma kwakweli na kurudia kauli yangu,

    "Wanaume ni mashetani sana ndiomana mimi sitaki kuolewa"

    Nikawapa lile gazeti Suzy na Lucy ili nao wapate kuona kilichoandikwa.

    Yule dereva alitabasamu kwa ile kauli yangu, nilipokuwa namuangalia hapa sasa kumbe ndio alikuwa yule yule kijana wa ndotoni ila kwa kipindi chote kile sikumkumbuka.

    Yule dereva akaanza kuongea na mimi huku akiniuliza,

    "Kwanini hutaki kuolewa Sabrina?"

    Hapa nilishtuka na kumuuliza kuwa amelijuaje jina langu akaniambia kuwa amewasikia rafiki zangu wakiniita jina hilo kisha akaniuliza tena kuwa kwanini sitaki kuolewa, nami nikamjibu,

    "Sitaki tu kwakuwa wanaume wanaroho mbaya sana"

    Akaniuliza tena na kufanya nishtuke,

    "Je, baba yako anaroho mbaya?"

    "Hapana, ni baba yangu pekee ndiyo mpole labda sijui kwasababu mengine anayajua mama pekee"

    "Basi usiwajumuishe wote, wapo wenye roho nzuri kushinda hata baba yako. Je una mpenzi?"

    "Sina na hata sifikirii kuwa naye"

    Lucy na Suzy wakacheka kule nyuma na kufanya nigeuke na kuwaangalia wanachocheka kuwa ni kitu gani ila wakajifanya kuwa wako bize kusoma lile gazeti nililowapa, kisha nikaendelea kusikiliza maswali ninayoulizwa na yule dereva,

    "Kwanini hufikirii kuwa na mpenzi?"

    "Wanaume wanaroho mbaya sana mi siwezi kuwa nao"

    "Ila wapo wenye roho nzuri"

    Nikacheka na kumjibu,

    "Wenye roho nzuri labda malaika ila sio binadamu wanaotembea"

    "Kwahiyo wewe akija malaika na kutaka kukuoa utakubali eeh!"

    Nikajibu kwa masikhara kwani najua wazi kuwa ni kitu kisichowezekana.

    "Ndio akiwa malaika nitakubali kuolewa ila sio binadamu wa kawaida yani hawafai kabisa"

    Yule dereva akacheka sana tena kwa furaha na kuniuliza,

    "Kama mimi je?"

    Nikamjibu kwa kucheka,

    "Hata wewe hufai"

    "Kwanini?"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Kwasababu ni mwanadamu"

    "Kama nisingekuwa mwanadamu je?"

    "Labda kama usingekuwa mwanadamu"

    Akafurahi sana na kusema kuwa maneno yangu yamemvutia na kumfurahisha sana, kisha akasema

    "Haya maneno kuna siku utayakumbuka sana Sabrina, ni maneno marahisi kuyatamka ila ni magumu kuyatekeleza. Umenifurahisha sana, nitampeleka kila mmoja hadi kwao"

    Na kweli akampeleka kila mmoja hadi kwao na mimi ndiye nilikuwa wa mwisho kurudishwa nyumbani kisha akaniaga na kusema kuwa atakuwa akinitembelea mara kwa mara.

    Nikamkaribisha sana na kumwambia kuwa asiwe na shaka akaribie tu kisha akaondoka zake.

    Niliingia ndani nikiwa sina shaka yoyote ile.

    Kesho yake rafiki zangu walinitania kuwa nimepata buzi dereva ambapo nilicheka tu.



    Baada ya hayo akanirudisha mawazo pale pale tulipokuwapo watatu na kuniuliza,



    "Umekumbuka Sabrina?"

    Nikaitikia kwa kichwa kuwa nimekumbuka kisha akaniuliza tena,

    "Je mimi ni binadamu?"

    Nikakataa kwa kichwa halafu akaniambia,

    "Basi nilikuwa na haki ya kukuoa kwavile mimi sio binadamu wa kawaida, mimi pia ni malaika ninayeitwa jini na ninyi binadamu. Mimi sio mwanadamu ndiomana ninauwezo mkubwa wa kufanya mambo makubwa ambayo binadamu wa kawaida hawawezi kufanya. Je unanilaumu kwa kukuoa wakati ulitaka mwenyewe kwa hiyari yako?"

    Nikaendelea kuwa kimya vilevile ila yule jini aliendelea kuzungumza

    "Siku ile uliwasaidia sana rafiki zako bila ya kujua, nikakupenda sana na kuanza kukufanyia mambo mbali mbali ya kuvutia, wengi wakakuona kuwa unauwezo wa ajabu bila ya wewe mwenyewe kujua kama mimi ndiye nikusaidiaye. Nilikuwa karibu na wewe huku nikingoja muda ufike wa wewe kukubali kuolewa ili niweze kukuoa. Ngoja nikuonyeshe nilivyomfanya mwenzenu mmoja mpenda lifti, lengo langu kwenu lilikuwa ni hilo ila wewe uliwaokoa wenzio kwa maneno yako ya kunivutia"

    Akanipulizia tena machoni kisha nikaanza kuona kama naangalia sinema fulani.



    Nikamuona binti mmoja tuliyezoea kumuita Chaurembo kipindi tupo shule akiwa kituoni na kusimamisha gari za lifti.

    Ikasimama gari kama ambalo lilitubeba sisi na dereva akiwa yule yule, moja kwa moja akampeleka Chaurembo pembezoni mwa bahari kisha akatokea kijana wa ajabu na kumbaka Chaurembo.

    Baada ya hapo Chaurembo hakuweza kwenda shule tena kwani alipatwa na ugonjwa wa ajabu aliopewa na yule kijana.

    Kisha akanirudisha tena katika fikra zangu za kawaida, nikafikiria na kugundua sababu ya mwenzetu huyo kutokuhudhuria tena shule tukaambiwa anaumwa hadi tulipomaliza shule.

    Walimu waliwahi kututangazia kwa kipindi hiko kuwa tusipende kupanda lifti kwenye magari ya watu tusiowafahamu ila hatukuwasikiliza na misheni zetu za lifti ziliendelea kama kawaida, wengine kama wakina Chaurembo madhara waliyapata mapema ila wakina sie ndio madhara tumeyapata badae sana kama hivi na ndio yananitesa na kufanya nionekane kuwa kama mtu wa ajabu kwa mambo ambayo nayafanya mara kwa mara.

    Yule jini alikuwa akiniangalia tu huku akitabasamu kisha akaniambia,

    "Na nyie nilitaka kuwafanyia kama hivyo maana tabia ile mliizidisha sana ila kwa maneno yako Sabrina nikaamua niwe karibu na wewe, nikakupenda sana na nimekusubiri kwa muda mrefu tangia unasoma. Hakuna kitu ulichonikera kama kukuona ukiwa na mahusiano na huyo Sam ila kwavile nilikupenda sana nikakuacha ufurahie hayo maisha ya kuwa na huyo Sam kwa muda kabla ya maisha ya kuwa na mimi ila wewe ukakolea kwa huyo Sam na kufanya chochote utakacho. Nilikaa pembeni nikikuangalia tu siku zote mpaka pale muda wangu ulipofika. Na je unajua kwanini nilimuweka Carlos kuwa karibu na wewe?"

    Sikujua ni kwanini, nikaishia kuwa kimya tu, kisha akasema

    "Najua hukumbuki na wala hujui ila mimi nitakuonyesha ni kwanini"

    Akanipulizia tena machoni halafu ikawa vile vile kama naangalia sinema,



    Nilikuwa na mama tukielekea kwenye hospitali Muhimbili, njiani tulipishana na kijana ambaye alimsalimia mama kwa ukarimu sana. Yule kijana alikuwa ni Carlos ambaye sikumjua kwa kipindi hiko.

    Mama nae akafurahi kusalimiana nae kisha tukaendelea na mambo mengine bila ya kujua kuwa yule kijana alikuwa akituangalia muda wote na alitufatilia kwa yote tuliyoyafanya, ni kipindi hiko ambacho baba yetu alilazwa hapo hospitali kabla ya umauti kumfika.

    Tulienda kumuona baba halafu baada ya hapo tukaondoka na kurudi nyumbani, kumbe nyuma yetu Carlos nae alienda pale alipolala baba, sikujua yote haya ila leo ndio nimeyajua.

    Akainama na kumsalimia baba kisha akaanza kumueleza kuwa amenipenda sana mimi,

    "Samahani mzee wangu naomba nikwambie hili, nimempenda sana huyu binti yako Sabrina nakuahidi nitamuoa na wala sitaki kumchezea kama ambavyo vijana wengine hufanya"

    Baba akatabasamu na kumwambia kuwa anampa baraka zake kwa swala hilo kwani yeye anaona umauti unamkaribia.

    Kesho yake tulipoenda hospitali, nilikaa karibu na baba akaniambia kuwa kuna kitu anataka kunieleza ila kabla hajanieleza mama alinituma nje kumfata ndugu yetu ambaye hakujua baba kalazwa wodi gani.

    Nikainuka na kumfata, tuliporudi nikakuta pazia za kijani zimezungushwa kwenye kitanda cha baba nilihisi kuchanganyikiwa kwani baba alikuwa ameshakufa.

    Kwakweli niliumia sana kwani nilitamani kujua kuwa baba alitaka kuniambia kitu gani.

    Hapakuwa na mahusiano yoyote ya karibu kati ya Carlos na familia yangu ila kumbe Carlos alihudhuria na kwenye msiba wa baba hadi wakati wa kumuaga alimuahidi kitu kimoja kuwa lazima arudi kunioa mimi pindi nikimaliza masomo yangu.

    Baada ya yote alionekana Carlos akirudi kwao akiwa na rafiki yake huku akimwambia swala lile lile kuwa amenipenda sana mimi na lazima aje anioe.

    Aliporudi kwao ndipo na yeye mauti yalipomkuta na ndoto yake ya kuwa na mimi ikaishia hapo kwani haikuwezekana tena, ikaonekana hadi anakata roho akisema

    "Nakupenda Sabrina"

    Kisha nikarudishwa kwenye mawazo ya kawaida sasa ila yule jini hakuwepo tena mbele yangu, ilikuwa kama natoka usingizini vile kwakweli sikuelewa kitu.

    Kuangalia pembeni nikamuona Sam akiwa chini huku damu zikimtoka mdomoni.





    Kisha nikarudishwa kwenye mawazo ya kawaida

    sasa ila yule jini hakuwepo tena mbele yangu, ilikuwa

    kama natoka usingizini vile kwakweli sikuelewa kitu.

    Kuangalia pembeni nikamuona Sam akiwa chini huku

    damu zikimtoka mdomoni.

    Nikatetemeka kwa uoga huku nikimtingisha tingisha Sam pale chini, kwakweli sikujua cha kufanya kwa wakati huo na nilihisi kuchanganyikiwa kabisa kwani haikuwa rahisi kwangu kukubali kumpoteza mtu nimpendaye kama Sam katika mazingira hayo.

    Nilimtingisha sana lakini hakuamka wala kutingishika, nikapiga makelele ili niweze kupata msaada lakini hakuna hata mtu mmoja aliyejitokeza yani ilikuwa ni mimi na Sam pale chini tu kwenye mazingira yale huku nikilia na kuomboleza bila ya kujua kuwa ni kitu gani kifanyie kumkomboa, ni nini nifanye kumtoa pale mbna ilionyesha wazi kuwa Sam amekufa.

    Niliwaza mengi bila ya majibu ya kueleweka kichwani mwangu, nikajiuliza kuwa je nikimbie niende kwenye watu kuomba msaada? Na kama nikiondoka halafu nikakosa msaada nafanyaje? Au nikiondoka halafu wakatokea wanyama wakali na kumtafuna Sam je nitaenda kutoa ushahidi gani nyumbani kwao? Je kuna mtu atanielewa kweli kwa hili? Najua hakuna wa kunielewa kabisa ila je nafanyaje katika kumkomboa Sam hata kama maiti ila ni bora kama nitarudi na maiti yake au kumuacha azikwe mahali ambako panaeleweka ili moyo utulie kiasi lakini kwa hili siwezi.

    Nilijikuta nikijilaumu kwa kila kitu huwa hata ningemkimbia Sam wakati tupo Dar ili nije mwenyewe maana kwa hili sitaweza kwakweli, nahisi kuchanganyikiwa na kuugua moyo.

    Ila nikakumbuka ile pesa iliyopo kwenye pochi yangu niliyoiacha kwa mama Amina kuwa inaweza kunisaidia kumsafirisha Sam hata kama maiti, ila je namuachaje hapo wakati nafata huo mkoba wenye hela?

    Nikaona ni bora nizidi kupiga kelele ili watu watokee na niweze kupata msaada, nilipiga sana kelele bila msaada wa aina yoyote kwani hapakuwa na mtu aliyekatisha wala kuonekana.

    Kwakweli nilijiona kama mtu niliyekumbwa na kiu kwenye jangwa kubwa kwani hata kelele zangu hazikusaidia kitu chochote kile zaidi ya kurudishwa na mwangwi tu.

    Sikuwa na la kufanya, nikaamua kukaa pale pale chini pembezoni mwa Sam huku nikilia na kusema kuwa liwalo na liwe, nilingoja kama atatokea mtu mpita njia kuwa nimuombe msaada wa aina yoyote ile.



    Nikiwa nimekaa pale pembezoni mwa Sam, niliinamisha kichwa changu kwake na kupitiwa na usingizi hapo hapo.

    Nikajikuta niko maeneo mengine kabisa halafu akatokea mbaba mmoja mbele yangu, huyu mbaba aliwahi kuja nyumbani kwetu na kusema kuwa atanisaidia na kuniambia vitu vingi vya ajabu ila alikimbia alipokuja Carlos.

    Nikamuangalia yule mbaba ambapo akaniuliza,

    "Unampenda sana Sam?"

    "Ndio nampenda sana"

    "Basi usimuache kwa lolote lile wala chochote, endelea kumpigania"

    "Unamaana gani?"

    "Usimuache Sam kama kweli unampenda sana"

    Nikashtuka toka kwenye ule usingizi mfupi na kujikuta nikiwa kwenye mazingira yale yale huku Sam wangu akiwa pembeni na zile damu, nikamtingisha tena

    "Amka Sam jamani"

    Ila Sam alikuwa vilevile wala hakutingishika kabisa, nikaanza tena kulia.



    Wakati nalia nikasikia sauti ya muungurumo kama wa mnyama hivi, moja kwa moja nikajua kuwa ule muungurumo ni wa simba maana nishawahi kuwasikia kwenye luninga ambavyo hulia.

    Nikaogopa sana na kuanza kutetemeka huku nikiombea kuwa asiwe yale maeneo ya karibu, ila nilivyoinua macho tu nikakutana macho kwa macho na simba akiwa anakuja pale nilipo mimi na Sam.

    Nikashikwa na kiwewe nikainuka na kuanza kumvuta Sam ila alikuwa mzito sana kwahiyo sikuweza kumvuta zaidi, nikaamua kukimbia na kujibanza pembezoni mwa mti wa karibu na pale ila ikanijia ile sauti ya kusema kwamba usimuache Sam.

    Ukizingatia ni kweli nampenda nikaona bora nirudi pale pale alipo kwani nishajitolea kutokumuacha Sam hata iweje, ingawa Sam pale alikuwa amekufa lakini sikuwa tayari kuona Sam akiliwa viungo vyake na mnyama mkali kama simba halafu mimi nikiwa pembeni huku nikitazama tu bila ya kufanya chochote kile.

    Nikajikuta narudi alipo Sam kisha nikapiga magoti karibu yake na kutubu dhambi zangu zote kwani najua kwavyovyote vile yule simba atatutafuna wote tu yani mimi na Sam.

    Nikatulia pale huku nimeinamisha kichwa na kungoja hatma yangu pale dhidi ya yule simba ila ulipita muda bila ya kuhisi chochote kwani nilijua wazi yule simba lazima atakuwa karibu yetu.

    Kwavile sikuhisi chochote nikajua labda kuna muujiza umetendeka kati yetu, nikainua macho kutazama.

    Nikaogopa sana kwani yule simba alikuwa katulia karibu na kichwa changu, nikainamisha tena kichwa changu chini huku nikiteteme ka mwili mzima na kujua mwisho wangu umefika ila nitakufa kwaajili ya Sam na kwavile nilishajitoa kwa chochote basi sikuwa na budi zaidi ya kutulia eneo lile lile na kungoja hatma yangu kwa yule simba.



    Nikahisi kama kuna mkono wa mtu ukinishikashika kichwani, nikaogopa sana hata kuinua kichwa tena. Yule mtu akaniambia

    "Inuka Sabrina"

    Sauti ilikuwa ni ya yule jini, nikashtuka sana na kumuangalia ni kweli alikuwa yeye.

    Aliniangalia na kuanza kunicheka sana wakati mimi nikizidi kutetemeka bila mwisho.

    Akaanza kuongea na mimi,

    "Katika wanadamu wajinga na wapumbavu basi wewe Sabrina nakupa ushindi huo kwamaana unawaongozea binadamu wenzio kwa upumbavu ulionao"

    Nikamuangalia tu huku nikimuangalia Sam wangu pale chini, lakini yule jini aliendelea kuzungumza pale na mimi

    "Yani upo tayari kufa kwaajili ya mwanaume? Wewe uliyekuwa unasema kuwa wanaume ni mashetani eti leo unajitoa kwaajili ya mwanaume! Kweli wanadamu ni vigeugeu kabisa yani, kwani hujui kuwa akifa Sam utampata mwingine zaidi yako? Ujitoe kufa kwaajili yake kwani ni mzazi wako huyu? Sabrina huna akili kabisa wewe"

    Niliendelea kulia pale, nikona ni vyema kumuomba huyu huyu msaada ingawa ananisema na hata kama ni jini, sina la kufanya kwasasa.

    Nikamsogelea na kumuomba msaada,

    "Naomba unisaidie, nihurumie tafadhari"

    Alicheka sana kisha akasema,

    "Kweli simba akizidiwa hata majani anakula, leo Sabrina unahitaji msaada wangu basi sinabudi kukusaidia mtoto mzuri"

    Alikuwa akiniangalia kwa makini sana kisha akaniamuru nisimame, nami nikasimama.

    Akaniambia nimuangalie maana nilikuwa nimeinama nikitokwa machozi tu, nami nikamuangalia kwa uoga kwani nilijua kuna jambo la ajabu anataka kufanya. Akaniuliza

    "Nimewahi kukufanyia mambo mangapi Sabrina?"

    Huku nikitetemeka nikamjibu,

    "Mengi tu"

    "Unaamini kuwa naweza kukufanyia na hili?"

    "Ndio naamini"

    "Basi huyo aliyelala hapo sio Sam kama unavyofikiria"

    Nikamuangalia yule aliyelala pale chini kisha nikauliza kwa mshangao

    "Sam yuko wapi sasa?"

    "Geuka nyuma Sabrina"

    Kwa uoga sana nikageuka nyuma.



    Nikamuona Sam akija upande wangu, kwakweli sikuamini macho yangu nilimuangalia mara mbili mbili bila kummaliza.

    Nikamsogelea na kumuangalia vizuri, kisha nikaangalia pale chini wala sikumuona yule wa chini tena zaidi ya Sam wangu anayeonekana mbele yangu sasa.

    Nikamkumbatia, hata yeye akashangaa ila akasema

    "Una haki ya kunikumbatia Sabrina"

    Nikamuuliza kwa mshangao kwani nilitaka kujua anachojua yeye,

    "Kwanini?"

    "Ningekufa leo ujue na sijui ungempatia wapi Sam mwingine"

    "Mmh! Niambie kwanza ulikuwa wapi?"

    "Jamani Sabrina! Si ulinituma nikafate mkoba wako wewe, inamaana umesahau gafla?"

    Nikamuangalia Sam na kujikuta nikijiuliza maswali bila ya majibu, maana kwa kumbukumbu zangu ni kuwa wakati nabishana na Sam kuhusu mkoba ndipo alipotokea yule jini, imekuwaje sasa aseme alifata mkoba wangu? Na kama alifata mkoba mbona amekawia sana kurudi? Inamaana matukio yote ambayo yalikuwa yakinipata mimi yeye hakuyaona? Ni nani niliyekuwa nashangaa nae muda wote?

    Nikamuangalia tena Sam na kumuuliza tena ili aniambie vizuri

    "Ulikuwa wapi? Niambie vizuri bhana Sam"

    "Nilifata mkoba wako Sabrina, hakuna lingine lolote zaidi ya hilo. Tulikubaliana mimi nikafate mkoba halafu wewe unisubirie hapo, ni hayo tu"

    "Haya na wapi ulitaka kufa?"

    "Kwanza kumbuka kwamba kule kuna msiba, kwahiyo nilipofika ikabidi nijigeleshe kiasi ndipo niende kuchukua mkoba. Wakati narudi, kufika njiani gafla nikaanza kuumwa na tumbo hadi nikaanguka chini. Kumbe huku kuna baadhi ya wanyama wakali bhana, akaja huyo mnyama hata sijui wa aina gani kwakweli angenimaliza jamani ila akatokea mwanakijiji na kumpiga mshale yule mnyama, nikaenda nae kwake yule mwanakijiji kanipa dawa za huku kwao kwaajili ya tumbo ndio hivi nimerudi ila nilikuwa na hali mbaya kwakweli"

    "Pole sana Sam"

    Kisha nikamkumbatia, nikasikia jina langu likiitwa kwa nyuma, nikageuka alikuwa ni yule jini ndiye aliyeniita na kusema

    "Uliamua kufa pamoja na Sam ila umefanikiwa kumkomboa, kabla hamjaondoka rudini kwenye msiba wa yule baba muhakikishe ameshazikwa ndio muondoke"

    Kisha akapotea, nikashtuka sana na kumuangalia Sam kama alimuona ila inaonyesha wazi kuwa Sam hakumuona yule jini.

    Nikamuomba Sam kuwa turudi kwenye msiba,

    "Hivi wewe Sabrina una kichaa?"

    "Kwanini?"

    "Mambo mangapi tumekumbana nayo hadi kutaka kupoteza maisha kabisa ila unataka eti turudi kulekule tena! Kwakweli mimi sipo tayari, tuondoke na turudi nyumbani"

    "Haiwezekani Sam"

    "Kwanini isiwezekane? Turudi bhana nimechoka kwakweli kila siku yanaibuka mapya, nishachoka jamani turudi tu Sabrina"

    "Sam, nakuomba jamani twende tukazike tu"

    Sam akanijibu kwa hasira

    "Sitaki na nimechoka kwakweli, yote yaliyotokea yanatosha"

    "Basi Sam isiwe tatizo, wewe nenda acha mimi nikazike kwanza"

    Sam akaanza kulia kwa hasira,

    "Hivi kwanini unanifanyia hivi Sabrina? Au kwavile unajua nakupenda sana na siwezi kufanya chochote juu yako,

    kwanini Sabrina unanitesa kiasi hiki?"

    Nilimuangalia Sam bila ya kumjibu chochote ila mimi simtesi kwavile sikumlazimisha kuja ila alitaka kwa hiyari yake mwenyewe na hajui jinsi gani mimi nateseka pia kwaajili yake, anachojua yeye ni kuwa mimi namtesa wakati sina wazo kama hilo katika maisha yangu wala fikra zangu.

    Sikutaka kuendelea kubishana nae zaidi ya mimi kuanza njia ya kurudi tena kule kijijini kwani najua vijijini huwa hawakawii kuzika na inawezekana wakazika siku hiyo hiyo halafu kesho tukaondoka na kurudi nyumbani.

    Sam nae akanifata kwa nyuma kwani hakuwa tayari kuniona mimi nikirudi mwenyewe wakati yeye yupo.



    Tulipofika pale kwa mama Amina, tuliwakuta katika harati za mazishi hata mama Amina nae alifurahi kuniona tena.

    "Bora mmekuja ili tuzike kwa pamoja, sijui hata mlienda wapi"

    Tulishirikiana nao pale kwa kila kitu hadi mwisho wa maziko na kurudi nyumbani kwao ambapo waliweka kikao kifupi cha familia ila mimi na Sam hatukutaka kushiriki kwani sio wanafamilia wao.

    Tulijipanga kuwa baada ya kikao ndio tuwaage rasmi ila kikao kilichelewa kumalizika.



    Baada ya kikao nilifatwa na baba mmoja ambaye ni mwanafamilia akaniambia,

    "Nakupa onyo binti, siku nyingine ukitaka kufanya upuuzi wa aina hii angalia na jina la ukoo. Ukija kama kwangu nakunyongelea mbali"

    Kisha akaondoka, nilimuangalia sana bila ya jibu la aina yoyote ile.

    Ingawa muda ulikuwa umeenda sana ila Sam akanilazimisha kuwa tuage siku hiyo hiyo ili twende mjini na kesho tuanze safari ya kurudi, sikutaka kubishana maana yote tushamaliza tayari.



    Nikamuita mama Amina na kuongea nae mawili matatu kuwa tunataka kuondoka ambapo alisikitika sana na kusema kuwa ameshatuzoea tayari

    "Ingawa asubuhi mliondoka bila kuaga sijui hata mlienda wapi?"

    Tukajigelesha tu pale kwakuwa ni kweli hatukuaga.

    Nikafungua pochi yangu na kutoa baadhi ya pesa na kumpatia, nadhani nilimuachia shilingi milioni moja na nusu maana kwenye pochi niliacha kiasi kidogo tu cha pesa kwani nilijua wazi kuwa pesa iliyobaki ingeweza kutusafirisha mimi na Sam hadi Dar bila ya tatizo lolote.

    Mama Amina alitushukuru sana maana hakutarajia kupata kiasi kile cha pesa, akasema anaenda ndani kuweka ila alikawia sana kutoka sijui alikuwa anazichimbia chini kuficha.

    Alipotoka akajikusanya na baadhi ya wanae na kutusindikiza huku akitupa tahadhari kuwa muda tulioondoka ni mbaya sana ule kwahiyo tuwe makini kwani hata kupata magari ni kubahatisha yale ya mizigo.



    Tulipofika stendi haikuchukua muda sana tukapata gari, kwakweli tuliondoka tukiwa na bahati sana.

    Sam akafurahi na kusema,

    "Bora tumepata gari, hata kama tutafika Kigoma mjini na giza sana ila afadhari kesho tuianze safari ya kurudi Dar hata kwa kuunganisha magari kwakweli nimechoka sana huku"

    Tulikaa kwenye gari bila ya kufika mjini, tukapitiwa na usingizi ndani ya gari.



    Konda ndiye aliyetushtua, kuangalia tulikuwa kwenye basi kubwa la magari ya mkoani.

    Ikabidi nimuulize kondakta,

    "Kwani hapa wapi?"

    "Ubungo hapa, tushafika Dar abiria wote wameshuka kasoro nyie, mnatakiwa kushuka sasa"

    Mimi na Sam tukaangaliana kwa mshangao na kusema kwa pamoja,

    "Ubungo!!"

    Ikabidi tushuke tu, ni kweli tulikuwa Ubungo jijini Dar Es Salaam.





    Mimi na Sam tukaangaliana kwa mshangao na

    kusema kwa pamoja,

    "Ubungo!!"

    Ikabidi tushuke tu, ni kweli tulikuwa Ubungo jijini Dar

    Es Salaam.

    Tuliangaliana pale Ubungo bila ya kujielewa, Sam akaniuliza

    "Tumefikaje hapa Sabrina?"

    "Hata mimi sielewi Sam maana nashangaa tu hapa"

    "Haya sasa tunaelekea wapi?"

    Sam akashauri kuwa anirudishe nyumbani kwetu kwanza ila pale Ubungo palikuwa pametulia kiasi tofauti na mishe mishe za mchana, moja kwa moja tukajua kuwa muda umeenda sana ila Sam akasema,

    "Kwavile muda unaonyesha kuwa umeenda sana, Sabrina basi twende kwenye hoteli tulale halafu kesho asubuhi nikupeleke wewe kwenu kisha mimi nirudi kwetu"

    "Ila sioni sababu ya kufanya hivyo Sam, kwavile pesa ipo kwanini tusichukue tax hapo twende nyumbani tu"

    "Hapana Sabrina, mi naona tutawatisha sana kwenda usiku huu bora tungoje pakuche kwanza"

    "Acha ujinga bhana Sam, hebu tuondoke. Tunavyozidi kulala pamoja ndio tunavyozidi kuingia majaribuni Sam, kheri tuondoke tu"

    Ikabidi Sam akubaliane na mimi kwani huwa hapendi kubishana muda wote, basi tukatoka pale Ubungo nje na kukodi gari ili ianze kutupeleka tunapoishi.

    Tukapanda ile gari na kumuelekeza tunapoenda.



    Safari ikaanza hadi nyumbani kwetu, dereva akataka kulipwa chake.

    Kabla sijashuka nikafungua mkoba ili nimlipe ila mkoba haukua na hata shilingi moja, nikahisi kuchanganyikiwa kwakweli ila kwavile tushfika nyumbani sikuona kama ni tatizo, nikataka kushuka ili nikamchukulie pesa yake ila kabla sijashuka yule dereva akaondoa gari na kusema kuwa tumemfanyia mambo mabaya kumbe hatuna hela, akawa anaendesha gari ilimradi tu.

    Sam akainuka na kuanza kupambana nae ili asimamishe ile gari.

    Alipofika mahali akasimamisha maana ugomvi ulimzidia, Sam akamsema sana yule dereva kuwa ni mpumbavu maana amechukulia hasira tu kuondoa gari kamavile tumesema hatumlipi.

    Ikabidi tushuke eneo lile kisha yule dereva akaondoa gari yake.

    Tukauliza kuwa pesa yote imekwenda wapi maana haikutumika hata kidogo sasa imekwenda wapi? Hakuna aliyeelewa kwakweli, hatukuweza kupata jibu kwa wakati huo kwakweli.



    Wakati tunaulizana tukaangalia na lile eneo tulilokuwepo kwa wakati huo.

    Tukapatwa na mshtuko kwakweli maana tulikuwa baharini.

    Sam akaniuliza tena,

    "Mbona tupo baharini Sabrina?"

    "Sijui, mi mwenyewe"

    "Kila kitu hujui Sabrina kwanini?"

    "Nitajuaje kitu cha ajabu namna hii? Hata wewe mwenyewe hujui ila unataka mimi nijue"

    "Poa tuache mabishano na tuangalie namna ya kutoka hapa baharini"

    Palikuwa na giza kwakweli na ilikuwa ngumu kujua ni wapi tupite ili tuweze kutoka eneo lile.

    Sam akaona ni bora tukae tu pale pale kwenye michanga ili pakikucha tuendelee na safari kuliko kuhangaika kwa usiku huo bila ya kujua tutakapoelekea.

    Nikakubaliana nae na kukaa pale chini.

    Kulikuwa na baridi sana kutokana na maji ya bahari na upepo wake, nilikuwa karibu na Sam nikamsogelea sana naye akanikumbatia, ingawa tulikuwa wenyewe pale baharini ila nilijihisi salama kuwa mahali pale na Sam.

    Sikuwa na shaka lolote sababu Sam yupo na mimi, tukaongea mengi pale baharini ingawa hatukujua kuwa pesa tuliyokuwa nayo imekwenda wapi, nikatamani hata kuitupa pochi yangu ila Sam aliniambia kuwa nisiitupe.

    Kilichotushangaza zaidi tangu tulipoingia Dar hatukuwa na mzigo mwingine wowote zaidi ya ile pochi pekee, nikamuuliza Sam

    "Hivi lile begi dogo liko wapi?"

    "Mmh mi nadhani tumeliacha kule kule Kigoma, ila achana na hayo tufikirie ya muhimu kwasasa mpenzi"

    Nikashtuka na kumuangalia Sam maana ni kipindi kirefu sana tangia ameniita mpenzi ila nikakaa kimya tu kama vile sijamsikia vizuri.

    Tuliendelea kuongea na kujikuta tukipatwa na usingizi pale pale.



    Tulishtuliwa na mtu mmoja alikuwa amevaa nguo nyeupe, kumuangalia vizuri alikuwa ni trafiki hata tukamshangaa ila yeye alikuwa anatushangaa sisi na kutuuliza

    "Mnafanya nini hapa barabarani?"

    Hapo ndipo tuliposhtuka na kuangalia, ni kweli tulikuwa katikati ya barabara ya Morocco tena kuna baadhi ya watu walikuwa wanatushangaa maana tulikuwa tumekumbatiana vile vile kama tulivyokaa kule baharini.

    Tuliinuka kwa aibu sana eneo lile na ilikuwa vigumu kuelewa kuwa tumefikaje hapo, hata maswali ambayo yule trafick aliyotuuliza hatukuweza kumjibu maana hata sisi wenyewe hatukujielewa ila yule trafick aliamua kutuacha tu tuondoke.

    Tuliondoka kwa aibu sana eneo lile, hata tukashindwa kupanda daladala na kuamua kukodi gari huku tukikubaliana na dereva kuwa tutamlipa tutakapofika tunapoenda, hakuwa na tatizo na akasema kuwa ni kawaida ya watu kulipa wanapofika kwahiyo hapakuwa na tatizo.

    Tulipomkumbuka dereva wa usiku tukamshangaa sana maana hakutaka niende kutoa hela ndani wakati mara nyingine wateja hufanya hivyo na ishakuwa kawaida tu.



    Safari ilikuwa vizuri sana hadi tulipofika nyumbani kwetu, hapakuwa na tatizo lolote lile njiani.

    Tulipofika, nikashuka ili nikamuombe mama au dada pesa ya kumlipa dereva ila nikakuta mlango wa nyumba yetu umefungwa, kwakweli hapo nikaishiwa nguvu na kukaa chini kabisa.

    Sam nae akashuka na kunifata, akauliza

    "Kwani vipi Sabrina?"

    "Angalia"

    Nikimuonyesha mlango, naye akachoka kwakweli na kuwaza kuwa tutamlipa nini dereva yule tuliyekuja nae.

    "Mbona majanga haya Sam!"

    "Kweli ni majanga Sabrina, tusipoteze muda basi twende kwetu ili tumlipe huyu dereva Sabrina"

    Ikabidi nikubaliane nae, yule dereva akatuambia kwamba itabidi tumpatie pesa zaidi ya usumbufu

    "Usijali tutakupa"

    Ikaanza safari ya kwenda kwa wakina Sam, huku nikiwaza kuwa endapo tusipowakuta na wao itakuwaje? Nikakosa jibu kwakweli.

    Mawazo yangu hayakuwa mbali na ukweli halisi kwani nako tulikuta mlango umefungwa, Sam akaniambia

    "Sabrina tumeumbuka"

    "Tena tumeumbuka haswaa Sam sijui hata tufanyeje kwakweli"

    Hakuna aliyejua cha kufanya ingawa yule dereva nae alikuwa akisubiria pesa yake.

    Sam alikuwa akicheza na akili yake bila ya majibu, kisha akaniuliza

    "Hivi kule kwenu hakuna jirani wa karibu wa kuweza kutusaidia Sabrina?"

    "Wapo, ila sidhani kama wanaweza kutusaidia kiasi hiki cha pesa ambacho tunadaiwa. Laiti kama ofisi ya kaka isingekuwa mbali tungeenda ila haitawezekana maana gharama itakuwa kubwa sana"

    "Sasa tufanyeje?"

    Sikujua la kufanya kwakweli na nilihisi kuchanganyikiwa, lawama zangu zote zilienda kwa dereva ambaye alitubeba usiku maana muda ule ningepata watu wa kunisidia nyumbani.

    Sam hakuweza kuwaambia jirani zake maana wangetucheka kwa lile swala kwani wangesema kuwa tumekodi vipi gari bila ya kuwa na pesa halafu wasingeweza kutukopesha kiasi kile cha pesa bora kule ambako alikuwa amepanga ila hatukuwa na uhakika wa kuwapata wale wenyeji ambao tuliwazoea.

    Ikabidi tumuombe dereva kuwa aturudishe kule kwa mwanzo ili nikaangalie kuwa pengine mama amesharudi nyumbani.

    Yule dereva alishatuchoka kwakweli na kutuambia,

    "Jamani mnipe hatma yangu kabisa kuhusu hiyo pesa"

    "Usijali kaka, tutakupa elfu hamsini ukiturudisha tafadhari tunakuomba"

    Tulimbembeleza hadi akakubali na kuamua kuturudisha.



    Safari ya kwenda tena nyumbani kwetu ikaanza. Nilitulia kimya kabisa kwenye gari huku nikiwa na mawazo ya kila aina kichwani mwangu, hata sikuelewa kuwa kwanini inakuwa vile.

    Tulipofika nyumbani hali ilikuwa vilevile hadi yule dereva akapandwa na hasira na kutamani hata kupigana na sisi ila Sam akamtuliza kidogo yule dereva kwa kumwambia kuwa asubiri na tutamlipa ya usumbufu ule.



    Tulisubiri kwa muda sana ila hapakuwa na dalili yoyote ya mama wala dada kurudi, nikatamani hata kubadili hii kitu ili iwe ni ndoto ila ilikuwa ni ukweli mtupu.

    Yule dereva alinuka sana na kutuambia,

    "Itabidi mnilipe hela yote niliyotakiwa kuingiza leo"

    Tukaona haya majanga sasa maana hata hiyo pesa tutamlipa kiasi gani.

    Njaa nayo ilituuma sana, Sam akaniambia kuwa inabidi tufanye kitu chochote cha kutusaidia.

    Tukapata wazo la kuvunja mlango kuliko kukaa pale nje bila ya kufanya lolote la kueleweka.

    Sam akasema kuwa atajaribu kulegeza kitasa, ndio hapo alipochukua pochi yangu ili kutafuta kibanio changu cha chuma afungulie.

    Alipofungua nikamshangaa akishtuka, ikabidi nimuulize

    "Mbona umeshtuka Sam?"

    "Angalia Sabrina"

    Nilipotazama tukakuta pesa yote ikiwa ndani ya ule mkoba na kujikuta tukishangaa maana tulijua kuwa tumeshaipoteza ile pesa.

    Sikutaka kupoteza muda, nikatoe ile pesa na kuhesabu kiasi cha shilingi laki tatu na kumpa yule dereva ili aondoke zake maana ilishakuwa kero tayari.

    Yule dereva hakuamini kama tungempa ile pesa kwahiyo akafurahi sana na kutushukuru mara mbili mbili kisha akaondoka.

    Tukabaki wawili sasa yani mimi na Sam tukitafakari haya mambo yalivyo na yanavyokwenda.



    Wakati tupo pale nje nikakumbuka kuwa mara nyingi wakiondoka nyumbani huwa wanaacha funguo pembezoni mwa maua pale nje.

    Lile wazo likafanya niende kupekua pale pembezoni mwa maua na kweli nikakuta funguo kwenye maua, tukajiona wajinga sana yani kuhangaika muda wote ule kumbe funguo zipo pembezoni mwa mauwa kwakweli mambo mengine ni khatari jamani.

    Tukafungua mlango na kuingia ndani, njaa ilikuwa inatuuma sana kwahiyo Sam alipokuwa sebleni mimi nikaenda jikoni kuangalia kama kuna chakula chochote kile ili tuweze kula.

    Nikakuta pilau kwenye hotpot tena pilau la nyama ya kuku nikashangaa sana kuwa walipika muda gani na imekuwa ni ajabu sana, sikutaka kuhoji sana zaidi ya kupakua kile chakula na kwenda kula na Sam.

    Kwakweli kile chakula kilikuwa kitamu sana, tulimsifu mpishi ingawa hatukujua kama alikuwa ni mama au dada.



    Tulipomaliza kula nikachukua ule mkoba na kuanza kuhesabu kiasi cha pesa kilichobaki.

    Nikashtuka kukuta ni milioni tatu vilevile, nikamuuliza Sam

    "Inamaana hatuja tumia pesa kabisa?"

    Hakuwa na jibu maana pesa tulitumia tena sana tu ila kwanini ziwe milioni tatu vilevile? Hapo ndipo penye mashaka na maswali mengi bila ya majibu.

    Tulichoka sana kwa haya mambo kwani yalikuwa ni ajabu kupitiliza.



    Wakati tunashangaa pale tukasikia sauti ya mama na dada wakiongea inamaana walikuwa tayari wamesharudi nyumbani.

    Wakafika moja kwa moja sebleni, kwakweli walifurahi sana kuniona na kunikumbatia kwa furaha huku wakiniangalia vizuri kuwa ni mimi.

    Leo hadi Sam alisalimiwa vizuri, kwakweli walikuwa na furaha sana kisha dada akatuuliza kama tumekula tukamwambia tayari halafu na yeye akaenda jikoni kuchukua chakula kwani alisema kuwa njaa inamuuma sana.



    Wakati anakula akaanza kukisifia chakula kuwa ni kitamu sana, mama akasema kuwa naye apakuliwe ili akionje.

    Dada akampakulia kisha mama nae akaendelea kula huku akikisifia kuwa ni kitamu sana.

    Walipomaliza kula, mama akaniuliza

    "Umetoka nacho wapi hiki chakula?"

    Mimi nikashangaa lile swali na kumjibu kuwa hata mimi nimekikuta ndani,

    "Hata mimi nilitaka kuwauliza kuwa chakula amepika nani maana ni kitamu sana"

    Mama na dada wakanishangaa sana kwa swali lile, kisha dada akainuka na kwenda tena jikoni.

    Aliporudi alikuwa na begi dogo ambalo tulihisi kuwa tumeliacha Kigoma

    "Mbona hili begi mmeliacha jikoni?"

    Mimi na Sam tukaangaliana kisha Sam akasema

    "Kwakweli haya ni maajabu jamani sijapata kuyaona katika maisha yangu, mbona mambo yanakuwa ya ajabu kiasi hiki? Eti Sabrina!"

    Mama akasema na yeye,

    "Ndio mtuambie hayo maajabu na sisi tuyajue jamani"

    Dada nae alikuwa akiendelea kuuliza kuhusu kile chakula

    "Mnachonishangaza mimi ni kusema kuwa chakula mmekikuta ndani wakati sisi hatukupika chakula"

    "Kweli dada, "Kweli dada tumekikuta humu humu ndani"

    Mama akauliza tena kwa hamaki zaidi,

    "Kama mmekikuta humu ndani, nani kapika sasa?"

    Tukasikia sauti ya kiume kutoka chumbani kwangu,

    "Mimi ndio nimekipika"

    Kila mmoja alibaki kaduwaa.



    Tukasikia sauti ya kiume kutoka chumbani kwangu,

    "Mimi ndio nimekipika"

    Kila mmoja alibaki kuduwaa.

    Tukaisikilizia kwa makini kuwa ni ya nani, mama akauliza kwa mshangao na uoga

    "Nani amejibu?"

    Ile sauti ikasikika tena

    "Mimi hapa ndiyo nimejibu"

    Mama akauliza tena huku akitetemeka sasa,

    "Wewe ni nani?"

    Tukasikia kicheko cha nguvu na kufanya tuzidi kuogopa, kisha akajibu tena

    "Mimi ni jini"

    Hakuna aliyepata uwezo wa kuuliza kitu chochote kile cha zaidi maana kila mmoja alikuwa akitetemeka, na ubaya zaidi hatukuweza kukimbia wala kufanya chochote kile.

    Kisha tukasikia mlango wa chumbani kwangu ukifunguliwa na kufungwa bila ya kuonekana mtu yeyote yule zaidi ya hayo mauzauza tu.

    Muda huo huo tukapitiwa na usingizi wa gafla sana na hakuna aliyeelewa kilichoendelea zaidi.



    Nilikuwa wa kwanza kabisa kushtuka toka kwenye ule usingizi wa ajabu, ilionyesha kuwa giza limeshatanda na pale sebleni palishawashwa taa, sikutaka kujihoji zaidi kuwa nani amewasha ile taa zaidi ya kuwaamsha wenzangu ambao bado walikuwa wamelala.

    Kila mmoja aliamka akiwa amechoka sana, walikazana kujinyoosha kana kwamba walilala usingizi wa maana.

    Kila mmoja alikuwa akimuuliza mwenzie kuwa kuna nini? Nadhani walishasahau kasoro mimi mwenyewe ambaye nakumbuka kila kitu ambacho kimetokea.

    Nikatulia pale nione kuwa watasema kitu gani ila hawakuuliza chochote zaidi ya kujishangaa kuwa wamelala sana, mama ndiye aliyeanza kuongea

    "Kweli pilau imetufanya kazi, yani baada ya kula na kulala moja kwa moja mmh!"

    Nikainuka na kwenda jikoni, nilipofika nikashanga kuona kuwa kuna nyama vimeokwa vizuri sana pale jikoni hadi udenda wa tamaa ukanitoka ila nikifikiria ya mchana nikaachana nayo na kurudi sebleni ambako Sam nae alikuwa akiaga kuwa anataka kuondoka ila mama na dada wakamzuia kuondoka kwa mara ya kwanza hadi nikashangaa.

    Dada alikuwa anamwambia Sam,

    "Leo ulale hapa hapa halafu kesho ndio uondoke Sam tafadhari sana tunakuomba"

    Mama nae akamwambia Sam,

    "Ingawa nilikuwa nakuhisi vibaya kwa mwanangu Sabrina ila nakuomba kwa leo ulale hapa kwanza ni usiku tayari, utaondoka kesho tu. Wewe Sam ni kama mtoto wangu tu, leo usiondoke"

    Ikabidi Sam akubaliane nao na kuamua kuwa pale pale nyumbani kwa usiku wa leo, kisha mama na dada wakainuka kwenda kufanya mambo mengine halafu Sam nae akaamua kwenda kuoga maana katika misukosuko yote ile hakuoga yeye wala mimi.



    Nilibaki mwenyewe pale sebleni huku nikijihoji kama niende chumbani kwangu au nibakie pale pale sebleni? Sikuwa na hamu ya kwenda kwenye chumba changu kabisa kwani hisia zangu zinanituma kuwa mauzauza yote yanaanzia chumbani kwangu.

    Nikatulia pale sebleni hadi Sam alipotoka kuoga ndipo nami nikainuka na kwenda kuoga wakati huo dada Penina alitoka kabisa nje ya nyumba sijui alienda wapi.



    Nilipokuwa bafuni nikawaza mambo mengi sana yanayonitokea na kujiuliza kuwa kwanini yananitokea ila sikupata jibu.

    Wakati namalizia kuoga nikahisi kuwa kuna mtu nyuma yangu ananisugua, hofu ikanijaa sana ila kabla sijafanya chochote nikahisi yule mtu amenikumbatia yani niliona mikono yake mbele yangu.

    Nikataka kupiga kelele, akaniziba mdomo kwa nyuma na kuniambia,

    "Sabrina, kumbuka wewe bado ni mke wangu tumefunga ndoa Sabrina, ndugu zangu wote walikuwepo kushuhudia ndoa yetu au umesahau jamani mke wangu?"

    Nilikuwa natetemeka mwili mzima huku nikihofia kufanywa kitu kibaya na yeye, nadhani aliyajua mawazo yangu kisha akaniambia

    "Sitakufanya chochote bila ridhaa yako ndiomana mimi ni jini, nipo tofauti na binadamu wa kawaida kama ambavyo ulitaka katika maisha yako. Hakuna mwanadamu yeyote wa kiume aliyekamilika na kumuacha mtoto mzuri kama wewe akiwa mtupu mbele ya macho yake, lazima angekulazimisha tu ila mimi naridhika ukiwa hivi mbele yangu"

    Moyo ulikuwa ukinienda mbio sana kupita maelezo ya kawaida na mwili wangu ulikuwa ukitetemeka muda wote ila hakulijali hilo zaidi ya kuendelea kuongea anayoyataka yeye

    "Leo mchana niliwaandalia chakula kizuri sana ila nilipowaambia kuwa ni mimi nimeandaa mkaogopa, na usiku wa leo nimewaokea nyama nzuri sana najua mtaipenda"

    Hapo ndipo nikagundua kuwa nyama ile ameitengeneza yeye, akanigeuza ili nitazamane nae macho kwa macho.

    Kwakweli sikuweza kustahimili na kujikuta nikianguka na kupoteza fahamu.



    Niliposhtuka nilikuwa nipo karibu na mama, kichwa changu kipo kwenye miguu yake.

    Nikainuka na kukaa huku nikikumbuka kilichotokea, nikahisi mwili mzima ukisisimka na kutetemeka kwa uoga baada ya kukumbuka yaliyonipata kule bafuni.

    Mama akanipa pole sana,

    "Tumekukuta ukiwa umeanguka bafuni mwanangu, bora leo Sam yupo maana ametusaidia sana. Pole mwanangu"

    "Asante mama"

    Mama akaendelea kuongea,

    "Tulikuozesha kwa mume asiye na maana kabisa maana tangu umeondoka hadi leo hajaja kukuulizia wala nini, tunaishia kuonana nae njiani tu huko tena wala hatusalimii kwakweli najuta kukuozesha mwanangu bila kuchunguza vizuri tabia ya anayetaka kuoa"

    Kwa maneno yale ya mama nikajua anajutia sana ila akiujua ukweli kwa hakika atajutia zaidi.

    Dada Penina naye alikuwepo pale pembeni akasema,

    "Tena wakati naenda dukani nimekutana naye huyo Carlos akija hivi, nikajua anakuja huku"

    Mimi na Sam tukashtuka sana kwani nilijua kuwa tayari tumeshamalizana na yale mambo ya Carlos wala sikujua kama atakuja tena katika maisha yetu, sikujua kama atarudi tena baada ya kumzika kwa mikono yangu mwenyewe. Nikajikuta nikiwauliza,

    "Kwanini lakini?"

    Mama nae akauliza,

    "Kwanini kivipi?"

    "Huyo Carlos mama ataacha lini kusumbua maisha yangu?"

    Nikainama huku machozi yakinitoka kwani nikikumbuka kuhusu kifo cha Carlos niliumia sana, sasa kwanini huyu jini anaendelea kumsumbua huyu marehemu badala ya kumuacha apumzike kwa yote aliyopitia?

    Mama alikuwa akinishangaa kuwa kwanini nalia kiasi kile, ikabidi aniulize

    "Kwani vipi Sabrina?"

    Nami nikaamua kumwambia mama ukweli,

    "Mama, Carlos ni marehemu"

    Mama na dada walishtuka sana, dada akaniuliza kwa makini

    "Sijakuelewa Sabrina unasema!!"

    "Carlos ni marehemu dada"

    Walizidi kushangaa tu maana ni kweli hawakunielewa kabisa, kama dada Penina ndio kabisa hakunielewa ukizingatia anasema kuwa ametoka kuonana na Carlos muda mfupi uliopita kwahiyo swala la kumwambia kuwa Carlos ni marehemu hawakuelewa wala kuamini.

    "Sikuelewi Sabrina hebu niambie vizuri, huyo Carlos ni marehemu kivipi?"

    "Jamani muulizeni hata Sam awaeleze labda ndio mtamuelewa yeye"

    Ikabidi wamuulize Sam ambapo akawajibu hivi,

    "Sidhani kama ni vyema kuzungumzia habari hizo muda huu, hebu tusubiri pakuche jamani"

    Dada alikuwa king'ang'anizi na kutaka kujua ukweli,

    "Tuambie tu Sam ukweli, usitufiche kitu tunahitaji kujua na sisi"

    Sam bado aliendelea na msimamo wake wa kutokuzungumzia chochote kwa muda huo

    "Jamani usiku una mambo mengi sana, habari za kushtusha na kutisha kama hizo si vizuri kuzizungumzia kwa usiku kama huu. Tungoje pakikucha jamani"

    Mama alimuelewa Sam kwa haraka sana ila bado alikuwa na maswali mengi sana dhidi ya yote yale

    "Nimekuelewa sana ila bado nina maswali mengi sana ya kuhoji kuhusu hayo myasemayo maana hapo ndio pagumu kwangu."

    Ikabidi tubadilishe mada kwa muda ule maana ni kweli usiku huwa na mambo sana kushinda tunavyotegemea au kutarajia.



    Dada akauliza kuhusu nyama za jikoni,

    "Jamani na zile nyama jikoni kaandaa nani maana zinanoga hizo balaa"

    Nikamuuliza kwa mshangao,

    "Inamaana umekula dada?"

    "Ndio nimekula kwani kuna tatizo gani?"

    Mama nae akajibu,

    "Hata mimi nimekula, natumaini wewe ndio uliziandaa Sabrina kabla ya kwenda kuoga"

    Niliwaangalia kwa zamu bila kuelewa wanawaza nini na akili zao zikoje maana wanakubaliana na mambo ya kijinga kama vile, niandae nyama mimi nimeitoa wapi? Kweli mama na dada bado wamevurugwa sana hawa.

    Nikawajibu sasa,

    "Ile nyama jikoni sijaandaa mimi ila ameandaa aliyeandaa pilau ya mchana"

    Sam akashtuka sana nadhani alishaelewa kila kitu, kisha akainuka na kusema

    "Jamani naomba mniruhusu niende maana sitaweza tena kukaa hapa"

    Dada akamzuia Sam,

    "Tafadhari Sam usiondoke"

    "Hii nyumba yenu ina mauzauza sana nadhani kama yale tuliyokutana nayo Kigoma. Kwakweli sitaweza kulala hapa, bora nirudi kwetu"

    Ikabidi nianze kumbembeleza Sam ili akubali kubaki na sisi, ila alikubali na kufanya niridhike na kufurahi.

    Dada Penina akauliza tena,

    "Kwani chakula cha mchana alipika nani?"

    Nikaamua kuwajibu tena kwa kifupi

    "Jamani hayo maswali yaishe, tuulizane kesho maana yasije yakatokea mengine ya kutokea tena muda huu"

    Wakakubaliana na mimi, ila Sam hakuweza kula zile nyama na wala mimi sikuweza kula zile nyama.



    Muda wa kulala ulipofika, tukajadiliana namna ya kulala ambapo dada akasema kuwa anaona vyema kama mimi nitaenda kulala kwa mama kisha Sam akalale chumbani kwangu chumba ambacho hata mimi mwenyewe mwenye chumba tangia nifike sijaingia ndani yake je huyo Sam ataweza kulala?

    Nikaamua kupinga hilo swala kwani niliona kuwa si swala jema. Dada akauliza,

    "Sasa unadhani Sam akalale wapi?"

    "Bora alale hapa hapa sebleni"

    "Kwani chumbani kwako kuna nini? Mwache Sam mwenyewe aamue pa kulala"

    Sam nae akakubaliana na mimi kuwa bora alale pale pale sebleni na akasema kuwa hata hivyo hana usingizi kwahiyo kukaa kwake pale sebleni ni vyema sana.

    Mama akaniuliza kuwa na mimi nitaenda kulala wapi maana chumbani kwangu napakataa.

    "Mimi nitalala hapa sebleni au chumbani kwako mama ila sitaki kwenda kulala chumbani kwangu"

    Dada akakumbusha kuhusu kile chakula cha mchana,

    "Mnakumbuka kuwa hata ile mchana tulipouliza chakula kapika nani sauti ikatoka chumbani kwa Sabrina? Ndiomana Sabrina anakikataa chumba chake"

    Hapo nikatambua kwamba kumbe wanakumbuka ila wanajigelesha ili wasiogope zaidi ila hatukuhoji sana zaidi ya kuangaliana tu.

    Dada akaona kamavile tunambabaisha tu kwahiyo akaenda zake chumbani kwake kulala kama kawaida, pale sebleni nikabaki mimi, mama na Sam.

    Nilikuwa namuhurumia Sam kulala mwenyewe pale sebleni ila kwavile mama alinitaka tukalale kwahiyo sikuwa na la kufanya zaidi ya kwenda kulala tu na kumuacha Sam pale sebleni huku nikijua wazi Sam anaogopa sema anajikaza kiume tu kulala pale.

    Tulipofika chumbani haukuchukua muda mrefu usingizi ukanichukua tayari.



    Niliposhtuka asubuhi nikashangaa kujikuta nimelala kwenye kibaraza nje ya nyumba, niliangalia pande zote na kujiona kweli nipo nje.

    Nikainuka kwa uoga ili nikimbilie mlango wa mbele wa nyumba yetu.

    Nilipofika pembezoni mwa nyumba nikamkuta dada Penina akiwa amelala hoi kwenye mchanga, ikabidi nianze kumtingisha na kumuamsha kwakweli alishtuka sana na kutoa mimacho kama mjusi kabanwa na mlango kisha akaniuliza mimi

    "Mbona nimelala nje?"

    "Hata mimi nimejikuta nje sielewi chochote dada"

    Ikabidi ainuke tu pale chini na kujishangaa mara mbili mbili bila ya kupata jibu la maana.

    Tukaingia ndani na kumkuta Sam akiwa amelala hoi pale kwenye kochi, ikanibidi nimuamshe naye alikurupuka tu huku akijiuliza mwenyewe

    "Sijui hata nimelala saa ngapi?"

    Dada akamjibu,

    "Kheri yako wewe usiyejua umelala saa ngapi kuliko wenzio tuliojikuta tumelala nje"

    "Mmelala nje!!"

    "Ndio, mi nimejikuta kwenye kibaraza na dada alikuwa pembeni kwenye michanga huko"

    Hapo hapo tukakumbuka kuwa mama nae yuko wapi? Ikabidi dada aende kumuangalia chumbani kwake, kisha akarudi na sura ya upole sana

    "Mama hayupo chumbani kwake"

    "Yuko wapi sasa?"

    "Sijui"

    Tukaamua kwenda kumuangalia nje kote kuwa labda na yeye amelala nje lakini hakuwepo, tukajikuta tukinyong'onyea sana na kujiuliza kuwa pengine mama nae aliamka na kwenda kututafuta maana pengine alitukosa vyumbani.

    Dada akasema,

    "Kama ni hivyo lazima angemuuliza Sam hapa, asingeweza kujiondokea tu kamavile mtu asiyejielewa"

    Hatukuwa na la kufanya, tukaamua kurudi tu ndani.



    Tulipofika sebleni tukamkva mama amekaa kwenye kochi tena huku akisikitika sana, tukamsalimia na kumuuliza kulikoni yeye kuwa vile.

    "Yani hamuwezi amini, eti nimejikuta nimelala chooni jamani"

    Tukampa pole sana mama na kumsimulia ya kwetu kuwa na sisi tumejikuta tumelala nje, yani kati yetu aliyesalimika ni Sam peke yake.

    Mama hakutaka kupoteza muda, akataka nimueleze kuhusu Carlos kwani wakati amelala huko chooni amepatwa na ndoto mbaya sana.

    Nami sikupenda yale mambo yaendelee kutendeka hivyo basi nikamwambia mama awaite wale ndugu bandia wa Carlos ili niwaeleze wote kwa pamoja kwani sikutaka kusema nusu nusu ili kuepuka yale matatizo yanayojitokeza bila sababu za msingi.

    Mama akawapigia simu nao wakasema kuwa watakuja.



    Mchana wa siku hiyo, wale ndugu bandia wa Carlos waliwasili nyumbani kwetu kisha tukaweka nao kikao kwenye sebule yetu.

    Nikawaeleza kuwa Carlos alishakufa miaka mitano iliyopita na kufanya wote wastaajabu na kushangaa.

    Yule mama bandia wa Carlos akauliza,

    "Sasa yule Carlos aliyekuwa anakuja nyumbani kwetu ni nani?"

    Hapo hapo ikasikika sauti,

    "Ni mimi hapa"

    Kisha akatoka yule jini toka chumbani kwangu na kufanya watu wote waogope.





    Kisha akatoka yule jini toka chumbani kwangu na

    kufanya watu wote waogope.

    Mwili wa yule jini ulitoa mwanga mkali sana uliofanya kila mmoja wetu kujiziba sura yake.

    Kwakweli hali ilikuwa ni mbaya sana maana kila mmoja alishindwa kustahimili, gafla tukasikia kicheko kilichodumu kwa sekunde tano na kutoweka kisha kimya kikatawala ndani ya nyumba.

    Kila mmoja aliogopa kutazama, ni mimi pekee niliyeweza kvoa kiganja changu na kuangalia pale kwenye mlango wa chumba changu ambako kulikuwa kimya kabisa, nikaamu kuwaambia wenzangu

    "Tayari ameondoka"

    Wote wakaangalia, kisha kila mmoja akakimbilia nje ya nyumba kwani hawakuweza tena kukaa mule ndani.

    Ni mimi tu niliyesimama na kuwaangalia wanavyopambana kukimbilia nje.

    Wote walitoka nje kasoro mimi kwani najua hata kama nikienda nje ni kazi bure kwamaana yule jini yupo kila upande katika maisha yangu.

    Nikiwa nimesimama tu bila ya kufanya chochote kile, akaja Sam na kunishika mkono kisha akanivutia nje na kuanza kunisema

    "Una nini wewe Sabrina?"

    "Kwani nina nini?"

    "Unajua wazi kuwa ndani kwenu kuna majanga halafu wewe unang'ang'ania ndani, tatizo ni nini wewe?"

    "Sina tatizo Sam ila najua tu kwamba hakuna pa kukimbilia, kazi ni bure tu"

    Wale ndugu bandia wa Carlos walikuwa wakijilalamisha tu pale nje huku wakisema kuwa yale mambo ni makubwa, wakadai kwamba hawataweza kuendelea kuwepo eneo lile zaidi ya kuondoka tu.

    Wakaanza kuondoka huku sisi wahusika wa nyumba yetu tukiwa pale nje bila ya uelekeo wa aina yoyote ile.



    Wakati wanaondoka ikawa ni kitendo cha kufumba na kufumbua kwani wote tulijikuta tukiwa ndani tena.

    Kila mmoja alizidi kustaajabu na kutetemeka huku wakishangaa, mama bandia wa Carlos akauliza

    "Tumerudi vipi tena humu ndani?"

    Hakuna aliyekuwa na jibu la aina yoyote ile, kila mmoja alikuwa akitetemeka.

    Wakajaribu tena kukimbilia mlango lakini haukufunguka ukawa kamavile mlango uliyojifunga wenyewe.

    Wakaanza kutafuta juhudi za kuweza kutoka nje ya nyumba ila Sam akawaambia kuwa watulie tu kila kitu kitaenda salama,

    "Tutulie vipi na hali kama hii?"

    "Tulieni tu, kila kitu kitakwenda vizuri kama tukitulia ila kwa fujo hatutafanikiwa kabisa"

    Ikabidi wote watulie pale ndani, hakuna kilichosikika wala hakuna aliyemwongelesha mwenzie tulitulia kabisa.

    Gafla tukapitiwa na usingizi wote pale ndani.



    Wakati nimelala ule usingizi mzito, nikajiwa na ndoto ya yule mbaba ambaye aliwahi kufika kwetu na kutaka kunisaidia ila akasema kuwa kwavile matatizo yangu yapo kwenye ndoto basi yataishia kwenye ndoto.

    Kisha akatokea yule jini na kuniuliza

    "Unafikiri matatizo yako yataisha?"

    Nikamuangalia bila ya kusema chochote, kisha akaniambia tena

    "Hayawezi kuisha hadi pale utakapoamua kuondoka na mimi, kumbuka kuwa wewe ni mke wangu tayari"

    Nikamjibu sasa,

    "Lakini ulinipa machaguzi mawili na ulisema kuwa nikifanikiwa utaniacha huru ila nashangaa unaponiambia kuwa hadi nikubali kuondoka na wewe"

    "Kwasababu nikikuacha utachukuliwa na mwanadamu mwenzio ndiomana sitaki kukuacha Sabrina, siwezi kushea na mwanadamu. Wewe ni wangu Sabrina ni wangu peke yako, uhuru wa familia yako ni wewe kukubali kwenda na mimi nitakupa pesa, dhahabu na chochote unachotaka katika ulimwengu huu"

    Kisha akatoweka na kutokea Carlos sasa na kuniambia

    "Pole sana Sabrina"

    Na kupotea kabisa, nikashtuka toka kwenye ule usingizi nikajikuta nipo nje ya nyumba yetu nikishangaa shangaa tu ila Sam alikuwa pembeni yangu nikamshtua naye akashtua.

    Nikamtaka turudi ndani ila Sam alikataa na kuniomba tuondoke hapo nyumbani

    "Mama na dada je?"

    "Wakishtuka nao watajua cha kufanya ila sisi tuondoke kwanza"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Sam akaniangalia kidoleni, leo akaniona na ile pete ya uchumba niliyowahi kuvishwa na Carlos kisha Sam akanivua nayo ikavuka halafu akairushia pale nyumbani kwetu na tukaondoka.

    Nikamuuliza Sam,

    "Tutaenda wapi sasa?"

    "Nitajie kwa ndugu yako ambako unaona ni salama zaidi kwako"

    "Labda kwa kaka Deo"

    "Basi ngoja nikupeleke, na kukuacha huko kisha mimi nirudi kwetu"

    "Mbona unajiamini hivyo Sam?"

    "Bila kujiamini hakitafanyika kitu chochote Sabrina"

    Tukapitia kwa rafiki yake Sam ambapo alimuomba kiasi kidogo cha pesa na kuondoka eneo lile.

    Nikamuuliza tena Sam,

    "Hivi ile siku tunahangaika cha kumlipa dereva tax kwanini hukukumbuka kuhusu rafiki yako huyu?"

    "Hata mi mwenyewe nashangaa Sabrina, kwakweli tulivurugwa ila Mungu atatusaidia"

    Tukaanza safari ya kwenda kwa kaka Deo huku nikiwaza kuwa nitamkuta nani maana sijapata taarifa zao zozote tangu lile sokomoko la wifi kuumbuliwa kuhusu mtoto James maana kaka aliondoka kwa hasira halafu wifi nae aliondoka na kufatwa na Carlos kwa nyuma sasa watakuwepo kweli? Namjua kaka yangu Deo alivyo na hasira, sidhani kama ni rahisi kwa yeye kuwa nyumbani kwake na ubaya zaidi sijawahi kumuuliza mama wala dada kuhusu kaka Deo na wifi Joy kuwa waliishia wapi.

    Kwakweli sikuelewa kama tutawakuta na je kama tusipowakuta nitaenda wapi? Sikvaka kwenda kwa ndugu yoyote na mauzauza haya niliyonayo, muda wote nilikuwa na mawazo tu hata Sam alilitambua hilo na kunipa moyo kuwa nisiwaze sana

    "Acha mawazo hayo Sabrina, amini kila kitu kitaenda salama"

    Nikatuliza mawazo na kuendelea na ile safari.



    Kufika nyumbani kwa kaka kulikuwa na kufuli kwenye geti lao moja kwa moja nikajua kuwa hawapo na kumwambia Sam.

    "Unaona nilichokuwa nawaza sasa! Hawapo"

    "Haina tatizo Sabrina, twende ukakae kwetu kwa muda"

    "Nani aende kukaa kwenu Sam? Hata kwa fimbo hunipeleki, kumbuka ndugu zako hawataki hata kuniona. Nilienda siku ile sababu ya shida tu ila kwasasa bora nirudi nyumbani tu"

    Sam akaniangalia kwa upole sana na kujaribu kunibembeleza kuwa bora kwao kuna usalama kuliko nyumbani kwetu ila mimi nilikataa kabisa swala la kwenda tena kwa wakina Sam na kuona kuwa ni vyema nirudi nyumbani tu.

    Mimi na Sam tukaamua kuondoka ila Sam akaniomba nimsindikize mahali kabla ya kwenda kwetu nami nikakubali ila sikujua anataka nimsindikize wapi.



    Tukiwa njiani kuna gari ikasimama mbele yetu kisha akashuka mdada, kumuangalia vizuri alikuwa ni wifi Joy aliyekuja na kunikumbatia kwa furaha huku machozi yakimtoka, nami nikamkumbatia wifi yangu huyu ambaye alikuwa akitokwa na machozi tu. Huku akisema,

    "Nafurahi kukuona Sabrina faraja yangu"

    Nikashangaa kwa yote yale yaliyotokea lakini bado wifi Joy alionyesha kunipenda sana kama ambavyo alikuwa akinipenda kabla.

    Alikuwa akiniuliza huku machozi yakimtoka,

    "Unaendeleaje mdogo wangu Sabrina?"

    Nikakumbuka kuwa wifi alikuwa na mtoto mdogo James, ikabidi nimuulize

    "James mdogo yuko wapi?"

    "Yupo kweli ile gari dogo"

    Kwavile dereva alianza kupiga honi ikabidi wifi akamtoe yule mtoto maana ile gari ilikuwa ya kukodi kisha dereva akaondoka zake.

    Wifi alionekana kuchoka sana hivyo nikamsaidia yule James mdogo, na kumuuliza

    "Dereva ulishamlipa yule?"

    "Nitamlipa na nini wifi yangu? Kanipa lifti tu kwa huruma yake"

    Basi akaomba tuongozane na kurudi tena kwenye nyumba yao.

    Nikajiuliza na kugundua kuwa wifi bado hajarudiana na kaka ndiomana yupo katika hali kama ile ya kulalamika kuwa anakosa hata pesa ya kukodi gari.



    Tulipofika, ikabidi Sam nae asiondoke tena ili ajue kuwa mambo yangu yataishia wapi ila mimi nikamuomba aende kwani nitakuwa salama nikiwa na wifi Joy mahali pale, pia nilitaka wifi Joy awe huru kunieleza chochote anachojisikia bila uoga wala aibu.

    Kwahiyo Sam akatuaga pale na kuondoka zake.

    Nikabaki na wifi sasa huku nikiwa na nia moja tu ya kujua ni nini kilimpata,

    "Kwanza pole sana wifi yangu kwa yote yaliyotokea, najua mimi

    ndio chanzo cha yote wifi yangu"

    "Usijali Sabrina, wewe sio chanzo ila kila jambo hutokea kwa sababu maalumu"

    "Kama ipi?"

    "Yale yote ni funzo kwangu, kwani nimejifunza kuwa kuna mambo hayatakiwi kuwa siri milele na pia kuna baadhi ya watu wa muhimu hawatakiwi kufichwa. Mume wangu Deo alikuwa ananiamini sana, laiti kama ningemwambia hili jambo mapema basi isingekuwa hivi maana jambo linalokuhusu ukiambiwa na mtu mwingine huwa linaumiza sana. Kwakweli nimejifunza mengi, sitarudia tena kumficha mume wangu mambo kama haya maana nimeteseka sana"

    "Pole sana wifi, kwanza niambie ilikuwaje tangu siku ile na je kwasasa mambo yakoje?"

    Wifi yangu alionekana kutokwa na machozi tu muda wote, kisha akanieleza

    "Kwanza napenda wote mtambue kwamba sikufanya kusudi kubeba mimba ya mtu mwingine tofauti na mume wangu"

    "Naelewa wifi"

    Wifi Joy akaanza kunisimulia ilivyokuwa.



    "Hakuna siku niliyoaibika kama siku ile, nilipata aibu ya miaka aibu ambayo sikuitarajia kabisa. Baada ya Deo kuondoka na kuniacha mahali pale kisha na mimi kuondoka huku nikifatwa na yule mtu wako wa ajabu ambaye alikazana kuniambia kuwa atanisaidia.

    Kwanza nilitamani kukubali msaada wake ila moyo wangu ukanikumbusha neno kuwa huwezi kutumikia mabwana wawili yani huwezi kumtumikia Mungu na shetani kwa muda mmoja, nikaona wazi kuwa yule mtu wako wa ajabu ni mfano wa shetani na sikutaka kumpa nafasi katika maisha yangu. Nikakumbuka neno lingine likisema kuwa shika sana ulichonacho mwovu asikitwae, nikaamua kumuelekezea Mungu matatizo yangu kwani najua atanijibu tu.

    Nilirudi hapa nyumbani huku ninalia, ila Deo hakutaka kuniona kabisa yani akanifukuza kama mbwa na kusema kuwa hayupo tayari kulea mwanaharamu, moyo uliniuma sana ila Deo hakutaka kuniona kabisa ikabidi nirudi kwetu huku nikiwa na maumivu moyoni.

    Nyumbani nako baada ya kuwaeleza kisa kizima hawakutaka kuniona, wakanifukuza tena, nimehangaika sana na huyu mtoto mdogo James.

    Sikuwa na pakwenda, kesho yake nikarudi tena hapa kwa Deo nikakuta kaniachia ujumbe kuwa amesafiri na hategemei kurudi leo wala kesho, ujumbe wenyewe niliukuta hapo chini ya geti.

    Sikuwa na pakwenda zaidi ya kulia, nikaona sina msaada zaidi ya kurudi nyumbani kwenu ila Penina akanifukuza. Wakati naondoka pale kwenu nikakutana na huu msaada, nikakutana na mdada mmoja aliyejitambulisha kwangu kwa jina la Zuhura, akanihurumia sana na kunipeleka kwao kisha nikamueleza kila kitu kilichonisibu.

    Akaona kwao hapatanifaa kuishi, nikaenda nae kwake, ana kipato cha kawaida ila ni mtu mmoja mwenye roho nzuri sana, akanieleza kuwa anaitambua familia yenu yote. Amekuwa akinihudumia hizi siku zote bila hata ya kulalamika ingawa mtoto James amekuwa akisumbua sana, alikuwa ananisisitiza kufanya ibada na kunipa moyo kila siku kuwa nisijali Mwenyezi Mungu atanifanyia wepesi. Amekuwa rafiki yangu tena ni zaidi hata ya ndugu yangu, ana roho ya kipekee na moyo wa upendo, nikampenda sana na nimeishi nae vizuri bila hata ya kujari tofauti ya dini zetu. Amekuwa mtu wa pekee kwangu, huku akinikumbusha kufanya ibada tu kwakweli anafaa kuigwa na jamii nzima nimeishi nae vizuri sana.



    Kuna kipindi nilikuwa nasikiliza semina ya neno la Mungu kwenye redio, somo lilikuwa linasisitiza kuwa na imani na yote yanawezekana. Zuhura nae akanisisitiza hivyo, sikuacha kuomba, sikuacha kujutia dhambi zangu, sikuacha kumuita Mungu katika maisha yangu.

    Mtoto James alipotusumbua sana, Zuhura akashauri twende hospitali ila mtoto hakuwa na tatizo ila tatizo nilikuwa nalo mimi. Nilimbebea mimba, kipindi naondoka kwa Deo nilikuwa na mimba changa yani hapa nilipo mimi ni mjamzito nina mimba ya kaka yako Sabrina.

    Nilifurahia ile habari ila nilinywea gafla nikikumbuka kuwa Deo kaniacha ila Zuhura amenifunza kuwa na matumaini siku zote na kutokukata tamaa.

    Niliendelea kufanya ibada bila ya kupata mawasiliano yoyote toka kwa ndugu, jamaa wala Deo ila jana usiku ikawa kama muujiza nilipopigiwa simu na Deo kuwa nije leo na yeye anarudi.

    Sikutaka kumsumbua sana Zuhura maana anatuhudumia vya kutosha, ndiomana nikachukua nauli tu na kuja huku.

    Ingawa geti limefungwa ila naimani Deo atarudi kweli kama alivyoniambia"

    Wifi Joy alimaliza huku akijifuta machozi, nilimuangalia kwa huruma sana nikamsogelea na kumkumbatia huku nikifurahia imani yake na kumshinda yule jini kwani angetumia nafasi hiyo kuteka akili zake kama ambavyo ameteka akili zangu na familia yangu. Nikamjua Zuhura anayemzungumzia ni yule dada ambaye hupenda kunisaidia mara nyingi, anastahili sifa kwakweli.



    Muda haukukawia sana kaka Deo akawasili na kutukuta pale nje, alishuka na kutukumbatia kwa furaha sana kisha akafungua geti lake na kuingiza gari lake ndani.

    Ilikuwa ni furaha sana, alimbeba yule mtoto James na kusema kuwa amemkumbuka sana kisha akaniangalia mimi na kusema neno kama vile anauliza swali

    "Kitanda hakizai haramu, eti mdogo wangu eeh!!"

    Nilimuitikia kwa kichwa kwani sikujua kuwa ile ni furaha kweli au ana mambo mengine tu kaka yangu huyu.

    Ila alikuwa amefurahi sana huku akimuuliza wifi za siku nyingi na maswali mengine mengi mengi na kumpa pole pia.

    Nilifurahi sana ila nilitaka kuwaacha waongee kwa uhuru zaidi, nikaamua kuwaaga kuwa naenda dukani mara moja. Wifi akainuka na kunishika mkono kisha akaniambia

    "Mtegemee Mungu katika kila kitu mdogo wangu"

    Nikaitikia kwa kichwa na kuondoka.



    Nikatoka nje na kujiuliza kuwa huko dukani naenda kufanya nini? Hapo nikapata wazo la kurudi ndani tu.

    Ila kabla sijarudi ndani nikashangaa nikiwa kando kando ya bahari na mbele yangu alikuwepo yule jini.





    Nikatoka nje na kujiuliza kuwa huko dukani naenda

    kufanya nini? Hapo nikapata wazo la kurudi ndani tu.

    Ila kabla sijarudi ndani nikashangaa nikiwa kando

    kando ya bahari na mbele yangu alikuwepo yule jini.

    Nikakodoa macho bila kujielewa, yule jini alikuwa akicheka tu na kuniambia

    "Niambie Sabrina unajisikiaje? Tupo pamoja tena mke wangu"

    Akanyoosha mkono wake na kunishika, nilikuwa natetemeka muda wote kama mtu mwenye degedege vile na sikujua la kufanya kabisa sikujua kama naweza kupona kwenye mikono ya jini huyu.

    Aliendelea kuongea huku akiniangalia machoni, macho yake hayakuwa sawa na binadamu wa kawaida yalikuwa ni makali na yanacheza cheza sana kitu ambacho kilifanya nizidi kuogopa,

    "Nimeshakwambia unizoee Sabrina, kwanini unaendelea kuniogopa? Ngoja nikuulize swali jepesi kabisa, kati ya mama yako na Sam unampenda nani?"

    Nikabaki kimya, akaniuliza tena

    "Swali gumu?"

    Nikaendelea kuwa kimya,

    "Nakuuliza Sabrina, kati ya mama yako na Sam unampenda nani? Nahitaji jibu, ukishindwa kunijibu inamaana hakuna unayempenda kati yao basi ni mimi tu unipendaye"

    Hapo nikamjibu,

    "Sikupendi wewe"

    "Basi niambie kati ya mama yako na Sam unampenda nani?"

    "Nawapenda wote"

    "Kuna mmoja unampenda zaidi, nitajie ili nikuonyeshe kitu"

    Huu ukawa ni mtihani kwangu kwani sikuelewa nijibu kitu gani na sikujua huyu jini ana lengo gani? Nikakaa kimya tena,

    "Nimekwambia kama huna jibu basi unanipenda mimi"

    "Sikupendi wewe"

    Akanyoosha mikono yake, akaniambia niitazame.

    Kwenye viganja vyake kulikuwa na sura kama kwenye kioo, kiganja cha kuume ilikuwepo sura ya Sam na kiganja cha kushoto kilikuwa na sura ya mama yangu kisha akaniambia nichague mmoja.

    Sikutaka kuchagua kwavile sikujua atamfanya nini na huyo nitakayemuacha naye atamfanya nini, ikabidi niendelee kuwa kimya tu akaniuliza

    "Umekataa kuchagua kwahiyo nikuchagulie mimi?"

    Nikatingisha kichwa kukataa, akanilazimisha kuchagua ila bado sikuweza kuchagua yeyote kati yao kisha akasema kuwa yeye ndiye atakayenichagulia kati ya wale wawili ambao mimi nimeshindwa kuchagua kisha akatoweka mbele yangu, nikatetemeka sana na kujikuta nikikaa pale chini huku nikijiuliza maswali bila majibu ya aina yoyote, nilijiuliza mwisho wa haya mambo utakuwaje na ni lini? Je yataisha kweli?

    Niliwaza sana bila ya majibu, giza likaanza kuingia na hapakuwa na mtu wa aina yoyote eneo lile yani ni mimi tu na machozi yangu.

    Wakati nawaza sana yule jini akatokea tena na kuniuliza,

    "Umeshindwa kuchagua Sabrina?"

    Nikashtuka kwani sikumuona vizuri wakati anakuja, nikakaa kimya bila ya kumjibu akaniambia

    "Nimekuchagulia Sabrina, huyu hapa"

    Akanionyesha kiganja chake cha mkono wa kuume ambacho kilikuwa na sura ya Sam kisha akaniambia

    "Nimeona nikuchagulie huyu maana hata akipotea utampata mwingine tu"

    Nikamshikilia mkono na kumuomba asimdhuru Sam, nilimuomba sana lakini akatoweka huku akicheka.

    Nilibaki mwenyewe huku ninalia tu bila ya kuelewa nifanye nini kumsaidia Sam kama yupo kwenye matatizo.



    Wakati nalia, gafla nikamuona mtu kama Sam akielekea kwenye maji ya bahari.

    Alikuwa akitembea kwenye maji tena bila hata ya wasiwasi, nikamuangalia vizuri na kumuita kwa nguvu

    "Saaaaaaam"

    Akasimama akiwa kwenye maji ila hakugeuka nyuma wala nini, ikabidi na mimi nijitose kwenye maji ya bahari na kumfata huku nikizidi kumuita.

    Nilipofika karibu nikanyoosha mkono ili kumshika lakini akatoweka mbele yangu, nikaogopa sana na kushtuka kwani sikutarajia kile kitu kabisa.

    Sam hakuwepo kabisa mbele yangu, nikahisi kuchanganyikiwa kabisa na nilikuwa kwenye maji nikatamani kukimbia ila lazima nitaanguka kwenye yale maji na kutembea na uoga ule mbona nitakufa kabisa.

    Nikageuka nyuma, gafla nikahisi kuna mtu amenishika mgongoni, kwa uoga nikaanza kukimbia na kama nilivyowaza kweli nikaanguka kwenye maji na kuyaona kuwa ni mengi sana.

    Nikashindwa kuogelea kwenye maji yale wakati kutembea niliweza, nikaona kifo kimenukia kwangu kwani maji yale yaliziba pua yangu na kufanya nishindwe kupumua na kujikuta nikiyanywa mdomoni na mwili wote kukosa nguvu na ikawa mwisho wa kujielewa.



    Nikajiona nipo katikati ya watu wengi sana wakinishangilia kwa kupiga makofi, uoga ukanijaa na kujiuliza kuwa nipo mbinguni au ndio kuzimu? Wale watu walikuwa wa ajabu sana yani tofauti na binadamu wa kawaida, sura zao zilitaka kufanana na sura za wanyama halafu walikuwa na rangi za ajabu yani hawakuwepo katika muonekano wa kawaida kabisa na kufanya niogope.

    Akanisogelea mmoja na kunipa ishara ya kusimama kisha nami nikasimama halafu akanipa ishara ya kuweza kumfata kwa nyuma, nami nilikuwa kama roboti nikimfata kwa nyuma.

    Niliongozana nae hadi mahali ambako kulikuwa kama na ukingo, mbele yake kulikuwa na kitu kama kioo ila ni kikubwa sana kwani sikuweza kukiona mwisho wake.

    Akanionyeshea ishara kuwa nipite pale, lakini kabla sijapita nikamuona baba yangu mzazi mbele ambaye ni marehemu wa miaka mingi iliyopita, nikashtuka sana ila nikataka kupita pale na kumfuata ila yeye akaonyesha ishara ya kunikataza na kunionyesha kuwa nirudi nyuma kisha akatokea na Carlos kule kule mbele ambaye nae alinionyesha ishara ya kurudi nyuma, ila yule mtu aliyekuwa akiniongoza kuwa nimfate, aliendelea kuniamuru kuwa nipite pale kwenye kile kioo.

    Nikashindwa cha kufanya na kuamua kupita, ile naweka mguu tu nikashtukia nikiporomoka kama maji kwenye mlima kumbe kile hakikuwa kioo bali ni sehemu iliyowazi.

    Nikapiga makelele sana kwani chini kulikuwa mbali na kunatisha, ila kabla sijafika chini nikadakwa na watu wawili ambao walikuwa ni baba na Carlos, hawakuniongelesha chochote ila walinirushia juu ili nirudi nilipotoka.



    Nikashtuka na kukohoa sana, pembeni yangu alikuwepo Sam ambaye alikuwa akinipulizia pumzi mdomoni.

    Alifurahi sana kuniona nimeshtuka ila nilikuwa sijielewi kabisa, Sam alinipa pole sana ikabidi nimuulize kuwa ilikuwaje kwani

    "Ulizama Sabrina, kwakweli Mungu mkubwa na anakupenda sana sikujua kama utapona kabisa"

    "Imekuwaje? Hebu nieleze vizuri Sam maana sielewi, nimefikaje huku pembezoni mwa bahari?"

    "Sijui umefikaje ila hata mimi mwenyewe nimefika kimiujiza kwakweli Sabrina"

    "Hebu nieleze Sam tafadhari ili niweze kukumbuka"

    Sam akaanza kunieleza na kufanya nirudishe kumbukumbu zangu nyuma na kugundua kuwa nilizama kwenye maji ya bahari, nadhani vyote hivi ni mbinu za yule jini katika kuniangamiza tu.

    Nilitulia na kumsikiliza Sam kwa makini kabisa, alianza kunieleza hivi

    "Mara ya mwisho kabisa nimekuacha ukiwa unazungumza na wifi yako kisha nikakuaga kuwa naenda nyumbani ila sikwenda nyumbani, kuna rafiki yangu mmoja hivi ndio nilienda nyumbani kwake.

    Muda ulipoenda nikaona ni vyema kuja kuangalia kama kaka yako amerudi na uko salama, nilipofika nilikuta geti liko wazi na kuingia ila nikakuta kama kuna mabishano kidogo kati ya wifi yako na kaka yako ila yale hayakunihusu kwahiyo nikafanya kilichonihusu ambapo nilikuulizia wewe.

    Wifi yako akanipa maelekezo kuwa umeenda dukani, ila roho yangu haikuwa tayari kukubali kuwa huko dukani upo salama kweli. Nilimweleza kwa kifupi wifi yako kuhusu mambo yaliyotokea kwenu akasema ni nguvu za giza na kusema kuwa atajitahidi kupeleka wanamaombi kwenu ili wakemee nyumba yenu kwa pamoja. Kisha nikawaaga ili niweze kwenda kukuangalia mwenyewe huko dukani, nilipofika nje nikakumbuka kuwa sijaulizia ni duka gani hivyo nikataka kurudi ndani nikaulizie ila kabla sijarudi nikajishangaa kujikuta ufukweni. Kwakweli nikakumbuka mauzauza yote ya Kigoma na yale ya nyumbani kwenu, akili yangu ikaniambia kuwa mauzauza bado yanaendelea tu.

    Nikamuomba Mungu aniepushe na haya, kwakweli sikujielewa kabisa.

    Wakati natembea tembea nikaona kuna mtu anatapatapa kwenye maji hivyo nikaamua kujitosa ili niweze kumuokoa.

    Nilipofanikiwa kufika kwenye mchanga ndio nikagundua kuwa ni wewe, ulikuwa na hali mbaya sana hadi nikapata hofu kuwa inawezekana usipone ila nikajipa moyo na kujaribu kukupulizia hewa na kukuminya tumbo ili maji yatoke.

    Hali yako ilikuwa mbaya kwakweli haswaa kwa sehemu hii isiyokuwa na mawasiliano, nashukuru umezinduka Sabrina"

    Nikamuelezea Sam sababu ya mimi kuzama, akashangaa sana nilipomwambia kuwa kuna Sam mwingine alitokea na nikamfata ndio nikazama.



    Sam akanishika mikono na kuniambia kuwa tunatakiwa kufanya maombi, ila kabla hatujafanya chochote akatokea yule jini pembeni yetu na kuachanisha mikono yetu.

    Tulibaki tukimuangalia tu bila ya kumwambia chochote, akanyoosha mkono wake kisha akatushika vichwa vyetu na kuvigonganisha pamoja, tulijikuta na maumivu makali sana na kuzimia.



    Nilikuwa wa kwanza kuzinduka na kushangaa kwani tulikuwa nyumbani tena ndani ya nyumba yetu, nikamshtua Sam ambaye alishtuka kamavile mtu anayekimbizwa na kuniuliza kwa mshangao

    "Tupo wapi?"

    "Nyumbani kwetu"

    "Tumefikaje?"

    "Sijui kwakweli, labda...."

    Akanikatisha nilichotaka kusema na kisha akaniambia,

    "Tusiongee sana, tunaweza kujikuta Kigoma hapa"

    Nikatulia kwani nikikumbuka ile misukosuko sikutaka ijirudie tena.

    Sikujua cha kufanya, tulitulia pale sebleni tu.

    Nikapata wazo la kwenda kuwatafuta mama na dada ili nijue wapo sehemu gani ndani ya nyumba ila nikaogopa kuwatafuta mwenyewe na kumuomba Sam kuwa tusindikizane.

    Sam akainuka na kuongozana na mimi kuwaangalia sehemu zote ila hakuwepo mama wala dada, tukajaribu kwenda kufungua na mlango wa nje ila haukufunguka kwamaana hiyo hatukutakiwa kutoka nje.

    Nikamuuliza Sam,

    "Tutafanyaje sasa?"

    Ila Sam alikuwa akiniangalia sana mkononi hadi nikamuuliza kuwa kwanini ananiangalia vile, nikainua mikono yangu na kujitazama ila yeye akaniuliza.

    "Hiyo pete si nilikuvua wewe?"

    Nilikuwa na ile pete ya uchumba kwenye kidole changu

    "Hata mimi mwenyewe nashangaa"

    "Tena niliitupa kabisa, imekuwaje umeivaa tena? Pete ina majanga sana hiyo"

    Nikajiangalia vizuri na kujisikitikia na ile pete kisha tukarudi sebleni na kukaa tena maana hatukujua cha kufanya.



    Wakati tumekaa bila kujielewa, tukamuona mama nae ameletwa mbele yetu halafu na yeye mwenyewe alikuwa akijishangaa wala hakuelewa chochote kisha akaniangalia mimi na kunishangaa sana. Akanisogelea na kuniuliza kuwa nilikuwa wapi, ikabidi na mimi nimuulize yeye kuwa alikuwa wapi.

    "Unafikiri naelewa basi, sijui nililala! Sijui hata nilikuwa wapi ila nimeshangaa tu kuwaona nyie mkiwa mbele yangu"

    Nikamuangalia mama kwa huruma kwani hakutakiwa kuteseka kwa makosa yangu, mimi ndio mwenye haki ya kuteseka sababu chanzo cha mambo yote haya ni mimi.

    Nikampa pole mama kwa kutokujielewa ambapo alikuwa akiongea kwa uchungu.



    Tulipokuwa tunaongea na mama, tukamuona dada Penina akiwa pale alipokaa mama mwanzoni naye alikuwa hajielewi kabisa maana alikuwa akishangaa shangaa tu na gafla akakimbilia tulipokaa sisi na kuwa kama mtu aliyewehuka, ikabidi tumtulize kwanza ili akae sawa.

    Baada ya muda akasema,

    "Maajabu gani haya? Sabrina umetuletea makubwa jamani"

    Sam akanitetea,

    "Tusimlaumu sana Sabrina maana hata na yeye hajapanga iwe hivi. Hali inamtesa sana hii yatupasa kushikamana ili tuweze kushinda"

    Kisha dada Penina akauliza,

    "Inawezekana kushindana na jini kweli?"

    Sam akajibu kwa unyonge,

    "Tutaweza tu dada"

    "Yani sisi binadamu wa kawaida tunaweza kushindana na jini kweli? Jini mwenye uwezo wa kufanya choch ote atakacho, akiamua kutulaza nje, chooni na popote pale anaweza leo hii tuseme kuwa tutashindana nae kweli?"

    Nikakumbuka maneno aliyoniambia wifi Joy kuwa nimtegemee Mungu kwa kila jambo na niamini kuwa inawezekana, nikaamua kuwaambia

    "Jamani tumtegemee Mungu kwa kila jambo"

    Sam naye akanisapoti kwa hili

    "Ndio, Mungu ni kila kitu katika maisha yetu tunapaswa kumtegemea yeye kwani hata hao majini wapo chini yake"

    Yale maneno yalionekana kuwaingia sana dada na mama na kuwafanya waulizie zaidi ikawa bado walikuwa wamejawa na mashaka na uoga mwingi.



    Tukaamua kujipanga sasa namna ya kufanya ili kupambana na hili, tukainuka na kuweka duara ila kabla ya kufanya chochote zaidi yule jini alikuwa katikati ya duara letu na kufanya wote tushikwe na uoga na kuanza kutetemeka.

    Akatufanya wote tukae na kumsikiliza yeye, akaanza kuongea

    "Nimewaleta hapa ili muwe pamoja sio muanze kufanya ujinga wenu"

    Tukamuangalia tu huku tukitetemeka kwani hapakuwa na yeyote mwenye uwezo wa kufanya chochote na kufanya huyu jini azidi kujitapa mbele yatu.

    Akaenda kukaa na kusema,

    "Si mmeamua kupambana na mimi? Tupambane sasa ila nikiwashinda mtakuwa watumwa wangu maisha yenu yote"

    Akanyoosha mikono yake kwetu, gafla tukaanza kuwashwa yani kamavile tumemwagiwa upupu.



    Akanyoosha mikono yake kwetu, gafla tukaanza

    kuwashwa yani kamavile tumemwagiwa upupu.

    Tulijikuna sana hadi kukosa raha huku yeye akituangalia na kucheka, kisha akatunyooshea tena mkono na muda huo huo muwasho ukakatika, akatuangalia vizuri na kusema,

    "Nyie si mmejitoa kupambana na mimi, nani kati yetu yupo tayari kwa mapambano zaidi?"

    Wote tukakaa kimya, naye akaendelea kusema

    "Kwamaana hiyo hakuna wa kumbambana na mimi, ngoja niwaonyeshe kitu kisha nitaendelea na maswali juu yenu"

    Tulikuwa tumetulia kabisa kama watu waliopumbazwa, kisha akaanza kutuonyesha.



    Ilikuwa kwenye nyumba yetu, na wote tulikuwa ndani. Tukamsikia mtu akigonga, mimi ndiye niliyemfungulia na kumkaribisha ndani ila hakusema chochote na aliingia moja kwa moja hadi sebleni, tukamshangaa kuwa kwanini haongei. Nikaenda kumwambia mama, akasema atakuwa ni chizi tu tuachane nae ila akizidi kukaa zaidi tukawaite watu watusaidie, kisha nikarudi pale sebleni.

    Nikamuona yule mtu akiinuka na kuondoka bila ya kutuaga, nikamshangaa sana.

    Kumbe kwa macho ya kawaida tuliona vile kuwa aliondoka bila ya kuaga, kumbe ni kivuli chake kilichoondoka na yeye alibaki ndani ya nyumba yetu na kuitawala atakavyo, akamtawala kila mmoja wetu atakavyo hadi leo hii tunapogundua ukweli kwa kuonyeshwa na yeye mwenyewe.

    Tulikosa raha kwakweli kwani jini huyu aliweza sana kucheza na akili zetu.



    Akatuangalia kwa makini tena na kucheka, kisha akasema.

    "Si mnaona jinsi nilivyo na akili kuwazidi? Humu ndani kwenu mlinikaribisha wenyewe ila sijawahi kuwaaga kuwa naondoka, nitaendelea kuwa na ninyi siku zote na hakuna mtakachoweza kufanya kunizuia mimi"

    Akacheka kwa kujisifia, mama akaniangalia kwa sura ya upole sana nadhani alikuwa anajutia mambo mengi ambayo hayawezi kutusaidia kwa muda huo. Inauma sana kuona kitu kinawachezea akili halafu akijitapa kuwa hakuna mtakaloweza kumfanya.

    Muda huo huo akatoweka mbele yetu na kufanya tushtuke sana na kuangaliana kwa uoga, tulikuwa kimya kabisa na aliyekatisha ukimya huo alikuwa ni Sam

    "Jamani tusipoteze muda, tupambane na hiki kiumbe ni khatari sana"

    Dada Penina akajibu,

    "Kupambana na kiumbe wa namna hii sio kitu rahisi kiasi hicho unabhofikiria Sam. Sidhani kama kati yetu kuna yeyote wa kupambana na kiumbe huyu"

    Inaonyesha dada Penina alishakata tamaa kabisa na hakuwa na tumaini tena huku akisisitiza kuwa tumsikilize na kumfatisha tu huyu kiumbe kwani hatuna ujanja tena na tusiende kinyume nae ili asitudhuru kwa chochote.

    Sam aliyapinga kabisa mawazo ya dada na kuendelea kutoa msimamo wake kuwa Mungu atatusaidia, tuendelee kuomba tu. Dada akauliza tena kwa ukali,

    "Tutaombaje wakati yupo? Hebu fikiria vizuri, hiki kitu hakiwezekani"

    "Tuwapigie simu watu wa maombi waje watusaidie"

    Nikaona wazo la Sam ni zuri, nikaamua kuchukua simu ya mama na kutawafuta watu ili niwapigie ila namba za watu wote hazikuwepo kwenye simu halafu si mimi wala Sam anayekumbuka mahali alipoiacha au kuipoteza simu yake.



    Hapakuwa na la kufanya, wakati nikiwaza mambo mengi ya kutusaidia.

    Mara nikaona simu yangu mezani pale sebleni, simu ile ile ya majanga ambayo mara ya mwisho Sam aliitumbukiza kwenye tundu la choo halafu nikaja kuikuta nyumbani kipindi nilipokuta zile pesa za safari ya kwenda Kigoma.

    Nikaogopa sana kuiona ile simu, ikaanza kuita na kufanya wote washtuke maana wao hawakuiona mwanzoni zaidi ya mimi mwenyewe.

    Mama akaniambia niipokee kuwa labda ndio msaada wetu ila Sam akakataa na kusema kuwa kwa majanga ya ile simu kuipokea ni sawa na kujiangamiza au kujiteketeza wenyewe.

    Iliita sana na badae ikatumwa ujumbe mfupi wa maneno ambapo nilisikia tu mlio wa ule ujumbe ila sikujua unahusu nini na umetumwa na nani.

    Nilipatwa na hamu ya kuchukua ile simu na kuiangalia lakini Sam aliendelea kunizuia, kwakweli kati yetu wote tuliokuwepo mule ndani, ni Sam pekee aliyekuwa akijielewa maana sisi wengine tulikuwa tumepumbazika kwakweli na hatuelewi chochote kwani kila kitu kwetu kilikuwa ni mauzauza tu.

    Dada Penina alipoona kuwa ile simu inapiga kelele sana na wala mimi siipokei, akaamua kuinuka ili aichukue yeye.

    Wakati anaishika tu, akarushwa juu kama mtu aliyepigwa na shoti ya umeme kisha akaanguka na kuzimia hapo hapo, uoga ukatuzidi.

    Mama ndiye alikuwa wa kwanza katika kumsogelea dada Penina ambapo nae wakati anamshika dada alirushwa kama umeme na kutupiwa pembeni yake, nikabaki mimi na Sam ambapo mimi nilitaka kumkimbilia mama ila Sam akanizuia kwa kunishika na kuniambia,

    "Si umeona kilichomtokea dada Penina baada ya kushika simu, na kilichomtokea mama baada ya kumshika dada!! Sasa wewe unataka nini? Huyu jini anacheza na akili zetu Sabrina, tunatakiwa kuwa makini sana. Tusifanye vitu kwa kukurupuka, anajua wazi kuwa wewe utakimbilia kumshika mama pale kisha na mimi nitakimbilia kukushika wewe halafu nini kitafatia? Wote tutakuwa tumeangamizwa kwa njia hiyo"

    Akanishtua sana na neno lake la kusema kuwa wote tutakuwa tumeangamizwa, nikamuuliza huku machozi yakinitoka

    "Inamaana dada na mama wameangamizwa? Sina umuhimu tena mimi, bora niangamizwe na mimi tu"

    Nikataka kwenda kinguvu ila Sam akanishikilia kwa nguvu sana na kuniambia

    "Usifikiri vibaya Sabrina, mimi na wewe ndio tunatakiwa kuwakomboa hao na hatutaweza kuwakomboa kwa mtindo ambao wewe unautaka. Inatakiwa tuwe makini sana maana huyu jini anacheza na akili zetu, unadhani tukiangamia wote tutaokolewa na nani? Bora sisi tuwaokoe wenzetu"

    "Basi tukawaamshe"

    "Sio kwa mtindo huo Sabrina, kuwa makini na utumie utashi usipende kukurupuka tu wakati Mungu amekupa akili"

    Sam akanikarisha kwenye kiti kisha na yeye kukaa ila muda mwingi alionekana kamavile mtu anayeongea peke yake ila kwa sauti ya chini sana, alionekana kutafakari mambo mengi sana ila mimi muda mwingi nilikuwa nikilia na kububujikwa na machozi.



    Ulipita muda mrefu sana bila ya dada wala mama kuzinduka, kitu ambacho kilinipa mashaka zaidi kwani sikutegemea kabisa kuwa hali itakuwa vile kwa muda mrefu kiasi kile.

    Giza liliingia na hali ilikuwa vilevile, uoga na kukata tamaa vilitawala kwenye moyo wangu ni Sam pekee ndiye aliyezidi kunipa moyo wa imani na tumaini.

    Mwanzoni umeme ulikuwepo na kufanya ule uoga uwe wa kawaida, ila muda kidogo umeme ukakatika na kufanya giza kubwa litawale ndani ya nyumba na kuzidi kutupa uoga ila Sam alikuwa jasiri sana na kufanya nitambue umuhimu wake kama mwanaume.

    Kwa ule uoga akaamua kunikumbatia huku akinipa maneno ya imani ili nisijefanya vitu vya kijinga wakati pale sebleni ni giza tupu.



    Tukiwa tumekaa vilevile nikaona kama kivuli cha mtu kikitembea halafu kikikazana kuwasogeza mama na dada nikajua tu ni yule jini na kunifanya nipatwe na uoga mara dufu, niliogopa sana na sikujua atawafanya nini zaidi ila Sam aliendelea kunishikilia kwa nguvu tu ili nisimponyoke.

    Gafla umeme ukawaka na mwanga kutawala tena pale sebleni, nikamuona dada na mama wakiwa karibu na miguu yetu pale chini huku kila mmoja amewekewa kisu kinachong'aa sana juu yake halafu yule jini akatokea mbele yetu tena na kuwa kama mtu anayechukizwa na kitu fulani, kisha akaniuliza

    "Wewe Sabrina, unaona ni vyema kumuona mama yako akiwa kwenye hali mbaya kiasi hicho halafu wewe umetulia na kukumbatiwa na mwanaume? Unaona vyema Sabrina?"

    Nikamuangalia huku nikitetemeka, kisha akaendelea kusema

    "Laiti kama mama yako akitambua ulivyo lazima ajutie kwanini alikuzaa mtoto wa aina yako, lazima alie na moyo wake. Wewe mtoto hufai kabisa, niambie unataka niwatende nini ndugu zako? Si unataka kuwa huru na huyo mpenzi wako? Basi chagua unachotaka mimi niwatende ndugu zako hapa mbele yangu"

    Nilimuangalia Sam huku machozi yakinitoka ila Sam alikuwa kimya kabisa akiendelea kuwa kama mtu anayeongea mwenyewe kimoyo moyo, nikamuona Sam hana msaada wowote tena kwangu na kufanya mimi nilie zaidi.

    Yule jini akaniambia tena,

    "Naondoka Sabrina ila nitakaporudi nataka unipe jibu moja, kumponya Sam au kuwaponya ndugu zako"

    Akatoweka mbele yetu.



    Nikamuangalia Sam kwa jicho la hasira sana na kuanza kumwambia,

    "Unanitakia nini wewe Sam? Niwe bila ndugu? Niishi kwa upweke siku zote? Maana sioni chochote ufanyacho katika kunisaidia na jambo hili, niachie nikaungane na ndugu zangu"

    "Tulia Sabrina, Mungu atatusaidia"

    "Atatusaidia muda gani? Tangu umeanza kuongea peke yako hapo hakuna chochote tulichosaidiwa, unanipa mashaka sana Sam. Maisha gani haya? Nimechoka kwakweli, mi nitafanya chochote liwalo na liwe"

    "Kuwa mvumilivu Sabrina, Mungu atatusaidia kwa wakati mahususi. Usipende kuchukua maamuzi ya gafla kiasi utakacho, tulia na tumuite Mungu tu atusaidie"

    Nilimuona Sam akiwa hana maana kabisa na maneno yake kwani mambo niliona yakizidi kuwa magumu mbele yangu na sikuwa na ujasiri wa kuwatazama zaidi mama na dada pale chini walipokuwa hawajitambui.



    Sam alizidi kunishikilia na kunikera zaidi kwani mimi nilitaka kuungana na mama na dada pale chini ila kama kuteseka basi tuteseke wote.

    Wakati nahangaika na Sam pale, alikuja tena yule jini ila safari hii alikuwa anatisha sana, alikuwa na umbo la ajabu na alitisha kumtazama ikabidi nijifiche kwa Sam.

    Nikamsikia yule jini akiunguruma kama simba ila Sam alikuwa ametulia tu, kisha yule jini akasema

    "Huwa sishindani na binadamu hata siku moja, binadamu kwangu ni watu wa kuwafanya nitakavyo na hakuna binadamu anayeweza kushindana na mimi. Sijawahi kuwatambulisha vizuri, mimi jini bahari, siku zote makazi yangu ni baharini na hakuna binadamu wa kushindana na mimi. Muda wowote nikitaka hata wewe Sam nakuteketeza ila sitafanya hivyo ili uonje machungu ya dunia na ujue maumivu ya kuwa mwanadamu hadi siku utamke mwenyewe kuwa unapenda kama ungekuwa jini ili uwe na uwezo kama nilionao mimi."

    Maneno ya huyu jini yakafanya nimtazame kwa macho ya wizi ili nijue kama amerudi katika hali yake ambayo tumeizoea au bado yupo kwenye hali yake ya kutisha, ila nikamuona akiwa kwenye hali tuliyomzoea nayo.

    Nikamuangalia sasa tena kwa macho ya uoga kisha akaniuliza

    "Wewe Sabrina unaweza kushindana na mimi?"

    Nikatikisa kichwa kuwa siwezi, akacheka sana na kusema

    "Najua huwezi kushindana na mimi, ngoja niwaambie kitu. Marehemu baba wa Sabrina ana mzimu wake mkali sana na siku zote umekuwa ukiizunguka familia yake ila kwa mimi umeshindwa. Nina nguvu kubwa kushinda hata mizimu, kuna mzimu mmoja wa baba yako ulikuja kwa nia ya kukusaidia ila ulikuja kwa umbo la binadamu. Alikuwa ni mbaba, akaongea na wewe mambo wengi sana ila nilipotokea mimi akaogopa na kuondoka. Mimi nilikuja kwa umbile la Carlos ila niliuogopesha ule mzima, akampa dawa dada yako ili wewe upake na kupata utambuzi ila nikakupumbaza na kufanya ile chupa ya dawa ivunjike. Nina nguvu sana mimi na siwezi kushindana na binadamu kama nyie hata mara moja"

    Nikamkumbuka yule mbaba aliyefika kwetu na kuniambia anataka kunisaidia, nikakumbuka aliniambia kuwa matatizo yangu yalianzia kwenye ndoto na yataishia kwenye ndoto. Nikakumbuka alivyoondoka baada ya kumuona Carlos, nikakumbuka pia yale mafuta aliyopewa dada Penina kuwa nipake ambayo yalimwagika baada ya chupa kuanguka na kuvunjika kisha yakageuka damu.

    Kwakweli huyu jini hafai kabisa, anayatesa maisha yangu.



    Yule jini alitulia kamavile kuna mambo anayatafakari kisha akaniambia tena kuwa nichague cha kuwafanya ndugu zangu, nikaendelea kuwa kimya akasema

    "Ngoja niamue mimi cha kuwafanya, nawachinja ndugu zako mbele ya macho yako na kisha nakuchukua wewe na kukupeleka kwetu rasmi"

    Akainuka na kuchukua vile visu alivyoweka juu yao, sikuweza kustahimili kwakweli nikachoropoka toka kwenye mikono ya Sam na kumkimbilia yule jini. Nikamshika mikono yake huku nikimsihi kuwa asiwadhuru, akacheka sana na kuniambia

    "Nitaacha kuwadhuru endapo utakubali kwa hiyari yako mwenyewe kuondoka na mimi, je upo tayari?"

    Sikuwa na jinsi kwakweli zaidi ya kukubali tu, nikamwambia yule jini kuwa nipo tayari.

    Sam alinitazama kwa macho ya huruma sana na kunisihi kuwa nisikubali ila nilishakubali tayari, muda ule ule mama na dada wakaduwaa kamavile watu wanaoshangaa kitu.

    Yule jini akawaambia kuwa tunaondoka naye na kuanza kuwaaga huku akiwa na lengo kuwa tuyeyuke machoni kwao, ila Sam akamuomba kitu

    "Kabla hamjaondoka naomba nikuombe kitu kimoja tu"

    "Haya kiombe kama na wewe umeridhia niondoke kwa amani nikiwa na Sabrina"

    "Ndio nakuruhusu uende naye ila...."

    Yule jini akamuuliza

    "Ila nini?"

    "Naomba wakati mnaondoka msiyeyuke bali napenda mtokee mlango wa kutokea ila na sisi tuwasindikize kidogo na muende zenu vizuri"

    Yule jini akafurahi sana kuona Sam naye ameridhia, roho iliniuma sana na kutambua kuwa kweli Sam hanipendi hadi ameamua kukubali tu! Nikajua sababu anatambua kuwa wanawake ni wengi kwahiyo atampata mwingine.



    Tulianza kuondoka huku macho yangu yakiwa yamejaa machozi, yule jini akanyoosha mkono wake mlangoni kisha Sam akafungua ule mlango maana mwanzoni haukuwezekana kufunguka.

    Nikawa wa kwanza kutoka nje, nikashangaa kumuona wifi Joy na dada Zuhura pale nje.





    Tulianza kuondoka huku macho yangu yakiwa

    yamejaa machozi, yule jini akanyoosha mkono wake

    mlangoni kisha Sam akafungua ule mlango maana

    mwanzoni haukuwezekana kufunguka.

    Nikawa wa kwanza kutoka nje, nikashangaa

    kumuona wifi Joy na dada Zuhura pale nje.

    Kwa mbali nikamuona dada Salome akiwa ameongozana na watu kadhaa akiongozana nao kuja pale nyumbani.

    Kabla ya kufanya chochote yule jini alinivuta kwa nyuma na kunirudisha tena ndani, akamwangalia Sam na kumwambia

    "Niliyajua yote haya, usifikirie umefanikiwa au umeweza kuzichezea akili zangu kiasi hiki"

    Akafunua mdomo kisha moto ukatoka kinywani mwake na kumuelekea Sam ila kabla haujamfikia ule moto Sam akaniambia kwa nguvu

    "Sabrina mwambie Mungu akusaidie na......."

    Ule moto ukamfikia na kumfanya Sam aanguke mahali pale akiwa hajitambui, kisha yule jini akaniangalia mimi kwa jicho kali sana huku yale macho yake yakiwa yanatisha sana.

    Nikawasikia wale wa nje wakigonga mlango wetu, nikataka kwenda kufungua ila nilipigwa na bumbuwazi kumuona Sam akiwa hajitambui pale chini.

    Kisha yule jini akanishika mkono halafu mimi na yeye tukayeyuka eneo lile.



    Nikaangushwa pembezoni mwa bahari, maji ya bahari yakanigusha na kunifanya nishtuke sana.

    Nikaangalia kila mahali na kujiona nipo mwenyewe tu wala sina pa kukimbilia.

    Nikainuka eneo lile, huku nikijaribu kukimbia kidogo pengine nitasalimika.

    Nilikimbia sana ila sikuweza kutoka eneo lile la bahari labda michanga ilikuwa ikinirudisha nyuma kwakweli sikujua kitu kabisa ila nilichoka sana kukimbia na kuamua kukaa chini.

    Nilipokaa tu, akaja yule jini mbele yangu na kusema

    "Naona binadamu mnajaribu kushindana na kiumbe mkubwa kama mimi, nina nguvu sana mimi na hakuna awezaye kunishinda"

    Akacheka na kuendelea kusema,

    "Nakushangaa Sabrina ulikuwa unakimbia nini wakati umekubali kwa hiyari yako mwenyewe kuja na mimi, mbio zako hazisaidii hata binadamu wenzenu husema mbio za sakafuni huishia ukingoni, je hujawahi kutafakari hilo katika maisha yako haya?"

    Akaniangalia machoni ila macho ya huyu jini yalikuwa yanatisha sana hadi yanaogopesha kuyatazama mara mbili mbili.

    Ila yeye hakuacha kunitazama, alikuwa akiniangalia kwa macho makali sana ili niogope na ninidi kutetemeshwa na yeye.

    Akaniambia,

    "Tazama kule Sabrina"

    Alionyesha mkono wake katikati ya bahari, nami nilielekeza macho yangu hapo ambapo ikawa kama naangalia sinema.



    Kulikuwa na eneo kubwa chini ya bahari, eneo lile limepambwa kwa vitu vya gharama na kung'ara.

    Eneo lile lilijaa madini ya kila aina, dhahabu za kupendeza na almasi.

    Watu wa eneo lile walivaa madini mwilini na pesa zilikuwa nyingi sana, nyumba zao gharama sana kwakweli walionekana kuwa wav wenye pesa kuliko wanadamu wote duniani, ni eneo la kuvutia na linalotamanisha kulitazama muda wote.

    Hadi nikajikuta kama navutika kwenda eneo lile na kujaribu hata kuvishika vitu vile ili nione kama ni vitu kweli.



    Akayarudisha mawazo yangu pale nilipokuwa na kuniambia,

    "Je! Hutamani kuwa katika eneo lile Sabrina?"

    Sikutaka kuitikia kwani bado sijaipima vyema tamaa yangu.

    Akaniangalia tena na kuniuliza,

    "Unajua alichokuwa anawaza Sam aliposema tutoke nje watusindikize?"

    Nikatikisa kichwa kuwa sijui na ukweli nilikuwa sijui zaidi ya kumuona Sam kuwa mbaya kwangu na kunitoa kirahisi kiasi kile kwa yule jini, kumbe wakati nikiwaza ya Sam yule jini nae alikuwa akiisoma akili yangu kwa umakini sana na kuniuliza,

    "Baada ya Sam kukuruhusu wewe kuondoka na mimi ulijisikiaje?"

    "Nimejisikia vibaya sana"

    "Ila Sam anataka uishi maisha ya kifahari ndiomana kakuruhusu uondoke na mimi"

    Nikatulia na kukumbuka kuwa mwanzoni aliniuliza kama najua alichokuwa anawaza Sam kwahiyo nikaamua kumuuliza kuwa Sam alikuwa anawaza nini naye akaanza kunielezea

    "Sam ni kijana mpumbavu sana, alitaka kucheza na akili yangu eti kwavile niliwaaga pale kwenu kuwa naondoka yeye akaamua kutumia muda huo kufanya mambo yake. Alitaka tukifika pale mlangoni, mimi ndio nitangulie kutoka kisha akuvute wewe na kukurudisha ndani na kufunga mlango ila hakujua kama mimi nina akili zaidi yake, hajajua kuwa mimi naweza kufanya mambo makubwa zaidi yake. Tutaondoka hapa nikiikamilisha kazi yangu kwa huyo Sam kwani amefanya nionane na vizuizi mbele yangu"

    Nikakumbuka vile vizuizi anavyovizungumzia itakuwa ni dada Zuhura na wifi Joy pamoja na dada Salome na kundi lake, nikaamua kumuuliza kuwa kwanini anawaita vizuizi wale akanijibu

    "Hawa watu wamekuwa siku zote wakiniwekea vikwazo katika kuondoka na wewe"

    "Ila si umeniambia wewe huwa hushindani na wanadamu! Kwanini hao utake kushindana nao?"

    Muda huo huo akatoweka kwenye macho yangu na sikumuona tena pale kwa muda huo.

    Nilibaki mwenyewe kama mwanzo, mawazo yangu yakanipeleka hadi Kigoma nyumbani kwa wakina Carlos.

    Nikakumbuka mambo mengi sana yaliyonipata na Sam wakati nipo huko, nilijiangalia na kujihurumia sana huku nikiwaza mwisho wangu tena mwisho wa kuishia katika ushetani ya kuwa sitakuwa tena mwanadamu wa kawaida.

    Nikawaza mengi sana bila kujielewa wala majibu.



    Nikainuka pale nilipokaa, kisha nikaanza kutembea kwenye ukingo wa bahari huku nikijisemea kuwa Mungu anisaidie, sikuwa na la kufanya kwani mawazo yangu hayakuwa ya kawaida kabisa, nilianza kujihisi kuwa na utofati mkubwa na binadamu wa kawaida kwani mimi nautumia muda mwingi wa sasa kuwa karibu na jini, je kuna hali ya ubinadamu ndani yangu? Maana sipo sawa kabisa.

    Nikaona kama kuna kibanda mbele yangu, nikajua labda ni mojawapo ya vibanda vya wavuvi baharini.

    Nikaamua kwenda kwa kujua kwamba nitapata msaada huko, nilisogelea taratibu kile kibanda na kugonga

    "Hodiiii......"

    Sauti nyororo ya mwanamke kutoka kwenye kile kibanda ikaniambia,

    "Usigonge ingia tu"

    Nikasimama pale nje na kutafakari kuwa ni mwanamke gani mvuvi? Au mvuvi wa humo kamuweka mwanamke wake?

    Ila ile sauti ikanisisitiza tena

    "Ingia"

    Nikatamani kujua ni sauti ya nani, na je huyo mwenye hiyo sauti anafanana vipi.

    Nikafungua mlango na kuingia ndani.



    Mule ndani kulikuwa tofauti kabisa na nje yani huwezi kuamini kama nje ni kibanda kidogo, ndani palikuwa ni pa kubwa na pazuri pa kuvutia hadi nikashangaa na kujikuta nikiangalia kila mahali huku nikijaribu kuona kama yule dada aliyeniitikia yuko wapi ila sikumuona na kujikuta nipo peke yangu, uoga ukanishika sana maana nipo mwenyewe.

    Nikageuka nyuma ili niangalie mlango nilioingilia niweze kutoka tena ila sikuweza kuuona, hapakuwa na mlango tena na kufanya nizidi kuogopa.



    Wakati nashangaa shangaa pale nikashtuka nikishikwa bega na mtu, nikageuka haraka sana.

    Nikamuona mwanamke mrembo akicheka mbele yangu, yule dada alikuwa ni mzuri sana sijapata mdada mrembo kama yule katika maisha yangu.

    Alikuwa akiniangalia huku akicheka kwa sauti yake nzuri sana, kisha akanishika mkono na kuniambia

    "Twende tukakae Sabrina"

    Nikashtuka sana kuwa amenijuaje, hofu ikanijaa tu kuwa huyu mwanamke ni jini tu ndiomana kanijua jina langu ila sikujua kama majini ni wazuri kiasi hiki nimuonacho huyu dada maana kwa mawazo yangu nilijua kuwa lazima majini wawe wabaya, lazima wawe wanatisha sana ila huyu alikuwa kawaida kabisa tena alikuwa mzuri sana.

    Akaniongoza hadi kwenye makochi yaliyokuwa mazuri sana huku akiwa anatabasamu tu kwa kuniangalia, kisha akaniulizahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Unanionaje mimi? Ni mzuri sana?"

    "Ndio wewe ni mzuri sana"

    "Kwanini amekuchagua wewe na kuniacha mimi?"

    Sikumuelewa, nilimuangalia tu maana sikujua anamuongelea nani na kwanini aniulize vile.

    Alipoona simjibu, akanionyesha kiganja chake na kuniuliza

    "Unamjua huyu?"

    Ilionekana picha kwenye kiganja cha yule dada, ilikuwa ni picha ya yule jini, nikashtuka sana kwani niliogopa. Nikatikisa kichwa kuwa namfahamu ndio, akatabasamu tena na kuniambia

    "Najua unamfahamu Sabrina, ni huyu ndiye ninayemuongelea hapa"

    Ikabidi niulize

    "Kwanini umemuongelea?Na je wewe ni nani?"

    Akatabasamu tena, na kuniambia

    "Mimi ni kama huyu, sina tofauti na yeye. Ameenda kupambana ili akishinda akuchukue wewe na kwenda na wewe huko kwetu, kwakweli ukienda kula hutorudi tena huku Sabrina. Kule kunatufaa sisi wenyewe, angalia"

    Akanionyesha tena kwenye kiganja chake.

    Nikaona nyumba yetu ikiwa na watu mbali mbali wakiwa kwenye maombi ila nje alikuwepo yule jini.

    Wakati tunaangalia, gafla kuna kitu kikapiga kama radi kwenye kile kiganja kisha yule dada akakwepesha mkono wake na kuhema kwa nguvu sana.

    Akakaa kimya kwa muda kidogo, kisha akaanza kucheka yani alicheka sana hadi kuanguka chini halafu akainuka tena na kuonekana kamavile amefurahi sana na kusema

    "Kwa ubishi ule, kama leo asiporudi na kilema basi Sabrina upo hatarini sana yani hapo kazi unayo kubwa sana"

    Bado nilimuangalia huku nikimsikiliza kwa makini maana nilikuwa kama simuelewi kabisa na wala sikutambua anachokiongelea, akaendelea kuniambia

    "Tena unishukuru sana Sabrina, mie nimekusaidia mambo mengi sana yani tangia siku nyingi wewe ungekuwa umeshaangamia ila mimi nimekusaidia sana Sabrina hadi leo nimeamua kujitokeza mbele yako, nilikufanyia mambo mengi ili upate utambuzi ila wewe hukujali kitu chochote kile zaidi ya kupumbazwa na huyu aliyekupumbaza. Pole sana, wanadamu wenzio wakishindwa leo itakuwa basi tena Sabrina"

    Nikamuangalia kwa jicho la upole sana yani kama mtu ninayehitaji msaada zaidi ambao msaada wenyewe unaonekana kuwa mbali sana.

    Nikajaribu kumuomba msaada yule dada ila alikuwa akitabasamu tu bila ya kunipa maelezo ya kitu chochote.

    Akainuka na kunishika mikono, akaniangalia machoni nilikuwa nikisema kimoyo moyo

    "Mungu nisaidie"

    Akaniangalia kwa macho makali tofauti na macho yake ya mwanzoni, kisha akaniambia

    "Wanadamu mmezidi sana tamaa na ndiyo inayowaponza siku zote, pole sana. Hata mimi umeniona sababu ya tamaa ndiomana nikaweka kibanda mbele yako kwani nilijua lazima utaingia tu. Ila jiepushe na tamaa ya kukuponza"

    Gafla akaanza kurefuka na kuwa mrefu sana, miguu yake ilitisha kuitazama mara mbilimbili nilijiziba sura yangu huku nikitetemeka kwani sikujua kuwa yule kiumbe angenitenda kitu gani sikujua kabisa.

    Nilifunika kwa nguvu macho yangu huku uoga ukiwa umenijaa.



    Nikahisi kupulizwa na upepo kitu kilichofanya nitake kujua nilipo, nikafungua macho yangu na kujiona nipo tena pembezoni mwa bahari, nikatetemeka sana.

    Nikaogopa sana kwani sikujua msaada wangu ni kitu gani, nilianza kukimbia hovyo hovyo tena bila ya kuwa na uelekeo wa maana ila sikufika mbali nikashangaa mkono mrefu ukinivuta na kunirudisha pale pale nilipokuwa mwanzoni, kisha ukatokea mti mkubwa mfano wa mti wa mbuyu, nikajikuta nikikandamizwa kwenye mti ule na kufungwa kamba mwili mzima muda ule ule.

    Nilishangaa sana kwani nilifungwa kamba na mtu asiyeonekana, kwa hapo sikujua kosa langu ni lipi kwahiyo niliendelea kulia na kuomboleza bila ya kujua msaada wangu ni nini.

    Gafla nikashtukia nikipigwa makofi ila mpigaji hakuonekana, nilipigwa sana hadi nilihisi hata kuvimba sura yangu, nikalia hadi machozi yakanikauka yani hayakunitoka tena ila nilikuwa nikilia tu.

    Yule aliyekuwa akinipiga akaacha gafla, nikahisi kuwa ameondoka ila mimi sikuweza kutoka pale nilipofungwa zile kamba na kufanya niendelee kulia tu.



    Mbele yangu akatokea yule mdada wa kwenye kile kibanda, aliniangalia sana kisha akanyoosha mkono wake kwangu na zile kamba zote zikakatika.

    Nikafurahi kuwa huru, nikataka kumsogelea ili niweze kumshukuru ila kabla sijafanya hivyo yule dada alianguka mbele yangu na kutoweka.

    Nyuma yake alikuwepo yule jini ila alionekana akiwa na hasira sana, akanishika mkono na kusema

    "Sababu ndugu zako wamefanya kitu kibaya kwangu, sasa naondoka na wewe na hawataweza kukuona tena katika maisha yao. Adhabu niliyokupa hapo ni kwa kosa lako la kuongea na yule mwanamke, na yeye adhabu yake inafatia. Huku tutakapoenda nitakubadilisha jina na kukuita......"

    Kabla hajatamka hilo jina alilotaka kusema, mwanga mkali kutoka juu ukamulika eneo lile ambalo alisimama na mimi.

    Nilishtuka sana na kuzidi kuogopa yale mauzauza yanayoonekana, na yeye akatetemeka kisha akanishika mkono na kuanza kukimbia na mimi ndani ya maji ya bahari kana kwamba anaukimbia ule mwanga uliotumulika eneo lile.



    Wakati anakimbia na mimi, nikasikia sauti ikiita kwa nguvu sana

    "Sabrinaaaaaa..... Sabrinaaaaaa..... Rudi Sabrina"

    Nikashtushwa na ile sauti pia kwani ilikuwa ni sauti ya mtu ninayemtambua, ilikuwa ni sauti ya mama yangu mzazi.

    Nikajikuta nikimuachia mkono yule jini na kugeuka nyuma huku nikikimbia sana ila safari hii yule jini hakuwa na uwezo wa kunikamata na mkono wake mrefu, hakuweza kunishika tena.

    Nikatamani kugeuka nyuma ili nimuone yule jini alipo ila nilipokumbuka maneno ya yule mdada kwenye kibanda kuwa wanadamu tunaangamizwa kwa tamaa sikutaka tena kugeuka nyuma, niliendelea kukimbia tu.



    Gafla nikajikuta nimefika mlangoni kwenye nyumba yetu, huku nikihema sana, waliokuwepo wote walikuwa kwenye maombi mazito pale ndani.

    Nikamtazama Sam aliyekuwa bado yupo chini, nikapiga magoti na kumsogelea pale alipo huku nikitaka kumgusa ila kabla sijamgusa Sam akaanza kutingishika mwenyewe.



    Gafla nikajikuta nimefika mlangoni kwenye nyumba

    yetu, huku nikihema sana, waliokuwepo wote

    walikuwa kwenye maombi mazito pale ndani.

    Nikamtazama Sam aliyekuwa bado yupo chini,

    nikapiga magoti na kumsogelea pale alipo huku

    nikitaka kumgusa ila kabla sijamgusa Sam akaanza

    kutingishika mwenyewe.

    Nilikuwa natetemeka huku nikishangaa, nilimuangalia Sam pale chini na kuweka mikono yangu pamoja kwenye kifua changu.

    Kwakweli hizi zilikuwa siku za mateso na furaha katika maisha yangu kwani kwa muda huu sikujielewa kabisa, nilikuwa sielewi kitu chochote kwakweli.

    Sam aliinuka na kukaa pale chini kisha akanitazama mimi na kutazama watu waliotuzunguka, mimi pia nikajikuta nikitazama watu waliotuzunguka ila sikuwatazama zaidi kwani macho yangu yalikuwa mazito sana na kujikuta nikisinzia pale pale.

    Nikawasikia wakipiga makofi kama watu wanaoshangalia kitu, na kuniinua mimi pale chini huku wakiwa na lengo la kuzungumza na mimi ila usingizi mzito ulinizidia, nikasikia sauti kwa mbali ya dada Zuhura ikiwaambia wale wengine

    "Mwacheni apumzike kwanza"

    Kuna mwingine alikuwa anahitaji bado kunihoji maswali, nikamsikia wifi Joy nae akisema,

    "Hayo marumbano ndio yatakayoturudisha nyuma kama mwanzo, kurumbana si kuzuri. Ilimradi Sabrina amerudi ni jambo la kumshukuru Mungu, cha muhimu hapo mwacheni apumzike kama ambavyo Zuhura amesema. Mapatano ni mazuri sana, tusitake kurumbana kwa mambo yasiyo na msingi si mnakumbuka kilichotokea wakati........"

    Usingizi ukawa umenichukua vizuri na sikuweza kuwasikia tena wanachozungumzia zaidi kwani nililala usingizi mzito sana.



    Wakati nimelala, nikajiwa na matukio mbali mbali yaliyowahi kutokea katika maisha yangu.

    Nikajiona wakati nilipokuwa mtoto mdogo sana na kupendwa na kila mtu aliyenizunguka, nikaona jinsi gani watu waliupenda uwepo wangu na jinsi gani baba alipomwambia mama kuwa

    "Huyu mtoto nitamuita Sabrina"

    Mama alimuuliza kuwa kwanini ameamua kuniita Sabrina, baba akamjibu

    "Kwasababu ni jina ninalolipenda, unapompa mtoto jina hakikisha kwamba wewe kama mzazi umelipenda jina hilo na linatoka katika moyo wako. Wazazi wengine hukurupuka tu kuwapa watoto wao majini ila mimi nimeamua kumpa jina hili kwakuwa...."

    Mama alimkatisha na kumuuliza kwa makini,

    "Kuwapa watoto majini?? Ndio nini?"

    Baba akacheka na kusema kuwa ameghafirika kusema majini ila alikuwa akimaanisha majina.

    Mama na baba wakafurahi pamoja na tangia hapo nikaanza kuitwa Sabrina, wazazi wangu wakanipenda sana tena sana na walinipa chochote nilichotaka.

    Nikajiona nilipoingia sekondari na tabia yangu na rafiki zangu ya kupenda kupanda lifti, si kwamba wazazi wetu walikuwa hawatupi nauli hapana ila ilikuwa ni tabia yetu na jinsi tunavyoshawishiana na wanafunzi wenzetu.

    Tukaona kuwa kwenda kwa lifti kwa kipindi kile ni furaha bila ya kujua mawazo ya kile tulichokuwa tunakipenda na kukifurahia.

    Ingawa madhara yake yalichelewa kuja kwangu ila yamenitesa kiasi cha kuiona dunia ni mbaya tena imejaa matesa.

    Ndoto yangu ikaenda mpaka kwa yule mbaba aliyewahi kuja nyumbani kwetu na kuniambia kuwa kwavile matatizo yangu yalianzia kwenye ndoto basi na yataishia kwenye ndoto vilevile ila huyu baba hakutamka maneno hayo tena zaidi ya kuongea na mimi kwa utaratibu sana na kusema amefurahi kuniona mimi nikiwa huru tena

    "Furahia uhuru wako Sabrina, unatakiwa kumpendeza Mungu na watu wote"

    Alikuwa akitabasamu tu huku akiniangalia kisha akatoweka mbele yangu.

    Niliwaona rafiki zangu wapenzi wawili Lucy na Suzy, walionekana kuwa katika hali ya kunishangaa sana na huku wakisema kuwa nimebadilika sana eti nimekuwa mpya,

    nami nikajitazama huku nikijifurahia nilivyokuwa.

    Zikanijia ndoto nyingi sana za maisha yangu, ndoto ambazo zilinionyesha mambo yote niliyopitia.

    Akatokea tena yule mbaba wa kunipa chupa na kusema

    "Yote uliyopitia Sabrina sasa yamegeuka kuwa ndoto ila unatakiwa kuwa makini ili ndoto hii isije ikajirudia tena katika maisha yako halisi. Nakutakia kila la kheri, Kwaheri Sabrina"

    Lile neno lake la mwisho kwangu likawa linajirudia kama mwangwi,

    "Kwaheri Sabrina, Kwaheri Sabrina, Kwaheri Sabrina"

    Nikashtuka na kuamka.



    Nikakaa na kujiona kuwa nimejawa na uchovu kwenye mwili wangu, nilijinyoosha viungo vyote vya mwili wangu.

    Mama na dada yangu Penina walikuwa wapo pembeni yangu wakiniangalia tu, na waliponiona nimekaa nao wakafurahi na kunikumbatia.

    Nikaangalia kule ndani na kukuona ni kwa tofauti sana, haikuwa kama nilivyozoea ilikuwa ni chumbani kwa mama ambapo wakaniongoza hadi sebleni, nikamkuta dada Salome, wifi Joy na dada Zuhura na wote walinipokea kwa furaha sana na kunikumbatia kwakweli nilijisikia raha na kujiona kuwa mtu mpya kabisa yani sikujifananisha tena na Sabrina wa zamani kwani nilikuwa Sabrina mpya na mwenye mawazo mapya.



    Mama alianza kunishika kila mahali kamavile ananikagua kuwa nipo sawa kweli, wifi Joy alimwangalia mama na kumtania

    "Ni yeye huyo mama usiwe na wasiwasi"

    Mama akacheka na kufurahi.

    Tukaongea mambo mbali mbali nadhani ni kwaajili ya kuiweka akili yangu sawa maana walijua jinsi nilivyokuwa nimevurugwa kwa kipindi cha nyuma.

    Muda mwingi dada Zuhura aliutumia kunipa moyo na kuniambia niangalie ya mbele na niendelee kufanya ibada

    "Usichoke mdogo wangu, ibada ndio Kila kitu katika maisha yetu kwahiyo hatutakiwi kuchoka katika kufanya ibada"

    Nikakubaliana na maneno ya dada Zuhura kwani aliniambia kitu cha kweli ambacho mimi nilikuwa sikifanyi.



    Kwavile niliamka na uchovu, ikabidi niende kuoga ila kutokana na yote ambayo yamewahi kunitokea nikawa na hali ya uoga katika nyumba yetu kwahiyo nikamuomba dada anisindikize kwenda kuoga na haikuwa tatizo kwake, alinipeleka tu. Nikaoga na kwenda kuvaa kisha kurudi sebleni, kitu ambacho nilimwambia mama ni kimoja tu kuwa sipo tayari kuendelea kuishi kwenye nyumba yetu. Nikamuomba mama kuwa ikiwezekana tuhame ile nyumba maana sikuwa tayari kuendelea kuishi kwenye ile nyumba nikijua kuwa tukiendelea kuishi pale nitazidi kuona kuwa ni mauzauza tu ingawa walikuwa wakinisihi pale kuwa nyumba yetu haina tatizo tena ila msimamo wangu uliendelea kuwa mmoja tu kuhama pale ndani kwani hata kile chumba changu nilichokuwa nikiishi sikutaka kukitembelea kwa yale mauzauza.

    Mama na dada walikubaliana na mimi katika swala hilo ila swali likawa je tutahamia wapi?



    Muda ule wakati tunazungumza hayo, kaka Deo alifika nyumbani na kufurahi sana kuniona ila alisikia lile swala letu la kuhama na kutusapoti pia kuwa ni maamuzi mazuri sana na kusema kuwa,

    "Msiwe na tatizo na mahali pa kuhamia kwani mimi nataka muhamie nyumbani kwangu"

    Wifi Joy naye akasapoti,

    "Tena itakuwa ni vyema sana tukiishi pamoja mama"

    Ila mama alikuwa kimya na nikagundua kuwa hajakubaliana na swala lile, kisha akamuuliza kaka Deo

    "Na nyie je mtaishi wapi?"

    Wifi Joy akajibu,

    "Tutaishi wote mama"

    "Hapana haitakuwa na picha nzuri"

    Kaka Deo akamwambia mama,

    "Usijali mama, pale tutaishi kidogo na ninyi kisha sisi tutahama maana mimi kuna nyumba nataka tuhamie si unajua yale matatizo yaliyotupata na sisi! Tumeona bora tuhame mtaa ule, sasa kuliko kuuza nyumba ni vyema nyie wote muende mkaishi pale kisha na sisi tuhamie mazingira mengine."

    Mama akakubaliana na kaka, kisha muda huo huo tukaanza kupanga baadhi ya vitu kwenye nyumba ili tuondoke na kwenda kuanza maisha mapya.

    Dada Zuhura na Salome wakatusaidia kupakia mabegi yetu kwenye gari ya kaka kisha nyumba ikafungwa na safari kuanza.



    Tulipofika na muda nao ulikuwa umeenda kwani jioni ilishaingia ila nilijisikia amani kuwa katika mazingira ya mbali na nyumbani kwani kila nikifikiria ule mzoga wa Carlos katika chumba changu nahisi kama mwili unanitoka kwani nasisimka sana, hata hapo kwa kaka Deo sikulala katika kile chumba nilichowahi kulala wakati nipo hapo, nilipewa chumba kingine kabisa na kuwa na maisha mapya katika maisha yangu.

    Usiku haukukawia kupita, tukalala mapema tu.



    Usiku wa leo nililala vizuri kabisa na kabla ya kulala nilimuomba Mungu kwanza na nilipoamka nilishukuru kwa kuamka kwani wengine huishia katika usingizi.

    Nilipokaa nikakumbuka kuhusu Sam na kwenda kumuuliza dada Penina,

    "Eti dada, kwani Sam yuko wapi?"

    "Nilikuwa nangoja uniulize Sabrina, kweli matatizo hayana adabu hadi unamsahau mtu wa muhimu kiasi hicho!"

    "Kupitiwa tu dada, niambie alipo Sam"

    Dada alikuwa akicheka, kisha akaniambia

    "Unajua Sam alizinduka pale akiwa na uchovu sana, wale wanamaombi wakaamua kuondoka nae na kumrudisha kwao kwahiyo yupo kwao kwasasa na wakati tunakuja huku nilimtaarifu kuwa tunahama hata hivyo asubuhi ya jana alinipigia simu kuwa anaendelea vizuri"

    "Kwani mimi nililala kwa muda gani dada?"

    "Unajua ile juzi ilikuwa jioni sasa, ulipolala ukaamka jana ule muda ambao mimi na mama tulikuja kukuamsha. Kwanza nisamehe sana mdogo wangu kumbe nilikuwa nakuletea matatizo katika maisha yako!"

    "Usijali dada, najua wazi ulikuwa unatumiwa ila usijali chochote"

    Nilitamani kujua mengi sana yaliyotokea wakati mimi nahangaika kule baharini ila dada nae hakuwa na maelezo yaliyonyooka, najua yote ni sababu hata yeye mwenyewe alivurugwa.

    Mtu pekee wa kunipa maelezo yaliyonyooka ni wifi Joy au kama ningekuwa karibu basi dada Zuhura na dada Salome nao wangeweza kunipa maelezo yaliyonyooka.



    Niliongea mengi sana na dada kule chumbani, alisikitishwa sana na namna ambavyo tuliwashika uchawi watu wasiohusika katika maisha yetu

    "Niliwachukia sana Zuhura na Salome, niliwaona kuwa ni watu wabaya sana ukizingatia uchawi niliokuwa nikiambiwa wanafanya. Kuna siku nimewahi kummwagia tope Zuhura wakati anaenda kuswali, kwa kipindi hicho nilijiona nimefanya kitu cha ufahari na kufurahia sana ila Zuhura hakupambana na mimi wala kunitupia maneno machafu ila alinipa baraka tu na kuondoka zake, kwakweli sasa najutia moyo wangu na kutambua kosa nililofanya kumbe nimefanya dhambi kubwa sana kwa kumuharibia swala yake. Sikuamini kama Zuhura angekuwa ni mmoja kati ya watu waliokuja kuisaidia familia yetu na ametusaidia sana kwa sala zake, nakumbuka siku nilipomfanyia kusudi njiani na kumvua kilemba chake ila yeye alinisamehe kabisa hakuwa na kinyongo na mimi hata nimemshangaa kwakweli. Anakuwa kuigwa huyu dada kwani ana moyo wa kipekee sana"

    Dada aliongea kwa msisitizo sana kwani aliyajutia yote aliyoyatenda kwa kipindi cha nyuma.

    Baada ya kuongea yote hayo tukaamua kutoka sebleni.



    Kufika sebleni nikashangaa kumuona Sam ambapo aliinuka na kujakunikumbatia kwa furaha kisha akasema

    "Natumaini wewe ni Sabrina niliyekuzoea, Sabrina wa zamani"

    "Ndio ni mimi"

    Nikamkumbatia Sam kwa furaha pia na kuongea nae mambo mbali mbali ila sikutaka kumkumbushia mambo ambayo yalitokea huko nyuma maana hata mimi mwenyewe sikutaka kuyaongelea tena mambo haya nikiwa na Sam.

    Ila Sam akaongea pale na mwisho wa siku akatuaga na kuondoka.

    Nikautumia muda huo kumuuliza wifi Joy kuhusu mambo yaliyotokea wakati nimetoweshwa, naye hakusita kuniambia kwani alinieleza mambo mengi sana

    "Ni jambo la kumshukuru Mungu Sabrina, nyumba yenu ilikuwa na mapambano makubwa sana ila kwavile wote tuliokuwepo pale tulikuwa na nia moja ya kuweka mambo sawa ikasaidia sana na Mungu akatusikia kwakweli, jambo la kwanza ilibidi tumzindue mama yako kwa maombi maana ufahamu wake ulikuwa umepotea, ila aliposhtuka na kuwa sawa ndipo alipoanza kuamini na kukuita binti yake uweze kurudi nyumbani. Mungu ni mkubwa sana kwani ni kweli Sabrina ukarudi, tulifurahi sana. Zuhura amefanya kazi kubwa sana tena sana kwakweli anastahili kupongezwa, kwani chumba chako kilikuwa na mambo mengi ya ajabu na yeye aliweza kuyabainisha na nd iomana mlipotaka kuhama hakuwa na pingamizi lolote kwani anaelewa kila kitu"

    Wifi Joy alinieleza mambo mengi sana na aliniambia vitu vingi sana, nilijengwa na imani katika maisha haya na kujifunza kumtegemea Mungu maana tangia mwanzo ningetambua uwepo wa Mungu basi yale yote yaliyokuwa yananipata kila mara yasingeweza kunipata kiasi kile.



    Baada ya wiki mbili, kaka Deo na wifi Joy walihamia kwenye nyumba nyingine na tukawa tunatembeleana nao kama ambavyo tulianza kutembeleana na wakina dada Salome na dada Zuhura kwani walikuwa ndugu zetu kwakweli, undugu kati yetu ukajengwa kwa imani na kuwa ndugu wa umoja na pamoja kwani ni kweli kwamba binadamu wote ni ndugu kwani sote tumeumbwa na Mungu mmoja.



    Sam alikuja nyumbani na kuniambia jambo lililofanya nifurahi,

    "Sabrina please, naomba tufunge ndoa mi na wewe"

    Kwa yote niliyopitia katika maisha yangu sikutaka kukataa hili, Sam amekuwa karibu sana na mimi katika kila hali na ndiyo mwanaume niliyetaka kuwa nae katika maisha yangu yote.

    Sam ni mwanaume wa kweli wa ndoto zangu za uhalisia, Sam ndiye mwanaume nimtakaye. Waswahili husema chelewa chelewa utakuta mwana si wako, sitaki kuchelewa kuwa na Sam kwani nahitaji kuwa naye katika maisha yangu.

    Nilikubaliana nae kuhusu hili huku machozi yakinitoka ya furaha.



    Nilienda ndani na kumuuliza mama,

    "Kama nikitaka kuolewa niolewe na mwanaume wa aina gani?"

    "Yeyote utakayempenda mwanangu ilimradi tu uwe unampenda naye anakupenda"

    Nikaamua kumwambia mama kuhusu Sam,

    "Mama, Sam anataka kunioa"

    Mama akaniangalia huku amekunja sura yake.



    Nikaamua kumwambia mama kuhusu Sam,

    "Mama, Sam anataka kunioa"

    Mama akaniangalia huku amekunja sura yake.

    Nikamuangalia mama huku nikijua kuwa atakataa swala langu la kuolewa na Sam ila hakuniambia chochote zaidi ya kukunja sura yake.

    Ikabidi nimuulize,

    "Inamaana mama hutaki niolewe na Sam?"

    "Sio sitaki uolewe na Sam ila swali langu ni moja tu juu yako"

    "Swali gani mama, niulize basi"

    "Je upo tayari kuolewa tena?"

    "Ndio mama nipo tayari"

    Akaniuliza tena,

    "Je upo tayari kuolewa tena?"

    Nikakaa kimya bila ya kumjibu mama, kisha nikaondoka pale alipo na kwenda mahali ambapo nilikaa na kutafakari swali la mama kisha nikajiuliza,

    "Kwani wasi wasi wangu ni nini ikiwa Sam nampenda naye ananipenda pia? Ni kitu gani mwanamke anakihitaji toka kwa mwanaume pindi anapotaka kuolewa zaidi ya upendo?"

    Nilijiuliza na kuona kuwa nipo sahihi kwa kile ninachokitaka katika maisha yangu, Sam ndiye mwanaume sahihi wa kuwa na mimi.

    Nikarudi tena alipo mama ila sikumuuliza swala la mimi kufunga ndoa bali nikamuuliza kuwa kwanini alikataa kukaa na kaka Deo pamoja na wifi Joy na sisi kwa pamoja naye akanijibu,

    "Mimi ni mtu mzima ninayetambua jema na baya, kukaa pamoja siku zote na mkwe si jambo jema. Kwanza mimi ni mtu mzima sana kwahiyo ningewanyima uhuru Deo na Joy, wangetamani kufanya vitu vingi pamoja lakini wangenihofia mimi na kama wangefanya nikiwaona ni kunikosea adabu. Huwa sipendi kuwabana watoto ndiomana kwa mzazi mwenye akili hata kama alikuwa anaugua na kuletwa augulie kwa watoto wake hukaa kwa muda ila akipona tu utamsikia kuwa naenda kuangalia kwangu, kuangalia mashamba yangu sijui mifugo yangu ili tu asiendelee kuwabana. Sisi ni waafrika, tuna mila na desturi zetu kwahiyo kuna mambo ambayo hayapaswi mzazi ayaone kwa mwanae"

    Nilimsikiliza mama na kumuona kuwa bado anaitikadi za kale ila alichozungumza kilikuwa ni cha kweli, pia akaniambia

    "Mnapokaa mbali mbali mnapata radha ya kutembeleana na kuonana kila mara, hata hivyo namjua mwanangu Penina laiti kama tungekaa kwa muda mrefu angegombana na wifi yake tu, sikulitaka hilo mwanangu"

    Nikamwelewa mama ila swala langu la ndoa nikapanga kumuuliza tena.



    Kesho yake nilifanya safari na kwenda kuwatembelea rafiki zangu Suzy na Lucy ambao pia walifika kwenye ile nyumba yetu tuliyohama na kunikosa kwahiyo waliponiona siku ya leo wakafurahi sana.

    Lucy aliniomba msamaha kwa aliyokuwa akiyafanya kipindi kile,

    "Unajua Sabrina hata mimi mwenyewe nilikuwa najishangaa kuwa nimekuwaje, mambo mengi niliyafanya bila kutarajia na mengine ulinipa shutuma bila ya kujua kama niliwahi kuyatenda, kwahiyo Sabrina kama nilikuwa nayafanya kweli basi naomba unisamehe rafiki yangu mpenzi"

    "Usijali Lucy, mimi nimekusamehe sana"

    Suzy naye akatoa utetezi wake kuhusu kutembea na kaka yangu Deo,

    "Kwakweli ile habari ya mimi kutembea na mume wa mtu hata nilishangaa kuwa wewe imekufikiaje Sabrina, nakumbuka uliponiambia nilikujibu kuwa hayakuhusu na uachane na mimi yani sikujua kabisa kuwa habari ile ingekufikia wewe wakati ilinihusu mimi tu"

    Nikamuuliza Suzy kama zile tuhuma zilikuwa za ukweli au uongo,

    "Je ni kweli ulikuwa unatembea na mume wa mtu? Je ni kweli huyo mume wa mtu alikuwa kaka yangu Deo?"

    "Ngoja nikueleze Sabrina ili pia uiambie familia yako ukweli maana huwezi jua kuwa wote bado wananichukia kwa hiyo sababu"

    Nilianza kuyasikiliza kwa makini maelezo ya Suzy ili na mie nielewe ni kitu gani kilichokuwa kinafanyika,

    "Ni kweli nilikuwa natembea na mume wa mtu ila...."

    Nikashtuka na kumuuliza,

    "Ila nini?"

    "Ila hakuwa kaka Deo, huwezi amini Sabrina kaka yako namuheshimu kama kaka yangu na siku zote najua kama ana mke kwakweli nisingeweza kufanya hivyo kabisa"

    "Kwahiyo ulikuwa unatembea na mume wa mtu gani na kitu gani kilikupata?"

    "Kuna mtu mmoja alinitaka kimapenzi ila mwanzoni sikujua kama ana mke wake. Siku moja nilipokuwa naye bar, kaka Deo akaniona na yule mwanaume alipoondoka ndipo kaka Deo akaja kuzungumza na mimi na kunipa tahadhari kama mdogo wake huku akiniambia kuwa yule ni mume wa mtu na yeye anafahamiana nae, nilimwambia kuwa nitalifanyia kazi swala aliloniambia na kumshukuru sana baada ya hapo sikuonana nae tena ila jioni yake ndio wewe ukanipigia simu na kuniambia kuwa niachane na mume wa mtu, nikakujibu kwa hasira kwavile nilikuwa nishachanganyikiwa tayari hata sikujua wewe umeyatoa wapi yale maneno kwani najua kuwa kaka yako sio mmbea kiasi hicho cha kukueleza wewe wakati ameshanionya tayari.

    Nilipochunguza nikagundua kuwa kweli yule mwanaume ana mke wake, nikakutana nae bar siku hiyo kwa lengo la kuachana nae ndipo nikafumwa na mkewe akiwa na rafiki yake. Yule mwanaume akakimbia na kuniachia msala, kisha wakaniburuta hadi karibia na njia ya kwenda kwetu, wakanipiga sana na kuondoka kisha akatokea nyoka alipotokea na kunigonga wakati naugulia yale maumivu ya kupigwa. Wakafika ndugu zangu kunipa msaada ndio muda huo mama akakupigia simu eti muda huo huo yule mtu wako akafika na kusema ametumwa na wewe"

    Hapo ndipo nikausoma ujanja alioutumia yule jini ndiomana akanikataza mimi kupiga simu kwakina Suzy ili nisishtuke kuwa mbona kuna Carlos wawili, Suzy alielezea kwanini ile sababu ikamfanya asimuamini zaidi

    "Eti akanipeleka hospitali, tena hiyo hospitali ndugu zangu walifika mara moja tu na hakuna anayejua hadi leo ile hospitali ilipo kwani ilikuwa hospitali hewa na alinitibia yeye mwenyewe na kunirudisha nyumbani. Kwakweli siwezi kusahau Sabrina"

    Nilisikitika sana kwa akili yangu kuwa gizani kwa kipindi chote kile maana hakuna chochote nilichokuwa naelewa, hata nikieleweshwa na watu mara ngapi ilikuwa kama wanajisumbua tu kwani akili ilikuwa imevurugwa vya kutosha, ikanibidi nipatane na marafiki zangu hawa na kurudisha urafiki wetu kama zamani kwani hali ilikuwa mbaya sana kwa hizi siku za matatizo.



    Tukaenda nyumbani kwa kina Suzy ambapo mara ya mwisho nilifukuzwa na ndugu zake ila leo walinipokea vizuri na kuongea vizuri sana na mimi kwani yote haya yamekuwa ni mojawapo ya mapito katika maisha yetu hapa duniani.

    Tukajaribu kutembea sehemu mbali mbali ambazo tuliwahi kutembea pamoja, na kufurahi sana.



    Niliporudi nyumbani, nikamuomba mama anifanyie mpango wa kazi kule ambako alinifanyia mpango ila nikavuruga kutokana na matatizo.

    Mama akakubali, nilimuomba anifanyie mpango huo ili nitakapoolewa niwe na kazi tayari labda mama ananiuliza kuwa nipo tayari kuolewa tena kwa kuhofia kuwa nitakuwa tegemezi kwa mume na kuzua matatizo mengine katika ndoa yangu ukizingatia sijazoea maisha ya shida kwani mara nyingi huwa napenda kupata nitakacho kwa muda sasa itakuwa ni usumbufu kwa mume atakayenioa kama sina kazi ya kufanya.

    Hapakuwa na matatizo kabisa, ingawa kwa uvivu wetu ila tuliimizana mara kwa mara kufanya ibada kwani yale matatizo yasingeisha kwetu bila ya Mungu kutusaidia.



    Sam alipokuja tena nyumbani swala lake bado lilikuwa moja tu nalo ni kufunga ndoa na mimi na si vinginevyo.

    "Sam usijali ilimradi tunapendana basi ujue tutaoana tu"

    "Ndio tuoane sasa Sabrina, unasubiri nini? Kubali niwatume washenga nyumbani kwenu na mipango ya ndoa ianze"

    "Nipo tayari Sam"

    Alifurahi sana na kunikumbatia, kwa mwanaume mwingine asingetaka tena kuwa na mimi baada ya matatizo yote yale ila Sam alikuwa mwanaume wa tofauti tena mwenye upendo wa kweli juu yangu, alinipenda sana nami nilimpenda sana na ndiomana imekuwa hivi ilivyokuwa.



    Dada yangu Penina akafanyiwa mipango tena na dada Salome kisha akarudishwa kazini, kazi ambayo aliiacha kwa mbwembwe zote kwa madai kuwa amepata kazi inayolipa vizuri zaidi, kazi ya kishetani aliyoifanya bila ya kujua ila sasa ndio anajutia na kuwashukuru wale waliomsaidia ingawa mwanzoni aliwachukia na kuwaona kuwa hawafai kabisa.



    Nilienda kumuuliza mama maswala ya ndoa kwani nilihitaji kweli kuolewa kiukweli na binadamu halisi sio kama yaliyojitokeza mwanzo.

    "Kwani mama hitaji kubwa la mwanamke katika ndoa ni nini?"

    "Ni upendo"

    "Basi mi nimelipata sababu Sam ananipenda sana nami nampenda"

    "Halafu katika ndoa kuna swala zima la malezi, wewe unakuwa mama wa familia na mwanaume anakuwa baba wa familia. Siku zote baba anakuwa kichwa cha familia unapaswa kumsikiliza kwa makini na kufanya anachokwambia na kuacha anachokukataza, mama nae anakuwa kiungo katika familia anapaswa kusikilizwa na pia anapaswa kueleweka. Mkiishi kwa maelewano katika nyumba basi utaiona raha ya ndoa na utaifurahia"

    "Sawa mama, wageni wanakuja kwaajili yangu"

    Nikamueleza tena mama kuhusu nia yangu ya kuolewa, safari hii mama hakukataa tena bali alikubali kwa moyo mweupe kabisa na kunipa baraka zake zote, kwakweli nilifurahi sana kwakuwa mama amekubaliana na mimi katika swala langu la kuolewa tena.



    Siku zilivyopita, nikaitwa katika kazi ambayo mama alienda kuniombea tena kisha nikaanza kufanyiwa majaribio ya ile kazi ili iwe rahisi kwangu katika kuifanya ile kazi.

    Wafanyakazi wa ile kampuni walikuwa karibu sana na mimi kutokana na mahusiano waliyokuwa nayo na baba yangu, kwahiyo nikapata mafunzo kwao kwa ukaribu sana huku maswala na mipango ya ndoa kati yangu mimi na Sam ikiendelea taratibu kwani sikutaka iwe haraka haraka ukizingatia mara nyingi haraka haraka haina baraka.



    Nilienda kwa kaka Deo na kumuomba wifi Joy pamoja na kaka wawe wasimamizi katika ndoa yetu ila wifi Joy alikataa kutokana na hali yake

    "Mmmh Sabrina, na huu mtumbo? Si vizuri kwakweli"

    "Ila mbona kuna wengine wanaolewa na mimba kubwa kabisa wifi yangu sembuse kuwa msimamizi tu!"

    "Kiukweli haitapendeza, hata hao wanaoolewa na mimba kubwa pia huwa haipendezi kwani unaweza kushtukia mtu akizalia ukumbini. Si vizuri kwakweli"

    "Ila mimi nakuomba wifi yangu tafadhari nikubalie hili"

    "Wewe Sabrina ni king'ang'anizi sana huwa unalazimisha kitu bila kujua madhara yake. Haitawezekana, sitaweza kuwa msimamizi wenu"

    Ila sikuacha kumlazimisha na kumbembeleza mpaka mwisho wa siku akakubali mwenyewe kuwa msimamizi wangu, nilimpenda sana wifi yangu huyu na ndiomana nikamchagua yeye kuwa msimamizi wangu.



    Niliporudi nyumbani nikamueleza mama kuhusu wifi Joy kuwa msimamizi wangu ila mama nae akakataa na kusema kuwa si vizuri ila kwavile mimi nilimng'ang'aniza ikabidi akubaliane na mimi tu kwani hata kupinga kwake ni kazi bure. Dada Penina ndio hakutaka kabisa kukubali kuhusu ili ila mwisho wa siku akaniambia

    "Sikio la kufa halisikii dawa"

    Na kuniacha nikiendelea na mipango yangu kama kawaida.

    Kiukweli sikutaka ushauri wa mtu yeyote kuwa wifi Joy hastahili kuwa msimamizi wangu wakati mi mwenyewe niliona kuwa ananifaa sana kuwa msimamizi.



    Nilipokutana na Sam pia nilimuambia kuhusu hili ambapo hakunipinga ila aliacha nifanye vile ninavyotaka mimi ilimradi tu ndoa ya mimi na yeye ifungwe basi.

    Mipango ya ndoa ilienda kwa kasi sana tofauti na nilivyofikiria mwanzo kuwa siku hazisogei ila zilienda kwa kasi sana.



    Kabla ya siku ya ndoa kufika nikamuomba Sam kuwa twende tukaitembelee ile nyumba ambayo mimi na familia yangu tulihama ila Sam akakataa na kusema

    "Ile nyumba mlihama wote kwa sababu yako, ulisema ukiendelea kukaa utakumbuka mambo ya nyuma sasa iweje leo twende tena sisi wenyewe tuliokuwa na majanga?"

    Nikajaribu kumuomba sana Sam kwani kuna vitu nilitaka kwenda kuviangalia ingawa mama alisema tusiende hadi mwaka upite ila mimi bado kuna kitu nilihitaji kujua zaidi.

    Sam akakubali kisha tukapanga siku ya kwenda huko kwenye ile nyumba kuangalia.



    Siku hiyo nikamvizia mama na kwenda kuchukua funguo alipouweka kisha nikaondoka na Sam kwenda kwenye nyumba yetu hiyo.

    Tulivikuta vitu vyote kama tulivyoviacha, tulienda moja kwa moja kwenye chumba alichokuwa akilala mama, nia yangu ni kuangalia lile kabati nililoweka ile droo yenye pesa wakati nimechukua kiasi na kwenda nacho Kigoma.

    Nikatoa lile droo na kushangaa kuziona zile pesa, nikamshtua Sam ili nae azione zile pesa.

    Tulishangaa sana kisha tukazihesabu, zilikuwa milioni tano kwamaana hiyo ile safari ya Kigoma hatukuenda na pesa au alituwekea pesa zingine hapo ndipo maswali yalipojaa kwetu.

    Nikamuuliza Sam,

    "Hivi inawezekana kweli kuwa bado anatufatilia?"

    "Sidhani Sabrina ila kama ni hivyo basi tumeyataka wenyewe"

    "Kivipi?"

    "Nini kimetuleta huku? Tunajua wazi karibia tunataka kuoana sasa itakuwaje kama tumejiletea mikosi wenyewe?"

    Sikupenda kuendelea kujiombea mabaya na kuamua kuondoka eneo lile. Ila hatukumwambia mtu yeyote kuhusu hili.



    Siku ya harusi ilifika na tukafunga ndoa vizuri kabisa kila mtu akafurahia tukio la ndoa yetu.

    Baada ya harusi kama kawaida wapambe wakasema twende ufukweni kwaajili ya kupiga picha za kupendeza na kuvutia, nikakumbuka mambo yale yaliyowahi kunitokea nikaogopa sana kwenda ufukweni ila wapambe walikazana na kufanya nitokwe na machozi.

    Ila kabla hatujaondoka, wifi Joy alianguka na kuanza kutapatapa pale chini.



    Baada ya harusi kama kawaida wapambe wakasema

    twende ufukweni kwaajili ya kupiga picha za

    kupendeza na kuvutia, nikakumbuka mambo yale

    yaliyowahi kunitokea nikaogopa sana kwenda

    ufukweni ila wapambe walikazana na kufanya nitokwe

    na machozi.

    Ila kabla hatujaondoka, wifi Joy alianguka na kuanza

    kutapatapa pale chini.

    Nilishtushwa sana na ile hali ya wifi huku nikiwaza

    kuwa labda mauzauza yamejirudia kutokana na

    kwenda kule kwenye nyumba yetu tuliyohama na

    kuzikuta zile pesa, hofu ikanijaa sana na kujikuta

    machozi yakinikauka na kuanza kujilaumu kwa kile

    ambacho nilimshawishi Sam kuwa tukifanye.

    Harakati za kumbeba wifi ilikumuwaisha hospitali

    zilifanyika, nilikuwa nimeduwaa tu hata sikutaka tena

    kwenda ukumbini ila Sam akanilaumu sana

    "Yote haya umeyataka mwenyewe Sabrina, ulijua

    wazi wifi yako ni mjamzito tena mimba kubwa kabisa

    ukamshawishi hadi awe msimamizi wako umeona

    sasa faida ya ubishi eeh!! Ilimradi tumeshafunga ndoa basi haina shida, tufanye mengine tu"

    Ni kweli nilikatazwa na wengi kuhusu hili ila mimi nikawa mbishi na kufanya yote haya yanitokee kwasababu ya ubishi, ila mama akashauri kuwa tuendelee kusherekea kwakuwa wifi alianguka kutokana na matatizo ya uzazi.

    Sikuwa na raha hadi pale tulipoletewa habari kuwa wifi amejifungua salama ingawa amejifungua kabla ya miezi lakini alijifungua salama kwahiyo ilibidi akae hospitali kuangalia afya ya mtoto aliyehitajiwa uangalizi wa makini sana, watoto wa hivi mara nyingi huitwa njiti.



    Baada ya wiki kadhaa aliruhusiwa kurudi nyumbani, kisha mimi na Sam tukaenda kumtembelea. Wifi alifurahi sana, mtoto wake nae alikuwa amechangamka tayari, alikuwa ni mtoto wa kike. Wifi akasema,

    "Kwavile wewe Sabrina ndiye uliyefanya huyu mtoto azaliwe kabla ya siku zake basi namuita Sabrina"

    Nikacheka sana na kufurahi kupata wajina, Sam akamwambia wifi kwa kumtania

    "Shauri yako, atakuwa na majanga kama ya Sabrina mwenzie"

    Wifi akacheka sana kuhusu alichokisema Sam na kusema

    "Mmh! Atakuwa na majanga tena mmh ila yasiwe kama ya Sabrina jamani"

    "Ndio hayatakuwa kama ya Sabrina ila lazima atakuwa na majanga sababu mwenye jina lake ana majanga sana"

    Dada Penina nae alifika kumuona wifi Joy na kutukuta na ile mada yetu tuliyokuwa tukiizungumzia kisha akadakia na kusema

    "Ila ndio atapendwa hadi na watoto wadogo maana mwenzie kapenda hadi na majini na...."

    Nikamkatisha na kuguna

    "Mmmh dada!!"

    "Mmh kitu gani kwani uongo? Hebu nipeni Sabrina mdogo nimbebe mie"

    Akamchukua mtoto na kumpakata kwa furaha na tangia hapo huyo mtoto akaitwa Sabrina mdogo.



    Maisha yakaendelea huku mawazo ya ile pesa kwenye kabati yakinisumbua kwani sikuelewa kama zile pesa ni za kweli au ni pesa mauzauza, sikuelewa kama ni yule jini ameziweka au ni vipi kwahiyo nikajikuta nikiwa na mawazo muda wote na huku nikiwa na hamu ya kujua kwanini tulizikuta siku ile tuliyoenda.

    Nikatamani sana kwenda kuzichukua na kuziangalia vizuri, nikajipanga kufunga safari kimya kimya kwa kuhofia kuwa Sam asijui.



    Siku hiyo nikajiandaa bila hata ya kumuaga Sam na kuondoka hadi pale tulipokuwa tunaishi zamani.

    Njiani nikakutana na dada Zuhura ambapo alifurahi kuniona na kuniuliza

    "Unaenda wapi Sabrina?"

    "Nafika kwenye nyumba yetu mara moja"

    "Unaenda kufanya nini?"

    Nikawaza moyoni kuwa kama nikimwambia kuhusu pesa basi lazima atataka twende wote ili tugawane, ikabidi nimwambie vitu vingine kwa kumgelesha tu. Kisha akaniuliza,

    "Unadhani ni salama wewe kwenda mwenyewe?"

    "Ndio dada hakuna tatizo"

    "Mmh Sabrina! Ila kama utahitaji msaada usisite kunipigia simu na kunipa taarifa, sawa?"

    "Sawa dada, ila kuna tatizo kwani?"

    "Sijui, ila nisingependa kukushauri kwenda peke yako"

    "Usijali dada, nitakuwa salama"

    "Kumbuka ibada Sabrina"

    Kisha akaondoka, nikaona kama anataka kuniharibia siku na mipango yangu tu kwahiyo nikashukuru kuondoka kwake kisha mimi nikaendelea na safari yangu huku moyo wangu ukiniambia kuwa nimejawa na tamaa, na kweli nimejawa na tamaa kwani yote haya ni sababu ya tamaa iliyonizunguka na ndiomana najikuta nikifanya haya ninayoyafanya, amakweli binadamu hatujakamilika kila mmoja na kasoro zake sema tu tumezidiana.



    Nilipo ukaribia mlango wetu na kutaka kufungua, mkono ukasita ila nikajipa moyo na kufungua mlango ule kisha nikaurudishia na kuingia ndani ambako nilikukuta kama ambavyo tulikukuta wakati nilipokuja na Sam.

    Moja kwa moja nikataka kwenda chumbani kwa mama ila roho ikasita, nikatazama mezani na kuona kitu kilichoyavuta macho yangu.

    Nikasogea na kukiangalia, ilikuwa ni pete yani pete ile ile niliyoveshwa ya uchumba na yule jini.

    Nikashtuka sana, nikaishika na kuiangalia vizuri nayo ilikuwa iking'aa vile vile kama ambavyo ilikuwa iking'aa mwanzoni.

    Nikaichukua na kuishika mkononi kisha nikaenda chumbani kwa mama kwenye kabati moja kwa moja na kutoa ile droo nikazikuta zile pesa zikiwa vile vile, nikatabasamu kwani najua ile ni mali yangu na kufanya niwaze vitu mbali mbali kichwani kuwa ingawa nilipata mateso kumbe na faida ipo. Nikachukua zile pesa na kujaza kwenye pochi yangu kisha nikajisemea kuwa,

    "Hii ni faida yangu, hizi pesa ni zangu na hii pete nitauza ili nipate pesa zaidi"

    Macho yangu yakavutika kuwa nitazame upande mwingine wa kile chumba, nikaviona vile viatu vyangu vya maajabu hapo nikaogopa sasa na kutetemeka kwani vile viatu hata kumbukumbu kuwa mara ya mwisho nilivivulia wapi na ilikuwaje sikuwa nayo ila sasa ndio vipo mbele yangu, je vimetokea wapi? Nani kavileta? Maana kipindi kile Carlos alisingiziwa kuyatenda yote yale kumbe ni yule jini aliyekuwa akipitia kwa Carlos, swali kwangu je yule jini bado ananifatilia? Na kama ananifatilia ni kwa misingi gani?

    Sauti ikanijia,

    "Uza na hivyo uongeze idadi ya pesa zako"

    Nikaogopa sana na kuamua kuinuka ili nitoke nje maana nilijua ni chumba changu tu chenye majanga kumbe hadi chumba cha mama.



    Nilitoka hadi sebleni napo nikashtuka pia, kwani nilikuta lile gauni la harusi yangu na jini likiwa limewekwa kwenye kiti.

    Kiukweli lile gauni lilikuwa zuri sana ila kutokana na mambo ambayo yalinitokea lile gauni lilikuwa baya machoni mwangu kama vile viatu vya maajabu ambavyo navichukia ingawa ni viatu vizuri sana tena vya gharama.

    Nikaliangalia lile gauni mara mbili mbili huku nikiogopa kulisogelea, ile pete mkononi nilihisi kama inatingishika hivyo nikaamua kuirudisha mezani pale pale nilipoichukua ili niondoke nikiwa huru.

    Nikakuta ujumbe mezani,

    "Uliolewa na jini bila ya kutarajia ila sasa jiandae kuolewa tena na jini kwa kutarajia maana unavitu vyake bado na nia yake kwako unaijua, utaolewa na na jini kwa kutarajia sasa"

    Nikatetemeka sana na kujua wazi nimejitakia mwenyewe haya mambo na sasa sina pa kukimbilia kwamaana nipo mwenyewe ingawa nishaolewa na mtu mwingine tayari.

    Nikajisemea mwenyewe, ila mimi nimeshaolewa tayari!

    Sauti ikasikika,

    "Hata mwanzo ulishaolewa tayari ila ukafanya hila na kuolewa na mwingine hata sasa itakuwa hivyo, unanikataaje mimi wakati vitu vyangu bado unavipenda?"

    Nikaangusha ule mkoba wenye hela chini na kujihisi kama naanza kuwehuka vile.

    Nikatazama tena mezani, nikaona ile simu yangu ya majanga hapa ndipo nilipotambua kuwa kweli nafatiliwa tena na yule jini, nikaanza kuilaumu tamaa ya moyo wangu na kuanza kujisemea

    "Mungu nisaidie"

    Huku nikiwa na mawazo kwani sikuweza kusogea mbele wala kurudi nyuma, nikasimama pale pale kama mlingoti huku nikiangalia yale mauzauza ya mbele yangu.



    Wakati nikishangaa yale mambo, nikahisi kushikwa bega na mtu. Hapo hapo miguu ikakosa nguvu na kujikuta nikianguka chini na kupoteza fahamu.

    Akaja yule mbaba wa kutaka kunisaidia na kuniambia

    "Kwanini kuiruhusu tamaa ikutawale? Kwanini utake kuharibu maisha yako kwa vitu vidogo? Una mume, una kazi pia, inakupatia kipato, ridhika na ulicho nacho. Fanya kazi kwa bidii kujiongezea kipato, hizi njia za pembeni zitakuangamiza Sabrina. Zitakuponza, kutenda kosa si kosa bali kurudia kosa, ulishayapitia yote haya kwahiyo usifanye tamaa yako kukurudisha tena ulikopita. Yote yaliyokupata mwanzo hukuyatarajia, ila hili ambalo lingekupata leo ungeritarajia sababu umejitakia mwenyewe. Tulia binti utengeneze maisha yako, haya uyatakayo sasa yatakuponza. Mshukuru yule aliyekuona ukienda mwenyewe kwenye mdomo wa mamba"

    Nikashtuka huku jasho likinitoka sana, nikamuona Sam pembeni yangu na dada Zuhura akiwa pembeni na mzee mwingine ambaye sikumfahamu kwa muda huo ambapo walinisaidia na kufanya nikae vizuri huku nikiwatazama, walinipa pole kwa yote yaliyonitokea.



    Nikawasimulia kila kitu nilichokikuta kwenye ile nyumba yetu, dada Zuhura akaniambia

    "Nilijua wazi kama ile nyumba bado haijatengemaa ndiomana nikakukataza Sabrina, nazijua tabia za majini wanamtindo wa kumtamanisha mtu ili aingie katika vishawishi ndiomana nikakuuliza vizuri unachoenda kufanya ila wewe hukutaka kuniambia ukweli. Ile nyumba yenu mlishamkaribisha jini ndani kwamaana kwamba alishaitawala, mlichotakiwa kufanya ni kusema vitu vyake vyote ili vichomwe moto na nyumba iwe huru"

    Nikakodoa macho tu kwani tamaa ndiyo imeniponza, ikabidi nimuulize Sam kuwa alijuaje kama nipo kule.

    "Nilipokukosa nikaenda kwenu kukuulizia ila hukuwepo, nikapatwa na hofu kuwa umeenda pale kwenye nyumba ndiomana hujaaga kwani unajua wazi ningekukatalia, wakati nakuja nikakutana na dada hapa ambapo akaniambia ni kweli umekuja mitaa ya huku basi ndio tukaongozana kuja kukufata. Yani tunaingia tu na wewe unaanguka chini, kwakweli Sabrina wewe una mambo ya ajabu na hata hujihurumii. Ndio tumekubeba hadi kwa Shekhe hapa amekusomea hadi umeamka na kuwa katika hali ya kawaida"

    Kwakweli nina majanga ila haya ya sasa yalikuwa ya kujitakia kweli.

    Dada Zuhura akanishauri mambo mbali mbali pale, kisha nikarudi nae hadi kwa mama ambako akawashauri cha kufanya na nyumba yetu pia.



    Baada ya wiki kadhaa, tulichoma vyote vilivyotupa mashaka hadi zile pesa kisha tukaibomoa ile nyumba na kuuza kile kiwanja, kisha kununua kiwanja kingine kama kumbukumbu ya kiwanja tulichokiuza.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    Nilipata ujauzito na kujifungua mtoto wa kike, nikamuita Zuhura kama kumbukumbu ya huyu dada katika maisha yangu.

    Dada yangu Penina pia alipata mchumba na kuolewa kisha akapata ujauzito na kujifungua mtoto wa kike aliyemuita Salome.

    Tulifanya hivi kutokana na mambo ambayo hawa watu walitutendea ingawa tuliwanena vibaya na kuwaona ni watu wabaya ila wao bado walitupenda na kuendelea kutufundisha mambo ya Mungu.

    Wifi yangu Joy nae alijifungua watoto wengine ambao walikuwa mapacha wa kiume na kuwaita mmoja Deo na wa mwisho Sam, kwahiyo akawa na watoto wanne, James, Sabrina, Deo na Sam huku Sabrina akiwa mtoto wake pekee wa kike.

    Mume wangu Sam akanishauri kuandika haya niliyoyaandika.



    ~~~~MWISHO~~~~

0 comments:

Post a Comment

Blog