Search This Blog

MTEMI NYANTUMU - 5

 

    Simulizi : Mtemi Nyantumu

    Sehemu Ya Tano (5)







    Jeshi kubwa lilikuwa safarini kusonga mbele kumsaka Nyoni pamoja na dada yake. Mara baada ya kuzika kwa heshima maiti za ndugu zao waliouawa usiku uliopita katika shambulio la wenyewe kwa wenyewe kabla hawajatambuana, huku kundi la watu wachache likiwa limebeba ndugu zao ambao walijeruhiwa katika tukio hilo …



    “Mnyama yoyote atakaye wasogelea tenganisheni kichwa chake, halafu kuweni makini kufuatilia kila hatua ambayo mbwa wanaipiga …”,



    Mtemi Nyantumu aliwasihi vijana wake kutomuhurumia mnyama yoyote yule atakayejaribu kuzuia msafara wao, huku akiwasihi kufuatilia kwa umakini mbwa waliokuwa wakiwaongoza na kunusa nyayo ambazo Matumaini na dada yake waliweza kupita …



    “Sawa mtemi,igweee”,



    Jeshi la mtemi Nyantumu kwa ushirikiano, walionesha nikiasi gani wako pamoja na mtemi wao kwa kuitikia kwa sauti ya juu iliyopelekea mwangwi kusikika kila kona ya msitu huku wakipiga hatua ndefu kuelekea kijiji cha Ukarimu kumfuatilia Nyoni pamoja na dada yake…



    ………………………………



    Kutokana na umbali mfupi wa takribani kiromita kumi na tano pekee, jeshi la kijiji cha Ukarimu lilianza kuingia mwanzoni mwa msitu wa Nyankonko …

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kutokana na uhodari wao katika vita, hawakuogopa jambo lolote lile. Japo wengi wao walisikia historia tu kuhusiana na pori la Nyankonko bila kushuhudia maajabu ya pori hili kwa macho …



    Bila kutegemea walikuta kundi kubwa la chui wakiwa wamejaa barabarani. Lengo na madhumuni yao makuu, ni kuzuia kiumbe chochote kile kitakacho jaribu kukanyaga ardhi ya Nyankonko kwa lengo la kutaka kumuokoa mzimu Ntema kutoka mahali alipokuwa ametupwa,ili kupelekwa mahali salama kitendo ambacho kingehatarisha utawala wa ukoo wa Nyantumu dhidi ya kijiji cha Mwantema …



    “Tushambulie!! “,



    !acha! acha! Wanyama gani wakubwa kiasi hiki! inawezekana kuna mbinu za kishirikina tunafanyiwa, ngoja tutumie nguvu zetu za kichawi kuwagundua! “,



    “Hata mimi naamini hivyo! tangu nisimuliwe maajabu ya msitu huu sijawahi kukubaliana nao. Kwahiyo fanyeni jambo lolote tuwatambue! “,



    “Lakini simliambiwa mzimu Nkuru aliwaweka wanyama hawa kuulinda msitu, pasiwepo na binadamu yoyote wa kuingia ama kutoka ndani ya msitu huu “,



    “Ndio! “,



    “,Basi kama jibu ni ndio, wanyama hawa wametengenezwa kishirikina ndio maana wanatisha namna hii. Tunachotakiwa kufanya nikuwaua kishirikina …”,



    “Kweli mkuu, hapo umenena!! “,



    Hatimaye kwa uwezo mkubwa wa kufikili na kushughulisha vichwa. Jeshi la kijiji cha Ukarimu waliamua kutoa siraha zao za mapembe ya ng’ombe kwa ajili ya kuwashambulia chui, chui ambao waliamini kwa asilimia mia moja walitengenezwa kishirikina!



    “Poooooh! Pooo! pooooo! Poooo! “,



    Sauti zenye mpangilio wa kupanda na kushuka zilisikika, baada ya jeshi la kijiji cha Ukarimu kuchukua mapembe yao ya ng ‘ombe na kuanza kupuliza kwa ushirikiano wa hali ya juu.Siraha ambazo zilitumika kupambana na viumbe hatari waliotengenezwa na kuumbwa kishirikina …



    Katika hali ya kushangaza,chui wale ambao walikuwa bado wakishangaa tu wakilisubili jeshi la Ukarimu litakapo taka kupita ili waweze kuwaanzishia vurugu.Damu zilianza kutoka katika masikio yao kutokana na mlio mkali wa mapembe haya yaliopulizwa kwa pupa! Kitendo ambacho kilipelekea chui mmoja baada ya mwingine kudondoka chini kisha kupoteza maisha.



    Nyankonko;

    Jeshi la kijiji cha Ukarimu liliendelea kupuliza pembe zao za ng'ombe, siraha ambazo walizitumia kupambana na maadui waliotengenezwa kishirikina. Kadri walivyo zidi kupuliza pembe hizo, chui mmoja baada ya mwingine waliendelea kutokwa damu katika masikio yao kutokana na mlio mkali wa pembe hizi, kiasi kwamba kwa muda wa takribani dakika kumi na tano, chui wote ambao walikuwa wamezuia njia waliweza kupoteza maisha …



    "Tusonge mbele, nazani mmeshatambua kuwa viumbe wote wa pori hili wametengenezwa kichawi na mzimu Nkuru, kwahiyo mtakapo muona mnyama yoyote pulizeni pembe hizi kumuua kirahisi. Mkitumia mikuki na mishale, kazi ya kupambana nao itakua ngumu kwenu na pengine mnaweza kujeruhiwa. ",



    "Ndio mkuu, igweeeh ",



    Jeshi la Ukarimu waliendelea kuonesha ushirikiano wao, kwa pamoja waliitikia amli ya kiongozi wao mara baada ya kuhakikisha chui wote waliokuwa wamezuia njia ya kuingia pori la Nyankonko wakiwa wamegeuka mizoga …



    Bila kupoteza hata sekunde, jeshi la kijiji cha Ukarimu liliendelea kusonga mbele kuingia katikati ya msitu bila kutambua kuwa walikuwa wakifuatiliwa na wanyama wengine wadogo wenye sumu kali sana. Wanyama waliotumwa na mzimu Nkuru kwa mara nyingine tena …



    ....…………………………………



    Nyoni pamoja na Matumaini waliendelea kukaza mwendo kulipita pori la Nyankonko, kwani ulibakia muda mchache waweze kulimaliza pori hili. Ghafla Nyoka wengi sana, pamoja na ng'e walitokea katika vichaka vya pori la Nyankonko na kuwavamia Nyoni pamoja na Matumaini…



    Wanyama hawa walikuwa wengi kupita kiasi, na kuanza kuwavamia Nyoni pamoja na dada yake kisha kutambaa katika miili yao. Jiwe la mzimu Nkuru lilitoa mionzi mikali yenye kung'aa, mionzi ambayo ilishindwa kufua dafu na kuwadhuru wanyama hawa hatari waliotumwa na mzimu Nkuru. Kwani nguvu za mzimu Ntema zilikuwa zimeshafifia kupita kiasi, kitendo ambacho kilipelekea nyoka wale pamoja na ng'e kuendelea kutambaa katika miili ya Nyoni pamoja na dada yake …

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Nyoni pamoja na Matumaini walishtuka sana, kwani nyoka hawa walikuwa wengi na waliwavamia kwa wakati mmoja, bila shaka walitambua walitumwa na mzimu Nkuru. Nyoni alisahau maneno aliyoambiwa na mzimu Ntema kuwa hanauwezo wa kupambana na nyoka hawa, lakini maji aliyowapita wanywe lazima yangewapatia ushindi. Lakini Nyoni hakukumbuka neno hata moja, aliendelea kujitahidi kuwatoa katika mwili wake Nyoka na ng'e ambao walikuwa wakimtambaa mwilini. Hakuishia kwake tu, bali alimsaidia hata dada yake kuwazuia wanyama hawa wasimdhuru huku akitumia panga lake kali aina ya jambia kuwakata kata na kuwazuia bila mafanikio …



    "Huwezi kupambana nao, lakini usihofu hawawezi kuwadhuru kutokana na maji mlio kunywa …",



    "Hawawezi kutudhuru wakati unaona wanataka kumdhuru dada yangu pamoja na mimi! ",



    "Amini maneno yangu nayo kwambia, kamwe hawawezi kuwadhuru ",



    Nyoni alishindwa kuamini maneno ya mzimu Nkuru hata kidogo, kwani wanyama wale hatari walikuwa wamemkunja vilivyo Nyoni japo alijitahidi kujitetea, na kumsaidia dada yake bila mafanikio …



    Katika mazingira yasiyo tarajiwa na wanyama hawa hatari waliotumwa na mzimu Nkuru, walijikuta wakidondoka chini na kupoteza maisha mmoja baada ya mwingine. Mara baada ya kujaribu kumng'ata Nyoni pamoja na dada yake, kwani walipigwa na shoti iliyowateketeza kama mchwa …



    "Duuuh maajabu haya sijawahi kuona, kweli mzimu Ntema wewe ni mungu wetu …",



    "Hata mimi siamini kama nimepona, nilikua nasubili kifo tu. ",



    Matumaini pamoja na kaka yake walizungumza huku wakishaangaa miili yao ikipiga shoti kila ng'e yoyote au nyoka alipojaribu kuwang'ata ili awadhuru, jambo ambalo liliwafanya waamini msaada wa maji waliyokuwa wameambiwa wanywe kama ulinzi wao na mzimu Ntema …



    Muda mfupi tu, wanyama walio wavamia walikuwa wameteketea na kukauka kama chapati iliyo kaangwa katika moto mwingi. Jambo ambalo liliwafanya kuendelea na safari yao, huku mapigo ya mioyo yao ikipungua mwendo kasi wake kwani hawakuamini kama walikuwa wameponyoka kutoka katika hatari …



    ………… ….……………………



    "Shambulia, puliza pembe zenu haraka iwezekanavyo!! ",



    Ghafla wanyama wengine walilivamia jeshi la mtemi wa kijiji cha Ukarimu, wanyama waliotumwa na mzimu Nkuru. Wanyama hawa waligawanyika mwanzoni wakati wakiingia katika pori hili la Nyankonko na kugawanya majukumu, wengine walilifuatilia kundi la askari wa kijiji cha Ukarimu, huku wengine wakiwafuata Nyoni pamoja na Matumaini …



    "Hawafi! pembe zetu hazifanyi kazi ",



    "Ninasema msikate tamaa, endeleeni kupuliza kwa umoja ili kelele ziathiri masikio yao …",



    Hali ya sintofahamu iliwakumba askari wa Ukarimu, kwani licha ya kutumia mapembe yao ya ng'ombe kupambana na wanyama hawa, lakini nyoka pamoja na ng'e waliendelea kuwasogelea kwa ajili ya kuwadhuru. Kiongozi wao aliziamini siraha zao, aliwahimiza askari wake kushirikiana kwa pamoja kupuliza siraha zao bila kufahamu kuwa nyoka hawa pamoja na ng'e walitengenezwa na kupatiwa nguvu nyingi na mzimu Nkuru tofauti na wanyama wa pori la Nyankonko.



    "Yalaaah "



    "Nakufaaah! ",



    "Twafaaah "",



    ",Uwiiih ",



    Hatimaye jeshi la kijiji cha Ukarimu walijikuta wakishambuliwa na kung'atwa na nyoka pamoja na ng'e wenye sumu kali. Kwani siraha zao zilishindwa kufua dafu mbele ya wanyama hawa hatari waliotumwa na mzimu Nkuru …http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



    …………………………………



    Hatimaye Nyoni pamoja na Matumaini mara baada ya kuponyoka kutoka katika mikono ya wanyama wadogo sana na hatari waliotumwa na mzimu Nkuru, walianza kukalibia mwisho wa pori la Nyankonko. Bila kutegemea walijikuta wakisikia kelele na sauti za maumivu, jambo ambalo liliwafanya kukimbia eneo la tukio kushuhudia watu ambao walikuwa wakiomba msaada …



    "Wasaidieni, wapatie kibuyu ……",



    "Sawa mzimu Ntema igweee, "



    Jiwe ambalo lilikuwa limeshikwa na binti mrembo sana Matumaini, jiwe la ajabu la mzimu Ntema. Liling'aa na kutoa mwanga mkali ulioumiza macho ya binadamu yoyote yule aliyelitazama kwa pupa, na kutoa amli kwa kijana hodari Nyoni kuwapatia kibuyu cha maji askari ambao walikuwa bado hawaja jeruhiwa. Mara baada ya kufika eneo la tukio, na kushuhudia askari wa kijiji cha Ukarimu wakiteketezwa na wanyama wenye sumu kali walio tumwa na mzimu Nkuru …



    Kwa uhodari na ushujaa mkubwa, Nyoni alirusha kibuyu kwa mkono wake wa kulia. Kibuyu ambacho kilipokelewa na kiongozi wa jeshi la Ukarimu. Askari aliyechaguliwa na mtemi wao, na kupewa uongozi wa jeshi la kijiji cha Ukarimu kutokana na umbile lake kubwa lililo tisha na kuogopesha binadamu yoyote yule. Kwani alikuwa mnene, mrefu na isitoshe alikuwa mweusi kupitiliza. Sifa ambazo zilimfanya aonekane shupavu na hodari …



    "Kunyweni! kidogo kidogo, mpatie na wenzako …",



    Nyoni alimpatia maelekezo kiongozi wa kijiji cha Ukarimu, huku Nyoni akiwasaidia kuwazuia nyoka na ng'e kwa kutumia panga lake wasiwadhuru askari wa Ukarimu. Askari yule alitii maagizo aliyopewa ili kujiokoa mwenyewe pamoja na jeshi lake, japo takribani askari wake kumi walikua tayali wameng'atwa na wanyama hawa kisha kupoteza maisha. Kwani walikuwa na sumu kali kupita kiasi, sumu ambayo ilikausha damu mara moja ilipoingia katika mwili wa binadamu.



    Vita kali iliendelea katika pori la Nyankonko, askari wa jeshi la kijiji cha Ukarimu waliendelea kuyapigania maisha yao wakisaidiwa na kijana hodari Nyoni …



    Kwakuwa walikuwa wameshatambua kibuyu chenye maji walichopewa na Nyoni kilikuwa ni ukombozi wao, kila askari alijitahidi kuepuka kung’atwa na nyoka pamoja na ng’e hatari huku akitumia panga kuwazuia. Yoyote yule aliyekuwa bado hajanywa maji yaliyokuwa katika kibuyu cha Nyoni, alipoteza maisha papo hapo alipojeruhiwa na wanyama hawa waliotumwa na mzimu Nkuru.



    Kwa uhodari na ushupavu wa hali ya juu, askari wote wa kijiji cha Ukarimu walipokezana kibuyu na kunywa maji ambayo ndio ulinzi pekee kuwaepusha na balaa ambalo liliwakumba. Kitendo ambacho kilipelekea vifo kupungua kwa askari wa kijiji cha Ukarimu …



    Hatimaye jitihada za kujikomboa zilianza kuzaa matunda, japo askari wengi sana takribani therathini wa kijiji cha Ukarimu walikuwa wamepoteza maisha ,lakini hawakuwa na sababu ya kumshukuru Nyoni pamoja na mzimu Ntema kwa msaada uliofanikisha kuyaokoa maisha yao …



    “Naitwa Nyoni na huyu ni dada yangu anaitwa Matumaini, bila shaka mlikuwa mnatambua ujio wetu katika kijiji chenu ……”,



    “Mimi naitwa Kamanda Lunzwoka, ni kiongozi mkuu wa jeshi la kijiji cha Ukarimu. Ndio tulitambua ujio wenu, lakini tuliwasubili kwa miaka mingi bila mafanikio. Tukaamua kuja wenyewe katika msitu huu kumtafuta mzimu Ntema,ili tuanze harakati za kukomboa kijiji chenu kutoka katika utawala unaohimiza mila potofu na hatari …”,



    “Basi sawa, nashukuru sana. Kilichobakia nikurudi kijijini kwenu na kukamilisha hatua ya mwisho ya kukikomboa kijiji changu …”,



    “Bila shaka, ndio jambo muhimu na la pekee lililobakia. Nawashukuru sana kwa kutusaidia kuepuka kifo cha nyoka hawa japo wengi sana wamepoteza maisha yao. “,



    “,Mimi sio wa kunishukuru, anayepaswa kupatiwa pongezi ni mzimu Ntema kwa kutupatia siri ya kujilinda, tunapaswa kumtendea haki kwa wema wake huu kuhakikisha anarudi kuwa mtawala wa Mwantema “,



    Yalikuwa ni mazungumzo yaliyoendelea kati ya kiongozi mkuu wa jeshi la kijiji cha Ukarimu aliyeitwa Lunzwoka, huku  Matumaini pamoja na umati wote wa askari wa kijiji cha Ukarimu wakiwa kimya kusikiliza mazungumzo yao. Hawakuwa na muda wa kupoteza katika mazungumzo yao, waliamua kuanza safari ya kuelekea kijiji cha Ukarimu bila kutambua kuwa walikuwa hatarini kushambuliwa na askari wa mtemi Nyantumu kwani walishuhudia kila kitu kipindi mapigano yao na nyoka yakiendelea.



    …………………………………



    Jeshi la mtemi Nyantumu waliamini uwezo wa Nyoni katika mapambano, hawakusita kukiri ushupavu wa kijana huyu ambaye alionekana hatari kupita maelezo. Askari wa mtemi Nyantumu wakiwa wamebeba askari wenzao waliokuwa wamejeruhiwa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe, huku askari wanne wakiwa wamembeba mtemi Nyantumu aliyekuwa ameketi na kustarehe katika kiti chake. Ghafla walishuhudia lundo la nyoka wengi aina ya koboko pamoja na ng’e wakiwa wameuawa kikatili, huku miili yao ikionekana kukaushwa …



    “Mtoto huyu kuna nguvu ya ziada anaitumia, sio bureee!! “,



    Mtemi Nyantumu hakusita kumlaani Nyoni kwa mauaji yale, huku roho ya uoga ikimtawala. Aliamini kwa asilimia mia moja mkufu aliopatiwa na mama yake na kuuvaa shingoni, mkufu ambao hata Matumaini alikuwa ameuvaa kitendo kilichowafanya wasidhruke na mzimu Nkuru. Ndio ambayo ilisababisha Nyoni kuwaua wanyama wengi wa pori la Nyankonko kikatili …



    “Mimi tangu nishuhudie chatu yule aliyeuawa, nilimvulia kofia kijana huyu …”,



    “Toka hukoo mpuuzi wewe! uoga tu!  hebu songa mbele tuondokee tukatenganishe kichwa na kiwiliwili chake kabla hajatoka ndani ya msitu huu. “,



    “Lakini mtemi ninaongea kwelii, nina imani atakuwa amefanikisha kumuokota mzimu Ntema, na anamsaidia kujilinda …”,



    “Nimesema toa upuuzi wako hapa, unasababisha wenzako wawe waoga kama wewe. Hebu songa mbelee! “,

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mtemi Nyantumu japo aliingiwa na hofu kuhusiana na Nyoni katika moyo wake, lakini alishindwa kuonesha uoga wake waziwazi mbele ya askari wake. Hasa askari ambaye alionekana kubishana naye, japo aliyokuwa akiyazungumza yalikuwa na ukweli kwa asilimia mia moja. Neno ambalo aliambiwa kuhusu Nyoni pengine alifanikiwa kumpata mzimu Ntema msituni, lilipenya katika masikio yake na kusababisha ubongo wake kuvurugika .Aliamini maneno aliyoambiwa yalikuwa na ukweli ndani yake, kitendo ambacho kilimfanya kuwahimiza askari wake kusonga mbele haraka sana ili kumshambulia na kumuua Nyoni kabla hajafika kijiji cha Ukarimu. Kwakuwa askari wake wali itambua hasira ya mtemi Nyantumu iliyojionesha katika macho yake, walitii maagizo yake kukwepa kifo na kusonga mbele kumzuia Nyoni kutoka nje ya pori la Nyankonko …



    …………………………………



    Jeshi la mtemi Nyantumu lilichapa mwendo zaidi ya kawaida, kitendo ambacho kilipelekea muda mwingine kukimbia kwa lengo moja tu, kumuwahi Nyoni kabla hajatoka ndani ya msitu na mzimu Ntema na kusababisha utawala wa Nyantumu kuporomoka. Mtemi Nyantumu hakufumba mdomo hata mara moja, muda wote aliongea kama chiriku ili kulihimiza jeshi lake kusonga mbele kumzuia Nyoni, jitihada ambazo zilizaa matunda. Kwani katika umbali wa mita takribani mia mbili, mbwa wao walisitisha kubweka ghafla baada ya kuhisi uwepo wa maadui zao ,umbali ambao ulikuwa mfupi sana. Harufu ya Nyoni ilipulizwa na upepo mpaka katika matundu ya pua ya mbwa wa jeshi la mtemi Nyantumu, na kujikuta mbwa hawa wakisimama huku wakifumba midomo yao ghafla na kuacha kubweka.



    “Mbona hamtembei nyau njinyi, nimesema songeni mbelee! “,



    “Hapana mtemi, mbwa wamesimama na kuzuia msafara ……”,



    “Sasa kama wamesimama si ukashuhudie nini kinaendelea. Askari gani wewe unashindwa kutambua fikra na hisia za mbwa wako! “,



    Askari mmoja aliyekuwa akiliongoza jeshi la mtemi Nyantumu, alianza kujongea taratibu kusogea sehemu ambayo mbwa wao walikuwepo. Aliweza kuwapita na kusogea mbele zaidi, kitendo ambacho kilipelekea kutokua amini kile alichokiona. Alishuhudia jinsi Nyoni alivyokuwa akitumia upanga wake kuwazuia nyoka wa ajabu kumdhuru, na kila nyoka aliyejaribu kumdhuru Nyoni alipigwa na shoti ya ajabu. Kitendo ambacho kilipelekea nyoka yule kufa na kukauka.



    Askari yule wa mtemi Nyantumu aliona ni bora kuwafahamisha wenzie, bila kuchelewa alitumia ishara za kijeshi kuwaita askari wenzake pamoja na mtemi Nyantumu. Ndani ya sekunde chache tu, mtemi Nyantumu pamoja na jeshi lake walikuwa makini kutazama vita baina ya Nyoni, askari wa Ukarimu dhidi ya nyoka pamoja na ng’e hatarii …



    Mtemi Nyantumu kwa mara ya kwanza aliweza kushuhudia jiwe la mzimu Ntema ambalo liling’aa sana na kutoa mionzi mikali. Jiwe ambalo lilikuwa limeshikwa na Matumaini katika mkono wake wa kulia, mtemi Nyantumu hakuwahi kuliona zaidi ya kusimuliwa na baba yake pamoja na babu zake, kuwa babu yao aliyeitwa Nyantumu ndiye aliyetupa jiwe la mzimu Ntema katika pori la Nyankonko kisha ukoo wake kuingia madarakani. Hivyo basi, walirithishana utemi huku wakitumia jina la Nyantumu na kusimuliana siri za utemi wao.



    “Mdogo wake Nyoni ni mrembo na mzuri sana, halafu kumbe jiwe la mzimu Ntema linaongea kweli, mimi nilikuwa siamini niliyokuwa nasimuliwa …”,



    “Hebu acheni ujinga wenu, angalieni siri za upambanaji wake na sio kusifia upuuzi “,



    Mtemi Nyantumu alimfokea mmoja wa askari wake aliyeonekana kupenda wanawake kupita kawaida, askari aliyewahi kuahidi kumubaka Matumaini mbele ya kaka yake Nyoni watakapo watia nguvuni. Kwa uwoga mkubwa, askari yule na wenzake waliendelea kushuhudia vita ile huku askari wengi wakishangaa uzuri wa Matumaini pamoja na jiwe la mzimu Ntema …



    Nyankonko;



    Jeshi la mtemi Nyantumu wakiwa wamejificha kwenye vichaka, waliendelea kufuatilia kila hatua ya vita vya Nyoni, jeshi la Ukarimu dhidi ya nyoka hatari waliotumwa na mzimu Nkuru. Walishangazwa sana kwani nyoka wote pamoja na ng’e walikufa na kisha kukauka kila walipojaribu kuwang’ata Nyoni na askari wa Ukarimu. Kitendo ambacho kiliwafanya watambue kuwa maji yaliyokuwa kwenye kibuyu cha Nyoni ndiyo yaliyofanikisha mauaji ya wanyama hao hatari. Jeshi la mtemi Nyantumu hawakuchoka kushuhudia kila jambo ambalo lilifanyika na Nyoni pamoja na wenzie, na kupelekea kugundua kuwa mzimu Ntema ndiye aliyefanikisha mauji ya nyoka kupitia mazungumzo ya Nyoni na Lwanzoka, kwani Nyoni alisema maji aliyowapatia kwenye kibuyu mzimu Ntema ndie aliyemfahamisha Nyoni kuhusu jambo hilo …



    “Wanataka kuondoka, kila mmoja achukue siraha zake tuwashambulie “,



    Mtemi Nyantumu aliamrisha jeshi lake kwa sauti ya chini ambayo haikusikika na mtu yeyote zaidi ya jeshi lake, kwani aliwashuhudia askari wa Ukarimu pamoja na wakina Nyoni wakijiandaa kuondoka kuelekea Ukarimu …



    Hali ya ukimya ikiwa imetawala ndani ya msitu, huku sauti za ndege zikisikika na kuupendezesha msitu. Askari wa mtemi Nyantumu walizikamata siraha zao na kujiandaa kuwafyatulia mishale Nyoni pamoja na watu wake …



    …………………………………



    Jeshi la kijiji cha Ukarimu wakiwa wamebakia takribani askari sitini, walisimama mbele kabisa na kuongoza kundi lote wakijion washindi kuelekea kijiji cha Ukarimu.



    Hawakutambua hata kidogo kuwa walikuwa wananyemelewa, jambo ambalo lilikuwa hatari kwao. Kwani muda wowote wangeshambuliwa na kuuawa kikatili, kwani askari wa mtemi Nyantumu walikuwa wamejiandaa kusambaratisha vichwa vyao bila kutambua. Lakini hali ilikuwa kinyume kabisa na matarajio ya mtemi Nyantumu na askari wake, kwani jiwe la mzimu Ntema liliweza kutambua siri hii na kujiandaa kutoa msaada kwa Nyoni pamoja na watu wake wote …



    Jeshi la mtemi Nyantumu baada ya kuamini walikuwa wamekaa kwenye tageti nzuri, sehemu ambayo ingesababisha kuua kiumbe chochote kile walichokilenga. Walifyatua kwa pamoja mishale yao, huku wakiamini Matumaini ndiye angekuwa wa kwanza kufa na kujeruhiwa vibaya sana. Kwani Matumaini alikuwa nyuma kabisa ya msafara ,huku akiwa amelishika jiwe la mzimu Ntema bila kutambua kitu chochote kilichokuwa kinaendelea …

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Yalaaaa!! “



    “Uwiiiiih “



    “Nakufaaaaa …”



    Kelele zilisikika na kupelekea mwangwi kusikika ndani ya msitu wote, kwani jiwe la mzimu Ntema liling’aa na kutoa mionzi mikali iliyosababisha mishale waliyoifyatua askari wa mtemi Nyantumu kuwarudia na kuwateketeza wao wenyewe. Hakuna kiumbe yoyote aliyesalia zaidi ya mbwa, kwani hata mtemi Nyantumu alifyatua mshale na uliweza kumrudia na kumuua kikatili.



    “Kuna nini?, mbona wamekufa. Nani kawadhuru? “,



    “Hata mimi nashangaa! hatujashambulia, lakini nashangaa wamekufa sijui hata mishale imetokea wapi …”,



    “Ila aliyefanya hivi katunusuru, inaonekana wametunyemelea kwa muda mrefu. Tungekufa kama nzigee! “,



    “Haswaaaa! tena mimi ndio nilikuwa nyuma yenu, bila shaka mishale zaidi ya ishirini ingenipiga mwilini “,



    Matumaini, Nyoni pamoja na askari wote wa kijiji cha Ukarimu walizungumza huku wakiwa hawa amini yaliyotokea. Kwani hawakumtambua mtu aliyewaokoa na kulishambulia kikatili jeshi la mtemi Nyantumu …



    “Mimi ndio nimewaua, mishale waliyowafyatulia imewarudia na kuwaua wao wenyewe. Nina amini hakuna kiumbe angebaki salama kati yenu, kwani walifatilia nyendo zenu kwa muda mrefu. Lakini yamekwisha! hakuna hatari tena, mmekuwa washindi! “,



    Mzimu Ntema alizungumza kwa mara nyingine tena baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, na kutoa siri ya ushindi wao. Jeshi lote la kijiji cha Ukarimu waliruka juu kusherekea ushindi, huku wakianza kuimba nyimbo za ushindi na kusifia upendo wa mzimu Ntema kwa binadamu. Walicheka, waliruka na kutabasamu huku wakisonga mbele kuelekea Ukarimu kuukata mti wa ubuyu wa mzimu Nkuru na kuhitimisha utawala wake katika kijiji cha Mwantema …



    …………………………………



    BAADA YA SIKU MOJA …



    Wananchi wa kijiji cha Ukarimu, pamoja na mtemi wao walifurahi sana kwani mwisho wa laana na majanga katika ardhi yao ulikuwa umefika. Waliamini hawatapata njaa tena, na swala la ukame katika ardhi yao litatoweka huku urafiki uliokuwepo zamani kati ya kijiji cha Ukarimu pamoja na Mwantema ukirejea na kufungua ukurasa mpya …



    “Kuanzia leo, mimi nitakuwa mtemi wa Mwantema. Nitapinga mila hatari ya ukeketaji, na kudumisha urafiki uliokuwepo zamani kati ya Mwantema na Ukarimu. “,



    Nyoni hakuamini, akiwa ameshika panga lake kubwa aina ya jambia alitamka maneno mazito kwa hisia nzito huku akishuhudiwa na maelfu ya wanakijiji wa Ukarimu. Kama mzimu Nkuru pamoja na mtemi Nyantumu walivyowekwa madarakani na mtemi wa kijiji cha Ukarimu, ndivyo walivyokuwa wakitolewa madarakani na mtemi huyu huyu ambaye aliishi kwa miaka mingi sana. Mtemi huyu alikuwa akimuapisha Nyoni huku akijiandaa kukata mti wa ubuyu wa mzimu Nkuru, mti mkubwa uliokuwa na mamraka ya kuitawala Mwantema. Miti hii ilitofautiana, mmoja ulipatikana Mwantema na mti mkuu ulipatikana kijiji cha Ukarimu. Hii ndio dawa pekee iliyokuwa ikisemekana kila siku, kwani ukifanikiwa kukatwa. Mila zote hatari na utawala wa mzimu Nkuru ungeyeyuka kama barafu ……



    “Wooooh woooh! “,



    “Igweeeh igweeeh “,



    Mti mkubwa ulidondoshwa chini baada ya kushambuliwa na kukatwa na askari wote wa Ukarimu wakimsaidia Nyoni, jambo ambalo lilipelekea shangwe kusikika kwani tayali kazi ilikuwa imemalizika. Matumaini alitabasamu, na kufurahia kaka yake kuwa mtemi mpya wa Mwantema. Alitamani wazazi wao wangekuwepo na kushuhudia kiapo cha kaka yake, lakini hakuna kilichoharibika kwani hata Mwantema bila shaka lazima watafanya sherehe kubwa dhidi ya Nyoni kwa kufanikiwa kupata dawa na kisha kuwa mtemi wao mpya …



    …………………………………

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Hatimaye baada ya mti wa Ubuyu wa kijiji cha Ukarimu kukatwa, hata mti wa mzimu Nkuru ulioko Mwantema ulianguka kwa kishindo kizito na kupelekea wananchi wote wa Mwantema kwenda kushuhudia …



    Hawakusita kufurahi, kwani waliamini mwisho wa matatizo yao ulikuwa umefika japo Mwanzoni waliwachukia familia yote ya mzee Mbutu pamoja na Nyoni kwani walimlinda  binti yao asifanyiwe mila, huku wananchi wengi wakifanya hivyo japo baadhi ya watoto wao walipoteza maisha. Waliona bora wote kukosa, kuliko mmoja kupata na kumkomboa  mtoto wake.



    Wanyama wote hatari wa pori la Nyankonko, waliowekwa kwa ajiri ya kulinda msitu walikufa kifo cha ghafla na msitu kuanza kurudi kama zamani. Kwa upande wa gerezani, wananchi walifika kwa shangwe na kuvamia ikulu ya mtemi Nyantumu kisha kuwatoa gerezani ndugu wote wa Nyoni hasa mzee Mbutu.Kisha kusherekea kwa pamoja kusubili ujio wa mtemi wao mpya, mtemi Nyoni Mbutu.



       ..……MWISHO …

0 comments:

Post a Comment

Blog