Search This Blog

CHOZI LA YATIMA - 2

 

    Simulizi : Chozi La Yatima

    Sehemu Ya Pili (2)







    Safina alikuwa peke yake na aliuona usiku huo kuwa mbaya sana katika maisha yake kwani mvua kubwa ilikuwa inanyesha na yeye alikuwa amejibanza kwenye kibanda kilichokuwa kinavuja. Hakuwa na pakwenda tena kwani kwao alishafukuzwa. Kwakweli Safina alilia sana usiku huo.

    "kifo, kwanini kifo? Umemchukua baba, umemchukua mama na kuniacha peke yangu ndani ya dunia hii. Ona sasa mvua kubwa inanyesha, nipo hapa peke yangu nalowa. Kwanini kifo usimrudishe baba na mama yangu ili niishi nao kama zamani?"

    Safina alilia sana bila ya kupata msaada wowote hadi panakucha.

    Asubuhi yake mvua ilikatika na Safina akaingia mtaani ili kutafuta chakula kwani alikuwa hajala chochote, ilikuwa si rahisi tena kwa mtu yeyote kutambua kama yule ni mtoto wa Sam na Latifa.



    Mchana wa saa saba, Safina alichoka kutembea huku na kule kwahiyo akajikalia kwenye gogo na kujiinamia chini huku akilia. Ndipo alipoguswa bega na mtu ambaye kwa muda huo Safina hakumjua ni nani.



    Mchana wa saa saba, Safina alichoka kutembea huku na kule kwahiyo akajikalia kwenye gogo na kujiinamia chini huku akilia. Ndipo alipoguswa bega na mtu ambaye kwa muda huo hakumjua ni nani.

    Safina akageuka nyuma ili kuangalia ni nani aliyemshika bega, akamuona ni mtoto wa kiume aliyekuwa mchafu sana.

    Mtoto huyo akamuuliza Safina,

    "unalia nini?"

    Safina akamjibu, "njaa inaniuma"

    Yule mtoto akamwambia Safina,

    "usijali nifuate"

    Safina akainuka na kuanza kumfuata yule mtoto, wakafika chini ya mti na yule mtoto akamwambia Safina asimame hapo ili amsubiri kwani anaenda kuleta hela ili waende kula. Safina alikuwa akimsubiri huyo mtoto bila ya kujua hiyo hela anaenda kuchukua wapi.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Safina akiwa mahali pale akimngoja yule mtoto mara akasikia sauti za watu,

    "mwizi huyo jamani nimeibiwaaa"

    Alipokuwa akisikiliza vizuri ili ajue zile kelele zinatokea wapi, mara akamuona yule mtoto akija na kumshika mkono huku akienda naye haraka haraka.

    Walitoka sehemu hiyo na kwenda hadi kwa mama ntilie ambapo yule mtoto aliagiza sahani mbili za chakula na kuanza kula, alipodaiwa pesa akatoa noti ya shilingi elfu kumi, kwakweli Safina alishangaa sana kwa mtu kama yule kuwa na hela ya aina ile.

    Walipomaliza kula, yule mtoto akaondoka na Safina, wakafika sehemu moja chini ya mti na kukaa huku wakifahamiana vizuri.

    "mimi naitwa Musa, je wewe mwenzangu unaitwa nani?"

    SAFINA: Mimi naitwa Safina.

    MUSA: Sasa nini kimekukumba hadi ukawa unalia?

    Safina akamuelezea Musa kuhusu kifo cha wazazi wake na jinsi alivyofukuzwa na ndugu zake, huku machozi yakimtoka.

    MUSA: Dah!! Pole sana Safina, hayo ndiyo maisha yanayotukumba watoto yatima.

    SAFINA: Na wewe pia ni yatima?

    MUSA: Ndio mimi ni yatima sina baba wala mama.

    SAFINA: Pole sana, nao walikufa kama wazazi wangu?

    MUSA: Historia yangu ni tofauti kidogo Safina, ila kwa kifupi simjui baba na wala sijawahi kumuona, mama alinambia kuwa baba alinikataa tangu tumboni ila hata hivyo mama yangu alishakufa.

    SAFINA: Mmh!! Na ndugu zako je?

    MUSA: Walinifukuza, hawakutaka kuniona tena. Wakanisingizia mambo mengi ambayo sikuwahi kuyafanya, nimekuwa mtoto wa mitaani na mitaa ndio baba, mama na ndugu zangu.

    SAFINA: Inasikitisha sana.

    MUSA: Ndio maisha yalivyo Safina.

    Musa na Safina wakazoeana, wakajenga ukaribu kama wa ndugu.

    SAFINA: Na ile pesa uliipata wapi?

    MUSA: Safina, maisha ya mtaani ni kuhangaika tu. Ile pesa niliiba.

    SAFINA: Uliiba? Si unajua kuiba ni dhambi!

    MUSA: Najua ndio ila tufanyeje ikiwa ukiwaomba hawakupi? Bora kuwaibia tu.

    SAFINA: Lakini Musa jua ukikamatwa utafungwa.

    MUSA: Kufungwa ni kawaida kwa watoto wa mitaani Safina.

    Musa na Safina wakaongea mambo mengi ya hapa na pale ili Safina aweze kujisikia amani tu.



    Basi Musa akamchukua Safina na kwenda kumtambulisha kwa watoto wengine wa mtaani.

    MUSA: Jamani, huyu ni mwenzetu anaitwa Safina. (halafu akamgeukia na Safina), Safina, hapa kuna Mirium, Tizo na Shida. Halafu kuna wengine, Sikuzani na Siza nadhani watakuwa mitaa mingine.

    Safina akaweza kufahamiana na watoto hao ambao walionekana kuwepo tu duniani bila matumaini yoyote ya maisha.

    MUSA: Safina maisha yetu pa kulala shida, pa kula shida. Sisi mvua yetu na jua letu kwahiyo naomba utambue hilo na taratibu utazoea.

    SAFINA: Sawa Musa.

    Siku zote tangu Safina aingie mtaani alikuwa akilia tu kwa ugumu wa maisha kwani hakuzoea kuomba wa la kuiba kwahiyo maisha yakawa magumu sana kwa upande wake, hakujua la kufanya kwakweli. Alitamani Mike aende kumchukua ili akaishi nae tena Marekani.

    "Anko Mike kwanini hata siku moja usiote kuwa mimi napata shida huku? Natamani uji kunichukua ili twende tukaishi wote Marekani"

    Mambo hayo yalikuwa kama ndoto tu kwa Safina, mara Musa akamshtua Safina toka kwenye lindi la mawazo.

    MUSA: Safina! Usipende kulia kila muda Safina, utaumwa na kichwa.

    SAFINA: Inaniuma Musa, yani kufukuzwa kwenye nyumba ya wazazi wangu!! Inaniuma sana.

    MUSA: Ni kweli inauma Safina ila Mungu yupo atatusaidia.

    SAFINA: Kwanini watoto yatima tunateseka hivi jamani?

    MUSA: Safina, mwanzoni nilijua kwamba mimi nimeteseka sana kwavile mama yangu hakuwa tajiri kwahiyo alivyokufa wakaona kuwa mimi nitakuwa ni mzigo kwao, ila nimeshangaa wewe Safina yani wazazi wako na utajiri wote ulioniambia bado ndugu wanathubutu kufanya hivi!! Kweli binadamu wengi hawana utu Safina ila jipe moyo tutashinda.

    SAFINA: Najaribu kufikiria ila nakosa jibu la mwisho wa maisha yangu.

    MUSA: Usiwaze sana Safina, inabidi ujitahidi kwenda kuombaomba ili tupambane na maisha haya.

    SAFINA: Musa, siwezi. (huku akilia).

    MUSA: Jitahidi Safina utaweza tu.

    Musa alimuhurumia sana Safina ingawa wote walikuwa kwenye matatizo lakini Musa alionyesha huruma kubwa sana juu ya Safina hadi watoto wengine wa mtaani walimshangaa Musa kwani yeye ndiye aliyejulikana kuwa na roho mbaya kuliko wote, ila alionekana kumuhurumia sana Safina. Na taratibu Safina akaanza kuzoea vile wanavyoishi watoto wengine wa mtaani. Musa hakutaka mtu yoyote kuonekana akimuonea safina.



    Suzan katika pitapita zake, akakutana na rafiki yake aliyesoma naye kitambo.

    SUZAN: Pendo rafiki yangu, unafanya kazi wapi?

    PENDO: Nafanya kazi hospitali, mwenzio siku hizi nimekuwa nesi.

    SUZAN: Mmh! Pendo kwa elimu gani?

    PENDO: Mbona niliendelea kusoma mwenzio.

    SUZAN: Basi shoga yangu ukisikia mahali wanatafuta msaidizi, nipo jamani naomba unishtue.

    PENDO: Hata pale hospital walikuwa wanahitaji mtu wa usafi ngoja nitaulizia.

    SUZAN: Dah!! Utakuwa umenikomboa kweli rafiki yangu.

    Siku zote Suzan alijilaumu kwa kutosikiliza ushauri wa dada yake Latifa, ambaye alikuwa akimshauri mara kwa mara kuwa asome lakini yeye hakufatilia, ila sasa anajutia kwani kila anapoomba kazi wanataka cheti, alijilaumu sana kwa kutnkukubali kuendelea na masomo.

    Suzan akapata bahati ya kupata kazi ya usafi kwenye hospitali anayofanyia kazi Pendo.

    Aliwekwa kwenye usafi na baadae mapokezi akiwaandikisha majina wagonjwa wanaoingia hospitalini hapo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Alikuwa hodari sana kitendo ambacho kilimvutia daktari mkuu wa hospitali hiyo na kuamua kumuweka mapokezi.

    Kwakweli Suzan alifurahi sana kitendo cha yeye kupata kazi kwenye hospitali hiyo na akaamua kuhamia nyumbani kwa Pendo na kuishi wote.

    PENDO: Hivi Suzy hunaga mpenzi? Sijakusikia hata mara moja ukimtaja shemeji yangu.

    SUZAN: Wee Pendo acha tu, nilikuwa nae anaitwa Frank ila akaenda masomoni Ujerumani, na tangu kipindi hiko sijawahi kuwasiliana nae hadi leo nadhani atakuwa amepata msomi mwenzake.

    PENDO: Na mbona hujatafuta mwingine sasa?

    SUZAN: Sitaki mtu yeyote, najipanga na maisha yangu kwanza.

    PENDO: Ila usijari, kama kweli huyo Frank alikupenda atakutafuta tena tu.

    SUZAN: Sidhani, mtu ameshaenda nje kusoma halafu arudi amkumbuke Suzy asiyesoma? Haiwezekani, acha tu nijipange kwa maisha yangu.

    PENDO: Sawa ila badae mi nitatoka na shemeji yako.

    SUZAN: Sawa shoga yangu hakuna tatizo.

    Suzan na Pendo wakaishi pamoja kama ndugu wa damu, na hapo ndio tunapata urafiki mwema kwani mnasaidiana kwa shida na raha.



    Watoto wa mtaani walijikuta, wakimshangaa sana Musa kwajinsi alivyobadilika.

    MIRIUM: Jamani, toka Musa akae na Safina, siku hizi amekuwa na huruma ya ajabu hata wizi kapunguza.

    SHIDA: Namshangaa sana sijui anafikiri ataishije bila ya wizi!

    SIKUZANI: Usimshangae, bora awe hivyo hivyo jamani, Musa alizidisha roho mbaya hadi sisi alikuwa anatufanyia unyama.

    Safina alikuwa hapendi kabisa tabia ya wizi ndiomana Musa akapunguza wizi sababu ya Safina.



    Siku moja baada ya mvua kubwa kunyesha, Safina alianza kuumwa, alikuwa akitapika na kutetemeka yani alikosa nguvu kabisa.

    Basi Musa alikuwa anamuangalia Safina tu, hakutaka kwena kudhurula na kumuacha Safina katika hali aliyokuwa nayo.

    Muda wote alikaa naye tu chini ya mkorosho kwani ilikuwa ndio sehemu kubwa ya kupumzika kwa watoto wengi wa mitaani.

    MUSA: Safina, ngoja nikaombeombe angalau nipate hata mia mbili ya kununua panadol.

    SAFINA: Sawa Musa.

    Musa akaondoka eneo hilo na kuanza kutafuta tafuta Pesa ya kununulia dawa.

    Safina akabaki mwenyewe akijisemea,

    "Hivi kwanini? Shida zote zinipate mimi? Naumwa mimi, hakuna msaada wowote. Mvua yangu na jua langu. Nitaishi hivi mpaka lini? Au ndio mpaka nitakapokufa kama wazazi wangu?"

    Safina alikuwa akilia lia tu mahali pale.

    Musa akaenda kwa watu ili apate msaada.

    MUSA: Saidia jamani, rafiki yangu anakufa. Naomba hata mia.

    MTU 1: Kama una hela ndogo si umpe!

    MTU 2: Wee siwezi kutoa hela yangu kuwapa hawa watoto, nakwambia hawa ndio vibaka wa mjini.

    Musa aliomba na kuomba bila ya kupata msaada wowote, akakumbuka hadi ule usemi usemao kuwa 'siku ya kufa nyani miti yote huteleza'

    Kwakweli Musa aliona ni mtihani mkubwa sana kwake, akaamua kurudi pale chini ya mkorosho.

    Akamkuta Safina akiwa na hali mbaya zaidi, Musa akaamua kufanya uamuzi wa haraka na kujisemea liwalo na liwe.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Musa aliporudi pale chini ya mkorosho akamkuta Safina akiwa kwenye hali mbaya zaidi, akaamua kufanya uamuzi wa haraka zaidi na kujisemea kuwa liwalo na liwe.

    Musa akaamua kumchukua Safina na kumbeba mgongoni mwake, akamfunika na kipande cha khanga huku akijisemea,

    "naenda nae hospitali hivihivi hata kama sina pesa"

    Musa akaanza safari ya kwenda hospitali, takribani hospitali kama tatu alifukuzwa yeye na mgonjwa wake kwani hakuwa hata na pesa ya kumuona daktari.

    Akaanza kukata tamaa ila akajipa moyo kuwa lazima apate hospitali ya kumweka Safina tu.

    Alipofika hospitali ya nne iliyoitwa hospitali ya Nile, alishangaa kupokelewa vizuri na moja kwa moja yeye na mgonjwa wake mgongoni wakapelekwa kwa daktari na yule muhudumu akatoka, kwakweli Musa alishangaa sana kwa kutokuulizwa pesa ya kumuona daktari.

    Yule daktari akamwambia Musa amlaze yule mgonjwa kitandani, halafu akamfanyia baadhi ya vipimo na

    Musa akangojea vipimo vya daktari akiwa na mgonjwa wake mule ndani.

    DAKTARI: Mgonjwa ameanza kuumwa lini?

    MUSA: Tangu juzi.

    DAKTARI: Hamkumpa dawa yoyote?

    MUSA: La, sikumpa dawa yoyote.

    DAKTARI: Ok, mgonjwa anaonekana kuwa na malaria kali sana, kwahiyo itabidi alazwe.

    MUSA: (Akashtuka), alazwe?

    DAKTARI: Ndio alazwe, mbona unashtuka?

    Musa alishtuka sababu hata hela ya kumuona daktari alikuwa hajalipa, sasa gharama za kulazwa je!!

    Baada ya hapo, daktari akamuandikia Safina matibabu na kuwapeleka sehemu husika ya kulazwa wagonjwa.

    Musa akatakiwa kwenda kuandikisha taarifa za mgonjwa, akaandikisha taarifa anazoelewa yeye kuhusu Safina basi.

    Nesi wa zamu akamuita Musa ili aweze kulipia gharama za kumuhudumia mgonjwa wake mahali hapo.

    Musa akamuomba kwa kuwa hana pesa yoyote. Nesi huyo aliyejulikana kwa jina la Rose.

    ROSE: Hivi wewe utamletaje mgonjwa kwenye hospitali binafsi wakati huna pesa?

    MUSA: Nihurumie dada yangu, si unaona hali yangu ilivyo.

    ROSE: Hali yako mimi inanihusu nini? Unafikiri hospitali ya bure hii?

    MUSA: Simaanishi kuwa hii ni hospitali ya bure, ila sina pesa kwasasa.

    ROSE: Sasa nakwambia, nenda uendako ukalete pesa hapa lasivyo mgonjwa wako hatumuhudumii chochote. Umesikia wewe?

    MUSA: Sawa nimesikia.

    Musa akawa anaondoka eneo lile, ndipo Suzan akamuona na kukumbuka kuwa alimpeleka yule na mgonjwa wake moja kwa moja kwa daktari bila kumuandikisha, akaamua kumuita na Musa akasogea pale dirishani akijua ndio yaleyale ya pesa.

    SUZAN: Unaitwa nani?http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MUSA: Naitwa Musa.

    SUZAN: Na yule mgonjwa wako anaitwa nani?

    MUSA: (Akijibu kwa hasira), nishamwandikisha kule kwingine.

    SUZAN: Mbona unajibu kwa hasira hivyo? Inabidi na hapa aandikishwe.

    MUSA: Msinichanganye bhana.

    Halafu akaondoka, kwakweli Suzan alimshangaa sana Musa na majibu yake na alijishangaa kwanini hakumuandikisha tangia mwanzo, akawa anajisemea,

    "mmh!! Wagonjwa wengine wamevurugwa kweli jamani."

    Musa nae alijiuliza sana kuwa kwanini amemjibu vibaya yule dada wa mapokezi wakati hakuna baya alilomtendea.

    "yule dada anaonekana kuwa na huruma, ila ndio hivyo tena nishamjibu vibaya dah"

    akaendelea na safari yake ya kutafuta pesa ya huduma kwaajili ya Safina.



    Kule hospitali nako Rose akamfata Suzan pale dirishani.

    ROSE: Hivi Suzy kazi imekushinda au??

    SUZAN: kwanini jamani dada Rose?

    ROSE: Unapokea wagonjwa ovyo ovyo, unawapeleka kwa daktari bila kadi wala nini.! Ona sasa yule chokoraa kamleta chokoraa mwenzie tena bila hata ya pesa. Unadhani yule mgonjwa atalipiwa na nani huduma hizi?

    SUZAN: Jamani dada, alikuwa hapa na mgonjwa wake akiwa hoi sana nikaona kuwa niwawaishe halafu maelezo nichukue wakitoka.

    ROSE: Kweli akili zako ni fupi sana, yani unangoja watoke ndio uchukue maelezo loh!! Umewekwa hapo mapokezi ili ufanye nini?

    SUZAN: Nipokee wagonjwa, na si ndio nimewapokea jamani.

    ROSE: Ngoja tu, huyu chokoraa asipoleta pesa tutakata mshahara wako kwa uzembe.

    Kwakweli Suzan alishangaa sana na hakujua cha kufanya ikambidi tu awe tayari kwa lolote.

    Suzan alipompokea Musa na Safina, hakujishughulisha kabisa kumuangalia yule mgonjwa ila aliwapeleka moja kwa moja, laiti kama angewaangalia angeweza kumgundua Safina mtoto wa marehemu dada yake.



    Musa akajaribu kuomba msaada kwa watu.

    MUSA: Naomba nisaidie japo pesa kidogo tu.

    MTU: Bora hiyo pesa nikaitupe baharini kuliko kukupa wewe.

    Musa alikata tamaa kabisa ya kupata pesa kwa njia hiyo ya kuomba,

    "hata kama Safina amenikataza maswala ya wizi lakini lazima nikaibe tu ili nipate pesa ya kupeleka huko hospitali"

    Akaamua kwanza aende kwa wenzie pale mtaani ili akapate ushauri.

    Alipokuwa anakwenda, wenzie nao wakawa wanaongea,

    SHIDA: Mmh jamani Musa anavyotia huruma utafikiri anayeumwa ni yeye kumbe Safina.

    SIKUZAN: Eti anamuhurumia Safina kisa mpeni wa maisha haya. Hivi nani mwenyeji wa maisha haya jamani? Mmh!!

    MIRIUM: Kwanza huyo Safina kila siku ni mgeni kwa lipi haswa jamani!! Kashazoea jamani, miaka nenda rudi tupo naye sasa huo ugeni usioisha ni upi?

    TIZO: Labda kwavile ni kadogo dogo ndomana anakahurumia jamani.

    Musa akawafata pale walipo na kuwaeleza kuhusu Safina,

    MUSA: Jamani, Safina kalazwa.

    WOTE: Kalazwa?

    MUSA: Ndio na hospitali wamesema kuwa nisipopeleka pesa basi hawatamuhudumia.

    MIRIUM: Musa usijali, watamuhudumia vizuri, wewe kwa hali yako hiyo wanafikiria pesa utaitoa wapi.

    MUSA: Sio nisijali Mirium, hapa tufikirie maisha ya Safina kwani yako hatarini.

    MIRIUM: Lakini si umesema kuwa amelazwa?

    MUSA: Ndio amelazwa.

    MIRIUM: Sasa wasiwasi wako ni nini? Akifa si atakufa mikononi mwao?

    MUSA: Ndio atakufa mikononi mwao lakini hasara atapata nani?

    SHIDA: Hasara gani sasa?

    MUSA: Shida, kuwa na akili. Tunampoteza mwenzetu, tunapoongea hapa mkumbuke kuwa tunaongelea uhai wa Safina!

    MIRIUM: Sawa, sasa tufanyeje?

    MUSA: Hilo ndio jambo la kusema, tukae chini na tujadiliane kitu cha kufanya ili mwenzetu aweze kurudi katika hali yake ya kawaida.

    Basi wakaanza kujadiliana namna ya kupata pesa,

    SHIDA: Jamani, naona mnapoteza muda tu. Musa wewe ni shujaa kwa wizi kwanini basi tusiende kupora watu pesa?

    MIRIUM: Shida, kumbuka juzi ulitaka kukamatwa!

    SIKUZAN: Ila hakuna njia nyingine rahisi zaidi ya hiyo, itabidi Musa uende kupora tu na hilo ndio suluhisho.

    Waliongea mengi na kuafikiana kuwa wakafanye uporaji tu.



    Manesi walishindwa kumuhudumia Safina aliyekuwa amelazwa kwani madawa yote aliyoandikiwa yalikuwa hayajalipiwa bado.

    Usiku wa siku hiyo ilikuwa ni zamu ya Pendo, na kama kawaida yao akiingia nesi mwingine anapewa maelekezo juu ya wagonjwa waliolazwa.

    Pendo na Suzan walikuwa wanaonana mara chache kamavile hawaishi nyumba moja, hii ilitokana na muda wa kuja kazini ambavyo ulitofautiana kati yao, mmoja akiingia mwingine anatoka. Mara nyingi wanakuwa pamoja ile siku ya mapumziko tu.

    Kwahiyo Pendo alipofika mahali hapo alimkuta Suzan akiwa amejiandaa kutoka, wakasalimiana tu na kuagana, halafu Suzan akaondoka kwenda nyumbani.

    Pendo alishangaa sana kumuona binti mdogo akiwa mgonjwa sana na bila ya kuhudumiwa kwa chochote, ikambidi Pendo akamchukulie binti huyo dawa na sindano kwa dhamana yake mwenyewe, akamuhudumia sana usiku wote wa siku hiyo, hadi ilipofika alfajiri alionekana kuendelea vizuri kwani dripu aliyomuweka ilimsaidia sana.

    Kama kawaida yake Pendo, kabla hajaondoka akawatembelea wagonjwa wote,

    PENDO: Unaendeleaje?

    SAFINA: Naendelea vizuri, asante sana kwa huduma yako.

    PENDO: Usijali, nipo kwaajili yenu.

    Alipomaliza akajiandaa na kuondoka ili kuwapisha manesi wengine na yeye kwenda kupumzika.

    Pendo alipofika nyumbani, Suzan alikuwa tayari ameshaondoka, hiyo ilikuwa ni kawaida kwao kwani mara nyingine zinaweza kupita hata siku tatu bila ya kuonana.

    Siku hiyo, Pendo akawa anafanya usafi, mara albamu ya Suzan ikadondoka, basi akaichukua na kuangalia picha, ndipo alipokutana na picha aliyopiga Sam, Latifa, Suzan na Safina. Basi akajikuta akimkazia macho sana yule mtoto na kuona kuwa hata hajabahatisha pale.

    "mbona sura hii inafanana na sura ya mtoto aliyelazwa hospitali? Au nimemfananisha? Hapana huku sio kufanana. Hivi inawezekana akawa ndiye huyu? Kama ndiye huyu inawezekana hata Suzan asimjue jamani?"

    Pendo alijiuliza maswali mengi kwani anajua wazi kuwa Suzan ndiye anayepokea wagonjwa, iweje sasa asimuone huyo mtoto. Pendo aliishika sana sura ya yule mtoto kutokana na kumuhudumia sana usiku huo.

    Pendo alipofika hospitali siku hiyo alikuwa na hamu sana ya kuonana na Suzan ili amweleze kuhusu ile sura ya yule mtoto, lakini alipofika tu akaambiwa kuwa Suzan alishaondoka kitambo kwani kuna vitu ameenda kufatilia.

    Mara Pendo akafatwa na Rose na kuanza kuambiwa,

    ROSE: Yule mgonjwa wa kitanda namba kumi na moja....

    Kabla hafamaliza, Pendo alishtuka sana kwani hicho kitanda ndicho alicholazwa Safina.

    PENDO: Amefanya nini?

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mara Pendo akafuatwa na Rose na kuanza kuambiwa,

    ROSE: Yule mgonjwa wa kitanda namba kumi na moja.....

    Kabla hajamalizia, Pendo alishtuka sana kwani hicho kitanda ndicho alicholazwa Safina.

    PENDO: Amefanya nini?

    ROSE: Kheee!! Mbona una haraka kama mkojo wa asubuhi!! Si unisikilize kwanza.

    PENDO: Sawa, amefanya nini?

    ROSE: Mwanzoni nilitoa amri kuwa asihudumiwe ila sasa nimeona bora muendelee kumpa huduma tu. Ila kesho asubuhi kuna kikao cha wafanyakazi wote wa hapa kwahiyo usiwahi kuondoka.

    Pendo sasa akapumua kwa amani maana mashaka yalimjaa sana kuhusu Safina.

    Na usiku wa siku hiyo akaendelea kumuhudumia kwa ukaribu zaidi ili amkariri vizuri ila hakuweza kumuuliza maswali mengi sababu ya wingi wa wagonjwa usiku huo.



    Suzan alipofika nyumbani alikuwa amechoka sana, alipoangalia mezani akaiona picha aliyopiga yeye, Latifa, Sam na Safina. Aliikuta pale mezani kwavile Pendo alisahau kwenda nayo.

    Aliichukua picha ile na kuiangalia, huku akijisemea,

    "Hivi kwanini Sam na Latifa mlikufa? Na Safina je unaishije huko ulipo? Umenisahau hata mimi? Ni bora shemeji na dada wangeendelea kuishi hukohuko Marekani kuliko walivyorudi hapa nchini, ona sasa wameteketea, loh kifo kweli hakina huruma"

    Asubuhi alipofika kazini kukawa na kikao cha wafanya kazi ambacho kiliwahimiza kufanya kazi kwa bidii, na pia kuacha uzembe katika kazi. Kwahiyo Pendo hakuweza kuzungumza tena na Suzan.

    ROSE: Hii ni hospitali ya mtu binafsi sio ya serikali kwahiyo mjue kwamba hospitali hii inalipiwa kodi hivyobasi kila mgonjwa anatakiwa achangie gharama za matibabu. Muache huruma za kijinga.

    Alipomaliza aliwataka wote waende sehemu zao za kazi kwani Rose ndiye aliyekuwa msimamizi mkubwa wa hospitali hiyo.



    Suzan alipokuwa pale mapokezi mara akaja mtoto mchafu mchafu, huyo mtoto alikuwa ni Shida mwenzake na Safina huko mitaani.

    SHIDA: Kuna mgonjwa kalazwa hapa anaitwa.....

    Kabla hajamaliza, Suzan akadakia kumjibu.

    SUZAN: Kama unaulizia wagonjwa waliolazwa nenda dirisha la pili.

    Kwahiyo Shida akaondoka hapo na kwenda kuulizia hilo dirisha la pili.

    SHIDA: Kuna mgonjwa kalazwa hapa, anaitwa Safina. Je amelazwa sehemu gani?

    Basi yule mdada akawa anapekua daftari la wagonjwa waliolazwa pale na kumuuliza,

    MDADA: Kalazwa lini?

    SHIDA: Juzi

    MDADA: Umesema anaitwa nani?

    SHIDA: Safina

    MDADA: Nenda wodi ya wanawake chumba cha tatu, kitanda namba kumi na moja.

    SHIDA: Sawa asante.

    Shida akaenda moja kwa moja hadi alipoelekezwa na kumkuta Safina kalala, akaamua kumuamsha.

    SHIDA: Safina, Safina, amka.

    SAFINA: Kheee! Shida umekuja. Musa yuko wapi?

    SHIDA: Pole sana, unaendeleaje? Je wanakupa huduma?

    SAFINA: Naendelea vizuri na huduma wananipa ndio.

    SHIDA: Pole sana, Musa ndio kanielekeza kuwa uko hapa.

    SAFINA: Kwani yeye yuko wapi? Sijamuona tangu juzi aliponileta hapa.

    SHIDA: Musa kakamatwa na polisi.

    SAFINA: Kafanywa nini? Kwani kafanyaje hadi kakamatwa?

    SHIDA: Kuna jamaa mmoja tulipanga kumpora kwa bahati mbaya Musa akakamatwa, mimi nilibahatika kukimbia. Yani hivi tunavyoongea hapa yupo kituoni.

    SAFINA: Masikini Musa, najua alikuwa anaiba kwaajili yangu. Nahitaji kumuona, kwahiyo itabidi nitoroke hapa hospitali.

    SHIDA: Hata mimi nilitaka kukushauri hivyohivyo kwani ukiwaambia kwamba unataka kutoka watakudai pesa wakati sisi pesa hatuna.

    Kwahiyo Shida na Safina wakawa wanapanga jinsi ya kutoroka hapo hospitali.

    SHIDA: Safina, hebu nijifanye kama nakufanyisha mazoezi halafu tukifanikiwa kufika nje tunatimua mbio. Sawa?

    SAFINA: Sawa, nimeelewa.

    Shida akajifanya kamshika Safina mkono huku anatembea naye taratibu hadi wakafanikiwa kutoka nje, na ikawa rahisi kwao sababu muda huo kulikuwa na watu wengi wakiingia na kutoka kuwaona wagonjwa wao. Walipofika nje wakaanzisha safari ya kwenda kituoni na wala hawakurudi tena hapo hospitalini.



    Pendo alipofika nyumbani, sura ya Safina bado iliendelea kutembea kichwani mwake.

    Ulipofika mchana akajiandaa ili aende hospitali kuzungumza na Suzan kuhusu yule mtoto kwani mchana huwa hakuna wagonjwa wengi.

    Na alipofika hospitali, akamkuta Suzan kapumzika sababu kulikuwa hakuna wagonjwa wa kupokelewa muda huo.

    Basi wakasalimiana na Pendo akatoa ile picha na kumuuliza Suzan.

    PENDO: Suzan, hivi hawa ni wakina nani?

    SUZAN: Aaah!! Hapa kuna marehemu dada yangu na shemeji ambao kipindi kile nilikwambia wapo Marekani pamoja na mtoto wao.

    PENDO: (Akionyesha sura ya Safina), umesema huyu ni mtoto wao?

    SUZAN: Ndio ni mtoto wao, vipi leo unawaulizia hao ndugu zangu kama vile umewahi kuwaona?

    PENDO: Hapana bhana, huyu mtoto wao anaitwa nani?

    SUZAN: Ooh! Anaitwa Safina hata sijui anaendeleaje jamani.

    PENDO: Umesema anaitwa Safina?

    SUZAN: Ndio anaitwa Safina, mbona unashangaa au umewahi kumuona kwenye Tv hapo zamani? Maana kanajua kuimba kweli yani.

    PENDO: Unajua Suzy, yule binti wa kitanda namba kumi na moja kafanana kweli na huyu halafu nae anaitwa Safina.

    SUZAN: Acha masikhara bhana Pendo, binti gani huyo? Mbona mimi sijamuona wakati mimi ndio napokea wagonjwa?

    PENDO: Si yule binti waliyesema mwanzo tusimuhudumie sababu ya pesa!

    SUZAN: Khaaa! Kwani kafanana na huyu? (akionyesha ile sura ya Safina)

    PENDO: Ndio, kwani wewe hujamuona?

    SUZAN: Ndio sijamuona.

    PENDO: Basi twende ukamuone.

    Suzan na Pendo wakaenda hadi wodini lakini Safina hukuwepo pale kitandani, wakaamua kumuuliza nesi wa zamu ya mchana siku hiyo.

    PENDO: Zena, hivi yule mgonjwa wa namba kumi na moja yuko wapi?

    ZENA: Kuna muda nilimuona na ndugu yake, ila sijui sasa atakuwa ameelekea wapi.

    Basi wakaamua kumtafuta kila mahali pale hospitali lakini hawakumuona.

    ROSE: Au ametoroka?

    ZENA: Pengine.

    PENDO: Hapana bhana, hawezi kutoroka.

    ROSE: Usikatae, yule binti anajua wazi kuwa anadaiwa inawezekana akawa ametoroka ili kukimbia deni.

    Rose akawaita kikao cha dharura na kuwaambia kuwa wanatakiwa kuwa makini na wagonjwa hapo hospitali kwani hawatatakiwa kutoka bila ruhusa ya daktari.

    ROSE: Wagonjwa wengine lawama tu, sasa kametoroka bila hata ya kumaliza dozi. Umakini wenu manesi ni muhimu sana la sivyo itakuwa tunatoa huduma zisizo na maana hapa kama wagonjwa hawamalizi dozi.

    ZENA: Masikini, kaliogopa kudaiwa.

    ROSE: Ndio lazima kaogope, kwani hospitali ya baba yake hii!!

    Baada ya hapo, Pendo na Suzan wakatoka nje.

    PENDO: Pole Suzan, kwani hujaweza kumuona.

    SUZAN: Nashindwa hata kuelewa kwanini sikumuangalia wala kumuhoji?

    PENDO: Kwani ilikuwaje?

    SUZAN: Alikuwa amebebwa mgongoni na yule kijana na mimi nilimpeleka moja kwa moja kwa daktari halafu nikatoka nje dah!!

    PENDO: Je, hukumuuliza huyo kijana wanakaa wapi?

    SUZAN: Yule kijana aligoma kunijibu halafu cha kushangaza wala sikumfatilia tena.

    PENDO: Usijari Suzy kila jambo na wakati wake na kila tukio maishani hutokea kwa sababu fulani, huwezi jua kwanini imekuwa hivyo ila Mungu pekee ndiye ajuaye. Ila amini kwamba milima haikutani lakini binadamu ukutaka, kwahiyo ipo siku mtaonana tena na tutaendelea kumtafuta huyo Safina.

    SUZAN: Asante sana Pendo, nashukuru.

    Pendo na Suzan walikuwa ni watu wa kupeana moyo sana katika mambo yote wanayoyafanya.



    Modesta alipata habari zilizomuumiza sana ikabidi aende nyumbani kwa dada yake Aisha kuuliza.

    MODESTA: Nasikia mmeuza mali zote za marehemu!

    AISHA: Ndio tumeuza kwani wewe tatizo lako nini?http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    MODESTA: Dada, mtapata laana nyie!! Sina ubaya ila mmechafua sana ukoo kwani kuna tetesi nimesikia kuwa mmewaroga Sam na Latifa ndiomana wamekufa.

    AISHA: Hayo mambo ya kuroga nenda kamuulike kaka yako Juta kwani mi sihusiki.

    MODESTA: Na mbona Safina hayupo huko kwa kaka Juta?

    AISHA: sasa umekuja kumuulizia kwangu, kwani umesikia kuwa hiki ni kituo cha kulelea watoto yatima?

    MODESTA: Ila dada, utayakumbuka maneno yangu, ipo siku tu. Haki ya mtu haiendi bure bure, nitajitahidi hata me mwenyewe kumtafuta huyo Safina hadi nimpate.

    AISHA: Nenda kamtafute bhana eeh hunipunguzii kitu wala huniongezei.

    MODESTA: Nitamtafuta ndio maana nyie mashetani msije mkammaliza na yeye bure.

    Kwakweli Modesta aliumizwa sana na matendo ya ndugu zake, na akaamua yeye kama yeye kuanza kumsaka Safina.



    Musa akiwa rumande, alipigwa sana na maaskari kama kawaida yao ila huko rumande akaenda kukutana na kitu tofauti kilichobadili taswira nzima ya maisha yake.



    Musa akiwa rumande alipigwa sana na maaskari kama kawaida yao ila huko rumande ndio alipoenda kukutana na kitu tofauti kilichobadili taswira nzima ya maisha yake.





    ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog