Search This Blog

MUUAJI WA KIKE - 5

 

    Simulizi : Muuaji Wa Kike

    Sehemu Ya Tano (5)







    Skola alikosa raha, alikuwa mtu wakulia kilasiku chuoni hakukuendeka babayake ndie alikuwa mfariji wake adi pale alipokuwa sawa, kila alichokifanya Jose alikiona hakupenda kumtesa vile ila ilimbidi ili nayeye ajisikie maumivu kama anayopata, alipokuwa anataka kujiua alimuona akamuwahi, lengo lake ni kumtesa na sio kumuacha afe, aliona siku tatu alizokuwa mbwa mateso aliyopata yalimtosha hakutaka kuendelea kumtesa akamuacha huru hakutaka kuonana nae tena, wakati huo yale maumivu yalipungua nakujikuta anazoea kuishi pekeyake bila Jose.

    Alijitajidi kusoma adi pale alipomaliza nakuwa nyumbani akipumzika nakufikiria kuanza kufanya biashara zake.

    Andrew yule rafiki yake aliesoma nae alimuarika kwao nakumwambia amepata mchumba leo ni siku yakumvalisha pete, Skola alifurahi kwailo akajiandaa nayeye aende akiwa chumbani anavaa mamayake akamtokea alifurahi kumuona wakakumbatiana kwa furaha.

    "Shaymaa mwanangu leo ni siku nzuri sana kwako naamini utafurahi milele"

    Alisema mamayake akitabasamu

    "Mama kunanini jamani mbona sielewi"

    "Usijal mwanangu utajua tu ila yule mwanaume unaetamani kumpata ambae hatokuumiza atakupenda milele leo utakutana nae"

    Alisema Meyan nakumfanya Skola ajawe na furaha.

    "Nimekuletea nguo hii naomba uvae leo"

    Alitoa kwenye mfuko gauni la pink lefu adi chini zuri lenye mfano wa tausi, Skola alivaa lilimkaa nakumchora umbo lake zuri, chini alivaa viatu vyeupe pamoja na ki hand bag kidogo cha mkononi cheupe pia alipendeza sana ata alipomaliza nakutoka babayake alimshangaa mwanae

    "Aya mama safari ya wapi? Yani umependeza kuliko malaika"

    Alisema nakumtania mwanae alifarijika kumuona anatabasamu kwani alipokuwa na hudhuni ata yeye pia moyo ulikuwa unamuuma.
    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Baba jamani naenda kwenye part ya rafiki yangu"

    Alimwambia babayake akamtakia safari njema.

    Alitoka nje akaingia kwenye gari nakuelekea nyumbani kwa Andrew ambae anaishi ubungo maziwa.

    Alifika akashuka nakuingia ndani ambapo kulikuwa kumepambwa vizuri nakupendeza alipofika alikuta watu wanasherekea wamejaa wengi sana ni nje uwanjani ndio walifanya ukumbi.

    Pafyumu yake ilizagaa kote nakufanya watu wageuke kumuangalia uzuri wake ulikuwa kivutio sana, alipokuwa anatembea kuingia Andrew alimuona akamuwahi nakumsalimia uku wakikumbatiana kwa furaha, wanaume wachache waliokuwepo walitamani iyo nafasi wangeipata wao.

    Skola alikuwa mrembo haswa tena wa asili hakujipaka mekapu wala nini ila alipendeza sana nakuvutia.

    Andrew akamshika mkono adi mbele kisha akachukua kipaza sauti nakuongea

    "Mabibi na mabwana habari zenu kwanza"

    Watu wote wakaitikia, alafu akaendelea kusema

    "Yule mtu aliefanya leo hii tukusanyike ni huyu apa ni mwanamke ninaempenda kuliko wote duniani"

    Aliposema ivyo akamgeukia Skola ambae alikuwa amepigwa butwaa haelewi

    Ghafla akaja mamayake Skola Meyan akiwa na babayake Saimon nyuma yao kulikuwa na binti mrembo ambae alishika kiboksi nakumpatia Andrew akafungua nakutoa pete

    "Suprise"

    Alisema Andrew



    Skola akiwa amepigwa na mshangao, akamsikia Andrew akisema

    "Skola will you marry me?"

    Aliulizwa lakini hakuweza kujibu alibaki kimya akiwa haelewi imekuwaje akiwa bado anashangaa, Andrew alishika mkono wake nakumvalisha ile pete ya thamani iliyonakishiwa kwa Almas, watu walishangiria uku wakipiga vigelegele, baadhi walisogea mbele nakuwapongeza, wazazi wake Skola pia walisogea mbele yao nakuwakumbatia kwa furaha.

    "Mama mbona sielewi"

    Skola alimwambia mamayake

    "Shiiii tulia utajua kilakitu"

    Alimwambia akamuachia sababu walikuwa wamekumbatiana.

    Akaja mamayake Andrew nakumkumbatia Skola kwa furaha sana.

    "Karibu mwanangu kwenye familia yetu"

    Alimwambia

    "Asante mama"

    Ilibidi atabasamu nakumuitikia kwa furaha muda huo Andrew alikuwa anapokea hongera kwa watu wengi wakimsifia mkewake mtarajiwa ni mzuri sana.

    Watu walikula wakanywa adi kusaza, mziki mlaini ukawekwa apo wakaanza kucheza hakika kila mtu aliekuwepo alifurahia.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Baada ya masaa kwenda sana usiku mkubwa sherehe iliisha na watu wakaagana nakuondoka.

    Familia ya bi Tamari iliikuwa fukara sana wengi waliwatenga kisa maskini, lakini tangu Skola awasaidie nakuyabadirisha maisha yao wakaanza kuonekana watu nakukubalika kwa jamii kupelekea kupata marafiki qengi na majirani ambao walishiriki kwenye sherehe ya kuvishwa pete mchumba wa Andrew ambae alikuwa gumzo kutokana na uzuri wake wa asili, Skola alivutia wengi walioomba kupiga nae picha uku watu wengi wakimpongeza Andrew kupata mke mzuri.

    Tangu wakati huo bi Tamari hakujua mumewake yupo wapi kwani alimkimbia kipindi kirefu tangu mtoto wake Andrew akiwa darasa la tano, akajitahidi kumsomesha adi apo alipofikia alimshukuru mungu pamoja na umaskini aliokuwa nao lakini leo hii kijana wake amekuwa mkubwa akiwa na elimu yakutosha.

    ****

    Sherehe iliisha watu wote wakaondoka ata wazazi wake Skola waliondoka pia, Skola hakusubiri alianza kumuongelesha Andrew akiwa na hasira sana.

    "Andrew kwanini umefanya ivi?"

    Alisema

    "Mmmh mamy jaman ebu twende ndani tukaongee kwanza"

    Alijiibu kiupole Andrew uku mwenzie akiwa amechukia, Mara mama yake Andrew akatokea nakuwaomba waingie chumbani kupumzika ilikuwa Usiku saa saba.

    Hakuwa na jinsi kwa heshima ya mama akaingia chumbani kwa Andrew ikiwa ndo mara ya kwanza kuingia.

    "Karibu Mrembo wangu, malkia wa moyo wangu mwanamke wa maisha yangu nikupendae kuliko chochote, mmh unanukia vizuri zaidi ya ua waridi hakika wewe ni mboni yangu bila kuwa nawe maisha yangu yote ni giza siwezi kusema nakupenda najua wengi wamekutamkia ilo ila nachoweza kukwambia nina kuhitaji maishani mwangu Skola"

    Alisema Andrew maneno matamu yaliyomshusha hasira zote Skola bila kutegemea alijikuta anatabasamu, Andrew alikuwa na sauti ya kiume haswa alijua kubembeleza aliongea kwa upole uku akimuangalia usoni Skola aliekosa ujasiri wakumtizama nakugeuka pembeni.

    "Andrew lakini mbona umefanya halaka kunivisha pete bila kuongea kabla"

    Alisema Skola, Andrew alicheka kwanza

    "Kwaiyo ulitaka nikutongoze alafu ukatae ili uniumize moyo wangu"

    Alimjibu nakumfanya Skola acheke pia.

    "Kwanza wazazi wangu imekuwaje wakaja nani aliwapa taharifa?"

    Aliulizahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Mama mkwe wangu bi Meyan najuana nae sana tu ata we Skola nakujua kama unauwezo wa ajabu"

    Aliisema Andrew nakumfanya Skola ashtuke sana.

    "Usiogope ngoja nikuelezee ilivyokuwa"

    Andrew alimwambia nakumsogelea karibu.

    "Siku moja nipo shuleni wakati wakuondoka ulifika nikiwa njiani naelekea kupanda daladala nikakutana na mwanamke mzuri sana ambae sura yake ilifanana nawewe Skola, alinisimamisha nakunisalimia nikamjibu pia, baada ya apo akanambia maneno niliyoshangaa sana.

    "Andrew najua unampenda sana binti yangu Skola, naamini utakuwa mume bora kwake endapo utamuoa nakuishi nae, nimekuchagua uwe mkwe wangu"

    Alisema nikaanza kutetemeka sababu sikuwahi kukwambia kama nakupenda Skola nikajiuliza amejuaje uyu mama sikupata jibu.

    Siku iyo tuliachana hatukuongea sana.

    Baada ya mwezi kupita tushamaliza mitihani chuo siku moja nikiwa bafuni naoga nilitoka nakumkuta mwanamke amekaa kitandani kwangu nilipoangalia mlangoni kumefungwa nikashangaa ameingiaje ndani kwangu, Mara nikamsikia akisema.

    "Andrew mwanangu usiogope mimi sio binadamu lakini pia siwezi kukudhuru, ata Skola pia ananguvu zakijini babayake ndio binadamu"

    Alisema nikaogopa

    "Mama siwezi kumuoa Skola"

    "Unaweza sana namimi nimekuchagua wewe"

    "Lakin ataniua"

    "Akuue kwa kosa gani unavyomuona Skola ni muuaji wa kike kwani bila mimi kukwambia ni jini ungejua ilo mbona babayake Skola ni binadamu lakini nipo nae adi sasa Andrew furaha ya mwanangu ipo mikononi mwako najua unampenda sana Skola na ndio maana nikakufuata nimekubali umuoe awe mkeo"

    Alisema mama nakunifanya nijifikirie kidogo kisha nikamjibu

    "Niimekubali mama nitamuoa Skola"

    Mama alinikumbatia kwa furaha uku akifurahia baada ya apo tukapanga mipango yakukuvisha pete kilakitu aligharamia mamamkwe ata pete alinunua yeye.

    Sikutaka kukueleza mapema Skola usingekja ndio maana ikawa surprise kwako"

    Alimaliza kusema Andrew nakumfanya Skola ashushe pumzi ndefu, alimkumbuka Jose ambae alimsaliti akajikuta machozi yanamtoka.

    "Skola mimi ni tofauti na Jose siwezi kuumiza moyo wako niamini"

    Aliongea Andrew nakumfanya Skola ashtuke

    "Umemjuaje Jose?"

    Aliuliza kwa mshangao

    "Kila unachowaza moyoni mwako nakijua nina uwezo wakutambua ata litakalo tokea kesho"

    Alisema akitabasamu.

    "Haa unajuaje wakati wewe ni binadamu wa kawaida?"

    "Sikukwambia kumbe nilipokumbatiana na bi Meyan nilipata nguvu pia"

    Skola aliishiwa pozi akabaki anamuangalia Andrew bila kummaliza.

    Akiwa kazubaa alishtuka Andrew kasogeza mdomo wake karibu nakumbusu alisisimka sana bila kutarajia wakajikuta wamekumbatiana. Hisia za Andrew zilikuwa juu sana alikuwa nahamu na Skola ambae alimkatalia

    "Ni mapema mno Andrew sitaki"

    Hakusikilizwa alichosema Andrew alipagawa namwili wa Skola akazidi kumtalii adi Skola akakubali.

    Walipitiwa na usingizi wa kwanza kuamka alikuwa Skola akajishangaa hana nguo mwilini kibaya zaidi ata Andrew hakuwepo kitandani alishtuka sana



    Skola alishangaa Andrew ameenda wapi akajiinua nakukaa kitandani uku akiangalia chumba kizima nakuona kilivyo kizuri, Usiku hakuwa ameona mule ndani kupoje ila sasa kumekucha aliweza kutambua Andrew anajielewa sana kwani chumba chake alikipamba vizuri nakuvutia tofauti na chumba cha Jose alikuwa kila akifika lazima afanye usafi chumba kipo ovyo nguo adi chini zimemwagwa.

    Akiwa bado anashangaa akasikia mlango unafunguliwa, akashika shuka nakulivuta zaidi mwilini mwake akijifunika sababu hakuwa na nguo nyingine

    "Wow Malkia wangu umeamka?"

    Kumbe ni Andrew alikuwa maliwatoni akamfanya Skola atabasamu alipomuona.

    Wakasalimiana kwa furaha sana,

    "Amka tukaoge mama watoto"

    Hakika Andrew alijua kucheza na hisia za Skola muda mfupi waliiokaa alijikuta anampenda sana ata kujizuia hakuweza.

    "Andrew kiukweli nakupenda sana"

    Alimwambia

    "Asante mke wangu ila unishindi mimi,ninavyokupenda adi nakuonea wivu"

    Alisema akitabasam nakumfanya Skola acheke, basi wakainuka nakuoga pamoja wakiwa kama mke na mume.

    Baada ya apo wakarudi chumbani.

    "Sina nguo yakubadirisha itakuwaje siwezi kuvaa ile nguo ya jana"

    Skola alisema akiwa na hudhuni.

    "Nakupa suluali yangu uvae"

    Alisema Andrew uku akicheka maana yeye mwembamba na Skola ni mnene amejazia hips kubwa na makalio yakutosha mwanaume ata uwe sio rijali ukimuona itasimama tu japo haina miguu. Alibalikiwa haswa tena hakuwa mweupe rangi yake kama chocolate alikuwa mzuri haswa Jose sijui alipatwa na matatizo gani adi akamsaliti.

    Skola alimtizama Andrew nakucheka.

    "Aya nipe nivae tuone kama itafika ata mapajani"

    Alimwambia akamuona Andrew anasogelea kabati lake alafu akachukua nguo zake nakuvaa kisha akatoka nje, alienda adi chumbani kwa mamayake ambae alikuwa ametoka akachukua kitenge kimoja nakurudi nacho chumbani kwake akatafuta kabatini t-shirt yake kubwa kidogo nakumpa Skola avae.

    "Umependeza mke wangu"

    "Asante mumewangu"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakatoka nakuelekea kupata kifungua kinywa.

    Baada yakumaliza Skola akaomba arudi nyumbani ambapo alijiandaa bahati nzuri alikuja na gari lakin Andrew alimuomba waende wote amrudishe kwao basi Wakakubaliana nakuondoka.

    ***

    Bibi Meyan kwasasa anaishi duniani aliongea na mamayake akaomba mizimu ya kwao imkubalie kuishi na mumewake ambae ni babayake Skola, bahati ilikuwa kwake kwani alikubaliwa.

    Ilikuwa furaha sana kwa Bwana Saimon kuishi na mwanamke anaempenda sana Meyan alifurahi kuwanae tena wakafungua ukurasa mpya nakuishi pamoja mume na mke.

    Wakiwa sebuleni wanakunywa chai walisikia geti linafunguliwa na gari kuingia ndani. Wote wakajua atakuwa Skola uyo, baada ya muda mfupi walishuka Andrew na Skola wakapiga hodi nakuingia ndani

    "Waooo wanangu karibuni"

    Alisema bi Meyan akiwakaribisha kwa furaha wakasalimiana na baba yake Skola pia nakukaribishwa chai lakini walikataa sababu tayari walishakunywa.

    Andrew akaaga kuondoka sababu hakutaka kukaa sana alimleta Skola basi wakaagana nakuondoka zake .

    "Naona jana ukanogewa ata kurudi ukashindwa"

    Mama yake Skola akasema uku akicheka

    "Mama bwana alafu we unatabia mbaya ukaniletea nguo yakuvaa nakunificha"

    "Nilikuficha nini mwanangu?"

    "Yani unauliza kama ujui sawa tu"

    Alisema Skola nakuwafanya wazazi wake wacheke.

    "Najua kilakitu Andrew amekwambia sioni haja yakurudia ila tambua Andrew anakupenda sana kiukweli ndio maana nimependa awe mwanaume wa maisha yako kuliko kuangaika kwa wengine wasiojua thamani yako mwisho wakuumize tu mwanangu"

    Alisema bi Meyan akiwa siriazi sasa nakumfanya Skola amsogelee nakumkumbatia mamayake

    "Nashukuru sana mamangu kwa kunijali"

    Basi waliongea mengi nakupanga harusi yao lazima bibi yake Malkia Zayuke awepo kwaiyo itahudhuriwa na majini pia Skola aliogopa kusikia ivyo

    "Watakuwa na umbo la binadamu usijali hawatojulikana"

    Alisema mamayake nakumuondoa hofu.

    Apo Skola akawa na furaha sasa.

    Maandalizi yakaanza ya harusi yao ikabaki wiki moja harusi ifungwe lakini Andrew alikuwa na wasiwasi itakuwaje anaoa jini lakini harusi ifanyike kanisani ikabidi amuulize Skola.

    "Andrew mpenzi kuna majini wengi kama binadamu tu wapo wanaoabudu mungu wa kweli wanamuita Allah pia wapo wakristo, kuna mashetani ambayo ayana dini wapagani, kuna wezi, wahuni, malaya wanaopenda wanaume au wanawake walevi wanaokunywa pombe nakwenda sehemu za starehe yani wakila aina wapo kwaiyo usijali mimi au mamayangu kuwa wakristo na padri atakae fungisha ndoa yetu ni jamii yetu ya majini si binadamu tena majini wanamwabudu mungu kiukweli kuliko binadamu ambao wanaigiza tu"

    Alisema Skola nakumfanya Andrew amuelewe maana alikuwa na wasiwasi.

    Hatimae siku ya ndoa ikafika sasa





    Hatimae siku ya ndoa ikafika sasa, watu wengi walikusanyika kanisani adi wazazi walezi wa Skola walikuwepo pia.

    Aliekuwa akifungisha ndoa ni mjomba yake alietoka ujinini, lakini hakuna aliejua ilo zaidi ya wachache wenye uwezo wakijini.

    Ilipoisha kufungwa bwana na bibi harusi walitoka nje uku kanisa zima likiwa na furaha sana wakiwashangiria adi walipoingia kwenye gari na safari yakuelekea ukumbini ikaanza.

    Watu wote wakajazana kwenye fukwe za bahari kulipokuwa na ukumbi mkubwa sherehe ikafanyika apo.

    Malkia Zayuke alikuwepo pia alipendeza sana.

    Baba na mama Skola walikuwa pamoja wakionyesha nyuso za furaha kwenye sherehe ya binti yao.

    Skola alivaa shela jeupe zuri mfano wa tausi lilimpendeza sana nakumfanya avutie urembo wake uliongezeka muda wote alikuwa anatabasamu tu.

    Muda wa zawadi ukafika walipata vitu vingi sana, bibi yake ambae ni Zayuke alimnunulia nyumba yakuishi bagamoyo karibu na bahari walipenda dana kukaa na bahari sijui kwanini.

    Usiku mkubwa sherehe iliisha bwana na bibi harusi wakatolewa ukumbini nakuelekea honeymoon yao ambayo ilifanyika hotel iliyokuwa karibu na bahari pia.

    Watu nao wakaanza kuondoka wote ata waujinini walitoweka bila kuonekana.

    Bi Meyan na mumewake walirudi nyumbani wakiwa na furaha sana.

    "Nashukuru tumemaliza hii harusi salama"

    Alisema bwana Saimon

    "Mie nangojea wajukuu zangu tu apa"

    Alisema Bi Meyan nakumfanya mumewake acheke.

    ***

    "Andrew siamini kama namimi nimekuwa mke wa mtu sasa"

    Skola alisema walikuwa wamefika, Andrew alitabasamu akamsogelea nakumbusu kisha akamwambia

    "Amini sasa mkewangu mimi ndo mwanaume wa maisha yako"

    Alipomaliza kusema akamvutia kifuani na kukumbatiana.

    Asubuh ilifika wakaamka nakujiandaa kuelekea bagamoyo hawakutaka kukaa hotel honeymoon yao wakaenda kumalizia nyumbani kwao.

    Walipendana sana muda wote wapo pamoja ilikuwa faraja kwao akuna alietamani kuwa mbali na mwenzake

    Baada ya mwezi kupita Skola akaanza kujisikia kuumwa mwilini mara atapike na kizunguzungu pia homa ilimshika ikambidi mumewake amkimbize hospital afanyiwe vipimo.

    "Wewe ni mume wa huyu mwanamke?

    Daktari alimuuliza Andrew akamuitikia walipokuwa ofisini

    "Hongera sana mkeo anamimba ya mwezi mmoja"

    Alimwambia Andrew alifurahi sana

    "Daktari naweza kwenda kumuona?"

    "Usijal hali yake ni nzuri ila mimba tu inamsumbua bado changa lakini anashauriwa kula matunda kwa sana na maji pia afanye mazoezi asiwe mvivu"

    "Nashukuru sana Daktari"

    Alijibu Andrew nakuonyesha furaha imemjaa muda huo Skola alikuwa wodini amelazwa kwani alitundukiwa dripu ya dawa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Andrew aliruhusiwa kumuona alimsogelea nakumkumbatia akimpiga mabusu yasiyo na idadi

    "Kuna nini mumewangu?"

    Skola alishangaa

    "Tunakaribia kuitwa baba na mama mwaah mwanangu nakupenda"

    Alimwmbia nakumbusu tumboni Skola alibaki anacheka tu, mwisho wakaruhusiwa kurudi nyumbani ambapo Andrew akutaka mkewe afanye chochote alifanya yeye mwenyewe.

    Skola alikuwa zaidi ya Malkia mimba ilimpendeza nakunenepa matunzo aliyokuwa anapewa yalimfanya ajione mwanamke mwenye thamani sana hakuacha kumshukuru mamayake kumpatia mwanaume mwenye upendo wa dhati kwake.

    Wazazi wote walijua Skola anamimba wakajiandaa kupokea mjukuu tu.

    Miezi ilizidi kusonga, hatimae akafikisha miezi tisa, uchungu ulimshika sana mumewake akataka kumpeleka hospital lakini akagoma nakumfanya mumewe ashangae

    "Sasa utaki kwenda hospital utajifungulia wapi?"

    Alimuuliza

    "Wanakuja wakunga wa jamii yangu watanizalisha usijali mumewangu"

    Alimwambia Andrew akutaka kupinga akamuelewa, Mara mlango ukagongwa ilikuwa Usiku saa tano

    "Acha nikafungue baki mumewangu"

    "We si unaumwa ngoja niende mimi"

    "Wanamaumbo yakijini usiende unaweza kufa ukiwaona"

    Alisema Skola nakumfanya Andrew amuelewe akamsogelea nakumbusu Skola pia akambusu mumewake nakumpulizia hewa usoni alipotoka tu nje Andrew alipitiwa na usingizi.

    Alienda kuwafungulia mlango wanawake wawili wakaingia ndani.

    Ni wamama hawakuwa wazee,

    Skola akatangulia chumba kimoja wakamfuata Uko

    Walikuwa wanatisha sana nywele zao ndefu waliziachia bila kufunga macho yao yalikuwa kama ya paka bluu sana yenye kuwaka makali zaidi vidole vyao vyembamba

    vilefu vinakucha ndefu pia zakutisha, maumbo yao yalkuwa ya kibinadamu uku wamevaa magauni marefu miguu yao kwato za ngombe wakitembea utazani wamevaa viatu vilefu kunalia ko ko ko.

    Walifika ndani wakamwambia Skola alale kitandani ambapo mmoja alimsogelea nakumpuliza usoni akapoteza fahamu baada ya apo wakafanya maombi yao na yule mtoto wa tumboni akatoka bila kusukumwa na mamayake.

    Alikuwa mtoto wa kiume mzuri sana.

    Alipozaliwa tu Skola akaamka akitabasamu hakusikia maumivu yoyote

    "Hongera umetuletea kidume"

    Alisema mwanamke mmoja uku moshi ukitoka mdomoni Skola alifurahi sana akawashukuru hao wamama wakamuaga nakupotea kimiujiza.

    Alimbeba mwanae adi chumbani kwa mumewake akambusu usoni nakumfanya ashtuke

    "Haaa mke wangu uyo nani umembeba?"

    Alishangaa

    "Mwanao huyu jaman"

    "Haaaa kwani ushajifungua?"

    Andrew alizidi kushangaa

    "Ndio au unaona nina tumbo apa"

    Alisema akiinuka Andrew alimuwahi mtoto nakumbeba uku akimbusu nakufurahia nae.

    "Tumwite junior"

    "Jina zuri"

    Basi wakakubaliana jina lakumpa hakuwa na tofauti na watoto wengine alikuwa kawaida tu kama binadamu.

    Asubuh ilifika ugeni ukawasiri ndani

    Wazazi wote wakaja wakifurahia mtoto aliezaliwa ilikuwa furaha sana.

    "Kuanzia sasa Skola sio muuaji wa kike"

    Alisema bi Meyan nakumfanya Skola afurahi kusikia ivyo.

    Jioni ilifika wakaondoka nakuwaacha wenyewe wanandoa.

    Siku zilizidi kusonga uku junior akiwa mkubwa aliongeza furaha kwenye familia yao upendo ulitawala sana.

    Hatimae akafikisha miaka miwili

    Siku moja wazazi wake wakiwa sebuleni yeye amelala Mara babayake akatoka nakuingia chumbani akamkuta amekaa kakunja miguu uku amefumba macho kitanda kilinyanyuka juu na kila kitu chumbani kikainuka alistaajabu

    "Uyu nae ni jini kwani"

    Alishangaa Andrew mara mkewe akaja nakumshangaa mwanae pia uwezo huo kaupata wapi basi walikaa kumuangalia adi alipomaliza akashuka chini nakila kitu kilarudi sawa akafumbua macho nakutabasamu.

    "Mama na baba"

    Aliwaita wote wakatoka mbio ajabu adi Skola alimkimbia mwanae.

    "Mama uyu mjukuu wako mchawi sijui jini uje kumchukua namuogopa mie"

    Alimpigia simu mamayake ambae alicheka sana

    "Sawa niletee mjukuu wangu"

    Basi wakaanza kushauriana nani aingie chumbani kumuita junior mara ghafla akatokea amevaa nguo nzuri nakupendeza

    "Twendeni kwa bibi"

    Alisema wakabaki wanamuangalia mwenyewe alicheka.

    Basi na wao wakajiandaa nakutoka

    "Mimi sipandi gari"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Junior alikataa

    "Utaenda kwa miguu au?"

    Skola alimuuliza mwanae

    "Njoeni apa tushikane mikono wote tufumbe macho"

    Basi wakafanya ivyo walipofumbua walijikuta wapo nyumbani kwao kwa wazazi wa Skola wakaingia ndani walipokelewa kwa furaha sana

    "Mama sisi atukai mjukuu wako uyo kwaheri"

    Aliaga Skola

    "Ngoja mwanangu nikuambie kitu Malkia Zayuke ndie aliempa uwezo wa ajabu uyu mtoto"

    Alisema nakumfanya Skola amuelewe lakini wakaondoka nakumuacha apo.

    maishs yao yalizidi kusonga junior alikuwa mkubwa nakuacha kufanya maajabu yake wazi.



    MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog