*********************************************************************************
Simulizi : Jeneza La Ajabu
Sehemu Ya Kwanza (1)
Ikulu kwa mfalme ;
“Siwezi kufa
kirahisi namna hii, dunia tamu bwanaaa weeeh, mali zangu hizi nitamuachia
nani?? “,yalikuwa ni maneno ya kejeli kutoka kwa mfalme wa nchi ya
Mwamutapa, baada ya kupokea taarifa kutoka kwa mganga wake wa kienyeji kuwa
kashindwa kumtibu maradhi yaliyokuwa yakimsumbua, hivyo asubili kufa tu. Hali
iliyopelekea mganga yule kujuta kauli yake kwani, mfalme aliamuru auawe kwa
kukatwa kichwa chake, na kisha kiwiliwili chake kitupwe ndani ya bwawa la mamba
waliofugwa na mfalme kwa ajili ya kula watu waliomchukiza na kumpinga katika
uongozi wake. “Yani mimi nife, siwezi kufa mimi, labda utangulie mpuuzi
wewe “,mfalme Mutapa, alijitamba kwa mala nyingine tena, huku akishuhudia
kichwa cha mganga wake kikitenganishwa na kiwiliwili,kutokana na kushindwa
kumtibu mfalme na kumwambia asubili kifo tu, jambo ambalo mfalme alilichukulia
kama katukanwa na kudharauliwa.
Mitaani katika nchi ya
Mwamutapa;http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hali ngumu ya maisha inazikumba familia
nyingi katika ardhi ya Mwamutapa, huku lawama nyingi zikitupwa kwa mfalme,
kwani wanaume wengi wenye nguvu na vichwa vya familia, walitumikishwa kwa nguvu
katika mashamba ya mfalme na kisha kulipwa ujira mdogo,jambo ambalo
lilimchukiza kila raia wa Mwamutapa. Kelele zao za mateso hasikusaidia
chochote, kwani kila mtu aliyejifanya kupinga kunyanyaswa, alijikuta akiuawa
kikatili, hali iliyowaogopesha wengine na kujikuta wakikubaliana na manyanyaso
kutoka kwa mfalme, kwani waliogopa kifo.
“Naamini ipo siku
yatakwisha, usilie mama yangu “,ilikua ni sauti kutoka kwa kijana mkakamavu
Njoshi, akimunyamanzisha mama yake, baada ya kupokea taarifa za kifo cha mume
wake kwani alishindwa kumtibu mfalme. “Mwanangu baba yako kaondoka,
tumebaki wawili tu, nakuomba uachane na Grace, mfalme atakuua na wewe, tegemeo na faraja langu lililobakia
“,mama Njoshi alizidi kulia kwa uchungu, huku akimusisitiza mwanae
kuachana na Grace,msichana mrembo sana na mtoto pekee wa kike wa mfalme. Jambo
ambalo kwake aliliona ni gumu sana na halitowezekana, kwani alimpenda sana
Grace licha ya kupokea vitisho mala
kadhaa kutoka kwa mfalme ili aachane na Grace. Na kila mala mfalme alipojaribu
kumuua Njoshi alishindwa, kwani alifanikiwa kutegua mitego yote aliyotegewa ili
aweze kufa, kwani alikua ni hodari sana na aliweza kulishinda jeshi la mfalme
mala nyingi, moja ya sababu ambazo Grace zilimfanya ampende sana Njoshi, kwani
alihitaji mwanaume atakaye muoa awe ni shujaa na si mwanaume suruali tu,
asiyeweza kumlinda na hatari yoyote.
“Usjali mama, mimi
nipo siku zote, nitakulinda, lakini naamini ipo siku Mwamutapa itakua huru, na
mimi nitakuwa kiongozi wake “,kijana Njoshi aliongea kwa ujasiri na
kujiamini kwani ziku zote alifanya mazoezi ya kila aina, ili tu siku moja
afanye mapinduzi na kuokoa wananchi dhaifu kutoka kwenye utumwa na uongozi wa
mabavu wa mfalme Mutapa, jambo ambalo mama yake aliliona kama ndoto ya mchana,
ambayo Njoshi alikuwa akiota.
“Mwanangu banaa
unanifurahisha, hebu toa upuuzi wako huko “,mama Njoshi aliongea huku
akitabasamu kwa mbali kutokana na maneno aliyoambiwa na mwanae, na kumfanya
asahau machungu ya kumpoteza mume, japokuwa alikuwa ameshazoea na kuona kama
vifo ni jambo la kawaida katika familia yake, huku akikumbuka jinsi wanae
watatu walivyopoteza maisha kutokana na njaa kali iliyotokea miaka kadhaa
iliyopita, na kumuachia Njoshi pekee. “Nakuombea mwanangu, ndoto zako ziwe
kweli “,mama alizungumza huku akimkumbatia mwanae, bila kutambua kuwa
Njoshi alijawa na hasira, huzuni na machungu kwa kumpoteza baba yake na kuapa
kulipiza kisasi, kwani hakutaka mama yake agundue huzuni hiyo na kuzidi kumpa
machungu mama yake aliyempenda sana.
Ikulu kwa Mfalme :
Mganga maarufu wa kienyeji aliyesifika
katika nchi ya Mwamuyeshi, nchi iliyopakana na Mwamutapa, na kuongozwa na
mfalme Muyeshi ,anafika ikulu kumtibu mfalme maradhi yake, baada ya Muyeshi
kupata taarifa za rafiki yake mpendwa kuugua kwa muda mrefu, hali iliyopelekea
kumtafuta muganga katika ardhi yake ili amsaidie rafiki yake asiweze kupoteza
maisha. “Karibu sana katika ardhi ya Mwamutapa,,, naamini rafiki yangu
ndiyo kakutuma hapa “,mfalme Mutapa aliongea bila shida yoyote huku
akitabasamu,huku akiwa amelala katika kitanda chake kwa takribani mwezi mmoja
sasa bila kuamka kutoka kitandani, japo aliweza kuzungumza vizuri kama vile hakuwa
mgonjwa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Ndiye mimi mtukufu mfalme, mganga
kutoka katika ardhi ya rafiki yako Muyeshi, nimekuja kukusaidia “,mganga
yule aliongea huku akijiamini, na kumfanya mfalme atabasamu kwani hakupenda
kufa, na alitamani aishi milele jambo ambalo mganga yule alikua ameshalitambua.
“Usjali mtukufu
mfalme, mpaka sasa nimeshachelewa siwezi kukutibu, muda wowote kuanzia sasa
utaweza kufa, lakini inatakiwa ukifa uzikwe ndani ya jeneza lililotengenezwa
kutoka katika miti iliyo katikati ya msitu hatari wa Majini, msitu ambao uko
katika ardhi yako ya Mwamutapa, ukizikwa ndani ya jeneza hilo, utaweza kufufuka
baada ya wiki moja na kuishi milele “,mganga yule alizungumza maelezo
marefu sana, huku jina la kijana Njoshi likijirudia rudia ndani ya kichwa cha
mfalme, kwani ndiye kijana pekee aliyemuona anafaa kufanikisha swala hilo, na
kutoka akiwa salama katika msitu hatari wa Majini, msitu ambao hakuna aliyewahi
kuingia humo akitaka mali, watoto au ufalme kutoka kwa mizimu ya msitu huo na
kutoka salama bila kupoteza maisha. “Na pia inatakiwa iwe siri, raia wako
wasifahamu labda tu atakayekwenda huko msituni “,mganga alizidi kuzungumza
huku mfalme mawazo yakiwa mbali sana, kwani mwanae Grace alishamuonya kuwa
Njoshi siku akipata matatizo yaliyosababishwa na yeye, ataweza kujiua, jambo
ambalo mfalme hakuwa tayali kumkosa mwanae wa kike pekee aliyenaye, kati ya
watoto arobaini kutoka kwa wake watano alionao ,mtoto ambaye alizaliwa na mke
wa tano baada ya wake zake wanne waliotangulia kushindwa kumzalia mtoto wa
kike.
“Sawa …sawa sa…wa ni…me…kusikia
“,mfalme alijibu bila kujitambua huku mawazo na maswali lukuki
yakikisumbua kichwa chake .
Ikulu kwa mfalme;
Ngome ya mfalme
inakumbwa na majonzi mazito ,kutokana na hali ya mfalme kuwa mbaya sana. Wapo
waliofurahi kumuona katika hali ile, hasa wananchi wake ambao hawakupendezwa na
uongozi wake huku wakitamani afe haraka, waweze kuwa huru kutoka katika taabu
na mateso yaliyosababishwa na uongozi wake wa kikatili wa mfalme Mutapa. Lakini
wachache walihuzunika sana, hasa watoto wake pamoja na wake zake mfalme, huku
wakimuomba Mungu amuepushe na umauti.
“Mfalme mimi
ninaondoka kurudi nyumbani, lakini zingatia yale yote niliyokuambia, kwani kama
unavyoiona hali yako inazidi kuwa mbaya, usipokuwa makini mali zako na ufalme
wako utakwenda na maji “,asubuhi na mapema, mganga kutoka katika ardhi ya
Mwamuyeshi, akiwa ameshika kila kitu kwa ajili ya safari yake ya kurudi
nyumbani, anamuaga mfalme huku akimsisitiza kuzingatia maelekezo aliyompatia na
kisha kupanda farasi na kuondoka, huku akiongozana na askari wawili aliokuja
nao kwa ajili ya kumlinda njiani, askari waliotoka katika ngome ya mfalme
Muyeshi.
Mfalme Mutapa akitikisa
kichwa chake kuashiria kukubaliana na maelekezo ya mganga, na kumshuhudia
akitokomea mbele ya uso wake, anaamua kutoa amli kwa kutumia maandishi Njoshi
kufika ikulu haraka sana, kwani mfalme alishindwa hata kuzungumza hali
iliyowatia hofu watoto wa mfalme pamoja na wakeze.
“Baba nakuombahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
usimdhuru Njoshi kwa chochote kile, lolote baya likimtokea sitajali hali yako
mbaya uliyonayo, nitakuua “,Grace aliongea huku akionesha kumaanisha kwa
maneno aliyoyazungumza, bila kujali ni kiasi gani alimpenda baba yake aliapa
kumtoa roho kwa mikono yake, kama tu kipenzi chake Njoshi akidhurika na jambo
lolote na kuacha familia nzima ya
mfalme ikiwa midomo wazi, kwani hawakuamini maneno yale kama yalitoka kinywani
kwa Grace, msichana aliyependwa sana na mfalme.
“Hahaa, sasa mpaka
wewe unamuua baba, sisi tutakua wapi, labda uanze kutuua sisi “,Kijana
mkubwa wa mfalme, kijana ambaye Mutapa alimuamini sana na kumuahidi kumrithisha
ufalme na mali zake, kutokana na uhodari wake alizungumza kwa kejeli, na
kupelekea familia nzima kucheka na kusahau hali mbaya ya mfalme aliyokuwa nayo.
Ghafla mfalme alitoa
amli ya familia nzima kukaa kimya kwa kutumia ishara, huku akitaka agizo la
Njoshi kufika ikulu, litekelezwe mala moja bila kujali onyo kali alilopokea
kutoka kwa binti yake Grace, mtoto pekee wa kike aliyempenda sana.
Nyumbani kwa kina
Njoshi;
Ilikua siku ya jumatatu
asubuhi, kama kawaida Njoshi hufanya mazoezi makali katika siku hii kwani wiki
nzuri huonekana siku hii, hivyo aliamini akifanya vizuri mazoezi siku ya
jumatatu, atakuwa fiti wiki nzima. Aliamka saa kumi na moja asubuhi, na kuanza
mazoezi ya kukimbia, siku zote alipenda kukimbia huku akiimba, kwani alikatiza
mitaa karibu yote ya nchi ndogo ya Mwamutapa, bila kujitambua kwani nyimbo
alizoimba zilimtia moyo na kumuondolea uchovu. “Ngoja nikimbie, nikimaliza
nije kunyenyua vyuma, ukombozi sio lelemama lazima wachache tuumie
“,Njoshi aliongea kwa ujasiri huku akitamani siku moja aweze kuishika nchi
na yeye kuwa mfalme, huku Grace akiwa malikia, kwani msichana mrembo Grace
alipendwa sana na wananchi na aliwaokoa mala nyingi walipokuwa wakionewa na
baba yake pamoja na kaka zake, kwani aliwaombea msamaha na kusikilizwa.
Walimuona kama ndio kondoo pekee aliyeishi ndani ya kundi la simba. Njoshi
alizidi kukimbia lakini bila kutegemea alijikuta akiishiwa na pumzi haraka sana
tofauti na siku zingine, bila kupoteza muda aliamua kurudi nyumbani kufanya
mazoezi mengine. “Mwanangu kweli wewe ni shujaa, natamani ndoto zako
zitimie nikiwa hai nishuhudie ukiwakomboa Wanamutapa wote “,ilikua tayali
imeshafika saa moja asubuhi, mama yake Njoshi aliweza kuamka na kumkuta mwanae
akiendelea na mazoezi, na kuzungumza maneno makali yaliyomshitua sana Njoshi,
haikuwa kawaida kwa mama yake kumwambia maneno mazito kiasi kile.
Njoshi alisitisha
mazoezi na kisha kutaka kumuulza mama yake, kwanini alizungumza vile, kwanini
mama yake asishuhudie ukombozi ambao mwanae alikuwa akiupanga, mama yake kaona
nini mbeleni katabili nini. Njoshi alizidi kujiuliza maswali kichwani mwake,
huku akimsogelea mama yake, mke wa marehemu Nyangoma, mganga na mtabili
aliyekuwa akitegemewa sana na mfalme Mutapa. Kutokana na kutabili kuwa ipo siku
mfalme atamuua kikatili bila kujali mema yote aliyomfanyia, aliamua kumfundisha
uganga na utabili mke wake, ili siku akifa mke wake aweze kurithi mikoba.
“Mwanangu Njoshi
Nyangoma, naona hatari kubwa iko mbele yako, utasafiri safari ndefu yenye visa
na mikasa ya ajabu ,mkanda huu mweusi na panga hili ndio siraha yako kuu,
iliyomuwezesha baba yako kutoka salama katika msitu wa majini, usikatae kwenda
huko, huko ndipo utaupata ufalme wa nchi hii, lakini ukirudi nyumbani utakuta
kabuli langu, mimi nikiwa tayali nimeshakuwa mifupa “,mama Njoshi
alizungumza kwa uchungu sana huku machozi yakimtoka, na kumkabidhi mwanae begi
dogo jeusi,kwani ndio ulikuwa mwisho wa kuonana yeye na mwanae mpendwa Njoshi.
“Sikuelewi mamahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
unaongea nini, mimi msituni huko niende kufanya nini sasa, kwanza huwezi kufa
mimi nitakulinda mpaka dakika ya mwisho “,Njoshi aliongea huku akimfuta
mama yake machozi, huku mama yake akiukumbuka ule msemo wa wahenga, msemo ambao
ulikua maarufu sana enzi zile afrika ikitawaliwa na wazungu, msemo uliosema
jambo usilo lijua ni kama usiku wa giza.
Njoshi akiwa
amemkumbatia mama yake, akizidi kumbembeleza aweze kunyamanza, alishangaa kuona
kundi kubwa la vijana shupavu, likiwa limevalia bukta fupi nyeusi, pamoja na
ngozi ya chui, huku mikononi wakiwa wameshika mikuki na kila aina ya siraha za
kivita, bila shaka aliweza kuwatambua, lilikuwa ni jeshi la mfalme Mutapa.
“Aiweeeeeeh
………Njoshi, aiweeeeh ………”,askari wale waliweza kumsalimu Njoshi, na
kumfanya mama yake kuacha kumkumbatia mwanae na kushuhudia watu wale
waliomsalimia mwanae. “Aiweeeeeh ………askari waaminifu wa mfalme wangu wa
ardhi ya Mwamutapa, niwasaidie nini? “,Njoshi aliitikia salamu kwa upole
na hekima, huku akiificha hasira yake na kisasi kizito kilicho rohoni mwake,
kutokana na baba yake kuuawa kikatili na mfalme.
Kwa upande wa mama yake
hakushangaa chochote, kwani alikwishaona kila kitu kitakachotokea mbele, na pia
siri ya mfalme ambayo wananchi hawakutakiwa kuifahamu, kuhusu kuzikwa mala
atakapokufa na kisha kufufuka bila wananchi kutambua chochote, ili aweze kuishi
na kutawala milele.
“Tumekuletea
ujumbe huu wa maandishi kutoka kwa mfalme, mkwe wako tafadhali pokea ……iweeeeh
“askari wale waliongea huku, mmoja aliyeonekana kuwa na cheo kikubwa kuwazidi
wenzake kutokana na kuvaa ngozi ya simba, ngozi iliyokuwa ikivaliwa na kila
kiongozi wa nchi ya Mwamutapa, akimkabidhi Njoshi karatasi yenye maandishi na
kisha kuisoma.
“Iweeeeeh …mkwe
wangu, nakuomba katika ikulu yangu, ninashida na wewe, nataka tuwekeane mkataba
ili uweze kumuoa binti yangu Grace “,Njoshi alisoma maneno yale na kisha
kutabasamu, tabasamu ambalo liliwafanya askari wale wa mfalme kuangaliana na
kisha kukonyezana, hali iliyoonesha kutambua siri fulani iliyokuwa imefichika.
“Mama peleka begi
hili ndani, mimi ngoja nikaonane na mfalme “,Njoshi aliongea huku
akionekana kufurahia sana, kwani hakuamini kama ipo siku mfalme atamtamkia kuwa
yeye ni mkwe wake,kwani siku zote aliambulia matusi na kutishiwa kifo,
alipoingia anga za mfalme Mutapa.
“Hapana mwanangu,
kama unanipenda, naomba hilo begi lisitoke mgongoni mwako “,mama yake
Njoshi aliongea huku akiwa na huzuni moyoni, huku akijaribu kutabasamu kuficha
huzuni yake, kwani huo ndio ulikuwa ni mwisho wa kuonana na mwanae katika ulimwengu
huu.
Msitu wa Majini;
Ilikua mida ya jioni siku ya jumatatu ,
tetemeko la kutisha linatokea katika msitu wa majini,Malikia wa msituni,
kiongozi aliyemiliki msitu na kuongoza viumbe vyote vilivyopatikana ndani ya
msitu anaamua kuitisha kikao, kwani tetemeko lile liliashiria jambo fulani,
kama ilivyozoeleka katika msitu huo, tetemeko likitokea basi muda wowote msitu
ulikua hatarini kuvamiwa.
“Ndugu zanguhttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
majini, mapepo na mizimu ya mababu zetu, msitu wetu uko hatarini kuvamiwa ,na
niwajibu wetu kuulinda msitu huu, pia inatakiwa tulipize kisasi kwani mtu
anayekuja kuvamia msitu huu, baba yake aliwahi kuja hapa msituni na kuua ndugu
zetu na kisha kutokomea na baadhi ya mali zetu ili awe mganga na mtabili
hodari, japo ameshapoteza maisha “,malikia alizungumza kwa hasira, katika
kikao cha ghafla alichokiitisha muda mfupi baada ya tetemeko kutokea, huku
umati wa viumbe hatari sana wa msitu wa majini, msitu uliokua na utajiri
mwingi, zikiwemo dhahabu na almasi, wakiwa makini kumsikiliza malikia wao na
kujiandaa na mapambano.
“Aiweeee mtukufu
malikia wa msitu huu,tuko tayali kutekeleza maagizo yako, na kuua chochote
kitakachokanyaga ardhi hii “,ilikua ni sauti ya majini waliohudhuria
kikao, huku wakijawa na uchu wa kulipiza kisasi hasa wakikumbuka jinsi mzee
Nyangoma, baba yake Njoshi jinsi alivyofanikiwa kuiba mkanda pamoja na panga
lenye nguvu za ajabu, na kutoroka navyo huku akiua baadhi ya majini, kitendo
kilichowakasilisha viumbe wote wa msituni.
Ikulu kwa mfalme;
Kijana Njoshi anafika ikulu kwa mfalme
na kushangazwa na jambo aliloliona mbele ya macho yake, hali ya mfalme ilikua
mbaya sana kiasi kwamba hakuweza hata kuinuka kitandani wala kufungua kinywa
chake na kutamka neno lolote lile, kwa upande mwingine alitamani mfalme apoteze
maisha kwani aliona ndio utakuwa mwanzo wa ardhi ya Mwamutapa kuwa huru kutoka
katika uongozi wake wa kidikteta ,na pia yatakua ndio malipo ya dhambi zote za
mauaji aliyoyafanya, huku baba yake akiwa miongoni mwa watu waliouawa kikatili
na mfalme.
Njoshi akiwa bado
amepigwa na butwaa, alianza kupata picha kuwa inawezekana aliweza kudanganywa
kuwa aliitwa na mfalme ili aozeshwe Grace,kwani kwa wakati ule, machozi ya
huzuni hayakukatika machoni kwa Grace,na kumfanya aamini mawazo yake, kuwa
palikuwa na tatizo nyumbani kwa mfalme.
“Aiweeeeeh mtukufu
mfalme, mtumwa wako Njoshi Nyangoma nimeitika wito wako, aiweeeeh ……mfalme
Mutapa udumu milele”,Njoshi aliongea huku akiwa amesimama mbele ya kitanda
cha mfalme, huku familia nzima ikiwa imekaa kimya, wakimuomba Mungu Njoshi
akubaliane na ombi la mfalme, kwani waliamini mfalme hata akipoteza maisha
ataweza kufufuka ndani ya wiki moja, jambo ambalo lingewezekana kama angezikwa
ndani ya jeneza la ajabu, jeneza ambalo Njoshi inatakiwa akalitengeneze kwa
kutumia miti inayopatikana katikati ya msitu wa majini na kisha kuja nalo ikulu
kwa mfalme.
“Kijana wangu
Njoshi, utafanikiwa kumuoa binti yangu Grace, na kumiliki nusu ya ufalme wangu,
kama tu ukikubali kwenda katika msitu wa majini, na kutengeneza jeneza kisha
kuja nalo hapa “,yalikuwa ni maneno yaliyoandikwa kwa maandishi na mfalme,
maneno ambayo Njoshi aliyasoma na kisha hofu ya kifo kumuandama, kwani hakuna
mtu aliyewahi kupona kutoka katika msitu wa majini, isipokuwa baba yake
pekee.Njoshi alikumbuka maneno ya mama yake alimwambia kuhusu hatari hii, na
kisha kumsihi asikatae kwenda kwani huko msituni ndiyo sehemu pekee ya kuupata
ufalme, pia Njoshi alikumbuka siraha alizopewa na mama yake na kuziweka ndani
ya begi kisha kumsihi asiweze kulitupa begi hilo.
“Ndiyo mfalmehttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/
wangu mtukufu, nimekubali, aiweeeh mfalme udumu milele, “Njoshi alikubali
ombi la mfalme, na kufanya nyuso za familia nzima ya mfalme kutabasamu kwa
furaha, isipokuwa Grace, kwani hakutaka mpenzi wake kwenda msituni ndio maana
alikuwa akilia toka mwanzoni, na wala hakulizwa na hali mbaya ya baba yake
aliyonayo, bali jambo ambalo Njoshi aliweza kuitiwa ikulu, lilikuwa la hatari
sana na aliamini atampoteza mpenzi wake kama atakubali ombi la baba yake.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment