Karibu Katika Maktaba ya Simulizi, Riwaya, Chombezo na Hadithi Afrika Mashariki. %% Welcome to the Library of Stories, Novels, Comedy and Stories in East Africa.
BURE SERIES: https://bure0.blogspot.com/
Hakujua
sasa cha kufanya. Kila mtindo alitumia lakini haikusaidia. Ilifikia kipindi
akawa anapitiwa na usingizi ingali amesimama. Alimweka mtoto kitandani kwa
kulazimisha akaendelea kumbembeleza hapohapo, kidogo akapitiwa na
usingizi.
Kama baada ya dakika mbili akakurupushwa na hodi ya
tatu mlangoni mwake. Akauliza, “Nani?”
“Dada wa
kazi!”
“Unataka nini?”
“Mtoto anasumbuliwa na
nini?” dada akauliza.
“Si nilishakwambia!” Darren akafoka
kidogo.
“Naomba nimbembeleze,” sauti ya dada
ikaomba.
“Nimesema nambembeleza mwenyewe.
Hukunielewa?”
Kukawa kimya kidogo.
Punde sauti
ya dada ikasema tokea mlangoni, “Utanipa nimbembeleze ama nije nimchukue
mwenyewe?” mara hii sauti ilikuwa na amri ndani
yake.
.
Darren akajawa na hofu. Akamnyakua upesi mtoto
wake na kumfichama kwenye mikono yake akiwa anatazama mlango kwa hofu. Punde
mlango ukaanza kubamizwa kwa nguvu na kwanguvu! Darren akajaribu kuteka simu
yake atoe taarifa polisi lakini hakuiona. Kwa muda alikuwa kama mtu
aliyechanganyikiwa. Hakujua cha kufanya.
Mlango ukaendelea
kubamizwa na kubamizwa. Mwishowe ukaanza kudhoofu na kubomoka. Vipande vyake
viliruka huku na huko. Ilikuwa ni ajabu mbomoaji alikuwa anatumia nyenzo gani
kufanyia zoezi lake hilo.
Darren alichofanya ni kutwaa kipande
kidogo cha mbao ya mlango na kubebelea kama silaha. Ni ajabu kama mtu ameweza
kubomoa mlango atamzuiaje kwa kipande cha mbao, lakini alikuwa na
imani.
Mkono wake uliobebelea kipande hicho cha mbao ulikuwa
unatetemeka. Macho yamemtoka na paji lake la uso linatiririsha
jasho.
“Ni nani wewe?” Darren akauliza kwa sauti yenye kusita.
Hakujibiwa. Kilichokuwa kinafanyika ni mlango kubamizwa tu! Tena kubamizwa
kwanguvu mno.
Kidogo, kwasababu ya hofu na kukurupushwa
usingizini, mtoto naye akaanza kulia. Alikuwa analia kwanguvu haswa kiasi cha
kumchanganya Darren. Ingawa Darren alimsihi anyamaze, haikusaidia
kitu.
Mwisho wa siku mlango wote ukawa upo chini na mlangoni
akiwa amesimama mwaname anayechuruza damu mikononi. Mwanamke huyo si mwingine
bali dada wa kazi. Mikono yake ilikuwa imejeruhiwa vibaya mno kwa kubamiza
mlango hata kuvunjika. Macho yake yalikuwa makubwa yanayong’aa, uso wake
umepauka kuwa mweupe.
Alimtazama Darren kisha akainamisha
shingo yake kwenda kushoto na kulia, kisha kulia na kushoto. Akamnyooshea kidole
Darren pasipo kusema jambo. Alafu kama mtu aliyegandishwa na barafu, akaanza
kupiga hatua kumwendea Darren.
Darren akamtisha na kipande
chake cha mbao, “Kaa mbali!” akafoka. “Kaa mbali na mimi!” lakini mwanamke yule
hakuwa anasikia wala kujali, akaendelea kusonga kumfuata Darren, na
alipomkaribia akanyoosha mikono yake yote miwili na kisha
akasimama.
Kukawa kimya kidogo. Darren akamtazama mwanamke huyo
kwa hofu na maulizo. Naye mwanamke huyo akawa anamtazama Darren kwa macho ya
kumpembua. Kidogo akashusha macho yake kwa mtoto na kumtazama kwa sekunde
kadhaa, alafu akasema kwa sauti ya kukoroma, sauti ya chini, “namtaka huyo
mtoto.” alafu akahema kwanguvu na kusema kwa sauti ya hewa, “Nipatie, nami
nitaenda nisirudi nyuma!”
“Wewe ni nani?” Darren akauliza akiwa
anamshikilia vema mwanaye. Alikuwa amejiminyia kwenye kona akitamani kutoboa
ukuta atokee nje.
Yule kiumbe akamtazama Darren alafu
akapindishia shingo yake kushoto. Aliporejesha shingo yake kulia, akasema, “Mimi
Melissa.”
“Melissa!” Darren akastaajabu. Hakujua alipata wapi
nguvu ila alijikuta akisimama huku akitusi na kulaani. “nimekwambia kaa mbali na
mimi Melissa!” punde akazabwa kofi lililomtupia ukutani yeye na mwanaye. Kwa
muda kidogo akashindwa kuelewa kinachoendelea. Kwa mbali alisikia sauti ya
mwanae ikilia sana lakini hakuwa anaweza kufanya kitu.
Kama
baada ya dakika tano, akiwa ameanza kupata nguvu, akasikia sauti
yaita,
“Hey! Helloooow!” kidogo mwanga ukatua kwenye macho yake
yalofumba, akayafinya na kuyafumbua akiwa anajikinga na mkono wake wa
kuume.
“Upo sawa?” alisikia sauti inauliza. Kidogo akabaini
sauti hiyo inatokea dirishani. Walikuwa ni majirani, wanaume wawili. Mmoja
alikuwa amebebelea bunduki kubwa na mwingine amebebelea gongo kubwa na kurunzi.
Walikuwa wamesikia zile kelele na walikuja kutazama jirani yao amepatwa na
nini.
Kabla Darren hajajibu kitu, alitazama kwanza kando yake
kumtafuta mwanaye. Akamwona akiwa amelala kama hatua tatu tokea alipo. Alikuwa
kwenye ukimya wa mbao. Na dada wa kazi alikuwa amelala kwa pembeni yake naye
akiwa kimya.
Upesi akamfuata mwanaye na kumtazama. Hakuwa na
dalili ya uhai. Alimwita na kumwita lakini ikiwa bure, mtoto hakuitika kwa
kucheka wala kulia. Darren akapatwa na hofu kubwa sana ya kumpoteza mwanaye.
Alimtikisatikisa aone kama ataamka lakini napo haikusaidia. Mtoto alikuwa
amenyamaza. Alikuwa amenyazama milele.
Darren
akapiga magoti na kugugumia kwa kilio. Alipata hasira sana. Alinyanyuka kama
mbogo akamwendea dada wake wa kazi na kumvuta kwanguvu akimuuliza amemfanya nini
mtoto wake, lakini dada naye alikuwa kimya. Hakuweza kuongea wala kujitetea kwa
njia yoyote ile.
Darren asijali, akaanza kumuadhibu dada huyo
kwa kumkandika mateke. “Shetani! Shetani! Shetani mkubwa wewe!
Nitakuua!”
Kama si majirani kuvunja mlango na kuja kumshika,
sijui hatma ilikuwa ni nini. Waligundua dada wa kazi alikuwa yu mzima, ila kama
mtu aliyekuwa kwenye ‘coma’, hali mfu ya kupoteza fahamu, ila mtoto alikuwa
amekwishafariki.
Basi dada wa kazi akawahishwa hospitali kwa
matibabu zaidi. Mtoto naye akapelekwa huko kuhifadhiwa kwa ajili ya mazishi, na
Darren pia, kwakuwa alihisiwa anaweza akawa si mzima, naye akapelekwa
hospitali.
**
Baada ya juma moja
…
Darren alikuwa ameketi kwenye kingo ya bahari. Alikuwa
amevalia bukta na miguu yake ikiwa tupu pasi na viatu.
Upepo
ukimpuliza taratibu, alikuwa anatazama bahari kwa umakini. Kuna kitu alikuwa
anawaza kichwani ingawa macho yake yalikuwa yanatazama mawimbi ya bahari. Mkono
wake wa kuume ulikuwa umebebelea mchanga, ila akiwa ameuminya kana kwamba
anataka kuukosesha hewa.
Macho yake mekundu yalitazama mbali na
karibu ya bahari. Yalitazama kushoto na kisha kulia ya bahari alafu akashusha
pumzi ndefu. Akanyanyuka na kuanza kurandaranda.
Alitembea
akiwa anawaza na kuwazua kichwani mwake. Kila alipofunga macho alimwona mwanae,
alimwona mkewe. Ilikuwa ni ajabu na ghafla kwake. Kuna muda hakuwa anaamini kama
Josephine hakuwapo naye, wala mtoto wao. Ilikuwa inamuwia ugumu sana kuamini
kuwa yu mwenyewe hatimaye.
Alihisi maisha yake yanaparanganyika
kama kioo kilichobondwa na jabali. Alikuwa anahisi hana umuhimu wowote maishani
hivi sasa. Alikuwa anajihisi mfu anayetembea.
Alikunja ngumi
yake akiendelea kutembea. Aling’ata meno yake na kutazama bahari tena, alafu
punde akasema, “Melissa!” kwa sauti ya kufifia. Akarudia tena, “Melissa.
Melissa. Melissa!” alafu akaapa, “Nitakumaliza kwa mkono wangu mwenyewe.
Nitakumaliza Melissa!” alipomaliza kusema maneno hayo macho yake yakawa
yanamwaga machozi. Alishindwa kujizuia kuumia. Moyo wake ulikuwa unavuja
damu.
Jua likiwa linaanza kuwa kali kumaliza asubuhi, Darren
akajirejesha kwenye gari lake na kutimka kuelekea upande wa magharibi. Alitembea
kwenye gari kwa takribani masaa matatu kabla ya kuja kukomea kwenye nyumba kubwa
namba 4089 kibaoni. Nyumba ya mwanamke yule aliyemwona mtandaoni kwa swala la
mtoto wake kuwa na chapa mwilini.
Kabla hajashuka na kuzama
humo, akalipekua kwanza jengo hilo kwa macho yake mepesi, kisha akashuka na
kuliendea. Alipogonga kidogo akafunguliwa na mlinzi, akajitambulisha na mlinzi
akamruhusu kuingia ndani maana alikuwa na miadi na mwenye
nyumba.
“Nilipata shida sana. Nilitafuta kila namna
lakini haikusaidia. Na nakumbuka vema ikiwa ni usiku wa manane, nikampoteza
mwanangu wa pekee!”
Darren akataka kujua zaidi kumhusu mwanamke
huyo. Mbali na mtoto je yeye alishawahi kukumbwa na kadhia yoyote ile? Basi
mwanamke yule akaeleza kuwa kwa kitambo kifupi baada ya mama na baba yake
kufariki, ndipo alipoanza kuona mambo fulani ya ajabu ndani ya mji wao. Mwanzoni
alikuwa anadhani anawehuka na labda ana laana na ule mji, hivyo akafanya kuhama
aende mbali.
Alipoenda huko, akatuama na kuanzisha familia
ambayo iliishi kwa amani mpaka pale mambo yalipokuja kuibukia katika namna
ambayo hakuwa anaweza kuelewa vema.
“Ninachokumbuka ni kwamba,
baada ya tetemeko kubwa la ardhi lilitokea miaka mitano nyuma, maisha yangu
yakaanza kubadilika kwa wepesi sana. Sikuwa tena mtu wa amani bali kuona vituko
na viroja. Mtu wa kuona mambo ya ajabu yasiyokuwa na mithili. Ajabu ni kwamba,
baada ya mtoto wangu kufariki, mambo hayo yalipotea mpaka
sasa.”
“Na vipi kuhusu mume wako?” Darren akadadisi. Charlie
akatabasamu kwanza ila macho yake yakiwa kinyume. Alitazama chini kwa sekunde
chache kabla hajabinua kinywa chake na kusema, “Alikuwa mwanaume niliyekuwa
namhitaji. Mwenye kujali na kujua kupenda. Nilijihisi nimekamilika nilipokuwa
naye. Alinifanya nisahau kifo cha wazazi wangu kwa muda kwani alikalia sehemu
tupu ambayo iliachwa wazi.”
Akadondosha chozi. Akalifuta kwa
kidole chake onyeshi kabla hajaendelea kuongea, “nilimpoteza kwenye ajali!”
akapandisha mabega yake akisema, “sijui nini kilitokea lakini aliacga daraja na
kutumbukia baharini. Waokozi walipokuja kumtazama, hakuwa hai
tena.”
“Gari lake lilipata hitilafu?” Darren
akauliza.
“Sidhani,” Charlie akajibu. “Gari lake lilikuwa sawa
kabisa isipokuwa tu sehemu ambayo iligonga daraja. Sijajua kumhusu yeye. Sijajua
alikuwa kwenye hali gani. Ila kwa mujibu wa shuhuda wa tukio, mume wangu
alibamiza kioo chake cha pembeni kwanguvu kabla gari halijapoteza mwelekeo na
kudumbukia.”
Kwa namna moja Darren akaona simulizi ya huyo
mwanamke inawiana na ya kwake. Kwa kutaka kuhakikisha zaidi, akamuuliza Charlie,
“Kuna mtu yeyote ambaye ulikuwa naye kwenye mahusiano kabla ya mumeo? Namaanisha
mpenzi wako wa kwanza?”
Charlie akafikiri kidogo kabla
hajasema, “Niliwahi kuwa naye. Ila ni kipindi cha zamani za utotoni. Sichukulii
mahusiano yale kama yalikuwa serious.”
“Je haujawahi kumwona
mwanaume huyo uliyewahi kuwa naye kwenye mahusiano? Yaani baada ya kuoana na
mumeo? Au kipindi chochote kwa namna yoyote?”
“Hapana,” Charlie
akakataa. “Sijawahi kuonana naye tangu kipindi hicho.”
Hapa
kidogo Darren akajiona ni wa tofauti na Charlie. Mbona yeye anasumbuliwa na
Melissa? Basi akaamua naye kumshirikisha Charlie kuhusu habari zake. Alipomaliza
kumweleza kila kitu, Charlie akamuuliza Darren, “Unapajua anapokaa huyo
Melissa?”
“Ndio, napajua,” Charlie
akajibu.
“Naweza nikaonana naye?” Charlie akauliza akiwa ametoa
macho kidogo.
Darren akanyamaza kidogo kisha akasema, “Si
mtu mzuri kama unavyoweza kudhani.”
“Najua,” Charlie
akamkatiza. “Sitegemei awe mtu mzuri, ila ningependa kuonana
naye.”
“Kwanini? Huoni utakuwa umejiweka kwenye
hatari?”
“Hatari ipi, Darren? Nimepoteza mume na mtoto wangu,
kuna hatari nyingine zaidi ya hiyo?”
Kimya kidogo. Charlie
akaendelea kuzungumza, “Nadhani kuna maswali yangu atakuwa na majibu
nayo.”
“Yapi hayo?”
Hapa Charlie akamweleza
Darren kuwa anahisi mama yake alikuwa ni mtu mwenye agano tokea nyuma. Mara kwa
mara mama yake alikuwa anamwambia kuwa maisha yake hayatakuwa ya furaha kwakuwa
yeye ni kizazi cha shetani. Damu yake inachembechembe za majini. Alipotaka kujua
zaidi, mama yake hakumweleza kwa kumwambia muda bado mpaka pale utakapowadia na
basi atajua.
“Una picha ya mama yako?” Darren akauliza. Charlie
akafungua simu yake na kumwonyesha Darren picha ya mama yake, “huyu hapa wa
kwanza upande wa kulia.” darren alipotazama vema, akagundua sura ya mama huyo
haikuwa ngeni. Ilikuwa ni sura anayoijua. Aliionea wapi? Akajiuliza akirusha
macho huku na kule.
“Vipi, Darren?” Charlie
akamuuliza.
“Nahisi namjua huyu mtu,” Darren akajibu akiendelea
kufikiri na punde akakumbuka. Sura hiyo aliionea kwenye ile picha ambayo
aliipata kwenye jengo la bibi yake! Akamweleza Charlie habari
hiyo.
“Kweli?” Charlie akastaajabu.
“Ndio, ni
kweli!” Darren akaapa. Basi Charlie akafikiria kwa udogo na kusema, “Darren,
nadhani sasa utakuwa unaona kuna haja gani ya kuonana na Melissa. Yeye anaweza
kutueleza mambo haya kwa undani.”
Darren akashika kichwa,
“Lakini Melissa si mtu mzuri hata kidogo. Ameyfanya maisha yangu yawe magumu
kupita kiasi. Sikutaka kabisa kuhusiana naye.”
Charlie akauweka
mkono wake begani mwa Darren, “sikia, Darren. Hatuna machaguzi hapa. Na kati ya
wewe na mimi, hakuna mwenye maelezo ya kumtosha mwenzake isipokuwa huyo Melissa.
Hima twende tukamwone!”
Darren akafikiri kidogo kabla
hajanyanyuka na kumpakia Charlie kwenye gari yake, safari ikaanza. Walitembea
kwa muda wa kama nusu saa pasipo kuzungumza. Charlie ndiye alikuja kuuvunja
ukimya kwa kumuuliza Darren, “Ulimpenda Melissa?”
Darren
akanyamaza kwanza kama mtu anayepangilia jibu kichwani kisha akasema kwa ufupi,
“Ndio.”
“Na yeye alikupenda?” Charlie akauliza akimtazama
Darren anayatazama mbele.
“Sidhani,” Darren
akajibu.
“Haudhani?”
“Ndio. Kama angekuwa
ananipenda basi angeniweka bayana kila kitu,”
“Kila kitu kama
kipi Darren? Kuwa yeye ni jini aliyeishi na bibi zetu tuokea huko nyuma? …
ungemwelewa? Ungeendelea kuwa naye?”
“Charlie, sijui haya mambo
yaendavyo. Ila nisingeweza kuishi na Melissa zaidi. Unawezaje kufanya hivyo
punde unapohisi kuwa uliyenaye si binadamu?”
Charlie akanyamaza
asinene tena. Wakaumaliza huo mjadala. Kwenye majira ya saa tano za usiku wakawa
wamewasili kwenye makazi ya Robson. Hapo waliposhuka, Charlie akauliza, “Hapa
ndipo kwake?”
“Hapana, bali kwa mpenzi wake! Nadhani atakuwapo
hapa,” Darren akaji bu wakisonga.
“Na vipi kama hatokuwapo?”
Charlie akauliza.
“Basi mpenzi wake atakuwa anajua alipo,”
Darren akamalizia kauli na kubisha hodi mara tatu. Punde akafunguliwa na Robson
ambaye alishangaa kumwona Darren hapo wakati huo.
“Vipi,
Darren?”
“Naweza kuonana na Melissa?” Darren akaenda moja kwa
moja kwenye lengo lililomleta.
“Vipi, kuna tatizo?” Robson
akauliza.
“Ndio, lipo,” Darren akajibu na kisha akarudia tena
kauli yake, “Naweza kuonana na Melissa?”
Robson akawafungulia
mlango wakaingia ndani. Ila walipoketi, simu ya Darren ikaingiwa na ujumbe.
Alipoutazama kuusoma, ulikuwa unatokea kwa Melissa.
“Sipo hapo.
Nikuteni fukweni,” ujumbe ulisoma.
Upesi Darren na Charlie
wakaelekea huko ufukweni ambapo Melissa alikuwapo, na kweli wakamkuta akiwa
ameketi mchangani akitazama maji ya bahari. Mbali na hivyo kulikuwa kimya sana
isipokuwa upepo.
Darren akamwita Melissa akiwa anamtazama, naye
Melissa akamtazama na kumkaribisha, “Nadhani hapa ni eneo zuri la kufanyia
maongezi.” Darren na Charlie wakaketi wakimweka Melissa katikati
yao.
“Ulimwambia Robson kama nipo huku?” Melissa
akauliza.
“Hapana, hajui hilo,” Darren akajibu kisha akamuuliza
Melissa kama anamjua mwanamke yule aliyekuja naye, yaani Charlie. Pasi na
kumtazama, Melissa akasema anamfahamu hata kabla hajaja
hapo.
Aliposema hayo akamtazama Darren. Macho yake yalikuwa
tayari yameelekea kuwa mekundu. Akamshika mkono na kumuuliza kwa upole, “Darren,
utasadiki nitakayokuambia?”
Darren alipojibu swali hilo,
Melissa akamuuliza na Charlie swali hilohilo. Alipolijbiwa ndipo akaanza kunena.
Darren na Charlie wakawa wametega masikio yao vema kabisa. Japokuwa upepo
ulikuwa unapuliza, bado sauti ya Melissa ilisikika
vema.
“Pengine mimi naweza nikawa mtu mbaya sana kwenye vichwa
vyenu. Hamtaki kuniona na sifai kuwa hai wala kuwa mbele yenu hapa nilipo. Ila
…” alipokomea hapo akamtazama Darren, “Kama si upendo wangu kwako, Darren. Basi
usingalikuwa hai mpaka sasa. Haujui ni makovu mangapi umenisababishia kwa maneno
yako lakini sikuwahi kuacha kukupenda.”
Aliweka kituo na
kutazama bahari kwa sekunde kama sita akiwa kimya. Kuna kitu alikuwa anawaza
kichwani mwake. Na basi alipojiona yu tayari ndipo akaendelea kunena ya kuwa
hapo zamani kabisa ya miaka takribani mia tatu iliyopita, walikuwa kwenye
familia kubwa ya bwana Roddeth. Bwana huyo alikuwa ni mtu mwenye nguvu kubwa na
mwenye kuhofiwa sana.
Alikuwa na nguvu za ajabu. Watu
wangekusanyika kwake awasaidie matatizo mbalimbali lakini kwa sharti la kutoa
sadaka. Alikuwa si mtu wa kawaida bali jini, lakini alistahimili kuishi miongoni
mwa binadamu. Na kwa uzao wake basi akapata watoto watano wa kike ambao kwa
mujibu wa maelezo ya Melissa, mmoja wa hao watoto alikuwa ni yeye, na wengine ni
pamoja na bibi yake Darren na Charlie na wengineo
wawili.
Walikuwa ni watu wapendanao mpaka pale siku moja baba
yao alipokufa na kugawa mali zao pasi na usawa. Walichukiana na kila mmoja
akaelekea upande wake. Lakini kwasababu Melissa alikuwa ni kipenzi kikubwa wa
baba yao basi ingali baba yupo kwenye kitanda chake cha kifo alimkabidhi mwanaye
huyo kito cha moja ya mkufu wake akimwambia, “Utaishi milele, mimi safari yangu
naona ikomee hapa.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Alificha
kito hicho kwa namna zote ili ndugu zake wasije kukiona na kumpokonya. Na kwake
haikuwa ngumu sana kwani walikuwa tayari wameshatengana na kila mmoja akaenda
njia yake binafsi.
Basi miaka ikapita kila mmoja akiwa na chuki
na mwenzake na uadui pia. Kila mmoja akapata kuishi kwa namna ajuavyo huko
mbali. Wengine wakafikia kuanzisha maisha kwa kuwa na mahusiano na
binadamu.
“Halikuwa jambo jema. Baba yetu wakati yu hai alikuwa
akitusisitiza juu ya hilo. Endapo tutakapokuwa kwenye mahusiano na binadamu basi
si kwamba tutawafanya watoto waingie kwenye damu yetu isiyo ya kawaida, bali
damu hiyo itawawinda na kuwaangusha,” alisema Melissa.
Lakini
kwasababu za mapenzi, wenzao wawili walizaa na binadamu. Na kama ilivyokuwa neno
la baba yao, watoto hao wakawa wanasumbuliwa kwa kutokewa na mambo ya ajabu
wasiyoweza kuyaeleza. Mengine hata yakitishia uhai
wao.
Kutokana na hayo ndipo binadamu hao wakawa wanatafuta tiba
ya kujikinga dhidi ya maajabu waliyokumbana nayo. Na kila tiba walipoipata
wakaifungia kwenye vitabu walivyovihifadhi maeneo ya mbali kabisa na makazi yao.
Maeneo salama ambayo hayafikiwi na binadamu.
Vitabu hivyo
vilikuwa ni vifungo vya kufunga yale yote yaliyokuwa yanawasumbua, na
wakafanikiwa kufanya vivyo kwa muda.
“Shida ni kwamba, vitabu
hivyo vinakuwa si vifungo tu bali hubeba roho za wale vinavyowalinda. Hivyo pale
vinapopata madhara, basi na wale waliokuwa wanavimiliki hufa kwa aina hiyohiyo
ya kifo,” maneno hayo ya Melissa ndiyo yakamkumbusha Darren kifo cha mama yake
kilivyorandana na moto wa msitu. Akamuuliza naye Charlie akasema kuwa mama yake
alikufa kwa kuzama maji ingali alikuwa chumbani mwake! Ikiwa ni muda mfupi baada
ya tetemeko la ardhi kutokea.
“Baada ya hapo basi ndipo
matatizo yenu yakaanza upya,” Melissa akaendelea soga, “Kwakuwa vifungo vilikuwa
vimeenda basi ndiyo maana mambo ya ajabu yakaanza kuwatokea upya kwenye familia
zenu, na itakuwa vivyo mpaka pale damu mliyobeba
itakapotulizwa.”
Darren akamuuliza Melissa, “Mbona maisha yangu
yalikuwa yametulia kabla ya kuja kukutana na wewe? Mbona kila mara ninapoonana
na wewe huwa nakutana na jambo baya?”
Melissa akamtazama Darren
akiwa anadondosha chozi, “Darren kamwe hautokuja kuelewa ni mangapi nilikuwa
nayapitia kwasababu yako. Maisha yako kutuama kabla ya kuja kukutana na mimi
haikuwa inamaanisha kuwa utakuwa sawa, lah! Na hilo halikuwa kwako peke yako
bali pia kwa Charlie.
Mambo yalianza kubadilika si kwasababu
ulikutana na mimi bali kwasababu ulikuwa umepata mtoto. Kama vilevile ilivyokuwa
kwa Charlie. Mlikuwa mmefufua upya agano lenu, Darren,” Melissa alisema kwa
sauti ya chini alafu akatazama chini kabla hajaendelea kunena, “Kila ulipokuwa
unakutana na baya lolote, nami nilikuwapo pembeni, na ndiyo maana ulikuwa
unatoka ama kushinda hai. Isingalikuwa hivyo, ungeshakufa muda mrefu
Darren.”
“Na vipi kuhusu ile siku nilipoenda kwenye ile nyumba
iliyotangazwa kwenye gazeti? Ilikuwa ni kweli ama ndoto kukuona pembeni ya gari
yangu?” Darren akauliza. Melissa, bado akiwa anamtazama mwanaume huyo, akamjibu,
“Yote yalikuwa ni uhalisia, Darren. Na ni mimi ndiye nilikurudisha pale kwenye
gari lako upesi baada ya kuzidiwa na wale wadhalimu. Lakini uliponiona pembeni
yako haukunipa muda nikajitetea, bali ukanijaza shutma na
kunifukuza!”
“Kwanini hukuniambia yote hayo, Melissa?” Darren
akauliza.
“Kwasababu
haukunipa muda huo Darren. Maisha yako yote umekuwa ukinichukulia kama adui
yako. Mtu ninayekusababishia mabaya na nuksi,” Melissa akieleza hayo machozi
yakamtiririka zaidi. Na Charlie akagundua kuwa mwanamke huyo alikuwa
akimomonyoka miguu yake kuwa udongo.
Akamshtua Darren atazame.
Darren akapayuka kuuliza, “Melissa, nini kinatokea?” akiwa amemshika mkono
mwanamke huyo. Melissa akatazama miguu yake inayomomonyoka na kisha akamtazama
Darren na kusema, “Hii ndiyo gharama yangu kwa kusema haya. Yanipasa niende
Darren. Maisha yangu yamekwisha hapa duniani.”
“Hapana Melissa,
si una kito cha kuishi milele?” Darren akauliza.
“Sina kitu
chochote Darren,” Melissa akasema akilaza kichwa chake kifuani mwa Darren, “Yote
nimeyatoa kwa ndugu zangu kama sadaka ya kukubakiza wewe hai.” kisha akamtazama
Darren na kumwambia, “lakini haikusaidia na wamenigeuka. Wanataka maisha yako,
wanataka maisha yenu. Wanataka kila ambacho bibi yako alikuwa anamiliki. Siwezi
kuwazuia tena, Darren. Sina nguvu hiyo.”
Melissa alipomaliza
kauli hiyo, mwili wake ukawa umeshapukutika mpaka kufikia tumboni. Mwili uwake
ulikuwa kichuguu cha mchanga. Akamwaga Darren, “Kwaheri,
mpenzi”
“Melissa!” Darren akaita akimshika Melissa vema.
“Usiondoke, Melissa! Tutawezaje kupambana wenyewe? Tafadhali usituache!” Lakini
tayari sasa mwili wa Melissa ulikuwa umepukutika zaidi mpaka kifuani. Maneno
pekee ambayo aliyasema kabla hajamalizika kabisa ni haya,
“Kuna
kitu kwenye jeneza la bibi yako,” alipotaka kunena zaidi, kichwa chake
kikamomonyoka na hatimaye akawa mchanga kabisa. Darren na Charlie wasiamini
macho yao wakautazama mchanga ule wa bahari.
“Amejitoa sadaka
kwa ajili yetu,” akasema Charlie akimtazama Darren kisha akauliza, “sasa
tunafanyaje?” Darren alipohakikisha kuwa kweli Melissa ameenda, akamwambia
Charlie waende kule kwa bibi yake. Lakini muda ulikuwa umeenda
sana.
“Vipi tukadamka asubuhi?” Charlie
akapendekeza.
“Hapana,” Darren akatikisa kichwa. “Huoni ni
hatari zaidi tukiendelea kungoja?” kweli Charlie akaafiki, lakini sasa
wangefanyaje na muda ulikuwa umewatupa mkono?
Wakiwa wanafikiri
namna ya kufanya, simu ya Darren ikaita, alikuwa ni Isabel. Alipokea na kumjulia
hali mwanamke huyo.
“Upo wapi, Darren?” Isabel akauliza. Darren
akamtazama Charlie na kujibu, “Nipo mbali.”
“Wapi? Tafadhali
waweza kuniambia?” Isabel akasisitiza, lakini kabla Darren hajajibu akamtazama
kwanza Charlie, mwanamke huyo akamtikisia kichwa. Darren akakata
simu.
“Darren, usimwamini mtu yeyote kwa sasa hivi,” Charlie
akamwambia akiwa amemkazia macho.
“Kwanini? Huyu nafahamiana
na--”
“Hapana!”
Punde simu ikaita tena, Darren
akamtazama Charlie. Ajabu mwanamke huyo akampoka simu hiyo na kisha akaikata na
kuizima. “Tuondoke, Darren!”
Basi upesi wakalifuata gari lao na
kujikwea. Charlie akamwambia Darren waelekee kwake alafu ndiyo waende huko
waendako, Darren akatii. Walipofika kwa Charlie wakapakia silaha kadhaa ndani ya
gari, Charlie akabeba na pesa, wakaanza safari ya kwenda kwenye nyumba ya
marehemu bibi yake Darren.
Wakatembea kwa muda mrefu sana mpaka
pale ambapo usiku sasa ukawa mkubwa. Wakiwa kwenye majira ya saa tano usiku,
wamebakiza kama kilomita ishirini kuwasili wanapoelekea, Charlie akahisi kuna
gari linawafuatilia. Alimshtua Darren na kumtaka aongeze
mwendokasi.
Darren alipojaribu kutazama kwa kutumia vioo
akaliona gari hilo wanalolishukia. Halikuwa ngeni machoni mwake. Alipoenda mbele
zaidi na kulitazama vema, akagundua kitu,
“Isabel!” alijikuta
akinena mwenyewe.
“Unamaanisha yule mwanamke?” Charlie
akauliza. “Yule aliyekuwa anakupigia simu?”
“Ndio!” Darren
akajibu. “Ndiye yeye!”
Charlie akatazama nyuma kuliangazia gari
hilo. Lilikuwa linakuja kwa kasi. Alihofia sana.
“Darren, sasa
tunafanya nini?”
“Sijui!” Darren akatikisa kichwa akiwa ametoa
macho kukodolea kioo cha juu ya kichwa chake. Alikanyaga pedeli ya mafuta zaidi,
gari likakimbia. Punde lile gari linalowafuata likatokomea wasijue limeenda
wapi!
“Unaliona?” Darren akamuuliza
Charlie.
“Hapana, silioni!” Charlie akajibu akiwa anaendelea
kukagua. Kwa muda kidogo akaendelea kutazama asilione tena gari lile
linalowafukuza, basi wakaendelea na safari yao mpaka waelekeapo. Walipofika
wakajitua toka kwenye gari na kabla hawajaenda mbali sana, wakatupa macho yao
kukagua.
Ilikuwa ni nyumba iliyomezwa na kiza. Kulikuwa kimya
sana. Kwa namna moja ama nyingine kulikuwa kunatisha.
Wakiwa
wanaendelea kutazama, Charlie akagundua kitu. Akamwita Darren na kumuuliza,
“Nini kile? Ni gari ama macho yangu?” Darren alipotazama akaona gari kwa mbali
upande wao wa kulia. Gari hilo lilikuwa limeegeshwa kwa ukimya. Lilikuwa ni lile
gari waliloliacha barabarani. Gari ambalo Darren hudhania ni la
Isabel.
“Umeliona likiingia muda huu?” Darren
akauliza.
“Hapana,” Charlie akajibu na kuongezea, “Nimeliona
likiwa tayari limeegeshwa.” kisha akauliza, “atakuwa amefika kabla
yetu?”
Darren hakuwa na majibu, upesi akamwamuru Charlie
wachukue kila kinachohitajika kwenye gari na waelekee eneo la kaburi upesi.
Walipofanya hivyo, mara gari lile likawasha taa zote kwa pamoja, pap!
likawamulika na kuwaumiza macho!
Upesi wakakimbia kule kaburini
na kuanza kuchimba kwa maelezo ya Darren. Wakiwa wanaendelea kuchimba, Charlie
akamwona mtu kwa mbali akija kwenye mwelekeo wao. Hakuweza kumwona vema maana
alikuwa yu mbali, kitu pekee alichoweza kubaini ni kuwa mtu huyo ni mwanamke
kutokana na umbo lake na mwendo pia.
Mikono yake iliyokuwa tupu
ilikuwa ikienda mbele na kurudi nyuma sababu ya
mwendo.
“Chimba, Charlie! Chimba!” Darren akabweka. Wakafukua
kana kwamba sungura udongoni na mtu yule alipokaribia, Darren akamsihi Charlie
aendelee na zoezi ilhali yeye akamkabili mtu huyo
anayekuja.
“Darren, una uhakika?” Charlie akauliza kwa
mashaka.
“Usijali, endelea,” Darren akasema akitoka shimoni na
kupiga hatua kadhaa kusonga mbele. Alipomfikia mtu yule ndipo akabaini kweli
alikuwa ni Isabel.
“Isabel,” Darren akaita na kuuliza, “Ni nini
unataka hapa?”
Isabel akatabasamu na kuuliza, “Darren mbona
haupokei simu yangu?” kabla Darren hajajibu, akauliza tena, “Kwani kuna tatizo
lolote baina yetu?”
“Hapana, Darren,” Isabel akajibu akiweka mkono
wake begani mwa Darren. “Kilichonileta hapa ni kuchukua kilicho changu
tu.”
“Kipi chako hapa?” Darren
akauliza.
“Vyote unavyoviona hapa,” Isabel akajibu na
kuongezea, “Vyote ni urithi wangu. Na kwakuwa haukutaka niuchukue kwa amani,
basi nitatumia nguvu!”
“Ebu tumia nione!” Darren akasema
akimkazia Isabel macho.
“Una uhakika?” Isabel akauliza
akipandisha nyusi yake moja. Punde Darren akaanza kuhisi maumivu makali ya
kichwa.
“Darren nisingependa nitumie nguvu dhidi yako.
Nitakumaliza. Kwahiyo kwa kunusuru maisha yako, songa kando nifanye
kilichonileta.”
Japo Darren alikuwa anasikia maumivu makali
bado hakuwa radhi kumruhusu Isabel atende kile alichokuwa amekusudia. Basi
akamvamia akimtupia maneno makali lakini alichoambulia hakikuwa kinasimulika
vema. Alitupiwa mbali tena kwa mkono mmoja tu. Akaangukia tumbo na kulalama kwa
maumivu makali!
Isabel akapiga hatua nzito kumfuata Charlie.
Alipomfikia akanyoosha mkono wake kumnyaka mwanamke huyo, ila upesi Charlie
akatumia kifaa alichokuwa anachimbia kumwadhibia Isabel! Alimchana na kumvujisha
damu!
Isabel akautazama mkono wake unaovuja damu kisha akakunja
ndita akimtazama Charlie. “Umekwisha!” akafoka na kujitupia ndani ya shimo.
Charlie alipotaka kumwadhibu tena Isabel, nyenzo yake ikadakwa na mkono wa
Isabel wenye nguvu.
“Kamwe usijaribu!”
Isabel
akampokonya Charlie dhana hiyo na kisha akataka kumbamiza nayo kichwa. Kheri
kabla hajatimiza adhma yake hiyo, nyenzo ikadakwa na mtu nyuma. Isabel
alipogeuka kutazama, alikuwa ni Darren. Na kabla hajafanya jambo, mwanaume huyo
akamwadhibu kwa kumzamishia ncha za reki usoni mwake! Kilikuwa ni kitendo cha
kinyama ambacho Darren amewahi kufanya tangu azaliwe.
Hata
wakati Isabel anaanguka chini, Darreb alikuwa ameachana asiamini kama amelitenda
hilo. Basi upesi, wakishirikiana, wakamtoa Isabel ndani ya shimo na Darren
akamburuza kwa hatua kadhaa mbali na shimo kisha wakaendelea kuchimba
kaburi.
Walipofanya hivyo kwa takribani dakika sita, mara
Isabel akanyanyuka akiwa na reki lake usoni. Si Darren wala Charlie aliyemwona.
Mwanamke huyo akachomoa reki usoni na kulitupia kando. Alikuwa anachuruza damu
lakini hakuwa anajali. Upande wake wa kushoto ulikuwa umefunikwa na damu
inayotiririka kama bomba.
Alipotupia reki kando ndipo Darren na
Charlie wakasikia na kuhisi. Darren alipotazama na kubaini hilo akahofia sana.
Hata Charlie vilevile. Ni mtu wa aina gani angenyanyuka baada ya kadhia ile?
Lakini kwa ujasiri Darren akatoka ndani ya shimo baada ya kumwambia Charlie
aendelee kufukua.
“Darren!” Charlie akaita kwa hofu. Aliogopa.
Aliona Darren angeenda kufa. Lakini Darren asijali akajiendea kifua mbele.
Alipomfikia Isabel akasema, “Nitakuua!” naye Isabel akamwambia, “Karibu tena!”
kisha akamnyaka shingo yake kwa nguvu na kumnyanyua juu
juu!
“Ndiyo kwanza tupo kwenye moja, Darren. Unadhani binadamu
kama wewe anaweza kuniua?” Darren akarusharusha miguu akijitahisi kujinasua toka
kwenye mikono ya Isabel. Hakika asingeweza kwani mikono ya mwanamke huyo ilikuwa
imeshiba nguvu haswa. Ilikuwa inaminya uhai toka kwenye mwili wa
Darren.
Darren akapapatika sana pasipo mafanikio. Akarusha na
mateke ambayo mengine yalikwenda hewa na mengine kumkita Isabel lakini
haikusaidia, mwanamke huyo alikuwa mithili ya gogo kavu!
Basi
Darren aliyekuwa anaelekea kufa alipoona amefanya kila jambo pasipo mafanikio na
sasa anaelekea kufa, akamtazama Isabela akilenga kumtusi ama kumlaani. Ni kheri
katika hilo akabaini jeraha alilokuwa nalo Isabel mkononi, lile jeraha ambalo
Charlie alimsababishia. Basi kama simba aliye na njaa, Darren akadaka kwa mikono
yote jeraha hilo na kuliparua sana. Isabel akashindwa kuvumilia na hatimaye
akamwachia Darren aliyejidondokea chini akikohoa.
Darren
alikuwa anahisi kifua kinambana, shingo nayo imeziba. Alikuwa anahema kwa tabu.
Koo lake bado halikuachia. Alikohoa mara kadhaa akiwa anahangaika kumeza
mate.
Hakukaa sana akamwona Isabel akimfuata kwa hasira.
Alipotaka kuamka akimbie, Isabel akamwendea kwa kasi sana na kumdaka. Darren
akajitahidi kurusha ngumi na kutumia nguvu zake za kibinadamu lakini akashindwa
kabisa! Isabel alikuwa ana nguvu mno!
Mwanamke huyo pasipo
kujiuliza mara mbilimbili, akadidimizia kucha za mkono wake wa kushoto kwenye
tumbo la Darren, na hakufanya vivyo mara moja bali mara tatu! Darren akalalamika
sana kwa maumivu. Isabel akamtupia mbali akiwa amemalizana
naye.
Darren, akiwa amelala kama mtu anayengoja kifo akiwa
ameshika tumbo lake linalovuja, akamtazama Isabel. Akamwona mwanamke huyo akiwa
anaenda kumfuata Charlie kule shimoni. Basi akapaza sauti kuu kumwita Isabel.
Halikuwa zoezi rahisi, alikuwa anahisi maumivu makali sana lakini alifanikisha
adhma yake hiyo.
Isabel alipogeuka kumtazama, Darren akapaza
sauti kumtusi na kumkebehi mwanamke huyo. Kitendo hicho kikamkasirisha sana
Isabel, akaamua kuachana na Charlie akammalize mwanaume huyo kabisa. Basi
akamjongea kwa madaha akiwa anamwambia ni kwa namna gani atakapofurahi akiona
roho yake inaenda.
“Kama bibi na mama yako, nawe utaenda
hukohuko!” akasema Isabel. “Mwana usiwe na haya ukatembea na bibi yako. Hujui
Melissa ni sawa na bibi yako, ati Darren?”
“Na mbona na wewe
ulikuwa unanitaka?” Darren akaguguma kuuliza. Saa hii kinywa chake kilikuwa
kinachuruza damu pia. Isabel akacheka akiwa anazidi kujongea, “Mimi? Darren
mpenzi nilikuwa nataka tu kukumaliza na si kingine. Unadhani mimi ni kama yule
mpofu Melissa? Mjinga kama yule?”
“Ni wewe ndiye mjinga, si
Melissa!” Darren akafoka.
“Pole sana, Daren,” Isabel akasema
akiwa anamalizia hatua yake moja kumfikia Darren. “Mpumbavu wako ameenda, nani
atakulinda sasa?” akauliza na kucheka. “Kwa akili yake amejitoa uhai kwa ajili
yako. Wewe binadamu. Kwa sababu tu ya kukwambia yote yale ambayo hupaswi
kuyajua. Shenzi kabisa!”
Alipomaliza kusema hayo akamnyakua
Darren na kisha anyanyue mkono wake ili apate kumkita tena tumboni kama
alivyofanya hapo awali. Lakini mara hii kabla hajafanya vivyo, akastaajabu kuona
mpini wa reki ukitokezea tumboni mwake! Hamaki alikuwa ni Charlie nyuma
yake!
Basi
akamwacha Darren na kisha akapiga magoti akiwa anatazama chuma kile
kilichomtoboa tokea mgongoni mpaka tumboni na kisha akadondoka puh! Na kutulia
tuli,
Charlie akamjulia hali Darren.
“Niko
sawa,” Darren akamjibu na kisha akamuuliza,
“Umefanikiwa?”
“Bado kidogo!” Charlie akajibu. Akatazama
tumboni mwa Darren, kulikuwa kunamwaga damu sana. Akashikwa na imani, “Darren,
nikuwahishe hospitali!” alisema akitaka kunyanyuka akaendee gari lakini Darren
akamdaka mkono na kumwambia, “Hapana, Charlie. Nenda kamalizie kwanza ile
kazi!”
“Darren, nitaendeleaje na upo kwenye hali hii?” Charlie
akauliza.
“Hapana! Hapana! Nenda kwanza, tafadhali nenda!”
Darren alisisitiza na basi kwa shingo upande, Charlie akaenda zake. Akazama
shimoni na kufukua zaidi na zaidi, ndani ya dakika tano akawa amefikia jeneza,
akafunua na humo ndani akakuta maiti ya bibi yake Darren ikiwa
mifupa.
Alipotazama vema akabaini kulikuwa na kito rangi ya
asamawati, basi akakibeba na kupaza sauti, “Darren,
nimekipataaaa!”
Haraka akatoka ndani ya shimo na kumkimbilia
Darren. Lakini alipofika akabaini Darren hakuwa anasogea wala kuashiria kama
mzima. Alipotazama vema akabaini pia mwili wa Isabel ulikuwa umesogea kidogo
toka pale alipouacha, na kama haitoshi, reki halikuwa tumboni, bali kwenye
kichwa likiwa limemtoboa!
Hapo Charlie akabaini ya kuwa Darren
na Isabel walipambana kwa mara nyingine. Akapata hofu zaidi juu ya uhai wa
Darren. Akamwita sana na kumtikisa, kwa mbali Darren akafungua macho yake
kumtazama. Alikuwa ana mjeraha kooni na kifuani. Karibia mwili wake wote ulijawa
damu.
“Umepata?” Darren akauliza kwa
kunong’ona.
“Ndio, nimepata!” Charlie akajibu kwa kitete. Macho
yake yalikuwa mekundu yakitaka kumwaga machozi. “Twende nyumbani, sasa!” akasema
akijaribu kumnyanyua Darren.
“Hapana, Charlie,” Charlie akasema
na kuongezea, “Hapa ndiyo nyumbani kwangu, sina pengine. We nenda mimi utaniacha
hapa.”
“Nitakuachaje Darren? Tumekuja wote hapa! Nyanyuka
tafadhali twende!”
Charlie alipoona ni ngumu kumnyanyua Darren
basi akaenda zake asogeze gari karibu. Alipojipaki kwenye gari, akaendesha upesi
sana kumrudia Darren. Alipoliweka gari tenge akashuka na kumwendea Darren, ila
kwa muda huo hakuwa Darren tena bali mwili tu.
Akapambana
kumweka kwenye gari, lakini kabla hajawasha gari Isabel akanyanyuka na reki lake
kichwani! Mwanamke huyo akakaa mbele ya gari akimtazama Charlie kwa macho ya
kukodoa.
Charlie akastajabu sana. Akahangaika kuwasha gari,
kabla hajafanikiwa, Isabel akawa tayari amezama ndani na kumkaba shingo
kwanguvu! Charlie akaweweseka sana kujiokoa.
Ajabu wakiwa
kwenye zoezi hilo, wakasikia mtu akigonga kwenye kioo cha dirisha. Isabel
alipotazama, akabaini ni Melissa! Akastaajabu akiwa ameachama
mdomo!
Kufumba na kufumbua
akafungua mlango wa gari na kumnyaka Isabel. Kwa mikono yake akamnyofoa mwanamke
huyo koo na kisha akamtupia mbali kana kwamba
kitenesi!
“Melissa!” Charlie akaita kwa kustaajabu.
Akamkumbatia Melissa kwanguvu na kisha akamwambia kumhusu Darren. Walipomtazama
wakabaini mwanaume huyo alikuwa amekwisha kufa.
Basi Melissa
akachukua kile kito ambacho Charlie alikipata kwenye jeneza la bibi yake Darren
kisha akakitazama na kusema, “Nilikuwa nayajua yaliyo mbele yangu hata kuhifadhi
sehemu ya maisha yangu kwenye jeneza lile.” aliposema hayo, akamtazama Charlie
na kumwambia, “Utakapokutana na Darren mwambie nampenda sana. Hatimaye amekuwa
huru. Hatimaye mmekuwa huru.”
Aliposema hayo akaingiza kile
kito kinywani mwa Darren na kisha kumfumba mdomo. Charlie akamuuliza, “vipi
kuhusu yule Isabel, hatarejea tena?”
Melissa akamjibu hatorejea
tena kwa roho zake zimekwisha. Ndani yake alikuwa na roho kadhaa na kadiri
walivyokuwa wanamuua ndivyo walivyozimaliza mpaka kubakia moja aliyoimaliza yeye
muda si mrefu.
“Umejuaje?” Charlie
akamuuliza.
“Kwasababu isingekuwa rahisi kummaliza kama
nilivyofanya,” Melissa akamjibu na kisha akamuaga. Moja kwa moja akaenda kwenye
shimo la kaburi na kudmbukia humo. Punde, Darren akaamka. Alikuwa mzima wa afya
kabisa asiye na jeraha.
Charlie alipomweleza kila lililotokea,
upesi akakimbilia kwenye kaburi kumtazama Melissa. Akamkuta mwanamke huyo akiwa
ana uhai amekwishakufa. Akamwita na kumwita pasipo mafanikio, Melissa alikuwa
ameenda.
“Sawa. Utakapokuwa tayari
utaniambia,” Isabel akasema akifunga pochi yake. “Nitakulipa pesa taslimu,
Darren.”
“Sawa.”
“Kwaheri. Nitakuja kukuona
siku nyingine.”
Kabla Darren hajatoka ndani ya gari, Isabel
akambusu shavuni na kumuaga kwa kumnong’oneza, “Kwaheri,
Darren.”
Darren hakusema kitu akatoka zake na kwenda ndani.
Alipoketi sebuleni, mkewe akatokea chumbani akiwa amembebelea mtoto. Macho yake
yalikuwa yanatiririsha machozi.
Kidogo mkewe
akajigeuza na kwenda zake ndani pasipo hata kuaga na huku akiwa anamwaga
machozi. Hali hiyo ikamfanya Darren ajisikie vibaya sana. Moyo ukamnyong’onyea
akiwa anajiuliza nini kimemsibu mkewe?
Hakuwa anajua kwamba
mkewe alimwona wakati Isabel akimbusu kwenye gari, kioo cha gari kilikuwa chini
hivyo ikapeleka kuonekana kwa urahisi na mkewe akiwa
chumbani.
Akaketi pale sebuleni kwa kama sekunde tano kabla
hajanyanyuka na kumfuata mkewe ndani kumjulia hali lakini kumuuliza nini shida.
Alipofika, akamkuta mkewe akiwa amejilaza kitandani analia. Mtoto alikuwa
amelala kwenye kitanda chake.
Akamwita, “Josephine!” mwanamke
hakuitika. Akarudia kuita tena na tena lakini bado kukiwa kimya. Akaketi
kitandani na kumshika bega.
“Mke wangu,” akaita kwa upole.
Mwanamke bado akawa kimya. Ni sauti ya mafua tu ndiyo ilikuwa inasikika na
miguno ya kilio.
“Nimekufanya nini?” Darren akauliza. “Niambie
basi nini tatizo?” Darren akahisi huenda mkewe aliumizwa na kile kitendo cha
mkewe kwenda kuonana na Isabel kando, basi akaomba msamaha huku akimhakikishia
kuwa hakufanya jambo baya, lakini bado tu. Josephine aliendelea kulia asiseme
jambo.
Zikapita kama dakika tano … sita … saba … bado Josephine
kimya. Mwishowe Darren akaona ni staha akimwacha mwanamke huyo yeye aende
sebuleni kutulia alafu baadae mwanamke huyo atakapokuwa sawa, aongee
naye.
Akaketi sebuleni kwa kama lisaa. Kimya. Akawasha runinga
na kutazama lakini akili yake yote ikiwa kwa mkewe. Akaitazama kwa kama nusu
saa, bado kimya. He! Akashangazwa na hali hiyo. Akapatwa pia na mkanganyiko wa
nafsi, je aende tena kumbembeleza mkewe au atulie hapo mpaka atakapokuja
mwenyewe?
Akiwa anawaza, mara akasikia mlango ukifunguliwa na
kisha vishindo vya mtu. Kidogo akamwona mkewe akifika sebuleni lakini
akipitiliza moja kwa moja kwenda jikoni.
Akarusha macho
kumtazama. Kidogo akahofu mkewe asije akawa ameenda kujidhuru. Akakodoa mpaka
pale Josephine alipotoka huko jikoni na kutembea kudaka korido. Akamwita tena,
mara hii Josephine akaitika kwa kumtazama.
Macho yake yalikuwa
yamekauka machozi lakini yakiwa bado mekundu. Uso wake ulikuwa umesinyaa kwa
huzuni na mdomo wake umevimba.
“Una nini Josephine?” swali hilo
likafungua tena mifereji ya machozi. Josephine akabubujikwa na machozi na mdomo
wake ukatetemeka akiumauma meno. Hakuwa anaweza kuongea. Kuna kitu alikuwa
anahisi kinamkaba kooni. Mdomo ulikuwa ni mzito na kichwa chake kilikuwa
kinagonga.
Hakuwahi kuwaza … hakuwahi kuwaza kabisa kama Darren
anaweza kumsaliti kwa kuwa na mwanamke mwingine.
Kila alipotaka
kuongea akajikuta taya zinagongagonga. Mdomo unajawa na uchungu usio wa kawaida.
Akaamua tu kuondoka zake. Mumewe akamsindikiza kwa macho yenye itilafu mpaka
alipozama ndani ya chumba kabisa, akaufunga mlango.
“Eh!”
Darren akahema akijilaza kitini. “Kazi nnayo.”
Akabaki hapohapo
akitazama runinga na kurudi mawazoni, akitazama runinga na kurudi mawazoni mpaka
mwishowe akabebwa na usingizi kabisa. Ulikuwa ni usingizi mwepesi lakini
uliomfanya akapata kidogo afueni ya rundo la mawazo alokuwa
anapitia.
Lakini katika namna ya ajabu, ya ajabu kabisa,
usingizi huo ukageuka kuwa mzito kupita kiasi! Darren akajikuta analala
akikoroma kabisa, hata kumwaga udenda akiachama kinywa. Ni kama vile hakuwa
amelala kwa juma zima, au amefanya kazi kubwa sana na hakupata muda wa
kupumzika.
Akiwa ndani ya usingizi huo akazamia ndotoni ambapo
alijiona yu ndani ya nyumba ya bibi yake, kule kijijini. Alikuwa sebuleni
akifanya usafi akiwa anangojea ugeni muda si mrefu.
Kidogo
akiwa anaendelea na kazi hiyo, mkewe akaja akiwa amembebelea mtoto. Mtoto
alikuwa analia lakini punde akanyamaza. Josephine akaketi kwenye kiti na
kumtazama Darren.
“Ungesogea kando kidogo na mtoto kwani kuna
vumbi!” Darren akamwonya mkewe kisha akaendelea na kazi yake akijua mkewe
atafanyia kazi ushauri wake. Lakini baadae alipokuja kutazama, akatahamaki mkewe
alikuwa bado amekaa kwenye kiti!
“Josephine!” Darren akaita.
Mkewe alikuwa bado anamtazama. “Si nimekwambia utoke hapo lakini? Huoni
vumbi?”
Josephine akaendelea kumtazama tu. Hakuonyesha dalili
yoyote ya kusikia anachoambiwa. Kidogo, mbele ya macho ya Darren, Josephine
akachomoa kisu toka nyuma ya mgongo wake. Kilikuwa ni kisu kipana na kirefu.
Kisu kinachometa kwa upya. Na ndani ya sekunde moja tu, kufumba na kufumbua,
Josephine akamdidimizia mtoto kisu chote kifuani!
Darren akatoa
macho haswa. “Mungu wang - Josephine! Nini unafanya?”
Josephine
akamweka mtoto kando na kisha akanyanyuka kumfuata Darren akiwa amebebelea kisu
chake mkononi. Darren akapiga yowe kali. Akashuka toka alipokuwa amekwa na
kuanza kupambana kujiweka mbali na Josephine kwasababu za usalama
wake.
Josephine akazidi kumjongea na kisu kinachochuruza damu.
Uso wake ulikuwa umekengeuka kuwa wa ajabu. Macho yake yamekuwa ya kijani na
mdomo wake unaapa kifo.
Hakuwa Josephine uliyemzoea, mkarimu,
mpole na mwenye kutenda yaliyo mema. Alikuwa ni Josephine kutoka kuzimu.
Josephine mwenye umbo la binadamu lakini roho ya
shetani!
“Josephine! Hapana! Tafadhali usifanye hivyo!” Darren
aliwaka kwa woga. “Tafadhali, Josephine. Mimi ni mume- ” hajamalizia, Josephine
akamrukia na kunyanyua mkono wake wenye kisu.
Hapo
ndipo Darren akaamka toka kwenye lindi zito la usingizi! Akiwa anahema kama
mbwa, akatazama kushoto na kulia kwake. Macho yamemtoka na mdomo
ameachama!
Kidogo tu, akasikia sauti kali ya mtoto ikilia.
Haraka akanyanyuka na kukimbilia chumbani. Upesi akamwangalia mtoto, alikuwa yu
kwenye kitanda chake analia haswa. Basi akamnyanyua na kujaribu kumbembeleza.
Kitandani Josephine alikuwa amelala.
“Josephine,” Darrena kaita
na kuuliza, “Hausikii mtoto
analia?”
Kimya.
Darren akaita tena na kuuliza.
Bado kimya. Basi akadhani bado Josephine ameendeleza mgomo wake. Lakini ndiyo
mpaka kwa mtoto? Akajiuliza. Akatoka chumbani humo na kwenda mpaka sebuleni
akiwa anambembeleza mtoto wake, hatimaye mtoto akalala.
Basi
akaona ni vema akamlaze mtoto kitandani chumbani. Alipofanya hivyo, kabla
hajatoka chumbani akamwita tena Josephine. Bado kimya. Saa hii akaamua
kutoondoka mpaka pale atakapotimiza adhma yake, kuongea na
mkewe.
Akamgusagusa na kumshtua. Akamsogezasogeza na kumwita.
Kidogo ndipo akabaini ya kuwa mkewe alikuwa amemeza vidonge vingi, kumbe pale
hakuwa mzima. Povu lilikuwa linamtoka mdomoni na macho yake yamekwisha panda
juu!
Akachanganyikiwa haswa.
Uopesi akambeba
mkewe na kumkimbizia kwenye gari, na pasipo kufunga mlango akatia moto gari na
kuendesha kwa haraka amwahishe hospitali. Lakini kufika mbele ndipo akabaini
hata na mtoto alikuwa amemwacha ndani!
“Mungu wangu!” akajikuta
anatoka na maneno. Akarudi nyuma upesi na kujitengenezea vema kwenye barabara
kisha akarudi nyumbani kwa kasi ya ajabu.
Alipofika akakimbilia
ndani na kumbemba mtoto, akamweka ndani ya gari na kutimka kama
kimbunga!
Laiti askari angemwona namna alivyokuwa anaendesha,
asingeshani hata kama mwanaume huyo amembembelea mtoto na mwanamke ndani. Akili
yote ya Darren ilikuwa imeruka! Alikuwa anamuwaza mkewe tu. Lakini pia akidhani
huenda akawa amempoteza, au atampoteza akiwa njiani.
Kheri
akafika hospitalini salama. Akamtua mke wake na kumwahisha kupatiwa huduma. Yeye
na mwanaye wakakaa kitini kungoja taarifa ya daktari.
Darren
akiwa amekaa hapo akawa anaomba kila aina ya sala mkewe
anusurike.
Kama baada ya dakika tatu, Isabel akampigia
simu.
Akaitazama simu hiyo na kusonya, hakutaka kupokea, lakini
ikaita pasipo kukoma, hatimaye, kwa kuepusha usumbufu, akapokea na kuiweka
sikioni.
“Hey Darren,” Sauti ya Isabel ikasalimu na kisha
kuuliza, “Kuna shida?”
Swali hili likamshtua kidogo Darren.
Alijiuliza kama Isabel amemwona ama? Mbona ni mara ya pili hii akimuuliza swali
hilohilo?
“Isabel,” Darren akaita na kuuliza, “Una maanisha
nini kuniuliza hivyo?”
“Najua una matatizo, Darren,” Isabel
akasema kwa kujiamini.
“Umejuaje kama nina
matatizo?”
“Uso wako tu unaonyesha. Niambie ukweli Darren,
hauna shida?”
Darren akawa kimya kidogo.
“Ni
sawa, Darren. Kama utakuwa una shida basi unajua pa kunipata.” kisha Isabel
akakata simu na kumwacha Darren akiwa kwenye lindi la mawazo. Ni kweli Isabel
anayajua anayoyapitia ama anahisi tu? Je ni sahihi kwake kumshirikisha mwanamke
huyo ama akaze kifua tu?
Alijiuliza pasipo na kikomo. Daktari
akaja na kumshtua amwitaji ofisini. Alipoenda huko Daktari akamweleza maendeleo
ya mkewe kuwa ameathirika sana na madawa aliyoyatumia. Kurudi kwenye hali yake
itawachukua muda kidogo.
“Laiti ungemuwahisha, kazi ingekuwa
nyepesi zaidi,” Daktari alisema vivyo na kisha kumpatia moyo bwana Darren,
“Usijali, atapona tu. Japo yatupasa tuchukue muda kwa mwili wake kurejea kwenye
hali ya kawaida.”
Basi Darren baada ya habari hizo, akajiendea
kwenye benchi kuketi zaidi. Hapo akawa na mwanaye aliyekuwa anambembeleza.
Mwanaye aliyekuwa anamwonea huruma kwa mama yake kuwa hoi kwa
ugonjwa.
Alikaa hapo kwa masaa mawili kabla hajaona ni vema
kumjuza Roby ili aje kumjulia hali. Punde kidogo, Roby akaja na angalau Darren
akapata muda wa kutoa yaliyo kifuani mwake. Angalau akajihisi mwepesi kwa kunena
yanayomsibu.
Kuongea napo ni tiba.
Roby akampa
pole sana na kumfariji. Akakaa naye kwa muda mrefu kabla hajamuaga aende
kupumzika nyumbani.
“Utaniambia kitakachotokea, Darren. Lakini
nakushauri kwanza uende nyumbani ukapumzike na kumpatia mahitaji huyo mtoto,”
alishauri Roby kabla hajajiendea zake. Darren akamsindikiza kwa macho akitamani
kumwambia mwanaume huyo asimwambie Melissa chochote
kile.
Alijua fika angemwambia hivyo Melissa basi mwanamke huyo
angefika hapo ndani ya masaa machache. Hakutaka kabisa kuwa karibu na mwanamke
huyo. Lakini angemwelezaje hivyo Roby?
Roby akaenda zake.
Darren akajikusanya na kwenda nyumbani kumlisha mtoto na kuweka mambo mengine
sawa. Alipohakikisha kila kitu kipo kwenye utaratibu, akaenda kuoga aondoe
uchovu.
Alipotoka bafuni na kutazama simu yake akakuta ‘missed
calls’ toka namba ya Roby. Baada ya kujiuliza kidogo akapiga na kupachika simu
yake sikioni. Baada ya kuita kidogo, ikapokelewa. Ajabu likuwa ni sauti ya kike.
Sauti ambayo si ngeni masikioni mwa
Darren.
“Pole
sana, Darren. Najua matatizo unayoyapitia hivi sasa.
Usi--”
“Melissa! Naomba niskize vema, sawa? Sitaki kuwasiliana
na wewe. Naomba uachane na mimi. Tafadhali. Na kama ukiendelea kunisumbua basi
nitamwambia Roby juu yako.”
Melissa akaangua
kicheko.
“Huoni utakuwa umenirahisishia kazi, Darren?”
akauliza. “Kama ukimwambia Roby kuhusu mimi na wewe, nami nitamkubalia kila kitu
na kumwongezea taarifa zaidi. Mosi, urafiki na ubia wenu utakuwa hatihati, pili,
utakuwa umenisafishia njia ya mimi kurudi kwa--”
Darren akakata
simu. “Shenzi!” akatupia simu kochini na kudaka kichwa chake kwa
mawazo.
Melissa akasonya akitazama simu yake, kisha akamtazama
Roby aliyekuwa amelala kitandani fofofo. Akanyanyuka na kujiondokea zake
akimwacha mwanaume huyo hajielewi A wala Z.
Akashuka mpaka
chini na huko akapanda gari la Roby na kutimka akienda
tusipopajua.
Baada ya muda kidogo, Darren akamwona akiwa
anasinzia. Alikuwa tayari ameshakula na ni usiku sasa. Aliwaza kumlaza mtoto
huyo alafu aende mwenyewe hospitali, lakini akasita. Atamwachaje mtoto hapo?
Akafikiri afanye nini.
Baada ya muda kidogo akaona ni kheri tu
kama ataenda na mtoto huyo hospitali. Asingekuwa na amani kama mtoto huyo
angelibaki mwenyewe nyumbani. Hakuwa na budi. Akajifungia mwanaye kifuani kwa
kibebeo maalum kisha akabeba chupa ya maziwa endapo kama mtoto atahitaji hapo
baadae.
Akajiweka kwenye gari na safari ya kwenda hospitali
ikaanza. Alifikiri sana alipokuwa njiani. Maisha yalikuwa yamebadilika pasipo
mkewe, inabidi atafute namna, hawezi akawa anaongozana na mtoto muda wote. Vipi
akihitaji kwenda kazini?
Akiwa kwenye foleni la mataa,
akakubali na nafsi yake kuwa kwa kipindi hiki ambacho mkewe anaumwa, inabidi
amtafute ‘babysitter’ atakayemtazama mtoto na kumpa mahitaji yake. Na pale mkewe
atakaporejea kwenye hali yake basi mhudumu huyo atajiendea
zake.
Ila akapata tena wazo jingine, vipi kama akiwa anampeleka
mtoto huyo mahali pa kutunzia watoto, ‘daycare’, huko awe anampitia akitoka
kwenye mihangaiko yake?
Kidogo wazo hili likawa gumu. Aliona ni
kama kumtupa mtoto wake kwa kufanya hivyo. Hapana, siwezi, akawaza. Hakuwa na
imani sana na hiyo njia hivyo akachagua ile ya kwanza, amtafute dada atakayekuwa
anamsaidia.
Akaendesha gari mpaka hospitali. Alipofika huko
akazima gari lake na kukwea kwenda juu. Aliposonga kuendea pale ambapo mkewe
alikuwa amepumzishiwa, akastaajabu kumwona Melissa!
Mwanamke
huyo alikuwa amesimama akitazamatazama huku na huko, mkononi mwake ana simu
kubwa nyeusi anayoipigapiga kiganjani. Alikuwa ni kama mtu
aliyepotea.
Darren akamfuata kwa hasira na kusimama mbele yake
akimuuliza, “Umekuja kufanya nini hapa Melissa?”
“Kukuona,”
Melissa akajibu kwa tabasamu. “Kwani kuna ubaya?”
“Melissa,
nikuambie mara ngapi wewe?”
“Kwani Darren mimi nimekuambia mara
ngapi? Ushawahi kunielewa?”
“Hivi hauogopi hata Roby akijua upo
hapa.”
Melissa akaguna kwa cheko. “Roby?” akauliza na kisha
akatabasamu. “Hawezi jua. Amejilalia hajiwezi!”
“Melissa,
nikuombeje uachane na maisha yangu? Nikuombeje, ebu niambie. Melissa achana na
maisha yangu. Naku--” Mara nesi akapita na kuzama ndani ya chumba alicholazwa
Josephine. Kidogo tena, mlinzi aliyekuwa amevalia sare zake akajongea eneo hilo
na kuuliza, “Kuna tatizo hapa?”
Darren akamtazama Melissa,
Melissa akamjibu mlinzi, “Hamna tatizo, bwana. Waweza tu kuendelea na majukumu
yako mengine.”
Lakini kabla mlinzi hajaondoka hapo, mara nesi
akatoka chumba cha mgonjwa akiwa anatembea kwa kasi sana. Darren akapatwa na
hofu. Kidogo tu, nesi akarejea na daktari wakazama mule
chumbani.
Kama baada ya robo saa, daktari akatoka na kumwambia
Darren kuwa mke wake amefariki.
Darren alihisi daktari
anamtania. Aliuliza mara nne kama alichoambiwa ni kweli na daktari asibadilishe
maneno akarejelea kauli yake ile ile na kisha kumpa pole Darren kwa kumpoteza
mtu wake wa karibu.
Darren akalia kama mtoto mdogo. Msalaba huu
ulikuwa ni mkubwa sana kwake. Hakujiona kama anaweza kuubeba. Bado alikuwa
anamhitaji mke wake haswa kipindi hiki ambacho mtoto ni
mdogo.
Ataishije? Alijiuliza akiwa anamwaga machozi kwenye
benchi. Melissa alijaribu kumtuliza lakini asifanikiwe. Bwana huyo aliendelea
kulia kwa uchungu kwa kumpoteza mpendwa wake. Mwishowe hata machozi na sauti
ikawa imemkauka.
Baada
ya watu wote kuondoka na kumwacha makaburini, Darren aliijipangusa mdomo wake na
kutazama kaburi la mkewe. Bado halikuwa limesimikwa jina wala maelezo yoyote
yale. Macho yake yalikuwa makavu na meupe, hakulia siku
hiyo.
Alichuchumaa na kusema mwenyewe akiamini anateta na
mkewe, “Nakupenda sana, mke wangu. Umeondoka tukiwa hatujamaliza tofauti zetu.
Roho inaniuma sana kwa hilo lakini sina cha kufanya. Nisamehe sana
mpenzi.”
Aliposema maneno hayo akanyamaza kwanza. Macho
yakaanza kujawa na machozi. Akajipangusa na kuendelea kusema, mara hii sauti
yake ikiwa inatetemeka. “Sijui nitaishi vipi pasipo wewe. Sijajua …”
akajipangusa chozi. Alikuwa anahisi kifua chake kinawaka moto. Moyo umekuwa
mzito sana. Alikuwa anajihisi hovyo, hovyo ambayo haiwezi
kuelezeka.
“Umekuwa mwanamke wangu wa kujivunia kwa muda wote
huo. Siwezi kueleza ni kwa namna gani ulijaza upendo na furaha ndani ya nyumba
yangu. Hakika hakuna wa kuziba pengo lako. Maisha yangu hayatakuwa sawa tena
pasipo na wewe.”
Kisha akanyanyuka na kuendea gari, akajipakia
kwenye viti vya nyuma na kufunga mlango, gari likaondoka. Dereva alikuwa Roby,
pembeni yake akiwa amekaa Melissa.
Japo watu walikuwa wawili
kwenye gari, Darren hakuongea chochote. Alikuwa kwenye ulimwengu wake wa pekee
kabisa. Akiwa amelaza kichwa chake kwenye kiti, alikuwa anatazama nje. Uso wake
ulikuwa umepooza na kupwaya. Alikuwa mbali sana kimawazo.
Gari
lilisimama mbele ya nyumba yake, Roby akamgeukia na kumuuliza kama yuko sawa,
lakini hakuwa anasikia kitu. Ilimbidi Roby arejelee swali lake mara tatu ndipo
Darren akamtazama na kumjibu. “Niko sawa, nashukuru.”
Na kabla
halijaongezewa neno lingine, akafungua mlango na kutoka ndani ya gari.
“Kwaheri!” akapunga mkono wake mara moja kwa Roby kisha akajigeuza na kuelekea
ndani kwake.
Basi baada ya hapo maisha ya Darren yakabadilika
kabisa. Hakuwa mtu wa kuzungumza bali kukaa kimya na kujitenga. Mara nyingi
alikuwa ni mtu wa mawazo sana na hata kulia. Ndani ya juma moja tu akapungua
uzito kwa kiasi kikubwa sana. Alikuwa ni kana kwamba mtu anayeliwa na kansa
hatua ya nne.
Hakuwa na raha. Ilikuwa ni nadra kwake kutabasamu
ama kucheka. Roby akajitahidi sana kukaa naye na kumhasa lakini haikusaidia.
Naye Isabel akajaribu sana kujiweka karibu na Darren, lakini bado jitihada zake
zikagonga mwamba. Darren hakuwa anataka kukaa karibu na mtu. Alikuwa anataka
kukaa mwenyewe tu.
Akirudi nyumbani humuuliza dada wa kazi juu
ya maendeleo ya mtoto kisha anamwona mwanaye kwa muda mfupi na kwenda kujilaza.
Siku nyingine akawa anarudi nyumbani akiwa na chupa za vinywaji vikali.
Anakunywa pasipo kujionea huruma na kisha analala kama mfu.
Siku
nyingine hata kazini akawa haendi. Anakunywa tu siku nzima. Afya yake ikaendelea
kuzorota.
Ikiwa ni mwezi mmoja umepita tangu Josephine afariki,
Darren akajiona sasa anahitaji msaada. Alionana na mwanasaikolojia na kumweleza
shida yake kwa ajili ya ‘counselling’. bwana huyo mwanasaikolojia, bwana Hamlet,
akajitahidi kadiri ya uwezo wake kumsaidia Darren kwa kumpatia ushauri, lakini
Darren akaenda mbele zaidi kwa kumwambia na yale mengine yakutisha. Mambo
anayoona usiku na viumbe wa ajabu.
Hapo bwana Hamlet akasita
kumshauri. Mwanzo alihisi Darren atakuwa amekanganyikiwa kutokana na kumpoteza
mtu wake wa karibu lakini baadae akaja kuelewa baada ya Darren kumwambia
alishawahi kuyaona mambo hayo hata kabla ya mkewe
kufariki.
“Tafadhali, unaweza kunisaidia?” Darren alilia. Bwana
Hamlet akamtazama kwanza mwanaume huyo kwa mafikirio kisha akamsihi apate muda
wa kupumzika zaidi, pia kama itakuwa inawezekana basi akatafute mahali pengine
pa kuishi mbali na hapo alipo. Pengine yaweza kumsaidia.
Darren
akashukuru kwa ushauri na kwenda zake. Alipojiweka kwenye gari akafikiria kwanza
maneno aliyoambiwa na bwana Hamlet.
Akiwa fikirani humo, mara
upepo wa wastani ukapuliza kiasi na kupeperusha gazeti fulani lililokuwa chini
mpaka kwenye kioo cha gari lake. Gazeti hilo lilikuwa la kale kidogo. Upande
ambao ulijipachika kiooni ulikuwa na picha ndogo tatu na maelezo kadha wa
kadha.
Katika maelezo hayo, mojawapo ilisomeka; *“MWANAMKE
ANAYESUMBULIWA NA VIUMBE WA AJABU, APOTEA.”*
Habari hiyo
ilikamata fahamu za Darren. Kidogo upepo ukalisomba gazeti hilo na kulitupia
kando na kuliburuza zaidi na zaidi. Darren akatoka kwenye gari na kulikimbilia.
Akalinyaka na kurudi ndani ya gari. Akatulia na kusoma taratibu habari ile
ambayo ilimkamata hisia.
Alipomaliza kusoma akaliweka gazeti
hilo kando na kutazama akiwa amejawa na mawazo. Kidogo akawasha gari na kuendea
anwani ya nyumba ambayo ameona taarifaze kwenye
gazeti.
Alitembea barabarani kwa masaa matano. Ilimlazimu aweke
mafuta ili akamilishe safari yake. Alipofika, ilikuwa ni nyumba ya mbao yenye
ukubwa wa wastani, akagonga na punde akafunguliwa na binti mwenye makamo ya
miaka ishirini, akaeleza shida yake anataka kuonana na
wazazi.
Binti akamkaribisha ndani na kidogo akaja mwanamke
mnene kidogo mwenye nywele fupi nyeusi. Mwanamke huyo alikuwa ana macho makali
na mkononi mwake alikuwa amebebelea kitambaa alichokuwa anatumia kukaushia
vyombo. Yule binti aliyemkarimu mgeni akaenda zake
chumbani.
“Habari, naitwa Darren.”
“Karibu,
naweza kukusaidia,” aliuliza yule mwanamke akiwa anatazama kwa mashaka. Hakuwa
na imani machoni. Darren akaeleza shida yake akionyesha lile gazeti. Alikuwa
anataka kusikia habari zaidi za yule mwanamke aliyepotea. Kwa namna moja ama
nyingine alikuwa anaona habari hiyo na ile ya maisha yake
zinawiana.
Baada ya kusema hivyo yule mwanamke mwenyeji
akatazama chini na kisha akarudi alipotokea, jikoni, kisha baada ta muda kidogo
akarudi akiwa hana kile kitambaa bali ana kisu. Kidogo Darren akahofia. Mwanamke
yule akaketi kiti kitazamanacho na Darren alafu akaweka kisu chake
mezani.
Kisu kilikuwa kina mpini wa bluu, na kama ungekitazama
vema ungeona maandishi yasomekayo ‘stainless steel’ kwenye shina la makali yake.
Kilikuwa ni kisu kirefu chenye ncha kali. Darren alishindwa kujizuia
kutokutazama kisu hicho.
“Upo tayari na utasadiki?” akauliza
mwanamke yule akiwa anamtazama Darren machoni.
“Ndio, nipo
tayari,” Darren akajibu. Basi mwanamke yule akanyanyua kisu kile na kukichomeka
kwanguvu mezani. Kisu kikachimba meza na kusimama dede. Darren akazidi
kuhofu.
Basi mwanamke yule akaanza kusimulia kwa sauti yake
inayofanana na kasuku. Akiwa ameongea sentensi mbili tu, upepo ukapuliza
dirishani na kupeperusha pazia kama bendera. Darren akatazama huko upesi akiwa
mjawa wa mashaka.
Mwanamke yule akiwa anamtazama
Darren machoni akasema ya kwamba yeye hana majibu ambayo Darren alikuwa
anayauliza, ila tu amefurahishwa sana na uwepo wa Darren hapo. Lakini
inawezekanaje hilo na ingali Darren hajuani na mwanamke
huyo?
Darren alipouliza, akatahamaki mwanamke yule anabadili
rangi ya macho yake na kuwa nyeusi kama bendera. Alafu mwanamke huyo akachomoa
kisu chake toka mezani na kumrukia Darren akitaka
kumchoma.
Ilikuwa ni swala la kufumba na kufumbua tu, nyumba
ile ikawa ghofu kabisa. Paa lake lilijawa na tando za buibui na madirisha yakiwa
yamepotea yasionekane. Kulikuwa giza, mwanga hafifu rangi nyekundu ikiwa
inatambaza kwa mbali.
Ilikuwa ni ajabu namna gani ambavyo mambo
yalbadilika kwa upesi namna ile! Nyumba iliyokuwa ni nzuri ikageuka na kuwa
nyumba ya mizimu, nyumba ya majini! Harufu ya damu ilitawala na mifupa huku na
kule.
Kwa
Darren yalikuwa ni kama mazingaombwe ama maigizo! Hakuwa anaelewa kinachoendelea
hapa. Kila kitu kwake kilikuwa ni kama amerukwa na akili. Kitu pekee alichokuwa
ana kijua na kupambana nacho ni kuokoa nafsi yake dhidi ya umauti uliokuwa
unataka kumkumba.
Hakujua alikuwa amezama. Tena amezama kwenye
lindi zito la kifo. Ameshikwa kwenye tego kali la
kummaliza.
Akapambana kumzuia mwanamke yule asimkite na kisu,
na alipofanikiwa kufanya hivyo baada ya kumtwanga mwanamke huyo kichwa cha
puani, akakimbilia mlango afungue na kwenda, lakini alipofika mlango
haukufunguka abadani! Haikujalisha ni nguvu kiasi gani alitumia, mlango
ukamtazama kodo pasipo mafanikio.
Yule mwanamke akacheka sana.
Akanyanyuka toka chini huku akijitoboatoboa na ncha ya kisu kana kwamba godoro.
Ilikuwa ni ajabu kwamba ahisi maumivu? Akavuja damu na kujichafua haswa lakini
hakuwa anajali hata kidogo.
Alimtazama Darren kwa macho ya
matamanio, alafu akalamba kisu chake kana kwamba mtoto na mche wa ‘ice-cream’,
alafu kufumba na kufumbua akamkimbilia mwanaume huyo akammalize. Mwendo wake
ulikuwa wa kasi sana, lakini kabla hajafika aendapo, kumbe Darren alikuwa
ameshakamata stuli kwa mikono yake miwili, akamkandika kwanguvu mno! Puuh!!!
Mwanamke huyo akasombwa na kubwagwa ukutani, kisha kukawa
kimya!
Darren, akiwa anahema kwa hofu, akamtazama mwanamke yule
kwa jicho la tahadhari. Bado mikononi akiwa ameshikilia ile stuli yake endapo
lolote litajiri. Ikapita dakika ya kwanza kukiwa kimya. Dakika ya pi… akasikia
mlango unafunguliwa! Akatupa macho yake kupambana na kiza kilichopo apate
kuona.
Hakuona kitu!
Moyo wake ulikuwa
unamwenda mbio sana. Kwasababu kulikuwa na ukimya wa kufanya masikio yawe
kiziwi, Darren alikuwa anaweza kusikia mapigo yake ya moyo kwa uzuri kabisa.
Angeliweza kuyahesabu pasipo matatizo kabisa.
Kidogo, akapata
wazo la kutumia stuli ile kubomolea mlango. Akabondea hapo mara kadha wa kadha.
Akaponda na kubonda lakini mlango haukufunguka. Ulikuwa ni migumu kama ile ya
kasri ya mfalme. Ulikuwa ni mgumu kana kwamba malighafi yake ni chuma na metali!
Badala ya mlango kukongoroka, ni stuli ndiyo ikaanza kuwa dhoofu na kuanza
kumomonyoka!
Mwishowe Darren akabakiwa na vipande tu vya stuli
mkononi mwake ingali mlango ukiwa madhubuti.
Akainama kwa
kuchoka. Akahema sana akivuja jasho. … lakini nyuma yake kule kulipotoka sauti
ya mlango kulikuwa na nini? Kama ungetazama vema, kwa kuyafinya macho na
kusisitiza maono yako basi ungeliona kuna kiumbe kilikuwa kinatembea gizani
kumjongea.
Miguu ya kiumbe huyu ilikuwa inakanyaga sakafu
taratibu. Kwasababu ya kiza, hakikuwa kinaonekana
vema.
Kilisonga kwa hatua ya karibu lakini
harakaharaka.
Darren alihisi kitu, upesi akageuka na kuangaza
koridoni, kizani. Hakuwa anaweza kuona kitu. Japo alikodoa bado hakuwa na uwezo
wa kuona jambo. Alipomtazaa yule mwanamke aliyemsomba kwa kumkita awali,
akamwona bado amelala palepale. Sasa ni nini hicho anahisi?
Akajiuliza.
Kufumba na kufumbua, Darren akastaajabu kuona kitu
juu ya paa. Hajakaa vema wala kujitengenezea, kiumbe hicho kikamvamia na
kumwangusha chini kikimkaba na kumng’ata shingoni!
Mdomo wake
ulikuwa wa baridi sana. Meno yake yaliyochongoka yalikita kwenye mishipa ya
shingo ya Darren na kisha koo lake likawa linamnyonya damu!
Kwa
ubaridi wa kinywa hicho, Darren akahisi mwili wake umezamishwa kwenye dimbwi la
barafu. Alihisi baridi toka kwenye nyayo yake mpaka utosini. Lakini baridi hili
likiwa linakera! Baridi linalotisha.
Pumzi ya kiumbe hicho
ilisabahi shingo yake na kuzidi kumtia hofu na
kimuhemuhe.
Kheri Darren bado alikuwa na vipande vile vya stuli
mkononi. Kama mtu aliyepandwa na kichaa, akatumia vipande hivyo kwanguvu na
pasipo mafikirio kumshabulia kile kiumbe
kilichomshikilia.
Akamtoboatoboa kiasi kwamba hata yeye
akajiumiza. Kile kiumbe kikapiga kelele na kuangukia chini. Kabla Darren
hajamtazama mvamizi wake huyo akagundua kuwa shingoni alikuwa anachuruzwa na
kimiminika cha moto. Alipojipapasa akagundua ni damu! Alikuwa anchuruzwa na damu
nyingi na akihisi maumivu makali.
Alimtazama kiumbe kile
alichoadhibu na kubaini alikuwa ni yule mtoto aliyemkaribisha na kumfungulia.
Alikuwa amejilaza akiwa ametulia na kuvuja damu. Alipotazama kule ambapo alikuwa
amelala yule mwanamke aliyemwadhibu mwanzoni, ajabu hakuona
kitu!
Akiwa ameweka kiganja chake shingoni kuzuiza damu
zinazotiririka, akajongea na kuangaza pale alipokuwa amemwona mwanamke yule
mwanzoni. Lah! Hakuwapo. Hapo akapata hofu sana. Kutokuwapo kwa mtu huyo
kulikuwa ni ishara mbaya kwa usalama wake.
Akatazama kushoto na
kulia, juu na chini asione kitu! Moyo wake bado ulikuwa unadunda kwa kasi, na
damu bado zamchuruza kufurika vidole vyake. Ni wazi alikuwa ana muda mfupi wa
kuwa hai kama jeraha hilo lisingepata huduma ya
upesi.
Aliendelea kuangaza na kuangaza. Kidogo akahisi upande
wake wa kulikuwa na kiumbe. Alirusha macho yake upesi akikodoa. Mkono wake wa
kuume alikuwa amebebelea kipande cha stuli na ule wa kushoto ukiwa umehifadhi
jeraha.
Baada ya muda kidogo, akaona kuna kitu chenye rangi
nyeupe ya kufifia mule kizani. Alipojaribu kukaza macho yake atazame,
akashindwa. Alikuwa ameanza kuishiwa na nguvu na macho yake yakijawa na
ukungu.
Kidogo akaona kitu kile chenye
rangi nyeupe kikisogea zaidi karibu yake. Alikuwa ni mtu lakini alishindwa
akumtambua kutokana na macho yake kudhoofu. Na hata alipotaka kumshambulia mtu
huyo kwa kutumia silaha yake, hakuweza. Hakuwa na nguvu hiyo tena. Jeraha
lilishamzidi nguvu.
Akazabwa kofi shavu lake la kulia na
kudondoka chini. Hata hakuhisi maumivu tena. Kitu pekee ambacho kilikuwa hai
kwenye mwili wake ni macho yake yaliyokuwa yamekodoa na kuoa ukungu. Aliona tu
kiza, kiza na yeye.
Na jambo la mwisho ambalo alilielewa ni
kushikwa shati lake na kuburuzwa. Kidogo tu akapoteza fahamu
kabisa.
Yalikuwa yamekwisha.
Hakuelewa
kinachoendelea hata kidogo. Alikuja kupata ufahamu wake akiwa kwenye gari, viti
vya nyuma. Alikuwa amechoka mno, kichwa kinamuuma. Mwili wake anauhisi dhaifu
viungio vyote vikiwa vinapwita.
Alijaribu kunyanyuka, akashika
kiuno kwa kulalama. Alijikaza akanyanyuka vivyo hivyo na kisha akatupa macho
yake kwenye kioo cha mbele cha gari. Ajabu alipotazama hapo akaona kipande kile
cha gazeti chenye taarifa juu ya mwanamke yule aliyekumbwa na mikasa kama yake.
Kipande kilekile cha gazeti ambacho kilimwelekeza kwenda kule kwa watu wa
ajabu.
Akashtuka baada ya kukumbuka mkasa alopitia. Hakika
haukufaa kusimulia. Kidogo gazeti lile likapeperushwa na upepo na punde
akaonekana mtu akiwa amekaa kwenye kiti cha pembeni ya dereva. Mtu huyo ametulia
tuli akitazama mbele.
Darren akashtuka kumwona mtu huyo maana
hakumwona hapo awali. Hakujua wapi ametokea. Akaita kwa woga na kuuliza ni nani?
Kidogo mtu huyo akageuka na kumwangazia Darren. Kumbe alikuwa ni
Melissa.
“Melissa!” Darren akafoka. “Kumbe ni
wewe?”
Alipandwa na hasira sana. Alijikuta ananyanyuka toka
kwenye kiti chake na kumvamia Melissa. Akamkaba na kumtwanga ngumi mfululizo kwa
hasira akiwa anafoka, “Niache na maisha yangu! Niache wewe mpuuzi! Niache!
Niache!”
Melissa akajikinga na mashambulizi makali ya Darren,
lakini alipoona yanamzidia, akamtupia mwanaume huyo nyuma ya gari! Alimnyanyua
kana kwamba usufi. Na Darren, kama mfuko wa saruji, akadondokea vitini na
kulalamikia maumivu ya kiuno chake.
“Niskize Darren!” Melissa
akapaza sauti yake kali. Vioo vikachipua nyufa. “Kwanini hautaki kunielewa?”
akauliza akiwa anamtazama mwanaume huyo kwa macho mekundu. “Kwanini unakuwa na
moyo mzito na kichwa kigumu?”
Akaongea sana lakini Darren
asijali. Alikuwa anagugumia maumivu ya kiuno huku akiwa anamtazama Melissa kwa
jicho la mbali. Melissa alipomaliza kujichosha kwa kuongea, Darren akamwambia
kwa sauti ya chini akiwa anachuruza chozi jicho lake la kushoto, “Toka kwenye
gari langu. Ondoka mbele yangu Melissa.”
Melissa akamtazama
Darren kwa sekunde nne pasipo kusema jambo. Macho yake yalidondosha machozi.
Alifungua mlango wa gari na kujiondokea, Darren akashusha pumzi ndefu. Alikuwa
anazidi kumwaga machozi aking’ata meno. Mwishowe alishindwa kabisa kujizuia,
akalia kilio kikuu.
Akalia sana akiwa anajiona yupo kwenye
lindi kubwa la matatizo. Akalia haswa akihitaji kusafisha kifua na kichwa chake.
Mwishowe alipojiona kuwa yu sawa, akasonga kwenye kiti cha dereva na kuwasha
gari lake aondoke.
Akiwa njiani akawaza sana namna gani
aenende. Aliwaza sana nini afanye kujiondokea na matatizo, hata akawaza kujiua,
lakini akifanya vivyo nani atakaye mwangalia mtoto wake? Mkewe
alishafariki.
Aliendesha akiwa anamwaga tu machozi. Alipofika
nyumbani akajilaza kitandani kwake pasipo kumtazama mwanaye. Alikuwa anawaza
sana. Ilipofika majira ya usiku, Isabel alimpigia na kumwomba
waonane.
Kulikuwa kumetulia kabisa, ungeweza kusikia
mdomo wa Isabel ukitafuna. Mwanamke huyo aliyekuwa amevalia suti rangi ya
zambarau alikuwa ameshikilia sambusa mkononi mwake na glasi ya sharubati ikiwa
mezani.
Mbele yake alikuwa ameketi Darren akiwa na glasi ya
mvinyo mwekundu pekee. Hakutaka kula maana hakuwa na hamu wala kujisikia kufanya
hivyo, uso wake ulikuwa umepoa, mara nyingi akitazama watu wanaoingia na kutoka
eneo hilo walilopo. Hakuwa sawa.
Kidogo Isabel akamshtua na
kumuuliza, “Utakuwa kwenye hali hiyo mpaka lini,
Darren?”
Darren akaminya lips zake asiseme kitu. Alitazama
glasi yake ya kinywaji kwa mawazo.
“Inabidi uniruhusu
nikusaidie Darren. Tafadhali.”
Bado Darren hakusema jambo.
Isabel akanywa sharubati yake na kisha akajifuta mdomo kwa
‘tissue’.
“Darren ukiendelea hivi utashindwa kufanya kazi zako.
Maisha yako yatapotea. Serious, inabidi ubadilike. Niambie nini
tatizo.”
Darren akanywa kwanza mafundo mawili alafu akashusha
pumzi ndefu kabla hajasema, “Unajua hapa karibuni nimepitia mambo makubwa sana.
Nadhani badi sijapata muda wa kutulia. Bado akili yangu haijakaa
sawa.”
“Najua, Darren,” akasema Isabel. “Najua umepitia milima
na mabonde hapa karibuni. Lakini inabidi uache vitu viende, sawa? Hauwezi kuishi
hivi milele? Hauoni namna unavypungua kwa mawazo? Inatosha Darren. Mfikirie
mwanao. Vipi kama ukipatwa na tatizo, atakuwa kwenye hali
gani?”
Darren akakosa majibu. Alifikicha macho yake akashika
tama.
“Sikia, Darren. Ningependa niwe karibu zaidi na wewe.
Naomba uniruhusu,” Isabel akapendekeza.
“Ukaribu kiasi gani,
Isabel?” Darren akauliza. “Kwani hapa hatuko karibu?”
“Tuko
karibu lakini nataka kuwa karibu zaidi. Naomba uniruhusu Darren. Nataka kuwa
karibu na wewe zaidi.”
Wakatazamana kwa kama sekunde tano.
Kulikuwa na kitu machoni mwa Isabel.
“Unaweza ukaja kuishi
kwangu,” Isabel akapendekeza. “Naishi mwenyewe pamoja na wafanyakazi. Nadhani
nitakuwa na wigo mpana wa kukusaidia. Mtoto wako pia hatapata shida. Unasemaje
Darren?”
Darren akabinua mdomo wake. Akanyanyua glasi ya
kinywaji na kupiga mafundo mawili tena kisha akamtazama Isabel
machoni.
“Hapana, Isabel. Haiwezi kuwa haraka kiasi
hicho.”
“Nini tatizo?” Isabel akauliza kwa kujiamini. Macho
yake makali yalikuwa yanamtazama Darren barabara.
“Si kwamba
kuna shida,” Darren akajibu. “Ila tu sijajiandaa kufanya hivyo. Hauoni kama ni
hatari?” Isabel akatikisa kichwa.
“Kwa upande wangu, sioni kama
kuna shida. Sijajua kwako.”
“Nipe muda nifikirie zaidi juu ya
hilo. Siwezi harakisha.”
“Sawa. Muda gani unakutosha kufanya
vivyo?”
“Nitakutaarifu, usijali.”
Lakini jibu
hilo halikumridhisha Isabel. Alipokunywa fundo moja kumalizia kinywaji chake
akauliza, “Kwanini usinipe muda halisia, Darren. Huoni unaweza kuningojesha
milele kwa kauli hiyo?”
Basi Darren kwa kulazimika, akasema
mpaka juma lijalo atakuwa tayari ameshampatia jibu. Angalau Isabel akafurahi.
Wakamalizia maongezi yao kwa kuongea biashara juu ya ile nyumba ya bibi yake
Darren kule ‘countryside’, wakaafikiana mpaka bei, ambapo ilikuwa pesa kubwa
sana.
Kwa mawazo ya Darren aliona ni kheri akamuuzia Isabel
nyumba hiyo kwani haikuwa na faida tena kwake, lakini zaidi apate kiasi cha pesa
kitakachomwezesha kuwa na makazi mapya, makazi ambayo yatakuwa salama kwake na
familia yake. Aliwaza pengine akihama, anaweza akapata pumziko la kichwa
chake.
“Kwahiyo utaingiza lini hiyo pesa?”
Akauliza.
“Kesho mchana,” Isabel akamjibu. Kidogo Darren
akashangazwa, kilikuwa ni kiasi kikubwa cha pesa kupatikana haraka namna
hiyo!
“Kuna shida, Darren?”
“Hapana. Hamna
tatizo kabisa.”
“Sawa. Kesho tazama akaunti yako kuanzia majira
ya saa sita mchana.”
Wakakubaliana hilo na basi kama
alivyomleta, Isabel akamrejesha Darren nyumbani kwake, lakini kabla hajashuka,
akamshika mwanaume huyo mkono wake wa kushoto na kumtazama
kidogo.
“Kama kutakuwa na tatizo nijulishe
Darren.”
Darren akatikisa kichwa chake kuafiki alafu akashuka
toka kwenye gari na kwenda ndani. Kulikuwa ni kimya. Alishangaa kukuta hali
hiyo. Akamwita dada wa kazi mara tatu pasipo majibu. Akapata shaka kidogo.
Akanyanyuka na kwenda vyumbani, akakagua kila chumba lakini hakumwona dada wa
kazi wala mtoto wake. Hapa shaka lake likakua zaidi.
Akajaribu
kupiga simu ya dada wa kazi, ikaita, ila alipotulia na kuskiza vema akagundua
simu hiyo inaitia ndani. Alipoenda chumbani kwa dada huyo akabaini simu ilikuwa
imefunikwa na shuka. Sasa ameenda wapi na mtoto?
Tumbo likaanza
kumsokota.
Alitoka ndani kwake akaenda kuuliza majirani kama
wamemwona msichana huyo na mtoto wake lakini hakupata kitu. Alihisi
kuchanganyikiwa. Alirejea ndani akaketi akiwaza na kuwazua. Muda ukaenda mpaka
majira ya saa tatu usiku.
Sasa akaona ni vema atoe taarifa
polisi kwa uchunguzi zaidi. Akatoa kila taarifa aliyoifahamu na polisi wakaanza
kazi yao. Lakini kwenye majira ya saa nne usiku, dada wa kazi akarejea akiwa na
mtoto.
Dada huyo mkononi alikuwa amebebelea vitu vya mtoto na
kwa kutumia kibebeo maaulum alikuwa amembelea mtoto kifuani mwake. Darren
akafurahi sana kumwona mwanae. Akamkumbatia kwanguvu na kumuuliza dada wa kazi
wapi alikwenda kwa muda wote huo.
“Nilienda kumchukulia mtoto
mahitaji yake,” dada akajitetea. “Lakini nilikutana na msongamano mkubwa wa
magari sababu ya ajali. Samahani sana.”
Baada ya maelezo hayo,
dada huyo akaenda chumbani kwake akimwacha Darren na mwanaye pale sebuleni.
Darren akatoa taarifa polisi juu ya kumpata mwanaye.
“...
Nashukuru sana, nitakuwa mwangalifu zaidi siku
nyingine.”
Alipokata simu ndipo akagundua kuna kitu kwa
mwanaye.
Nyuma ya mgongo wa mwanaye, chini kidogo ya
bega la kushoto, aligundua kuna chapa fulani ndogo. Chapa hiyo ilikuwa nyeusi
yenye ishara kama ya msalaba lakini ikiwa na mikono
miwili.
Hakujua maana ya chapa hiyo lakini alijikuta akiwa na
wasiwasi nayo. Alijaribu kuifuta kwa kutumia kidole chake, haikufutika.
Akajaribu kumfuta na kitambaa bado napo haikufutika, ilikuwa ni alama ya
kudumu!
Upesi akamuuliza dada wa kazi apate kujua nini
kimemtokea mtoto. Lakini dada, akiwa ameparamiwa na uso wa hofu, akajitetea
sana. Hakuwa anafahamu lolote. Hakuwa anajua hata kama mtoto ana chapa hiyo?
Amemwogesha jana yake na hata siku hiyo asubuhi lakini hakuona alama kama
hiyo.
Darren
akatingwa na maswali lakini pia na hofu. Hakuhisi kama mwanaye yuko salama. Kila
mara alitazama alama hiyo na kujiuliza maswali mengi kichwani. Mwishowe aliona
ni kheri akafanya jitihada zaidi kung’amua chapa hiyo na hapo ndipo akazama
kwenye mtandao na kusaka alama ile baada ya kuiweka kwenye mashine
yake.
Baada ya muda kidogo akapata kuona taarifa chache juu ya
chapa hiyo ikiwa inahusishwa na habari za zamani sana kuhusu huko Uajemi tena ni
ishara aghalabu ya majini!
Alipotafuta sana akabaini kuwa
mwanawe hakuwa mtu wa kwanza kuwa nayo, takribani watu watatu walikuwa nayo, ila
mwisho wao wote ilikuwa ni kifo! Alipohangaika zaidi kutafuta mengineyo, akapata
kukutana na mwanamke mmoja ambaye mwanaye alikuwa na chapa hiyo. Alituma hilo
swala mtandaoni kuomba ushauri.
Basi hilo likawa kama neema kwa
Darren. Alitafuta zaidi taarifa za mwanamke huyo akafanikiwa kupata anwani yake,
akapanga kesho yake akamtafute amwambie zaidi kuhusu hiyo
chapa.
Alihofia sana juu ya mwanaye. Na kwa hofu hiyo akataka
alalae nae ndani ya chumba chake.
Ulipofika usiku wa manane,
Darren akiwa amelowea kwenye usingizi mzito, na pia nyumba ikiwa imetulia tuli
sawa sawa na mtaa mzima, taratibu mlango wa chumba alalacho dada wa kazi,
ulifunguliwa na kisha ukatuama pasipo lolote kutokea.
Kulikuwa
kimya.
Zilipopita kama sekunde tano, ndipo mkono uliobebelea
kisu ukatoka kwenye mlango huo. Bada ya punde, ukafuatia na mguu na kisha mtu
mzima kabisa. Alikuwa ni yule dada wa kazi.
Aliyatoa macho yake
akikodoa. Alitazama kushoto na kisha kulia, alafu akauendea ule mlango wa chumba
cha Darren. Alipoufikia, hakugonga, lah! Akapindua kitasa taratibu na mlango huo
ukafunguka. Alipousogeza vya kutosha, akatulia hapo
akisimama.
Zikapita kama sekunde nne. Basi taratibu akazamisha
mguu wake ndani ya chumba, na taratibu sana, akaweka nyayo zake sakafuni
akisonga. Alimwendea mtoto na kumpakua toka kwenye kitanda chake. Lakini mikono
yake ilikuwa ya baridi sana. Alipomshika mtoto tu, akaanza
kulia.
Akakodoa kumtazama Darren. Darren alikuwa amelala bado
fofofo. Lakini sauti ya mtoto iliyokuwa inaendelea kupaza na kupaza ilimshtua
sasa akaamka na kuangaza.
alipotazama kwenye kitanda cha mtoto,
hakukuwa na kitu. Kitanda kilikuwa tupu kikianza kujenga ubaridi!
Akachanganyikiwa sana. Alitazama kushoto na kulia kwake asione kitu, mlango
ulikuwa umefungwa, ila sauti ya mtoto bado akiisikia!
Sauti
hiyo ilikuwa ikiishilia!
Haraka akatoka kitandani na kudaka
korido. Akatazama na kupekua kwa macho yake, kidogo, masikio yake yakamwambia
kuwa sauti ya mtoto inatokea kwenye chumba cha dada yake wa
kazi!
Akauendea mlango huo na kubisha kwa kuutwanga ngumi.
Akaukandika na kuukandika lakini haukufunguliwa. Mtoto bado aliendelea
kulia!
Akiwa amepandwa na akili za ukichaa, Darren akaubamiza
teke kali mlango huo na kuuvunjia mbali. Alipotazama, akamwona dada wa kazi
akiwa amemkabia mtoto kitandani kwa kutumia mkono wa kushoto na ule wa kulia
ukiwa umeshikilia kisu akitaka kumchoma.
“Tafadhali, usimuue
mwanangu!” Darren akapaza sauti akimtazama dada wa kazi kwa imani. Dada
akatabasamu na kusema, “Lazima afe, Darren. Hata kama nisipomuua
mimi!”
“Kwanini?” Darren akalia. “Kwanini afe? Sina kitu
kingine mbali na huyo mtoto. Nambie unataka nini
nitakupatia!”
Dada akatabasamu almanusura kucheka. Alimtazama
mtoto kisha akayarudisha macho yake kwa Darren na kusema, “Sitaki chochote
Darren. Kama ningekuwa nataka chochote kile basi ningekitafuta na kukichukua
mwenyewe. Kwa sasa ninachotaka ni roho ya huyu kiumbe tu, si
kingine!”
“Lakini amekukosea nini?” Darren akauliza. Macho yake
yalikuwa mekundu yakikaribia kudondosha chozi.
“Hajafanya
kitu,” Dada akajibu akitikisa kichwa. “ila si mali yako tena. Huyu ni mali ya
majini, na ni wa kufa tu!”
Dada aliposema hayo akamkandika
mtoto kisu cha kifuani, chote kikazama na kutosha kumfanya mtoto mfu. Darren
akalia sana. Akakurupuka toka kitandani mwake na kumtazama mwanaye pembeni.
Nalikuwa ni ndoto. Mtoto alikuwa yu kwenye kitanda chake ila akilia
sana.
Upesi akamnyanyua na kujitahidi kumbembeleza …
sh!-sh!-sh!-sh!-sh!-sh! … lakini alipotazama dirishani akabaini kuwa li wazi.
Akalisongea na kutazama nje kama kuna lolote lile, hakuona jambo. Mtaa ulikuwa
umetulia sana. Ni upepo wa baridi ndio ulikuwa ukipuliza tena kwa
mbali.
Akalifunga dirisha hilo, bado mtoto akilia, alipomaliza
akasikia hodi mlangoni mwake. Kidogo mapigo yake yakaruka. Akiwa amemshikilia
mtoto wake vema, akapaza sauti
kuuliza,
“Nani?”
“Dada wa kazi!” sauti
ikamjibu toka mlangoni. Kidogo akajawa na mashaka.