Search This Blog

MAMA USINIFUNDISHE UCHAWI - 5





    Simulizi : Mama Usinifundishe Uchawi

    Sehemu Ya Tano (5)







    Tarehe 25, mwezi 3, mwaka 2017. Kilimo cha nyanya kikaanza katika kijiji cha Maharaka. Shamrashara za kilimo zikaanza katika kipindi hicho kwa shangwe kubwa. Vijana wengi wakalima na kipindi cha mavuno wengi wakapata mazao mengi. Katika hatua hizo zote Sharifu akapitia na akavuna nyanya kwa wingi shambani kwake. Akauza nyanya zake kwa pesa ndefu kushinda miaka yote iliyopita. Safari hii akafanikiwa kweli kweli kipesa hadi akafanikiwa kujenga jumba la wadhifa. Akafungua maduka mawili ya nafaka pale kijijini hatimaye akaonekana mtu katika watu. Japo alipata utajiri kilingeni alikuwa anaudhuria na kama kawaida.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sharifu, sasa ushapata utajiri ila zingatia kitu kimoja” alieleza Mzee Damanda siku hiyo katika kilinge. Kabla ajaendelea Mzee Damanda kuongea Sharifu akauliza.



    “Kitu gani, hicho?.”



    “Nisikilize kwa makini...utajiri wako haupaswi kuwa na mke. Ukiwa na mke tu unasababisha kilinge chetu chote kuteketea hivyo basi tulinde nasi tukulinde.”



    “Kiongozi, sasa mali zote nilizopata nani atakuwa mrithi wangu!!!?,” Sharifu aliuliza kwa kustaajabu.



    “Mrithi hatokuwepo, wewe tumia ukifika mwisho wako na mali zako zote zitateketea nadhani tumeelewana.”



    “Haya,” Sharifu aliitika kinyonge kama sitaki nataka. Mzee Damanda baada ya mazungumzo na Sharifu akanyamaza kidogo kisha akaangalia juu kwa muda huku akinena maneno ya kichawi.



    “Sundu cha ukoo, kalula manyakara,” Mzee Damanda aliomba kichawi kwenye mizimu wamletee kitu anachohitaji.



    Sekunde haikupita kikatokea chungu ndani yake kukiwa na Paka watatu. Akamtoa paka mmoja mweusi akamnyofoa shingoni kwa meno kisha akaanza kumnyonya damu Paka yule. Alipomaliza kumnyonya damu akatulia kidogo kisha akawatazama wanachama wake na kusema kwa kuanza na salamu yao.



    “Chanoga.”



    “Chanoga twala, kibakile twahipazi,” Wachawi wote kwa pamoja waliitikia salamu hile.



    “Leo ni siku muhimu sana kwa kijana wetu Sharifu.......... Tutamfanyia tafrija fupi ya kumpongeza kwa kupata mafanikio makubwa kama wanachama wengine humu,” Mzee Damanda alisema mara akanyamaza kidogo kisha akaendelea kusema.



    “Hivyo basi kwa kuwa leo ni siku ya furaha kwetu, tunyweni kwa pamoja,” Mzee Damanda aliongea huku akiwatoa Paka wawili waliobaki na kuwapa wanachama wake wanywe kwa kupokezana kama glasi ya mvinyo iliyotolewa na Yesu Kristo kwa wanafunzi wake.



    Baada ya tafrija kuisha wachawi wote wakatawanyika kwa kunyanyuka na kurudi majumbani. Sharifu na mama yake siku hiyo walichoka sana kuliko siku zote. Hivyo walivyofika kwenye mjengo wao kila mmoja akaingia chumbani kwake kupunguza usingizi. Saa moja ya asubuhi Sharifu akawahi kuamka akamwamsha na mama yake wakajiandaa kila mmoja akaenda kufungua duka lake. Maduka yao yana umbali kidogo Sharifu duka lake lipo kijijini Maharaka na mama yake duka lake lipo kijiji cha pili kutoka Maharaka. Kila mmoja alipofika kwenye duka lake akachakarika kwa kuuza anavyojua yeye. Jioni katika duka la Binti Mngane wateja wakapungua kwa muda ndipo alikuja dada mmoja aliyevaa kinadhifu akiwa anahitaji soda. Baada ya kupewa soda na kumaliza kuinywa huyo alitaka aondoke asahau kulipa lakini Binti Mngane akakumbuka kama binti yule hakulipa pesa. Hivyo akamzuia binti yule kuondoka hadi alipe pesa.



    “Binti hujanilipa pesa,” Binti Mngane alisema huku akimkodolea macho binti yule.



    “Aaaah, samahani sana nilijisahau,” Binti yule alisema huku akitoa pesa kwenye mfuko wa suruali yake na kumpatia Binti Mngane.



    “Msheeenzi wewe unadhani mimi wa kujaribiwa.... Ndiyo nini unanipa kijiti badala ya pesa,” Binti Mngane alitusi mara baada ya kugundua kama kapewa kijiti na si pesa na binti yule.



    “Fyoooo,” Binti yule aliachia sonyo takatifu kwa Binti Mngane mara baada ya kujua kagundulika.



    Binti Mngane siku zote atakagi dharau haswa kwa mtoto mdogo kama yule hivyo akaona bora amwonyeshe kuwa kuna watu si wa mchezo mchezo. Akakusanya nguvu za giza mwilini mwake kisha akamtupia kombora la haja binti yule. Looooh! Binti yule kumbe ni jini akaliona kombora la Binti Mngane akaligandisha angani kimiujiza kisha akachezesha macho ghafla. Kombora likamrudia Binti Mngane. Likampata Binti Mngane akadondoka chini puuuuuuuu! akaanza kuonekana kutokwa na damu pamoja na mapovu mdomoni hatimaye akazima ghafla. Hilo jini lilipomaliza kufanya mauaji kwa Binti Mngane akapotea eneo lile akaondoka sehemu isiyotambulika.



    **********

    Sharifu akiwa dukani machale yakamcheza, mapigo ya moyo yakaenda kasi hata raha akuwa nayo akiwa kwenye hali hile mara ghafla alikuja mtoto wa kijiji cha jirani akiwa kwenye mbio ya hatari. Alipofika dukani kwa Sharifu akapiga breki isiyo ya mfano akahema kwa kasi huku akisema kwa haraka.



    “Kaka Sharifu, mama yako kadondoka dukani kwake.”



    “Kadondoka!!!,” Sharifu aliongea kwa mshangao na haraka akafunga duka akaongozana na mtoto yule hadi kwenye duka lake la pili.



    Kufika dukani akashangaa kuona umati wa watu umejaa, akajikongoja hadi ndani ya duka hakuweza kuamini nguvu zote zikamwisha mara baada ya kumwona mama yake chini akiwa anatoka damu na mapovu mdomoni. Sharifu akachutama chini akajaribu kumfumbua macho mama yake lakini macho yakakataa kufumbua. Akachunguza mwili wa mama yake na akiwa kwenye uchunguzi katika shingo ya mama yake akaona nembo ya Mbwa Mwitu iliyoachwa na jini. Sharifu akagundua kuwa mama yake ameuwawa na kiumbe hatari kilicho na nguvu kuliko wao. Akainamia mwili wa mama yake na kulia. Akalia sana bila ya kunyamazishwa na mtu, ndipo kwa kuwa katika umati ule alikuwepo Mzee Damanda na ndiye aliyemtuma mtoto yule amuite Sharifu. Basi akasogea alipo Sharifu na kumtia maneno ya kufariji na ujasiri, kweli. Sharifu akapata ujasiri akamtoa mama yake nje na kufunga duka kisha akaita TOYO ili ichukue mwili wa mama yake na kuupeleka nyumbani. Mzee Damanda akasaidiana na Sharifu kupakiza mwili wa Binti Mngane kwenye TOYO kisha nao wakapanda na kumwamuru mwenye TOYO awapeleke nyumbani. Mwenye TOYO akawafikisha nyumbani ili waweze kuendelea na ratiba za mazishi. Sharifu akaandaa ratiba ya mazishi akishirikiana na Mzee Damanda kama inavyotambulika zaidi mazishi kufanyika jioni hivyo naye akapanga siku hiyo jioni. Mazishi bila mabadiliko yoyote yakafanyika na kila mmoja wao akatawanyika kurudi majumbani mwao. Sharifu akiwa njiani na Mzee Damanda wakielekea nyumbani huku akiwa na majonzi ndani ya moyo nyuma yao walikuwepo wamama wawili wakizungumza kwa sauti ya chini chini huku wakijua hakuna mtu anayesikia. Wakaachia vicheko vya kumsengenya Sharifu.





    “Mwenzangu, yaani ilikuwa hatari mama mchawi, mtoto mchawi ndani kulikuwa ni vurugu mechi. Mama ana wanga na mtoto ana wanga wakirudi wamechoka mmmm!, yaani hatari tupu,” Mama mmoja wapo aliongea kwa kumweleza mwenzake asiyefahamu siri za kina Sharifu.



    “Mh! Mwenzangu mbona unaniogopesha nishindwe kukaa kwa amani katika kijiji hiki,” Mama mwingine alisema kwa hofu kuhofia mambo ya kichawi yasimkute.



    “Sio kama nakutisha, ni ukweli mtupu...usimuone vile kijana yule ni mchawi puuuu!,” Mama yule alizidi kutoa siri za Sharifu kwa mwenzake na mwisho akatema mate chini kumkebehi na kumdharau Sharifu.



    Sharifu mazungumzo yale akayasikia tokea muda akayapotezea. Hili la mwisho likamchoma akageuka akamkazia macho yule mama kisha akapeleka kidole kwenye mdomo kwa ishara kumwonya yule mama asiendelee kuongea. Yule mama kwa kuwa ni kiroporopo hakusikiliza onyo akaendelea kubwabwaja siri zote za Sharifu kwa yule mwenzie. Mdomo ukaponza kichwa, yule mama akaendelea kubwabwaja. Sharifu safari hii akanyanyua mkono wake wa kushoto kisha akapeleka shingoni na kufanya ishara ya kuchinja. Papo hapo yule mama hakuomba hata maji akaenda chini na kuaga dunia. Kisha Sharifu wakati akikamilisha tukio hilo akaonyesha kuendelea na safari yake kurejea nyumbani na Mzee Damanda huku nyuma wakimwacha yule mama mwengine akisumbuka kujaribu kumwamsha mwenzake aliyenyongwa kwa nguvu za giza. Walipofika njia panda Sharifu na Mzee Damanda wakaagana na kila mmoja akaelekea kwake. Mzee Damanda akayeyuka akatokea kwake na Sharifu akayeyuka akatokea kwake sebuleni.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    **********

    Miezi ikayoyoma mwaka ukakatika Sharifu alikuwa mpweke siku zote, toka udogo wake alizoea kuwa na mama. Kwa sasa mama amemtoka amekuwa kama mtoto aliyetelekezwa mtaani. Hana mbele wala nyuma, hana wa kumfariji wala wa kumshauri. Chama nacho kinampa pingamizi tata kinachomletea utata katika maisha pindi afikiriapo maneno ya Mzee Damanda.



    “Nisikilize kwa makini...utajiri wako haupaswi kuwa na mke, ukiwa na mke tu unasababisha kilinge chetu chote kuteketea hivyo basi tulinde nasi tukulinde,” Sharifu akaona ni upuuzi inawezekana vipi aishi kwenye mjumba wa wadhifa pekee yake kama msukule bila ya kuwa na mke wala watoto wa kumchangamsha na kumfariji. Ndipo hapo akaamua kukaidi maneno ya Mzee Damanda na kusema;



    “Kama liwalo na liwe tu, mimi siwezi kaa jumba lote hili kama zindiko kisa chama kinataka.”



    Adhima yake kweli akaitekeleza. Akaenda kijiji cha mbali kuchumbia na kuoa huko huko ili wachawi wenzie wasigundue kama ameoa. Akarudi kijijini kwao akiwa na jiko akaishi na mkewe kisiri sana katika kijiji cha Maharaka, takribani miezi mitatu bila ya wachawi wenzake kujua na wala mkewe kujua kwamba yeye ni mchawi. Ndani ya mwezi wa tatu siku moja ndipo siri ikagundulika. Ikajulikana na kuanza kuchunguzwa wakati mama mmoja aliye miongoni mwa wachawi wa Marahaka, akipita karibu na nyumba ya Sharifu na kusikia sauti ya mwanamke na ya Sharifu zikiongea. Akasogea jirani zaidi na dirisha ili asikilize kinachoendelea ndani humo.



    “Sharifu, nimechoka kukaa humu ndani. Wewe fikiria mwenyewe nitakaa humu ndani hadi lini........ Kila siku unaniambia kesho kesho imekuwa nyimbo ya taifa,” Mama yule alimsikia mke wa Sharifu nadhani akinung'unika kwa nini hatoki nje.



    “Vumilia kidogo Sauda, kuna mambo nataka niweke sawa mke wangu...hivyo yakiisha nitashughulikia ombi lako,” Mama yule safari hii alisikia sauti ya Sharifu ikiongea kwa upole ikimbembeleza mkewe.



    Mama yule mshakunaku akatimua mbio kupeleka umbea kwa Mzee Damanda kuwa Sharifu kakaidi sharti alilompa. Akafika kwa Mzee Damanda na kumkuta Mzee Damanda ndani akijisomea kitabu cha KUBALI TUYAMALIZE kilichoandikwa na kutungwa na mwandishi AMRI BAWJI. Akamkurupua ndani kwa kumuita nje. Mzee Damanda akasikiliza wito wa mwanachama wake akafunika kitabu na kutoka nje kumsikiliza. Mama yule alipoona Mzee Damanda ametoka akavuta pumzi ndefu kisha akauliza swali.



    “Mzee Damanda, una habari kama mwanachama wetu kaoa?.”



    “Nani tena?.”



    “Si Sharifu...inamaana huna habari?.”



    “Sina habari...lakini kaoa lini mbona sijasikia tetesi hizo?.”



    “Naona kaoa muda kidogo, maana leo nimesikia kwa masikio yangu mwanamke wake akisema...nimechoka kukaa humu ndani. Wewe fikiria mwenyewe nitakaa ndani humu hadi lini...kila siku unaniambia kesho kesho imekuwa nyimbo ya taifa.”



    “Kwa hiyo hapo tuseme Sharifu ameoa kisiri siri amemficha mkewe tusijue...si ndiyo?.”



    “Haswaaa, bila shaka.”



    “Sasa mtoto huyu, anapoelekea sipo.”



    “Kabisaaa...anapoelekea huko ndiyo mwanzo wa kuleta matatizo.”



    “Basi asante kwa kuniletea taarifa...ngoja mimi nithibitishe. Nikigundua ni kweli nitakuwa sina chaguo.”



    “Sawa kiongozi, ngoja nami niende.”



    “Sawa...tutaonana baadae kilingeni.”



    Mama yule baada ya kutoa taarifa akaondoka huku nyuma akamwacha Mzee Damanda naye akiingia ndani kwaajili ya kuendelea kusoma kitabu. Akasoma kwa muda mrefu na hatimaye pale pale akapitiwa na usingizi sebuleni na kusababisha kitabu kidondoke na udenda kuanza kumtoka. Akiwa usingizini habari za Sharifu kuoa zikamjia ndotoni na pia utekelezaji wa mauaji ya wanachama wenzake watano walioeneza habari za kwamba Sharifu kaoa zikamtawala. Ghafla akiwa katika ndoto akashtushwa na Panya aliyemng'weng'wesa miguuni na kukimbia. Mzee Damanda akasonya kwa hasira huku akitukana.



    “Sheeenzi wewe!. Unatumwa mapema unakubali tu, nitakuangamiza ukaungane na wafu,” Mzee Damanda alijisemea kisha akanyanyuka akaingia chumbani kwenda kumalizia usingizi kitandani.



    Akapiga usingizi hadi mishale ya saa mbili kamili akaamka na kuketi kitandani kwa muda kisha akayayuka na kutokea ndani mwa Sharifu kwenye mlango wa kuingilia ndani. Akanyoosha mkono mbele kikatokea kikopo cha mafuta yenye rangi ya kijani akajipaka ili asipate kuonekana na mtu yeyote. Alipojipaka akayayuka akatokea sebuleni akamkuta Sharifu anapiga mahesabu ya mauzo ya dukani. Akaachana naye na kuendelea kufanya uchunguzi kama ni kweli maneno aliyoambiwa na mwanachama wake kama yanaukweli. Akayayuka na kutokea chumbani kwa Sharifu huko ndipo akajithibitishia kama maneno aliyoambiwa ni ya kweli. Akamkuta binti mweupe na mrefu wa wastani amelala kwenye kitanda cha Sharifu. Hakuwa na haja ya kuuliza akajua bila shaka yule ndiye mke wa Sharifu. Mzee Damanda hakuchukua uamuzi wowote kwa binti yule akayayuka chumbani akarudi tena sebuleni alipo Sharifu akanena maneno ya kichawi.



    “Guto charumba, zenga chelo mangamba” ghafla ukatokea unga mweupe mkononi mwa Mzee Damanda mara baada ya kumaliza kuzungumza maneno yale.



    Akapuliza unga ule kwa Sharifu ili alale muda mrefu ashindwe kwenda kilingeni. Sharifu muda huo huo akashikwa na usingizi wa ajabu na kushindwa kuendelea na mahesabu. Akalala pale pale sebuleni. Mzee Damanda baada ya kufanya jambo kwa Sharifu akatoweka na kuelekea kilingeni. Alipofika akawakuta wachawi wenzake wote washafika wanamngoja yeye. Akatoa salamu kisha akanzisha mdahalo na wanachama wake.



    “Mtoto huyu, mbona simwelewi?,” Mzee Damanda alisema huku akiwaangalia wanachama wake.



    “Mtoto gani huyo?,” Mama Kitenya kama atambulikavyo aliuliza swali mara baada ya kutomjua mtoto azungumziwaye na kiongozi wao.



    “Sharifu,” Mzee Damanda akajibu.



    “Kafanyaje tena?,” Mama Dungo naye kama atambulikavyo aliuliza mara baada ya kutofahamu kitu alichofanya Sharifu.



    “Si kaoa!,” Mzee Damanda akajibu.



    “Mtumeee!!!, si tulimwambia asioe sasa kaoa anataka atuangamize,” Fatuma alisema kwa mshangao mara baada ya kusikia hayo.



    “Sasa huyu mtoto tukimchekea tu anatuangamiza wote,” Mama Shura kama atambulikavyo aliongea kwa sauti ya juu kidogo na kuonekana kuchukizwa mno kwa kitendo alichokifanya Sharifu.



    “Kweli kabisa unavyosema Mama Shura...mtoto huyu tumdhibiti kabla mizimu haijachukia” aliongezea kusema Mzee Damanda.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kwa lini sasa anatakiwa kudhibitiwa?,” Fatuma aliuliza huku akiwaangalia wenzie kwa kutaka jibu.



    “Kwa leo haitowezekana kesho kabla atujaingia kilingeni yatupasa tukalidhibiti hili kwa kumuua mkewe maana yeye ndiye tatizo kwetu” alisema Mzee Damanda kwa kumaanisha kisha akamaliza kwa kusema.



    “Manjo, kuye,” Mzee Damanda aliwatakia usiku mwema wanachama wake kwa maneno ya kichawi kisha akapotea pale kwa kuyayuka huku nyuma wanachama wake nao wakayayuka mara baada ya kuthibitisha kuwa mdahalo umeisha.



    **********

    Sauda akaamka mapema lakini akashangaa kujikuta peke yake kitandani. Akanyanyuka akatoka chumbani akaelekea sebuleni. Alipofika sebuleni akafurahi sana, alipomuona mumewe kwenye sofa amelala huku akijikuna kutokana na mbu wa jana usiku waliomng'ata. Akamsogelea mumewe karibu kisha akamwamsha kwa sauti ya unyenyekevu yenye kubeba jumbe la upendo. Sharifu akashtuka nusura anguke mara baada ya mkewe kumwamsha akakaa wima sofani kisha akamtazama kwa kuduwaa. Mahabuba wake na laazizi wake wa ubani kwa muda akiwa ameduwaa sauti ya mkewe ikamzindua kwa kuuliza pindi ilipopenya kwenye ngoma ya masikio.



    “Sharifu, inamaana leo umelala hapa?.”



    “Eeenh...yaani jana nilikuwa kama mfu hata nilivyolala nilikuwa sijitambui.”



    “Wachawi, walikunyemelea nini?,” Sauda aliuliza kiutani.



    “Acha zako wewe, umeona mwili huu wakutembelewa na wachawi hovyo,” Sharifu alijibu naye kimasihala.





    “Haya bwana...jiandae basi unywe chai uende kazini siunajua ufunguo wa duka lile lengine unao wewe. Mtoto wa watu atakusubiri hadi atachoka sasa bora yaani uwahi ukampe ufunguo afungue duka anze kuuza.”



    “Kweli kabisa, ngoja nijiandae maana wateja ni asubuhi tukiwakosa wa asubuhi ujue ishakula kwetu hiyo,” Sharifu alisema kisha akainuliwa na mkewe akapelekwa chumbani kujiandaa mara baada ya kusafisha mwili na meno.



    Baada ya kujiandaa, akatoka chumbani akaelekea kufungua kinywa kwa chai ya maziwa na mkate. Alipomaliza kunywa na kula akamuaga mkewe kisha akaelekea kwenye duka alilokuwa akiuza mama yake ambalo kwasasa kamwajiri mtoto mmoja mchangamfu anayeishi kijiji hicho hicho cha Maharaka. Alipofika hapo dukani akamkabidhi mtoto yule funguo wa duka kisha yeye akaondoka kuelekea kwake kufungua duka. Nyakati za asubuhi hadi usiku akauza barabara, muda wa kufunga duka uliporuhusu akafunga duka na kujikongoja mdogo mdogo kurudi nyumbani. Kabla hajafika nyumbani njiani kwenye eneo la makaburini akasikia vifaranga vikilia kwa sauti ya juu. Alijipa ujasiri akaendelea na safari yake. Akapiga hatua tatu hakusikia tena vifaranga vikilia, hatua ya nne akataka kumkanyaga Chatu mbele yake akasita haraka akarudi nyuma kisha akaanza kutoa pumzi isiyo ya idadi.



    “Aaaaah!,” Sharifu hajatulia sawia akashtuka kumuona Chatu yule akiangua kicheko.



    “Wewe ni nani?,” Sharifu aliuliza kwa ujasiri. Swali halikujibiwa bali Chatu yule akajibadili akawa si Chatu tena bali akajibadili kuwa Mzee Damanda.



    “Leo nakuhitaji ufike kilingeni mapema,” Mzee Damanda alisema bila kung'ata maneno mara baada ya kutoka kwenye umbile la uchatu.



    Mzee Damanda alipomuhabarisha Sharifu akayeyuka. Akaenda kupita kila nyumba ya wanachama wake ili wasuke mpango wao. Wakausuka ukasukika kisha Mzee Damanda akarudi nyumbani kwaajili ya kusubiri muda wa kilingeni utimie. Muda ukatimia yapata saa nane kasoro tano ya usiku Mzee Damanda akajiandaa na kwenda kilingeni. Akamkuta Sharifu ameshafika muda kidogo kama alivyomwambia akiambatana na wanachama wenzake. Mzee Damanda akamtazama Sharifu kisha akaonyesha ishara ya kutikisa kichwa kumpongeza Sharifu katika kutii agizo. Hatimaye akawaangalia wanachama wengine kisha akatoa ishara ya kuinua kichwa juu. Ghafla wanachama wale wakapotea na kuwaacha kilingeni Sharifu na Mzee Damanda tu.



    “Kiongozi mbona wanachama wote wameondoka?” aliuliza Sharifu mara baada ya kuona wameachwa wenyewe.



    “Watarudi nimewatuma sehemu” alijibu Mzee Damanda kwa kumuondoa hofu Sharifu.



    **********

    Wachawi ambao ni Fatuma, Mama Shura, Mama Dungo na Mama Kitenya wakawasili nyumbani kwa Sharifu. Watatu wakabaki nje wakamtuma ndani Mama Kitenya akafanye mauaji kwa mke wa Sharifu. Mama Kitenya akayeyuka akatokea ndani akapita kila kona na kila chumba akimtafuta Sauda. Haweze kukamilisha mpango wake. Alikuja kumuona Sauda jikoni akiosha vyombo huku mkononi kashika kisu. Mama Kitenya akiwa nyuma ya Sauda akazungusha macho yake na Sauda akapinduka kumwangalia. Mama Kitenya akafumba macho yake kwa mara moja na kufumbua pale pale. Sauda akajichoma na kisu alichokishika papo hapo akaaga dunia. Baada ya mauaji Mama Kitenya na wenzake wakarudi kilingeni yapata saa kumi kamili wakamkuta Mzee Damanda na Sharifu wakiwasubiri. Sharifu alipoona wenzake wamerudi akawakaribisha na swali lenye kubeba jumbe tata kichwani kwa Mzee Damanda na wanachama.



    “Mmetoka wapi?,” Wachawi wote hawakulijibu lile swali la Sharifu wakabaki wakitazamana na kuonyesha sura ya kumficha Sharifu.



    “Mmetoka wapi?...maana ninavyojua kila pahala huwa tunatakiwa kwenda wote ila leo mmeenda wenyewe, kuna kitu mnanificha,” Sharifu aliuliza tena kisha akasema kwa manung'uniko mara baada ya kuona wenzake wote hawajamjibu mwanzoni.



    “Hakuna tunachokuficha, hawa niliwatuma kijiji cha jirani kuchunguza wachawi wa kule wanautaratibu upi,” Mzee Damanda alijaribu kudanganya ili Sharifu asijue kilichofanyika.



    “Huko ulikowatuma naona kulikuwa na vita sana...eeenh?,” Sharifu aliuliza mara baada ya kumuona Mama Kitenya akiwa na damu shingoni.



    “Kwanini umeuliza hivyo?,” Mzee Damanda akauliza.



    “Namuona Mama Kitenya ana damu shingoni,” Sharifu akajibu.



    “Oooh, hii damu ni ya Bundi.......... Tulivyokuwa njiani tulikutana na Bundi na ukiangalia nilikuwa nina kiu ya damu hivyo sikuwa na budi kumkamata na kunyonya damu yake,” Mama Kitenya alidakia mazungumzo na kujitetea kwa kudanganya.



    “Mmmh,” Sharifu alikubaliana na maelezo yaliyotolewa na Mama Kitenya japo kwa kuguna.



    Mzee Damanda baada ya mazungumzo akaanzisha mkutano, ndani ya saa moja alikuwa kashamaliza. Wakatawanyika wachawi wote kurudi majumbani. Sharifu akarudi nyumbani lakini hali aliyokutana nayo ikamshtusha na kumshangaza. Akakuta hali ya nyumbani imepoa kuanzia nje mpaka ndani. Yaani ilikuwa sio kama siku zote akashangaa zaidi kukuta jikoni kulivyokuwa rafu. Kutupa macho kwenye kona ya jikoni akamuona mkewe akiwa kalala chini na kisu kikiwa juu ya tumbo amechomwa. Akamsogelea karibu na kujaribu kumwamsha kwa kumuita jina lakini wapi mtu tayari alikuwa wajuzi. Nguvu zikamuisha na kuanza kunyong'onyea kama mtoto wa utapiamlo. Machozi yakamtiririka kwa wingi kama mama mjane aliyefiwa. Akakaa chini tuli huku akitafakari nini chanzo cha kifo cha mkewe na nani kafanya mauaji haya. Akafikiria kwa muda mrefu bila kupata majibu ya papo kwa papo. Ndipo baadaye akatuliza akili sawasawa akapata kukumbuka maneno yaliyoongelewa kilingeni.



    “Mmetoka wapi?,” Wachawi wote hawakulijibu lile swali alilouliza Sharifu wakabaki wakitazamana na kuonyesha sura ya kumficha.



    “Mmetoka wapi?...maana ninavyojua kila pahala ni kawaida kwenda wote ila leo mmeenda wenyewe. Kuna kitu mnanificha?,” Sharifu aliuliza tena kisha akasema kwa manung'uniko mara baada ya kuona wenzake wote hawajamjibu mwanzoni.



    “Hakuna tunachokuficha, hawa niliwatuma kijiji cha jirani kuchunguza wachawi wa kule wana utaratibu upi,” Mzee Damanda alijaribu kudanganya ili Sharifu asijue kilichofanyika.



    “Huko ulipowatuma naona kulikuwa na vita sana...eeenh?,” Sharifu aliuliza mara baada ya kumuona Mama Kitenya akiwa na damu shingoni.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kwanini umeuliza hivyo?,” Mzee Damanda akauliza.



    “Namuona Mama Kitenya ana damu shingoni,” Sharifu akajibu.



    “Oooh, hii damu ni ya Bundi...tulivyokuwa njiani tulikutana na Bundi na ukiangalia nilikuwa nina kiu ya damu. Hivyo sikuwa na budi kumkamata na kunyonya damu yake,” Mama Kitenya alidakia mazungumzo na kujitetea kwa kudanganya.



    “Mmmh, Sharifu alikubaliana na maelezo yaliyotolewa na Mama Kitenya japo kwa kuguna.



    “Inamaana hawa ndiyo waliyomuua mke wangu!. Ndiyo maana walijaribu kunificha nisijue” alisema Sharifu mara baada ya kukumbuka na kugundua kuwa waliomuua mkewe ni wanachama wenzake.



    Sharifu akapatwa na hasira pamoja na ghadhabu usiku ule ule. Akatoka akaenda kulipiza kisasi. Akayeyuka na kutokea chumbani kwa Fatuma. Akamkuta Fatuma yupo kitandani kalala. Akapuliza kitu mdomoni kikatoka mfano wa mawingu kikaenda kuvaa pua ya Fatuma. Baada ya kumaliza kufanya tukio akayeyuka na kurudi nyumbani. Kesho yake Sharifu akaendelea na utaratibu wa mazishi, mazishi ya mkewe akayafanya jioni na majirani kila mmoja kurejea nyumbani kwake.



    **********

    Mama Kitenya asubuhi na mapema akaamka ili aelekee shambani kama kawaida yake. Mara nyingi akiwa anakwenda shambani au mtoni lazima ampitie shosti yake Fatuma. Hivyo siku hiyo akampitia shoga yake waende wote shambani kama siku zote. Lakini alichokutana nacho akastaajabu ya Musa. Akamkuta chumbani shoga yake mara baada ya kuita kwa muda mrefu bila majibu akiwa amelala kitandani huku akitokwa damu puani. Akajaribu kupeleka mkono puani asikie kama anahema hamna chochote. Alikuwa ahemi wala mapigo ya moyo yalikuwa hayatembei. Hapo ndipo machale yakamcheza kwa kugundua kuwa alikuwa ameshaaga dunia kitambo shoga yake. Ukunga wa hali ya juu ukapigwa na Mama Kitenya kuwaita majirani wengine waje kwa wingi kwa ajili ya kufanya utaratibu wa mazishi, ni kweli majirani wakaja akiwemo na Mzee Damanda. Mzee Damanda alipofika akabeba majukumu yote ya mazishi akapanga mazishi yafanyike kesho yake. Watu wakatimka wakarudi majumbani wakisubiri hiyo kesho iwasili wakamzike Fatuma. Siku iliyofuata wote wakaenda kumzika Fatuma kasoro Sharifu tu ndo akagoma kuhudhuria mazishi ya mwana kilinge mwenzake kutokana na kinyongo alichokuwa nacho baada kuhisi hao wenzake kumuulia mke wake. Mara baada ya mazishi watu wote wakatawanyika na hatimaye kurudi majumbani mwao.





    Siku tano zikafika kwa Sharifu hakumsahau mkewe na pia wale waliosababisha kifo cha mkewe. Akajitahidi kwa udi na uvumba aweze kutimiza dhamira yake. Akaanza kumwandama mwanachama mmoja baada ya mwengine. Siku hiyo akampania sana Mama Dungo. Sharifu kwa kutimiza dhamira yake siku hiyo alikwenda nyumbani kwa Mama Dungo yapata saa nane ya mchana. Akamkuta Mama Dungo yupo nje ya nyumba yake akifua nguo. Wakasalimiana na mara baada ya salamu Sharifu akapiga jicho huku na kule ili kuangalia kama kuna mtu anapita hakuona mtu yeyote. Akafurahi mno na kujua muda wowote atatimiza dhamira kuu kama aonavyo. Kama wasemavyo siku ya kufa nyani miti yote huteleza na mchagua pema pabaya panamuita. Hapo ndipo pabaya palimuita Mama Dungo. Akiwa yupo bize na kufua asijue dhumuni na dhamira ya Sharifu ghafla akamshtukia. Sharifu akawahi na kumkaba koo Mama Dungo. Akakukuruka na kutaka kupiga kelele lakini akashindwa kutokana na Sharifu kumdhibiti madhubuti kooni. Akiwa amelishikilia koromeo la Mama Dungo kwa mkono wa kuume huku mkono wake wa kushoto akakunja ngumi kisha akafanya kupeleka mbele na kurudisha nyuma kama dereva wa trekta anapochezesha gia. Pale pale Mama Dungo koromeo lake likatoka nje na kuning'inia kama bembea. Hapo ndipo ulikuwa mwisho wake wa kuishi duniani Mama Dungo. Mama Dungo baada ya kufariki Sharifu akapotea eneo lile kwa kuyeyuka na kutokea chumbani kwa Mama Shura. Akamkosa chumbani akayeyuka tena na kutokea sebuleni. Hapo ndipo alipomkuta Mama Shura akiwa amejilaza kitini kwaajili ya kupunguza usingizi. Akapitisha macho kila kona ya nyumba ya Mama Shura kama ataona kitu chochote kinachoweza kumwangamiza. Katika kuangalia angalia akaona nyundo pembezoni mwa mlango wa Mama Shura. Akanyanyua kichawi ile nyundo na kuleta mikononi mwake kisha akashika vizuri kwa mkono wa kuume na kumpiga nayo Mama Shura kwa nguvu kichwani kama mara tatu hivi. Ghafla Mama Shura akaonekana kuvuja damu kichwani na hapo hapo hakulemba tena kuendelea kukaa pale. Upesi upesi akaweka nyundo pembezoni ya kiti kichawi kisha yeye akayeyuka na kurudi nyumbani kwake. Baada ya masaa kadhaa kupita mara baada ya mauaji kutendeka mjumbe wa nyumba kumi Mzee Bemele alikuwa anapita kila nyumba kutoa vipeperushi vya kuwahamasisha wanakijiji wake wapende kuhudhuria vikao vinavyopangwa na uongozi wa kijiji. Katika pita pita zake akiendelea kufikisha vipeperushi kwa wanakijiji wake mara ghafla akamuona kijana mmoja akimfuata mbio ikabidi asimame amsubiri kijana yule ajue ana shida gani. Kufika karibu na Mzee Bemele akaongea kwa haraka huku akihema kwa kasi ya ajabu.



    “Mjumbe, kuna mauaji yametendeka.”



    “Mauaji!!!?” aliuliza Mzee Bemele kwa mshangao.



    “Eeenh.”



    “Mauaji hayo ya nani?.”



    “Mama Shura na Mama Dungo.”



    “Wewe ulijuaje kama ni mauaji?.”



    “Vifo vyao ni vya utata na vya kutisha.”



    “Ebu...twende tukaone” alisema Mzee Bemele na haraka wakaongozana na yule kijana hadi sehemu ya matukio.



    Mzee Bemele akashangaa na kusikitika mara baada ya kupitia nyumba zote zilizofanyiwa mauaji. Haraka akaingiza mkono kwenye mfuko wake wa suruali akatoa simu akatafuta namba kisha akapiga.



    “Haloooh! Halooooh! mimi ni mjumbe kutoka kijiji cha Maharaka...natumaini hapo ni kituo kidogo cha polisi cha Doma. Ninayeongea naye ni mkuu wa kituo?,” Mzee Bemele alijitambulisha na kuuliza mara baada ya simu kupokelewa.



    “Hujakosea ndiyo mwenyewe,” Mkuu wa kituo alikubali kama ndiye.



    “Asante...sasa kijiji chetu kuna mauaji yanatendeka na hivi tunavyoongea kuna watu kama wawili wameuawa kwa mauaji ya kutisha.”



    “What!!!?.”



    “Ndiyo...naomba mje mfanye uchunguzi maana suala hili litawaogopesha sana wanakijiji.”



    “Sawa sawa, nitatuma vijana wangu waje kufanya hiyo kazi...ila naomba chonde chonde mtu yeyote asiguse hizo maiti mpaka tuje kufanya uchunguzi” alieleza mkuu wa kituo kisha Mzee Bemele akakata simu mara baada ya kupokea tahadhari kutoka kwa mkuu wa kituo.



    **********

    Ndani ya kituo kidogo cha polisi cha Doma mkuu wa kituo akaitisha kikao cha polisi wenye vyeo vidogo. Akawachagua na kuwatuma vijana wake wawili waaminifu na wenye uweledi na kazi yao. Afande Chacha na Afande Regan ndiyo wanaoaminika na ndiyo waliochaguliwa kwenda kwenye kijiji cha Maharaka kufanya upelelezi wa mauaji hayo ili kuweza kumtia mikononi mhalifu. Polisi hao wakaingia Maharaka jioni wakafika maeneo ya matukio na kuzichunguza maiti na kisha kuruhusu kesho wanakijiji waweze fanya maandalizi ya mazishi. Wakagundua kama si mauaji ya kawaida bali kikatili. Siku hiyo ikabidi wakodishe chumba cha bei nafuu ili waendelee na uchunguzi wao. Wakaingia kona baada ya kona ili kuona kama wanaweza pata fununu zozote lakini wapi. Siku ile walitoka kapa wakajirudia chumbani kwao wakiwa wamechoka hoi.



    “Afande Chacha, wewe unaonaje hizi kesi za jinai?” aliuliza Afande Regan mara baada ya ukimya wa muda mrefu.



    “Naona hizi kesi ni ngumu mno japo hatujaanza kuzifanyia utafiti wa kina,” Afande Chacha alijibu huku akipiga miyayo ya kuchoka.



    “Kweli...ila nakusihi tusikate tamaa maana nakujua wewe ukiona kesi uielewi unapotezea.”

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Kesi nyingi napotezea, lakini kwa hizi siwezi nitapambana mpaka mwisho niweze kufanikisha kilichotuleta.”



    “Sawa kabisa...basi tulale kesho tutajua tuanzie wapi upepelezi wetu.”



    Kwa kuwa usiku ulishaingia Afande Chacha na Afande Regan wakalala. Asubuhi na mapema wakaamka wakajiandaa kisha wakavaa kiraia wakatoka kwenda kufungua kinywa mgahawani. Wakafika mgahawani wakaagiza chai na chapati wakanywa. Wakiwa wanakunywa chai wakamsikia mama yule muuza mgahawa na mteja mmoja wakizungumza habari ya Sharifu.



    “Bi Zuena, ujue yule mtoto mchawi sana,” Mteja yule alimwambia mama yule wa mgahawani.



    “Nani...Sharifu?,” Mama yule wa mgahawani aliuliza huku akipepesa macho kila njia asije kusikiwa na Sharifu mwenyewe.



    “Eeenh, huyo huyo.”



    “Wewe ndiyo unajua leo, wakati si tumejua kitambo...hata na mama yake alikuwa mchawi.”



    “Kumbee!!!.”



    “Eeenh...tena licha ya uchawi yaani wanaua watu balaa kitu kidogo tu wanakuua” alisema Mama yule wa mgahawani kisha akajifanya kukohoa huku akitupia macho kila kona kumwangalia Sharifu anakuja mwisho umbea ukajamponza. Alipoona dalili ya Sharifu kuja haipo akaendelea kuongea.



    “Lakini iwe siri yako usije ukaropoka huko mtaani ukaniponza mimi.” Kabla ajaongea Mteja yule Afande Chacha akadakia yale mazungumzo kwa kuuliza.



    “Hivi huyo Sharifu mnayemzungumzia anaishi kijiji hiki?.”



    “Eeenh na nyumba yake si mbali na hapa umeona ile inayotuangalia,” Mama yule alisema huku akimuonyesha Afande Chacha kwa kidole nyumba ya Sharifu.



    “Oooh! nyumba yake nzuri inaonekana ana utajiri mkubwa?,” Afande Chacha akazidi kupeleleza.



    “Ni nzuri, ila nasikia amepata kwa njia ya ushirikina” aliropoka Mama yule wa mgahawa asijue anayeongea naye ni polisi.



    “Mmmh, kumbeee!!!,” Afande Chacha aliongea huku akitingisha kichwa kwa kukipeleka juu na chini. Kisha akaendelea kuongea kwa kuuliza.



    “Nimesikia hapa mkisema anaua watu balaa ni kweli?.”



    Mama yule wa mgahawa alipoulizwa swali lile akachungulia kila pahala na akaangalia nyumba ya Sharifu iliyo mbele yake hakumuona Sharifu ndipo akalijibu lile swali.



    “Eeenh, anauwa balaa...nahisi hata mama waliokufa jana amehusika yeye.”



    “Kwa sasa huyo Sharifu yupo?,” Afande Chacha akauliza.



    “Kwa sasa nahisi yupo dukani kwake.”



    “Kumbe ana duka!!!?.”



    “Tena sio moja anayo maduka mawili.”



    “Oooh maduka yake yapo wapi?.”



    “Moja lipo hapa kijijini Maharaka na lingine lipo kijiji cha pili kinachoitwa Kipunguri.”



    “Oooh! Sasa yeye anauza duka lipi hapo?.”



    “Anauza duka lililopo hapa Maharaka.”



    “Oooh, huyu bwana tajiri sana,” Afande Chacha aliongea kwa kumsifia Sharifu na huku akificha makucha yake asitambulike kama ni polisi na mama yule wa mgahawani pamoja na yule mteja.



    Baada ya muda kadhaa Afande Chacha na Afande Regan wakamaliza kula wakalipa pesa kisha wakaondoka. Wakiwa wamepata mwongozo wa kuanza utafiti wao wakaanza kumpeleleza Sharifu hatua moja hadi nyengine. Siku iliyofuata kama kawaida wakavaa kiraia wakaingia mtaani kuulizia duka la Sharifu. Wakiwa katika harakati za kufuatilia njiani wakakutana na kijana mmoja mtanashati aitwaye Kondo wakamsimamisha na kumuuliza.



    “Hallo kijana habari yako,” Afande Regan alimchangamkia yule kijana.



    “Salama,” Kondo aliitikia ile salamu huku akijaribu naye kuwatathimini kwa kuwakazia macho kila idara.



    “Wewe ni mwenyeji wa hapa?,” Afande Regan alizidi kumchangamkia Kondo.



    “Ndiyo...niwasaidie nini?” alijibu na kuuliza Kondo.



    “Eti unajua duka la Sharifu lilipo?.”



    “Hapana sijui........ Kwani nani kawaambia kuna mtu kijijini kwetu anaitwa Sharifu?,” Kondo akauliza.



    “Kuna mama mmoja wa makamo ndiye aliyetuambia...na labda nikutoe hofu sisi tunamtafuta kwa nia njema kabisa.”



    “Sharifu ni nani yenu?.”



    “Ni wajomba zake,” Afande Regan akadanganya.



    “Kwake mnapajua?.”



    “Kwake tunapajua ila tumemkosa.”



    “Aaah nami napajua kwake tu huko dukani sipajui” alizidi kudanganya Kondo.



    “Basi sawa...Samahani kwa usumbufu,” Afande Chacha alimalizia hivyo kisha wakaagana na Afande Regan wakaondoka.



    Kondo mara baada ya kumaliza mazungumzo na wale polisi akatimua mbio moja kwa moja dukani kwa Sharifu kupeleka umbea. Akampasha umbea Sharifu kisha akaendelea na safari yake. Sharifu sasa akakaa kwa makini kila pahala aendapo akijua kuna watu wanaomtafuta na si kwa lengo zuri ni kwa lengo baya.



    **********

    Siku zikayoyoma kwa Sharifu na kisasi chake kipo pale pale. Hakuogopa hao wamekusanyika tafuta hata kama watu walimpasha habari juu ya ujio wa hao polisi. Siku moja usiku mnene akiwa nyumbani akapanga aende kuendeleza kisasi kwa Mama Kitenya. Akajiandaa na kuyayuka akatokea nyumbani kwa Mama Kitenya chumbani. Akamkuta Mama Kitenya kalala usingizi wa Kobe. Usingizi ambao ulikuwa ni ule wa kuibia ibia, ile anaingia chumbani tu Mama Kitenya akakurupuka usingizini na kuvaana na Sharifu. Wakaburutana wakiwa kwenye umbile la kibinadamu. Walipochoka wakaachiana kwa muda wakawa wanatazamana kwa usongo na kila mmoja kumpania mwenzie. Baada ya mapumziko ya muda Mama Kitenya akaona akiwa katika umbo la kibinadamu hamwezi Sharifu. Hivyo akabadilika kuwa Mbwa mwitu kisha akamrukia Sharifu shingoni akamrarua kwa makucha Sharifu katika purukushani zile akaona anaelemewa. Akayeyuka na kumwacha pale chumbani Mama Kitenya mwenyewe. Sekunde kadhaa zikapita akarudi tena akiwa kwenye umbile la Jaguar na kumuweza Mama Kitenya. Mama Kitenya alipokea mikong'oto babu kubwa akaomba msamaha lakini kwa kosa walilolifanya kwa Sharifu hakutaka maridhiano wala msamaha wa aina yoyote kutoka kwa Mama Kitenya. Akaendelea kumpa mkong'oto hadi umauti ulipomchukua. Baada ya mauaji kufanyika Sharifu akarudi katika umbile lake kisha akapotea na kwenda nyumbani kujipumzisha.



    **********

    Yapata saa kumi na moja alfajiri simu ya Afande Chacha inaita kwa sauti ya juu. Afande Chacha akasikia simu yake inaita akaamka na kuipokea.



    “Afande, kuna mauaji mengine yamefanyika huku” ilisikika sauti ya mjumbe upande wa pili ikiongea mara baada ya kupokelewa simu.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    “Sehemu gani yamefanyika?,” Afande Chacha akahoji.



    “Ni jirani na nyumbani kwangu,” Mjumbe akajibu.



    “Okay nakuja sasa hivi” alitoa ahadi Afande Chacha kwa mjumbe. Kisha akakata simu na kumwamsha mwenzie waondoke.



    Wakafika sehemu ya tukio wakiwa wamevaa kiraia wakachunguza ile maiti na kugundua kuwa maiti zote zile za mwanzo na sasa muuaji ni mmoja. Hawakuwa na uthibitisho dhahiri kuwa anayeuwa ni Sharifu au laah. Baada ya uchunguzi wakatoa ruhusa ya mazishi iendelee na wao waendelee na uchunguzi stahiki. Kutokana na ugumu wa kesi hii wakalazimika usiku wasilale. Walikuwa mitaani tu wakiendelea na uchunguzi wao kisiri japo Sharifu alijua ujio wao. Siku inayofuata wakiwa wapo katika uchunguzi tena nyumbani kwa Sharifu wakasikia upepo mkali uliokuwa unapenya hadi kwenye viungo vya mwili. Wakaamua kujibanza kwenye kichaka kimoja kilichopo maeneo yale yale ya nyumbani kwa Sharifu wakijikinga na ule upepo. Wakiwa kwenye kile kichaka wakajishuhudia kwa macho yao kumuona Sharifu akijibadilisha katika umbile lake la kibinadamu na kugeuka umbile la Tembo. Wakataharuki na kuacha vinywa wazi kwa kuduwaa wasiamini wakionacho mbele yao. Tembo lile likakamata barabara ya vumbi na kuelekea hadi kwa Mzee Damanda. Afande Chacha na Afande Regan kwa kuwa walikuwa kazini hawakupaswa kujenga uwoga miyoni mwao. Wakajijengea ukakamavu na ujasiri ndani ya roho kisha wakamfuatilia Tembo yule hadi mwisho alipoishia. Wakaamua kujificha ili waweze shuhudia Sharifu atafanya nini akiwa kwenye umbile lile.Tembo yule akaishia nyumbani kwa Mzee Damanda akazunguka nyumba ile kama mara kumi kisha akaanza kubomoa nyumba ya Mzee Damanda kwa kutumia meno yake mawili yaliyochongoka kama sururu. Mzee Damanda akiwa yupo ndani amelala akasikia vishindo vya miguu ya Tembo na kishindo cha nyumba kuanguka haraka. Akakurupuka ndani kabla mjengo haujaanguka kumletea maafa. Akatoka nje na kumuona Tembo akiendelea kufanya uharibifu katika nyumba yake. Nyumba Ikabomolewa yote kisha huyo Tembo akamrudia mwenyewe Mzee Damanda ili kutaka kutimiza dhamira yake. Kabla hajafikiwa Mzee Damanda akanyoosha mkono wake wa kuume kwa yule Tembo kukatokea mwanga mkali kwenye uso wake. Katikati ya mwanga ule ikaonekana sura ya Sharifu. Mzee Damanda akaangua kicheko kwa dharau kisha naye haraka akajigeuza Nyati kabla Sharifu hajamdhuru. Mzee Damanda alipojibadili tu Afande Chacha na mwenzie wakaonesha kuwa na uwoga tena. Wakaogopa mno nusura wapige yowe lakini wakajipa tena roho ya ujasiri na kuzidi kushuhudia mchezo wote unaoendelea bila ya chenga huku wakiongea kwa kunong'ona wasisikiwe na wachawi wale.



    “Kijiji hiki kina wachawi sijapata ona,” Afande Chacha akanong'ona.



    “Aisee, yaani katika kazi niliyopeleleza na kunipa hofu hii namba moja,” Afande Regan alitoa ushirikiano wa kuongezea kuongea kwa kunong'ona.



    Wakazidi kunong'ona huku wakiendelea kuangalia mpambano kisiri sana. Dakika zilikwenda na masaa yakaenda lakini ngoma ikawa droo droo hakupatikana mshindi. Ngoma ikaungurumishwa hadi mishale ya saa tisa na nusu usiku Tembo na Nyati wakawa hoi bin taaban. Mishale ya saa kumi kasoro usiku Nyati akachoka mno ndipo Mzee Damanda akarudi kwenye umbile la kibinadamu akiwa yupo chini na kachafuka siyo mfano. Sharifu naye akaona asimchezee rafu kiongozi wake akapata fair play ya bure ikabidi naye arudi kwenye hali yake ya ubinadamu. Katika hali hiyo ya ubinadamu akamsogelea kiongozi wake ili ammalize. Akafika karibu na Mzee Damanda akamnyanyua kiongozi wake kisha akamtupilia huko kichakani jirani na mapolisi. Afande Regan uwoga ukazidi alipoona Mzee Damanda katupwa jirani walipo wao. Akatimua mbio kujaribu kunusuru maisha yake lakini ilikuwa kazi bure hakufika mbali. Sharifu akamtokea kwa mbele kabla ajaenda kumtangazia mbovu huku amemkunjia ngumi. Akafanya kama anampiga kisha akarudisha lile konde nyuma papo hapo Afande Regan akatapatapa na roho hatimaye akaaga dunia. Afande Chacha akashuhudia mwenzake akiuawa. Roho ikamuuma na majonzi yakamtawala lakini atafanyaje wakati mtuhumiwa wake anatumia nguvu za giza ukienda kichwa kichwa unaumia. Ikabidi awe mpole na kutumia akili nyingi kwaajili ya kumdhibiti mtuhumiwa. Sharifu akaendelea kumtafuta Mzee Damanda aliyemkimbia wakati akifanya mauaji ya Afande Regan. Akamkosa lakini hakuweza kukata tamaa. Akazidi kumtafuta kwa hali na mali lakini ikashindikana ndipo wazo likamjia kichwani mwake akanena baadhi ya maneno.



    “Dukila chamkwanda buchula,” Sharifu baada ya kunena maneno yale likatokea vumbi zito na likaenea maeneo yote ya pale.



    Baada ya vumbi kusambaa Mzee Damanda akasikika kwenye kichaka kimoja wapo akikohoa kwa tabu. Kukohoa kwa Mzee Damanda kukamfanya Sharifu aweze kusikia. Akajaribu kutega sikio vyema ili aweze kusikia sauti inatokea wapi. Ndipo alipogundua kuwa sauti ya Mzee Damanda inatokea kwenye kichaka kimoja wapo kilicho jirani na nyumba yake. Akapotea ghafla na kutokea kwenye kichaka alichokuwepo Mzee Damanda. Akamkuta kiongozi wake akitetemeka kwa hofu kisha akamnyanyua kwa nguvu pale alipochuchumaa na akapepesa macho pande zote juu, chini na pembeni. Alipotazama juu akaliona tawi nene la mti wa mpingo likining'inia kichwani kwa Mzee Damanda. Sharifu akaangalia anga kwa muda punde machoni mwake kukatoka miale ya bluu. Miale ile ikaambatana na mawingu. Hayo mawingu yakaleta bonge la radi hadi ikapelekea tawi lile la mpingo kumdondokea Mzee Damanda kichwani. Mzee Damanda akafariki pale pale huku Afande Chacha akishuhudia mauaji yale. Baada ya mauaji yale kuyafanya Sharifu akaondoka na kutokomea eneo lile.



    **********

    Simu inapigwa kituo kidogo cha polisi cha Doma na anayepiga si mwingine bali ni Afande Chacha. Simu aliyoipigia ikaita kwa muda mrefu na mwisho kukata. Hata hivyo hakukata tamaa akajaribu tena kupiga kwa mara ya pili. Kwa mara nyingine simu ikaita kwa sekunde kadhaa kisha ikapokelewa.



    “Halooh!” ilisikika sauti ya mkuu wa kituo upande wa pili ikiongea kwa ustadi.



    “Eeenh mkuu,” Afande Chacha akaongea.



    “Mmefikia wapi hadi sasa?,” Mkuu wa kituo aliuliza huku akionyesha dalili ya kutojua kitu kilichotokea.





    “Japo tumefikia hatua nzuri...nasikitika kuwaambia kuwa Afande Regan hatunaye.”



    “Nini?.”



    “Afande Regan amefariki.”



    “Amefariki lini? na aliyemuua ni nani?,” Mkuu wa kituo akadodosa.



    “Amefariki leo muda huu na aliyefanya mauaji ni mtuhumiwa yule yule aliyefanya mauaji ya mwanzo.”



    “Mtuhumiwa mwenyewe ushalipata jina lake?.”



    “Ndiyo.”



    “Anaitwa nani?.”



    “Anaitwa, Sharifu.”



    “Sawa, fanya juu chini umkamate huyo mtuhumiwa...mimi kukipambazuka nitachukua polisi wawili nitakuja kufuata mwili wa Afande Regan” alielekeza mkuu wa kituo kisha akakata simu.



    Baada ya kumaliza kuongea na simu Afande Chacha akasogelea maiti ya Mzee Damanda kisha akapiga simu kwa mjumbe kumpa taarifa za mauaji yaliyotoka kutendeka muda si mrefu. Mjumbe baada ya kupata taarifa hakuchelewa kuja. Alikuja akathibitisha kisha kulipopambazuka akaita ndugu na majirani waweze kufanya utaratibu wa mazishi jioni.



    **********http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Mkuu wa kituo akawasili katika kijiji cha Maharaka asubuhi na mapema kuchukua mwili wa mwenzao. Wakachukua na wakaondoka kwenda kuendelea na mazishi huku nyuma wakamwacha Afande Chacha akiendelea kufuatilia kesi yake. Baada ya mwili wa Afande Regan kuchukuliwa Afande Chacha akazidi kuendelea na kesi yake ya uchunguzi kisiri siri ili mtuhumiwa asishtukie kama kuna mtu mwengine anampeleleza. Akapita kila eneo ambalo Sharifu hupita ili kuzidi kumtafutia njia mbadala ya kumweka nguvuni. Akaweka kila mbinu lakini ikawa ngumu kumnasa Sharifu. Siku moja baada ya kutumia kila njia na kila mbinu kumkamata Sharifu na ikashindikana ndipo hapo akakaa chini akatafakari ni jinsi gani ya kumdhibiti mtuhumiwa akiwa ndani. Katika kutatafakari hayo ghafla usingizi moja kwa moja ukamchukua kisha ndoto ikampeleka mbali na ikampatia majibu. Hayo yote yalikuwa ni majibu ya kukabiliana na nguvu za giza. Afande Chacha akaota yupo juu ya maji ya mto huku akiwa amezungukwa na wachawi wa rika mbalimbali. Ghafla akiwa amezungukwa, akamuona juu angani Bundi akipita. Baadaye akanya kinyesi chake kikamdondokea mchawi mmoja. Mchawi yule alivyodondokewa na kinyesi cha Bundi wote wakamong'onyoka na kupukutika kama udongo. Na hapo ndoto ikakata na Afande Chacha akaamka akakaa kitako kitandani akatafakari ndoto.



    “Hii ndoto, ina maana gani kwangu?.”



    “Inamaana nimeonyeshwa dawa ya kumdhibiti Sharifu.”



    “Lakini kama kweli ni dawa...... sitofanikiwa kumkamata Sharifu akiwa hai na kumsweka rumande.”



    “Kwa maana inampukutisha na kuwa mavumbi...sasa nitafanyaje?.”



    “Ndiyo...sitojali kama litakalo kuwa na liwe,” Afande Chacha alichekecha kichwa kwaajili ya kuwaza na kuwazua alipopapata suluhu akakamata simu yake kisha akapiga simu kituoni kwa mkuu wa kituo.



    “Mkuu, mtuhumiwa huyu ngumu kumkamata,” Afande Chacha alisema mara baada ya mkuu wa kituo kupokea simu.



    “Kwa nini!!!?,” Mkuu wa kituo aliuliza kwa mshangao kwa kutotegemea kijana wake kushindwa kesi ile.



    “Anatumia nguvu za giza.”



    “Eti...nini?.”



    “Anatumia uchawi.”



    “Sasa wewe, kama wewe umechukua uamuzi gani?.”



    “Uamuzi wangu ni kuua tu, kuliko kumkamata nikafa mimi.”



    “Basi fanya unavyojua, kwa kuwa kesi umeishikilia wewe ya huyo mtuhumiwa.”



    Basi baada ya kupewa oda Afande Chacha akakata simu na kujua nini cha kufanya juu ya kiumbe hatari Sharifu. Akaendelea kukong'ota usingizi hadi mishale ya saa nne na robo ya asubuhi ndipo akashuka kitandani. Akajiandaa kuelekea kwa mwenyeji wake Mzee Bemele ambaye ni mjumbe wa kijiji cha Maharaka.



    “Mzee kinyesi cha Bundi hivi naweza kukipata wapi?,” Afande Chacha alimuuliza mwenyeji wake mara baada ya kufika nyumbani kwa mjumbe.



    “Cha nini kijana?...maana kupata ni adimu,” Mzee Bemele alimchangamkia mgeni wake kwa swali na kuongea kwa ucheshi.



    “Nina kazi nacho muhimu sana.”



    “Oooh, sasa kile kinyesi kinapatikana kwenye milima ile ya Mlazamrungu na kinapatikana usiku... Ukienda asubuhi, jioni au mchana hukipati hadi usiku muda wakurejea Bundi kwenye viota vyao,” Mzee Bemele alimweleza Afande Chacha kwa uwelevu zaidi huku akimuonyesha milima yenyewe kwa kidole.



    “Mmmh!!!, usiku unaweza kunipeleka?,” Afande Chacha aliuliza huku akijaribu kuangalia ile milima.



    “Ondoa shaka, nitakupeleka ila unipitie.”



    “Sawa mzee,” Afande Chacha walikubaliana na Mzee Bemele kisha akaondoka kwenda kupata chakula mgahawani.



    Huku nyuma akamuacha Mzee Bemele akikaza kitanda chake kamba. Afande Chacha alikunywa chai na maandazi mara baada ya kufika mgahawani. Alikunywa kisha akalipa pesa na kuondoka kurudi kwenye chumba alichopanga. Alipofika chumbani akalala huku akisubiri muda wa kwenda milima ya Mlazamrungu kuchukukua kinyesi. Muda wa kwenda milimani ulipowasili Afande Chacha akaamka kisha akatoka ndani akafunga mlango kwenda kwa Mzee Bemele kumpitia amsindikize. Akamkuta Mzee Bemele yupo nje akimsubiri. Wakachukuana na kuongozana milimani. Wakafika na kuchukua wanachokihitaji kisha wakarudi kijijini. Wakaachana na Mzee Bemele njiani huku Mzee Bemele akienda nyumbani kwake. Afande Chacha alikwenda kwenye chumba chake kupumzika kwaajili ya kesho kujiandaa na mashambulizi kabambe mara baada ya kupata dawa aliyoonyeshwa kwenye maono. Kulipokucha tu Afande Chacha hakuwa na muda wa kupoteza tena akavaa ujasiri kuchukua pistol JF 2 na kuichomeka kiunoni. Akachukua pia kinyesi cha Bundi na kutia kwenye maliboro nyeusi kisha akaanza safari ya kwenda kwa mtuhumiwa wake kuanzisha pambano baada ya kukamilika kila idara.



    “Upo chini ya ulinzi!. Usikukuruke wala usiyumbe yumbe,” Afande Chacha alimweka chini ya ulinzi Sharifu mara baada ya kutia timu kwenye ngome yake.



    Sharifu aliposikia na kuona silaha akatii amri. Akapiga magoti na kunyoosha mikono juu kana kwamba amesalenda. Afande Chacha alipoona mtuhumiwa kasalenda mwenyewe akataka asogee ampige pingu aende naye kituoni. Lakini haaaah wapi!. Sharifu si mjinga hivyo kama unavyodhani. Kabla hajasogea Afande Chacha, Sharifu akainua macho juu na hapo akampiga kombora la haja Afande Chacha. Afande Chacha silaha ikadondoka kule akawa yupo chini akiugulia maumivu. Hajakaa sawia akataka aongezwe kombora lingine. Wee!. Afande Chacha hakukubali. Alipoona kombora linakuja akatoa kinyesi cha Bundi akarusha kwa Sharifu ikawa ngoma droo. Katika kukuru kakara wakati Afande Chacha anajipanga ghafla kombora likampata likamuumiza na akaaga dunia papo hapo. Sharifu naye kinyesi cha Bundi kilimpata kwa wingi pale pale nae akaungua na kuanza kupukutika kama udongo wa kichanga akatoweka duniani. Mwili wa Afande Chacha ulikuja kuchukuliwa na wenzie ukazikwe baada ya taarifa ya kufariki kwa Afande Chacha kufika katika kituo kidogo cha polisi cha Doma. Taarifa za polisi kuwawa zikamfikia mkuu wa wilaya ya Mvomero Mh. Gidion Julius Mongi, akawasili kituo cha polisi cha Doma akatoa rambi rambi kwa polisi waliofariki kisha akaelekea kijiji cha Maharaka. Akakutana na uongozi wa serikali ya kijiji akaitisha mkutano wa wanakijiji wote, wanakijiji wote wakakusanyika akatoa rambi rambi napo kwa vifo vilivyotokea katika kijiji cha Maharaka. Serikali ya kijiji ikapokea rambi rambi na wanakijiji wote wakatulia tuli wamsikilize mkuu wa wilaya wao.



    “Wanakijiji...safiii,” Mkuu wa wilaya alipaza sauti mara baada ya kuona wanakijiji wamekusanyika kwa wingi.



    “Safiii,” Wanakijiji wote wakaitika kwa huzuni kidogo.



    “Poleni sana, kwa misiba iliyotokea.”



    “Tushapoaaa,” Wanakijiji wote wakaitika tena kwa kupaza sauti.



    “Wengi wenu, naamini ujio huu amkutegemea...ujio huu umewasili kwenu kwa lengo moja tu kutokomeza uchawi,” Mkuu wa wilaya aliendelea kusema.



    “Wengi tunaamini kijiji chetu kipo shwari......uchawi hamna tena baada ya kufa wachawi katika kijiji chetu. Basi ningependa kijiji chetu kiendelee hivi hivi kwasababu uchawi hauna maana, kisasi akina maana. Sasa ya nini tuendelee kung'ang'ania vitu visivyo na faida yatupasa tubadilike sasa tuwe kitu kimoja tushirikiane pamoja pia tupendane. Tukitekeleza hayo naamini kijiji chetu kitakuwa tulivu na amani.....tumeelewana?.”



    “Ndiyo, Mheshimiwaaa” walipaza sauti wanakijiji wote kwa kumuitika Mkuu wa wilaya wao.



    Baada ya kuhitimisha kikao na kuondoka Mkuu wa wilaya. Wanakijiji wote wa Maharaka tokea siku hiyo wakaishi kwa upendo na amani hakukuwa tena na uchawi wala visasi, wakapendana na kushirikiana kwa kila jambo.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    **********

    Majanga tunamwachia Mwenyezi Mungu naamini atatupigania hapa duniani. Kumbuka kipindi chote mchawi hana rafiki. Mchawi ni nani?, mchawi ni mnafiki, mchawi ni mgombanishi, mchawi ni yule mkosaji. Mchawi si mtu mzuri katika jamii. Sababu mchawi ataroga mchana kweupe pee hata haya aoni. Yaani hana huruma hata kidogo kwa jamii, huyo ni mtu gani asiye na huruma. Inamaana ajui kama kuna Mungu? na kama ajui mbona akiwanga anamtanguliza Mungu?. Naona ni unafiki umemjaa. Yaani unaroga halafu unampenda Mungu uoni kama ni kosa, lakini sikatai fanya yote ila kaa ukijua ipo siku zamu yako yaja, si unajua kutesa kwa zamu. Adhabu ya kaburi aijuae maiti na mkataa pema pabaya panamuita. Wachawi wote sasa pabaya patawaita, kwa kuwa sisi wanyonge kwenu basi tunasema Insha Allah! sisi tunamwachia Mungu awadhibiti nyie wachawi.



    _____MWISHO_____

MAMA USINIFUNDISHE UCHAWI - 4

 






Simulizi : Mama Usinifundishe Uchawi

Sehemu Ya Nne (4)





Binti Mngane alipohakikisha mwanae amemaliza kufagia banda la kuku alikwenda ndani kukaa kwenye mkeka ukumbini. Sharifu alipomwaga taka akajongea hadi chumbani na alipofika kitandani akajitupa kifudifudi masaa mawili mbele. Sharifu akakamatwa na usingizi mzito, akiwa amesinzia akaingia Mzee Damanda chumbani kwake kimiujiza na kuanza kuzungumza naye kupitia ndoto.



“Kibaraka wangu,” Mzee Damanda akaita.



“Naam” aliitika Sharifu ndotoni.



“Nimekuja, kuna jambo limenileta.”



“Jambo gani?.”



“Umepita mwezi sijawaona kilingeni kulikoni?.”



“Kulikuwa kuna mambo kidogo tunaweka sawa.”



“Unakumbuka katiba yetu?.”



“Nakumbuka.”



“Zipi?.”



“Usimjaribu mwanachama mwenzio. Usitangaze siri za chama na kuhudhuria kilingeni kila siku.”



“Safi...mbona nyinyi mnakiuka katiba?.”



“Tunapitiwa kiongozi wetu...lakini kuanzia leo nakuahidi hatutokosa kilingeni.”



“Sawa...naondoka ila mkae mkijua nisipowaona siku zijazo nitajua cha kufanya.”



“Nimekuelewa kiongozi, kuanzia leo tutakuwa kilingeni pamoja wala hatutokuangusha tena.”



Mzee Damanda alipoondoka, Sharifu akakurupuka ndotoni. Akanyanyuka kitandani akaelekea moja kwa moja alipo mama yake. Akamkuta mama yake ukumbini ameketi kwenye mkeka na hawamu hii akiwa anamenya ndizi.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Mama,” Sharifu akaita.



“Eeehe niambie...naona umeshaamka,” Binti Mngane aliongea huku macho yake yakitazama chini akichukua ndizi nyingine.



“Nimeamka...lakini nimeamka na habari mbaya” aliongea Sharifu kisha akasimama mbele ya mama yake sawa sawia.



“Kutoka, wapi?” aliuliza Binti Mngane kwa kutahamaki.



“Kwa, Mzee Damanda.”



“Anashida gani tena?.”



“Kaja kutupa onyo kwa sababu hatuhudhurii kwenye kilinge.”



“Mh! ni kweli...sasa wewe ulimwambiaje?.”



“Sikumwambia chochote, zaidi ya kukiri kosa na kuomba msamaha.”



“Nakuasa mwanangu tujirekebishe bila hivyo mwaka huu tutaumbuka.”



Sharifu baada ya kuzungumza na mama yake akamuaga mama yake kuwa anakwenda nyumbani kwa kina Kondo kupiga stori kidogo. Mama yake akamruhusu aende lakini wakati anaanza safari njiani akakutana na bibi kikongwe asiyeweza kutembea kutokana na kuvimba miguu.



“Mjukuu wangu” aliita Kikongwe yule mara baada ya kumuona na kupishana naye Sharifu.



“Naam” aliitika Sharifu kwa busara.



“Naomba msaada.”



“Msaada upi?.”



“Wa kunipeleka nyumbani.”



“Sitoweza bibi kuna mahali nawahi.”



“Naomba unipeleke nitakupa zawadi tukifika nyumbani kwangu,” Kikongwe yule alimrubuni Sharifu kwa zawadi.



“Zawadi ipi?.”



“Wewe nipeleke zawadi hiyo utaiona tukifika,” Sharifu akakubali kumpeleka Kikongwe yule kwake kwa kumbeba mgongoni kwa sababu ya kutoweza kutembea vizuri.



Wakiwa wapo njiani Sharifu akahisi maumivu makali mgongoni. Akapeleka nyuma mkono wake wa kuume kulipo na maumivu ili apate kuthibitisha kama kweli ana jeraha au laa. Ghafla yule bibi akabadilika kuwa Chui mwenye miguu minne na kumrarua Sharifu mkono alioupeleka nyuma kupapasa. Sharifu akamtupa pembeni kikongwe yule kwa hasira. Baada ya kutupwa kikongwe yule akawa anacheka kwa sauti ya juu huku sauti yake ikisikika kufika masafa ya mbali.



“Msaada ninaotaka kukupa unaona haufai?. Unaamua kunidhuru?,” Sharifu aliongea kwa ghadhabu.



“Lengo langu si msaada kutoka kwako lengo langu ni kukuua,” Kikongwe yule alisema kwa ujasiri uliotukuka. Sharifu akacheka kisha akasema naye kwa ujasiri bila hofu.



“Unajiamini sana...ngoja nami uone nipoje.”



Sharifu muda huo huo naye akabadilika kuwa Simba mwenye pembe ndefu na meno makali mithili ya sindano. Alipojibadilisha vile tu moja kwa moja akamvamia kikongwe yule aliyejibadili Chui na kupeana mikong'oto ya haja. Mikong'oto ikatembezwa yapata masaa mawili kisha kila mmoja akawa pumzi kisoda. Sharifu hakukubali kushindwa japo alichoka lakini akamkabili vyema kikongwe yule na hatimaye kikongwe yule akashindwa akatafuta upenyo akakimbia. Sharifu akacheka sana na akaongea kwa dharau.



“Ulijua nipo kijingajinga, nina nguvu balaa. Nenda kajipange na nguvu zako za mtoto mchanga.”



Sharifu akahairisha hadi safari yenyewe kutokana na kuchafuka mara baada ya kurudi kwenye hali ya ubinadamu akarudi nyumbani. Akafika nyumbani akakuta kumetulia na hadi mama yake hakuwepo. Hakuwa na shaka sana, hivyo akaingia chumbani huku moyoni akijiuliza baadhi ya maswali.



“Kikongwe yule katokea kijiji gani?...na lengo la kuniua ni nini?.”



“Mama anaweza kumjua kweli?...looh! simjui hata jina kikongwe yule.”

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Nitamweleza mama kwa maumbile, kama atamjua anitajie jina lake nimjue.”



Sharifu akiwa yupo kitandani bado akiwa anajisemesha mara usingizi ukamjia na akawa anakoroma bila kujijua. Masaa kadhaa mbele alikuja kushtuka mara baada ya kusikia mlango wake wa chumbani ukigongwa. Akakurupuka kutoka kitandani na kwenda kumfungulia anayegonga.



“Mama ulikuwa wapi?,” Sharifu aliuliza mara baada ya kuona kuwa aliyekuwa anagonga ni mama yake.



“Nilikuwa mtaa wa pili nikiazima pipa la kupikia pombe...si unajua kesho pombe kwangu?,” Binti Mngane akajibu na kuuliza.



“Umelipata pipa lenyewe?.”



“Nimelipata...ila ni chafu kanisaidie kuliosha.”



“Kuna kazi kwa sasa unataka kufanya?.”



“Nataka nifue nguo mara moja maana zimekuwa chafu sana.”



“Sawa...mimi ngoja nikasafishe pipa hilo,” Sharifu baada ya kupeana majukumu na mama yake, kila mmoja akaingia katika kazi yake.



Baada ya saa moja wote wakawa wamemaliza kazi wakaenda kuketi ukumbini kwa pamoja wapige soga. Sharifu akaanzisha mazungumzo mara baada ya ukimya wa mama yake wa muda mrefu.



“Mama, hivi hapa kijijini kwetu kuna bibi vikongwe wangapi?.”



“Wawili,” Binti Mngane alijibu huku akitabasamu.



“Nani na nani?.”



“Bi Kazimoto na Bi Tuni...kuna nini kwani?.”



“Leo njiani, nimekutana na bibi kikongwe akanidhuru.”



“Yupoje, kikongwe huyo?.”



“Miguu yake, imevimba na mfupi.”



“Oooh!, huyo atakuwa Bi Kazimoto.”



“Unamjua?.”



“Eeenh!.”



“Anaishi wapi?.”



“Ni jirani yetu, anaishi nyumba tatu za mbele zinazofuata...alitaka kukudhuru kisa nini?.”



“Sijajua...sio kunidhuru tu, alitaka aniue kabisa.”



“Toba!!!, majirani wananitafuta nini?...ujaumia sana?.”



“Sijaumia sana ameniweka kajeraha kidogo tu...lakini nina hasira naye.”



“Unatakaje?.”



“Kama unapajua kwake, baadaye unipeleke nikamalize hasira zangu.”



“Usijali, baadaye tukitoka kilingeni nitakupeleka,” Binti Mngane alipiga soga na mwanae hadi nyakati za kupika chakula zikafika.



Akanyanyuka kwenye mkeka pale ukumbini na kuelekea jikoni kupika chakula cha usiku. Sharifu hakutaka kuendelea tena kukaa pale ukumbini. Akaamua kuchukua mkeka na kwenda kujilaza nje kwaajili ya kupunga upepo wa jioni.



**********

Nyumbani kwa Bi Kazimoto furaha haikuwepo. Alikuwa anawaza na kuwazua kwa jinsi alivyokosa ushindi.



“Mtoto yule anatumia uchawi wa aina gani?...atakuwa anatumia uchawi wa kale nini?.”



“Yaani kitoto kile kinishinde mimi............?. Sikubali nitajipanga tena.”



Bi Kazimoto kwa siku ile ilikuwa ya huzuni kwake na mbaya zaidi kila akifikiria tukio lile. Akahisi homa, yaani hakutamani hata chakula cha aina yoyote kipite kinywani mwake. Yaani siku ile chakula hakikuwa kitamu upande wake hivyo akalala bila kula kitu chochote siku hiyo.



**********

Binti Mngane alipoivisha chakula na kula yeye na mwanae wakaingia kila mmoja kwenye chumba chake kwa ajili ya kwenda kujipumzisha mwili. Binti Mngane akiwa usingizini akazama moja kwa moja kwenye ndoto, ndoto ikampeleka ajione yupo na mumewe wanazungumza.



“Mwanamke mbaya sana, yaani umeniua kwa kunitoa kafara kwasababu ya kunufaisha uchawi wako,” Baba Sharifu alinung'unika kwa kumnung'unikia mkewe kwa kumwaisha kaburini.



“Si kusudi langu, ni kusudi la mizimu kunilazimisha kutoa kafara kinguvu,” Binti Mngane alijitetea ili asionekane mbaya na mumewe.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Mbona hujamweleza mtoto uchafu uliofanya...halafu unajitetea leo. Lazima nikuue,” Baba Sharifu aliongea na kutaka kupeleka mikono yake kwenye shingo ya mkewe amkabe.



“Tobaaa!!!, roho yangu,” Binti Mngane alishtuka kwa kukurupuka ndotoni huku akihema kwa kasi kama mwizi aliyekimbizwa na raia.



Sharifu kwa makelele ya mama yake akashtuka usingizini. Akaamka na kwenda chumbani kwa mama yake akaone kilichomkuta mama yake.



“Mama kuna nini?” aliuliza Sharifu mara baada ya kufika chumbani kwa mama yake.



“Hamna kitu mwanangu” alificha kusema Binti Mngane.



“Siwezi kuamini, makelele yote yale unaniambia hakuna kitu...nahisi kuna kitu unanificha.”



“Mh! basi uchelewi kukuza mambo nitakuambia.”



“Hayo ndiyo maneno.”



“Nimeota ndoto mbaya sana.”



“Ndoto gani hiyo?.”



“Nimeota baba yako anataka kunikaba shingoni,” Sharifu alicheka sana baada ya kuelezwa ndoto aliyoota mama yake kisha akasema huku akitabasamu.



“Kumbe nawe mama muoga?.”



“We!!!!!! lazima mtu uwe muoga, yaani uote unakabwa na marehemu unafikiri mchezo.”



“Si mchezo, lakini nawe usiwe unapuuzia ndoto za wenzako.”



“Nimekuelewa...hata hivyo muda umekwenda sana nenda kalale upunguze usingizi ili baadae uwahi kuamka,” Binti Mngane baada ya kumwambia mwanae akaendelea kulala.



Sharifu alipomuaga mama yake akarudi chumbani kwake kuendelea na usingizi. Saa nane kamili ya usiku ikagonga wote kwa pamoja wakaamka wakajibadili mwonekano. Sharifu akavaa kaniki nyekundu kiunoni na akajifunga usongo mwekundu kwenye paji la uso. Binti Mngane yeye akavaa kaniki nyeusi kiunoni na akajifunga kiremba cheusi kichwani. Wote kwa pamoja wakayayuka chumbani wakaja kukutania nyuma ya nyumba yao kisha safari ya kuelekea kilingeni ikanzia hapo. Walipofika kilingeni wakakuta wanachama wenzao na Mzee Damanda wamefika muda na wanaendelea na mkutano.



“Mh, kuonekana kilingeni hadi mfuatwe nyinyi mmekuwa nani?. Hata huyo raisi mwenyewe hawi hivyo............. Nawashangaa nyie kajamba nani mnavyojisikia kuja kilingeni,” Mwanachama mmoja mwanamke anayetambulika kwa majina ya Fatuma Nyanduru alisikika akiongea kwa kuwakejeli Binti Mngane na mwanae.



Binti Mngane akamtuliza mwanae kwa ishara ili kuepusha shari mbele ya mkuu wao. Hivyo basi wakanyamaza kimya bila kujibu chochote. Wakasikiliza kikao kile mwanzo mwisho kwa umakini mkubwa kisha kikao kilipoisha Sharifu na mama yake wakataka kuondoka. Mzee Damanda akawazuia mara baada ya kuona wachawi wote washaondoka kilingeni.



“Mmenifurahisha sana kuja kilingeni leo, pia mmenifurahisha kwa kuonyesha utii mbele yangu pindi Fatuma Nyanduru alivyowatupia maneno makali.............. Kweli nawapa hongera sana kwa hili” alitoa pongezi Mzee Damanda kwa vibaraka wake.



“Kiongozi siku zote sisi ni wapole sana kwa wanachama wenzetu. Yote hayo ni kwaajili ya kutovunja katiba iliyowekwa,” Binti Mngane akasema.



“Vizuri sana...endeleeni kuwa hivyo mkiendelea hivyo mtanipa heshima mimi na chama kwa ujumla” alizidi kuongea Mzee Damanda.



“Tunakuahidi sasa na siku zijazo mimi na mwanangu hatutokuangusha.”



“Nitafurahi sana na nitajivunia kuwa nanyi siku zote.”



“Shukrani...sasa kiongozi ngoja tukuache kuna mahali tunawahi,” Binti Mngane aliaga huku akiangalia hali ya hewa juu ya anga ilivyotulia.



“Mnaweza kwenda ila nawaombeni chonde chonde msiache kuhudhuria kilingeni.”



“Tutaudhuria usihofu juu ya hilo...acha sisi leo tuondoke,” Binti Mngane alipomaliza kuongea maongezi na Mzee Damanda, wakayayuka na mwanae wakatokea kwenye uwanja wa nyumbani wa Bi Kazimoto. Walipofika wakakuta mazingira ya nyumbani kwa Bi Kazimoto yamepoa sana.



“Huyu kikongwe yupo kweli?,” Binti Mngane akauliza.



“Kwa ukimya huu sidhani, nahisi katoka,” Sharifu alijibu huku akipiga jicho kila pahala kama pengine ataweza kumuona Bi Kazimoto.



“Ana nguvu kiasi hiki hadi anajua ujio wetu.”



“Sidhani.”



“Kama kweli ana nguvu kiasi hiki, kikongwe huyu kiboko.”



“Hana lolote subiri nimtafute, nikimpata atajuta.”



“Lakini kuwa makini,” Sharifu pale alipokuwa akayayuka kwaajili ya kwenda kumtafuta adui yake. Hatimaye alikuja kumuona kikongwe yule msalani akitetemeka kwa hofu.



”Ajuza huku unafanya nini?,” Sharifu aliuliza kwa kebehi.



“Nilifahamu ujio wenu nikajificha.”



“Sasa kilichokufanyisha ujifiche ni nini...wakati wewe ni galacha wa nguvu za giza.”



“Nimegundua kuwa wewe ndiye galacha, nguvu zako sikupati hata kidogo.”



“Naona unapiga tantalila nyingi, ebu twende ukapigie huku,” Sharifu alimaliza mazungumzo na Bi Kazimoto kisha upesi akamkumbatia na kuyayuka naye hadi alipo mama yake. Binti Mngane alipoona Bi Kazimoto analetwa na mwanae akaangua kicheko cha ajabu kilichokuwa kikijirudia kama mwangwi.



“Wewe kikongwe, kula kwako kote chumvi unashindwa hadi na mtoto wa juzi...kweli unanistajabisha.”



“Nakustajabisha kweli, lakini ukweli mwanao ana nguvu za ajabu ambazo sijawahi kukutana nazo tokea nizaliwe,” Bi Kazimoto aliongea huku rohoni akiwa na roho ya uwoga.



“Umeligundua hilo...kwanini sasa umetafuta vita?.”



“Sikujua, lakini kwasasa nimeshajua sitoendeleza tena vita nae,”



“Sharifu mwanangu kikongwe huyu simwelewi...tumpe hukumu gani?,” Binti Mngane alimgeukia mwanae na kumuuliza swali mara baada ya kuona Bi Kazimoto mbabaishaji.



“Tumsamehe tu mama” alijibu Sharifu bila kufikiri.



“Tumsamehe!!!, haiwezekani yaani mtu alitaka kukuua bila sababu halafu leo hii tumsamehe kirahisi.... Jambo hili siafiki,” Binti Mngane alimwambia mwanae kwa sauti ya kukalipia hadi Sharifu akashikwa na uoga.



“Mimi siwezi kutoa hukumu kwa kikongwe huyu, kwasababu roho ya huruma ishanijia...kama kuna uwezekano tumwachie tu,” Sharifu alizidi kumpigia kampeni Bi Kazimoto asiweze kupatiwa hukumu na mama yake.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Nishakuambia kuwa mimi siafiki jambo hili...na kwa kuwa hutaki kutoa hukumu kwa kikongwe huyu mimi nitatoa,” Binti Mngane alizidi kung'ang'ania Bi Kazimoto apate hukumu. Akazidi kuongea kwa sauti ya ukali kidogo.



“Nitampa hukumu moja tu, kuanzia leo atakuwa Mbuzi,” Kikongwe yule aliposikia kuwa atakuwa Mbuzi akaomba msamaha kwa kupiga magoti aweze kusamehewa.



“Nisameheni jamani, mkinigeuza kuwa Mbuzi unadhani kwa maisha haya si mtaniweka kwenye wakati mgumu” alizidi kuomba asamehewe Bi Kazimoto.



Sharifu akamuonea huruma sana Bi Kazimoto. Akafikiria sana jinsi ya kumsaidia na akaumiza kichwa kuwazua ni jinsi gani atamtoa Bi Kazimoto kwenye hukumu, lakini ikashindikana kumsaidia kutokana na mama yake kutilia mkazo. Binti Mngane kwa nyakati zile roho ya huruma hakuwa nayo akasimama kwenye dhamira yake kuu. Akanyoosha kidole cha husda kwa Bi Kazimoto na papo hapo Bi Kazimoto akageuka Mbuzi mweusi anayelia na kutapatapa kwa huzuni.



“Kwisha, habari yako,” Binti Mngane aliongea na kuachia kicheko cha pongezi chenye kubeza.



“Sijapenda,” Sharifu aliongea kwa unyonge huku akimtazama Bi Kazimoto kwa jicho la huruma.



“Kwanini?.”



“Alikiri kosa.”



“Shenzi kabisa, ebo!!! kwanini unakuwa kama Kinyonga?,” Binti Mngane aliuliza huku akionyesha kuchukizwa.



“Najuta,” Sharifu alijibu huku akisikitika.



“Ebu...usiniletee ujinga na usinipotezee muda kazi ishaisha tuondoke,” Binti Mngane alifoka hadi macho yakawa mekundu kwa hasira.



Sharifu hakutaka kumtibua mama yake akatii amri wakainama kisha wakayayuka na kila mmoja akatokea chumba chake. Alipofika chumbani Sharifu hakuwa na furaha alizidi kufikiria hukumu ile aliyopewa Bi Kazimoto siku hiyo akakosa kabisa lepe la usingizi akawa anajilaumu tu.



“Kwanini, sikumsikiliza Bi Kazimoto?,” Sharifu roho ilimsuta na kujiona mkosaji.



“Ona sasa nimekusababishia hukumu ya kinyama.”



“Nisamehe sana, Bi Kazimoto.”



Sharifu akiwa kitandani anajisemesha mara usingizi ukamrubuni hatimaye akalala usingizi wa pono. Kutaharuki asubuhi kumekucha akasogea dirishani kuhakikisha asubuhi hile kama kweli imewasili, mwanga mkali uliopenya dirishani na kuwika kwa Jimbi kukamthibitishia Sharifu kuwa kumekucha.





“Nilijua nimewahi kuamka!!!...kumbe mama ameshaamka,” Sharifu aliongea huku akimshangaa mama yake mara baada ya kutoka chumbani.



Akazubaa kwa muda kwa kuganda kama sanamu la Michelini kwenye mlango wake wa chumbani, akimwangalia mama yake akifagia ndani huku akiimba nyimbo ya kichawi inayovuta nyota kwa binadamu ambaye hana kinga.



“Habari,” Sharifu baada ya kumsogelea mama yake jirani akatoa salamu.



“Salama,” Binti Mngane aliitika salamu ya mwanae.



“Naona kumekucha.”



“Kumekucha...hali ya hewa ya ubaridi ya leo ni nzuri na siku nzuri.”



“Inapendeza.”



“Kabisa...uwanja umefagiliwa?.”



“Bado!.”



Sharifu akachukua ufagio wa chelewa akatoka nje kufagia uwanja. Dakika kadhaa zikapita akawa amemaliza kufagia akarudi ndani, awamu hii akamkuta mama yake amekalia Kigoda anamenya Mihogo ya chai.



“Nakuona mama yangu, unatayarisha maakuli” aliongea Sharifu kwa utani huku akienda kukaa sakafuni kando ya mama yake.



“Eeeh, ujui kama uhai ni kula.”



“Mambo hayo ni ya kisayansi, nitajulia wapi wakati hata kielimu ngazi za juu sijafika.”



“Najua ni jinsi gani unaumia, tungefanikiwa kukusomesha nahisi sasa ningefurahia matunda...ila usijali sana maana kufeli mtihani si kufeli maisha,” Binti Mngane alimfariji mwanae.



“Sitojali na wala sitojilaumu, nitapambana mpaka tone la mwisho.”



“Kabisaa...wengine wengi hawajasoma lakini wana maisha bora kutokana na kujiongeza,” Binti Mngane alimweleza mwanae kisha akaelekea jikoni kubandika Mihogo mara baada ya kumaliza kumenya.



Sharifu akanyanyuka sakafuni mara baada ya mama yake kuelekea jikoni, akatoka nje na kuelekea kwenye banda la kuku kufagia. Alipofika eneo la bandani akaruka kimo na kupiga ukunga mara baada ya kudhurika mguuni.



“Mamaaaaa.”



“Nini, kimetokea?,” Binti Mngane aliuliza mara baada ya kufika sehemu ya tukio na kumkuta mwanae amekaa chini akiugulia mguu.



“Nyoka.”



“Amekufanyaje mwanangu.”



“Amening'ata mguuni.”



“Kakung'ata!!!!,” Binti Mngane alishangaa kisha akanyanyua mguu wa mwanae na kusotea. Muda kadhaa tu Sharifu akarudi katika hali yake na akatoa shukrani kwa mama yake.



“Asante.”



“Usijali, ni wajibu wangu kukutunza.”



“Lakini mama kwanini ukunifunga kamba?.”



“Kamba ingekukinga tu na isingekuponyesha, ndiyo maana nimetumia nguvu zangu kukuponyesha.”



“Umewezaje?.”



“Nimeweza kwa kuwa hujarogwa. Mara nyingi wachawi kumponyesha mtu aliyerogwa ni ngumu kutokana na nguvu za giza zilizotangulia lakini kwa mtu aliyepata matatizo kwa uwezo wa Mungu tunaweza kumtibu kwa kuwa hazijatumika nguvu zetu za giza.”



“Nimekuelewa...inamaana Nyoka huyu hajatumwa kwa nguvu za giza?.”



“Hajatumwa ingekuwa katumwa kwa nguvu za giza nisingeweza kukuponyesha na ingepelekea sumu kukudhuru,” Binti Mngane alimweleza mwanae huku akimnyanyua kisha akarudi jikoni.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Sharifu aliponyanyuliwa akaingia bandani kufagia, ndani ya dakika tano Sharifu akamaliza kufagia banda la kuku hatimaye akarudi ndani. Aliporudi ndani akamkuta Binti Mngane kashaandaa chakula ukumbini.



“Upo shapu!!!?,” Sharifu alimuuliza mama yake kwa mshangao mara baada ya kuketi kwenye mkeka kilipo chakula.



“Kwanini?.”



“Ushaivisha chakula, mara hii!!!.”



“Kupika mbona aichukui muda mwingi dakika kadhaa tu unaivisha chakula.”



“Kwako...lakini wengine ni wazito wakiwa jikoni, unalijua hilo?.”



“Sio wote, ni baadhi.”



“Kweli?.”



“Eeenh.”



“Najivunia kuwa na mama, shapu na mwenye hekima,” Sharifu alimpatia sifa mama yake.



“Ushaanza kunipaka mafuta, kwa mgongo wa chupa.”



“Kwanini nikufanyie hivyo?.”



“Haya...chai ya leo unaionaje?.”



“Haina sukari.”



“Ni kweli...leo sukari imeisha na nimeona uvivu kwenda dukani.”



“Haina shida, kwa kuwa tushazoea shida zetu.”



Wakati Sharifu na mama yake wakiendelea na maongezi na vicheko huku wakiendelea kula, wakakatishwa maongezi na mtu aliyekuwa anabisha hodi katika mlango wao wa ukumbini.



“Nenda kamwangalie, anayegonga mlango,” Binti Mngane alimtuma mwanae.



“Sauti hiyo kama naijua,” Sharifu aliropoka kwa kukisia.



“Sauti hiyo ya nani?.”



“Sio ya jirani yetu.”



“Jirani yetu nani?.”



“Mama Nguya.”



“Ebu...kaangalie usikisie,” Binti Mgane alimwamrisha mwanae awahi kwenda kufungua mlango.



Sharifu alikwenda kufungua mlango hakuamini japo moyo wake ukaamini na kujawa na furaha. Alipokutana ana kwa ana na shangazi yake mara baada ya kufungua mlango.



“Hausindile?,” Sharifu alimsalimu shangazi yake kwa lafudhi ya kirugulu.



“Hanoga...Mai nimemkuta?,” Shangazi yake Sharifu alijibu na kuuliza kwa lafudhi ya kirugulu naye.



“Umemkuta...ataenda wapi kwani?. Yupo mng'anda ametulia tu,” Sharifu alijibu hatimaye akamkaribisha Shangazi yake.



Sharifu akaongozana na shangazi yake ndani, wakamkuta Binti Mngane akiendelea kula huku kavuta mdomo mbele kama mtu aliyechukuliwa mume. Alimchukia sana wifi yake kutokana na ugomvi wao wa awali wa kurushiana vijembe vya majivuno.



“Wifi mbona mvivu kutembea?,” Shangazi yake Sharifu aliuliza kwa upendo.



“Unadhani, nimelishwa miguu ya kuku kama wewe,” Binti Mngane alijibu kwa kubeza.



“Wifi sijaja kwenu kwa shari nimekuja kumuona mtoto wa kaka yangu,” Shangazi yake Sharifu aliongea kwa upole.



“Umesikia mwanangu, anaumwa au amefariki?.”



“Nilijua umebadilika wifi.”



“Nimekuwa kinyonga siku hizi?.”



“Sharifu mwanangu mbona simwelewi mama yako?.” Sharifu hajasema, akadakia kusema Binti Mngane kwa kumtupia wifi yake maneno ya shombo.



“Unielewi kwani nimelewa?...na kwanza una uwezo wa kuwa na mtoto wewe?.”



“Maneno gani unaongea mbele ya mtoto?” aliuliza Shangazi yake Sharifu.



“Kama tasa tusiseme?.”



“Kweli, hadi hapo nishagundua wifi yangu kwamba bado unanichukia..........sawa bwana lakini Mungu yupo, ipo siku atasikia kilio changu,” Shangazi yake Sharifu aliongea kwa simanzi huku machozi yakitiririka.



Shangazi yake Sharifu akaendelea kutoa machozi na kichwa akiwa kainamisha chini. Sharifu akaona huruma kwa shangazi yake. Akamsogelea karibu akamwinua shangazi yake kisha akambembeleza anyamaze. Haikuwa kazi rahisi kumnyamazisha, ilikuwa ni kazi pevu kweli kweli.



“Nyamaza shangazi, utaendelea kulia hadi saa ngapi...uoni kama unachokoza homa,” Sharifu aliongea huku akizidi kumbembeleza shangazi yake na kumfuta machozi kwa kutumia mkono.



“Siwezi kujizuia kuacha kulia...labda hivi mama yako ndiyo anapenda.”



“Kulia umelia vya kutosha, ebu...sasa nyamaza niweze kuwapatanisha,” Binti Mngane alicharuka mara baada ya kusikia mwanae anataka kumpatanisha na adui yake akavunja ukimya na ndimi yake ikapayuka.



“Sharifu unasemaje?” aliuliza Binti Mngane.



“Nataka, niwapatanishe” alijibu Sharifu.



“Mimi siwezi kupatanishwa na tasa.”



“Mamaaa una nini?.”



“Kwani, unanionaje?.”



“Matendo yako leo siyaelewi!.”



“Kivipi?.”



“Sasa unachomfanyia shangazi ni sawa?.”



“Wewe unaonaje?.”



“Si sawa.”



“We mtoto nawe usinichanganye haya ni maamuzi yangu mimi sihitaji mtu yeyote aniingilie..................... Kwanza naona anavyoendelea kukaa anazidi kunipa kero hebu aondoke tu,” Binti Mngane alimchukia sana wifi yake hatuwezi jua kwa kosa gani kubwa mno labda ni haki yake kumchukia.



“Shangazi haondoki hapa. Akiondoka tu bila yeye mwenyewe kuamua nami naondoka,” Sharifu akatetea.



“Ondoka! Si umeamua?. Ila yakikushinda utarudi,” Binti Mngane alisema kwa jazba.



Binti Mngane baada ya kuona wanamchelewesha kufanya shughuli zake, akaenda mlangoni akafungua mlango kisha akawatoa kwa kuwatimua. Sharifu hakutaka kubisha na kuendelea kuleta mzozo, akamshika mkono shangazi yake kwa hasira na kuondoka naye.



“Kwa nini usingebaki?. Ungeniacha mimi niende?,” Shangazi yake Sharifu wakiwa njiani alimuuliza mtoto wa kaka yake.



“Nishaamua kuondoka nawe...acha tu twende wote shangazi,” Sharifu alijibu kisha akamfariji shangazi yake kwa kumshika mkono huku wakiwa wanaendelea na safari.



Shangazi yake Sharifu hakupinga sana chaguo la mtoto wa kaka yake. Akakubali kwenda naye nyumbani lakini wakiwa bado wapo njiani Binti Mngane akatuma Njiwa kimiujiza ili aende kumdhuru wifi yake. Huyo Njiwa akatii agizo na kwenda moja kwa moja na kutua kwenye kichwa cha shangazi yake Sharifu kisha akamdonoa na kuondoka. Ghafla shangazi yake Sharifu mara baada ya kudonolewa akajihisi kizunguzungu kisha akadondoka chini.



“Umepatwa na nini?,” Sharifu aliuliza huku akijitahidi kumwinua shangazi yake.



“Kichwa kinaniuma sana,” Shangazi yake Sharifu alijibu mara baada ya kuinuliwa na mtoto wa kaka yake.



“Kinaumaje?.”



“Kina gongagonga kama nyundo.” Sharifu akagundua kitu na akajua zaidi kuwa mama yake anahusika asilimia mia kwa ugonjwa uliompata shangazi yake kutokana na mzozo uliotendeka hivi punde tu.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Jitahidi kutembea, tukifika nikakutengenezee dawa,” Sharifu alisihi kisha akamkokota shangazi yake polepole.



“Siwezi kutembea, naona viungo vya mwili vyote vimekaza,” Shangazi yake Sharifu aliongea kisha akapata kizunguzungu tena. Kizunguzungu kikamfanya alegee mwili na kumfanya Sharifu akose nguvu ya kummudu shangazi yake na kusababisha kudondoka tena chini kwa pamoja.



“Tutafanyaje?,” Sharifu aliuliza huku akilaza kichwa cha shangazi yake kwenye miguu yake mara baada ya kudondoka.



“Tupumzike kidogo, nikipata ahueni tutaondoka.”



“Hapana.”



“Kwanini?.”



“Ukipumzika njiani unaweza kuzidiwa...ngoja tu nikubebe ukapumzike nyumbani.”



Shangazi yake Sharifu akakubaliana na ushauri wa mtoto wa kaka yake . Akakubali kubebwa ili mradi awahi kujipumzisha nyumbani, walipofika Sharifu akatandika mkeka nje shangazi yake apunge upepo huku yeye akimtengenezea dawa. Dakika chache akachemsha dawa na ikawa tayari kwa kunywa.



“Dawa, tayari amka unywe,” Sharifu alimwamsha shangazi yake mara baada ya kuonekana kulala nyakati zile.





“Shangazi amka basi,” Sharifu aliendelea kumwamsha shangazi yake kwa muda mrefu bila matokeo yoyote ya kujibiwa.



Ndipo akaja kugundua kuwa shangazi yake hayupo naye tena duniani, kwa maana ameaga dunia. Sharifu akaumia sana na hadi akashindwa kujizuia kuachia kilio. Akatoa kilio huku akipiga yowe kuwaita majirani, punde baadhi ya majirani wakasikia wito wakafika sehemu ya tukio wakamkuta Sharifu nje akiwa ameshikilia mwili wa shangazi yake.



“Nini kimewakuta?,” Jirani mmoja mwanamke aliyetambulika kwa jina la Mama Chausiku aliuliza na kuonyesha dalili ya kutotambua kilichotokea.



“Mama Chausiku, jirani yetu amefariki,” Jirani mwengine wa kiume aliyeelewa kilichomkuta shangazi yake Sharifu alijibu swali la Mama Chausiku.



“Eti?,” Mama Chausiku alimuuliza Sharifu apate uhakika na kuonyesha kutoamini.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Eeenh, amefariki shangazi yangu,” Sharifu alijibu huku akiwa bado analia.



Mama Chausiku akamuonea huruma sana. Pale alipokuwa Sharifu akachutama, akasogeza kichwa cha Sharifu kwenye kifua chake kwa kumfariji kisha akaomba baadhi ya vijana wabebe mwili wa jirani yao waupeleke ndani. Vijana wakauinua mwili wa shangazi yake Sharifu na kuingiza ndani kisha wakatoka nje wakasaidiane na Mama Chausiku kumnyamazisha Sharifu. Wakamnyamazisha na hatimaye Sharifu akanyamaza kisha akapanga siku na majira ya mazishi. Kwa kuwa shangazi yake Sharifu alifariki jioni Sharifu akapanga mazishi yafanyike kesho yake jioni ya saa kumi na moja kasoro. Kesho yake jioni muda uliopangwa watu wakajiandaa kwenda kuzika wakazika na watu wakatawanyika kurudi majumbani.



**********



ITAENDELEA

MAMA USINIFUNDISHE UCHAWI - 3

 






Simulizi : Mama Usinifundishe Uchawi

Sehemu Ya Tatu (3)





“Sharifu, ina maana unioni au?,” Mama Abuu aliuliza mara baada ya kuona amepitwa bila kupewa salamu na Sharifu.



“Unataka nifanyeje?,” Sharifu naye akauliza huku akibetua mdomo kwa dharau kumdharau Mama Abuu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Mama yako huwa unampita bila kumsalimia kama hamjaonana?.”



“Mama ni mama na wewe utabaki kuwa wewe tu...kwani ni lazima, kukupa salamu?.”



“Hama kweli mtoto umleavyo, ndivyo akuavyo yaani matendo yako ayafanani nawe kabisa,” Mama Abuu alisema kwa kutoamini majibu anayojibiwa na Sharifu.



“Unataka kunilea wewe au?, halafu mimi naona kama unachelewa nyumbani kufanya shughuli zako,” Sharifu alizidi kuonyesha dharau kwa mama Abuu wazi wazi.



“Sasa hivi, ushaanza kuvuta bangi na kama sio bangi unaugua uchizi.”



“Wewe mama sasa unanivunjia heshima, katika siku niliyokosewa leo umenikosea.”



“Acha nikukosee tu maana hujiheshimu.”



“Unijui?.”



“Kwa hiyo!,” Mama Abuu naye aliongea kwa dharau mara baada ya kugundua Sharifu anamdharau.



“Utaona,” Sharifu aliongea kwa kumaanisha japo Mama Abuu alichukulia kama mzaha.



“Aisee!!!, yaani wewe kisisimizi unanitishia maisha Tembo.”



“Unachukulia ninayoongea ni mzaha, utakuja juta baadae,” Sharifu alisema na kutoa sonyo lililojaa vitisho ndani kisha akaondoka na kumwacha Mama Abuu ameduwaa.



Sharifu akafika kwa Mama Stumai na kumkuta yupo nje kakaa kwenye kisturi anasuka mkeka. Sharifu akakaa pembeni ya mlango wa kuingilia ndani mwa Mama Stumai mara baada ya kukaribishwa.



“Eeenh, za nyumbani?,” Mama Stumai aliuliza mara baada ya kumuacha Sharifu kwa muda apumzike.



“Salama.”



“Kilichokuleta ni nini?, maana sio kawaida kuja nyumbani kwangu,” Mama Stumai alizungumza huku macho yake yakiwa bize na kusuka mkeka.



“Nimetumwa na mama nije kufuata pesa zake.”



“Mama yako siku hizi chizi eeenh!.”



“Kwa nini?.”



“Nishamueleza kuwa pesa zake simpatii hadi anilipe posho yangu ya kijumbe,” Mama Stumai aliongea kwa kukataa kukabidhi pesa. Akapumzika kuongea hatimaye akaendelea kuongea.



“Siwezi kutoa pesa mpaka nilipwe kwanza, nenda kamwambie akae akijua hivyo,” Mama Stumai alikataa katakata kutoa pesa za Binti Mngane.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Sharifu hakutaka kujibizana tena na Mama Stumai alichokifanya ni kuaga na kuondoka kuelekea kwa kina Kondo kuchukua mpini. Alipofika nyumbani kwa kina Kondo akamkuta Kondo yupo nje ya nyumba yao akitengeneza huo mpini.



“Karibu,” Kondo alikaribisha mara baada ya kuona Sharifu kawasili nyumbani kwao.



“Asante...lakini sikai nimefuata mpini wangu,” Sharifu aliongea na Kondo huku amesimama wima.



“Sawa...mpini wako ndiyo huu namalizia kwa hiyo subiri kidogo.”



“Sawa” alikubali Sharifu na hakupinga hata kidogo akasubiri, ndani ya dakika tano Kondo alikuwa kashamaliza kutengeneza mpini na akamkabidhi mwenyewe.



“Utanipa, bei gani?,” Kondo aliuliza mara baada ya kumkabidhi mpini hule Sharifu.



“Nitakupoza, na elfu tano,” Sharifu aliongea kisha akatoa pesa mfukoni na kumkabidhi Kondo.



Kondo baada ya kulipwa, Sharifu akaaga na kurudi nyumbani. Alifika ikiwa ni jioni akamkuta mama yake anamenya kunde kwaajili ya mboga.



“Mbona, umechelewa?” lilikuwa swali la kwanza la Binti Mngane akimuuliza mwanae.



“Mama Stumai, ndiye aliyenichelewesha” alijibu Sharifu kisha akakaa sakafuni.



“Kwanini?.”



“Kagoma, kunipa pesa!.”



“Kwanini?.”



“Kasema, hadi umlipe pesa za kijumbe!.”



“Mama huyu mpumbavu...naona ajanijua vizuri hivi punde atanijua tu,” Binti Mngane aliongea kwa kupayuka na kuonekana mwenye hasira mara baada ya kupewa taarifa zile na mwanae.



Sharifu alipompatia taarifa mama yake akaingia chumbani akawasha redio sauti ya juu. Masaa mawili mbele Binti Mngane akaivisha chakula na kukitenga ukumbini kwenye mkeka baada ya hapo akaenda kumuita mwanae kipenzi.



“Genda Heka,” Binti Mngane kutokana na kuwa na hasira bado ya kutopewa pesa yake ikampelekea hadi kumuita mwanae jina la ajabu.



Sharifu kwa kuwa alifungulia redio kwa sauti ya juu hata mama yake alivyomuita hakusikia. Binti Mngane kwa kuona mwanae haitiki ikabidi aende hadi mlangoni kumgongea huku akiendelea kuita jina lile la ajabu lisilostahili hata kwa jamii.



“Genda Heka.”



“Eeeh” aliitika Sharifu kwa kukurupuka kitandani mara baada ya kupunguza sauti ya redio.



“Muda wote nakuita hadi sauti inataka kukauka, kumbe ulifungulia redio lako?,” Binti Mngane aliuliza mara baada ya kugundua mwanae alifungua redio.



“Nisamehe,” Sharifu aliomba msamaha kwa unyenyekevu.



“Endelea lakini ukija kuwa kiziwi, hamna mtu atakaekupeleka hospitali,” Binti Mngane alimuonya mwanae.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Lakini mama, redio inakufariji,” Sharifu aliongea kwa utani.



“Nitokee huko...lakini sishangai sana kwa kuwa wewe si mluguru ubishi ni jadi yako.”



“Sikatai, mimi ni mzalendo na kabila langu hivyo acha nidumishe ubishi.”



“Ebu, tufute mazungumzo maana nikiendelea kubishana nawe utasababisha tule ugali jiwe,” Binti Mngane aliongea huku akichota tonge la ugali mara baada ya kufika ukumbini na kuanza kula.



Wakafuta mazungumzo kwa muda wakala chakula. Sharifu akala matonge kadhaa akaanza kutapika mfululizo pembezoni mwa mkeka.



“Unafanya, upuuzi gani?,” Binti Mngane alibwata mara baada ya kuona mwanae anafululiza kutapika.



“Ni hasira, tu,” Sharifu alijibu kisha akatoka kutupa matapishi.



“Hasira, gani hizo?,” Binti Mngane aliuliza kwa kufura mara baada ya mwanae kurudi kwenye kutupa matapishi.



“Nina hasira, na Mama Abuu na Mama Stumai.”



“Mama Abuu, kakufanyaje tena?.”



“Mama Abuu wakuniita mimi chizi, hama zangu hama zake leo ataona.”



“Wewe umempania Mama Abuu, ila mimi nimempania sana Mama Stumai...kwa hiyo katika pilikapilika za leo hutokuwa peke yako tutakwenda wote,” Binti Mngane alisema huku akijaribu kuleta furaha moyoni.





Walipomaliza kula Sharifu akatoa vyombo akaenda chumbani na kumwacha mama yake kwenye mkeka pale ukumbini akishona khanga. Safari hii Sharifu hakutaka kusikiliza redio, alipofika kitandani akajitupa chali na kujibembeleza kwa kujitingisha miguu punde tu akapitiwa na usingizi. Alikuja kushtuka mishale mingine kuchungulia dirishani akaona giza limetanda pande zote kuashilia usiku umeingia huku likisindikizwa na wingu zito la mvua na mweku mweku zikimurika na kuzima kuwa giza. Hali ile kwa mtu muoga asingethubutu kunyanyua miguu yake na kutoka nje.



“Giza hili, naona linaniruhusu kwenda kilingeni ngoja nikamwamshe mama,” Sharifu alijisemea nafsini kisha akajibadilisha muonekano akayayuka chumbani kwake na kutoka nje kuelekea kwenye mlango wa chumbani wa mama yake na hatimaye kuongea kwa hisia na mama yake.



“Amka mama.”



“Naona leo umewahi sio kawaida yako, ama kweli umepania,” Binti Mngane aliongea naye huku akijibadilisha muonekano mara baada ya kuamka.



“Ninashauku sana na wamama wale, si wanajifanya wanajua sasa leo watakiona cha mtema makuni,” Sharifu alizungumza huku akizungusha macho yake kimiujiza.



“Kweli dhahiri, umewapania.”



“Wewe, acha tu mama,” Sharifu alimsubiri kwa muda mama yake, ghafla akamuona mama yake ametokea kimiujiza alipo yeye. Akiwa tayari kashajiandaa wakayayuka pamoja tayari kuanza safari na kabla ya kufika kwenye tukio wakashauriana.



“Unavyoona wewe, tuanze wapi?,” Binti Mngane akauliza.



“Naona kama vile kwa Mama Abuu ni karibu tuanze kwake, baadae tukishatoka kwa Mama Abuu ndiyo twende kwa Mama Stumai,” Sharifu alimjibu mama yake huku akitupa usinga huku na kule kwaajili ya kusafisha njia.



Waliposhauriana na mama yake wakaelekea moja kwa moja kutua kwenye uwanja wa nyumbani wa Mama Abuu. Walipotua wakashangazwa sana na hali waliokumbana nayo, wakakuta zizizi kumetulia huku kukichochewa na giza. Hali ile tulivu ikawafurahisha sana.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Inaonekana Mama Abuu yupo kwenye usingizi mzito, lengo letu tulifanye haraka tuondoke,” Binti Mngane alimweleza mwanae huku akiusogelea mlango wa kuingilia ndani.



“Basi niache niingie ndani, kinachojiri nitakujuza,” Sharifu alimwambia mama yake huku akiegemea mlango wa Mama Abuu na kuyayuka kutokea chumbani.



Sharifu akamkuta Mama Abuu yupo kitandani amelala na mumewe usingizi wa pono. Akamchukua kimazingara mtuhumiwa wake na kutoka naye nje. Binti Mngane alipomuona mwanae amerudi na Mama Abuu kwa kumkokota kama mkokoteni akafurahi sana.



“Naam!!!, huo ndiyo uwanaume,” Binti Mngane alimsifia mwanae mara baada ya Sharifu kufika alipo.



“Mtu wetu, huyu hapa,” Sharifu aliongea huku akimkabidhi Mama Abuu kwa Pilato.



Alipokabidhiwa kwa Binti Mngane akamwagiwa unga mweupe wa chengachenga unaofanana na mchanga unaosaidia mtu asiweze kuamka mapema. Akiwa hajitambui wala kuonyesha dalili ya kufumbua macho akawapa moyo na kuwafurahisha Binti Mngane pamoja na mwanae.



“Huyu mtu inaonyesha dawa tuliyompatia, itatufanya tufanye kazi yetu bila kipingamizi,” Binti Mngane alimwambia mwanae huku akipanda tumboni mwa Mama Abuu aliye na ujauzito wa miezi nane.



“Umejuaje?,” Sharifu aliuliza huku akimkodolea macho mama yake.



“Nimeona kuwa Mama Abuu, hana kinga.”



“Kwa hiyo tutafanikiwa, kufanya kazi yetu kwa uzuri,” Sharifu aliongea kisha kwa pamoja wakafurahi na mama yake huku wakicheza kwa kukata viuno kwa maringo.



Baada ya muda kadhaa Binti Mngane akafungua kitambaa cheusi kisha akatoa kimzizi chenye miiba mikali. Akakitemea mate kimzizi kile hatimaye akamlisha kinywani Mama Abuu. Walipohakikisha wamemaliza kumlisha kimzizi wakamrudisha Mama Abuu chumbani aendelee na usingizi.



“Mama Abuu dawa yake ipo jikoni inachemka, baada ya muda mfupi atainywa,” Binti Mngane alimweleza mwanae mara baada ya kumrudisha Mama Abuu.



“Nikiwa nawe nafarijika na kujifunza, mambo mengi sana mama yangu.”

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Yakupasa ujifunze mengi tunayofanya, ili baadae uweze kuwa mwanachama madhubuti,” Binti Mngane alimweleza mwanae huku akinusisha pua kila upande ajue kama kupo shwari.



“Nitajifunza kila kitu kutoka kwako...lakini mama muda ushakwenda twende kwa Mama Stumai sasa tukamalize kazi yetu,” Sharifu alimwambia mama yake mara baada ya kuona wanachelewa kwenda kwa Mama Stumai.



“Kweli tuondoke, tusije kuchelewa tukaumbuka kukipambazuka,” Binti Mngane safari hii alinusa juu ya anga kisha akamshika mikono mwanae na kuyayuka eneo lile.



Binti Mngane na mwanae wakaelekea nyumbani kwa Mama Stumai. Hali ya hewa kwa wakati ule ilionyesha anga ikiwa na mwanga hafifu huku nyota zikiendelea kumelemeta kwa mbali ikiashilia kuwa kunakaribia kupambazuka.



“Tushafika sehemu husika, nisubiri nje safari hii mimi niende nikamalize mchezo.” Binti Mngane alinong'ona mara baada ya kutua kwenye uwanja wa Mama Stumai.



“Ila kuwa makini, si unajua madhara ya hii nyumba?,” Sharifu aliuliza kwa kumhabarisha mama yake.



“Madhara gani tena? mbona unanitisha,” Binti Mngane aliuliza kwa kutaka kujua madhara ya nyumba ile.



“Wewe ushasahau, kama Mama Stumai ni mrokole?.”



“Mmh!!! nilikuwa nimeshasahau, nitakuwa mwangalifu usijali kuhusu hilo mwanangu,” Binti Mngane alisema huku akienda ndani kinyume nyume mara baada ya kufungua mlango.



“Sawa, nitakusubiri,” Sharifu aliongea huku akizunguka nyumba ya Mama Stumai kwa kusota makalio kuhakikisha usalama.



Binti Mngane alipokaribia mlango wa kuingia chumbani mwa Mama Stumai akasotea mlango kwa makalio hatimaye mlango ukafunguka kisha akaingia chumbani. Alipofika chumbani akamkuta Mama Stumai akiwa amelala nafasi ile Binti Mngane hakutaka kuichezea.



“Wewe si mjanja!. Sasa leo nakuonyesha kama kuna wajanja zaidi yako,” Binti Mngane alijisemea moyoni kwa kumtupia vijembe mzazi mwenzake.



Baada ya kutupa vijembe hakuchelewesha akanyoosha mkono wa kushoto mbele kisha likatokea pembe la ng'ombe. Akampiga Mama Stumai miguuni na lile pembe, alipoona kamaliza mchezo bila kipingamizi chochote akajipongeza kwa kicheko hatimaye akayayuka pale chumbani na kutokea nje alipomwacha mwanae.



“Sasa kazi imekwenda vizuri bila kuchelewa tutoweke eneo hili kabla akujapambazuka,” Binti Mngane alimwambia mwanae kisha wakaondoka na kuja kutua kwenye uwanja wao wa nyumbani na kila mmoja akaingia chumbani kwake kujipumzisha kwaajili ya kuondoa uchovu.



**********

Asubuhi ya alfajiri mume wa Mama Abuu akawahi kuamka kwaajili ya kuwahi shamba kama desturi yake ya siku zote, lakini alivyoamka akashangazwa na jambo aliloliona kwa mkewe.



“Wewe Siawezi,” Baba Abuu alimwamsha mkewe kwa kumpiga vibao.



“Kuna nini, Chang'ari?,” Mama Abuu aliuliza akiwa bado usingizini.



“Tumbo umelifanyaje?,” Baba Abuu alifoka na uso kaukunja kama Nyati.



“Kwani lina nini?,” Mama Abuu aliuliza na hakuelewa mumewe ana maanisha nini kutokana kuwa alikuwa bado anaendekeza usingizi.



“Mtoto wangu wa tumboni umempeleka wapi?...ushaenda kumtoa kafara nini?,” Baba Abuu aliuliza kwa sauti ya juu huku akionyesha kuwa na hasira.



“Mungu, wangu!!!,” Mama Abuu alishtuka toka usingizini mara baada ya kuona ujauzito wake kupotea. Kisha akameza mate kwa muda na kumtazama mumewe aliyefura kama mzoga wa Bata na kulijibu swali aliloulizwa.



“Mimi sielewi kitu,” Mama Abuu alijibu huku akijiangalia tumbo lake mara mbili mbili asiweze kuamini kilichotokea.



“Wewe mwanamke usinifanye sina akili, nina akili zangu timamu niambie mtoto yupo wapi?.”



“Sijui Chang'ari.”

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Nakuambia hivi kuanzia sasa sihitaji kukuona katika nyumba yangu mpaka pale utakapomrejesha mtoto wangu. Mwanamke gani unaendekeza ushirikina,” Baba Abuu alimfukuza mkewe kwa kumvuta atoke nje huku akimpiga ngumi za tumboni mara baada ya kuona mkewe mbishi kutoka ndani. Hakumsikiliza kabisa mkewe, akamfukuza mkewe kama Mbwa aliyemlia mboga ya ngama.



**********

Mama Stumai akaamka asubuhi akiwa na furaha tele, lakini furaha yake ikaja kuzizima bila kutarajia mara baada tu ya kunyanyua mguu wake wa kuume na kuona umepooza.



“Looh!!!, nini tena hiki?,” Mama Stumai akajiuliza.



“Siamini, mbona haya maajabu nilale mzima niamke nimepooza,” Mama Stumai alijisemea huku akijikokota kushuka kitandani na kukaa sakafuni kwaajili ya kujinyoosha miguu athibitishe.



“Nimeamini uchawi upo japo sikuamini mwanzoni, kweli usilolijua ni kama usiku wa giza,” Mama Stumai alizidi kusema na kujuta pale sakafuni. Furaha yake yote ikapotea kwa siku ile na punde tu akajikuta mwenye msongo wa mawazo. Akashindwa hata kujizuia kutoa chozi na asimuone wa kumfariji kwa nyakati ile ya matatizo kwake.



**********

Binti Mngane asubuhi na mapema akawahi kuamka na kuzifanya shughuli zake za nyumbani. Muda ulikwenda sana akaona mwanae hana hata dalili ya kuamka ndipo ikamlazimu aende kumwamsha.



“Sharifu, Sharifuu” aliita Binti Mngane kwa kupaza sauti.



“Naam!!!,” Sharifu aliitika kwa kukurupuka toka usingizini mara baada ya kuamka na kufikicha macho.



“Kulala gani hadi saa hizi?.”



“Nimechoka mama, niache nipumzike,” Sharifu alijibu kiuchovu kisha akajilaza tena kitandani.



“Mwenye usingizi peke yako, mbona nami nina usingizi ila nimeamka kufanya kazi...ebu nawe amka,” Binti Mngane alimwambia mwanae kwa kumlazimisha aamke.



“Naomba mama niache nilale kidogo. Nikiamka nitafanya hizo kazi,” Sharifu aliomba mama yake amwache alale kisha akavuta shuka akaendelea kulala.



“Lala ila jua, ukiamka kuna kazi zinakusubiri,” Binti Mngane alimuhabarisha mwanae kisha akaenda jikoni kupika. Baada ya masaa kupita Binti Mngane akawa kashaivisha uji na viazi vitamu. Akatenga chakula ukumbini kisha akaenda kumwamsha tena mwanae.



“Wewe, mtoto.”



“Naam.”



“Uji! tayari.”



“Nakuja.”



“Fanya haraka.”



Sharifu akatoka chumbani kwake mara baada ya kuitwa na mama yake huku akipepesuka kama mlevi wa gongo kutokana na usingizi. Akajifikicha macho ili aweze kuona mbele vizuri. Akajikongoja taratibu hadi ulipo mswaki kisha akauchukua na kuelekea uwani ili kusafisha meno na uso nyuma akimwacha mama yake akimngoja ukumbini.



“Sharifu,” Binti Mngane alimuita mwanae mara baada ya kuona anachelewa kurudi.



“Na naam,” Sharifu aliitika kwa shida kutokana na mswaki kuwa kinywani.



“Huko kunawa, mwaka!.”



“Nakuja, ndiyo nafunga mlango wa uwani.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Harakisha bwana, tuje tule,” Sharifu punde tu alirudi ndani na kuketi kwenye mkeka ukumbini mara baada ya kuchomeka mswaki ukutani.



Walipomaliza kunywa uji Binti Mngane akatoa vyombo nje avioshe. Sharifu akapumzika kidogo kisha akanyanyuka kwenye mkeka na kwenda kufagia banda la kuku. Akafagia huku akijiburudisha wimbo ambao aliwahi kufundishwa na baba yake kipindi cha nyuma kabla ya uhai wake.





“Mdooogo mwanangu mdogo...aowa owa,

Jisomeee mwanangu jisomee...aowa owa,

Uniokoooe mwanangu uniokoe...aowa owa,

Nakuombeeea baba yako nakuombea...aowa owa,

Kwa mwenyeeezi nakuombea kwa mwenyezi...aowa owa,” Sharifu aliimba nyimbo hiyo kama mara mbili na kucheza kwa kutingisha kichwa na kunyanyua miguu.



Binti Mngane alipomaliza kuosha vyombo akaenda kwenye banda la kuku kumwangalia mwanae kama anafagia au lah. Kufika akashangaa kuona mwanae akiimba nyimbo aliyoipenda kuiimba mumewe kipindi cha nyuma.



“Leo unafuraha, eenh?,” Binti Mngane aliuliza mara baada ya kufika bandani.



“Sina furaha, yoyote,” Sharifu akajibu.



“Mbona nakuona, unaimba na kucheza kwa furaha?.”



“Najiimbia tu mama yangu, nisichoshwe na kazi,” Sharifu alijibu huku akizoa kinyesi cha kuku na kukiweka kwenye ndoo ya taka.



“Umenikumbusha mbali.”



“Kivipi?.”



“Nyimbo hiyo unayoimba inanikumbusha miaka ya tisini na nne hivi, kipindi alichonioa baba yako alikuwa anapenda kweli kuimba nyimbo hiyo.”



“Kweli?.”



“Eehe!.”



“Nyimbo hii unajua, kanifundisha nani.”



“Sijajua.”



“Kanifundisha baba huyo huyo.”

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Nilijiuliza huyu mtoto nyimbo hii kaitoa wapi, kumbe umefundishwa na baba yako.”



“Eenh...natoka siku hiyo nimetokea kuipenda kweli hiyo nyimbo.”



“Ulikuwa kumbe na baba mzuri sana?.”



“Sana tena sana kwa jinsi alivyokuwa ananipenda baba hadi leo hii angekuwepo nisingetaabika,” Sharifu alijibu kisha akabeba ndoo na kwenda kumwaga kinyesi cha kuku.





ITAENDELEA

Blog