Search This Blog

MKE WANGU NUSU JINI, NUSU MTU - 3

 






Simulizi : Mke Wangu Nusu Jini, Nusu Mtu 
Sehemu Ya Tatu (3)






Niliondoka na mfuko wangu wa fedha kurudi ndani huku mapigo ya moyo yakinienda kwa kasi ya ajabu, niliogopa sana kuhusu ile harufu ya manukato.Niliwatuma vijana fulani kwa ajili ya kwenda kukodisha mikeka ya kukalia, sufuria na kununua chakula. Hayo yote nilishirikiana na akina mama majirani wa pale kwa kaka.



Kifupi, msiba uliisha salama, tukamzika kaka na maisha yakaendelea.

Nakumbuka ilikuwa wiki imepita tangu kumzika kaka, siku moja usiku, licha ya kwamba tulikuwa tukiendelea kuwasiliana, Munil alikuja nyumbani mimi nikiwa bafuni. Alifungua mlango huku nikimuona, akaingia.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Nilipomaliza kuoga, nikaenda kwangu nikiamini nitamkuta Munil lakini sikumkuta, nikashtuka na kusema kwa sauti:

?Ina maana Munil hajaingia humu ndani??



Nilikiwa nimesimama niliangalia kulia kushoto na sehemu kubwa ya chumba, nikachuchumaa pia nikiamini kwamba huenda alijificha chini ya kitanda japokuwa kitanda chenyewe kilikuwa kazi kutoa chaga na kuingia chini. Hakuwepo!

Nilishika simu na kumpigia huku bado nikiwa na majimaji mwilini kwa vile nilitoka kuoga. Akapokea:



?Mume wangu.?

?Mke wangu, mzima??

?Mi mzima, vipi wewe??

?Mi mzima, uko wapi??

?Niko kwangu. Vipi kwani??

?Hujaja kwangu leo??

?Haa! Jamani baby, nilikuja kwako saa ngapi na wewe ulikuwa wapi??

?Mh! Kweli hujaja??

?Sijaja bwana, tena nilitaka kukupigia nikwambie nina mazungumzo makubwa sana na wewe, tuonane leo.?

?Oke, utakuja au??

?Nitakuja muda si mrefu.?

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Nilipokata simu tu, nilikaa kwenye kochi dogo palepale chumbani kwangu na kuanza kumfikiria Munil kwa undani sana huku nikisema moyoni anaweza kuwa si binadamu wa kawaida?

Nilipowaza hivyo tu kuna sauti ikaniambia akija mkague miguu yake uone ni nini? Nikashtuka kwa wazo hilo.



Ndani ya dakika kumi, Munil aliingia. Alikuwa amevaa gauni jeupe likiwa na urembo kwenye mikono na shingoni. Alionekana kama bi harusi. Siyo siri alipendeza sana. Kwa kweli Munil aliumbika, hata kama wewe ungekutana naye mahali popote ungekubaliana na mimi.



Kwanza, kila alipoonekana alikuwa hapendezi kuwa anaishi eneo hilo hata kidogo. Yaani ninamaanisha kwamba, hata kwa hapa Kibaha Munil alionekana hapendezi kuishi.

?Vipi mpenzi wangu?? aliniita na kunikumbatia kisha akanipiga mabusu. Lakini ghafla akaachana na mimi na kukaa akionesha umakini wa hali ya juu huku akisema:



?Mume wangu hebu tuongee suala hili, wazazi wangu wanataka kukuona na pia wanauliza je, utanioa au unanipotezea muda tu??

Nilishtuka sana kusikia maneno hayo. Nikamuuliza kwa woga:

?Kwani wazazi wako wanajua uko na mimi??

?Niliwaambia, mimi huwa sifichagi kitu kwa wazazi wangu.?

?Oke, lini tutakwenda??

?Hata leo.?

?Ni wapi kwani??

?Bagamoyo.?

?Oke, basi twende leo, saa ngapi??

?Tujiandae hata sasa twende, nitakodi teksi.?



Nilikubali kwani sikutaka kumpoteza wala kumkera mpenzi wangu Munil. Nilijiandaa, tukatoka mpaka kituo cha teksi. Tuliikuta teksi moja tu, tukapanda hiyo na kuanza safari.

Ndani ya dakika arobaini na tano tulifika Bagamoyo. Lakini kabla ya kushuka kwenye teksi, nilihisi



kuchoka sana. Mwili uliishiwa nguvu, nikalegea na kujikuta namwambia Munil.

?Munil, mwili hauna nguvu kabisa, hapa kama nataka kulala.?

?Kwa nini mpenzi wangu, unaumwa kwani??



Sikumbuki kama nilimjibu naumwa au la! Ila nikajikuta mimi na Munil tupo nje ya geti kubwa sana la mlango. Kwamba ndiyo tumefika nje kwao. Munil aliinua mkono akabonyeza mahali, kengere ikaita.

Mara, geti likafunguka na kuwa wazi. Ndani niliona jumba kubwa sana la kifahari. Nilishangaa



hakuna mtu aliyekuja kufungua geti lakini geti lilifunguka, kwangu ilikuwa ajabu sana.

Mara, msichana mmoja mweupe sana, alifanana sana na Munil. Yaani kwa kila kitu ni kama Munil, ila yeye alikuwa kama amemzidi umri. Mimi niliamini ni mtu na mdogo wake.



Alimkumbatia Munil, akaja kwangu, akanikumbatia akatushika mikono na kutuingiza ndani huku akisema karibu sana wapendwa.



Tulifikia kwenye sebule la kifahari, mimi sijawahi kuona tangu nimezaliwa. Sebule kubwa sana, lilisheheni kila aina ya mapambo. Sofa nyeupe, meza za vioo vya kuwaka, mashelfu meupe ya kuvutia na seti ya muziki wa kisasa, mkubwa sana.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mara alitokea mwanaume. Naye alifanana sana na Munil. Akaja kumkumbatia Munil kisha na mimi nikasimama na kumkumbatia, tukakumbatiana. Akakaa huku akisisitiza karibuni sana.

Mimi nilijua wale ni kaka na dada wa Munil kwa jinsi walivyofanana kama chupa za bia.



?Baby, hawa ni wazazi wangu. Yule mama, yule baba. Nawapenda sana wazazi wangu,? alitambulisha Munil na kunifanya nipate mshtuko kwani sikutegemea kama wangekuwa wazazi wake.

?Ni wazazi wako hawa?? nilijikuta nikiuliza bila kutarajia.

?Ndiyo, kwani vipi??

?Mbona wadogo sana??

?Hapana, mimi nina miaka hamsini, mke wangu huyu ana miaka arobaini na tano, ni wadogo sisi?? baba mtu alidakia.



B

ado kwangu ilikuwa ajabu kwani hakuna aliyeonekana kufikisha hata miaka thelathini na mitano…

"Ina maana…mbona hata mimi ni mkubwa kwenu," nilisema nikibabaika.

Kwanza walicheka wale wazazi wote kisha baba yake Munil akasema:



"We huwezi kuwa mkubwa, wewe una miaka thelathini na moja kama sikosei."

Nilishtuka sana kusikia vile japokuwa alisema kama hakosei, yaani alibashiri lakini ni kweli nilikuwa na miaka thelathini na moja wakati huo. Kwa nini asingesema nina miaka thelathini? Nilimwogapa sana lakini nikajibu:



"Ni kweli kabisa."

"Sasa utasemaje sisi ni wadogo?"

Yaliishia hapo, nikajikuta nikiuliza:

"Hivi hii ni Bagamoyo gani? Maana sikujua kama Bagamoyo kuna majengo ya kifahari kama haya."

"Hii Bagamoyo ya Majini," alijibu mama'ke Munil.



"Majini maji au majini wale viumbe wabaya wanaoogopwa na binadamu?" nilidadisi tena.

"Majini maji," alijibu baba Munil lakini sura ya mkewe na hata ya Munil zilionesha kutokuwa sawasawa. Nikawa najiuliza ni kwa swali la mwisho au! Nikakosa jibu lakini pia nikaamua kuwa mpole.



"Sasa kijana wewe ndiyo unataka kumwoa binti yetu, upo tayari au bado unapanga mipango?" swali hilo lilitoka kwa baba wa Munil."Kusema ukweli wazazi wangu mimi nimenuia kumwoa kabisa Munil na nimejipanga kwa hilo, huenda baada ya mwezi ujao nikaleta posa kwenu."



"Posa ndiyo nini?" baba Munil aliniuliza kwa mshtuko.

"Ni barua ya kujitambulisha."

"Utambulisho gani tena? Si hivi umekuja kujitambulisha! Sisi tunachotaka kama kweli umeamua kumuoa binti yetu Munil tukufungishe ndoa sasa hivi hapahapa," alisema baba.



"Nipo tayari," hii kauli ya ‘nipo tayari' nilijikuta inatoka bila kutarajia. Mdomo ulikuwa kama umeongozwa kusema hayo bila mimi mwenyewe kutaka. Sijui ni kwa nini!

Basi, baba Munil alisimama akaenda kuingia kwenye chumba f'lani. Alipotoka alikuwa ameshika



mkeka si mkeka, kapeti si kapeti, sijui kilikuwa kitu gani. Akautandika chini, akamwita Munil, akakaa juu yake. Nikaitwa na mimi, nikaenda kukaa sambamba na Munil.

Baba alitushika vichwa, akasema maneno kama kiarabu kwa muda wa kama dakika tano nzima anasema tu. Alipomaliza akatusimamisha huku akisema:

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Munil, kuanzia sasa huyu ni mumeo, mkaishi pamoja na mzae watoto lakini usikose kuja kututembelea wazazi wako kila mara.

Kwa kuwa unaweza kuendesha gari, utaondoka na lile la mama yako, nitamnunulia lingine. Pia kabla hamjaondoka, nitakupa pesa ukafanye biashara yoyote ile."



Nilijikuta moyo wangu ukiwa baridi, nilijishika masikio na kuyatanua kwa vile nilihisi yamekaa vibaya ndiyo maana nikawa nasikia vile wakati si kweli.

"Wazazi ninaomba kusema kidogo," nilisema nikiwa nanyoosha mkono juu.

"Ndiyo bwana, sema."

"Mimi ninaishi kwenye chumba kimoja tu, halafu uswahilini, sasa mnaposema mnampa gari huyu nitapata tabu ya sehemu ya kuliegesha, afadhali tukajipange kwanza, kwa leo tutarudi na ile teksi tuliyokuja nayo."



Mara, baba Munil alisimama na kwenda ndani, sikujua ni chumbani au kwenye nini! Aliporudi alikuwa ameshika mfuko mweusi, ndani sikujua mna nini, akauweka chini akiwa ameubana na miguu, akasema:



"Mimi ni mfanyabiashara mkubwa sana, fedha kwangu si tatizo ilimradi binti yangu asiishi maisha ya tabu."



Akainama kidogo na kuingiza mkono kwenye ule mfuko, ulipotoka ulikuwa umeshika dola za Kimarekani tupu tena mpyaa! Ilikuwa ngumu kwangu kukubali kwamba baba Munil anaweza kuwa milionea kiasi kile tena akisema ni mfanyabiashara wa siku nyingi wakati umri ulionesha bado kabisa.



Alihesabu zile dola kisha akatumbukiza mkono tena na kutoa nyingine, akahesabu halafu akatumbukiza tena mkono, akatoa nyingine, mwishowe akawa ametoa zote. Kama ni wingi wa fedha ya noti ya shilingi elfu kumi za Tanzania palepale ningesema ni zaidi ya shilingi milioni hata mia moja.



Alizitumbukiza zile fadha kwenye uleule mfuko mweusi, akauinua na kuniletea nilipokaa huku akisema:

"Hizi ni dola, Munil," alimwita binti yake.

"Abee baba."



"Kama mtachenji mtapata kama shilingi milioni mia mbili. Lakini nashauri muweke banki, we unajua. Na kama ni benki, itumike akaunti ya mumeo, si ya kwako, wewe sasa huna amri juu ya mambo yako ila mumeo."



Sijui nini kilitokea, ila nilianguka puu! Nilipokuja kuzinduka, nilijikuta nipo hospitali, nimezungukwa na Munil, shemeji yangu, yaani mke wa marehemu kaka na wauguzi watatu.

"Pole sana baby," Munil alisema baada ya kuona nimefumbua macho na kuangalia.



Shemeji naye akasogea na kunipa pole kama Munil huku akisema Mungu atanisaidia.

"Kwani hapa ni wapi?" niliuliza.

"Ni zahanati hapa," alijibu Munil.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Ni wapi?"

"Bagamoyo."

"Nimekujaje?"

"Ulianguka ghafla baby, wazee wakakumbiza hapa na gari."

"Wao wako wapi?"

"Wameondoka, huenda wakarudi baadaye."

"Shemeji umejuaje?"

"Nilimpigia simu mimi."

"Ulipata wapi namba yake?"

"Nilichukua kwenye simu yako baby."



Nilitaka kumuuliza Munil swali lingine kwamba, aliingiaje kwenye simu yangu? Maana ilikuwa na password lakini nikaacha.Wale wauguzi waliondoka, akaja daktari.









?Sasa mgonjwa wangu unaweza kuondoka, drip imeisha kwa hiyo unaendelea sawasawa, jiamini bwana,? alisema daktari bila kuniambia nijiamini kwa lipi.

?Basi kama umeruhusiwa tuondoke, gari letu liko nje,? alisema Munil huku akimwangalia shemeji ambaye naye alionekana kuwa na uso wa mshangao.

?Tunakwenda wapi??

?Si tunarudi Dar.?

?Oke, wazee utawaambia??

?Nitawaambia,? alisema Munil huku akichukua mfuko f?lani hivi na kutoka nao nje. Nikabaki na shemeji.

?Hivi shemeji, kwani wewe umeoa siku hizi??

?Hapana shemeji.?

?Sasa huyu ni nani??



?Huyu ni mchumba wangu shemeji, iko siku nitakuja kukutambulisha rasmi.?

?Mh! Mbona hali yake ya mwili inaonekana ana maisha mazuri sana??

?Hata mimi nitakuwa na maisha mazuri shemeji.?



Mara, Munil aliingia:

?Tunaweza kwenda sasa.?

Nilitoka mwenyewe kitandani, nikatembea huku Munil akiwa amenishika mkono japokuwa sikuwa nahitaji msaada huo.



Lilikuwa gari la kifahari, jipya, jeupe pee, zuri sana. Ndilo ambalo Munil alikwenda kufungua mlango. Kwanza alizunguka na kunifungulia mlango wa mbele kwa abiria mimi kisha akarudi kufungua kwake, akapanda shemeji naye akapanda maana wakati huo tayari milango ilishajitoa kwenye loki.



Kusema kweli lilikuwa gari zuri sana. Sikuamini kama ni letu mimi na Munil. Niliona ni la Munil peke yake tena nilijikuta nikiamini kwamba, mimi na Munil hatutaweza kudumu.

?Gari zuri sana, jipya,? nilisema.



?Tena ndiyo nimeanza kuliendesha mimi leo,? alisema Munil.

Ukimya ulitawala barabarani, muda mrefu nilikuwa nawaza kuhusu gari na zile hela alizotoa baba yake Munil ambazo alisema ziingie kwenye akaunti yangu.



Nilitamani kumuuliza Munil kama zile pesa tunazo au baba yake alizirudisha kufuatia hali yangu ya kuanguka!

?Ule mzigo vipi?? nilimuuliza kwa wasiwasi.

?Upo, si huo huko nyuma.?



Niligeuka kuangalia, nikauona ule mfuko, ulikuwa jirani kabisa na shemeji ambaye naye alipoona naangalia mfuko akautupia macho.

?Huogopi Munil?? nilimuuliza.

?Nini??

?Kuibiwa.?

?Ha! Katika maisha yangu hakutakuja kutokea kitu kama hicho, yaani mimi niibiwe haitatokea hata siku moja.?



?Usiseme hivyo, huwezi kujua,? alisema shemeji kwa sauti ndogo sana.

?Yaani nakuapia, hakuna siku hata moja ambayo mimi nitaibiwa na mtu,? Munil alisisitiza.



Mimi niliamua kukaa kimya lakini si kwa sababu nilipenda bali nilimtafakari Munil kwa jicho la tatu, kwamba yeye ni nani mpaka ajiapize kutoibiwa na mtu.

Shemeji yeye hakuendelea kukaa kimya, akaongea. Lakini ilionekana wazi kwamba aliongea ili kuvunja ukimya wa ghafla.



?Nimeipenda hiyo pafyumu yako we dada mdogo,? alisema shemeji.

?Hii inayotoa harufu??

?Ee.?

?Nimeipata mbali sana, Dubai.?



?Kwani huwa unakwenda Dubai?? alihoji shemeji.

Kidogo nilianza kufurahi kwamba, maswali ya shemeji kwa Munil yanaweza kutoa mwanga wa mimi kuzidi kumjua Munil.

?Siendagi mimi, ila kuna mtu ananileteaga.?

?Naweza kupata na mimi kama hiyo kwa kumwagizia huyo mtu??

Munil badala ya kumjibu, alinyoosha mkono kwenye boksi ndani ya gari hilo kushoto jirani yangu



akaminya mahali, mfuniko ukafungua, akatoa boksi lenye pafyumu, akampa shemeji kwa nyuma huku yeye akiangalia mbele barabarani.

?Kumbe unazo??

?Ilibaki hiyohiyo moja,? alijibu Munil.



Lakini kusema ule ukweli, wakati mfuniko wa lile droo unafunguka, mimi kama niliona hakuna kitu lakini ghafla niliona mkono wa Munil ukishika boksi na kulitoa.

Halafu kwa mujibu wa baba yake kule Bagamoyo, lile gari lilikuwa jipya kabisa sasa yeye aliingiza boksi muda gani mle ndani? Na hata Munil mwenyewe alisema gari ameanza kuliendesha siku hiyo.

***



Tulifika Dar mpaka kwa shemeji, tukamshusha, kisha mimi na Munil tukaenda mpaka nyumbani kwangu. Munil aliegesha gari nje ya nyumba ambako ulinzi wake ni wasiwasi mtupu.

?Itabidi gari likalale kwenye sehemu yenye ulinzi,? nilishauri.

?Hapahapa, ulinzi upo mkubwa sana,? alinijibu Munil huku akishusha vitu vichache ukiwemo ule mfuko mkubwa wenye fedha.



Tulizama ndani kwetu, eti kuanza maisha mapya ya mke na mume. Mimi nimekuwa mume wa Munil, kwangu ilikuwa ndoto za kila usiku.

?Munil,? nilimwita kwa upole.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

?Niambie mume wangu.?

?Baba alisema pesa tukaweke kwenye benki gani??

?Benki yako. Hata kama huna itabidi ufungue tu.?

?Unadhani ni sahihi mimi kumiliki fedha za baba mkwe wangu wakati wewe upo??

?Ni sahihi, mimi ni mke, wewe ni mume, tatizo liko wapi sasa??

?Siku tukiachana je??

?Haitatokea. Kwanza kwa nini tuachane mume wangu? Una mpango huo kichwani??

?Sina ila sisi ni binadamu??

?Weee?weee! Binadamu peke yako, mimi si binadamu, nikwambie kabisa.?

?Sawa wewe ni nani Munil, mbona unanitisha??







ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog