Simulizi : Jini Mauti
Sehemu Ya Pili (2)
Mama hakuamini, akamkumbatia mzee Abdallah na siku hiyo akampa mahaba motomoto. Huo ndiyo ukawa mwanzo wa uhusiano wao wa kimapenzi.
Tumbo la mama likaanza kuonekana, katika kipindi hicho ndiyo alikuwa na wakati mgumu, mauzauza yaliendelea huku kila siku bibi akimtokea na kumwambia ni lazima achukue mkoba wake wa uchawi kama yeye alivyouchukua kwa mama yake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Mama aliendelea kukataa, kuna kipindi alikuwa radhi apate tatizo lolote lile, yaani hata kama kufa afe lakini si kukubali kuwa mchawi kama bibi alivyotaka awe.
Baada ya miezi tisa, mama akajifungua katika Hospitali ya Mwananyamala. Siku hiyo alipojisikia uchungu na kwenda hospitali, kulikuwa na paka mmoja aliyependa sana kwenda hospitali hapo.
Mama aliniambia kwamba kulikuwa na magazeti yaliandika kuhusu paka hao kwamba walikuwa wengi mno katika kipindi kile, acha niseme wazi kwamba hao walikuwa wachawi, yaani bibi alifika hospitali hapo na wenzake katika umbo la paka na kuanza kumfuatilia mama.
Mpaka mama anajifungua, paka wale waliendelea kuwepo. Si mama peke yake ambaye hakujua
kama wale paka walikuwa wachawi bali hata watu wengine nao hawakulijua hilo kwani kwa kuwaangalia, walikuwa paka kwa asilimia mia moja.
Madaktari hawakuweza kugundua kitu chochote kile, kwao, walipowaangalia, waliwaona kuwa
paka wa kawaida kabisa. Mama hakulala usiku, macho yake yalikuwa wazi na kama kulala, alilala mchana tu.
Alikaa kwa siku tatu hospitalini ndipo aliporuhusiwa na kurudi nyumbani. Mzee Abdallah alifurahia sana, maishani mwake, japokuwa alikuwa ameoa lakini mama alikuwa chaguo la moyo wake.
Hakutaka kurudi nyumbani kwake, mama alimpenda kwa mapenzi ya dhati. Wakati mwingine mzee Abdallah aligombana na mkewe baada ya kugundua kwamba alikuwa na mwanamke wa nje, mzee huyo hakujali, alimwambia mkewe kwamba ndiyo alikuwa na mwanamke na kamwe asingeweza kumuacha.
Mara kwa mara bibi alimtokea mama, aliendelea kumsisitiza kwamba ilikuwa ni lazima awe mchawi lakini mama aliendelea kuwa na msisitizo wake kwamba iwe isiwe hakutaka kuwa mchawi kabisa.
Kama hautaki kuwa mchawi, binti yako atachukua hii mikoba, alisema bibi huku akionekana kumaanisha alichomwambia mama.
Hawezi kuwa mchawi, Davina hawezi kuwa mchawi.
Tutaona.
Nasikia paka wananiita.
Paka? Ndiyo mama.
Wapo wapi?
Huwasikii hao wanalia?
Hapana!
Mama! Nawasikia paka wakilia, nilimwambia mama.
ENDELEA
Mama akasimama na kuelekea katika pembe ya nyuma, nikasikia akisema maneno kwa sauti ya chini kisha kusikia maneno machache aliyoongea kwa sauti kubwa.
Ole wako umsumbue mwanangu, ama zako ama zangu, niliyasikia maneno hayo toka kwa mama yangu, aliyaongea huku akiwa na hasira mno, akarudi kitandani na kulala.
Kuanzia kipindi hicho, zile sauti za paka zinakata, sikujua nini kiliendelea lakini kutokana na akili za kitoto, nikashukuru
Mungu hivyo kulala. Kilichofuata, ghafla nikajikuta nikiwa kwenye kundi kubwa la watu, walikuwa watupu, nilipowaona,
nao wakaniona, nikawa nawaangalia kwa zamu, cha kushangaza, nikamuona yule mwanamke mzee niliyemuona ndotoni,
mwanamke aliyetaka kunipa mkoba ambao sikujua wa nini. NIKASHTUKA NA KUOGOPA.
****
Nilibaki nikitetemeka pale nilipokuwa, kila nilipowaangalia watu wale, niliyahofia maisha yangu kwani niliona nikiwa kwenye hatari kubwa. Kumbuka nilikuwa mdogo, miaka saba na nilikuwa nikisoma shule ya msingi darasa la kwanza.
Mwanamke yule mzee ambaye ndiye alikuwa bibi yangu akaanza kunifuata kule niliposimama, nilipoona akipiga hatua
kunifuata, niliogopa sana, nilibaki nikitetemeka mno. Alionekana kuwa mwanamke hatari, macho yake yalikuwa makubwa.
Mkononi mwake alishika mkoba mkubwa, alinifuata huku uso wake ukiwa na tabasamu pana. Aliponifikia, akanikazia macho hali iliyonifanya nitetemeke zaidi, akaunyoosha mkono wake na kutaka kunipa mkoba ule.
Mjukuu wangu! Wewe ndiye mrithi wangu niliyekusubiri kwa kipindi kirefu, aliniambia bibi huku mkoba ule ukiwa umenifikia.
Wewe ni nani? nilijipa ujasiri wa kuuliza.
Mimi bibi yako.
Huo mkoba wa nini?;
Wewe chukua.
Nilikuwa muongeaji sana, tangu nilipokuwa mdogo, nilikuwa kama nilivyokuwa. Sikumuogopa mtu yeyote, nilipotaka kuzungumza jambo fulani, nilizungumza tena kwa haraka sana. Nilipofikishwa hapo, kiukweli niliogopa lakini baada ya kukaa
kwa dakika fulani, nikayazoea mazingira ya hapo, hofu ikaanza kunitoka.
Unakwenda kuwa malkia Pwani yote, aliniambia bibi.
Malkia wa nini?
Malkia wa uchawi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Aliponiambia hivyo tu, kuna hali niliisikia moyoni mwangu, sikujua ilitoka wapi, nilijisikia nikipata nguvu, nikiwa na imani kubwa juu ya kile alichoniambia, hapohapo, pasipo kulazimishwa nikanyoosha mkono wangu na kuuchukua mkoba ule, nikakabidhiwa uchawi na kuwa mrithi wa bibi yangu.
Nikaanza kusikia ngoma zikipigwa kwa shangwe, watu wakaanza kucheza huku wakishangilia, kitendo cha mrithi kupatikana kilimfurahisha kila mtu. Nilibaki nikiuangalia mkoba ule, sikujua ndani kulikuwa na nini lakini ulikuwa mzito.
Baada ya kukaa hapo kwa muda kama wa dakika ishirini, bibi akaniambia kwamba ilinipasa niondoke kurudi nyumbani na kesho angekuja kunichukua na kunileta hapo kwa ajili ya mafunzo, yaani nilitakiwa kufundishwa mambo mengi kuhusu uchawi ili niwe na nguvu.
Nilikubaliana naye na hivyo kuambiwa nifumbe macho, nikaze meno na nibane pumzi, nikafanya hivyo huku mkoba ukiwa mkononi mwangu, baada ya hapo, ghafla nikajikuta nikiwa kitandani, nilishtuka, kijasho kilikuwa kikinitoka, nilihisi joto kali sana.
Kuna nini? aliniuliza mama, alikuwa ameshtuka kutoka usingizini.
Mama nilimuita.
Unasemaje?
Mkoba wangu upo wapi?
Nini?
Nilikuwa na mkoba, upo wapi?
Mkoba gani?
Nilipewa mkoba.
Na nani? aliuliza kwa mshtuko.
Mwanamke mzee! Upo wapi? nilimuuliza mama.
Mama akaonekana kufahamu kilichotokea, nilipomwambia hivyo tu, akajua kwamba tayari bibi alinipa mkoba baada ya yeye kukataa, sasa mkoba ule aliamua kunipa mjukuu wake.
Kwa mara ya kwanza nikamuona mama yangu akianza kulia, sikujua kilichomliza ila mara kwa mara alikuwa akimtaja bibi kwamba ilikuwa ni lazima amkomeshe.
Kwa mara ya kwanza nikamuona mama yangu akianza kulia, sikujua kilichomliza ila mara kwa mara alikuwa akimtaja bibi kwamba ilikuwa ni lazima amkomeshe. Sikujua alimaanisha nini na sikujua kwa nini alimsema sana bibi, tena kwa mabaya.
ENDELEA NAYO?
Mama hakutaka kuzungumza kitu kingine, alichokifanya ni kulala huku akiangua kilio kilichojaa kwikwi. Asubuhi ilipofika, hakutaka niende shule bali aliniambia nijiandae kwani kulikuwa na sehemu alitaka twende, hakukuwa na tatizo, nikajiandaa.
Baadaye akanichukua na kwenda sehemu moja hivi, sikumbuki ilikuwa eneo gani ila kulikuwa na kijipori kidogo, kimlima kidogo huku kwa mbali nikiona nyumba moja ya nyasi. Tukaanza kuisogelea nyumba ile, tulipoifikia, mama akapiga hodi, nikasikia sauti ya mzee f?lani ikitukaribisha.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Tulipoingia ndani ndipo nikagundua kwamba hapo kulikuwa kwa mganga wa kienyeji, aliponiona, alishtuka mno lakini hakutaka kuonesha hali yoyote ile, akatuambia tukae na kumsikiliza mama alikuwa akisema nini.
Babu nimekuja, kuna tatizo,? alisema mama.
Tatizo gani??
Huyu mtoto wangu, usiku alichukuliwa na wachawi,? alisema mama.
Mmmh!? aliguna mganga.
Kuna nini tena??
Ooppss?? alishusha pumzi nzito.
Niambie kuna nini!?
Mtoto wako amekabidhiwa uchawi, tena mkubwa wa wachawi kanda yote ya Pwani,? alisema mganga.
Unasemaje??
Siwezi kufanya lolote, chochote akikitaka juu yangu, kitatokea, ninaogopa, naomba muondoke,? alisema mganga yule huku akionekana kuogopa.
Ninahitaji msaada wako babu.?
Naomba muondoke,? alisema mganga yule kwa sauti iliyojaa ukali, alionekana kuogopa.
Sikupenda kumuona mama yangu akikaripiwa au kulalamikiwa na yeyote yule kama alivyofanya mganga yule. Japokuwa sikumjua, nikamwangalia kwa macho makali yaliyobadilisha hali ya hewa mule ndani, ghafla, huku nikimwangalia, nikamuona mganga akianguka chini na kuanza
kurusha miguu na mikono huku na kule, mapovu yakaanza kumtoka mdomoni.
Tukaogopa, kumuona mganga yule akigaragara chini huku mapovu yakimtoka, hakikuwa kitu cha kawaida hata kidogo. Tulichokifanya ni kuondoka mahali hapo, tena kwa mwendo wa harakaharaka.
Mama hakufahamu kama mimi ndiye niliyekuwa chanzo lakini wakati tukiwa njiani, alianza kuwa na wasiwasi mno juu yangu kwa kuona kwamba inawezekana nilimfanyia jambo lile mganga yule.
Davina aliniita.
Abeee.
Umefanya nini
Nimefanya nini mama nilimuuliza, hata mimi sikuwa nikifahamu chochote.
Umemfanya nini yule mganga aliniuliza.
Sijui! Sikumfanya kitu.
Huo ndiyo ukweli nilioufahamu, kipindi hicho, hasa muda huo wa kuwa mchawi kwa mara ya kwanza sikuwa nikifahamu kitu chochote kile, sikufahamu kama zile nguvu nilizokuwa nazo ndizo zilizomfanya mganga yule kuwa kwenye hali ile.
Naweza kusema kwamba sikujitambua. Tuliondoka na mama mpaka nyumbani, bado aliendelea kuwa na wasiwasi mno. Aliniambia wazi kwamba bibi alinikabidhi uchawi, alitaka niwe mchawi baada ya yeye kukataa.
Japokuwa nilikuwa na umri mdogo lakini nilifahamu kidogo masuala ya uchawi, hivyo nikaogopa sana. Mama alikuwa mtu wa kulia, alionesha dhahiri kwamba hakupendezwa na uchawi ambao nilikabidhiwa ila hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya.
Usiku ulipoingia, tulipomaliza kula na kulala, ghafla nikaanza kusikia sauti za watu waliokuwa wakicheka, sauti hizo zilitokea chumbani, niliangalia huku na kule, sikuona mtu lakini sauti zile ziliendelea kusikika.
Nikamuamsha mama lakini hakuamka, nikaanza kuwa na hofu kubwa. Nikasimama na kuifuata swichi ili niwashe taa, umeme haukukatika lakini cha ajabu, taa haikuwaka.
Sikujua nini kiliendelea. Wakati najiuliza, ghafla wakatokea watu watatu katika pembe moja ya chumba kile, walisimama imara huku wakiwa watupu kabisa, mara nikajiona kuwa na kitu
mkononi, nilipojiangalia, nilikuwa na ule mkoba wa kichawi alionipa bibi.
Nikaanza kuwafuata wachwi wale ambapo baada ya kuwafikia, wakanishika mkono na hapohapo tukapotea, tulipoibukia, kulikuwa kwenye ule uwanja mkubwa uliokuwa na wachawi wengi waliokuwa uchi wa mnyama.
Bibi akanipokea kwa furaha na kuniambia kwamba siku hiyo ilikuwa ni siku ya kujifunza kuroga na kufanya mambo mengine.
Ndugu yangu, haya ninayokuandikia hapa yalinitokea, uchawi upo, uchawi unaua na katika miaka mingi ya kufanya uchawi, sikuona faida yake zaidi ya kupewa Jini Mauti ambalo liliyagharimu sana maisha yangu.
Siku hiyo nilipelekwa makaburini, japokuwa niliogopa sana kufika huko hasa nyakati za usiku lakini kitu cha kushangaza, siku hiyo sikuwa nikiogopa chochote kile.
Tulifika kwenye makaburi hayo, wachawi wakasimama juu ya kaburi moja la mtoto na kuanza kuongea maneno ambayo kwa kipindi hicho, sikuwa nikiyafahamu, ghafla nikaanza kuliona kaburi
lile likianza kujifukua na sauti kali za paka kusikika na baada ya dakika kadhaa maiti ya mtoto ikatoka kaburini.
Sikuwa na hofu, moyo wangu ulibadilishwa na kuwa wa kichawi, kila kitu kilichotokea, nilionekana kukizoea japokuwa ndiyo ilikuwa siku yangu ya kwanza.Hiyo ndiyo ikawa safari yangu
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
ndefu ya kuwa mchawi, nikaanza kuzoea na kuzoea, nikafundishwa mambo mengi likiwemo la kupaa na ungo, kuwaroga watu na hata kupanga mapambano dhidi ya wachawi wengine, yaani kwa kifupi, nilikuwa hatari kwenye uchawi.
****
Miaka saba ikapita, nilikuwa mchawi kamili, katika kipindi chote hicho sikutaka kumuoneshea mama kitu chochote kile, sikutaka ajue kwani nilijua namna alivyokuwa akimchukia bibi mara baada ya kuniingiza kwenye uchawi.
Alilalamika sana kuhusu bibi, lakini kitu cha ajabu, kila alipokuwa akinifuatilia, hakubaini kama nilikuwa mchawi. Nilimaliza darasa la saba na hatimaye kujiunga na kidato cha kwanza katika
Shule ya Sekondari ya Mkuyuni iliyokuwa Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Katika kipindi hicho nilikuwa nimepevuka, nilivunja ungo na kwa kweli nikajiona kuwa kwenye nafasi ya kuwa na mpenzi wangu. Marafiki zangu wa kike akiwemo Anita na Maria, kila mmoja
alikuwa na mpenzi wake, waliniambia kwamba na mimi nilitakiwa kuwa na mpenzi lakini kwangu nililiona suala hilo kuwa gumu.
Ulipofika mwezi wa sita ndipo macho yangu yakatua kwa mvulana mmoja, alikuwa mzuri wa sura, shuleni alikuwa msafi sana, kila alipokuwa akitabasamu, uzuri wake ulionekana dhahiri, mvulana huyu alikuwa akiitwa Thomas.
Ninaposema mzuri wa sura, ninamaanisha kwamba Thomas alikuwa mzuri hasa.
Wasichana wengi walimtaka kimapenzi lakini hakuwa mtu wa namna hiyo, hakuwa mtu wa kupenda wasichana kabisa.
Naye alikuwa kidato cha kwanza kama nilivyokuwa mimi lakini kitu cha kushangaza, hata wasichana wa kidato cha nne walimtaka kimapenzi. Niliogopa kumwambia ukweli, kila
nilipopishana naye, nilijisikia kitu cha tofauti moyoni mwangu, mapenzi yaliukaba moyo wangu.
Kwa kuwa nilikuwa mchawi, nyakati za usiku nilimfuata Thomas chumbani kwake, nilisimama
pembeni yake, nilikaa kitandani kisha kuanza kumwangalia. Japokuwa pamoja na uchawi wote huo lakini Thomas alikuwa kipenzi cha moyo wangu.
?Thomas, ninakupenda mno, kuwa wangu,? nilisema kila nilipomfuata chumbani usiku.
Kwa mwaka huo wa kwanza shuleni hapo, moyo wangu uliteseka sana, mpaka mwaka unakwisha na kuingia kidato cha pili, sikuwa nimemwambia ukweli. Naomba niwaambie kitu kimoja.
Nilikuwa na uwezo mkubwa wa kumfanya Thomas anipende sana, asilale kwa ajili yangu lakini kilichonifanya kutokufanya hivyo ni kwamba nilihitaji anipende kwa moyo wa dhati kwa hiari yake na si kwa kutumia uchawi.
Nilimuogopa Thomas, labda kwa sababu alikuwa mvulana mwenye akili nyingi darasani zaidi ya mwanafunzi mwingine. Nilivumilia na kuvumilia lakini mwisho wa siku nikaona kwamba uvumilivu wangu unakwenda mwishoni, nilichokifanya ni kumfuata huku nikiwa nimeupiga moyo konde.
?Thomas,? nilimuita mvulana huyo, alikuwa akiondoka kuelekea kwao, aliposikia nimemuita, akasimama na kugeuka nyuma, akaniangalia usoni.?Davina?? alilitamka jina langu, nikashtuka kuona kumbe alikuwa akinifahamu.
Je, nini kiliendelea? Usikose wiki ijayo.
Nikamsogelea pale aliposimama, mapigo yangu ya moyo yakaanza kudunda kwa nguvu, kwa mbali kijasho chembamba kikaanza kunitoka, mwili wangu ulisisimka kupita kawaida. Thomas akaachia tabasamu pana, tabasamu lililouburuza vilivyo moyo wangu, nikajiona kama nimekutana na malaika.
Thomas, nilimuita mvulana huyo, alikuwa akiondoka kuelekea kwao, aliposikia nimemuita, akasimama na kugeuka nyuma, akaniangalia usoni.
Davina alilitamka jina langu, nikashtuka kuona kumbe alikuwa akinifahamu.
SASA ENDELEA
Nikamsogelea pale aliposimama, mapigo yangu ya moyo yakaanza kudunda kwa nguvu, kwa mbali kijasho chembamba kikaanza kunitoka, mwili wangu ulisisimka kupita kawaida. Thomas akaachia tabasamu pana, tabasamu lililouburuza vilivyo moyo wangu, nikajiona kama nimekutana na malaika.
Nilimwangalia Thomas usoni, sikuamini kama siku hiyo mvulana huyo alisimama mbele ya macho yangu, alionekana kuwa mzuri wa sura, alitoa tabasamu ambalo kwa hakika liliongeza uzuri wake wa sura na kunipagawisha mno.
Nilisimama naye karibu sana na hata kama ungekuwa unapita karibu yetu ungegundua kwamba wawili sisi tulikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi. Nilimwangalia kwa macho yaliyoelezea hisia zangu, hisia za mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwangu.
Sikuwa na cha kuongea, niliona kama maneno yote niliyotakiwa kuongea yalikwisha na hivyo kubaki kama bubu tu. Thomas alikuwa akinisikilizia, alitaka kusikia kile nilichotaka kumwambia mara baada ya kumuita.
Davina aliniita huku akinishangaa, sauti yake ikanitoa kwenye lindi la mawazo.
Abeee
Unasemaje? aliniuliza.
Nani? Mimi? Hapana! Sina la kusema, nilitaka kukusalimia tu, nilimwambia huku nikitetemeka.
Haikuwa kweli, nilikuwa na mengi ya kumwambia lakini niliogopa, sikujua angenichukuliaje, nilionekana msichana mdogo lakini nami nilikuwa mrembo kiasi fulani kutokana na wanaume wengi kunisifia, tena hasa nilivyokuwa nimejazia kwa nyuma.
Nilipomwambia hivyo, akashukuru kisha akaondoka, nyuma nilibaki nikimwangalia, nilijuta kwa nini sikumwambia kwamba ninampenda. Nakumbuka siku hiyo nilikuwa na mawazo mengi, kila nilipokaa, mawazo juu ya Thomas yaliutawala mtima wa moyo wangu.
Mama aliligundua hilo, alijaribu kunidadisi lakini alishindwa kujua niliwaza nini na aliponiuliza, sikumwambia ukweli, nilimdanganya tu kwa kumwambia kwamba nilikuwa sawa.
Ilipofika usiku, kama kawaida yangu nikachukua ungo wangu, nikajipaka unga maalum kwa ajili ya kuwangia kisha kupotea chumbani, tulikutana katika uwanja wetu wa kukutania kisha kuanza kupanga ni kitu gani tulitakiwa kufanya.
Nilikuwa malkia wa wachawi lakini kwa kipindi hicho sikutakiwa kuuchukua huo uongozi kwani bado sikuwa nimekomaa, niliendelea kufundishwa zaidi. Tulipopewa majukumu na bibi, tukatakiwa kuyafanyia kazi.
Kabla sijafanya kitu chochote kile, ilikuwa ni lazima nimfuate Thomas chumbani kwake, nimwangalie kwa muda ndipo niendelee na kazi nyingine. Wakati nafanya hivyo kila siku, kumbe bibi alikuwa akinifuatilia tu.
Hakuniambia kitu ila alijua kwamba nilikuwa kwenye mapenzi ya dhati na kijana huyo mwenye sura nzuri, alichokifanya kama kunisaidia ni kumchukua Thomas kila siku na kuniletea, nilimwangalia, niliporidhika, alimrudisha kwao.
Ninataka uwe na furaha maisha yako yote, aliniambia bibi.
Nitashukuru sana.
Ila naomba uwe makini.
Kivipi bibi?
Kuna kitu tunakuwekea mwilini mwako.
Kitu gani?
Hutakiwi kukifahamu kwa sasa, ila hutakiwi kufanya mapenzi na mwanaume yeyote yule, aliniambia bibi.
Kwa nini?http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Hakuna sababu. Usifanye mapenzi na mwanaume yeyote mpaka utakapoolewa, aliniambia, tena kwa sauti ya kunisisitiza hasa.
Sawa bibi, nilimuitikia, sikujua alitaka kunipa kitu gani.
Baada ya siku kadhaa, bibi alinifuata na kunipa maji fulani, yalikuwa kama na mchanganyiko wa damu, akaniambia niyanywe kwani hayo ndiyo yalikuwa na kitu kile alichotaka kunipa, nikafanya hivyo.
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment