Search This Blog

MAMA USINIFUNDISHE UCHAWI - 2

 






Simulizi : Mama Usinifundishe Uchawi

Sehemu Ya Pili (2)





“Mke wa Mzee Kaoneka alipotoka sokoni akamkuta mumewe ukumbini kalala kwenye mkeka. Akashangaa sana ulalaji wa mumewe maana hakumzoea akilala vile alilala chali huku mdomo ukiwa wazi na kutokwa mapovu. Ile hali ikamchanganya kichwa akajaribu kumwamsha lakini akagonga mwamba. Akajaribu kumshika kifuani kusikiliza mapigo ya moyo lakini nako hola. Mke wa Mzee Kaoneka ndipo akajua fika mumewe kashafariki kilio cha kuwashtusha majirani kilitawala kwenye nyumba punde majirani wakajaa kumfariji mwenzao.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Mbona kaaga dunia kwa kifo cha kutatanisha, nakumbuka mara ya mwisho nilimuona jana akipita nyumbani kwangu akiwa na afya,” Mama mmoja jirani alisema akimwambia jirani mwenzake aliyekaa karibu yake.



“Kwani wewe ukijui, kijiji chetu kilivyo na ushirikina?,” Mwenzake yule mama akamuuliza yule mama kwa kunong'ona asisikiwe na baadhi ya majirani wengine.



“Nilikuwa sijui, kumbe kijiji hiki hakifai.”



“Akivumi lakini kimo, tuwe makini yasije kutukuta,” Wamama wale wakaendelea kupiga soga chini chini wasisikiwe na mtu yeyote pale msibani.



Mzee Kaoneka kwakuwa alifariki jioni mazishi yake yakapangwa yafanyike kesho jioni, kesho ilipofika wakafanya mazishi kisha majirani wote wakatawanyika kurudi majumbani kwao.



**********

Sharifu na mama yake walikuwa na furaha wakasherekea sherehe babu kubwa. Binti Mngane siku hiyo akampongeza mwanae kwa ujasiri uliotukuka.



“Sasa unaelekea kuwa galacha...tukio hili nakupongeza,” Binti Mngane alisema huku akimtingisha kichwa mwanae.



“Siku zinavyosonga, naamini uwezo wangu utakuwa mkubwa zaidi,” Sharifu aliongea huku akijikuna kichwa mara baada ya Binti Mngane kumuacha kumtingisha.



“Kweli kabisa...sasa kilichobaki ni kunywa na kula, kwa kujipongeza,” Binti Mngane alisema huku akinyanyuka kwenye mkeka na kuanza kucheza kwa furaha.



Ghafla baada ya muda akaacha kucheza, akatazama juu ya paa akanyoosha mkono wa kushoto kikatokea kikombe chekundu chenye damu ya binadamu. Mama Sharifu akaendelea kuunyoosha tena mkono wake wa kuume juu nako kukatokea nyama mbichi ya Paka. Wakaangua kicheko kwa muda kisha Binti Mngane akamgawia mwanae damu na nyama kidogo wapate kusheherekea siku hiyo. Wakatumia vyema kwa kusheherekea, siku iliyofuata saa moja usiku Binti Mngane akamtuma mwanae kwenye duka lililokuwa jirani na kijiji.



“Pesa zimetuishia cha msingi kabla hatujakumbwa na janga la njaa, nenda na hili pembe ikachote pesa dukani kwa Msambaa,” Binti Mngane alimwambia mwanae kisha kumwelewesha kwa makini asije kuumbuka mbele ya umati wa watu.



“Nitatekeleza, mama,” Sharifu alisema huku akipokea pembe mara baada ya kusikiliza maelekezo kwa mama yake.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Alipopokea lile pembe pale pale pembe likageuka kuwa pesa akaenda nalo moja kwa moja dukani. Akalikabidhi kwa muuza duka kisha akataka huduma kwa haraka, kwa kuwa pembe si la kawaida ni la kishirikina hivyo msambaa hakubahatika kugundua chochote akaona kama amepewa pesa na si kitu kingine. Hii tabia hata kwenye mazingira yetu tunayoishi tunakutana nayo inatambulika sana kwa jina la chuma ulete. Hali hii hutokea sana kwenye biashara unaona mtu anakupa pesa umhudumie ukishakuja kuchanganya pesa yake na pesa zako unakuta pesa zako zipo pungufu. Maskini Msambaa hakugundua chochote hadi muda ule akaendelea kumhudumia Sharifu kama wateja wengine hatimaye kumrudishia na chenji juu. Alivyompa Sharifu chenji ndiyo amejiroga kabisa alimpatia pesa zote alizouza kwa siku hile bila mwenyewe kujua. Sharifu alipopewa chenji akapokea upesi akarudi nyumbani. Alipofika nyumbani akamkuta mama yake kajilaza kwenye mkeka akimsubiri ukumbini.



“Mwanangu umefanikiwa kupata ulichofuata?” aliuliza Binti Mngane kwa shauku ya kutaka kujua huko atokapo amekutana na nini kilichomkuta mwanae hadi achelewe kurudi.



“Nimefanikiwa ila....”



“Ila nini...umekamatwa?.”



“Hapana...kumbe?.”



“Nilikuwa na hofu.”



“Hofu ya nini?.”



“Ya kukamatwa,” Sharifu alijibu huku akihema kwa kasi kama mtu aliyetoka kukimbizwa.



“Pole sana...usingekuwa na hofu mwanangu” alisema Binti Mngane kwa kumwondoa hofu mwanae.



“Kwa nini?” aliuliza Sharifu kwa kutahamaki.



“Kwasababu wafanyabiashara wengi wa kijiji hiki hawana kinga” aliongea Binti Mngane kwa kujiamini.



Baada ya mazungumzo ya Sharifu na mama yake Sharifu akaenda kufunga mlango wa ukumbini kisha akarudi kukaa chini ya mkeka. Akazitoa pesa ambazo zilizofungwa kwenye mfuko mweusi wa malibolo akamkabidhi mama yake, Binti Mngane alipozihesabu zile pesa akakuta zipo laki tano tasrimu.



“Hizi pesa mwanangu, zinaweza kutusogeza kiasi fulani” alisema Binti Mngane kwa kuonyesha tabasamu.



“Tusipotumia kwa kufuja, zinaweza kutusogeza,” Sharifu aliongea kwa kuchangia huku akinyanyuka kwenye mkeka na kuelekea chumbani kwake.



Akaingia chumbani kwake na kutoka huku akimuaga mama yake kuwa anakwenda kujumuika na wenzake kwa ajili ya kubadilishana mawazo mawili matatu. Binti Mngane hakumzuia akamruhusu mwanae kisha yeye akaingia chumbani kwake kuzihifadhi pesa. Mara baada ya kuziweka mahali pasala akatoka chumbani akarudi ukumbini kuendelea kujilaza tena. Sharifu alipofika mtaani akaungana na vijana wenzake kwa kucheza bao. Akacheza hadi saa mbili, ndipo polepole aliporejea nyumbani na kumkuta mama yake kashaamka sasa anachakalika kupika chakula cha usiku.





“Leo naona umeenda dukani mwenyewe” aliongea Sharifu kwa utani mara baada ya kurudi nyumbani.



“Nimeenda mwenyewe, maana uliniahidi unarudi mapema hujarudi sasa ningefanyaje,” Binti Mngane alisema huku akigeuza chakula.



Sharifu akafurahi moyoni jinsi anavyomwona mama yake akinung'unika, baada ya muda kidogo akatulia na kuanza kumtia moyo mama yake kwa kumchangamsha na stori za hapa na pale huku wakisubiri chakula kiive. Wakaendelea kupiga soga mpaka nyakati za saa nne ya usiku ndipo chakula kikawa kimeiva kikapakuliwa kikawekwa mboga na kikaliwa. Binti Mngane alimfurahisha mwanae kwa kumpikia chakula akipendacho ambacho pia baadhi ya watu ukipenda si chakula kingine bali ni wali na maharagwe. Walipomaliza kula Sharifu akatoa vyombo kisha akamuaga mama yake kuwa anakwenda kulala. Binti Mngane hakupinga anajua fika kama mwanae alikuwa amechoka hivyo akamruhusu akalale. Hata yeye pia hakukaa sana nyuma naye akashindwa kuendelea kukaa peke yake akanyanyuka akaenda kufunga milango yote kisha akaenda kulala. Usiku mnene usio na makadirio Binti Mngane akaamka toka kitandani kisha akaenda chumbani kwa mwanae.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Wewe mtoto, mbona unalala sana hujui kama muda ushafika” alisema Binti Mngane mara baada ya kumwamsha mwanae.



“Najua, lakini leo najisikia uchovu,” Sharifu aliongea huku akijinyoosha viungo vya mwili mara baada ya kuamka na kukaa kitako kitandani.



“Ebu nyanyuka, tushachelewa” alinena Binti Mngane kwa kutotaka kuelewa anachosema mwanae. Akamvuta mwanae mkono kwa kumlazimisha waondoke.



Sharifu hakuwa na ujanja tena akanyanyuka kwa kujivuta hivyo hivyo na uchovu. Akajibadilisha muonekano kimiujiza kisha wakatoka nje ya nyumba yao. Walipotoka nje Binti Mngane akanyoosha kidole cha husda chini ya ardhi papo hapo kikatokea kiungo kidogo na usinga. Akakiongeza kile kiungo kimiujiza kisha wakapanda na mwanae wakakipaisha juu hatimaye wakakielekezea upande wa magharibi karibu na kijiji cha jirani kwenye nyumba ya kijana mmoja mwenye utajiri mkubwa pale kijijini. Kiungo kilipofika kwenye nyumba ya huyo kijana wakakitua kile kibeko juu ya paa la nyumba ya huyo kijana bila huyo kijana kujua kitu chochote kinachoendelea kwenye mandhari yake. Mara baada ya kutua wakadumbukia na hatimaye kutokea chumbani mwa huyo kijana na kumkuta amelala fofofo. Binti Mngane na mwanae wakamnyanyua huyo kijana kisha wakatoka naye nje kwenye mti wa ukwaju mrefu. Walipofika nje Binti Mngane akanyoosha usinga wake kila upande kisha akampiga nao huyo kijana kichwani. Huyo kijana baada ya kupigwa akaanza kuzunguka mti wa ukwaju kwa kutambaa huku akihema kwa kasi kama jibwa koko aliyetoka kukimbizwa. Hii hali inatokea sana katika maisha yetu unakuta unaamka umechoka mpaka unajiuliza hivi jana kazi gani nimefanya ya kunichokesha namna hii?. Hukumbuki kama unapolala muda mwingine wachawi wanakusulubisha kwa kukufanyisha kazi zao bila malipo. Wala huwezi kujijua ndiyo maana ukiamka unajikuta umechoka unashindwa hata kufanya kazi zako binafsi. Lakini kumbuka wachawi wanafanya hayo yote bila faida bali tu kwasababu ya wivu tu. Anasurubishwa pasipo sababu kijana wa watu asiye na hatia. Wakaendelea kumtesa mpaka kufikia hatua ya kuchoka yote hayo kisa utajiri wake ndiyo umemponza.



“Tumuache mtoto wa watu, akapumzike,” Sauti ya Sharifu ya huruma ikasikika kinywani mwake.



“Mbona unataka kuwa mpumbavu au umeridhika kuonyeshwa majivuno” aliongea Binti Mngane kwa kupayuka kwa hasira.



Binti Mngane akakasirika sana na hakutaka kumsikiliza mwanae hata kidogo. Akaendelea kumtesa kijana wa watu kwa kumkomoa, lakini baada ya muda roho ya huruma ikamtanda akaja kukumbuka maneno ya mwanae haraka. Akashirikiana na mwanae kumrudisha huyo kijana chumbani akaendelee na usingizi na wao wakachukua uamuzi wakutoweka pande zile kimiujiza wakatokea ndani ya nyumba yao. Asubuhi ya siku iliyofuata wote wakachelewa kuamka kutokana na uchovu wa jana usiku. Binti Mngane asubuhi ile akaanza kuamka kwa kujivuta kutoka kitandani akatoka nje kufanya shughuli zake za kila siku. Baada ya muda kidogo kupita Sharifu naye akatoka nje na kukuta mama yake anafagia uwanja.



“Shikamoo” alitoa salamu Sharifu kwa mama yake huku akipiga miyayo ya uchovu.



“Marahaba mwanangu,” Binti Mngane aliitika salamu ya mwanae huku akiweka ufagio sehemu husika mara baada ya kumaliza kufagia uwanja.



“Inaonekana, umechelewa kuamka maana kazi zako mpaka saa hizi inakuaga ushamaliza kufanya,” Sharifu alisema huku akilivaa shati aliloshika mkononi.



“Nimechelewa mno kwa kuwa jana nilichoka sana,” Binti Mngane aliongea huku akiingia ndani kwenda kupika uji.



Binti Mngane alipoingia ndani Sharifu akachukua mswaki ambao anatundikaga nje ya kuta yao ya nyumba huku akielekea uani. Alipomaliza akarudi ndani akakuta uji tayari ushaiva na ushatengwa kwenye vibakuli, wakaketi kwenye kirago na mama yake tayari kwa kuanza kunywa.



“Najihisi sipo sawa” aliongea Sharifu mara baada ya kunywa uji kijiko kimoja.



“Unajisikiaje?,” Binti Mngane aliuliza huku akiendelea kunywa uji.



“Mwili unauma, na hata akili yangu kwasasa haijatulia,” Sharifu akaeleza.



“Usiwe na hofu, hiyo hali haina shida lazima itokee kwa maana unapoenda kuwanga mara nyingi unatumia mwili na akili” aliongea Binti Mngane kwa kujaribu kumtoa uoga mwanae.



Binti Mngane akamueleza mwanae kisha akaachilia kunywa uji akaingia chumbani kwenda kuchukua dawa iliyo ya unga mweupe uliyofungwa kwenye karatasi ya kaki. Akachota ile dawa kiasi kupitia vidole vyake viwili dole gumba na husda. Baada ya kuchota akamkabidhi mwanae ili anyunyuzie kwenye uji. Sharifu akapokea dawa kinyenyekevu kisha akanyunyuzia kwenye uji wake na kuanza kunywa. Alipomaliza akaweka kikombe jikoni kwenye vyombo vichafu na hatimaye akaingia chumbani kwake kujilaza. Mchana alipoamka usingizini ndipo akatokea kuamini kuwa kweli ile dawa imefanya kazi yake. Hakusikia tena uchovu wala mwili kuuma, akatoka chumbani akaelekea ukumbini cha kushangaza hakumkuta mama yake ndani. Akajitahidi kumtafuta huku na kule ndipo akaja kumkuta nje nyuma ya nyumba yao tayari amejitandikia mkeka na kujipumzisha.



“Mama,” Sharifu alimwamsha mama yake kwa kumtingisha mwili.



“Eeeh!!!” aliitika Binti Mngane kwa mshtuko na mapigo ya moyo wake yakidunda kwa kasi. Akatulia kidogo akimtazama mwanae kwa jicho kali kisha akasema kwa kigugumizi na huku akihema bila mpangilio.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Kumbe ni wewe, utaniua na presha mwenzio unaona kabisa umri wangu wenyewe ulivyokwenda ukinitoa roho yangu je” alisema Binti Mngane kwa jazba kidogo mara baada ya kujua aliyemshtua ni mwanae.



“Samahani sikuwa na lengo hilo, lengo langu nilitaka kukuhabarisha kuwa kwasasa sisikii uchovu wala maumivu ya aina yoyote tokea unipe ile dawa,” Sharifu alieleza huku akionyesha nyuso ya tabasamu.



“Ile dawa ni nzuri, ndiyo tunayotumia karibia wachawi wote wa chama chetu pindi tusikiapo hali hiyo,” Binti Mngane aliongea huku akijinyoosha miguu.



“Kwanini mama, ile dawa nami sijapewa?.”



“Mzee Damanda anatoa hii dawa kwa kila mwanachama ambaye ni kiongozi wa familia ili ije kutumiwa na mrithi wake,” Binti Mngane akanyamaza kidogo akamsikilizia mwanae atasema nini katika hilo alilolisema, alipoona kimya mwanae ajaongea chochote akaendelea yeye kuzungumza.



“Kwa hiyo wewe kwa kuwa ni mrithi wangu, dawa hii tutatumia wote aina haja kupewa nyingine ukaharibu utaratibu wa kiongozi.”



“Sawa mama...lakini mama leo nakuacha naenda kwa shangazi mara moja kumsalimu,” Sharifu alimuaga mama yake bila kujua mama yake na shangazi yake hawapatani.



**********

Shangazi yake Sharifu anaitwa Leah, alizaliwa baba mmoja na mama mmoja na baba yake Sharifu. Pia walizaliwa wawili tu katika familia yao baada ya kufariki kaka yake katika mazingira ya kutatanisha akabaki peke yake katika ulimwengu wa baradhuri.



“Mkumbuke bwana shangazi yako, siunajua wakati huu yupo mpweke” alisema Binti Mngane kinafki. Kisha akamuuliza swali mwanae kwa kebehi mara baada ya kuagwa na mwanae.



“Kwahiyo, nikuwekee chakula?.”



“Usiniwekee nitakula kwa shangazi, huenda nikakuta chakula huko” alijibu Sharifu kisha akaondoka.



Nyumba ya shangazi yake Sharifu haikuwa mbali na kijiji cha Maharaka, ilikuwa ni kijiji cha pili tu na wala ulikuwa hutembei kilometa nyingi hadi ufike katika nyumba ya shangazi yake Sharifu. Sharifu hakuchukua masaa mengi kufika kwa shangazi yake. Akafika na kumkuta shangazi yake nje ya nyumba yake akisuka mkeka.



“Mwanangu, leo umenikumbuka?” aliuliza Leah mara baada ya kumuona mtoto wa kaka yake.



“Nimekukumbuka shangazi ...................nimeamua nije kukutembelea japo wewe mgumu kuja kwetu,” Sharifu alijibu huku akikaa kwenye mkeka mara baada ya kukaribishwa na shangazi yake.



“Sio hivyo mwanangu, shangazi yako nina majukumu mengi yanayonikabili,” Leah alisema huku akipakaza mate kwa kulamba kidole cha husda kisha akaendelea kusuka mkeka wake. Akasuka kidogo kisha akaachia na kuanza kuongea kwa majonzi.



“Halafu si unajua kuwa nipo peke yangu toka mume wangu afariki, hivyo sina budi kujitafutia pesa ya kukidhi mahitaji yangu ya hapa nyumbani kwa kujiuzia mikeka miwili mitatu.”

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Nimekuelewa shangazi, basi acha kuwa na majonzi” aliongea Sharifu kwa kufariji.



“Sawa lakini mwanangu umekuja wakati umekuta shangazi yako nishakula...vipi ulipotoka umekula?.”



“Nisifiche shangazi yangu, sijaweka kitu chochote tumboni mwangu,” Sharifu alijibu huku akipiga miayo akiashilia njaa.





“Pole mwanangu ngoja nikakupikie chakula maana kuna Vinguruka viwili niliviacha vitakutosha kwa mboga,” Leah alizungumza huku akiinuka na kuelekea jikoni kupika chakula.



Dakika kadhaa ugali ukaiva ukawekwa kwenye sahani kisha ukafunikwa usipoe. Wakachukuliwa Nguruka wakachomwa jikoni. Walipokuwa tayari kuliwa wakawekwa kwenye sahani pembezoni mwa ugali kisha Leah akatoka nje na chakula kwaajili ya kumtengea mtoto wa kaka yake ale. Sharifu baada ya kutengewa hakuchukua muda kumaliza kula, dakika chache tu akawa amemaliza na kutoa vyombo vichafu kisha akavipeleka jikoni. Akarudi kupiga soga na shangazi yake. Akakaa kwa shangazi yake hadi muda wa jioni alipoona muda umekwenda akamuaga shangazi yake na kurudi nyumbani, alipofika nyumbani akamkuta Binti Mngane yupo ukumbini akichambua tembele la mboga ya usiku.



“Mama nimerudi, nahisi ulipooza” aliongea Sharifu kwa utani mara baada ya kuwasili nyumbani.



“Nilipooza sana mwanangu tangu muda ule ulivyoondoka labda ulivyorudi utanichangamsha,” Binti Mngane aliongea huku akionyesha sura ya uchangamfu na kutabasamu kwa mbali.



“Lakini mama unajua kama shangazi analalamika,” Sharifu alianzisha mada iliyomchukiza na kumkera sana mama yake.



“Kuhusu nini?,” Binti Mngane alionyesha kuuliza kwa sauti ya juu sana.



“Kuhusu kumtembelea.”



“Kuhusu kumtembelea!!!, yeye kwani anatutembelea?” aliuliza Binti Mngane kwa ghadhabu kubwa.



“Lakini mama tusimlaumu bure, yeye unajua fika tokea afiwe na mumewe majukumu yote yanamwelemea,” Sharifu alimtetea shangazi yake.



“Naona siku hizi mwenzangu, ushakuwa mwanasheria wa kutetea watu,” Binti Mngane alisema huku akinyanyuka kwenye mkeka na kwenda jikoni kupika mara baada ya kumaliza kuchambua matembele.



Sharifu kwa kuona wakuongea naye kaenda kwenye shughuli yake akaingia chumbani kwake naye kujipumzisha mwili. Baada ya masaa kadhaa chakula kikawa tayari Binti Mngane akakitenga ukumbini kwenye mkeka kisha akaenda kumuita mwanae waje kula.



“Sharifu baba,” Binti Mngane alimuita mwanae kwa upendo.



Ukweli kabisa Binti Mngane anampenda mwanae kwa kuwa wakati wa kumleta duniani alimpatia shida sana. Nusu afe wakati anajifungua na pia mwanae huyo ndiye aliyesababisha kizazi chake kuondolewa na kushindwa kupata watoto tena, hivyo ndiyo maana anampenda mwanae kupitiliza kama yai vile.



“Naam,” Sharifu aliitika kwa sauti ya juu pindi alivyoitwa na mama yake kisha akanyanyuka kitandani akaenda kufungua mlango atoke chumbani akajumuike na mama yake.



“Chakula tayari njoo tule, nikalale mapema,” Binti Mngane alisema huku akiongoza ukumbini.



Mama na mwana wote kwa pamoja wakajumuika kwenye chakula cha usiku. Walikula na walipomaliza Binti Mngane akaaga kuwa anakwenda kulala. Akaenda kulala huku nyuma akimuacha mwanae akitoa vyombo walivyolia na kupeleka jikoni. Mara baada ya kutoa vyombo Sharifu naye akaingia chumbani kujilaza kitandani, mwanga hafifu wa koroboi ukamfanya Sharifu kudondila kama kuku wa mdondo baada ya kujilaza. Usingizi palepale ukampitia alikuja kushtuka muda mwengine kabisa wa usiku ambao uliokuwa umejaa giza totoro na huku sauti za ndege wa ajabu zikilindima huku na kule. Sharifu katika kushtuka haraka haraka akajifunga usongo kwenye paji la uso kisha akavaa kaniki nyeusi kiunoni na uso wake papo hapo ukabadilika ukawa na unga mweupe. Alipohakikisha kamaliza kujiandaa akatoweka kimiujiza na kwenda moja kwa moja hadi kwenye nyumba ya jirani yao. Dhumuni ya kwenda huko ni kumdhuru kijana mmoja ambaye huwa analima na kusoma kwa bidii na pindi msimu wa mavuno unapofika huwa anapata mavuno mengi pale kijijini kushinda vijana wenzake wote. Kutokana na bidii yake shuleni na shambani Sharifu akatokea kuweka wivu kwa huyo kijana hivyo http://deusdeditmahunda.blogspot.com/hakutaka kumuacha salama. Akatokea chumbani kwa yule kijana na kumkuta kitandani kalala usingizi wa pono polepole akatoa kichupa kidogo cha rangi ya Gold kilichojaa maji ya betri. Akammiminia kijana wa watu machoni punde tu akatoweka akatokea chumbani kwake pembezoni mwa ukuta wake wa chumbani. Chapuchapu akajibadili kimiujiza muonekano wake kisha akaendelea kurudi kulala. Asubuhi na mapema majogoo ya alfajiri yakamwamsha kwa kuwika bila kikomo taratibu akajikongoja kutoka kitandani moja kwa moja akaenda kupiga mswaki. Alimaliza na kuelekea bustanini kwake huku akiwa na jembe lake mkononi kwenda kuchuma mbaazi kwa ajili ya mboga. Hakuchuma mbaazi peke yake pia akachimba na mihogo kwaajili ya kunywea chai ile asubuhi. Aliporudi ndani akaimenya mihogo kisha akabandika jikoni, nyakati ya masaa mawili mbele naye Binti Mngane akaamka na kumkuta mwanae kashaivisha chakula na kuitenga kwenye mkeka.



“Hujambo,” Binti Mngane alimsalimu mwanae huku akifunga kiremba chake cha mtelezo. Sharifu akaitika ile salamu kisha kumpa heshima mama yake.



“Marahaba...hongera.”



“Ya nini?.”



“Kwa kuwahi kuamka leo mapema.”



“Ooh kumbe...asantee” alitoa shukrani Sharifu kisha akaendelea na kula mara baada ya kutenga mihogo na kujumuika kwa pamoja.



**********

Kijana aliyemwagiwa maji ya betri alipoamka akashtuka sana kuona macho yake yana kasoro yalikuwa hayaoni chochote zaidi ya giza. Alipoona ile hali akapayuka kumuita mama yake kwa sauti ya juu ili aweze kusikia. Mama huyo aliposikia kupayuka kwa mwanae hakuchelewa kufika chumbani kwa mwanae akaone kilichotokea.



“Nini kilichokupata?,” Mama yule aliuliza kwa hofu.



“Mama, sioni,” Kijana yule alimwambia mama yake huku machozi yakimtiririka.



“Kwanini unasema hivyo...na unamaanisha nini?,” Mama yule aliuliza huku akijitahidi kumfuta machozi mwanae.



“Mimi ni kipofu, siwezi kuona tena,” Kijana yule alieleza kwa nyuso ya huzuni.



“Kipofu!!!...huo ukipofu umeanza lini?,” Mama yule aliuliza huku akiwa aamini anachoelezwa na mwanae.



“Imenianza asubuhi hii,” Kijana yule alisema huku akijaribu kunyanyuka kitandani atembee.



Alipojaribu kutembea akaenda kupalamia kisturi kilichokuwa mbele yake. Hapo ndipo mama wa yule kijana akaamini kama kweli mwanae aoni. Hakutaka tena kuchelewesha muda kwa kumhoji mwanae akamkokota taratibu mwanae na kumwaisha hospitali akafanyiwe vipimo na kupata matibabu pale tatizo litakapoonekana. Alipofika hospitali akaingia na mwanae moja kwa moja kwenye ofisi ya daktari mwanae akapimwe. Yule kijana alipopimwa macho ikagundulika kuwa macho yake hayana matatizo yoyote. Jambo lile likamstajabisha yule mama pamoja na mwanae moja kwa moja yule mama akajua mwanae karogwa si bure. Ikabidi akubaliane na vipimo vya daktari hivyo bila kizuizi akamchukua mwanae kisha wakaondoka kinyonge pale hospitalini.



**********

“Na leo, yaani umenifurahisha sana” alizidi kuongea Binti Mngane kwa kumpa pongezi mwanae.



“Kivipi?,” Sharifu aliuliza huku akitoa tabasamu mwanana kinywani mwake.



“Kwa kunisaidia kupika, kifungua kinywa.”



“Oooh, siku moja moja niwajibu wangu kukusaidia,” Sharifu alizidi kuongea huku akichukua kipande cha mhogo na kula.



“Kweli kabisa, siku moja moja yakupasa unisaidie nami mama yako nipumue,” Binti Mngane alisema huku naye akiendelea kushindilia mihogo kinywani.



“Sawa...lakini mama, mbona leo ulilala kama mfu?,” Sharifu akauliza.



“Kwanini?,” Binti Mngane naye akauliza badala ya kujibu swali la mwanae.



“Nilikuamsha ili twende ukanipe ushirikiano, lakini hukuamka.”



“Nilichoka sana...kwani ulitaka ushirikiano upi?.”



“Wa kwenda, kumshikisha adabu mtoto wa jirani yetu,” Sharifu alijibu huku akichota maji ya kunywa kwenye mtungi.



“Mtoto wa jirani yetu!!!, yupi?,” Binti Mngane alimuuliza mwanae kwa kutaka kujua.



“Yule Issa, mtoto wa Mama Zakia.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



“Aaah, nishamjua kumbe yule kijana?.”



“Eeeh.”



“Kisa nini, cha kumshikisha adabu mtoto wa watu?.”



“Ana majivuno...nami watu wenye majivuno siwapendi hata kidogo,” Sharifu akaongopa.



“Mh...ikawaje?.”



“Nilimmwagia maji ya betri machoni,” Sharifu alieleza huku akionyesha tabasamu pana kwa kuona kitendo alichofanya ni sahihi.



“Mh, mbona umemfanyia ubaya mkubwa mtoto wa watu?,” Binti Mngane aliuliza na kuonyesha kitendo alichokifanya mwanae ajapendezwa nacho.



“Kama nilivyosema mwanzo kuwa majivuno yake, ndiyo yaliyonifanya nimshikishe adabu.”



“Aisee, siku hizi umejivika roho ya ujasiri au unataka Mzee Damanda akupe vyeo?,” Binti Mngane aliuliza huku akimkazia macho mwanae.



“Cheo lazima nitapata na nitakuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa wanachama wenzangu,” Sharifu alisema kwa utani huku akitoa vyombo mara baada ya kumaliza kula.







“Binti Mngane shibe ilimlevya akaona uvivu kuendelea kufanya kazi. Akajipumzisha kwenye mkeka kidogo pale pale ukumbini. Sharifu alipomaliza kuviosha vyombo akavirudisha jikoni kisha akaingia chumbani kwake kujipumzisha, muda wa jioni ya saa kumi alikuwa kashaamka akajikongoja kwa kutoka hadi ukumbini, akamkuta mama yake bado yupo akiendelea kuchalaza usingizi. “Mama



*****************

************************



Binti Mngane alipomaliza kutoa risala kwa mwanae akatoka nje kuchuma maboga na akachukua fursa ya kumpisha mwanae aendelee na usafi. Dakika kadhaa zikapita Sharifu alimaliza kufagia ndani akachukua mswaki kisha akatoka nje kusafisha kinywa. Binti Mngane alipomaliza kuchuma maboga akarudi ndani na hatimaye kuelekea jikoni kupika maboga yale. Binti Mngane akayaandaa maboga kwenye sahani kisha akayatenga kwenye mkeka ukumbini na kumuita mwanae mara baada ya maboga kuiva.



“Sharifu.”



“Naam.”



“Bado, ujamaliza tu?.”



“Namalizia.”



“Hebu fanya haraka uje tule chakula kitapoa.”



Sharifu akapiga mswaki haraka kisha akarudi ndani kuungana na mama yake kula. Hawakuchukua muda mwingi kwenye kula dakika kama tano wakawa washamaliza kula.



“Ukimaliza kutoa vyombo nakuomba nikutume ukanichukulie pesa zangu” aliongea Binti Mngane mara baada ya kumaliza kula.



“Kwa, nani?,” Sharifu akauliza alipofika jikoni.



“Kwa, Mama Stumai.”



“Haina shida...lakini nitachelewa kurudi.”



“Kwanini?.”



“Nitapitia kwa Kondo, kuchukua mpini wangu wa jembe.”

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Usijali, pesa hiyo sina shida nayo kwa sasa...wewe pitia tu,” Binti Mngane aliongea huku akijaza maji kwenye ndoo ya uhani akaoge.



Sharifu akaingia chumbani kwake kubadilisha nguo mara baada ya kupeleka vyombo na kutoka nje tayari kwa kuanza safari ya kwenda kwa Mama Stumai. Akiwa njiani kabla hajafika alikotumwa akakutana na Mama Abuu jirani yao aliye na ujauzito wa miezi nane tumboni.





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog