Simulizi : Niliwaroga Walimu Mpaka Basi
Sehemu Ya Tatu (3)
Muda wa kurudi nyumbani ulipofika tuliruhusiwa kuondoka. Nilipofika nje ya nyumba yetu nilijiangusha na kuanza kulia kwa sauti. Mama alitoka mbio, aliponiona alinifuata na kuniinamia akiuliza:http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Mwanangu umekumbwa na nini?”
Nilijishika makalio huku nikiendelea kulia.
“Yamefanyaje?” mama aliniuliza huku akinisimamisha, nikamwambia kuna mwalimu amenichapa fimbo.
“Mwalimu akuchape wewe na fimbo, amekuzaa?” mama alikuja juu.
“Amekuchapa fimbo ngapi?”
“Kumi na mbili mama.”
“Ha! Ha! Ha! Mwanangu mimi, achapwe fimbo kumi na mbili na mwalimu wake, sikubali hata kidogo.”
Nilidhani mama atasema twende hukohuko shuleni akapambane na huyo mwalimu lakini sivyo, akasema:
“Huyo leo ana mimi, lazima na yeye nimchape viboko vyake ishirini na nne muwe sawasawa.”
“Nitafurahi sana mama,” nilisema huku nikijifuta machozi na kuingia ndani na mama.
***
Usiku uliingia, tukala, kisha tukakaa sebuleni kuongea. Mama alikuwa akinisimulia hadithi mbalimbalai za zamani huku mimi nikicheka. Ghafla, kwenye saa tano huko alisimama na kusema tukalale. Lakini akaongeza:
“Usilale sana mwanangu nitakuja kukuchukua twende kwa mwalimu akapate viboko vyake.”
“Sawa mama.”
Nilikwenda kupanda kitandani, nikapitiwa na usingizi. Niliamshwa na mama kwenye saa nane usiku. Alisimama chumbani kwangu, mkononi alishika fimbo nyingi sana.
“Twende sasa mwanangu, muda umefika,” mama aliniambia kwa sauti ya upole.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Niliamka kutoka kitandani, nikashusha miguu chini na kuanza kutembea kuelekea sebuleni ambapo mama alikuwa amenitangulia.
Pale sebuleni, mama aliusogelea ukuta mkubwa na kusimama akiutazama. Na mimi nikamfuata, nikasimama nyuma yake. Aligeuka kuniangalia, alipojiridhisha nipo, alipiga kofi ukuta, kufumba na kufumbua tukawa tupo nje ya nyumba ya Mwalimu Cecilia.
Hapa niseme kidogo, uchawi wetu mimi na mama ulikuwa wa kisasa zaidi. Tulikuwa tukitaka kutoka nyumbani, nguo tulizovaa zinajivua zenyewe, tukirudi zinajivalisha tena. Kwa hiyo mama alipopiga ukuta, nguo zetu zilijivua palepale, ina maana sisi tulitoka uchi wa mnyama.
Basi, tulifika nje ya nyumba ya Mwalimu Cecilia, mama akapiga kofi mlango, ukafunguka na kuzama ndani. Kule ndani tulitokea sebuleni. Mama akasimama na kunyoosha mkono huku akizunguka, akafika mahali akaganda, akasema:
“Huku ndiko chumbani kwake.”
Hapo alikuwa amenyoosha mkono kuelekea kwenye mlango mmoja wenye pazia limeandikwa maandishi ya kufuma yanayosomeka: Muomba Mungu Hachoki
Tulielekea kwenye huo mlango. Mama akaupiga kofi tukazama ndani.
Mama alisimama katikati ya chumba akainua mkono juu. Midomo ilionekana kusema maneno fulani, mara mkononi kwake kukajaa fimbo kama kumi hivi.
Alichukua moja akanipa na kuniambia nianze kumchapa mwalimu yule. Nilifanya hivyo. Lakini mwalimu mwenyewe kwa wakati ule alikuwa amelala chali. Kwa hiyo kabla sijaanza kumchapa mama alikwenda akamfuta macho kwa kiganja cha mkono wake wa kushoto, mwalimu akageuka na kulala kifudifudi.
Nilianza kumtandika. Nilimchapa mwalimu akawa analalamika huku akijishika makalio kwa maumivu makubwa. Mama aliniambia nikazane kumchapa, nilimchapa sana.
Mwalimu Cecilia aliendelea kulalamika huku mimi nikizidi kumchapa. Fimbo ya kwanza iliisha, mama akanipa nyingine, nikaendelea na adhabu yangu kwa mwalimu. Lakini nilikumbuka kwamba, mama alisema atampa mwalimu huyo fimbo kumi na mbili. Kwa wakati huo zilifika hata mia.
Nilianza kuingiwa na huruma, kwani nilihisi makalio ya mwalimu yalianza kuvimba kwa kuchapwa. Nilimwangalia mama kwa ishara ya kumuuliza niendelee au niache, akaninyanyulia mkono juu akinihimiza niendelee kumchapa.
Ghafla mama akanishika mkono kisha akaninyang’anya fimbo. Nilijua sasa basi, kumbe alitaka iwe zamu yake. Alimchapa sana Mwalimu Cecilia huku akisema ni kwa nini amekuwa akinionea.
Mwalimu hakuwa anajibu kwa sababu hakujua kinachoendelea. Yeye alikuwa akitesekea usingizini kama ndoto lakini maumivu yalikuwa ya kweli.
Mama alimchapa zaidi kuliko mimi. Nilianza kuona damu inachuruzika sehemu ya makalio, nikajua mama ameshamuumiza mwalimu. Mama naye aliiona ile damu, akaacha kumchapa lakini huku akitingisha kichwa kama anayekubaliana na kipigo alichompa.
Tulitoka kurudi nyumbani, kila mtu aliingia chumbani kwake.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Asubuhi na mapema, mama alikuwa wa kwanza kuamka, akaja kuniamsha na kuniambia nisije nikachelewa shule nikapigwa. Usingizi ulikuwa bado kwani safari ya usiku kwa Mwalimu Cecilia ilinifanya nichelewe kulala.
Nilifika shuleni kwa muda mwafaka, nikawa naangaza macho kila upande kama nitamwona Mwalimu Cecilia, lakini sikumwona. Nilijikuta nikimwambia mwanafunzi mmoja:
“Mwalimu Cecilia hawezi kuja leo.”
“Umejuaje?” aliniuliza yule mwanafunzi lakini sikumpa jibu maana nilijishtukia kwamba nilichokifanya sicho.
Tulifanya kwanza usafi kisha baadaye tukapigiwa kengere na kwenda mstarini kwa ajili ya kuingia madarasani kuanza masomo.
Tulipoingia tu darasani, mwalimu wa somo la kwanza alikuja. Lakini alisahau kitabu kimoja kwenye ofisi ya walimu, akanituma mimi niende kumchukulia kwenye meza yake.
Nilipofika kule, mwalimu mmoja akaniuliza ninachokitaka, nikamwambia kitabu cha Mwalimu Paschal. Aliangalia mezani kwa mwalimu huyo na kuniambia kile cha kijani pale.
Wakati nakifuata kitabu hicho, Mwalimu huyo akasema:
“Basi unaambiwa ameamka asubuhi ya leo makalio yote yamechanika na vidonda juu. Huko alipo hawezi kusimama wala kukaa. Ni maumivu tu. Wachawi bwana.”
Mwalimu mwingine aitwaye Mage akadakia:
“Tena nasikia wachawi wanaweza kukuchukua ukaenda kulima. Mimi kuna dada’angu alichukuliwa na wachawi akaenda kulimishwa shamba kubwa, alipoamka asubuhi alikuwa amechoka mwili wote, hana hamu nao.”
Mwalimu mwingine akadakia pia:
“Sasa hao wachawi wampige bakora Mwalimu Cecilia shida yao nini hasa? Au wanamuona anaringa mtaani?”
Mara akadakia mwalimu mwingine na kusema:
“Mchawi hana sababu. Lakini mwenyewe nilipoongea naye kwenye simu amesema ataenda kwa mganga ili awatoe roho waliomchezea, hivi pale alipo anasubiria kupona tu.”
Niliondoka kwenye ofisi hiyo nikiwa na jibu kamili. Na utabiri wangu ulitimia hapo. Kwamba Mwalimu Cecilia asingefika shuleni siku hiyo.
Wasiwasi wangu mkubwa ulikuwa juu ya tamko la mwisho la yule mwalimu aliyesema hivi:
“Mchawi hana sababu. Lakini mwenyewe nilipoongea naye kwenye simu amesema ataenda kwa mganga ili awatoe roho waliomchezea, hivi pale alipo anasubiria kupona tu.”
Nilijikuta nikiogopa. Nilijua Mwalimu Cecilia anataka kuniua mimi na mama. Hivyo nilisoma kwa tabu sana siku hiyo. Akili yangu yote ilitaka nirudi nyumbani kumwambia mama juu ya madai ya Mwalimu Cecilia kutaka kutuendea kwa mganga. Nilijua mama angekasirika sana na pengine usiku wa siku hiyo tungerudi tena nyumbani kwake kumfanyia kitu kibaya zaidi.
Muda wa kutoka shuleni ulipofika naweza kusema mimi nilikuwa mwanafunzi wa kwanza kuwa mbele ili niwahi nyumbani. Baadhi ya wanafunzi wanzangu walinishangaa, wengine waliniita lakini sikugeuka kuwasikiliza, moyoni nilisema si wao tu, hata kama mwalimu mkuu ndiyo angeniita nisingegeuka. Kufika nyumbani niliita mara mbili bila kumsikia mama akiitika. Nikaita mara ya tatu, nikasikia akiitika kwa sauti nzito sana kama ya kiume na mwanaume mwenyewe mzee, lakini mwenye nguvu zake. “Unasemaje wewe?” Sauti hiyo ilitokea chumbani kwake , nikaingia bila kupiga hodi. “Mama. Nasikia Mwalimu Cecilia amepanga kutuendea kwa mganga wa kienyeji.” “Kwa ajili gani? We umesikia kwa nani?” “Nimesikia walimu wakisema, kwa sababu tumemchapa fimbo usiku.” “Hao walimu wamejua ni sisi?”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ “Hapana, hakuna aliyesema ni sisi, ila nimemsikia mwalimu mmoja akisema Mwalimu Cecilia amesema atakwenda kwa waganga ili awashughulikie wachawi waliomchapa usiku.” Mama alicheka sana, alicheka mpaka akakaa chini. Hapo alikuwa na sauti yake ya kawaida na nilikuwa nataka tumalize hili ili nimuulize kisa cha kunitolea sauti nene kama ile. Alipomaliza kucheka mama alisema: “Namtaka huyo mwalimu aliyesema. Na yeye leo itakuwa zamu yake, sitaki ujinga mwaka huu.” “Ah! Mama! Yaani Mwalimu Cecilia tumemshughulikia, sasa unataka na mwalimu huyu naye?” “Ndiyo, tena lazima leoleo ashughulikiwe.” “Mama, mimi naogopa sana,” nilijitetea, lakini mama akaja juu akisema ni lazima akale fimbo yule mwalimu. Lakini ghafla akaniuliza: “Kwanza hebu nipe maelezo kamili yalivyokuwa mpaka ukajua hilo suala la huyo mwalimu kwenda kwa mganga wa kienyeji.” Niliamua kumsimulia mama kwa kuanza kumwambia kuwa, niliingia ofisi ya walimu, nikamsikia Mwalimu Paschal akisema kuwa,http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ Mwalimu Cecilia aliamka asubuhi ya leo makalio yakiwa yamechanika na vidonda juu. Huko nyumbani kwake alipo hawezi kusimama wala kukaa. Ni maumivu tu. Akasema wachawi bwana! Mama akaniuliza, sasa kwa kusema hivyo ndiyo ameahidi kutuendea kwa mganga wa kienyeji? Nikamwambia asubiri kwanza nimalize mazungumzo. “Haya mwanangu, nakusikiliza, malizia basi.” “Mwalimu mwingine anaitwa Mage akadakia, akasema, ‘tena nasikia wachawi wanaweza kukuchukua ukaenda kulima. Mimi kuna dada ‘angu alichukuliwa na wachawi usiku akaenda kulimishwa shamba kubwa, alipoamka asubuhi alikuwa amechoka mwili wote, hana hamu nao.’ “Sasa hapo ndiyo ina maanisha watatuendea kwa mganga mwanangu?” alidakia tena mama. “Mama, subiri kwanza nimalize.” “Haya binti yangu, sema mpaka mwisho sasa.” “Kuna mwalimu mwingine pembeni akadakia, akauliza, sasa hao wachawi wakampige bakora Mwalimu Cecilia shida yao nini hasa? Au wanamuona anaringa mtaani?’ “Yule Mwalimu Paschal naye akajibu, akasema, ‘mchawi hana sababu. Lakini mwenyewe nilipoongea naye kwenye simu amesema ataenda kwa mganga ili awatoe roho waliomchezea, hivi pale alipo anasubiria kupona tu.’” Mama alicheka tena huku akisema: “Huyo Mwalimu Paschal usiku wa leo tunaye. Tena nataka wewe mwanangu ndiyo uifanye kazi hiyo. Tutakwenda wote, lakini tukifika, mimi nitabaki nje, wewe utaingia ndani. Ukifika umchape mpaka wewe mwenyewe uridhike, sawa?” “Sawa mama.” Tuliendelea na mambo mengine ya nyumbani. Mama aliniambia usiku wa siku hiyo mimi ndiyo niende kumwamsha kwa ajili ya safari ya kwa Mwalimu Paschal. Mimi siku hiyo ndiyo nilitangulia kwenda chumbani kwangu. Nilipopanda kitandani sikuchukua muda mrefu, usingizi ukanipitia. Niliamka nikiwa najisikia nashikwashiwa miguu, nikashtuka. Kuangalia hivi kumbe mama. “Mbona hujaamka, utaiweza kazi hii kweli?” “Nitaiweza mama,” nilimjibu huku nikinyanyuka kitandani. Alinishika mkono kama anayenipokea. Tukatoka nje ambako mama aliniamuru mimi ndiyo niongoze safari ya kwenda kwa Mwalimu Paschal. Ilikuwa kufumba na kufumbua, tulitua nje ya nyumba ya mwalimu huyo. Hali ya hewa ilikuwa ya upepo mkali kila kona. Tulitembea kuelekea upande wenye mlango mkubwa, tukaingia ndani huku mimi nikiwa mbele ya mama. Ghafla mama akanishika mkono, nilipogeuka akaniambia: http://deusdeditmahunda.blogspot.com/“Mimi nakusubiri nje, hakikisha unamshikisha adabu huyo mwalimu.” Nilimwitikia kwa kutingisha kichwa kisha nikaendelea kwenda ndani, mama akarudi nje. Nilisimama sebuleni, nikaangaza kulia na kushoto kisha nikanyoosha mkono mbele ili kupata mwelekeo wa chumba cha mwalimu huyo, nikabahatika kukipata. Nilikwenda kusimama mlangoni, nikapiga mlango kwa kofi moja tu, ukafunguka wenyewe. Nilipoingia ndani, hakuwepo Mwalimu Paschal wala mdogo wake achilia mbali binadamu mwingine yeyote yule. Nilisimama nikiwa nimechoka sana, nikapiga mwayo mmoja na kutoka nje. Nilimkuta mama amekaa kwenye jiwe, aliponiona akasimama ghafla. “Imekuwaje?” “Hayupo.” “Haweizekani!” “Kitandani hamna mtu mama.” “Hata mke wake?” “Hata nduguye. Kitanda cheupe.” “Sasa umeshindwa kupata mwelekeo wa mahali alipo?” “Nilitaka kusikia kwanza wewe unasemaje?” “Mtafute haraka sana.” Nilisimama, nikanyoosha mkono ili kupata mweleko wa alipo Mwalimu Paschal
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment