Search This Blog

TROPEA MJI WA WAFU - 5

 






Simulizi : Tropea Mji Wa Wafu
Sehemu Ya Tano (5)






Hayo yalipopita alionekana Bingo na Michael wakiwa kwenye moja ya ukumbi wakipata chakula baada ya mpambano.

"Bingo.. Unajua kwa sasa kila sehemu unazungumziwa wewe?.." Aliongea Michael.

"Hahaha hahahah.. Najua yote sababu ya kile nilicho kifanya ila kwa kuwa tayari nimejitoa muhanga kwenye hili jambo basi nitapambana mpaka hatua ya mwisho.."http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Safi sana kijana, lakini mbali na upiganaji wako. Kuna maneno ambayo umeyaongea, hakika ulionyesha ushupavu Bingo. Hongera yako jamaa" Aliongeza kusema Michael, maneno ambayo yalimfurahisha sana Bingo. Muda huo nje kulikuwa na wafu wengi wakigombea kumuona Bingo. Bingo alishangazwa na jambo hilo lakini muda huo huo ndani humo aliingia Roya huku akionyesha mtu mwenye tabasamu pana. Roya alizipiga hatua kumsogelea Bingo, alipomfikia akamwambia "Tayari upo ndani ya Tropea Bingo, hongera kwa kufanya vizuri kila hatua. Na pia siku ya leo ndiyo siku ambayo unatarajia kwenda kuonana na baba yako. Sultan Abatish"

"Roya nashukuru saba, ndio nafurahi uwepo wangu huku Tropea kwani najua kurudi kwangu duniani ndio kutampelekea mama yangu kupona.." Alijibu Bingo wakati huo akikunjua miguu yake ambayo alikuwa amekaa style ya nne. Roya alicheka kwanza kisha baadae akajibu" Bingo hebu acha kunichekesha bwana.. " Alisimama Bingo kisha akahoji" aunamaana gani Roya, je wataka kuniambia ahadi mliyoniahidi haitotimia?.. "

" Hapana Bingo wala Sina maana hiyo, lakini mbona ameshapona? Yani siku ile uliyoanza safari ndio siku ambayo mama yako alipona maradhi. Kwa maana hiyo basi wewe ni wa kwetu kamwe hutoweza kurudi duniani " Alisema Roya, safari hiyo akiwa amebadilika asiwe na hata chembe ya asiri ya binadamu. Bingo alishtuka, hakuyaamini yale ayasikiayo. Ghafla akajihisi kuishiwa nguvu ilihali kijasho chembamba kikimtoka. Pumzi ndefu alishusha wakati huo akijitazama mwilini, machozi yalimtoka hasa baada kujigundua kuwa hapo alipo ni nafsi ila mwili upo duniani. Na endapo mwili huo utazikwa basi habari yake itakuwa imekomea hapo.

"Inamaana kuwa huu ulikuwa mtego?.." Alijiuliza kijana Bingo ndani ya akili yake. "Laah! Hapana sasa inatakiwa kubadilisha maamuzi... Lazima nirudi duniani.." Aliongeza kujisemea hivyo Bingo wakati huo huo akiingiza mkono mfukoni kuchukua ramani yake ili ajihakikishie safari yake ya kurudi duniani. Lakini ajabu alipoitoa ramani hiyo aliona hakuna mahali palipochorwa zaidi ya karatasi kuonekana tupu..





Bingo alishangaa sana baada kuona mchoro wa ramani umetoweka kimiujiza, akawaza ni vipi atafanikiwa kuondoka hapo Tropea kwenye mji huo wa wafu pasipokuwa na ramani yake. Lakini wakati anatafakari suala hilo ghafla aliwekwa chini ya ulinzi akafungwa nyororo miguu mwake kisha akapelekwa kwenye chumba mahususi chumba ambacho muda wote kilikuwa kimya huku kikinukia marashi ya udi na ubani. Bingo aliwekwa humo. Punde Roya akatokea humo ndani, akaangua kicheko kisha akasema "Bingo maisha ya huku raha sana, nakushangaa unang'ang'ana kurudi duniani, wakati dunia ni sehemu iliyojaza shida za kila aina. Huku Tropea hakuna kuumwa wala hatuna shida ya utajiri sababu kila kitu kipo. Na endapo kama utakubali kuishi huku basi mali zote za Tropea zitakuwa chini yako... "

" Roya, kwanza siamini kama ni wewe ambaye umeniingiza mkenge, haya hayakuwa makubaliano yetu. Sasa iweje niishi huku?.. "Alijibu Bingo huku akiwa amemkazia sura mwanadada huyo aitwae Roya.

" Ahahah ah hahaha ha " Roya alicheka kisha akaongeza kusema" Pole sana ila huu ndio ulikuwa mpango wetu,uwezo wa wewe kuja huku bila kupata misukosuko ungewezekana ila tuliamua upite njia ya misukosuko ili kupima uwezo wako na ndio maana tulikupa ramani ili ikupitishe huko tulipopataka sisi. Kweli hatimaye ukavuka vigingi, kwa maana hiyo wewe ni kidume na unafaa kuongoza jeshi la Tropea ambalo lipo katika kampeni kubwa ya kuimalisha ngome yake "

" Sipo tayari.. Nasema sipo tayari ni bora mniue kuliko kuendelea kuishi huku"Alifoka Bingo, muda huo mlango wa chumba hicho ulifunguka, akaingia mzee wa makamo ambaye ulionekana kutisha kwa muonekano wake. Mzee huyo alikuwa na vichwa viwili. Kichwa kimoja cha kawaida na kingine kilikuwa upande wa bega la kulia. Macho yalishabiana vema na macho ya nyoka hali ya kuwa upande mmoja wa mwili wake ilionekana mifupa ya mbavu iking'aa mithili ya dhahabu. Mzee huyo alikuwa ameketi kwenye kiti maalumu chenye magurudumu.

"Bingo mwanangu" Mzee huyo aliongea. Sauti yake ilikuwa nzito sana. Sauti ambayo ilimfanya Bingo kustuka ingawa alitulia na kisha kumsikiliza ili ajue kipi kitajili hapo.

"Safi sana kwa kutii agizo la baba yako, nadhani tayari vita hii imekuwa rahisi kwangu kwa sababu taarifa zako nimezipata zamani sana tangu sikuile uianze safari ya Tropea.. Bingo wewe ndio mwanangu ninaye kukubali na ndio maana nimepanga kukukabidhi Tropea ili uiongoze.. "

" Sipo tayari.. "Alijibu Bingo. Jibu hilo lilimshangaza Sultan Abatish, ndipo akamuuliza" Unamaana gani?.. " Bingo hajajibu, ambapo hapo ndipo Sultan Abatish alipoamua kupotea. Lakini licha ya kutoweka, ilisikika sauti yake ikisema" Hapa ndio Tropea, kuingia ni rahisi ila kutoka ni vigumu.. Bingo wewe ndio mrithi wa mji huu, ondoa vikra za kurudi duniani. Haha hahaha hahaha "Ilimaliza kwa kicheko sauti hiyo.

Hali hiyo ilimfanya Bingo kuwa na hofu dhofu lihali,mawazo chungu nzima yalitawala kichwa chake. Akiangalia ramani imetoweka, lakini pia maneno aliyoambiwa kuwa kuingia Tropea rahisi kuliko kutoka, nayo vile vile yalimtisha sana kwa sababu alipata tabu wakati wa kuja, tabu ambayo haikuwa rahisi kuivuka.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Unamaana kwamba kurudi ndio kuna shida zaidi ya zile nilizopata?.." Alijiuliza Bingo. Ila wakati suala hilo liliendelea kupasua kichwa, upande wa pili. Ngome ya Sultan Abatish inapokea taarifa kutoka kwenye ngome ya Sultan Starlon. Taarifa hiyo ilieleza kuwa unahitajika mpambano wa wafuasi kwa wafuasi.

" Hili suala kwa upande wetu ni gumu sana, hatuwezi kulikubali kwa sababu bado Bingo hajakaa kwenye mstari ulio nyooka. Hivyo mara moja taarifa hii ipuuzwe.." Aliongea kiongozi msaidizi wa ngome ya Abdy iliyopo chini ya Sultan Abatish. Hivyo kibaraka mmoja akaagizwa kupeleka jibu, alichukuwa farasi wake kisha safari ya kuelekea kwenye ngome ya Sultan Starlon ikaanza. Ngome hiyo ilijaza watu katili sana, kwani kibaraka huyo kutoka ngome ya Abatish hakuweza kurudi aliuliwa huko huko na kisha kugeuzwa kitoweo. Walikula na kufurahi,.. Kiongozi wao alisikika akisema "Ndio maana ngome ile naitamani sana, tazama chakula cha huyu mtu kilivyokuwa kitamu..."

"Ahahaha hahaha ah.." Wote walicheka kisha shughuli ya kuendelea kupata chakula ikaendelea.

Upande wa pili, kiongozi msaidizi ndani ya ngome iliyopo chini ya Sultan Abatish, ghafla akaingiwa na hofu juu ya kibaraka wake aliyemuagiza kwa Starlon. Na hivyo hakutaka kuzihukumu mapema hisia zake, ndipo alipoamua kuchukuwa jukumu la kumfuatilia yeye mwenyewe katika ngome ile. Alipofika alikuta lango la lipo wazi,,aliingia bila wasi wasi wowote. "Ni kipi ulicho sahau, au na wewe unataka kugeuzwa chakula siku hii ya leo?.." Mmoja ya wafuasi waliopo ndani ya hiyo ngome alisikika akisema hivyo. Jamaa huyo, kiongozi msaidizi wa ngome ya Sultan Abatish ambaye aliitwa Yuli alicheka kisha akajibu "Hiyo itakuwa ni hadithi. Kwahiyo wataka kunimbia kuwa mtu wangu kageuzwa kitoweo?.."

"Ahahaha hahahah" Mfuasi huyo alicheka sana halafu akamwambia "Hilo ndilo jibu.. Kajipange upya, na tena kawambie wenzako,wakati wowote wategemee ghalika kubwa.."

"Karibuni sana.." Yuli alijibu kisha akampindua farasi wake, safari ya kurudi kwenye ngome yao ikaanzia hapo.

Alipofika alionekana ni mtu mwenye hasira mno, hivyo ikabidi akaongee na Sultan Abatish kwa dhumuni la kumwambia kile kilichojili mara baada kukataliwa takwa waliloleta maadui zao. Habari ya kuwawa mfuasi wake kiukweli ilimuumiza sana Abatish, na hapo akaita askari wake baadhi, askari ambao waliongozwa na mwandada Roya.

"Roya.. Tayari bwana Starlon ameanza kuchochea moto. Hivyo basi nawapa kazi moja. Fanyeni juu chini Bingo akubali matakwa yangu, iwe kwa kipigo aidha kwa vyovyote vile ilimladi asalie Tropea. Baada ya hapo sasa mpambano yaanze"

"Sultan Abatish, unadhani bila huyo Bingo vita hii hatuiwezi?.." Aliuliza Yuli kiongozi msaidizi katika ngome hiyo.. Abatish hakumjibu swali hilo zaidi alipotea maeneo hayo..ilihali muda huo huo Roya na jeshi lake walielekea kwenye kile chumba alichohifadhiwa Bingo, ajabu walipoingia hawakumkuta.. Roya na wenzake walistuka, hima wakatoka ndani ya chumba hicho, moja kwa moja walielekea mahali ilipo kengere ya kutoa taarifa.. Punde kengere hiyo yenye sauti kali yenye uzito wake ililia kisha Roya akasema "Bingo katoweka, haraka sana lango la Tropea lifungwe na kila askari afanye jitihada za kumtafuta.. Asirudi duniani..". Aliongea hivyo Roya kwa sauti ya juu.. Hapo sasa ndipo Tropea ilipoachafuka, makaburi yalipasuka wafu wakazidi kutokea, viumbe wa ajabu nao walionekana katika mji huo..





Hatari kubwa inazuka Tropea, makaburi yanajifukuwa ilihali jopo la wafu nalo likizidi kuongezeka. Sultan Abatish ilipomfikia habari hiyo ya kwamba Bingo haonekani, alitaharuki sana. Haraka akamuita Yuli ili aweze kusaidia harakati hiyo ya kumsaka Bingo popote pale alipo huku akiamini kuwa kijana huyo bado hajaondoka Tropea.

"Yuli.. Nahitaji Bingo aonekane, ukishamleta mbele yangu nitakupa asilimia stini ya uongozi wako" Alisema Sultan Abatish. Yuli alicheka kwanza halafu akajibu "Sidhani kama bado unamawazo mgando ya kuendelea kunidanganya. Miaka mingapi imepita na ahadi zako zisizo tekekelezwa? Baba mimi ni mwanao lakini namna tunavyoishi ni kama vile mimi ni kibaraka wako. Leo hii mtoto wa juzi Bingo unamlazimisha kumpatia madaraka ambayo yeye hana mpango nayo. Sasa basi nasema hivi sipo tayari kumtafuta Bingo.."Yuli alipokwisha kusema hayo alipotea.

Yuli naye ni mmoja wa familia ya Sultan Abatish, kijana huyo hakufurahishwa na namna baba yake anavyomwamini Bingo kuliko yeye. Kwa maana hiyo alilazimika kukaidi matakwa ya baba yake ilihali pole pole ndani ya moyo wake akiwa na nadhiri dhidi ya mji huo wa Tropea. Jambo la kwanza alimuita Roya,ambapo Roya nae alitii wito. Ni ndani ya chumba maalumu, chumba ambacho wawili hao waliweza kuteta.

"Ndio Yuli umeniita, nami nimetii wito?.." Aliongea Roya.

"Roya, nahitaji msaada wako kama upo tayari kunisaidia"

"Masaada gani huo Yuli? Na je, hujui kuwa muda huu tupo katika harakati za kumtafuta Bingo?.."

"Ahahah ah hahahah.." Yuli aliangua kicheko, Roya alimshangaa sana ilihali muda huo huo Yuli akaongeza kusema "Achana na suala hilo la Bingo, hebu fanya kama unalisahau kwa muda..."

"Haya zungumza.."http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Vizuri sana kwa kunipa nafasi... Roya kuna siri nzito sana imejificha ambayo wewe usingeweza kuijua pasipo mimi kukwambia. Bingo na Abatish wana agenda nzito sana juu ya mjini huu wa Tropea, na ndio maana Sultan anamuhitaji Bingo kwa udi na uvumba ili amrithishe mji huu. Amini kwamba Roya, Bingo sio mfu kama tulivyo sisi. Bingo anauwezo wa kurudi dunia akaishi maisha mengine tofauti na sisi. Lakini pia mbali na hilo, Starlon anaitamani hii ngome,hivyo sioni sababu ya mtu kama Bingo ambaye sio jamii yetu atuongoze sisi. Ngome hii itapotea zaidi na zaidi.. "Alisema Yuli huku akiwa amempa mgongo Roya.

" Kwahiyo?.. "Alihoji Roya kwa taharuki ya hali ya juu. Hapo Yuli alimgeukia kisha akamwambia" Mapinduzi yanahitajika,uamuzi nitakao chukua ni mgumu sana. Kwa kuwa nimeona kuna ubaguzi unaoendelea kimya kimya.. "

" Yuli uamuzi gani huo?.. "

" Abatish nitamuua kwa mikono yangu kisha siku kadhaa mbele nitajitangaza kuwa mliki wa Tropea, na vile vile nitaanda jeshi nguvu kazi la kupambana na jeshi la Sultan Starlon.. Ahahah hahahah.. "Yuli alijibu hivyo huku akimaliza kwa kicheko. Maneno ya Yuli yalimshtua sana Roya, ghafla akajikuta akiingiwa na hofu juu ya Yuli, uamuzi huo ulimtisha sana. Lakini wakati Roya akiwa na hofu, Yuli aliongeza kusema" Bingo yupo katika mikono yangu.. Kwahiyo mpango huu nilioanzisha utaenda sawa kabisa " Hapo Roya alishusha pumzi baada kusikia Bingo bado yupo ndani ya mji huo wa Tropea..

" Wapi alipo Bingo?.. "Roya alimuuliza Yuli, lakini Yuli alikataa kumuonyesha akidai kuwa mpaka pale atakapo kamilisha mpango wake ndipo atakapo muelekeza mahali alipo. Vile vile Yuli alihitaji kujua kama Roya yupo tayari kuungana naye katika harakati hizo za kufanya mapinduzi. Jambo hilo kwa Roya lilikuwa gumu sana ila akahofia huwenda akawa rehani endapo kama atapingana na matakwa ya Yuli mtoto wa kwanza wa Sultan Abatish ingawa moyani Roya alitamani sana Bingo ndio achukue nafasi hiyo. "Nipo tayari.." Alijibu Roya. Jibu ambalo lilimfurahisha mno Yuli na hapo ndipo ulipofanyika mpango wa kuwatuliza wafu pamoja na kuwarudisha jeshi ambalo tayari lilikuwa likihangaika kumtafuta Bingo.

Wakati huo ghasia hiyo inatulizwa, upande wa pili kijana Bingo alikuwa ndani ya chumba kile ambacho mara ya kwanza alipata kulia chakula ambacho kilikuwa ni nyama ya mtoto mchanga. Bingo akiwa ndani ya chumba hicho, aliwaza atatoka vipi ndani ya Tropea ili arudi duniani kuvaa mwili wake kabla haujazikwa sababu endapo kama mwili wake utazikwa basi habari zake zitakuwa zimeishia hapo, hata afanyeje Tropea hatotoka tena. Lakini pia mbali na suala hilo la mbinu ya kuchoropoka Tropea, vile vile Bingo alijiuliza siku ngapi amemaliza Tropea. Kabla hajapata jibu ghafla alitokea mzee Ndelo. Mzee huyo akiwa ndani ya mavazi meupe alimsogelea Bingo kisha akasema "Bingo unatambua kuwa muda mrefu upo Tropea? Hivi unajua kuwa mwili wako.....



"Bingo unatambua kuwa muda mrefu upo Tropea? Hivi unajua kuwa mwili wako mpaka sasa unaleta utata kijijini na kushangaza watu?..". Bingo alistushwa na maneno hayo aliyoyaongea mzee Ndelo. Akiwa na hofu dhofu lihali kijana Bingo akamuuliza mzee huyo "Unamaana gani mzee?.." mzee Ndelo alishusha pumzi ndefu kwanza kisha akajibu "Jambo la kwanza utambue umemaliza miezi miwili sasa huku lakini pia..." Kabla Ndelo hajaendelea kuongea Bingo alimkatisha kwa kusema "Miezi miwili? Akha! Tafadhali mzee wangu usitake kuniambia kuwa tayari mwili wangu UMEZIKWA, katu sitofurahia maisha ya Tropea, nahitaji kurudi duniani ikiwezekana hata sasa tuondoke wote.."

"Bingo.." Aliita mzee Ndelo, punde akasema "Ni ngumu sana mimi kuondoka na wewe? Lakini pia usiwe na hofu juu ya mwili wako kwa sababu tayari kuna imani nimewaingizia wanakijiji. Kijiji chote nimekitangazia kuwa wewe bado hujafa na si muda mrefu utarejea katika maisha ya kawaida. Hebu tazama ukutani.. "Alisema hivyo mzee Ndelo halafu akanyoosha kidole chake ukutani, ukatokea moto mwembamba kwenye kidole chake, moto wenye rangi ya blue. Punde pale ukutani palipogota moto huo ilionekana TV.. Tv ambayo ilionyesha namna mzee Ndelo alivyofanikiwa kuwatuliza wanakijiji ambao ambao tayari walitaka kumzika Bingo. Hapo ndipo Bingo alipotupa macho yake kwenye ukuta ili atazame namna ilivyokuwa.

******

"Katu hatuwezi kuamini suala hili, mtu alishakufa amekufa kamwe hawezi kurudi tena duniani. Hapa lazima Bingo azikwe" Sauti ya mmoja ya wanakijiji. Alisikika akiongea maneno hayo kwa sauti ya juu kabisa baada kuona mzee Ndelo Katia mkazo juu ya suala la mwili wa Bingo kuzikwa. Wanakijiji baadhi walimuunga mkono mzee huyo ingawa wengine walikubaliana na mzee Ndelo kwani walijua dhahili shahili mzee huyo anajihusisha na mambo ya jadi. Ndelo akajitokeza akasema "Ni nani anaweza kutuambia kuwa umauti wa Bingo umesababishwa na nini? Je, Bingo aliumwa? Aidha aliuliwa?. Nasema hivi Bingo karogwa na huwenda aliyemroga ni huyu huyu mzee anayeshinikiza kuwa azikwe, kwa sababu anaamini endapo kama leo hii Bingo atazikwa basi zoezi lake atakuwa amelikamilisha. Nasema hivi Bingo hatozikwa, na mchawi wa hiki kijiji nitqmuumbua hadhalani jua la utosi.. " Mzee Ndelo maneno hayo aliyasema kwa kujiamini kabisa, hapo sasa msibani ndipo minong'ono ilipoanza kusikika, kila mmoja alizungumza lake.

" We mzee Ndelo wewe?!..hivi kweli wewe wa kuniita mchawi mimi?.. "Yule mzee aliyekuwa akisisitiza Bingo azikwe alisema kwa hasira kali. Mzee Ndelo akajibu" Naam! Tena narudia kusema wewe ndio ni mchawi, na Bingo atapona halafu sasa nitakuumbua hadhalani jua la utosi.. ". Hayo maneno ya mzee Ndelo yalizidi kumchukuza huyo mzee, ambapo ndipo alipo amua kumsogelea kwa dhumuni la kupigana. Lakini kabla wazee hao wajafikia muafaka waliamuliwa, ogomvi huo ukawa umetoweka. Baada ya siku mbili kupita, bado Bingo alionekana ndani ya jeneza pasipo kurudi duniani kama alivyokuwa akieleza mzee Ndelo. Suala hilo liliwafanya wanakijiji kuingiwa na hofu mioyoni mwao, hivyo haraka sana mwenyekiti wa kijiji akamuita Ndelo ili alete majibu muafaka juu ya mwili wa marehemu.

"Katika vitu ambavyo serikali yako haiamini ni ushirikina, mzee unataka kutuletea matatizo hapa kijijini. Hivyo basi nia na dhumuni ya kukuita hapa, nataka ule mwili ukazikwe la sivyo utakifanya kijiji hiki kuchafuliwa. Sasa iweje mtu mmoja utie doa kijiji chenye mamia ya watu?.."Alisema Mwenyekiti wa kijiji, maneno hayo aliyokuwa akiongea kwa msisitizo alikuwa akimwambia mzee Ndelo. Ndelo alicheka kwanza kisha akajibu" Mwenyekiti, jambo hili wala lisikupe shida, mimi ndio najua ukweli wa yule kijana. Bingo bado hajafa, yupo hai kabisa ila huko aliko ndio nafanya mpango wa kuonana na watalamu wa masuala haya ya giza ili waweze kumtoa. Hebu mzee mwenzangu fikiria kwanza,mama Bingo ataishi maisha gani pasipo mwanae? Nakuomba kuwa mtulivu ". Ndelo na mwenyekiti walikubaliana hivyo, ila siku kadhaa mbele wanakijiji waliona Ndelo hana ubinadamu, na hapo ndipo walipoamua kuandamana mpaka nyumbani kwa mwenyekiti kuomba kibali cha kufanya jambo lolote juu ya mzee Ndelo.

" Mwenyekiti... Mwenyekiti, sisi wanakijiji ndio tuliokuweka hapa na vile vile sisi ndio tutakao kuondoa.." mwanakijiji mmoja alisema kwa hasira huku akiwa na shoka begani. Mwenyekiti aliogopa ujio huo wa siraha, akiwa na hofu akasema "Jamani mbona hivyo sasa? Mnakuja namna hiyo sio vizuri ndugu zangu!.. Haya niambieni kosa langu nini?.."

"Usibane sauti kama mama mjamzito aliyeshikwa na uchungu wa mimba, sisi tunachotaka utupe kibali chako tukamfanye chochote mzee Ndelo, haiwezekani maiti imalize wiki ikiwa bado haijazikwa kwa Mila na tamaduni zetu hiyo sio haki ya marehemu.."

"Ndugu zangu si nyinyi mlikuwa mnamuunga mkono Ndelo au?.." Aliuliza Mwenyekiti.

"Kaaa kimya. Mpumbavu wewe,tunachotaka sisi ni kibali chako tu na sio maneno yako ya kubwabwaja"

"Sawa nendeni nimewaruhusu" Alijibu mwenyekiti. Fujo ilizuka mahala hapo, wanakijiji hao walishangilia sana. Muda huo ilikuwa yapata saa kumi na moja ya jioni, hivyo kikao cha muda mfupi kwa vijana nguvu kazi kilikaa na kuanza kujadili namna gani ya kupola jeneza na kisha kumuadabisha mzee Ndelo ikiwezekana kumuua kabisa.

"Hakuna mtu asiyemjua huyu mzee, ukweli mzee ni moto wa kuotea mbali. Ukienda kichwa kichwa anakupoteza"

"Enhee kwahiyo tufanyeje sasa jamani? Na wakati huo mkumbuke anashinda pale kulilinda jeneza na analala pale pale.."

"Sikilizeni vijana, kwa kuwa suala hili tumeamua kulivalia njuga basi hakuna haja ya kuhofia wala kuogopa. Twendeni Twendeni tukamnyooshe kisha Bingo azikwe" Wanakijiji hao, vijana shupavu walipokubalina hivyo waligongeana mikono kisha wakaondoka mahali hapo kusubiri giza litakapo ingia ndipo wakatimize azma yao. Lakini walipotoka tu hapo mzee Ndelo akatokea, alicheka sana halafu akajisemea "Pumbavu sana nyinyi, mlipolalia ndipo nilipoamkia. Kajipangeni".

*********http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Tv hiyo ikawa imepotea, Bingo Alistaajabu sana mambo hayo aliyoyashuhudia. Punde mzee Ndelo akasema "Baada vijana hao kuamua mambo hayo, kuna dawa niliupaka mwili wako, dawa ambayo ni kiini macho ya kuwafanya watu kuamini kuwa muda wowote utafumbua macho kwa sababu ulikuwa ukihema ingawa dhahili shahili haukuwa unahema. Hivyo ilibidi nizidi kutangaza kuwa bado hujafa na muda wowote utaziduka. Ila sasa kijana wangu Bingo. Hii dawa inamadhara tena makubwa sana endapo kama utachelewa kuuvaa mwili wako.. Fanya ujuavyo, ndani ya siku tano uwe tayari umeuvaa mwili wako la sivyo habari habari yako itakuwa imekomea hapo" Mzee Ndelo alipokwisha kusema hayo alipotea. Akabaki Bingo akiwa na wingi wa taharuki, na ndani ya kichwa chake akajiuliza.

"Siku tano? Mmh yani muda mchache tu niliokaa huku naambiwa nimekaa miezi miwili, je siku tano itakuaje sasa?..





Jambo hilo lilimtia hofu Bingo, suala la kurudi duniani lilimfanya aumize kichwa akiwaza namna gani ataondoka ndani ya mji huo uishio wafu. Lakini wakati yupo katika tafakari hiyo, mara ghafla ndani ya chumba hicho alitokea Yuli. Bonge la mtu. Jibaba lenye milaba minne. "Habari yako Bingo, awali uongozi wa Tropea ulipanga kukukabidhi mji huu, kitendo ambacho kipo kinyume sana na ingekuwa ubaguzi mkubwa sana kwa sababu ndio ninayefaa kumiliki hii ngome na wafu waliomo. Lakini pia nisingetaka kukuacha hivi hivi kijana, kwa sababu wewe ni jamii ya Abby hivyo nitakupa wadhifa fulani hapa hapa ili uendelee kufurahi maisha ya huku " Alisema Yuli. Maneno hayo alikuwa akimwambia Bingo.

" Kwahiyo unataka kusema kwamba Tropea inaweza kutawaliwa na watu wawili?.. "

" Mmh! Unamaana gani? Mimi ndio kiongozi kwa sasa. Namanisha kuwa Abatish nimeshampoteza na kuanzia sasa mimi ndio Sultan mkuu. Hivyo basi uwezo wako wa kupambana umenifanya nikupe wadhifa katika mji huu ila endapo kama hutakubaliana na hitaji langu basi utakosa vyote, duniani hutorudi na vile vile Tropea hutoishi " Yuli alisisitiza. Hapo Bingo akaingiwa na hofu zaidi, lakini baadae akaona hamna njia nyingine bali ni kukubali cheo hicho ingawa moyoni akiwa na nadhiri ya kufanya mapinduzi.

" Yuli.. Nipo tayari kwa hilo.. "Alikubali Bingo. Yuli alicheka sana, ndipo akapeana mkono na kijana Bingo wote wakawa kitu kimoja.

Nje, kengere kubwa ya mji wa Tropea iligongwa kisha mtangazaji akawataka wafu wote ndani ya mji huo watulie." Wafuasi wote katika mji huu wa Tropea, kuna taarifa ya mpya ambayo imejitokeza. Nayo ni kuhusu mapinduzi. Tropea kuanzia sasa itakuwa chini ya Yuli kwa sababu aliyekuwa kiongozi hapo awali Sultan Abatish kaachia ngazi. Hivyo basi hatutegemei kuona mfu akienda kinyume na sheria na taratibu ya Tropea, maisha yataendelea kama kawaida. Lakini mbali na hayo, jeshi mnatakiwa sinagogi ili mpewe utaratibu mpya jinsi ya kulinda mipaka ya mji wetu ". Mtoa taarifa aliongea maneno hayo, taharuki ikazuka Tropea kila mmoja akishangazwa na maamuzi hayo. Lakini wakati taarifa hiyo ikienea Tropea, hatimaye taarifa hiyo ikafika kwenye ngome ya Sultan Starlon. Ajabu shangwe zilizuka, kiongozi mkuu akaita jeshi lake ndani ya sinagogi na kisha akaanza kuzungumza nao jambo ingawa habari kuu ambayo iliwafurahisha ni juu ya kijana Yuli kuuchukua mji wa wafu. "Nafikiri kila kitu kinaenda sawa, Abenego, Joyka, Bluyner. Nyie ni watu wangu wa nguvu. Huu ndio wakati wa kukamilisha azma yetu ili Tropea iwe chini yetu. Anzeni kuwanoa vijana kujiandaa kwa ajili ya mapambano.." Alisema mkuu huyo aitwae Rauu.

"Hilo shaka andoa, tutapigana mpaka tone la mwisho, mji ule kwa vyovyote vile lazima uwe chini ya Sultan Starlon.." Aliongea Bluyner. Jitu ambalo lilionekana la ajabu sana.

"Safi sana. Je, Joyka unaniahidi nini?.." Rauu alihoji huku akimtazama Joyka. Joyka akacheka kidogo kisha akajibu "Hapa ni kipigo tu hakuna namna"

"Ahahah aah hahahah" Wote kwa pamoja waliangua kicheko wakati huo wakigongeana mikono. Kwingineko mambo sio mambo, Tropea Bingo anapata kukutana na Roya falagha. Hapo ndipo Bingo alipomueleza Roya juu ya uamuzi wa kijana Yuli aliochukuwa. Ukweli Roya hakufurahishwa na kitendo cha Yuli kwani alijua Yuli ni kiumbe mwenye roho mbaya sana, hivyo sio ajabu akaanza kuuharibu mji huo. "Roya! Hivi kwanini Yuli ameamua kuchukuwa uamuzi wa kumuondoa Abatish?.." Bingo alimuuliza Roya, muda huo walikuwa wawili kitaka moja ya chumba ndani ya sinagogi.

"Je, upo tayari na sisi tupindue meza?.." Aliongeza kuhoji Bingo ikiwa Roya bado akionekana kutafakari kitu ndani ya moyo wake hali iliyopelekea kukaa kimya. Lakini punde baada kusikia swali hilo la pili alilouliza Bingo.. Aligeuka kisha akasema "Bingo katika hili nipo tayari, Yuli hafai hata kidogo ila naomba uniahidi utakuwa tayari kushika nafasi ya mzee wako?.."

"Ndio Roya ila kuna kitu nataka kufahamu kidogo maana kinanishangaza sana!.."

"Aah Bingo kitu gani hicho?.." Alihoji Roya huku akiwa na wingi wa tabasamu baada kusikia Bingo kukubali kusalia Tropea. Bingo akasema "Hivi masaa ya huku na duniani yapo sawa kweli?.."

"Hahahah hahahah.. Bingo Bingo tofauti kabisa. Masaa ya huku yanaenda kasi sana mbali na duniani.." Alijibu Roya.

"Mmh! Kwahiyo siku tano duniani ni sawa na siku ngapi huku?.."

"masaa sita tu.." Alisema Roya. Bingo alishtuka sana. Mshtuko ambao ulimfanya Roya kumuhoji "Mbona unashtuka?.." Bingo kabla hajamjibu Roya, ghafla fujo zilisikika nje, mayowe ya hapa na pale yalitamalaki. Haraka sa Roya alikwenda dirishani kuchungulia ili ajue kinajili nini? Alistaajabu sana kuona umati wa wanajeshi kutoka ngome ya Starlon ikiwa imevamia.

" Bingo kaa tayari kazi imeanza.." Aliongea Roya akimuasa Bingo, na hivyo kijana huyo hakutaka kupoteza muda, hima alivaa vema koti lake, upanga begani tayari kwa niaba ya kulikabili jeshi hilo ambalo lilijaza watu wa ajabu ajabu. Wapo waliokuwemo wenye macho makubwa na masikio marefu, lakini pia wapo waliokuwemo wenye jicho moja huku ngozi zao zikiwa zimeshabiana na ngozi za nyoka. Ndimi za watu hao ni hatari sana kwa maisha. "Bingo yakupasa kuwa makini" Roya aliongeza kumwambia Bingo hali yakuwa jeshi la Tropea ambalo kwa muda huo lilikuwa chini ya Yuli lilikuwa limeshalivagaa jeshi la Starlon linalo ongozwa na Rauu. Patashika nguo kuchanika Tropea mji wa wafu,.. Hakika wafu walivyekwa vyekwa, jeshi la Yuli liliteketea. Baadae kidogo Bingo alitua chini kutoka juu kwenye majengo mrefu.. Vumbi ilitimka wakati huo koti lake likipepea nyuma. "Wewe ni nani?.." Rauu Aliuliza. "Bila shaka salamu zangu mmeshazipata. Mimi ndio Bingo mwana wa Abatish. Nimekuja Tropea kuharibu mipango yenu ya kuuteka mji huu, huu mji utabaki chini ya Batish miaka yote.." Alijibu Bingo.

"Ahahaha ha hahahah.." Rauu alicheka sana kisha akamwambia Bingo "Ni vigumu nafsi kushindana na mfu..." kwisha kusema hivyo, akaruhusu jeshi limshambulie Bingo. Bingo kwa nguvu zote akajinyanyua juu, punde akashuka.. Kitendo hicho kiliweza kutimua vumbi nyingine kwa mara nyingine tena, katikati ya vumbi hiyo Bingo akaanza kuwashambulia. Muda mchache jeshi lote la Rauu liliteketea,hapo Rauu akajikuta akibaki peke yake.. Alishangaa sana asiamini kama kweli Bingo anauwezo namna hiyo. Ila baadae akaona sio vizuri kama hatodhihilisha ubora wake mbele ya Bingo hatakama anaonekana ni mtu mwenye uwezo mkubwa. Hivyo basi Rauu alinyoosha mkono juu, ukatokea upanga kwenye mkono wake, wakati huo huo kwa mbali kabisa kwenye jengo ndefu ilisikika sauti ikimtaja Bingo. Bingo akainua macho yake kutazama kule ilipotokea sauti hiyo akapata kuona mtoto mdogo mwenye umri usiozidi miaka mitano. Mtoto huyo akamtupia Bingo upanga kisha akapotea.

Hapo sasa wawili hao kila mmoja akawa na siraha mkononi mwake. Shangwe zilizuka za kumshangilia Bingo. "Bingooo.. Bingoooo.. Bingoooo Bingooo". Muda huo huo pambano likaendelea. Na wakati mpambano huo unaendelea, upande wa pili Roya alionekana ndani ya chumba alichokuwa akitumia Batish. Roya alikuwa na haraka sana kutafuta kitu kwani alifungua kila sanduku. Alifungua hili akaliacha, akafungua lile akaliacha. Lakini mwishowe kitu alichokuwa anakitafuta alikipata, nacho sio kingine bali ni ramani ya kurudi Duniani. Hima aliihifadhi kwenye mfuko wa koti lake kisha akaendelea kusaka kitu kingine. Safari hiyo alitafuta pete ya miujiza na ufunguo wa Tropea. Navyo alivipata, na hivyo aliondoka ndani ya chumba hicho, lakini sasa kabla hajatoka, Yuli aliingia chumbani humo. Alicheka sana kisha akasema "Roya, hatimaye unanisaliti. Si ndio? Hahahah. Hahahah. Nasema hivi umechelewa, kwa usalama wako nipe kila kitu ulicho chukuwa humu ndani.." Alifoka Yuli. Roya kamuuliza "Kitu gani?.."

"Hujui? Sasa ngoja nikunyooshe" Alijibu Yuli na mara moja akaanza kumshambulia Roya kwa mateke na ngumi, ila Roya alionekana kuwa makini sana kukwepa wakati huo akijaribu kumkimbia Yuli ambaye nae alionyesha umahili wa kumdhibiti.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Nje mambo bado yalikuwa sio mambo baina ya Bingo na Rauu.. Hao mabwana walionyeshana umwamba mbele ya umati wa wafu ingawa Bingo aliweza kutawala vema pambano. Na wakati mpambano huo ukiendelea kupamba moto, ghafla Roya aliingilia kati huku nyuma akifuatwa na Yuli. Lakini kabla Yuli hajamfikia, Michael aliingilia kati, muda huo sasa wafu walimvamia Rauu na kisha kumshambulia. Bingo akamaliza mchezo kwa urahisi kabisa.. Roya alimkumbatia Bingo, akamkabidhi funguo na Pete pia ramani kisha akamwambia "Bingo naimani ipo siku tutakutana kwa mara nyingine tena ila kwa sasa kimbia. Tropea haifai tena.. Funguo hii hakikisha uki..." Kabla Roya hajamaliza kusema alichotoka kuongea, alkchomwa upanga na mtu wa kuitwa Yuli. Muda huo huo Michael tayari alionekana akiwa chini mwili wake ukiwaka moto.

" Bingo kimbia.. Kimbia niache mimi?.. "Roya alipasa sauti akisema hivyo baada kuona Bingo amemng'ang'ania. Muda mchache makaburi yalipasuka, mikono ya wafu ilionekana na punde tu wafu waliandamana kumfuata Bingo." Bado nusu saa Bingo.. Na mwili wako tayari upo katika maandalizi ya mwisho ili uzikwe.." Sauti hiyo ilikuwa ya mzee Ndelo, sauti hiyo Bingo aliisikia kwa mbali sana huku akitimua mbio ilihali jopo la wafu likimfuata nyuma. Bingo alikimbia sana, alibahatika kulipita lango lakini baada ya lango hilo la Tropea lilionekana giza hakuna pwa kwenda njia imefikia kikomo. Pumzi ndefu alishusha kijana Bingo, akitazama nyuma aliona kundi kubwa la wafu likimfuata nyuma huku likiongozwa na Yuli,hofu ikazidi kumjaa hasa baada kuona njia imefika mwisho ilihali ananusu saa tu ya kuendelea kusalia Tropea kwani mwili wake upo katika maandalizi ya mwisho ili uzikwe..



"Niende wapi?.." Bingo alijiuliza baada kuona njia imefika ukingoni hali ya kuwa huku nyuma kundi la wafu likiongozwa na Yuli likizidi kumfuata. Akili ya ghafla ikamjia Bingo, akili hiyo ikamtuma kuwa afunge lango hilo la Tropea kabla wafu hao hawajawakaribia. Uamuzi huo Bingo aliuona unafaa sana, bila kupoteza muda aliusogelea mlango huo kisha akaufunga na kufuli halafu akajitosa kwenye lile giza lililokuwa mbel yake. Mayowe yalisikika.. Bingo akilalama huku akizidi kutokomea kwenye giza lile nene. Lakini muda mchache baadae alipoteza fahamu, ila punde fahamu zilimrudi na hapo ndipo alipokohoa ndani ya jeneza kisha akajinyanyua akaketi huku akuwatazama watu waliokuwa kando ya jeneza.

Taharuki inazuka, watu waliokuwepo hapo walikimbia baada kuona Bingo kafufuka, na wale wenye roho ngumu waliishia kustaajabu tu ilihali mboni za macho yao hata zisiamini kama kweli marehemu kafufuka.

"Bingo habari yako.." Alisikika akisema moja ya wanakijiji. Mwanakijiji huyo alimsalimu Bingo ambaye muda huo alionekana kutofahamu kinacho endelea,hali iliyomfanya asimjibu mtu huyo.

"Tulieni kwanza fahamu zimrejee vizuri" Alisema mzee Ndelo wakati huo huo akamsogelea Bingo, akachuchumaa kisha akamwambia "Hongera sana kwa kurejea duniani muda muafaka, hakika wewe ni shupavu kwa sababu ilikuwa imebaki dakika moja tu kati ya yale masaa matano niliyokwambia..". Ndelo alipokwisha kusema hivyo aliinuka akachukua kibuyu chake chenye dawa za asiri, akamnynyuzia Bingo mulemule ndani ya jeneza. Muda wa dakika sita Bingo alirejea kumbukumbu zake sasa, na hivyo mzee Ndelo akaruhudu kila mwanakijiji kumsalimia kijana huyo pasipo kumuogopa wakati huo huo baadhi ya vijana walionekana wakilifukia kaburi kwani aliyetajiwa kuzikwa kafufuka.

"Pole sana Bingo.."

"Pole sana kijana mwenzetu kwa mtihani.."http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Pole sana Bingo wangu kwa jambo hili jamani"

"Bingo, pole Sana kwa kweli". Hizo zilikuwa pole za baadhi ya wanakijiji waliokuwa wakimpa pole Bingo. Walikuwa vijana kwa wazee, wamama kwa wababa. Wote kwa pamoja walimsabahi Bingo ingawa hawakujua kama kijana huyo alielekea Tropea mji uishio wafu.

Mambo ndivyo yalivyokuwa, ila ghafla ya Bingo ilizidi mara mbili ya hapo awali baada kumona mama yake kipenzi akiwa na wingi wa afya. Mama Bingo alijikuta akidondosha machozi kwa furaha. Alisema "Bingo mwanangu, awali wa yote naomba unisamehe mwanangu, najua umeteseka kwa sana kwa sababu yangu. Umeishi maisha ya tabu kwa sababu yangu. Lakini nilifanya hivyo nikiamini kwamba nitaimalisha ndoa yangu, ingawa mawazo yangu hayakwenda kama niliyo tarajia. Maradhi yaliyokuwa yameniandama kwa kipindi kirefu yalimfanya baba yako kunitelekeza akaoa mwanamke mwingine na hata pia akaamua kuhama kijiji pasipo kunijali hata kwa salamu.. "Maneno hayo mama Bingo aliyaongea kwa uchungu mkubwa huku machozi yakimtiririka. Bingo alishusha pumzi ndefu kisha akasema" Hilo ondoa shaka mama, kila kitu nakifahamu, kwanza nafurahi kukuta ni mzima kabisa hayo mengine tufanye yamepita.. "

*********

Kijiji kuzima kinapata kujua kuwa Bingo kafufuka, jambo hili linampa heshima mzee Ndelo kwa kufanikisha kumrudisha kijana Bingo.

Jioni moja Bingo alikutana na mzee Ndelo, wawili hao waliweza kuteta mambo mengi sana, lakini katika mazungumzo yao walizama sana kuhusu safari ya ajabu ambayo ilimtokea Bingo.

"Ndio bwana pole na hongera pia kwa safari ndefu" Alisema mzee Ndelo huku akiwa na wingi wa tabasamu.

"Daah! Asante sana lakini mzee safari ilikuwa ngumu mno ingawa namshukuru Mungu nimerejea salama. Na moja ya vitu nilivyorudi navyo ni funguo wa huko pia na pete, vile vile nimerudi na ramani. Vitu hivi vyote alinipatia Roya.."

"Loh! Bingo? Kweli wewe ni noma. Pete hii sio ya kawaida kijana, na hii ndio Pete ambayo ilikuwa ikitafutwa watu wengi sana ingawa wengi walioifuata walipotelea huko huko."

"Kwahiyo mzee naweza kusema sisi umasikini basi tena?.."

"Ndio maana yake!.." Alijibu mzee Ndelo. Wote kwa pamoja walifurahi sana.

Usiku wa siku hiyo hiyo Bingo akiwa usingizini, kwa njia ya ndoto alikuja Roya. Roya akamuomba Bingo atupe ufungo huo aliotoka nao Tropea kisha akamwambia "Bingo tayari upo duniani, hivyo huna budi kuichana ramani hiyo. Lakini pia pete niliyokupatia unaweza kuomba kitu chochote na ikakupatia. Tropea imefunikwa na majivu ya moto, mji umeyeyuka. Ila mbali na hiyo Bingo, bado kuna laana inakuja nyuma yako, nayo itakufanya uishi kwa shida sana hapa duniani" Roya aliongea.

"Laana? Laana ipi tena Roya? Kwanini iwe hivyo?.." Bingo aliuliza huku akiwa na wasiwasi. Roya alikaa kimya kidogo halafu akasema "Hilo lisikutishe, mimi sio binadamu ingawa nilitamini kuishi na wewe ikiwezekana tujenge familia kwa sababu nakupenda sana, lakini kwa kuwa hili limeshindikana basi nitakusaidia kwa lingine ikiwa kama upendo wangu kwako..." Bingo alitaharuki moyoni mwake. Hapo akahoji kwa mara nyingine tena." Utanisaidiaje Roya?" Roya akajibu" Ili uiepuke laana iliyokuwa ikija nyuma yako, ingekulazimu ufe moja kwa moja,ila kwa sasa nitazikwa mimi kwenye kaburi lako ingawa nitahitaji msaada wako. Nao sio mwingine ni msaada wa damu.. Bingo fanya ujuavyo, kila siku usiku wa manane vaa nguo nyeusi kisha njoo kwenye kaburi langu, jichanje damu idondokee kwenye kaburi na hapo nitapunguziwa adabu juu ya kile nilicho fanya Tropea. Damu yako kwangu ya thami Bingo tafadhali usisite kufanya hivyo.. "Maneno hayo Roya aliongea huku akilia kwa uchungu. Bingo alisikitika sana, maneno ya Roya yalimuumiza vilivyo. Na mwishowe akasema" Nipo tayari kwa hilo Roya. Na pia nakupenda kama unipend a to wewe "

" Nashukuru sana "Roya kwisha kusema hivyo alipotea ambapo muda huo huo Bingo naye alizinduka kutoka usingizini.

Kweli kijana huyo alifanya kama alivyoagizwa, lakini pia aliomba utajiri..kufumba na kufumbua Pete ikampatia nyumba nzuri kuliko zote kijijini,hakuweza kumsahau mzee Ndelo, mzee cha pombe ambaye alikuwa na umasikini wa kutupwa. Naye alitajirika vya kutosha. Kijiji kikajawa na neema, Bingo alitoa msaada mbali mbali kwa wasio jiweza hata waliopungukiwa.

*******

Hivyo ndivyo ilivyo mke wangu, nadhani umepata maana kamili ya mimi kutoka hapa usiku wa saa nane kisha baadae nikirudi nanukia ubani na udi. Namuenzi Roya kwa sababu nisipo fanya hivyo kuna hatari ya mimi kupata matatizo. Alisema Bingo akimwambia mkewe wa kuitwa Millander. Millander hapo awali alikuwa na wasi wasi kuhu mumewe baada kuona kila siku usiku Bingo huamka huondoka akirudi huwa na damu sehemu mbal mbali ya mwili wake hali ya kuwa hunukia ubani na udi. Na ndio maana siku hiyo akamuwa kumwambia Bingo "Bingo mume wangu, tayari tumefikisha miezi takribani mitatu sasa tangu mimi na wewe tufunge pingu za maisha. Ukweli nafurahia sana uwepo wako katika maisha yangu na najivunia kuwa na mwanaume mzuri mkamirifu vile vile muaminifu, ukweli uko Sawa kwangu. Lakini licha ya kwamba maisha yetu ya ndoa kuwa yenye furaha na amani ila kuna suala moja huwa linanitatiza akilini mwangu na nashindwa kulielewe,hivyo natuamini leo utanipa uvumbuzi ili niweze kulielewe. Bingo nakupenda sana mume wangu tena zaidi ya sana, kwahiyo nakuomba unambie ukweli usinifiche mimi ni mkeo". Hitaji hilo la Millander kutaka kujua ukweli ndio lililomfanya Bingo kumsimulia safari ngumu iliyompeleka TROPEA-mji wa wafu. Hakika ilikuwa ni simulizi tata iliyomshangaza Millander. "Pole sana mume wangu, nadhani Pete yenyewe ndio hiyo mkono mwako!.." Millander alisema.

"Ndio mke wangu ila hapa ilipo imeshapoteza uwezo wake kwahiyo naivaa tu ikiwa kama kumbukumbu ya kutoka Tropea " Alijibu Bingo kisha akacheka. . Millander aliachia tabasamu pana huku akimkumbatia mpenzi wake kwa kuwa na moyo wa kijasiri.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/



MWISHO

0 comments:

Post a Comment

Blog