Search This Blog

TROPEA MJI WA WAFU - 4

 






Simulizi : Tropea Mji Wa Wafu
Sehemu Ya Nne (4)




Pembezo mwa mto huo alionekana Ajuza akipita pita huku akichimba mizizi ya miti, muda huo Bingo alifumbua macho yake akapata kumuona Ajuza huyo. Bingo alitamani sana kumuomba msaada bibi huyo lakini alishindwa sababu hakuwa na sauti wala nguvu ya kujinyanyua pale alipokwama. Ila mwishowe ajazu alimuona, hivyo alimfuata akamsaidia kumtoa mahala pale. Ajuza huyo alimpeleka Bingo nyumbani kwake, ambapo huko alimpa dawa mbali mbali zilizo weza kumtibu majeraha.. Na jambo ambalo lilimfurahisha Bingo ni baada Ajuza huyo kuongea lugha ambayo aliielewa.. "Pole sana, utapona tu" Alisema Ajuza huyo. Kwa sauti ya upole Bingo akajibu "Asante sana.."

"Lakini kuna jambo nataka nikuulize tafadhali.." Aliongeza kusema Bingo.

"Lipi hilo?.."

"Hapa ni wapi.."

"Hapa ni Ambatapra"

"Ambatapra na Tropea kuna umbali sana?.."

"Ndio ingawa sio sana, ramani yako ndiyo itakufanya upaone karibu"

"Unamaana gani?.." Alihoji Bingo, muda huo akijinyanyua kitandani.

"Maana yangu ni kwamba kama usingekuwa na ramani basi ungefuata mto huyu moja kwa moja ungekufikisha Tropea, lakini vile vile kwa njia ya mto kwako ingekuwea vigumu sana kukanyaga mji ule sababu kabla hajaingia Tropea kuna ulinzi mkali sana kutokana na hali iliyopo sasa.. "

" Laah! Sawa Asante kwa majibu yako, lakini mbali na haya mazungumzo. Bado nina swali lingine.. "

" Lipi tena?.. "http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

" Nataka kujua watu mnao ishi huku mmefikaje fikaje?... "

" Acha maswali yako ya kipuuzi.. "Aliwaka Ajuza baada Bingo kumuuliza hilo swali. Ni swali ambalo lilimchukiza sana. Hapo alinyanyuka akatoka ndani ya chumba hicho alichomlaza Bingo wakati huo Bingo akijutia kuhoji hilo swali..

" Nafikiri hali yako imeimalika vema, sasa unaweza kuendelea na safari yako. Lakini kabla hujaanza safari, kuna kitu nataka kutoka kwako.." Alisikika akisema ajuza,ni mara baada hali ya Bingo kuonekana imekaa sawa. "Asante kwa masaada wako,.. Enhe niambie kitu hicho.." Alijibu Bingo huku akimkodolea macho Ajuza. Kabla Ajuza hajaongeza neno lolote, ghafla katika chumba ambacho mlango wake ulionekana kujazwa na kutu, alitokea binti mlemavu wa mgongo. Binti huyo alitembea akiwa ameinama ilihali sehemu mbali mbali za mwili wake zilikuwa zikitoa funza ilihali harufu mbaya nayo ikimtoka. "Laah!.." Alitaharuki Bingo wakati huo kinywa chake kikiwa kimejaa mate, kichefuchefu nacho kisimuwee mbali. Hapo Ajuza alimtazama Bint huyo kisha akarudisha uso wake kumtazama Bingo halafu akamwambia "Huyu ni binti yangu,siku ya leo nataka ufanye nae mapenzi kabla hujaondoka. Hapo alipo anamiaka zaidi ya hamsini, wala hamjui mwanaume. Hivyo basi nataka wewe ndio uwe wa kwanza kwake.." Alisema hivyo Ajuza huyo, na safari hiyo sauti yake ilikuwa ikijirudia mara mbili mbili kama mwangwi huku macho yake nayo yakibadilika rangi.. Bingo aliogopa suala hilo, kwani alishaambiwa kuwa hatakiwi kufanya mapenzi na mtu yoyote ndani ya safari yake,hivyo aliona hakuna njia nyingine zaidi ya kutimua mbio. Bingo alikimbia muda huo nyuma yake ilionekana mikono ya wafu ikichomoza ardhini.. Kwa sauti juu kabisa vicheko vilisikika,na punde si punde juu ya ardhini lilionekana kundi la wafu nlikimkimbiza Bingo.. Hali ambayo ilimpelekea kijana kukaza mwendo ingawa mwishowe alikubali matokeo baada mbele yake kuonekana kundi lingine, ghafla kulia na kushoto nako makundi mengine. Sasa Bingo akajikuta yupo katikati.. Hofu dhofu lihali ilimganda Bingo, akaamini tayari mwisho wa safari yake umewadia. Lakini wakati akiwaza hilo, mara ghafla alitokea msichana mrembo akiwa na upanga mrefu mkali, msichana huyo alimtazama kwanza Bingo akaachia tabasamu kisha mara moja akaanza kazi ya kuwashambulia wale wafu. Ilikuwa shughuli pevu ila mwishowe mwanadada huyo aliwamaliza ambapo hapo ndipo alijitokeza yule Ajuza aliyemsaidia Bingo..Ajuza huyo naye alikuwa na upanga makali vile vile ajabu ni ule upanga ambao Bingo alikabidhiwa na mzee Ndelo kabla hajaanza safari ya Tropea...





Alistaajabu sana Bingo wakati huo akiwa pembeni akiacha uwanja uchafuliwe na binti huyo aliyepania kumuokoa kwa kuteketeza kundi lile la wafu lililokuwa likimfuata. Lakini wakati Bingo akiwa na hali hiyo ya taharuki, yule msichana alimgeukia kwanza kisha akaachia tabasamu "Khaa Roy?.." Alijisemea Bingo baada kugundua kuwa yule msichana ni Roya, binti ambaye alikuwa akimtokea mara kwa mara na kumuasa juu ya habari ya Kufika Tropea.. Punde si punde ajazu alirusha upanga wake kuelekea pale aliposimama Roya, ambapo naye kwa umakini kabisa alipotea akaibukia sehemu nyingine. "Hahaha hahahah" Ajuza aliangua kicheko kisha akajitoa mara nne, yaani nafsi nne na kila nafsi ilikuwa na siraha yake. Bingo alishangaa sana, bado alitulia pembeni huku akishuhudia mpambano mkali baina ya Roya na Ajuza. Wote walionekana sio sio binadamu wa kawaida ingawa Roya alionyesha kuwa na baadhi ya vitu ambavyo vilifanana na vya Binadamu. Basi patashika nguo kuchanika liliendelea mahali hapo, Roya alionyesha umahali wa kuzikabili hizo nafsi za ajazu, hivyo moja baada ya jingine aliteketeza mpaka pale alipobaki Ajuza mwenyewe. Mbinu hiyo ikawa imegonga mwamba.. "Lahaa! Kweli hii ni hatari" Alirudia kujisemea Bingo akistaajabishwa na hayo mpambano. Na kipindi anashangaa ghafla upanga aliokuwa akiutumia Ajuza ulitua mbele yake, manusura umjeruhi ni baada Roya kuupangua ambapo uliweza kumtoka kiganjani moja kwa moja ukadondokea mahali aliposimama kijana Bingo. Hapo sasa Bingo akapata kuuona vizuri kabisa upanga huo, haukuwa mwingine ni ule ule aliopewa na mzee Ndelo. Muda huo huo Ajuza akawa anajitahidi kumkabili Roya ili aufuate upanga huo. Na hapo Roya akamwambia Bingo auchukue huo upanga na kisha aondoke mahala hapo "Bingo chukua panga ukimbie.." Alisema Roya kwa sauti ya juu kabisa huku ikijirudia mara mbili mbili. Bingo baada kusikia maneno hayo kidogo aliogopa, lakini mwishowe akaona heri lawama kuliko fedheha. Liwalo na liwe, hima aliuchukua upanga huo akaurejesha kwenye kala lake. Ukakaa sawa kisha mara moja akatimua mbio huku nyuma akiacha Roya akipigana na yule ajuza wa ajabu.

Ila kabla Bingo hajafika mbali.. Alisimama kwanza, machale yakamcheza akahofia usalama wa Roya. Hivyo aligeuka nyuma ajabu kwa mbali akapata kuoana makundi mengine ya wafu yakielekea kwenye mpambano. Pumzi ndefu alishusha Bingo wakati huo akijiuliza "Mmh Naam! Huu ni muda wa mimi kuonyesha msaada wangu kwa Roya. Kwa kuwa amnisaidia kuupata upanga wangu, basi Sina budi kuutumia upanga huu.. Lakini nitaweza kukabliana na hawa wafu?.. Ngoja niende liwalo na liwe kama kufa nitakufa tu" Maneno ya kijasiri aliyanena Bingo ndani ya nafsi yake kisha akachomoa upanga wake akaushika kwa nguvu zake zote. Kwa mara nyingine tena alishusha pumzi halafu akatimua mbio kwenda kumsaidia Roya. Vurumai la maana lilizuka mahali hapo, Bingo alitembea dozi kwa umalidadi wa hatari mpaka akashinda huku Ajuza naye aliamua kupotea kimazingara.

"Pole sana Roya" Bingo alimwambia Roya huku Roya akionekana kuwa hoi bin'taabani. Lakini Roya hakusema chochote alikaa kimya kwanza ingawa baada ya dakika kadhaa kupita alijibu "Usijali.. Ila Bingo bado unasafari ya kuingia mji wa wafu.. Hebu fumba macho.." Bingo alifumba. Muda mchache baadae akaambiwa afumbue ambapo hakuweza kumuona Roya.

"Royaaa.. Royaaa.. Royaaaaaa" Bingo akipasa sauti ya kumuita Bingo huku akigeuka kila upande na hata asimuone. Na pindi yupo kwenye hali hiyo ya mshangao mbele yake alitokea mzee Ndelo.. Mzee huyo akamwambia kijana Bingo "Unajua unafanya sana mzaha kwenye safari hii, sifikirii kama utaweza kufauru huu mtihani. Kwa sababu unaenda na kurudi nyuma. Bingo kuwa makini na safari yako. Hebu achana na huo upanga ulionao sababu utakufanya ukutane na wingi wa maadau ambao watakufanya safari unione chungu.. "

" Mzee wangu! Unamaana gani sasa? Wewe si ndio uliyenipa upanga huu?.. "Alistaajabu Bingo.

" Ahahaha hah hahahah.. Hahahah hahaha ah "Mzee Ndelo aliangua kicheko kisha akaongeza kusema" Hebu nikabidhi huo upanga halafu nikuonyesh njia nyepesi ya kukufikisha Tropea.. "

" Mmmh!.. "Aliguna Bingo wakati huo akimtilia shaka mzee Ndelo. Baada kukumbuka namna upanga ulivyomsaidia akahisi kuwa huwenda ukawa mwisho wa maisha yake.

" Hapana hii ni siraha yangu. Na wewe sio mzee Ndelo.. Hujanipata kwa mtindo huo" Kwisha kusema hivyo alionekana zake ilihali huku nyuma mzee Ndelo aligeuka akawa yule yule ajuza aliyekuwa akipigana na Roya hapo awali. Ujuza huyo aliamua kutumia njia hiyo akiamini kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kijana Bingo kumuamini akamkabidhi upanga huo. Hapo alipotea. Bingo alipogeuka nyuma hakumwona hivyo aliamua kutimua njia kwa kutumia ramani yake.

********http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Millander, hapo nikawa nimefauru huo mtihani yani kiasi kwamba endapo ningemkabidhi upanga yule ajuza aliyechukua taswira ya mzee Ndelo. Bingo ningekwisha. Basi niilitimua mbio kwa kumfuata ramani, ila pindi safari inaendelea mbele yangu nilimuona mama mjamzito akiwa kando ya njia. Mama huyo uchungu ulikuwa umemshika kwahiyo alikuwa akigaaagaa huku na kule wakati huo anapiga kelele akihitaji msaada. Sasa basi mimi pasipo kufikiria ama kujiuliza mama huyo kafikaje mahala hapo, haraka sana nikataka kumgusa ili nimuulize maswala kadhaa ikiwezekana niweze kumsaidia.

"Mmh kumsaidia? Sasa ungemsaidiaje wakati wewe sio doctor?.." Aliuliza Millander mkewe Bingo.

"Ndio hapo sasa maajabu hayo. Tulia nikusimulie ili hata siku nyingine usinishangae pindi takapo toka nyakati za usiku huku nikirudi nanukia ubani ilihali sehemu mbali mbali za mwili wangu zilionekana damu. Tropea mamaa Tropea hiyo.. Oonhoo hatari sio mchezo nakwambia "Bingo alijibu huku akitia utani kidogo. Millander alionyesha utulivu, na hapo Bingo akapata wasaa wa kuendelea kusimulia. Basi kabla sijamgusa, niliguswa mgongoni. Nikishtuka haraka sana nikageuka kumtazama mtu huyo aliyenigusa, cha ajabu mtu huyo na yule mama mjamzito walifanana kila kitu. Nilishangaa sana, niliporudisha macho yangu kumtazama yule mama aliyekuwa anagagaa chini ajabu sikumuona, yule naye aliyenigusa alipotea.

******

Bingo alipagawa akatoka mbio, alikimbia sana. Mbele zaidi aliona njia tatu. Njia moja ilielekea kulia na nyingine ilielekea kushoto vile vile njia ya tatu ilinyooka. Hapo sasa akachomoa ramani ili impe muongozo. Ramani ikamuonyesha kuwa anatakiwa anyooshe, jambo ambalo lilimfanya kijana Bingo kuachia tabasamu kisha akaendelea na safari. Alitembea umbali mrefu sana pasipo kubuguziwa na mauzauza yoyote, hali ambayo ilimfurahisha sana. Hatimaye anapata kuona ngome iliyojengwa kwa dhahabu huku ngome hiyo ikiwa imepambwa nembo mbali mbali za kuzimu,juu ya ngome hiyo kuna ubao uliandikwa maneno ya kuitambulisha ngome hiyo, hivyo Bingo aliinua uso wake ili ayasome maandishi hayo yaliyoandikwa kwenye huo ubao ili ajue kama yameandikwa Tropea ama la! Lakini kabla hajaanza kusoma, ghafla aliguswa bega, hima aligeuka akakutana uso kwa uso na mtu aliyefahamu, mwanakijiji mwenzake ambaye alifariki miaka kadhaa iliyopita. Kifo chake kikisababishwa na ajari ya gari. "Habari yako Bingo, vipi mama na baba yangu wazima?Vipi mke wangu na mwanangu! .." Alisema mtu huyo wakati huo.





"Habari yako Bingo, vipi mama na baba yangu wazima?Vipi mke wangu na mwanangu! .." Alisema mtu huyo. Bingo alitaharuki sana, akajiuliza ndani ya moyo wake "Inamaana Michael hajafa au macho yangu?.."

"Huna budi kujiuliza maswali mengi Bingo, kwanza kabisa karibu Tropea. Nafikiri uwepo wako huku utaweza kuleta manifaa kwenye ngome ya baba yako.." Aliongea mtu huyo, mtu ambaye Bingo alifahamu fika sababu alikuwa moja ya wanakijiji mwenzake, ila alifariki kwa ajari ya kugongwa na gari. Maneno hayo yalimshtua Bingo, na hapo ndipo alipoinua macho yake kuutazama juu kwenye ngome ambapo lilionekana bango. Bango hilo liliandikwa kwa lugha ya ajabu sana, lugha ambayo ilimuwea ngumu Bingo kufahamu kilicho andikwa

"Pale juu pameandikwaje?.." Bingo alimuuliza yule mtu aliyeitwa Michael. Michael aliangua kicheko kisha akajibu "Karibu Tropea.. Bingo huu ndio mlango wa kuingia Tropea,mji uishio wafu. Sisi huku ni watumwa.. Kuwa makini sana Bingo, sababu tayari mji huu umechafuka sana shauri ya pande mbili tofauti kuzozana..." Aliongea Michael kwa kirefu zaidi. Pumzi ndefu alishusha Bingo, hata asiamini kama kweli kafika mji huo aliotakiwa kufika. Na wakati yupo katika dalali hiyo ya taharuki mara ghafla Michael alipotea, na punde si punde wakatokea watu wawili waliovaa koti nyeusi huku nyuso zao zilionekana kutisha kutokana na namna walivyofanana. Walikuwa warefu kuliko binadamu yoyote duniani, miili yao mikubwa. Macho yao yalifanana fika na macho ya nyoka ilihali midomo yao nayo ikiwa ya kawaida kama ilivyo ya binadamu kasoro rangi ya ngozi yao ambayo kwenye nyuso walionekana kuwa na rangi nyekundu.

"Bingo..!.." Moja ya watu hao wawili alipasa sauti kumuita Bingo. Bingo akaitika.

"Karibu sana Tropea.." Mtu wa pili alisema kisha wote kwa pamoja wakainamisha nyuso zao wakitii heshima kwa kijana huyo. Ni heshima ambayo ilimshangaza Bingo, jambo hilo lilimfanya sasa roho yake kuwa na imani akiamini kuwa tayari yupo katika lango la kuingilia Tropea. Muda mchache baadae lango la ngome hiyo ulifunguka kisha mmoja akaongoza kuingia ndani akifuatia na mwenzake ambaye naye alimtaka Bingo amfuate nyuma. Bingo alifanya kama alivyoambiwa lakini kabla hajaingia ndani.. Nyuma yake alitokea mzee Ndelo. Mzee huyo alikohoa kidogo kisha akamuita Bingo. "Bingooo!.." Bingo alishtuka kusikia sauti hiyo, haraka sana akageuka akakutana na uso wa mzee huyo ambaye alimpa njia ya kuelekea Tropea. Mzee Ndelo akiwa na tabasamu bashasha alinyooshea Bingo kidole gumba akimanisha kuwa mambo sio mabaya,ambapo Bingo naye tabasamu hilo alilijibu hivyo hivyo kisha naye akamnyooshea kidole kama alivyofanya Ndelo. Lango likafungwa, Bingo akatokomea na watu hao. Ajabu alipata kuona majengo marefu kwa mifupi, mikubwa kwa kidogo. Na jambo ambalo lilimshangaza zaidi Bingo ni baada kuona maisha ya Tropea hayajapishana sana na maisha ya ulimwenguni. Watu waliendelea kufanya shughuli zao kama kawaida,watembea kwa miguu walionekana wakitembea ilihali vile vile waendesha magari waliyaendesha magari yao kwa kasi. Hali ya hewa ya mji huo ilikuwa hafifu mfano wa hali ya hewa ya duniani pindi jua lizibapwo na mawingu mzito ya mvua. Mbali na hayo yote, lakini pia watu wa Tropea hubadilika kutokana na siku. Juma tano, ijumaa pamoja na juma pili. Hizo ndizo siku ambazo watu wa huo mji hubadilika kuwa wafu ambapo hapo ndipo huchaguliwa baadhi ya watu hutumwa duniani kufanya mauaji kwani siku hiyo ndio siku ambayo Tropea hutakiwa damu ili kupata chakula ambacho ndicho huwafanya watu hao kuishi. Watu waishio ndani Tropea hutegemea nyuma za binadamu ikiwa kinywaji nacho hutumia damu.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Bingo.."

"Naam! Naona umekipenda kitabu hicho lakini pia unaonekana kukiogopa.. Na yote sababu ya mambo yaliyoandikwa humo ndani.." Aliongea mtu mmoja kati ya wale wawili waliompokea Bingo. Mtu huyo alikuwa kando ya Bingo, mmoja alisimama kulia na mwingine alisimama kushoto. Ni kitabu kikubwa alichokabidhiwa Bingo mara baada kuingizwa ndani ya chumba ambacho ndani yake zilisikika sauti za watu wanaolalalma na wengine kupiga kuomba msaada. Hivyo Bingo baada kusoma baadhi ya mambo yaliyoandikwa katika kitabu hicho, pumzi ndefu alishusha ilihali muda huo huo ndani ya chumba hicho aliingia mwanadada ambaye alionekana kuvaa gauni ndefu huku miguu yake ikiwa kwato za ng'ombe. Dada huyo mkononi alishika plet moja ya iliyojaza sahani na bakuli. Alitembea kwa madaha kuelekea mahali aliposimama Bingo,ambapo mara baada kumkaribia aliichukuwa kitabu hicho ambacho alikuwa akikisoma kisha akamsogezea plet hiyo ambayo ilionekana kuwa na hasani pia na bakuli iliyojaza vyakula.

"Karibu mwana Abd. Chakula hiki ni mahususi kwa ajiri yako.." Aliongea dada huyo halafu akapotea.

Ukweli muda huo tumbo la Bingo lilihisi njaa kali mno, kwahiyo haraka sana alipitisha stick ndani ya bakuli ili aanze kula.. Ajabu alipouvuruga mchuzi uliokuwemo katika bakuli hilo, aliona macho ya binadamu pamoja na ulimi.. Ilihali muda huo mchuzi wa mboga hiyo ulitoa harufu mbaya sana..

"Nini hii?.. Aliuliza Bingo. Wale watu wawili ambao muda wote walikuwa wamemsimama walitazamana kisha mmoja akasema kwa sauti nzito" Bingooo mwana wa Abd.. Unakazi ngumu iliyopo mbele yako. Hupaswi kuuliza zaidi ya kula ili uanze kufanya kile kilicho kuleta ndani ya mji huu.. " Maneno hayo yalisikika kwa ukali kitendo ambacho kilimuogopesha sana Bingo, na hivyo hakuwa na namna alikula japo kwa tabu sana.

Muda mchache baadae, Bingo akaingia mtaani sasa mjini Tropea kuangalia maanzali ya mji ikiwa wale watu wawili tayari wameshapotea kwani shughuli yao ilikuwa imeshamalizika. Shughuli ya kumpokea Bingo na kisha kumsimamia katika suala nzima la chakula. Lakini kitendo ambacho lilimshangaza Bingo ni pale kila alipokuwa akipita watu walimsujudia, si mkubwa wala mtoto. Wote heshima walimpa.

Hatimaye kwenye tembea tembea yake kwa mara nyingine tena anakutakana na Michael, kwa sauti ya juu Michael akamwambia Bingo "Bingo, naona tayari upo mtaani.. Heshima yako mkubwa.."

"Michael, hebu subiri kwanza, hivi mbona kila ninapo pita watu wanainisujudia?.." Aliuliza Bingo kwa taharuki baada kuonana na Michael mtu ambaye anaishi kwenye ulimwengu wa kiroho ilihali duniani akihesabika kuwa ameshafariki. Michael baada kuyasikia maneno hayo ya Bingo alicheka sana, sauti ya cheko lake lilijirudia mara mbili mbili. Alipolikatisha akamjibu "Bingo wewe ni mtu mkubwa sana hapa Tropea,muhimu kumbuka ulichofuata huku ili uweze kurudi salama..."

"Unamaana gani?.." Alihoji Bingo. Michael akajibu "Kwanza kabisa wewe kula nyama ya mtoto mchanga mwenye sekunde kadhaa tangu azaliwe. Hiyo ni heshima kubwa sana kwako, sababu chakula hicho huliwa na viongozi wakubwa wa mji huu..."

"Khaa? Michael unataka kuniambia kuwa nimekua nyama ya binadamu?"

"Ndio Bingo.."

"Doh!.. Kwahiyo huku Tropea mnazaliana?.."

"Hapana, kwanza fahamu huu mji ulipotea karne ya 15. Mji ambao ulifukiwa baada kutokea tetemeko kubwa la ardhi. Mengi nitakueleza Bingo, sababu kila kitu nakifahamu juu ya mji huu. Nitakueleza namna watoto tunavyowaiba hospitalini, lakini pia nitakueleza ajari tunazo sababisha mjini angani na nchi kavu. Hata meli kubwa kuliko zote duniani iliyowahi kuzama akapona mtu mmoja. Sisi ndio chanzo.. "

" Meli gani?... "Aliuliza Bingo kwa mishangao wa hali ya juu. Michael aliangua kicheko kisha akajibu..







"Meli gani hiyo?" Ndilo swali alilouliza Bingo. Michael aliangua kicheko. Alicheka sana kisha akamwambia "Nifuate huku" Bingo alifanya kama alivyoambiwa. Wawili hao walielekea kwenye moja ya nyumba kubwa. Nyumba ambayo ndani walikuwemo watu wengi sana wakiimba na kucheza.. Michael akamtaka Bingo wakaketi kwenye meza kisha aendelee kumueleza maisha na maajabu mbali mbali yaliyopo kwenye ulimwengu wa pili. "Bila shaka unawaona watu hawa" Aliongea Michael.

"Ndio nimewaona.." Bingo aliitikia. Ambapo hapo ndipo Michael alipongeza kusema "Watu hawa ni wale waliopata ajari kwenye iliyokuwa Meli kubwa kuliko zote duniani. Na katika ajari hiyo alipona mtu mmoja tu. Na sababu nzima iliyopelekea Meli ile kupata ajari ni baada kiongozi wa wafu kuingiwa na tamaa ya wingi wa watu wale, akaamini kabisa endapo kama atapiga ndege wawili kwa jiwe moja basi itakuwa moja ya faida kubwa sana na istoshe siku ile ambayo Meli ile ilianza safari ilikuwa siku ya sikukuu Tropea.. Si kweli kwamba angeokoka mtu mmoja, la hasha wangeokoka watu zaidi ya elfu ila siku mji huu uliamua kuishangaza dunia " Alisema Michael kwa kirefu zaidi, akilini mwake akiifahamu fika Meli hiyo.

" Naam! Nakuelewa Michael. "Aliunga mkono Bingo, Michael alicheka sana kisha akasema" Sasa watu hawa unao waona huku ndani ndio wale waliokuwemo katika Meli ile. Labda ngoja nikuulize swali Mr Bingo. Hivi hujawahi kuambiwa na mtu kuwa kuna wakati baharini huonekana mauza uza?.. "

" Ndio mara nyingi tu. "Alijibu Bingo.

" Basi,ukae ukijua kuwa kuna wakati roho zinatoka Tropea zinatembea kwenye uso wa dunia iwe baharini ama nchi kavu. Lakini pia ukae ukijua kuwa Meli ile iliyozama akapona mtu mmoja kuna wakati huonekana iliendelea na safari yake saa za usiku ingawa kwa macho ya kawaida huwezi kuiona... " Aliongeza kusema Michael. Ukweli yalikuwa ni maneno ambayo yalimshangaza sana kijana Bingo, hivyo macho yake akayarudisha kutazama kule wanakoonekana watu wale waliokuwepo kwenye Meli ya Titanic. Watu ambao muda wote walikuwa wakiimba na kucheza huku wengine wakila na kunywa.

Hatimaye wawili hao walitoka ndani ya jengo hilo, wakazipiga hatua kuingia kwenye jengo lingine ambalo nalo ndani lilisheheni watu mbali mbali pamoja mashine za ajabu ajabu, mashine hizo zilikuwa zikilindima huku sauti za watoto wachanga zikisikika wakilia. "Hiki nacho ni kiwanda.." Aliongea Michael.

"Kiwanda?.. Kinatengeneza nini?.." Bingo alihoji. Michael akajibu "Ndio maana nakakwambia kuwa kuna wakati maisha ya huku hushabiana vema na maisha ya ulimwenguni. Bingo huu ni mji, kwahiyo dhumuni kuu la mji huu ni kuzidi kutia sumu ulimwengu ili magonjwa yazidi mpaka kupelekea kifo.. Kifo pekee ndio njia ya kumfanya mtu afike Tropea.. Ingawa kuna baadhi ya nafsi hurejea duniani, na ndio pale unaposikia kuwa marehemu fulani kaonekana sehemu fulani.. "

" Na hawa watoto nao vipi?.. "http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

" Hawa wengine hunyofolewa wakiwa tumboni kwa mama zao, na wingine huchukuliwa pindi wanapozaliwa. Kuna watu wanatumwa kuzungunga hospital kubwa zote kufanya kazi hii. Kuna baadhi ni madaktari na wingine ni nafsi tu..."Alisema Michael. Hapo Bingo alistuka, kwa taharuki ya hali ya juu akamuuliza Michael mara mbili mbili" Michael unataka kusema katika hospital kuna madaktari wa uongo?.. "

" Ahahaha haha " Michael aliangua kicheko kwanza kisha akajibu" Asilimia mia moja kijana. Na ndio pale mama mjamzito anaweza kujifungua mtoto kisha akaambiwa mtoto bahati mbaya kafariki aidha mtoto anapoteza katika mazingira tatanishi. Wakifikishwa huku sasa, wanasagwa kisha baadhi hugeuzwa kitoweo huku na baadhi hupelekwa kwenye maduka ya vyakula Duniani..."

"Na hayo magonjwa nayo husababishwa na nini?.." Alihoji Bingo, lakini kabla Michael hajamwambia. Mara ghafla nje ilisikika shangwe za wafu wakitimua mbio. Jambo ambalo lilimshtua Bingo, hima akamtazama Michael kisha akarudia kumuuliza nini kinacho endelea nje. Michael akamtaka atulie, kisha akasogelea dirisha akapata kumuona mtu wa ajabu akifanya fujo mtaa huo. Ajabu mtu huyo alitishia amani zaidi huku akimtaka Bingo popote pale alipo ajichomoze..

"Mbona nasikia jina langu?.." Michael alimgeukia Bingo akamtazama kisha akamjibu " Hii ndio sababu kuu iliyokuleta Tropea Bingo,.."Michael alisema wakati huo aking'atuka kwenye dirisha na kuzipiga hatua kumsogelea. Alipomkaribia zaidi akaendelea kusema" Huyu ni mfuasi wa Buda, kundi linalo ongozwa na kijana wa Sultan Starlon. Nadhani baada kusikia mtoto wa jamii ya Abdy, mtoto wa Sultan Abatish tayari yupo katika mji huu, anataka kukumaliza mapema ili mpango wake uweze kutimia... Tambua unakibarua kizito sana Bingo, usimuangushe mzee wako na najua anahamu sana ya kukuona.. " Alisema Michael wakati huo huo nje fujo ziliendelea na punde si punde ikatokea ulingo mrefu uliojengwa kwa dakika kadhaa kisha mfuasi huyo wa Starlon akaendelea kupasa sauti yake kumuita Bingo huku akidiliki kutisha kuteketeza wafu wengine na kisha kuwageuza kitoweo.

"Michael kipi sasa nifanye?.."

"Kupigana unaweza?.."

"Ndio.."

"Kweli unaweza kuutumia vizuri upanga?.."

"Hilo ondoa shaka kabisa.."

"Basi.. Jitokeze, nje tayari kuna ulingo mkubwa ambao upo kwa niaba yako.." Aliongeza kusema Michael kwa sauti ya upole iliyojaa huzuni ndani yake.

Hapo ndipo Bingo alipovaa stahiki koti lake kisha akafungua mlango akajitokeza kukabiliana na yule mtu ambaye kimuonekano sio mtu wa kawaida... Ajabu fujo za vilio zilitoweka, safari hiyo ikisikika sauti ya kumshangilia Bingo..

"Bingo.. Bingoooo.. Bingoooo.. Bingoooo.." Na Kadili shangwe hizo zilipokuwa zikisikika ndivyo wafu wengine walivyozidi kuongezeka kumshuhudia kwa mara ya kwanza mtoto wa kiongozi wao bwana Sultan Abatish.. Bingo alishangazwa na shangwe hizo, muda huo akamtazama yule mtu wa ajabu anayetarajia kupigana naye kisha akarudisha uso kumtazama Michael. Michael akamnyooshea dole gumba. Na hapo na hapo wawili wa wakapanda kwenye ulingo.. Ndivyo shangwe zilipozidi, jina la Bingo lisikauke midomoni mwa wale wafu.. "Bingo... Bingoooo Bingoooo.."





Shangwe zalizo sikika zilimfanya Bingo kujawa na mzuka mara mbili ya hapo awali, hivyo haraka sana alichomoa upanga wake kisha akawa tayari kwa mpambano. "Bingooo.. Bingoooo Bingooo" Bado sauti za wale wafu ziliendelea kumshangilia Bingo. Muda huo huo yule mfuasi wa ngome ya Starlon naye akachomoa upanga wake, na hivyo wote wakawa tayari kwa niaba ya mpambano. Punde mtu huyo alirusha panga lake.. Bingo alikwepa kwa style ya kutembelea magoti, panga hilo likawa limepiga moja ya mbao zilizojenga ulingo. Na kwa nanamna panga hilo lilivyokuwa na makali ilipelekea mbao hiyo kukatika vipande viwili. Bado patashika ilizuka ulingoni hapo, kijana Bingo alionyesha ushujaa wa kumkwepa vilivyo mtu huyo ambaye kimuonekano alionekana ni mahali sana kuchezea panga. "Bingo.. Hapa ndio mwisho wako.." Aliongea mtu huyo kwa sauti ya kutisha wakati huo huo akarudia tena kutembeza kichapo ingawa alionyesha sio chochote kwa kijana Bingo. Bingo aliruka samasoti aliruka salakasi ya kila aina.. Jambo ambalo liliwafanya wafu hao waliokuwa wakishuhudia pambano kuzidisha nguvu ya kushangilia. Michael alionekana kubaki mdomo wazi, na hata asiamini kama kweli ni huyu huyu Bingo anayemfahamu yeye.

"Laah! Noma sana" Alijisemea Michael huku mikono ikiwa kichwani akikoshwa na uwezo wa Bingo.

Baada muda wote Bingo kuonekana akikwepa mapigo ya mtu huyo mfuasi wa ngome ya Starlon, hatimaye sasa akaona ni wakati wa yeye naye kuonyesha umwamba mbele ya mtu huyo kwani kwa muda wa taklibani dakika therathini alikuwa akimsoma namna anavyopigana na janja anayotumia. Hapo kwanza Bingo aliangua kicheko "Ahahaha hahahah" Alipokwisha kukatisha kicheko chake akamnyooshea kidole kisha akamwambia "Wewe.. Hebu nisikilize. Jina lango naitwa Bingo. Mimi ni nafsi na sio mfu. Kwahiyo sijaja Tropea kushangaa majengo yenu sababu kama ni majengo basi hata duniani yapo mengi sana. Nimekuja Tropea kufanya mapinduzi, tazama uma wa wafu hao hapo chini. Wafu hao wanangoja kuona maajabu yangu, hivyo basi nakupiga, nakuchalaza kisha nikutumie ukamwambie mkubwa wako kuwa, maji yameingia upupu na hivyo sio rahisi kuyaoga.. " Aliongea Bingo huku akionyesha kujiamini asilimia mia moja. Ni majigambo ambayo yalifanya eneo hilo kulipuka shangwe, na mwisho wa shangwe hizo jina la Bingo lilitajwa ilihali likisindikizwa na makofi ambayo yalipigwa sambamba na jina" Bingo.. "Hapo makofi yalisikika, hivyo hivyo ilimladi kumfanya Bingo ajihisi amani. Amani ambayo itampelekea kujiamini, na mwisho wa kujiamini kinacho fuata ni ushindi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

" Ahahaha hahahah "Alicheka sana mtu huyo baada kuyasikia maneno ya dharau aliyoyaongea kijana Bingo. Kicheko cha mtu huyo kilisindikizwa na ngurumo nzito ambazo ziliambatana na miale ya radi. Na mara baada ya kuhitimisha kicheko hicho alinyoosha mkono juu, punde katika kiganja chake lilitokea rungu kubwa lenye misumari ilihali muda huo huo nywere zake ziligeuka nyoka. Bingo alishtuka lakini kwa kuwa toka awali alishaonyesha moyo wa kujiamini.. Hivyo hakutishika na mambo hayo, nywere hizo ambazo ziligeuka nyoka alizichukulia ni rasta hali ya kuwa rungu hilo la misumari alichukulia kama fimbo tu. Hapo Bingo alishusha pumzi ndefu kisha akautupa kando upanga wake na mara moja kwa kasi ya ajabu akamvagaa huyo mtu. Pambano kwa mara nyingine tena likaendelea,safari hiyo Bingo hakuogapa. Japo huyo mtu mfuasi wa kutoka ngome ya Starlon alionekana kuwategemea nyoka walipo kichwani mwake ila bado mipango yake ilishindwa kumpa matokeo chanya, alipigwa kama mbwa mwizi. Bingo baada kuona mtu huyo hana tena Jeuri alichukuwa upanga wake kisha akamsogelea, akafungua kifungo cha koti lake upande wa kifuani, akajichana kwa upanga wake, upanga huo ukiwa unatiririsha damu akamnyooshea mtu huyo kisha akasema "Nakuacha ili upeleke ujumbe huko kwenye ngome yenu, mwambie kuwa Bingo yupo ndani ya Tropea.."



*********



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog