Search This Blog

JOTO LA MSHUMAA - 1

 






IMEANDIKWA NA : MUDHIHILI H. MNALI



*********************************************************************************



Simulizi : Joto La Mshumaa 
Sehemu Ya Kwanza (1)


 ...Ndani ya kijiji kimoja kijulikanacho kwa jina la BWAWANI. Kwenye familia moja ambayo ilikuwa chini ya usimamizi wa bwana Mzee MAMBO SASA, alikuwa anishi na familia yake mkewe pamoja na mwanawe wa kike aliyejulikana kwa jina la SIKITU. Katika maisha ya mzee huyo alijiwekea utaratibu ambao ulihusiana na kumuweka mwanae katika utaratiibu na desturi za adabu na heshima, pia aliweza kumsomesha mwanae japokuwa ndani ya kijiji cha Bwawani hakikuwa na muamko kabisa na swala la usomeshaji wa watoto zao. Hivyo ilikuwa ngumu sana katika maendeleo ya elimu ndani ya kijiji hiko. Mzee Mambo sasa siku moja aliokaa na mwanae na kumuambi mambo muhimu sana ambayo hayakuenda mbali na maswala ya kumjenga kielimu zaidi.

''Mwanangu mimi baba yako naomba nikueleze jambo ambalo lina manufaa sana katika maisha yako ya sasa pamoja na baadae, kwanza naomba ushike sana masomo mkwani hata wengi wetu wanasema kuwa elimu ni ufunguo wa maisha sawa Sikitu''http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mzee Mambo sasa aliweza kumueleza mwanae swala hilo huku sikitu akiwa makini sana katika kumsikiliza baba yake. alionekana kumuelewa vyema sana baba yake kutokana na umakini wake wa kusikiliza.

''Baba nimekuelewa na nitafanya kama hivyo unavyoniambia nifanye baba yangu''

baba yake hakuwa na neno zaidii ya kumsisitizia kwa yale ambayo alishamueleza ayazingatie. lakini Mzee huyo alionekana kuwa na shauku kubwa ya kutaka kumueleza mengi sana mwanae juu ya umuhimu wa hayo mambo kuyashika kwa makini.

''Nakuomba SIKITU uyashike sana haya mambo usiwe kama wasichana wenzako hapa kijijini sitaki hata kusikia ukifanya upuuzi kama wanaoufanya hao wenzako, jitahidi ufikie hatua kama aliyofikia baba yako mdogo ambae kwa sasa yuko mjini nilimsomesha vyema mpaka kafikia pale na wewe napenda ufikie kama alipo yeye, haya mimi naelekea shambani nitakukuta baadae nikisharudi''

Mzee MAMBO SASA aliinuka na kuelekea ndani na kuchukua baadhi ya vifaa kama jembe, panga na dumu la maji. kwa kuwa ilikuwa majira ya asubuhi yeye alikuwa kachelewa kidogo kutokana na mambo ya nyumbani ambayo alikuwa akiyafanya hapo nyumbani kwake. Alifanya haraka kuelekea shambani huku akiwa anaimba nyimbo za hapa na pale. Baada ya muda fulani aliweza kufika hadi shambani na kumkuta Mmama sikitu akiwa anaendelea kulima. Kumbe mama sikitu alitangulia na kumuacha mumewe akiwa anaongea na mwanae sikitu, Mzee huyo alimueleza mkewe kuhusu mipango yake ya kutaka mwanae akae katika maisha yenye mwenendo wa kusoma ili atofautiane na wanawake wengine wa pale Bwawani. Baada ya muda Mama sikitu aliweza kuondoka kwani alikuwa tayari keshachoka hivyo akamuaga mumewe na kumuacha mzee huyo akiendelea kupiga jembe.

Baada ya muda kupita naye aliweza kuchoka na kuacha kuendelea kulima kisha akakusanya vifaa na kuanza kuondoka. Akiwa njiani anakutana na Mzee mwenzake alioyejulikana kwa jina la Mzee SIKUJUA. Alisalimiana nae kisha wakaongozana pamoja katika safari nzima ya kwenda majumbani kwao, Mzee Sikujua alianzisha mazungumzo ambayo hata mzee Mambo sasa aliweza kuchangia kwa ufasaha, lakini kila muda ulipozidi mazungumzo hayo yali0onekana kuwa chachu kwa Mzee Mambo Sasa.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

''Bwana Sikujua unafahamu kuwa mwanangu kwa kipindi hiki alichonacho nataka ajitahidi afike mbali kupitia elimu yake mana bila kusoma hawezi kuendelea kabisa kwa sasa'' Aliongea maneno hayo kumueleza rafiki yake huyo

''Mh! Sawa lakini wewe hukusoma sasa mbona maisha yako yako mazuri tu bwana Mambo Sasa, alafu kwa biti wa kike haki ya nani nakuhakikishia kuwa unamaliza fedha zako tu kumsomesha mwanao wa kike hivyo cha kufanya acha kumsomesha kabisa mwanao huyo na hizo fedha ni boira upeleke kwenye mashamba na upate fedha nyingi sana''

Maneno hayo yalimchoma kabisa bwana Mambo sasa hivyo alimuangalia sana bwana Sikujua na kumtoa umaana kabisa kwa mtu mzima kama huyo.

'' yani wewe nilikuona kama mtu mkubwa wa umri na utakuwa na mawazo mazuri yenye maendeleo lakini una ukubwa wa mwili na miaka lakini hakuna kitu kabisa kichwani mwako unafikiria pumba tu yani niache kumsomesha ,mwanangu kwa akili zako finyu kweli '' Mambo sasa alionekana kukasirika sana

'' kwa hiyo unanitukana mimi, sasa hii taarifa itawafikia viongozi wa kijiji kuwa umenitusi kama uanaona kuna ubaya wa haya niliyokuambia basi tutaona nani mjanja na kama huyo mwanao utafikia hatua ya kumsomesha mbali na akafika mjinga wewe, yani wewe ni mdogo kabisa kwangu na unanitukana mimi tutaona'' Mzee Sikujua nae hakuwa mbali aliweza kujibu mashambulizi na hapo pakawa hapaeleweki kabisa na mtafaruku ulitaka kufika mbali ndipo alitokea bwana mwingine kijana kwa umri ambae nae alikuwa anatokea shambani na kuwakuta wakiw wanazozana hapo wazee hao wawili. Aliamua kuwatawanya kwa busara sana ambazo ziliweza kueleweka kwa Mzee Mambo sasa na si kwa Sikujua.

'' Jamani wazee wangu mbona mnataka kufikia mbali hivyo nyinyi ndio tunawategemea hapa kijijini na ndio kioo ambacho mnatufunza sisi vijana na kutukanya pale tunapokosea sasa mkionekana mnazozana hapa njiani sisi mnatufunza nini ambao tunawaona cha kufanya nendeni mkae chini na mtatue msije kufika pabaya jamani''

Kijana huyo alimaliza na kuwaondoa kwani walikaribiana na kutaka kuonyeshana umwamba. lakini mzee sikujua hakutaka kuelewa chochote kabisa zaidi ya kuendelea kuongea maneno makubwa ambayo hayakuwa na sitara kwa Mee mwenzake.

'' Yani nakuambia kuwa utanitambua siji kukusaidia kwa chochote yani unanitukana mimi kuwa ni mpumbavu nisiyejua kufikili na nina ukubwa wa umri lakini sina akili sawa mimi naenda lakini utanitambua''

Mzee Sikujua aliondoka na kumuacha kijana na Mzee Mambo sasa wakiwa wanaongea. Walirudi na kuachana pale kisha Mzee Mambo sasa akaenda nyumbani. Ulipita muda sana mpaka jioni wakiwa nyumbani hapo walikaa kama familia na Mzee Mambo sasa akiwa na mawazo juu ya ugomvi ule ambao ulijitokeza muda mchache uliopita. Hali hiyo iliweza kuonekana kwa mkewe na sikitu ambae alikuwa karibu sana na mama yake. kutokana na hali ya maisha yao yalivyo yalikuwa ni ya duni sana ndio maana mzee huyo alijikita zaidi kwenye kilimo cha korosho na kupata fedjha ambazo zinatumika kumsomeshea mwanae ambae yuko shule ya msingi Bwawni darasa ;la saba akiwa anakaribia kumaliza elimu yake.

'' Mume wangu mbona leo hauko sawa kabisa kama siku zote kuna nini ambacho kinakusibu maana tangu mchana nimekuacha shambani uko na furaha yako lakini umerudi aaah umebadilika kabisa'' Mke wa Mzee huyo alihoji baada ya kumuona mumewe hayuko kwenye hali ya kawaida kama alivyoizoea.

'' Ni kweli mke wangu lakini si ya kuzungumza sasa hivi tutaongea baadae au ngoja kwanza sikitu ebu kaangalie kwanza kuku kama wametimia ndani humo alafu uje uniambie''

sikitu alinyanyuka na kuelekea kwenye banda la kuku ambalo aliambiwa na kuwaacha wazazi wake wakiendelea kuongea

'' Mke wangu nimemtoa mtoto ili nikueleze kuwa nimegombana na mzee Sikujua'' Aliongea kimyakimya

'' Heeee kwa yapi tena mume wangu mpaka ugombane nae jamani''

'' Eh wakati narudi nyumbani, njiani tulikutana na sikujua sasa akili yake anataka nisimsomeshe sikitu kwa kuepusha gharama kubwa aliyoifikilia mimi nikamuambia msimamo wangu juu ya huyu mtoto ndipo ugomvi ulipoanzia lakini akawa ananitishia amani jambo ambalo maishani mwangu siliogopi''

wakati wanamalizia maongezi ndipo sikitu alirejea na kumuambia kuwa wameshatimia. Walilala usiku huo mpaka asubuhi lakini mzee Mambo sasa hakutaka kwenda shambani kwani hakuwa sawa kiakili kutokana na mambo mengi sana yanayoendelea pale kwake. Wakati huo anagongewa mlango akiombwa atoke nje alivyotoka anakutana na mwenyekiti ambae mkononi alikuwa na barua na akapatiwa aisome baada ya salamu na kukabidhiwa karatasi hiyo akaaga na kuondoka zake. Mzee huyo aliduwaa sana kisha akaingia ndani na kutaka kuanza kuisoma...

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

...Wakati huo anagongewa mlango akiombwa atoke nje na alivyotoka anakutana na mwenyekiti ambae mkononi mwake alionekana kuwa na karatasi ndipo akapatiwa aisome hiyo ilikuwa ni barua. Baada ya salamu na kumkabidhi karatasi hiyo ndipo akaaga na kuondoka zake. Mzee huyo aliduwaa sana ndipo akaingia ndani na kutaka kuanza kuongea alishika tamaa kwanza huku akizungukazunguka ndani humo huku akijiuliza kipi ambacho kimeandikwa ndani ya karatasi hiyo. Alihifadhi kwenye koti lake na kutoka nje huku akiangaza huku na kule na kuanza kumuia Sikitu ambae hakujulikana wapi aliko.

''Mh! jamani huyu mtoto kaenda wapi jamani,.....''

Ndipo alirudi ndani na kuchukua karatasi ile pamoja na kiti akatoka nje na kukaa barazani hapo akafungua ile karatasi ile na kuangalia angalia. Alionekana kutofahamu chochote ambacho kimeandikwa ndani yake ndio maana akawa anamhitaji mtoto wake Sikitu ili aweze kumsomea barua hiyo. Akiwa kapumzika anwaza jinsi gani mambo ambayo atayafanya kuhusu swala lake la kumsomesha mwanae, Sikitu alifika na kumkuta baba yake akiwa kazama kimawazo sana, alimuuliza kulikoni kukaa na hali ile ambayo aliyonayo.

''Haa! mwanangu afadhali sana umefika nilikuwa nakutafuta, embu kaa hapa kwanza mwanangu unisomee hii karatasi maana macho yangu hayaoni vizuri''

Mzee Mambo sasa aliweza kumuambia mwanae atulie chini, Sikitu alikaa na kuchukua karatasi ile ambayo baba yake alimpatia ili aisome. Sikitu alikaaa tayari kwa kuanza kuisoma huku baba yake akiwa anasikiliza kwa makini sana.

''Husika na taarifa ya hapo juu kuwa Mzee Mambo sasa unahitajika ofisi ya mtendaji wa kijiji kuja kusikiliza shitaka lako bila kuchelewa''.

Sikitu alimaliza kusom kisha akamuuliza baba yake kuwa ni kitu gani ambaho kakifanya mpaka ahitajike huko ofisini, Baba yake aliona swali gumu sana ambalo kaulizwa kwani alishindwa kuelewa shida ni kitu gani na kwa kosa gani ambalo anaitiwa, Mzee Mambo sasa alimuomba Sikitu ili akamuite kijana mmoja ambae anaitwa SUSU, Sikitu alienda haraka kule ambako alielezwa na baba yake, alifika pale kwa bwana susu ambako aliambiwa kwenda kumfuata na hatimae aliweza kumkuta na kumuambia ile salamu ambayo aliagizwa na baba yake.

Waliongozana mguu kwa mguu kuelekea kwa bwana Mambo sasa, njiani sikitu aliweza kuuliza swali kuhusu baba yake kama anweza kutambua nini ambacho kimemtokea, kijana huyo alimueleza kuwa hatambui chochote kuhusu jambo hilo na yeye ankwenda kumsikiliza nini alichomuitia. Walipofika hadi kwenye nyumba husika walimkuta mzee huyo akiwa katulia tu, alionyesha furaha baada ya kumuona kijana susu kwa kumuitikia wito wake ule, walipata nafasi nzuri kwenye mwembe mmoja uliopo karibu na nyumba yake.

'' Kijana nimekuita hapa kuna tatizo ambalo limejitokeza ndani ya muda mchache tangu jana pale ulipotuacha tukizozana na wewe ukatutoa katika mzozo huo unakumbuka?'' kijana huyo alionekana kuwa na wasiwasi na akawa anavuta kumbukumbu, '' Haaa! sawa mzee wangu nimekumbuka si pale jana nikiwa natoka shambani mh sawa nini kimetokea?''

'' swa nashukuru sasa leo hii kaja mwenyekiti mapema sana na kanipa hii karatasi '' Aliitoa na kumpatia aweze kuisoma, ndipo kijana Susu aliikamata vyema huku akiwa na shauku ya kutaka kuisoma barua hiyo, alivyoimaliza alivuta pumzi ndefu kisha akamuangalia vyema mzee huyo na kushindwa kusema chochote

'' Ina maana Mzee susu kaamua kukupeleka katika ngazi ya serikali kwa sababu gani sasa ambayo mmeshindwa kuelewana''

'' Ndio hivyo haswaaa ndio maana nikakuita ili muda wa saa sita tuende na wewe uwe kama shahidi wangu pale nitakapohitajika kutoa ushahidi, yani leo kanivurugia kila kitu leo''.

Alionyesha kuomba msaada mkubwa kwa yule kijana ambae jana yake walivyozozana na mzee mwenzke Sikujua aliwakuta sasa kidogo anaweza kumsaidia kwa matatizo hayo aliyo nayo. Kijana susu alikubali na akaomba kwenda kujiandaa kwa ajlili ya hiyo. Mzee Mambo sasa alimuambia mwanae sikitu kuwa aende akamuite mama yake haraka sana ili amueleze habari hiyo kabla hajaenda huko ofisini, Sikitu alikwenda hatimae baada ya muda mchache alirudi na mama yake. Mzee huyo alimueleza kila kitu na hatimae muda uliwadia alitoka na kumpitia kijana susu na wote wakaelekea ofisi ya mtendaji wa kijiji. Njiani walifundishana jinsi gani ya kuepukana na kesi hiyo inayomkabili,susu alikaa nje na Mzee Mambo sasa aliingia ndani na kumkuta mwenyekiti,mtendaji pamoja na bwana sikujua. mwenyekiti alionyesha kumkaribisha kwa bashasha sana mzee huyo na kumueleza kuwa aketi kwenye kiti kilicho karibu yake na waanze maongezi yao.

''Bwana Mambo sasa kwanza tunashukuru na kukupongeza kwa kuhitikia wito wetu hapa kwani ni wachache wenye kutii amri hiyo je? unamfahamu huyu mzee aliyokaribu yako'' mwenyekiti aliuliza swali huku akimnyooshea kidole sikujua, '' Ndio namfahamu vyema kabisa''

'' Sawa unakumbuka miaka sita iliyopita muliuziana mashamba ya mikorosho lakini haukuweza kummalizia fedha zake je? unakumbuka'' Mzee mambo sasa alistaajabu sana kwani akili yake haikuwa katika swala la jana kule shambani, alivuta pumzi ndefu na ndipo akakohoa kidogo '' Kumbe ndio hiyo kesi niliyoitiwa, ninachokumbuka tuliandikishiana kuwa kila mwaka nampatia kiasi cha fedha kadhaa na nilishamlipa imebaki ya mwaka huu tu sasa sjajua tatizo ni nini'' mambo sasa alijiamini sana kwa kuongea na kuwafanya waulizaji wawe kimya muda wote.

'' lakini hatukukubaliana hivyo ulisema kuwa mwaka jana ndipo unamalizia na kitendo na maneno yako ambayo jana uliyaongea ndio yamenifanya nije kushitaki hapa'' Sikujua aliongeam kwa jazba sana hiuku akipayuka kwa sauti kali.

''Ngojeni kwanza musianze kulumbana hapa mupo kwenye sheria ebu sema taratibu je ni maneno gani ambayo aliweza kuyaongea hapo jana?'' mwenyekiti aliuliza.

'' bwana huyu alisema kuwa hatoweza kunilipa kabisa na pia akanitusi kwa matusi ya nguoni ambayo kiukweli alinidhalilisha na shahidi ninae atakuwa njiani anakuja anaitwa susu''

Aliongea bwana Sikujua kuwa susu ndie shahidi yake lakini bwana mambo sasa alionekana kushituka iweje awe susu wakati susu ndie shahidi yake ambae kaja nae. Walimuita susu ambae alielezwa kuwa yupo hapo nje kwa ajili ya kutolea ushahidi, ajabu iliyoje susu aliongea kwa kujiamini sana pia akamtetea bwana sikujua na kumfanya mambo sasa kuduwaa, aliulizwa sikujua nini ambacho anataka afanyiwe ili kupata fidia ya ile kesi yake baada ya kuonekana yeye ndie mwenye haki

'' nashukuru sana mimi nahitaji huyu bwana lile shamba la mikorosho aniachie mpaka aje kulipa kiasi ambacho tulikubaliana''

Mzee mambo sasa alijiinamia chini huku akitokwa na machozi kwa ile ambacho anakisikia masikioni mwake. Hivyo baada ya miezi kadhaa bwana mambo sasa alikuwa hana hili wala lile kwani hakuwa na hata fedha ya kujikimu kwani alikuwa anategemea sana lile shamba lake la mikorosho ambalo kwa sasa kazurumiwa, Ndipo akafikiria jambo kuwa sasa kutokana na maisha yale hata sikitu ataachan hata kusoma kutokana na mahitaji muhimu kukosekana....

Mzee mambo sasa aliamua kuchukua uamuzi mgumu sana ambao hata familia yake ilimshangaa sana...





.Mzee Mambo sasa aliamua kuchukua uamuzi mgumu sana ambao hata familia yake ilimshangaa, kikubwa alichoamua ni kutaka kumuendea kijana susu ambae alimfanya aweze kushindwa katika kesi ile kumbe susu alikuwa tayari keshapangwa na bwana Sikujua. Alimuita kwanza mkewe ndipo akamuambia kuwa anahitaji kumuendea susu ili akamuonyeshe adabu kwani hawezi kumyumbisha kiuchumi namna ile, mkewe hakupenda kabisa kumruhusu mumewe kwenda huko kwani kuna uwezekano wa kufikia hatua mbali ya kuumizana. '' Mume wangu nakuomba sana haitosaidia wewe kwenda kwa huyo kijana kwani utasababisha matatizo na kupata kesi kubwa zaidi'' Mume wa Mambo sasa, alimuomba sana bwana huyo lakini kwa mzee huyo hakuonekana kama muelewa hivyo alinyanyuka na kuingia ndani, alichukua panga na kuiweka kwenye kiuno chake ambacho uliweza kushikiwa na suruali yake ambayo haikuwa na mkanda kama kuishikia, alitoka nje na kuongoza njia ya kwenda kwa susu kama alivyohitaji. Sikitu alianza kulia kwa huzuni sana kwa kumuona baba yake akielekea huko kusababisha matatizo

'' Baba tafadhali usiende baba yangu sasa ukisababisha matatizo na ukafungwa mimi atanisomesha nani babaaaaa naomba usiende baba yangu hukoo'' Alikuwa analia kwa uchungu huku akigalagala chini mama yake alimuinua na kumuingiza ndani huku wakijawa na huzuni kubwa.

''baba sikitu tatizo ni nini jamani mume wangu mpaka unataka kufanya hayo, mimi sijapendezwa kabisaa aaaah eeeh mungu weee tuone sisi na hizi shida zetu mnusulu mume wangu huko aendako''

Mzee Mambo sasa alidhamiria kabisa kwenda kuufanya unyama ambao aliuhitaji, lakini maneno ya mama sikitu kama yalifanya kazi kumuomba mungu amuangalie bwana huyo huko aendako, ndipo mzee huyo alisimama kidogo akisuasua alite,mbea mbele karibu na shamba moja hivi humo njiani na kuwakuta watu wengi wakilima kama vibarua hivi, alijiuliza sana kichwani mwake kwa lile ambalo anakwenda kulifanya kwa bwana susu.

'' Mh! hivi nikienda kumpiga na panga huyu kijana alafu nikifanikiwa kuua au kumjeruhi nitaishia jela alafu mwanangu atashindwa kusoma pamoja na mkle wangu wataishi maisha magumu sana, lakini haya maisha mpaka lini sina thamani tena mimi hapa kijijini...ngoja nifanye jambo kwanza''

Aliamua kuwasogelea wale watu ambao walikuwa wanalima pale akamfikia mama mmoja na kumshtua kwanza ili apate kumuuliza jambo. '' Heee mama MENGI, habari ya asubuhi ndugu?''

Mama huyo aligeuka nyuma na kuonana uso kwa uso na mambo sasa '' Mambo sasa haya karibu vipi umekuja kutualika shambani kwako kulima au'' Swali alilouliza lilikuwa gumu sana kujibiwa kwani aliona kama anamkejeli kabisa '' hapana nimekuja kuuliza nani ambae anakatisha vipande hapa vya kulima na analipa kiasi gani?''

''ina maana unataka kuja kulima na wewe? ''

''Naomba unijibu mama mengi swali langu''

'' Si yule mzee MAPATO pale mbelee, kipande kimoja anakatisha shilingi elfu mbili tu'' Baada ya kumuelekeza kuwa ni mzee mapato alinyanyua miguu na kumfuata haraka sana alimueleza shida yake kisha mzee mapato akamsogeza pembeni na kuanza kuongea nae vizuri.

'' Hapana bwana wewe ni mzee mwenzangu pia sio vizuri hawa vijana wakikuona unainamisha mgongo cha kufanya leo hii nitakupa shilingi elfu sita ambayo itakusaidia kwa miezi hii'' Mambo sasa hakuamini kabisa baada ya kuambiwa kuwa anasaidiwa tu japo hakupenda lakini kutokana na shida ilimbidi kupokea ili akafanye matumizi yake nyumbani. Mzee Mambo sasa aliondoka na kiasi cha shilingi elfu sita, kipindi hiko ilikuwa fedha nyingi sana pia ukizingatia ni maisha ya kijijini.

Alifika nyumbani mama sikitu na sikitu hawakuamini kabisa kama karudi mzima bwana huyo kwani hofu yao kubwa atarudi na alama yeyote itakayoashiria kuwa kafanya mauaji kama aliyodhamilia. Aliwakuta pia wakiwa na majonzi, aliwaita na kuwaeleza kuwa alifikilia sana hivyo aliamua kuachana nalo,lakini kwa bahati nzuri pale kwenye shamba la bwana mapato niliwakuta watu wakilima na mimi nikaenda kuomba kulima lakini alinikatalia ila akanipatia kiasi hiki hapa kwa kunisaidia pia kaniambia kesho nitaenda kwake kuongea nae zaidi kuhusu kutafuta kazi zaidi ambayo itaweza kunisaidia katika mabo yangu.

Walishukuru sana kwa hilo, baada ya yeye kuachana na lile swala lake la kutaka kufanya mambo ya ajabu. Majira ya jioni moja ya kijiwe cha kahawa ndani ya hiko kijiji cha bwawani kwani pia wanajishughulisha na ulimaji wa kahawa kama mahitaji ya kawaida na si biashara kama maeneo mngine ilivyozoeleka kama mikoa hiyo ya kagera, eneo hilo alionekana mzee Mapato na bwana sikujua wakipiga domo pale wawili tu huku wakishushia na kahawa yao halisi,

'' Eeh! bwana sikujua nikuchekeshe, kuhusu ile kesi uliyonihadithia wiki ziliozopita kuhusu bwana Mambo sasa''

Mapato aliongea, '' Ehee kuna nini tena ''

'' leo hii si unafahamu kama nalimisha lile shamba langu la mikorosho ili niwahi kupulizia salfa mapema!''

'' Ndio nafahamu vizuri kabisa''

'' Sasa baada ya muda Mambo sasa leo akafika pale mala akaanza kunililia mala nina shida sana naomba vipimo nilime maana hali yangu sasa haieleweki kule nyumbani......''

Bwana sikujua akawa hana mbavu kwa kucheka sana huku akishikilia mdomo wake pamoja na kuiweka kabisa kahawa yake chini. '' haaa haa haa haa haa eeeeh ukamuambiaje sasa''

'' Mimi kumuonyeshea jeuli nikampa elfu sita ya vipimo vitatu, alafu nikamuambia kuwa jioni aje nimsaidie zaidi yani sasa hana jauli kabisa sasa hivi na mpaka tutamkomesha anajifanya mzee wa mambo sasa na kujifanya tajiri wa kijiji tena ulivyomnyang`anya lile shamba nilifurahi sana''

Aliongea bwana Mapato huku akitikisa kichwa kuonyesha msisitizo mkubwa sana kwa jambo ambalo alikuwa analiongea. Mzee sikujua nae hakuwa mbali aliweza kuongezea maneno ya kumkashifu na kumfanyia vitimbi mzee mwenzao huyo bwana Mambo sasa, '' yani hata mimi nataka nihakikishe yule mtoto wake namtia mimba kutokana na shida zao alafu nione sasa wanachotaka kujivunia mana kwa yule binti, mzee mambo sasa atakubali kuiba,kutapeli, kufanya kazi ngumu ili mradi sikitu aingie shuleni''

Waliachana pale ndipo mzee sikujua akatoka na kuelekea nyumbani kwake lakini njiani aliweza kukutana na sikitu akitoka dukani kununua mboga, kwa akili ya sikujua alijua fika kuwa ile ela aliyofanya matumizi basi imetoka kwa Mapato, alimuita binti huyo na kumuomba asogee karibu yake kwa kuwa alimuona mwenye wasiwasi sana.

'' Sikitu nataka kukuambia kitu kizuri utakubali?'' aliuliza Mzee sikujua '' Mh! kitu gani hiko?''

'' Sawa leo jioni naomba uje kule nyumbani kwangu kuna kazawadi kazuri nimekuandalia sawa'' Aliongea bwana sikujua kwa kumshawishi sikitu lakini sikitu alionekana mwenye kupinga

'' Sasa unavyokataa utafanya ukose masomo yako na wewe unapenda sana kusoma ukikubali tu mimi namrudishia baba yako mashamba yale ya korosho na sasa yamezaa vyema atayatumia kupata fedha nyingi za kukusomesha wewe, lakini iwe siri yetu wawili wewe njoo alafu utaona nitakachokufanyia kwa baba yako''

kauli yake ya kumrudishia mashamba baba yake aliipenda kwani alifahamu kuwa atakuwa kamsaidia sana baba yake bila kujua dhamira ya bwana huyo kumuambia aende kwake majira ya jioni hayo. Sikitu alikubali ndipo akaelekea nyumbani kwake na bwana sikujua akelekea kwake pia akiamini kuwa atafanikisha njama zake. Majira ya jioni Mzee mambo sasa alimuambia mkewe wafuatane kwenda kwa Mapato huku wakimsii mtoto wao asitoke pale nyumbani ili asubirie kuku wamalizikie kuingia na yeye abaki pale baadae wamkute.

Waliongozana mke na mume kuelekea kwa Mapato wakati huo nyuma wakimuacha Sikitu na yeye akiacha kazi aliyoambiwa na kwenda kwa bwana sikujua kwa kuamini atawahi kurudi mapema na kufanya kazi hizo alizoambiwa. Sikitu anafika kwa mzee sikujua na kupokelewa kwa bashasha sana lakini wakati anamuingiza ndani mwake Mama Mengi aliweza kuwaona alishtuka sana baada ya kumuona binti Sikitu akiingia ndani ya nyumba ya Sikujua, Ilichukua muda sana sikitu kuwa humo ndani wakati huo Mama na Baba yake tayari wanarejea nyumbani wakiamini kuwa watamkuta mtoto wao, walishangaa sana kuona kuku wakizagaa nje ya nyumba hiyo na hapakuwa na mtu yeyote ambae yupo karibu, waliimuita sana Sikitu bila mafanikio ndipo walianza kuchanganyikiwa sana pale.

Nyumbani kwa Sikujua mzee huyo alionekana kukurupuka ndani mwake na kutoka kwa haraka sana huku akifunga vizuri suruali yake akikimbilia njia ya kwenda kwa bwana Mapato................





....Nyumbani kwa Sikujua, mzee huyo alionekana kukurupuka ndani mwake na kutoka kwa haraka sana huku akifunga vizuri suruali yake akikimbilia njia ya kwenda kwa bwana Mapato. alikimbia sana kwa nguvu zake zote, ilikuwa jiono sana kiasi giza likawa linaingia alipofika alifikia chini kwa kuanguka hadi kwenye mlango wa Mapato. Mapato akiwa ndani alisikia kelele za kuanguka ndipo akatoka kwa nje, alimkuta Sikujua akiwa hoi paale chini pia akitweta kwa hofu,

''Heeeh! vipi tena bwana mkubwa mbona hali hiyo kipi kilichotokea huko?''

Mzee Mapato alimuuliza rafiki yake aliyeonekana kuwa kwenye hali ya mshangazo kwake. Bwana Sikujua alikuwa bado kabisa kuongea kwani alikuwa anatapatapa kuongea, hivyo mapato hakuweza kumuelewa vizuri baada ya muda ndipo akamshika mkono na kuanza kumueleza jambo ambalo alitaka kumuambia

''Bwana mapato naomba unisaidie kuna tatizo nyumbani limenikuta naomba twende ukanisaidie ''

Mapato alimshangaa sana kwani ni jambo la ghafla sana lakini haikuwa shida sana kwani walinyanyuka na kwenda haraka haraka kwenda kwa bwana Sikujua, wakati wapo njiani wanakutana na Mzee Mambo sasa akiwa na hofu kubwa usoni mwake uso ukiwa na jazba alipowakuta wawili hao hasa bwana Sikujua hakumtaka hata kumuongelesha kabisa alimuita bwana Mapato pembeni ili amueleze tatizo lake

''Bwana Mapato, samahani kuna tatizo nyumbani'' mzee sikujua aliongea kumuambia mapato huku akionekana kuwa na mshangao sana

''Mh! nini tena bwana Mambo sasa''

'' wakati nakuja kwako nyumbani kwangu tulimuacha yule binti yangu Sikitu sasa nimerudi sijamkuta alafu kuku wakiwa wamezagaa mlango umefungwa na si kawaida yake kabisa hivyo unavyoniona hapa nimechanganyikiwa kabisa ndugu yangu hapa naelekea kwa mwenyekiti'' Mzee mapato alishika mdomowake akishangaa sana kwa yale ambayo aliambiwa

''Sawa ngoja niende kwa huyu ndugu kwani hata yeye kuna tatizo alilokuja kuniambia pale kwake limetokea nikitoka huko nitahakikisha nakuja kwako ila ngoja usiharakie kwenda kwa mwenyekiti kwanza kabla ya kumtafuta''

Mzee Mambo sasa alimuacha pale na yeye akaelekea njia nyingine ili kumtafuta mwanae, Mzee sikujua alimuuliza kuwa kakueleza nini huyu mzee, '' Aaah! usijali eti kapotelewa na mwanae yule sikitu ndio kaja kuniomba mimi ushauri afanyaje''

Alionekana kuduwaa sana sikujua na kuanza kupooza hata mwili wake, mapato alimuuliza vipi yuko vile lakini alisimama huku akiwa mnyonge sana huku akielekea nyumbani kwake, walipofika nyumbani Mzee Sikujua akamueleza Mapato '' Kaka haya nendan humo ndani utakachokikuta hapo kitandani kwangu ndio nilichokuitia ndugu yangu mana nimeshindwa hata nifanye nini''

Aliingia ndani akiwa hana wasiwasi wowote baada ya muda alitoka na kumshangaa sana hatimae mzee mapato alimtandika kofi rafiki yake huku akimlaumu sana kwa kile ambacho alikona kule ndani '' Sikujua nini umefanya baba yake anamtafuta kule kumbe wewe umemfanyia kitu cha ajabu ona sasa hatujui kafa au kazimia bwana mbona unakurupuka hivyo hata kama una nia ya kumkomesha baba yake lakini si kumharibu huyu mtoto ona sasa unafanyaje sasa'' Mapato alifoka sana kuhusu swala lile aliloliona kule chumbani kwa sikujua, '' Rafiki yangu samahanindio maana nikaja kwako sasa ili tujue unanisaidiaje, mimi sio mjinga kuja kwako naomba uniambie nini nifanye'' Mapato alifikilia sana ndipo akamuambia rafiki yake jambo kwa kumnong`oneza sikujua walionekana kuingia ndani, baada ya kufika ndani sikujua alifunua shuka ndipo akaonekana sikitu akiwa hajitambui huku miguuni mwake mukivilia damu nyingi pamoja na mapovu mdodmoni, hali hiyo iliwashangaza sana na wakawa wanaduwaa hawajui nini wanakifanya. walichukua tenga pamoja na mkeka mkubwa hivi walimvirigia vizuuri na kumfungia kamba nyingi ya kutosha alafu wakamuweka kwenye tenga hilo, ''Sasa sikujua hapa umeshaua na haitajiki mtu yeyote ajue zaidi yetu na hapa tunaenda kumtupa mbali sana tena usiku mkubwa sawa?''

Walikubaliana kwa pamoja ndipo wakaliandaa vyema na wao wakakaa nje wakijadili kwa kuhusu lile swala lililotokea,

Upande wa bwana Mambo sasa alienda hadi kwa mwenyekiti na kumueleza lile tatizo lililotokea, Kwa upande wa mwenyekiti alimueleza kuwa kesho aende tena ndipo watamtatulia shida yake, taarifa ya kupotea kwa sikitu ilikuwa haijaanza kusambaa kwa haraka sana kwani walianza kumtafuta kimyakimya kabla ya kuwashirikisha wanakijiji wote, alirudi nyumbani akiwa hana furaha kabisa.

Alimkuta mkewe akiwa analia tu hana hata hamu ya kuendelea na shughuli za pale nyumbani hii yote kutokana na uchungu wa mwana. Majira ya saa saba za usiku bwana sikujua na mapato walilala pamoja ndipo wakafungua mlango tayari kwa kwenda kumtupa sikitu, lile tenga walilipakiza kwenye baiskeli huku sikujua akishikilia mbele kunyoosha muelekeo na mapato akiwa anasukuma kwa nyuma, walipita kwenye nyumba moja ndipo wakakutana na mtu akiwa anajisaidia haja mbele ya nyumba yake hawakutambulika kutokana na lile giza lililotanda usiku ule, walifanikiwa kufika porini maeneo ambayo ilionekana kuwa ngumu sana kufikiwa na mtu yeyote kwa haraka, walilitua lile tenga kutoka kwenye tenga na kulitupia humo porini.

Walirejea na Mapato akaenda nyumbani kwake huku akiwaza kwa lile swala ambalo wamelifanya alibaki akishika tamaa akiwa kitandani kwake katulia, Kwa upande wa bwana Sikujua alighaili hata kulala kwenye kitanda chake hivyo akalala chini na akaacha kitanda, hii yote kutokana na uoga wa lile walilolifanya, Asubuhi na mapema sana Sikujua aliamka na kufagia kama kawaida yake ilivyo, alionekana Mama Mengi kupita pale nyumbani kwa sikujua

'' Baba vipi hali, shikamooo''

'' Marhabaa, ''

''Baba naona jana ulikuwa na kabinti mambo yako si mabaya sana''

Mzee sikujua alishtuka sana kwa kushangaa kuwa alijuaje kuhusu ile mada wakati alipokuja yule binti hakuna ambae aliona vipi huyu mama afahamu lile jambo, baada ya hapo alionekana kugoma sana kwa kauli ile ya mama Mengi

'' Wewee mama wewee kuwa na adabu kabisa mbele yangu, uzee huu unione kuniambia maneno hayo khaaa unanitukana ina maana hata baba yako Mzee MANYENYE hanikuti kabisa kuwa na heshima binti''

Mama Mengi alikuwa na mshangao kutokana na yale maneno aliyoambiwa,

'' Sawa baba nilikuwa nakutania tu baba nisamehee sitorudia'' Aliomba msamahaa kwa bwana Sikujua

'' samahani ya nini na sasa kuanzia sasa nisikie uo upuuzi wako kokote wa kunisingizia nitakuonyesha mjinga sana wewe nitokee hapa''

Mama Mengi aliondoka kwa aibu na haya aliyonayo kutoka kwa Sikujua, Alinyoosha mbaliga zake za miguu bila hata kuangalia nyuma,, Upande wa Mambo Sasa akiwa kwa mwenyekiti anaonekana kuandiaka moja ya karatasi aliyokabidhiwa na hapohapo mwenyekiti akamuita kijana mmoja na akawa anampa majukumu

''kijana naomba ukapige kengele ya kijiji ile ya dharura kuna jambo tunahitaji kulifanya. Kengele iligongwa kwa mlio wa dharura na sifa moja wapo ya kijiji cha Bwawani wasikiapo kengele kama hizo basi wao huitikia kwa haraka sana bila kukosa, baada ya muda watu walifika pale wakiwa karibia wote wakihitaji kusikiliza. Wengi wao walidhania kuhusu swala la mazao yao ya pale, kwa kuwa hawakuwa na dodoso yoyote kuhusu kupotea kwa binti Sikitu.

Walionekana wazazi wa sikitu wakihuzunika wakitokea ofisini kwa mwenyekiti na huku mama yake sikitu akiwa analia kwa uchungu sana.

Mwenyekiti alinyamazisha watu na kuanza kuongea ili kuwaeleza nini wameitiwa pale baada ya kengele ya dharura kujitokeza, alionekana mzee sikujua, mzee mapato na Manyeyepamoja na Mama Mengi ndani ya kundi hilo la watu wakimsikiliza mwenyekiti.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

''Kwanza tunaomba radhi sana kwa usumbufu uliojitokeza ila tatizo tulilonalo ni kuwa hawa wazazi mnaowaona wameleta malalamiko yao juu ya kupotelewa kwa mtoto wao anayejulikana kwa jina la Sikitu'' watu walishangaa kwa pamoja kwa kile kilichosikika masikioni mwao,

Zaidi kwa Mama Mengi, aliyeshangaa zaidi, mwenyekiti aliendelea kwa kusema

'' lakini kutokana na maelezo yaliyotolewa tunatuma laeo jeshi la kijiji yani sungusungu, pamoja tunaruhusu wanakijiji kujumuika katika msako huu wa huyo binti popote pale atakapoonekana, lakini tunamhitaji mzee Mapato katika kutolea maelezo ya mambo fulani kuhusiana na hili swala ahsanteni tunaomba ushirikiano wenu. Wanakijiji waliondoka wakiwa hawaamini kwa kile wakisikiacho. Mapato alifika ofisini na kuulizwa baadhi ya maswali na hivyo akaruhusiwa kuondoka ila pale atakapohitajika basi asisite kuja.

Mzee sikujua hali haikuwa vizuri kabisa kwani alichosikia pale kilimtia shaka juu ya maisha yake, aliona dunia ndogo sana kwa wakati ule. Maneno ya hapa na pale yalianza kusikika kila mahali na wengine wakilaani vitendo vile vya ajabu ambavyo vilianza mapema ile ndani ya kijiji chao. Kila kona sasa walinzi wa usiku sungusungu walianza kutanda kwa kasi kubwa sana na baadhi ya wanakijiji wakishirikiana kumtafuta binti Sikitu aliyepotea. Mzee Mapato alimendea sikujua na kumpasha habari ile ambayo aliitiwa kule. ''Sasa sikujua mambo si unayaona kuwa yamepamba moto kiasi kwamba hali inakuwa tete kwa sasa, andaa fedha za kutosha tumalize kesi hii kwani keshokutwa nitaitwa pale na ndipo nitakapokwenda kumaliza kabisa.''

Mzee sikujua hakuwa na shida zaidi ya kuhitaji lile swala asije kujulikana ''Lakini. kuna mama Mengi huyu mtoto wa Mzee Manyenye jana wakati naingia nae aliniona sasa sijui nafanyaje hapo'' Mapato aliwaza kidogo kisha akasema

''Usijali usiku wa leo namfanyia dawa yake hawezi kutuumbua rafiki yangu ''

waliagana pale lakini wakiwa na ahadi na wao kuungana na watu wanaomtafuta sikitu ili kuficha aibu yao.......





...Mzee Mapato alimtoa wasiwasi rafiki yake Sikujua kuwa atalifuatilia kwa umakini sana na pia atajitahidi kumtia mkononi huyo mwanamke ambae aliweza kumuona sikujua wakati akimuingiza ndani Sikitu, pia waliagana kuwa wajitahidi sana kujiingiza kwenye msako huo ambao unaendelea hapo kijijini wa kumtafuta Sikitu ili na wao wasijulikane kuwa ndio wahusika wa hilo tukio lao walilolifanya. Nyumbani kwa Mambo sasa hali haikuwa nzuri kabisa kwani furaha ilipotea kwa mara moja baada ya kuondokewa na mtoto wao kipenzi, baba sikitu hakuchoka aliamua kwenda shambani labda atakuwa kakamatwa na mnyama alipita njiani huku akiwa anaita jina la sikitu kama ataweza kuitika au kuona hata dalili ya kuonekana kwake, kwa bahati mbaya haikuweza kuwa bahati yake kwa siku hiyo hivyo alirudi akiwa na kilio cha uanaume. ''Mwanangu nini kimekupata mama uko wapi baba yako na mama yako tuna hangaika kukutafuta, ebuu njoo mbele yangu niweze kukuona hata kwa mara ya mwisho''. Aliongea peke yake Mzee mambo sasa akiwa anarejea nyumbani. Alipofika nyumbani kwake anakutana na bwana Mapato na yeye akiwa anahuzunika machozi yakimtoka kwa unafiki, mambo sasa alimkaribisha kwa kumshika mkono na akitikisa kichwa kumaanisha ndio hayo yaliyomkuta, ''Bwana rafiki pole sana pia nimekuja kutoa kiasi cha fedha kuonyesha pole yangu naomba upokee wewe ni mwanaume jikaze hayo ni mapito ambayo unaweza kuvumilia na yakapita kabisa'' Alipokea kisha akawa anamfuta machozi na yeye akageuka nyuma na kuondoka.Haukupita muda mwingi walikuja vijana kadhaa pale kwake akiwemo na bwana Sikujua aliweza kuwepo pale kwenye msako ambao ulikuwa unaendelea kufanyika vijana hao walionekana kuchoka sana hivyo walikuja kutoa taarifa juu ya msako wao. '' Baba dah tumezunguka karibia kijiji kizima lakini hakuna dalili zozote ambazo zinaonyesha kuwa yupo mwanao'' mzee huyo alipewa taarifa lakini alionekana kutoamini kabisa ''Ina maana mwanangu atakuwa kapotea kweli jamani eeeh! aah Sikitu nini kimekukuta mwanagu '' Walimtuliza asiendelee kulia pale, walimuaga ili waelekee kwa mwenyekiti wakampe taarifa juu ya kazi waliyotumwa. Baada ya wiki kupita tayari yalishafanyika mazishi ya kimyakimya huko aliko kuonyesha kuwa kama kafariki pamoja na matanga kabisa na familia ilionyesha kuridhika na ile hali ambayo imewatokea na kuona kawaida kabisa japo machungu hayapingiki kutoka mapema. Mzee Mambo sasa alitoa madaftari ya mwanae pamoja na sare za shule akaweka pamoja kisha akamuita mkewe mna kumueleza jambo kuwa ''Mke wangu tumeshaondokewa na mwenetu sasa hizi daftari zake pamoja na hizi sare nahitaji kwenda kumpa mtoto wa Mama Mengi mjukuu wa Manyenye ili akatumie mana hatuna jinsi sasa'' Mama Sikitu hakuwa na kipiingamizi kabisa hivyo aliondoka navyo na kuelekea kwa mzee Manyenye. Alikaribishwa kwa bashasha sana, alipokaa ndipo akatoa ule mzigo na kuuweka chini ''Bwana manyenye hivi huyu mjukuu waako yupo,alafu kwanza habari za kushinda mana wee acha tu hatujielewi hapa'' Alikurupuka bwana Mambo sasa kutokana na ile hali ya kufiwa na mwanae. ''Usijali kabisa bwana wee hapa wazima naaa huyuuuu Mengiii mh katoka na mama yake hapa muda mchache tu kabla hujafika wewe yani mmepishana'' Alionekana bwana mambo sasa akifungua ule mzigo '' Bwanaaa hapa kuna mzigo huu utampatia Mengi alizoacha mwenzake mana hata tukisema tuzichome moto inakuwa uharibifu kabisa ambao sio mzurii'' Manyenye aliupokea kwa mikono miwili huku akishukuru sana ''Mhhh nashukuru sana rafiki yangu mana hapa utakuwa umeturahisishia kwani mimi pia nafuata ile sera yako bwana lazima tusomeshe ili waje kusaidia hapo baadae'' walionekana kupongezana huku wakifurahishana. ''Sasa bwana mambo sasa kesho uje hapa asubuhi sana mana nataka kwenda kuondoa mahindi yangu kule shambani na wewe upate chochote bwana sawa'' Wakati huo akianza kumsindikiza ''Haya usijali ngoja niende kuandaa tenga langu kule kwa ajili ya hapo kesho ahsante sana'' waliachana na kila mmoja akaelekea kwake.

Njiani anaonekana SUSU akielekea njiani kutoka pale kwake huku akiwa anaongea yeye mwenyewe bila mtu mwingine kuongea nae ''Mh lakini nafahamu kwa kile nilichokifanya miezi kadhaa iliyopita wala sio kizuri ona sasa mwanae kafariki na mimi sijui atanionaje, lakini haina shida ngoja kwanza niende kwa bwana huyu Sikujua akanipe tenga langu nikamsaidie Manyenye kesho mana tenga la muda mwingi'' kumbe alikuwa anaenda kwa sikujua kuchukua tenga lake ambalo aliliazima kwa muda sasa, alipofika alimkuta akiwa nje kajiinamia kana kwamba ana mawazo mazito yanayomkumba, ''Sikujua mzee wangu vipi mbona hivyo?'' alimuuliza ''Hapana mjukuu wangu nimetulia tu hapa'' susu alikaa pembeni yake ''Haya babu nimekuja kuchukua tenga langu kesho kuna kazi ya kumsaidia Manyenye kurudisha mahindi shambani'' Mzee sikujua alionekana kushtuka sana baada ya kuambiwa hivyo wakati huo anakumbuka kuwa lile tenga ndilo ambalo alimuwekea sikitu na kwenda kumtupa porini. ''Susu ngoja niende kukuchukulia jingine mana unakuwa na tenga lililochakaa kama nini jamani'' aliingia ndani na kuchukua tenga jingine ambalo jipya pia ni dogo alirudi nalo na kumpatia ''Khaa wee mzee vipi tenga langu lile ndilo nalihitaji sio hili naomba tenga languu hili rudisha'' Alianza kuwa na jazba bwana sikujua ''Wee kijana vipi nakupa tenga jipya hulitaki umezoea shida wewe '' Susu hakutaka kuelewa kabisa ''Yani nakuambia kuwa nimekufanyia kazi yako kipindi kile umemdhurumu Mambo sasa hukunipa hela yangu leo unataka kunidhurumu mali yangu hapa sikubali mpaka unipe tenga langu''. Hiyo ndio hali halisi ambayo bwana sikujua ilimkumba na kushindwa amueleze vipi kijana huyo '' Sawa ngoja kuna vitu nimevihifadhi cha kufanya njoo asubuhi utalikuta liko tupo'' aliondoka susu pale kwa sikujua huku akiacha mikwara ya aina yake 'Mh! hapa itakuwaje au niende kuangalia kule porini na nikalitoe lile tenga na asubuhi akija alikute mana kachachamaa huyu kijana asije akafumbua yaliyofichwa'. alijiuliza sana ndipo akafunga mlango na akaelekea kwa bwana Mapato.......





Baada ya kuweza kufunga mlango aliongoza njia ya kwenda kwa rafiki yake bwana Mapato, hatimae alifika kwake na kuwakuta wakiwa wanakula bwana Mapato pamoja na familia yake, aliishia kusimama tu pale al;ipo akiwa hafahamu nini ambacho anaweza kukifanya, alikuja rafiki yake huyo baada ya kumuona kuwa haeleweki.

''Vipi mbona umeishia kusimama tu hapo na huji kukaa'' aliuliza bwana Mapato

'' yani hapa hata hapakaliki kabisa yani nimechanganyikiwa kabisa hapa unaponiona,'' aliongea bwana sikujua akiwa anataka kukaa chini, kabla hajafika chini aliweza kuinuliwa na mapato na kumsimamisha tena

''Aaah haifai bwana mbona unachoka hivyo ndugu yangu ebu eleza bwana kipi kinakusibu''

Sikujua alivuta pumzi ndefu akimuangalia kwa umakini sana rafiki yake huku na yeye akimtumbulia jicho kwa kusubiri aambiwe kitu na sikujua

''Bwana wewe ni rafiki yangu sina haja ya kukuficha, kama unakumbuka ile kesi ya mimi na bwana Mambo sasa?''

sikujua aliuliza swali

'' Ndio naifahamu haswaa, ila ngoja tusogee huku hpa mke wangu asije akasikia si unawajua hawa wakipataga habari matumbo yao yanajaa upepo hivyo bila kuutoa hawaoni sawa''

walisogea pembeni kando na pale nyumbani kwake bwana Mapato ndipo mapato akakumbushia mada ile ambayo iliwafanya wasogee pembeni.

''Haya niambie sasa hiyo kesi naikumbuka sana''

'' Sawa ile kesi mimi nilimdhurumu bwana Mambo sasa, yani nilimtumia kijana mmoja aitwae Susu anayekaa kwa yule mpiga ngoma maarufu bwana MANUALI, unamjua'' Alimuuliza Mapato huku akionyesha kwa mkono mahali amabapo anaishi huyo Manuali na susu

''Hao tena bwana mbona nawapata si yule mzee mtata mtata kwa dawa zake anazozitumia kutibu watu na mambo mengine hata kukamata wachawi hivi'' alimkumbushia Sikujua ili kumhakikishia kuwa anamfahamu vyema

'' Haswaaaa sasa yule kijana nilimuahidi kumpa kiasi fulani baada ya kushinda kesi pia nilimuazimaga Tenga ambalo tumelitumia kumtupa yule binti sasa kaja analihitaji tenga lake lakini nilimpa jipya akakataaa katakata, ndipo nikamuambia aje asubuhi atalikuta''

Mapato alionekana kuwa makini sana kusikiliza akavua kofia yake ambayo aliiva akanyanyua mkono wake akachagua kidole cha kati kukuna kichwa chake kilichojaa mvi za kutosha, hii yote ilikuwa kuonyesha jinsi gani mambo yalivyokuwa magumu kwa pande zote.

''Sasa, hilo tenga mpaka alitake hilo lake na akakataa jipya kwa nini pia alazimishe hivyo?""

''Mhhh wee huna taarifa kuwa kesho asubuhi kuna kazi ya kuondoa mahindi kwenye shamba la bwana Mnyenye ''

''Aaaa kweli hata mimi hapa alikuja asubuhi kunipa hizo taarifa sasa wewe umeamuaje?''

aliuliza mapato kuhusu uamuzi wa sikujua juu ya hilo swala.

''Mh! mimi nimeona ni bora turudi kulekule ili tukalichukue lile tenga''

Walikubaliana vyema kuhusu swala la yeye na bwana Mapato kwenda polini kuchukua tenga la kijana Susu ili lisije kuzua tafrani.

Majira hayo upande wa bwana Mambo sasa majira kama saa tano hivi za usiku yeye akiwa kalala na mke wake, pia usingizi ukiwa umewakolea vilivyo, ilisikika sauti ya binti wa kike ikiita ''Babaaa, babaaa, Mamaa,Mamaaa, mbona mnaniachaa nateketea bado sijafa mamaaa''

Bwana Mambo sasa aliamka ghafla na kuangaza huku na kule kijasho kikimtoka, alimgusagusa mkewe ambae alikuwa bado usingizini, "Mke wangu amka haraka amka kwanza usikie" Mama huyo aliamka akiwa na lundo tele la usingizi alifuta baadhi ya ukungu ambao ulimfanya kutokuwa sawa kwa kuona ''Nini mume wangu''

''Mke wangu nimesikia sauti ya mwenetu Sikitu akituita''

Mama sikitu alikuwa kama mtu ambae kama katoneshwa kidonda hivi '' Mume wangu acha hizo kauli naumia moyoni, itakuwa ni ndoto hizo zinakusumbua sikitu anakaribia mwezi tangu apotee leo uniambie kakuita alafu usiku huu kweli''

Baba sikitu alimtuliza kidogo mkewe kisha pakawa kimya kabisa ndipo kauli ya mkewe kuwa ilikuwa ni ndoto likasimama kidete ndipo wakalala tena.

Safari ya kwenda polini ilikuwa imetawala tayali katika akilini mwao, walisubili mpaka ilipofika majira ya saa sita mwezi umetanda vyema ndipo wakaanza mwendo taratibu sana na baiskeli yao. Wakiwa njiani wanamalizia nyumba za kijiji cha bwawani moja ya nyumba ilisikika ikifunguliwa mlango japo hakujulikana ni nani. walitembea kwa haraka sana kumuepuka huyo mtu ambae anatokeza kwa nje, walitembea kwa muda fulani ndipo wakafika eneo la tukio.

Upande wa huku watokako nyumba jirani na Bwana Sikujua ilionekana kuungua moto hivyo kelele zilianza kusikika

''Jamani weeeeeee nyumbaaaaaa motoooooooo njoni mtusaidieeee''

Zilisikika sauti hizo zikiomba msaada kwa majirani kweli walijitokeza kwa wingi sana huku wakisaidia kumwaga maji juu ya paa ya nyumba hiyo kwani iliezekwa kwa nyasi isipokuwa ya bwana Sikujua ilikuwa ni ya bati'

Upande wa Mapato na Sikujua walishtuka bada ya kusikia kelele hizo pamoja na moto ulioambatana na moshi ukitanda kwenye kiza kizito kilicho shindwa kufichwa na mwezi ulioanza kufifia kutokana na dalili za wingu kutanda angani,

''Mapato angalia kule tunakotoka ule si moto na nadhani nyumba itakuwa inaungua pale''

''Haswaa itakuwa hivyo sasa pia hizoooo kelele za watu zikishamili sasa je hawatotushangaa sisi wakati tunarudi''

''Hapa itabidi tufanye haraka hivi lile tenga ile siku tulilitupia wapi?''

walianza kulitafuta bila kuwa na mafanikio lakini walibahatika kukuta mkeka na kamba ambazo walizitumia kumfungia baada ya kugundua kuwa wameua,

''Jamani hivi hii si ndio ile kamba ambayo tulitumia ile siku, kuna kamba tupu hapa na tenga hakuna jamani''

walihangaika vya kutosha sana bila kufanikiwa kuliona tenga walilolikusudia,Kila mmoja kwa upande wake alichoka sana kiasi kwamba walitamani ardhi ipasuke wasionekane au wawe na uwezo ambao ungewawezesha kuliona tenga la kijana Susu.

''Bwana sikujua hapa cha kufanya turudi alafu tupitie pale nyumbani uchukuie kiasi cha fedha ambacho kitasaidia kumpa huyo kijana na hilo tenga lako jipya najua hawezi kukataa mbele ya fedha''

waliamua kurudi majira hayo ya usiku sana ndipo wanakutana na baadhi ya watu wakitokea kwenye tukio. Waliona hatari itawajia ndipo wakapitia bwawani kabla ya kwenda huko kwao katikati ya kijij walibahatika kupata chombo cha kubebea wakateka maji na kuanza kukimbiza baiskeli yao huku na wao wakikimbia walifanikiwa kukuta watu bado wakihitaji maji bado hivyo iliwapa kunusurika na kutambulika wao wanatoka wapi,

Ndipo alionekana mama Mengi akimfuata mzee sikujua na kumuuliza

''Wee mzee wewe wakati watu wanahangaika kuzima moto huu nyumba yako ilikuwa imefungwa mpaka sasa hivi ulikuwa wapi?''

Swali hilo lilikuwa gumu lenye kuchoma moyo ulioficha mengi ya siri kubwa sana; Alishindwa kujibu zaidi aliondoka pale lakini bado aliendelea kumfuata huku akisimamia msimamo wake wa kutaka kujua yeye aliyekaribu kashindwa vipi kutoa msaada hata wa kuondoa vitu mpaka matatizo yanamkuta mwenye hiyo nyumba kwa kushindwa kuokoa hata kitu kimoja.

''Naomba uniambie sikujua unafahamu kuwa wewe una tabia mbaya sana siku hizi wewe mzee wewe''

Aliona sasa dharau zinazidi

'' Weeee mwanamke wewe kuwa na adabu hapa tupo kwenye matatizo unafahamu baada ya kuona hii dalili mimi nilikwenda kuwaita watu waje kusaidia unajua kuwa huyu mzee mapato taarifa ya hapa kapewa nani au unatukosea adabu tuu''

Mama Mengi hakuwa na neno aliona kama kaumbuka lakini kichwani mwake alionekana kumtilia shaka sana Mzee Sikujua.

Asubuhi na Mapema sana watu walijiimia kumpa pole aliyekutwa na matatizo ya kuunguliwa na moto nyumba yake pia walijiandaa akiwemo Mambo sasa na mke wake. waliongozana shambani kwa bwana manyenye. Kazi ilianza kuondoa mahindi na kuweka sehemu moja ili baadae waweze kubeba kupeleka kwa Manyenye. Mzee Mambo sasa alionekana akiwa na bwana Manuali karibu huku kila mmoja akishika mstari wake wa kuondoa mahindi alisimama kidogo bwana Mambo sasa huku akijiuliza

''Mh! ile ndoto au itakuwa kweli ila ngoja nimueleze bwana Manuali labda anaweza kunipa mwangaza kidogo''

Alimsogelea pale alipo bwana manuali ambae ni mzee kidogo wa makamo alimsalimia kisha wakaanza mazungumzo

''Bwana manuali nipo hapa nina shida moja kubwa inayonisibu mpaka sasa'' Aliongea Mambo sasa

''Wewe tena usijali ongea nakusikiliza ''

''Bwana tangu nifiwe na mwanangu au kupotelewa na mwanangu siku nyingi zimepita hapa"

Mzee Manuali alionekana kuacha ile kazi kidogo na kumgeukia Mambo sasa na kumsikiliza vyema

"Haswaa nafahamu ndugu yangu"

"Sasa jana usiku kuamkia leo hii nilipo hapa nilisikia sauti ya Sikitu mwanangu ikiniita mimi pamoja na mama yake ikisema ""Babaaa,Babaaa Mamaa,Mamaaa mbona mnaniacha mimi sijafa babaaa"" alafu ilikuwa inamalizia kwa kilio kidogo sasa sijaelewa mpaka sasa hivi bwana Manuali"

Mzee manuali alishika kidevu chake akitafakari nini aseme kuhusiana na hilo swala alilonalo kwa rafiki yake.

"Sawa nimetambua nini nitakusaidia cha kufanya njoo jionijioni hivi leo tufanye dawa fulani na maelezo kuhusu ilo pia njoo na mke wako" Mambo sasa alishukuru sana

Wakati huo anaonekana Mapato kwa mbali akiwashuhudia wanachokiongea alionekana kutikisa kichwa huku akikunja uso ndipo akatokomea ndani ya shamba ilo kujichanganya na watu wengine .........



...Bwana Mapato alijichanganya kwenye kundi la watu huku akiwa anaangalia nyuma kana kwamba kuna mtu ambae anamtafuta au kumkimbiza, alitwikia tenga lake huku akihitaji kuondoka lakini kabla hata ajafanikiwa kuondoka ndipo kijana susu aliweza kumfikia pale alipo huku akijishika kiuno alichopoka mara moja na kwenda kumshikia lile tenga lake lililojaa mahindi alishusha chini wakati bwana mapato anahitaji kupandisha juu ya kichwa chake, alimshangaa sana ndipo akashusha chini.

'' haya kilichokutuma uje unitue mzigo huu ni nini?''

Aliuliza bwana Mapato kumuuliza kijana huyo ambae alikuja pale kwa ajili ya kumtua mzigo wake badala ya kumsaidia kupandisha kichwani mwa bwana mapato.

''Bwaana mzee sio kwamba nimekukosea heshima hapana ila shida yangu kujua kuwa bwana sikujua yuko wapi?"

Aliuliza swali ambalo lilimfanya Mapato kuangua kicheko pale alipo, alipomaliza kucheka akamuuliza swali

''Sasa kijana habari za sikujua unaniuliza mimi hapa je kwake hukwenda?''

''Mimi sitaki kujua habari za kwenda kwake au kutokwenda nilikwenda asubuhi lakini sikumkuta na wakati tuliagana kuwa asubuhi ya l;eo nitalipata tenga langu''

Alionekana kuongea kwa jazba sana kijana susu huku akitumbua macho yake yaliyokuwa makubwa kama ya paka

''sasa mimi unaniuliza nalala nae?''

''Wee si ndio rafiki yake bwana sasa mwambie nikimaliza kazi hii nakuja kwake asiponipa tenga langu sitojali yeye ni nani atanitambua''

aliondoka pale alipokuwa na bwana Mapato akimuacha anafuta jasho kwa uchovu alioupata, alimuangalia sana kijana huyo mwishowe akafyonya tu na asijue amfanye nini kwa wakati ule.

''yani huyu kijana ngoja cha moto atakiona yani kanichefua sana sasa habari za sikujua na mimi wapi na wapi, tena alafu huyu sikujua ipo siku nitamchoka mana naona naingia kesi ambayo hainiusu kabisa ''

Majira ya mchana kila mmoja alikusanyika nyumbani kwa mzee Manyenye, baada ya kumaliza kazi ya kukusanya mahindi ambayo yalikuwa shambani kwake. Kwa upande wa akina mama walikuwa wakimaliza kazi ya upishi ili kuwaandalia wale wote ambao walishiriki vyema sana katika swala la kuondoa mahindi hayo shambani kwake.

Upande wa akina mama alionekana Mama Mengi ambae waliambatana na mama wengin e pamoja na mabinti kadhaa walikuwa na mazungumzo ya hapa na pale.

''Jamani wanawake wenzangu sasa hivi tuwe makini sana mana swala la kupotea watotot wetu sio zuri tena hata ikibidi tuwe nao karibu sana''

Kauli hiyo iliwafanya hata wengine waweze kuacha shughuli zao na kumgeukia mama Mengi ambae alionekana kutopendezwa na matukio ambayo yanajitokeza.

''Mh! ni kweli kabisa ila kuhusu huyu Sikitu jamani inatia hata huruma yani kupotea wakati yeye alikuwa ni mtoto mtiifu kwa wazazi wake jamani''

Mada hiyo iliwaumiza wengi sana lakini hata mama mengi alionekana kuwa na mawazo sana, ndipo mama mwengine ambae alikuwa kama rafiki yake alimshitukia na akataka kumuuliza

''Mama Mengi, mbona kama unataka kulia kuna jambo gani''

''hapana bwana dada wee ebu andaeni vyombo huko tuwapelekee watu wananjaa sana''

Chakula kilikuwa tayari na ndipo sahani zilipelekwa kwa wanaume. Wakiwa wanakula kijana susu aliangaza macho yake akafanikiwa kumuona mzee sikujua akiwa moja ya kundi la watu ambao walikuwa wanakula, alikula harakaharaka ili aweze kumuwahi.

Ilitoka sauti moja ambayo iliwashtua sana sauti hiyo ilitoka kwa Mzee Mambo sasa ikisema

"Jamani mnakula mkiwa na furaha sana lakini mimi chakula hakipandi hapa"

Alisema bwana Mambo sasa

''Sasa kwa nini tena iwe hivyo na wakati tupo hapa pamoja kuna nini kimekufanya useme hivyo au chakula hakijapikwa vizuri"

Sauti hiyo iliwafanya watu watulie sana na kusikiliza maongezi ambayo yalikuwa yanatawala kwa muda huo

"Jamani mtoto wangu sikitu jamani yani wanakijij wote tumeshindwa hata kumuona kweli jamani aaah mwanangu sikitu huko uliko bado nakupenda ssna mwanangu ona ninavyohangaika hapa sina furaha kabisa"http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Baadhi ya watu walinyanyuka na kwenda kumpa matumaini na pole kuhusu swala zito kama hilo, fahamu kuwa ni bora kufiwa kwa kuwa unajua hutomuona tena lakini si kupotelewa ambako huna uhakika kama yupo hai au kafariki ndicho kilichomtokea bwana Mambo sasa.

''''Jamani tena naombea akijulikana kama kuna mtu kijijini hapa ndio kafanya hivyio haki ya mtungi shahidi kata awe mtu au mnyama akijulikana mimi najitolea namchinja na mimi ""

Kumbe lile swala liliwauma wengi sana kiasi kwamba walichangia kwa kuhitikia kuwa sawa kabisa. Walimtuliza hatimae chakula kiliisha na watu wakatawanyika lakini Mzee manyenye akamkabidhi mahindi ya kutosha kama alivyomuahidi hapo mwanzo kabla.

Majira ya jioni hivi bwana Mapato na sikujua walikutana na wakawa wanaelekea shamba la bwana Mapato ambalo alikuwa analimisha kwa vipimo shilingi elfu mbili.

''Bwana sikujua wewe ni kama kaka yangu kwani tunatokea ukoo mmoja tu, sasa nina jambo ambalo nahitaji kukushirikisha kwa sasa ili uone unaweza kufanya nini"

Sikujua alikuwa anatikisa kichwa kuashiria kuwa yuko tayari kwa lolote.

''Sasa nikiwa kule shambani nilimsikia kwa masikio yangu Baba sikitu na bwana Manuali wakiongea jambo"

Alionekana kushituka sana baada ya kusikia hivyo

"Nini tena walichokuwa wakiongea"

Sikujua alikuwa na wasiwasi mpaka akawa anasimama

"Kha! unasimama nini sasa twende nikuhadithie"

Alimuangalia huku akimuimiza waendelee na mwendo

" Leo hii bwana Mambo sasa wanakutana majira ya jioni lakini japo sijajua wanakutana kwa lengo gana zaidi, lakini kama unaenda kwa manuali hakuna jingine zaidi ya tiba" Hapo alinyong`onyea sana sikujua kiasi akabaki kusimama akifikilia

""Sasa hawatakwenda kwa ajili ya lile swala lakini, alafu mimi sikufanya kusudi ujue,""

"'weee mjinga hukuwaona wazee wenzako au hata akina mama kama yule Mama Mengi ukaishi nae, yani tangu mkeo kafariki umekuwa na tabu pamoja na tamaa za kishetani kabisa sasa hata kama atakwenda kwa ajili ya hilo swala wewe utafanya nini?'"

Sikujua aliduwaa halijua ajibu nini pale

"Ukiacha hilo yule kijana akaja kunipiga mkwala tena na mimi"

"Kijana yupi?"

"si huyo anayekudai tenga lako"

Walisimama kwa muda kidogo huku wakipitiapitia shamba hilo, Sikujua alionekana kupata wazo muhimu sana ndipo akataka kumshirikisha m wenzake, lakini alikuwa na hisia mbaya na bwana Mapato.

"Sasa bwana Sikujua mimi nataka kukusaidia jambo fulani......"

Kabla hajamaliza aliweza kukatishwa na sikujua ambae aliomba kumueleza jambo fulani,

''Au.....mimi ninawaza kuondoka ndani ya kijiji hiki kabla hata hayajafika mbali mana nahisi haja zote kunitoka kila siku zinapokuja" Alicheka sana bwana mapato baada ya kusikia kuwa sikujua anataka kuhama pale kijijini kukimbia ile kesi inayoanza kufufuka taratibu. ""Wewe aliyekuambia kuwa kukimbia kesi ndio kumaliza kesi nani, jikaze ujue unalimaliza vipi, kwanza tukakague kule mpaka tuhakikishe kuwa hatuoni hata alama moja ya kuonyesha kuwa sikitu yupo au laa''

Sikujua alionekana kukubali lakini kwa nafsi yake ilionekana kuwa na kipingamizi kikubwa sana juu ya maamuzi ya kubaki pale. Waliondoka pale na kurudi kijijini wakiwa wako makini sana, hadi sasa maisha ambayo aalikuwa anaishi bwana sikujua ni ya wasiwasi sana. walipanga kufika kwanza kwa bwana Manuali ili kwenda kumuelza kuhusu huyo mjukuu wake ambae anawatia jambajamba kila siku zinapokwenda, walifika pale wakiwa na wasiwasi wa kumkuta bwana Mambo sasa lakini haikuwa hivyo. Waliodikia na kukaribishwa ndani, hawkautaka kuingia ndani hivyo walimuita nje kwa mzungumzo zaidi.

"Haya karibuni sana mana nilikuwa ndani humo nina mgeni ila haina shida tuendelee nawasikiliza sasa"

Waliposikia kuna mgeni walishtuka sana japo hawakujua rasmi kuwa ni nani, walijua kuwa ni bwana Mambo sasa kwa hali yeyote ile walimuomba bwana Manuali wasogee pembeni.

"Manuali, hapa tunashida moja,"

Walimueleza manuali aliyeonekana kushangazwa na ujio wao huo, "Mh! haya nawasikiliza":

"Mmmmh tunashida kwamba mjukuu wako susu alinipaga tenga lake, sasa lile tenga limeliwa na mchwa na yeye alivyokuja kulihitaji nilishindwa kumuambia kuwa li,meharibika kwani alikuwa na hasiira sana, "

"kwa hiyo mlitakaje labda"

Aliuliza bwana Manuali

" Ehee ninachokihitaji tumpatie tenga jipya pamoja na fedha kidogo ili tumalizane na hiyo kesi yake".

alivuta pumzi bwana manuali baada ya wao kumaliza mazungumzo yao. "Jamani kuhusu huyu susu mimi mtakuwa mnanishirikisha kwa makosa tu kwani mambo yake anayafanya yeye kama yeye ndio maana akajenga nyumba yake ile kwa hiyo mkimuhitaji yeye mumuendee pale"

waliishiwa nguvu kabisa kwani matarajio yao ni kuwa mzee huo angeweza kuwasaidia kwa namna moja ama nyingine.

"Sasa utanisaidiaje ndugu yangu" aliuliza sikujua

"Labda tufanye kesho mapema sana nitamsimamisha shughuli zake ili niweze kuongea nae kwanza na nyinyi mkifika kesho tutayamaliza".

Walimaliza ndipo wakaondoka zao, kwa kuwa ilikuwa jioni sana ambapo usiku ulikuwa unaingia zaidi, Mzee manuali aliingia ndani, kumbe mule ndani kulikuwa na bwana Mambo sasa akiwa ana mazungumzo na Manuali. "bwana samahani nilikuwa naongea na sikujua hapo nje haya tuendelee na mazungumzo yetu"

Manuali alianza kwa kumueleza kuhusu lile tatizo lake alilo nalo. " Ehee hapo kinachotakiwa kesho mapema kama saa za mchana hivi nakuja kwako kufanya dawa fulani ambazo zitamfukuza kama atakuwa mzimu au ni ndoto za ajabu basi zitaondoka kabisa, lakini hii dawa utaondoka nayo utaiweka chini ya kitanda chako yani ulalie kichwani na hii nyingine utampatia mkeo najua haitojitokeza tena"

Aimkabidhi zile dawa kisha akamruhusu aende nyumbani kwa kuwa ni usiku sana. Majira ya usiku kama saa sita hivi, nyumbani kwa sikujua , mzee huyo hakuweza kulala kabisa kwani alihisi kuna vitu vinamuangaisha sana, ndoto za ajabu ambazo alishtuka sana, mwishowe aka amka kabisa kwa kukosa usingizi.

"Mh! Mbona kwenye ndoto namuona Sikitu, akiwa ananikalipia kwa vitisho ina maana ni mzimu au bado hajafa, mh lakini hapana hii ndoto inanitia shaka"

Alishindwa kulala kabisa ndipo akakaa kwenye kitanda chake huku akiwa anasikiliza milio ya wadudu tu huko nje.

Ghafla sauti iliyokuwa ikitokea nje ikilalamika huku ikitoa lawama kali sana, Sikujua alishtuka, ndipo akaishikilia shuka yake vyema kutaka kujifunika gubigubi,

""Aaah...Aaah...Mbona ulinidanganya babu, mbona umeamua kunitesa na kunifanya niwe hivi baridi kali, linanipiga nifungulie hata mlango, uliamua kunitendea haya ili niwe hivi...ila ipo siku...."

Sikujua aliweweseka kweli huku kijasho kikimtoka, alifikia hatua hata kuachia haja ndogo pale alipo na usiku ulikuwa mkubwa sana kwake, alianza kulia japo ni mzee lakini sasa yamemkuta na hakuamini kabisa. Aliinuka na kuchukua meza pamoja na kinu ambalo linatumikaga kutwangia nafaka, akaliweka kwenye mlanga huku akitetemeka,

Asubuhi na mapema aliamka na alikuwa wa kwanza kabisa kuamka, alifungua mlango ndipo alikuta damu zikiwa zimetawala pale mlangoni, " Ieeeewiiiie" alipiga yowe kali wakati huo Susu kama kawaida yake alijiimia kwa bwana Sikujua kudai tenga lake kama kawiada, alimkuta akiwa mlangoni akizishangaa zile damu.

"Eeeeh babu jana tulikosana haya niambie liko wapi?"

Hakujibiwa kabisa kwani yeye alikuwa anaangalia ile damu tu. Alimuonyesha kwa mkono tu pale huku akiwa anarudi nyumanyuma,

"Nini unachonionyesha?" Aliuliza susu "Susu hivi huoni hizi damu, hapa mlangoni"

'Damu ziko wapi?" aliendeleaa kuonyeshwa lakini susu alienda hadi pale kwenye mlango na kukanyagakanyaga

"Hapa hakuna damu wapi angalia". Zamani sana bwana sikujua alikuwa keshakimbia kuelekea kwa kwa Mapato huku akipiga yowe

""Damuuuuu, damuuuuuu jamani damuuu". mapato alishangaaa damuuu kivipi damu jamani,.

Alimuona rafiki yake kama mtu aliyechanganyikiwa kabisa, sikujua alimuonyesha kuwa kwake kuna damu na hataki hata kusogelea......







Ukimbiaji ambao alikimbia bwana Sikujua haukuwa wa kawaida kabisa, aliweza kumshangaza hata rafiki yake Mapato kwa ile kasi ambayo alikuwa nayo. Hata alipoulizwa kuhusu ile damu ambayo alikuwa anaitamka hakuweza kusema sentesi nzima akaeleweka, alijisemea mwenyewe mapato kuwa rafiki yake atakuwa kachanganyikiwa na si bure kabisa. Alijitahidi kumtuliza ndipo mkewe bwana mapato akaingia ndani na kuchukua kikombe kilichojaa maji na kutoka nayo ili aje kumpaa sikujua anywe.

yale maji yalisukumwa na mapato huku akifoka kuwa haitajiki kupewa maji sasa hivi unaweza kumuua, subiri apumzike kwanza. Wakati wanaendelea kupumzika ndipo anajitokeza susu na yeye akiwa kakunja sura yake akimaanisha kujawa na hasira sana. "Mh! mtu wako huyo anakuja"

Alijisemea mapato, sikujua huwa anakosa raha sana pindi anapomuona susu. Susu alipofika alisalimia wote na kukaa kwenye benchi karibu na mapato. "Mzee habari za asubuhi kwanza pili huyu bwana sijamuelewa jinsi alivyotoka pale kwake". Alisema susu, "Bwana wee yani hata mimi sijaelewa kabisa kaja hapa anaweuka tu ndio tunamsubili apumzike kidogo"

"Mh! haya bwana ila nilimkuta pale kwake, nilikuwa na lengo la kuchukua tenga langu sasa nikamsikia damuu, damuu nikashangaa sana ndipo nikafika mpaka pale mlangoni sioni chochote ndipo nikamuona kakimbia".

Kufikia hadi hapo susu alikuwa haamini kabisa, ndipo mapato akaingia ndani na akatoka na tenga kubwa na mkononi akiwa kashika kiasi cha fedha mkononi.

"Sasa baba tumalizane hili tenga utalichukua alafu hiki kiasi tunakiongezea hapa juu ili tumalizane kabisa umuache mzee wa watu apumue wewe mwenyewe si unamuona alivyo".

Susu alishika na kile kiasi cha fedha akakitia mfukoni. akamuangalia mapato kisha akaanza kuondoka "Ahsante yani hapa nimekubali basi tu ila kuanzia leo asije kuniazima tena kitu changa, pia akumbuke kesi niliyomsaidia lazima anipe hela yangu baada ya mavuno kufika"

Aliondoka pale na kuwaacha wazee hao wakiendelea na shughuli zao. Baada ya muda kupita ndipo sikujua alikuwa na hali nzuri na akaanza kumsimulia kilichotokea, wakati huo wakiwa wawili tu mke wa mapato alishatoka. "Haya niambie rafiki yangu nini kilichotokea"

"daah yani kwanza usiku nilishtuka baada ya kusikia nikiitwa jina langu na binti nje, nilipoamka ndipo nikamsikia kwa masikio yangu mawili Sikitu binti wa mambo sasa akilalamika kwa kunilalamikia mimi, isitoshe vitisho navyo vilikuwa vingi...nilipoamka asubuhi ajabu sasa ndipo nikaikuta damu mlangoni na wakati huo susu anaingia yeye akasema damu hiyo haioni ukweli nilijikuta nakimbia huku sijielewi".

Mapato alimsikiliza kwa makini sana. "Sawa nimekuelewa hilo linawezekana kwani baada ya kufanya ule unyama na ikiwa kama alikufa kweli yule binti basi, unatakiwa kuoga dawa aina ya makombe yani uandikiwe makombe kisha yatiwe maji alafu uoge kuondoa nuksi na mizimu yake isije kukufuatilia tena"

"Fanya hivyo kabisa mana hapa nimekoma kabisa na sina hata hamu"

Upande wa bwana Mambo sasa na mkewe wakiwa barazani kila mmoja na majonzi yake japo muda sasa tangu wapotelewe na mtoto wao. Mambo sasa aliamua kuvunja ukimya ambao ulikuwa umetawala kwa muda mrefu sana alimuita mkewe na kumueleza habari ambayo baadae ilionekana kuzuwa utata na malumbano baina yao.

"Mke wangu, kuna jambo nataka kukuambia na linahitajika kulifanyia kazi muda huu"

Mkewe alistajabu kwanza

"lipi hilo mume wangu" aliuliza mama sikitu

"Nafahamu muda mwingi sana tangu tutoke nyumbani SHIMOMO, kutokana na lile swala letu mpaka wakatufukuza pale kijijini"

Mama sikitu alitulia kwanza

"Ndio nakumbuka ehee" Alionekana kuwa na uhitaji wa kutaka kipi kitakachoendelea

"Usiwe na jazba mke wangu nia yangu kuwa tangu tupotelewe na mwenetu hawana taarifa kabisa juu ya hili swala pia sioni sababu ya kuendelea kuishi kwenye miji hii ya watu hali hatuna furaha pia hakuna ushirikiano ninachokihitaji sisi turudi kule kijijini"

Mkewe alitikisa kichwa huku akipinga kabisa swala la kurudi SHIMOMO, japo haikujulikana huko shimomo kulitokea nini mpaka wao wafukuzwe na wakakimbilia huku kijiji cha BWAWANI. "Hapana kabisa baba sikitu, kwanza siamini kama mwenetu kafa hapana pili sitaki kurudi kule ambako mimi walinikataa nisiolewe na wewe na wakatufukuza kwa kututishia kabisa kwamba tukiendelea mahusiano yetu watatuua hapanaaa"

Ilimbidi Mambo sasa atumie akili ya ziada kumshawishi mkewe ili akubaliane na yeye kwenye swala hilo na hatimae mama sikitu alikubali.

Mzee Mambo sasa aliondoka muda huohuo na kwenda kwa bwana Manyenye kumpa taarifa ya kuondoka pale yani kuhama kabisa. "Bwana manyenye, nimekuja hapa kukupa taarifa kuwa nina hama kabisa hapa kijijini naelekea shishimo nyumbani kwetu"

Manyenye alisimama kwanza huku akishika kiuno chake kilichchoka kwa ajili ya uzee wake " Eeeeh haya mbona mapya tena unaondoka alafu ndio nini sasa"

"Ndo hivyo tunaenda kuhangaikia maisha sehemu ya kwetu maana hapa hatuna kitegea uchumi sasa nisije kuwa mzigo wa kijiji cha watu" Alisema Mambo sasa,

"kuwa mzigo vipi tena na wewe mimi nimeshakuzoea bwana kama kitegea uchumi nina mikorosho yangu pale miambili na shamba la kule juu kuna mikorosho themanini vijana wangu wavivu na mikorosho inaungua tu moto mwaka hadi mwaka sasa ni bora nikukabidhi ile themanini uifanyie kazi kwa miaka tano najua utakuwa umeshajijenga tena"

Mambo sasa alifikilia sana kabla hata ya kujibu mana asije kukurupuka.

"Ahsante sana nashukuru sana ila nipe siku ya leo na kesho nakuja kukupa jawabu zuri ngoja nikaongee na mama watoto tujue tunafanyaje kuhusu ilo" Bwana Manyenye alimuomba sana asiondoke na kama uchumi isiwe sababu kabisa yeye atamsaidia.

"Bwana fanya hivyo bwana kesho uje unipe jawabu"

Aliondoka pale na kumfuata bwana Mapato lakini kwa bahati nzuri au mbaya alimkuta na sikujua ambae kipindi cha nyuma alimdhurumu mikorosho na yeye, alisalimia wote mana hata mambo ya sikujua alishayasahau yani aliyaacha kama yalivyo. "Bwana mapato nashukuru nimekukuta, lakini kuna jambo ambalo tuliliongea kuhusu uniazime mikorosho yako kadhaa unakumbuka?"

Mapato alikuna kichwa chake kwanza " Aaa hilo nalikumbuka lakini kwa sasa hali ngumu labda tufanye msimu ujao kwanza"

"Sawa ila sikuja kwa nia hiyo lengo kuja kuwaaga siku zijazo ninaondoka hapa kijijini naelkea nyumbani kwetu"

Mapato alishusha pumzi kwanza

"Sawa hilo ni jambo jema kwanza ni bora hata ukapote mawazo ya kufiwa na mwanao sikitu mana hata sisi tunahuzunika sana". Mambo sasa ndipo akagundua kuwa kuna watu hawampendi kabisa na wapo watu ambao wanamkubali aendelee kuishi pale.

Mpaka jioni alivyorudi nyumbani alikuwa na majawabu kamili ambayo yalimpa uhakika wa kufanya maamuzi. Hakutaka kuchelewa alielekea kwa bwana Manyenye na kumpa taarifa kuhusu msimamo wake.

"Nimekubali kuendelea kuishi hapa lakini nitaenda kijijini kwanza kwa siku tatu nikirudi nitakuja kukuambia "

"Haina shida bwana mambo sasa wewe nenda ukirudi utakuta huku nimeshakuandalia mambo yote yako sawa"

Upande wa mwenyekiti anaonekana jamaa mmoja hivi akiwa na shida ya kuonana na mtu mmoja pale kijijini

"Kijana unaitwa nani?" Mwenyekiti aliuliza

"Mimi naitwa, KATUNJE" kijana huyo alijibu kuwa anafahamika kwa jina la katunje.

"Katunje unatokea wapi?" Mwenyekiti aliuliza tena huku akiandika mahali fulani iliyoonekana kama sehemu ya kumbukumbu.

"Mimi natokea MLIMALONDO" alijibu pia kuwa anatokea mlima londo.

"sawa hapa umekuja kwa lengo gani hapa kijiji chetu kizuri cha BWAWANI"

"Baba hapa nimekuja kumtafuta ndugu yangu anaitwa bwana CHITO"

Mwenyekiti alifungua kwenye orodha yake ya wahamiaji wa pale lakini hakupat bahati ya kumpata huyo mtu anayejulikana kwa jina la CHITO aliendelea kufungua lakini hakulipata.

"Kijana hapa hakuna jina la mtu anayejulikana kwa jina hilo na hatuna utaratibu wa kumpokea mgeni bila kumuandikisha, mgeni wa mwisho hapa alikuwa mzee ambae alikuwa na mkewe anaitwaa MZEE MAMBO SASA basi hakuna mwingine.

kijana chito alishusha pumzi akaona hapa hatoweza kupata msaada wa nguvu bila kufanya jambo la kumshawishi mwenyekiti huyo.

"baba samahani huyo mambo sasa hata mimi kweli simfahamu ila naomba nikae siku tatu tu nihangaike hapa kijijini ili nimtafute mwenyewe nikibahatika kumuona nitakuja kukuambia na nisipofanikiwa basi,

Alikataliwa kabisa kupewa nafasi ile ya yeye kuishi pale kwa siku tatu. Hivyo aliombwa aondoke pale ukweli alifukuzwa kabisa kama mwizi, mfukuzaji mmoja wapo alikuwa susu ambae alipewa kazi hiyo. kijana Katunje aliondoka na kukimbilia sehemu ambayo hakuifahamu lakini hakutaka kwenda mbali na hapo kijijini, alifika porini sehemu iliyokaribiana na msitu, alihisi kwa mbali kama kuna maji yanatembea hivyo aliona vyema kuyafuata na kwenda kujimwagia kidogo tena hata kunywa,

wakati anatembea alibahatika kuliona tenga ambalo lilikuwa na damu pembezoni aliliacha lakini alivyozidi kutembea alizikuta nguo za mtoto wa kike zikiwa nazo zimegandia damu ya muda mrefu. Aliachana nazo huku akiwa na wasiwasi sana alitembea kwa utaratibu wenye umakini wa hali ya juu kuhofia majanga ambayo anaweza kuyaona, alisita kidogo akaona vyema arudi nyuma akachukua tenga na zile nguo, aliendelea mbele kuyafuata yale maji alipofika akaona bwawa kubwa sana lenye maji mazuri ya kuvutia pia haikuonyesha dalili ya watu kufika pale, aliliweka chini lile tenga alitaka kuanza kunawa lakini alipopiga jicho pembeni kwa usalama alimuona binadamu aliyekondeana sana akiwa kalala kwenye moja ya poli pembezoni mwa bwawa, alisimama akaenda taratibu, alimuomba mungu kwanza amsaidie isije kumdhuru kwa lile alifanyalo.

Alipomfikia alihisi tu kama moyo unafanya kazi lakini mwili haufanyi kazi haoni, mbavu zinaonekana kakondeana zaidi ya maelezo, alifanya harakaharaka kuchukua tenga lake aliloliokota na kuchukua zile nguo na kuvisha lakini zilikuwa kama zinamfunika tu, alimuweka kwenye tenga na kulitwikia kichwani, alianza kunyoosha njia ya kwenda kijijini akiwa njiani alisikia sauti ya mwnamke ikisema " Tafadhali usinipeleke huko"

Alihisi kama ni mawazo tu aliyokuwa nayo lakini alijiuliza yale mambo aliyofanyiwa na mwenyekiti inawezekana huyu binti kafanyiwa jambo,

Aliamua kurudi na kutokomea nae msituni safari ya kwenda kwao MLIMALONDO. Alitembea umbali mrefu kiasi alianza kuchoka mpaka kiasi cha chakula alichonacho alimlazimisha kumlisha yule kiumbe ambae hata umbile alilipoteza la usoni, alikula lakini si kama kawaida hapo ndipo akaona kuwa ni mzima hivyo lazima amsaidie. Hatimae wanafika kijiji cha MLIMALONDO bila watu kufahamu kabisa. Aliingia nae ndani kwake na kumhifadhi vyema, alifunga mlango wake na kwenda kwa mzee mmoja maarufu kwa miti shamba hapo MLIMALONDO, aliyejulikana kwa jina la KAUZIBE "Babu nina mgonjwa wangu kule nyumbani naomba ukamsaidie"

"wewe katunje ulisema unaenda bwawni kumtafuta nduguyo chito sasa ndio huyo uliyekuja nae na sasa ni mgonjwa au" aliuliza mzee KAUZIBE

"hapana twende huyo anakaribia hata kufa sasa hivi baada ya hayo nitakuhadithia kipi kilitokea kwenye safari yangu"

Waliambatana kwa pamoja kwenda kwa Katunje ili kwenda kumtibia binti ambae hakufahamika ila kwa huruma ya katunje ndio ilimfanya kuchukua majukumu hayo.





ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog