Search This Blog

JOTO LA MSHUMAA - 4

 






Simulizi : Joto La Mshumaa 
Sehemu Ya Nne (4)






Ndani ya kijiji cha MPOLONI ambako kijana KATUNJE alifika baada ya mwendo mrefu kutoka kule ambako aliwaacha wale wenzake na kutokomea na kuacha neno la kusema kuwa yeye kuwa kafariki na lile jitu kule msituni, alifika akiwa na furushi la majani na magome ya miti ambayo ilipatikana kule lakini mkono ungine akiwa kashikilia mche wa ule mti.

Haikujulikana aliubeba kwa lengo la kwenda kuupanda au laa! Mzee Ukelele alizidi kumsubilia lakini Katunje alikuwa na hali mbaya sana alikuwa hajielewi kutokana na kuzidiwa na hali aliyonayo lakini jambo ambalo lilimsaidia sana ni kule kufika ndani ya kijiji cha Mpoloni. Akiwa ndani ya kijiji hiko ndipo baadhi ya watu ambao walishawahi kumuona katika moja ya nyumba ambayo alikuwa anapita walianza kumsemasema "banahivi yule si ndio alikujaga siku moja kuja kumuulizia bwana Ukelele?"

Huyo ambae alikuwa anaulizwa wote walikuwa wenye umri wa makamo. "Ndio ndio yeye haswa, sasa unakumbuka tulimlisha nyama yule sasa hawezi kutupotea kabisa sasa ngoja nianze kumfuatilia nyumanyuma". Kumbe walikuwa ni wale watu ambao katunje kwa mara ya kwanza kuja katika kijiji hiki cha Mpoloni aliweza kukutana na hii familia ambayo aliweza kuwaomba kama msaada wa kuelekezwa kwa Mzee Ukelele lakini alichofanyiwa alipewa chakula chenye nyama ya mtu.

Yani ni umafia na unyama uliokithiri ambao hauelezeki kabisa. Basi Katunje alizidi kuyumbayumba kama mtu ambae alikuwa kanywa pombe kali. "ngoja kwanza usiende hivihivi yule pale alipo hajielewi si unamuona sasa kachukue usinga humo ndani kwenye nyungo ile alafu uje nayo hapa haraka", Bibi huyo alimtuma mwenzake ambae hakufanya ajizi kabisa alienda na kurudi na ule usinga.

"Sasa hapa nenda na huu ukimkaribia tu basi mpige nao kichwani hizi nywele baada ya hapo atakuwa akili zake tumemchanganya na hatoweza kabisa kuona mbele". Yule mtu aliyafanya hayo na kuanza kumfuatilia bwana Katunje, wakati anaendelea kwenda Katunje mkono wake ambao ulifungwa na ile dawa ulianza kumuuma sana ndipo akasimama "Mh! mkono mbona unavuta sana hapa kuna hatari inabidi niwe makini sana'

Sasa alianza kwenda huku akiangalia nyuma, hatimae alipata nguvu na kukimbia na akaondokana na majanga ambayo aliandaliwa na wale watu waliokuwa wakimuandama hali ya kuwa hawamfahamu kabisa. Katunje aliendelea kuyoyoma na njia ile hadi alipokaribia kwenye nyumba ya Mzee Ukelele, alishindwa hata kuodikia zaidi alianguka palepale na kupoteza fahamu.

Wakati huo mzee Ukelele yeye kwa upande wake alikuwa maeneo ya shambani akipalilia mahindi yake ambayo yalikuwa yanaonyesha hali nzuri huko bustanini kwake. Hakuwa anafahamu lolote kuhusiana na ujio wa bwana Katunje. Kumbe yule bibi ambae alikuwa anamfuatilia alifika hadi kwenye nyumba ya mzee Ukelele lakini aliweza kuishia mbali na pale kutokana na ulinzi mkubwa sana uliopo pale.

Alibaki kufyonya tuu kisha akageuza njia na kurudi alikotokea, Kwenye nyumba hiyo alitokea binti mmoja ambae anajulikana kwa jina la MWAIJA alitoka nje baada ya kusikia kishindo cha mtu kudondoka, "Mamaaa huyu kadondoka jamani alafu babu hayupo hapa..." Aliamua kukimbia sana kuelekea kule aliko babu yake ili kwenda kumpa taarifa alimkuta mzee Ukelele akiwa anamalizia na akijiandaa kurudi nyumbani kwake.

"Babuuu kuna mgonjwa kaanguka pale nyumbani" "Mgonjwaaa haya twende haraka tukamuone". Walitembea kwa mwendo wa haraka sana hadi walipofika kwenye ile baraza walimkuta Katunje " Aaaah kumbe huyu kijana " Alisema mzee Ukelele

"Babuu unamjua kwani?'' Mwaija aliuliza " Ndio yule niliyekuambia kuwa atakupeleka kwa mama huyu ndiko anakotokea anaitwa Katunje, sasa tumpeleke ndani kwanza kwa ajili ya matibabu". Walisaidizana kumpeleka ndani kisha wakamlaza matibabu yaliendelea kuwa mazuri mpaka jioni akawa amepata nafuu kidogo. Mzee huyo aliyatumia yale majani pamoja na mizizi kwa kuisugua na kupata dawa ambayo alimlisha kijana Katunje. "Muda mchache tu katunje anatapika nyama na kitu kimoja aina ya Irizi ambayo alilishwa. "Unaona hii ndio ambayo ingekuua maisha yako mjukuu wangu, lakini kama ulivyosema walikufuata ni kweli kwani kupitia hiki kairizi walikuwa wanakuona popote pale ulipo hivyo ingekuwa rahisi kwao kukukamata.

Siku ya pili yake matibabu yalimalizika na yeye akawa vyekma kabisa ndipo akaanza kumueleza kuhusiana na kumjua mtu ambae siku hiyo alikuwa anamfuatilia Lyoto.

"Sasa naomba unisikilize, dawa hii siku ukifika tu isugue kwenye jiwe kisha kula nyingine jipake mwilini mzima wakati unakaribia kulala baada ya hapo utalala na usiku utamshuhudia nani ambae alikuwa anamfuatilia mtu wako na ilikuwaje, Pia baada ya hapo utamuendea na kumhoji akikataa dawa hii nyingine utaenda pale sehemu ya mwisho ambayo utaiona kwenye ndoto ambapo waliishia na huyo mtu akageuza nenda kaifukie hii kwenye moja ya Mguu wake wa unyayo"

Katunje alikubali na akalipokea kwa mikono miwili kabisa.

"Alafu itabidi leo hii muondoke na huyu binti utaenda kumuacha kwa huyo mama aliyekuagiza ni mtoto wake." Baada ya muda kupita safari ilianza huku wakiwa wametengenezwa vyema kwa kutosumbuliwa na mtu yeyote yule kama mwanzo alivyokakaribishwa na wenyeji wa MPOLONI,

Majira ya usiku wanafika kijiji cha KILIMALONDO kwa lengo la kutimiza ile ahadi ambayo alidhamilia kuweza kuifanya kuwa lazima LYOTO apatikane kwa hali yoyote ile kama yuko hai. Ndipo Katunje alipomueleza binti huyo wa makamo kama Katunje kuwa "Mwaija tumefika tayari lakini sasa ni usiku sana itabidi tukapumzike kwenye nyumba yangu alafu asubuhi nakupeleka kwa mama yako".

"swa haina shida twende" waliongozana na wakati huo sasa mvua ikaanza kunyesha na ukizingatia majumba ya kijiji cha KILIMALONDO, yapo mbalimbali hivyo upepo wa kibaridi unaingia ndani ya miili yao bila kizuizi kabisa. walifanikiwa kufika hadi kwenye kibanda cha Katunje akafungua kisha wakaingia ndani.

Nyuma iliezekwa kwa nyasi kiasi mahali ambako palikuwa salama ni kitandani palikuwa hapalowi, lakini sehemu nyingine nyingi mlikuwa mnalowa maji yalikuwa yanapenya vyema tu, hivyo iliwabidi aibu wazitoe kabisa wakalala kitanda hikohiko, ndipo radi zilianza kuamsha hisia za wawili hao bila kujijua baridi nalo likaendelea kuchombeza na kuwafanya wajione kama waliohalalishwa kushikana na kukamatana, walishasahau kama ni watu wawili ambao hawakuwa na mahusiano kabla.

Sauti za kimahaba ziliendelea na bwana Katunje kwa miaka kadhaa hakuwahi kuona ndani hivyo siku hiyo Mbuzi alifia kwa muuza supu, Walimaliza na Mwaija akajikuta anajishangaa sana kwa kufanya lile tendo kwa kijana Katunje, 'Kwa nini nisimtamkie kuwa nampenda kisha iwe rahisi mimi kuwa nae ili anisaidie baadhi ya kazi hapa nyumbani' yalikuwa ni mawazo ambayo alikuwa nayo kijana Katunje.

Asubuhi na mapema kila mmoja anamuonea aibu mwenzake lakini wakajikuta kila mmoja anamuonyeshea hisia za kwa nini tusikubaliane kuoana kabisa. " Mwaija samahani ila muda huu twende nikupeleke kwa mama yako ukamuone", Walifuatana wote kwa pamoja hadi kwenye nyumba ya mama Mwaija.

Kwa bahati mbaya kubwa sana wanamkuta mama Mwaija kafariki na ilionyesha ni wa muda mrefu sana tangu afariki, masikitiko yalianza pale hasa binti Mwaija, alilia sana kwa kufiwa na Mama yake. Alishindwa kuamini kwa kile ambacho anakishuhudia. Waliondoka pale na Katunje alienda kutoa taarifa kwa kiongozi bwana SWAI ambae taarifa hiyo ilipokelewa na Kijana KIMOLO ambae kama mlinzi wa mzee huyo aliyejiita mfalme wa Kilimalondo.

Baada ya mazishi kupita ndipo Mwaija alidai kurudi nyumbani kwa babu yake, ' Ngoja nitakupeleka lakini dawa ile ambayo alinipa yule babu sijaifanya nikiiifanya keshokutwa tunaenda sawa".

Katunje alimuonea huruma sana Mtoto Mwaija ambae alionekana kutokuwa na furaha kwa wakati wote, Katunje aliikanda dawa ile kwenye jiwe kama alivyokaelekezwa na mzee Ukelele na kwa kuwa ilikuwa ni majira ya kulala alilamba na nyingine akajipaka, akamuambia na Mwaija nae ajipake tu na ailambe na wote wakafanya hivyo,

'''Mama mwaija mbona unapenda kufuatilia mambo yangu kwa nini?

""Wee mzee Kauzibe na mwenzako Udevu ndio mnahusika kumpoteza Lyoto nyinyi""

"""Mama Mwaija usitake nikufanyie kitu ambacho hutokuja kusahau maishani mwako"". Mzee Kauzibe aliongea kwa kupaniki akimueleza mama Mwaija aliyeonekana kuwa anafuatilia mambo yake, "Hata kama lakini huniwezi na lazima tukatangaze kesho wajue kuwa wewe na akiludi katunje haki ya nani namuambia" Mzee Kauzibe aliondoka hadi kwake akachukua upinde ambao aliupaka sumu ambayo huwa anatumia sana katika mambo yake. alifikilia lakini akaghaili ndipo akafungua kikopo kimoja na akaanza kukiongelesha kile kikopo ndipo moshi wa aina yake ukatoka ukaelekea hadi kwenye nyumba ya mama Mwaija ule moshi ulikuwa kama uchawi ambao ulimuingia Sehemu za uwazi kama Masikio,mdomo, puani na ungine ukatambaa kuingia sehemu za haja zote na hatimae anakufa.

"'Heeeeeiiiiheee heee Mamaaaaa". Katunje alipiga kelele kubwa sana mpaka pale Mwaija alipoamka, Mwaija alishangaa kwa nini Katunje kapiga mikelel kama ile, " Vipi kuna nini?" Aliuliza Mwaija

"Hapana Ndoto tu itabidi tukiamka asubuhi turudi kwenu ili nikuache kule kwanza sawa!"

Kweli kama kawaida walishakuwa kama wapenzi sasa walianza safari ya kurudi nyumbani kwa Mzee Ukelele ili kwenda kumueleza yale aliyoyaona kwenye ndoto.

Walifika salama kabisa na wakapokelewa ndipo wakamhadithia yale yaliyotokea kule mpaka mwisho "Mh! mimi nimewasikia lakini kati yenu nahisi kuna jambo ambalo mmeshalifanya ila haina shida kijana naomba umtunze binti yangu aliyebaki baada ya mama yake kufariki" Aliongea mzee Ukelele "Haina shida babu

"Eheee vipi kuna ndoto yoyote ambayo umeiota baada ya kufanya ile dawa?"

"Ndio lakini nimeota kuwa mzee Kauzibe kamuua mama yake Mwaija kwa uchawi mweusi ulioambatana na Moto, lakini sikuota ile niliyokuja nayo yani kuhusu yule binti".

"Sawa kuhusiana na huyo mzee niachie mimi nitamuonyesha, lakini sasa kama mwaija nae alikual hiyo dawa basi ndoto kuhusiana na Huyo binti aliyepotea ataiota huyu kwa hiyo tumsubiri lini ataota na atuambie nini kaota, kwa hiyo kazi yako ni kumuuliza kila siku kaota nini".

Katunje akaona bado kazi mbichi.

Ndani ya kijiji kimoja kijulikanacho kwa jina la KALULU kuna familia moja ilikuwa na kikao ambacho kilionekana kikao cha maana sana kwani walikuwa makini sana pindi mtu mmoja akiongea, Bwana mmoja alisimama na kusema " Jamani sisi kama wanafamilia wa hapa basi hatuna budi kusema kuwa hili jambo ni la kwetu sasa inatakiwa wote kulitekeleza, mada iliyokuwepo hapa kuwa Mke wangu pamoja na mimi kama mzee UWESU nipo hapa mbele yenu kusema kuwa tunamhitaji mwenetu NYAMALI tangu aende kwenye familia ya mzee MAMBO SASA mpaka sasa kila nikituma taarifa hakuna inayorudi sasa tuna wasiwasi na huko aliko."

Kumbe mada ambayo iliwekwa mezani ilikuwa inamhusu Mama SIKITU ambae kaolewa na bwana CHITO kwenye familia ya mzee Mambo sasa.

walikubaliana kuwa mwenyekiti wa kijiji cha Kalulu itabidi asafiri kabisa na aelekee kwenye kijiji cha SHISHIMO ili kwenda kujua kama mtoto wao Nyamali atakuwa ni mzima au laah! jambo hilo lilipita vyema kabisa na ndipo mwenyekiti huyo alijiandaaa kwa ajili ya kusafiri kwenda kwa bwana MASANJA ambae ni mwenyekiti wa kijiji cha Shishimo ili akajue anaweza kulitatua kwa namna gani ili siku isije kuleta ugomvi baina ya hivi vijiji viwili.

Siku ya pili yake ndipo mzee Mwenyekiti wa Kalulu anaingia ndani ya kijiji cha Shishimo ili kuonana na bwana Masanja.

Walikutana na wakati huo bwana Mapato anaonekana kujiandaa kama kuhitaji kuondoka pale kwa mwenyekiti na kwenda mahali pengine.

"Mzee vipi sule unaondoka leo kwa nini usiondoke kesho?" Masanja alimhoji mapato aliyejulikana kwa jina la SULE. " Yani hapa nashukuru kwani hapa mwanga wa kumpata ndugu yangu unaonekana sasa nataka kwenda kuwataarifu familia kisha nije kwa awamu nyingine." Ndipo bwana Mapato akawa anajiandaa na wakati huohuo mwenyekiti wa kijiji cha Kalulu anaingia.

"Haaaah! rafiki khaaaaa! umepotea sana"

"Si kupotea kazi za kuwatumikia wana kijiji lazima zituweke mbali kabisa"

walikaa mahali kwa kuwa walijua kuna jambo ambalo linahitajika kuzungumzwa kwa wakati huo. "Haya bwana kutoka kalulu nipe habari".

"Habari kubwa ni kuhusiana swala letu la kuhakikisha uongozi wa kifalme tunaufutilia mbali na tunauingiza wa uenyekiti, inatakiwa hii kauli itambae maeneo yote kabla hata hatujaamua kuanza kutembelea kimoja hadi kingine kwa upande wangu tayari kampeni hizo zinaendelea baada ya kujua kuwa ufalme wa kurithishana huwa tunawapata viongozi wasiojitambua na kuwaacha vijana pembeni kama sisi tukikaa tu"

Kwa manen aliyokuwa akiyaongea alionekana kuwa mwenye utimamu mkubwa sana.

"Ni kweli bwana unalolisema "

"Kingine kama unakumbuka mwanakijiji wenu mmoja anayejulikana kwa jina la CHITO mtoto wa mzee MAMBO SASA alikuja kuchumbia kule Kalulu, kwenye familia ya bwana UWESU kwa mtoto wao NYAMALI unakumbuka?"

Msanja alikaa kimya maana mada hii ya pili kwake ni ngumu sana kuingilia ovyo. " Haswaaa nakumbuka vyema sana na hata maandishi yao hapa tunayo."

"Sasa miaka takribani amchukue ingali Nyamali yuko binti mpaka sasa hajawahi kurudi nyumbani japo walikuwa wanaleta taarifa za kumhitaji yeye aje nyumbani kwa kuwa wazee wake hawawezi kutembea lakini hakuna majibu yeyote waliyoyapata, kikubwa wanachotaka kuona kama ni mzima huyo mtoto wao basi."

Mzee Masanja akakaa akawa anakumbuka siku moja alipofika Chito

"""Yani mwenyekiti nakuambia leo ni siku ya nne mke wangu sijamuona, kapotelea wapi sijui lakini namhisi baba yangu kwa kuwa siku ya kwanza niliyaona maji yakielekea chumbani kwake siku ya pili makana na leo yote kwa pamoja asije akawa anamlisha makana...makana...mke wangu....mke wangu...mke wangu".http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

aliwaza na kuwazua hajui nini aseme wakati huo sauti ya Bwana Chito ikirudia rudia kichwani mwake kila mara kwa kule kukumbuka kwake. " Bwana Masanja vipi mbona sikuelewi au kuna chochote ulichogundua?" Aliuliza bwana huyo kutoka Kalulu.

"Ni kweli lazima niwaze sana kwa hili maana linanitia shska sana, kukupa taarifa iliyokamili kutokana sina uhakika wa kile nilichokisikia ila ningependa kupata taarifa kamili ndipo niweze kukueleza kila kitu".walikaa kwa muda kidogo kisha yule mwenyekiti akasema "Sawa basi mimi naomba niitiwe huyo bwana Chito kwani nadhani anaweza kunipa maelezo ambayo yanaweza kunipa nguvu kule niendako kuwapa moyo wale wazazi wake". Kwa upande wa bwana Masanja ilionekana kama kikwazo japo haikujulikana kwa sababu gani.

"Itabidi nikupeleke kwa bwana Mambo sasa ili ukaongee nao kule kwao nadhani itakuwa njema zaidi". Waliinuka wakati huo tayari bwana Mapato alikuwa anayasikia hayo yote ambayo walikuwa wakiyaongea huku akiwa anajiandaa kwa safari ya kurudi ndani ya kijiji cha BWAWANI. Safari ya kuelekea kwa bwana Mambo sasa haikuwa na mafanikio ya uharaka kama walivyoifikilia kwani hawakufanikiwa kumkuta mtu,

Wakiwa wanaondoka ndipo bwana Mambo sasa anaonekana kuja kwa haraka kwenye nyumba yake, baada ya kufika pale aliingia chumbani kwake kisha akaingia uvunguni na kutoa furushi lake. alitoa usinga pamoja na irizi nyingi sana za kutosha ambazo hazikujulikana zinatumika kwenye mambo gani zaidi. alimuendea Mama Sikitu na kumkokota hadi kwenye nyungo akaanza kuimba huku na kule kisha ghafla wapotea, safari yao ilifika kule sehemu ambayo aliambiwa kuwa anahitajika kumpeleka yule mtu ambae kamkamata.

Baada ya kumfikisha alisifiwa na kiongozi yule na kuahidiwa pindi akimleta mjukuu wake hakika atapandishwa cheo kikubwa sana. "Haaah haaah haaah! hapa umenifurahisha sana kwa jambo hili, sasa ujionee nini tunakifanya kwa huyu mwanamke".

Walimvua nguo zote na akabaki uchi wa unyama, kama alivyozaliwa, walianza kumdhihaki kwa maneno ya ajabuajabu sana wakati huo akiwa kafungwa kamba. Mzee Mambo sasa alikuwa hapo akiwaza jambo moja ambalo alikuwa analikumbuka kichwani mwake """Babaa...unafikili hii kazi uliyonayo itakufaidisha kitu gani unaua ndugu yako wa karibu nani atakuzika au kukusaidia pindi ukiwa na shida....mama umemuua unadhani hapa kijijini nani anakupenda kutoka moyoni baada ya kufanya haya mambo....au unadhani mwisho wa wewe kuua unapata nini baba mke wangu yuko wapiiii?".

Maneno aliyokuwa akiyakumbuka kipindi anaambiwa na mtoto wake, aliona kuwa kweli kile akifanyacho siyo kizuli kabisa na sasa itabidi afanye jambo lakini kachelewa na pale yupo kwa wakubwa wake yani mizimu ya NYAMNYENA iko pale hana sauti mbele yao. Waliendelea kumtesa ndipo mkuu huyo akachukua kisu na kumfuata alimshika mdomo kisha akaushika ulimi na kuukata kabisa, damu nyingi zilimtoka na alishindwa kulia kwani alifanywa kama zezeta hivi asiyejitambua, Mzee Mambo sasa aliona huruma kutokana na ule ukatili ambao alikuwa anafanyiwa mkwewe yani mke wa mtoto wake.

Hawakuishia hapo walimtoa macho yote huku akiwa mzima kabisa sijui maumivu ambayo aliyapata yalikuwa ni ya aina gani jamani, baada ya aliitwa mzee Mambo sasa akapewa kisu na kuambiwa sasa amchinje hapo shingoni, alianza kuogopa kabisa """KIJANA UOGA WAKO UNANIFANYA NIBADILI MAAMUZI YA KUKUPA NGUVU NA UWEZO MKUBWA KAMA Nyandu UKATILI WAKO HAPO NDIPO NAUHITAJI UUFANYE HARAKA SANA""" Aliongea huyo kiongozi kumuimiza bwana Mambo sasa afanye harakja kwa jambo lile aliloambiwa.

Vijana walimfungua mama Sikitu aliyeonekana kuzimia na wakamlaza, mzee huyo kwa mkono wake mwenyewe anategesha kisu chake kwenye shingo la mke wa mtoto wake wa kumzaa mwenyewe, huku akiwa anatetemeka wanamuimbia wimbo wa ushujaa kumpa nguvu ya kutenda lile jambo akapitisha kisu kwa nguvu akarudisha kwa nguvu akafanya hivyo mara kadhaa hakika damu nyingi sana ziliruka pale na zingine zikamfikia mwilini mwake kwenye nguo..Alikuwa na wasiwasi kwa lile ambalo alikuwa analifanya.

Ikatoka kauli nyingine ya kuse,ma sasa amtoe sehemu za siri za Mama Sikitu kwa haraka bila kuogopa na bila kuchelewa na bila kukosea, Mzee huyo alikuwa kama ndondocha ambae alikuwa anafuata kile alichokuwa akiambiwa, wakati sasa Mama Sikitu tayari keshakuwa Maiti mzee alitoa nyeti zake pamoja na vitu alivyoambiwa kuvitoa. baada ya hapo akapewa nyama iliyotokana na Mwanadamu huyo na kuambiwa.

"HII ITABIDI UONDOKE NAYO NA UMPATIE MWANAO AILE AKISHAKULA HATOWEZA KUKUSUMBUA TENA, KWANI NA YEYE ATAKUWA MUHUSIKA WA HILI WEWE UMEUA YEYE KALA"". Baada tya hapo aliondoka baada ya kujihakikishia yuko vizuri katika mwili hakuna damu yeyote bila kujua kuwa nyuma ya mgongo wake kuna damu nyingi sana ambazo hakuziona. alifika nyumbani anamkuta mtoto wake akimsubiri " Chito mwanangu vipi mbona umehuzunika yani bado unanituhumu kuwa nimemchukua mkeo".

Wakati anamkaribia harufu ya mwanamke ikamjia maana alikuwa akishika nyeti za Mama Huyo kwa fujo ili aweze kuzikata vyema 'huyu baba katoka kwa mwanamke alafu hajaoga huyu uzee wote huu anakuwa malaya hivi duu' Alimshuku baba yake katoka kwa mwanamke kutokana na ile harufu iliyokuja.

"Baba unatokea wapi sasa hivi?" Chito aliuliza

"Natokea maporini kuangalia mtego wangu na hiki ndicho kitoweo cha leo mana tulikuwa wawili na bwana Nyandu tumegawana huko huko". Chito alipokea kisha akamuacha baba yake atangulie ndani alishangaa sana kuona damu nyingi alafu anatembea akiwa hajiamini, pia harufu ile ndio inamshangaza sana " Baba kuna mgeni kafika hapa leo alikuwa anatuulizia sisi"

"Mgeni gani huyo?" "Mwenyekiti kutokan kijiji cha Kalulu alikuja kufuatilia swala la mtoto wa mzee UWESU mkwe wangu wanamhitaji mtoto wao wamuone NYAMALI yaani mke wangu sasa sijui baba utawaeleza nini hapo mana ushanitia mashakani kabisa na wanatusubili kwa bwana MASANJA mana hili jambo limefika kwake na hatujui kamueleza nini huko kwa hiyo kajiandae alafu tuende huko"

Ghafla mzee Mambo sasa anadondoka chini na kuzimia.

Taarifa ya mzee KELEBU iliwafanya kuwa na amani sana pale kijijini kwani hali ya binti Lyoto iliweza kuwa salama kabisa, afya yake ilikuwa nzuri baada ya kupata huduma kutoka kwenye miti ile aliyokwenda kuichukua kijana BAMUZI mfalme ambae anatarajiwa kukaa. Mzee huyo alimshauri Mzee Ngololo kuwa aitishe mkutano wa wanakijiji wote wa CHAMLO ili kuweza kuelezana baadhi ya mambo yenye faida katika kile kijiji kwani tabia ya wanakijiji hao kukataa kujitolea kumsaidia mfalme kutafuta dawa si nzuri kabisa.

Mzee Ngololo alimuita bwana Mwalami na kumuelza kitu "Bwana wewe nakupa siri ambayo niliiweka kwa muda mrefu pia niliona kuitoa mapema inaweza kuzua utata kwa mambo mawili kwanza siri yenyewe tulipata taarifa ambayo sina uhakika nayo kuwa "Mfumo wanataka kuubadilisha hawataki tena kutawala kwa nja ya ufalme wanataka kuwa na mwenyekiti ambae atachaguliwa kwa sifa watakazoleta, pia wakatoa tamko kuwa tupeleke majina ya vijiji ambavyo vinaongozwa kwa ufalme, sasa jambo gumu kuwa hapa kijijini watu wanaishi kwa amani lakini huu mfumo utakuja kumaliza watu, pili wanasema hawataki kuamini mambo haya ya mizimu tunayotaka sisi wanataka kuishi kawaida tu bwana wewe".

"Mbona habari mpya hiyo, imetoka wapi?" aliuliza bwana Mwalami. " Kiongozi wangu wa habari ndie alifuata hizo taarifa wakati anatembea kijiji na kijiji ili kujua yanayojili na kutuletea na hivyo kabahatika kapitia kijiji cha KALULU kinavyoitwa kpo mbali sana na mimi sijawahi kufika sasa kesho nadhani atakuwa anarejea katika moja ya safari zake sasa atatueleza zaidi kwani nadhani atakuwa huko akipita kijiji kila kijiji kupata taarifa".

"Basi tusubiri nini cha kufanya baada ya yeye kurudi, nitajua nini nikushauli lakini mkuu usisahau kuwa kuna safari ya kwenda mpoloni kuhani msiba wa kijana yule aliyemsaidia Bamuzi". "Hilo usijali itapangwa safari kubwa lakini kwanza tumalize hali ya huyu malkia baada ya hapo tukimkabidhi basi tutakwenda"

Upande wa binti Naomi akiwa na mama yake alimueleza kuhusiana na kijana ambae katokea kumpenda sana kutoka moyoni na anashindwa kuzuia hisia zake pindi akimkumbuka " Mama kuna kijana alikuja juzi hapa yani mzuriii huyo, nimempenda sana mama yani hata kwa kitu chochote naomba ufanye ili nimpate huyo kijana". mama yake alimuangalia sana Naomi akaona jinsi gani anavyoteseka kimapenzi, alimuonea huruma sana mwanae na mzazi siku zote hapendi kuona kiumbe alichokitunza tumboni kwa muda mrefu kinalalamika kwa jambo ambalo linawezekana.

"Mwanangu ebu niambie jina lake unalifahamu?' " Mama nimelisahau kabisa japo aliniambiaga".

"Sawa ngoja keshokutwa nakwenda kwa Bwana Ukelele naamini tutafanikiwa sana kwa hilo. Hatimae siku zilikwenda na keshokutwa ikafika wakafunga safari ya kwenda kijiji cha MPOLONI, walipofika hadi kwenye nyumba hiyo ya mzee Ukelele walimkuta yeye mwenyewe.

walimueleza shida yake na kwa kuwa huwa alikuwa anakuja sana Mama Naomi ilikuwa rahisi kukubaliwa 'Mzee huyu mwanangu ana shida na kumpata mwanaume ambae anampenda sana sasa naomba umsaidie".

"Naomi unamfahamu jina la huyo mwanaume?" " Hapana"

"Haya chukua hiki kitu sema kisirisiri alafu taja kwa sifa zake zote kama jina humjui na itakuwa rahisi mimi kumjua na mkifika kwenu haitochukua siku nyingi atakuja hapo." waliondoka wakiwa na imani kuwa watasaidiwa na mwanaume huyo atakuja kulealiko Naomi. wakati wao wanaondoka ndipo Katunje na Mwaija walikuwa shambani ndipo wakafika wakiwa wamechoka sana.

Mzee huyo alianza kufanya kazi ile lakini anashangaa kuona Katunje analalamika mkono kuwa dawa yake inambana kuonyesha kuna hatari fulani, mzee ukelele akamuuliza " Kijana samahani isije nakuumiza wewe unamjua NAOMI siku uliyekwenda Chamlo ulishaonana nae?".

"Ndio babaaa nilikutana nae na ndie ambae alinipeleka kwa mzee Mwalami..."

"Tobaaaaaaaaa........kumbe ndie wewe anayekuhitaji huyu mama mpuuzi kweli alafu mjukuu wangu abaki na nani shenzi " akavurugavuruga mitego yote ambayo aliweka ili kumfanya mwanaume huyo kwenda kumfuata Naomi na kumbe alikuwa Katunje ambae kwa sasa ni mchumba wa Mwaija.

Baada ya siku kupita Mwaija alitamani kwenda kupajua nyumbani kwa Katunje ambako alimtajia kuwa ni SHISHIMO "Sawa siku moja tutakwenda kwani hata mimi nimepakumbuka nyumbani sana ".http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Walifurahi sana hasa Mwaija kumpata mwanaume ambae hakutarajia kama atakuja kumpa raha na amani moyoni mwake..............





Mzee UKELELE aliamua kuacha kabisa kuifanya kazi ile ya Mama yake NAOMI aliyekuja kwa ajili ya kumganya kijana ambae anamhitaji Naomi basi aweze kurudi ndani ya kijiji cha CHAMLO. "Kwani vipi babu kuna jambo gani kwani lililotokea?"

Aliuliza KATUNJE

"Hapana kwani nilitaka kufanya jambo ambalo lingetutenganisha kati ya sisi na wewe" Mzee huyo alisema kumuambia kijana Katunje. Jambo hilo lilifanya kijana huyo kuwa na maswali mengi sana ambayo hayakuwa na majibu kamili kwenye kichwa chake. "Sasa babu hapo sijaelewa kuwa kutengana kwa namna gani yani mimi na nyinyi?"

Katunje hakuwa na amani kwani alikuwa na shauku ya kujua nini ambacho alikuwa anamaanisha Mzee huyo. Lakini japo na juhudi zake za kutaka kujua kile ambacho kipo nyuma ya pazia lakini mzee huyo alikuwa mgumu kumueleza kiundani zaidi nini ambacho wale wageni yani mama Naomi na Naomi mwenyewe walikuwa na shida gani. Katunje na Mwaija walitoka na kumuacha peke yake mzee huyo akiendelea na shughuli zake za utengenezaji wa dawa na mambo yake mengine.

" Mwaija najua bado hatujaanza kujuana vyema lakini mapenzi yetu unayaonaje?. Aliuliza Katunje huku akimkodolea macho kwa makini kana kwamba anataka kummeza kwa hamu iliyotokana na njaa ya muda mrefu sana.

"Mh! mhhh weee Katunje kiukweli sijui hata nikuambie nini kwani nakuona kuwa wewe pekee ndie ambae umebakia katika msaada wangu ndani ya maisha haya ya sasa na kuhusu mapenzi yangu mimi na wewe najiona mwenye furaha sana Ehee! je kwa upande wako".

Baada ya kueleza kipi ambacho moyo wake unajisikia ndipo na yeye akrudisha swali hilo kwa mwenzake ili ajue nini na yeye anachojisikia.

"Kweli pia nashukuru sana unajua kuwa bado tuna safari ndefu sana kwenye mapenzi yetu, alafu mimi kiukweli bado sina furaha kabisa maishani mwangu". Katunje aliongea kuwa hana furaha akimuambia Mwaija ambae alitarajia jibu zuri kama alilompatia yeye wakati kaulizwa. "Niniii? huna furaha kipi kinakufanya usiwe na furaha?" Muda huo wako kjikoni wote wakiandaa chakula cha wakati huo.

"Sina furaha kweli na sijui furaha yangu itarudi lini tena kwani, nilikuja hapa kwa sababu ya kumtafuta ndugu yangu aliyenipotea kwa muda mrefu sasa yani sijui wapi ambako kaelekea, yani LYOTO ananiumiza kichwa sana kiukweli mpaka sasa hivi".

"Mwaija nae aliona huruma sana ndipo akainuka na kukunja upande wa kanga yake na kumfuta chozi ambalo kijana Katunje alikuwa anamwaga kutoka kwenye mboni mbili za macho yake. "Pole sana sikujua kuwa hiko ndicho kinakufanya ukose furaha ila ngoja tumuulize babu atatusaidia tu na wala usijali kabisa"

Majira ya usiku kuingia Mwaija alianza kuhangaika huku na kule akiyumbisha kichwa chake na kumfanya Katunje aweze kuamka na kumuangalia, alishtuka baada ya dawa ambayo ipokwenye mkono wake maeneo ya msuli kumbana kuonyesha kama kuna hatari kubwa sana iliyopo. Alimuangalia huku akim shangaa kwa jinsi anavyohangaika huku na kule.

" huyu si bure itakuwa ni ndoto hii ila inaweza kuwa ndio ile ndoto ya kumfahamu nani ambae alihusika na tukio la Lyoto ngoja nimuache kwanza" Aliongea Katunje baada ya kuhisi kuwa kama ni ndoto basi itakuwa ile ambayo alihitajika kuiota yeye kuhusiana na kupotesa kwa Lyoto ila sasa anaiota huyu Mwaija. Ghafla anashangaa ananyamaza na akatulia kabisa na ndipo wote wakawa wamelala mpaka asubuhi ya siku iliyofuata.

Asubuhi na mapema sana Mwaija alimsimulia yote ambayo aliyaota kwenye ndoto ambayo yalikuwa ni kama msaada mkubwa katika ile kazi ya kumtafuta mtu wao.

"Basi tuende tumuelekeze babu inawezekana akatusaidia kwani yeye mwenyewe alisema pindi utakavyo ota ndoto hiyo hapo ndipo na sisi tumuambie kila kitu". waliondoka kutoka kwenye chumba chao na kumuendea mzee Ukelele ili kumpa taarifa.

"Hodiii Babuuu, babuuuu " walimuita mpaka pale alipofungua mlango

"Naam vijana wangu kuna tatizo lolote asubuhi hii?" Aliuliza kwa shauku kwani ni mzee mwenye tabasamu kwa muda wote ambao alikuwa nao.

"Ndio baba, usiku nimeiota ile ndoto yote ambayo ulisema ikitokea tuje kukuambia" Mzee hakika alianza kufurahi na akawaomba haraka sana waingie ndani, kweli wote waliingia ndani na wakaanza kumhadithia huku Katunje akiwa na hamu ya kumjua nani huyo kwani ndoto haikutaja jina lolote japo alikuwa na hisia juu ya mtu fulani.

"Sawa hiyo ndoto tayari kwani ilivyoelezwa na mimi imenisaidia kujua wapi naanzia sasa Katunje kachukue ile dawa ambayo ulienda kuchukua kule msituni siku za nyuma".

Alienda kwa haraka sana na kurudi aliagizwa na maji akachukua kisha vyote akavileta mbele ya mzee Ukelele. Muda kadhaa alikuwa tayari keshamaliza kazi yake ya kuiandaa dawa hiyo muhimu sana kisha akaanza kumpa maelekezo juu ya matumizi ya yale dawa.

"Sasa hapa naomba mnisikilize kwa makini kwanza nataka kujua kijijini kwenu unakwenda lini?" Aliuliza mzee Ukelele "Huko natarajia kwenda siku chache baada ya kufanikisha kurudisha binti Lyoto". Katunje akajibu

"Sawa hii dawa itakubidi uioge siku tano asubuhi na usiku siku tatu ukiwa KILIMALONDO siku moja ukimtafuta huyo binti siku moja wakati unapanga kwenda kwenu hapo utamaliza kila kitu".

katunje alipatwa na bumbuwazi kwa jambo lile.

"Sasa babu inakuwaje kwenye swala la huyu mtu ambae anahusika kwa upotevu wa binti lyoto?"

"Kuhusu hao usijali ndio maana nikakuambia wewe kaoge kwa hizo siku tatu mimi nitajua pia nitakukuta hukohuko maana najua itakuwa kazi ngumu sana nitakuja na kuhakikisha huyo aliyemuua binti yangu Mama Mwaija basi atanitambua lakini kumbuka hata kama ukafika usiku wa muda gani lazima uioge hii dawa pia naomba mzingatie yasije kuwakuta mabaya kwani mtakuwa mnawindwa kama nyinyi mnavyowawinda wao".

Walipanga safari ya kurudi tena hadi ndani ya kijiji cha Kilimalondo ambako alitokea na mambo yote yalianzia mpaka kumfanya awe pamoja na Mwaija. Walifika usiku kama kawaida kutokana na umbali uliopo. walifika kwenye nyumba ya kijana Katunje lakini katunje anashangaa kuona mazingirz yako tofauti sana na kawaida ambayo huwa kaizoea. "Mwaija hapana hapapo salama kabisa hapa"

"Aaah mimi nimechoka nahitaji kwenda kulala" Mwaija alikuwa kachoka sana lakini Katunje nafsi yake inakataa kabisa kuingia mule ndani, haikujulikana kuna nini ndani humo mpaka awe na wasiwasi namna hivyo, kutokana na kuwepo kwa mwanamke basi Katunje alikubali na wakaingia ndani, walisafisha kidogo maeneo yao ya kujidai/kulala kisha wakajitupa kitandani hiyo yote ilitokana na uchovu walionao wa safari na kufanya Katunje kusahau kabisa juu ya kuiandaa dawa na kuoga.

wakiwa usingizini Jogoo anawika kijana Katunje anasikia sauti ambayo kama inamkumbusha jambo fulani "''Kijanaaaa, onaaa niniiii unafanyaaaa onaaa unampotezaaaaa Mwaija....umeshindwa kufuata masharti.....".

Alikurupuka toka kitandani na akiangalia ubavu wake wa kushoto ambako alilala Mwaija hayupo kabisa. aliinuka akakumbuka na ile ndoto ya asubuhi iliyomueleza kuwa umeshindwa kufuata masharti.

"Mamaa yangu sijaoga ile dawa sasa Mwaija yuko wapi jamani...Mwaijaaaaa"

Alikurupuka na kutoka nje ambapo mlango wenyewe ulifunguliwa na haikujulikana nani ambae alikuwa kaufungua. alitoka nje huku akiita lakini hakuna ambae alikuwa anamsikia. Mwaija haonekani kabisa machoni mwake. Akili iliyomtuma ni kurudi ndani na kuchukua ile dawa na kwa kwa kulikuwa na maji aliyaweka kwenye ndoo na kisha akachanganya huku akiwa na wasiwasi kabisa kwani alikuwa akitetemeka.

"Jamani mbona haya mambo yananikuta mimi tu"

Alienda chooni wakati anatoka nje anakutana na mzee Udevu ambae alikuwa anamshangaa sana kijana huyo kwani alipotea kwa muda kidogo tangu atoke pale hakujulikana wapi ambapo alikwenda.

"Weee si Katunje weweee umerudi ulikuwa wapi?"

Aliuliza Bwana Udevu huku akimsogelea

"weee mzee komaaa tena usinijie ondoka mbele yangu shetani wewe na mzee mwenzko KAUZIBE tena mpe taarifa yani nawachukia nyinyi hamnijui tu..." Alipandwa na jazba kubwa sana ukizingatia hawa wazee wawili ndio anawatuhumu alafu hapohapo mjukuu wa Mwaija kapotea kwa mazingirz ya kutatanisha. "kijana nakuuliza kwa upole unaniletea fyongooo unataka kujua nani mbabe si ndio ngoja wewe mdogo sana ".aliondoka na huku kijana katunje akaingia chooni na akawa anajimwagia maji yote yale yenye dawa.

Alivyotoka anasikia sauti ikimuita

"Katunjeeeee ukom wapi jamaniiii?" Akajua fika kuwa Mwaija karejea ilibidi na yeye afurahi na kuacha ndoo chini na kumkimbilia kule alikosikia sauti ya wito. Alimuona akiwa mlangoni akihaha kumtafuta Katunje "Mwaijaa mimi hapa hunioni".

"Uko wapi Katunje nasikia sauti tuuu jamani" Alilalamika kuwa yeye anamsikia sauti tu lakini hamuoni kabisa

"Mwaija mimi mbele yako hunioni kweli Mwaija ebu nitazame kwanza". Aliendelea kumsisitiza ili aweze kumuona ukweli Katunje alimkaribia na akaanza kumshika mkononi pale mlangoni kwao.

"Katunje nahisi kweli unanishika lakini hapa sikuoni kabisa yani sikuoni mbona uko hivyo vipi jamani Katunje "

"Mwaija macho yako yameharibika una maana kuwa hunioni kweli?"

Katunje alianza kutoa chozi likisaidiana na Mwaija ambae alijihisi mpweke bila kumuona Katunje akimsikia sauti tu

"Katunje niamini angalia hii ni ndoo uliyotoka nayo kuoga ina rangi nekundu na ulitoka kuioga ile dawa si hii lakini wewe sikuoni jamani huniamini"

"Aaaaaah mamaaaa weee sasa nimekuaje mimi mbona matatizo kila nilifanyalo jamani". Ghafla ndipo KIMOLO akiwa katika doria yake ya kama kawaida kumtafutia mzee binti wa kucheza nae kwa siku hiyo kwani huwa ndio kawaida ya Mzee SWAI kufanya hivyo, alipokaribia ndipo Katunje alipomuambia Mwaija jambo.

"Mwaija kama kweli sionekani huyo anayekuja ana kawaida ya kumtafutia mzee wake Swai wanawake kama saizi yako sasa akija mimi nipo hapa ongea nae".

Kweli alifika mpaka pale na akashangaa kumuona binti mzuri sana katulia kwenye nyumba ya kijana Katunje na wakati katunje mwenyewe yuko pembeni.

"Eweee binti mzuri uliyependezwa na Swai wa Kilimalondo, unaonekana kuwa mgeni na nyinyi wageni ndio anawataka sana mbona uko peke yako?"

Katunje alishangaa kuona kuwa yeye haonekani mpaka anaulizwa Mwaija kwa nini yuko peke yake, alijishika huku na kule ili ajue nini ambacho kimemtokea mwilini mwake lakini haikufaa chochote. " Namsubuli mchumba yangu anakuja" Alijibu Mwaija.

"Mchumba yako yupo unayemsubili wewe sasa jiandae twende kwa mzee Swai haraka sana utakula kila ukitakacho mzee mwenye mali nyingi sana na asiyejua kutumia nyinyi ndio watumiaji wake". Katunje alishuhudia jinsi Kimolo anavyolazimisha kumbeba Mchumba wake. Hakika alikasirika sana ndipo akampiga ngumi nzito ambayo ilimpeleka chini kama mzigo utupavyo chini kutoka umbali mrefu.

Kimolo alishangaa kuwa ngumi inatokea wapi, alisimama ili ajipange kama jemedari wamzee SWAI apambane na mtu huyo, wakati upande wa Mwaija nae alishangaa kuona jamaa kaanguka wakati alishikwa mkono huku akilazimishwa kutoka pale aliposimama.

"Mjingaaa wewe mwanamke unadiriki kunipiga mimi kabisa unanifahamu mimi eeeh?" Swali lake halikujibiwa na Mwaija bali ilijibiwa na ngumi nyingine nzito ambayo ilimpelekea kumtoa damu nyingi puani na mdomoni. Mwaija alishangaa sana akaamini kweli Katunje yupo ila haonekani kwa hali ya kawaida kabisa.Hapo ilimbidi bwana Kimolo na nguvu zake atafute njia ya kukimbilia ili kuokoa maisha yake huku akiwa na wasiwasi mkubwa sana.

Huku nyuma Kijana Katunje alimsogelea Mwaija na kumshika mkono ambae Mwaija kwa upande wake aliona tu mikono yake ikinyanyuka lakini mtu mwenyewe haonekani.

"Mwaija basi inanibidi na wewe inakubidi ukubaliane na hali yangu niliyokuwa nayo kwa sasa hakuna jinsi nahisi kujitambua kwa upande ungine labda inaweza kuwa sababu ya mimi kumrudisha lyoto wangu" Mwaija alifuta chozi kisha akamkubalia ndipo walipoingia ndani.

Mzee udevu ile taarifa akaipeleka kwa mzee Kauzibe ambae hakuwa na hili wala lile. " Kauzibe unayajua haya ya asubuhi hii?"

"Yapi hayoo tena ?" aliuliza bwana Kauzibe

"Leo asubuhi wakati naelekea kwa yule ndugu yangu niliyekuambia jana kuwa ni mgonjwa si nikapita pale kwa kijana yule Katunje!"

"Eheeee"

"Huwezi kuamini kijana kwanza karudi maana nimemuona kwa macho yangu haya mawili" Mze Kauzibe akasimama kwanza "Unasema yaliyo ya kweli kuwa karudi huyu kijana?"

"ndio kabisaaa"

"Ahsante maana nilikuwa nimembakisha mpuuzi huyu kwani ananifanya niishi kwa hofu hapa unajua pia kuwa uongozi wa Ufalme unaanza kufa sasa ndio maana nataka kuondoa hawa vikwazo vyangu nije kuwa mwenyekiti"

Aliongea bwana Kauzibe kumpa taarifa kuwa uongozi wa ufalme unaenda kufa na sasa unaingia mfumo mpya wa mwenyekiti ambae atachaguliwa na wanakijiji wake husika.

"Lakini si hayop tu ya kuja yeye kuwa makubwa sana kuna makubwa aliyoyafanya na ndio yaliyonileta hapa kwako mpaka sasa"

"yapi tena hayooo?"

"Yani yeye katutukana kwanza, pili anasema sis ndio wabaya wa hapa kijijini sisi anatuchukia tena zaidi ya maelezo mpaka nimeogopa kwenda kumuangalia ndugu yangu yani sijui anachojivunia kitu gani"

kauzibe alikunja sura na kumshika mkono na kumeleza kuwa atamtumia vijana ambao watamfanyia kazi kubwa sana na kumuangamiza kama alivyoangamia binti Lyoto.

Mzee swai anashangaa kumuona kijana wake mdomo umevimba damu zinamtoka ilimbidi amuulize kwanza "Bwana wee nini kimekutokea huko na mbona hujarudi na mwali yeyote leo?"

"Mfalme wangu bwana nilichokutana na huko wee acha tu, kuna mtu anapiga lakini haonekani kabisa"

walicheka sana baada ya ksikia hayo maneno

"Sijawahi kuona siku ya maajabu kama ya leo sasa ngoja siwezi kuacha dharau wakati kila mwanakijiji hapa anajua kuwa mimi ikifika siku ninayotamani kumpata mwanamke namchukua na hawakatai sasa nani ambae kakukataza huyo?".

Walishtushwa baada ya kumuona mzee Kauzibe kafika pale, "Mkuu nina shida sana naomba vijana wako wakamuadhibu Kijana Katunje maana katutukana sana mimi na bwana Udevu".

"Hapo umekuja pazuri sana kinachotakiwa fuatana na hawa vijana sita wanatosha kumshikisha adabu na inatakiwa mukimkamata nendeni mbele za watu alafu mumpige mpaka kifo chake alafu mimi nitakuja kutoa tamko"

Waliondoka kumfuata bwana Katunje.

Wakati huo katunje tayari yuko ndani "Mwwaija naomba utulie humu ndani na usitoke mimi hunioni ila mimi nakuona nitakuwa mlinzi kwako muda wote, nakuja mara moja".

"Katunje ni bora ukaenda kuniweka nyumbani kabisa siwezi kuishi hivi mimi" ghafla mlango unafunguliwa kwa nguvu na vijana hao waliotumwa kazi na bwana Swai.

"Katunje toka njeee haraka sana tena sana, " katunje alimficha yule mwanamke chini ya kitanda kisha yeye akatafuta upenyo kati yao kwa kuamini kuwa haonekani akapita hadi nje. wale walikagua ndani humo na hapakuwa na kitu mmoja alipata wazo kuwa wachome ile nyumba ili kumdhoofisha kijana katunje.

Kabla hawajatekeleza ilisikika mtu akianguka chini huku zikimtoka damu kichwani, " jamani mwenzetu kaanguka chini, kuna kitu kimempiga hapa"

Mmoja wa viajana waliongea lakini haikuchukua dakika kadhaa, ilisikika kitu kikianguka kwenye kichwa cha mtu """nduuuu""" na yeye akadondoka chini na palepale marehemu. hawakuchukua muda walikimbizana huku wakiwa hawajui wapi ambako wanakimbilia.

Mzee Kauzibe alikimbia zaidi ya vijana wote kuogopa yale yaliyowatokea wale alio waona kwa macho yake wakianguka chini. Lakini mwingine aliyekamatwa baada ya kupigwa akapewa ujumbe " nakuomba uende kwa mzee Swai akamueleze kuwa aachane na kuwaharibu watoto wa kike wa hapa".

kijana huyo alisimama huku akiyumbayumba na kukimbia zake kwenda kutoa taarifa kama alivyoambiwa.

MAPATO anaingia kijiji cha BWAWANI kutoka kijiji cha SHISHIMO ambako alikwenda kwa shida yake ya kumhitaji bwana Mambo Sasa. Aliona vyema sana endapo akirudi kwanza nyumbani kujipanga baada ya kupata taarifa tofauti na ile aliyotarajia.

Alipofika ndani ya kijiji chake alikutana na rafiki yake bwana SIKUJUA walioachana nae kwa muda kadhaa wakati yeye nasafiri kwenda Shishimo " Bwana karibu sana sijui habari za huko utokako hawajambo?" Sikujua aliuliza baada ya kumkaribisha Mapato pale kwake.

Mapato alianza kufika kwa rafiki yake kabla hata ya kufika kwake mwenyewe. "Nashukuru sana na pia nimefika salama lakini sasa kitu ambacho nilikiendea kule sikukipata kwani nimekuta mkanganyiko mkubwa sana". Sikujua alishtuka kidogo ndipo akainuka na akaenda kufunga mlango wake ili kuwa na usalama kabisa.

"Sijaelewa ehee mkanganyiko gani huo ambao uliukuta?"

"Unakumbuka kuwa kule bwawani aliyehitajika ni bwana Mambo sasa kama tulivyotamka kule ile siku"

"ndio nakumbuka vyema sana " sikujua alijibu

"Sasa, nimefika kule nikapokelewa na mwenyekiti ambae alinikaribisha vyema sana baada ya kumuelezea kuwa nakuja kumuangalia ndugu yangu, lakini sasa kumbe yule mzee Mambo sasa sio jina lake bwana wewe"

Sikujua alishtuka tena

"Unasema kuwa....!"

"Ndio hivyo jina lake bwana CHITO" lakini baba yake anaitwa Mambo Sasa.

Sikujua alikohoa kidogo kisha akaanza kusema "koh!...koh!...koh!..hapo sasa ndipo nakuja kusema kuwa kesi ambayo inatukabili kwa SUSU anasema kuwa sasa anaanza kuwa na kumbukumbu baada ya kumpiga kipindi kile kumbukumbu inamrejea...sasa......" Akiwa anafikilia

"Sasas nini tena....?"

"Mapato tunachotakiwa kukifanya ni kuwa kuweka uwazi kuwa Mambo sasa sio jina lake anaitwa Chito na ndie ambae alimfanyia unyama Mama Mengi kwa kumchoma kisu na akamtolosha mwanae sikitu ili ajulikane kuwa kakamatwa lakini ni mchezo wa kufanya mambo yake huku akijificha kivuli cha kupotelewa na mwanae, pia ndie ambae kampiga SUSU kwa kuwa alimpaga kama ushahidi lakini susu akasema ukweli mbele ya mwenyekiti akaamua kumfanyia hayo"

Mapato alibaki kuduwaa...http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"yani wee jamaa wewe una mbinu nzuri sana ehee baada ya hapo"

aliuliza mapato

"Baada ya hapo itatumwa taarifa ya kuitwa yeye akija si ndio njia ya kupelekwa bwawani kumaliziwa".

Hapo umecheza vizuri sana sasa ngoja nikafike nyumbani kwanza". Alifika nyumbani kwake huku akiwa na bashasha kutokana na ushauri mzuri wa rafiki yake.

Alipofika kwa mkewe hakika alipokelewa kwa furaha sana na kuandaiiwa kama mume kisha baada ya hapo walipumzika baada ya kula chakula. " Haya mke wangu habari za kuwaacha huku?" aliuliza bwana Mapato

"Huku salama kabisa yani sijui za huko na biashara?".

"Mke wangu hakika kule nilifanikiwa kupata, shamba ambalo tayari lipo kwangu lakini kilichobaki ni mimi kwenda kulifanyia kazi na lipo kijiji cha Shishimo kule, haya hakuna jipya tangu nitoke hapa"

Aliuliza

"Mme wangu mwenyekiti alitoa tamko akiwa na bwana MANUALI kuhusiana na SUSU"

"Ehee...koh!"

"walisema kipindi cha nyuma ajitokeze mwenyewe aliyemfanyia kitendo kile susu lakini hakujitokeza kabisa "

"ndio nakumbuka na jinsi wanakijiji wa hapa walivyo wabaya yani wamemuua mama Mengi hakujitokeza sembuse huyu kijana kweli!" Mapato alidakia

"Sasa wamesema juzi kuwa SUSU hali yake nzuri kumbukumbu anazo na nadhani siku hazijatajwa lini kuwa atasema rasmi ni nani ambae alimfanyia hivyo vitendo kwa hiyo tunamsubiri hapa ili akimtaja wanakijiji tuishi kwa amani hapa kwetu". Alimaliza Mke wa Mapato na kumuacha mapato akiwa hoi hajielewi,

"Nashukuru sana sasa ngoja niende kwa bwana Sikujua ili nikamsalimie kwanza si unajua nina hamu nae rafiki yangu"

Alinyanyuka na kuondoka huku akitembea kwa mwendo mkali sana ili afike mapema.

Alimkuta rafiki yake huyo akiwa anasuka mkeka ndipo akamuomba waondoke mapema kwenda kwa mwenyekiti ambae ataweza kuwasaidia na kujificha kwa mambp waliyoyafanya.

waliondoka hadi kwa mwenyekiti bwana SEMENI.

"Mwenyekiti tumekuja hapa bwana tuna mazungumzo ya hapa na pale kwa ajili ya maendeleo."

"Karibuni alafu sijakuona kwa muda hapa bwana Mapato ulienda wapi?"

"Mizunguko ambayo nayo imenileta hadi hapa kwako"

Walianza mazungumzo watatu hao. "Mh! kweli hilo jambo ni kweli kijana susu anasema anaweza kuongea ukweli pindi siku akitaka lakini ajataja lini kasema akiwa tayari anakuja hapa na ataomba aseme na wanakijiji ili aseme jambpo hilo"

"Sasa sisi tunamjua aliyemfanyia hivyo na waliofanyiwa hivyo akiwemo mama Mengi"

Mwenyekiti alishtuka akakaa vizuri "Ehee yupi huyo?"

"Kwanza tunaomba ulinzi maana kuja kumsema mtu hapa inatakiwa moyo ili kesho mtuhifadhi tukipata taarifa zingine tuje kukuambia mwenyekiti"

Walijiwekea ulinzi kwanza kisha wakaendelea kuongea kwani bwana Mapato alikuwa muongeaji mkuu

"Muuaji na msababishaji wa yale yote ni mzee Mambo sasa"

"Weeeeee....Naniii inawezekana vipi mzee aliyepotelewa na mwanae na kama ni yeye sasa nani ambae kamchukua mwanae?"

Aliuliza mwenyekiti kwao ilikuwa rahisi kwani walishalijadili mapema sana

"Mwenyekiti hili swala nilikuwa nalijua tangu muda sana, Mzee Mambo sasa alimtorosha mwanae kipindi kile sikujua aligombana nae akaingilia SUSU, sasa akaja na kesi nadhani unafahamu mpaka akaitwa mzee yule, lakini susu alikuwa upande wa kumtetea sikujua hilo swala likamuuma sana ndipo akaona arudishe kisasi"

Mwenyekiti alikuwa makini kusikiliza

"Ehee nakusikiliza endelea"

"Sasa baada ya kushindwa kesi akaamua kumtorosha mwanae kwenda kijijini kwao Shoshimo alafu huku akaanza mambo yake yule mama Mengi alimkuta siku moja akipanga njama za kumuua mtu, mama yule akamsikia lakini akajishtua kitu kilichomfanya bwana mambo sasa kumuona, Kama unakumbuka akasema kuwa jioni namsema nani ambae kampoteza lyoto..."

"Nakumbuka vyema sana"

"Eheeeeh! alienda kumuua shambani alikokuwa anakata kuni kisha akarudi kwa haraka, haikutosha lengo lake amuue mzee sikujua na susu watu wake kwa kuwa huyu niko karibu nae ndipo akamfanikisha bwana SUSU". Mwenyekiti aliamini kwa asilimia zote.

"Ujue mwenyekiti kwa nini ili uamini" Mapato aliendelea

"Ehee"

"Unamjua kwa jina gani yule mzee?" Mapato alimuuliza sikujua

"Si jina lake hilo la Mzee Mambo sasa!" alijibu mwenyekiti

"Aaaaaah ha! ha! ha! ha!...hapana, mwenyekiti haitwi hilo jina kabisa" Mwenyekiti alishangaa zaidi siku hiyo kwa kuwa habari anazopewa ni motomoto.

"Lipi tena jamani mnanichanganya"

"Umeniuliza nilikuwa wapi, nilienda Shishimo kufuatilia mambo yangu lakini ajabu sasa jina ambalo nililikuta kule kwani nilifanikiwa kumuona ndio kwake, anaitwa CHITO na nilimkuta siku hiyo anataka kumkata baba yake panga bwana Mambo sasa yeye anaitwa Chito".

Mwenyekiti ilibidi shtuke na kusikitika jinsi jamaa alivyokuwa katili, lakini alionekana kama anafikilia jambo fulani hivi kutokana na maelezo ya bwana Mapato " Choitoooo...chitooooo".

"Vipi mwenyekiti?"

"Hili jina la Chito kama nalikumba hivi hebu ngojaaa" Alikagua katika makarabasha yake na kutoa daftari moja ambalo lina majina ya wageni waliowahi kuja pale. kwa bahati alilikuta lile jina. aliwapa wasome yale maelezo

JINA; KATUNJE

KUTOKA; Kilimalondo

SHIDA; Namtafuta ndugu yangu anaitwa CHITO

Hapo kila mmoja akawa kachanganyikiwa kuona kuwa jina la bwana Chito kuna mtu alikuja kumuulizia pale hivyo wakawa wanjiuliza huyu bwana Katunje anakaa wapi?.

"Sasa hapa ndipo ninapojua kuna kitu kimejificha kwa sababu huyu kijana tulimtimua kwa hofu ya watu wageni kufanya uhalifu katika eneo letu bila kujua kuwa nduguye ni bwana Chito ambae tulimfahamu kuwa ni Mambo sasa"

Mwenyekiti alijiuliza.

Jambo la kufanya ni kumtafuta kwanza huyu kijana KATUNJE ili tujue kuwa anajuana nae vipi huyu muuaji.

"Lakini hapa kuna kijana alikuwa anakujaga kuuza mbuzi alisema anatokea kijiji cha Kilimalondo sasa siku akija tutambana ili atuambie kama yupo huyu kijana".

Alisema bwana Mapato. Hapo ndipo wakatawanyika na wakajihakikishia kuwa wamemkamata vyema sana mwenyekiti na wao wataishi kwa raha kabisa pale.





.Muda ambao mzee Mambo sasa alidondoka na kuanguka chini, jambo ambalo bwana Chito lilimshangaza sana iweje apewe taarifa alaf ghafla kama ile adondoke chini na kupoteza fahamu. Haikuweza kujulikana na siku zote damu nzito kuliko maji, pia baba ni baba hata kama kakufanyia nini atabaki kuwa mzazi wako tu hisia za maumivu ya moyo zilimuingia na kumfanya afungue mlango wa huruma hatimae akainama na kumbeba baba yake kisha akauelekea mlango wa chumbani kwa baba yake.

Ajabu ule mlango uligoma kabisa kufunguka mithili wanafanya mashindano Chito anataka kuufungua lakini ilionekana kama kuna mtu yumo ndani anaukandamiza usifunguliwe mlango huo. Lakini kwa hasira za bwana Chito ili kumuokoa baba yake alimuachilia chini kwanza kisha akapiga hatua kuelekea mwichi uliokaribu na mlabo wa nje, alienda nao moja kwa moja hadi kwenye mlango kisha akaupiga na ule mwichi ndipo ulipoachia, alimbeba tena baba yake na kumpitisha chumbani kwake.

Baada ya kuhakikisha kamuweka vyema, anastaajabu kuona Moja ya pambo la mwanamke kwenye kona ya chumba hiko, Wakati anatafuta uwezekano wa kumsaidia baba yake aliweza kuelekea ile bangili ambayo huwa inavaliwa zaidi kwenye mkono. Alifanikiwa kuishika na akawa anaiangalia kwa makini sana, alikumbuka jambo "Baba Sikitu unajua kuwa mzee MANYENYE ni fundi mzuri sana wa kutengeneza Mikufu na bangili za mikononi?....nahitaji uninunulie ili nipendeze" Jambo kubwa sana alilokumbuka kipindi anaiangalia ile bangili ni pale alipokumbuka utani wa mama Sikitu wakiwa kijiji cha BWAWANI,

"Mme wangu chooonde usiwaangalie wanawake wa watu walivyopendeza ninunulie na mimi ili nipendeze kama wao....". Hiyo siku ndipo akamuendea Mzee Manyenye na akaweza kupata ile bangili.. Chito alifura kwa hasira sana lile jambo ambalo analishuhudia pale " Ina maana baba yangu unadiliki kulala na mke wangu au kama hukulala nae hii ringi imefikaje huku na wakati siku ya mwisho nilimvalisha mimi mwenyewe...aiseee hapana sijakuelewa bado"

Hakika bwana Chito alijawa na hasira ambazo ilikuwa ngumu kuelezeka. Lakini aliachana na hayo yote na kuanza kumpulizia baba yake ili apate kuzinduka lakini huku akiangalia zaidi ile bangili ya mkewe ambayo kaikuta kwenye chumba cha Baba yake.

Baada ya masaa kadhaa Mzee mzima Mambo sasa aliamka huku akishangaa yale mazingira ambayo kawekwa pale alafu anamuona mtoto wake yuko pale kitandani akiwa kasinzia. Aliinuka taratibu bila yeye mwenyewe kufahamu alimuangalia mkononi alikuwa na ile bangili, aliichukua kisha akaelekea kwenye sanduku lake akachukua bangili ambayo inafanana na ile ambayo Chito alikuwa nayo aliweza kumbadilishia kisha akamlaza yeye sasa pale kitandani, hakuishia hapo alichukua kaniki yake na usinga wake.

"Nyamnyena Nyamnyena......Nyamnyena kulumbila kulumbilolo, Kalilolisema kama lilombilo chito kuliona alama cha mkewe, kalitafunaye nnyama kulipingolo asahau kabisaaa". Mzee huyo alikuwa akiyazungumza maneno ambayo alikuwa anamaanisha kuwa anaomba mizimu ambayo huwa wao wanaikubali sana kipindi chote pale wanapokuwa na shida, Chito kaiona alama ya mkewe hivyo anaogopa akaja kujua kila kitu na yeye anampenda sana mwanae sasa anahitaji asahau kila kitu pale alipo.

Muda wa jioni unaingia hapo ndipo Baba Sikitu anaamka kutoka kwenye usingizi mzito alishtuka anaona yuko kwenye kitanda cha baba yake alishtuka hivyo alijiona mtu ambae hana adabu bila kukumbuka aliingia mule ndani kwa sababu ipi. Alielekea kwenye chumba chake huku akiwa na ile bangili yake, kabla ya usiku anafika bwana Mwenyekiti MASANJA akiwa ana haraka sana. Mzee Mambo sasa alikuwa wa kwanza kumuona hivyo alihitaji kuondoka nje na nyumba yake ili awe mbali kabisa asiweze kuonana nae, " Mambo sasa unaenda wapi bwana wakati mgeni wako nimekuja hapa", Mbio zake hazikusaidia jambo kwani alishaonekana na mwenyekiti huyo hakuwa na jinsi aliamua kumsubiri ili amsikilize.

Masanja alifika pale na kuweza kusalimiana wa kwanza bwana Masanja alimpelekea mkono lakini bwana Mambo sasa alikataa katakata, " sema shida yako nina kazi nataka kwenda kuifanya"

Alionekana kuwa na jazba bwana huyo, "Sawa lakini haya mambo niliyokuja nayo yahitajika mimi na wewe tukae chini ili tuyazungumze lakini ukiwa kwenye hali hiyo sielewi nini una maanisha!" Mwenyekiti alijitahidi kumuelewesha vizuri sana Baba yake Chito.

"Nimekuambia hivi kama hauna cha kuongea nitafute siku nyingine kwa sasa siwezi kukusikiliza" Alionekana bwana Masanja kucheka kwanza kana kwamba anastaajabu pia haamini kwa yale anayoyaona. "Mzee unanifahamu mimi vyema, unajua kuwa mimi kama serikali ambayo naweza kukushtaki kwa kukataa maelezo yangu wakati wewe na mtoto wako ndio yanawahusu". Ilimbidi mwenyekiti atumie cheo chake baada ya ustaarabu kushindikana.

"Kijana kuwa kiongozi hakuwezi kunitisha mimi au kama unataka kutishana tuanze wewe bado mdogo sana haya nakusikiliza sema "

"Taarifa kutoka kijiji cha KALULU kule ambako mlikwenda kuoa wewe na mtoto wako, kwamba alikuja mwenyekiti wa kijiji hiko sasa Mzee Uwesu kama unavyomfahamu na anavyofahamika katoa kauli kusema kama hamumpeleki mtoto wao yeye atajua la kufanya lakini kwa ustaarabu aliokuwa nao mwenyekiti huyo wakakaa kikao kujadili na ikaonekana kuwa waje hadi hapa kuja kujua maendeleo,".

Mzee Mambo sasa alishusha pumzi kwanza huku akionekana kutafakari " Bwana waeleze kuwa mtoto wao sisi tulimchukua huko kwa mahali kubwa tu sasa sisi ndio tunajua jinsi gani ya kumtumia kama kumla nyama au kumfanya nini tunajua sisi kikubwa mwambie yeye ni mzima"

Jambo ambalo halikumuingia akili bwana Masanja

"Baba wewe ni mtu mzima kuniambia kumla nyama sishangai kwani unajulikana kijiji kizima kuwa wewe ni mwanga mkubwa tu ila sasa nakuomba kabla yule mwenyekiti hajaondoka kesho mumlete NYAMALI mtoto wao la sivyo nitakudhalilisha mzee japo nakuheshimu".

Hali ya maelewano haikuwepo tena baina yao kwani kila mmoja alikuwa anatupia maneno yake kwa mwenzake ambayo yanaonekana kuvunjika kwa amani kati yao. "Haaa haaaa! kijana utajisumbua sana usijaribu kufuatilia mambo ya watu ebu yaache pia mwenyekiti una tabia ya kuwakaribisha wageni hapa bila sisi kujua sasa ukome kabisa la sivyo nitakugeuza kinyago".

Mwenyekiti na yeye hakuwa mjingamjinga kama mzee alivyomfikilia hakuogopa vitisho vya huyu mzee kabisa aliendelea kumpa ukweli wake.

"Wewe Mzee nakuambiaje huniwezi, yani hata hutamaniki kabisa hapa kijijini na yule mpumbavu mwenzako, unadiliki kumla nyama mkeo wako wewe mwenyewe wewe ni mtu au mnyama, na hili swala nitakuja kumuambia Mtoto wako Chito, haya angalia umemkimbiza mpaka Kijana ambae ni mfanya kazi sana hapa kijijini kijana mdogo huko aliko KATUNJE, hufai...."

Mzee Mambo sasa alianza kukasirika baada ya kuona mwenyekiti anayoyasema yote yana ukweli asilimia miamoja zote. "Kijana usiongee vitu ambavyo huna uhakika navyo unajua nini kuhusiana na mke wangu mjinga wewe"

Mwenyekiti alirudi wakati alikuwa anaondoka na wakati huo huku ndani bwana Chito anatoka kwenye usingizi mzito na anasikia sauti ya mwisho ya bwana Masanja.

"Unadhani sijui siku nikimuona mwanao hakika namueleza kama uongo unamfahamu mzee UPENGO unamjua alikufanya nini yule mzee mpaka sasa huna hata hamu kwenda kijiji chake tena nimekumbuka ili kukomesha upuuzi wenu wa kichawi ni kumleta mzee Upengo na kukuambieni ukweli baada ya kuwapa taarifa wanakijiji na mimi naenda kumueleza kila kitu Mwenyekiti hapo ndipo akija mzee uwesu utakuja kujua....."

Mwenyekiti aliondoka zake na huku mzee Mambo sasa alikuwa akijikuna kichwa baada ya kukumbushiwa jina hatari sana la Mzee Upengo, japo haijulikani mpaka sasa kuwa mzee Upengo alimfanya nini Mzee Mambo sasa mpaka amuogope kiasi kile.

Aliingia ndani huku akielekea kwenye chumba cha Chito, wakati huo chito alivyohisi mzee wake anakwenda alijifunika gubigubi na huku akiazima usingizi wa ghafla baada ya kuanza kukoroma. "Huyu umri nao unakwenda analala sana lakini inabidi nimkomeshe kabisa bwana Masanja anaweza kuharibu kila kitu, nampenda sana Chito pamoja na ndugu yake japo sijui wapi yeye kafia basi urithi wangu huyu ndie ataukamata...alafu nilikabidhiwa nyama yayaaaaaa ngoja niandae haraka sana".

Alielekea jikoni japo na uzee wake aliandaa nyama ya binaadamu tena mkwewe yani mke wa Mwanae Mama SIKITU aliiandaa vyema na baada ya maandalizi hayo aliweza kupika chakula kizuri sana, Muda wa usiku uliingia ndipo Chito alitoka kutoka usingizini na kufika pale alipoitwa na baba yake.

"Chito unalala sana mwanangu haya mimi nishakula chakula changu wewe kula mimi naenda kwanza huku kwa baba yako mdogo narejea sasa hivi?".

Chito alikaa tayari na kuangalia ile mboga jinsi ilivyonona, akiangalia ugali jinsi unavyoita kwa ajili ya kuliwa. Alinawa maji kisha akamega tonge la kwanza alipamba mchuzi tu kisha akala,tonge la pili akachukua kipande cha nyma lakini akakumbuka maneno ambayo muda fulani walikuwa wakiongea baba na Mwenyekiti....

"......Unamuua mkeo alafu unamla nyama.....Unamla nyama....unamla nyamaa...nyamaaaa....wewe si mtuuu bali ni mnyamaa....mnyamaaa....kama unabisha ....Mzee UPENGO.....upengooooo huna hata hamu kwenda kijijini kwake pumbavu weeeee........"

Alivyoyakumbuka hayo wakati yeye kajilaza chumbani aliacha kwanza lile tonge, kisha akajiuliza "Ina maana nikimpata mzee huyu Mzee UPENGO nitajua kila kitu na atanisaidia hata kumjua mke wangu yuko wapi....lakini inaonesha safari ya baba kwenda kwa rafiki yake yule si ya amani ngoja nikamueleze Mwenyekiti ajipange na kama kuondoka kwanza kijijini basi aondoke kwa muda ".

Ndipo akauacha ule ugali na ile nyama japo alilamba mchuzi kwenye tonge ile ya kwanza, alinyanyuka na kwenda hadi kwa Mwenyekiti, lakini kwa bahati mbaya hakumkuta alimkuta mkewe ambae alipata kumuuliza "Naaam mke wa mwenyekiti habari yako?'

"Salama sijui za kwenu huko?" aliuliza mke wa mwenyekiti

"Sisi salama sijui mzee Masanja nimemkuta?"

"Hapa katoka aliniaga alikuja kwenu alivyorudi tu, akamsindikiza mgeni wake aliyekaja jana sasa mpaka sasa ajarudi bado labda kapitia kwa watu wengine kwenye mambo yao ya kubadilisha uongozi wao". Mzee Chito hakuwa na hamu tena zaidi aliondoka na kuanza kumtafuta mwenyekiti lakini hakufanikiwa kumuona. Kwa upande wa Mambo sasa na rafiki yake waliyoyaongea yalionekana vitendo vikifanyika.

"Yani maliza kabisa yani nyonga kabisa kazana zaidi usimpe pumzi ya kupumua kabisa" Aliyasema rafiki wa Mzee huyo wakati huo bwana Mambo sasa akinyonga moja ya kitambaa cheusi aina ya kaniki kwa nguvu zake zote mpaka pale alipoambiwa basi.

"Walichukua maji na kuyaweka kwenye chombo kisha akapitisha usinga wake kama mara tatu kisha ikaonekana sura ya mtu akiwa kwenye baiskeli kisha anaanguka chini huku akishikilia shingo yake, mwishowe ana pupapupa kama kuku anayechinjwa na hatimae anafariki dunia palepale na baiskeli ikiwa pembeni.

"Hapa sasa tumemaliza kazi hawezi kutusumbua sasa aende kwa huyo mzee UPENGO, yani wanamuita nyuki aje kutuamisha makazi uliona wapi...sasa mambo sasa nenda nyumbani ila hakikisha mwanao anakula ile nyama uliyoambiwa na wakubwa wa Nyamnyena sawa?" aliulizwa " sawaaaa"

Mzee huyo aliondoka kwa mwendo ambao aliufahamu yeye mwenyewe kwa bahati nzuri bwana Chito baada ya kushindwa kumpata mwenyekiti alirudi nyumbani akipiga tafakari za hapa na pale atamjuaje huyo mzee na atafikaje huko ili akamalize kazi zake na yeye maana kachoka.

Aliinuka na kuchukua vile vyombo na kwenda kutupa vilivyomo ndani kama mboga na ugali, mbali kidogo kisha akaosha.

"Chito habari mwanangu unaendeleaje vipi umeshakula chakula ?" Chito hakuwa na wasiwasi wa kujibu "Baba yani sikuamini kama chakula ulipika wewe mana ile mboga tamu sana yani sijapata kuona kabisa " Mzee Mambo sasa alivyopumbazwa akaamini kama kweli mwanae kala ile nyama maana ndio lengo kuu kuila ile nyama.

Asubuhi na mapema vilio vikasikika kuwa Mwenyekiti kafariki, hakika jambo ambal;o kila mmoja alisikitika kupotea kwa mwenyekiti baada ya kumkuta akiwa kafa kabisa.

Maiti waliikuta ikiwa njiani njia ya kuelekea kijiji cha KALULU na mke wa Mwenyekiti aliona kuwa hakuna mwingine ambae kamuua mumewe isipokuwa Mwenyekiti mwenzake kutoka kijiji cha Kalulu kwani ndie ambae alimsindikiza wakati anaondoka pale nyumbani kwake. Kwa hiyo baada ya maziko kesi iliyopo ni kuwa Kiongozi wa Kalulu kamuua kiongozi wa Shishimo na hakuonekana kabisa Mzee Mambo sasa na rafiki yake. Kuna msemo watu husema



(Kuna binti mmoja ambae alikuwa akiishi na bibi yake. Siku moja Binti huyo alimuuliza bibi yakje kuwa "Bibi hivi kumloga mtu kwa uchawi na ukishamloga usijulikane unafanyaje?....

Lilikuwa swali la binti huyo kumuuliza bibi yake sikiliza jibu la bibi kwa mjukuu alimjibu nini

"Ngoja jua lizame" Ilikuwa siku ya kwanza ilipofika jioni, binti akamueleza bibi yake " Bibi jua limezama tayari" lakini bibi neno lake kwa mjukuu wake lilikuwa lilelile kuwa " Ngoja jua lizame" baada ya siku tatu nyumba ya jirani walianza kutoelewana ndipo kauli za hapa na pale walitoleana kauli nzito ilikuwa """Yani nitakuua kwa chochote kile"""" hapo ndipo bibi akamuita mjukuu wake na akamuambia " Kila siku nilikuwa nakuambia ngoja jua lizame sasa leo limezama" mjukuu akauliza "Mbona mchana bado..." Bibi huyo akamfunulia ufafanuzi wote kuwa " Unaposikia watu wanagombana kama hao, na sisi tukienda kumuua kwa uchawi huyo anayeambiwa atauliwa na mwenzake hakika sisi hatutoonekan sawa na usiku kuwa na kiza hatutoonekana nini tunafanya zaidi ya yule aliyetamka neno tulilolitekeleza sisi....."



Haya maneno ya juu ni mfano wa kile alichokifanya mzee Mambo sasa na rafiki yake kumuua Mwenyekiti lakini anayekuja kujulikana na kuonekana kama muuaji ni Mwenyekiti wa Kalulu.

Siku moja Chito akiwa na nia ya kwenda kijiji cha Kalulu kwenda kumuita kiongozi wa kule kutokana na ile kesi hakutaka kwenda hivi hivi alimuita baba yake na kumuambia mambo fulani.

"Baba, ujue mimi nakuamini sana wewe kuliko mtu mwingine hapa"

Mzee huyo aliona kuwa mtoto wake kweli kala nyama ya mkewe na inamfanya asahau kila kitu

"Mwanangu kweli kabisa"

"Lakini baba kuna mzee mmoja mchawi sana tena simpendi kiukweli nimemsikia wakimsifia kuwa mzuri anasaidia yani natamani nimuue ili sifa upewe wewe baba yangu"

"Anaitwa nani huyo kwani" Aliuliza mzee huyo bila kujua kama anategwa

"Anaitwa naniiiiii ehee anaitwa UPENGO....upengoooo"

Jina hilo lilikuwa kama linazibua masikio yake pindi likitajwa

"Huyo kumbe hata mimi namsikiaga" " Sasa anakaa wapi, huyu mzee bhana mana kila sifa anachukua yeye alafu wewe hupewi sifa wakati unayafanya mazuri hapa"

"Mwanagu ila si mtu wa kumchezea kabisa anaishi kijiji kimoja hivi kinaitwa MIPINGONI huyu mtu kweli ni mchawi wa kutupiliwa mbali"

"Ahaaa kumbe sasa si unajua mimi nimechaguliwa kwenda kijiji cha Kalulu nikirudi tu nakuja na tunapanga jinsi ya kummaliza huyu mzee sawa baba!".

Bwana Chito alimdanganya baba yake kutokana na udhaifu ambao huwa anamjua kuwa anaudhaifu gani na akapata jina la sahihi la mahali ambapo anaishi huyo mzee.

BAMUZI alionekana akiwa na LYOTO huku Bamuzi akimshika Lyoto begani na kumtembeza kwenye uwanja ambao ulikuwa maalumu kwa ajili ya mazoezi ya kurusha mishale kwa vijana ambao wanafundishwa mapigano. Hakika walionekana kupendezwa na kila mmoja akiwa na furaha kubwa sana. Lyoto alikuwa na kumbukumbu chache sana kutokana na msukumo wa maji na kusafirishwa umbali mrefu sana, walikuwa wanaenda lakini Lyoto alisimama na kumuangalia kwa makini sana kijana Bamuzi.

"Mke wangu najua huwezi kunijua vyema kwa sasa mimi ni mumeo na utanijua zaidi endapo dawa mwilini mwako zikifanya kazi." Alimtoa wasiwasi binti aliyeonekana kuwa mzuri sana pale kijijini Chamlo zaidi ya Mrembo NAOMI. Wakati wanacheka na kufurahi huku pembeni wakiwa wanawake wale ambao wanamhudumia kama malkia wa pale kwani siku chache tu zijazo hawa wanawekwa kuwa Viongozi rasmi.

Naomi aliona wivu sana baada ya kumuona Bamuzi akila penzi zito lenye bashasha ndani yake lisilokuwa na uchafu wa hasidi na fitina, penzi ambalo wazungu wanatumia neno quality yani safi zaidi. Naomi binti wa mama Naomi aliona wivu uliojaa chuki na ndipo akaelekea nyumbani kwake kwa mama yake kama kawaida. (Mtoto kwa Mama).

"Mama hivi tangu tuende kwa mzee Ukelele mpaka leo bado haonekani atakuwa kafanya kweli yule maana naona Bamuzi na kile kisichana kake wananifanyia makusudi"

Mama huyo alimuangalia sana mwanae huku akimuonea huruma sana ndipo akamueleza kuwa "Mwanangu usijali yule mzee namuamini sana ".

Naomi aliondoka na kukutna na wanawake wenzake ambao walikuwa na mawazo kama ya kwake "Eti hivi huyu mwanamke ambae kamchukua Bamuzi akajifanya eti sisi hatuoni yani eheee..."

"Naomi yani mimi nahisi kuwa siku moja tuongee na yule msichana ambae kaka yake ZWELI alitangazwa kuwa kafa baada ya kwenda kule msituni najua atatusaidia sana".

"Mh mwenzangu kweli una mawazo makubwa sana sikufahamu hilo tutakalolifanya ni kuwa tunamdanganya kuhusu kaka yake Zweli kuwa kauliwa ili afanywe sadaka huko, ili wapate ile dawa ndio maana waliporudi wakatudanganya "

Naomi aliusuka uongo uliofanana na ukweli ili kuwakosanisha Bamuzi pamoja na Lyoto.

"Yaaaa hapo najua atakasirika na atafanya kile ambacho tunakitaka eti...kwanza najua leo atakuwa kwake twende kwanza"

Waliondoka kuelekea kwenye familia ya bwana Zweli kijana aliyejitolea kufa kwa ajili ya Kiongozi wake apate ile dawa ya kumtibia mchumba yake. Walipofika walimkuta ndipo wakamuomba mama yake Zweli yani huyo binti ili watoke nae kwa muda.

"MWANA, tumekuita hapa kukuambia yale usiyoyajua!" Naomi aliongea.

"yapi hayo?"

"Kwanza unamuonaje yule mwanamke pale unapomtumikia kama hana mikono na miguu". "Paleee yule mwanamke kiukweli anapendwa sana na Bamuzi tena mpaka raha sana alafu anaongea vizuri sio mkorofi".

Naomi aliona njia ya kuingilia hapa itakuwa ngiumu lakini hakukata tamaa alianza kuongea

"Sasa unajua kuwa kaka yako Zweli aliuliwa na Bamuzi ili afanywe sadaka ya kupata dawa ambayo itaenda kumtibia yule mwanamke ambae mnamtumikia yani mimi mpaka nikaanza kulia sana baada ya kujua hilo yani". Mwana alianza kutoa chozi na huku wakiendelea kumjaza sumu mpaka akatamani kupasuka kwa hasira alizo nazo.

"Sasa naomba utusikilize kwanza, tunachotaka ikiwezekana umuue yule mwanamke na yeye kama alivyosababisha kaka yako kuuliwa sawa?"

"Sawa Naomi pia nashukuru kwa ushauri wako na leo jioni naenda kwenye zamu yangu ya kukaa nae, alafu hapo nifanya ukatili ambao sikuwahi kuufanya katika maisha yangu......"

Walijua kwa njia ile wamefanikisha kutoa mapenzi ya wawili hawa.

Wakati huo Mzee MANUALI na Mzee KELEBU wakiongozwa na mzee NGOLOLO hawa walipanga safari tayari ya kwenda kijiji cha MPOLONI wakiwa na lengo la kutoa pole ya msiba kwa kijana yule aliyejitokeza ba kumsaidia kijana Bamuzi kupata dawa. Safari ilipangwa wazee hawa watatu pamoja na kijana Bamuzi waelekee wakiwa na vijana wa ulinzi wa njiani.

Bamuzi kabla hata ya kwenda alimuita yule mwanamke aliyejulikana kwa jina Mwana "Mwana Nakuacha na huyu mke wangu na unajua hali yake bado haijatengemaa sasa nakuomba sana umtunze nirudi nikute hali yake iko nzuri au iko vilenilivyoacha lakini isirudi nyuma nadhani unanifahamu".

Maneno hayo ya nadhani unanifahamu yalimuongezea uchungu sana binti huyo na kufikilia kuwa kweli Bamuzi kamuua kaka yake kwa ajili ya huyu mwanamke anayepewa amlinde.

Safari ilianza kama kawaida wakielekea kwa Mzee UKELELE ndani ya Kijiji cha MPOLONI kwa lile lengo la kwenda kutoa pole ya msiba wa kijana wake. Huku nyuma sasa binti Mwana anajiuliza kwa jinsi gani ataweza kumdhuru Lyoto aliyekuwa hafahamu chochote. aliamua kumpikia kwanza uji ambao alihitajika kuweka dawa ambayo ingemuwezesha kuwa na nguvu kama kawaida.

Lakini ajabu alichanganya na vitu mbavyo alikuwa anavifahamu yeye mwenyewe kwa lengo kuu la kumuangamiza. alimpelekea, Lyoto lakini hata kabla hajampatia alidondoka na uji wote ukamwagika na kwa purukushani ya kujiokoa ulimfikia mikononi na kumuunguza kiasi Mwana. Hivyo alishindwa kumuandalia mwingine na hatua yake ya kumuangamiza kwa njia hiyo ikagonga mwamba.

Muda wa kumpeleka mazoezini alitumia nguvu kumsukuma mpaka pale lyoto akadondoka na akawa analalama kwa maumivu, mlinzi mmoja aliayaona hayo yote ndipo alipomuendea na kumuonya " Mwana tabia yako imebadilika kwani huna huruma na mke wa mfalme wako, unadhani hasira zako zitakupeleka wapi?"

"Hapana kabisa hawa wauwaji wamemuua kaka yangu kwa ajili ya huyu kinyago sasa ni bora na yeye afe"

Wakati huo sasa binti huyo alishika mtii mkubwa ambao alidhamilia kumpiga na kumuua kabisa apotee duniani, wakati huo Naomi na mwenzake wakisubiria majibu.

"Hapana haya ubayoyafanya naamini kaka yako huko aliko atakuwa anaumia sana kwani yeye alijitoa kwa ajili ya kumsaidia mfalme wako na akajitpoa muhanga, lakini hayo maneno uliyopandikiziwa na wenye chuki utakuja kujutia pale tu ukiufahamu ukweli na wao wakakucheka kwa akili potofu uliyo nayo"

Mlinzi huyo alitumia kauli nyepesi na nzuri sana ili kumuelimisha binti huyo aliyekuwa akimsogelea Lyoto ili ammalize wakati huo lyoto hana nguvu alikuwa anatoa machozi tu.

"Mwanaaaa achaaa nitakupiga na mkuki kabla hata hujamgusa huyo mwanamke pia nakuonya usipige hatua hata moja kumsogelea hufai kabisa na nakuahidi kukulipoti pindi Bamuzi akifika mnyama mkubwa wewe unasikiliza utumbo wa watu wasiojua hata majina yao yana manisha nini tokaaaaa......."

Binti huyo alipigwa na butwaa ndipo mlinzi huyo alimkamata na kwenda kumuweka ndani ya selo ya wale watia vurugu na akamuita mwanamke mwingine kwa ajili ya kuendelea na huduma kwa Lyoto.

Wazee hao walifika hadi kwa mzee Ukelele na walishukuru sana baada ya kumkuta akiwa pale kwake. Walikaribishwa na Mzee huyo alijawa na furaha kubwa sana baada ya kutembelewa na mkuu wa kijiji cha cha Chamlo hakika kwake ulikuwa ni ujio mkubwa sana yani.

"Jamani karibuni sana hapa ndio nyumbani na elezeni shida yeyote mimi kama nitaiweza nitawasaidia."

"Kwanza tunashukuru kama unavyoona ujio huu si wa kukaa sana tunarudi leoleo hata kama usiku mfano wa baba kaja huku kule mtoto ata lala na njaaa".

Maneno ya mzee Manuali hayo yaliwafanya kucheka wote kwa pamoja.

"Sasa Bwana Ukelele hapa tumekuja kutoa pole kwanza " Mzee ukelele alishangaa

"Pole gani tena jamani mbona sielewi"

"Kuna kijana ambae ulimtuma aje pale nyumbani kwangu na nimuelekeze kwenye ule msitu sasa alikutana na huyu kijana wa mfalme bwana Bamuzi sasa wakati wanarudi kwa bahati mbaya hawakumuona kwa nyuma ndio maana tukajua yaliyotokea kule atakuwa kakamatwa, kilichotufanya tuje huku kutokana na msaada wake kumsaidia huyu kijana ndio maana tukaja kutoa pole...."

Mzee huyo alifikilia jambo na kujisemea ndani ya nafsi yake 'Hawa itakuwa wanamtafuta yule kijana Katunje na nikiwapa taarifa kamili watamfanya mtoto wangu MWAIJA kukosa mtu wakuishi nae baada ya mimi kufariki hapana tena afadhali walivyoondoka'. Yalikuwa ni mafikilio ya mzee huyo.

"Mzee mbona huongei?" aliuliza Mfalme

"Itakuwa anafikilia maumivu ya kufiwa unajua kweli inauma sana mfalme wetu" Aliongezea Mzee KELEBU. Baada ya dakika kadhaa ndipo mzee Ukelele akaona la kusema

"Jamani mnanikumbusha niliyokwisha yasahau, kwani taarifa nilizipata hata kabla hamjaja, kwani kweli kaliwa kabisa na pia sasa hivi nimepoa kabisa msijali na nawashukuru kwa kuja kunipa pole."

Waliagana kwa pamoja kisha wale wazee pamoja na Bamuzi waliondoka kurudi kijiji cha Chamlo kuendelea na mabo mengine muhimu ya maendeleo.



Bwana Sikujua na Mapato walikutana baada ya Mapato kuwa na wasiwasi mkubwa sana wa maisha yake kwani alimfuata jamaa yake huyo ili kapate kumueleza kitu muhimu sana ambacho alihisi kinamtatiza, lakini hata bwana Sikujua nae alijiuliza kipi ambacho kinamsikitisha bwana Mapato aliishia kumtazama tu kwani hakujua nini amsaidie

"Bwana sikujua kuna tatizo hapa ambalo kiukweli nahisi maisha yangu yanaelekea kuwa mwisho"

Alisema bwana Mapato,

"Ehee kivipi tena maana hata ulivyokuja ulionekana kuwa na jambo ndio maana hata mimi umeniona nikiwa na wasiwasi sana".

"Kiukweli usiku nimelala lakini nikiwa usingizini niliota ndoto mbaya sana kabisa"

Alisema bwana Mapato huku akishika tama. "Yani usiniambie bwana weee ilikuwaje hiyo ndoto?"

"Yani nilikuwa natembea barabarani, sasa nikamkuta Sikitu..."

"Sikitu tena kwenye ndoto eheee....!"

"Sasa....baada ya kuonana na huyu binti akanijia karibu alafu akaniambia na wewe nitakuua kwa mkono wangu mimi mwenyewe kama nilivyomuua rafiki yako Sikujua...."

Hapo bwana sikujua hakuamini alitamani kukimbia kabisa pale alipo "Aaaah hakuna bwana sitaki kabisa swala hilo maana haiwezekani mtu aliyekufa hawezi kunielezea mimi kuwa kaniua bwana....''

Alilalama sana bwana sikujua huku akitokwa na jasho la ghafla maana swala la kuambiwa kuwa Mapato atauliwa kama alivyouliwa yeye lilikuwa swala gumu sana kwake kukubaliana na hilo.

"Hapa cha kufanya si kupaniki maana hapakuwa na swala la kuzunguka sana na kulaumiana zaidi ya hapo ni kuweza kujua nini tunafanya ili kujua majawabu yake".

Alinywea kabisa bwana Sikujua na akakaa chini huku akihemwa na mwili wake ukitokwa na jasho. waliongozana wote kwa pamoja lakini bwana Mapato akaona kuna sababu ambayo inawezekana inapelekea yeye kuota zile ndoto za ajabu ajabu "Lakini bwana sikujua unalionaje swala hili la kumpata bwana Chito maana nahisi ndio sababu ya kutokea haya"

"Alafu inawezekana kuwa na ukweli kabisa"

"Unajua kwa nini inatubidi kumtafuta huyu kijana anayejulikana kwa jina la KATUNJE alafu mwingine aelekee kijiji cha Shishimo, sasa itakubidi wewe uende huko kijiji cha Kilimalondo alafu mimi niende kule kwa Chito na inatubidi tufanye haraka sana na hili sio swala la kumueleza mtu yeyote kabisa hata mwenyekiti". "Sasa kwa nini tusimshilikishe mwenyekiti maana kwa jambo kama hili tufanye huku tukijificha kwenye mgongo wa mwenyekiti".http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Mapato aliona sasa ni swala ambalo lipo na linahitajika kufanyika,

Wakati wapo njiani walikutana na bwana Manuali akiwa na Susu, wakiwa wanaongea mambo ambayo hayakujulikana kwani walikuwa wanaongea kwa sauti ya chini na ilikuwa inaonekana wanaelekea njia ya mzee manyenye. Walijiuliza kwa nini na wanaelekea kufanya nini kule.

"Mapato unahisi, kuwa watakuwa wanaelekea wapi?" aliuliza sikujua

"Mh! hata mimi sifahamu kabisa, alafu kwani mbona kimya sana si alisema kuwa siku kadhaa anasema wale ambao wamemkamata na wakamsababishia yale mambo sasa mbona kimya mpaka sasa"

"Inawezekana mana lile swala ambalo tumekwenda kuliongea kwa mwenyekiti limebana kabisa njia zote sasa hapa tufanye kweli nenda Kilimalondo mimi naelekea Shishimo sawa!".

safari ambayo iliandaliwa kwa upande wa bwana Sikujua ilikuwa na madhumuni ya kwenda kuhakikisha kuwa wanampata kijana Katunje na bwana Mapato alirudi tena ndani ya kijiji cha Shishimo ili kuhakikisha anafanikisha pale ambapo alipaacha.

Kwanza kabla ya yote waliamua kwenda kwa mwenyekiti ili kumueleza kuhusiana na safari yao hiyo ina dhamira gani kwao na hata kijiji chao cha Bwawani.

"Mwenyekiti nakuomba sana kuna jambo ambalo tunahitaji msaada wako kwetu"

Sikujua alisema kumuambia mwenyekiti

"Ehee lipi hilo ambalo mnahitaji niwasaidie jamani". "Yani hapa tumeona kujitolea kwenda kuhakikisha bwana Chito ambae anajulikana kwa jina la Mambo sasa nakwenda kuhakikisha kumleta hapa na huyu mwenzangu atahitajika kwenda kijiji cha Kilimalondo kwa ajili ya kumuona bwana Katunje na tutakapokuja hapa tunawaleta ili waje kujibia mashitaka yao".

Mwenyekiti aliwaza kwa muda kidogo alafu akavuta pumzi ndefu kisha akashusha alafu akawaangalia na kuwaeleza kile ambacho anakihisi kama ni kizuri kutokana na maelezo yao.

"Sasa kwanza nashukuru sana kwani sikufikilia kama mtatokea watu kama nyinyi na kutaka kusaidia kutokomeza matatizo kama haya kwangu hakuna wasiwasi kinachotakiwa tuwaeleze wanakijiji alafu tuwaeleze...."

"....Aaaaahaaa hapanaaa kabisa utaaribu kabisa endapo ukiwaambia wanakijiji "

"Kwa nini wakati ni jambo zuri...." alishangaa mwenyekiti

"ndio kwa sababu jua kiuwa miongoni mwa wanakijiji haohao wapo ambao ni wako pamoja na bwana huyu sasa akipata taarifa hiyo watakwenda kumpa na atakimbia"

Mwenyekiti aliwakubali sana kwa hatua moja hadi nyingine kutokana na maneno ambayo walikuwa wanaongea.

Hatimae walikubaliana na wakapewa kiasi cha fedha kwa ajili ya kujikimu ndani ya safari yao.

Kwa upande wa bwana Sikujua siku ya pili yake alifika ndani ya kijiji cha Kilimalondo mzee huyu ana sifa moja ambayo huwa anayo, kwanza huwa ni mcheshi sana pia mjanja kupiliza, Lakini ni mtu ambae hana huruma kabisa pindi pale unapomkera kwenye mambo ambayo anahisi kuwa yatamharibia maisha yake kama tulivyoona mzee Mambo sasa kipindi yupo bwawani aligombana nae hakuishia hapo akamteka kiakili kijana susu na kumfanya apindue ushahidi na akafanikiwa pia akasababisha matatizo kwa binti Sikitu, baada ya kumbaka na kumtupa porini, hakuishia hapo alisababisha mauti kwa mama Mengi kwa kuficha zile siri ambazo alikuwa nazo mama huyo.

Hapa sasa anaagizwa na rafiki yake kwenda kuhakikisha uwepo wa kijana mmoja Katunje.

Alikuta kijiji kipo kimya kabisa hapakuwa na patashika za hapa na pale aliweza kushangaa kabisa mana si kawaida pindi unapokwenda kijiji chochote lazima uhisi uwepo wa watu lakini hapo ilikuwa tofauti kabisa. 'Ina maana hapa kijijini hapana watu au sijafika kabisa'

Wakati huo anaonekana kijana Katunje akitoka kwenye nyumba yake hapo ndipo anakutana na bwana Sikujua lakini sikujua alikuwa anashangaa tu pindi anapouona mlango umefunguliwa na kurudishwa bila kumuona mwenyewe. 'Mh! hapa panaonekana kuwa na hatari mana uchawi njenje kabisa haya mlango kufunguliwa na unafungwa bila mtu kuonekana haya tangu lini'

Alipata kujiuliza maswali baada ya kuona ile hali. Katunje hakuwa na habari kabisa na mgeni huyo maana hali aliyokuwa nayo ilizidi kumpa wasiwasi sana alielekea kwa njia ya kwenda kwa mzee Kauzibe, alitembea moja kwa moja maana alikuwa na lengo moja tu alifika na kwa bahati nzuri aliweza kumkuta akiwa na mzee udevu ndipo katunje alinyemelea na kukaa pembeni yao akiwasikiliza nini wanachokiongea.

"Sasa, unadhani tunafanyaje maana tangu juzi kile kipigo haki ya nani sijui hata nifanye nini"

"Lakini sijajua kuwa huyu kijana anatumia nini maana si kwa hali ile na naamini atatumia njia nyingi sana kufanya yale anayoyataka">

"Sawa lakini, hivi nilisikia kipindi kile kuwa kuna binti ambae alikuja nae na wewe ndie ulikuwa mganga wake ukamtibu mpaka akapona sasa sijajua mmegombana wapi yani"

Maneno hayo aliyaongea bwana Udevu kumuuliza bwana Kauzibe. "ni kweli lakini bwana ilikuwa ni ajali kubwa sana kwanza si unamjua bwana Swai anapenda vibinti kama umri wa yule na mimi ndie alinipa nafasi ya kumtafutia ndio maana nikajitahidi sana kumfanyia matibabu yote mpaka akapona kwa lengo la baadae nimpelekee bwana Swai...."

"Eheeee ikawaje......?"

"Daaah ndugu yangu siku nilivyogundua kuwa wanaishi polini ndipo na mimi nikaangaika kupatafuta sana hatimae nikapafahamu ndipo nikatafuta njia ya kuingia pale jambo zuri lilikuwa ni pale ambapo Katunje alitoka hayo maeneo na mimi nikaenda kule......alinigundua kuwa naenda kwa nia mbaya ndipo tukaanza kukimbizana mpaka anafika kwenye lile korongo la maji daaah akaangukia mule na akafa kabisa...."

Hayo maneno ambayo alikuwa anayaongea bwana Kauzibe alijimwaga huku akiwa hafahamu kuwa bwana Katunje anayasikia yote na alikuwa na hasira sana kuzidi mpaka.

"Alafu mtu kama yule inabidi ushike ile sehemu ambayo anaitegemea kwa Katunje kumzibidi ni jambo dogfo sana tunamkamata yule binti anayeishi nae alafu atajitokeza tu...."

Mala wanahisi pumzi zikihema kwa kasi maeneo yale waliyokuwepo "Mh! mbona kama kuna mtu mwingine karibu yetu hapa" "kweli au....."

kabla hata ajamalizia aliipata ngumi ya uso na palepale akawashika kwa pamoja na kuanza kuwashikisha adabu huku akiwaomba waeleze wapi wamemtupa binti LYOTO maana yeye ndio maisha yake yatakuwa vyema akimuona binti huyo tofauti na hapo hapakuwa na njia nyingine.

wakiwa katika harakati hizo huku nyumbani anaonekana bwana Sikujua akiodika kwenye nyumba ile ambayo alikuwa na wasiwasi nayo pale mwanzo.

"...hodiiiii....hodiiiiiiii wenyeweee"

"Kaaribuuuuu....."

Sauti ya kike ilisikika na ndipo akatokea mwaija, hakika alishangaa sana baada ya kumuona mgeni ambae hamfahamu kabisa pale, "karibu nikusaidie nini mgeni?"

"Ahsante sijui hapa ndipo kwa bwana Katunje?" Sikujua aliuliza ili apate uhakika kama si pale basi aelekezwe na huyohuyo.

"Ndio nikusaidie nini....." Mwaija aliuliza huku akionyesha dalili za kutaka kuingia ndani na kufunga mlango "Kwanza mimi nimekuja kutoa taarifa kubwa muhimu sana akija mwambie kaka yake anamtafuta anayeitwa CHITO na akitaka kumpata aje anitafute mimi kwenye kijiji cha BWAWANI kule ambako alikuja kwa mara ya kwanza aniulizie mimi naitwa mzee Sikujua akinipata hata ndugu yake atampata....."

Baada ya kutoa taarifa hiyo mzee huyo aliondoka kuanza kutafuta njia ya kwenda kwao Bwawani. Aliamini kabisa baada ya kumpa taarifa ile basi njia rahisi sana yeye kumpata kwani jinsi anavyompenda kaka yake hatakuwa na ujanja.

kweli kijana Katunje baada ya kuwashikisha adabu wale wazee na haikujulikana kawafanya nini huko waliko alirudi nyumbani na kawaida yake ni kupiga mluzi wa aina yake ili mwaija afahamu kuwa katunje anarejea na yeye mwaija hutoka nje na kusimama akisubiria kukumbatiwa kwani hamuoni zaidi ya kuhisi kuwa kashikwa na mtu na maongezi tu basi.

Baada ya kuhakikisha kuwa ametulia ilimbidi Mwaija autue mzigo na kumuambia Katunje yale yote ambayo kaagizwa aseme kwake.

"Nina maswali kabla sijakupa ujumbe wako" Alisema Mwaija "Haya niulize na nitakujibu pia kabla ya hayo nina hoja kwanza nataka kukuambia"

"Hapana mimi ndio wa kwanza ngoja nikuulize ndipo utaongea hoja yako" walikubaliana na ndipo katunje akawa tayari kujibu kwa kile ambacho atakuwa analielewa.

"Wewe huko kwenu baba na mama yako wazima?"

"Nilimuacha baba yangu pamoja na kaka yangu akiwa na mkewe,"

"Sasa hivi wako wapi hao uliowaacha....?"

"Kwa sasa sijui kabisa kwani nilikuwa wa kwanza kabisa kuondoka pale baada ya baba yangu kumuua mama yangu ili awe mchawi mkubwa pia niliondoka mpaka sasa hivi japo niliwahi kupita maeneo ya kijijini kwetu nikaulizia kaka yangu nikaambiwa kaama na yeye miaka mingi iliyopita"

"Eheee ulifanya juhudi gani kumtafuta kaka yako....na anaitwa nani huyo kaka yako?"

".....Mh! leo umeniamulia....kaka yangu anaitwa CHITO na mkewe anaitwa Nyamali juhudi za mwisho ziliishia kijiji cha Bwawani ambapo mwenyekiti alinifukuza na nikaondoka ila ikawa ndio chanzo cha kumpata binti Lyoto....ukweli ni stori ndefu na ndie yeye aliyenikutanisha na wewe"

Katunje wakati anajibu maswali alionekana kama kulia.

"Nyamaza basi kuna mzee mmoja hapa anaitwa Sikuja alikuja hapa sijui kama unamfahamu?"

"Sikujuaaa.... nahisi sijui ndio yule ambae nilimuacha hapo nje wakati mimi naelekea kwa mzee Kauzibe....ila simfahamu kwa hilo jina hata sura"

"Haya alikuja hapa akauliza hapa ndipo kwa katunje nikamjibu ndio akasema kuwa akija muambie kuwa anatafutwa na ndugu yake ndani ya kijiji cha Bwawani na akija aulizie mtu anayeitwa Sikujua hapo atampata ndugu yako Chito...."

hakika Katunje alishukuru sana baada ya kupata taarifa hiyo huku akijisemea kuwa kumbe kaka yangu ni mzima wa afya kabisa nilijua siku moja tutakuja kuonana.

Alipewa nafasi ya kuongea na ili mwaija amsikilize.

"Sasa nilitaka uelekee nyumbani kwa baba yako mimi niaelekea huko kijijini kisirisiri kwanza kusaka kila kona ya kijiji kwani sasa hivi hawatoniona ndipo nitamkuta kabisa kaka yangu kama yupo na kama hayupo basi nitamuulizia huyo mzee ili aniambie.

Walipanga hivyo na mwaija akenda kwa baba yake na huku kijana katunje akaondoka kuelekea kwa mzee sikujua.

Upande wa mzee Mapato alishangaa sana baada ya kufika kwa mwenyekiti Masanja anapewa taarifa ya kifo chake alilalamika sana, lakini aliweza kupewa nafasi ya kuishi pale kwa muda.

Chito na yeye kwa jana yake alijiandaa kuondoka bila kusahau kabisa ile bangili ambayo aliamini kama ni ile ya mkewe akiwa na lengo la kwenda kwa mzee Upengo ili akamuulize baadhi ya vitu fulani, hatimae safari ilianza na yeye akiwa pamoja na baadhi ya vijana kadhaa ambao walifuatana ili kwenda kwenye kijiji cha Kalulu, Chito alitembea huku akiwa na mawazo ya kutaka kujua anaanzia wapi kwenda kwa mzee huyo Upengo hali ya kuwa hata klijiji cha Mipingoni hapafahamu anapitia wapi na anaingilia wapi.

Ilimbidi aweze kuuliza kwa wale ambao wapo nae safari moja kabla ya kuwauliza aliwataka wamalize kwanza mada ambayo walikuwa wanaiongelea lakini haikuwa nyingine zaidi ya ile ambayo wanaenda nayo kule "Kiukweli hii si nzuri kabisa haiwezekani kabisa mtu anakuja kukusalimia alafu ukizingatiia kuwa wote ni marafiki huku tuendako tutajua la kufanya mpaka aelewe">

Japo wapo kwenye harakati za kwenda huko lakini bwana Chito alikumbuka kuwa huko ndiko iliko familia ya Mama Sikitu sasa wakati anaelekea huko itambidi awe makini sana akiwa huko.

"Jamani naombeni mnisikilize kwanza...." aliwaomba wamsikilize "Haya mzee tunakusikiliza kwani wewe ndio mkubwa wa hii safari"

"Ninaomba kuuliza huku tunakokwenda ninawezaje kukipata kijiji cha mipingoni...." Baada ya kuuliza lile swali kila mmoja wao alimuangalia mwenzake kana kwamba wanaulizana baina yao. Ndipo kijana mmoja akajitokeza na akamuelekeza kuwa anapafahamu njia ambayo inapitia kwenda huko ila kwa bahati mbaya hakuwahi kwenda kabisa, Lakini kwa maneno hayo yalimpa faraja kubwa sana bwana Chito akiwa na imani kuwa aliko mtu siku zote hapotei atafanya kila juhudi ili afike huko.

"jamani nina jambo jingine nahitaji mnisaidie huku tunakokwenda mnaweza kurudi peke yenu pindi mkiachwa?"

Aliwauliza ili ajue kama akiwaacha na yeye akaelekea huko je? wataweza kurudi salama wote?

"Huku mimi napajua vyema sana hatuwezi kupotea kabisa yani na tutarudi wote kwa salama usalimini"

Safari ilizidi kuwa tamu kipindi kile jua sasa limetua na kuuanza usiku taratibu, wakati wanakaribia usiku huo na kijiji kwa mbali wanakiona kwani taa zilikuwa zinaendelea kuonyesha njia ya pale walipo. Kila mmoja alifurahi sana moyoni mwake baada ya kupata matumaini ya kupajua pale wanapokwenda kuwa wanakaribia, Waliona vyema wapumzike mahala ili asubuhi waamkie kule kijijini kabisa. Wazo alilitoa Mzee huyo Chito ambae alikuwa na nia yake ya kutimiza nia yake ya kuwaacha na yeye akatokomea kupatafuta huko kwa mzee Upengo.

Kila mmoja hakuwa na wasiwasi wa kutorokwa na hata mawazo ya kuwa mmoja wao atakimbia pale. Majira machache baada ya watu kulala fofofo kabisa.

Chito hakusubiri hata sekunde japo na umri wake wa uzee kumuanza japo sio sana lakini alikuwa na nguvu zake, alinyanyuka na kuwaangalia wale wote akahakikisha kuwa wamelala ndipo na yeye akatafuta njia ya kuongoza katikati ya kijiji kile cha Kalulu, ilikuwa mwendo kama wa nusu saa hivi alifika na ukizingatia i usiku alafu hakuna anayemfahamu zaidi kwa mzee Uwesu ambae ni ngumu pia kwenda kwani bado hana uhakika wa wao kumpokea bila kuulizwa mbona umekuja peke yako mtoto wetu yuko wapi?

Aliamua kukatisha katikati ya kijiji na kwa jinsi alivyo hakuwezekana kuonwa vyema na kujulikana na yeyote yule.

Kwa bahati nzuri alimkuta mmoja wa kijana akiwa na baiskeli akiwa anaelekea mahali lakini alionekana kuhemwa kama anayetokea mbali sana.

"Ndugu samahani kwanza bwana...unaweza kunisaidia kuna mahala napatafuta kijiji kimoja kinaitwa Mipingoni sijui kama unapafahamu?"

Aliuliza Bwana Chito.

"Oooh! tena kwa bahati nzuri sana kuwa mimi mwenyewe naelekea huko huko, kama hautojali twende alafu nitakuacha huko ukifika" Mzee Chito alihofia ile safari lakini alishukuru kwa kuwa safari yake imefupishwa sana.

"Lakini hatutofika usiku huko?"

"Hapana yani mwendo mchache sana hapa tunafika ". Waliondoka kwa pamoja huku wakiendelea kupashana habari na kuulizana baadhi ya maswali ambayo ilionyesha ishara ya kuhitaji kujuana zaidi. "Mimi naitwa Chito naishi pale Shishimo...."

"Sawa mimi naishi Chamlo, nafanya kazi kwenye himaya ya mfalme Ngololo sasa nimekuja huku kwa ajili ya kutafuta habari za nje ya kijiji chetu ili na sisi tujulinde kwa kile kipindi cha shida kutokea....."

"Chamlo....nakisiki hiko kijiji kipo mbali sana yani"

Kwa bahati nzuri sana wanafika na Bwana Chito aliweza kuachwa mahali na yule jamaa aliondoka zake, Giza llilikuwa kubwa sana na watu walikuwa wamelala na yeye ilimbidi atafute nyumba ambayo ina sehemu safi ya kujihifadhi, Alianza kuupata usingizi wa mang`amung`amu kutokana na mazingira kwake kuwa mageni kabisa yalikuwa hayaeleweki.

Upande wa bwana Mapato na yeye alipofika kwa mke wa Masanja ambae ni marehemu na kupewa ile habari hakika alijifanya kuchanganyikiwa sana, alipewa nafasi ya kulala huku akiwa na nia ya kwenda kwa Chito kwao ili akaongee na Chito amshawishi arudi nyumbani Bwawani ili amkutanishe na ndugu yake Katunje ambae mwenye jukumu la kumleta ni Sikujua na kama tulivyosoma kuwa Katun je alikubali kuja lakini ataanza kuchunguza uwepo wa kaka yake na asipofanikisha kumuona ndipo atakubali kumtafuta sikujua ili aongee nae.

Mapato bila hata kujua usiku huohuo kwa kuwa ndani ya kijiji cha Shishimo wengi walichangamka sana hivyoi ngoma za kiasili zilikuwa kawaida kwa kila siku.

Aliondoka usiku huo baada ya kuufunga mlango wake taratibu ili asijulikane nini anafanya na wapi anakwenda. Mzee Mambo sasa na rafiki yake Nyandu usiku huohuo ujio wa bwana Mapato waliupata na hawakutaka kuchelewa kwani walimtambua ni mtu wa aina gani.

"Nyandu yule mtu ambae anatufuatilia anatoka kwenye kile kijiji cha SONGAMBELE ambacho siku hizi kinaitwa Bwawani kaja tena baada ya kumuacha kwa mara ya kwanza...."

Alisema mzee Mambo sasa.

"Sasa yeye kaja kusema nini au kafuata nini na kamfuata nani?"

"Ukweli kaja na gia ya kumfuata mwanagu ambae kwa sasa hayupo, ingawaje anaweza kurudi kwa siku mbili hizi karibuni...."

"Sawa inatakiwa kumkamata alafu atueleze kwa makini sana kama kuna jambo anajivunia lazima atupatie....kwanza nenda kamjaribu kama kakomaa"

Nyandu alimueleza mwenzake kuwa aende kumjaribu kama kakomaa yani kama ana dawa za kujikinga basi wajue ili waone wanamzibidi au kumuendea vipi. Baba yake Chito alikwenda haraka nyumbani kwake na kuweza kulifanya jambo, wakati huohuo ndugu bwana Mapato hana hili wala lile alikusanya miguu yake na kuielekeza kwenye njia iendako kwa bwana Chito, alishangaa sana baada ya kufika kwenye uwanja wa bwna Chito alikuta kuna moshi mkubwa sana....ukifuka kutoka ndani, alijua labda kuna moto unaunguza nyumba alikimbia haraka hadi pale mlangoni laaa haulaaaaa!....bwana chito haikuwa bahati yake alisikia vicheko vya dharau sana

Haa ha ha haaaa.... Haa ha ha haahaaahaaa!.. baada ya hapo pakawa kimya aligeuka nyuma kutaka kukimbia alichelewa alijikuta anaingia kwenye mikono ya watu wenye uchu wa nyama.

Alikamatwa na kuingizwa ndani kwa mzee mambo sasa akiwa hajitambui.

Mzee chito aliendelea kulala kwenye ile nyumba kwa nje japo kwa mawenge mpaka pale usingizi ulivyomchukua ki urahisi. Majira ya asubuhi wale vijana ambao walikuwa pamoja na Chito walipoamka wakajikuta wako wao bila kuwepo mwenzao ambae ni mzee Chito. Kila mmoja alishangaa kivyake na kujiuliza wapi kaelekea. Mwishowe ile kauli ya kusema yeye kuwa anaulizia kijiji cha jirani na kuuliza kama atawaacha peke yao kama wataweza kurudi walihisi kuwa kaelekea huko.

Wao walisonga hadi kwa mwenyekiti wa kile kijiji. walieleleza shida ambayo imetokea hadi mwisho na kwa ustarabu tu mzee huyo aliwaelewa na akawaomba warejeshe majibu kuwa ataomba kukaa na wazee wa hapo kijijini na yeye atakuja kisha watajilijadili ili ajulikane nani ambae alifanya hivyo, pia akasisitiza kuwa waje kutoa taarifa kuwa mzee uwesu sasa kaamua kuchukua maamuzi magumu juu ya mwanae litakalompata yeyote kati yao baba na mtoto atalijua yeye mwenyewe.

Wale vijana walirudi.

Bwana chito katika pitapita yake alifanikiwa kupelekwa kwa mzee Upengo na akafanikiwa kuonana nae ana kwa ana. Walikaa chini na chito akaanza kueleza nini kafuata kule.

"Baba...samahani sana kuja kote huku nimepata taarifa yako kuwa wewe mzuri sana katika swala la kuwakomesha wachawi....sasa mimi baba yangu ni mchawi sana na sitaki aendelee kufanya ile kazi naomba unisaidie sana".

Mzee huyo aliangalia kwenye kibuyu chake na kumuonyesha

"Baba yako ni huyu hapa?"

"Ndio huyuhuyu kabisa" Alijibu Chito

"Sasa huyu nilishamtia adabu kwani mwanzo alikuwa mkali sana huyo anayeshirikiana nae anaitwa Nyandu...nyandu alikuwa mwanafunzi wa Baba yako yani baba yako alikuwa mkuu baada ya mzimu wao wa Nyamnyena....sasa alikuwa anamfundisha huyu rafiki yake..nilipata taarifa hiyo miaka mingi iliyopita nikaja pale na kumdhibiti yani kumfunga kwa miaka kadhaa asijihusishe na mambo haya...ilisaidia na ndipo nikamtoa na uchawi kabisa...lakini juhudi za rafiki yako hakika zinamfanya kurudi kule japo hatakuwa kama mwanzo....pia huyu baba yako ni mtu mzuri sana ila tamaa na marafiki wanaomshauri vibaya"

Chito alishtuka sana lakini aliendelea kuuliza maswali na kumsikiliza kwa makini.

"Sasa kuna siku nilikuuta hii bangili kwwnye chumba cha baba na hii ni ya mke wangu...." aliitoa na kumkabidhi

"Hapana kabisa...hii si ya mkeo kabisaaaa"

"Bali ni ya nani?"

"Hii ni bangili ya marehemu mama yako....na kwa kukuhakikishia aliyetengeneza bangili hii ndio yule ambae katengeneza bangili ya mkeo...na kuhusu swala la mkeo sijajua mpaka uhakikishe unaipata bangili ile ya mkeo ndipo unaweza kuifanyia kazi na ukajua mkeo yuko wapi mpaka sasa hivi....Lakini nikuulize swali?"

"Niulize baba ...."

"Hakuna siku ambayo ulikula nyama ambayo mlikuwa wewe na ndugu yako....pamoja na baba yako baada ya mama yenu kufa?" Chito alifikilia kwa umakini ili apate kumbukumbu sahhi

"Nakumbuka sana kwani baada ya hiyo siku mbele mtafaruku ulitokea pale baada ya mke wangu kukataa kula"

"Safi... basi ile nyama mliyokula ilikuwa ni nyama ya mtu ambae ni....."

'"Babaaa usiniambie kama nilikula nyama ya mama yangu jamani.....mamaaaa nisamehee sikujua kama nilikuwa nakula mwili wako mama...."

Aliendelea kulia sana kwa maumivu makali hata kusikiliza tena hakuweza. Baada ya muda aliendelea

"Lazima nikuambie ukweli upate hasira ya kufanya jambo la kumsaidia baba yako....Juzi napo nadhani kuna nyama ulikula...hiyo sina uhakika sana kama ni ya kawaida ila kachukue ile bangili ili....tukiipata ile na hii ni rahisi kupata mambo mengi sana ambayo yamejificha na ikiwezekana kuwa kufutilia mbali kabisa kwa mambo haya..."

"Sasa naomba unisaidie kuwa tukiachana na mke wangu naomba unieleze kuhusu mtoto wangu na ndugu yangu katunje".

"Mtoto wako anaitwa nani.....na kapotelea kijiji gani" Upengo aliuliza.

"Alipotelea kijiji cha BWAWANI, majira ya jioni wakati sisi tulikwenda kwa mzee Mapato na kisha tukapitia kwa manyenye baada ya kurudi hatukumkuta"

"Sasa nisikilize kwa makini hapa nimeona kuwa mwanao bado mzima na hakika anaishi kwa maisha ya furaha sana lakini hana kumbukumbu ya kukujua wewe ni nani zaidi ya ndugu ya mtu mmoja tu ambae kwa sasa sijamfahamu vyema ni nani na kujua mtoto wako yuko wapi sijafahamu..."

"Hakika mke wangu akirudi na akasikia hii habari atafurahi sana....ila mzee kesho kutwa naimani nakuletea bangili ya mke wangu kwa hali yoyote"

"Sawa safiri salama....sitokupa kinga yoyote katumie nguvu zako za kawaida ukija hapa wakati wa kuuwa haya mambo basi ndipo nitakutengeneza na kuhakikisha kila kitu kinakuwa salama ila msalime baba yako mwambie nitakuja kumsalimia....pia jambo la mwisho hata usiyemzania ndie atakuja kukusaliti"

Chito alipumzika baada ya kuonyesha mahala pa kupumzika ili jioni aianze safari ya kurudi kijijini kwao.

Ndani ya kijiji cha Chamlo, wakati wale viongozi wanarejea wanakuta kwenye moja ya selo kuna mwanamke ambae ni msaidizi wa binti Lyoto. Bamuzi alikuwa na hasira sana alijua kuwa kuna kosa kalifanya alienda kumuangalia mke wake alimkuta akiwa analia lakini hasemi chochote ilibidi aombe afungue mlango wa ile sehemu ambayo yule mwanamke Mwana kafunga na kuanza kuhojiwa. yule mlinzi aliyasema kila kitu na hatimae Bamuzi alitaka kuchukua maamuzi magumu lakini Lyoto alikataa na akasema aachwe hana hatia.

Baada ya siku kadhaa kupita, ndani ya kijiji hiko majira ya mchana wanashtuka upande fulani wa kijiji wanaona nyumba inaungua moto bila hata kuchomwa na mtu. Watu waliangaika sana ili kuokoa lakini kila walipojaribu kumwaga maji ni kama walikuwa wanaongeza moto kukua.

Hatimae kila mahali moto ulionekana kutanda na kijiji kikawa katikati ya moto. Ilikuwa kama laana kwa jinsi walipoiona hapo ndipo mzee Mwalami alitumia nguvu zake za uganga akagundua jambo "Khaaa ili ni aina ya jini kabisa la moto ndio maana linatema moto na kusababisha maafa. Alienda moja kwa moja hadi kwa viongozi wake aliwaonyesha jinsi gani lile jitu lenye sura mbaya linavyohitaji kuangamiza mahali pale.

Bamuzi alipomuona alilijua ni lile ambalo walikutana nae kule msituni wakiwa na lengo la kuchukua dawa na wakakutana ana kwa ana na mmoja wao ambae ni ZWELI akajitoa muhanga ili kunusuru wengine sasa linataka kuja ndani ya kijiji chao kufanya nini.

Wana kijiji wote waliombwa kusimama sehemu moja wasikimbie ovyo kuepusha madhara zaidi. "Jamani huyu kiumbe ndie ambae nilikutana nae kule na ndie ambae alimmeza yule kijana ambae alikuja kutusaidia kule polini." hapo sasa masikio ya watu yakafunguka na hata yule mwana aliona kuwa alikuwa anakosea na wale waliomdanganya walikuwa na nia mbaya kwao na pamoja na Lyoto.

"Lakini mzee Ngololo...inaonekana anashindwa kuingia ndani ya hiki kijiji kwa kuwa kuna nguvu kubwa sana hapa ipo laiti bila hivyo, tungeteketezwa wote sisi...."

"Sasa hiyo nguvu ni ile ya mizimu yertu au" aliuliza bwana Ngololo

"Hapana kwani siioni kabisa yani kwa hili jini limezidi nguvu ila anamilikiwa na nguvu ambayo ipo hapa karibu sana sasa inabidi kufanya haya ....watu wote waje hapa kwani inaonekana nguvu iko hapa...pili wa hapa sisi tusitoke kabisa tusubiri hapahapa....."

"Sasa inatakiwa kuijua hiyo nguvu kama iko kwa mtu basi tujue tunamlinda vipi asitoke inatubidi tuffanye hivyo bwana Mwalami"

Ngololo na bamuzi wakishirikiana na Kelebu walimsii mzee mwalami afanye vile kwa watu waliopo pale kwa mfalme Mzee huyo aliwaomba haraka sana mmoja mmoja atoke wakati huo yeye akiendelea kuangalia kwenye internet yake ya kienyeji au GPRS ya kienyeji.

Alianza Mwana na baadhi ya wafanyakazi wa pale lakini ilionekana hawana kwani nguvu iliendelea kubaki vilevile, akaja Mzee Kelebu nae hapana akafuatia Bamuzi nae hapana akaja mzee Ngololo nae hapana wakashangaa ni nani huyo Bamuzi akaingia ndani na kumchukua Lyoto ili atoke nae nje kwani walimsahau japo baadhi ya wazee pale walianza kumchukia.

Kitendo cha yeye kutoka tu kuelekea kule upande wa moto ambako ulikuwa unaambaa ambaa ajabu zaidi mzee Mwalami akasema Lyoto katunje ndie mwenye hizi nguvu hakika ona hapa inapungua na kule moto unazimika unyewe, hakika ilikuwa ni jambo la ajabu sana kwao.

Naomi alikuwa pale karibu alipolisikia lile jina la Katunje alilikumbuka kuwa ndio yule kijana ambae alikutana nae siku moja na akampenda sana ila jina lake alilisahau. akawa anajiuliza huyu Lyoto na Katunje wana uhusiano gani......http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Waliamua kumtembeza kila eneo ambalo liliathirika na moto wa ajabu ndipo kila anapolisogelea lile eneo hakika moto una zimika kabisa.

Katunje akiwa na hali yake ile ya kutoonekana aliondoka kwenda kijiji cha Bwawani akiwa na imani kuwa kaka yake atakuja kumuona kama alivyoahidiwa na Mzee sikujua bila kujua kuwa anaitiwa pale kwa nia mbaya kabisa alienda mwendo wake wa haraka sana lakini akiwa njiani alishangaa kuona wanyama wanamuangalia na kumkodolea mcho lakini kwa binadamu hawezi kitu kama hiko, alijipa imani kuwa labda yupo vile kwa lengo la kumtafuta ndugu yake na akishamuona labda inaweza kuwa ni dawa kubwa ya kupona.......................



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog