Search This Blog

KARIBU KUZIMU - 3

 






Simulizi : Karibu Kuzimu

Sehemu Ya Tatu (3)





Sulesh alipotoka mkoani Tanga, kata ya Muheza na kijiji cha Mwarera. Kuzungumza na Mzee Mahonge pamoja na Binti Binge, akiwa njiani ghafla gari lake likapotea kimiujiza. Yeye akaja kutokea baharini akatembea hatua kadhaa kwa madaha akionyesha dhahiri kuwa mandhari yale ni mzoefu, akatembea chini ya bahari hadi alipofikia pango kubwa mfano mgodi akazama ndani yake. Ndani kukaonekana tulivu vikaonekana vito vya thamani viking'aa na kuleta mwanga mzuri usoni mwa viumbe ajabu waliokuwepo kwenye pango, walionekana viumbe vya ajabu na vya kutisha. Kama vile viumbe wenye jinsia ya kiume wenye pembe fupi mfano wa Mbuzi na nyuma ya makalio wakiwa na mikia mirefu mfano wa http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Ng'ombe, pia viumbe wenye jinsia ya kike wenye kuvutia sana na muonekano mzuri mfano wa Malaika waliovalia vazi refu mfano wa shela jekundu linalomeremeta. Nywele zao ni ndefu zinafika makalioni na zinang'aa kwa mwanga hafifu mfano wa Mbalamwezi izamapo mawinguni, macho yao yakikutazama yana mwanga mkali mfano wa Paka. Kucha zao sasa usiseme wana kucha ndefu zilizochongoka mfano wa ncha ya mkuki, bila shaka wala kupinga viumbe wale wanaonyesha si binadamu ni majini. Sulesh akuonyesha kuogopa akazidi kuingia ndani ya pango, anaonyesha ni kijana jasiri na anaonekana ni kijana aliyezoea mandhari ile kwa muda mrefu sana ndiyo maana wazi wazi anaonyesha hana hofu kabisa sababu nae ni jini!. Tena ni jini lenye heshima kubwa katika koo yao, wazazi wake ni viongozi wakubwa wa majini. Mwendo wake ukafika tamati pale alipofika katika kumbi kubwa la kifalme hapo akakutana na mfalme akiwemo na malkia ambao hao ndio wazazi wake, akawasalimu kwa lafudhi ya kijini.



“Pyuno,” Jini Sulesh alisalimu kwa heshima.



“Pyunoka magalanta,” Wazazi wa Sulesh, Binti Surya na Kadhir bin Shadhir kwa pamoja wakaitika salamu ya mtoto wao.



“Utokapo umefanikiwa?,” Binti Surya akauliza mara baada ya mtoto wao kukaa katikati yao.



“Sijafanikiwa,” Jini Sulesh akajibu.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Kwanini?,” Safari hii Binti Surya aliuliza huku akimwangalia mwanae kwa jicho angavu. Ajue kama Sulesh anaongopa au anaongea kweli.



“Ametoroka amekuja Dar, yote chanzo ni mimi. Awali nilivaa nguo kuu kuu akachukua nafasi hiyo kunikataa.... Ila wazazi wake wamesema kuwa dada yake kashampatia nauli ya kurudi nyumbani, hivyo atarudi nyumbani,” Jini Sulesh akaeleza kwa uweledi mkuu.



“Mwanamke uliyemtafuta, inaonyesha anapenda pesa.... Ajui kama mapenzi si pesa. Pesa ni mapambo tu katika mapenzi, ajui hilo?,” Kadhir bin Shadhir aliuliza mara baada ya kusikiliza maelezo ya mwanae kwa muda.



“Nahisi ajui hilo.... Lakini sitokata tamaa sababu nishampenda.”



“Sawa, sisi tunakusubirini nyie tu. Upande wetu hali tete muda wowote tunadondoka, hivyo ndiyo maana sisi kama wazazi tunaimiza sana. Wewe na kaka yako mtafute wenza mapema, ili hapo baadae mmoja wenu tumwachie kiti cha kifalme” alisema Kadhir bin Shadhir huku jicho lote akimwangalia Sulesh mtoto wa mwisho na wa pili katika uzawa wake.



“Nimekuelewa baba.... Sasa kaka leo yeye kaelekea wapi?,” Sulesh aliuliza kwa nia njema ya kutaka kujua alipokwenda kaka yake.





**********

Nikamaliza kuzungumza na Dada Dotinatha tukaendelea na safari ya kurudi nyumbani na Mama Chodo, tukafika nyumbani usiku wa saa moja. Tukamkuta Chodo kasharudi shuleni muda tu yupo sebuleni anajisomea na mwanga hafifu wa mshumaa baada ya umeme kukatika, Chodo alipotuona akaja kumpokea mama yake ndoo kubwa iliyo kichwani. Tuliyobebea chakula kutoka mgahawani akaweka mezani kisha akaingia chumbani kurudisha daftari, akarudi sebuleni kujumuika nasi kwa chakula. Tukala chakula huku Chodo akinitupia jicho la chuki, chuki ile nikazoea nikapotezea na nikajifariji kuwa. Ipo siku Chodo atanipenda tu, lakini wapi Chodo kila siku chuki kwangu alikuwa anaibua. Maumivu! kweli siku moja nikayapata nakumbuka ilikuwa siku ya mapumziko kwa Chodo namaanisha akwenda shule, pia nami mgahawani sikwenda sababu ya kuumwa Malaria. Mgahawani alikwenda Mama Chodo nyumbani akaniacha mie na Chodo, hiyo ilikuwa ni mbaya kwangu. Nakumbuka nimetandika kirago nje nilale kwa ajili ya kutuliza homa lakini mara Chodo akanijia na pesa na begi la shule, ili nimpelekee kwa fundi akamshonee. Sikukataa nikamkubalia japo naumwa nikampelekea begi kwa fundi nimeenda vizuri wakati narudi sasa kimbembe, Chodo kumbe alinifuatilia kama mkia ile napiga hatua kadhaa. Nikasikia sauti ya Chodo akiniitilia mwizi taharuki ikanizonga kichwani mapigo ya moyo yakaenda kasi mpaka nikahisi moyo unataka kuchomoka, na miguu ikafa ganzi sikuweza kujitetea kwa lolote nikatulia tuli nikisubiri raia waje waniuwe nikaungane na wafu. Dakika moja tu raia wakanizunguka kisha kila raia nikasikia akisema neno lake.



“Hei, tulieni kwanza kidogo.... Tokea lini ukaona mrembo anaiba?. Mie nahisi kuna mchezo unachezeka kama si mchezo basi, huyu binti ana sababu za kufanya aibe. Hebu...tumpeni nafasi azungumze labda tutajua kuliko kuchukua maamuzi kumbe dada yetu akawa hana kosa,” Kijana mmoja mwenye hekima nikamsikia akinitetea kwa kuwatuliza raia wenye hasira.



Kijana yule mkombozi kwangu licha ya maneno ya hekima lakini hakusikilizwa hata na raia mmoja. Basi kidole kimoja akivunji chawa na umoja ni nguvu utengano ni udhaifu, kijana yule hakashindwa kunitetea na raia wakang'ang'ania waniue. Raia wakaridhisha mioyo kwa kutaka kunipeleka haela mchana kweupe, walinizunguka wakashirikiana wakanivamia wakanipa kipondo hadi nikajihisi nishawasili kuzimu.



**********

Kadhir bin Shadhir kabla ajajibu swali la mwanae mdogo ghafla ukatokea moshi na wingu zito kati kati yao, ndani ya ule moshi akatokea mwanae mkubwa anayefahamika kwa majina Suleiman bin Kadhir.



“Nipo nchi kavu, nasikia mnanitaja.... Kuna nini?” aliuliza Suleiman mara baada ya kuwasili majini.



“Mdogo wako, ndiye aliyekuwa akikuulizia,” Binti Surya alijibu huku akijipepea mwili kwa kutumia kipande cha ngozi ya Ng'ombe kilichokauka.



“Kulikuwa na shida?,” Suleiman aliuliza tena huku akimkata jicho la mshangao mdogo wake.



“Nilikuwa nataka nijue tu kama mwenzangu umeenda wapi leo. Kutafuta wa hubani,” Sulesh akajibu. Akaondoka kwenye kumbi ya kifalme akaelekea kwenye pango lake analoishi.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Suleiman akuwa mkaaji kila wakati alikuwa bize kwa ajili ya kumtafuta mwenza aje kufunga nae ndoa katika koo yake, alirudi mara moja hatimaye akaaga akaondoka tena kuendelea kutafuta mwenza. Dar es salaam eneo la Kigogo safari hii ikamhusu alikwenda kulanda landa eneo lile la Kigogo bila mafanikio, akakata tamaa akataka kuondoka akiwa njiani sasa kurudi majini. Eneo la Kigogo Jaba kwa mbali akiwa ndani ya gari aina ya HARRIER akaona kadamnasi ya watu imejaa eneo moja, akashuka garini akasogea mpaka kwenye ule umati. Huruma ikamshika baada ya kufika na kuona nimezilai huku nikiwa ninatokwa na damu katika baadhi ya maungo ya mwili akahamua kudadisi kwa raia.



“Eti, wandugu. Kuna nini?,” Jini Suleiman akauliza.



“Ni mwizi,” Kijana mmoja mwenye sura ya kikakamavu alijibu swali la Suleiman kifupi.



“Mwizi mwenyewe, ndiye huyu dada aliyezimia?,” Jini Suleiman akaendelea kudadisi.



“Ndiye,” Kijana yule nae akaendelea kumjibu Suleiman kifupi vile vile.



“Naruhusiwa kumuona?.”



“Bila shaka,” Kijana yule akajibu. Suleiman akatafuta nafasi akapenya kati kati ya umati akanisogelea kisha akachutama akapindua sura yangu ili apate kunitambua. Akasikitika kwa majonzi baada ya kunipindua na kuona sura yangu, akatulia kidogo huku akinikagua kagua punde akawageukia raia akaendelea kudadisi.



“Wandugu, mna uhakika gani kuwa huyu dada ni mwizi?,” Jini Suleiman akauliza.



“Ni baada ya kusikia, huyu binti akipiga ukunga wa mwizi,” Mwanadada mmoja alieleza huku akionyesha kidole cha husda kwa Chodo. Akimaanisha ndiye aliyepiga ukunga wa mwizi.



“Sidhani kama huyu mlimbwende ni mwizi. Kuna mchezo kachezewa tu, si bure” aliongea Suleiman huku akimkazia jicho Chodo. Papo hapo akagundua kuwa Chodo kweli amesingizia mchezo mchafu kwangu.



Suleiman akiwa bado kachutama kando yangu huku tumezingirwa na raia, akasikia sauti ya mwanaume mbavu ikiongea na wenzake kwa kusengenya. Akapinduka akamkata jicho kwa hasira punde papo hapo mwanaume yule akaaga dunia, baada ya kuangaliwa kwa jicho kali na jini Suleiman. Raia wakashangazwa baada ya kuona kifo cha mwenzao ni cha ghafla bin vu haraka wakamuwahisha mochwari, Chodo hakutaka kuendelea kukaa tena baada ya kuona kifo kile cha kushangaza akachomoka mbio akarudi nyumbani. Wote wakiwa wametawanyika Suleiman akapotea nami tukaja kutokea kwenye gari lake, akanipeleka nyumbani bila ya kujitambua. Nilipozinduka nikajikuta nipo ndani ya gari nikaogopa sana nikajua tayari nishatekwa, lakini nikamsikia jini Suleiman akijitambulisha.



“Ni Suleiman bin Kadhir,” Jini Suleiman akamtambulisha.



“Unaishi wapi?,” Nikauliza nijue.



“Naishi Majini,” Suleiman akajibu.



“Unaishi Majini!!!.... Kule wanapoishi majini?,” Nikauliza kwa mshangao.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Hapana sio huko. Kijiji kimoja kinaitwa Majini, kipo mkoani Ruvuma. Huko ndipo ninapoishi,” Jini Suleiman alidanganya ili nisijue sirika lake akanikazia macho. Kisha akaendelea kuongea mara baada ya kuona nipo kimya.



“Hata hivyo kijiji cha Majini nishatoka, sasa nimehamia Dar es salaam. Eneo la Mabibo Hostel.”



“Mh,.... Unaweza niambia. Kwanini nipo humu?.”



“Naweza. Nilikukuta umezimia kutokana na kipigo walichokupiga raia. Katika mtaa wa Jaba, nikahamua kukusaidia kukutoa katika dhahama,” Jini Suleiman akadadavua.



“Asante,” Nikashukuru.



“Usihofu...lakini niliambiwa kuwa, wewe ni mwizi. Ni kweli?.”



“Si kweli. Mtu alinisingizia tu.”



“Mtu mwenyewe, ni Chodo.”



“Eehe.... Wewe umemjuaje?.”



“Nilimuona, kwenye tukio.”



“Ni sawa, sasa umejuaje kama ni yeye ndiye aliyeniuzia msala?.”



“Nina uwezo, wa kujua kuliko viumbe vingine.”



“Eti nini!!!?. Una uwezo kuliko viumbe vingine.... Wewe kwani ni kiumbe wa aina gani?,” Nikauliza kwa sauti ya juu ili nitambue. Kuwa Suleiman ametokea kwenye jamii gani huku nisijue kama naongea na jini.



Suleiman hakujibu bali akaniangalia kisha akapeleka mkono wa kushoto kwenye paji langu la uso. Ghafla ukatokea mwanga mwekundu kwenye paji, mara majeraha na maumivu yakaisha kwenye mwili punde nikazimia tena baada ya Suleiman kutoa mkono kwenye paji la uso wangu. Akanikumbatia tukatoweka tukatokea chumbani, kuja kuzinduka nikajikuta nipo kitandani lakini jini Suleiman alishaondoka. Nikajikagua mwili nikastaajabu mwili haukuwa na maumivu na majeraha, nikajaribu kuvuta kumbukizi mara nikasikia Mama Chodo akiniita huku akigonga mlango wa chumbani. Nikamfungulia mlango kisha nikamsikiliza kwa usikivu.



“Mwanangu, homa vipi?,” Mama Chodo akauliza.



“Naendelea vizuri,” Nikajibu huku nikinyoosha mikono kwa kutupa kila pande kwa ajili ya kuondoa uchovu.



“Vizuri.... Mdogo wako yupo?.”



“Atakuwepo, chumbani.”



“Kamgongee, tuje kula.”

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Sawa,” Nikakubali, nikaenda kumgongea mlango Chodo na kumuita.





**********

Jini Suleiman akarudi majini jioni, akakuta familia kijumla imepumzika akaingia pangoni anapoishi akajipumzisha. Kesho asubuhi ikakaribishwa kwa pilika pilika na majini. Majini Tuuntu wao ni walinzi katika makazi, majini Shufaa wao ni watoa msaada kwa binadamu. Majini Laadu wao ni utesa na uua binadamu waovu, majini Zaadu wao ni watafuta chakula kisha uleta majini. Majini wote hao asubuhi ile wakachochea pilika pilika, wakasimama kwenye vitengo na majukumu. Wanandugu wawili wao asubuhi ile wakaaga wazazi wakaelekea katika majukumu huko katika ulimwengu wa wanadamu. Jini Sulesh akaelekea Kimara mwisho eneo la Bonyokwa akatembelea katika nyumba ya wageni “Guest” kwa ajili ya kwenda kutesa na kuua binadamu waovu, akaingia kimiujiza katika nyumba ya wageni inayofahamika kama Marambolo. Akatokea katika chumba namba tano ambacho kilikodishwa na mume na hawala, akaketi katika sofa. Hata alipowasili katika chumba hicho hakukuta mtu. Mwenyeji Dunga Chunga kama afahamikavyo, alikuwa bafuni anaoga na hawala. Sulesh akaendelea kuketi katika sofa huku akisubiri wenyeji, punde akiwa anasubiri akawaona wenyeji wakitoka bafuni wakiswagana huku wakiwa kwenye huba zito. Wakafika jirani ya kitanda wakatomasana miili kisha wakabwagana kitandani bila kujua kama katika chumba chao kaingia kiumbe hatarishi. Dunga akiwa amelala chali na hawala kitandani, akainuka akaelekea kwenye kipima joto cha hawala akatoa marashi aina ya GALAXY. Kisha akafuata henga iliyotundikwa suruali yake katika mfuko wa mbele akatoa kondomu aina ya BULLS, hatimaye akarudi tena kitandani akavaa kinga na kupulizia marashi mwili na chumba. Marashi makali upande wa majini si mazuri yakampalia Sulesh na yakamfanya aone chumba kile kibaya, akatoka katika chumba kile akiwa amekasirika kufika nje akanyanyua mkono wa kushoto. Akapeleka kiganja cha mkono ule kwenye sikio, kiganja akakifanya simu haraka akawasiliana na mwanamke.



“Hallow...nani mwenzangu?” ilisikika sauti ya mwanamke ikiuliza kwa sauti ndogo mara baada ya kupokea simu ya jini Sulesh.



“Ni Sulesh.... Natumai naongea na Nzota, mke wa Dunga Chunga. Si ndiyo?,” Jini Sulesh akauliza.



“Ndiye mimi.... Kwani kuna nini?, halafu. Wewe ni Sulesh wa wapi?,” Nzota akadadisi kwa kimuhe muhe cha kutaka kufahamu.



“Huwezi kunijua ila, mimi ni raia mwema. Njoo nyumba ya wageni ya Marambolo iliyopo Kimara Bonyokwa, chumba namba tano. Ujionee.”



“Wewe ni Sulesh gani?, namba yangu umepataje? na jina langu umefahamu vipi?,” Nzota akazidi kudadisi.



“Sina muda wa kujieleza saana.... Wewe njoo nilipokuelekeza,” Jini Sulesh akajibu kisha akakata simu. Hatimaye akaondoka katika eneo lile la fumanizi.



Nzota haraka akajiandaa akaelekea kupanda daladala aelekee Kimara Bonyokwa kama alivyopokea maelekezo. Akafika Kimara Bonyokwa akaulizia gesti ilipo akaelekezwa, akaelekea katika gesti akaonana na mhudumu wa mapokezi akajieleza kisha akaonyeshwa chumba alichokodi mumewe. Ila alipoingia kwenye chumba kile hakuweza kuamini alichokiona, akamuona mumewe juu ya hawala kitandani akifanya tendo la ndoa. Presha ikamshika, kiwewe kikampata, akili ikaruka mbali hakuweza hata kufikiri cha haraka akaambulia kutoa kilio tu. Mbele ya mumewe na hawala asiyejua thamani ya ndoa, Nzota alipokuja kunyamaza akamkazia jicho kwa hasira yule hawala. Wakati huo Dunga na hawala wakitetemeka kitandani baada ya lile fumanizi, tendo la ndoa lote likaingia mdudu radha yote ikapotea. Uwoga ukawajaa wakapoa mfano maji ya mtungini, unajua fumanizi lilivyo baya mfano jehanamu. Haswaa lile la wanandoa ni baya yaani ukifumaniwa tu unafanya ushenzi lazima uwe mpole, Dunga basi alikuwa mpole mfano mwanamke anayetaka kubakwa na njemba zilizoshiba. Nzota uvumilivu ukamshinda kwa jazba akaenda kumrarua kofi hawala papo hapo akamvaa akamchakaza na kipigo hadi hawala akakimbia, akuongea na mumewe akarudi nyumbani akiwa na hasira akakusanya begi zake akaondoka kurudi kwa wazazi.



**********http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Nikaongozana na Chodo mpaka sebuleni kula chakula cha pamoja baada ya kutoka kumuita chumbani. Chodo aliongozana nami lakini huku akishangazwa nami nimeponaje, hakakosa jibu hofu ikamshika tu. Tulipofika sebuleni tukamkuta Mama Chodo kashaandaa chakula mezani tulikula tulipomaliza Chodo akarudi chumbani kulala, nikakusanya vyombo nikataka kwenda kuosha lakini Mama Chodo akanizuia sababu ya homa aliyoniacha nayo. Akutaka nioshe vyombo akaniamuru nami niende kulala ataosha. Nikamsikiliza nikaenda kulala nyuma Mama Chodo akaendelea kupambana na vyombo, akaosha mpaka usiku wa saa tatu akamaliza nae akaenda kujilaza chumbani. Asubuhi kukakucha Mbwa wa jirani akawa anabweka mfululizo katika dirisha la chumba cha Chodo, akamfanya Chodo hashindwe kuendelea na usingizi. Akaamka akajiandaa akaondoka shule. Asubuhi ya saa moja ikawa zamu yangu kuamka nikakurupuka kitandani nikaelekea katika chumba cha Mama Chodo kumuamsha kwa ajili ya kujiandaa na kwenda mgahawani, tukajiandaa tukaelekea katika mgahawa tulipofika mgahawani tukagawana majukumu yetu ya siku zote. Tukachapa kazi na siku hiyo tukamaliza kuuza chakula mapema, saa kumi tu tukajirejesha taratibu nyumbani. Kufika tukamkuta Chodo amelala sebuleni baada ya kujisomea baadhi ya vitabu, amechoka sana akahamua ajipumzishe. Mama Chodo akamsogelea mwanae akamuamsha kwa kutumia sauti ya upole mno.



“Chodo...Chodo mwanangu,” Mama Chodo akaita huku akimtikisa Chodo mwili mzima.



“Abeeh!,” Chodo aliitika katika usingizi huku akijifikicha macho mara baada ya kuamka na kukaa kitako kitini.



“Hujambo?,” Mama Chodo akauliza.



“Si jambo...shikamoo,” Chodo akajibu kisha akasalimu.



“Marahaba...umesoma leo?.”



“Nimesoma.”



“Sawa, sasa ngoja niandae chakula. Tuleni,” Mama Chodo alimwambia mwanae kisha tukakaa vema kitini. Ili tupate chakula kwa pamoja.



Tukala hatimaye tukamaliza madikodiko. Chodo akapewa agizo na mama yake la kuosha vyombo, akaosha nasi tukapoteza muda kwa kwenda kuangalia runinga. Kutokana na Chodo amepangiwa kuosha vyombo, badala ya mimi. Hivyo Chodo alipomaliza kuosha akajenga chuki, akaelekea kwenye jokofu akachukua pilipili kisiri akaongoza chumbani kwangu. Akasambaza pilipili ile kwenye shuka langu, muda wa kulala ulipowasili tukaenda kulala lakini mie sikulala vema. Nililala kwa mang'amu ng'amu sababu ya pilipili aliyoweka Chodo kwenye shuka, pilipili ikaniwasha mwilini baada tu ya kulaza mwili kitandani na kujifunika shuka.



**********

Jini Suleiman akatembelea Tegeta eneo la Kibaoni kwa ajili ya matembezi, akatembea Kibaoni nzima akidadisi baadhi ya vitu vya wakazi wa Kibaoni. Wakati wa usiku baada ya kutembea siku nzima akataka kurudi majini kujipumzisha lakini ghafla, alipofika eneo la Kibaoni mtaa wa Changazi karibu na barabara kuu. Bahati akafanikiwa kusikia sauti ya changudoa akiomba msaada, akageuka akaona changudoa akitaka kubakwa na njemba zilizoshiba. Akasogea jirani akapiga busu angani kuhabarisha zile njemba kuwa eneo lile kuna mtetezi, njemba zile zikageuka kuangalia ni nani aliyewakatisha jambo. Kugeuka ndipo wakamuona Suleiman kasimama nyuma, kwa dharau wakaendeleza dhamira ya kutaka kubaka. Suleiman akazidi kusogea jirani alipofika akamvuta njemba moja akamtupia pembeni, akaongea.

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Wandugu, wanaume wote watano mnataka kumuingilia mwanamke mmoja.... Hamuoni kama fedheha,” Jini Suleiman aliongea huku akimuangalia kwa jicho la huruma yule changudoa ambaye tayari ameshawekwa vumbini kwa kutaka kuingiliwa bila idhini.



“Wewe ni nani?, na kwanini. Umetukatisha jambo letu?,” Njemba moja mwenye jicho chongo alimuuliza Suleiman kwa hasira mara baada ya kuona amewaingilia katika jambo lao.



“Naona mna shauku sana ya kutaka kunijua.... Si ndiyo?,” Jini Suleiman akauliza. Akawakazia jicho kali zile njemba.



“Ndiyo.... Wewe ni nani?,” Njemba la pili mwenye kovu la kukatwa na panga shingoni akauliza kwa umwamba zaidi.



“Mkitaka mnijue kuwa mimi ni nani. Endeleeni na huo ufuska...hapo ndipo mtanijua kuwa mimi ni nani,” Jini Suleiman akajibu.



“Una kauli za kishujaa.... Umetoka mafunzo ya jeshi nini?,” Njemba la tatu nae akauliza huku kana kwamba anaongea utani. Wala asijue anayeongea nae utani ni jini.



“Hei...tuendeleeni na starehe muacheni huyo taila abwabwaje mwenyewe,” Njemba la nne akasikika akisema kwa kebehi, akimkebehi Suleiman bila kujua madhara yatokanayo na kiumbe huyo.



Njemba zote zikamkebehi Suleiman wakaendelea na dhamira, wakataka kuvua vazi la changudoa. Lakini Suleiman akaona ule ni ufedheheshaji mkubwa, hakuruhusu lile litokee akakunja ngumi kwa hasira akazungusha angani akashusha akafanya kama kurusha ile ngumi kwa zile njemba. Ghafla kimbunga kikaambatana na mwanga mweupe ukatokea baada ya Suleiman kurusha ile ngumi, kimbunga kikawadhuru njemba kwa kuwapa ulemavu kasoro changudoa tu. Changudoa kuona maajabu akatimua mbio akatokomea eneo lile bila kutoa shukrani, Suleiman baada ya kutenda wema akapotea akatokea katika eneo la makazi kando ya fukwe ya bahari. Hapo akakutana na mdogo wake Sulesh kalala chali akipunga upepo.



“Sulesh, nakuona unabalizi tu. Mdogo wangu,” Jini Suleiman akaongea huku akionyesha chochezi ya utani.



“Naam, siunajua tena kaka. Baada ya miangaiko sasa mapumziko,” Jini Sulesh akadokeza. Ndiye cha udele wa mfalme Kadhir.



“Lakini majini, kwema?.... Au lahasha?.”



“Majini ni shwari tu, sijui wewe utokapo.”



“Ni. Alhamdulillah.... sijui wewe nawe katika matembezi yako.”



“Namshukuru Allah, amenisaidia nimerudi salama.... Kaka, wewe tayari ushapata mwenza?.”



“Kumpata nishampata, bado kumtamkia tu.”

http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Ooh. Kaka, fanya upesi mwambie usije kuchelewa. Ukakuta mwana si wako.”



“Ni kweli...lakini si hofu, sababu nipo kwenye taratibu za kumueleza hisia zangu,” Jini Suleiman akaongea. Akakuna kichwa chake chenye nywele laini mfano singa singa hatimaye akaongea tena.



“Wewe vipi. Mdogo wangu, mwanamke wako kashakukubali?.”



“Bado.... Nasubiri kwanza taarifa kutoka kwa wazazi wake. Kama karudi niendelee kutema cheche mpaka kieleweke,” Jini Sulesh akaeleza.



O...

**********



ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog