Search This Blog

JOTO LA MSHUMAA - 2

 






Simulizi : Joto La Mshumaa 
Sehemu Ya Pili (2)




Walipofika kwenye ile nyumba ya bwana KATUNJE, alifungua mlango kisha wakaingia wote kwa pamoja. Katunje alifunnua lile shuka na kumuonyesha mtu huyo, kikweli mzee KAUZIBE alishtuka kabisa mpaka mwili wake ukaanza kutetemeka. Aliona kabisa kuna umuhimu wa kumsaidia kwa haraka sana.

"Kauzibe hii ni hatari sana, tena sana usipoangalia anaweza kukufia hapa, sasa ngoja nikachukue dawa zangu haraka sana.". Aliondoka huku akiwa anakimbia kwa haraka ili aweze kumkuta akiwa hai binti huyo.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

akiwa njiani mzee kauzibe alijiongelesha mwenyewe " Mh jamani watu wanapona huyu alikuwa na hali gani alinyimwa kula au anaumwa "

Alirudi haraka sana akiwa na furushi la mitishamba yake ambayo aliona kuwa itamfaa., alianza kukusanya dawa kutoka kwenye lile furushi, "haya lete maji haraka sana". Katunje alifanya hivyo kwa haraka ile ambayo mzee kauzibe alihitaji ili amsaidie mtu huyo. Aianza kusugua kijitim kimoja hivi huku akikinga sehemu baada ya kumaliza akamuomba amuinue binti huyo ili amnyweshe.

"sasa katunje, hii dawa ninayompatia, itabidi uandae sehemu ya kuhifadhia uchafu utakaotoka tumboni kwake"

Katunje alifanya hivyo na akamuweka katika hiko kifaa kwani alikuwa mwepesi sana. baada ya kumywesha dawa ile alionekana kushtukashtuka hivi, hatimae alitoa uchafu mwingi sana kwa njia ya haja kubwa. Hata hivyo haja yake haikuwa na harufu kali ilikuwa kama ni ya mtoto mdogo. baada ya hapo mzee Kauzibe akasugua nyingine kwenye jiwe na ikiwa inakingwa kwenye kifaa kingine.

"Haya katunje hii ninayompatia hapa ni kumpatia nguvu mana hapo hana nguvu kabisa, lakini fanya haraka umuandalie uji mzito sana akinywa hii anywe na uji huo".

Katunje kwa kuwa alikuwa safarini hakuandaa mazingira ya nyumbani kwake hivyo alitoka nje na kwenda jirani kuomba moto ili aweze kumpikia uji mgonjwa wake, wakati anayafanya hayo alikuwa anatokwa na machozi sana kwa huruma sana, alikuwa analani watu ambao walimtupa kule aliko.

alifanikiwa kuandaa uji mzito ambao ulikuwa unatakiwa, ndipo mzee Kauzibe akamnywesha dawa ile kwa nguvu sana japo alionekana kutohitaji kutokana na uchungu uliopo, lakini pia nguvu ya kufumbua macho haikuwepo kabisa hivyo hawakujua kama macho yake mazima na masikio yake mazima kwani hali ambayo alimkuta nayo haielezeki. baada ya kufamikiwa kumywesha dawa hiyo basi akanyweshwa uji huyo kwa kumlazimisha sana mpaka ukaisha, akaambiwa amuwekee mwingine."babuu huyu kashiba si unamuona".

"Hapana ukimsikiliza mgonjwa siku zote hutomsaidia kabisa sasa fanya hivyo". Kweli alipika mwingine lakini huku akiwa na wasiwasi, Hatimae alimaliza na akanyweshwa kwa kulazimishwa mpaka alipomaliza. Mzee kauzibe alimuaga na kijana katunje na yeye akaenda zake kwake. Huku nyuma katunje alifikilia sana kuhusu swala la kuishi na yule binti kutokana na hali yake,aliingia ndani na kwenda kulala kabisa. Hakuwa na usingizi kabisa usiku mzima kwani alikuwa akimsikia binti yule akilalama, aliamka na kumuangalia alikuwa akitapika alafu akiwa kajishika tumbo lake huku akitetemeka kwa baridi kali.

Alihangaika sana katunje kutokana na ile hali hivyo alimtafutia nguo zake na kumfunika baada ya kusafisha matapishi yale na kuyaweka kwenye sehemu moja. hatimae alikuwa kimya ndipo akalala, katunje alisimama huku akimuomba mungu amsaidie sana katika kumhudumia binti huyo mpaka hali yake itakavyokuwa vizuri. Majira ya asubuhi ya siku ya pili Katunje aligongewa mlango na mzee Kauzibe.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"Eti vipi kaamkaje mgonjwa wetu" aliuliza bwana kauzibe

"Ahaa kweli, usiku nilimsikia akilalama nilipoamka kumbe ilikuwa baridi kashikilia tumbo lake nikamfunika na mashuka mengi ndipo nikaona kuwa yuko sawa mpaka sasa hajaamka" Mzee kauzibe alitikisa kichwa huku akifurahi sana kwa ile taarifa aliyopewa.

"hapo sasa matumaini yanaonekana nadhani akiamka nitampa dawa moja hivi kiboko ambayo itamfanya awe kamili kabisa". Walishikana mikono na kupongezana lakini mzee kauzibe alimuomba aweze kumhadithia yaliyojiri huko atokako, "Ehee katunje, nambie habari za huko utokako yapi yamekukuta na huyu mgeni ulimkuta kwa hali gani "

Aliuliza ili aweze kupata taarifa nyingi zaidi.

"kweli nilizunguka kama mbwa mwizi kumtafuta ndugu yangu, nilianzia kule nyumbani SHIMOMO ambako kiukweli nilipita juu juu tu nilimpata ndugu mmoja nikamuuliza akaniambia hayupo kaama tangu kipindi cha nyuma, "

"ehee ukafanyaje sasa baada ya hapo" aliuliza mzee kauzibe

"Ndipo nikatembea sana hata sikufahamu naenda wapi hatimae nilifika kijiji kimoja kinaitwa BWAWANI hapo nilifanikiwa kuonana na mwenyekiti lakini kwa bahati mbaya iliyoje, majibu niliyoyapata kuwa bwana CHITO hawamfahamu kabisa pale "

"hawamfahamu aaah kweli umepitia maisha magumu wewe na ndugu yako ehee"

"basi nikaomba wanihifadhi pale ili ndani ya siku tatu nimtafute ndugu yangu pale kijijini kama sitomuona basi nirudi, lakini wakanikatralia na kunitumia vijana wanifukuze, njia niliyokuwa nikikimbilia kumbe ilikuwa naelekea msituni pia karibu na bwawani"

mzee kauzibe alikuwa makini sana kusikiliza hatua kila hatua "haya ikawaje"

"ndipo hapo wakaniacha na mimi nikaanza kutembea ghafla nikaliona tenga lililopo ndani pale mbele yake nikaona nguo zilizochakaa alafu zimegandia damu, nikazikusanya mpaka bwawani ajabu nataka kuanza kunawa yale maji ambayo eneo hilo linaonyesha hapafikiwi na mtu kwani pachafu sana, ndipo nikamuona huyu binti pembeni wadudu wakimuingia masikioni na kachafuka yani kwa hali ile mungu mkubwa jamani ndipo nikakutwa na roho ya huruma nikamuweka kwenye tenga na kuja nae huku".

Alikuwa anahadithia huku machozi yakimtoka kwa wingi sana, kwani alionekana kuwa na uchungu wa wale wanaowafanyia mabaya watu hasa wanawake pia wadogo kama yule. Ukweli kwa muonekano wa binti huyo ulikuwa wa kutosha kabisa kuwa na mtu kwani maumbile yao huwa makubwa.

"Kijana kwanza hongera huo ndio utu na si vinginevyo hakuna jambo zuri kusaidia watu wenye shida kama hawa"

mala ghafla alisikika akitoa sauti humo ndani, akigugumia kwa maumivu makali. walisimama na kwenda ndani kwa haraka, walimkuta akishikilia tumbo lake huku akijaribu kurusha miguu. "sasa mzee tunafanyaje, hapa?"

aliuliza katunje,

"yani hapa naona sasa utumbo unafanya kazi na mwili unaitikia unataka kurudi kwenye hali yake sasa mpikie uji haraka sana". Baada ya muda ulikuwa tayari na alinyweshwa.

Baada ya miezi kadhaa kupita upande wa kijiji cha BWAWANI, mzee mambo sasa alikabidhiwa shamba la mikorosho lenye mikorosho themanini, alianza nayo kuitengeneza vyema sana kwa mara ya kwanza. Ndipo mavuno yalipokaribia utata ulipoanza, vijana wa mzee Manyenye, walikuja juu kuwa yale ni mashamba ya baba yao hivyo wana haki ya kufanya wakitakacho hivyo walianza kuchukua korosho na kujiwekea wao majumbani kwao, mzee mambo sasa aliligundua hilo mapema sana akamshirikisha mzee manyeye ndipo akawakemea sana vijana hao watatu.

wale vijana walikutana siku moja na kupanga njama ambayo watamfanya mzee mambo sasa aache ile mikorosho ambayo kaihudumia kwa muda mrefu baada ya kupewa. Moja ya njia ni kuichoma moto kabisa ili wakose kila kitu na kuwaacha wakiwa watupu.

Kwa bwana Sikujua alikuwa vizuri na anaendelea na shughuli zake lakini, muda huo alipita Mama Mengi ambae binti yake yupo kama Sikitu aliyepotea kwa muda mrefu. "Mzee naona unajisikia vizuri tu sasa hivi"

kauli ya mama mengi ilimfanya ashtuke sana sikujua,

"Wee mwanamke usiyekuwa na adabu unanitafuta sasa hivi"

"sio kukutafuta hivi unakumbuka kuna siku nilikuona unaingia na Sikitu chumbani kwako, alafu siku ya pili tukasikia kapotea nilipokuuliza ukanitishia looo mzee mzima na najua wewe ndio utakuwa umehusika na hilo swala"

Mzee sikujua alipandwa na hasira sana kwani aliona kuwa mama mengi ni nuksi kwake. "Wee mama wewe kuwa na adabu fahamu kuwa hiyo ni kesi kubwa sana unayonipakazia sitaki na nisikusikie ukiniambia mambo hayo"

"sawa utanifanya nini sasa kwa sasa hivi? na ukileta ujinga natangaza kijiji kizima hiki wajue na mzee mambo sasa unajua alivyokuwa na hasira akijua">

mama huyo aliondoka pale akimuacha bwana sikujua kijasho kikimtoka. alijifikilia mengi sana kwani aliona sasa huyu mama atamfanya ajulikane wakati mambo yalipita kitambo sana.

Akiwa nyumbani alisikia kauli ya watu ambao walikuwa wanapita karibu hapo alipokuwepo, "Nimesikia kuwa mama mengi leo jioni anamtaja mtu aliyesababisha kupotea kwa Sikitu".

Sikujua hakuweza kuamini kusikia hayo maneno, alisimama na kuwasimamisha wale watu waliokuwa wakisema zile habari.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

"jamani ina maana mama mengi anamfahamu msababishaji kwa kupotea kwa sikitu?" aliuliza.

"ndio bwana sikujua anamfahamu japo hakutaka kutuambia hivyo kasema leo jioni itapigwa kengele na tutafika pale alafu atamtaja " Mzee sikujua alionekana kuchanganyikiwa akijisemea moyoni 'huyu mama hanitambui kalianzisha ngoja nilimalize mpumbavu sana'. "vipi bwana sikujua unawaza nini?" walimuuliza baada ya kumuona kimya kwa muda.

"hapana yani najifikilia kwa nini hakumtaja mapema hivyo, inabidi, ataje haraka tumshughulikie sisi wenyewe kabla ya bwana mambo sasa au mnaonaje"

aliongea kwa kujipa ujiko ili asijulikane kuwa yeye ndiye muhusika mkuu, "ni kweli jamani anachosema bwana sikujua ila tunajiandaa sasa kwa ajili ya kwenda kupokea ujumbe mzito huo, ".

waliachana pale, na yeye akakimbilia kwa Mapato, kumueleza jambo lile hakika mapato alionekana kumgeuka rafiki yake kwani alijiepusha kutajwa na yeye kama alishiriki kwenye swala lile "Haaa ndugu yangu hapo mimi sihusiki kabisa nimekusaidia vya kutosha kufanya unyama tena sitaki".

"ina maana unanikana leo kwa kuwa umesikia mtoto wa mzee Manyenye leo anaenda kunitaja".

Taarifa ilimfikia bwana Mambo sasa pa,moja na mke wake hivyo walijianda vilivyo kusubilia jioni kwa hamu tena waliona kuchelewa.Baada ya mapato kujitenga na lile swala, alirudi nyumbani bwana sikujua na akaingia ndani, alichukua kisu kikali na akakinoa vyema yakawa na makali yote, akatoka nje huku kile kisu akakiweka kwenye ala yake yani hifadhio. alitembea mkuku mkuku huku akiangaza huku na kule kama kuna mtu anamuangalia, alifanya hivyo akiwa na nia yake yeye mwenyewe anayoifahamu.

Hatimae alimuona Mama Mengi akliwa anachukuam kuni kule ambako alimhisi lazima muda huo atakuwepo, alipomuona akachomoa kisu chake na kujificha njiani ili amsubiri apite amuonyeshee, kwa kuhofia kuonekana alijificha na nguo usoni akabakiwa na macho yakiangaza huku na kule, Mama mengi alihisi hatari wakati anarudi, ndipo mzee sikujua akamtokezea na kumsukuma hatimae akadondoka chini na zigo lake la kuni. Hakufanya ajizi yeyote, alimtumbukiza kisu tumboni bila huruma na akahakikisha kimechanachana utumbo wake vyema kisha akatoa,

Mama Mengi alilalamika sana tena sana ndipo katika harakati za kutafuta uzima, alimshika nguo yake ya usoni na kumfungua, "Aaaaah mzee sikujua una..ni...iiiiuaaa ".

"Pumbavu haya nenda kaseme sasa huko kuzimu kuwa nimembaka sikitu mpaka kifo chake unapenda kuingilia kitu kisichokuhusu">

Aliondoka pale kwani alikimbia utadhani kuwa sim kama mzee, alifika nyumbani kwake akachukua maji na kuoga kwanza. baada ya hapo akachukua mkeka akalala nje kama kawaida yake, hivyo ilimfanya kila apitae kumuona pale alipo na kuondoa dhana ya yeye kuwa kasababisha mauaji.

Kengele kama ada iligongwa na watu walifika pale kama kawaida akiwemo mama sikitu na mumewe akiwa na huzuni akiwa na hamu ya kumla supu huyo atakayetajwa, mwenyekiti alitoa maelezo machache ambayo yalimfanya kila muhusika pale atulie kumsubiri mama Mengi, muda ulipita mtu haonekani, ndipo aliulizwa baba mtu mzee Manyenye, kuwa yuko wapi ndipo akaelekeza kuwa yeye alienda kuchukua kuni na akirudi atajiandaa kuja hapa.

Walitumwa vijana akiwemo susu, walikimbia kuelekea huko walikoelekezwa muda mchache wanrudi na mwili wa mama Mengi hakika hayupo ambae aliamini kama mama mengi kafariki kwa kuchomwa kisu.

Upande wa MLIMALONDO baada ya miezi ile kupita hali ya yule binti ilikuwa nzuri na kuridhisha sana. wakati ulifika wa kuhojiana ili kumfahamu vyema ndipo walikuwepo na mabinti kadhaa ambao walitoa ushirikiano wa kucheza nae na kumchekesha lakini alikuwa na tatizo hajui kuongea, macho yamefunga kama alivyomkuta kule mara ya kwanza lakaini mwili ulianza kurudi hata mifupa na mbavu zilianza kujificha.

KATUNJE alikuwa hana raha alijitahidi namna kila namana binti arudi kama hali yake lakini akaona labda tangu mwanzo alikuwa vile alivyo, hata jina lake hakulifahamu kabisa kumbukumbu zilimpotea ndipo wakampatia jina jipya ambalo watamzoesha mpaka atalifahamu na kulitumia walimuita LYOTO. Likiwa na maana ya joto jina hili alilitoa mzee kauzibe ambae alilifafanua kama joto ni kama moja ya changamoto ambayo unakutana nazo kama joto linavyokuzidi na kushindwa kujizuia, hiyo ndio maana halisi hivyo binti LYOTO alikuwa changamoto kwao ndani ya kijiji cha Mlima londo...





Ilikuwa ni kizaazaa sana kwa tukio la kufa kwa mama Mande pale kijijini, wasiwasi ulianza kutanda kuonyesha kuna jambo ambalo lipo miongoni mwao, wengi waliongea vile walivyofikilia na kudhania nini kinaendelea pia wengine walifikia hata kuwaongelea vibaya viongozi wao vibaya kuwa wanahusika kwa namna moja ama nyingine.Upande wa mzee manyenye alipatwa na presha kabisa kutokana na ile hali.

Hayo yote yakiwa yanafanyika kwenye uwanja wa mkutano karibu na ofisi za mwenyekiti, pamoja na mtendaji wa kijiji cha bwawani.

watu walisindikiza haraka mwili wa marehemu hadi kwenye nyumba ya mzee manyenye, huku wengine wakijaribu kumpepea mzee manyenye. Kwa upande wa Mzee mambo sasa na mkewe waliweza kuondoka pale kwa haraka kwenda nyumbani kwao. "Mke wangu hakika tunahitajika kuondoka haraka sana mana hii inanionyesha picha mbaya sana hapa kijijini". aliongea bwana Mambo sasa.

"Inakuonyesha picha gani eeeh"

"wewe huoni?, Mama mande katangaza kuwa anamfahamu aliyesababisha mtoto wetu sikitu kupotea na anataka kwenda kutuambia lakini muda umefika inaletwa maiti yake unadhani hapo kuna nini" Mama sikitu aliduwaa tu na kwenda kumshika mumewe akimpokonya zile nguo alizokuwa anazipanga tayari kwa safari.

"Sawa mume wangu ina maana kuwa yeyote ambae atahitaji kufuatilia kupotea kwa mwenetu atafanywa kama alivyofanywa Mama Mengi?"

Aliuliza mama sikitu, "Ndio na hapo ipo siku kabisa muuaji huyo ina maana kamuua mwenetu, alafu atakuja kutudhuru hata sisi ili kuondokana na hilo lazima tuondoke"

"Lakini kule si kuna msiba alafu yule aliyekufa baba yake kakufanyia nini na unataka tuondoke inafanana kweli"

kauli hiyo iliweza kumuingia vyema bwana Mambo sasa, Akamuelewa vyema mkewe ndipo akamsogelea na kumkumbatia huku chozi likimtoka,

"Sawa mke wangu nimekuelewa na nakuahidi mpaka tunamaliza maziko yote na kuhakikisha hali ya mzee manyenye inakaa sawa ndipo tunaondoka".

Kijiji kizima kilirindima majonzi yenye mshangao mkubwa sana, kwa upande wa bwana Mapato alihisi jambo fulani kwani baada ya kutoka kule kwenye mkutano uliozua mabaya alikwenda moja kwa moja hadi kwa Sikujua kumuangalia kwanza. Alimkuta akiwa analia chozi likimdondoka hivyo hata dhana yake ya kwenda kumhisi vibaya ilitoweka kabisa.

Alimsogelea na kumuuliza kipi ambacho kinakuliza rafiki yangu?. Sikujua aliongea huku akitetemeka kwa hofu `ndugu yangu haya mauaji yaliyotokea ukweli sina amani sasa` aliongea hivyo kumueleza rafiki yake mapato, lakini mapato hakuridhika na yale majibu aliyojibiwa na sikujua `lakini kwa nini unachukua maamuzi mkononi, ninakutilia shaka` alimueleza kweli kuwa anamtilia shaka.

`unanitilia shaka. kivipi unanitilia shaka' aliuliza sikujua kwa mshangao wa dhati kabisa. "ndio nakutilia shaka kwa sababu unakumbuka muda ambao ulikuja nyumbani kuniomba eti ama mengi kakutisha na mimi nikakuambia kuwa sitoweza kukusaidia kwa hilo ukaniambia kuwa utajua la kumfanya wewe mwenyewe si ndivyo".

Sikujua alikaa kimya sana huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi, jasho jembamba likimtoka mzee huyo wa makamo, alimgeukia bwana Mapato na kumueleza, "Ndugu yangu, sikia mimi sijasababisha mauaji kabisa kwanza siwezi kuua nina kesi hii naitaji niikwepe tena niweze kusababisha mauaji kwa mtu nisiyemkosea wala kunikosea jamani". Mapato alisimama na kumnyooshea kidole

"hakuna cha kupinga hapa, wewe ndio msababishi na nimekuchoka, sasa kama unaweza njoo uniue mimi kwani tukikuachia hivi utawamaliza watu".

Sikujua jicho lilimtoka kama kabanwa na mlango, moyo wake ulionekana kama unaotaka kusema jambo lililopoila likashindwa, "mapato naona sasa umenichoka ila kama unaenda kusema huko wewe nenda alafu mimi nitajua la kufanya". Mtafaruku uliendelea pale wakiwa wawili zao.

"Wewe nenda ila kumbuka miaka nane iliyopita undugu wetu uliunganishwa na nini, ulifanya tukio gani kumbuka alafu leo unajifanya eti kwenda kusema nenda na mimi naenda kutegua kile kitu mbavu zako".

Baada ya hapo mapato alionekana kukaa kimya sana bila hata kusema ndipo akamsogelea mwenzake na kumuomba msamaha ili yaweze kuisha na waendelee kufichiana yale mambo yao wanayoyafahamu wao wenyewe.

Alirudi kwake bwana, Mapato huku akisubiri matangazo ya kujua lini wanazika, alianza kukumbuka miaka nane iliyopita baada ya kukumbushwa na sikujua, urafiki wao ulianzia miaka kadhaa ya nyuma iliyopita,

Siku moja, bwana mapato akiwa anatafuta kuni ndani ya kijiji cha SONGAMBELE, huku akitembea tembea na kuimba, aliukuta mti mmoja ambao aliuona kama unafaa kwa kupata kuni,

alianza kukata tawi moja baada ya jingine, ghafla wakati anaendelea alisikia sauti zikisemezana maeneo ya bwawa ambalo lipo ndani ya kijiji chao, bwawa hilo lilikuwa linatumika na watu kwa mabo mengi sana hasa kama uvuvi pamoja na matumizi ya nyumbani, alikaribia bwana mapato huku akitega sikio kujua nini ambacho kinazungumzwa hapo, alizisikia sauti za ajabu ambazo hakuwahi kuzisikia kamwe, cha ajabu zaidi kwenye lile bwawa ilionekana kama kuna watu ambao wanaogelea lakini hawaonekani.

Alirudi kinyumenyume, na ndipo akaanza kukimbia kurudi kijijini. Enzi hizo palikuwa panaongozwa na kiongozi mmoja tu aliyejulikana kwa jina la ZAMALIO, huyu mzee uongozi wake ulitegemea sana nguvu za wale anaowaongoza, yani ushirikiano wa wanakijiji wenyewe ndani ya songambele. aliwapenda sana watu wake na alijitahidi kufanya kila njia ili kuwafurahisha wanakijiji na wao walimpenda,

Alipofika kijijini ndipo akaelekea kwa zamalio kumueleza yale aliyoyashuhudia na kumchanganya, ukweli ilikuwa ni habari nzito sana siku hiyo hivyo bila kuchelewa walitumwa watu na wazee ambao alihisi kuwa wanaweza kutambua kama kuna aina yeyote ya ushirikina unaendelea hapo.

Walipofika kule karibu na lile bwawa, hawakuweza kukuta chochote lakini ajabu walifika nyuki kutoka sehemu ambayo hawakutambua walivamiwa kasoro bwana Mapato, wengine walikimbia akabaki mzee mmoja ambae walimvamia mpaka kifo chake palepale, Mapato alishtuka na kuweuka pale na asijue nini afanye, wakati anajiandaa kuondoka basi alihisi kama kashikwa na kitu asichokifahamu, ""Mpato ahsante sana wewe ndie umetuona sisi na wewe ndie unachaguliwa kuwa kiongozi wa kutuletea watu hapa mpaka zamalio afike ""

alishindwa kuelewa ghafla alihisi kichwa kikimbangua na mwili kubadilika kuwa na joto kali alianza kutoka pale akiwa hajielewi kabisa, Siku ya pili alikaa na kufikilia kile kilichotokea jana yake, hakuamini kwa yale yote ambayo yamemfika na kusababisha mtu kuda mbele yao.

Alinyanyuka na kwenda kwa kiongozi wake zamalio ili akajue hata kama kuna kitu chochote ambacho atakitambua kuhusu lile bwawa.

"Zamalio kiongozi wa songambele, nina maswali mengi juu yako kuhusiana na lile bwawa, kwa lina vitu gani ambavyo sisi kama wanakijiji hatuvifahamu?" aliuliza mapato ili apate kujua zaidi kuhusu kile alichoambiwa. Zamalio hakuweza kabisa kumjibu vizuri ili kijana mapato afahamu.

"mh kijana, ni swala zito sana ambalo hata mimi sikupata ufafanuzi kama wewe unavyohitaji kufahamu hivyo kikubwa zaidi achana nayo tu"

Mapato hakuweza kabisa kuridhika, alirudi nyumbani kwake. majira ya usiku hakulala kwani kuna vitu aliweza kuvisikia hivyo alitoka nje na hatimae anakutana na watu wa ajabu sana ambao walimpa amri kali sana. "kijana, endapo usipotekeleza kauli yetu huwezi kukaa salama." "Jamani nini ambacho nimekosa na mnahitaji ninikutoka kwangu".

Walimcheka sana kisha wakamuuliza `unataka tukuonyeshe, nini tunakihitaji? kumbuka wewe ndio wa kwanza kabisa kutuona maeneo yale kwani hatukutaka kuonekana sasa ili tufiche siri hii lazima ufanye." walisambaa zao na kumuacha mapato akihemwa. Muda ulipita bila mapato kufanya shughuli ile ambayo aliambiwa ya kuwapeleka watu karibu na bwawa, kwani tangu siku hiyo mzee zamalio aliwakataza watu wakewasisogelee tena lile bwawa. Sikum moja mapato alishuhudia kifo cha mama yake mzazi lakini ilitokana na wale watu wasiojulikana. baada ya miaka kama mitatu hivi kupita ndipo wakamuambia atamkosa baba yake, alikuwa mbishi sana mapato ndipo. wakamuua baba yake mapato, haikutosha wakamueleza kuwa asivyotekeleza wanaanza familia yake mmoja mmoja.

Hapo ndipo alipokubali

siku ya kwanza alianza na mmoja wa watu wa kiongozi wa zamaliom kumpeleka karibu na bwawa lile, na akapotelea hukohuko, akifanya hivyo basi anaona mabadiliko ya hali yake ya maisha kuwa ,mazuri, alianzisha mashamba na yakanawiri sana zaidi ya wengine.

zamu ilipofika ya kumpeleka zamalio aliambiwa kuwa amuue kwa mkono wake. Mapato kwa kuwa alifaidika na akapendezwa na yale mafanikio ambayo alikuwa anayaona haikuwa shida kwake. Majira ya usiku wakati wanaomlinda kiongozi zamalio wamelala, aliingia kiurahisi na kwenda kumvamia mzee zamalio, akamkaba mpaka alipohakikisha kuwa kafariki.

Aliondoka bila kufahamika, wale viumbe walimpongeza sana kwa kazi ambayo aliifanya na ndipo akaambiwa kuwa bado kazi ya kutunza siri. Iliwezekana kupelekwa taarifa kwa mtu mmoja tu na yeye anahitajika kutunza sana siri hiyo walimpeleka na nyakati hizo hakuweza kuogopa kwani kafanya nao kazi nyingi kunusuru maisha yake, Walimpeleka hapo bwawani katikati wakamuonyesha kitu ambacho kinafanana na pembe hivi, walimuambia kuwa hiki ndio siri ya mafanikio yako kikija kutolewa hapa huna maisha, pia hiki unaweza kutumia pale unapoona kuwa maisha yako yanaenda kubaya unafanya kazi ambayo itakuamuru ili upate maisha mazuri.

Baada ya mwaka kupita iliwekwa tangazo kwa wanakijiji wote kuwa yeyote atakayemfahamu muuaji wa mzee Zamalio ni ruksa kumuua kwa muda wowote apatikanapo, na kila kizazi kijacho basi hii kauli iliweza kulithishwa jambo mapato hakutambulika kama ni yeye ndie muhusika.

Ujio wa bwana sikujua ndani ya kile kijiji akiwa na baba yake enzi hizo, mapato ndie aliwapokea kwa kuwa yeye pekee ndie alionekana kuweza kuwahudumia wenye shida hivyo aliweza kuwakaribisha, waliishi kwa muda lakini vitendo vya mapato vilimfanya baba yake sikujua afahamu kuwa ni mtu wa aina gani, hivyo baada ya uchunguzi wao kwa wao waliweza kumjua na yeye mwenyewe akakiri kuwa kweli na akawa hadithia, baada ya kupatwa kwa umauti baba yake sikujua walianza kuishi kama ndugu. Mpaka wanafikia miaka ya waliyopo yanampata sikujua kumbaka binti sikitu na kumuua mama mengi, basi mapato alibaki kuumia akikumbuka msaada wa baba yake sikujua mpaka kumfanya atoke kwenye himaya ya watu waliokuwa wakimtumikisha kuua watu, ndipo pia ikawa sababu ya kuvunjika jina la SONGAMBELE na kuitwa BWAWANI ili iwe rahisi kukumbuka pindi mtu akikatazwa kuwa asikaribie lile bwawa.

Wakati anaendelea kukumbuka bwana mapato yaliyopitahttp://deusdeditmahunda.blogspot.com/

alishtushwa na mkewe ambae alimuita kwa ajili ya chakula, kipindi hikohiko mambo sasa anafika kwa mapato,

Upande wa KILIMALONDO binti LYOTO alionyesha maajabu mpaka bwana KATUNJE na Mzee KAUZIBE walifurahi sana siku hiyo........







Ndani ya kijiji hiko cha kilimalondo, ambako alipatikana binti lyoto akitibiwa na Katunje pamoja na Mzee kauzibe. Majira ya mchana lyoto akiwa peke yake, katunje alifanikiwa kumuona akipikicha macho yako na kutazama kitu kwa makini huku akisogelea kwa ukaribu sana. Kitendo hiko kilimfanya katunje apatwe na bashasha kubwa sana kiasi ambacho alimsogelea zaidi ili amkague kama kweli kile anachhokifikilia ni kweli. alizidi kumshangaa huku lyoto akikisogelea moja ya kijiti kilichopo karibu na yeye lakini akiangalia kama wanavyoangalia kuku. Katunje alienda muda huohuo kwa mzee Kauzibe kumpasha habari ile. Hakika hata mzee huyo alifurahi sana kwani aliona matumaini ya dawa zake kuwa zinafanya kazi. walienda kumshuhudia wote kwa pamoja wakiwa kwa mbali walimuona akiendelea kupapasa vitu fulanifulani hivi, `Ina maana anaanza kuona japo nilidhani kuwa ni kipofu kumbe hata ni mzima kabisa binti wa watu' Aliongea bwana Katunje, Mzee nae alipatwa na hamu zaidi ya kumsogelea `katunje kumbe huyu binti ni mzuri hivi haki ya nani'. Katunje alivyosikia hivyo akamsogelea na kumuambia mzee huyo. `Hapana babu usiingiwe na tamaa kabisa huyu bado hajafikia hatua ya kufikilia wanaume, lakini hata hivyo wewe mtibie mambo mengine niachie mwenyewe' Ulikuwa kama utani ambao ulikuwa unaendelea kwa wakati huo, ndipo walipomkalibia na kuanza kuongea nae. 'Lyoto haya unaniona mimi babu yako?' aliuliza mzee kauzibe. lakini binti lyoto hakugeuka kabisa ndipo kauzibe akamgeukia katunje. `Mh bado masikio hayafanyi kazi ndio maana hajajibu' kweli alikuwa na matatizo kama kutosikia kutoona kabisa na mwili kudhoofika lakini kwa jitihada na hawa watu walijitahidi na kumsaidia mpaka sasa angalau anaonekana kuona mwili unaanza kurudi lakini tatizo kusikia. Kufikia hapo waliandaa utaratibu mwingine wa kumpatia dawa za kutosha ili aweze kuwa sawa zaidi kiafya. Taarifa za kuja kwa binti huyo ndani ya kijiji cha kilimalondo kilianza kutawala mwishoni huku ambako hali yake ilianza kuwa nzuri sasa. Hata watu walianza kwa kumshangaa baada ya kumuona nje ya nyumba ya katunje. Ndani ya kijiji hiko ambacho kuna kiongozi maarufu ambae wanamtumikia kama bwana, aliishi takribani miaka kadhaa na mkewe bila kufanikiwa kuwa na mtoto ambae angeweza hata kumsumbuasumbua, katika harakati zake na yeye aliweza kupata taarifa hizo za kufika binti huyo mwenye matatizo kadhaa ambayo alipatiwa na wale wanaomkusanyia habari na kumpatia. `KIMOLO njoo mara moja hapa' kiongozi huyo aliweza kumuita mmoja wa wafanya kazi wake waliopo pale ili aweze kumueleza jambo fulani, kijana huyo alifika pale karibu na huyo mzee. `Nimeitikia kiongozi wangu na pia nipo mbele yako kutekeleza amri yako utakayoniagiza' Alimhakikishia kiasi kwamba hata huyo mzee alifurahi. `vizuri kijana wangu, sasa naomba uelekee nyumbani kwa katunje ili ukamuangalie binti huyo na ikiwezekana mueleze katunje afike hapa haraka. Baada ya hiyo kauli hakukawia alitoka pale, hatimae alimkuta katunje akimkogesha binti Lyoto maeneo hayo ya kwake. Kimolo alifik Hdi pale karibu na kumpa ishara kama ya heshima katunje kama ilivyo kawaida ya hiko kijiji kuwa yeyote ambae yuko anatembea amsalimie aliyetulia au kukaa, na yule aliyekuwa akitembea mwendo mkali amsalimie mwenye mwendo mdogo au wachache wawasalimie wengi. Katunje alimuitikia lakini kwa haraka sana alimmaliza na akamshika mkono na kumuingiza ndani mgonjwa wake, baada ya kuhakikisha kuwa kamaliza ndipo akatoka na kufunga mlango na kumkaribisha kwenye moja ya viti vilivyomo karibu na pale kwake. `bwana Kimolo karibu sana sijui leo umekuja na lipi kutoka kwa mzee' alimuuliza huyo mjumbe aliyetumwa na kiongozi wake. Alionekana kushangazwa kwanza kabla ya kuanza na mzungumzo yoyote. `Ni kweli ujumbe kutoka kwa Mzee SWAI kuwa anakuhitaji ufike harka sana kule kwake ikiwezekana tuongozane sasa hivi au kama huna nafasi basi fahamu kuwa kesho ufike mapema.' Ktunje alishtuka sana baada ya hiyo kauli `Huyu mzee swai ananiitia nini kwake, tangu lini ananiita hakuwahi kabisa kufanya kitu kama hiki jamani'. Kimolo aliondoka mbele ya katunje na kurudi alikotokea, Katunje hakuridhika kabisa na lile swala kwani alihisi kuna jambo baya ambalo litafika mbele yake hivyo lazima aende kwa huyu mzee akapate ushauri kwanza. Siku ya pili yake kweli alijiimia kwa mzee kauzibe baada ya kuhakikisha kuwa lyoto kamuweka kwenye hali nzuri ya kiafya na mambo mengine. `babu jana kuna yule kijana mtumwa wa swai huyu anaitwa kimolo alikuja jana akaniambia kuwa mzee swai ananiita sasa mimi nashangaa kuna jambo gani kwani hajawahi hata kumleta mtu nyumbani kwangu sasa iweje leo anihitaji?' alimueleza bwana kauzibe. `sasa wewe una wasiwasi gani kuitwa na mkubwa wa kijiji hiki, nenda kwanza alafu msikilize kisha ndipo utajua unasemaje kutokana na hiko alichokuambia'. Kweli baada ya muda alifika kwa mzee swai na kuketi kwenye kiti ambacho alikabidhiwa `kijana nimekuita hapa lwa jambo moja tu, nimesikia kuwa unaishi na mtu ambae hakuwa hapa kabisa mwanzo yani ni mgeni'. Katunje akaona sasa ishakuwa balaa sasa. `Mh ndio ninaishi nae lakini ni mgonjwa kabisa hawezi hata kujitambua' mzee swai alimtazama kwa jicho la kumtamani sana kijana katunje, `sijali yeye ana hali gani, kwa nini unamleta mtu ndani ya kijiji chetu bila hata taarifa' Alishidwa kujibu kabisa swali lile ambalo aliulizwa na mzee swai. `Unakumbuka kuwa wewe ni mgeni hapa japo umekaa miaka mingi sasa unajulikana kama mwenyeji lakini mimi ndie niliyekukaribisha hapa iweje wewe hukuleta taarifa ya kuwa umakwenda kumchukua mtu ambae hatumfahamu kwanza anatokea wapi?'. Aliendelea kutundikwa na maswali mengi sana kiasi aliona kuwa kweli ana makosa kwa kutokupeleka taarifa kwanza na ili aweze kupewa ruhusa ya kukaa nae huyo binti, `sawa mzee wangu nimekosea kabisa kufanya hilo jambo lakini sikuwa na budi kufanya hivyo kwani ilikuwa kwenye mazingira ambayo sikuyategemea ndani ya kijiji kimoja kinaitwa bwawani'. Alipomaliza kueleza kutokana na swalli ambalo aliulizwa ndipo akatulizwa asiendelee kusema lolote kwa muda huo. `ngoja katunje, kwanza una makosa ya kumleta mtu bila taarifa pia tunaogopa kutuletea ugomvi na watu wanaommiliki huyo mtu sasa naomba utuletee huyo mtu kesho na sisi tutafanya juhudi kumrejesha kule alikotokea tunao usafiri hapa na watu na wewe ukiongozana nao'. Katunje aliruhusiwa kurudi huku kichwa chake kikiwaka moto kwa mawazo makubwa sana juu ya binti yule aliyemzoea na kumfanya kama nduguye au mtoto wake kabisa, `Ina maana nikubali kweli kumpeleka kwa bwana Swai hivi wanatambua nguvu niliyotumia kumsaidia huyu na wanajua kweli wakimpeleka huko atakuwa kwenye hali gani aaah aaah hapana siwezi'. Alijiongelea mwenyewe huku akiwahi nyumbani kwenda kuhakikisha kama lyoto atamkuta salama, kweli aliweza kumkuta salama usalimini akiwa na bwana Kauzibe, ndipo alimhadithia yaliyotokea kule alikotoka kuhusu wao kumhitaji yule binti ili wamrejeshe kijiji cha bwawani ili kuepusha ugomvi na watu ambao wanammiliki yule binti. Mzee kauzibe alishtuka lakini alionekana kama mwenye kufahamu jambo fulani hivi. `unajua katunje, mimi kama nilifahamu hilo kwani yule mzee tangu awe kiongozi na kumuoa yule mwanamke wake hawajawahi kumpata mtoto, sasa unakumbuka kulitokeaga ugomvi mkubwa hapa kijijini miaka kadhaa iliyopita' Alivuta kumbukumbu kijana Katunje `Aaaaah! sawailikuwa mzee swai na mzee Korongo,' `Haswaaa kumne una kumbukumbu nzuri ule ugomvi japo mzee korongo alifariki ilikuwa njama za mzee huyu lengo lilikuwa mke wa korongo apate mimba alafu mtoto atakayezaliwa ndipo amchukue mzee swai na awe wake jambo ambalo mzee korongo hakutaka kabisa sasa naona kama lina amia kwa huyu binti lyoto' Katunje alishtuka sana kisha akagundua mpango mzima ambao mzee swai anataka kuuucheza kwa mara ya pili baada ya kuushindwa kwa bwana korongo. `sasa babu hapa nifanye nini kuepukana na huyu mzee mana kasema kesho nimpeleke' `Hapana usimpeleke cha kufanya wewe mlete kwangu alafu nyumba yako ufunge wakati huo wewe na mimi tukipanga jinsi gani ya kumuweka salama huyu binti na pia tufanye juhudi ya kujua kwake na wazazi wake'. Wazo la yule mzee alilikubali kwa asilimia karibia zote bila upingamizi alikubali na kumuahidi kuwa atafanya hivyo kunusuru maisha ya binti lyoto. Kwa upande wa kijiji cha bwawani mzee Mapato baada ya kumaliza chakula ambacho aliandaliwa aliamua kupanga safari ya kwenda kule bwawani japo haikufahamika anataka kwenda kufanya nini, kabla hajaenda aliitwa na mtu nyuma yake, alivyogeuka alimuona kuwa ni Mzee sikujua alishtuka sana kwani alisha anza kumuogopa sana kwa nyakati hizo. alimsogelea na kumuuliza kipia mbacho kamuitia, `mapato najua unaanza kunigeuka ila jua kuwa mimi sifanyi kwa makusudi lakini najiokoa kwa aibu nitakayoipata yule mama alikuwa kidomodomo sana lakini sikuwa na jinsi' aliongea mzee sikujua kumueleza bwana mapato. `Aaah sikujua mimi na wewe tena hatuna shida kabisa usijali'. limsogelea na kumkumbatia ili kumuondoa kwenye mawazo ambayo alikuwa nayo kwake. Sikujua alikubali na yeye kumkumbatia kisha wakafuatana umbali flani na kuanza kuongea jambo fulani, `sasa sikujua ujue ulivyonikumbusha kuhusu miaka iliyopita nimekumbuka mengi sana, sasa nikaona kuwa niende kule bwawani kuna kitu ambacho niliambiwaga kuwa nikiwa nacho hiko hali ya maisha yetu hapa yatabadilika kabisa'. `Mh yani unataka kwenda wakati baada ya kwenda kule kwa mzee manyenye ili tuonekane nisijulikane kuwa kama ni mimi ambae niliyafanya yale. Baada ya siku hiyo kupita, mazishi yalifanyika huku mzee manyenye hali yake ikiwa inaendelea vyema, kwa upande wa bwana Mambo sasa alidhamilia kuhama pale na kutaka kurudi kijijini kwao shimomo yeye na mke wake. Alikubali kabisa kuacha lile shamba la mikorosho na kuwaachia watoto wa mzee manyenye na kuepusha ugomvi ambao aliwaza kuwa utakuja kutokea, kila mmoja ndani ya kijiji kile aliweza kujua kuwa mzee mambo sasa anaondoka pale kijijini. Majira ya jioni akiwa mazingira ya kwake alijiwa na kijana mmoja hivi alikuja na kumpa taarifa ambayo ilimsisimua mwili na kupatwa na shauku ya kujua. Kwa upande wa kijiji cha kilimalondo, katunje alimchukua binti lyoto na kuondoka nae akielekea kwa bwana kauzibe, lakini kabla hajafika kule aliweza kusimamishwa na mama mmoja ambae alikuwa njiani mithili ya mshumaa akimsubilia yeye apite pale. `mama shikamoo' alimsalimia mama huyo `marahaba samahani ebu njoo kwanza hapa unaelekea wapi?' Aliulizwa swali huku akiwa kambeba lyoto.. Katunje hakumficha chochote mama huyo kwa kuwa anamfahamu vizuri kipindi chote ambacho kaishi pale. `Mh! hapana naomba usimpeleke huyo binti kwa huyo mzee cha kufanya njoo umuweke nyumbani kwangu, huyo mzee si mtu mzuri kabisa nakuambia'. Katunje alishangaa sana kuambiwa kuwa mzee kauzibe kuwa si mtu mzuri kwa nini? alimuuliza `kwa nini unasema mzee kauzibe ni mbaya na wakati nilikuhadithia kuwa huyu aliyemtibia ni yeye mpaka kufika hatua hii unayomuona' Mama huyo alizidi kumsisitizia sana `Katunje najua huwezi kuniamini kwa nini nakuambia hivyo, sasa njoo umuweke nyumbani alafu wewe nenda kaangalie kwa mzee kauzibe kama kuna usalama ukiukuta njoo umchukue niamini'. Hakutaka kupoteza muda kwani siku hiyo ndiyo aliahidiwa kuja kuchukuliwa baada ya kutompeleka kwa ridhaa yake, alifika hadi kwa mama huyo na kumuweka ndani na yeye akaondoka kwenda kwa mzee Kauzibe. Hatimae anafika karibu na njia hiyo lakini hakuamini macho yake baada ya kumuona kijana wa mzee swai yani Kimolo akirandaranda maeneo ya nyumba ya mzee kauzibe pia akamuoana mzee kauzibe akitokea ndani na kufuata njia ambayo alikuwapo yeye. Alijificha na kumuangalia anakoelekea, "Kauzibe unaelekea wapi sasa ". kijana kimolo aliuliza swali kumuuliza mzee kauzibe "nimewaambia mjifiche hapo naenda kumuangalia kwake kule ili nije nae hapo mbona mnakuwa na haraka". Hapo ndipo chozi lilianza kumtoka kijana Katunje huku akiwa haamini kwa lile analoliona kusalitiwa na mzee ambae alipata kumuamini kwa asilimia zote.......





Kijana Katunje chozi liliendelea kumtoka pale alipo na asijue nini afanye, akifikilia kuwa yule mzee ndie ambae alimsaidia kwa kila kitu mpaka hali ya Lyoto inaelekea kuwa sawa kabisa sasa iweje leo aweze kumgeuka kiasi kile alishindwa kuamini. Alijitoa pale kimyakimya hadi kwenye nyumba ya yule mama ambae aliweza kumsaidia kumpa taarifa kuhusiana na bwana Kauzibe kuwa hana roho nzuri. Alipofika alifanikiwa kumkuta mama huyo akimnawisha maji ambayo ndani ya chungu ambacho kimehifadhi maji hayo yalikuwa yamechanganywa na majani ambayo hakuyatambua kabisa ni majani ya aina gani. Hakutaka kuhoji kwanza ndipo akaa chini huku uso wake ukiwa umejaa makunyazi kwa hasira kubwa, "Vipi mwanangu katunje nipe taarifa huko utokako". Aliuliza Mama huyo, "Mama wee acha tu yani sijui bila wewe kunipa ile taarifa sijui ingekuwaje mpaka sasa hali ya huyu mtoto, ukweli nimemkuta kauzibe lakini maneno niliyoyasikia na yale niliyoyaona ni ukweli mtupu kuwa ni mtu mbaya". Mama huyo alivuta pumzi na kumshika bega katunje kisha akamueleza "Mwanagu dunia ya sasa si kama enzi zile za wazee wetu ambao walikuwa wanafahamu thamani ya mtu kama huyu, si kila ambae atakusaidia basi ujue kuwa anakusaidia kwa moyo mmoja wakiwemo basi ni wachache ila wengi wao wanadhamila fulani ndani mwake baada ya kukupa huo msaada wao". Kauli za mama huyo zilimuingia barabara kijana Katunje huku akitikisa kichwa kuashiria kuwa anaelewa vyema. Pia aliweza kuuliza kuhusu yale maji ambayo alimkuta nayo akimnawisha mgonjwa huyo. "Mama sasa hayo maji yanahusiana na nini". aliuliza katunje, "Mh haya ninamnawisha baada kumgundua kuwa ana tatizo la kutoona lakini haya yatamsaidia kabisa hadi anafikia hatua nzuri ya kuona". Katunje alimuaga yule mama na kisha akatoka na kwenda zake kule anakoishi kwenda kuangalia mazingira yaliyopo. Alifika kwa bahati nzuri alimkuta mzee kauzibe akiwa anamsubiri kwa muda mrefu, kauzibe alipomuona tu katunje alinyanyuka kutoka pale alipoketi na kumuwahi katunje na kumpa habari kama mgeni aliyemsubiri kwa muda mrefu bila mafanikio. "Katunje unafanya nini sasa mpaka sasa hukumleta mtoto kule nyumbani unajua kuwa wanakutafuta kijiji kizima hapa". Alibaki kumuangalia tu bila kumjibu huku akimmezea mate, alikumbuka asionyeshe sura ya ukauzu ili asije kuharibu vitu "Babu usijali nimemhifadhi sehemu salama kabisa haina shida kwa hiyo". Kauzibe alimsogelea katunje huku akionekana kuwa na mshangao mkubwa sana juu ya lile swala, "Unasemaje haya umempeleka sehemu salama wapi?". Aliuliza kauzibe. "Babu elewa kuwa nimemuweka sehemu salama lakini pia wewe si ulitaka aletwe kwako ili afichwe sasa tatizo nini hata huko nilikomuweka yuko salama". Alitikisa kichwa akiwa haamini kwa lile alilokuwa akilisikia kutoka kwa kijana huyo katunje na kumfanya apatwe na hasira ya ghafla. "yani wee kijana unaniweka sehemu mbaya mimi kwa nini hukufanya jinsi tulivyokubaliana sasa unadhani kule nyumbani zile dawa nani akazinywe na wakati nimeziweka kwa ajili yake yeye, eeeh!" Alifoka sana hapo ndipo katunje aliamini maneno ya yule mama. Ghafla kundi moja la vijana takribani saba walifuatana huku mbele akionekana kijana shupavu kutoka kwa Mzee Swai anaejulikana kwa jina la Kimolo. Huyu kijana Mzee Swai anamuelewa sana kuliko hata mtu yeyote kwani ndie anamsaidia katika kazi zake muhimu, Mzee kauzibe aliwaona lakini hakutaka kumsitua katunje, Ndipo kwa msaada wa masikio yake ambayo yalihisi kusikia sauti za miguu ambayo ilikuwa inakaribia kwa kasi ndipo aligeuka na kuwaona wakija huku wameshikilia mishale na mikuki yao. Katunje alijua hapa hakuna usalama kabisa wakati anataka kujaribu kukimbia alidakwa kwa haraka sana na vijana hao na kutiwa mikononi mwa kijana Kimolo, ambae jinsi alivyo akimshika mtu ni ngumu sana kutoka mikononi mwake. "Vijana nendeni humo ndani kwake mkaangalie kamuweka wapi huyo bionti", Walitoka na kuanza kuangalia ndani kote hatimae wanatoka na zile nguo ambazo alikuja nazo Lyoto zikiwa ndani ya tenga. Walikuja nalo hadi pale kwa Kimolo na kumpatia. "Kimolo, hivi ndivyo tumevikuta humo ndani," walimpa taarifa hiyo. Katunje alishangaa sana kwa nini Mzee kauzibe anaachiwa na kupewa nafasi ya kuondoka pale alafu yeye ndie kashikiliwa. "Twendeni atakwenda kusema huyu wapi kamuweka hawezi kutufanya sisi kama wajinga namna hiii" Mwendo ambao alipelekwa kwenda kwa swai haukuwa wa kawaida alipelekwa kama mwizi. Upande nyumba ya yule mama akiwa ndani na binti lyoto akimpa baadhi ya matibabu, alishangaa utokaji wa katunje mpaka muda ule hakuweza kutokea ilimbidi afunge mlango akimuacha ndani humo lyoto akiwa kalala, aliongoza njia ya kwenda kwa kijana katunje ili aweze kwenda kujua nini kimemtokea. Akiwa njiani anakutana na mama mwingine ndipo wakaanza kusalimiana, "Mama MWAIJA mbona kanga kiunoni wapi tena?" Mama huyo aliyekuwa anaelekea kwa katunje aliulizwa. "Mwenzangu kweli kuwa uyaone naenda kwanza kwa katunje pale kuna swala tulikuwa tunaliongea muda fulani si unajua kuwa Mwanangu Mwaija ndie atakae muoa yule baadae". Walianza kucheka kwanza. "Mh! lakini nadhani huna taarifa kuhusu katunje zilizomtokea " http://deusdeditmahunda.blogspot.com/Alishtuka kitendo kilichomfanya aache kucheka kwa bashasha kutokana na utani ambao waliufanya muda mchache uliopita. "Mh! hapana nini ebu nieleze kuna nini tena kilichomtokea?". Walijikuta wanaingia kwenye dimbwi la simanzi zito kwa pamoja, "Wakati niko njiani kuelekea kisimani nikaliona kundi likija mbele yangu, nilipowapisha kumbe walikuwa vijana wa mzee Swai yani yule Kimolo wakimburuta Katunje sasa sijaelewa kafanya nini?" Kauli hiyo ilimfanya Mama MWAIJA kutoamini kwa kile ambacho kakisikia kutoka kwa rafiki yake huyo. "Sawa ahsante kwa taarifa ngoja niende nyumbani tutaongea kesho". Waliachana pale kila mmoja akaelekea njia yake. Mama Mwaija alichoamua ni kufika hadi kwa mzee Kauzibe ili amdadisi chanzo nini kilichomfanya ashikwe na bwana Swai kipi alichokosa zaidi. Uelekeo wake haulkuwa na faida sana kwani hakumkuta mlengwa aliyemkusudia, aligeuza na kuelekea nyumbani kwake. Upande wa Mzee swai walichokifanya ni kumfunga makamba ya kutosha mbali na himaya ya nyumba yake hiyo. Mzee huyu anajulikana kama ni Mtemi ambae alichukua uongozi kwa nguvu na kutaka kuongoza vitu vyote yeye kama yeye binafsi. Walianza kumtesa kijana Swai huku wakimlazimisha aseme wapi kamuweka binti lyoto, Kwa ujasiri aliokuwa nao kijana huyo alikubali kuumia lakini si kuruhusu Lyoto aingie mikononi mwa watu hawa. Waliendelea kumpa mateso mpaka Katunje akatoa siri. "Jamani nataja ila naomba msimfanye chochote ndugu yangu,". walimcheka sana tena mbele ya Kimolo hapashindikani kitu. "Haya sema haraka kabla hatujakumaliza hapa" "Jamani binti nimemuweka kwa mama Mwaija". Kwa kuwa ilikuwa ni usiku hawakutaka kwenda waliacha na kuhitaji asubuhi waende kumchukua huyo mtu, baada ya kutajiwa wapi anapatikana, jamani mateso kama huna uvumilivu utaongea chochote ambacho utatakiwa kusema. Majira hayo ya usiku, mlinzi mmoja alimuonea sana hruma kijana Katunje, hivyo alimuendea na kumshika mkono pale alipofungiwa, Katunje alishtuka kwani alijua anakuja kudundwa tena ndipo alipomziba mdomo na kumnong`oneza masikioni mwake, "Usipige kelele nimekuja kukusaidia utoke hapa". Katunje alitikisa kichwa mbele na nyuma mara kadhaa kuonyesha kukubaliana na lile swala. Alimfungua kisha akamuonyesha njia ya kupitia ambayo hapakuwa na wale walinzi wa mzee swai. Majira hayo kijana alichanja mbuga zote hadi kuingia Kijijini kabisa kwani alipita njia ya nje ya kijiji kutokana na nyumba ya mzee swai ilivyojengwa na nafasi ya kutoroka pale. Wakati huo mlinzi huyo aliona atajulikana kuwa yeye ndie aliyemruhusu kwani alipewa kazi ya kumlinda asiweze kudhurika na wanyama wala kukimbia, alichukua kisu chake na kujikata mguuni pamoja na mkononi huku damu zikimvuja alianza kupiga yowe la maana pale akiomba msaada. Baadhi ya walinzi waliamka na kuanza kuangaza nini wafanye, Ndipo bwana Kimolo akafika na kumuuliza kipi kimetokea. "Kimolo kijana aliomba maji ya kunywa, nilikwenda kumpa ndipo akanipiga kichwa huku akanipokonya kisu na kunikata humu kisha akakimbia njia hii", Aliongea pasi na kuogopa ule uongo ambao alikuwa akiutunga mbele ya mtu mbaya kama Kimolo asiye penda mzaha ndani ya kazi. Alicheka kisha akasema kuwa haina shida kwa kuwa tayari wanafahamu wapi kawekwa hivyo watamfuatilia huyo mama. Majira hayo katunje alifika hadi kwenye nyumba ya mama Mwaija na kugonga mlango kwa nguvu sana akiomba afunguliwe, mama huyo alifungua kwa haraka na kumuingiza ndani haraka na kuanza kumhoji kulikoni majira yale ya usiku. "Mama nimetoroka, nimetoroka " Alisema huku akiwa mwenye jazba "Umetoroka?" Alishangaa mama mwaija. "Hali yangu mama si nzuri sasa namuomba LYOTO niende nae kujificha polini usiku huu kabla hata asubuhi hakujafika". Mama Mwaija alianza kukataa sana haitowezekana kwani ni usiku na kwa nini aende na binti huyo? "Naomba unielewe kama nilivyokuelewa mimi mwanzo tunakuja humu ndani, fahamu kuwa nilipewa adhabu kubwa baada ya hapo nikafanikiwa kutoroka lakini nilimtaja kuwa hapa kwako ndiko umemhifadhi mtu huyu, sasa asubuhi watakuja hapa wakimkuta lazima watamchukua na sijui wanaenda kumfanyia nini". Mama hakuwa na kipingamizi chochote juu ya hilo alimkusanyia baadhi ya dawa na kumpatia nguo nyingi ili amhifadhi na baridi. Japo na maumivu aliyo nayo alikubali kumbeba na kuondoka nae maeneo ya polini mbali sana na pale kijijini. Majira ya asubuhi msako ulifanyika lakini hawakuambulia kitu chochote. Ndani ya eneo la mzee Swai anafuga mbuzi wengi sana. Kijana mmoja ambae hufanya kazi kwa mzee huyo ya kumuuzia mbuzi wake siku hiyo alifika pale akiwa na baiskeli yake alimshika mbuzi ambae alihitajika siku hiyo kuuzwa, Kwa bahati mbaya hapakuwa na kitu cha kubebea ndipo KIMOLO akampatia lile tenga na zile nguo ambazo alizifanyia kama kamba baada ya kuzichana na kumfungia miguu mbuzi huyo. Safari hii ya kijana huyu muuza mbuzi wa Mzee Swai ilienda mbali sana huku mbuzi wake akiwa ndani ya tena hilo, hatimae anaingia ndani ya kijiji cha BWAWANI huku akimnadi yule mbuzi. Huwa anasafiri mbali sana ili apate kuuza kwa beim kubwa na sehemu ambayo ni nadra kupatikana mbuzi. Watu walianza kufika taratibu pale uwanja wa matangazo ambapo aliruhusiwa kutangaza bei ya mbuzi huyo na kufanya mnada. Kwanza alimtoa ndani ya tenga lile na kumfungua kamba ya zile nguo. alimfunga kamba ya shingoni na kumuweka kwenye mti uliokaribu na hapo. Hakika mbuzi alinona na watu walimsifia sana. Kwa mbali wanaonekana marafiki wawili MAPATO na SIKUJUA wakiwa wanakaribia pale "Bwana wee acha utani ngoja nikaangalie bidhaa tunaweza kumnunua mbuzi na kumchinja kisha tukamla na wanakijiji ili wasituone wabaya bwana au unaonaje" Alisema bwana Sikujua. Walifika pale na hapo vilevile Mzee Mambo sasa alifika ili apate kujua nini kinaendelea. Hapakuwa mbali sana nae SUSU anaingia akiwa na shauku ya kujua nini kinaendelea. Susu alishtuka sana baada ya kuliona lile tenga alilifananisha kama lile ambalo lilipotea kipindi cha muda sana kwa bwana Sikujua, nae Mee Sikujua aliliona lile Tenga na kulifananisha na lile ambalo walienda kumtupia SIKITU. Kwa upande wa Mzee Mambo sasa alimuangalia sana yule mbuzi miguuni kwa ile nguo ambayo alifungiwa nayo, machozi yalianza kumtoka baada ya kuvuta taswira kuhusu mwane kupotea. Ndipo Mzee MANYENYE akajitokeza kumnunua yule Mbuzi na kijana akafunga tenga lake na kutaka kuondoka, kabla hajaondoka ndipo susu alimfuata na kumuuliza jambo "Kijana unakaa wapi mana unauza Mbuzi wazuri sana", Susu aliuliza "Mimi naishi KILIMALONDO tena karibu japo mbali ukifika uliza kwa Mzee Swai utanipata". Walipeana mikono na kijana akaondoka zake, upande wa Mzee Mambo sasa alimfuata mzee Manyenye hadi kwake, alipofika alimsalimu kisha akaenda hadi miguuni kwa mbuzi na kumfungua lile guo lililochanwa na kusema, "Hakika mwanangu bado naamini yuko haiiii". Mzee Manyenye alishtuka kuambiwa yuko hai "Wee yuko hai una maana gani kusema hivyo?". "Ndugu naamini yuko hai amini hilo kwa sababu hii nguo ndio mara ya mwisho alivaa hii hatimae leo naiona kipande cha kitambaa mwananguu kama upo popote hakika nitakutafuta". Upande wa Mzee sikujua hakuamini alimueleza mapato alichokiona kuhusiana na ule mnada wa leo uliowajia pale kwao.







Bwana sikujua alifikia hatua ya kuhamaki kabisa kwani jambo ambalo limetokea punde lilimfanya kuathirika kisaikolojia kabisa, kwa upande wa mzee mapato alifikilia jambo fulani ndipo akamsogelea na kumshika bega huku akimueleza jambo fulani. "Unajua hapa kuna kitu ambacho nakihisi kipo na tusipokichukulia hatua mapema basi tutajikuta tunaingia sehemu mbaya". aliongea bwana mapato akimueleza rafiki yake kwa jambo ambalo alilifikilia. "Mh! unadhani mimi kuna kitu ambacho nitakipinga mbele yako kwani najua wewe pekee ndio msaada wangu mkubwa sana kwa sasa" na yeye alimtoa wasiwasi na kumuahidi kuwa anamuamini sana kuliko kitu kingine ndani ya kijiji cha bwawani, Wakati wanaendelea kuongea wakati huo ndipo anajitokeza kijana susu ambae alipita kama njia na kuwakuta wazee hao wakiongea mada ambayo alihisi kama inamhusu, Alijibanza mahali huku akiwa makini katika kusikiliza kile ambacho wanakiongelea wawili hao, alibaki kushika mdomo tu kwa yale ambayo alikuwa anayasikia. "Sasa bwana sikujua unajua mpaka sasa baada ya kumpoteza mama Mengi basi hakuna mtu yeyote ambae atajitokeza kuonyesha anatambua jambo lolote katika lile". Susu baada ya kusikia hayo alishindwa kuamini kabisa kwa yale ayasikiayo ndipo mwili wake ulianza kubadilika na kuanza kutetema kwa hofu iliyochanganywa na hasira kubwa sana. `ina maana hawa wazee wanahusika kwenye mauaji ya mama mengi?". Kwa bahati mbaya hayo ambayo alikuwa anayaongea ilimfanya kutoa sauti ambayo iliwafikia vyema wazee hao wawili, "Mh! kuna mtu anaongea huku nyuma ya nyumba". Aliongea bwana sikujua, "Ngoja nipite huku" Mzee sikujua alitoka kwa haraka sana na kuzunguka upande wa pili na hatimae akamkuta kijana susu kajiinamia akijitega kusikiliza. Sikujua alichukua gongo la mti na kumtwisha nalo kichwani kitendo kilichomfanya susu kutoa ukelele mdogo sana ambao haukuwa rahisi kuusikia kabisa hatimae akaanguka chini na akazimia palepale. Alirudi na kumpasha taarifa rafiki yake, "Mapato njoo haraka sana njooo" Mapato alishangaa kuitwa vile haraka sana kuna nini, "Nini tena?" aliuliza mapato. "sasa huyu kijana alikuwa anatusikiliza mwanzo hadi mwisho na unajua allivyo msumbufu sasa nimemtia adabu kinachotakiwa sasa tumuweke ndani humo haraka sana". Walifanya hivyo lakini huku mzee mapato akihofu sana juu ya lile swala ambalo mwenzake kalifanya bila hata kumshirikisha. "Yani ndugu yangu sasa unazidi kabisa kwa hatua hii mbona unafanya vitu vya hatari hili halijaisha unalileta lingine jamani aaah!". Walimuingiza ndani kisha wakamfunika mahali huku wakimfunga kamba. "Mapato bila hivi haki ya mungu huwezi kuishi vizuri kabisa hawa ndio ambao wanatufanya tuishi kwa wasiwasi hapa kijijini hatuna raha kwa ajili ya hawa vinyago bwana na nasemaje yeyote ambae atajifanya kunifuatilia au kufuatilia kesi hii basi halali yangu". Kwa upande wa mzee MANUALI mjukuu wa Susu ilifika mpaka mpaka jioni kwenye nyumba ya mjukuu wake hamuoni kabisa. Alianza kupatwa na wasiwasi mkubwa juu ya huyo mjukuu wake, ndipo alipoanza kutembea kijijini hapo na kuulizia kwa kila kijana mwenzake. "Jamani hamjamuona susu majira haya?" alimuuliza kijana mmoja ambae alijulikana kwa jina la NDUNYA. "Babu hapana japo susu ni rafiki yangu sana kwani tangu tuachane pale uwanjani kwenye mnada wa mbuzi nilimuona tu akiongea na yule kijana aliyekuja kuuza baada ya hapo sijamuona tena" Mzee alianza kuchanganyikiwa "Ndunya unajua kuwa leo ni kitu cha ajabu sana kwani hakuna hata siku moja ambayo alifika mpaka sasa hivi yani kuchelewa kurudi". Ndunya alisikitika sana baada ya kusikia taarifa hiyo. "lakini babu susu ni kijana mkubwa sasa si wa kumfuatilia sana labda tusubiri kesho mimi asubuhi nitakuja mapema sana ili nijue kama karudi au laah alafu tutajua nini la kufanya". Mzee huyo alikubali na akarudi nyumbani kwake lakini hakuamini. Kijana Ndunya alianza kutembea katika kila eneo ambalo alijua kuwa lazima susu atapatikana lakini hakuweza kupatikana, alifika hadi hadi kwa mzee Mambo sasa na kumueleza jinsi mzee manuali anavyohangaika kuhusu kijana wake Susu, "Ndunya una maanisha kwamba?" aliuliza mzee mambo sasa "Ninacho maanisha kuwa mzee Manuali analalamika kuwa kijana wake susu hajamuona mpaka sasa hivi. Kwani sio kawaida yake kuchelewa kurudi lakini pia hata mimi sijamuona" alimueleza kila kitu. "Mh! hivi haya mambo mpaka lini jamani ila itabidi lifanyike jambo sasa". Ndunya aliondoka na kwenda nyumbani kwake. Asubuhi na mapema sana, alionekana kijana Ndunya nyumbani kwa mzee Manuali, jambo la kwanza alifika kwenye nyumba ya kijana susu na kukuta kufuli alishangaa sana ndipo akaenda kuchungulia dirishani lakini hakuona chochote kabisa. Ndipo akamgongea mlango mzee Manuali, alipotoka ndipo akamueleza kitu, "Mzee kuna kitu hapa ambacho nahisi sio kizuri susu hayupo kabisa mlango wake umefungwa pale". Mzee manuali alikaa kwa muda kidogo kisha akaanza kufuta machozi yake, "Mjukuu wangu susu ni kijana ambae alikuwa ananisaidia sana katika kazi zangu za utabibu hapa nyumbani, sasa sijui hata nifanye nini". Mala muda mchache anafika mzee Mambo sasa akafika na yeye kuungana na huzuni hiyo iloyomkumba bwana Manuali. Walijadili jinsi gani watalifanya kabla hata hawajatoa taarifa. Asubuhi hiyo ndani ya kijiji cha KILIMALONDO anaonekana kijana KATUNJE akiamka huku pembeni akiwa na binti LYOTO, "Daah haya maisha sasa niliyoyaanza sasa itakuwaje " Alimuangalia yule binti kwa muda sana kisha akajiuliza "Mh! sasa kwa nini nilikubali kumchukua huyu mtu na huku anakuja kuniletea matatizo kama haya au nimuue kabisa ili niondokane na haya". Alifikilia sana kwenye swala la yeye kutaka kumuua binti huyo. Alisimama na kutembea mbele kidogo na kuchukua gongo kubwa sana la mti. Alilinyanyua na kumsogelea binti lyoto na kutaka kumshindilia jiti hilo kichwani ili amuue kabisa ili aepukane na yale ambayo aliyafikilia. Ndipo lyoto akageuka huku akijinyoosha akitoka usingizini jinsi alivyo lyoto ilimfanya Katunje afiche lile gongo na kulitupa pembeni. Alianza kulia sana na kumkumbatia binti huyo kwa uchungu mzito alio nao, Alimuinua na kumkalisha huku akimuangalia kwa makini sana.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/ "Mbona unataka kuniua nimekosa nini?" , Ilikuwa ni ajabu sana kusikia maneno ambayo yalimtoka lyoto kumwambia katunje. "Ina maana unaona sasa hivi?" Katunje alishindwa kuamini kwa lile ambalo alilisikia kutoka kwa lyoto, kwani ana muda mwingi sana akiishi na tatizo lake la macho pamoja na masikio. "Mh! samahani sana lyoto siwezi kukuua kabisa naomba unisamehe na nakuahidi nitakulinda kwa kila hali mpaka hali yako inaporejea" Lyoto alikuwa anaonyesha dalili za kuona baada ya kuanza kuonyesha viini vya macho. "Ndio naona sasa hivi". Lyoto alijibu. "Kha! ina maana kuwa pia unasikia vizuri sasa hivi!" Alishangaa sana baada ya kujibiwa na lyoto. Nyumbani kwa Mzee Swai palianza sasa kuamka baada ya kutangaza rasmi kutafutwa kwa kijana Katunje. Ndani ya kijiji hiko watu waliambiwa tayari kuwa kwa yeyote ambae atahusika kumficha kijana katunje basi atapewa adhabu. Kwa upande wa Kimolo walifika kwa mama mwaija na kumkuta, walimbeba mkuku mkuku kutokana na kauli ya Katunje ya kuwa anahusika katika katika kumhifadhi Binti lyoto. Wanakijiji hawakuweza kuvumilia kwa hali ile ndipo maandamano yalianza. vijana wa kijiji kile walijiunga na kusambaa mitaani ili kuwafanya watu kupinga yale ambayo yanaendelea kutendeka. Walifika karibu najumba hilo la bwana Swai. "Uonevu hatuutaki kabisa jamani huyo mama wa watu kawakosea nini!". Maneno ya watu yaliendelea huku wakishinikiza katika swala la kuachiwa huyo mama ambae alikamatwa. Kimolo alimuendea mzee Swai na kumueleza jambo "Mzee unawasikia hao wanakijiji wanavyoongea huko" Mzee Swai alisimama na kusema "Hakuna kitu ambacho kitasababisha kunirudisha nyuma kwenye shughuli zangu hata kidogo ngoja niende hapo". Alitoka nje na kuwaona wakiendelea kuongea. "Nyinyi wanakijiji ebu kaeni kimya niwaeleze kitu" watu walikaa kimya na kumsikiliza. "Nataka niwaambie jambo sasa mnafahamu kuwa vijana ambao tumewakaribisha sasa ndio wanakuwa karibu katika kutuharibia utaratibu wetu wa hapa kijijini, sasa mmoja wa haya mambo ni kijana Katunje, tulimuita ili tumuulize kwa nini alichukua jukumu la kumchukua mtu wakati yeye mwenyewe ni mgeni hapa" Watu walianza kuelewa nini ambacho mzee swai anazungumza "pia nataka munielewe huyu mama ndie anahusika kumhifadhi huyo binti, tumemkamata ili atueleze wapi kamuweka na nyinyi nawataka sasa muelewe yeyote ambae atamkamata kijana huyo basi atapatiwa mifugo ya kutosha kutoka kwangu". Kwa upande wa katunje aliandaa sehemu nzuri ambayo iliweza kumhifadhi kisha akamuacha pale lyoto na kwenda kutafuta chakula kwani hawawezi kuishi pale bila kuwa na chakula, alitembea haraka haraka hadi karibu na kijiji chao kwa bahati nzuri alikutana na shamba la mihogo aliweza kung`oa mihogo kadhaa na kuondoka nayo. Alifika hadi kule eneo ambalo alimuacha lyoto na akaiweka chini. Walianza kutafuna taratibu lakini Lyoto alionekana kutoridhika na ile hali katunje alilitambua hilo ndipo akanyanyuka na akamueleza amsubiri kwa muda kidogo. Katunje aliondoka na kuelekea kijijini kwa uharaka ambao alikuwa anaufanya alifanikiwa kufika mapema katika majumba ya kwanza kabisa na kijiji chao, "sasa hapa nifanye haraka sana kupata sufuria kadhaa za kupikia". Alifika kwenye nyumba moja na kufanikiwa kuiba sufuria na baadhi ya mahitaji ambayo aliyakuta kule. Alirudi hadi kule polini ndipo alipoanza kuandaa na kupika mihogo ile, hakika lyoto alionekana kufurahi sana juu ya lile ambalo katendewa na kijana Katunje ambae alimfahamu kama ndugu pekee wa karibu sana. Hatimae mama mwaija anafanikiwa kutolewa bila hata kudhulika lakini taarifa ya kukimbia kwa kijana Katunje wengi wao wanaifahamu sana. Majira ya usiku wa saa nane katunje alifika kijijini kwao na kufungua nyumba yake na kuchukua nguo zake zote, wakati anatoka akiwa njiani alidondosha moja ya nguo yake bila kufahamu kwani alikuwa anafanya kwa uharaka sana, hakuishia hapo alifika hadi kwenye nyumba moja na kuiba kuku mmoja bila hata wenyewe kufahamu. Alipofika kule polini alimkuta bado lyoto kalala. Kwa kuwa alimfanya kama ndugu yake wa damu hivyo hayo yote aliyafanya kwa lengo la kumfurahisha lyoto na kumfanya ajisikie hali nzuri sana kwani hata hapo sasa mwili wake ulizdi kurudi na kuwa nzuri sasa. "Eeehee! huyu kuku ni kumchinja kisha asubuhi na mapema nampika, nishakubali kuwa maisha yangu sasa niyaweke hukuhuku mpaka pale lyoto akikamilika na hali yake." Aliyaongea hayo huku akimchinja kuku yule. Ndani ya kijiji cha Kilimalondo majira ya asubuhi Bwana mmoja aliyejulikana kwa jina la UDEVU kutokana na sehemu yake ya kidevu kuwa ndefu sana ndipo wakampachika jina la utani ambalo lilizoeleka sana na hata watu kumsahau kwa jina lake halisi la MWANYALI. Bwana kidevu alisikika akilalamika kuhusu kuibiwa kwa kuku wake mkubwa sana alafu jogoo, wakati huohuo mama mwaija anaenda kwenye nyumba ya Katunje ndipo anakutana na mzee Kauzibe. mama mwaija alishangaa sana asubuhi ile yote mzee huyu kafuata nini kwenye nyumba ya katunje. Alichoamua ni kukaa pembeni ili amuangalie kwa umakini nini ambacho anakifanya pale. Mzee kauzibe alisukuma mlango wa nyumba hiyo bila mafanikio, ghafla bwana udevu anapita maeneo hayo huku akiendelea kutangaza "jamani jamani, kuku wangu nimeibiwa na huyo aliyeiba basi naomba ajiangalie sana namhitaji kuku wangu". Hapo ndipo mama mwaija alimshuhudia bwana kauzibe akijibanza pembezoni mwa nyumba ya katunje. Alishangaa kwanza kisha alimuona bwana udevu akifika kwenye nyumba ile akigonga mlango bila mafanikio na kuondoka zake baada ya yeye kutoka ndipo kauzibe akajitokeza akiwa na gongo kubwa akiwa na nia ya kuvunja kufuli ambayo ilionekana pale mlangoni. Mama Mwaija palepale alijitokeza huku akikohoa kiunafiki ili ajue kama kuna mtu. Mzee kauzibe alipatwa na mshangao sana. "Aaah! mama mwaija kumbe upo hapa karibu ukiniangalia tu!". alisema bwana kauzibe. "Ndio hayo yote uliyoyafanya nimeyaona haya kinachokufanya asubuhi yote hii kuja kuvunja nyumba ya kijana aliyeijenga kwa nguvu zake nini?". Swali ambalo aliuliza mama mwaija lilimfanya ababaike sana kauzibe na kushindwa kujibu chochote zaidi ya kubung`aa m,acho tu. "Nakuuliza mzee wewe usiyekuwa hata na huruma, wakati unaona kijana anavyopata matatizo na wewe baada ya kumsaidia unamshindilia haaaa". Mzee Kauzibe hakuwa na la kuongea wakati huo ndipo akapata wazo la kumzubaisha mama mwaija "Mama mwaija alipo kauzibe mimi napafahamu, ndio maana kaniagiza nije kufungua mlango wake ili nimchukulie kitu ambacho aliniagiza". Mama mwaija hakuchoka kumuuliza maswali ambayo yalimfanya bwana kauzibe ashindwe kabisa kujitetea na hatimae na kuamua kuondoka, "sawa unaweza kunionyesha wapi alipo huyo katunje?" aliuliza mama mwaija " hapana siwezi kukuonyesha kwani hataki ajulikane wapi alipo". Kauzibe alijitetea "sawa mimi naenda kwa swai na kumuambia kuwa kauzibe anafahamu wapi katunje kakimbilia sasa ndipo utakija kuwatajia". Neno hilo lilimtoa kijasho mzee kauzibe na kumfanya kuanza kuangaika pale na asijue nini ambacho atakisema. Ghafla wanaoinekana vijana kadhaa wa mzee swai wakikaribia pale kwenye nyumba ya katunje, Baada ya kushuhudia jambo hilo wote waliondoka pale kuwaepuka watu hao ambao wanajulikana kuwa wakorofi sana. Kwa upande wa mzee swai alimuita kijana ambae anatumika katika swala la kuuza mbuzi wake, kwani huyu mzee alikuwa na mbuzi wengi sana. "Ehee kijana sasa hivi mbuzi unauzaga wapi?' Swai alimuuliza kijana huyo "Kuna kijiji kimoja hivi kipo mbali kidogo na hapa huko hakuna mbuzi kabisa inakuwa rahisi kufika tu na watu hununua lakini wanendelea kuwahitaji tena wengi wa kutosha". Mzee swai alimsifu na kumuahidi mengi mazuri sana katika kazi yake. Ndani ya kijiji cha Bwawani wanaonekana Mambo sasa na mkewe wakiondoka pale kijijini wakiwa njiani kuelekea kijiji kimoja kiitwacho Shimomo, walitembea kwa mwendo mrefu sana na hatimae wanakaribia kijiji cha shimomo. "Mke wangu sasa tunaingia ndani ya kijiji chetu cha shimomo kinachohitajika wewe ujikaze na ujiamini kama kutakuwa na kesi yeyote mimi ndie nitakae jibu" Mambo sasa alimueleza mkewe. "Sawa mume wangu ila naogopa sana wanaweza wakatufanyia mabaya zaidi ya yale ya kwanza." Mama sikitu aliongea kumueleza mumewe kuwa hofu yake ni ile ya kufanyiwa kama mwanzo. "usiwe na hofu pia naomba usidiriki kuniita jina la Mzee Mambo sasa tena nadhani jina langu litafaa huku ukiniita sawa?". Alimueleza mkewe kuwa asijaribu tena kumuita jina ambalo alikuwa analitumia kijiji cha Bwawani na badala yake amuite jina lake halisi ambalo analitumia "Mh! sawa lakini nilizoea lile jina ila nitajitahidi". Hatimae wanaingia ndani ya kijiji hiko na kukuta sherehe kubwa sana ambayo ilikuwa inaendelea pale. Mambo sasa alimuomba mkewe akae pembeni kwanza ili yeye akakague jinsi gani wanaweza kuingia pale ndani ya kijiji kile, wakati huo sherehe zimetanda kila kona watu wamelewa sana baada ya kunywa pombe za kutosha. Mama sikitu hakutaka kabisa kusikia swala la yeye kubaki pale alfu mumewe aende kule alichokihitaji yeye na mumewe waongozane hadi kule sehemu husika. Waliongozana wote kwa pamoja wakiwa wameshikana mikono, haikujulikana kwa nini na nini ambacho kiliwapata mwanzo. Walifika hadi kwenye nyumba ambayo waliifahamu kuwa familia yake ilikuwa pale kwa kipindi chote. Lakini hawakubahatika kukuta mtu mkubwa zaidi ya mtoto mdogo ambae baada ya kuulizwa aliweza kuelekeza wapi ambapo wazazi wameelekea. Walitulia pale na kumuacha kijana huyo mdogo akielekea kule ambako zilikuwa zinaendelea sherehe za pale kijijini. Baada ya muda ndipo anatokea mzee wa miaka kadhaa akiwa na yule kijana "Mke wangu kuwa na ujasiri baba yangu yulee anakuja". Kweli alisimama bwana Mambo sasa na kumfuata baba yake, hakika mzee huyo aliangua chozi kwa kutoamini kabisa kama aliye mbele yake ni mwane yeye. "Mwanangu CHITO mwanagu kweli umerudi mwanangu". Kumbe bwana Mambo sasa anafahamika kwa jina la CHITO japo haikufahamika kwa nini alibadili jina kwa kipindichote na ndio sababu ambayo ilimfanya amuambie mkewe asizoee kumjuita kwa jina la Bwana Mambo sasa. "Baba mim i mwanao nimerejea tenanaomba mnipokee baba yangu". Walionekana kuwa na huzuni wote kwa pamoja huku machozi yakiwatoka. walikaa mahali na kuanza kuongea, Mzee huyo aliwaondoa shaka kabisa kuhusu wao kupokelewa. "Mwanangu ondoa hofu kabisa mana yule mtu ambae aliwazuia nyinyi na kuwafanya hapa muondoke kafariki zamani sana, hivyo ikatufanya sisi kama wanafamilia kuanza kuwatafuta nyinyi mpaka sasa hatujafanikiwa lakini leo kama maajabu unarudi mwanagu". Mzee Chito alishtuka kidogo kutokana na kauli ya baba yake iliyosema kuwa "kuwatafuta nyinyi" ilimfanya kujenga swali hapo "Baba sijaelewa hapo kwmba mlikuwa mnahangaika kututafuta na nani?". "Mwanagu unanikumbusha mbali na hivi ninavyokuona furaha yangu inazidi kupaa hewani, nduguyo KATUNJE tangu hapa aondoke baada ya wewe kufukuzwa basi na yeye akakasirika akaondoka kabiosa na hatujui wapi ambapo kaenda na kila kijiji tumefika lakini hatukupata taarifa yeyote kuhusiana na yeye basi tukajua mmekufa wanagu". Hakika ilikuwa simanzi kubwa sana kwa chito. "Baba baada ya kutoka hapa nilibahatika kupata mtoto wa kike ambae tulimpa jina la mama yangu kwa kumkumbuka SIKITU lakini unyama wa kile kijiji tulichofikia basi wamemuua mtoto wangu hayupo yani kapotea kwa mazingira ya kutatanisha baba". Mzee huyo aliyejulikana kwa jina la MAMBO SASA mwenyewe, alishtuka kwanza "Mjukuu wangu wamemuua? kijiji gani hiko", aliuliza baba yake huku mkewe chito akiwa mbali akisikiliza tu bila hata kuchangia chochote. "Baba kinaitwa BWAWANI". Mzee alivuta taswaira na kumbukumbu kisha akauliza "Hakuna jina lingine la hiko kijiji?" Ndipo chito akakumbuka kisha akasema "ukweli sifahmu vyema hiko kijiji kwani hata sisi kukifikia tulipata tabu na muda mwingi lakini kina sheria kali ambayo ilikuwa inatukataza kuwa tusifike kwenye bwawaa amb......." kabla hajaendelea ndipo mzee huyo alimkatisha na kumuambia jambo "Eheeee! nakifahamu tayari kilikuwa kinaitwa SONGAMBELE na alikuwa anaongoza mzee mmoja kipindi sisi bi vijana aliitwa ZAMALIO". alimkumbusha "Haswaa baba kweli unakumbukumbu nzuri. "Ni kwweli kwani nakifahamu na pia kilifutwa hiko lakini hilo jina labda kifufuliwe sasa hivi na kupewa jina hilo.". Basi walipokelewa vyema baada ya kufika ndugu wengine. Upande wa kijiji walichotoka tafrani ilikuwa kubwa watu hawakai kwa amani kwani kila kukicha mambo yalizidi kuwa mambo makubwa sana. Sasa ndipo mzee mapato anamshawishi mwenzake waende kwenye lile bwawa ambalo lilikatazwa kwa muda mrefu sana ili kwa sababu bwana mapato kapata ndoto ambayo ilimkumbusha jambo ambalo linamhitaji kuelekea kwenye hilo bwawa, "Rafiki yangu unataka kwenda tena kuanzisha mambo ya ajabuajabu tena" alisema sikujua "hapana sasa hivi kipindi cha mavuno kinakaribia sasa unadhani fedha tunazipata wapi sasa". waliondoka hadi bwawani ndipo mzee mapato akaingia katikati ya bwawa hilo na kuchinja kuku kama kafara la damu pale na kisha akachukua lile kitu kama pembe ambalo lilihifadhiwa kwa muda sana katikati ya bwawa hilo. Alilichukua na kuanza kusema baadhi ya vitu kisha akaliacha na likazama tena chini na yeye akatoka. bwana sikujua alimuuliza "Sawa sasa umemnuia nani wa kufa " Mapato hakuwa na wasiwasi sana kwani hakuwa na wasiwasi wowote "niliyemnuia ni Mzee Mambo sasa tutaenda kumshawishi pale kwake kwa kumdanganya tumeuona mwili wake kwenye bwawa na akija si ndo kaisha" walipongezana kwa fikra walizonazo."sasa susu tunamfanya nini mana unajua kuwa alipo pale hajala kabisa" walitulia kisha mapato akasema "ahaa usijali akiwa msumbufu sana tunampiga tena nyuma ya kichwa atapoteza kumbukumbu kisha tunamuachia hatoweza kabisa kutukumbuka". walirudi nyumbani lakini taarifa wanayoipata kuwa mzee Mambo sasa kaondoka hata bila taarifa yani kaama kabisa.... mapato aliishiwa pozi kabisa kwani atampatia wapi na wakati yeye ndie nia kubwa kwenye lile swala pale.........





Taarifa ya kuondoka kwa Mzee Mambo sasa ilishaenea kijiji kizima, nz kila mmoja alishangaa kwa upande wake. Taarifa ilipofika kwa mwenyekiti na yeye ilimchanganya ilimbidi atumie akili ya ziada kujiuliza analitatuaje. Muda mchache anakuja bwana Manuali kwa mwenyekiti. Mzee manuali hakika alikuwa na majonzi sana kupotelewa na mjukuu wake ambae alikuwa anamtegemea sana kwenye mambo ya utabibu wa pale kijijini. Alikaribishwa na mwenyekiti huyo na kupewa kigoda ili akalie. Baada ya kukaa anaonekana Mzee Manualiakianza kulia taratibu. Ilibidi mwenyekiti asitaajabu kwa nini mzee mzima kama huyo aanze kulia mbele yake. "bwana SEMENI aaah hii siku ya tatu sasa mjukuu wangu haonekani kabisa jamani sijui mmechukua uamuzi gani". Mwenyekiti alishtyuka kama ndio kwanza anafunguliwa kichwa na masikio. Mwenyekiti huyu anayejulikana kwa jina la SEMENI ambae alipewa wadhfa wa kuongoza kijiji cha Bwawani alitulia kwa muda sana huku mzee Manuali yakimtoka maneno. "unajua bwana Manuali haya mambo sasa yanazidi kuwa magumu kila baada ya siku hapa sasa hivi nimeletewa taarifa kuwa bwana Mambo sasa kaondoka bila hata ya taarifa yani kaama kabisa". Baada ya kusikia kuwa mzee Mambo sasa kaondoka, ndipo manuali akanyamaza kidogo kuongea. "Mwenyekiti ina maana kaondoka kabisa hapa, je? sababu gani ambayo imemfanya aondoke". Mwenyekiti huyo alitikisa kichwa kuonyesha kuwa hakuwa na la kumjibu kabisa kwa upande wake. "Labda tufanye hivi, nitaitisha kikao cha dharura alafu tuone tunasaidia vipi haya mambo". Mzee Manuali aliondoka pale kuelekea nyumbani kwake. Alikutana na kijana Ndunya njiani alimpatia taarifa iliyotoka kwa mwenyekiti na pia akamueleza kuhusu kuondoka kwa bwana Mambo sasa. Ndani ya kijiji cha SHISHIMO anaonekana bwana Chito ambae alijulikana sana kama Mambo sasa kipindi yupo bwawani, na alitumia jina la baba yake mzee mambo sasa kwa malengo yake yeye mwenyewe, kwa wakati huo yuko shambani akipalilia mahindi pamoja na mihogo. Wakati anaendelea huku akiwaza vitu vingivingi ndipo aliposimama na kuanza kubana kidole kuashiria kama kuna jambo ambalo analifikilia sana. alionekana akibeba jembe lake na kuondoka Katika tembea yake ndani ya shamba hilo alishangaa sana kwa kutoiona njia ya kutokea kwani ndio ilikuwa mara yake ya kwanza kufanya kazi shambani baada ya maelewano ya kifamilia. Alizunguka shamba zima njia haioni, Huku nyumbani mkewe na baba mkwe wake mzee Mambo sasa wanaendelea kuongea ndipo mada ya chito ilivyoingia. "Mh! mbona mume wangu mpaka sasa hivi jioni inaingia hajarudi?" Mama sikitu alihoji kwa hofu, " Usiwe na shaka atakuwa ana hasira ya maendeleo yani wanangu wote wana akili ya maendeleo kama jina langui lilivyo Mambo sasa hivyo ndivyo walivyo". baada ya kuambiwa hivyo alitulia na wakaendelea na shughuli zao, lakini kadri muda ulivyozidi ndipo kiza kilianza kuingia na Chito au baba sikitu hakuonekana kabisa. Ilimbidi kwa hofu kubwa sana mama sikitu aondoke pale na kumfuata huko shambani ili ajue nini sababu inayomfanya achelewe sana. Wakati anaelekea huko ndipo na mzee mambo sasa anashtuka kuwa muda umekwenda sana alimuita mkwewe lakini hakuitika alimtafuta kwa kuzunguka nyumba nzima lakini hakufanikiwa kumuona kabisa "Au atakuwa kamfuata mumewe shambani, lakini chito na yeye mpaka sasa kulima tu" aliamua kuongoza njia japo kwake ni tabu sana kutembea hatua zake ni kama kinyonga ambae yupo kwenye mwendo wa malingo, alikuwa anatembea na mkongojo wake, kumbe mama sikitu katembea na kwa bahati mbaya alishindwa kabisa kutambua wapi shamba lipo hivyo aliamua kugeuza njia ili kuepuka kupotea. wakati anarejea kwenye moja ya kona alifanikiwa kumuona mzee huyo ndipo aliamua kumfuata taratibu bila hata kumstua ili amuone anataka kwenda wapi kwani alishakuwa na mashaka nae tangu mwanzo wanafika pale na yale matatizo ambayo ambayo waliyapata tangu mwanzo. Kwenye mwendo wao walifika shambani hapo giza likiwa limeingia tayari na sauti na za wanyama pamoja na wadudu mbalimbali zikipishana. Kwenye shamba hilo chito alikata tamaa kabisa ndipo alishangaa kuona mwanga ukiwa unamulikwa mahala fulani, kumbe yule mzee kuna kitu fulani ambacho kilitoa mwanga kama taa inayotumia nguvu ya umeme ikiwa imewashwa. Mama Sikitu alishangaa ndipo akajiziba mdomo ili asije kutoa ukelele ambao utamchanganya pale alipo, alivumilia kisha akatulia, ""Nyamyena Nyamyena, kulumbila kulumba, mwanenu kalumbilolo Chito, kumchamba mwangu, kamililombile kulilima mpaka kujioni Nyamyena Nyamyena kulumbila kulumba"". Ni maneno yaliyomtoka mzee mambo sasa kwa wakati huo, ghafla Mama sikitu anashangaa kumuona mumewe akitoka shambani humo, alitaka kupiga ukelele lakini alishindwa alikuwa sawa na mtu ambae kawekewa gundi kali mdomoni na hatimae anapatwa na usingizi mzito sana. Alilala pale na hakutambua nini ambacho kiliendela pale, muda mchache tu alizinduka kutoka usingizini na kupata nguvu kubwa ambayo ilimfanya kukimbia toka pale na kuelekea nyumbani kwao. Alikuwa na hofu kubwa sana juu ya baba mkwe wake. Aliwakuta wakimsubilia yeye ndipo aliposhtukia kofi la maana toka kwa mumewe alipohitaji kuhoji akatandikwa lingine na lingine hadi akadondoka chini kwani alikuwa akipiga kwa hasira sana, Hakumjali kabisa pale alipodondoka mama Sikitu alimuacha huku akilopoka maneno ya ajabu sana. Majira ya usiku wa manane mama sikitu anazinduka toka usingizi wa nusu kifo kutokana na kipigo kikali kutoka kwa mumewe lakini anashangaa kama kabanwa na kitu kizito ambacho hakukifahamu, fikra zake zilikuwa mbali kuwa mumewe kamkumbatia wakiwa wawili kitandani, alishindwa kuwa na maamuzi kwa kuwa raha aliyokuwa akiihisi ya joto ilimfanya kuwa kama mtoto anayedeka. Lakini ajabu anashangaa kuona kichwa chake kinaburuzwa taratibu huku akianza kupata maumivu taratibu. Wakati huo mvua ilianza kutia nanga toka safari ya mbali na kuanza kuporomosha neema ya mwenyezimungu, chini ya ardhi ya Shishimo na kufanya mimea kufurahi kutokana na hiyo neema inayoendelea kushuka kwa muda huo. Mama sikitu akili yake bado ilikuwa inatafuta mtandao ili iweze kuchambua data kuwa yuko sehemu gani maana hata kichwa chake kilianza kupigwa na matone ya mvua, Wakati huo Mzee chito akiwa ndani anashtuka na kukaa kitandani baada ya mvua kuanza kupenya kwenye tundu za nyasi zilizoshoindikana kuzibwa huko juu ya paa, alipapasa pembeni kama kawaida yake kuwa atamkuta wa ubavu wake wa kushoto lakini wapi. Alishuka toka kitandani na kwenda kuangalia mlango kama umefunguliwa lakini alikuta umefungwa. Alisimama kama sekunde kadhaa ndipo akakumbuka kuwa usiku alimpiga mkewe na hakumjali kabisa na muda wa kulala alikuja kulala peke yake. "mke wangu mke wangu" alianza kuweuka pale bila hata kujua nini ambacho kilimfanya amfanye vile mkewe na sasa anajilaumu kwa sana. Alifungua mlango na kwenda nje mpaka pale alipomuachaga mkewe lakini hakumkuta kabisa, mvua iliendelea kulindima na radi za kutosha zilikuwa nyingi sana. Alimpenda sana mkewe kuzidi neno nakupenda aliangaika sana huku na kule ndipo akaanza kuita kwa nguvu "Mama sikituuuuuu mama sikituuuu mke wangu uko wapiii!". Ile sauti ilisafiri kwa umbali fulani kwa kasi sana hadi pale alipopatikana mama sikitu mwenyewe. Mama sikitu aliipata sauti hiyo ndipo akaondoka kwenye fikra zake na ndipo akajiuliza wakati hata macho hajafumbua, kama huyu aliyembana hivi ni mumewe je huyo anayeniita mke wangu ni nani pia akili ilimjia muda ambao alipigwa na akaachwa pale kama zigo la kuni, alifumbua macho kumbe alibebwa na kitu hatari sana ndipo alipopiga ukelele mkubwa sana uliompa taarifa bwana Chito kuwa mkewe kapatwa na matatizo makubwa yanayohitaji msaidizi. Ndani ya kijiji cha KILIMALONDO, baada ya miezi kadhaa kupita lyoto alikuwa na afya nzuri sana tena sana na alikuwa kamili. Matatizo yake yote yalipona alisikia vyema aliona vyema aliongea vyema kama kawaida na sasa lyoto kawa binti mzuri sana wakati huo akilelewa na kijana Katunje ambae yeye kama mwanaume alijihisi hata kumtamani binti huyo, lakini alishindwa baada ya kumchukulia kama ndugu yake wa karibu hivyo baada ya kutambua kuwa alibakwa hakutaka kumpa taarifa yeyote kuwa alikuwa wapi kipindi cha nyuma. Binti lyoto tatizo alilonalo ni moja tu kuwa alipoteza kumbukumbu kuwa yeye ni nani na alikuwa wapi alijihisi kama mtu ambae kazaliwa upya katika ulimwengu wa Kilimalondo. siku moja kijana katunje alimkalisha chini lyoto akifikilia jambo la kumuambia. "Ndugu yangu lyoto, siku moja ikifika mimi nikipotea machoni mwako basi familia yangiu inapatikana kijiji cha Shishimo kwamba utajitahidi kufika hapo na kupeleka taarifa yeyote ambayo itanilazimu mimi kupoteana na wewe kwa muda mrefu umenielewa". lyoto alitabasamu na kumuuliza. "sawa nimekuelewa lakini mbona hujawahi kunionyesha mama yangu wala baba yangu na wewe umeniambia kuwa kaka yangu sasa baba yetu na mama yetu wako wapi na wanaitwa akina nani". Swali hilo lilimchesha bongo kijana katunje na alifikilia ili amjibu vyema "yani kiukweli dada yangu baba na mama wanaishi mbali sana ila mimi nikaamua niishi na wewe ila siku zishafika za kuwajua wewe wazazi sawa, ila ngoja kwanza niende kijijini nikatafute chakula alafu nitarejea". Walikuwa wanaishi huko polini na hapakuwa na mtu ambae anapafahamu zaidi ya wao kama wahusika. Alifanya safari ya kwenda kijijini ambako watu wengi huwa wanaishi huko. Katunje lifanikiwa kufika kwenye nyumba ya mama mwaija ambae alimuamini kuwa ni mmoja kati ya watu ambao wanampa msaada wakati wote. lakini alikuwa anajiuliza sana kwa nini moyo wake umetokea kuridhika sana kumsaidia mtu ambae hamfahamu kabisa lakini aliachana na hayo mambo. baada ya kufika kwa mama huyo alimkuta akiwa anaanda chakula, "mama mama upoo katunje hapa". alijitambulisha ili aweze kujulikana mapema na mama huyo asipate wasiwasi wowote. "Mwanangu katunje haya ingia ndani haraka sana": aliingia baada ya kuhakikisha kuwa hakuna mtu ambae anamuona wakati huo, "katunje muda sasa bado hujaniambia wapi ambapo unaishi kwa sasa na wala hujawahio kuniambia maendeleo ya huyo mgonjwa anaendeleaje". katunje alishusha pumzi kwanza kisha akamueleza jambo fulani. "mama kweli lakini haina budi kukuambia leo hii, mama hali yangu bado kwa sasa mbaya sana itabidi leo hii nikueleze wapi ambako ninaishi ili chochote kitakachonitokea basi uweze kumsaidia binti yule kumrudisha kwake, pia naomba iwe siri yako kabisa kwa sasa niko pale karibu na makorongo, na binti hali yake ni mzima kabisa tena utamshangaa sana" Basi mama mwaija akafurahi sana ndipo akamueleza kuwa Mzee Swai kwa sasa hawezi kukufuatilia kwani anasumbuliwa na maradhi na anapoonyesha kuwa anaenda ukingoni kabisa". Kumbe wakati huo mzee Kauzibe alikuwa nje ya nyumba hiyo akimfuatilia bwana Katunje, aliposikia kauli ya kusema kuwa yule http://deusdeditmahunda.blogspot.com/binti kafichwa kwenye pori lililokaribu na makorongo basi aliondoka kwa haraka sana ili kwenda kuhakikisha, aliondoka na mitego yake ili ajulikane kuwa ni mzee mtegaji kama kawaida yake, alipofika ndani ya msitu huo basi alianza kutafuta lakini hakupata mafanikio kabisa ndiopo akatafuta mahali na akaanza kutega mitego yake ya wanyama. Baada ya kumaliza hapo akaondoka akiwa na matumaini kuwa siku moja atafanikiwa kumkamata binti huyo. Haikujulikana kwa nini mzee huyo anafanya hivyo yani anamfuatilia binti lyoto. Upande wa kijiji cha bwawani mambo si mambo sasa bada ya wazee wawili maarufu sana mapato na sikujua kushirikiana kwenda mahali ambapo wamemficha kijana susu, waliamua kumtoa kwa sababu tayari vitisho vimeshatoka kwa mzee Manuali kuwa yeyote ambae kahusika kumpoteza kijana wake basi ajiandae kuipata cha mtema kuni kwani hatoweza kumvumilia kamwe mtu yeyote. Waliulizana sasa watamfanya nini kijana huyo na endapo wakimuacha basi na wao watajulikana ndipo wakaamua kumpiga na gongo la kichwa yani upande wa kisogo ambako upo ubongo wa kutunza kumbukumbu. kitu hiko kilimfanya aanguke chini na azimie kabisa, walimuinua na kwenda nae karibu na kijiji kwenye nyumba moja ndipo wakambwaga nyuma ya nyumba hiyo, waliondoka pale na wakaenda kuungana na wengine ambao walikuwa kwwnye kikao. Kwa bahati mbaya walishindwa kukumbuka kuwa kule mahala ambako walifanya unyama ule waliacha vitu ambavyo ni kama ushahidi tosha kabisa endapo mtu ataamua kufuatilia. Kila mtu sasa alikuwa tayari kumtafuta kijana huyo na huku wengine wakisema kwamba itakuwa ni mzee mambo sasa ndie alikuwa anayafanya haya ili kulipisha malipo ya mwanae ambae alipotea kwa muda sasa na ndipo kaamua kumpoteza kijana huyo. kauli hiyo ilishikiliwa na sikujua kuwa itakuwa kweli japo kijana ndunya na Mzee manuali walipinga vikali sana kuwa haiwezekani kabisa mtu kama yule afanye vile "nasemaje mtu aliyempoteza kijana wangu yumo humuhumu kijijini sasa asipoonekana leo hii atanitambua" alimaliza hivyo na yeye akaondoka zake. Kijijini shishimo mama sikitu anaonekana kulia baada ya kukoswa kuuliwa na mnyama mkali ambae alimbana, kumbe alikuwa chatu mkubwa sana ambae alionekana kumvirigia huku akimburuta, ndipo chito kwa ujasiri alimfuata lakini ajabu nyoka hilo lilimuachia na kukimbia zake kusikojulikana alimchukua mkewe na kuondoka nae kwenda ndani lakini anamshangaa kumuona baba yake akiwa uwanjani, wao waliingia ndani na kulala. kwa upande wa mama sikitu hakuweza kabisa kulala kwani kwa yale yaliyomtokea ni tosha kabisa kuwa yuko hatarini. Alimueleza mumewe kuwa pale hawako salama "mume wangu nakuapiza kuwa hapa hatupo salama kabisa ni bora hata kule ambako tumetoka lkakini si hapa" kauli hiyo ilikuwa kero sana kwa bwana chito kwani anampenda sana baba yake kuliko kitu kingine..........


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog