Search This Blog

NILIWAROGA WALIMU MPAKA BASI - 2

 






Simulizi : Niliwaroga Walimu Mpaka Basi
Sehemu Ya Pili (2)




Niliwaona wamesimama nje ya mlango wa chooni. Nikawafuata kulekule ambapo mama alinielekeza nifike pale kwa kutembea vilevile tulivyoelekezana awali. Nilisimama, nikageuka na kuanza kutembea kinyumenyume mpaka pale.

Mama na yule mwanamke waliniingiza chooni na kunisimamisha jirani na bomba la maji kisha wakasema natakiwa kuwa pale nikiwa nimesimama wima hadi watakaporudi. Wakati wanaondoka, mama aliniambia kazi yangu itakuwa kupokea vitu watakavyokuwa wanavileta pale na kuvishika kwa kusubiri maelezo mengine.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Baada ya muda, yule mwanamke alikuja, akanikabidhi watoto wachanga wawili. Akaniambia wakitaka kulia tu, niweke mikono juu ya vichwa vyao ili watulie, kisha akaondoka.

Niliwashika wale watoto kwa umakini kwani walikuwa wazito sana. Baada ya muda, alikuja tena yule mwanamke, alikuwa amebeba watoto wawili, akanikabidhi, lakini nilikuwa sina pa kuwaweka, akasema niwabebe mgongoni. Alinisaidia kunibebesha halafu wale wawili nikaendelea kuwashika mkononi.

Dakika kama tatu baada ya yule mwanamke kuondoka, aliingia mgonjwa mmoja, akawa kama amenikazia macho mimi. Nilimnyooshea kidole kisha nikakielekezea kwenye mlango wa choo kimoja, naye akaingia huko.

Pale nilichofanya, niliishika akili yake na kuielekeza iingie kule kwenye choo. Wachawi wengi hufanya hivyo. Pale wanapokumbana na kikwazo mbele yao, hujihami kwa vidole, mchawi akikunyooshea kidole kisha akakielekezea kwenye moto mfano, utajikuta ukienda.

Ndiyo maana kuna watu wanagongwa na magari njiani kisha wanaoshuhudia wanashangaa kwamba, jamaa ilikuwaje akasogea barabarani wakati gari lilikuwa linatoka kwa mbele yake?

Kinachofanyika ni kwamba, kama kuna mchawi ametumwa kwako akumalize na ni ‘mwepesi’, yaani huna kinga yoyote, basi akishakupatia shabaha, anakuelekezea mahali pa hatari. Iwe kwenye moto, barabarani au hata kwenye maji, lazima utaelekea huko tu kwani wenyewe wanasema wanashika akili.

Basi, yule mwanamke aliingia kule chooni. Akafunga mlango na kujisaidia. Baada ya muda alitoka, akageuka kuangalia niliposimama mimi, nikamnyooshea tena kidole na kukielekezea mlango mkubwa, akatoka. Huku nyuma nikasonya.

Niliendelea kuwa pale nikiwa na wale watoto wachanga. Lakini huku nikiwa na maswali mengi, kwani uchawi wa kupata mazao mengi shambani kupitia watoto nilikuwa siujui. Mawazo yangu yaliamini kwamba, wale watoto tutaondoka nao kwenda nyumbani ili kuufanya huo uganga kumbe sivyo.

Baada ya dakika chache tena, alikuja mama, naye alibeba watoto wawili, akasema nikae chini ili niwapakate. Kulikuwa na ugumu kwani sasa nilikuwa na watoto wawili mgongoni na wawili mkononi nikiwa nimekaa chini.

Baada ya kuwakumbatia wale watoto, mama akaniambia nivumilie kwani bado mawili tena. Akasimama na kuondoka kwenda kuungana na yule mama.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Baada ya dakika tano, mlango ulisukumwa, akaingia mwanamke mmoja akiwa anavua gauni, akajisaidia nje ya mlango wa chooni. Nilikasirika sana kwa kitendo kile.

Ili kuikomesha tabia ile, niliwashika wale watoto vizuri kisha nikamnyooshea mkono, kidole kimoja nikakikunjua kukielekeza kwake na kukibatulia chini, akaanguka kama gunia, puu!

Aliposimama, nikasonya. Inaonekana alisikia kusonya kwangu kwani alitoka haraka huku akigeuka kuangalia nyuma. Kwa pale nilipokuwa nimekaa palikuwa wazi sana lakini aliyekuwa na uwezo wa kuniona mimi ni mmoja tu. Ni mtu mwenye nguvu za kichawi kama sisi.

Baada ya hapo, mama aliingia. Alikuwa ana watoto wawili, akawaweka kwa kuwachomeka kwangu lakini nilishindwa kuwabeba sawasawa. Aliwaacha hivyohivyo, mama akaondoka. Lakini baada ya dakika mbili alirudi akiwa ameongozana na yule mwanamke mwenzake. Hawakuwa na kitu chochote mkononi. Walipofika, walipiga magoti jirani yangu. Mama alianza kumchukua mtoto mmoja mmoja na kumkabidhi mwenzake ambaye naye aliwachukua na kuwaweka sakafuni.

Mama yeye, alikuwa akimchukua mtoto mmoja, anamuweka mkono kichwani kisha anampindua miguu juu, kichwa chini kabla ya kumpa mwenzake ambaye naye kila alipowapokea, aliwaweka kwa kuwalaza kifudifudi.

Walipowaliza watoto wote, mama alisimama, akanyoosha mkono mmoja juu, akasema:

“Mje mchukue watoto wenu haraka, sisi tunaondoka.”

Kufumba na kufumbua, kweli wanawake waliingia, kila mmoja akamchukua mwanaye, tena walikuwa wakigombeana na kuondoka. Hapa palikuwa na maswali mengi sana na nilipanga kumuuliza mama nyumbani.

Tuliondoka muda huohuo kwa njia ya kichawi hadi nje ya hospitali. Yule mwanamke akasimama getini na sisi pia. Aliangaza kulia na kushoto, akasema twende kwenye mti mmoja wenye matawi marefu na chini yake palikuwa na kivuli kikubwa.

Pale chini ya mti, yule mwanamke alimpa mkono mama na mimi, kisha akasema ameshukuru sana kwa ushirikiano wetu. Akasema ikitokea na sisi tuna shida kama yake au nyingine, tusisite kumwambia muda wowote hata kama itakuwa saa nane za usiku.

Mama alimwambia hakuna shida, akatoa mkono kwangu akauegemeza kichwani, akaniangalia akasema:

“Hakika wewe utafika mbali sana siku za usoni, jitahidi kuwa shupavu kama hivi. Mungu akulinde sana Yusta.”

Tulipofika nyumbani, nilimuuliza mama kama nilivyokuwa nimepanga. Kwamba, wale wanawake waliofika kugombea watoto wao walikuwa wanajijua?

Mama alisema hakuna hata mama mmoja aliyejua mtoto wake amechukuliwa. Ila akasema kwa wale ambao watoto wao walichukuliwa, dalili kubwa kwao ni watoto ‘feki’ waliowashika mikononi walikuwa wakilia sana hata pale mama zao walipowapa maziwa walizidi kulia mpaka kupatwa na kwikwi.

“Sasa mama, pale ulipowaita waje kuwachukua mama zao, kule ndani hospitali wao walijua wanakwenda wapi?”

Mama alinishika kichwani, akanisifia kwamba nina akili sana, kisha akasema:

“Wale hawakujijua chochote. Kila mmoja alipomchukua mwanaye na kurudi naye wodini waliendelea kujiona kama hawakutoka. Ila walijua watoto wao wametulia kulia baada ya kuwabembeleza sana.





“Mlizuia vipi mama? Sijaelewa.”

“Tuligundua ulichomfanyia. Kwa hiyo baada ya kufika wadini mimi nilimkimbilia na kumsukumia kitandani, alipotua pale ikawa ndiyo uzima wake.”

***

Usiku wa siku hiyo, mama aliniamsha kwa kunitingisha sana. Usingizi ulikuwa mzito sana siku hiyo. Nilipoamka akasema anaomba tukamalizie kazi ya yule mwanamke mwenzake. Nilimuuliza inamalizika usiku? Akasema ndiyo wakati wenyewe ndiyo ule.

Kimsingi alinishtua lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kumkubalia kila alichotaka. Niliamka, nikavaa kaniki kwa staili ya kuizungusha mwilini, nikachukua na kibuyu cha dawa kisha nikatoka kumfuata mama ambaye alikuwa nje akinisubiri. Alinishika mkono na kupaa angani hadi nyumbani kwa yule mwanamke ambaye naye tulimkuta nje akitusubiri . Alisalimiana na mama kisha akanisalimia na mimi huku akisema:

“Binti kazi nzuri, wewe ni mwanajeshi mkubwa sana katika kazi yetu, unahitajika kuwa juu zaidi ya hapo maana nakukubali.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Nilimjibu asante sana mama. Kisha yule mwanamke akamshika mkono mama na mimi kwa pamoja na kusema tuondoke.

Mawazo yangu yalikuwa juu ya namna ambavyo safari hiyo itakavyokuwa, nikawa mpole na kusubiri maelekezo. Kufumba na kufumbua tulikuwa ndani ya nyumba moja. Tulitembea kuingia kwenye chumba kimoja ambacho tuliwakuta wanandoa wawili wamelala. Ulikuwa ni usiku mnene na walikuwa wakikoroma.

Mama aliwaita kwa kutumia ishara ya mkono, wote wakainuka taratibu na kukaa kitandani wakiangalia mbele ukutani. Mama akaendelea kuwaita huku sisi tumesimama sambamba naye. Wale watu wakatoa miguu nje ya kitanda na kushuka kisha wakasimama.

Mama na yule mwanamke walinitangulia kisha wale watu wakawa wanawafuata kwa nyuma. Baada ya sekunde kadhaa, mama alinifuata na kuniambia nimpe kibuyu kilichokuwa na dawa ndani yake ambacho wakati wa kuanza safari yule mwanamke rafiki wa mama alinikabidhi kukishika.

Alitoa makaratasi mawili yenye dawa, akanipa mkononi na kuniambia:

“Changanya haraka hiyo nyeusi na hiyo ya kahawia. Ukimaliza, niambie.”

Nikatekeleza maagizo aliyonipa kisha nikamkabidhi. Tayari wale wanandoa wakawa kama wamechanganyikiwa kimiujiza.

Mama, aliwaamuru kuvua nguo walizovaa wakiwa kitandani, wakatekeleza hilo. Walikuwa kimya ingawa walionekana wanatamani kuzungumza chochote, nadhani walishindwa kwa sababu ya dawa walizofanyiziwa na mama.

Mama akawapaka dawa mgongoni, kwenye mapaja na miguuni huku akizungumza maneno ambayo sikuyaelewa maana yake na najua yalikuwa ya kichawi kwani siku zote wachawi wanaongoza kwa kusema maneno yenye ishara ya kunuwiza. Aliendelea kusema maneno hayo kwa muda huku sisi tukimuangalia. Mimi nilimkazia macho kabisa.

Kuna wakati nilishindwa kujizuia, ikabidi nimuulize mama kama anahitaji msaada wowote kwani alionekana kuzidiwa nguvu, alianza kurudi nyuma taratibu.

“Hawa wanaonekana waliwahi kujiwekea zindiko, ndiyo maana hii dawa niliyowapaka inaonekana haijawafaa sana,” alisema mama akiendelea kurudi nyuma.

“Kwa hiyo mama kama waliwahi kuwekewa zindiko tunatakiwa kufanya nini ili tukamilishe kazi yetu?” nilimuuliza.

***

Nyumba ya pili ambayo mama aliwahi kuwaroga zamani kama walishtuka baada ya mbwa kubweka mfululizo kuashiria kuna kitu kibaya kinaendelea maeneo yale.

Hapa nataka kusema kidogo kwamba, kati ya viumbe ambavyo Mungu amevipa uwezo wa kuwatambua wachawi ni mbwa. Asikudanganye mtu. Ukisikia mbwa wanabweka sana, hasa usiku mwingi ujue kuna wachawi hasahasa kama hutaona watu wakitembea kwa uwazi. Majirani waliamka na kutilia shaka ule ubwekaji wa mbwa, wakahisi kuna kitu kibaya kinaendelea usiku huo. Mara tuliwasikia majirani wakisali, mbwa nao walizidi kupiga kelele huku wakiizunguka ile nyumba ambayo sisi tulikuwa ndani tukiendelea na kazi zetu za kichawi.http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Mama lakini mbona hawa mbwa wanabweka sana na hawa watu wa humu ndani mbona hawasogei mbele tena kama walivyoamka kitandani?”

Mara tena tukasikia sauti ya mwanamke kutoka ile nyumba jirani wanayosali ikisema:

“Kutakuwa kuna kitu, si mnakumbuka hata sisi tuliwahi kuingiliwa? Cha msingi tuendelee kusali ili mabaya yasitukute.”

Hofu iliwajaa watoto pamoja na mama zao, walikumbuka namna walivyoteseka siku waliporogwa na kupata mateso makubwa.

Wakakumbuka neno ambalo waliambiwa na mchungaji John aliyekuwa maarufu maeneo hayo kwa kuombea mapepo. Aliwaasa juu ya kusali bila kikomo hasa wanapoona hali ya hatari kama hiyo.

Waliendelea kupiga maombi ambayo kwa kiasi fulani yaliathiri kazi tuliyokuwa tukiendelea nayo. Vurugu ya kelele za mbwa ilizidi kuwa kubwa.

***

Mama akabadili mbinu, akawaamuru wale wanandoa walale chini kwa kuwaelekezea mikono yake yenye kucha ndefu huku akiwatazama kwa macho makali ambayo yalimulika kama tochi.



Wale walitii hatua kwa hatua na mwishowe ushindi mkubwa ukawa kwetu.

Aliwaamsha, akawaamuru watembee mbele yetu hadi nje. Kufika nje, akawashika mkono mmoja mmoja kila mmoja, yule mwanamke shoga wa mama akanishika mimi, tukafutika, kufumba na kufumbua tukatua kwenye shamba kubwa lenye majani yaliyokauka.

Ni shamba lililoonesha kwamba mwaka uliopita lililimwa, kwa hiyo lilitakiwa kulimwa kwa mwaka mwingine. Nilihisi ni shamba la yule mwanamke mwingine maana sisi hatukuwa na shamba kama lile.

Baada ya kufika pale shambani, yule mwanamke alisimama kama askari kisha akanyoosha mkono mmoja juu na kusema kimoyomoyo. Baada ya sekunde kadhaa, jembe na mpini wake lilikuwa mkononi. Akampa mama.

Halafu akanyoosha tena mkono na kusema kama mwanzo, jembe jingine likatua palepale kwenye mkono, akaendelea kulishika mwenyewe huku akimfuata mama.

Waliwapa majembe wale watu, kila mmoja na lake na kuwaamuru waanze kulima haraka sana. Palepale, walianza kulima kuanzia kwenye mpaka wa shamba kuelekea katikati. Mwanamke ndiye aliyetangulia kuchoka sana lakini mama akawa anamsukuma. Kwa hiyo ilibidi alime kwa nguvu.

Mimi, yule mwanamke na mama tulikuwa tunawafuata kwa nyuma baada ya kila hatua kadhaa za kulima. Nilipata mawazo ya kumuuliza mama kama wale watu wanajua nini kinaendelea kwao.

Mama akasema wanajua wanalima, lakini shamba liko wapi, la nani, kwa nini wanalima hilo hawalijui. Pia, akaniambia pale walipo japokuwa wanalima kwa pamoja lakini hakuna anayejua kama mwenzake yupo pembeni.

Kifupi ni kwamba, walikuwa wakilima kila mmoja akijijua yeye tu kwamba yupo shambani analima. Baada ya hapo nikamuuliza mama watarudi vipi kwao?

“Kwao tutawarudisha baada ya kumaliza kulima. Kwa sababu wanalima kwa nguvu za kichawi watamaliza leo, ila kesho watashinda wamechoka sana.”

Nilimuuliza mama itakuwaje wakiamka na kujikuta wamechafuka sana?

“Huo ni uchawi wa kizamani sana, mtu anakwenda kulima halafu asubuhi anajiona alivyochafuka kwa udongo au vumbi la shambani, lakini uchawi wa siku hizi mtu anaamka anahisi kuchoka kupita kiasi, wakati mwingine anaamini anaumwa lakini kumbe alikuwa shambani usiku akilima.”

Basi, wale watu walilima hadi kwenye saa kumi alfajiri ambapo tuliwachukuwa na kuwarudisha nyumbani kisha sisi tukaondoka zetu kurudi majumbani.

Asubuhi, niliwahi kuamka kwani nilitakiwa kwenda shuleni kama kawaida. Kufika shule, mwalimu Cecilia aliniita kwenye ofisi ya walimu wenzake. Akaniuliza:http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

“Wewe ni kwa nini jana tulipogonga kengele wanafunzi wote warudi wewe hukufanya hivyo na ulikuwa bado hujafika mbali?”

Nilifanya kibuli, sikumjibu na sikuwa namwangalia usoni. Macho yangu yalicheza kwenye miguu yake.

“Mimi nakuuliza wewe hujibu siyo? Halafu ni kwa nini unanikodolea miguuni na hiyo mimacho yako mikubwa?”

Pia sikumjibu. Ndipo waalimu wenzake wakasema mimi ni mjeuri tangu siku nyingi na dawa yangu ni moja tu, fimbo. Mwalimu Cecilia akasema nikachukue fimbo mwenyewe.

Nilitoka kwenda kutafuta fimbo kisha nikarudi nayo. Aliniambia nilale kifudifudi ili anipige fimbo saba, nikalala. Kwa kweli fimbo ziliuma sana. Alipofika ya tatu ilikuwa shida kukubali kuendelea.

Walinilazimisha kwa maneno makali mpaka zikatimia fimbo zote saba, makalio yalikuwa yanauma na yakavimba ghafla. Niliposimama nikashindwa kuvumilia nikamwambia Mwalimu Cecilia: “Utaona wewe.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

Akasema: “Ha ha ha! Wewe mtoto mdogo unaweza kuniambia maneno hayo mimi mwalimu wako, rudi haraka sana. Njoo nikupe viboko vingine vinne ili nione vizuri.”

Nililazimika kurudi kupigwa viboko vingine vitano ambapo safari hii makalio kidogo yatoke maji ya malengelenge. Nililia sana tena kwa sauti ya juu. Baadhi ya wanafunzi walikuja kwenye madirisha ya ofisi ya walimu kutaka kujua kinachoendelea.

Nilitoka nikiwa bado nalia lakini moyoni niliendelea kumwambia yule mwalimu ataona kwani ukweli ni kwamba nilipanga kumshughulikia. Tena si yeye tu na walimu wote walioonesha kumuunga mkono Mwalimu Cecilia.

***


ITAENDELEA

0 comments:

Post a Comment

Blog