Search This Blog

OSAKA MJI ULIO POTEA - 5

 





    Simulizi : Osaka Mji Ulio Potea 
    Sehemu Ya Tano (5)




    "Kuna ujumbe Bravo aliniachia, unaweza kutusaidia kama tutafuata ushauri wake", pindi mfalme alipokuwa akiitafakari hili na lile, ghafla binti yake wakuitwa Rinda alimwambia maneno hayo.



    "Najua hata tukiwaambia kuwa kitabu hatupo nacho hawataweza kutuamini", aliongeza kusema Rinda, maneno hayo aliyasema kwa sauti ya chini iliyojaa simanzi ndani yake.



    "Umepoteza malengo yangu yote Rinda, usivuruge mpango wangu nina muda mchache sana wa kutoa jawabu kwa washenzi hawa, kaa kando kabla sijakutenda vibaya", mfalme aling'aka hakutaka kujua wala kusikia kile alichokuwa akitaka kukielezea binti yake. Lakini kwa kuwa Rinda alimuamini Alexandra, kamwe hakutaka kuacha kuufanyia kazi ushauri, ndipo alipoamua kutoka mahali hapo akawafuata wanajeshi sita akawaamulisha waingie ndani ya chumba kile cha mateso, chumba chenye wadudu wakali waishio ndani ya himaya maji machafu. Hao walikuwa na sumu, mwili hufa ganzi pindi wanapo kung'ata, na ndio walio mpa heshima Alexandra baada mwili kuingiwa na nguvu ya ajabu iliyotoka kwa wadudu hao, nguvu hizo zilipelekea kumpa kipigo cha mbwa koko Josh mpaka kumpeleka kuhama mji. Wazo hilo tata liliweza kuzaa matumaini, wanajeshi wale sita walifanya makubwa, ilikuwa vita ya kutumia mapanga na mikuki sanjari na mishale.

    "Hili ndilo wazo alilo nipa Bravo, chumba cha mateso kina wadudu wakali wenye sumu, amrisha mmoja baada mwingine aingie ndani ya chumba kile, vita hii utaimudu baba", baada kuona jitahada za kujitetea zinaonekana, upesi Rinda alimfuata baba yake na kisha kumueleza jambo hilo. Basi mfalme hakuwa na pingamizi tena, aliagiza jeshi lake lifanye hivyo ili kujitetea kwani hata kitabu hakuwa nacho, kitabu cha Osaka alitoweka nacho Alexandra.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Wakati hayo yanajiri Mozana, upande mwingi, Alexandra alipoelea, aliokolewa na jamii ya watu wale wafupi, mmoja wao aliyekuwa akifanya shughuli ya kuvua samaki alimuona akamuopoa kwenye maji na kisha kumpeleka kwa kiongozi wake ambaye ni yule aliye muomba afanye jitihada ya kuliua Joka lile hatari. Majonzi yalitawala, walimsikitikia sana Alexandra, upesi wakafanya jitihada ya kumkamua maji tumboni, mwishowe walikamilisha zoezi hilo, baada kuyafumba macho yake kwa mrefu hatimaye anayafumbua, alikuwa amechoka kila idara huku sehemu mbali mbali za mwili wake zikivuja damu, mboni zake zilijaa ukungu. Licha ya kuyafumbua macho yake ila hayakuweza kuona vizuri. Walau tabasamu bashasha likaonekana kwenye nyuso za mbilikimo wale, sasa wakaanza kutengeneza dawa za miti shamba ili kumtibu. Wakati zoezi hilo linaendelea, mara ghafla anakuja mwenzao mmoja ambio mbio, akatoa ishara kuwa ameliona Joka lile hatari likiwa hoi halijiwezi. Ilikuwa ni habari njema, wakateuliwa watu watatu, mbilikimo wakaelekea huko kushuhudia kama kweli alicho kuja kuwaeleza wenzake.

    Walikuta Joka limelala lipo hoi bin'taabani likipumua kwa tabu huku ndani na wadudu wakali wakilishambulia kwenye kidonda chake, halikuwa na ujanja tena zaidi ya kungojea kifo. Hakika ilikuwa shangwe, raha mustarehe kwa kila kiumbe kilicho ishi ndani ya msitu ule, mbilikimo wale walimsifu Alexandra kwa juhudi zake, walimuheshimu na kumuona shujaa wao zaidi wakamuandalia kalamu.. Wanyama wote, ndege na wadudu wakajumuika pamoja kusherehekea, mbawa za ndege na sauti za wanyama mwitu sanjari na wadudu ziliweza kuunda wimbo mzuri wa iana yake ulio mpeleke Alexandra kufurahi, mwisho wa yote akahitaji kuendelea na safari yake ya kwenda Osaka! Kiongozi wa mbilikimo alimpa mafuta kisha akamtaka ajipakae mwilini kisha akampa jiwe la dhahabu ikiwa kama shukrani kwa kile alicho kifanya. Na sasa wakaongozana mpaka kwenye bwawa lile, kiongozi yule wa mbilikimo akamwaga mafuta kwenye maji ya bwawa lile, maji yakapotea likaonekana giza nene. Kwa ishara akaambiwa ajitupe katika giza lile akihakikishiwa kuwa ndio mlango wa kufika Osaka! Alex alikubali, alivaa vizuri kibegi chake chenye kitabu kisha akajitosa akapotea katika giza lile, maji nayo yakarejea kwenye bwawa lile kama awali..!!





    Alexandra alishtuka kujikuta yupo sehemu nyingine tofauti kabisa, alistaajabu. Lakini baadaye aliachia tabasamu murua sambamba na kuwashukuru mbilikimo wale walio mpa njia fupi ya kufika Osaka. Alisimama kidete, hakujua elekee wapi, aliona majengo mengi sana, magari pia yalipita na watembea kwa miguu nao walikatiza kando ya barabara zile, mzunguko wa maisha uliendelea. Watu wa Osaka walivaa kawaida kama ilivyo binadamu wa kawaida Duniani, hata maumbile yao pia yanafanana fika na maumbo ya binadamu japo walikuwa tofauti lakini sio saana.

    Watu wa huko wanamasikio marefu, vile vile meno yao ya mbele mawili ni marefu mithili ya viumbe aina ya vampire. Lakini pia mbali na jami ya watu hao kuwa rukuki, hata binaadamu wa kawaida bao waliishi lakini ni wale ambao walifika huko kwa shida zao mbalimbali, ikiwa kama kusaka utajiri au kutia saini kujiunga vyama mbali mbali vilivyo chini ya umiliki wa utawala wa kishetani. Akiwa katika hali ya kupigwa na taharuki huku akishangaa kila kona ya mji ule, ghafla alizungukwa na jopo wale watu au viumbe waishio Osaka. Kimuonekano walikuwa ni wahuni wa jiji, walimvamia baada kumtilia mashaka kutokana na kuvaa mavazi tofauti na waliyo yavaa wao, lakini pia walihisi kuwa ndani ya kile kibegi chake kutakuwa na kitu cha maana alicho kubeba.



    Kwa kuwa hakuwa na siraha yoyote ambayo angeliweza kujitetea, woga ukamjaa. Lakini hakuwa tayari kupokonywa kitabu alicho toweka nacho kutoka Mozana, hivyo alikabaliana nao. Alipambana kwa udi na uvumba kuhakikisha anawaondoka watu hao wanye nia mbaya juu yake, alipo pata upenyo alikimbia. Alijaliwa mbio Alexandra jambo ambalo lilipelekea kuwaacha katika hali ya taharuki na labda wahuni wale wa Osaka kwani hata walipo mfukizia hawakumuona.

    *Osaka ni mji uliojengeka hasa, una majengo marefu sanjari na vichochoro vya hapa na pale. Ni mji ulio changamka, una kila aina ya maisha, uchawi, utemi na mambo mengi yasiyo mpendeza muumba. Mji huo ulitoweka miaka mamilioni iliyo pita baada kukumbwa na janga la tetemeko kubwa la ardhi lililo zua balaa la mpasuko wa ardhi. Baada kutoweka kwenye uso wa dunia, utawala wa kishetani ukajenga makazi yao upesi kwa dhumuni la kuuteka ulimwengu kasi ikiwa kama tawi anzirishi baada kufanikiwa kujenga famle mbali mbali kuzimu na chini ya bahari kuu. Ujenzi huo ni kwa dhumuni la kujiweka karibu na wanadamu, na ndio maana binadamu hufika huko na kurejea japo njia ya kufika katika makazi hayo ni nyembamba kama ile iendayo kwenhe mafanikio ya halali. Yote kilieleza kitabu alicho beba Alexandra kwenye baadhi ya kurasa.



    Baada kukimbia kwa muda mrefu, mwisho alijibanza kwenye moja ya uchocho. Alihema haraka haraka huku akichungulia kila pande kwa hofu, moyoni alidhania lile jopo la wahuni wa Osaka bado linamfuatilia. Alipo jihakikishia kuwa yupo salama akashusha pumzi ndefu kisha akajitokeza, sasa alikuwa kwenye mtaa mwingine alitembea hatua kadhaa halafu akasimama, akavua begi lake akatoa kitabu na kisha kuanza kufunua kurasa ili kusoma baadhi ya kanuni za kuishi Osaka, lakini baadaye alikata shauri baada kukumbuka ndoto alizoota pindi alipokuwa kwenye pori lile la jamii watu wafupi. Akaruka kurasa alizoona hazina maana upande wake, zaidi alidondokea kwenye ukurasa ambao ulimuonyesha mahali ilipo pete ile anayo takiwa kuondoka nayo.

    Aliachia tabasamu kidogo huku akiendelea kusoma ramani ilipo na kuna ulinzi wa aina gani, alipo maliza akakirudisha ndani ya begi lake. Zaidi akawaza kupata mavazi ili kuendana sawa na watu alio wakuta huko ili awe salama kwa kila hatua atakayo tembea. Kando yake alipita mtu, alikuwa ni mzee wa makambo. Alimvuta akampiga kichwa, mzee yule binadamu wa kawaida ambaye haijulikani alifika huko kwa dhumuni gani akazimika mithili ya mshumaa uzimikapo.



    "Nyie ndio wale washenzi mnao fanya mambo mabaya ulimwenguni", huku akijivisha mavazi ya mzee yule aliye mzimisha alijisemea maneno hayo Alexandra. Lilikuwa ni koti, koti ambalo lingemtambulisha mbele ya raia wa Osaka kuwa yeye ni mtu mwenye cheo kikubwa katika mji huo. Aliogopa, alihisi atawahi kugundulika kabla hata mpango wake haujenda sawa. Hivyo aliamuwa kuligeuza koti lile, ndani pakawa nje, nje pakawa ndani. Akavaa na begi lake, safari ikaendelea, sasa alilisaka jengo lile lenye pete ambayo Devis anaihitaji ampatie ili amrudishe nyumbani kwao ikiwa kama njia ya kumuepusha na kifungo cha kunyongwa huko ughaibuni aliko kamatwa na madawa ya kulevya ikiwa kama harakati ya kutafuta maisha bora.



    Wakati anatembea, mbele yake alipata kuona jopo la watu likiwa kwenye kuta ya matangazo. Jopo lile lilikuwa likitazama matangazo, upesi Alexandra naye aliunga tela kushuhudia ni kitu gani kilicho kuwa kikijili, alipotazama akapata kuona picha yake sambamba na picha ya Joka lile alilokuwa akikabiliana nalo kule kwenye msitu wa watu wafupi hapo kabla hajakanyaga Osaka. Taarifa Alexandra akafahamu kuwa anasakwa kama shilingi baada kubainika tayari ameingia Osaka baada kutokea mauaji, na zaidi viliorodheshwa vigezo vya kumtambua. Jambo hilo lilimtatiza Alexandra, alijiinamia huku akitafakari namna gani atawaaacha kibingwa kama alivyo fanya Mozana. Lakini kabla hajapata jawabu akahitaji kuvisoma vigezo walivyo viorodhesha, hivyo aliyainua macho yake kutazama bango lile, ghafla alishtuka kumuona mtu aliyefanana na Devis, mfungwa yule mzikaji ambaye ndeye aliye fanya mpango mzima wa kumtuma Osaka. Alimfuata upesi upesi huku akiwa na shauku ya kutaka kujiridhisha kama ni Devis au amemfananisha, lakini kabla hajamkaribia mtu yule aliondoka zake akaishia kwenye wingi wa watu wale waliokuwa wakipata habari. Zaidi alicho ambulia kuona vizuri Alexandra ni chata mgongoni iliyo kwenye vazi alilovaa mtu yule , kwenye kitabu kile alicho toweka nacho kutoka Mozana kimeelezea kuwa chata ile huvaliwa na wakala! Lakini hakujua hilo kwa kuwa mawazo yake yote yalikuwa ni kuipata pete kwanza, ila pindi alipoona chata ile, akakumbuka kuwa katika pekua pekua yake alibahatika kuona mchoro wa aina ile ila hakushugulika nao. Sasa akaona umuhimu wa kurudisha macho kwenye kitabu kile, akatafuta eneo tulivu akakichomoa ndani ya kibegi chake na kuanza kuisaka chata ile, kabla hajapata ukurasa ule wenye mchoro ule ulio fanana a ile chata, ghafla akasikia kicheko nyuma yake, na kabla hajageuka kumtazama mtu huyo anaye angua kicheko akafananisha cheko hilo na cheko la Devis yule mzikaji, punde si punde kitabu kile chenye kila aina ya muongozo juu yake ndani ya OSAKA kikamponyoka na kisha kikateketea kwa moto.





    "Hapanaaaa.. Hapanaaaa", alipaza sauti Alexandra baada kuona kitabu chake alicho toroka nacho Mozana kikiteketea. Alifikiria atarejea vipi Mozana na akaweza kuaminika kuwa hakuwa na nia mbaya juu yao, wakati huo huo akageuka kutazama nyuma yake. Akapata kumuona mtu akiishia kwenye moja ya uchochoro, mtu yule alikuwa amevalia joho jeusi huku nyuma kwenye mgongo wake ukionyesha mchoro ule ulio mtambulisha kuwa yeye ni wakala. Ni yule yule mtu ambaye Alexandra alimtilia shaka, na ndio yule yule aliyeangua kicheko ambacho kili landana vyema na cheko la Devis. Upesi akamfuata ili athibitishe kabisa, mtu yule alizidi kukaza mwendo, alitembea hatua moja na nyingine alipotea na kuibuka sehemu nyingine. Aliachia tabasamu bashasha, meno yake yalionekana marefu lakini pia kwenye kona ya kinywa chake palikuwa na damu, alikata kona na kuibukia sehemu nyingine bila shaka alijua fika nyuma yake anafuatwa na mtu.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Lazima nikujue", alisisitiza Alexandra huku akiendelea kumfuata mtu yule, baada ya hatua za kitambo, hatimaye mtu yule alimpotea Alexandra no kutokana na namna mji wa Osaka ulivyo jengeka, wingi wa majengo ulimpa tabu Alexandra, ila hakuweza kukata tamaa alizidi kumsaka kwa udi na uvumba. Naam! Hatimaye alimuona kwa mara nyingine tena kwa mbaali kabisa, upesi alimkimbilia ingawa mpaka pale mtu yule alipo ingia ndani ya jengo kubwa lenye urefu na mapana. Jengo hilo lilijengwa kwa vioo vilivyo nakshiwa tinted nyeusi, alipoingia kumfuata mtu yule, lango la jengo lile likafungwa, giza nene likavagaa kwenye macho yake jambo ambalo lilipelekea Alexandra kushindwa kuelewa yupo sehemu gani. Muda mfupi baadaye taa iliwaka, mbele yake akapata kumuona mtu akiwa ameketi kwenye kiti huku akiwa amepa mgongo, mtu yule alivalia koti jeupe lenye madoa ya damu.

    "Koho Koho kohooo", alikohoa mara tatu mfululizo kisha akageuka, wakakutana uso kwa uso na Alexandra.



    Ni yule yule, Devis mfungwa mzikaji katika Gereza la Diyarbakir. Devis alinyanyuka kwenye kiti chake, akampigia makofi matatu Alexandra kisha akasema "Hongera sana kwa kufika Osaka kijana, nafikiri dhamira yangu sasa inakwenda kutimia vilivyo. Hii ilikua ni ndoto yangu ya muda mrefu. Wewe ni mtu wa mia nane uliye pitia kwenye mikono yangu. Mimi ni wakala.. Aah! Mimi ni wakala, natumwa, naenda duniani kufuata watu wenye nyota au wale wenye ushawishi mkubwa ulimwenguni. Hivyo baadhi kwenye orodha hiyo na wewe umo. Wewe una Nyota yenye mvuto, nyota yako ni faida kwetu"



    "Bado sijakuelewa Devis, naona kama unanichanganya. Wewe ni mshenzi mkubwa, unajivisha ngozi ya kondoo angali wewe ni mbwa mwitu, nilihisi jambo hili hata kabla sijakubali ombi lako la kuja Osaka. Wewe ni shetani Devis", alifoka Alexandra.

    "Ahahaha hahaha hahah", Devis aliangua kicheko. Alipokatisha cheko lake akasema "Kifo ni hali yako, lazima utanyongwa Alexandra, na sio wewe tu karibu wafungwa wote wanao hukumiwa kifo huchukuliwa kile chenye thamani kwetu kabla hawajafa, yakupasa uwe mpole ili uzidi kuyajua mengi, huwenda nikakupa mbinu ya kurudi duniani ila ni pale tu vitu vyetu vya msingi vitakapo kuwa vimechukuliwa"



    "Hamchukui kitu chochote kwangu", Alexandra alipinga, Devis alicheka kidogo kisha akasema "Uwezo wako ni mdogo sana, sina muda wa kuendelea kubishana na wewe ngoja vijana waje fanye kazi maalumu. Mimi naenda kuapishwa, sasa nenda kuwa kiongozi msaidizi wa Osaka, ila pindi nitakapo kuwa kiongozi mkuu, hakika nitawavuta wengi Osaka, jumla ulimwengu wote utaujua mji huu, nguvu ya mwanadamu ni dhaifu sana. Ahahahaha ", alimaliza kwa cheko pana Devis, muonekano wake ulikuwa tofauti kabisa na ule ambao Alexandra alimkuta nao Diyarbakir. Hakuwa mzee sana kama alivyo mtambua, alionekana kuwa kijana wa makamo tu, macho yake yaliwaka mithili ya macho ya paka, kwenye paji la uso wake alikuwa na nembo ya kichwa cha binadamu kikiwa kimenakshiwa mapembe. Huku akijiamini akiwa na wingi wa tabasamu, akamkaribia zaidi Alexandra na kumwambia "Kuwa mpole, udhaifu wako ndio ulio kuponza, shukrani kwa kuniletea kitabu hiki", akanyoosha mkono juu Devis kwenye kiganja chake kikatokea kitabu kile ambacho awali Alexandra alikishuhudia kikiteketea.

    "Huu ni muongozo wangu, kweheri nakwenda", aliendelea kusema, maneno hayo Alexandra aliyachukulia kuwa kebehi upande wake, sasa akahitaji kuthibitisha kuwa mpango wake umeota mbawa. Hivyo alimrushia ngumi, ajabu ngumi ile ilipitiliza upande wa pili kwenye mwili wa Devis ingawa hakumgusa, ni kama alipiga hewa.



    "Ahahaha hahaha", alicheka kwa dharau Devis huku akizipiga hatua kuel kwenye lango. Hatua kadhaa akasimama akamgeukia Alexandra ambaye kwa wakati ule alikuwa amepigwa na butwaa na kushindwa kumuelewa Devis. Lango lilifunguka, nje alionekana Dragon, pasipo kuchalewa Devis alimpanda, Alexandra aliona huo sio wakati wa kusubiri, bado alikuwa na nia ya kutaka kumuonyesha uwezo shetani Devis. Hivyo alimkimbilia, ila kabla hajatoka ndani ya jengo lile, alizuiwa na watu wa ajabu. Walisimama mbele yake, lilikuwa ni jopo la watu wasio pungua nane, wote mkononi mwao walishikilia siraha. Vinywa vyao vilikuwa vikitema damu, walikuwa na uchu, kwenye paji za nyuso zao zilikuwa na mihuri kama ule ule alio nao Devis.

    Mapigano kwake ilikuwa ni jambo la kawaida, kwa kuwa alijua fika njia ya kumrudisha duniani anaweza kuipata kupitia kitabu kile, hivyo hakuona haja ya kuhofia. Alikabiliana nao, patashika nguo kuchanika ilizuka, hakuwa na siraha ya kujibu mashambulizi ila alifanya juhudi ya kuwakwepa huku akitafuta nmna ya kulifulifungua lango ili amfuate Devis huko aliko elekea kuapishwa. Alipigwa mkumbo mkubwa, alianguka chini mfano wa ngunia la mchele pindi lidondoshwapo na kuli, lango likafunguka kwani alipo angukia ndio pale pale ambao Devis alisimama na lango likafunguka. Licha ya kupata mauvi ila alihitaji kutoweka mahali hapo amfuate Devis, hivyo alijinyanyua ili aanze safari ya kuelekea huko makao makuu ya Osaka ambapo huko ndio Devis anataraji kuapishwa, anapata cheo kikubwa huko Osaka baada kukidhi vigezo. Watu wale walio pewa jukumu la kuumaliza Alexandra walimfuata, lakini safari hiyo walionoa, walichelewa kwani hawakubahatika kumkamata. Alex alitimua mbio, muda huo huo maadhari ya OSAKA yalikuwa tofauti.. Yalionekana makaburi, hivyo watu wale nane walifanya jitihada za kuwafufua wafu walio kufa miaka gede gede iliyo pita kwa dhumuni la kuungana kumkabili Alexandra.. Vumbi kubwa lilipaa, radi na Ngurumo nzito ikalindima, kila baada ya muda mfupi skeleton walionekana kwenye uso wa ardhi ya Osaka, kwa muda mchache tu mamilioni ya skeleton walifurika na wote waliandamana kumfuata Alexandra ambaye naye anamfuata Devis ili kumkabili na hata ikiwezekana achukue kitabu kile alicho toweka nacho Mozana, aliamini kinaweza kumrudisha ulimwenguni..!!



    Wakati anakimbia, ghafla chini aliona upanga. Upanga mkali, aliuchukua na kisha kuendelea kutimua mbio, punde si punde mbele yake makaburi mengine yalijifukua, skeleton wale waliendelea kuongezeka, kuna waliomkimbiza kutoka nyuma, na wengine walitoka mbele. Hapo sasa Alexandra hakuona haja ya kuogopa, alipambana nao hasa wale waliojitokeza mbele yake, aliwafyeka mikono, vichwa aidha kila sehemu ambayo aliona itawafanya kushindwa kumkimbiza. Patashika ilikuwa kubwa Osaka mji ule wenye maajabu ya aina yake, vita ilikolea baina ya Alexandra na jopo la skeleton.



    Upande wa pili, Devis anashuka kwenye mgongo wa Dragon baada kuwasili kwenye makao makuu ya Osaka, jopo la watu wa ajabu liliungama ikiwa kama ishara ya kumheshimu bwana huyo. Walikuwa ni watu wenye jicho moja, maumbile yao makubwa kiasi, lakini pia ngozi zo zilikuwa za kijani huku nyuma walionekana kuwa na mkia. Walitisha viumbe wale, walikuwa wengi mamia na mamia. Makao makuu ya Osaka yalijengwa nje mji, si rahisi kufika huko hasa kutokana na aina ya viumbe wakali waliowekwa mbalimbali wafananao na binadamu na wengine wanyama.

    Tabasamu lilimjaa Devis huku akitembea kwa madaha kuzidi kuzama ndani ya jengo lile, alielekea mahala maalumu pa kuweza kula kiapo ili apate kile alicho kuhitaji kwa kipindi kirefu.



    Lango likafunguka, lango kubwa lililopo ndani ya jengo lile. Ndani zaidi palikuwa na chumba kikubwa chenye urefu na mapana, walionekana watu watatu wakiwa wamesimama huku nyuso zao wakiwa wameziinamisha. Chumba kilikuwa kikunukia manukato mbali mbali, moshi ulitaradadi kwa ustadi wa hali ya juu na kukifanya chumba kile kionekane kujaa ukungu.

    "Kariiiibu sana Devis", sauti nzito iliyojaa mwangwi ilisikika ikimkaribisha Devis.

    Devis akainamisha uso wake sanjari na kuitikia "Ahsanteni nimekaribia"

    ''Nadhani mmejionea, kila kitu kimeenda sawia. Na zaidi nimekileta mbele ya u kitabu hiki ambacho kitanipa muongozo mzuri. Samahani kwa kuchelewa ila nafikiria hakijaharibika kitu'', aliongeza kusema Devis kwa furaha, alikuwa na uchu wa kupata cheo kikubwa ndani ya mji wa Osaka huku ndoto yake kubwa ikiwa ni kuumiliki kabisa mji huo.



    Watu wale watatu walikaa kimya kwa dakika kadhaa, punde mmoja akavunja ukimya akasema ''Unafanya kazi nzuri lakini kwa sadaka hii ya mwisho umechemka vibaya sana''

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Unamaanisha nini!?", aling'aka Devis. Mtu yule akacheka sana kisha akamvuta Devis kwenye chumba cha pili ili amuonyeshe maana ya yeye kusema vile ikiwa kwingeneko patashika bado iliendelea, Alexandra alijitahidi kupambana na wale skeleton mpaka akafanikiwa kuwatoka, mbele zaidi ardhi ya shaba. Ardhi ile ilikuwa ikitoa mfuke kwa namna gani ilivyo kuwa ya moto. Palikuwa na joto kali mahali hapo, na huo ulikuwa ni moja ya ulinzi madhubuti kwa kiumbe kisicho rasmi kitakacho taka kufika makao makuu ambapo huko kuna mali mbali mbali nao kila aina ya uchawi.

    "Daah! Hapa bado kuna kimbembe! Lakini sikubali lazima nile sahani moja na Devis. Iwe isiwe atatapika nyongo huku huku Osaka", huku akihema haraka haraka alijisemea maneno hayo wakati huo akiangalia ardhi ile ya shaba ikiwa nyuma yake zikisikia fujo za skeleton zikijongea kumfuata.

    Radi ikapaza kwa mara nyingine tena, muda mfupi baadaye ukungu unyevu unyevu ukatanda, hapo sasa hakuona haja ya kuendelea kupoteza muda. Bila kujali alikanyaga ardhi ile huku akitimua mbio, katu hakusikia maumivu ya kuungua nyayo zake, maumivu aliyo yapata ni kwenye bega mahali alipo pigwa mhuri wa Mozana. Alipo ivuka ardhi ile akasimama kisha akageuka kutazama kule aliko toka, kwa mbaali ukungu ule ulianza kutoweka huku radi na Ngurumo kubwa zikiendelea kulindima. Alexandra akapata kuliona jopo la skeleton likiendelea kumiminika lilishindwa kumfuata. Alishusha pumzi ndefu na kusema huku akipiga kifua chake "Njooni sasa wajinga nyinyi, njooni kama kweli nyie mnaweza. Ahahaha hahahaha hahaha", alimaliza kwa kicheko kikubwa mara baada kujigamba.



    "Mimi ndio Alexandra, hakuna habari ya kujiita Bravo wala ujinga gani. Naitwa Alexandra, washenzi nyinyi, napita mnapo shindwa kupita nyinyi msio na nyama", aliendelea kujinasifu Alexandra kisha akavua koti lile alilo livaa akalitupa kwenye ardhi ile ya shaba, nalo likayeyuka upesi kwa muda mfupi tu, alistaajabu, akashusha pumzi ndefu kwa mara nyingine tena, na sasa akatazama bega lake mahali ambapo alipigwa muhuri, aliona muhuri ule ukiwa na rangi tofauti kabisa huku maumivi yakiishia kwa mbaali sana.

    "Ahsante sana Mozana, nahisi pasipo nyinyi hapa nisinge pavuka", alijisemea kisha akaendelea kuisaka makao makuu ya Osaka ambapo huko ndipo Devis alipo kimbilia akienda kuapishwa.



    Ulikuwa ni msitu mkubwa wenye kila aina ya viumbe, ili kufika makao makuu itabidi akabiliane na balaa lolote litakalo mtokea. Naam! Hatua ya kwanza wakati anatembea, ghafla mbele yake akatokea mnyama wa ajabu mwenye vichwa viwili, mnyama yule alikuwa akitema moto kila baada ya dakika mbili za duniani. Haraka sana Alexandra aliukamatia upanga wake kisawa sawa kwa dhumuni la kupigana jasho na damu mpaka ampate Devis, na zaidi aondoke na pete ile ambayo imepelekea kufika huko.



    Upande mwingi, Devis na yule mtu waliingia kwenye moja ya chumba. Chumba kile kilikuwa kimesheheni mishumaa lukuki. Na yote ilikuwa imezimwa kasoro mmoja tu.



    "Devis, nadhani unaiona hii mishumaa yote iliyo hap mbele yetu. Unatakiwa kutambua, hii iliyo zimika inawakilisha kuwa tayari wamechukuliwa nyota zao na kila kitu cha muhimu kwetu, sasa basi huu mshumaa ambao unauona bado unawaka, unabainisha kuwa mtu huyu hado yupo hajafanyiwa kitu chochote ", alisema mtu yule aliye ingia na Devis kwenye chumba kile kilicho sheheni mishumaa. Devis hakutaka kukubaliana na jambo hilo, aliamini kazi alio waachia wale viumbe kumtengeneza Alexandra watakuwa wameitengeza ila bwana huyo na mwenzake wanataka kumgeuka. Alifoka, alilalamika sana huku akiendelea kupingana na jambo hilo, alikuwa ni mkuu wa mji huo, pasipo woga huku akiwa na uchu Devis alimfokea.



    "Devis", mkuu huyo alipaza sauti kumuita, ghafla macho yake yaliwaka, hasira nazo zikimjaa. Na pindi kiongozi huyo anapo pata hasira kuna baadhi ya mambo hutokea, tetemeko kubwa huzuka na, viumbe kadha wa kadhaa waishio katika mji huo huangamia. Hivyo Devis hakuwa na budi kujishusha, alikuwa mpole, akapiga magoti ishara ya kuomba msamaha. Sasa wakatoka ndani ya chumba hicho cha mishumaa, chumba cha nafsi. Pindi mshumaa unapo zima, basi mwenye nafsi habari yake hukomea hapo. Hautakiwa kuzimwa bali huzimika wenyewe, lakini pindi unapo zimwa hata akirejea duniani hupagawa, hupoteza kumbukumbu mpaka mwisho wa uhai wake.



    "Huyu binadamu hatari sana, bila shaka ananisaka. Siwezi kupoteza muda wangu bure, nitauzima mshumaa mimi mwenyewe", wakati wanangoja mlango ufunguke, Devis aliwaza kufanya unyama kwa Alexandra baada kuona mpango wake unakwenda kuota mbawa. Alipania kuuzima mshumaa ili hata ikitokea Alexandra karudi duniani basi apoteze kumbukumbu zote, na mwishowe ageuke kuwa mwendawazimu.

    Naam! Mlango ulifunguka, ghafla walishtuka kukuta maafa kwa watu wale wawili walio salia kwenye kile chumba cha kiapo. Kiongozi wa Osaka alipigwa na butwaa, kama ilivyo ada Machi yake yalibadilika, yakang'aa samabamba na kuwasogelea ili kujua jambo wakati huo Devis naye akitazama kila kona ya chumba. Muda mfupi baadaye akapata wazo, nalo ni kwenda kuuzima mshumaa huku akihisi kuwa tayari Alexandra yupo mahali hapo. Mlango ulipo funguka akaingia, mlango huo hufunguliwa mara tatu tu, ili kufungua mara ya nne yakupasa uvute subira kwanza. Hivyo Devis safari hiyo alipo ingia katika chumba kile akakutana uso kwa uso na Alexandra kwa mara nyingine tena, alikuwa ametapakaa damu mwili mzima huku akionyesha kujawa hasira!.







    "Siku zote ujanja wa nyoka nyasi, pete tayari ipo kwenye yangu Devis, lakini pia nut nakihitaji kitabu hicho ili nikirudishmikonoe Mozana, na zaidi nahitaji kukumaliza kabisa. Siwazi kurudi duniani kutumikia kifungo cha kunyongwa, acha nikanyongwe tu ila kukupotezea wewe itakuwa ni furaha yangu tosha", alisema Alexandra huku akiivaa pete kwenye kidole chake, pete hiyo aliiweka kwenye himaya yake baada kufanikiwa kupigana jasho na damu mpaka kwenye chumba maalumu ambacho alifanikiwa kuingia na kuikuta ikiwa ipo ndani ya sanduku maalumu.

    Alistaajabu sana Devis baada kuona kuwa pete ile muhimu ipo kwenye himaya ya Alexandra, alipigwa na butwaa kwani hakudhania kuwa kijana huyo angeweza kuifikia, alimpeleka OSAKA kwa dhumuni lingine kabisa na sio kuichukua pete ingawa hakuwa muwazi.

    "Umepoteza muda wangu Devis, na kamwe sitoweza kuondoka Osaka pasipo kukupoteza. Shetani mkubwa wewe", aliongeza kusema Alexandra huku akihema haraka haraka, damu nayo ikiendelea kumvuja sehemu mbali mbali za mwili wake. Devis alikaa kimya, alitulia tulii mfano wa maji ya mtungini. Lakini punde si punde akapata wazo, siku zote aliamini kuwa mwanadamu ni kiumbe dhaifu sana, hivyo hakuona haja ya kumuhofia Alexandra kwa kuwa yeye sio mwanadamu wa kawaida.



    Alinyoosha mkono mmoja juu, mkono wa kulia, ukatokea upanga mkali, misuli ya mikono yake ilibadilika, damu nyeusi iliivaa kwa kasi ya ajabu sambamba na macho yake kubadilika rangi, yakawa ya blue huku meno yake ya mbele nayo yakionekana kurefuka, sasa Devis akazidi kujitanabaisha mbele ya macho ya Devis kuwa yeye sio mwanadamu bali yeye sheteni, huenda duniani na kujifanya mwanadamu kwa shughuli maalumu akiwa kama wakala.



    "Alexandra", alipaza sauti Devis, sauti yake ilijirudia mara mbili mbili wakati huo huo akamrushia upanga, kwa umahiri wa hali ya juu Alexandra akaukwepa lakini upanga ule ulienda kulenga kwenye mshumaa, upesi akaupoteza malengo, upanga ule ukagonga kuta, nayo pole pole ukaanza kutililisha maji. Alexandra hakujali, haraka sana akauchomoa upanga ule na kisha akajibu mashambulizi ya kasi, Devis alijitahidi kukwepa lakini teke moja lilimpata, alianguka chini. Na hapo ndipo Alexandra fahamu kuwa ule uwezo aliokuwa nao mwanzo Devis sio wa sasa. Devis wa awali katu asingeweza kuguswa na kiungo chochote cha Alexandra. Lakini mara hiyo hali ilikuwa tofauti kabisa, hapo Devis alichezea kichapo cha mbwa koko, kila alipo jaribu kujitetea, ndivyo alivyo zidi kuchapika. Pete ile ilimpa uwezo wa ajabu sana Alexandra, upande wa pili. Mkuu yule wa Osaka alipagawa baada kuikosa pete ile. Upesi akapanda juu ya kilele kwenye jengo ndefu, akatazama mazingira, alizidi kupigwa na bumbuwazi baada kuona jeshi lote limengamia kasoro wale skeleton wa ambao walifufuka kutoka kwenye makaburi, walikuwa wengi mno.



    Mkuuu huyo akajua fika adui yao bado yupo ndani ya Osaka, na ni hatari kama ataondoka na pete ile ya ajabu. Hivyo basi akahitaji kumdhibiti kwa vyovyote vile. Alishikwa na hasira, mavazi yake yakararuka, nyama za mwili wake zikamomonyoka. Dakika chache baadaye kiongozi huyo akabaki mifupa mitupu kikisalia kichwa tu ambacho chenyewe kilibaki kama kilivyo. Alipiga mwayo, radi ikamulika, Ngurumo nzito nayo ikapaza, akanyoosha mkono juu, ikatokea mbiyu akaipuliza. Sauti kubwa ya mbiyu ilizidi kufukua skeleton wengine ikiwa muda huo huo Alexandra akatoka ndani ya chumba kile alicho kuwa akipigana na Devis. Akimuacha akiwa hoi hata asiweze kunyanyuka. Alipofika nje akajikuta yupo kwenye jengo ndefu, alihitaji kama ili kushuka chini. Ghafla kaona waya mrefu uliotambaa kwenye jengo la pili, pasipo kujali Alexandra alijirusha kwenye waya ule, nao ukakatika akaanguka chini. Pale alipo angukia ardhi ilikuwa ya ajabu, ilimomonyoka. Upesi Alexandra alinyanyuka upesi akakishika vyema kitabu chake kisha akaanza kutimua mbio ikiwa muda huo huo huo mkuu wa Osaka alizama kwenye chumba kile akamkuta Devis yupo hoi bin'taabani. Alishikwa na hasira, kamwe hakutaka kusikia chochote kutoka kwake. Alimmalizia kabisa halafu akatoka ndani akafanya miujiza ya kuipoza ardhi ile ya shaba ili kuwapa nafasi wale skeleton wapite na wamfuatilie Alexandra ambae mara hiyo alionekana kukimbia kuzama zaidi ndani ya himaya ya Osaka.



    Jopo kubwa la skeleton lilivamia, dragoni naye akatokea. Aliitwa Vaku, ndio jina la kiongozi mkuu wa Osaka, aliongoza jopo hilo la Skelton kumfuata Alexandra kijana machachari kuliko kawaida. Sauti za ajabu ajabu zilipenya vyema kwenye masikio ya Alexandra, jambo hilo lilimfanya Alexandra kufanya kazi kubwa kutoweka Osaka. Hakupata nafasi ya kuketi na kusoma ramani ya kurudi duniani, alikimbia tu bila mpangilio. Baada kukimbia kwa muda mrefu hatimaye alifika kikomo, mbele hapakuwa na ardhi. Ulionekana ukungu, na rangi ya blue. Mahali hapo palifanana kila kitu na namna anga lifananavyo. Kitendo hicho kilimtia mashaka Alexandra, alihema haraka haraka, aligeuka nyuma, kwa mbali akapata kuona jopo la skeleton likiongozwa na Vaku likija kwa kasi.



    "Hapana sipo tayari kuona hatma yangu ikipotekea huku, nimevuka vigingi vingi, iweje leo nikamatwe kirahisi!?", alijisemea ndani ya nafsi yake Alexandra, papo hapo akajitosa kwenye anga lile wakati huo huo jopo lile la Skelton lilifikia mahali hapo, likabaki na labda, tumaini lao likaenda kinyume na walivyo tarajia. Vaku akalaani sana jambo lile, punde si punde akarudi kwenye hali yake ya kawaida, akaamrisha kundi lake lirudi kwenye makazi. Nalo likatii, skeleton wale walirejea makao makuu ya Osaka huku Vaku akiendelea kutazama mahala pale alipo jitosa Alexandra. Bado alionekana kutoamini kilicho tokea, ghafla akakumbuka kitu. Nacho si kingine bali ni mshumaa, akampanda Dragon wake na kisha kurudi upesi makao makuu kuuzima mshumaa, baada kumkosa akataka kufanya jitihada ya kummaliza kwa kuuzima mshumaa ili hata akirejea duniani asiwe na kumbukumbu yoyote kuhusu Osaka.



    Kwingineko, alionekana Alexandra akiwa emelala chini. Punde si punde akanyanyuka kwa kugugumia, na hatimaye alisimama kabisa japo bado alikuwa akiyumba yumba. Alikishika vyema kitabu chake, hakika alionekana kuchoka dhofu ilhali. Alitazama kulia na kushoto, nyuma yake kisha akatazama mbele yake. Aliona bango kubwa chini lililo andikwa jina MOZANA. Mji ulikuwa umeharibika vibaya, palikuwa na kila aina ya dhiki kuuu. Jambo hilo lilimsikitisha sana Alexandra, alijihisi kupata nguvu, na sasa akazipiga hatua pole pole kuzama zaidi ndani ya mji ule. Alipo fika katika ya wigo alipiga magoti chini na kisha kuomba msamaha kwa kile alicho kifanya. Haukuishia kuomba msamaha tu, bali aliangua na kilio kabisa.



    "Furaha yangu ni kukuona umerejea salama, tumesha kusamehe Bravo", sauti ya binti wa mfalme aitwaye Rinda ilipenya kwenye masikio ya Alexandra. Aligeuga nyuma ambapo ndipo ilipokuwa ilisikika sauti hiyo, alitaharuki kuona mji mwingine, mji ule ule wa Mozana, Safar hiyo uliona ukiwa vile vile kama alivyo uacha. Akiwa bado na taharuki akarudisha macho yake kutazama kule alikokuwa akiuona mji wa Mozana ambao uliona umejaa dhiki kuu. Mara hii hakuona kitu zaidi ya jangwa kubwa ambalo hakuona mwisho wake.

    Alexandra alizidi kupagawa, lakini aliondolewa hofu kwani hakuwa sawa kisaikolojia, ilikuwa ni picha ambayo alijenga upande wake kwa kudhania kuwa huenda mji huo ukawa umeharibika namna hiyo ambapo ni jambo ambalo lipo kinyume na alivyo kuwa akiwaza.



    Baada kuondolewa hofu na Rinda binti mfalme, hatimaye alikaribishwa kwa shangwe ndani ya mji huo, hivyo ujio wake ndani ya Mozana ulimpa heshima kubwa, kwani alileta kitu ambacho mfalme wa mji huo alikuwa akikitamani kwa kipindi kirefu sana, si yeye tu bali hata miji mingine kadha wa kadha iliitamani pete ile aliyo kuja nayo shujaa Alexandra ambaye kwa Mozana walimfahamu kwa jina Bravo.



    Mbali na kufanya kitendo hicho cha kishujaa, vile vile Alexandra alijenga uaminifu mkubwa baada kurudisha kitabu chao.

    Hakika Mozana yote ilisimama, jopo la watu ulijipanga lilikusanyika huku ikiimba kwa kulitaja jina la Bravo kama shujaa mkubwa kuwahi kutokea Mozana.

    "Bravoo.. Bravoo.. Bravoo"

    Mfalme wa mji huo alikumbuka maneno ya binti yake siku ile aliyo mwambia kuwa mwanadamu huyo anaweza kuwa msaada mkubwa kwake, utetezi huo ukapelekea Alexandra kuponyoka adhabu kali iliyokuwa imeandaliwa upande wake. Hatimaye maneno ya binti yake yakawa yametimia vilivyo pasipo shaka yoyote. Hivyo ikiwa kama shukrani, Alexandra akapewa nafasi ya kuchagua kitu chochote ambacho angehitaji kupewa. Wakati huo fujo zile ambazo zilikuwa zikimtaja zilikoma.



    "Nahitaji kurudi duniani, hii ndio furaha yangu pekee", alisema Alexandra kwa sauti kubwa iliyojaa ushujaa ndani yake.



    "Bravooo", Rinda binti mfalme baada kusikia chaguo la Alexandra alitaharuki na kupaza sauti kumtaja ikiwa wakati huo kule Osaka, mambo yalikuwa si mambo, Vaku hakwenda kwenye chumba kile cha mishumaa, aliingia kwenye chumba maalumu cha roho. Akaziingiza roho zipatazo saba mwili mwake kwa dhumuni la kuelekea duniani kufanya jambo..

    "Tutakutana duniani, hapo ndipo zitakapo julikana zipi mbivu na mbichi", alisema Vaku kwa hasira mara baada kujivika roho saba.





    Rinda alitaharuki alitamani kijana huyo aendelee kuishi Mozana, zaidi alijua atachagua kupewa asilimia kadhaa ya uongozi wa Mozana kwani alicho kifanya ni kitu kikubwa sana. Lakini basi Mfalme hakuwa na kinyongo juu ya hilo, alifunga kwanza nguvu zote za miji iliyo potea, jambo hilo lilipelekea hata Vaku kiongozi mkuu wa Osaka kuishiwa nguvu kabisa na kushindwa kufanya kile alicho kuwa amedhamilia. Kila alipo jaribu kwenda kwenye uso wa dunia, alishindwa kabisa.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    Kwisha kufanya hivyo jeneza lile alilo tua nalo Alexandra mwanzo wa safari yake, likatokea. Watu wa Mozana walikaa kimya kila mmoja akimtazama Alexandra kwa jicho la aina yake. Rinda alimkazia macho, Alexandra alipogeuka aligundua hilo, muda huo huo alizipiga hatua kumfuata. Alipo mkaribia alimtazama usoni kisha akasema "Wewe ni shujaa, nadhani unatambua hilo. Unarudi duniani, ila kaa ukijua umeacha historia kubwa ambayo haiwezi kufutika hapa Mozana. Bravo nataka nikupe zawadi yangu ambayo itakusaidia, utatimiza malengo yako na ndoto zako, hii itakuwa ishara ya kuendelea kuukumbuka huu mji na kunikumbuka mimi. Pokea ", alipo kwisha kusema hivyo, Rinda alimpa pete Alexandra, ilikuwa pete ambayo ipo tofauti na ile aliyo toka nayo Osaka. Alexandra alipokea akaivaa kisha akasema "Ahsante sana Rinda, daima nitawakumbuka watu wa mji huu"



    "Tunakupenda sana",alijibu Rinda kwa sauti ya chini huku akizipiga hatua kurejea mahali alipokuwa amesimama, muda huo huo Alexandra aliambiwa aingie ndani ya jeneza lile, aliingia kisha akalala chali mlango wa jeneza ukafungwa, radi ilimulika jeneza lile likatoweka. Si jeneza tu bali hata nyaraka mbalimbali zilizo elezea kesi yake ya kesi ya kukamatwa na madawa ya kulevya, kesi ambayo alihukumiwa kunyongwa ndani ya gereza la Diyarbakir lilipo nchini Uturuki, nazo zilitoweka tangu siku ile ambayo Devis alipo ondoka gerezani hapo baada mpango wake kabambe kukamilika, huku wahusika hata wasiwe na kumbukumbu kama ndani ya gereza hilo aliwahi kuishi mfungwa aliye itwa Devis wala Alexandra. Ajabu sana hii.



    Kwenye uso wa dunia, jiji Arusha kwenye makaburi ya jiji ndipo jeneza hilo lilipo ibuka. Ulikuwa ni usiku wa manene, siku hiyo mvua kubwa ilikuwa ikinyesha, ni mvua iliyo ambatana na upepo mkali sambamba na radi za hapa na pale. Mwili ule wa Alexandra ulijinyanyua kutoka ndani ya jeneza lile, kisha jeneza likatoweka kimaajabu huku likiuacha mwili juu ya kaburi la kale, jina la marehemu aliyeshikwa kwenye kaburi lile liliandikwa Devis Haroon, kwa mbaali yakioanisha tarehe ya kuzaliwa na kufa kwa marehemu yule.

    Radi kubwa ilimulika kisha Ngurumo nzito ikalindima, Alexandra alipotezwa pale akiwa bado hajayafumbu macho yake, akatupwa kando kando ya barabara. Alionekana kupoteza fahamu. Alilala hapo mpaka palio kucha, lakini alipitwa tu kwani baadhi yao walijua kuwa ni mwendawazimu ambaye ameamua kuisheherekea mvua ile asubuhi ile ya mapema kutokana jinsi Alexandra alivyo kuwa amevaa. Vazi lile la kustili sehemu yake ya siri, vazi asiri kutoka mji wa Mozana ndiyo alilo kuwa amelivaa. Hivyo ilipelekea wapita njia kumuona Alexandra ni kichaa, ingawa pia wapo waliodhania kuwa amegongwa na gari. Ndipo mtu mmoja akaenda kutoa taarifa kituo kidogo cha polisi kilichokuwa karibu na hapo alipo angukia Alexandra, polisi walipo fika eneo la tukio waligundua kuwa ni bado yupo hai. Hivyo basi upesi alilimbizwa hospitalini kufanyiwa matibabu.



    Jitahada zilifanyika haraka sana wakati huo kifikra Alexandra alikuwa akikumbuka baadhi ya matukio pindi alipokuwa kwenye mazingira ya ajabu huko kwenye miji iliyo potea. Akili yake ilillala japo alikuwa akipumua ila hakujua kilicho kuwa kikiendelea ulimwengu. Lakini katika kumbukumbu zake, hatimaye alifika hatua ile ambayo alijitosa Mtoni wakati anakabiliana na Joka lile ambalo lilikuwa likiwakosesha amani watu wafupi ambao walikuwa wakiishi katika msitu ule, mkumbo mkubwa ulio tokea pindi Joka lile lilipogeuka ilimpelekea Alexandra kupiga kelele na kuamka huku akihema haraka haraka. Kelele hizo zilipelekea madaktari waliokuwa wakimpa huduma hapo kabla hawaja muacha apumzike, walirudi wodini kumuangalia. Walimkuta Alexandra ameketi kwenye kitanda huku akihema haraka haraka sambamba na kujitazama mwili wake kisha macho yake kuyapeleka kwa madaktari wale ambapo mmoja alikuwa wa kike na mwingine wa kiume.



    "Khee samahani.. Samahani sana. Hivi nipo duniani? Hapa ndio duniani?", kwa taharuki kubwa Alexandra aliwauliza wale madaktari. Nao wakatazamana kabla hawajamjibu kisha mmoja akajibu "Ndio upo duniani"



    Aliachia tabasamu bashasha Alexandra mara baada kusikia jibu hilo, alijawa na furaha mno, punde akaongeza kuhoji "Nimefikaje hapa?."

    "Umeletwa kwa kibali cha jeshi la polisi, unahitaji kupumzika kwanza akili itulie", alijibu daktari mmoja kati ya wawili hao, naye alikuwa daktari wa kiume.



    "Polisi?", alihoji Alexandra. Kabla hajajibiwa alijilaza kitandani, nao madaktari wale walitoka wodini wakaenda kuendelea na majukumu mengine. Alexander alipo sikia kuwa yupo hapo kwa hisani ya jeshi la polisi hakuona haja ya kuendelea kukaa mahali hapo, dakika kumi baadaye alitoweka ndani ya Hospitali ile ndogo, akiwa na vazi lake lile lile alikimbia kwa kujificha kwenye baadhi ya majengo lakini alionekana kituko kila alipo pita. Mwishowe alipata sehemu ya kutulia, siku iliyo fuata ilibidi kwanza aishi maisha ambayo wengi walimchukulia, kwa kuwa alidhaniwa kuwa ni mwendawazimu, hivyo naye ilibidi aanze kuishi maisha hayo hayo.

    Alitembea bila woga na vazi lake lile lile alilo toka nalo Mozana, aliilinda vyema pete yake aliyo pewa na Rinda, kamwe hakuthubutu kuivua. Hakujua ni muda gani alio ishi huko ulimwengu mwingine, alicho shukuru ni kurejea tena duniani.



    Basi katika tembea tembea yake ndani ya jiji, alipata kuona tangazo la pambano kubwa la ngumi siku hiyo saa tatu usiku, kwa kuwa alipenda sana mchezo huo akajiapia kwenda kuhudhuria wakati huo akiwa katika maisha hayo hayo ya kujifanya mwendawazimu huku akitafakari namna ya kufika mbele ya wadogo zake alio waacha katika mazingira magumu.

    Hakucheza mbali na eneo hilo, lilikuwa pambano kubwa lililo jumuisha wapiganaji kutoka mataifa mbali, nje na ndani ya bara la Afrika.

    Mapambano ya utangulizi yalifanyika, mwishowe ilifika pambano lenyewe. Hapo ndipo Alexandra alipoamua kwenda kushuhudia pigano hilo, lakini alikumbana na vikali wakati wa kuingia kwani hakuwa na tiketi, baada mzozo mkubwa kutokea, mwishowe aliruhusiwa pindi tu amri ilipo toka kwa muaandaji mkubwa wa pambano hilo. Alipenda utu, alimuheshimu kila mwanadamu bila kujali mapungufu yake.

    Furaha iliyoje kwa Alexandra, aliketi nyuma kabisa huku macho yake yakiwa makini kutazama mpambano. Hakika ilikuwa patashika mtu mmoja aliye julikana kwa jina Benjamin Franklin alikuwa akipigana na mzungu kutoka Amerika ya Kusini aliitwa Jackson Juger. Mpambano ulikuwa mkali sana, pambano lenye raundi kumi, katikati ya mpambano Banjamin alionekana kuzidiwa, alipigwa kama mtoto mdogo. Baada kipigo kuzidi sana, kijana mdogo aliingilia kwenda kumtetea Benjamin ili asiuliwe kwani mapambano hayo hayakutambulika na serikali, ni wapiga dili wachache ambao walijikusanya na kuliandaa ili kuingiza pesa.

    Kijana yule aliendelea kumzuia Jackson asiendelee kumuadhibu Benja, kitendo kile kilimuudhi sana Jack alimshika kwa nguvu zote na kunyanyua juuu na kumtupia lugha chafu. Bwana mdogo alipiga mayowe, ghafla kule nyuma alipo simama Alexandra alipata kumuona vizuri kijana yule, alijaribu kuvuta kumbukumbu vizuri. Ilikuja na kupotea, lakini mwisho akamtambua vizuri, ni mdogo wake. Upesi alivamia ulingo ule na kisha kugawa dozi kwa mzungu yule, wengi walishangaa uwezo alio uonyesha Alexandra, na kwa kuwa alihofia kuwa mapambano hayo yapo kinyume na sheria katu hakuona haja ya kuendelea kusalia humo, hivyo alipo mchakaza vibaya yule mzungu alitoweka na mdogo wake huku nyuma akiacha gumzo. Mwendawazimu shujaa ikawa ndioo habari ya jiji.



    "Uliamua kutoweka na kutuacha peke yetu kaka, kwanini ulifikiria jambo hilo?", mdogo wake Alexandra alisema kwa uchungu.



    "Sikupenda ila yote harakati za maisha, mtajua mengi sana kwa yale niliyo pitia. Yule ni nani ambaye ulienda kumtetea. Na wapi alipo dada. Je, mpenzi wangu amesholewa?", Alexandra alihoji kwa hofu na taharuki kubwa. Kijana huyo aliyeitwa Carlos alishusha pumzi ndefu kwanza kisha akajibu " Mpenzi wako aliolewa, lakini baadaye alifariki wakati wa kujifungua, na kuhusu yule mtu pale ulingoni, ni bosi wangu, hunilipa pindi anapo nituma mzigo kwa rafiki zake?."



    "Mzigo, mzigo gani mdogo?"



    "Mdawa ya kulevya"



    "Mungu wangu na vipi kuhusu Angel?", alihoji tena Alexandra.

    http://deusdeditmahunda.blogspot.com/

    "Yupo, ila kwa sasa ni anajiuza kwenye kumbi mbalimbali za starehe, ndio maisha ambayo tulichagua kaka baada kuona umetutelekeza huko kijijini kwa miaka mitano, tuliamua kukufuata huku pasipo jitahida zozote za kukupata", Carlos aliongea kwa uchungu, kamwe hakusita kutoa machozi pia Alexandra naye alilia, alimlilia mpenzi wake ambaye pindi alipokuwa kwenye poli lile la mbilikimo aliota kuwa ameolewa, maumivu zaidi ni baada kusikia kuwa alifariki. Aliumia sana moyoni mwake huku akifikiria ameishije miaka yote hiyo kwenye miji ya ajabu, sasa alimtaka mdogo wake wamtafute dada yao, ni baada Alexandra kujiondoa ule muonekano wa awali. Jitihada zao zilifanikiwa walimpa. Kwa kuwa pete ile ilikuwa mali, aliuza gharama kubwa, pete hiyo ikawa imayabadilisha kwa asilimia kubwa maisha ya kijana huyo mtafutaji, kijana shujaa mwenye ujasiri wa aina yake.. Alexandra akawa tajiri baada kusota kwa kila aina ya maisha katu hakumsahau Rinda binti mfalme wa Mozana wala Devis wakala wa Osaka.. Alexandra Big boss!



    MWISHO.

0 comments:

Post a Comment

Blog