Simulizi : Jini Mauti
Sehemu Ya Nne (4)
Haikuwezekana watu wawili wafe kipindi walichokuwa wakifanya mapenzi na mimi, nilihisi kulikuwa na kitu ambacho bibi yangu alikuwa akikifahamu.
Usiku wa siku hiyo sikulala, nilibaki nikilia tu. Sikutaka kwenda uwanjani kukutana na wachawi wenzangu zaidi ya kukaa tu nyumbani. Ilipofika usiku bibi na wachawi wengine wawili wakafika chumbani kwangu.
Kitu cha kwanza kabisa kukifanya ni kuviinamisha vichwa vyao mbele yangu kisha kunipongeza kwa kazi niliyokuwa nimeifanya ya kumchukua mtu wa pili na kumpeleka kule kulipokuwa na kundi kubwa la misukule.
“Kwa nini mimi?” niliuliza huku nikilia.
“Wewe ni kiongozi wetu.”
“Ndiyo niue? Sitaki kuua.”
Nilisema huku nikilia mno. Hawakuniambia kitu chochote kile zaidi ya kuondoka. Katika kipindi chote hicho sikuwa nikijua kwamba bibi yangu aliniwekea jini mauti mwilini mwangu.
Nilisema huku nikilia mno. Hawakuniambia kitu chochote kile zaidi ya kuondoka. Katika kipindi chote hicho sikuwa nikijua kwamba bibi yangu aliniwekea jini mauti mwilini mwangu na kwamba kwa kila mwanaume ambaye ningefanya naye mapenzi ilikuwa ni lazima afariki dunia. Endelea….
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Siku iliyofuata, nilikwenda shuleni kama kawaida, nilipofika, nikaanza kusikia vilio kutoka kwa wanafunzi mbalimbali, moyoni niliumia mno, nilijua fika kwamba kile kilichokuwa kikiwaliza ni kuhusu kifo cha Mudi aliyefariki dunia mbele ya macho yangu.
Nikashindwa kuvumilia, machozi yakaanza kunibubujika, nilihisi moyo wangu kuwa na maumivu makali mno. Sikuamini kama nilikabidhiwa umalkia ambao ulinifanya kumuua mwanaume yeyote ambaye ningelala naye.
Moyo wangu ukakosa amani kabisa, nilipokuwa nikiwaangalia walimu na wanafunzi waliokuwa wakilia, moyo wangu ulijisikia hukumu sana. Wengi walijua kwamba nilikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mudi lakini hakukuwa na aliyefahamu kama jana usiku tulikuwa wote hivyo kuona kwamba nisingeweza kugundulika.
Kitu kilichonishangaza ni wanafunzi wengi kuanza kuninyooshea vidole. Kwanza nikashangaa, haikuwa kawaida hata kidogo, kwa nini sasa waninyooshee vidole? Niliwafanya nini mpaka kunifanyia kitu kama hicho, kila nilichojiuliza, nikakosa majibu kabisa.
Sikutaka kujali sana, nikazidi kuendelea mbele mpaka nilipoingia darasani, huko nako kila mwanafunzi aliogopa kunisogelea ni marafiki zangu wawili tu ndiyo walionifuata, alikuwa Anita na Maria.
“Mbona watu wananikimbia na kuninyooshea vidole?” niliwauliza huku nikilia.
“Wanasema wewe ndiye umemuua Mudi,” alinijibu Anita.
“Mimi nimuue Mudi?”
“Ndiyo! Wanasema haukuanza kuua hapo, hata ulipokuwa na Thomas, ilikuwa hivyohivyo, alikufa kifo kama hiki, tena chumbani kwake,” alisema Maria, maneno yale yakaniongezea uchungu.
“Yaani mimi nimuue Mudi?” niliuliza kwa sauti ya juu na kuanza kulia.
Ndiyo nilimuua lakini sikujua nilimuua vipi. Wanafunzi waliniogopa sana na wengi wakayaamini maneno aliyokuwa akiyapakaza Agape kwamba nilikuwa mchawi. Kuanzia siku hiyo sikuwa na amani na hata nilipotaka kwenda mazishini na wanafunzi wengine, wote wakanitenga.
Niliachwa shuleni nikilia peke yangu, kilio changu kilikuwa ni kumlilia bibi yangu kwa kile alichokuwa amenifanyia. Sikutaka kabisa kuua, watu wote waliokuwa wamefariki dunia walikuwa wale niliowapenda kwa moyo wa dhati.
Hakukuwa na wa kunibembeleza tena, kila mtu alinikimbia na hawakutaka hata kunisogelea. Nilijisikia aibu kubwa, shule ikawa chungu, kuanzia siku hiyo nikajuta kuwa mchawi, sikuwa na uhuru hata kidogo, sikuwa na uhuru wa kuwa na mwanaume yeyote.
Wakati nikikaa hapo darasani huku nikilia tena shule nzima kukiwa hakuna mtu yeyote zaidi ya mlinzi, ghafla nikaanza kusikia kizunguzungu kikali, nikajikaza lakini ikashindikana kabisa, kizunguzungu kile kikanipelekesha mno, nikajaribu kusimama, nikashindwa, nikaangukia viti na hapohapo nikaanza kuona giza, sikujua tena ni kitu gani kiliendelea.
***
Nilikuja kupata fahamu na kujikuta nikiwa kitandani, dripu ilikuwa ikining’inia juu yangu na maji yalikuwa yakiingia taratibu katika mshipa wangu. Macho yangu yalikuwa mazito, kitendo cha kuiona dripu ile tu nikajua kwamba mahali nilipokuwa palikuwa ni hospitalini.
Nikaanza kuangalia huku na kule mle chumbani nilimokuwa peke yangu. Nikaanza kuvuta kumbukumbu ilikuwaje mpaka nikafika hapo pale.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
kwani nilichokikumbuka ni kwamba ulipita mwaka wa nne sikuwa nimeumwa ugonjwa wowote.
Hapo ndipo kumbukumbu zangu zilipoanza kurudi nyuma kabisa, nikaanza kukumbuka kipindi kile nilichofika shuleni ambapo wanafunzi wenzangu walikuwa wakilia, baada ya hapo wote wakaanza kuninyooshea vidole, kilichoendelea ni kwenda darasani, baada ya hapo, sikujua kitu gani kiliendelea.
Wakati nikifikiria hayo ndipo mlango ulipofunguliwa, mwanamke mmoja, alikuwa mtu mzima akaingia ndani ya chumba kile, alivalia koti jeupe, lilikuwa kubwa na hapa kifuani, upande wa kushoto kulikuwa na kibati kidogo kilichoandikwa Dk. Lucy.
“Umerudiwa na fahamu, kweli Mungu mkubwa,” aliniambia daktari yule huku akiachia tabasamu pana usoni mwake.
“Nipo hospitali gani?”
“Mtakatifu Tabitha,” alinijibu.
“Ipo wapi?”
“Hapa Manzese,” alinijibu tena.
Nilikaa hospitalini hapo nikimsubiri mama aje, wala haikuchukua saa nyingi mama akafika hospitalini hapo, aliponiona, alionekana kufurahi sana na ndipo aliponiuliza ni kitu gani kilitokea mpaka kuwa kwenye hali hiyo.
Sikumficha, nikaanza kumuhadithia kila kitu kilichotokea, alisikitika mno, kila nilipomwangalia, nilijisemea kwamba muda wowote ule angeweza kumwaga machozi yake kitu ambacho kingeniuma sana kwani sikutegemea kuyaona machozi ya mama.
“Pole sana Davina…” aliniambia.
“Asante mama. Baba yupo wapi?” nilimuuliza.
“Amekwenda kazini, tukirudi utamuona,” aliniambia.
Hakukuwa na mwanafunzi yeyote aliyekuja kuniona, nilijisikia mpweke sana hata marafiki zangu wawili niliowategemea, Maria na Anita hawakuweza kufika hospitalini hapo. Moyo wangu uliniuma mno, sikuamini kama mimi ndiye niliyekuwa nikipitia yale au mtu mwingine. Wakati mwingine nilitamani kila kitu kilichokuwa kinaendelea kiwe ndoto na baada ya dakika kadhaa niamke kutoka usingizini.
Ilipofika saa sita mchana nikaruhusiwa kurudi nyumbani. Njiani nilitembea kwa unyonge, kila mtu niliyekuwa nikimuona niliamini kwamba na yeye aliambiwa juu ya kile kilichokuwa kimetokea hivyo watu wote kuniona mchawi.
“Mama….” nilimuita.
“Abee mwanangu.”
“Mudi amekufa?” niliuliza huku nikionekana kutokuamini.
“Ndiyo! Kazi ya Mungu haina makosa,” aliniambia mama, nikaanza kulia.
Ukweli ni kwamba nilimpenda sana Mudi, baada ya Thomas kufariki dunia, mtu ambaye aliuteka moyo wangu vilivyo alikuwa Mudi tu. Sikuamini kilichokuwa kimetokea, kitendo cha kumpoteza Mudi muda mchache baada ya kuanza kufanya mapenzi hakika iliniuma sana.
Wanafunzi na walimu hawakutaka kuwa nami, hawakutaka kunifariji kwani walijua ni kwa jinsi gani nilikuwa karibu na Mudi, matokeo yake, badala ya kunifariji ndiyo kwanza wakanitenga na kuniacha shuleni nikiwa peke yangu.
Baada ya kufika nyumbani, saa moja baadaye mzee Abdallah, baba wa kambo alipokuja mama alimwambia kile kilichotokea. Baba hakuamini kama kweli walimu na wanafunzi, pamoja na elimu yao walikubaliana na maneno kwamba nilikuwa mchawi. Waliona kwamba ninasingiziwa na hata hao watu waliokufa ni kwamba siku zao zilifika.
“Hawa walimu ni wapumbavu sana,” alisema baba huku akionekana kukasirika.
“Tena sana, yaani umtenge mtoto kisa tu mnasema yeye ni mchawi,” alisema mama, wote kwa pamoja walionekana kuwa na hasira mno.
Japokuwa mama alionekana kunitetea sana lakini alikuwa na wasiwasi mno, kila nilipomuona akiwa peke yake, mawazo yalimsonga na alionekana kufikiria mambo mengi sana. Ukweli ni kwamba mama alikuwa na wasiwasi mwingi, kila kitu kilichokuwa kikitokea kilimfanya kuwa na mawazo mno.
“Davina…” aliniita.
“Abee mama.”
“Hebu niambie ukweli, wewe ni mchawi?” aliniuliza, alinikazia macho.
“Mimi?”
“Si ndiyo naongea nawe.”
“Hapana mama! Mimi si mchawi.”
“Kweli?”
“Ndiyo mama!”
“Na mbona kila unayefanya naye mapenzi anakufa?” aliniuliza.
“Mama! Mimi sijui.”
“Hapana! Lazima kuna kitu. Utakuwa umepewa mkoba wa uchawi ni lazima nikupeleke kanisani kuombewa,” aliniambia.
“Kwenda kanisani?”
“Ndiyo!”
“Sitaki, siwezi kwenda kanisani.”
“Kwa nini?”
“Basi tu.”
Sikutaka kwenda kanisani, nilikuwa na hofu kubwa kwani nilijua mambo ya kanisani yalikuwa vipi. Nilimkatalia mama, sikuwa radhi kuona nikienda kanisani kwani maisha yangu hayakuwa mazuri hata kidogo.
Sikwenda tena shule, nilimuomba baba anichukulie uhamisho na kweli akafanya hivyo, nikahamia katika Shule ya Sekondari ya Mbezi. Shule hiyo ilikuwa tofauti na Manzese, pale Manzese ilikuwa ni shule ya serikali lakini hii ilikuwa ya mtu binafsi.
Hapo kulikuwa na wasichana warembo walioonekana kuwa na maisha mazuri. Kuna wengine waliokuwa wakijiita majina mazuri ya Kizungu ilimradi kuwaonesha watu ni jinsi gani walikuwa warembo.
Mimi sikuwa msichana mrembo ila Mungu alinibariki kwa kunipa umbo zuri kwa nyuma, nilikuwa nimeumbika na kila nilipopita mbele ya wanaume ilikuwa ni lazima kunitazama kwa nyuma na kama ukinitazama ilikuwa ni lazima unitamani.
Nilipoingia shuleni hapo ilikuwa gumzo, wanaume wengi walinizungumzia, wengine wakawaambia wasichana wawaunganishie kwangu lakini sikuweza kukubaliana nao.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Bado nilikumbuka kilichotokea kwa Thomas na Mudi, sikutaka kitokee kwa mtu mwingine. Wanaume wengi walikuwa wakinifuata kila siku lakini sikutaka kukubaliana nao. Kidogo hapo Mbezi nilionekana kuwa na amani, hakukuwa na mtu aliyenisimanga kwa kuwa nilikuwa mchawi.
Kati ya wanaume wote waliokuwa wakinifuata, kulikuwa na watatu ambao walionesha uhitaji mkubwa wa kuwa nami, wa kwanza aliitwa Michael, huyu alikuwa mwanafunzi wa kidato cha nne, wa pili alikuwa Sifael, mwanafunzi wa kidato cha tatu kama mimi na mwingine alikuwa dereva bodaboda ambaye alikuwa akiegesha pikipiki yake katika eneo ambalo halikuwa mbali na shuleni hapo, huyo aliitwa Hemed.
Kama msichana nilionesha msimamo wangu, halikuwa jambo jepesi kunilaghai, mbali na hiyo nilikuwa na wasiwasi kwamba kama ningemkubali mwanaume yeyote basi ingekuwa ni lazima afe wakati wa kufanya mapenzi.
Kuroga sikuacha, bado niliendelea kama kawaida. Tulisafiri usiku na ungo, tulikwenda sehemu mbalimbali huku nikisimama kama kiongozi. Nilipata nafasi ya kula nyama za watu na kunywa damu zao na mambo mengine ya kishirikina.
Katika maisha yangu yote ya uchawi nilikuwa naogopa kwenda kwa watu wa makanisani ambao walisimama imara na Mungu. Wakati mwingine nilitoa hofu na kwenda kuwaroga watu hao majumbani mwao.
Huko, tulikuwa tukikutana na mambo ya ajabu mno ambayo yalitushangaza. Nakumbuka kuna siku tulipanga kwenda kumroga mchungaji wa kanisa moja la Praise And Worship la pale Mwenge, tulitaka tumpe uchovu wa kufika kanisani kwake kwani alikuwa akitusumbua sana.
Tulipofika katika eneo la nyumba yake, hatukukuta nyumba yoyote ile zaidi ya bahari iliyokuwa ikipiga mawimbi makubwa.
Tulishangaa sana, tulihisi labda tulikuwa tumekosea njia, tuliondoka na kurudi tena usiku huohuo, tena kwa kuangalia vizuri njia, tulichokiona mara ya kwanza ndicho tulichokiona tena, bahari kubwa iliyokuwa ikipiga mawimbi makubwa.
Haikuwa hivyo tu, wakati mwingine tulipokuwa tukija, hatukukuta kitu chochote zaidi ya jangwa kubwa lililokuwa na mchanga wa moto. Matukio hayo yalitushangaza mno hivyo tukaachana na mambo ya kumfuatilia mchungaji huyo.
Sikutaka kuona mtu mwingine akifa tena kwa ajili yangu na ndiyo maana kila mwanaume aliyeniambia ukweli hakuweza kunipata. Hemed ndiye aliyeonekana kuwa msumbufu sana kwangu, kila nilipotoka shule ilikuwa ni lazima kunifuata na pikipiki yake, akinichukua na kunirudisha nyumbani, aliponifikisha, hakuwa akiondoka, alikuwa akizungumza na mimi kwanza ndiyo aondoke.
Alinisumbua sana. Simu yangu ya kwanza kutumia nilinunuliwa na yeye. Sikutaka kuichukua kwa mara ya kwanza lakini baada ya kunibembeleza sana, nikajikuta nikiichukua. Tulikuwa tukizungumza usiku, kuchati kama kawaida na aliendelea kuniambia kwamba alinipenda sana.
“Ninakupenda Davina,” aliniambia mara kwa mara simuni.
“Lakini bado nasoma.”
“Hakuna tatizo. Kwani nitakatisha masomo yako?”
“Hapana. Ila naogopa mimba.”
“Kwani si kuna kinga jamani, kuwa wangu Davina,” aliniambia kwa sauti ya kubembeleza.
“Hemedi.”
“Naam.”
“Najua unanipenda lakini naomba unipe muda jamani,” nilimwambia.
Hapo ndipo nilipoamini kwamba mwanaume anapoamua kumtafuta mwanamke huamua kwa nguvu zote. Sikupumua vizuri, Hemedi anapiga, sikutulia vizuri, Hemedi anatuma meseji, yaani alifanya mambo yote kuonyesha kwamba alikuwa akinipenda mno. Pamoja na hayo yote, wasiwasi wangu ulikuwa mmoja tu kwamba sikutaka kufanya naye mapenzi kwa kuwa sikutaka kuona akifariki dunia.
“Hemedi…”
“Naaam!”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
“Sitaki ufe…”
“Hutaki nife?”
“Ndiyo! Nataka uishi mpaka kifo cha kawaida kitakapokukuta.”
“Unamaanisha nini?”
“Ukifanya mapenzi na mimi, utakufa.”
“Hahaha! Davina acha kunipiga saundi, au ndiyo unaninyima kijanja?” aliniuliza Hemedi huku akicheka kwenye simu.
“Hemedi! Sitaki ufe, naomba unielewe.”
“Na kama nikitaka kufa kwa ajili yako, kuna tatizo kwani?”
“Hemedi! Mbona wewe mwanaume unakuwa mbishi?”
“Nakuwa mbishi kwa sababu nakupenda. Davina, kwanza hebu naomba tukutane sehemu tuongee,” aliniambia.
“Wapi?”
“Popote pale.”
“Sema wewe.”
“Tukutane Sinza.”
“Sinza gani?”
“White Inn kwenye Bar ya Shika More.”
“Sawa.”
Kilichofuata ni kupanga mikakati ya kuonana. Tulipanga kuonana majira ya saa kumi na moja. Nilikuwa na mawazo mengi, nilijitahidi kwa nguvu zote kumkataa Hemedi lakini hakutaka kunielewa kabisa, kila wakati alikuwa akinisumbua.
Nilimwambia kwamba endapo angefanya mapenzi na mimi ilikuwa ni lazima afariki dunia lakini hakutaka kusikia kabisa na ndiyo kwanza aliniambia maneno mengi ya kimahaba kwamba alikuwa tayari kufa kwa ajili yangu.
Siku hiyo nilikubali kuonana naye lakini sikutaka kufanya naye mapenzi kabisa, yaani ilikuwa ni kukutana, kupiga stori kisha kila mtu kuondoka zake. Nilipofika katika Baa ya Shika More, nilimuona akiwa ametulia kwenye meza moja iliyokusanya viti vinne, aliponiona, akaanza kutoa tabasamu pana.
“Karibu mrembo,” alinikaribisha na kutulia kitini.
Tukaanza kuongea, kila sentensi moja aliyoizungumza ilikuwa ni lazima kuniambia kwamba alikuwa akinipenda sana. Nilibaki nikimwangalia usoni. Si kwamba sikumpenda, nilimpenda mno lakini kitu ambacho sikukitaka kabisa ni kufanya naye mapenzi tu.
Alijitahidi kuniambia maneno mengi ya kunishawishi lakini wapi, sikukubaliana naye kabisa. Alichokifanya akanisogelea, kwa sababu giza lilianza kuingia, akanishika kiuno.
Hapo ndipo aliponichanganya, ni kama aliijua sehemu hiyo ndiyo iliyokuwa ikinipa mzuka, hapohapo nikatoa mguno mmoja, akaligundua hilo hivyo kuendelea kunishika kiuno.
Ndani ya dakika kumi nilikuwa hoi, akausogeza mdomo wake na kunipumulia, pumzi yenye joto fulani ikanipiga shingoni, ikanichanganya, akaninyanyua na kwenda kwenye gesti iliyokuwa karibu na baa hiyo, tulipofika huko, akachukua chumba.
“Hemedi,” nilimuita, tayari alinitupia kitandani, nilikuwa hoi.
“Unasemaje mpenzi?” aliniuliza huku mkono wake ukiendelea kuwa kiunoni mwangu, alizidi kunipagawisha.
“Unataka tufanye nini?”
“Mpenzi yaani unakuwa hauelewi? Kwani gesti kazi yake nini?”
“Unakumbuka nilik…ahhaa…ooiishiii…” nilimwambia lakini nikashindwa kumalizia sentensi, nikaishia kuguna.
Ndani ya dakika kadhaa, wote tulikuwa kama tulivyozaliwa. Nilikuwa nahema kwa kasi, Hemedi alionekana kuwa na haraka mno, kila kitu alichokifanya alikifanya huku akiwa na presha.
Hapo ndipo nilipopata kumbukumbu juu ya kile alichokuwa akitaka kukifanya Hemedi kilikuwa cha hatari sana kwa maisha yake. Kama mtu niliyeshtuka kutoka katika jambo fulani, nikamwangalia usoni tena kwa kumkazia macho, yeye mwenyewe alinishangaa.
“Hemedi, utakufa….” nilimwambia huku nikijaribu kumsukuma.
“Nipo tayari kufa…nipo tayari kufa,” aliniambia, hakuonekana kuwa tayari kuniacha kwa siku hiyo.
Kutokana na kuwa na nguvu, nikashindwa kumsukuma, tayari alikuwa juu yangu na alianza kufanya mchezo ule ambao sikutaka kufanyiwa na mwanaume yeyote yule. Moyo wangu uliumia mno, nilijua kile ambacho kingekwenda kutokea, nilijua kwamba Hemedi angeweza kufa kama ilivyokuwa kwa Thomas na Mudi.
Kile nilichokifikiria ndicho kilichotokea, tukaanza kufanya mapenzi, baada ya dakika moja huku akiwa juu yangu, palepale, nikaanza kuyaona macho ya Hemedi yakianza kubadilika, yakawa mekundu kama yaliyojaa damu. Akaanza kutetemeka na kutoa miguno iliyoashiria aliumia.
Akatoka juu ya mwili wangu, mapovu yakaanza kumtoka mdomoni huku damu zikitoka katika sehemu zilizokuwa wazi, puani na masikioni. Nilipoona hivyo, niliogopa mno, sikuamini kama Hemedi alikuwa akienda kufa kama ilivyokuwa kwa Thomas na Mudi.
“Aagghh….” alilia kwa maumivu makali pale chini alipokuwa.
Macho yake yakaanza kubadilika, yakatoka katika wekundu mithili ya damu na kuwa meupe kabisa, ulimi ulijigongagonga kwenye meno, kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika mwili wake, kiliniogopesha.
Nilishindwa kumsaidia kabisa, nikabaki nikimwangalia huku nikivaa haraka. Nilipomaliza, sikutaka kupoteza muda, nikaondoka kurudi nyumbani, tena huku nikikimbia.
Kifo cha Hemedi kilinitisha mno achilia mbali kuniumiza, nikawa najiuliza kwa nini hakunielewa nilipomkataza na kumweleza angefariki dunia.
“Wewe dada!” aliita msichana wa mapokezi, aliniita baada ya kuniona nikikimbia.
Nilimwacha Michael aondoke lakini ukweli ni kwamba hata mimi mwenyewe nikaanza kumuonea huruma, alikuwa kijana mpole, hakustahili kukaripiwa, alikuja kwangu kwa ajili ya kunijulia hali tu lakini kutokana na hali niliyokuwa nayo, likatokea la kutokea.
Stori za kifo cha Hemedi ziliendelea kusikika shuleni hapo, taarifa zikatapakaa kwamba usiku uliopita aliaga kwamba anakwenda kuonana na msichana maeneo ya Sinza, akaondoka kuelekea huko lakini hakurudi na maiti yake ilikutwa chumbani ikiwa imekakamaa.
Marafiki zake walihuzunika mno, hawakujua ni mwanamke gani aliyekuwa naye ambaye alimsababishia kifo hicho kwani ni mara nyingi sana Hemedi alifanya mambo yake kisiri ili aweze kutembea na wasichana wengi.
Tetesi zile ziliendelea kusikika kwamba kulikuwa na msichana ambaye alikuwa akitembea naye kutoka shuleni hapo, inawezekana ndiye ambaye alisababisha kifo cha Hemedi, marafiki zake wakaanza kuulizana, huyo msichana alikuwa nani? Na si kwao tu, hata wanafunzi walipozipata taarifa hizo nao wakaulizana, huyo msichana alikuwa nani? Kila walipoulizana, hawakupata jibu lolote lile.
******
“Naomba unisamehe Michael.”
“Umenikasirisha sana.”
“Najua, naomba unisamehe.”
“Au kwa sababu ulijua kwamba ninakupenda ndiyo maana ukaamua kunidhalilisha?”
“Hapana! Naomba unisamehe.”http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Nilisimama mbele ya Michael, nilikuwa nikimuomba msamaha kwa kile nilichokuwa nimekifanya, nilimdhalilisha, alijisikia aibu na hakukuwa na kitu kingine cha kumwambia zaidi ya kumuomba msamaha.
Moyo wangu ulinihukumu sana, kitendo nilichomfanyia Michael kilikuwa cha aibu sana hivyo nilipaswa kumuomba msamaha. Katika hilo naye akaanza kuunganisha mambo yake, aliniambia wazi kwamba alinisamehe kwa sababu alikuwa akinipenda.
Alionekana kuwa na mapenzi ya dhati kwangu, alionesha kila dalili ambazo mwanaume mwenye mapenzi ya dhati alitakiwa kumuoneshea mwanamke. Niliziona dalili zote hizo lakini pamoja na hayo yote, sikutaka kuwa na mvulana huyo hata mara moja.
Wiki moja ilikuwa imepita tangu Hemedi afariki dunia chumbani, sikutaka kuona mwanaume mwingine akifariki kwa sababu yangu, niliogopa, nilikuwa na moyo wa huruma, sikutaka kumuona Michael akifariki dunia.
“Davina…”
“Abee…”
“Nakupenda sana.”
“Najua.”
“Kwa hiyo?”
“Siwezi kuwa nawe.”
“Kwa nini?”
“Sina sababu! Siwezi tu kuwa nawe.”
“Au hunipendi?”
“Sijui.”
“Hujui nini sasa?”
“Kama nakupenda au sikupendi.”
Sikutaka kumwambia ukweli, kiukweli sikutaka kuwa naye lakini bado nilikuwa na moyo wa huruma juu yake. Nilijua fika kwamba endapo ningemwambia ukweli kwamba simpendi angehuzunika sana, angeumia na hivyo kumuonea huruma kila nitakapokuwa nikimuona.
Michael alining’ang’aniza lakini msimamo wangu ulikuwa uleule kwamba nisingeweza kuwa naye kwa sababu niliamini ilikuwa ni lazima siku moja tufanye mapenzi na baada ya hapo ambacho kingefuatia ni mauti tu.
Kila siku ilikuwa ni lazima Michael anifuate darasani kisha kunichombeza kwa maneno yake matamu kwa lengo la kukubali niwe naye lakini msimamo wangu haukulegea, bado niliendelea kuwa vilevile kwamba sikutaka kuwa naye.
Wakati Michael akiendelea kunifuatilia, naye Sifael alikuwa kwenye kasi ileile, kila siku alionekana kuwa mtu mwenye hasira mno kila alipomuona Michael akija na kukaa pale nilipokuwa. Alimchukia kwa kuwa alimpenda msichana ambaye hata naye alimpenda kwa mapenzi ya dhati.
Japokuwa alinipenda sana lakini Sifael alikuwa muoga, hakuwa tayari kunifuata na kuniambia ukweli kwamba alikuwa akinipenda ila kila nilipomwangalia niligundua alikuwa akinipenda sana.
Siku zikaendelea kukatika, niliendelea kuroga pasipo kujulikana, tulikesha sana makaburini tukiroga, hakukuwa na mtu aliyekuwa akitutisha zaidi ya wachungaji tu. Wakati mwingine tulikuwa tukienda mochwari, huko tulikuwa na kazi ya kuchukua viungo vya binadamu.
http://deusdeditmahunda.blogspot.com/
Baada ya siku kadhaa, kidato cha nne wakatarajia kufanya mahafali, walipanga kufanyia katika Ufukwe wa Coco. Ki ukweli sikutaka kwenda lakini Michael alinisisitiza kwamba nilitakiwa kwenda kwa ajili ya kumpa kampani, nikakubaliana naye.
Siku hiyo tulikusanyika kwa wingi sana, ilikuwa kama saa nane mchana hivi. Watu tulikula na kunywa na wengine kwenda kuogelea. Sikuwa sawa, nilikuwa na mawazo yangu tu kwani tangu kujiunga na kuwa mchawi, kwa kweli sikuona faida yoyote ila kujitoa lilikuwa suala gumu.
“Mbona upo hivyo?” aliniuliza Michael.
“Nipo vipi?”
“Hauna furaha! Tatizo nini?’
“Hakuna tatizo.”
“Kweli?”
“Ndiyo!”
ITAENDELEA
0 comments:
Post a Comment